Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110114 articles
Browse latest View live

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AHUDHURIA DHIFA ILIYOANDALIWA NA RAIS WA NAMIBIA MJINI WINDHOEK

$
0
0

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika ukumbi wa Country Club mjini Windhoek kuhudhuria dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Mwenyekiti mpya wa SADC na Rais wa Namibia Dkt. Hage Geingob kwa heshima ya viongozi wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Afrika ya Kusini (SADC) Ijumaa usiku Agosti 17, 2018
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na viongozi wenzake wakisimama wakati nyimbo za taifa zikipigwa katika ukumbi wa Country Club mjini Windhoek kuhudhuria dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Mwenyekiti mpya wa SADC na Rais wa Namibia Dkt. Hage Geingob kwa heshima ya viongozi wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Afrika ya Kusini (SADC) Ijumaa usiku Agosti 17, 2018
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi wezake katika ukumbi wa Country Club mjini Windhoek kuhudhuria dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Mwenyekiti mpya wa SADC na Rais wa Namibia Dkt. Hage Geingob kwa heshima ya viongozi wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Afrika ya Kusini (SADC) Ijumaa usiku Agosti 17, 2018
Mwenyekiti mpya wa SADC na Rais wa Namibia Dkt. Hage Geingob (wa tatu kushoto) na wageni wake kwenye dhifa ya kitaifa aliyoandaa kwa heshima ya viongozi wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Afrika ya Kusini (SADC) Ijumaa usiku Agosti 17, 2018. Wengine kutoka kushoto ni Rais Edgar Lungu wa Zambia, Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika ya Kusini, Mama Geingob, Katibu Mtendaji wa Sadc Dkt. Sergomena Tax na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Nambia, Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hasna Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Dkt. Augustine Mahiga, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Edwin Paul Mhede (wa pili kushoto), Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Ali Khamis, Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini Mhe. Sylvester Ambokile na afisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika ukumbi wa Country Club mjini Windhoek baada ya dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Mwenyekiti mpya wa SADC na Rais wa Namibia Dkt. Hage Geingob kwa heshima ya viongozi wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Afrika ya Kusini (SADC) Ijumaa usiku Agosti 17, 2018
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiondoka ukumbi wa Country Club mjini Windhoek kuhudhuria dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Mwenyekiti mpya wa SADC na Rais wa Namibia Dkt. Hage Geingob kwa heshima ya viongozi wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Afrika ya Kusini (SADC) Ijumaa usiku Agosti 17, 2018


RAIS DKT. MAGUFULI AMJULIA HALI DADA YAKE ALIYELAZWA KATIKA HOSPITALI YA BUGANDO

$
0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali Dada yake Monica Joseph Magufuli ambaye amelazwa katika Chumba cha uangalizi Maalum ICU katika hospitali ya Bugando mkoani Mwanza. Picha na Ikulu

NEWZ ALERT:KOFI ANNAN AFARIKI DUNIA AKIWA NA MIAKA 80

$
0
0
Na Leandra Gabriel, blogu ya jamii

ALIYEKUWA katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Atta Annan (80) amefariki dunia leo katika hospitali ya Bern nchini Uswizi baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Kofi alikuwa  Mwafrika wa kwanza kutoka nchini Ghana kuchaguliwa kuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa na alihudumu kwa awamu mbili kuanzia Januari 1997 hadi Desemba 2016.

Baadaye alichaguliwa kuwa mmoja wa wajumbe katika kusuluhisha mzozo nchini Syria na alichangia katika kuleta suluhu.

Kofi Atta Annan alikuwa mwanzilishi na mwenyekiti wa taasisi ya Kofi Annan na mwenyekiti wa wazee katika shirika la kimataifa lililoanzishwa na aliyekuwa Rais wa Afrika ya kusini Nelson Mandela.

Kofi alizaliwa  Aprili 8, 1938 huko Kumasi nchini Ghana na alisoma taaluma mbalimbali ikiwemo Uchumi aliyosoma katika Chuo cha Macalester na Uhusiano wa Kimataifa katika chuo cha Geneva ,Alianza kuitumikia UN mwaka 1962 katika shirika la afya Duniani  (WHO.) Na ameshinda tuzo mbalimbali ikiwemo ya kulinda amani 2001.

Kofi ameacha mke (bi Nane Maria Annan) na watoto (Kojo, Ama na Nina) ambao walikuwa karibu naye  hadi umauti unamfika.
 Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Atta Annan

WAZIRI KAMWELWE AAGIZA TANROADS KUICHUNGUZA KAMPUNI YA CHICO

$
0
0
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe, ameuagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Njombe kumchunguza mkandarasi wa Kampuni ya China Henan International Cooperation (CHICO), anayejenga barabara ya Njombe-Moronga yenye urefu wa KM 53.9 kwa kiwango cha lami kama ana wataalaamu wa kutosha.

Waziri Mhandisi Kamwelwe ametoa agizo hilo katika wilaya ya Wanging’ombe mara baada ya kukagua hatua zilizofikiwa katika mradi huo na kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wake ambapo mpaka sasa umefikiwa kwa asilimia 14.Mhandisi Kamwelwe amesema hana uhakika na kampuni hiyo kama ni wenyewe CHICO waliozoeleka katika uendeshaji wa miradi mingi hapa nchini hasa ya barabara.

“Sijaridhishwa na kasi ya huu ujenzi, Meneja wa TANROADS hakikisha unafuatilia kwa makini mradi huu na kubaini sababu zilizopelekea kusuasua kwa mradi na kuondoa wataalamu ambao wataonekana wanaudhaifu na kukwamisha mradi huo”, amesisitiza Mhandisi Kamwelwe.

Amebainisha kuwa hakuna sababu ya mkandarasi huyo kuchelewesha mradi huo kwani vifaa na mitambo yote ipo katika eneo la kazi na tayari Serikali imeshamlipa fedha alizozidai kwa asilimia 95.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, (wa pili kushoto) akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Wanging’ombe, Gerson Lwenge (wa pili kulia), Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole-Sendeka (kushoto) wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Njombe-Moronga yenye urefu wa KM 53.9, mkoani humo. Kulia ni Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Njombe Mhandisi Yusuph Mazana.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole-Sendeka akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya Njombe-Moronga yenye urefu wa KM 53.9, mkoani humo.
Mhandisi kutoka kampuni ya Smec International Pty, Adarsh Nayyari, akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (katikati), ukubwa wa kazi unaoendelea wa kupasua mlima unaofanywa katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Moronga-Makete KM 53.5 kwa kiwango cha lami, mkoani Njombe.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akitoka kukagua moja ya kalvati katika mto wa Lyamadovela lililopo katika barabara ya Moronga-Makete yenye urefu wa KM 53.5 inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Njombe.


RC PWANI APIGA MARUFUKU UINGIZWAJI WA MIFUGO ENEO LA UWEKEZAJI KIWANDA CHA SUKARI CHA BAKHRESA

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,BAGAMOYO

MKUU wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo amepiga marufuku uingizwaji wa mifugo katika eneo la kampuni ya Said Salim Bakhresa Group Ltd,ambalo amekusudia kuanza ujenzi wa kiwanda cha sukari Juni 2019 na uzalishaji ifikapo septemba 2020-2021. 

Aidha amewasihi wafugaji kuheshimu maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji na kilimo . Ndikilo aliyasema hayo ,wakati kamati ya siasa ya mkoani humo , ilipotembelea shamba hilo kujionea utekelezaji wa agizo la Rais alilolitoa kipindi cha nyuma baada ya kufungua kiwanda cha vinywaji baridi cha kampuni hiyo kilichopo Mkuranga.

Alisema agizo la Rais lilikusudia kuondoa pengo la uzalishaji wa sukari kwa matumizi ya kawaida nchini . Ndikilo, alisema mradi huo ni mkubwa na ni hazina kwa mkoa na kujivunia kupiga hatua ya kiuchumi na ujenzi wa viwanda.

Mkuu huyo wa mkoa alishauri sehemu ya mradi kuwe na wakulima wa nje ili kuwaondolea umasikini. Kuhusu fidia walioguswa na mradi huo alisema fidia inalipwa kwa awamu na taratibu za kuwafanyia tathmini hivyo ambao bado wavute subira lakini hawatolipwa wavamizi. Nae msimamizi wa mradi huo, Muharami Mkenge alielezea, kampuni ya Said Salim Bakhresa (SSB) Group LTD imekusudia kuanza ujenzi wa kiwanda Juni 2019 na uzalishaji wa sukari kiwandani ifikapo septemba 2020-2021. 
MKUU wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza mbele ya Viongozi wa Serikali na Chama cha CCM,alipokuwa akitoa tamko la kupiga  marufuku uingizwaji wa mifugo katika eneo la kampuni ya Said Salim Bakhresa Group Ltd,ambalo amekusudia kuanza ujenzi wa kiwanda cha sukari Juni 2019 na uzalishaji ifikapo septemba 2020-2021.

WAZIRI MKUU AWAONYA MADIWANI TABORA

$
0
0

NA RS TABORA.

MADIWANI wa Manispaa ya Tabora wameonywa kutojihusisha na biashara ya aina yoyote zinazotolewa na Ofisi ya Mkurugezi na wametakiwa kubaki kuwa wasimamizi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao.

Onyo hilo limetoelwa leo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipokuwa akizungumza na Madiwani,Watumishi wa Manispaa, watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora na Watendaji wa ngazi mbali mbali wa taasisi za umma zilizopo Manispaa ya Tabora ikiwa ni siku ya tatu ya ziara yake mkoani humo.

Waziri Mkuu amewataka Madiwani ambao wanajihusisha na Kampuni zinazofanya biashara na Halmashauri ya Manispaa hiyo wajiondoe ili waweze kuchukua hatua pale inapotokea tatizo au dosari yoyote.

Alitoa wa mfano wa mradi wa ununuzi wa Magari mawili na kontena za kubebea taka ambao alipewa mmoja wa madiwani wa Manispaa hiyo ambaye hakumtaja jina. Waziri Mkuu alisema kuwa kampuni hiyo ilinunua magari hayo huku moja likiwa bovu na ili kuwadanganya zaidi alilipaka rangi ili lionokane ni jipya na hadi leo halijafanya kazi na hakuna hatua zilizochukuliwa kutokana na kulindana.

Aliongeza kuwa kampuni hiyo ambayo ilipewa kazi hiyo pamoja na kupewa msamaha wa kodi lakini cha kushangaza tangu mwaka 2015/16 hadi sasa haijarejesha kwa Manispaa ya Tabora fedha ilizolipwa kama kodi.

Kwa upande Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Bosco Ndunguru alisema ni kweli kampuni hiyo ilileta gari moja likiwa ni bovu lakini malipo yake bado hawajamlipa hadi hapo atakapoleta gari jipya.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora na wa Manispaa ya Tabora na viongozi mbalimbali leo ikiwa ni siku ya mwisho ya ziara yake Mkoani humo.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora na wa Manispaa ya Tabora na viongozi mbalimbali leo ikiwa ni siku ya mwisho ya ziara yake Mkoani humo.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa maelezo mafupi leo kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu kwa ajili ya kuzungumza na watumishi na viongozi mbalimbali wa Manispaa na Ofisi yake.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa akizungumza na watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora (Kitete) leo mara baada ya kukagua majengo Chuo cha Afya. Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(wa pili kutoka kulia) , Mkuu wa Wilaya ya Tabora Erick Komanya (kulia) , Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Gunin Kamba(wa pili kutoka kushoto) na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora Hassan Wakasuvi(kushoto)

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa akikiongozana na viongozi mbalimbali leo kukagua majengo ya Chuo cha Afya cha Tabora ambacho hakijaanza kutumika. 

Rais Magufuli awahakikishia Watanzania kuwa mambo yanakwenda vizuri, atembelea Bugando na asafiri na abiria wa Dreamliner

$
0
0
 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Njia panda ya Bugando mjini Mwanza wakati akiwa njiani kuelekea Chato mkoani Geita. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Sengerema mkoani Mwanza kuelekea Chato mkoani Geita.

SPIKA AMJULIA HALI WAZIRI MALIASILI NA UTALII HOSPITALI YA TAIFA YA MUHUMBILI ALIKOLAZWA KWA AJILI YA MATIBABU

$
0
0

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akiwa ameambatana na Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai na baadhi wa Waheshimiwa Wabunge wamemtembelea Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Khamis Kigwangalla kwa lengo la kumjulia hali katika Hospitali ya Taifa ya Muhumbili alikolazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu baada ya kupata ajali ya gari. 

WAZIRI MPINA ATEMBELEA BENKI KUU YA TANZANIA (BOT), TAASISI YA SEKTA BINAFSI TANZANIA (TPSF),AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA JAPAN HAPA NCHINI

$
0
0

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina kushoto akipokea zawadi ya mtungi wa kiasili kutoka kwa Balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshida mara baada ya kufanya mazungumzo katika ofisi ndogo ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi jijini Dar es Salaam leo. Picha na Mpiga Picha Wetu.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akisisitiza jambo wakati akizungumza na watendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) kuhusu mchango wa sekta binafsi katika maendeleo ya sekta za mifugo na uvuvi alipowatembelea ofisini kwao Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa TPSF, Godfey Sembeye. Picha na Mpiga Picha Wetu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Florens Luoga (kushoto) na Naibu Gavana wa Benki Kuu anayeshughulikia Uchumi na Fedha, Dk. Yamungu Kayandabila mara baada ya kufanya mazungumzo na watendaji wakuu wa benki hiyo alipowatembelea ofisini kwao Dar es Salaam.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (kulia) akifurahia jambo na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Florens Luoga (kushoto) mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika makao makuu ya BOT Dar es Salaam .
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (kulia) akiagana na Balozi waJapan nchini, Masaharu Yoshida mara baada ya kufanya mazungumzo katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dar es Salaam

RAIS SHEIN AZINDUA KONGAMANO LA TIBIRINZI PEMBA

$
0
0

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Viongozi mbali mbali na wanadiaspora katika Kongamano la Tano la Diaspora Tanzania lililofanyika leo katika ukuimbi wa Uwanja wa Tibirinzi Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba,[Picha na Ikulu.] 18 Aug 2018.
Baadhi ya Wanadiaspora wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa akizungumzanao pamoja na Viongozi mbali mbali katika Kongamano la Tano la Diaspora Tanzania lililofanyika leo katika ukuimbi wa Uwanja wa Tibirinzi Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba,[Picha na Ikulu.] 18 Aug 2018.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na Viongozi wengine wakipiga makofi baada ya wimbo wa Taifa wa Zanzibar,Tanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki ulioimbwa katika Kongamano la Tano la Diaspora Tanzania lililofanyika leo katika ukuimbi wa Uwanja wa Tibirinzi Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba

Baadhi ya Wanadiaspora wakisimama wakati Wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,Wimbo wa Taifa wa Zanzibar na Tanzania wakati wa Uzinduzi wa   Kongamano la la Tano la Diaspora Tanzania lililofanyika leo katika ukuimbi wa Uwanja wa Tibirinzi Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Issa Haji Ussi (Gavu) alipowasili katika uzinduzi wa Kongamano la tano la Diaspora Tanzania lililofanyika leo katika ukumbi katika kiwanja cha Tibirinzi Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba,[Picha na Ikulu.] 18 Aug 2018.

SAUTI YA SHANGAZI YABAMBA KWA MABINTI MASHULENI...

$
0
0
Wanafunzi wa shule ya sekondari Lyoto wanufaika na Sauti ya Shangazi mara baada ya kuwatembelea Shuleni hapo, Shangazi Mary Steward Mwenisongole ni Mwanamke alie jitoa kuwasaidia mabinti wa mashuleni kupunguza na kuondoa mazingira hatarishi katika ukuaji wao pindi wakiwa masomoni na wakiwa majumbani kuepuka vishawishi mbalimbali vinavyowapelekea kujiingiza katika njia zisizo sahihi zinazo pelekea kupata magonjwa ya zinaa, mimba na athali mbalimbali katika ukuaji wa Mwanafunzi.
Shangazi Mary Steward Mwenisongole akizungumza na wanafunzi wakike wa shule ya sekondari lyoto iliyopo eneo la Ilemi jijini Mbeya juu ya Sauti ya Shangazi inavyo jenga kujiamini na kujikubali kwa mabinti waliopo mashuleni.
Moja kati ya mwanafunzi wa kike wa shule ya Sekondari Lyoto akichangia jambo juu ya namna ambavyo mwanamke anatakiwa kujiamini na kujikubali pindi awapo shuleni na nyumbani kwa kupitia muongozo mzuri wa Sauti ya Shangazi. PICHA NA MR.PENGO MBEYA 

MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA NYUZI , HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA TABORA

$
0
0


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama nyuzi za pamba wakati alipotembelea kiwanda cha nyuzi cha Tabora kiichopo kwenye Manispaa hiyo, Agosti 18, 2018. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, Urvesh Rajani. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama nyuzi za pamba wakati alipotembelea kiwanda cha nyuzi cha Tabora kiichopo kwenye Manispaa hiyo, Agosti 18, 2018. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha nyuzi cha Tabora, Urvesh Rajani (kulia) kuhusu pamba chafu wakati alipotembelea kiwanda hicho katika Manispaa ya Tabora, Agosti 18, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia akinamama waliojifungua katika wodi ya wazazi kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora ya Kitete Agosti 18, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua chumba cha upasuaji kilichojengwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora ya Kitete wakati alipotembela hospitali hiyo katika Manispaa ya Tabora, Agosti 18, 2018. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TANZIA

MRADI WA UJENZI NYUMBA ZA KISASA NYAMANZI VISIWANI ZANZIBAR WAZINDULIWA

$
0
0


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akikata Utepe kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Nyumba za kisasa wa “Fumba Town Development” huko Nyamanzi wilaya ya Magharibi “B”leo,[Picha na Ikulu]. 18Aug 2018.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Maopinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimkabidhi hati ta Nyumba kwa Bibi Yasmin Din na Mumewem Khalil Din wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa Nyumba za kisasa wa “Fumba Town Development” huko Nyamanzi wilaya ya Magharibi “B”leo,[Picha na Ikulu]. 18Aug 2018. 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipotembelea Nyumba ya Bw.Khalil Din ikiwa ni miongoni mwa Nyumba Sitini zilizokabidhiwa wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa Nyumba za kisasa wa “Fumba Town Development” huko Nyamanzi wilaya ya Magharibi “B”leo,[Picha na Ikulu]. 18Aug 2018. 

Miongoni mwa Nyumba za Kisasa “Fumba Town Development” huko Nyamanzi wilaya ya Magharibi “B” ambazo leo jumla ya Nyumba 60 zimekabidhiwa katika sherehe za uzinduzi rasmi uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(hayupo pichani) [Picha na Ikulu]. 18Aug 2018.
Wananchi waliohudhuria katika sherehe za uzinduzi wa Mradi wa Nyumba za kisasa wa “Fumba Town Development” huko Nyamanzi wilaya ya Magharibi “B”leo wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa akitoa hutuba yake,[Picha na Ikulu].18/08/2018.

DK.BASHIRU ATOA ONYO KALI KWA BALOZI ZINAZOINGILIA SIASA ZA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

$
0
0

NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Dk.Bashiru Ally amezitadharisha baadhi ya nchi za kigeni kuacha tabia ya kuingilia siasa za ndani ya nchi.

Amesema lazima nchi hizo hasa zenye balozi Tanzania ziheshimu Katiba na miongozo ya kisheria ya nchi, vinginevyo Tanzania itashindwa kuvumilia uchochezi unaofanywa na baadhi ya balozi nazowakilisha nchi hizo Tanzania.

Hayo ameyasema leo wakati akizungumza na wananchi na wanachama wa CCM katika viwanja vya Afisi kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar makuu, Dk. Bashiru amesisitiza kuwa Tanzania ni taifa huru linalojitawala lenyewe na hakuna nchi yoyote itakayoweza kuyumbisha demokrasia ya nchi hiyo.

Amesema kumejitokeza baadhi ya mataifa yanayojifanya viranja wa demokrasia ambayo yamekuwa na tabia ya kutoa matamko ya kuhusu ushindi wa CCM wakati haijasajiliwa kufanya kazi za kisiasa. Katibu Mkuu huyo ameeleza kuwa katika siku za hivi karibuni kumetokea taifa moja la kibeberu linatuma matamko kwenye mitandao ya kubeza ushindi wa CCM hivyo wanatakiwa waheshimu utawala na demokrasia ilioko nchini.

Dk.Bashiru amefafanua kuwa hakuna taifa lenye haki ya kubeza ushindi wa CCM inaoupata katika chaguzi ndogo zinazofanyika nchni, kwani kufanya hivyo ni kuingilia siasa za ndani za taifa hili. Katika maelezo yake amebainisha kwamba kinachotakiwa kitambulike ni kuwa CCM haitishwi na matamko ya aina hiyo ya kuibeza na kwamba hawache kuidharau.


Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Dk.Bashiru Ally akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi Taifa Ndugu Abdallah Haji Haidar ambaye ni mmoja kati ya viongozi mbali mbali walioshiriki katika mapokezi hayo.


KATIBU Mkuu wa CCM Tanzania Dk.Bashiru Ally, akiwa na viongozi mbali mbali wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali wakipokea maandamano ya vijana na Wana-CCM walioshiriki katika mapokezi hayo. 


SADC YAMTEUA RAIS DKT. MAGUFULI KUWA MAKAMU MWENTEKITI WA SADC

$
0
0
Mkutano wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), unaofanyika mjini Windhoek, Namibia, kuanzia tarehe 17 hadi 18 Agosti 2018, umemteua Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Makamu Mwenyekiti wa SADC kwa kipindi cha Agosti 2018 mpaka Agosti 2019. 

Kufuatia uteuzi huo, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atapewa rasmi jukumu la Uenyekiti wa SADC katika Mkutano mkuu ujao wa 39 utakaofanyika Tanzania mwezi Agosti 2019. 
Makamu wa wa Rais Mhe .Samia Suluhu Hasan akitoa hutuba ya kushukuru mara baaada ya Tanzania kukabidhiwa Umakamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika - SADC katika ukumbi wa Mikutano katika hoteli ya SAFARI COURT ,Windhoek Namibia,leo Jumamosi tarehe 18 Agosti 2018.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini moja kati ya nyaraka nne za kisheria ambazo ni Tamko la Kutokomeza Malaria katika ukanda wa SADC, Itifaki ya Kulinda Hakimiliki ya Wagunduzi wa aina mpya za Mbegu za mimea katika Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, itifaki ya ajira na kazi pamoja na Maboresho ya Katiba inayosimamia masuala ya kamati Ndogo ya Wakuu wa Polisi katika Organ.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (wa pili kulia) akiwa kwenye siku ya mwisho ya mkutano wa 38 wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliomalizika leo mjini Windhoek Namibia ambapo Tanzania imechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa kipindi cha Agosti 2018 hadi Agosti 2019. 
Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini na Mwenyekiti wa SADC aliyemaliza muda, Mhe. Cyril Ramaphosa akikabidhi nafasi ya Uenyekiti kwa mwenyekiti mpya na Rais wa Jamhuri ya Namibia, Mhe. Hage Geingob. 
Mwenyekiti wa SADC na Rais wa Namibia, Mhe. Hage Geingob akihutubia mara baada ya kukabidhiwa nafasi ya uenyekiti wa SADC mjini Windhoek, Namibia ambapo aliishukuru Serikali ya Afrika kusini kwa uongozi mahiri kwa kipindi chote cha uongozi wake na aliahidi kushirikiana na wanachama wote katika kuiletea kanda maendeleo na kupunguza umasikini.

Bonanza la mpira wa miguu kwa timu za wasichana shule za sekondari na msingi manispaa ya Kigoma ujiji lafana sana

$
0
0

Bonanza mpira wa miguu kwa timu za wasichana kwa shule za sekondari na msingi limefanyika jana katika manispaa ya Kigoma ujiji, Mkoani Kigoma. Jumla ya timu nane zilichuana vikali ambapo timu ya Shule ya msingi Klasta ya Kigoma Kaskazini iliibuka mshindi kwenye mashindano hayo.
Lengo la bonanza hilo ilikuwa ni kuwezesha watoto wakike katika kukuza vipaji na kugundua vipaji vipya  vya watoto wa kike, lililoratibiwa na Muwakilishi UWT Mkoa wa Kigoma, Miriam Ntakisivya (kushoto pichani) ambalo litakua ni muendelezo kila baada ya miezi kadhaa, bonanza hili limedhaminiwa na radio Joy 90.5 Kigoma, Riam Bookstore pamoja na Tanganyika Water. anayeonekana kushika kipaza sauti ni Mkurugenzi wa radio Joy 90.5 Kigoma, Mwenge Muyombi alipikuwa akizungumza na wanafunzi hao katika ufunguzi wa Bonanza hilo.
Sehemu ya wageni waliofika kwenye Bonanza hilo wakifatilia michezo hiyo.
Picha ya pamoja.

MAELFU WAFURIKA KATIKA TAMASHA LA KOMAA CONCERT NA EFM JIJINI DAR

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na Wakazi wa Dar es Salaam juu ya umuhimu wa kutunza amani tuliyonayo na umoja wetu kama watanzania wakati wa Tamasha kubwa la Komaa Concert lililoandaliwa na kituo cha Radio cha EFM  katika Viwanja vya Tanganyika Parkers, Kawe

Msanii wa Muziki wa Hip Pop Nchini Roma Mkatoliki akiimba na kundi kubwa la Mashabiki wake waliofika katika Tamasha la Komaa Concert kwenye Viwanja vaya Tanganyika Parkers Dar es Salaam

Msanii wa Bongo Fleva Mr Blue akiimba kwa hisa mbele ya Mashabiki wake waliofika katika tamasha la Komaa Concert katika Viwanja vya Tanganyika Parkers Dar es Salaam
 Msanii wa Hip Pop Nchini Yound D akiimba katika jukwa ala Komaa Concert Lililofanyika katika Viwanja vya Tanganyika Parkers Kawe Jijini Dar es Salaam.

BREAKING NYUZZZ....: MAGARI KADHAA YADAIWA KUSHIKA MOTO KATIKA KITUO CHA FORODHA CHA RUSUMO, NGARA

$
0
0
Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii hivi punde, inaeleza kuwa Magari kadhaa yakiwemo malori ya kubeba mafuta, yanateketea kwa moto muda huu katika kituo cha Forodha cha Rusumo wilayani Ngara, mpakani kwa Tanzania na Rwanda. Taarifa za awali zinaeleza kuwa moto huo umeibuka kutokana na ajali ya moja ya magari hayo kugonga magari mengine, jirani na Ofisi ya Idara ya Uhamiaji. Aidha Ofisi kadhaa katika mpaka huo zinadaiwa kushika moto. taarifa zaidi itawafikia baadae.

Jundokan Austria watoa mwaliko katika chama cha Jundokan Tanzania semina 2019, Vienna

$
0
0
Mkuu wa maandalizi ya kongamano la kimataifa la Karate chama cha Jundokan, mtindo wa Okinawa Goju Ryu Sensei Dr. Friedrich Gsodam mwenye 9 Dan toka mji wa Vienna, Austria ametuma barua ya kuialika Jundokan tawi la Tanzania.

Uthibitisho wa mwaliko huo ulipokelewa kupitia mkuu wa chama hicho tawi la Tanzania, sensei Fundi Rumadha mwenye Dan 4, na mum wenye kutambuliwa na chama hicho huko Okinawa, Japan.
Sensei Dr.Friedrich Gsodam dan 9 kushoto na sensei Gabriella wa Austria kulia, na sensei Fundi kati.

 " European Jundokan Gasshuku", linategemewa kufanyika mwezi Julai 19 hadi 21 litawakusanya walimu wote wa chama cha Jundokan toka Okinawa, Japan na nchi za ulaya zote.

Pia, mwenyekiti wa chama hicho Sensei Kancho Miyazato na walimu wakuu walio kuwa naidhini ya ufundishaji wa semina toka chama kijulikanacho kama "Okinawan Budokan", ni sensei Tsuneo Kinjo dan 9, Tetsu Gima, dan 9 nk.

Tanzania ni nchi pekee katika Afrika mashariki kuwa chini ya Jundokan. Pia vilevile, ikiwa imesalia miezi miwili na nusu kwa maadhimisho ya kusheherekea miaka 65 tangu chama hicho kimeanzishea ambayo itafanikiwa huko kisiwa cha Okinawa.
Masensei wa Jundokan Austria chini ya mkuu wake Sensei Dr. Friedrich Gsodam, kulia.
Sensei Dr. Friedrich Gsodam dan 9 mkuu wa Jundokan Austria kushoto na mwnyekiti wa Jundokan duniani sensei Kancho Miyazato kulia.
Viewing all 110114 articles
Browse latest View live




Latest Images