Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109606 articles
Browse latest View live

HAFLA MAALUM YA BUNGE KUCHANGIA ELIMU KWA MTOTO WA KIKE

0
0
Waweza kuchangia kiasi chochote kwa ajili ya kuboresha mazingira ya mtoto wa kike nchini kupitia:
Acc. NMB 50510007935 National Assembly Fund

Simu: 
0677055807
0738787755
0755019111

DC MPYA BAGAMOYO AFUNGUA RASMI MAFUNZO YA AWALI JESHI LA AKIBA KWA VIJANA 183 CHALINZE

0
0
VICTOR MASANGU,  CHALINZE.

MKUU mpya wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa amewataka vijana ambao wanahitimu  mafunzo ya jeshi la akiba  kuhakikisha wanakuwa wazalendo na nchi yao na kuachana kabisa na vitendo vya kujiingiza katika matukio ya kihalifu na badala yake wahakikishe wanazingatia sheria na taratibu zote zilizowekwa  kwa lengo la kuweza kulinda hali ya ulinzi na usalama wa wananchi na mali zao.

Kauli hiyo aliitoa wakati wa sherehe za ufunguzi rasmi wa mafunzo  ya awali ya  jeshi la akiba ambayo yamefanyika katika kata ya Bwilingu  na kuwajumusiha vipana wapatao 183 kutoka  katika halmashauri ya Chalinze Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani.

Mkuu huyo pia aliwahimiza vijana hao kuhakikisha wanakuwa na nidhamu ya hali ya juu katika kipindi chote cha mafunzo hayo ya kijeshi na kuzingatia maelekezo ambayo wanapatiwa na walimu wao kwa lengo la kuweza kujifunza   mbinu mbali mbali ambazo zitaweza kuwa ni mkombozi mkubwa katika kulilinda Taifa la Tanzania na kuweza kukabiliana na wimbi la matukio ya uhalifu.

“Napenda kuchukua fursa hii  kuwapongeza vijana ambao mmeweza kujitokeza katika mafunzo haya ya jeshi la akiba,lakini kitu kikukbwa ninawaomba muwe wazalendo na nchi yenu kwa kuhakikisha mnazingatia sheria na taratibu za nchi ikiwa ni sambamba na kuyatumia vizuri mafunzo mliyopatiwa kwa maslahi ya nchi na sio vinginevyo,”alisema
Mkuu mpya wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Rashid Kawawa kulia akiwa na  Mshauri wa jeshi la akiba wilayani humo wa kushoto Maj Chinguku wakati wa sherehe za ufunguzi rasmi wa mafunzo wa jeshi la akiba kwa vijana wapatao 183  ambayo yamefanyika katika  kata ya Bwilingu halmashauri ya Chalinze.
  Mkuu mpya wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa wa kati kati akirukaruka mara baada ya kufungua mafunzo rasmi ya jeshi la akiba kwa vijana wapatao 183 hawapo pichani  kutoka kata ya  Bwilingu katika halmashauri ya Chalinze pembeni yake kulia ni Mshauri wa jeshi la akiba Wilayani Bagamoyo Maj Chinguku.
Mkuu mpya wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa wa kati kati akirukaruka mara baada ya kufungua mafunzo rasmi ya jeshi la akiba kwa vijana wapatao 183 hawapo pichani  kutoka kata ya  Bwilingu katika halmashauri ya Chalinze pembeni yake kulia ni Mshauri wa jeshi la akiba Wilayani Bagamoyo Maj Chinguku.

JUMAA AWAUNGA MKONO WAKAZI WA MADEGE KATIKA HARAKATI ZA UJENZI WA ZAHANATI

0
0
NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA VIJIJINI
WAKAZI wa kijiji cha Madege, kata ya Dutumi Kibaha Vijijini ,wanakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa zahanati hali inayosababisha kufuata huduma ya afya katika zahanati ya Dutumi ,umbali wa km .5-7.

Aidha wagonjwa wanaohitaji huduma za rufaa kutoka kijiji cha Madege hadi kituo cha afya Mlandizi hutumia km.45 jambo ambalo ni kero kwao.

Katika kukabiliana na changamoto hiyo ,mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini ,Hamoud Jumaa amechangia mifuko ya saruji 80 pamoja na diwani wa kata ya Dutumi Mkali Kanusu amechangia mifuko ya saruji 20 ambayo itasaidia kuanza kwa ujenzi wa zahanati kijijini hapo .

Wakipokea msaada huo ,baadhi ya wakazi hao  akiwemo Nassoro Malolela na Nuru Shaban walisema wanataabika kukodi usafiri wa pikipiki kwa sh.10,000 na baiskeli kwenda zahanati ya Dutumi .

Malolela alisema, kusafiri km.5 kufuata huduma hiyo Dutumi ni umbali mrefu kwakuwa wajawazito wanaokwenda kujifungua na watoto hupata shida hasa wakati wa mvua na nyakati za usiku .

"Fikiria mjamzito ama umeshikwa na uchungu unakaaje kwenye pikipiki au baiskeli ,tunapata shida sana " alisisitiza Nuru .

Nae mganga mfawidhi wa zahanati ya Dutumi Pius Gwade, alisema wagonjwa wanaopata rufaa kutoka kijiji cha Madege hupata shida kuwasafirisha kwakuwa hutoka kijiji km.5-7 kufika Dutumi na kuwatoa Dutumi km.45 kwenda Mlandizi.

Awali diwani Kanusu alisema ,Jumaa aliahidi kupeleka mifuko hiyo ya saruji baada ya kufanya ziara ya kawaida kijiji cha Madege na kufikishiwa kero hiyo.

Akikabidhiwa mifuko hiyo ya saruji ,mwenyekiti wa kijiji cha Madege Iddi Msiga alielezea ,kukamilika kwa ujenzi wa zahanati hiyo itakuwa mkombozi katika kupata huduma za afya.

Alisema ,mkutano wa kijiji umekubaliana kila mkazi kushiriki kuchangia ambapo wameshafikisha sh.400,000 na wanaendelea na michango ili kukamilisha adhma yao.

Wakati huo huo ,Jumaa pia ,alimsaidia Halima Nassoro( 65 ),mabati 20 kwa ajili ya kuezeka nyumba yake ambayo imeezekwa kwa nyasi na kupitisha maji wakati wa mvua .

Halima ,alimshukuru mbunge huyo kwa jitihada zake na kujitolea misaada kwa makundi maalum ikiwemo wazee.
 Bibi Halima Nasorro (65) mkazi wa Dutumi akikabidhiwa mabati 20 kutoka kwa mbunge wa Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa wilayani Kibaha leo.
Mbunge wa Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa wilayani Kibaha leo kikabidhi mifuko ya saruji kwa niaba ya mbunge wa Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa,diwani wa kata ya Dutumi Mkali Kanusu (kushoto )kwa  Mwenyekiti wa kijiji cha Madege Iddi Msiga (wa pili kulia) na wa kwanza kutoka kulia ni katibu wa mbunge wa Kibaha Vijijini.
Mganga Mfawidhi wa zahanati ya Dutumi ,dokta Pius Gwade akizungumza na waandishi wa habari.

MAHAKAMA JUMUISHI MBEYA KUSOGEZA HUDUMA ZA KIBENKI NDANI YA MAHAKAMA HIYO

0
0

Na Rajabu Singana. Mahakama Kuu Mbeya

Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Mhe. Robert Makaramba amekutana na uongozi wa benki ya NMB na kufanya mazungumzo juu ya uanzishwaji wa huduma za Kibenki katika jengo la Mahakama Kuu Mbeya linalotoa huduma kwa Mahakama Kuu, Mahakama ya Hakimu Mkazi na Mahakama ya Wilaya.

Mhe. Makaramba alikutana na uongozi huo mapema Agosti 28, aliwaeleza viongozi wa NMB kwamba Mahakama ipo katika maboresho makubwa ya huduma zake kupitia mpango mkakati wa miaka mitano (2015-2020) unaolenga kumsogezea mwananchi huduma.

Kutokana na changamoto ya kufanya malipo ambayo wamekuwa wakiipata wananchi Mhe. Makaramba aliwaomba NMB kusogeza huduma zao katika jengo la Mahakama Kuu Mbeya. Akichangia katika mazungumzo hayo, Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Bw. Straton Chilongola alisema kwa sasa Benki ya NMB imekuwa ikifanya kazi kwa kushirikiana na Mawakala ambao hufanya kazi za Kibenki.

Bw. Chilongola aliongeza kwa kusema kwamba watafanya utaratibu wa kuanzisha ‘Cash Collection Point’ kwa ajili ya wananchi kufanya malipo ya Huduma za Mahakama. Meneja wa Wakala wa Benki wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Bw. Respicious Denis aliongeza kuwa kwa sasa benki ya NMB imekuwa ikifanya vizuri kwa kutumia Mawakala kwenye malipo na makusanyo mbalimbali ambapo tayari baadhi ya taasisi za serikali zinatumia huduma hiyo. 

Viongozi wa Mahakama Kanda ya Mbeya (kushoto) wakiwa katika majadiliano na Viongozi wa Benki ya NMB, majadiliano juu ya uanzishwaji wa huduma za kibenki ili kuwarahishia wateja wanaofika katika Mahakama hiyo.Mjumbe kutoka NMB akichangia jambo katika majadiliano. 
Picha ya pamoja baada ya majadiliano, (wa pili kushoto) ni Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya. (Picha na Rajabu Singana, Mahakama Kuu, Mbeya) .

RC TABORA AWAONYA WAVAMIZI WA ARDHI MAENEO YA SERIKALI

0
0


Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akizungumza wakati wa mkutano wa pamoja baina ya wananchi na watendaji wa Serikali mkoa wa Tabora jana.
Mkuu wa Wilaya ya Tabora Komanya Erick Kitwala akizungumza wakati wa mkutano wa pamoja baina ya wananchi na watendaji wa Serikali mkoa wa Tabora jana.
Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Kizigo Kata ya Ng’ambo mkoani Tabora, Bw. Said Thabit Mnwagi akizungumza wakati wa mkutano wa pamoja baina ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (kulia),wananchi na watendaji wa Serikali mkoa wa Tabora jana.Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Komanya Erick Kitwala na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora Joseph Kashushura.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa pamoja baina ya wananchi na watendaji wa Serikali mkoa wa Tabora wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri wakati wa mkutano huo uliofanyika katika ukubi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo jana.(Picha na Frank Shija – MAELEZO, Tabora)

DC SOPHIA MFAUME ATEMBELEA SEKONDARI YA NASULI, AWAFUNDA WANAFUNZI WA KIKE, AELEZA MIKAKATI

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Mfaume  akiwa katika picha ya pamoja na walimu wa shule ya sekondari Nasuli iliyopo wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma leo Agosti 30,2018.
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Nasuli iliyopo Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvumawakimsikiliza MKUU wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Mfaume katika wilaya hiyo leo Agosti 30,2018.
 Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Mfaume akimsikiliza mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Nasuli leo

Na Ripota Wetu, Globu ya jamii
MKUU wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Mfaume ametembelea Sekondari ya Nasuli yenye kidato cha kwanza hadi cha sita iliyokuwa kwanza kimkoa katika matokeo ya Baraza la Mitihani la Taifa(NECTA) mwaka jana.

Akiwa shuleni ametumia nafasi hiyo pia kueleza kuwa malengo yao ni kuhakikisha shule hiyo inashika nafasi ya kwanza kitaifa huku akitoa ushauri kwa wanafunzi wahakikishe wanasoma kwa bidii na kuachana na mambo ambayo hayana uhusiano na masomo.

Akizungumza leo na Michuzi Blog, DC Mfaume amesema ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha wanafunzi kwamba kitu chochote kikikaa eneo lisilo sahihi kinakua uchafu.

Amewapa mfano kwamba “Karatasi safi nyeupe nikiichukua na kuitupa pale 'smart area' ya shule basi itageuka na kuwa uchafu.... hivyo hata kuchanganya masomo na mambo yasiyohusu inakua ni uchafu.”

Mfaume amewasisitiza wanafunzi wa kike kuzingatia kanuni ya magauni manne ili wafikie ndoto zao.

Maafisa Habari Wasisitizwa Mawasiliano Kupitia Mitandao ya Kijamii

0
0

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri akizungumza katika kikao baina yake na viongozi wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Seriikalini (TAGCO) na Idara ya Habari –MAELEZO wakati wa ziara ya kutembelea Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri za Kanda ya Kati leo Mkoani Tabora. Kutoka kulia ni Mjumbe wa Kamati Tendaji wa TAGCO, Inocent Byarugaba, Afisa Tehama wa Mkoa wa Tabora, Frank Lema, Makamu Mwenyekiti wa TAGCO, Bi. Sarah Kibonde Msika na Mweka Hazina Msaidizi wa TAGCO, Gerald Chami. Kutoka kulia ni Mjumbe wa TAGCO, Innocent Byarugaba,Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari –MAELEZO, Bi. Zamaradi Kawawa, Makamu Mwenyekiti wa TAGCO, Bi. Sarah Kibonde Msika, Mweka Hazina Msaidizi wa TAGCO, Gerald Chami na Kaimu Mkuuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Mkoa wa Tabora, Frank Lema. Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari –MAELEZO,Bi. Zamaradi Kawawa akielezea jambo walipokutana na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Frank Lema katika ziara ziara ya kutembelea Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri za Kanda ya Kati leo Mkoani Tabora. Kutoka kulia ni Mjumbe wa Kamati Tendaji wa TAGCO, Inocent Byarugaba, Kaimu Mkuuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Mkoa wa Tabora, Frank Lema, Makamu Mwenyekiti wa TAGCO, Bi. Sarah Kibonde Msika na Mweka Hazina Msaidizi wa TAGCO, Gerald Chami. Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO), Bi. Sarah Kibonde Msika akifafanua jambo katika kikao baina ya viongozi wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari – MAELEZO na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Frank Lema wakati wa ziara ya kutembelea Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri za Kanda ya Kati leo Mkoani Tabora. Kutoka kulia ni Mjumbe Afisa Tehama wa Mkoa wa Tabora, Frank Lema na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari –MAELEZO, Bi. Zamaradi Kawawa(katikati). Mweka Hazina Msaidizi wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO), Gerald Chami akielezea jambo katika kikao baina ya viongozi wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO), Idara ya Habari – MAELEZO na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Frank Lema(wapili kulia) wakati wa ziara ya kutembelea Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri za Kanda ya Kati leo Mkoani Tabora. Kutoka kulia ni Mjumbe wa TAGCO, Innocent Byarugaba,Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari –MAELEZO, Bi. Zamaradi Kawawa, na Makamu Mwenyekiti wa TAGCO, Bi. Sarah Kibonde Msika . Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora, Ignas Mjwahuzi(kulia)akielezea jambo mara baada ya kikao baina yake na viongozi wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari – MAELEZO wakati wa ziara ya kutembelea Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri za Kanda ya Kati leo Mkoani Tabora. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari –MAELEZO, Bi. Zamaradi Kawawa, Mjumbe wa Kamati Tendaji ya TAGCO, Innocent Byarugaba,Mweka Hazina Msaidizi wa TAGCO, Gerald Chami, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Frank Lema na Makamu Mwenyekiti wa TAGCO, Bi. Sarah Kibonde Msika . Mjumbe wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO), Innocent Byarugaba akisisitiza jambo katika kikao baina ya viongozi wa Chama hicho, Idara ya Habari – MAELEZO na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Frank Lema (katikati) wakati wa ziara ya kutembelea Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri za Kanda ya Kati leo Mkoani Tabora. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari –MAELEZO, Bi. Zamaradi Kawawa, na Makamu Mwenyekiti wa TAGCO, Bi. Sarah Kibonde Msika . Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali (TAGCO) na Idara ya Habari – MAELEZO, wakati wa ziara ya kutembelea Maafisa Habari na Mawasiliano katika mikoa ya Kanda ya Kati jana mkoaniTabora. (Picha zote na: Frank Shija- MAELEZO, Tabora)

ALAT TABORA YAIPONGEZA UYUI KWA MATUMIZI MAZURI KWENYE UJENZI WA VYUMBA VYA SHULE YA LOLANGULU

0
0

NA TIGANYA VINCENT-TABORA

Jumuiya ya Serikali za mitaa Tanzania ( ALAT) Mkoani Tabora imeipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Tabora -Uyui kufanikisha ukamishaji wa ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika Shule ya Msingi Lolangulu kwa kiasi cha shilingi milioni 38.

Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Tabora Adam Malunkwi wakati wajumbe wa Jumuiya hiyo wakiwa katika kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo kwa ajili ya kubadilishana uzoefu.

Alisema juhudi za Kamati ya Shule hiyo kwa kushirikiana na wananchi zimewapa fundisho kuwa miradi mingi inaweza kutekelezwa kwa fedha kidogo na kwa ubora wa hali ya juu. Mbunge wa Jimbo la Manonga Seif Gulamali alisema Vyumba vipya vya madarasa katika Shule hiyo vinapaswa kutumika kama funzo kwa watu wanaosimamia miradi ya ujenzi katika Mkoa wa Tabora.

Alisema hali hiyo imeonyesha kuwa wakipewa na Serikali shilingi milioni 64 wanaweza kujenga vyumba zaidi ya vinne vikiwa vimekamilika na samani zake kama walivyoona katika Shule ya Lolangulu. Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega Kiwele Bundala alimwagiza Mkurugenzi Mtendaji wake kuhakikisha anatuma wataalamu wake wa ujenzi ili waweze kujifunza mbinu walizotumia wakazi wa pale na Kamati yao kufanikisha mradi huo kwa kiwango cha juu.

Alisema hatua ya wao kuweza kujenga vyumba vitatu vikiwa na samani kwa fedha hizo kimeonyesha jinsi miradi mingi ya maendeleo ya wananchi inaweza kufanyika kwa kiwango kidogo cha fedha. Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Margaret Nakainga alisema wataalamu wa ujenzi katika Halmashauri za Mkoa wa Tabora watakiwa waige mfano wa ujenzi wa vyumba vingi vya madarasa kama vya shule ya Lolangulu ambapo vimewekewa na makinga maji.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Lolangulu Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora Mary Zacharia akisoma taarifa jana ya ujenzi wa mradi wa vyumba vitatu vya madarasa na uwekaji wa samani kwa gharama ya milioni 38 kwa wajumbe 
Jengo lenye vyumba vitatu vya madarasa na samani zake lilipo katika Shule ya Msingi Lolalungu wilayani Uyui Mkoani Tabora ambalo limegharimu milioni 38 hadi kukamilika. 
Wajumbe wa Jumuiya ya Serikali za mitaa Tanzania ( ALAT) Mkoani Tabora wakikagua na kupata taarifa jana ya mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa matatu katika Halmashauri ya Wilaya ya Tabora -Uyui kwenye Shule ya Msingi Lolangulu vilivyogharimu milioni 38. 


NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA UCHUKUZI AAGIZA WAFANYAKAZI WALIOJIGAWIA VIWANJA WANYANG'ANYWE

0
0
Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii
NAIBU Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Atashasta Nditiye, ameagiza wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) ambao walijigawia viwanja katika viwanja vya fidia za wananchi wanyang'anywe na kufikishwa mahakamani ili sheria ifuate mkondo wake.

Ameyasema hayo wakati alipofanya kikao na wawakilishi wa mkuu wa mkoa pamoja na wawakilishi wa kampuni ya Tanzania Remic centre jijini Dar es Salaam leo Agosti 30,2018.ambapo alieleza wasiwasi wake kuwa kampuni iliyopewa kandarasi ya kuwatafutia viwanja wananchi hao haijatekeleza wajibu wake ipasavyo licha ya kuwa tayari imelipwa kiasi cha shilingi bilioni 3.7.

Nditiye pia ameagiza Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, wakakague viwanja 537 vilivyotengwa maeneo ya Msongola, kwa ajili ya waliokuwa wakazi wa eneo la Kipawa jijini Dar es Salaam Jumanne wiki ijayo ili kujiridhisha kama viwanja hivyo vipo na vinafaa.

“Nakuagiza Mkurugenzi wa TAA, kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Wilaya Jumanne ijayo muende mkakague eno hilo la viwanja 537 muone kama vipo kwa sababu kumekuwa na shida sana na hawa wenzetu wa Tanzania Remix Centre nyinyi wenyewe mnajua, kuna shida ya miundombinu, sasa lazime mjue eneo hilo linafikika, na viwanja hivyo vinajengeka.” Amesema.

Amesema Wananchi wako tayari kushirikiana na serikali katika kuhakikisha upanuzi wa uwanja unakwenda vizuri. Kampuni ya Tanzania Remix Centre ilipendekezwa na Manispaa ya Ilala na kupewa kandarasi ya kutafuta viwanja kwa ajili ya makazi mapya ya wananchi waliokuwa wakiishi eneo la Kipawa jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo kulikuwepo na mivutano kati ya Mamlaka na Wananchi ambapo baadhi yao walipeleka shauri hilo mahakamani na hivyo kufanya zoezi hilo la kuwahamisha wananchi hao kwenye eneo hilo jipya kusuasua.

“Mradi huu ulihusisha upatikanaji wa viwanja 1,600 kwa mujibu wa mkataba wa awali ambapo fidia yake ilipaswa kufanywa kwa awamu mbili ya watu 800, hata hivyo kwa mujibu wa sheria kipinde kile ilitaka mwananchi apewe eneo lakini alipwe fidia pia.” Amefafanua.
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Atashasta Nditiye akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kikao kati ya wawakilishi wa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam na Kampuni ya Tanzania Remix Centre katika ukumbi wa VIP terminal II uliopo Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere.
 Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Atashasta Nditiye akiteta jambo na  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA),Richard Mayongela. 
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA),Richard Mayongela akizungmza wakati wa kikao na  Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Atashasta Nditiye kulia leo jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa kampuni ya Tanzania Remix centre akizungumza wakati wa kikao kilichofanyika leo katika ukumbi wa VIP terminal II uliopo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere kulia ni  Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Atashasta Nditiye.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

AfDB YARIDHISHWA NA MIRADI YA NISHATI MIUNDOMBINU MIBOVU NA CHAKAVU KUONDOLEWA DODOMA

0
0
Yaahidi kuendelea kutoa ufadhili utakaohusisha uondoaji wa miundombinu mibovu ya umeme jijini Dodoma

Na Zuena Msuya, Dodoma

Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), imeahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali ya Tanzania katika kuimarisha miundombinu ya umeme nchini hususan katika Mkoa wa Dodoma ili kuboresha upatikanaji wa huduma ya umeme kutokana na kuongezeka kwa shughuli za uwekezaji.

Uboreshaji wa hali ya umeme mkoani Dodoma unahusisha uondoaji wa miundombinu mibovu na chakavu zikiwepo takribani transifoma 75, kujenga njia ya kusafirisha umeme yenye urefu wa kilometa 135 kuzunguka Jiji, pamoja na kujenga vituo viwili vya kupokea na kupoza umeme katika eneo la Msalato na Kikombo vitakavyokuwa na uwezo wa kufua umeme wa takribani Megawati 200.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani alisema hayo katika kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Zuzu jijini Dodoma,wakati wa ziara ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) nchini Marekani, Steve Dowd, aliyekuwa akikagua utekelezaji wa baadhi ya miradi ya nishati ya umeme inayofadhiliwa na Benki hiyo katika mikoa mbalimbali nchini. 

“Katika mazungumzo yangu na AfDB kabla ya kufanyika kwa ziara hii, pia wameonyesha nia ya kujenga kituo cha kuzalisha umeme wa Jua wa megawati 100 katika eneo la Zuzu jijini Dodoma katika kipindi cha miaka miwili ili umeme huo uingizwe katika Gridi ya taifa,” alisema Dkt Kalemani.

Akizungumzia miradi ya nishati, Dkt. Kalemani aliutaja mradi mkubwa wa umeme na wa kwanza nchini wa megawati 400 (National Backbone), kuwa ni miongoni mwa miradi mikubwa iliyotekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali ikiwemo AfDB. 
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika( AfDB) nchini Marekani,Steve Dowd(kulia),  baada ya viongozi hao kufanya mazungumzo kuhusu miradi ya nishati inayofadhiliwa na AfDB katika ofisi ya Waziri wa Nishati jijini Dodoma.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ( wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika( AfDB) nchini Marekani, Steve Dowd (wa pili kulia), wakikagua kituo cha kusambaza umeme cha Zuzu jijini Dodoma, ikiwa ni moja ya miradi ya nishati inayofadhiliwa na AfDB kwa kushirikiana na Serikali. 
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ( katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) nchini Marekani,Steve Dowd (wa pili kulia), wakikagua kituo cha kusambaza umeme cha Zuzu jijini Dodoma. 
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ( katikati) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Benki ya maendeleo ya Afrika ( AfDB), watendaji wa Wizara ya Nishati, pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) baada ya kufanya ziara katika kituo cha kusambaza umeme cha Zuzu jijini Dodoma. 
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ( wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika( AfDB) nchini Marekani,Steve Dowd (wa pili kulia), wakiwa katika picha ya pamoja katika moja ya Transfoma zilizopo katika kituo cha kusambaza umeme cha Zuzu jijini Dodoma. 


RAIS MAGUFULI MGENI RASMI KWENYE UZINDUZI WA TAMASHA LA URITHI FESTIVAL JIJINI DODOMA

0
0
NA. LUSUNGU HELELA-DODOMA
RAIS wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha la Mwezi wa Urithi linalotambulika kama Urithi Festival, Celebrating Our Heritage litakalozinduliwa rasmi  kitaifa katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Septemba 15, 2018.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma,  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga amesema lengo la Tamasha  hilo  ni kuenzi, kudumisha, kuburudisha na kujifunza masuala muhimu yanayohusu Urithi wa Mtanzania hususani tamaduni zetu, historia, malikale na maliasili.

Aidha, Amesema kwa kutambua hazina kubwa ya malikale na utamaduni wa makabila zaidi ya 128 yaliyopo nchini, tamasha hilo litaongeza wigo wa mazao ya utalii kwa kukuza utalii wa utamaduni wa malikale hatua ambayo itaongeza ushindani wa Tanzania kama kituo bora cha utalii kwenye masoko mbalimbali duniani.

Ameongeza kuwa Urithi  Festival itasadia kukuza utalii wa ndani kwa kuongeza muda wa watalii wa kimataifa kukaa nchini kwa vile Tamasha hilo lifanyika katika kipindi ambacho watalii wengi wanatembelea Tanzania.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya   Urithi Festival walioshiriki kwenye mkutano wa Waandishi wa Habari uliofanyika leo jijini Dodoma. Tamasha hilo linalotarajiwa kuzinduliwa Septemba 15, 2018 na  kuenzi, kudumisha, kuburudisha na kujifunza masuala muhimu yanayohusu Urithi wa Mtanzania hususani tamaduni zetu, historia, malikale na maliasili.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dodoma kuwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli, anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha la Mwezi wa Urithi linalotambulika kama ‘’Urithi Festival, Celebrating Our Heritage’’ litakalozinduliwa rasmi  kitaifa katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Septemba 15, 2018.


Baadhi ya Wajumbe wakiangalia  nembo ya Urithi Festival inakayotumika kwenye Tamasha hilo.

  (Picha zote  na Lusungu Helela-WMU)

WAZAZI NA WALEZA SERENGETI WATAKIWA KUWA NA MGAWANYO SAWA WA MAJUKUMU YA KAZI KWA WATOTO WAO

0
0
Na Frankius Cleophace Serengeti
WAZAZI na walezi Wilayani Serengeti mkoani mara wametakiwa kuachana na suala la ubaguzi katika mgawanyo wa majukumu ya kazi majumbani ili kuleta usawa wa kijinsia huku mtoto wa kike akilimbikiziwa kazi nyingi kuliko mtoto wa kiume majumbani. 

Hayo yamebainishwa na wanafunzi katika tamasha la kutoa elimu juu ya masuala ya kupinga Mila na desturi zilizopitwa nawakati ukiwemo Ukeketaji, Ndoa za Utotoni pamoja na mimba za utoto tamasha lililoandaliwa na Shirika la RIGTH TO PLAY nakushirikisha shule za Msingi Nyamisingisi,Nyiberekera kata ya Isenye Wilayani Serengeti Mkoani Mara.

Elizabert Kirinda ni mwanafunzi wa shule ya msingi Nyamisingisi amesema kuwa majumbani watoto wa kike wamekuwa wakipewa kazi nyingi za kufanya kuliko watoto wa kiume jambo amabalo linachangia kukosa muda mwingi wa kijisomea wao kama mabinti hivyo wameomba wazazi na walezi kutoa mgawanyo sawa wa kazi ili kuondoa ubaguzi wa jinsia.

“Sisi wasichana majumbani tunapewa kazi nyingi kupika, kuchota maji kulea watoto na wavula hawafanyi kazi zozote na wakati mwingine tunachunga mifugo hatuna muda wa kusoma tukiwa nyumbani tunaomba wazazi waweze kugawanya sawa majukumu ya kazi majumbani” alisema Elizabert.
 Picha 1 ni Wanafunzi wa shule ya msingi Nyiberekera pamoja na shule ya msingi Nyamisingisi wakiwa katika maandamano kwa lengo la kufikisha ujumbe kupitia mabango mabalimbali waliyobeba kabla ya kuanza kwa Tamasha hilo.
 Wanafunzi wa shule ya msingi Nyamisingisi wakiimba wimbo ulibeaba ujumbe wa kupiga vita ukatili kwa watoto.
 Leah Kimaro ambaye ni mwezeshaji kutika shirika la RIGHT TO PLAY akitoa elimu juu ya madhara ya ukatili wa kijinsia katika Tamasha hilo.

TFDA YAWATAKA WALISHAJI HAPA NCHINI (CATERING) KUJISAJILI

0
0
Na Agness Francis,blogu ya Jamii.
MAMLAKA ya chakula na dawa (TFDA) imesema utoaji wa huduma katika Mikusanyiko lazima uzingatie sheria pamoja kanuni ili kwepusha mad hara kwa walaji wa chakula katika mikusanyiko.

Mkutano huo ulilenga watoa huduma ya chakula kwenye mikusanyiko hapa nchini na kuwataka kujisajili katika mamlaka hiyo na kufuata sheria ya utoaji wa huduma hiyo ikiwemo na mazingira ya uandaji wa Chakula na kufahamu matakwa ya sheria kuhususiana na utoaji huduma hizo kuboresha mifumo ya biashara wa huduma hiyo pamoja na usalama wa chakula kinachotolewa katika mikusanyiko na hivyo kulinda afya ya walaji.

Hayo aliyasema Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Agnes Kijo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa utoaji wa huduma ya chakula katika Mikusanyiko, amesema kuwa kutokana na mabadiliko ya mtindo wa maisha kumekuwa na ongezeko la uhitaji wa huduma ya chakula katika Misiba, Mikutano,MaofisiHarusi.

Kijo amesema ni muhimu kutambua kuwa utoaji wa huduma ya chakula unapaswa kuzingatia Sheria na kanuni bora za usafiri ili kuhakikisha kuwa chakula kinachoandaliwa ni salama ili kulinda afya ya jamii.

"Uandaaji wa chakuka pasipo kuzingatia matakwa ya sheria na kanuni husababisha uchafuzi wa vimelea vya maradhi na hivyo kuweza kusababisha madhara ya kiafya Kama vile Kuhara,Kuhara Damu,Homa ya Matumbo,pamoja na Kipindupindu"amesema Kijo.
Kusoma zaidi bofya hapa
Kaimu Mkurugenzi Mkuu Agnes Kijo akizungumza wakati akifungua mkutano wa wadau wa watoa huduma ya Chakula Katika Mikusanyiko uliofanyika Jijini Dar es Salaam. 
(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
Kaimu Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula wa TFDA Justin Makisi akizungumza kuhusiana na madhumuni ya wadau utoaji huduma katika mkusanyiko ,jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya wadau wa watoa huduma ya Chakula katika Mikusanyiko.

KAZI KAZI.....

0
0

 Wavuvi wakiondoka kwenda kuvua mapema  asubuhi katika kisiwa cha Gana wilaya ya Ukerewe mkoa wa Mwanza.
(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)

Wavuvi wa kisiwa cha Gana wilaya ya Ukerewe mkoa wa Mwanza  wakielekea maneno mablimbali ya ziwa Victoria kwenda kuvua ambapo waliiambia michuzi blog kwamba upatikanaji wa samaki kwa sasa mwingi kutokana na operesheni ya Uvuvi haramu unaoendelea umeweza kusaidia samaki kuwa rahisi kuwapata kutokana na kutokuvuliwa kabla ya wakati wake.

Gari lapiga mweleka jijini Mwanza

0
0
 Gari  limepiga mweleka na kuingia mtaroni katika eneo la kona Kona ya bwiru jijini Mwanza  chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika kwa haraka.(picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
Askari Polisi wakiwa katika eneo la tukio wakiendelea na juhudi za kuliondoa gari hilo lililo piga mweleka katika enao la Kona ya bwiru jijini Mwanza.

WIZARA YA UJENZI YATOA ELIMU SHERIA MPYA YA UDHIBITI WA UZITO WA MAGARI.

0
0

Baadhi ya washiriki wakiwa katika kikao kazi cha utoaji Elimu juu ya Sheria mpya ya Udhibiti wa Uzito wa Magari ya Jumuiya ya Afrika Mashiriki (2016) na Kanuni zake za mwaka 2017. Kikao hiki kimefanyika mkoani Morogoro na kuhusisha Kanda ya Mashariki iliyojumuisha mikoa ya Dar es salaam, Pwani na Morogoro.


Mkurugenzi wa Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), kupitia Kitengo cha Usalama na Mazingira, Mhandisi Julius Chambo, (wa tatu kushoto waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kikao kazi cha utoaji Elimu juu ya Sheria mpya ya Udhibiti wa Uzito wa Magari ya Jumuiya ya Afrika Mashiriki (2016) na Kanuni zake za mwaka 2017. Kikao hiki kimefanyika mkoani Morogoro na kuhusisha Kanda ya Mashariki iliyojumuisha mikoa ya Dar es salaam, Pwani na Morogoro.




Msimamizi wa Mizani za Mkoa wa Pwani, Charles Ndyetabula, akichangia mada wakati wa kikao kazi cha utoaji Elimu juu ya Sheria mpya ya Udhibiti wa Uzito wa Magari ya Jumuiya ya Afrika Mashiriki (2016) na Kanuni zake za mwaka 2017. Kikao hiki kimefanyika mkoani Morogoro na kuhusisha Kanda ya Mashariki iliyojumuisha mikoa ya Dar es salaam, Pwani na Morogoro.
PICHA NA WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.

MULTICHOICE YAWAPA FURSA YA MAFUNZO YA FILAMU VIJANA WANNE WA KITANZANIA

0
0
Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania, ndugu Alpha Mria akielezea kwa undani namna mchakato huu wa kupata vijana wenye vipaji na mapenzi kwenye sekta ya Filamu na mwisho kupatikana washindi hawa wane ambao mnamo Octoba 2018 wataenda kuiwakilisha Tanzania kwenye ya Mafunzo Maalum ya Tasnia ya Filamu MultiChoice Talent Fatory, huko Jijini Nairobi Kenya kwa kipindi cha mwaka mzima.
Meneja Uendeshaji MultiChoice Tanzania Ronald Baraka Shelukindo pamoja na Meneja Masoko MultiChoice Tanzania Alpha Mria wakiwapongeza vijana hawa wakitanzania walioibuka washindi wa mpango huu wa kukuza tasnia ya Filamu Afrika unaotambulika kama Multichoice Talent Factory, vijana hawa wataliwakilisha Taifa kwenye mauzo haya maalum ya mwaka mzima yatakayofanyika Jijini Nairobi Kenya, kwa ukanda wa Afrika Mashariki yakiwa yameandaliwa na kugharamiwa na MultiChoice Afrika.
Picha ya Pamoja ya Uongozi wa Multichoice Tanzania wakiwa na Vijana walioibuka kidededea watakao kwenda kuiwakilisha Tanzania kwenye Mafunzo Maalum ya Filamu Multichoice Talet Factory, jijini Nairobi Kenya, kutoka kusho ni Jamal Kishuri kutokea Arusha, Jane Moshi kutoka mkoa wa Kilimanjaro, katikati ni Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania Ronald Baraka Shelukindo akifuatiwa na mshindi Sarah Kimario  kutokea Dar es Salaam, pembeni ni Menejea Masoko MultiChoice Tanzania Alpha Mria na mwisho kulia ni mshindi wetu mwingine Wilson  Nkya kutoka Kigoma wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa halfa hiyo.


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
KAMPUNI ya Multichoice Tanzania imetawatangaza vijana wanne wa ktanzania waliofanikiwa kushinda shindano la Multichoice Talent Factory watakaoungana na wenzao kutoka nchi mbalimbali barani Afrika kwa ajili ya kupata mafunzo ya filamu kwenye vituo vitatu tofauti.

Washindi hao waliofanikiwa kushinda wataelekea nchini Kenya kwa ajili ya mafunzo hayo yatakayokuwa ya mwaka mmoja yakianzia Oktoba Mosi mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania Ronald Shelukindo amesema kuwa mchakato mzima wa kuwapata washindi hao ulichukua muda wa miezi miwili baada ya kuzinduliwa mwezi Mei mwaka huu, na zaidi ya vija a 160 walituma maombi na mchujo ulifanyika tarehe 20 Julai na kuwapata vijana hawa walioshinda.

Shelukindo amesema kuwa, maendeleo ya nchi kwa muda mrefu yamekuwa yakitambuliwa kwa uwekezaji katika maliasili nyingi zilizopo kama vile madini, kilimo, mifugo, wanyamapori huku sekta ya sanaa na ubunifu ikiwa haijapewa kipaumbele kikubwa na hivyo kupelekea mchango mdogo kwenye ukuaji wa uchumi.

Amesema kuwa ili kuhakikisha wanasaidiana na serikali katika mkakati wake wa kuifanya sekta ya ubunifu na sanaa kuwa moja ya wahimili wa uchumi wa nchi , Multichoice imeweza kuanzisha program hizo na wameanza na sekta ya filamu na tayari wameshapatikana vijana hao watakaoanza mafunzo mwezi Oktoba nchini Kenya.

Shelukindo amewataja vijana hao ni Sarah Kimario kutoka Dar es Salaam, Wilson Nkya wa Kigoma, Jamal Kishuli kutoka Arusha na Jane Moshi wa Kilimanjaro na safari yao tayari imeshapangwa wanasubiriwa kusafiri tu.

Mmoja wa washindi waliotangazwa kufuzu program Sarah Kimario amesema kuwa hii ni moja ya nafasi nzuri ya kuweza kujifunza zaidi masuala ya sanaa na amewaomba wazazi kutokuwakataza watoto wao kufanya kile wakipendacho kwani watakuwa wanashindwa kuonyesha vipaji walivyonavyo.

VIGOGO BENKI YA POSTA WATUPWA JELA MIAKA MITANO

0
0
NA TIGANYA VINCENT-TABORA
VIGOGO wawili wa Benki ya Posta Tawi la Tabora na mfanyabiashara mmoja waliokuwa wanakabiliwa na jumla ya mashitaka saba ikiwemo utakatishaji wa zaidi ya shilingi milioni 700 wametupwa jela miaka mitano au kutakiwa kulipa faini ya shilingi milioni mia moja (100).

Mbali ya adhabu hiyo Mahakama hiyo baada ya kuwatia hatiani imewataka washitakiwa hao kulipa shilingi milioni 710 waliziibia Benki ya Posta na vinginevyo mali zao zitaifishwe na serikali kufidia kiasi cha fedha zilizoibwa.

Uamuzi wa shauri hilo la jinai namba 154/2015 umetolewa jana na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Tabora Jocktan Rushwela baada ya kuwatia hatiani washitakiwa hao kwa makosa matatu kati ya saba.

Vigogo wa benki ya Posta Tabora waliopata adhabu hiyo ni Boaz Lunyungu aliyekuwa meneja, George Ngatunga(mhasibu) na mfanyabiashara Umaiya Makiliga.

Katika hukumu hiyo iliyosomwa kwa saa mbili Hakimu Rushwela aliwatia hatiani watuhumiwa hao kwa makosa matatu kati ya saba waliyokuwa wanashitakiwa nayo ambayo ni kula njma ya kutnda kosa la wizi, kutakatisha fedha na wizi.

Awali upande wa mashitaka ukiongozwa na wakili mwandamizi wa Serikali Shedrack Kimaro aliiambia Mahakama hiyo kuwa watuhumiwa walitenda makosa hayo kati ya Januari 2014 na julai 2915 katika benki ya posta tawi la Tabora.

Wakili Kimaro alidai kwenye shitaka la kwanza kuwa katika kipindi hicho washitakiwa kwa pamoja walikula njama ya kutenda kosa la wizi.

Ilidaiwa na wakili Kimaro kuwa washitakiwa wote watatu katika tarehe tofauti kati ya mwezi Januari 2014 na mwezi julai 2015 waliiba jumla ya shilingi milioni 710 katika benki ya Posta tawi la Tabora.

Shitaka la tatu ambalo lilikuwa likiwakabili aliyekuwa meneja na Mhasibu wake ilidaiwa kuwa wakiwa ni watumishi wa benki wa Posta walitakatisha fedha shilingi milioni 710 huku wakijua wamezipata kwa njia zisizo halali.

Upande wa jamuhuri wakati wa usikilizwaji wa shauri hilo ulileta jumla ya mashahidi 16 ambao waliweza kutoa ushahidi uliopeleka mahakama kuthibitisha pasipo shaka kwamba watuhumiwa walitenda makosa hayo.

Mahakama imewahukumu kwenda jela miaka mitatu mitatu kwa kosa la kula njama na lile la wizi na miaka mitano kwa kosa utakaktishaji wa fedha, kwa vile adhabu hizo zinakwenda pamoja watutumikia kifungo cha miaka mitano jela.

Washitakiwa hao watatu pamoja na kupata adhabu hiyo ya kifungo bao wanakabiliwa na kesi nyingine ya kuhujumu uchumi wakiwa na watu wengine 13 shauri amabalo bado alijaanza kusikilizwa kwani jalada lake lipo ofisini kwa DPP likisubiri kutolewa uhamzi.

MAHAKAMA JUMUISHI MBEYA KUSOGEZA HUDUMA ZA KIBENKI NDANI YA MAHAKAMA HIYO

0
0
Viongozi wa Mahakama Kanda ya Mbeya (kushoto) wakiwa katika majadiliano na Viongozi wa Benki ya NMB, majadiliano juu ya uanzishwaji wa huduma za kibenki ili kuwarahishia wateja wanaofika katika Mahakama hiyo.
Mjumbe kutoka NMB akichangia jambo katika majadiliano.
Picha ya pamoja baada ya majadiliano, (wa pili kushoto) ni Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya.
              (Picha na Rajabu Singana, Mahakama Kuu, Mbeya)   

Na Rajabu Singana. Mahakama Kuu Mbeya
JAJI Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Mhe. Robert Makaramba amekutana na uongozi wa benki ya NMB na kufanya mazungumzo juu ya uanzishwaji wa huduma za Kibenki katika jengo la Mahakama Kuu Mbeya linalotoa huduma kwa Mahakama Kuu, Mahakama ya Hakimu Mkazi na Mahakama ya Wilaya.

Mhe. Makaramba alikutana na uongozi huo mapema Agosti 28, aliwaeleza viongozi wa NMB kwamba Mahakama ipo katika maboresho makubwa ya huduma zake kupitia mpango mkakati wa miaka mitano (2015-2020) unaolenga kumsogezea mwananchi huduma.

Kutokana na changamoto ya kufanya malipo ambayo wamekuwa wakiipata wananchi Mhe. Makaramba aliwaomba NMB kusogeza huduma zao katika jengo la Mahakama Kuu Mbeya. 

Akichangia katika mazungumzo hayo, Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Straton Chilongola alisema kwa sasa Benki ya NMB imekuwa ikifanya kazi kwa kushirikiana na Mawakala ambao hufanya kazi za Kibenki. 

Bw. Chilongola aliongeza kwa kusema kwamba watafanya utaratibu wa kuanzisha ‘Cash Collection Point’ kwa ajili ya wananchi kufanya malipo ya Huduma za Mahakama. 

Meneja wa Wakala wa Benki wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Bw. Respicious Denis aliongeza kuwa kwa sasa benki ya NMB imekuwa ikifanya vizuri kwa kutumia Mawakala kwenye malipo na makusanyo mbalimbali ambapo tayari baadhi ya taasisi za serikali zinatumia huduma hiyo. 

Alizitaja taasisi hizo ni paoja na TRA, Idara ya Maji Mbeya na walitumia mfumo huo katika makusanyo ya NaneNane mwaka huu.

Ifahamike kwamba baada ya ukarabati mkubwa wa jengo la Mahakama Kuu Mbeya, Uongozi wa Mahakama ya Tanzania ulifikia maamuzi ya kulifanya jengo hii kuwa Kituo Jumuishi cha kutoa huduma za Mahakama. 

Wadau muhimu wa Mahakama walipatiwa ofisi za kuendeshea shughuli zao ikiwa ni njia mojawapo ya kumsogezea mwananchi huduma na kuondoa usumbufu kwa wananchi. Wadau walipotiwa ofisi ni pamoja na Mawakili wa Kujitegemea, Mawakili wa Serikali, Polisi na Huduma kwa Jamii. 

Pamoja na mambo mengine viongozi hawa wameafikiana kuanzisha Huduma za Kibenki wiki ijayo kwa kumtumia Wakala wa Benki.

UCHAGUZI WA CHABATA KUFANYIKA OKTOBA 06 DODOMA

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
BARAZA la Michezo la Taifa limetangaza uchaguzi mkuu wa Chama cha Baiskeli Tanzania (CHABATA) utakaotarajiwa kufanyika oktoba 06 mwaka huu katika Jiji la Dodoma.

Akizungumzia uchaguzi huo, Afisa habari wa BMT Najaha Bakari amesema kuwa fomu za uchaguzi zimeanza kutolewa katika ofisi za baraza hilo kuanzia leo hadi Oktoba Mosi mwaka huu.

Najaha amesema kuwa usaili utafanyika Oktoba 05 kuanzia saa 3 asubuhi kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo siku inayofuata katika nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu na wajumbe sita wa kuchaguliwa.

Najaha amesema sifa za wagombea hao ni lazima wawe  na elimu ya kidato cha nne au zaifi, taaluma na uongozi katika mchezo wa baiskeli, awe raia wa Tanzania, awe na nidhamu pamoja na asiwe na historia ya kukutwa na hatia ya kufungwa zaidi ya miezi sita.

BMT imetoa wito kwa wenye nia ya dhati ya maendeleo ya mchezo huu, waone umuhimu wa kuchukua fomu na kugombea nafasi stahili ili kuendeleza chama cha michezo huu pamoja na kuiletea sifa nchi.

Mbali na hilo Najaha amewasihi viongozi wa vyama vya michezo kuona umuhimu wa kuwa na ofisi zao kwani kuanzia sasa hivi Baraza halitalifumbia macho suala hilo kwa kuona vyama havina ofisi wala hawajulikani wanapatikana wapi.
Viewing all 109606 articles
Browse latest View live




Latest Images