Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

WASHINDI WA SPRITE BBALL KINGS WAPATIWA ZAWADI ZAO

$
0
0
Mkuu wa Vipindi wa Kituo cha Redio EA Nasa Kingu akimkabidhi Nahodha wa Mchenga Bball Stars Mohamed Yusuph kitita cha Shilingi Milioni 10 baada ya kufanikiwa kuwa mabingwa wa michuano ya Sprite BBall Kings 2018 yaliyomalizika mwishoni mwa wiki, kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Nchini (TBF) Mwenze Kabinda akishuhudia tukio hilo.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
KAMPUNI ya Sprite kupitia kwa muandaaji wa wa Michuano ya Sprite Bball Kings kituo cha Luninga cha Eatv na Ra Rredio wamekabidhi zawadi kwa washindi wa michuano hiyi kwa  2018 yaliyomaliza mwishoni mwa wiki iliyopita.

Zawadi hizo zilienda kwa mshindi wa kwanza ambaye aliweza kutetea ubingwa Mchenga Bball Stars, mshindi wa pili Flying Dribblers na mchezaji bora wa mashindano hayo (MVP) Baraka Sadick kutoka Mchenga Bball Stars.

Wakikabidhiwa zawadi hizo mbele ya uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu (TBF) washindi hao wamewashukuru sana Eatv na Sprite kwa kuleta mashindano hayo ambayo yamekuwa na tija kubwa sana kwa vijana wanaocheza mchezo wa mpira wa kikapu.

Akizungumza kwa niaba ya Mchenga Bball Stars, Nahodha wa timu hiyo Mohamed Yusuph amesema kuwa mashindano hayakuwa rahisi ingawa wamefanikiwa kuchukua ubingwa kwa mara nyingine tena kwani kwa mwama huu ushindano ulikua mkubwa sana.

Yusuph amesema, wanaenda kujiandaa kwa ajili ya michuano inayofuata mwakani na huu hautakuwa mwisho bali wataendelea kujituma kuhakikisha wanafanya vizuri tena.

Kwa upande wa MVP Baraka Sadick amesema kuwa yeye hana maneno mengi sana ila vitendo vyake vinakuwa uwanjani, huu ni mwaka wake wa kwanza kushiriki kwakuwa msimu wa kwanza hakushiriki ila anaamini atakapoendelea kushiriki atajituma vyema ili afanye vizuri zaidi.

Naye Mkuu wa Masoko wa EATV Roy amesema kuwa kwa michuano ya mwaka huu ilikua na ushindani mkubwa sana na amewataka washiriki wajiandae kwani mashindano ya mwakani yatakuwa zaidi huku akiahidi zawadi kutangazwa mapema zaidi.

Roy pia amemuahidi MVP Baraka Sadick kwenda nae katika shule aliyosoma kwa ajili ya kupeleka baadhi ya vitu mbalimbali ili wafaidike na matunda yake na kuwapa hamasa kuwa mchezo wa kikapu unafaida kubwa sana katika kujiendeleza kiuchumi.

MUHAS YATANGAZA KIFO CHA MAREHEMU PROFESA EMIL N. KIKWILU

$
0
0
MAKAMU Mkuu wa Chuo anasikitika kutangaza kifo cha Profesa Emil Namakuka Kikwilu kilichotokea usiku wa tarehe 27/08/2018 maeneo ya Kimara, Dar es Salaam.

Prof. Kikwilu ametumikia Chuo katika nyadhifa mbalimbali kama Mkuu wa Skuli ya Afya ya Kinywa na Meno mwaka 1991 – 1997 na mwaka 2006 – 2009 na pia kama Naibu Mrajisi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Sayansi za Afya Muhimbili mwaka 2002 - 2003. Kabla ya kifo chake marehemu Emil N. Kikwilu alikuwa Profesa katika Idara ya Afya ya Kinywa na Meno kwa Watoto na Jamii (Department of Orthodontics, Paedodontics and Community Dentistry) katika Skuli ya Afya ya Kinywa na Meno.

Mwili wa marehemu Prof. Kikwilu utaagwa na wanajumuia wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi siku ya Alhamisi tarehe 29 Agosti 2018, kuanzia saa nane kamili mchana katika eneo la Chuo kampasi ya Muhimbili. Marehemu anatarajiwa kuzikwa siku ya Ijumaa tarehe 31 Agosti 2018, Kimara mwisho.

Makamu Mkuu wa Chuo pamoja na jumuiya ya MUHAS wanaungana na familia ya marehemu Emil N. Kikwilu katika kuomboleza msiba huu.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina
IMETOLEWA NA:
OFISI YA HABARI NA MAWASILIANO YA UMMA - MUHAS
29/08/2018

MTUHUMIWA WA UHUJUMU UCHUMI SINGH SETHI AIAMBIA MAHAKAMA HAJAONANA NA MKEWE KWA MIEZI SITA SASA

$
0
0

Na Karama Kenyunko,Globu ya jamii

MSHITAKIWA  Harbinder Singh Sethi  anayekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa ana miezi sita sasa hajawahi kuonana na mke wake.

Sethi ameeleza hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi wakati kesi yao ilipokuja kwa kutajwa.

Ameeleza hayo, baada ya Wakili wa Serikali Mwanaamina Kombakono kuieleza Mahakama kuwa kesi ilipangwa kwa ajili ya kutajwa, upelelezi bado haujakamilika na akaomba ipangiwe tarehe nyingine.

Kutokana na maelezo hayo kutoka kwa Kombakono Wakili anayemtetea Sethi,  Dorah Mallaba alidai kuwa bado hawajapata kibali kwa  ajili ya mshtakiwa Sethi kuonwa na mkewe.

Kutokana na hayo, aliiomba Mahakama iruhusu japo kwa dakika tano Sethi aonane na mkewe.

"Naomba Mahakama itumie busara kwa kuwa make wake yupo hapa mahakamani," amesema.

Wakili Kombakono alipinga hoja hiyo ya wakili Mallaba na kueeleza  kuwa  taratibu za kuwaona mahabusu zifuatwe.

Hata hivyo, Hakimu Shahidi amewaeleza upande wa utetezi kuwa taratibu za kuwaona na kuwatunza mahabusu ipo chini ya Magareza hivyo, kama kuna jambo lolote mahususi walete mahakani.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 13 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Katika kesi hiyo Sethi  anashtakiwa pamoja na James   Rugemarila, ambapo  wanakabiliwa na mashtaka  12 ya  uhujumu uchumi  kwa kula njama, kujihusisha mtandao wa uhalifu , kighushi,  kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu,  kutakatisha fedha  na kuisababisha hasara ya USD 22, 198,544.60 na Sh 309,461,300,158.

RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA MADIWANI PAMOJA NA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA CHATO MKOANI GEITA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Madiwani, Viongozi mbalimbali pamoja na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato mkoani Geita. Wengine katika picha ni Mkuu wa Wilaya ya Chato Eng. Mtemi Msafiri Semeon(kushoto) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chato Eliud Mwaiteleke(kulia).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato mara baada ya kumaliza mkutano huo na Madiwani, Viongozi mbalimbali pamoja na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato. Wengine katika picha ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato Christian Manunga wapili kutoka (kulia) mstari wa kwanza mbele, Mkuu wa Wilaya ya Chato Eng. Mtemi Msafiri Semeon watatu kutoka (kulia), Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani, wanne kutoka (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chato Eliud Mwaiteleke.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono Madiwani pamoja na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato wakatika akiondoka katika Ofisi za Halmashauri hiyo Chato mkoani Geita.
Baadhi ya Watumishi wa halmashauri ya Wilaya ya Chato wakifatilia kwa makini wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akizungumza masuala mbalimbali katika ukumbi wa Halmashauri hiyo Chato mkoani Geita. 
PICHA NA IKULU

FM ACADEMIA KUTOA BURUDANI SEPTEMBA 1 KATIKA UKUMBI WA FILOMENA MKOANI KILIMANJARO

$
0
0
Na Woinde Shizza, Kilimanjaro
BENDI ya FM Academia ya jijini Dar es Salam imeahidi kutoa burudani ya nguvu Septemba moja katika ukumbi wa Filomena Klabu uliopo Hai mkoani kilimanjaro.

Akizungumza na waandishi wa habari Kiongozi wa bendi hiyo Pacho Mwamba amesema bendi hiyo ikiwa chini yake itaangusha burudani ya nguvu katika usiku wa  kuazimisha miaka minne  ya tangu kuanzishwa kwa Bendi ya Filomena Pamoja na ukumbi wa sherehe na klabu ya Filomena tangu ianzishwe. 

Amefafanua kuwa wamejipanga vizuri kwa ajili ya kuwapa burudani wakazi wa moshi Pamoja na vitongoji vyao huku wakibainisha kuwa siku hiyo watatumia pia kuwatambulisha wimbo wao wa Rivasi nakuwaonyesha wakazi wa kilimanjaro na vitongoji vyake jinsi unavyochezwa. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Filomena band na klabu Swaumu Kileo amewaambia waandishi wa habari kuwa onesho hilo litafanyika Septemba 1.

Amesema mbali na FM Academia kutoa burudani siku hiyo  pia kutakuwa na burudani zingine za aina mbalimbali zitakazo tangulia kabla ya bendi ya nyumbani pamoja na Fm Academia kupanda jukwaani majira ya sa a mbili usiku. Amesema kama ilivyo kawaida ya Filomena kuwapa burudani watu wa mkoani kilimanjaro, hivyo hivyo wataendelea kuwapa burudani wananchi wote ikiwa ni desturi yao

Saumu ametaja viingilio vya siku hiyo kuwa kwa viti maalumu(V.I.P)ni Sh.10, 000 na kawaida huku kawaida ikiwa ni Sh. 7000 tu.

Ametoa rai kwa wananchi wa mkoa huo na mikoa jirani kufika siku hiyo kwani kuna mambo mazuri wameyaandaa kwa ajili yao na kubwa zaidi ni siku ambayo wanasheherekea miaka minne tangu ilipoanzishwa bendi na klabu ya Filomena.
Baadhi ya Wacheza shoo wa bendi hiyo 

YANGA YAREJEA NCHINI, YAJIANDAA NA MIKAKATI YA UBINGWA

$
0
0
Kikosi cha Yanga.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
UONGOZI wa Klabu ya Yanga umesema kuwa wana mikakati ua kuhakikisha wanafanya vizuri katika michezo ya ligi kuu ili kuweza kupata nafasi ya kucheza tena michuano ya Kimataifa kwa kuchukua ubingwa msimu huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JKNIA Mwenyekiti wa Mashindano Hussein Nyika amesema kuwa kwa wamejiwekea mikakati mipya ya kuweza kuona wanafanya vizuri ikiwemo kupata ushindi katika kila mchezo ili wapata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa.

Nyika amesema kuwa ratiba yao ilikuwa ni kucheza na Mwadui ila kwa kuwa ratiba ya ligi imesimama  wanasubiri maamuzi ya mwalimu kuona wanaendelea na mazoezi ambapo wachezaji walioitwa na timu ya Taifa watajumuika kambini ila hawa ambao hawajaitwa watapewa mapumziko ya siku moja.

Amesema kuwa, baada ya kuhairishwa kwa mechi yao hiyo dhidi ya Mwadui kulikuwa na ratiba ya mechi ya kirafiki dhidi ya Singida United uliokuwa ufanyike mkoani Kigoma ila mpaka sasa hawajapata maamuzi ya mwalimu.

Nyika amesema kuwa hawajarejea na Kocha Mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera kwasababu amekuwa na majukumu ya kitaifa akiwa kama Kocha msaidizi wa timu ya taifa ya DRC na atarejea pindi pale atakapokamilisha majukumu yake.

Akijibu swali huku mchezaji Feisal Salum kuondolewa katika timu ya Taifa, Nyika amesema kuwa yeye ndo amerejea nchini kwa sasa na hajapata taarifa hizo hawezi kujibu lolote na kusema hawezi kufanya kazi kwa kusoma kwenye mitandao ya kijamii.

Yanga imerejea nchini Leo baada ya kukamilisha ratiba ya Kombe la Shirikisho katika hatua ya makundi baada ya kufungwa goli 1-0 dhidi ya Rayon Sports ya nchini Rwanda na kushika nafasi ya mwisho wakiwa na alama 4 huku Rayon na USM Alger wakifanikiwa kutinga hatua ya robo  fainali.

RAIS MAGUFULI ATOA MSIMAMO MAKONTENA YA RC MAKONDA DAR

$
0
0

*Ataka yalipiwe kodi kwa mujibu wa sharia, aonya 
*Asema sheria za kodi ni mtu mmoja tu ndio amepewa dhamana 
*Abaini ujanja ujanja, ataka wafanyakazi wasitumike 



Na Said Mwishehe,Globu ya jamii 
RAIS Dk.John Magufuli ameamua kuvunja ukimya kwa kuamua kuzungumzia suala la makontena ambayo yameletwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda. 

Amesema makontena hayo lazima yalipwe kodi na kuwataka viongozi wa ngazi zote kokote walipo kuhakikisha wanajenga utamaduni wa kuwatumikia Watanzania na si kufanya kazi kwa kuwatumikia watu fulani. 

Rais Dk.Magufuli akizungumza leo mkoani Chato ameamua kuzungumzia suala hilo la makontena ya Makonda na ambapo amesema eti kuna Mkuu wa Mkoa(hakumtaja jina) ameleta makontena na ameambiwa alipe kodi na kuhoji kwanini asilipe kodi. 

Amesema kuwa katika sharia za nchi ni kwamba sharia namba 30 ya mwaka 1974 ya sharia ya fedha, sharia ya madeni na misaada ni mtu mmoja tu ndio anahusika na masuala ya msamaha. 

“Kupitia sharia namba 30 ya mwaka 1974 nafikiri kifungu cha 3, 4 na 5 ndio kinatoa mamlaka kwa anayehusika katika hilo na hakuna mtu mwingine yeyote,”amefafanua. 

Rais Dk.Magufuli amesema “Sasa ukichukua makontena kule, umezungumza na watu wengine labda wafanyabiashara unasema una makontena yako.Halafu unasema ni ya walimu wakati hata shule hazitajwi 

“Maana yake unataka kuchukua machache na kisha uyapeleke kwenye shule mbili au tatu na yaliyobakia ufanye biashara kwa kuyapeleka kwenye ‘Shoping Mall’, kwani walimu wamesema wanataka masofa wakalale?. 

Kabla ya kauli ya Rais Magufuli ambayo ameitoa leo mkoani Chato, Jumatatu ya wiki hii Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Philip Mpango alishatoa msimamo wake kwamba lazima makontena hayo yalipiwe kodi na ikishindikana yapigwe mnada. 



Dk.Mpango akaenda mbali zaidi kwa kusema anashangazwa na namna ambavyo jambo hilo linazungumzwa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii lakini amekaa kimya kwasababu hana tabia ya kuzozana. 

Dk.Mpango alisema kuwa lazima sharia ichukue mkondo wake na yeye amepewa dhamana ya kusimamia. Akatoa tahadhari kwa viongozi kuwa makini na kauli zao. 

Alisema inashangaza kusikia Mkuu wa Mkoa akisema atakayenunua samani zilizopo kwenye makontena hayo atapata laana ambapo akafafanua hakuna laana yeyoye na kuwataka watu wayanunue baada ya TRA kutangaza mnada. 

Wakati Makonda anazungumzia Makontena akiwa kanisani wilayani Ngara mkoani Kagera aliamua kuelezea namna ambavyo baadhi ya watu wanakwamisha kutolewa kwa makontena hayo na kwenye orodha hiyo na alimtaja Waziri wa Fedha. 

Makonda akasema kuwa watakaonunua makontena hayo watapaata lakini huku akieleza wazi iwapo wataendelea kukwamisha atamwambia Rais. 

MICHUZI TV: KAULI YA RAIS MAGUFULI KUFUATIA SAKATA LA MAKONTENA YA RC MAKONDA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Madiwani, Viongozi mbalimbali pamoja na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato mkoani Geita. Wengine katika picha ni Mkuu wa Wilaya ya Chato Eng. Mtemi Msafiri Semeon(kushoto) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chato Eliud Mwaiteleke(kulia).


WAZIRI LUGOLA MGENI RASMI MKUTANO MKUU WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI, JIJINI DODOMA.

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akimsalimia Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhan Kailima, wakati Waziri huyo alipokua anawasili katika Ukumbi wa Mikutano wa Polisi, jijini Dodoma leo kwa akili ya kufungua kikao kazi cha Makamanda wa Jeshi hilo. Wakati Makamanda hao wanajitambulisha, Lugola aliwafukuza kikaoni robo tatu ya makamanda hao kwa kutamka Jeshi la Zimamoto pekee bila kumalizia neno naUokoaji. Hata hivyo, makamanda hao baadaye waliruhusiwa kuingia ukumbini kuendelea na kikao. Kulia ni Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, (CGF) Thobias Andengenye, na wapili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma,  Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhan Kailima, na wapili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi.

 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CGF) Thobias Andengenye, akizungumza na Makamanda wa Jeshi lake katika kikao kazi kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Polisi, jijini Dodoma leo. Mgeni rasmi katika ufunguzi wa kikao hicho ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (watatu kulia). Katika kikao hicho, Lugola aliwafukuza kikaoni robo tatu ya makamanda waliohudhuria kikao hicho kwa kutamka Jeshi la Zimamoto pekee bila kumalizia neno Uokoaji, hata hivyo baadaye aliwaruhusu kuendelea na kikao hicho.
.

 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CGF) Thobias Andengenye, akizungumza na Makamanda wa Jeshi lake katika kikao kazi kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Polisi, jijini Dodoma leo. Mgeni rasmi katika ufunguzi wa kikao hicho ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (watatu kulia). Katika kikao hicho, Lugola aliwafukuza kikaoni robo tatu ya makamanda waliohudhuria kikao hicho kwa kutamka Jeshi la Zimamoto pekee bila kumalizia neno naUokoaji, hata baadaye aliwaruhusu kuendelea na kikao hicho
 Sehemu ya Makamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji waliofukuzwa kikaoni na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (hayupo pichani), katika Kikao Kazi cha Jeshi hilo kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Polisi, jijini Dodoma leo. Lugola aliwafukuza kikaoni robo tatu ya makamanda hao waliohudhuria kikao hicho kwa kutamka Jeshi la Zimamoto pekee bila kumalizia neno naUokoaji.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na Makamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika Kikao Kazi chao kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Polisi, jijini Dodoma leo. Lugola aliwafukuza kikaoni robo tatu ya makamanda waliohudhuria kikao hicho kwa kutamka Jeshi la Zimamoto pekee bila kumalizia neno naUokoaji.

Rais Magufuli kufanya ziara ya kikazi katika mikoa ya Mwanza, Mara na Simiyu

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Description: Description: Description: Description: Description: Coat of Arms
Simu: 255-22-2114512, 2116898
Baruapepe: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz              

Nukushi: 255-22-2113425


OFISI YA RAIS,
     IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,   
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, atafanya ziara ya kikazi katika mikoa ya Mwanza, Mara na Simiyu kati ya tarehe 03 Septemba, 2018 na tarehe 10 Septemba, 2018.
Katika ziara hiyo Mhe. Rais Magufuli ataweka mawe ya msingi na kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo, pamoja na kuzungumza na wananchi katika mikutano ya hadhara.
Taarifa zaidi kuhusu ziara ya Mhe. Rais Magufuli katika mikoa husika zitatolewa na viongozi wa mikoa hiyo.
Aidha, baada ya kumaliza ziara katika mikoa hiyo Mhe. Rais Magufuli anatarajia kufanya ziara katika mikoa ya Katavi, Rukwa, Songwe na Mbeya katika tarehe zitakazopangwa.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Chato, Geita

30 Agosti, 2018

JAJI MKUU PROFESA IBRAHIM JUMA AWAASA WANASHERIA KUZINGATIA MISINGI YA TAALUMA Na. Idara ya Habari-MAELEZO

$
0
0
Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma, amewaasa wanasheria walio kwenye utumishi wa umma kuzingatia misingi ya taaluma wakati wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku. 
Kauli hiyo ameitoa wakati akifungua mkutano wa pili wa wanasheria walio kwenye utumishi wa umma unaofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Mipango, jijini Dodoma. 
“Mkiwa maafisa wa Mahakama tunawatazamia kufanya kazi zenu kwa kuzingatia misingi ya taaluma iliyowekwa kwa kuzingatia maadili, weledi, uwazi na usiri” alisisitiza Profesa Juma.
 Profesa Juma pia amewakumbusha wanasheria hao walio kwenye utumishi wa umma kuhakikisha kuwa sheria wanazosimamia zinalenga kuleta ustawi wa wananchi wanyonge na kuiwezesha serikali kutimiza azma yake ya kifanya Tanzania iweze kufikia hadhi ya nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025. 
 Vilevile, wanasheria hao wa serikali wameaswa kuzingatia matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika kutekeleza majukumu yao ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya karne ya 21. 
 Aliongeza kuwa, wanasheria wanalo jukumu kubwa la kukidhi matarajio ya wananchi ikiwemo Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025, amani, usalama, umoja, utawala bora, na kujenga uchumi imara. Kabla ya Jaji Mkuu Profesa Juma, kuhutubia mkutano huo Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palagamba Kabudi alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kufanya mabadiliko katika muundo wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambao unategemewa kuleta ufanisi. 
Kwenye mabadiliko hayo yaliyoidhinishwa na Rais Magufuli, yamesababisha kuanzishwa kwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Wakili Mkuu wa Serikali. 
 Mkutano huo wa siku mbili unawakutanisha wanasheria zaidi ya mia tisa kutoka Wizara, Serikali za mitaa, Mashirika, Wakala na Idara mbalimbali za Serikali.
 Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma (pili kulia), Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi (pili kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge (kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Profesa Sifuni Mchome wakiimba wimbo wa taifa kabla ya kuanza mkutano wa pili wa wanasheria walio kwenye utumishi wa umma unaofanyika Chuo cha Mipango, jijini Dodoma.
 Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma, akiwahutubia washiriki wa mkutano wa pili wa wanasheria walio kwenye utumishi wa umma (hawako pichani). Kwenye hotuba yake Profesa Juma amewaasa wanasheria walio kwenye utumishi wa umma kuzingatia misingi wa maadili kwenye utekelezaji wa majukumu yao.
 Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi, akitoa neno la utangulizi mbele ya wanasheria waliohudhuria mkutano wa pili wa wanasheria wa walio kwenye utumishi wa umma.
Wanasheria kutoka Wizara, Serikali za Mitaa, Mashirika, Wakala na Idara  za Serikali wakifuatilia kwa makini hotuba ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibarhim Juma, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa pili wa wanasheria walio kwenye utumishi wa umma.
 Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma (pili kulia), Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi (pili kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge (kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Profesa Sifuni Mchome kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali waliohudhuria ufunguzi wa mkutano wa pili wa wanasheria walio kwenye utumishi wa umma. Mkutano huo wa siku mbili unafanyika jiji Dodoma, ukumbi wa mikutano Chuo cha Mipango.  

MAKAMPUNI YA ULINZI YATAKIWA KUACHA KUTUMIA MAGARI YAO YA DHARURA VIBAYA.

$
0
0
Na Gasto Kwirini wa Polisi Arusha
Jeshi la Polisi Mkoani hapa limeyaonya baadhi ya Makampuni ya Ulinzi kuacha tabia ya kutumia magari yao ya dharura vibaya kinyume na utaratibu pindi wawapo barabarani.
Hayo yamesemwa leo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng’anzi wakati akiwakaribisha ofisini kwake  Viongozi wapya wa Makampuni ya Ulinzi Mkoa wa Arusha waliochaguliwa tarehe 11 Agosti mwaka huu katika Ukumbi wa Maofisa wa Polisi Arusha.
“Kuna baadhi ya Magari ya Makampuni ya Ulinzi yanatumiwa vibaya kwa kigezo cha kuwahi dharura japokuwa wakati mwingine huko waendako hakuna hiyo dharura inayowataka wafanye hivyo. Lakini pia pale kwenye ulazima msitumie magari hayo ya  dharura kwa kubeba vitu haramu  kama vile bhangi”. Alionya kamanda Ng’anzi.
Aidha aliwahakikishia kufuatilia na kuzifanyia kazi changamoto zao hasa za ucheleweshwaji wa utolewaji wa vibali vya umiliki wa silaha, ucheleweshwaji wa utolewaji wa matokeo ya alama za Vidole kwa Askari wapya wanaoajiriwa. Ameyataka Makampuni yenye changamoto hizo kuorodhesha majina yao kupitia viongozi hao, na kuyapeleka ofisini kwake ili aweze kuyafanyia kazi kwa kushirikiana na idara husika na matokeo ya Alama hizo na Vibali hivyo viweze kutolewa haraka na kwa wakati.
Mwenyekiti wa Makampuni ya Ulinzi aliambatana na Viongozi wenzake ambao ni Makamu Mwenyekiti Bwana James Rugangila, Bi. Malima Macha ambaye ni  Katibu, Naibu katibu Bwana James Babu na Mjumbe mmoja Bwana Rashid Mtungi.
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng’anzi akiwa akiwa katika kikao na Viongozi wa Makampuni ya Ulinzi Mkoa wa Arusha waliofika Ofisini kwake kwa ajili ya kujitambulisha
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng’anzi akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa makampuni ya ulinzi mkoa wa Arusha pamoja na Baadhi ya Maofisa wa Polisi mkoani humo.

Mkutano wa Kamati ya Ufundi ya Makamishna wa Upelelezi wa Kodi wa Mamlaka za Mapato Afrika Mashariki

$
0
0
Na Oliver Njunwa, Zanzibar
Wapelelezi wa Kodi wa Mamlaka za Mapato Afrika Mashariki wametakiwa kuharakisha mchakato wa kuandaa mtaala wa kuwajengea uwezo wapelelezi wa kodi pamoja na mfumo wa kisheria ili kuweza kushirikiana katika kupambana na uhalifu katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Wito huo umetolewa na Kaimu Naibu Kamishna wa Upelelezi wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Salim Kessi wakati akifungua Mkutano wa Wajumbe wa Kamati ya Ufundi ya Makamishna wa Upelelezi wa Kodi wa Mamlaka za Mapato Afrika Mashariki unaofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu Zanzibar.
“Tunataka mchakato huu umalizike mapema ili tuweze kupambana na uhalifu katika ukusanyaji wa kodi kwani kadri tunavyochelewa ndivyo na wahalifu wanaendelea kusababisha upotevu wa kodi kwa mamlaka zetu za mapato”, alisema Bw. Kessi.
Aliongeza kwamba kwa siku nne ambazo watakuwa Zanzibar wanatakiwa kukamilisha hiyo kazi ili iweze kuwasilishwa katika kikao cha Makamishna wa Upelelezi wa Kodi Afrika Mashariki ambao walikubaliana kushirikiana kufanya upelelezi wa kodi kwa pamoja kupampana na kudhibiti uhalifu katika masuala ya kodi.
Aidha aliwapongeza wajumbe wa kamati hiyo ya ufundi kwa jitihada zao ambazo zimewezesha kuundwa kwa chombo cha uendeshaji ambacho kitasaidia ubadilishanaji wa taarifa na upepelelezi wa pamoja katika ukanda wa Afrika Mashariki.
“Ni kutokana na jitihada hizo sasa tayari tuna rasimu ya mkataba wa huduma ambayo itatoa uhalali wa operesheni katika kubadilishana taarifa na upepelezi wa pamoja”, alisisitiza Bw. Kessi na kuongeza kwamba pia kuwepo kwa mwongozo wa upelelezi wa pamoja na kanuni za maadili ni jambo la kujivunia.
Mkutano huo unahudhuriwa na wapelezi wa kodi kutoka Mamlaka za Mapato za Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi na Tanzania ambao ni wajumbe wa Kamati ya Ufundi ya Makamishna wa Upelelezi wa Mamlaka za Mapato Kodi Afrika Mashariki.
Kaimu Naibu Kamishna huyo wa Upelelzi wa Kodi aliwaambia wajumbe hao kwamba ishara ya kwamba mwelekeo wa kushirikiana katika upelelzi ni mzuri inaonekana hata kama chombo cha kisheria hakijakamilika kwani tayari wamebadilishana taarifa za Himaya ya Pamoja ya Forodha na kufanya usuluhishi katika jumuiya.
Naye Meneja wa Upelelezi wa Mamlaka ya Mapato Kenya (KRA) Jonah Ogalo amesema kwamba mkutano huo ni muhimu kwa nchi za Afrika Mashariki katika kuweka mikakati ya pamoja kukabiliana na uhalifu katika ukusanyaji wa kodi na kuongeza kwamba kukamilika kwa mtaala wa mafunzo kwa wapelelezi wa kodi kutawasaidia kushirikiana na kubadilishana taarifa za kiintelijensia na hivyo kuokoa mapato ya serikali.
Kamati ya Ufundi ya wapelelezi wa kodi inatarajiwa kutoa mtaala wa pamoja wa mafunzo ya kuwaongezea ujuzi wapelelezi wa Kodi pamoja na kuunda mfumo wa pamoja wa kisheria utakao wawezesha kufanya upelelezi kwa pamoja kutokana na kila nchi kuwa na sheria zake isipokuwa katika masuala ya Forodha ambapo nchi za Afrika Mashiriki zinatekeleza sheria moja ya Usimamizi wa Forodha.

Kaimu Naibu Kamishna wa Upelelezi wa Kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Salim Kessi akisisitiza jambo wakati akifungua mkutano wa Kamati ya wapelelezi wa Kodi Afrika Mashariki.
Wajumbe wa Kamati ya wapelelezi wa kodi wakifuatilia kwa makini hotuba ya Kaimu Naibu Kamishna wa Upelelezi wa Kodi TRA Salim Kessi (hayupo katika picha) wakati akifungua rasmi mkutano.
Wajumbe wa Mkutano wa Kamati ya Wapelelezi wa Kodi Afrika Mashariki katika picha ya Pamoja na Kaimu Naibu Kamishna wa Upelelezi wa Kodi TRA Salim Kessi (katikati walioketi) mara baada ya ufunguzi wa mkutano katika ukumbi wa Benki Kuu Zanzibar. 

DC MPYA BAGAMOYO AFUNGUA RASMI MAFUNZO YA AWALI JESHI LA AKIBA KWA VIJANA 183 CHALINZE

$
0
0
VICTOR MASANGU,  CHALINZE.

MKUU mpya wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa amewataka vijana ambao wanahitimu  mafunzo ya jeshi la akiba  kuhakikisha wanakuwa wazalendo na nchi yao na kuachana kabisa na vitendo vya kujiingiza katika matukio ya kihalifu na badala yake wahakikishe wanazingatia sheria na taratibu zote zilizowekwa  kwa lengo la kuweza kulinda hali ya ulinzi na usalama wa wananchi na mali zao.

Kauli hiyo aliitoa wakati wa sherehe za ufunguzi rasmi wa mafunzo  ya awali ya  jeshi la akiba ambayo yamefanyika katika kata ya Bwilingu  na kuwajumusiha vipana wapatao 183 kutoka  katika halmashauri ya Chalinze Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani.

Mkuu huyo pia aliwahimiza vijana hao kuhakikisha wanakuwa na nidhamu ya hali ya juu katika kipindi chote cha mafunzo hayo ya kijeshi na kuzingatia maelekezo ambayo wanapatiwa na walimu wao kwa lengo la kuweza kujifunza   mbinu mbali mbali ambazo zitaweza kuwa ni mkombozi mkubwa katika kulilinda Taifa la Tanzania na kuweza kukabiliana na wimbi la matukio ya uhalifu.

“Napenda kuchukua fursa hii  kuwapongeza vijana ambao mmeweza kujitokeza katika mafunzo haya ya jeshi la akiba,lakini kitu kikukbwa ninawaomba muwe wazalendo na nchi yenu kwa kuhakikisha mnazingatia sheria na taratibu za nchi ikiwa ni sambamba na kuyatumia vizuri mafunzo mliyopatiwa kwa maslahi ya nchi na sio vinginevyo,”alisema
Mkuu mpya wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Rashid Kawawa kulia akiwa na  Mshauri wa jeshi la akiba wilayani humo wa kushoto Maj Chinguku wakati wa sherehe za ufunguzi rasmi wa mafunzo wa jeshi la akiba kwa vijana wapatao 183  ambayo yamefanyika katika  kata ya Bwilingu halmashauri ya Chalinze.
  Mkuu mpya wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa wa kati kati akirukaruka mara baada ya kufungua mafunzo rasmi ya jeshi la akiba kwa vijana wapatao 183 hawapo pichani  kutoka kata ya  Bwilingu katika halmashauri ya Chalinze pembeni yake kulia ni Mshauri wa jeshi la akiba Wilayani Bagamoyo Maj Chinguku.
Mkuu mpya wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa wa kati kati akirukaruka mara baada ya kufungua mafunzo rasmi ya jeshi la akiba kwa vijana wapatao 183 hawapo pichani  kutoka kata ya  Bwilingu katika halmashauri ya Chalinze pembeni yake kulia ni Mshauri wa jeshi la akiba Wilayani Bagamoyo Maj Chinguku.

SUPER D BOXING PROMOTION INAWALETEA MPAMBANO MKALI SEPTEMBA 15, 2018


BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI 30.08.2018

MKUU WA WILAYA YA BAGAMOYO ZAINABU KAWAWA AFUNGUA RASMI WA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA KWA VIJANA 183

$
0
0
MKUU wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Zainabu Kawawa amewataka vijana ambao wanahitimu mafunzo ya jeshi la akiba kuhakikisha wanakuwa wazalendo na nchi yao na kuachana kabisa na vitendo vya kujiingiza katika matukio ya kihalifu na badala yake wahakikishe wanazingatia sheria na taratibu zote zilizowekwa kwa lengo la kuweza kulinda hali ya ulinzi na usalama wa wananchi na mali zao. 
 Kauli hiyo ameitoa wakati wa sherehe za ufunguzi rasmi wa mafunzo ya awali ya jeshi la akiba ambayo yamefanyika katika kata ya Bwilingu na kuwajumusiha vipana wapatao 183 kutoka katika halmashauri ya Chalinze Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani. 
 Mkuu huyo pia amewahimiza vijana hao kuhakikisha wanakuwa na nidhamu ya hali ya juu katika kipindi chote cha mafunzo hayo ya kijeshi na kuzingatia maelekezo ambayo wanapatiwa na walimu wao kwa lengo la kuweza kujifunza mbinu mbali mbali ambazo zitaweza kuwa ni mkombozi mkubwa katika kulilinda Taifa la Tanzania na kuweza kukabiliana na wimbi la matukio ya uhalifu.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuomgoza ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya Afrika na China (FOCAC) mjini Beijing

$
0
0
Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya Afrika na China (FOCAC) utafanyika Beijing kuanzia tarehe 01 hadi 04 Septemba, 2018.

Ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano huo utaongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa. Viongozi wengine watakaoshiriki Mkutano huo ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga; Mhe. Khalid Salum Mohamed, Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mhe. Rashid Ali Juma, Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, na Viongozi wengine Waandamizi.

Mkutano huo utafunguliwa na Rais wa China, Mhe. Xi Jinping ambaye pia ni Mwenyekiti wa jukwaa hilo, kwa kushirikiana na Mwenyekiti Mwenza, Rais wa Afrika Kusini, Mhe. Matamela Cyril Ramaphosa, utahudhuriwa pia na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika ambaye pia ni Rais wa Rwanda, Mhe. Paul Kagame, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. Antonio Guterres na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Afrika ambaye pia ni Rais wa Chad, Mhe. Moussa Faki Mahamat. Mkutano huo pia utashuhudia uchaguzi wa Mwenyekiti Mwenza mpya kutoka Afrika.

Kaulimbiu ya Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika kwa mwaka 2018 ni “China na Afrika: Kuelekea Jumuiya Imara kwa mustakabali wa wote kupitia ushirikiano kwa manufaa ya wote” (China and Africa: Toward an Even Stronger Community with a Shared Future through Win-Win Co-operation).

Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali utatanguliwa na kikao cha Makatibu Wakuu kitakachofanyika tarehe 01 Septemba, 2018. Kikao hicho pamoja na mambo mengine kitapitia agenda za mkutano huo na kuziwasilisha kwenye kikao cha Mawaziri kitakachofanyika tarehe 02 Septemba, 2018.

Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati Afrika na China pamoja na mambo mengine utajadili namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Afrika na China na kufanya mapitio ya mikakati ya pamoja ya maendeleo iliyopo kati ya Afrika na China. Jukwaa hilo ambalo lilianzishwa mwaka 2000 huwaleta pamoja viongozi wa Afrika na China kujadili masuala ya ushirikiano na maendeleo na kutathmini utekelezaji wa makubaliano mbalimbali yanayofikiwa kati yao.

Aidha, masuala ya ushirikiano katika uendelezaji Miundombinu kama Barabara, Reli, Bandari na upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa Bara la Afrika yatajadiliwa kwa kina. Agenda nyingine itahusu kilimo cha kisasa ambapo China itatoa uzoefu wake katika kutumia sayansi na ubunifu wa kiteknolojia katika kufikia uzalishaji wenye tija na kuongeza thamani kwa mazao ili kuwa na soko la uhakika.

FOCAC 2018 pia itajadili masuala ya biashara na uwekezaji ambapo kwa kuona umuhimu huo, Mhe. Xi Jinping, Rais wa China atafungua rasmi Mkutano wa Jukwaa la Biashara kati ya China na Afrika utakaofanyika tarehe 03 Septemba, 2018.

Mkutano wa kwanza wa Wakuu wa Nchi wa Jukwaa hili ulifanyika Beijing mwaka 2006 na Mkutano wa Pili ulifanyika nchini nchini Afrika Kusini mwaka 2015.

Wakati wa Mkutano wa pili, China ilitangaza mpango kabambe wa kuhamasisha mapinduzi ya viwanda na kilimo cha kisasa kwa Afrika wenye gharama ya Dola za Marekani bilioni 60 katika utekelezaji wake. Kufuatia ushirikiano kupitia Jukwaa hilo biashara kati ya China na Afrika imeongezeka pamoja na ongezeko la ushirikiano wa kiutamaduni na biashara baina ya watu wa China na Afrika.

Pembezoni mwa Mkutano huo, Tanzania na China zimeandaa Kongamano la Biashara ambalo litafunguliwa rasmi na Mhe. Waziri Mkuu tarehe 02 Septemba, 2018. Kongamano hilo ambalo litajadili kwa kina masuala ya uwekezaji na biashara kati ya Tanzania na China litashirikisha takribani makampuni 80 kutoka nchi hizi mbili.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dodoma.

30 Agosti 2018

MGOMBEA MMOJA WA UDIWANI AENGULIWA, SABA WANUSURIKA

$
0
0
Na Idara ya Habari-NEC 
 Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imefanya uamuzi wa rufaa nane za wagombea udiwani wa kata saba zinazoshiriki uchaguzi mdogo na kukubali rufaa ya kumuengua mgombea mmoja wa kata ya Sisimba katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya. 
 Akitoa taarifa ya uamuzi wa rufaa hizo jijini Dar es Salaam leo (Agosti, 30) Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dkt. Athumani Kihamia amesema mbali na kumuengua mgombea huyo, Tume imeamua kuwa wagombea saba (7) wataendelea na uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Septemba 16. 
 Mbali na uamuzi wa rufaa hizo, Dkt. Kihamia amevikumbusha vyama vya siasa na wagombea wanaoshiriki katika uchaguzi huo, kuzingatia Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015, wakati wote wa kampeni na hata siku ya uchaguzi.
 Dkt. Kihamia alifafanua kuwa uamuzi wa rufaa hizo umezingatia matakwa ya kanuni ya 29(3), (4) na (5) ya Kanuni za Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Uchaguzi wa Madiwani) za mwaka 2015. 
 “Tume, ilipokea, ilijadili na kufanya maamuzi ya Rufaa hizo nane (8) ambazo kati ya hizo rufaa, mbili (2) zilipinga kuondolewa kugombea na kutaka kurejeshwa kugombea na rufaa sita (6) zilikuwa zikipinga wagombea walioteuliwa”, alisema Dkt. Kihamia na kuongeza kuwa: “Tume imeamua kuwa wagombea saba (7) wataendelea na uchaguzi na mgombea mmoja ameenguliwa na hivyo kutoendelea kuwa mgombea.
Taarifa za maamuzi ya rufaa hizo, zimetumwa kwa wahusika kupitia kwa Wasimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri husika”. 
 Aliongeza kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilipokea rufaa nane (8) kutoka kwa wagombea udiwani wa Kata za Sisimba, Maanga, Nsalaga na Iwambi katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya. Alisema wagombea wengine walitoka Kata ya Nkuyu katika Halmashauri ya Wilaya ya Kyela; Kata ya Kizota katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma na Kata ya Mwanhuzi katika Halmashauri ya Wilaya ya Meatu.

MICHUZI TV: UHAMIAJI MBEYA YAZINDUWA PASIPOTI MPYA ZA KIEREKTRONIKI.

Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images