Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

DK.SHEIN AKUTANA NA BALOZI WA BURUNDI NCHINI TANZANIA

$
0
0








Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi wa Burundi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Gervais Abayeho alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kwa mazungumzo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Balozi wa Burundi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw.Gervais Abayeho alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kwa mazungumzo.Picha na Ikulu.

WAZIRI KAMWELWE AAGIZA WALIOJENGA JIRANI NA UWANJA WA NDEGE WA NJOMBE WAONDOLEWE

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Njombe na Halmashauri yake pamoja na uongozi wa kiwanja cha ndege cha mkoa huo kuona namna ya kuziondoa nyumba zote zilizopo mita 500 kutoka katika kiwanja hicho ili kupisha ujenzi unaotarajiwa kufanyika katika kiwanja hicho hivi karibuni. 

Waziri Mhandisi Kamwelwe ametoa wito agizo hilo mkoani humo mara baada ya kutembelea kiwanja hicho na kujionea nyumba zilizojengwa kwenye hifadhi ya kiwanja hicho. Amesema kuwa ujenzi wa makazi hayo umesababishwa na Halmashauri kupima viwanja mpaka kwenye maeneo ya kiwanja hicho hivyo ni lazima waangalie namna sahihi ya kuwahamisha wakazi hao kwa kuwalipa fidia kwa wale wnaaostahili. 

“Kiwanja hiki kipo eneo zuri la tambarare, lakini tumeona wenyewe wananchi wamejenga hadi magorofa katika maeneo karibu ya kiwanja hivyo ni lazima waondolewe ili kupisha ukarabati na watakaoonekana wanahaki ya kufidiwa wafidiwe,” amesema Waziri Mhandisi Kamwelwe. 

Aidha, Mhandisi Kamwelwe amefafanua kuwa eneo hilo ambalo limejengwa ndio linalotumiwa na ndege kupaa, hivyo kama itashindwa kupaa au kutua inaweza kutua juu ya paa la nyumba ya wakazi hao na kusababisha maafa. Ameongeza kuwa Serikali ina mpango wa kujenga kiwanja cha ndege cha kimataifa mkoani humo hivyo ni lazima hatua za haraka zichukuliwe ili
kuhakikisha ujenzi huo unaanza. 

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, (kushoto) akitoa maelekezo kwa Meneja wa Kiwanja cha Ndege Njombe Bi. Hana Kibopile (wa pili kulia), wakati akikagua Kiwanja hicho, mkoani Njombe. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole-Sendeka.

Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole-Sendeka, akimuonesha maeneo yaliyovamiwa na wananchi katika Kiwanja cha Ndege cha Njombe Waziri wa  Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, wakati alipokuwa akikagua kiwanja hicho.

Muonekano wa jengo la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Njombe. Kiwanja hicho ni miongoni mwa viwanja 11 vilivyopo katika mpango wa kujengwa na Serikali ambapo upembuzi yakinifu na usanifu wa kina umekamilika. 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akikagua hatua zilizofikiwa katika ujenzi wa nyumba ya makazi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe inayojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), mkoani humo. 
Muonekano wa nyumba ya makazi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe inayojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania. 



KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>>

Serikali yatatua Mgogoro wa eneo la Wasanii Wachongaji na Wafanyabiashara hiyo uliodumu kwa miaka 33

AMANA BENKI IMEANZA KUTOA HUDUMA KWA WATEJA KUPITIA WHATSAPP

$
0
0
Amana Benki inaendelea kujivunia kuwa benki ya kwanza Tanzania inayoendeshwa kwa kuzingatia misingi ya kiislamu, yenye malengo ya kutoa huduma za kibenki za kisasa na za kipekee, kwa njia iliyowazi na kwa kutumia teknolojia ya kisasa kwa manufaa ya wateja na wadau wote. Amana Benki kwa takribani miaka saba sasa imekuwa kwa kasi huku ikihudumia watu wote bila kubagua dini zao.

Katika kurahisisha kutoa huduma za kibenki kwa wateja, Amana Bank imekuwa ikiwafikia wateja kwa njia mbalimbali ikiwemo matawi yake, mawakala, huduma za kibenki kupitia simu ya mkononi na intaneti na hata ikibidi kuwafata wateja mahali walipo.

Kwa mujibu wa benki hiyo mnamo mapema mwezi Agosti,imezindua rasmi njia rahisi ya mawasiliano na wateja wake kwa kutumia mfumo mpya wa njia ya simu maarufu kwa jina la Whatsapp.

Kwa sasa wateja wa benki hiyo na watu wote kwa ujumla wanaweza kutumia programu ya simu ya mkononi maarufu kwa jina la Whatsapp kupata huduma moja kwa moja kutoka kitengo cha huduma kwa wateja kupitia namba 0657 980 000.

Akizungumza ofisini kwake Mkurugenzi Mtendaji wa Amana Benki Dkt Muhsin Salim Masoud alisema kuwa “tumeshawishika kuanza kutumia mtandao wa WhatsApp katika kitengo chetu cha huduma kwa wateja ili kwenda sambamba na matumizi ya teknolojia ya mawasiliano katika kuboresha huduma kwa wateja wetu,  matumizi ya WhatsApp yatawezesha wateja wetu kuwasiliana na kitengo chetu cha huduma kwa wateja hata wakiwa nje ya nchi au mahali popote ambapo hawawezi kupiga simu ya kawaida”. Aliongeza kuwa kwa sasa matumizi ya mawasiliano kwa njia ya WhatsApp na Intaneti kwa ujumla yameshika kasi kubwa hivyo ni busara kutumia njia hii ilikuwapa fursa na urahisi watu na wateja wenye kumudu kutumia njia hii kupata huduma kwa wepesi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Amana Bank, Dk. Muhsin Salim Masoud akizungumza jambo wakati akizungumzia huduma ya mtandao wa WhatsApp katika kitengo cha huduma kwa wateja ili kwenda sambamba na matumizi ya teknolojia ya mawasiliano katika kuboresha huduma kwa wateja.

Teknolojia inakua kwa kasi sana na wateja sasahivi wanahitaji njia mbadala na rahisi ili waweze kuwasiliana na kupata taarifa za kibenki kwa muda wowote. Hii ndio sababu inayotusukuma kubuni namna ya kurahisisha njia zetu za mawasiliano na wateja popote pale walipo”, alisema Kaimu Meneja Mkuu wa Biashara Bw. Dassu Mussa.

Njia hii itawawezesha watu wote wanaotumia simu pendwa (smart phone) zilizomo katika mfumo wa IOS na Android kuweza kupata huduma mara moja bila ulazima wa kufika katika matawi ya Amana Benki.

Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Amana Benki ametoa rai kwa watu kutumia njia hii ya mawasiliano vizuri ili kupata huduma kwa wakati na ameahidi kuwa Amana Benki itaendelea kutoa huduma bora za kibenki kwa kuzingatia matumizi ya teknolojia ya kisasa kwa manufaa ya wadau wote.

SPORTPESA NA EVERTON ZASHINDA TUZO ZA SPORTS INDUSTRY AWARDS

$
0
0
Kampuni ya michezo ya kubashiri SportPesa na Klabu ya mpira wa miguu ya Uingereza ya Everton zimezawadiwa zawadi kutokana na ushirikiano wao kwenye tuzo za Sports Industry Awards kwenye vipengele vya Best African Sponsorship na Pan-African Campaign of the year.

Kwenye udhamini huo ambao ulianza kwa klabu ya Everton kusafiri kwenda Dar es Salaam Julai 2017 kucheza na Mabingwa wa SportPesa Super Cup ambao walikuwa klabu ya Gor Mahia kutoka Kenya, umetambuliwa na kusherekewa kwa kuwaleta Everton wanaoshiriki ligi kuu ya Uingereza kwenye Ukanda wa Afrika Mashariki kwa mara ya kwanza.

Kutokana na mafanikio ya safari hiyo ambayo ilijulikana kama 'Everton in Tanzania' , ambayo pia ilileta hamasa kwenye michezo na kuipa ushindi wa tuzo hizo ambazo zilitangazwa Sandton Convention Centre jijini Johannesburg Ijumaa ya tarehe 17 Agosti 2018.

Mkuu wa Ushirikiano na Utawala wa klabu ya Everton Mark Rollings alisema "Tunayo furaha kuwa ushirikiano wetu na SportPesa umetambulika kwenye ngazi  muhimu ya Sports Industry Awards. Tuzo za Sports Industry Awards ndio tuzo zenye heshima kubwa Afrika Kusini kwa upande wa michezo na kwa hivyo kushinda tuzo zote mbili za Best African Sponsorship na Pan-African Campaign of  the Year ni udhibitisho wa kuendeleza ushirikiano wetu na SportPesa pamoja na wadau wake.
 Meneja masoko SportPesa South Afrika Gail Rodgers, Mkuu wa kitengo cha masoko SportPesa Kelvin Twissa, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Susan Mlawi, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti SportPesa Tanzania Tarimba Abbas na Mkuu wa kitengo ca Ushirikiano Everton Mark Rollings mara baada ya kukabidhiwa tuzo za Sport Industry Awards.
 Wawakilishi kutoka SportPesa Tanzania, Kenya, South Africa,Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Tanzania, Timu ya Everton wakipokea tuzo mara baada ya kutangazwa kuwa washindi.
 Katibu wa wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Susan Mlawi akiwa na Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti SportPesa Tanzania Tarimba Abbas  wakiwa na tuzo mbili za Sport Industry Awards ambazo kampuni ya SportPesa imeshinda kwenye vipengele vyote viwili.


DC NAMTUMBO AKERWA NA UHABA WA MAJI,AIAGIZA MAMLAKA YA MAJI KUANZISHA MKAKATI WA KUNUSURU HALI HIYO

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma bi. Sophia Kizigo alikerwa na uhaba wa maji katika mji wa Namtumbo na kuagiza mamlaka ya maji mjini Namtumbo kuanzisha mkakati wa makusudi kunusuru hali hiyo.

Akipokea taarifa za idara na vitengo kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe na Mh.Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Drt. John PombeMagufuli kuwa mkuu wa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.

Aidha mkuu wa wilaya huyo alionesha kukerwa na uhaba wa maji katika mji wa Namtumbo na kuitaka mamlaka ya maji mjini Namtumbo kuanzisha mkakati wamaksudi ilikutatua tatizo la uhaba wa maji Mjini hapa.

Mohamedi Mmbaga kaimu Meneja wa mamlaka ya maji mjini Namtumbo (NAUWASA)alimwambia mkuu wa wilaya hiyo tatizo la uhaba w a maji huo linalotokana na miundombinu ya maji inayotegemewa ni ya kijiji na sio yawilaya.Bwana Mmbaga alidai mradi wa unaotumika mjiniNamtumbo ulijengwa mwaka 1981 ukihudumia vijiji vine ambavyo ni Libango,Suluti,NahoronaLuegu na kiasi cha maji kinachozalishwa ni mita zaujazo 1,211 kwa siku huku mita zaujazo 580 pekee kwa siku ndizo zinazofika na kutumika.

Mmbaga pia alidai kiasi hicho cha maji ni kidogo ukulinganisha na watu wanaohitaji huduma hiyo ni 40,697 mpaka sasa niwatu 8,932 ambao wanapata huduma hii sawa na asilimia 21 na kuwaachan watu 31,765 kukosa huduma hiyo.

Pamoja na hayo Mamlaka ya maj iMjin I Namtumbo kwa kushirikiana na Mamlaka ya maj I safi na usafi wa Mazingira manispaa ya Songea inatekeleza mradi wa maji mjini Namtumbo kwa kukarabat I bomba kuu umbali wa km.1.08 na pia ujenzi watenki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa M135 ambapo mradi huo ulifikia asilimia 82 na utachangia ongezeko la maji kwa asilimia 14katika mji wa Namtumbo pamoja nautekelezaji wa mradi wa maji wa mto Rwinga ambao na utaongeza kiasi mita zaujazo 1000 kwasiku.

Wilaya ya Namtumbo ilitangazwa kuwa wilaya mwaka 2002 ambapo miundo mbinu ya maji katika mji wa Namtumbo ilikuwa ya vijiji na sasa ni makao makuu ya wilaya ambapo panaongezeko kubwa la watu wakihitaji huduma hiyo ya maji huku miundombinu ni ya mwaka 1981.

NHIF YAPATA CHETI CHA UBORA WA VIWANGO VYA KIMATAIFA "ISO 9001:2015"

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile (wa pili kulia) akipokea Cheti cha Mfumo wa Uhakiki bora wa kiwango cha Kimataifa (ISO 9001:2015) kutoka kwa Muwakilishi wa Taasisi ya BSI (British Standards Institute), Mini Sharma (kushoto) iliyotolewa kwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF). Wanaoshuhudia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko huo, Spika wa Bunge Mstaafu, Anna Makinda (wa pili kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile (katikati) akikabidhi Cheti cha Mfumo wa Uhakiki bora wa kiwango cha Kimataifa (ISO 9001:2015) kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Spika wa Bunge Mstaafu, Anna Makinda kilichotolewa na Taasisi ya BSI (British Standards Institute) kwa Mfuko huo leo Agosti 20, 2018.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Spika wa Bunge Mstaafu, Anna Makinda (katikati) naye alikabidhi cheti hicho kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga akionyesha cheti hicho kwa wageni mbalimbali waliohudhulia hafla hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza wakati akitoa hotuba yake katika hafla ya kupokea Cheti cha Mfumo wa Uhakiki bora wa kiwango cha Kimataifa (ISO 9001:2015) kilichotolewa na Taasisi ya BSI (British Standards Institute)  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), leo Agosti 20, 2018.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Spika wa Bunge Mstaafu, Anna Makinda akifurahi jambo wakati akizungumza katika hafla hiyo.

WIZARA YA NISHATI YAWAKABIDHI BARUA ZA UDAHILI WATANZANIA WALIOPATA UFADHILI KWENDA KUSOMA CHINA

$
0
0

Na Avila Kakingo,globu ya jamii.
KATIKA kukuza sekta ya mafuta na gesi hapa nchini serikali ya china yawapa ufadhili watanzania 20 kwenda nchini chini kusomea maswala ya mhimu ya gesi na mafuta ikiwa ni njia mojawapo ya kupunguza changamoto ya ukosefu rasilimali watu watakao simamia sekta hiyo.

 Akizungumza wakati wa kuwaaga watanzania hao 20 watakaoenda nchini china kusoma masuala ya mafuta na gesi, Katibu mkuu wa wizara ya nishati, Dk. Khamisi Mwinyimvua amesema kuwa wizara imekuwa ikidhamini watanzania kupitia serikali yawatu wa China katika fani ya mafuta na gesiipasavyo ili kutatua changamoto ya ukosefu wa lasilimaliwatu katika sekta hiyo.


“Kukua kwa sekta ndogo ya mafuta na gesi kumeleta changamoto ya upungufu wa rasilimali watu ya kusimamia sekta hiyo sasa wizara ya nishati ikishirikiana na serikali ya watu wa china imetoa ufadhili kwa watanzania 20 watakaoenda kusoma nchini China maswala ya mafuta na gesi, na leo tunawakabidhi barua za udahili.”


Mwinyimvua amesema kuwa serikalikupitia wizara ya Nishati na madini ilikubaliana na serikali ya watu wa china ili kutoa ufadhili huo wa masoma kwa fani ya mafuta na gesi kwa ngazi ya shahada ya uzamili na uzamivu kwa watanzania kwa kila mwaka kwa kipindi cha miaka mitano hadi 2019.

Pia amewaasa watanzania waliobahatika kuchaguliwa kupata ufadhili huo kutumia fursa hiyo vizuri kwa manufaa ya taifa kwa ujumla katika kuliwezesha taifa kutimiza malengo na dira ya maendeleo ya taifa katika sekta ya mafuta na gesi.

Katibu mkuu wa wizara ya nishati, Dk. Khamisi Mwinyimvua akiwakabidhi barua za udahili watanzania 20 waliopata ufadhili kwenda nchini china kusoma masuala ya gesi na Mafuta.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.


NAIBU WAZIRI ATEMBELEA KIWANDA CHA MZAVA MOROGORO

$
0
0
 Naibu Waziri Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Mhandisi Stella Manyanya (Mb) atembelea kiwanda cha Mazava kilichopo mkoani Morogoro.

Naibu Waziri Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Mhandisi Stella Manyanya (Mb) akiangalia nguo zilizozalishwa katika kiwanda cha Mzava alipotembelea kiwanda hicho kilichopo mkoani Morogoro.

Katika ziara hiyo Naibu Waziri amepokea taarifa ya kiwanda ambacho kinaendelea na uzalishaji wa fulana na bukta mbalimbali ambazo kwa asilimia 100 husafilishwa nje ya nchi kwa mauzo,Kiwanda kimeajiri wafanyakazi 2180 wenye mikataba ya kudumu ambao asilimia 70 ni wanawake na asilimia 30 ni wanaume pia kiwanda kinaendesha programu ya mafunzo kwa Vijana 210 ambao huajiriwa na kiwanda baada ya kuhitimu kuziba nafasi mbalimbali kiwandani hapo.

Meneja Msaidizi wa kiwanda cha Mazava, ndugu Nelson Mathias Mchuke alimweleza Naibu Waziri changamoto mbalimbali za kiwanda ikiwemo ufinyu wa eneo la uzalishaji kwani kiwanda kimekodi eneo jingine lakini changamoto imekuwa ni idhini ya kutumia eneo husika, pia ubovu wa Barabara kufika na kutoka kiwandani hapo.

Meneja Msaidizi wa Kiwanda hicho amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa juhudi anazofanya kupitia Viongozi aliowateua kwani serikali ya awamu ya tano imeweza kutatua changamoto mbalimbali kiwandani hapo ikiwemo ya umeme.

Naibu Waziri Mhandisi Stella Manyanya, amewapongeza menejimenti ya kiwanda kwa kutengeneza ajira kubwa katika Mkoa wa Morogoro, pia amewahakikishia kushughulikia changamoto walizomweleza kwa haraka zaidi hasa ya kuanza kutumia jengo jipya ambalo litaongeza ajira ya watu 1000.

KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI MEJA JENERALI JACOB KINGU ATEMBELEA NIDA

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Jacob Kingu amefanya ziara kwenye kituo Kikuu cha Uchakataji, Uzalishaji na Utunzaji wa Taarifa (Data Centre) kilichoko Kibaha mkoani Pwani na kukagua shughuli za uchakataji wa taarifa na uzalishaji wa Vitambulisho.

Pia amefanya mazungumzo na Menejimenti ya NIDA na kusisitiza umuhimu wa kuongeza kasi ya Uzalishaji kwa kuharakisha mchakato wa upatikanaji wa mitambo ya kisasa haraka ili kuongeza nguvu ya Uzalishaji kufuatia asilimia kubwa ya wananchi kukamilisha hatua ya awali ya Usajili na uchukuaji alama za kibaiolojia.

Akizungumza kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu; Mkurugenzi wa Uzalishaji Ndg. Alphonce Malibiche ameeleza mpaka sasa Mamlaka imefikia hatua nzuri katika Usajili na uzalishaji wa Namba za Utambulisho na kazi kubwa iliyopo sasa ni ya uzalishaji ambao umekuwa ukienda taratibu kutokana na uwezo mdogo wa  mashine zilizopo kushindwa kuzalisha kadi nyingi kwa mara moja.

Hata hivyo amesema tayari Mamlaka ilishachukua hatua za kuagiza mashine mpya na za kisasa kusaidia kuongeza kasi ya Uzalishaji na tayari mchakato wa kumpata mzabuni umefikia hatua nzuri na pindi taratibu zitakapokamilika mashine hizo zitafungwa mara moja.

Meja Jenerali Kingu amepongeza jitihada kubwa na nzuri zinazofanywa na Mamlaka na kusisitiza umuhimu wa wafanyakazi kufanya kazi kwa uzalendo na uadilifu mkubwa huku akiielekeza Menejimenti kuangalia namna bora ya kulinda na kuongeza maslahi ya watumishi wake; ili kuongeza morali na ufanisi katika utendaji.

Mamlaka inaendelea na zoezi la kuwasajili wananchi nchi nzima na mpaka sasa imeshasajili zaidi ya wananchi mil 19.2 nchi nzima; na hadi kufikia mwezi Desemba 2018 imelenga kuwa imesajiliwa zaidi ya watanzania mil 22.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Jacob Kingu  (kushoto mwenye Kaunda suti nyeupe) akisikiliza maelezo ya jinsi uchakataji wa taarifa unavyofanywa na maafisa wa NIDA alipotembelea kituo cha Uchakataji wa taarifa. Kulia ni Ndg. Alphonce Malibiche (mwenye tai nyekundu) Mkurugenzi wa Uzalishaji akitoa maelezo; na waliomzunguka ni baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya NIDA.

 Watumishi katika kitengo cha Uchakataji wa taarifa wakiendelea na hatua za uhakiki wa taarifa wakati wa ziara ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Jacob Kingu
 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Jacob Kingu akikagua kazi inayofanywa na watumishi katika kituo cha Uchakataji wa Taarifa
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Jacob Kingu akibadilishana mawazo na Mkandarasi wa Ujenzi wa kituo cha Uchakataji wa Taarifa Kibaha Mr. Kim(Mwenye tai ya bluu), akiwa amezungukwa na wakurugenzi na wakuu wa Vitengo wa Mamlaka.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Jacob Kingu katika picha ya pamoja na viongozi wa Menejimenti ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa inayoundwa na Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo na Meneja.

CMSA,CISI WAZINDUA MPANGO WA KUENDESHA MAFUNZO ENDELEVU YA KITAALUMA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Glogu ya jamii

MAMLAKA ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA)kwa kushirikiana na Taasisi ya mafunzo ya masoko ya Mitaji na uwekezaji (CISI) wamezindua mpango wa kuendesha mafunzo endelevu ya kitaaluma kwa washiriki wa masoko ya mitaji nchini, (CPD).

Ushirikiano huo ni sehemu ya mkakati ya kuwajengea uwezo na kuimarisha ufanisi kwa watendaji na wataalamu wanaishiriki katika mitaji ili kufikia viwango vya ubora wa kimataifa,
(EASRA).

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo jijini Dar es Salaam Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa CMSA, Nicodemus Mkama amesema,    mpango huo unaweka utaratibu na vigezo vya ushiriki kwa washiriki wa masoko ya mitaji kufikia angalau masaa 10 ya ushiriki wa mafunzo ya masoko ya mitaji kwa mwaka.

Na kuwa hiyo itakuwa kigezo kimojawapo cha utoaji wa lesebi ya ushiriki katika masoko ya mitaji ifikapo Januari mwaka 2020.

Ameongeza kuwa washiriki wa masoko ya mitaji walio na leseni watatakiwa kufanya mafunzo na kutekeleza mipango inayotambuliwa na CMSA na CISI katika kutekeleza vigezo vya mpango wa mafunzo endelevu na kupewa idhini itakayotolewa kwa taarifa maalumu itayowasilishwa CMSA kwa ajili ya taarifa na kuweka kumbukumbu.

" Mpango wa mafunzo endelevu utawawezesha watendaji ndani ya masoko ya mitaji kutoa huduma kwa umahiri mkubwa zaidi kwa kuendana na maendeleo yanayotokea katika masoko ya mitaji duniani,"amesema Mkama na kuongeza.

"Ushirikiano kati ya Mamlaka ya taasisi ya CISI unayaweka masoko ya mitaji ya Tanzania katika ramani ya masoko ya mitaji ya dunia kwa kuwa na wataalamu wanaokidhi viwango vhhya kimataifa," amesema.

Kwa upande wa Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya CMSA, Emmanuel Kakwezi kwa niaba ya mwenyekiti, ameitaka mamlaka kuhakikisha inakuwa na wataalamu wa kutosha katika masoko ya mitaji wanajiunga na mpango huo ili kulinda uwezo wa kitaaluma na uhalali wao katika ulimwengu wa ushindani.

Amesema masoko ya mitaji ni sekta inayobadilika kwa kasi na yenye kuhusisha viashiria vya aina mbali mbali,

Wakati huo huo Mkurugenzi wa DCSI, Kevin Moore ushirikiano huo utawawezesha watanzania kuongeza uwezo wa kuelewa kwa nji ya mitandao na hata ile njia halisi.

Pia amesema mafunzo hayo endelevu yatasaidia wataalamu na kuifanya Tanzania kuendelea kuongeza ufanisi katika soko la kimataifa.
   Mjumbe wa Bodi  ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Masoko ya mitaji na dhamana, Emmanuel Kakwezi akisoma taarifa yake kuashiria uzinduzi wa mpango wa kuendesha mafunzo endelevu ya kitaaluma kwa washiriki wa masoko ya mitaji nchini, (CPD).
Mkurugenzi wa CISI,  Kevin Moore akifafanua jambo kwa washiriki wakati wa uzinduzi wa mpango wa kuendesha mafunzo endelevu ya kitaaluma kwa washiriki wa masoko ya mitaji nchini, (CPD).
Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa CMSA, Nicodemus Mkama akielezea umuhimu wa wa mpango wa ushirikiano wa CMSA na CISI kwa washiriki wakati wa uzinduzi wa mpango wa kuendesha mafunzo endelevu ya kitaaluma kwa washiriki wa masoko ya mitaji nchini, (CPD).

CASTLE LITE YANOGESHA TAMASHA LA MUZIKI LA STR8UP JIJINI DAR

$
0
0
Wakazi wa vitongoji mbalimbali vya jiji la Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki wakipata burudani moto moto ya muziki katika tamasha la muziki lililoandaliwa na kampuni ya masuala ya burudani ya STR8UP na kufanyika katika ukumbi wa Velisas-Kawe, chini ya udhamini wa bia ya Castle Lite.
Meneja wa Mawasiliano ya Wateja wa TBL, David Tarimo, (katikati) akiwa na Mtalaamu wa Ubunifu nchini Ally Remtulla (kulia) wakati wa tamasha la la Muziki la STR8UP, lililofanyika katika ukumbi wa Velisas Kawe, wakipata burudani kwa udhamini wa bia ya Castle Lite .
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam, waliohudhuria katika tamashala la Muziki la STR8UP, lililofanyika katika ukumbi wa Velisas Kawe wakipata burudani kwa sambamba na kinywaji cha Castle Lite.
DJ akionyesha umahiri wake wakati wa tamasha la Muziki la STR8UP, lililofanyika katika ukumbi wa Velisas Kawe jijini Dar es Salaam, kwa udhamini wa bia ya Castle Lite.
Mtaalamu wa kupiga drum, Haidery Vagu, akionyesha umahiri wake katika tamasha hilo.

YALEYALE

$
0
0
 Wajasiria mali wakiwa wameweka biashara katika miundombinu ya DART Kimara jijini Dar as Salaam.
Kamera Globu ya jamii leo imenasa  wakazi wa jiji Dar es Salaam wajasiriamali maarufu kama machinga wakiwa mameweka biashara zao katika enao Kimara kwenye miundombinu ya (DART) huku pakiwa na kibao kinacho zuwia kufanya biashara katika eneo hilo.
Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii.

TFDA YASHIRIKIANA NA HALMASHAURI YA URAMBO KUTOA MAFUNZO KWA WAJASIRIAMALI WA VIWANDA VIDOGO VIDOGO VYA USINDIKAJI VYAKULA

$
0
0
Na Gaudensia Simwanza – Urambo.

TFDA kwa kushirikiana na uongozi wa Wilaya ya Urambo, mkoani Tabora, wanaendesha mafunzo ya siku tano kwa wajasiriamali wadogo 150 wa usindikaji wa vyakula wilayani humo kuanzia leo tarehe 20/8/2018  ili kuchangia  ukuaji wa Sekta ya viwanda nchini sanjari na kuinua uchumi wa wananchi wa Urambo.



Mafunzo hayo yamefunguliwa na Mgeni Rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe. Angelina Kwingwa na kuhudhuriwa na viongozi wengine wa Wilaya hiyo wakiwemo Mbunge,  Mhe. Margareth Sitta (Mb.), Katibu wa CCM wa wilaya, Bi. Jesca Mbogo na Mkurugenzi wa wilaya, Bi. Margareth Nakainga miongoni mwa viongozi wengine.



”TFDA inatambua mchango mlio nao katika kukuza viwanda vidogo vya chakula kwani kutokana na uwingi wake vina mchango mkubwa katika; kuongeza ajira na kipato katika ngazi ya kaya, kukuza kilimo cha mazao ya chakula na kuyasindika na hatimaye kuiwezesha Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda na ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025”, alisisitiza Mgeni Rasmi huyo.



Ili kuwawezesha wajasiriamali wadogo nchini kutatua changamoto zinazowakabili katika usajili wa majengo na bidhaa zao, uongozi wa Wilaya umeamua kuweka mkakati wa makusudi ikiwa ni pamoja na kuwaalika wataalam wa Serikali kuja kutoa mafunzo kama haya ili kuinua maisha ya wananchi wake na Taifa kwa ujumla”, Mkuu huyo wa Wilaya aliongeza.



TFDA inaendelea kushirikiana uongozi wa Mikoa na Halmashauri zake ili kuwawezesha Watanzania kuanzisha viwanda vidogo, vya kati na vikubwa kwa kuzingatia vigezo vya usalama na ubora ili kupata soko la ndani na nje ya nchi kwa bidhaa zetu kwa maendeleo ya Taifa
 Mgeni Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Urambo Mhe. Angelina Kwingwa, (aliyesimama) akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mafunzo yanayoendeshwa na TFDA kwa Wajasiriamali wa Wilaya ya Urambo. Viongozi wengine wa wilaya hiyo kutoka kushoto ni Mbunge wa wilaya Mhe. Margareth Sitta (wa tano), Mkurugenzi wa wilaya, Bi. Margareth Nakainga (wa sita), Meneja wa TFDA Kanda ya Magharibi, Dkt. Edgar Mahundi (wa saba), Katibu wa (CCM) wa wilaya, Bi. Jesca Mbogo (wa tatu), na Mwenyekiti wa semina hiyo, Bi. Martha Susu (wa n ne).

 Mbunge wa wilaya ya Urambo Mhe. Margareth Sitta (aliyesimama), akiwasalimia wajasiriamali wanaohudhuria mafunzo wilayani Urambo.
Sehemu ya Wajasiriamali  wilaya ya Urambo wakifuatilia mafunzo yanayotolewa na (TFDA).

POLISI KILIMANJARO YANASA KILOGRAMU 520 ZA MIRUNGI

$
0
0
Na Dixon Busagaga wa 
Globu ya Jamii kanda ya Kaskazini.
 JESHI la Polisi mkoa wa Kilimanjaro limefanikiwa kukamata viroba saba vya Dawa za kulevya aina ya Mirungi sawa na kilogramu 520 zikiwa zimebebwa na watembea kwa miguu ambao walikuwa wakivusha kutoka nchi jirani ya Kenya kuingia Tanzania. 
 Mbali na viroba hivyo Polisi pia inamshikilia mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Samwel Muro(21) raia wa Kenya mkazi wa Kitobo baada ya kukutwa akiwa amebeba kichwani moja ya Viroba hivyo huku wengine kadhaa wakifanikiwa kuwakimbia askari baada ya kutupa mizigo ya dawa hizo. 
 Kamanda wa Polisi mkoa wa KilimanjaroKamishna Msaidizi wa Polisi Hamis Issah alithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo jana majira ya 8:30 mchana pamoja na pikipiki moja iana ya Haojue yenye namaba za usajili MC 909 BUZ ambayo inatajwa kuhusika katika usafirishaji wa mizigo hiyo. 
 “Hii mirungi ilikamatwa katika  kijiji kinachoitwa  Mnoa, kata ya Kileo wilayani Mwanga. Askari Polisi wakiwa doria walikamata viroba saba vya mirungi na  walienda kwenye bonde moja na kukuta watu wametoka Kenya wamejaza hii mirungi kwenye magunia wakiwa wameificha kwenye hilo bonde.
"Kumbe wana utaratibu wao bonde likijaa wanachukua pikipiki zaidi ya 30 kwa ajili ya kusafirisha mirungi na wanasafiri kwa makundi makubwa ya pikipiki”, alisema Kamanda Issah. 
Kamanda Issah alisema baadhi ya vifurushi hivyo vya Mirungi vimekutwa vikiwa vimeandikwa majina ya vijiji kuanzia njia Panda ya Himo kuelekea Dar es Salama yakiwemo maeneo ya Segera, Chalinze hadi Kibaha.
Mtuhumiwa wa usafirishaji wa Dawa za kulevya aina ya Mirungi akiwa kwenye gari la polisi na viroba vilivyojaa dawa hizo za kulevya zilizokamatwa katika moja ya bonde mpakani mwa Kenya na Tanzania.
Askari polisi wakishusha viroba vyenye dawa za kulevya aina ya mirungi kituo kikuu cha polisi Kilimanjaro.
Mtuhumiwa wa usafirishaji wa Mirungi Samwel Muro mkazi wa Kitobo nchini Kenya akiwa chini ya ulinzi na pemebeni yake ni vifurushi vyenye mirungu alivyokutwa navyo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ACP Hamis Issah akitoa maelekezo kwa askari wake mara baada ya kukamatwa kwa mirungi hiyo. Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

MANZESE UNITED YAKABIDHI KOMBE KWA MEYA UBUNGO

$
0
0
 Mabingwa wa Mashindano ya Mpira wa Miguu yanayoandaliwa na CLOUDS MEDIA GROUP,ambayo ni NDONDO CUP. Leo 20August 2018 wamefika Ofisini kwa Mstahiki Meya  Boniface Jacob na kulikabidhi kombe hilo kama ishara ya Shukrani kwa Uongozi wa Manispaa ya Ubungo na Mshikamano na wanamichezo. Mstahiki Meya amehaidi ushirikiano wanamichezo wote wa Ubungo watakao kuwa wanaiwakilisha manispaa kwenye michuano mbalimbali.
Picha ya pamoja baada ya meya wa ubungo kupokea kombe.

ZIWA SINGIDANI NA KINDAI KUTANGAZWA KAMA MAENEO LINDWA KIMAZINGIRA

$
0
0
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe.
January Makamba amesema Ofisi yake inaangalia uwezekano wa kutangaza
Ziwa Singidani na Ziwa Kindai katika Halmashauri ya Singida kama maeneo
lindwa kimazingira kwa kuwa yako hatarini kutoweka.

Waziri Makamba ameyasema hayo hii leo Mkoani Singida ikiwa ni siku ya
kwanza ya ziara yake katika Mikoa 9 hapa nchini yenye lengo kukagua,
kutathmini na kuzungumza na viongozi, wataalam, watendaji na wananchi
kuhusu maeneo yanayopendekezwa kuhifadhiwa kwa mujibu wa Sheria ya
Mazingira kifungu namba 51.

Aidha, Waziri Makamba amesema kuwa mara baada ya kutoa tangazo hilo
katika gazeti la Serikali matumizi sahihi ya maziwa hayo yataainishwa ikiwa nipamoja na kupanda miti rafiki kuzunguka maeneo yote na kuzingatia makatazo yatakayotolewa.

“Ziwa Singidani liko hatarini kutoweka kutona na shughuli za kibinadamu,
hivyo kwa kutumia Sheria ya Mazingira nitashauriana na wataalamu wangu
kuona namna bora ya kunusuru maziwa haya ikiwa ni pamoja na
kuyatangaza kwenye gazeti la Serikali kama maeneo lindwa kimazingira.”
Makamba alisisitiza.

Imebainika kuwa, lengo la kuainisha na kutangaza maeneo hayo ni kulinda
mifumo muhimu ya kiikolojia (ikiwemo vyanzo vya maji, mito, maziwa,
mabwawa, milima na vilima, chemichemi, ardhi oevu, mazalia ya samaki na
misitu) ambayo hayana ulinzi wa Sheria nyingine.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akifafanua vifungu vya Sheria ya Mazingira mbele ya Watendaji na Viongozi wa Mkoa wa Singida juu ya maeneo lindwa. Wengine katika picha ni viongozi wa Mkoa wa Singida wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Rehema Nchimbi (wa pili kutoka kushoto).
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akijionea uharibifu wa mazingira katika Ziwa Singidani ambao unatokana na shughuli za kibinadamu. Waziri Makamba ameazimia kunusuru Ziwa hilo pamoja na vyanzo vyake. Wengine katika picha ni viongozi kutoka Manispaa ya Singida.

Ziwa Singidani ambalo liko hatarini kutoweka kutokana na shughuli zisizo endelevu za kibinadamu. Waziri Makamba yuko katika ziara ya kikazi ya kukagua na kuona namna bora ya kunusuru Ziwa hilo pamoja na mengine kwa mustakabali wa nchi yetu.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>

BODI YA WAKURUGENZI YA TIB YATOA POLE KWA RAIS MAGUFULI

Mwakyembe amaliza mgogoro wa ardhi Mwenge Vinyago uliodumu kwa miaka 33

$
0
0
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (kushoto) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari na wasanii wa kuchonga vinyago (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya kumaliza mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka 33 katika eneo la vinyago Mwenge jijini Dar es salaam. Katikati ni  Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa nchini (BASATA) Geofrey Mngereza na kulia ni Rais wa Shirikisho la Sanaa za Uchongaji, Adrian Nyangamale.
 Baadhi ya wasanii wa sanaa za uchongaji wakimsikiliza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) wakati akitoa taarifa ya kumaliza mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka 33 katika eneo la vinyago Mwenge.
Rais wa Shirikisho la Sanaa za Uchongaji, Adrian Nyangamale (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari na wasanii wa kuchonga vinyago (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya kumaliza mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka 33 katika eneo la vinyago Mwenge. Kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe na katikati ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa nchini (BASATA) Geofrey Mngereza. Picha na MAELEZO

KATIBU MKUU WA CCM AAGANA NA VIONGOZI WA CCM ZANZIBAR BAADA YA KUKAMILISHA ZIARA YAKE PEMBA

$
0
0


Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Dk. Bashiru Ally akiagana na Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Shaka Hamdu Shaka mara baada ya kukamilisha ziara yake ya kujitambulisha kwa Wana-CCM Pemba.
Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Dk. Bashiru Ally akiagana na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Organazesheni CCM Zanzibar Bakari Hamad Khamis mara baada ya kukamilisha ziara yake ya kujitambulisha kwa Wana-CCM Pemba.
Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Dk. Bashiru Ally akiagana na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Uchumi na Fedha Zanzibar Ndugu Afadhali Taib Afadhali (kushoto) mara baada ya kukamilisha ziara yake ya kujitambulisha kwa Wana-CCM Pemba.
Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Dk. Bashiru Ally akiwa katika ndege ya Kampuni ya Assalam Air akiwapungia mkono wana CCM na viongozi wa CCM walioshiriki kumuaga katika uwanja wa ndege Pemba.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images