Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

MAADHIMISHO YA SIKU YA MAJESHI NCHINI


MADIWANI WANNE WA CHADEMA ,MOSHI WAUNGANA NA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA KILIMANJARO KUHAMSISHA MAENDELEO KATIKA KATA YA SHIRIMATUNDA

$
0
0
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini,

MADIWANI wanne kutoka  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika manispaa ya Moshi  pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Kilimanjaro Patrick Boisafi wamejitokeza kumuunga mkono Diwani wa kata ya Shirimatunda ,Francis Shio (Chadema) kuhamasisha uchangiaji katika shughuli za maendeleo.
Madiwani waliojitokea katika mkutano maalumu wa Diwani  kata na wananchi wa kata hiyo ,ni pamoja na Diwani wa kata ya Soweto,Collins Tamimu,Diwani wa kata ya Njoro na Naibu Meya wa manispaa ya Moshi,Jomba Khoi ,Diwani wa kata ya Ng’ambo Genesis Kiwhelu na Diwani wa kata ya Kiboriloni ,Frank Kagoma.
Akizungumza wakati wa mkutano huo uliofanyika katika ofisi ya kata ya Shirimatunda  ,Diwani wa kata ya Shirimatunda ,Fransic Shio alisema maendeleo ya wananchi katika maeneo yao yataletwa na wananchi wenyewe na si itikadi za kisiasa kama baadhi ya wanasiasa wanavyoamini.
“Shirimatunda yetu ni ya kwanza kuliko vitu vingine,haya ninayo yasema ni ya uwazi tukikubali kuyaingiza mambo ya kisiasa katika maendeleo ya kata yetu ,yapo mambo mengi sana yatasimama  ,ni lazima kaul yetu ya wana Shirimatunda,umoja ya wana Shirimatunda na amani yetu tuweze kuilinda kwa gharama yoyote”alisema Mh Shio.
Shio aliwataka wakazi wa Shirimatunda kuwaondoa katika misingi ya umoja wa wakazi wa kata ya Shirimatunda huku akiwaomba kupitishwa azimio la kuchangisha fedha kwa kila familia katika kata hiyo kutoa kiasi cha Sh 10000 kwa ajili ya ujenzi wa darasa la wanafunzi wa shule ya awali.
Kwa upande wao ,Madiwani waliofika kumuunga mkono Diwani huyo,walisema ili kushawishi wadau mbalimbali pamoja na serikali kujitokeza kuchangia maendeleo katika kata hiyo wakazi wa eneo hilo wanapaswa kuwa wa kwanza katika kuchangia.
“Mgeni akija nyumbani akakuta wewe mwenyewe hujielewi ,hata kama amekuja na zawadi atarudi nayo ,watu wa Shirimatunda wanaangaliana nani anatoa nini ,endapo kila mkazi wa Shirimatunda akiguswa na hiki tunachokifanya basi angechangia katika eneo hili la elimu”alisema Diwani Kagoma.
Diwani wa kata ya Shirimatunda katika Manispaa ya Moshi,Fransic Shio (CHADEMA) akizungumza wakati wamkutano wa kata uliolenga kujadili masuala ya maendeleo pamoja na kutambulisha wajumbe wanaounda kamati ya maendeleo ya kata hiyo.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Kilimanjaro,Patrick Boisafi akizungumza katika mkutano wa kata ya Shiriamtunda ambapo yeye amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya maendeleo ya kata hiyo.
Baadhi ya wananchi wakifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na viongozi .
Naibu Meya wa Manispaa ya Moshi na Diwani wa kata ya Njoro,Jomba Khoi akizungumza katika mkutano huo ambapo yeye na madiwani wenzake walifika kumuunga mkono Diwani wa kata hiyo katika kuchangia shuhghuli za maendeleo .

Serikali yawatoa hofu wavuvi kuhusu vibali vya nyavu.

$
0
0
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega amesema Serikali inaratibu vyema upatikanaji vibali vya kuagiza nyavu bora kwa ajili ya shughuli za uvuvi.

Ulega ametoa kauli jana katika mkutano wa hadhara na wakazi wa kisiwa cha Gana kilichopo wilayani Ukerewe alipofanya ziara ya kutembelea na kusikiliza kero za uvuvi.

Ulega ambaye pia ni mbunge wa Mkuranga amewaeleza wanakisiwa hao wa Gana kuwa Serikali imeshaanza kutoa vibali vya kuagiza nyavu kwa utaratibu unaofaa.

Wakazi hao walitumia fursa hiyo kumuuliza Ulega kuhusu hatima ya samaki aina ya Furu, Gogogo, Nembe na Ningu ambao hawatajwi na sheria ya uvuvi.

Ulega amewajibu "Serikali inaanda muongozo utakaowasaidia kuvua samaki hawa kwa uhuru " amesema .Pia amewataka wavuvi wa Gana wajiunge kwenye vikundi vya ushirika ili wapekelekewa mradi wa Mfuko wa Hifadhi ya Taifa ya Jamii (NSSF) wa wavuvi skimu.

"Mradi huu utakaokopesha na utawasaidia kuimarisha shughuli zao kupitia vikundi watakavyoviunda,"amesema Ulega.
Pichani kati ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Abdallah Ulega akiwa sambamba na baadhi ya viongozi wa chama cha CCM,Ulinzi na usalama wilaya,wakienda kwenye mkutano mara baada ya kuwasili katika kisiwa cha Ghana wilayani Ukerewe Pichani kati ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Abdallah Ulega akiwa sambamba na baadhi ya viongozi wa ulinzi na usalama wilaya,wakiwa ndani ya boti kueleka kisiwa cha Ghana wilayani Ukerewe kukutana na wananchi wakiwemo wavuvi katika ziara yake ya kutembelea na kusikiliza kero zao 
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Abdallah Ulega akizungumza na Wananchi wa kisiwa cha Ghana wilayani Ukerewe katika mkutano wa hadhara,alipofanya ziara ya kutembelea na kusikiliza kero za Wavuvi 
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Abdallah Ulega akiagana na baadhi ya viongozi (hawapo pichani),wakati akipanda boti kuelekea kisiwa cha Ghana wilayani Ukerewe kukutana na wananchi wakiwemo wavuvi katika ziara yake ya kutembelea na kusikiliza kero za Wavuvi hao. 

JAMHURI KUWASILISHA MASHAHIDI 34 NA VIELELEZO 15 LIKIWEMO PANGA LINALOTAJWA KUTUMIKA MAUAJI YA MWANAFUNZI SHULE YA SCOLASTICA.

$
0
0
Na Dixon Busagaga,MOSHI

JUMLA ya Mashahidi 34 wanatarajia kutoa ushahidi katika shauri la mauaji ya kukusudia ya mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Scholastica iliyopo Himo,Humphrey Makundi.

Mbali na Mashahidi hao pia upande wa Jamhuri umepanga kuwasilisha vielelezo 15 vikiwa katika mfumo wa nyaraka pamoja na Panga linaloaminika kutumiwa na mshtakiwa wa kwanza katika shauri hilo.

Hayo yamo katika maelezo ya awali yaliyosomwa jana Mahakama Kuu ,Kanda ya Moshi na Wakili Mkuu wa Serikali,Joseph Pande mbele ya jaji wa mahakama kuu ,kanda ya Moshi,Haruna Songoro.Miongoni mwa mashahidi hao ni baba mzazi wa marehemu,Humphrey,Bw Jackson Makundi,madaktari kutoka hosptali za rufaa za KCMC na Mawenzi,maofisa wa jeshi la Polisi kutoka ofisi ya mkuu wa upelelezi wa mkoa (RCO) na kituo cha Polisi Himo.

Mashahidi wengine ni wahudumu chumba cha kuhifadhia maiti ,hosptali ya rufaa ya mkoa ,Mawenzi na mfanyakazi wa kampuni ya mawasiliani ya simu za mkononi ya Vodacom kutoka Dar es Salaam.Upande wa vielelezo vilivyopangwa kuwasilishwa ni pamoja na simu saba za mkononi zikiwemo za washtakiwa ,ripoti ya uchunguzi wa mawasiliano ya simu pamoja na ripoti ya uchunguzi wa mwili wa marehemu na taarifa ya vina saba (DNA).

Kwa upande wa utetezi unatetewa na wakili Elikunda Kipoko akisaidizana na Wakili Gwakisa Sambo ulieleza mahakama kuwa ushahidi wao utawasilishwa kabla kesi haijaanza.Shauri hilo lilikuja kwa ajili ya washtakiwa kusomewa kosa lao pamoja na maelezo ya mashahidi ambapo washtakiwa wote watatu walikana shtaka lao.

Washtakiwa katika shauri hilo ni pamoja na mlinzi wa shule hiyo Hamisi Chacha ambaye anatajwa kama nshtaliwa wa kwanza,Mkurugenzi wa Shule za Scholastica, Edward Shayo ambaye anatajwa kama mshitakiwa wa pili na Mwalimu wa nidhamu, Laban Nabiswa anayetajwa kama mshitakiwa wa tatu.
Watuhumiwa  wa Mauaji ya Mwanafunzi shule ya  SCOLASTICA,Himo mkoani Kilimanjaro.

MSHINDI MASHINDANO YA MISS TANZANIA 2018 KUJULIKANA SEPTEMBA 8 JIJINI DAR

$
0
0
Na.khadija Seif,Globu ya jamii

Muandaaji wa kinyang'anyiro cha Wanamitindo nchini ambae pia alishawahi kuwa Miss Tanzania mwaka 1998, Basilla mwanukuzi amezungumza jijini Dar es salaam na wanahabari kuhusu hafla ya mashindano hayo yanayotarajiwa kufikia kilele septemba 8 mwaka huu katika ukumbi  wa Julius Nyerere international convention Centre (JNICC).

Aidha Mwanukuzi ametoa shukrani kwa Waziri wa Sanaa,utamaduni na michezo Mh.Harrison Mwakyembe kwa kushirikiana na mashindano hayo tangu yalipoanza mchakato wake  April mwaka huu, na kufungua rasmi kwani kulikuepo na changamoto mbalimbali hapo awali likiwemo suala la kufungia mashindano hayo kutokana na sababu mbalimbali, ambapo kimsingi ziliwanyima warembo wengi fursa ya kushiriki.

"Hivyo basi kwa sasa wamepatiwa fursa hiyo na tunategemea tutapata mshindi ambae ataipeperusha bendera yetu Kwenye mashindano ya miss World ambayo yatafanyika nchini China ",alieleza Basilla.Pia ametolea ufafanuzi kuhusu vigezo ambavo vimewekwa bayana kwa mrembo atakaeshinda taji hilo, ikiwemo umri pamoja na uraia wa Tanzania sambamba ukiwekwa mbele zaidi .

Mshindi wa miss Tanzania atapatiwa taji lenye thamani ya shilingi za kitanzania millioni 6 pamoja na gari lenye hadhi nzuri na viwango pamoja na kupata fursa ya kusaidia jamii yake.
Muandaaji wa mashindano ya Miss Tanzania Basilla Mwanukuzi akizungumzaa na wanahabari jijini Dar es salaam kuhusu mashindano ya warembo hao yanayotarijiwa kufikia kilele chake mwanzoni mwa septemba mwaka huu

DIWANI MAMUYA ACHAGULIWA MAKAMU MWENYEKITI HALMASHAURI YA WILAYA YA MOSHI.

$
0
0
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.

DIWANI wa kata Marangu Mashariki katika jimbo la Vunjo,Mh Exaud Mamuya amechaguliwa kushika nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Moshi baada ya kushinda kwa kura 45 zilizopigwa .

Katika kinyang’anyiro hicho ,Mh Mamuya alikuwa akichuana na wagombea,Filbert Shayo kutoka chama cha NCCR-Mageuzi na Chata Madata wa Chama cha Mapinduzi ambaye hata hivyo baadae alienguliwa.

Akizungumza wakati wa Uchaguzi huo, Afsa Uchaguzi wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Patrick Nyavanga alitoa ufafanuzi wa namna mshindi anavypatikana katika uchaguzi huo ikiwemo mshindi kupata kura za ndio zisizopungua asilimia 50 ya kura zote zilizopigwa.

Alisema uchaguzi huo unafanyika kwa mujibu wa kifungu namba 6 cha kanuni za kudumu za Halmashauri na baraza la madiwani wa Halmashauri wa Wilaya ya Moshi likaridhia kufanyika kwa uchaguzi wa Makamu mwenyekiti.Uchaguzi huo ulilazimika kufanyika kwa awamu mbili baada ya awamu ya kwanza kukosekana mshindi baada ya wagombea wote kutofikisha zaidi ya nusu ya kura zote zilizopigwa.

Katika marejeo ya awamu ya piliya zoezi la upigaji kura jumla yakura 45 zilipigwa ambapo Mh,Mamuya alipata kura 45 baada ya mgombea kwa tiketi ya chama cha NCCR-Mageuzi Mhe,Shayo kuamua kujitoa wakati wa uchaguzi wa marudio na Mhe.Chata kuenguliwa.

Msimamizi wa uchaguzi ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi Peter Malendecha alimtangaza Mhe.Exaud Willison Mamuya mgombea kwa tiketi ya CHADEMA kuwa Makamu Mwenyekitiwa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi kwakipindi cha mwaka wa fedha 2018/2019.

Akizuzngumza mara baada ya kumtangaza mshindi,Malendecha alisema uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki na umeendeshwa kwa amani na utulivu kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya uchaguzi.
Mbali na uchaguzi huo baraza la madiwa wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi limeunda kamati na kufanya uchaguzi wa wenyeviti wa kamati mbalimbali za kudumu za Halmashauri ikiwemo kamati ya Elimu ,afya na maji, kamati ya maadili, kamati ya mipango miji na kamati ya Uchumi, ujenzi na mazingira.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Exaud Mamuya (katikati) akiwakatika vazi maalumu baada ya kuchaguliwa kwamara nyingine kushika nafasi hiyo.

FILAMU YA BAHASHA YAPATA MAPOKEZI MAKUBWA TOKA KWA WANANCHI

$
0
0
 Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) Valentino Mlowola amesema njia nzuri ya kusambaza na kupeleka ujumbe kwa wananchi kuhusu mapambano dhidi ya rushwa ni kutumia sanaa.

Mlolowa amesema hayo wakati wa uzinduzi wa filamu inayojulikana kwa jina la BAHASHA iliyoandaliwa na ubalozi wa Uswisi na Uholanzi kwa kushirikiana na Takukuru inayozungumzia madhara yanayojitokeza katika sehemu mbalimbali inayosababishwa na rushwa.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa filamu hiyo, Mlolowa amesema sanaa ni njia nzuri ya kuweza kufikisha ujumbe kwa urahisi kwakuwa wananchi wanapenda sana sanaa na filamu hii itawasaidia zaidi katika kuona madhara yanayokuja baada ya rushwa.

Amesema kuwa, filamu hii ina ujumbe mzuri sana na wanatarajia mwakani katika mbio za mwenge isambazwe ili nchi nzima ili wananchi waelewe madhara yatokanayo na rushwa na wananchi wameipokea kwa muitikio mkubwa sana.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) Valentino Mlolowa akizungumza na wageni waalikwa waliofika katika uzinduzi wa filamu ya BAHASHA uliofanyika jana usiku Jijini Dar es Salaam.
Muandaaji wa Filamu hiyo Louise Kamin akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa uzinduzi wa filamu ya BAHASHA uliofanyika jana, filamu hiyo inayohusu Rushwa imewezwa kuandaliwa baina ya ubalozi wa Uswisi na Uholanzi pamoja Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU).
Waalikwa mbalimbali wakifuatilia kwa makini filamu ya BAHASHA iliyozunduliwa jana usiku na Ubalozi wa Uswisi kwa kushirikiana na Ubalozi wa Uholanzi na Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU).




NEC YAENDELEA KUTOA DARASA KWA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI MDOGO YAENDELEA JIJINI DODOMA

$
0
0


Afisa Uchaguzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Stephen Elisante akimtazama mmoja wa Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi aliyekua akifunga kituturi cha kupigia Kura leo jijini Dodoma wakati wa mafunzo kwa vitendo ya Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi mdogo wa Ubunge na Udiwani utakaofanyika Septemba 16, 2018.
Mafunzo kwa Vitendo yanayoendeshwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi yakiendelea jijini Dodoma kwa Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi mdogo wa Ubunge na Udiwani utakaofanyika Septemba 16, 2018 katika jimbo la Ukonga na Monduli na kwenye Kata 13 za Tanzania Bara.
Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo kwa Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa mafunzo ya Usimamizi wa Uchaguzi Mdogo wa Ubunge na Udiwani utakaofanyika Septemba 16, 2018 katika jimbo la Ukonga na Monduli na kwenye Kata 13 za Tanzania Bara.
Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo kwa Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa mafunzo ya Usimamizi wa Uchaguzi Mdogo wa Ubunge na Udiwani utakaofanyika Septemba 16, 2018 katika jimbo la Ukonga na Monduli na kwenye Kata 13 za Tanzania Bara.
Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo kwa Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa mafunzo ya Usimamizi wa Uchaguzi Mdogo wa Ubunge na Udiwani utakaofanyika Septemba 16, 2018 katika jimbo la Ukonga na Monduli na kwenye Kata 13 za Tanzania Bara.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo kwa Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi akichangia na kuuliza maswali wakati wa wa mafunzo ya Usimamizi wa Uchaguzi Mdogo wa Ubunge na Udiwani utakaofanyika Septemba 16, 2018 katika jimbo la Ukonga na Monduli na kwenye Kata 13 za Tanzania Bara. 

Wanakijiji Arumeru wafurahia kupata Mawasiliano ya uhakika kutoka Halotel.

$
0
0
Wakazi wa kijiji cha Timbolo,Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, wamepongeza jitihada za mtandao wa simu wa Halotel kwa kufikisha mawasiliano kijijini hapo baada ya kuhangaika kwa muda mrefu kupata huduma za Mawasiliano ya uhakika jambo ambalo limechangia kwa ukuaji wa shughuli za kiuchumi kwa wakazi wa kijiji hicho hususani huduma jumuishi za fedha(financial inclusion). 

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa kijiji hicho, Bw. Samwel Kivuyo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali walipokwenda kutembelea katika kijiji hicho ili kuona na kujifunza shughuli mbalimbali za kimaendeleo ambazo zimechangiwa na mtandao huo kuwekeza katika maeneo ambayo awali hayakuwa na huduma za mawasiliano ya uhakika.

‘’Halotel wamesaidia sana kufikisha huduma jumuishi za kifedha kwa wananchi masikini wa kijiji hiki ambao awali walikuwa wanataabika na kupitwa na huduma hizo hivyo kulazimika kutembea kilometa nyingi kufuata huduma za kifedha,kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kijiji hicho, Bw. Samwel Kivuyo.

Baadhi ya wanakijiji wa kijiji hicho katika kata ya Sambasha,wameelezea kufurahishwa na huduma ya Halopesa,ambapo wamesema,imekuwa rafiki kulinganisha na huduma kama hizo zinazotolewa na kampuni nyingine,kufutia Halotel kutotoza makato pindi mtumiaji wa huduma hiyo akituma pesa kwenda mtandao huo.

“ Kwakweli ukiwa na huduma za Haloteli,unafurahia kupata muda wa maongezi wa kutosha,data ndiyo siwezi kuelezea,yaani ni huduma rafiki sana kwa sisi hasa wa huku kijijini ambao kipato chetu ni cha chini. Alisema,Rehema Joshua,mkazi kijiji cha Timbolo,kata ya Sambasha,Wilaya ya Arumeru,mkoa wa Arusha.

“Sisi kama wananchi wa Timbolo tunashukuru kwanza kabisa jitihada za serikali kwa kuiwezesha kampuni ya Halotel kuweza kuweka minara ya mawasiliano katika kijiji chetu ili wananchi waweze kupata huduma za mawasiliano katika maeneo yao na kusaidia wananchi kutumia huduma za mawasiliano katika kujiendeleza kiuchumi kwani hapo awali hatukuwa na huduma ya mawasiliano ya uhakika.,”
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel, Mhina Semwenda (katikati), akiwaelekeza wakazi wa Kijiji cha Timbolo namna ya kutumia huduma za mtandao wa Halotel wakati wa ziara ya waandishi wa habari kutembelea miundombinu ya kampuni hiyo. 
Mwenyekiti wa Kijiji cha Timbolo Halmashauri ya Wilaya ya Arusha DC, Samwel Kivuyo, akifafanua jambo wakati kwa waandishi wa habari waliotembelea kijiji hicho kuangalia miundombinu ya mawasiliano iliyowekwa na Kampuni ya Halotel. Kushoto ni Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Josephine Mhina. 


Waziri Mwakyembe akutana na Wamiliki wa Televisheni nchini

$
0
0
Na Immaculate Makilika na Bushiri Matenda- MAELEZO
Serikali imesema kuanzia septemba 5, mwaka huu visimbuzi vitaanza kuonesha channeli zote za ndani bila kutoza gharama yoyote kwa mtazamaji.

Akiwaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, kuhusu yaliyozungumzwa katika kikao kati ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe na wadau na wamiliki wa televisheni nchini, Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi amesema kuwa serikali imefikia uamuzi huo baada ya visimbuzi vya AZAM, ZUKU na DSTV kutoonesha channeli za ndani, kulingana na aina ya leseni zao.

“Ningependa watanzania wafahamu kwamba kuanzia septemba 5 mwaka huu, visimbuzi vya TIN, Starmedia, Continental na Digtek vitaonesha takribani channeli 34 za ndani bure, ili kutoa fursa ya kila mwananchi kuwa na haki ya kupata taarifa” alisema Dkt. Abbasi

Aidha, alielezea kuwa wadau hao na wamiliki wa televisheni wameonesha kuridhishwa na hatua hiyo ya kwa vile Serikali imetengeneza miundombinu itanayoruhusu channeli zao kuonekana nchi nzima.

Dkt. Abbasi, alisisitiza kuwa “nchi imeandaa mfumo, ambao unaweza kufanyakazi bila kutegemea kampuni kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kuonesha channeli za ndani au matangazo, kwa hivyo wadau au wamiliki wa vyombo vya habari wasihofu kuhusu hilo”

Kikao kati ya Waziri Mwakyembe na wadau na wamiliki wa televisheni nchini, kimefanyika kwa lengo la kuwa na majadiliano ya pamoja baina serikali na wadau hao ili kupata muafaka kuhusu kutooneshwa kwa chaneli za ndani katika visimbuzi vilivyokiuka masharti ya leseni zao.

Aidha, kikao hicho pia kilihudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Injinia James Kilaba, pamoja na wataalamu wake.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (katikati) akizungumza na wawakilishi wa wamiliki wa televisheni nchini (hawapo pichani) wakati alipokutana nao mapema hii leo jijini Dar es Salaam ili kusikiliza matatizo ya visimbuzi, kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Mhandisi James Kilaba na kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abbasi.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abbasi (kushoto) akizungumza na wawakilishi wa wamiliki wa televisheni nchini (hawapo pichani) wakati Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (katikati) alipokutana nao mapema hii leo jijini Dar es Salaam ili kusikiliza matatizo ya visimbuzi, kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Mhandisi James Kilaba.

Baadhi ya wawakilishi wa wamiliki wa televisheni nchini wakimsikiliza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) wakati alipokutana nao mapema hii leo jijini Dar es Salaam ili kusikiliza matatizo ya visimbuzi.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMUWAKILISHA RAIS JOHN MAGUFULI KATIKA UFUNGUZI WA MKUTANO MKUU WA 18 WA TPSF

$
0
0

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. kwa niaba ya Rais John Magufuli akifungua Mkutano Mkuu wa 18 wa Wanachama wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF). umefanyika leo Agosti 28/2018 Jijini Dar es salaam
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. Akiwa katika Picha ya pamoja na Washriki wa Mkutano Mkuu wa 18 wa Wanachama wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF). leo Agosti 28/2018 Jijini Dar es salaam.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. Akiwa katika Picha ya pamoja na Washriki wa Mkutano Mkuu wa 18 wa Wanachama wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF). leo Agosti 28/2018 Jijini Dar es salaam

KITUO CHA TRENI STESHENI DAR SASA KUHAMISHIWA SHAURIMOYO

$
0
0
*Ni kuanzia keshokutwa , Mkurugenzi Mtendaji TRC azungumza
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
SHIRIKA la Reli Tanzania(TRC) limesema kuanzisha keshokutwa treni inayofanya safari zake kati ya Stesheni na Ubungo na ile ya Stesheni Gongolamboto zote zitaishia eneo la Shaurimoyo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo Mkurugenzi Mtendani wa shirika la reli Tanzania, Masanja Kadogosa amesema hatua hiyo wanaendelea kuboresha eneo la Shauri Moyo na kesho wanatarajia kukamilisha mahitaji yote muhimu na baada ya hapo hapo ndipo itakuwa Shesheni ya treni hizo sambamba na ile ya mkoani.

"Hivyo wananchi wanaotumia usafiri wa treni za Dar es Salaam badala ya kuanzia Stesheni na kuelekea Ubonga au Gongolamboto sasa watakuwa wanapanda au kushuka eneo la Shauri 
moyo,"amefafanua.

Kadogosa amesema sababu za kuhamishia Stesheni hiyo Shauri moyo ni kupisha ujenzi wa Stesheni ya Reli ya Kisasa ambayo ujenzi wake unaendelea kuanzia Dar es Salaam hadi Morogoro ambapo ujenzi umefikia asilimia 22 hadi sasa.

"Kesho tunakamilisha ujenzi wa eneo hili la Shauri Moyo na kesho kutwa treni zetu zitakuwa zikianzia safari zake hapa na kumalizia hapa.Tunaomba wananchi wafahamu kuwa Stesheni tunataka kuanza ujenzi wa Shesheni ya Reli ya Kisasa.

"Ujenzi huo utafanyika kati ya miezi sita hadi nane hivyo wananchi tunaomba tuwasumbue kwa kuwahamisha.Bahati nzuri ni usumbufu wenye neema kwetu sote,"amesema.
 Mkurugenzi Mtendani wa shirika la reli Tanzania, Masanja Kadogosa akizungumza jijini Dar es Salaam leo Augusti 28,2018 wakati wa ziara ya bodi ya wakurugenzi wa shirika la reli Tanzania(TRC) kufanya ziara kwenye mradi wa reli ya kisasa, (Standard Gauge Railway )ambayo imeanzia Shaurimoyo mpaka kituo cha Soga na kuendelea mpaka Kirosa mjini Morogoro.

Baadhi ya nondo zilizosukwa kwaajili ya kutengeneza nguzo  kwaajili ya kutengeneza daraja la juu ambalo reli ya kisasa itakuwa ikipita maeneo ya Shaurimoyo Kariakoo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya nguzo zilizowekwa tayari kwaajili ya kutengeneza reli ya kisasa itakayopita juu ili kupisha shughuli nyingine za chini kuendelea kama kawaida katika eneo la shaurimoyo jijini Dar es Salaam mradi huo wa reli ya kisasa umekaguliwa leo Augusti 28,2018 na wakurugenzi wa bodi ya shirika la reli Tanzania kwaajili ya kujua maendeleo yake.
 Treni ya Pugu ikipita chini katika njia ya reli ya kati ambapo juu yake itapita reli ya kisasa itakayotumia umeme.
Picha na Avila Kakingo,lobu ya Jamii.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TRC WADHIBITI WIZI WA MAFUTA KATIKA UJENZI RELI YA KISASA

$
0
0

*Mkurugenzi Mtendaji Kadogosa asema ujenzi umekamilika kwa asilimia 22
*Wajumbe Bodi ya Wakurugenzi washuhudia kasi ya ujenzi kuanzia Dar 

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii.
MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania(TRC) Masanja Kadogosa amesema kwa sasa wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kudhibiti wizi wa mafuta huku akieleza kuna baadhi ya madereva wamefukuzwa kazi kutokana na tuhuma hizo.

Kadogosa amesema hayo leo katika eneo la Soga mkoani Pwani ambapo kuna kambi ya wafanyakazi wanaojenga Reli ya Kisasa ambapo ameelezea namna ambavyo wamedhibiti wizi wa mafuta kwa kuimarisha ulinzi kwa kushirikiana na mamlaka za ulinzi na usalama.

Sababu za kuelezea hayo ni baada ya baadhi ya waandishi waliokuwa kwenye ziara ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TRC  wakiongozwa na Mwenyekiti wao Profesa John Kondoro kutaka kufahamu hali kutokana na kuwepo kwa taarifa za uwepo wa wizi wa mafuta.

"Tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa kudhibiti wizi wa mafuta katika mradi huu.Ni tofauti na hapo awali, tumeimarisha ulinzi na sasa tumefanikiwa kudhibiti wizi huo.

"Kuna watu 30 wamekamatwa kwa tuhuma za wizi wa mafuta na tayari wamefunguliwa kesi.Pia katika kukomesha vitendo vya wizi kuna baadhi ya madereva ambao tumewafukuza,"amesema Kadogosa.


VIPI KUHUSU UJENZI WA RELI?
Akizungumzia ujenzi wa reli hiyo ya kisasa ambayo awamu ya kwanza ni kutokea Dar es Salaam hadi Morogoro, Kadogosa amewaeleza wajumbe wa bodi hiyo  kwamba ujenzi umekamilika kwa asilimia 22.

Amesema katika ujenzi wa reli hiyo kuna hatua mbalimbali za ujenzi zinazoendelea na kila eneo kwa asilimia tofauti na eneo jingine lakini kwa ujumla wake ujenzi umefikia asilimia 22 na ujenzi unaendelea kwa kiwango cha kuridhisha.

Ameongeza ujenzi wa madaraja unaendelea na tayari zimeanza kuwekwa , ujenzi wa tuta nao unaendelea na maeneo maeneo mengine wameanza kuweka kokoto kwa ajili ya kuanza kutandika mataluma.
 Mradi mradi wa reli ya kisasa ya standard gauge ulipofikia baadhi ya maeneo.
 Mataaluma yakiwa tayari kwaajili ya kwenda kuwekwa kwenye maeneo ambayo reli ya kisasa itapita. 
Maeneo yanayoendelea kujengwa reli ya kisasa eneo la Mlandizi.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya jamii.
 

PANITA, ASASI ZA KIRAIA WATOA USHAURI KWA SERIKALI KUHUSU NAMNA BORA KUBORESHA HALI YA LISHE NCHINI

$
0
0
Tumaini Mikindo Mkurugenzi mtendaji wa PANITA  akitoa salamu kwa niaba ya Asasi za Kiraia kwa Waziri Jaffo wakati wa kikao hicho
Picha ya pamoja na Makatibu tawala waliohudhulia kikao

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii.
SERIKALI kupitia Halmashauri imeshauriwa kujenga tabia ya kutenga fedha kupitia mapato yao ya ndani ili kuweka mfumo thabiti na endelevu katika kuboresha hali ya lishe na ambao utajengeka juu ya msingi bora unaowekwa na fedha za wafadhili pindi miradi hii itakapokwisha.


Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa PANITA Tumaini Mikindo kwa niaba ya Asasi za kiraia ambazo zimejikita katika masuala ya lishe nchini wakati wa kikao kati ya na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi) Suleiman Jaffo.

Lengo la kikao hicho kimekutana kwa ajili ya kuifanya tathimini taarifa ya utekelezaji wa mkataba wa lishe baina ya Makamu wa Rais, Wakuu wa Mikoa wa Tanzania Bara na viongozi wengine wa ngazi mbalimbali.

Hivyo Mikindo ameshauri ni vema pia halmashauri ziweke vipaumbele kwenye afua za lishe ambazo zitaleta matokeo chanya kwa haraka. Pia Serikali iongeze bajeti ya lishe kutoka Sh.1,000 ya sasa kwa mtoto hadi kufikia Sh. 23,000 ambayo ni takribani dola 8.5 za kimarekani kwa mwaka kwa kila mtoto chini ya miaka mitano na iwapo wanalenga kufikia maazimio ya Baraza la Afya Duniani (WHA) kuhusu lishe kufikia 2025. 

"Baada ya maneno haya machache namshukuru Waziri Jafo kwa kutushirikisha katika kikao hiki adhimu cha kujadili utekelezaji wa mkataba wa lishe,"amesema Mikindo kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa leo kuhusu kikao hicho cha tathimini.

Awali wakati anaanza kuzungumza Mikindo amesema asasi za kiraia zinatoa shukrani kwa Waziri Jaffo kwa kuwaalika kwenye mkutano huo na kwao ni fursa ya kutoa maoni yao kuhusu lishe nchini.

"Hii ni uthibitisho tosha Serikali ya Awamu ya tano chini ya Rais Dk.John Magufuli inavyothamini na kutambua mchango wa wadau ikiwemo Asasi za kiraia katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya taifa hili kuelekea uchumi wa kati kupitia viwanda ifikapo 2025.Waziri tunaomba utufikishie shukurani zetu za dhati kwa Rais,"amesema. 

Aidha amesema wanamshukuru Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kwanza kwa kukubali kuwa kinara wa lishe na pili kwa kutimiza ahadi aliyoitoa siku ya uzinduzi wa ripoti ya lishe ya dunia nchini Tanzania Julai 20 mwaka 2016 jijini Dar es Salaam.

"Naomba nirejee baadhi ya maneno aliyoyatamka siku hiyo. Ninanukuu, “…Ni kweli kwamba kwenye “Political will” jambo lolote linaweza likafanyika; kwa hiyo niseme kwamba na hili suala la lishe tutalipa msukumo mkubwa wa kisiasa ili kila mmoja wetu aimbe lishe na kupunguza Utapiamlo,"amesema wakati anatoa nukuu hiyo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MTOTO WA JINSIA MBILI YA KIKE NA KIUME AZALIWA MULEBA MKOANI KAGERA

$
0
0
Na Dotto Mwaibale, Kagera
MTOTO wa Jinsia mbili ya kike na kiume amezaliwa katika Hospitali Teule ya Rubya iliyopo wilayani Muleba mkoani Kagera.

Kuzaliwa kwa mtoto huyo kumethibitishwa na Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dkt.Geore Kasibante (pichani), ambaye alisema hali ya mtoto huyo kuwa inaendelea vizuri na kuwa wakati wowote atapelekwa hospitali kubwa kwa ajili ya uchunguzi ili afanyiwe upasuaji kwa vile katika hospila hiyo hawana madaktari bingwa wa kuweza kufanya upasuaji huo.

WAKUTUBI WAPATIWA MAFUNZO YA KUHIFADHI TAFITI KWA NJIA YA TEHAMA

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa tume ya Sayansi na Teknolojia , Dkt .Amos Nungu akizungumza na watalaamu wa Maktaba wakati akifungua mafunzo ya Tehama kwa wakutubi  kutoka taasisi mbalimbali nchini
 Kaimu Mkuu wa Chuo cha Biashara cha CBE , Profesa  Frolence  Luoga, akizungumza wakati wa Mkutano wa wakutubi juu ya masuala ya Tehama katika kuhifadhi tafiti zinazofanywa hapa nchini na nje ya nchi kwa ajili ya kusoma.
 Sehemu ya Wakutubi walioshiriki  mafunzo ya kuhifadhi tafiti kwa njia ya Tehama wakisikiliza somo kwa makini
Mkurugenzi Mkuu wa tume ya Sayansi na Teknolojia , Dr .Amos Nungu akiwa katika picha ya Pamoja na wakutubi walioshiriki mafunzo ya Tehama kwa ajili ya kutunza tafiti katika Maktaba

Wapelelezi wa Kodi Afrika Mashariki Kushirikiana Kupambana na Uhalifu

$
0
0
Na Oliver Njunwa 

Wapelelezi wa Kodi wa Mamlaka za Mapato Afrika Mashariki wametakiwa kuharakisha mchakato wa kuandaa mtaala wa kuwajengea uwezo wapelelezi wa kodi pamoja na mfumo wa kisheria ili kuweza kushirikiana katika kupambana na uhalifu katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Wito huo umetolewa na Kaimu Naibu Kamishna wa Upelelezi wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Salim Kessi wakati akifungua Mkutano wa Wajumbe wa Kamati ya Ufundi ya Makamishna wa Upelelezi wa Kodi wa Mamlaka za Mapato Afrika Mashariki unaofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu Zanzibar.

“Tunataka mchakato huu umalizike mapema ili tuweze kupambana na uhalifu katika ukusanyaji wa kodi kwani kadri tunavyochelewa ndivyo na wahalifu wanaendelea kusababisha upotevu wa kodi kwa mamlaka zetu za mapato”, alisema Bw. Kessi.

Aliongeza kwamba kwa siku nne ambazo watakuwa Zanzibar wanatakiwa kukamilisha hiyo kazi ili iweze kuwasilishwa katika kikao cha Makamishna wa Upelelezi wa Kodi Afrika Mashariki ambao walikubaliana kushirikiana kufanya upelelezi wa kodi kwa pamoja kupampana na kudhibiti uhalifu katika masuala ya kodi.
Kaimu Naibu Kamishna wa Upelelezi wa Kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Salim Kessi akisisitiza jambo wakati akifungua mkutano wa Kamati ya wapelelezi wa Kodi Afrika Mashariki. 
Wajumbe wa Kamati ya wapelelezi wa kodi wakifuatilia kwa makini hotuba ya Kaimu Naibu Kamishna wa Upelelezi wa Kodi TRA Salim Kessi (hayupo katika picha) wakati akifungua rasmi mkutano. 
Wajumbe wa Mkutano wa Kamati ya Wapelelezi wa Kodi Afrika Mashariki katika picha ya Pamoja na Kaimu Naibu Kamishna wa Upelelezi wa Kodi TRA Salim Kessi (katikati walioketi) mara baada ya ufunguzi wa mkutano katika ukumbi wa Benki Kuu Zanzibar. 


BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 28.08.2018

WAZIRI LUGOLA ATOA MAAGIZO KUHUSU UMILIKI WA ARDHI KWA WIZARA ZILIZO MAMBO YA NDANI

MICHUZI TV: SERIKALI YATOA VIBALI VYA UINGIZAJI NYAVU ZA UVUVI KWA WANAOFUATA SHERIA

Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images