Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

SERIKALI KUBORESHA KISIWA CHA MAGAFU KATIKA ZIWA VICTORIA WILAYANI CHATO MKOA WA GEITA

$
0
0
Na Richard Bagolele, Chato
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano) January Makamba amesema serikali inaangalia uwezekano wa kilinda na kukihifadhi kisiwa cha Magafu kilichopo Wilayani Hapa ili kiwe kivutio cha Utalii na eneo maalumu kwa ajili ya mazalia ya Samaki.
Waziri Makamba amesema hayo alipotembelea kisiwa hicho kufuatia ombi la Halmashauri ya Wilaya ya Chato kwa Wizara hiyo la kuomba kisiwa hicho kihifadhiwe na kuwa eneo lindwa  kuwa eneo tengefu kwa ajili ya mazalia ya samaki kwa ziwa Viktoria.
‘’kutokana eneo la kisiwa hiki kuwa ni chanzo kikubwa cha mazalia ya samaki lakini  kumekuwa na hatari kubwa za uvamizi wa kisiwa hiki kutokana na shughuli za kilimo, uvuvi haramu na ufugaji ambao umeathiri ukuaji wa samaki na shughuli nzima za kiuchumi” alisema Waziri Makamba.
Amesema kutokana na umuhimu wa kisiwa hicho, Wizara yake itaandaa mpango wa matumizi mazuri ya kisiwa hicho ili kiweze kurudi kwenye mazingira yake ya asilia kwa kushirikiana na uongozi wa Wilaya ya Chato na Jamii inayozunguka eneo hilo.
Kwa upande Mkuu Wa Wilaya ya Chato Mhandisi Mtemi Msafiri amesema kutokana na umuhimu wa kisiwa hicho kiuchumi ni lazima kisiwa hicho kihifadhiwe ili kuongeza samaki ziwa viktoria na shughuli za kiutalii kwani mahali hapo panaweza kujengwa hoteli ya kitalii kwani kisiwa hicho kipo karibu na hifadhi ya kisiwa cha Rubondo.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri Christian Manunga ameomba kisiwa hicho kianze kulindwa ili kunusuru maliasili zilizomo kwa manuaa ya serikali hususan Wilaya ya Chato.
Kisiwa kidogo cha Magafu kipo ndani ya Ziwa Viktoria eneo la kata ya Nyamirembe. Kisiwa hicho kinakadiriwa kuwa na ukubwa eneo wa mita 3 za mraba.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano) January Makamba akiwa ameongozana na viongozi wa Wilaya ya Chato wakiangalia mazingira ya kisiwa Cha Magafu kilichopo kata ya Nyamirembe wilayani Chato.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano) January Makamba akiangalia mazingira ya kisiwa Cha Magafu kilichopo kata ya Nyamirembe wilayani Chato.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano) January Makamba pamoja na viongozi wengine wakiwa kwenye lango la kuingilia kisiwa cha Magafu kilichopo kata ya Nyamirembe wilayani Chato.


MBUNGE CCM ACHARUKA UBADHIRIFU ULIOFANYIKA JIMBONI KWAKE

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

MBUNGE wa jimbo la Manonga, Mh. Seif Gulamali ambaye siku za karibuni amegeuka mwiba mkali kwa watendaji wabadhirifu ndani ya wilaya ya Igunga na hii ni baada ya kuona kasi ya watendaji wake ikiwa legevu, na  wakati wa ziara ya Waziri Mkuu, Mh.Kasimu Majaliwa Jimboni humo Mbunge huyo aliibua ufisadi wa zaidi milioni 170, na Waziri Mkuu aliagiza wahusika wote kukamatwa.

Leo akizungumza na blogu ya jamii Gulamali ameeleza mwenendo na msimamo wake katika kuhusu azma yake ya kuleta mandeleo Jimboni humo.

Gulamali ametoa angalizo kwa watendaji wa kijiji cha Kijiji cha Bulangamilwa na kusema kwamba; "Zimepotea Milioni 141 na Mifuko 90 ya saruji katika Kijiji hicho licha ya  kupata shilingi Milioni 700 za Mradi wa Maji ambao umetekelezwa chini ya kiwango na Maji hayatoki, huo ni Ubadhirifu tena wa Fedha za Umma. Siwezi kunyamaza" amesisitiza.

 Akieleza kuhusu sakata la Kijiji cha Choma Mbunge Gulamali amesema; "Zimetolewa Milioni 35 za Mashine ya Mpunga na badala yake ikanunuliwa  mashine iliyotumika na mpaka leo hakuna kinachoendelea. Nilipiga sana kelele juu ya masuala haya lakini waliweka nta kwenye masikio huku wakiendelea kunibeza wakitumia nafasi zao kuwalinda wezi, nimeomba kuwatumikia Wana Manonga na wakaniamini kwa Miaka 5 nitahakikisha fedha zenu za Miradi ndani ya Miaka yangu 5 hazipotei kirahisi tutakula nao Sahani Moja. Narudia tena, haitapotea hata mia moja nikanyamaza"amesisitiza Gulamali.

Kuhusu watendaji wanaofanya kazi chini ya viwango Gulamali amesema kuwa; "kwa wale ambao wanawaza kufanya kazi chini ya Viwango ndani ya Jimbo langu hao hawana nafasi na wasipoteze muda wao kwani watarudia kazi zao mpaka wakae sawa"ameeleza.

Aidha ameeleza kuwa anashukuru Mungu kwa kuwa  hadi sasa ahadi alizotoa nyingi zimekamilika na chache zipo katika hatua za mwisho za utekelezaji.

Gulamali ameeleza kuwa Ubunge sio Ufalme, Udikteta wala Usultani ni Utumishi  na aliomba kuwatumikia wana Manonga kwa Miaka 5 na aliwaambia wapiga kura wake kuwa  akishindwa kutimiza Ahadi alizotoa wampige chini.

"Niliahidi na Ninatekeleza, Sina Muda wa Kuupoteza" Gulamali.

Waziri Mkuu Majaliwa amjulia hali Dkt. Kigwangalla MOI

$
0
0
Na Andrew Chale
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa leo Agosti 26,2018 amemtembelea na kumjulia hali Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla aliyelazwa katika wodi maalum kitengo cha Taasisi ya mifupa MOI, hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Hii inakuwa ni kwa mara ya pili kwa Waziri Mkuu Majaliwa kumtembelea kumjulia hali ambapo awali alimtembelea Jumapili ya Agosti 5, 2018), wakati Dkt. Kigwangalla akipatiwa matibabu ya awali katika Wodi ya Mwaisela. Akiwa wodini hapo, Waziri Mkuu Majaliwa amemtakia kila lakheri katika kuuguza mkono wake ambapo pia amepata kuzungumza nae juu ya maendeleo ya afya yake.
Aidha, Waziri Majaliwa amewashukuru Madaktari wa MOI pamoja na uongozi wake kwa pamoja kutoa huduma bora kwa watanzania na raia wa Nchi za nje ambao wamekuwa kimbilio kuja nchini kupata tiba.

“Nakutakia kila lakheri Kigwangalla. Nimekuja baada ya kusikia umefanyiwa operesheni ya pili. Pia nawashukuru Uongozi na Madaktari wetu wa hapa MOI kwa kutoa tiba nzuri tiba zenu kwa sasa zimezifanya nchi zingine wananchi wake kukimbilia hapa. Viongozi wakuu pia Hospitali hii ndio kimbilio letu kwa sasa na tunawashukuru kwa huduma bora inayofanya Nchi kuwa na heshima kuwbwa,” amesema Waziri Mkuu Majaliwa.
Kwa upande wake Dkt. Kigwangalla amemwakikishia Waziri Mkuu kuwa kwa sasa anaendelea vizuri kwani ameweza kufanya mazoezi ya ikiwemo kutembea umbali wa kilometa nne pamoja na mazoezi mepesi kila siku majira ya asubuhi na jioni.
“Kwa sasa naendelea vizuri sehemu kubwa ni mkono ndio nauguza. Ila kwa hali ya maendeleo kwa sasa naendelea vizuri pamoja na mazoezi kidogo kidogo naendelea. Alisema Kigwangalla. Aidha, mbali na Waziri Mkuu Majaliwa, jana jioni Agosti 25,2018, Rais Mstaafu wa awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete aliweza kumtembelea tena na kumjulia hali. 
Dkt. Kigwangalla alipata ajali asubuhi ya Jumamosi, Agosti 4, 2018) katikati ya vijiji vya Mdolii na Minjingu wilaya ya Babati mkoani Manyara baada ya gari lake kupinduka na kusababisha kifo cha Afisa Habari wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Hamza Temba na wengine watano akiwemo Dkt. Kigwangalla kujeruhiwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimjulia hali Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla, leo Agosti 26/2018,akiwa anaendelea kupatiwa matibabu katika Wodi aliyo lazwa ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Muhimbili (MOI), PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

TANZIA : MAMA MZAZI WA MBUNGE JOSEPH MBILINYI 'SUGU' AFARIKI DUNIA

$
0
0
*Sugu asema msiba upo nyumbani kwake Salasala Dar es salaam, 
mwili kusafirishwa Mbeya baada ya taratibu zitakapokamilika

Na Said Mwishehe, Globu ya Jamii

MAMA mzazi wa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi 'Sugu' kupitia Chadema, amefariki dunia leo akiwa  Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).Mama wa Sugu alikuwa amelazwa katika hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Wateja, Aminiel Aligaesha amethibitisha kutokea kwa msiba huo. 
Kwa upande wake Sugu ameiambia Michuzi Blog kwa njia ya simu kwamba msiba wa mama yake npendwa upo nyumbani kwake Salasala jijini Dar es Salaam."Kama ambavyo mmesikia mama amefariki leo tena mchana huu, hivyo nachoweza kusema mama hatunaye na msiba upo nyumbani Salasala.

" Hata hivyo tutasafirisha msiba kuelekea mkoani Mbeya kwa ajili ya kuupumzisha mwili wa mama. Tutatoa ratiba rasmi hapo baadae. Ila itoshe kusema msiba upo Salasala wakati tunaendelea na taratibu nyingine,"amesema Sugu.
Michuzi Media Group(MMG) inaungana na Watanzania wengine kutoa pole kwa familia ya Sugu, ndugu, jamaa na marafiki.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMEN

=====  =======  ========  ========
Mbunge wa Mbeya mjini Mhe.  Joseph Mbilinyi almaarufu kama  SUGU akiwa na Mama yake MzazI enzi za uhai wake.

Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) chajizatiti kukabiliana na Ebola

$
0
0
KITENGO cha Afya katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) kimeweka udhibiti madhubuti wa kujikinga na usambazaji wa magonjwa ambukizi ukiwemo ugonjwa wa Ebola. Ugonjwa wa Ebola unaosambazwa kwa virusi vya Ebola, husababisha homa kali inayoweza kuambatana na kutokwa damu mdomoni, puani, masikioni, machoni na sehemu nyingine za wazi na unaenea kwa haraka. 

Hivi karibuni umetangazwa kutokea nchini Kongo na kusababisha vifo. Akizungumzia kuhusiana na mikakati hiyo ya kupambana na magonjwa ambukizi ukiwemo wa Ebola, Afisa Afya Mfawidhi wa JNIA, Dk. George Ndaki amesema wanatoa mafunzo kwa watumishi na wahusika wote wanaotumia kiwanja hicho katika kujikinga na magonjwa hayo. 

 “Sisi tumejiandaa vizuri na tumeshafanya jitihada zote tumeshatoa maelekezo, mafunzo na kamati mbalimbali za kiwanja zimejipanga kudhibiti magonjwa yote ya kuambukiza, ikiwemo sisi wenyewe kujikinga na kuwakinga na abiria wote wanaotoka katika nchi hatarishi”, amesema Dkt. Ndaki. 
 Aidha akizungumzia kuhusiana na utaratibu ambao Kiwanja kimeweka ili kuhakikisha abiria wenye maambukizi wanapokelewa kwa tahadhari, ambapo wanapowasili na ndege zinazotoka nje ya nchi zinazopakia abiria wanaosafiri kutoka katika nchi zinazoshirikiana na Kongo hutakiwa kusafisha mikono kwa dawa maalum mara waingiapo katika eneo la kuwasili. 
 Pia abiria hao wanapoingia katika lango la kuwasili la abiria kutoka nje ya nchi, kumekuwa na mashine maalum inaangalia joto la mwili na likizidi nyuzi joto 38 wanamtaka kutoa maelezo Zaidi ya afya yake.
 “Abiria wote wanapowasili hupita katika eneo maalum ambalo wote hutakiwa kuosha mikono, lakini pia kuna mashine ambazo zimewekwa ili kuweza kuwatambua abiria ambao wanawasili wakiwa na hali ya joto isiyokuwa ya kawaida mfano kuwa na joto la juu sana kuanzia 38oC, ukiachana na hilo kuna fomu maalum ambazo abiria wanapowasili hujaza na pia taarifa kutoka kwa rubani wa ndege kama kuna abiria ana maambukizi kwenye ndege. 
Baada ya kumtambua mgonjwa basi atapitishwa katika njia ya tofauti na abiria wengine na kupakiwa katika gari la wagonjwa na kupelekwa Temeke Hospital,” amesema Dk. Ndaki. 
 Naye Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Paul Rwegasha akitoa ufafanuzi juu taarifa za uwepo wa ugonjwa wa Ebola, ameeleza kuwa tayari JNIA wanazo taarifa za mlipuko wa ugonjwa huo na taratibu zote zimeshachukuliwa kwa kuwakagua abiria wanaotoka nje ya nchi. 
 “Kwanza kabisa kwa abiria wote ambao wanatokea katika nchi ambazo zinasadikika kuwa na maambukizi wanapowasili wanakuwa sanitized (wanaosha mikono na dawa maalum) ili wasiweze kuleta maambukizi ndani, lakini pia tuna thermo scanners (mashine ambazo zinaangalia hali ya joto la mtu) anapowasili ambapo tunapogundua mgonjwa anamatatizo tunapeleka isolation (Chumba cha wagonjwa wa kipekee) na baada ya hapo anapelekwa katika vyumba vya waonjwa waliotengwa katika hospitali ya Temeke” alibainisha Bw. Rwegasha. 
 Katika hatua nyingine Dk. Ndaki amesema mpaka sasa hakuna mgonjwa yeyote ambaye amebainika kuwa na ugonjwa wa Ebola kupitia JNIA. Dk Ndaki ametaja namna ya kujikinga na ugonjwa wa Ebola ni pamoja na kuepuka kugusa damu, machozi, jasho, matapishi, kamasi, mkojo au kinyesi cha mtu mwenye dalili za ugonjwa; pia mtu hatakiwi kugusa, kuosha au kuzika maiti ya aliyekufa kwa Ebola; pia usiguse au kula wanyama kama popo, sokwe au swala wa msituni. 
 Dalili za Ebola ni pamoja na homa kali, maumivu ya kichwa na misuli, mwili kulegea, kutapika, kuharisha, vipele ma kutokwa damu 
 “Natoa wito tu kwa wananchi kuhakikisha wanafuata taratibu zote tulizoziweka ili kuhakikisha kwamba hatupati mgonjwa yeyote katika nchi yetu. 
Kama kila mtu atatekeleza wajibu wake kwa abiria kufuata taratibu, wanaosimamia masuala ya afya wakitimiza wajibu wao, na Kiwanja kikitimiza wajibu wake basi hakika magonjwa ya mlipuko hayataweza kufika katika nchi yetu” alieleza Dkt. Ndaki.
 Mlango wa kuingilia abiria kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), wanaotoka nje ya nchi ambao baadhi ya ndege zimelengwa kutokana na abiria wake aidha kupita au kuanzia safari kwenye nchi ya Kongo iliyotangazwa kuwepo kwa ugonjwa wa Ebola.
 Eneo maalum la ukaguzi wa afya kwa abiria mara baada ya kuingia kwenye sehemu ya wanaowasili kutoka nje ya nchi, ambapo kumefungwa mashine maalum zenye kuonesha joto la mwili na likizidi 38 abiria huyo hufanyiwa mahojiano ya afya yake, kwa kuwa moja ya dalili za ugonjwa wa Ebola ni kuwa na joto kali.

 Mmoja wa abiria aliyewasili na ndege ya Rwanda Air kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), akinawa mikono kwa dawa maalum inayoua vijidudu vya maradhi mbalimbali yanayoambukiza, ukiwemo Ebola uliotangazwa hivi karibuni umeibuka nchini Kongo.
 Afisa Afya Mfawidhi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Dkt. George Ndaki akionesha mashine maalum inayompima abiria (thermo scanners) mara anapopita eneo la ukaguzi wa afya, ambapo linakuwa likisomwa na Afisa Afya kwenye komputa iliyopo (kulia). JNIA wamejidhatiti na makonjwa ya milipuko ukiwemo wa ebola uliotangazwa kuwepo nchini Kongo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Paul Rwegasha (kulia) akizungumza na waandishi wa habari juu ya udhibiti wa magonjwa ya mlipuko kwenye kiwanja hicho. Hivi karibuni ugonjwa wa Ebola umetangazwa kutokea nchini Kongo.
Bango linalotoa maelezo yanayohusiana na ugonjwa hatari wa Ebola likiwa eneo la wasafiri wanaowasili kutoka nje ya nchi kweney Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).

Spea za magari ya Landlover kutoka UK sasa zinapatikana Tanzania

Morogoro yafana baada ya kushinda gari la nane la M-Pesa

$
0
0
Mstahiki Meya wa Mji wa Morogoro Paschal Kihanga Mwendashule (Kushoto) akimkabidhi funguo ya gari bi Glory Lyatuu kutoka Morogoro baada ya kuibuka mshindi wa nane wa promosheni ya Tumia M-Pesa ushinde gari, mteja wa M-Pesa anatakiwa kufanya miamala mingi zaidi ili kuweza kujishindia gari.
Mstahiki Meya wa Mji wa Morogoro Paschal Kihanga Mwendashule (Kushoto) akimkabidhi kadi ya gari Glory Lyatuu kutoka Morogoro baada ya kuibuka mshindi wa nane wa promosheni ya Tumia M-Pesa ushinde gari, mteja wa M-Pesa anatakiwa kufanya miamala mingi zaidi ili kuweza kujishindia gari.
Mkuu wa kitengo cha usambazaji M-Pesa Julius Kastabu (Kulia) akimuonesha kifaa cha pembetatu (triangle) Glory Lyatuu kutoka Morogoro baada ya kuibuka mshindi wa nane wa promosheni ya Tumia M-Pesa ushinde gari, mteja wa M-Pesa anatakiwa kufanya miamala mingi zaidi ili kuweza kujishindia gari.
Mshindi wa nane wa promosheni ya Tumia M-Pesa ushinde gari, Glory Lyatuu akiwa ndani ya lake alilojishindia kwenye promosheni ya Tumia M-Pesa ushinde gari, mteja wa M-Pesa anatakiwa kufanya miamala mingi zaidi ili kuweza kujishindia gari.

JK AMUWAKILISHA JPM KWENYE SHEREHE ZA KUAPISHWA RAIS MPYA WA ZIMBABWE LEO

$
0
0
Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais wa Zimbabwe, Mhe. Emmerson Mnangagwa baada ya kuapishwa kwake jijini Harare, Zimbabwe leo. Dkt. Kikwete amehudhulia sherehe hiyo akiwa amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo aliambayana na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Phillip Mangula pamoja na Mwenyekiti wa UDP, John Momose Cheyo.
 Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu Mtendaji Mkuu wa SADC, Dkt. Stergomena L. Tax walipokutana kwenye sherehe za kuapishwa Rais mpya wa Zimbabwe, Mhe. Emmerson Mnangagwa zilizofanyika leo mjini Harare, Zimbabwe. Dkt. Kikwete amehudhulia sherehe hiyo akiwa amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo aliambayana na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Phillip Mangula pamoja na Mwenyekiti wa UDP, John Momose Cheyo.
 Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na viongozi mbalimbali baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Robert Gabriel Mugabe, mjini Harare Zimbabwe, alikokwendwa kwa kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, kwenye sherehe za kuapishwa Rais mpya wa Zimbabwe, Mhe. Emmerson Mnangagwa zilizofanyika leo mjini Harare, Zimbabwe.


HATUTARUDIA MAKOSA SIMBA MJIANDAE-MBEYA CITY

$
0
0
Na Agness Francis,blogu ya Jamii.

Kikosi cha Mbeya city chatamba kufanya vizuri katika mchezo wao dhidi ya mnyama Simba sc hapo kesho katika muendelezo wa michuano ya Ligi kuu Tanzania bara.

Mpambano huo utakao tifulia katika dimba la Uwanja wa Taifa huku Mbeya city wakiwa wageni wa mchezo huo.Mechi ya kwanza Mbeya city ilipata kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa wana lamba lamba Azam fc katika dimba la Azam complex Chamazi,ambapo simba alishinda 1-0 dhidi ya Prisons.

Lakini katika kuelekea mtanange huo dhidi ya mabingwa watetezi Simba,kikosi cha Mbeya city imejihakikishia kutorudia makosa waliyoyafanya katika mchezo uliopita 

"Kambi ipo salama vijana wanajituma kwa kuwa tunajua tumekosea wapi tunafanyia kazi makosa tunarekebisha pale tulipokosea ili tuweze kufanya vizuri gemu inakuja dhidi ya Simba,hatuturudia tena makosa tuliyoyafanya"amesema kocha msaidizi Josiah Steven. 

Meneja wa Mbeya city Deo Julias amesema vijana wanamorali ya kufanya vizuri kuhakikisha wanapata ushindi na kurudi nyumbani wakiwa na pointi 3.
Kikosi cha Mbeya City.

MCHENGA BBALL STARS WANYAKUA TENA UBINGWA WA SPRITE BBALL KINGS 2018

$
0
0


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Mchenga Bball Stars imefanikiwa kutetea ubingwa wake wa Sprite Bball Kings kwa mara ya pili mfululizo baada ya kufanikiwa kuwafunga wapinzani wake Flying Dribbllers kwa pointi 87 dhidi ya 76 kwenye mchezo wa game 3 ya 'best of five' za fainali uliochezwa mwishoni mwa wiki kwenye uwanja wa ndani wa taifa.

Mechi hiyo iliyoanza kwa kasi kwa pande zote, Mchenga alifanikiwa kushinda katika quarter zote nne na kuzidi kuonesha ubabe kwa timu zingine kwenye michuano ya Sprite BBall Kings.

Mchenga wamefanikiwa kuchukua ubingwa huo kwa kushinda game zote tatu mfululizo yaani (Swipe) kati ya tano za fainali hivyo kuwanyima furaha wapinzani wao Flying Dribbllers kwa mara ya pili mfululizo baada ya kuwafunga kwa aina hii hii kwenye nusu fainali ya michuano hiyo mwaka 2017.

Katika game 1 Mchenga walishinda kwa pointi 103 dhidi ya 73 za Flying Dribblers, kabla ya kushinda kwa pointi 85 kwa 65 kwenye game 2 na leo kumalizia kazi kwa ushindi wa pointi 87 kwa 76.Katika ushindi huo wa Mchenga Bball Stars mchezaji Baraka Sadick amekuwa na msaada mkubwa hali ambayo imepelekea kuibuka kama 'Most Valuable Player' wa mashindano kwa mwaka 2018.

Baraka amefunga pointi 239 katika michezo 8 aliyocheza. Katika michezo hiyo amekuwa na wastani wa kufunga pointi 30 katika kila mchezo. Katika mchezo wa leo Baraka amefunga pointi 33 kati ya 87 za timu yake.ainali hiyo ya aina yake iliweza kushuhudiwa na Rais wa Shirikisho la Kikapu (TBF) Phares Magesa akiwa na viongozi wengine na kujionea michuano hiyo ilivyokuwa na ushawishi mkubwa kwa vijana wa kitanzania.

Timu zote zimekabidhiwa zawadi zao na Rais wa TBF Phares Magesa akiwa sambamba na Katibu Mkuu wa TBF Mike Mwita ambazo ni shilingi milioni 3 kwa mshindi wa pili Flying Dribbllers, milioni mbili na tuzo kwa 'MVP' ambaye ni Baraka Sadick na milioni 10 kwa mabingwa ambao ni Mchenga Bball Stars. Sprite Bball Kings inaandaliwa na East Afarica Television chini ya udhamini wa kinywaji baridi cha Sprite.

Michuano hiyo ilianza rasmi mwaka 2017 kukiwa na timu 54 na Mchenga Bball Stars kufanikiwa kuchukua ubingwa huo kwa mara ya kwanza , msimu wa pili ulioanza mwezi June uliweza kuzikutanisha timu 51 zilizoanzia hatua ya mtoano na fainali kufanikiwa kuingia kwa timu mbili na Mchenga kutetea ubingwa wake tena.


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu (TBF) Phares Magesa akimkabiidhi kombe Nahodha wa timu ya Mchenga BBall Stars Mohamed Yusuph sambamba na hundi ya Milioni 10 baada ya kunyakua ubingwa wa pili mfululizo wa Michuano ya Sprite BBall Kings 2018 yaliyofanyika katika Uwanja wa Ndani wa Taifa Jijini Dar es Salaam
Mchezaji Baraka Sadick (aliyebebwa) akishangilia pamoja na wenzake baada ya kutangazwa kuwa mchezaji bora wa michuano hiyo ya Sprite BBall Kings 2018 (MVP) na kujinyakulia kikombe pamoja na hundi ya Milioni 2.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Nchini (TBF) Phares Magesa akimkabidhi Kikombe na hundi ya milioni 2 mchezaji bora wa mashindano ya Sprite BBall Kings 2018 (MVP) Baraka Sadick kutokea Mchenga BBall Stars katika fainali iliyofanyika Uwanja wa Ndani wa Taifa

KAMPUNI YA EY TANZANIA YAWAKUTANISHA PAMOJA WAFANYAKAZI WAKE KATIKA BONANZA LA MICHEZO

$
0
0
Sehemu ya Wafanyakazi wa Kampuni ya EY Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa Bonanza lao la Michezo, lililofanyika mwishoni kwa wiki kwenye Viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM). Zaidi ya michezo kumi ilichezwa uwanjani hapo, Wafanyakazi hao walijigawa katika makundi matano kutokea kila kitengo na kutengeneza timu tano katika kila mchezo (Kilimanjaro, Tigers, Rockets, Eagles pamoja na Wolves), ambapo ushindi wa jumla ulinyakuliwa na Timu Kilimanjaro.
 Mtendaji Mkuu Mwenza wa Kampuni ya EY Tanzania, Ukaguzi wa Hesabu (Audit Partner), Neema Kiure Mssusa akingumza wakati wa ufunguzi wa Bonanza la Michezo kwa Wafanyakazi wa Kampuni hiyo, lililofanyika mwishoni kwa wiki kwenye Viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM).
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya EY Tanzania wakichuana vikali katika mchezo wa Soka wakati wa Bonanza lao la Michezo, lililofanyika mwishoni kwa wiki kwenye Viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM).

MAGAZETINI LEO

Jukumu la kuendeleza Sanaa Nchini ni la Serikali ,Wadau wa Sanaa na Wananchi

$
0
0
Na Lorietha Laurence-WHUSM,Shinyanga.

Jukumu la kuendeleza sekta ya sanaa nchini ni la Serikali kwa kushirikiana na wadau wa sanaa na wanachi ambao wako mstari wa mbele kuhakikisha sekta hiyo inaleta manufaa ndani na nje ya nchi.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa Leah Kihimbi kwa niaba ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza katika halfa ya ufunguzi wa filamu ya Ruanda Mkoani Shinyanga.

Leah Kihimbi anaeleza kuwa Serikali kwa kuona umuhimu wa sekta ya sanaa nchini imeandaa Sera ya Maendeleo ya Sanaa itakayotoa muongozo kwa taifa kuhusu masuala yote ya sekta hiyo ikiwemo hakimiliki, urasimishaji wa kazi za sanaa na uendelezaji wa sekta hiyo nchini.

“Sera hii itakuwa dira na muongozo wa kazi zote za sanaa, hivyo kuwanufaisha wasanii pamoja na nchi” amesema Leah Kihimbi.

Aidha Leah Kihimbi amewapongeza wasanii kikundi cha Viwawada kwa kutoa filamu nzuri ya Ruanda ambayo inapinga na kukemea mimba na ndoa za utotoni, mauji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) na watu wenye umri mkubwa (Vikongwe).
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Leah Kihimbi akizungumza na wadau wa sanaa (hawapo katika picha) alipokuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Naibu Waziri wa Wizara hiyo katika halfa ya ufunguzi wa filamu ya Ruanda,jana Mkoani Shinyanga.
Afisa Utamaduni Mkoa wa Shinyanga Bi. Mariam Ally akiongea katika hafla ya ufunguzi wa filamu ya Ruanda iliyoigizwa na wasanii wa Viwawada wa Mkoa huo yenye maudhui ya kukemea na kupinga mimba na ndoa za utotoni, mauji ya watu wenye ulemevu wa ngozi (Albino) pamoja na watu wenye umri mkubwa (Vikongwe), jana Mkoani Shinyanga.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Leah Kihimbi (kushoto) akipokea risala kutoka kwa Bi. Elizabeth Vedastus (kulia) wakati ya halfa ya ufunguzi wa filamu ya Ruanda jana Mkoani Shinyanga.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Leah Kihimbi (kushoto) akisaidiana na Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Mariam Ally kufungua boski lilikuwa limewekwa CD ya filamu ya Ruanda ikiwa ni ishara ya kuizindua, jana Mkoani Shinyanga.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Leah Kihimbi akionyesha CD ya filamu ya Ruanda baada ya kuifungua rasmi wakati wa hafla hiyo jana Mkoani Shinyanga
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Leah Kihimbi (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na waigizaji wa filamu ya Ruanda mara baada ya kuifungua hapo jana Mkoani Shinyanga.
(Picha na Lorietha Laurence-WHUSM,Shinyanga)

VIFUNGASHIO VYA KISASA VYA BLISTA VYARAHISISHA KAZI YA UGAWAJI DAWA KWA WAGONJWA

$
0
0
Na Dotto Mwaibale, Muleba

WATENDAJI wa Vituo vya kutolea huduma za afya wilayani Muleba mkoani Kagera wamesema vifungashio vya dawa za serikali viliboreshwa kutoka kwenye makopo kwenda kwenye Blister pack vina uhakika wa kubakiza dawa katika ubora unaohitajika pamoja na kurahisisha kugawa dawa kwa wagonjwa.

Wakizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti mkoani Kagera, watendaji hao wamesema hata kwa upande wa watumiaji ambao ni wagonjwa vifungashio vya blister hata wakiangusha ama bahati mbaya zikamwagikiwa na maji hazitaathiriwa wala kupoteza ubora wake.

"Kupima dawa kwa kijiko kwa ajili ya kuziweka kwenye bahasha wakati wa kuwahudumia wagonjwa kulituchukulia muda sana na mara nyingine unakuta kopo linakaa wazi hadi msururu mzima unaohitaji aina hiyo ya dawa uishe"

Kwa upande mwingine wananchi wa Kata ya Nyakabango wilayani Muleba mkoani Kagera wameipongeza serikali kwa kufanikisha kuwapelekea dawa kwa wakati kupitia Bohari ya Dawa (MSD).Julius Kamuhaba alisema hivi sasa hali ya upatikanaji wa dawa katika zahanati hiyo ni nzuri na hakuna mtu atakayekwenda kupata matibabu akatoa malalamiko ya kukosa dawa.

"Naipongeza serikali inayoongozwa na Rais John Magufuli kwa jitihada inayoifanya ya kuhakikisha wananchi wake tunapatiwa dawa kwa wakati kupitia MSD" alisema Agnes Mganga mkazi wa kata hiyo.Alisema kila anapokwenda kupata matibabu katika Zahanati ya Nyakabango amekuwa akipata dawa tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma ambapo walikuwa wakiandikiwa kwenda kuzinunua.
Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kata ya Nyakabonga katika Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, Fausta Rugalinda, akizungumza na waandishi wa habari, kuhusu upatikanaji wa dawa katika zahanati hiyo pamoja na vifungashio vya dawa.
Ofisa Mauzo wa MSD Kanda ya Mwanza, Conoria Godfrey (kulia), akimuelekeza jambo Mganga Mfawidhi wa zahanati hiyo,Fausta Rugalinda wakati alipokuwa akikagua dawa zilizohifadhiwa kwenye stoo ya zahanati hiyo.


WAZIRI LUGOLA AITAKA POLISI, MAGEREZA KUWAONDOA WANANCHI WALIOVAMIA MAENEO YA JESHI NCHINI

$
0
0
Na Felix Mwagara, MOHA-Lindi 

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewataka wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya Wizara yake kuwaondoa mara moja wananchi wote waliovamia katika maeneo ya majeshi nchini. 

Lugola alisema hayo baada ya kulikagua Gereza jipya la Wilaya ya Ruangwa linalojengwa ambalo lina ekari 100 lakini ekari 20 limevamiwa kwa kujengwa kiwanda cha kukamua mafuta ya alizeti, ufuta na korosho katika eneo hilo la Jeshi la Magereza. 

Akizungumza baada ya kulikagua Gereza hilo, mjini Ruangwa leo, Lugola alisema kuanzia sasa viongozi wa vyombo vyake wahakikishe hawaruhusu mwananchi yeyote kuingia katika maeneo ya jeshi na atakua mkali kulifuatilia suala hilo. 

Lugola ambaye pia aliikataa kuipokea taarifa ya ujenzi wa gereza hilo ambayo ilikua inasomwa na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Lindi, Rajabu Nyange, alisema taarifa hiyo ina upungufu mkubwa na hawezi kuipokea licha ya kua imeeleza kuhusu ardhi ya jeshi hilo kuvamiwa. 

“Mimi huwa nashangaa sana inakuaje wananchi wanavamia ardhi ya jeshi tena bila woga, halafu jeshi linakaa kimya linabaki kunung’unika, hii haijakaa sawa kabisa na kamwe sikubaliani nalo,” alisema Lugola. 

Lugola aliongeza kua, “uvamizi wa ardhi mara nyingi unakua kwa jeshi la polisi na magereza, mbona Jeshi la Wananchi silisikii hili, kwanini nyie mnakaa kimya wananchi wakivamia ardhi yenu, sasa nawataka muhakikishe ardhi ya jeshi popote nchini iliyoporwa inarudishwa ndani ya jeshi, na wote waliovmia waondooeni haraka iwezekanavyo.” 


MKURUGENZI MKAZI UNDP ALETA HERI SAME

$
0
0
Mkurugenzi mkazi wa UNDP, Natalie BOUCLY ametembelea Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro kwa ziara yake ya siku mbili, na kukagua miradi iliyofadhiliwa na UNDP kupitia shirika la SIPRO na TFS.

Katika ziara yake hiyo, Bi. Boucly alibidhi majengo 4 yaliyojengwa kupitia mradi wa Kuboresha usimamizi wa Misitu ya Mazingira Asilia na kukuza utalii kwa ufadhili wa UNDP kwa TFS, Majengo yaliyojumuisha ofisi ya msitu wa Chome na ofisi 3 (ranger outposts) kwa ajili ya usimamizi wa msitu katika kata ya Chome, Bwambo na Bombo. 

Mradi huo pia umejenga majengo kama hayo katika misitu sita nchini ambayo ni Minziro, Uzdungwa, Mt Rungwe, Magamba na Mkingu. Baadaye alitembelea mradi wa ujenzi wa Daraja Heikapombe kata ya Makanya na mradi wa jengo la kijiji cha Mhero kata ya Chome.

Naye Mtendaji Mkuu wa TFS, Prof. Dos Santos Silayo aliyeambatana naye aliahidi kuendelea kuimarisha utalii katika hifadhi ya Chome kama ilivyo kipaumbele cha serikali katika hifadhi zote za misitu nchini.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Senyamule, alitoa shukrani kwa UNDP na kuwaahidi usimamizi makini wa fedha zote zinazotolewa, pia aliwakumbusha TFS kuongeza tija kwa miradi inayotolewa kwa wananchi wa vijiji 27 vinavyozunguka msitu wa TFS kama mbadala sahihi na kuongeza utayari wa wananchi kulinda msitu huo.

"Nategemea tukiimarisha utalii kwenye eneo la Shengena, tutawashirikisha wananchi wengi wawe sehemu ya utalii huo. Wakiona tija ya utalii, wataulinda msitu wetu ambao ni kama moyo wa Wilaya ya Same" . Alisema DC Huyo.

Ziara ya viongozi hao ilifanyika Tar. 20 na 21 Aug. 2018. Ambapo pia walikuwepo wawakilishi toka wizara ya Fedha na TAMISEMI .

Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Senyamule akimkabidhi sehemu ya zawadi, Mkurugenzi mkazi wa UNDP, Natalie Boucly alipomtembelea ofisini kwake.
Mkurugenzi mkazi wa UNDP, Natalie Boucly akiwasilikiza baadhi ya wananchi wakati alipotembelea kijiji cha Mhero kata ya Chome.
Mapunziko baada ya ziara ndefu.
Moja ya majengo 4 yaliyojengwa kupitia mradi wa Kuboresha usimamizi wa Misitu ya Mazingira Asilia na kukuza utalii kwa ufadhili wa UNDP kwa TFS

Bodi ya maji bonde la mto Pangani yajenga kituo cha polisi Sakale-Muheza

$
0
0
Bodi ya maji mto pangani yajenga kituo cha polisi katika kitongoji cha Kwelusanga kijiji cha Sakale kata ya Mbomole baada ya changamoto za uchimbaji madini kukithiri katika chanzo cha maji cha mto Zigi na katika hifadhi za mazingira.

Akisoma taarifa ya Ujenzi wa kituo cha polisi Agosti 21, 2018 Bi Arafa Magidi kaimu Afisa bonde la Pangani, amesema bodi ya maji bonde la mto Pangani limejenga kituo hicho kupitia mkandarasi Kumba Quality Contractors kwa gharama ya Tsh. 76,088,000/= (Milioni sabini na sita na elfu themanini na nane tu.) ambazo ni mchango wa pamoja wa Serikali ya Tanzania na wadau wa maendeleo.

Ameongeza kuwa kituo hiki kina vyumba viwili vya mahabusu, mahabusu ya wanaume na mahabusu ya wanawake, ofisi ya polisi, maliwato mbili (vyoo), na sehemu ya kupokelea malalamiko.

Akikabidhiwa kituo hicho Mkuu wa Wilaya muheza Mhe. Mhandisi Mwanasha Tumbo amesema, Kituo hiki kitawasaidia wananchi wa Sakale kuimarisha hali ya ulinzi na usalama kwa raia na mali zao, pia kuwasogezea huduma wananchi karibu kwani kituo cha awali kipo mbali sana na kijiji chao.

Pia aliwahasa wananchi wa Sakale kuendelea kuhifadhi mazingira na vyanzo vya maji kwa kuhakikisha hakuna uchimbaji wa madini utakao endelea katika kijiji hicho. “Kila mmoja awe mlinzi wa mwenzie, tuendelee kuwaondoa watu wanaoharibu mazingira” Alisema Tumbo.
Mhe. Mwanasha Tumbo(wakatikati) akishuhudia tukio la kusaini mkataba wa makabidhiano ya kituo cha polisi kati ya Mwenyekiti wa bodi la bonde la mto Pangani Ndugu Segule Segule na Kaimu Kamanda Mkuu wa Polisi Tanga Ndugu Lissu Jingi

Picha ya pamoja.


Exim Bank Tanzania yasheherekea Miaka 21 ya huduma nchini

$
0
0
 Wafanyakazi wa benki ya Exim Tanzania wakikata keki kuadhimisha miaka 21 ya huduma za benki hiyo nchini wiki iliyopita katika tawi la Samora Avenue. Kutoka kushoto ni mkuu wa shughuli za matawi, Eugen Masawe, Afisa wa benki- mafunzo na maendeleo, Melkiada Makongela na manager utoaji huduma mbadala, Mita Shah.
 Mkuu wa rasilimali watu wa Exim Bank Tanzania akiongea na wafanyakazi wa benki hiyo wakati wa maadhimisho ya miaka 21 ya kutoa huduma nchini wiki iliyopita katika tawi la Samora Avenue.
Wafanyakazi benki ya Exim benki.

TSN OIL YAIBUKA KIDEDEA TUZO ZA AFRICA LEDERSHIP 2018

$
0
0
TSN Oil imeshinda tuzo ya Africa Leadership Oil and Gas Retail of the Year.
TSN Oil imeshinda tuzo hiyo ya ‘Oil and Gas Retail of the Year’ ya Africa Leadership Awards 2018, katika hafla iliyofanyika jana (tarehe 26 Agosti 2018) katika ukumbi wa hoteli ya Sandton Sun, Johannesburg Afrika ya kusini.


Tuzo hizo za Africa Leadership zinalenga kutunuku Washikadau mbalimbali na viongozi waliochangia mafanikio makubwa katika kukuza uchumi na uongozi bora. Tuzo hiyo kwa TSN Oil inatambulisha Mchango wake katika sekta ya Mafuta Nchini na pia jitihada zake katika kupeperusha bendera wa ukuwaji wa sekta hiyo hapa Tanzania. Tuzo ya TSN Oil ilikabidhiwa na Senator wa Marekani jimbo la Georgia, Michaael Rhett, na kupokelewa na Mkurugenzi wa TSN Group , Bwana Farough Ahmed Baghozah mwenyewe.

Mr Farough ametambuliwa kama Mchangiaji Mkubwa katika ukuaji wa sekta na biashara ya Mafuta Nchini kutokana na Mchango wake, Muda wake wa thamani katika kupigania sekta hiyo na kwa nafasi ambayo TSN Oil imecheza hapa nchini.Mkurugenzi wa TSN Oil kampuni dada ya TSN Group yenye zaidi ya Miaka 10 kwenye sekta ya Mafuta, Farough Ahmed Baghozah akipokea tuzo hiyo amesema “Ushindi huu unamaana kubwa kwetu kama kampuni na kama Nchi kwa ujumla, unatambulisha kukua kwa sekta hii katika uchochezi wa ukuwaji wa sekta ya viwanda hapa nchini, Unaelezea safari yetu kama kampuni kwa kusimamia ubora na mhimili wa kauli mbiu yetu, Tanzania Sisi Nyumbani. “
“Tunashukuru na kuendela kuwashukuru wateja wetu kama wadau wakuu kwenye utambulisho huu, Tanzania hii ni ya kwenu.”


Kampuni ya TSN Oil yenye makazi yake makuu Dar es salaam na depo ya mafuta iliyopo Kisosora Tanga inamiliki vituo vya mafuta zaidi ya 28 na kushika asilimia 5% ya soko la Mafuta nchini Tanzania, kwa zaidi ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwake 14th November, 2006.

Mafanikio ya TSN Oil ambayo ilitokana na Chemoil yanaonekana kwa kuzalisha pia kampuni nyingine dada kama.

2009 - TSN Supermarket Ltd
2010 - TSN Logistics Ltd
2012 - TSN Distribution Ltd / TSN (UK) Ltd / TSN General Traders FZE UAE
2015 – Prime Brands Distribution Co. Ltd / TSN Media / TSN Foundation

MKURUGENZI MTENDAJI TIC AWAONYA VIONGOZI WANAOTOA MAAGIZO KWA WAWEKEZAJI BILA KUFUATA UTARATIBU

$
0
0
*Wamo wakuu wa wilaya,mikoa na mawaziri,awataka waheshimu mamlaka nyingine
*Aahidi kuandika barua kwa Kamishna wa TRA,aeleze namna wanavyowatafuta wawekezaji

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MGURUGENZI Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) Geoffrey Mwambe amewataka viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwamo baadhi ya wakuu wa wilaya,wakuu wa mikoa na mawaziri kuacha kutoa matamko na maagizo kwa wawekezaji nchini.

Amesema ni vema kila mamlaka ikatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria na kufafanua iwapo kuna tatizo lolote likiwemo la kodi,vibali au bora wa bidhaa kwa muwekezaji yoyote kuna haja ya kufuata taratibu wa kutafuta ufumbuzi kupitia mamlaka husika badala ya kutolewa maagizo ambayo hazingatii sheria.

Mwambe amesema hayo leo jijini Dar es Saalam wakati anazungumzia ziara ambayo TIC pamoja na wadau wanaohusika na sekta ya uzalishaji dawa na vifaa tiba nchini ambayo waliifanya Korea Kusini na China, ushiriki wao katika Maonesho ya Nanenane pamoja na kueleza majukumu yao ya kuelimisha umma na  kuhamasisha uwekezaji.

Hivyo ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa  kuna wimbi la viongozi  kutoa maagizo na matamko na hasa yanayohusiana na masuala ya kikodi,vibali na mambo mengine.Amesema kwamba TIC  wanafanya kazi kubwa na ngumu ya kuhamasisha wawekezaji na mitaji kuja nchini na wanatumia gharama katika kufanikisha

"Kama kuna muwekezaji yoyote ana tatizo lolote wa kufahamishwa ni kituo cha wawekezaji.Ni jambo la kushangaza Mkuu wa Wilaya anatoa makadirio ya kodi, anatoa siku mbili kodi ilipwe wakati sheria haiko hivyo.

" Unapozungumzia suala la kodi kuna utaratibu wake na sheria zake,hivyo iwapo kuna tatizo la kikodi kwa muwekezaji kiongozi wasiliana na mamlaka husika watatafuta ufumbuzi wake."Kama ni suala la vibali wapo wanaohusika na vibali kwa ajili ya wawekezaji,hivyo fuata utaratibu badala ya kutoa maagizo wakati huna mamlaka ya kufanya hivyo," amesema.

Ameongeza kwamba viongozi wote jukumu lao ni kutoa taarifa kwa mamlaka husika na si kutoa maagizo na miongozo bila kufuata taratibu.Ametoa mwito kwa viongozi wote kushirikiana na TIC katika kuhakikisha wanaendelea kuweka uaminifu kwa wawekezaji ili kifikia uchumi wakati.Pia ameomba ngazi zote za kimamlaka kila mmoja kusimama katika mipaka yake kwani kila mmoja yupo kisheria na sababu za kueleza hayo ni kukumbusha wajibu wa kila taasisi kutekeleza majukumu yake bila kuingia mipaka ya mwingine.


Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji TIC Bw. Geoffrey Mwambe akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya ofisi hizo jijini Dar es salaam leo wakati alipozungumzia kuhusu Viongozi mbalimbali wa serikali wakiwemo wakuu wa wilaya, Wakurugenzi, Wakuu wa mikoa na Mawaziri wanaotoa matamko kuhusu wawekezaji hapa nchini.
Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji TIC Bw. 
Geoffrey  Mwambe akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya ofisi hizo jijini Dar es salaam leo. Alipozungumzia kuhusu Viongozi mbalimbali wa serikali wakiwemo wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Wakuu wa mikoa na Mawaziri wanaotoa matamko kuhusu wawekezaji hapa nchini.

Waandishi wa habari na wakuu wa vitengo mbalimbali kutoka kituo cha Uwekezaji TIC wakimsikiliza Mkurugenzi wa Kituo cha hicho Bw. 
Geoffrey  Mwambe akizungumza leo.

Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images