Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110151 articles
Browse latest View live

MKUU WA WILAYA NAMTUMBO AWAOMBA WAWEKEZAJI KUJENGA KIWANDA CHA SOYA ILI KUONGEZA THAMANI YA ZAO HILO

$
0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

MKUU wa Wilaya ya Namtumbo Sophia Mfaume ametoa ombi kwa wawekezaji kuwekeza kwa kujenga kiwanda ambacho kitaisaidia kuongeza thamani ya zao la Soya ambalo linalimwa kwa wingi wilayani hapo.

Mfaume ametoa ombi hilo leo wakati anazungumzia jitihada zinazofanywa na wakulima wa Wilaya ya Namtumbo na hasa katika zao la Soya.

Amesema ombi kubwa ni kupata kiwanda cha Soya ndani ya Wilaya ya Namtumbo kwani kitakapojengwa kitasaidia kuongeza thamani ya zao la Soya."Tunaomba muwekezaji iwe anatoka Marekani au Taifa lolote aje awekeze kwa kujenga kiwanda cha kuchakata Soya kwa lengo la kuongeza thamani ya zao hili.

" Kwa mwaka huu wakulima wamepata tani 50,000 za Soya na kukiwa na kiwanda ambacho kitasaidia kuongeza thamani wanaweza kuzalisha zaidi ya tani za mwaka huu,"amesema.

Mfaume amesema kuwa mbali ya kuomba kiwanda kwa ajili ya kuongeza thamani ya zao la Soya ,pia ombi lao lingine ni kiwanda cha mbolea.Amefafanua changamoto waliyonayo wakulima ni mbolea na hivyo kukiwa na kiwanda katika wilaya hiyo watakuwa na uhakika wa mbolea na hivyo kuongeza uzalishaji.

Awali wakati anazungumzia zao la Soya amesema wakulima wengi wanalitumia zao hilo kwa chakula na chakuka cha wanyama.Amefafanua kuwa Soya inaweza kuzalisha maziwa,Soseji na nyama lakini hiyo ili ifanyike kunahitajika kiwanda cha kuchakata Soya.

TRA YATAJA WALENGWA WANAOSTAHILI MSAMAHA WA RIBA NA ADHABU YA MALIMBIKIZO YA KODI

$
0
0
Na Veronica Kazimoto-Tabora

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewataja walengwa wanaostahili kuomba msamaha maalum wa riba na adhabu ya malimbikizo ya madeni ya kodi kwa asilimia 100 ambapo mwisho wa kutuma maombi ya msamaha huo ni tarehe 30 Novemba, 2018. 

Akizungumza wakati wa mkutano wa washauri wa walipakodi (Tax consultants) mkoani Tabora, Afisa Elimu Mkuu kwa Mlipakodi wa mamlaka hiyo Rose Mahendeka amesema Walengwa wa msamaha huu ni makampuni, taasisi na watu binafsi ambao wamewasilisha ritani za kodi lakini bado wanadaiwa kodi yote au sehemu ya kodi zitokanazo na ritani hizo.

"Walengwa wengine ni wale wote ambao hawajawasilisha ritani za kodi, hawajasajiliwa na kupatiwa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) au Namba ya Usajili wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na wale walio wasilisha pingamizi au rufaa za kodi ambazo bado zinashughulikiwa katika ofisi za TRA, Bodi ya Rufaa na Mahakama ya Rufani za kodi", alisema Mahendeka.

Aidha, amewataja wasiohusika na msamaha huu kuwa ni pamoja na wale ambao wangestahili kupata msamaha lakini tayari wameshalipa madeni yao, ambao masuala yao ya kikodi yapo katika hatua ya ukaguzi au uchunguzi, wana madeni ya nyuma ya kodi ambayo yanatokana na kesi za jinai za kodi, utakatishaji fedha, usafirishaji wa binadamu au shughuli nyingine haramu kama ilivyothibitika kisheria.

"Wengine ambao hawahusiki na msamaha huu ni taasisi, makampuni na watu binafsi ambao wana madeni ya nyuma ya kodi yanayotokana na adhabu zilizoamuliwa tayari au adhabu za makosa yatokanayo na uzembe wa kukusudia uliobainika kisheria pamoja na wenye riba au faini zilizotokana na kutoa au kutumia risiti za kielektroniki za kughushi," alibainisha Mahendeka.

Kwa upande wake Afisa Elimu kwa Mlipakodi wa TRA Chama Siriwa ametoa wito kwa washauri wa walipakodi mkoani hapa kuendelea kuwaelimisha wafanyabiashara na wale wote wenye taasisi na makampuni mbalimbali yenye malimbikizo ya madeni ya kodi kuwahi kutuma maombi ya msamaha huo kabla muda uliopangwa haujamalizika.

"Mimi napenda tu kusisistiza kuwa mwisho wa kutuma maombi ya msamaha huu ni tarehe 30 Novemba, 2018. Hivyo, natoa wito kwenu washauri wa walipakodi muendelee kuwaelimisha wafanyabiashara na wote wenye taasisi na makampuni kutuma maombi mapema ili waweze kunufaika na msamaha huu," alieleza Siriwa.

Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania ilitangaza msamaha wa riba na adhabu ya malimbikizo ya madeni ya kodi mwezi Julai, 2018 kwa lengo la kutoa unafuu kwa walipakodi wenye malimbikizo ya madeni ya riba na adhabu kwa kusamehe madeni yao na kuwapa fursa ya kulipa malimbikizo ya madeni ya msingi ya kodi - principal tax mara moja au kwa awamu ndani ya mwaka wa fedha wa 2018/19.

MAHAKAMA YASEMA MKURUGENZI WA ZAMANI WA TBC TIDO MHANDO ANA KESI YA KUJIBU

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii

MAHAKAMA  ya Hakimu Mkazi Kisutu imedai kwamba  Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando anayekabiliwa na mashtaka ta matumizi mabaya ya madaraka ana kesi ya kujibu.

Uamuzi huo umetolewa leo mahakamani hapo na Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shahidi baada ya upande wa mashtaka kufunga kesi yao kwa kuleta mashahidi watano.

Hakimu Shaidi amesema amepitia ushahidi wote wa mashahidi watano ulioletwa na upande wa mashtaka na kuona mshtakiwa ana kesi ya kujibu.Katika kesi hiyo Tido anakabiliwa na mashtaka manne ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh.milioni 887.1.

Kabla ya kutolewa kwa uamuzi huo, leo shahidi wa tano wa upande wa mashtaka, Dominic Mahundi alitoa ushahidi wake.Miongoni mwa  mashahidi  wa upande wa mashtaka waliotoa ushahidi ni ofisa uchunguzi wa Takukuru, Victor Lesuya;  mwanasheria wa TBC, Gwakisa Mlawa na mkurugenzi Mkuu mstaafu wa TBC, Clement Mshana.

Katika kesi hiyo inadaiwa kuwa Juni 16, mwaka 2008 akiwa  Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Tido  aliyekuwa Mkurugenzi wa TBC, kwa makusudi alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mkataba wa kuendesha na utangazaji wa vipindi vya televisheni kati ya TBC na Channel 2 Group Corporation (BV1) bila ya kupitisha zabuni, kitu ambacho ni kinyume na Sheria ya Manunuzi na kuinufaisha BVl.

KESI YA VIGOGO TISA CHADEMA ITATAJWA SEPTEMBA 27 MWAKA HUU

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii

KESI dhidi ya vongozi tisa wa Chadema akiwamo Freeman Mbowe wanaokabiliwa na mashtaka 13 likiwemo la uchochezi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, itatajwa Septemba 27 mwaka huu.

Washtakiwa hao walipaswa kusomewa Maelezo ya awali leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri lakini imeshidikana kwa sababu mshtakiwa wa tano, Esther Matiko hakuwepo mahakamani na mdhamini wake alieleza kuwa anatatizo la kiafya kwenye mfumo wa uzazi.

Pia Wakili Peter Kibatala anayewatetea washtakiwa hao, aliieleza Mahakama kuwa mshtakiwa Peter Msigwa ambaye ni Mbunge wa Iringa Mjini alikuwa akitetewa na Wakili Jeremiah Mtobesya ambaye amejitoa.

Aidha, mshtakiwa Peter Msigwa aliiomba Mahakama kuandikia hati ya wito (Summons) Mahakama ya Iringa kwa kuwa muda mwingi yupo katika Mahakama ya Kisutu na yeye bado ana kesi kwenye mahakama hiyo.

Pia ameiomba Mahakama impatie muda wa wiki tatu ili aweze kutafuta wakili mwingine,Washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendajia jinai kati ya Februari 1 na 16, mwaka 2018, Dar es Salaam.

Mbali Mbowe na Msigwa wengine ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu na Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa Kibamba John Mnyika, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe Halima Mdee na mbunge wa Bunda Esther Bulaya.

Wengine ni Mbunge wa Tarime Mjini Esther Matiko na katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk. Vincent Mashinji.
Viongozi wa Chadema wanaokabiliwa na mashtaka 13 likiwemo la Uchochezi

UBALOZI WA MAREKANI NCHINI TANZANIA WAGAWA MAGARI MATANO KWA MIKOA YA NYANDA ZA JUU KUSINI

$
0
0
Nchi ya MAREKANI kupitia ubalozi wake nchini Tanzania na kuwakilishwa na kaimu balozi INMI PATTERSONI umegawa magari matano kwa tume ya kudhibiti UKIMWI nchi TACAIDS katika mikoa ya nyanda za juu kusini ikiwemo RUVUMA,MBEYA,KATAVI,RUKWA NA SONGWE kwa ajili ya kwenda kudhibiti maambukizi wa ugonjwa wa UKIMWI katika mikoa hiyo ambapo ugawaji wa magari hayo umefanyika mkoani Ruvuma na kukabidhiwa kwa waziri ofisi ya waziri mkuu sera ,bunge ,ajira,na watu wenye ulemavu mh JENISTER MHAGAMA

TATIZO LA NYAVU KWA WAVUVI ZIWA VICTORIA LATATULIWA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega ameendelea na ziara yake katika ukanda wa ziwa Viktoria katika kugagua na kuangalia utekelezaji wa sekta hiyo.

Baada ya malalamiko ya wavuvi kuhusiana na nyavu hasa za dagaa wamejiridhisha kuwa na tatizo na wametoa idhini ya uingizaji wa nyavu nchini ili kumaliza tatizo hilo.Ulega ameeleza kuwa nyavu chini ya milimita nane kutumika kuvulia dagaa ni shida na haikubaliki na zile zenye macho ya inchi 26 zinafaa zaidi.

Kuhusu ukataji wa leseni Ulega amesema kuwa wasiofuata taratibu lazima wakamatwe na wafanyabiashara wote lazima wawe na vibali maalumu vya kufanya shughuli za uvuvi.Aidha amesema kuwa wana maboresho ya sheria na kanuni za uvuvi na kodi ili wafanyao shughuli hizo kuwa na uwezo wa kutambua shughuli wanazozifanya.

Kuhusu kuingiza nyavu haramu Ulega amesema kuwa wamejipanga na watachukua hatua kwa wale wote watakaokiuka kanuni na sheria katika kuhakikisha sekta hiyo inakwenda mbele na Wizara hiyo haina tatizo na watu watakaofata sheria.

Makabidhiano hayo kuwakabidhi wafanyabiasharavibali vya kuagiza nyavu nchini yamefanyika katika mpaka wa Tanzania na kenya Sirari.Wafanyabiashara hao wameishukuru Serikali kwa kuwapatia vibali vya kuingiza zana hizo na wamehaidi kufanya kazi kwa kufuata sheria kwa manufaa yao na ya taifa kwa ujumla.

Naye Meneja wa kiwanda cha Musoma Fish, George Fernandez ameishukuru sana Serikali kwa kuendelea na kupambana na uvuvi haramu kwa sasa samaki wanapatika kwa wingi na amesema kiwanda hicho kinafata sheria ya kutokuchakata samaki ambao sheria haiwatambui na wanalipa kodi kulingana na sheria inayo waelekeza ili kuongeza mapato kwa Serikali.
  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akimkabidhi  mfanya biashara,Majani Masangati  kibali cha kuingiza nyavu za Uvuvi nchini ambapo amewaomba wafanyabiasha wote  waingize zana hizo kwa kufaata sheria za nchi.(picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii) 
 Naibu Waziri wa  Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Musoma, John Kayombo na viongozi wengine wakikagua uzalishaji wa kiwanda cha samaki  Musoma Fish.
 Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akisalimiana na Mkurugenzi halmashauri ya wilaya ya Musoma,John Lipesi Kayombo mara baaday a kuwasili mkoa wa Mara.

Watanzania Enzini Mila na Desturi nzuri Rithisheni Vizazi vijavyao

$
0
0
Na. Vero Ignatus. ARUSHA

Watanzania wameshauriwa kuenzi mila na desturi nzuri ili kuzirithisha kwa vizazi vijavyo na kuwa na Taifa lenye utamaduni madhubuti.

Rai hiyo imetolewa katika tamasha linalokutanisha familia 172 zenye jumla ya watu 323 kutoka katika kabila la wanyambo kutoka wilaya za Karagwe na Kerwa waishiao mkoani Arusha. Akizungumzia lengo la tamasha hilo mwenyekiti kikundi cha Kanono Wilbard Ngambeki amesema lengo kubwa ni kuimarisha umoja na kuzifanya familia zilizozaliwa kufahamu tamaduni zile nzuri za wazazi wao.

'' Katika tamasha hili michezo imekuwa ni kivutio kikubwa, wazazi wanawaleta watoto wao ila sisi tunapitisha mila zetu na desturi zetu njema kwao ili wakue wakitambua wazazi wao ndipo tulipotoka hata watakapokuwa kwenye miji mingine ya watu mbali na wazazi wao.''

Ngambeki amesema umoja huo wa Kundi la Kanono tayari walishaanzisha Saccos ambayo inawanachama 105 waliojiunga na tayari wameshakopeshana zaidi ya milioni 800 kwa riba nafuu. Afisa Ushirika Jiji la Arusha Huruma Kibendwa aliyekuwa mgeni rasmi katika tamashaa hilo amepongeza umoja kwa kuwa na saccos ambayo inawasaidia kukopeshana wao kwawao na kujikwamua kiuchumi na kimaendeleo

'' Kwani mara nyingi tunawashauri wanamchi wajiunge kwenye vikundi ili waweze kujikwamua kiuchumi kwa kukopeshana wao kwa wao mkopo wenye riba nafuu uzuri kikundi hiki kimesajiliwa na mna saccos inayofanya vizuri '' Alisema Kibendwa.
Mgeni rasmi Afisa Ushirika Jiji la Arusha Huruma Kibendwa akimkabidhi cheti mmoja wa kundi la Kanono, aliyepo kushotonkwake ni Mwenyekiti wa Kundi la Kanono Wilbald Ngambeki, na wakwanza kulia ni Davis Kalegea mtendaji wa kundi hilo. 
Wakina mama pamoja na wanaume kutoka kabila la Wanyambo waishio mkoani Arusha wakifanya maandalizi ya kutengeneza vyakula vya asili katika tamasha hilo. Picha na Vero Ignatus
Maandalizi ya chakula cha asili yakiendelea kama inavyoonekana pichani.


VIWANDA VYA SARUJI VYATAKIWA KUZALISHA SARUJI YA KUTOSHA PAMOJA NA KUSIMAMIA BEI YA SOKONI

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

SERIKALI imesema kuwa wenye viwanda vya saruji wazalishe saruji ya kutosheleza mahitaji ya ndani pamoja na kusimamia bei ya bidhaa hiyo mpaka kwa mlaji wa mwisho.

Hayo ameyasema Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charle’s Mwijage wakati alipotembelea viwanda vya Saruji vya Camel na Twiga , amesema amekosa hivi usingizi kwa kuadimika kwa saruji nchini na kuwataka viwanda hivyo vizalishe saruji ya kukidhi mahitaji ya ndani kutokana na kuwepo miradi mbalimbali ya ujenzi.

Mwijage amesema kuwa hivi karibuni kulikuwa kuadimika kwa saruji iliyotokana na baadhi ya viwanda kuwa katika matengenezo pamoja na makaa ya mawe kuzalishwa kwa kiwango kidogo.Amesema kuwa katika kusimamia wizara hiyo kwa mzalishaji ambaye hatakwenda na kasi ya uzalishaji wa saruji anatomlaka ya kuifuta leseni hivyo wenye viwanda lazima wakidhi mahitaji ya saruji.

Aidha amesema kuwa kwa mwaka tani milioni 10.5 zinalishwa hivyo lazima kila kiwanda kiongeze uzalishaji na kuweza kuuza hata masoko ya nje ya nchi kwa kupata fedha za kigeni zinazotokana na saruji.Amesema kuwa kuna viwanda vitatu vya saruji vinajengwa nchini ambavyo vitaongeza uzalishaji wa wa saruji hiyo.

Mwijage amesema kuwa viwanda vikizasha saruji na kuweza kuuza katika masoko ya nje kuna uwezekano wa bidhaa ya saruji ikwa inachangia uchumi wa nchi na kuongoza katika uchangiaji huo kwa pato la taifa.Meneja wa Masoko wa kiwanda cha Saruji cha Twiga , Danford Semwenda amesema kuwa kwa sasa wanazalisha tani 6000 kutoka tani 300O kwa siku 15 zilizopita iliyotokana na matengenezo ya mtambo.

Waziri Mwijage leo Augusti 27,2018 ametembelea viwanda vya kutengeneza Saruji kuanzia cha Camel kilichopo Mbagala rangi Tatu na cha Twiga kilichopo Tegeta jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akitembelea kiwanda cha Camel kilichopo Mbagala jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuangalia utendaji kazi wa kiwanda hicho kutokana na kukosekana kwa saruji hapa nchini.
  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akitembelea kiwanda cha Twiga kilichopo Tegeta jijini Dar es Salaam na kushoto ni Mkurugenzi Mkuuwa Kiwanda cha Twiga, Alphonso Velez.
 Mchanga wa kutengeneza Saruji katika kiwanda cha Saruji cha Twiga Tegeta jijini Dar es Salaam.

Meneja wa Masoko wa kiwanda cha Saruji cha Twiga , Danford Semwenda akijibu swali kutoka kwa  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alipotembelea kiwanda cha Twiga kilichopo Tegeta jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mkurugenzi Mkuuwa kiwanda cha Twiga kilichopo Tegeta jijini Dar es Salaa, Alfonso Velez.

Vyama visivyokuwa na Ruzuku vyaitaka Chadema iache kuingilia wagombea wake

$
0
0
Katibu Mkuu wa Chama cha AFP Taifa, Rashid Mohamed akizungumza na waandishi wa habari  kupinga Tamko la ubalozi wa Marekani kuhusu uchaguzi wa Igunga na kutaka Chadema isiwaingilie kwenye maamuzi yao

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
UMOJA wa vyama visivyokuwa na Ruzuku nchini ikiwemo chama cha AAFP, DP pamoja na Chama cha Demokrasia Makini wamelaani vitendo vya wagombea wa vyama hivyo kujiunga na chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kulalamikia tume ya uchaguzi kutotenda haki kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge kwenye jimbo la Korogwe vijijini.
Wakizungumza na Waandishi wa Habari leo, Katibu mkuu wa chama cha AAFP Rashid Mohamed Rai amesema kuwa baada ya kukagua fomu ya mgombea wa chama chake alibaini kuwa kuna baadhi ya tozo ambazo mgombea huyo alikuwa hajalipia licha ya kutumiwa fedha hizo na baada ya hapo akalalamika kuwa miongoni mwa watu ambao fomu zao hazijapokelewa wakati alikuwa hana vigezo na fomu yake ingekataliwa kwasababu hakulipia fedha za baadhi ya ada za uchaguzi.
“Kuna baadhi ya  magenge ya matapeli ambao wamevamia hivyi vyama kwa nia tofauti, kuna watu wanachukua fomu kwa nia ya kugombea wanaweka mfukoni halafu baada ya muda wanaanza kulalamika ukimwambia lete fomu uangalie unakuta yeye mwenyewe hakujaza fomu aliiweka tu” alisema
“Mfano mzuri ni Mgombea wangu, hata ile hela ya uchaguzi ya tume hakulipa halafu siku ya uchaguzi ananiambia fomu haipokelewi na mkurugenzi hayupo mpaka mida ya saaa 9 nauliza wenzake pale wananiambia bado mgombea huyo hajafika eneo la kurudisha fomu, anaingia pale saa 10 na yeye anaungana na hao wanaolalamika kuwa wamefamnyiwa ubaya” aliongeza Rai.
Amebainisha kuwa uchukuaji wa fomu na urejeshaji ni tofauti lakini baadhi ya watu walikuwa wakidanganya ili kutengeneza mazingira ya kugombanisha tume na vyama vya siasa kwa nia mbaya, ambapo CHADEMA waliungana na Mgombea wao na kuanza kutumia maneno makali akilalamikia tume jambo ambalo ni uongo.
“Kama hata ada hakulipa lakini na eye anaungana kwenye mkutano wa  Chadema halafu anatoa povu hapo unajua kabisa kuwa kuna baadhi ya watu wamekuwa wakiwaambia wasirudishe fomu” aliongeza Rai kwenye taarifa yake
Kwa upande wake Naibu katibu mkuu wa chama cha DP Abdul Mluya amesema kuwa alipokea simu kutoka kwa mgombea wake majira ya saa saba akilalamika kuwa hamuoni mkurugenzi lakini baada ya hapo alikuja kupata kipande cha video ya mgombea wake akiwa kwenye ofisi ya Chadema akilalamika wakati CHADEMA haina mahusiano mazuri na chama cha DP.
“Sisi DP na Vyama wenza ambavyo havina ruzuku tutaungana  wakati tukienda kwenye uchaguzi wa Monduli kushiriki uchaguzi wa marudio lazima tupite korogwe tuonane na mkurugenzi tukajue tatizo lilikuwa ni lipi kisha tutatoa tamko pamoja au chama kimoja kimoja” alisema Mluya
Aidha amebainisha kuwa  kuna baadhi ya watu ambao wamekuwa wakiwapigia simu wagombea wa vyama hivyo wanaoshiriki uchaguzi wa marudio kwenye Jimbo la Monduli, wakiwatishia na kuwaambia wajiunge na vyama vyao na wawaunge mkono na kusema kuwa vyama hivyo vitaenda kushughulika na kuhakikisha wanakabiliana na watu hao wenye nia mbaya ya kugombanisha tume na Vyama Vyao.

LUGOLA AMSWEKA NDANI MKUU WA KITUO KIKUU POLISI MTWARA KWA KUSHINDWA KUWAWEKA MAHABUSU WATUHUMIWA

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akimuuliza maswali Mkuu wa Kituo cha Polisi Mtwara mjini, Ibrahim Mhando (kushoto) baada ya kushindwa kuwaweka mahabusu watuhumiwa wanne akiwemo Mhandisi Mshauri wa Kampuni ya Y&P Architects ambaye ni mshauri mkuu wa ujenzi wa Ofisi Kuu ya Uhamiaji Mkoani Mtwara. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali, Jacob Kingu. Wapili kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Lucas Mkondya. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akitoka Kituo cha Polisi cha Kati mjini Mtwara mara baada ya kumsweka ndani Mkuu wa Kituo cha Polisi hicho ambaye aliwaweka watuhumiwa chumba cha upelelezi badala ya mahabusu kituoni hapo. Nyuma ya Waziri ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali, Jacob Kingu. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Lucas Mkondya. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akimuangalia Mkurugenzi wa Ufundi wa Kampuni ya Ujenzi ya Lucas, ambaye pia kandarasi aliyejenga Jengo la Uhamiaji Mkoa wa Mtwara, Theophilius Kessy, wakati alipokua anambana maswali ya kutaka kujua kwanini Jengo la Uhamiaji Mkoa wa Mtwara limejengwa chini ya kiwango. Aliyeshika kitabu ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali, Jacob Kingu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.   
                                                                                                                         
Na Mwandishi Wetu, Mtwara
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amemweka ndani Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Kati mjini Mtwara (OCS), Ibrahim Mhando, kwa kushindwa kuwaweka mahabusu watuhumiwa wanne akiwemo Mhandisi Mshauri wa Kampuni ya Y&P Architects ambaye alitoa taarifa ya uongo kwa Waziri huyo kuhusu ujenzi wa Makao Makuu ya Uhamiaji Mkoani humo.

Tukio hilo lilitokea saa 12:46 asubuhi Agosti 27 leo Jumatatu, wakati Waziri Lugola na Katibu Mkuu wa Wizara yake, Meja Jenerali, Jacob Kingu walipofika Kituo hicho kikuu cha mkoa kwa kushtukiza wakati alipokua anakwenda Uwanja wa Ndege kwa ajili ya kurudi jijini Dar es Salaam, ndipo Waziri huyo alitaka kuthibitisha kama mtuhumiwa ambaye alielekeza jana usiku akamatwe awekwe mahabusu endapo Polisi walitekeleza agizo lake.

Hata hivyo, Waziri Lugola alimkuta mtuhumiwa huyo, Benjamin Kasiga akiwa chumba cha upelelezi badala ya kuwekwa mahabusu ya polisi hiyo, ndipo akamuuliza Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Lucas Mkondya, kwanini agizo lake halijatekelezwa.

“Hivi ndivyo polisi mnafanya hivi, haya ndio madudu mnayoyafanya? Tabia hii siku zote tunaipinga ikichafua Jeshi la Polisi, na hii ndiyo tabia yenu, najua ndio mana nimekuja ghafla, mnafahamu maadili ya Jeshi? RPC hawa polisi wako wanafanya nini, OCS njoo hapa, kwanini umeweka hawa watuhumiwa chumba cha upepelezi badala ya mahabusu, nawe unaingia ndani kwa kushindwa kuwaweka ndani hawa watuhumiwa, RPC muweke ndani sasa hivi huyu,” alisema Lugola akiwa amekasirika. 

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo (RPC), Mkondya alimweleza Waziri Lugola kituoni hapo kuwa, Polisi wake walifanya makosa kwa kutowaweka mahabusu watuhumiwa hao.

Kwa upande wake mkuu wa kituo huyo, Mhando kabla ya kuwekwa mahabusu pamoja na wale watuhumiwa ambao alishindwa kuwaweka mahabusu, alisema sababu kuu yakutowaweka mahabusu watuhumiwa hao ni kwasababu mahabusu ilijaa na wanafanya hivyo mara chache inapotokea mahabusu wamekuwa wengi kituoni hapo. 

DKT MPANGO-AAGIZA MAKONTENA YA MAKONDA YAPIGWE MNADA LICHA YA VITISHO VYAKE

$
0
0
Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amefanya ziara ya kushitukiza katika eneo la kuhifadhia makontena-Bandari Kavu Dar es Salaam (DICD), na kukagua makontena 20 yaliyoingizwa nchini na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na kuiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania -TRA kuendelea na mnada wa makontena hayo ili kupata kodi ya Serikali inayokadiriwa kufikia shilingi bilioni 1.2.

Dkt. Mpango amesema kuwa kodi hiyo inadaiwa kwa mujibu wa sheria za nchi baada ya mwenye mali kushindwa kulipa kodi na kwamba amesikitishwa na vitisho vinavyotolewa na Mkuu huyo wa Mkoa na vilivyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini  akitumia vifungu vya Biblia kwamba yeyote atakaye nunua mzigo huo atalaaniwa.

"Sheria za nchi hazichagua sura wala cheo cha mtu, na mimi ndicho nilicho apa, kutekeleza sheria za nchi, sheria za kodi, ndiyo dhamana niliyo pewa kwahiyo Kamishna, simamia sheria za kodi bila kuyumba" alisisitiza Dkt. Mpango akitoa maelekezo kwa Kamisha wa Forodha Bw. Ben Usaje.

Alifafanua kuwa mzigo wa Samani ulioagizwa kutoka nje ya nchi hauna msamaha wa kodi na kwamba huyo aliye agiza (RC Paul Makonda) alipe kodi stahidi na asipo lipa kodi hiyo mchakato unaoendelea wa kuyapiga mnada makontena hayo uendelee.

"Napenda niwaombe viongozi wenzangu Serikalini, ni muhimu tukachuja maneno! unasema mtu anayekuja kununua samani atapata laana, tena laana ya Mungu, kwa nini tunamhusisha Mungu kwenye vitu vya namna hii" alieleza kwa masikitiko Dkt. Mpango

Dkt. Mpango alitoa wito kwa watanzania wanaotaka kununua bidhaa hizo ambazo nyingi ni vifaa vinavyoweza kutumika shuleni ama maofisini kama vile viti meza na makabati, kujitokeza bila hofu kununua mali hizo.
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akiwasili kukagua Kontena  ishirini za Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Paul makonda, zilizo na Samani vikiwemo viti na Meza katika Bandari ya Dar es Salaam.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akifunguliwa Kontena Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Paul Makonda, zenye Samani za Viti na Meza ili kushuhudia kilichopo kabla hajaagiza taratibu za mnada ziendelee ili kodi inayodaiwa ya thamani ya Sh. Bilioni 1.2 iweze kupatikana.
 Baadhi ya meza zilizopo katika moja ya Kontena  ambazo  zinadaiwa kodi ya Sh. Bilioni 1.2, wakati Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) alipofanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam na kuagiza Kamishna wa Forodha kuchukua hatua za kisheria ikiwemo kupigwa mnada kwa vifaa hivyo ili kodi ya Serikali ipatikane.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akitoa maagizo kwa Kamishna wa Forodha  wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Benny Usaje, ya kuendelea kupigwa mnada kwa Kontena ishirini za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Paul Makonda, zinazodaiwa kodi ya Sh. Bilioni 1.2 ili Serikali iweze kupata kodi yake kama kodi kutoka kwa mmiliki wa Kontena hizo hatalipa kodi kwa wakati.
Baadhi ya meza zilizopo katika moja ya Kontena  ambazo  zinadaiwa kodi ya Sh. Bilioni 1.2, wakati Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) alipofanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam na kuagiza Kamishna wa Forodha kuchukua hatua za kisheria ikiwemo kupigwa mnada kwa vifaa hivyo ili kodi ya Serikali ipatikane.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA KUAPISHWA KWA MAJAJI WATEULE WATATU WA MAHAKAMA YA AFRIKA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu Mhe. Jaji Sylvain Ore muda mfupi kabla ya kuapishwa kwa Majaji wapya watatu wa mahakama hiyo mjini Arusha. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla ya kuapishwa kwa majaji wapya watatu wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu mjini Arusha.
  Majaji watatu wapya wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu wakiwa wameketi pamoja muda mfupi kabla ya kuapishwa, kutoka kushoto ni Mhe.Jaji Blaise Tchikaye (Congo), Mhe. Jaji Stella Isibhakhonem Anukam (Nigeria) na Mhe. Jaji Imani Aboud (Tanzania). (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi kutoka kwa  Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu Mhe. Jaji Sylvain Ore mara baada ya kuapishwa kwa Majaji wapya watatu wa mahakama hiyo mjini Arusha.
 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha mpya na Majaji wateule wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu ambao wameapishwa leo mjini Arusha  kushoto ni Mhe.Jaji Blaise Tchikaye (Congo), Mhe. Jaji Imani Aboud (Tanzania) na kulia ni Mhe. Jaji Stella Isibhakhonem Anukam (Nigeria)  . (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Moto Hauzimi na DStv, Star Life nyumba ya Bollywood sasa ndani!

$
0
0
 Kampuni ya Multichoice inajivunia kuongeza chaneli mpya ya filamu inayojulikana kwa jina la Star Life mahususi kwa ajili ya wapenzi wa filamu na Tamthilia za kihindi.

Chaneli hii yenye maudhui ya kihindi inayorusha matangazo kwa Lugha ya kingereza imeanza rasmi kupatikana tarehe 27 Agosti 2018 chaneli namba DStv 167 iliyopo kuanzia kifurushi cha DStv Family.

Wateja wa DStv na watanzania wote kwa ujumla wataweza kufurahia filamu nzuri na za Kisasa za kihindi, Tamthilia na Series kali zenye kugusa hisia na tamaduni na maisha ya kihindi na vipindi vingine mbalimbali vya burudani kupitia chaneli hii vitakavyokuwa rushwa hewani kwa lugha ya kiingereza.

Kwa zaidi ya miaka 20 chaneli hii imekuwa ikipeperusha bendera kwa kuwa chaneli namba moja kutokana na ubora wa maudhui ya filamu na sinema zilizosheni ndani yake.

“Nyongeza ya chaneli hii ni matokeo ya kuhakikisha kuwa wateja wetu wanaendelea kufurahia huduma za DStv kwa burudani za kisasa kabisa ambazo hawatoweza kuzipata kwingine kokote. Chaneli hii itakuwa ikipatikana ndani ya DStv kupitia chaneli namba 167 kuanzia kifurushi cha Family 39,000.

BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU AGOSTI 27, 2018

SERIKALI YAWEKA MIKAKATI THABITI ILI KUDHIBITI UGONJWA WA EBOLA USIINGIE NCHINI.

$
0
0
Na WAMJW - KAGERA, NGARA

Serikali kupitia Wizara ya Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto yaendelea kuweka mikakati thabiti katika maeneo yote hatarishi ikiwemo mipakan na njia za panya ili kudhibiti ugonjwa wa Ebola kuingia nchini.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu leo wakati alipofanya ziara katika Mpaka wa Rusumo kati ya nchi ya Tanzania na Rwanda ili kuangalia ni jinsi gani Mkoa wa Kagera umejipanga katika kudhibiti mlipuko wa ugonjwa wa Ebola kuingia nchini.

Waziri Ummy amesema kuwa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola ambao umetokea eneo la Kivu katika Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo unaiweka Tanzania katika hatari zaidi ya kuweza kupata wagonjwa wa Ebola kutokana na muingiliano wa wananchi baina ya nchi hizo.

"Mlipuko huo wa Ugonjwa wa Ebola ambao umetokea katika Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo sasa hivi inatuweka Tanzania katika hatari kubwa zaidi kupata wagonjwa kutokana na mlipuko huo kutokea eneo la Kivu Kaskazini ambalo ni karibu na Tanzania na muingiliano wa wananchi baina ya nchi hizi mbili ni mkubwa " Alisema Waziri Ummy Mwalimu.

Aidha, Waziri Ummy alisema kuwa Serikali inaendelea kutoa mafunzo kwa wahudumu wa Sekta ya Áfya ili kufahamu jinsi ya kuwahudumia wanaohisiwa kuwa na Virusi vya ugonjwa wa Ebola sambamba na hilo Serikali imeleta vifaa kinga watakavyovaa wakati wakitoa huduma kwa mgonjwa au mhisiwa wa ugonjwa wa Ebola.

Waziri wa Áfya Mhe Ummy Mwalimu akisisitiza jambo juu ya mikakati ya kudhibiti ugonjwa wa Ebola usiingie nchini wakati alipofanya ziara katika Mpaka wa Lusumo Wilaya ya Ngara Mkoa wa Kagera
Afisa Afya wa kituo cha uhamiaji Mpaka wa Lusumo Stanley S. Chipasula akipokea maelekezo kutoka kwa Waziri wa Áfya Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipofanya ziara ya kuangalia utayari wa Kagera kuzuia ugonjwa wa Ebola usiingie nchini kupitia Mpaka wa Lusumo.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera Dkt Marco Mbata (aliyevaa suti ya bluu) akimwelekeza jambo Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu (wakatikati) Leo wakati alipofanya ziara katika Mpaka wa Lusumo Wilaya ya Ngara Mkoa wa Kagera
Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu akimwelekeza jambo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera Dkt Marco Mbata mikakati ya kudhibiti ugonjwa wa Ebola usiingie nchini, wakati alipofanya ziara katika Mpaka wa Lusumo Wilaya ya Ngara.
Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Ngara Luten Kanali Michael M.


PONGEZI

MAGAZETINI LEO

AfDB YATEKELEZA MIRADI YA SH. TRLIONI 4.4 NCHINI TANZANIA

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam

Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zinapewa fedha nyingi kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) katika kutekeleza miradi ya maendeleo katika Sekta ya Nishati, Maji, Kilimo na Barabara ili kuchochea uchumi na kutimiza malengo ya kuwa nchi yenye uchumi wa kati unaotegemea viwanda ifikapo mwaka 2025 ambapo mpaka sasa Benki hiyo imewekeza nchini zaidi ya shilingi trilioni 4.4.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayeiwakilisha Marekani Bw. J. Steven Dowd katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango, alieleza kuwa Tanzania inapata fedha nyingi za kutekeleza miradi kutoka Benki ya AfDB kutokana na vipaumbele vya Benki hiyo kuendana na vipaumbele vya Serikali ya Tanzania katika Awamu ya Tano ya Uongozi wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

“Miradi inayotekelezwa kwa fedha za AfDB ni pamoja na mradi wa kusafirisha umeme kutoka Mbeya, Sumbawanga hadi Nyakanazi utakao gharimu shilingi dola za Marekani milioni 123, miradi mingine ni ile ya ushirikiano na Sekta Binafsi (Dola Milioni 57.6m), ujenzi wa barabara ya Nyakanazi mpaka Burundi kupitia Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma na pia mradi wa ujenzi wa uwanja wa ndege wa Msalato Jijini Dodoma ambao AfDB imeahidi kutoa shilingi bilioni 200 kwa kuanzia”, alieleza Dkt. Mpango.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) wa pili kulia, akiagana na mgeni wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayeiwakilisha Marekani Bw. J. Steven Dowd (wa pili kushoto) Nje ya jengo la Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa AfDB Dkt. Alex Mubiru na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayeshughulikia nchi nane za Afrika Dkt. Nyamajeje Weggoro. 
Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Mkurugenzi Mtendaji wa wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayeiwakilisha Marekani Bw. J. Steven Dowd ukiendelea katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), akijadiliana jambo na Mwakilishi Mkazi wa AfDB nchini Tanzania Dkt. Alex Mubiru (kushoto) na katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayeshughulikia nchi nane za Afrika Dkt. Nyamajeje Weggoro. 
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akisalimiana na Mgeni wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayeiwakilisha Marekani Bw. J. Steven Dowd alipowasili katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam katika Mkutano ulioangazia ushirikiano wa Maendeleo kati ya Tanzania naBenki hiyo. 


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>

Vodacom yazindua njia ya kipekee ya kuhamisha data kwa kutumia duka la kidijitali

$
0
0
 Mkurugenzi  Mtendaji wa Dar Teknohama Business Incubator (DTBi), Mhandisi Dkt, George Mulamula ( kulia) akikata utepe  wakati wa  uzinduzi wa duka jipya la Vodashop lenye sehemu maalum ya kutengenezea simu (Techzone) na kuhifadhi na kuhamisha kumbukumbu lililopo  makao makuu ya kampuni  hiyo Vodacom Tower Morocco jijini Dar es Salaam.Kushoto  ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Plc,  Rosalynn Mworia.
 Mkurugenzi  Mtendaji wa Dar Teknohama Business Incubator (DTBi), Mhandisi Dkt, George Mulamula ( katikati) na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Plc,  Rosalynn Mworia (kulia) wakimsikiliza mtaalamu wa Data,   Hendrick  Rupia wakati wa  uzinduzi wa duka jipya la Vodashop lenye sehemu maalum ya kutengenezea simu na kuhifadhi na kuhamisha kumbukumbu lililopo  makao makuu ya kampuni  hiyo Vodacom Tower Morocco jijini Dar es Salaam
 Mkurugenzi  Mtendaji wa Dar Teknohama Business Incubator (DTBi), Mhandisi Dkt, George Mulamula (wa pili kulia)  akiongea   na wafanyakazi wa Vodacom    wakati wa  uzinduzi wa duka jipya la Vodashop lenye sehemu maalum ya kutengenezea simu na kuhifadhi na kuhamisha kumbukumbu  lililopo  makao makuu ya kampuni  hiyo Vodacom Tower, Morocco jijini Dar es Salaa , wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Plc,  Rosalynn Mworia,  Kushoto ni Mkuu wa Kanda ya Dar es Salaam na Pwani George Lugata na Meneja wa maduka ya Rejareja ya Vodacom Tanzania, Happiness Macha.
 Mkurugenzi  Mtendaji wa Dar Teknohama Business Incubator (DTBi), Mhandisi Dkt, George Mulamula (wa pili kulia)  akikata keki  wakati wa uzinduzi wa duka jipya la Vodashop lenye sehemu maalum ya kutengenezea simu na kuhifadhi na kuhamisha kumbukumbu uliofanyika leo  katika  makao makuu ya kampuni  hiyo Vodacom Tower, Morocco jijini Dar es Salaam, wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Plc,  Rosalynn Mworia,  (wa pili kushoto) na wafanyakazi wa kampuni hiyo.
 Mkurugenzi  Mtendaji wa Dar Teknohama Business Incubator Mhandisi Dkt, George Mulamula  (kulia) na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Plc,  Rosalynn Mworia wakigongea glasi ya shampeni wakati wa hafla ya uzinduzi wa duka jipya la Vodashop lenye sehemu maalum ya kutengenezea simu na kuhifadhi na kuhamisha kumbukumbu  lililopo Makao Makuu ya kampuni hiyo,Vodacom Tower, Morocco jijini Dar es Salaam.

BENKI YA NIC YAZINDUA KADI ZA DEBIT ZA VISA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

BENKI ya NIC imezindua kadi yake kwa mara ya kwanza kabisa ya Visa Debit iliyopewa jina la "Move" itakayowapa wateja wake njia rahisi na haraka zaidi katika kufanya malipo popote ndani na nje ya nchi.

Akizungumza katika ufunguzi huo Mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo Mick Karima ameeleza kuwa uzinduzi huo unaashiria hatua muhimu sana kwa benki yao na wanaendela kutoa huduma mbalimbali kwa wateja  zitakazoboresha maisha yao.

Aidha amesema kuwa benki hiyo inaendelea kutafuta ufumbuzi wa kuwaboreshea wateja matumizi ya huduma zao kwa kwenda mbele na kuwa wabunifu zaidi.

Pia ameeleza kuwa watanzania wengi wameonesha hamasa ya malipo ya kidigitali hivyo watahakikisha huduma hizo za kufanya malipo kwa njia ya mtandao zinawafikia wateja wao  na wana malengo makubwa mbeleni katika kujenga uchumi wa nchi hasa kwa  kwa kuzingatia sera ya nchi kwa sasa inayohamasisha na kuongeza kasi ua ukuaji wa malipo kwa njia ya kadi.

Naye Mkuu wa kitengo cha fedha na manunuzi wa benki hiyo Msafiri Kibebeti ameeleza kuwa lengo la uzinduzi wa kadi hiyo ni pamoja na kurahisisha na kuwawezesha wateja wao kufanya huduma (miamala) na hii yote ni katika kutimiza matakwa ya wateja na kutimiza azma ya serikali ya kujenga Tanzania ya viwanda.

Kibebeti amesema kuwa wapo imara na wamejizatiti kufanya kazi na wapo katika hatua za mwisho katika kufungua matawi katika Mikoa ya Dodoma na Zanzibar.

Benki ya NIC ilinunua hisa katika benki ya ya Savings and Finance Commercial Bank Group Tanzania na kuibadili chapa na kuwa benki  NIC  Tanzania na hadi sasa imezindua huduma kadhaa za kidigitali kwa lengo la kuwasaidia  wafanya biashara wadogo wadogo na hadi sasa wana matawi matano katika Mikoa ya Arusha, Mwanza(matawi 3,) na Dar es salaam matawi 3 (Ohio, Samora na Kariakoo.)
Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya NIC Tanzania Mick Karima akizindua huduma ya kadi yake ya kwanza ya Visa Debit leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya NIC Tanzania Mick Karima akimkabidhi mteja wao mfano wa kadi ya visa Debit iliyozinduliwa na Benki hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Benki ya NIC Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya zoezi hilo la uzinduzi wa kadi mpya ya Visa Debit kumalizika leo Jijini Dar es Salaam.
Viewing all 110151 articles
Browse latest View live




Latest Images