Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

FAINALI YA BBALL KINGS KUANZA WIKIENDI HII

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
MICHUANO ya Sprite Bball Kings 2018 imefikia hatua ya fainali baada ya timu za Flying Dribblers na Mchenga Bball Stars kushinda mechi zao za nusu fainali.

Msimu wa pili wa mashindano ya Sprite Bball Kings 2018 ulizinduliwa Juni 11 mwaka huu katika Viwanja vya Mlimani City Mall na jumla ya timu 51 na zikiwa na jumla ya washiriki zaidi ya 510 kutoka pande mbalimbali Tanzania walijisajili na kushiriki michuano hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Vipindi wa EA Radio, Nasa Kingu amesema kuwa michuano hiyo ilianza rasmi Juni 30 kwa timu 51 kucheza hatua ya mtoano na kupatiakana kwa timu 16 zilizoingia hatua iliyofuata.

Kingu amesema kwa sasa mashindano ya Sprite Bball Kings 2018 yamefikia hatua ya fainali na timu ya Flying Dribblers pamoja na timu ya Mchenga Bball stars zitachuana vikali kuwania ubingwa mechi hizo zikiwa katika Game 5.

Ameeleza kuwa, timu ya Mchenga Bball stars ndiye bingwa mtetezi akiwa na kumbukumbu ya kumtoa mpinzani wake Flying Dribblers hatua ya nusu fainali msimu uliopita na sasa hivi wanakutana katika hatua ya fainali.

Fainali za mashindano ya Sprite Bball Kings 2018 yanatarajiwa kuanza rasmi  Jumamosi Agosti 18 - Game 1 utakaochezwa katika Uwanja wa ndani wa Taifa , jumatano Agost 22 - Game 2 katika Viwanja vya Don Bosco, Jumamosi Agost 25- Game 3 Uwanja wa Ndani wa Taifa na kama italazimika kuendelea na game 4 na 5, mechi hizo zitachezwa Jumamosi  Agosti 29 Game 4 na Jumatano Septemba  01- Game 5 na mechi hizo zitachezwa katika Viwanja vya  Don Bosco Oysterbay.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Ufundi na Mashindano wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Nchini (TBF) Manase Zablon amesema kuwa michuano hii imeweza kuonyesha njia kwa wachezaji ambapo katika msimi uliopita wapo wachezaji waliofanikiwa kupata timu na wengine wakipata nafasi za kusoma kupitia mchezo huo.

Kwa mara ya kwanza mashindano ya Sprite Bball Kings yalifanyika 2017 na timu ya Mchenga Bball Stars iliweza kuwa bingwa na kufanikiwa kupata fedha taslimu shilingi million 10 pamoja na Kikombe, Mshindi wa pili wa mashindano alipata shilingi milioni 3 na Mchezaji bora (MVP) Rwehabura Munyangi aka Barongo ambaye alipata kikombe na fedha taslimu shilingi milioni 2.
Mkuu wa Vipindi wa EA Redio Nasa Kingu akizungumza na wawakilishi wa timu za Flying Dribllers na Mchenga BBall Stars pamoja na waandishi wa habari kuelekea fainali ya Michuano ya Sprite BBall Kings 2018 mchezo utakaoanza kutimi vumbi Agosti 18 mwaka huu katika Viwanja vya Ndani wa Taifa. Kulia ni Mkurugenzi wa Ufundi na Mashindano wa Shirikisho la Kikapu Tanzania (TBF) Manase Zablon.

Wasanii waaswa kujua thamani yao

$
0
0
Wanatasnia wa filamu na michezo ya kuigiza nchini wameaswa kujua thamani yao na kazi zao katika kulinda maadili na utamaduni wa kitanzania ili kujijengea heshima mbele ya jamii na wapenzi wa kazi zao. Rai hiyo imetolewa leo na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Bibi. Joyce Fissoo alipokuwa akizungumza na viongozi wa Kamati ya Matukio, Maadili na Mikataba wa Chama cha Waigizaji Mkoa wa Kinondoni (Tanzania Drama Film Actors Association - Kinondoni) walipotembelea na kufanya kikao katika Ofisi za Bodi ya Filamu Mtaa wa Samora Jijini Dar es salaam.

Bibi. Fissoo alisema baadhi ya wanatasnia ya filamu wanaonyesha mwenendo unaokinzana na maisha na maadili ya kitanzania huku miongoni mwao wakifanya vitendo vinavyodhalilisha utu na heshima hivyo kuitia doa tasnia nzima ya filamu na michezo ya kuigiza.

“Nawapongeza Chama cha Waigizaji kwa kushirikiana na serikali katika kukemea wale wanachama wachache wanao chafua taswira ya tasnia. Ni muhimu kuendelea kuongeza nguvu katika nidhamu, matumizi ya lugha zenye staha, mavazi yanayoonyesha taswira chanya ya taifa letu; hivyo endeleeni kuiunga mkono Serikali katika hatua inazozichukua” alisema Fissoo.

Kwa upande wake Msemaji wa Chama hicho Bw. Masoud Kaftany alisema lengo la kukutana na Bodi ya Filamu Tanzania ni kuwatambulisha viongozi na kamati ya matukio, maadili na mikataba kutoka kwenye chama cha Waigizaji Kinondoni kwa uongozi wa Bodi ya Filamu kama njia mojawapo ya kuendeleza ushirikiano katika tasnia hiyo.

“Kamati yetu inaundwa na wawakilishi 13 wakiongozwa na Mwenyekiti bwana Ahmad Hussein, Katibu bwana Khalifan Ahmed na Msemaji bwana Masoud Kaftany na leo tumekuja Bodi ya Filamu kujitambulisha na kujifunza Sheria, Kanuni na Taratibu zinazotakiwa kufuatwa ili zitusaidie katika utendaji wa kila siku wa kazi zetu” alisema Kaftany.

Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati ya Chama hicho Bi. Vanitha Omari ameiomba Bodi ya Filamu kutochoka kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau wa sekta ya filamu ili waweze kupata uelewa stahiki katika tasnia kwa ujumla.

Chama cha waigizaji wa filamu Mkoa wa Kinondoni ni miongoni mwa vyama vinavyounda vyama vya waigizaji wa filamu taifa na ni chama ambacho kimekuwa mfano katika kutetea maslahi na haki za wanachama wake.
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo (katikati) akiongoza kikao na viongozi wa Kamati ya Matukio, Maadili na Mikataba wa Chama cha Waigizaji Mkoa wa Kinondoni (Tanzania Drama Film Actors Association-Kinondoni) walipotembelea ofisi za Bodi ya Filamu kuwatambulisha viongozi wa chama hicho kwa uongozi wa Bodi ya Filamu hivi karibuni katika Ofisi za Bodi ya Filamu Mtaa wa Samora jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wanachama na viongozi wa Kamati ya Matukio, Maadili na Mikataba wa Chama cha Waigizaji Mkoa wa Kinondoni (Tanzania Drama Film Actors Association-Kinondoni) wakifuatilia taarifa iliyokua ikitolewa wakati wa kikao na Bodi ya Filamu kuwatambulisha viongozi hao hivi karibuni katika Ofisi za Bodi ya Filamu Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo (wanne kulia) katika picha ya pamoja na Wanachama na Wajumbe wa Kamati ya Matukio, Maadili na Mikataba wa Chama cha Waigizaji Mkoa wa Kinondoni (Tanzania Drama Film Actors Association-Kinondoni) baada ya kikao na wajumbe hao walitembelea ofisi za Bodi ya Filamu kuwatambulisha viongozi wa chama hicho kwa uongozi wa Bodi ya Filamu hivi karibuni katika Ofisi za Bodi ya Filamu Jijini Dar es salaam.

Dk.Shein akutana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akiwa na ujumbe wake.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai (wa pili kulia) wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akiwa na ujumbe wake.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa zungumza na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaoongozwa na Spika Mhe.Job Ndugai (wa nne kulia) baada ya mazungumzo ujumbe huo ulipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo. Picha na Ikulu, Zanzibar.

MKUTANO WA WAGANGA WAKUU WA MIKOA NA HALMASHAURI WAFANYIKA JIJINI DODOMA

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto ( Idara ya Afya) Dkt. Mpoki Ulisubisya akiongea na Waganga wakuu wa Mikoa na Halmashauri wakati wa kufunga mkutano wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri hawapo pichani ,kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa OR-TAMISEMI Dkt. Zainabu Chaula.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasirimali watu kutoka Wizara ya Afya Deodata Makana akiongea na Waganga wakuu wa Mikoa na Halmashauri wakati wa kufunga mkutano wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri hawapo pichani uliofanyika jijini Dodoma.
Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri wakifuatilia kwa makini maada mbalimbali zilizokuwa zinatolewa na wawasilishaji mbalimbali hawapo pichani wakati wa kufunga mkutano wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri uliofanyika jijini Dodoma.

INTRODUCING: Peter Msechu - MAGUFULI JEMBE (Official Audio)

Maugo, Misanjo, Class Mazola kuonyesha ubabe leo PTA

$
0
0
Bondia nyota nchini, Mada Maugo leo ataonyeshana kazi na Mmalawi, Charles Misanjo katika pambano la kimataifa la uzito wa Super middle kwenye ukumbi wa PTA, Sabasaba. Wakati Maugo akionyeshana ubabe na Mmalawi, bondia bingwa wa Dunia wa uzito wa Super feather, Ibrahim Class atazipiga na bondia nyota, Baina Mazola katika pambano lingine lenye ushindani mkali kwa mashabiki wa ngumi za kulipwa nchini.

Mabondia hao wanne jana walipima afya na uzito kwenye viwanja vya Las Vegas, Mabibo ambapo mabondia wote walitambiana kila mmoja atashinda. Wakati Maugo aliomba waandaaji, kampuni ya Lady In Red Promotion chini ya Mbunge, Sophia Mwakagenda, tambo zaidi zilitawala kati ya Mazola na Class ambao walizindikizwa na ‘vigoma’ ambavyo kulikuwa na akina dada wakimwaga ‘radhi’ mbele ya mashabiki na maofisa wa ngumi za kulipwa.

Mabondia hao walipima uzito na afya jana Ijumaa huku kila mmoja akitamba kumchakaza mwenzake katika pambano hilo la raundi 10 litakalopigwa kwenye ukumbi wa PTA, Sabasaba jijini Dar es Salaam.

“Nipo serious, naomba waabdaaji waje na machela ili kumbeba Misanjo, nimefanya mazoezi makali na sitaki mchezo mchezo, najua ataleta upinzani kidogo, lakini nimedhamilia kuweka historia kwa kumchapa mwanzoni tu,” alisema Maugo.

Misanjo naye alijibu mapigo kwa kusema hana sababu ya kupoteza pambano hilo na hasa ukizingatia amesafiri umbali mrefu kuja nchini kupambana.

“Namjua Maugo, hawezi kunitisha na kunishinda, nipo kwa ajili ya kumfundisha ngumi kwani nina uzoefu wa muda mrefu na nimepigana na mabondia tofauti katika mataifa mbalimbali,” alisema Misanjo.

Muuandaaji wa pambano hilo, Sophia Mwakagenda alisema maandalizi yote yamekamilika na milango ya ukumbi wa PTA itakuwa wazi kuanzia saa 8:00 Mchana ambapo msanii maarufu nchini, Juma Nature atatumbuiza kabla ya mapambano.

Mwakagenda alisema kuwa pia kutakuwa na mapambano ya utangulizi ambayo yatawahusisha mabondia wakike, Flora Machela ambaye atapambana na Sarafina Julius katika uzito wa Bantam na Asha ‘Ngedere atazichapa na Happy Daudi katika pambano la uzito wa Super-lightweight. Mapambano hayo yamepangwa kuwa ya raundi sita.
Promota wa kwanza kike wa ngumi za kulipwa nchini, Sophia Mwakagenda (Kati kati) akiwatambulisha mabondia, Mada Maugo wa Tanzania (Kulia) na Charles Misanjo wa Malawi ambao watapambana leo Jumamosi kwenye ukumbi wa PTA, Sabasaba.
Promota wa kwanza kike wa ngumi za kulipwa nchini, Sophia Mwakagenda (Kati kati) akiwatambulisha mabondia, Asha Ngedere (Kulia) na happy Daudi ambao watapambana leo Jumamosi kwenye ukumbi wa PTA, Sabasaba.
Promota wa kwanza kike wa ngumi za kulipwa nchini, Sophia Mwakagenda (Kati kati) akiwatambulisha mabondia, Baina Mazola (Kushoto) na Ibrahim Class ambao watapambana leo Jumamosi kwenye ukumbi wa PTA, Sabasaba.
Promota wa kwanza kike wa ngumi za kulipwa nchini, Sophia Mwakagenda (Kati kati) akiwatambulisha mabondia, Saraphina Julius (Kulia) na Flora Machela ambao watapambana leo Jumamosi kwenye ukumbi wa PTA, Sabasaba.

JKCI kwa kushirikiana na Kampuni ya Merck waandaa mkutano wa kwanza wa kutathimini magonjwa ya moyo nchini

$
0
0
Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Delila Kimambo akielezea jinsi mashine ya kupima moyo (Echocardiogram) inavyofanya kazi ya kutambua matatizo yaliyopo katika moyo wakati wa mkutano wa kwanza wa kitaifa wa kutathmini magonjwa ya moyo nchini uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa JKCI uliopo Jijini Dar es Salaam.

Na Salome Majaliwa - JKCI

Madaktari wa Hospitali za Rufaa nchini wameshauriwa kuwatuma mapema wagonjwa wa moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) pindi wanapowapima na kugundulika kuwa na ugonjwa huo ili waweze kupatiwa matibabu mapema.

Rai hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi ambaye pia ni Daktari bingwa wa magonjwa ya Moyo kutoka JKCI Delila Kimambo wakati wa mkutano wa kwanza wa kitaifa wa kutathmini magonjwa ya moyo nchini uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo.

Dkt. Delila alisema wagonjwa wa moyo wanaotibiwa katika Hospitali mbalimbali hapa nchini rufaa yao huwa ni Taasisi ya Moyo hivyo basi ni muhimu wagonjwa hao wakafika katika Hospitali hiyo kwa wakati.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Shirika la Madaktari Afrika la nchini Marekani Prof.Matthew Sackett akielezea jinsi mtambo wa Cathlab unavyotumika kutibu na kupima magonjwa ya moyo wakati wa mkutano wa kwanza wa kitaifa wa kutathmini magonjwa ya moyo uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) uliopo jijini Dar es Salaam.

“Wagonjwa wengi tunaowapokea mioyo yao huwa imechoka, kama wagonjwa hawa wangefika mapema kwetu wangepata matibabu madogo kuliko kupatiwa matibabu makubwa ya upasuaji wa kifua au bila kufungua kifua kwa kutumia tundu dogo”.

“Kutokana na wagonjwa wengi kuchelewa kufika hospitalini ama kutokupata matibabu ya moyo kwa wakati, tumeona tuwe na mafunzo haya hii itawasaidia madaktari wengi kupata ujuzi zaidi na kuweza kutambua wagonjwa kwa wakati”, alisema Dkt. Delila.

Akizungumzia kuhusu mkutano huo Dkt. Delila alisema lengo ni kuwapatia madaktari ujuzi hususani wa namna ya kupima moyo kwa kutumia mashine za ECHO na umeme wa moyo (Electrocardiography – ECG).

Kwa upande wake Daktari kutoka hospitali ya Amana Natalius Kapilima alisema mafunzo hayo yamewasaidia kupata ujuzi utakaowawezesha kuwatambua wagonjwa wa moyo kupitia vipimo vya ECHO na ECG.

Naye Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka hospitali ya Aga Khan Prof. Mustafa Bapuma aliishukuru Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete kwa kuona mbali na kuwezesha kufanyika kwa mafunzo hayo kwa madaktari. Kupitia mafunzo hayo wataweza kutibu wagonjwa wa moyo kwa ustadi na ufanisi zaidi kuliko hapo awali.

Mkutano huo wa siku moja umeandaliwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete kwa kushirikiana na Kampuni ya Merck ambapo jumla ya washiriki 80 kutoka Hospitali mbalimbali za mkoa wa Dar es Salaam walishiriki.
Baadhi ya Madaktari wa Magonjwa ya Moyo kutoka Hospitali mbalimbali za mkoa wa Dar es Salaam wakifuatilia mada ya jinsi ya kumtambua mgonjwa mwenye matatizo ya moyo kwa kupitia kipimo cha ECHO wakati wa Mkutano wa kwanza wa kitaifa wa kutathmini magonjwa ya moyo nchini uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) uliopo jijini Dar es Salaam. Picha na Genofeva Matemu - JKCI

LUGOLA AWAPA WIKI MOJA POLISI KUWAKAMATA WANAFUNZI WATORO, WANAOWARUBUNI WATOTO WA KIKE

$
0
0
Na Felix Mwagara, MOHA

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewapa wiki moja Jeshi la Polisi Wilaya Bunda, kuwakamata wanafunzi watoro, wazazi wa wanafunzi watoro pamoja na watu waliowarubuni wanafunzi wa kike ambao wameacha shule wilayani humo.

Lugola ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, wilayani Bunda, Mkoa wa Mara, alisema inamsikitisha sana idadi kubwa ya wanafunzi wilayani humo wameacha masomo yao na kurubuniwa wanaume ili waweze kuolewa huku Serikali ikitangaza elimu bure kuanzia shule za msingi mpaka kidato cha nne.

Akizungumza na mamia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa mpira wa miguu wa Busambara, Kijiji cha Busambara, Kata ya Kitengule, wilayani humo, Lugola alisema kiwango cha wanafunzi kuacha masomo inatisha, hivyo serikali haiwezi kukaa kimya, lazima kuhakikisha wanafunzi hao wanasoma ili waje kuwa viongozi wa nchi.

“Mkuu wa Polisi wa hapa Bunda, nawapa wiki moja, mtumie elimu zenu za upelelezi mliofundishwa, wakamateni, wachunguzeni, wahojini ndugu, jamaa, majirani mtawawapata wote wanaowarubuni watoto hawa, halafu mushughulike nao,” alisema Lugola.

Pia Lugola aliongeza kua, kuna sheria zinazoshughulika na wanafunzi watoro na pia zipo sheria zinazoshughulika na wazazi wa wanafunzi watoro, pia zipo sheria zinazowashughulikia wanaume wanaowarubuni wanafunzi, hivyo haiwezekani wanafunzi wa kidato cha tano wakatae masomo, na wengi wao wanaokataa masomo ni wasichana.

Aidha, Lugola alisema ujenzi wa sekondari mbili za kidato cha tano na sita unaendelea ambapo katika kata za Nansimo na Muramba katika Jimbo lake la Mwibara zitanaanza kuchukua wanafunzi mwaka ujao watakao fanya mtihani wa kidato cha nne mwaka huu. “Tunaendelea kuweka miundombinu katika shule hizo ili ziweze kuchukua wanafunzi wa kidato cha tano katika maeneo haya na hatutarajii wanafunzi kukosa shule wamalizapo kidato cha nne,” alisema Lugola.

Hata hivyo, Lugola pia aliwataka polisi nchini kuwakamata waendesha magari na bodaboda ambao hawafuati sheria za barabarani ikiwemo baadhi ya bodaboda uvunja sheria kwa makusudi kwa kupakia abiria wanne na kuendelea ambapo ni hatari kwa usalama wa dereva na abiria hao. “Idadi kubwa ya polisi wanafanyakazi kwa umakini na uaminifu mkubwa, ila wachache sana ndio wenye tabia hizo mbaya, nawataka askari hao wafuate sheria na pia kuendelea kuzikamata kama ni magari au bodaboda au wananchi wowote ambao wanavunja sheria za nchi,” alisema Lugola.

Waziri Lugola yupo katika ziara jimboni kwake kwa kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuwaunganisha wananchi kupitia Bonanza lake la michezo ya mpira wa miguu ambalo linashirikisha kila kata wakitoa washindi mbalimbali ambao anawapa zawadi pamoja na kuingia moja kwa moja katika mashindano ya kugombea Kombe la Kangi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Busambara, Kata ya Kitengule katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Busambara jimboni humo, Wilaha ya Bunda, mkoani Mara. Lugola aliwaagiza Polisi wilayani humo kuwakamata wanafunzi watoro pamoja na wanao warubuni watoto wa kike katika shule mbalimbali wilayani humo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kulia) akimsikiliza mwananchi wa Kijiji cha Busambara, Kata ya Kitengule, Kaitila Jumbula, alipokua anauliza swali kuhusu maendeleo ya Kata hiyo katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Busambara, jimboni humo, Wilaha ya Bunda, mkoani Mara. Lugola aliwaagiza Polisi wilyani humo kuwakamata wanafunzi watoro pamoja na wanao warubuni watoto wa kike katika shule mbalimbali wilayani humo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

KONGAMANO LA BIASHARA NA UWEKEZAJI LAFANYIKA JIJINI SEOUL, KUHAMASISHA WADAU WA MADAWA NA VIFAA TIBA KUWEKEZA NCHINI TANZANIA

$
0
0
Katika kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ubalozi wa Tanzania Seoul kwa kushirikiana na “Korea-Africa Foundation” na “Korea Chamber of Commerce and Industry” uliandaa Kongamano la Biashara na Uwekezaji kwa wadau wa sekta ya Afya lililofanyika Seoul, Jamhuri ya Korea. Kongamano hilo la aina yake, lilijumuisha Wizara na Taasisi za kuitendaji katika eneo husika ambazo ni: Wizara ya Afya; Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki; Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji; Kituo cha Uwekezaji (TIC); MSD; TFDA, na TAPI (Tanzania Association Pharmaceutical Industries).

Aidha, Kongamano hilo lililolenga kuhamasisha uanzishwaji wa viwanda vya madawa na vifaa tiba nchini Tanzania, lilihudhuriwa pia na makampuni zaidi ya 100, kutoka pande zote mbili ikijumuisha: Makampuni ya utengenezaji madawa na vifaa tiba; Vyuo Vikuu; Taasisi za utafiti; Hospitali; Vyama vya watengenezaji wa madawa na vifaa tiba; Makampuni kutoka katika sekta binafsi; na Diaspora wetu waliopo Seoul.

Katika Kongamano hilo, mada mbalimbali ziliwasilishwa zikijumuisha: Fursa zilizopo Tanzania katika sekta ya utengenezaji wa madawa na vifaa tiba, mazingira ya ufanyaji biashara na vivutio “incentives” vinavyotolewa na Serikali; Hali ya soko na uhitaji (Market Potentiality); Taratibu za kufuatwa katika uingizwaji wa bidhaa za madawa na uanzishwaji wa viwanda husika; na utayari wa sekta binafsi katika kushirikiana na wenzao wa Korea katika biashara na ubia katika viwanda vya madawa na vifaa tiba. Upande wa Korea pia ukiwakilishwa na Vyama vya watengenezaji wa madawa na vifaa tiba walitoa mada iliyokuwa na lengo la kubadilishana uzoefu na upande wa Tanzania. Kongamano lilihitimishwa kwa B2B, ambapo makampuni na Taasisi zilikutana kujadiliana zaidi fursa, maeneo ya ushirikiano, na kupata ufafanuzi wa kina katika maeneo mbalimbali; na baadaye kutembelea Makampuni ya Madawa.
Mgeni Rasmi katika Kongamano la kuhamasisha uwekezaji katika viwanda vya madawa na vifaa tiba, Bw. Geoffrey Mwambe, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) akitoa Hotuba ya Ufunguzi, kwa niaba ya Mhe. Ummy Ally Mwalimu (Mb), Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini, Mhe. Matilda Swilla Masuka akitoa neno la ukaribisho katika Kongamano hilo.
Rais wa “Korea-Africa Foundation” waandaaji wenza wa Kongamano hilo, Balozi CHOI, Yeon-ho, akitoa neno katika hafla ya ufunguzi.
Sehemu ya washiriki katika Kongamano la kuhamasisha wawekezaji wa viwanda vya Madawa na vifaa tiba Seoul, Jamhuri ya Korea, August 13, 2018.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

WAZIRI MKUU AHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA KATIKA MJI MDOGO WA NZEGA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Parking katika mji mdogo wa Nzega Agosti 17, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wakati alipowasili kwenye uwanja wa Parking katika mji mdogo wa Nzega kuhutubia mkutano wa hadhara, Agosti 17, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na  Mbunge wa Viti Maalum, Munde Tambwe wakati alipowasili kwenye uwanja wa Parking katika mji mdogo wa Nzega kuhutubia mkutano wa hadhara, Agosti 17, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

HATUTAONGEZA MUDA WA UJENZI BARABARA YA CHUNYA-MAKONGOLOSI: NAIBU WAZIRI KWANDIKWA

$
0
0
Serikali imesema haitamwongezea mkataba mkandarasi China Railway 15 Bureau Group Corporation anayejenga barabara ya Chunya –Makongolosi kwa kiwango cha lami muda wake utakapomalizika.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias John Kwandikwa amesema muda wa miezi 27 aliyopewa kujenga barabara hiyo yenye urefu wa KM 39 unatosha na hivyo ni jukumu lake kuhakikisha kuwa anakuwa na vifaa na wafanyakazi wa kutosha wakati wote.

“Mkishindwa kukamilisha barabara hii kwa wakati hamtapata tena kazi hapa nchini kwani mtakuwa mmeshindwa kazi kwa kukiuka mkataba na kuiongezea Serikali gharama”, amesema Mhe. Kwandikwa.

Naye Kaimu meneja wa wakala wa barabara (TANROADS) mkoa wa Mbeya Mhandisi Selemani Lawena amesema barabara ya Chunya –Makongolosi ni sehemu ya barabara ya Mbeya-Rungwa yenye urefu wa KM 293 ambayo inaunganisha kwa njia fupi mkoa wa Mbeya na mikoa ya Singida na Tabora.

“Barabara hii ikikamilika itafungua uchumi wa mikoa ya Mbeya na Songwe na kuhuisha shughuli za kilimo,mifugo, uchimbaji madini na ufugaji nyuki na hivyo kuongeza fursa za maendeleo kwa jamii na serikali kwa ujumla”, amesema mhandisi Lawena.

Mhandisi lawena amesema sehemu ya Mbeya- Chunya KM 72 imekamilika na ujenzi wa Chunya –Makongolosi KM 39 unatarajiwa kukamilika Januari 2020.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Kwandikwa amekagua ujenzi wa barabara ya mchepuo ya Iwambi-Mbalizi KM 6.5 jijini Mbeya ambayo itatumiwa na magari madogo ili kupunguza msongamano na ajali katika mlima Mbalizi na kusisitiza umuhimu wa wadau wote wa usafiri kushirikiana ili kupunguza ajali na hivyo kulinda maisha na mali.
Ujenzi wa daraja la Kikamba wilayani Songwe linalounganisha Mkoa wa Songwe na Katavi ukiendelea daraja hilo linatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.
Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias John Kwandikwa akisisitiza jambo kwa Mbunge wa Songwe Mhe. Philipo Mulugo alipokagua ujenzi wa daraja la Kikamba wilayani Songwe, daraja hilo linaunganisha Mkoa wa Songwe na Katavi.
Muonekano wa barabara ya Chunya –Makongolosi KM 39 ambayo ujenzi wake unaendelea, barabara hiyo ni sehemu ya barabara ya Mbeya- Rungwa yenye urefu wa KM 293 inayounganisha kwa njia fupi mkoa wa Mbeya na mikoa ya Singida na Tabora.
Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Mbeya mhandisi Selemani Lawena wa kwanza (kulia), akitoa taarifa ya ujenzi wa barabara ya Chunya –Makongolosi KM 39, kwa Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias John Kwandikwa (wa tatu kulia), alipokagua ujenzi huo, (katikati) ni Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mary-Prisca Mahundi.

GULAMALI AMUOMBA WAZIRI MKUU KUONDOA FAINI KANDAMIZI KWA WAKULIMA WA PAMBA WILAYANI IGUNGA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii.
MBUNGE wa Jimbo la Manonga Seif Khamis Gulamali amemuomba Waziri Mkuu  Mh. Kassim Majaliwa kutoa tamko juu ya faini zinazotozwa kwa wakulima wa Pamba Wilayani Igunga wakati huu wa urejeshaji wa mbegu za Pamba.

Akieleza hayo kwa Waziri Mkuu aliyeko ziarani Mkoani humo Gulamali amesema kuwa faini hizo zilikuwa zinalipishwa bila hata risiti na baada ya kumuomba Mkuu wa Mkoa alitekeleza kwa kuagiza ofisi ya Mkuu wa Wilaya (Igunga) kutotoa risiti kwa faini zozote.

Gulamali ameeleza kuwa faini hizo  zimekuwa kero kubwa kwa wakulima wa Jimbo lake la Manonga na kwa masikitiko makubwa amesema zinatekelezwa Igunga tu lakini hazipo kabisa Wilaya ya Nzega ambapo kilimo cha pamba kinafanyika pia.

Aidha Alimwomba Waziri Mkuu kutoa tamko juu ya faini hizo zinazowanyanyasa wakulima ndani ya Wilaya ya Igunga hasa katika Jimbo la Manonga. Pia Gulamali alihoji  zinapokwenda fedha hizo za faini kwani mpaka sasa haieleweki.

Akijibu kero hiyo, Waziri Mkuu ameonesha kuchukizwa na faini hizo na amemuagiza Mkuu wa Wilaya apitie upya Sheria hiyo na Madiwani kwani haimpendezi hata kidogo.

 Akihutubia mamia ya wakazi wa Jimbo la Bukene, ameeleza kuwa faini hiyo kwenye Pamba inakosa maana kwani msimu haujafika mwisho na amempongeza Mh. Gulamali kuwatetea wapiga kura wake.

 Waziri Mkuu amemtaka Mkuu wa Wilaya Kukaa na Madiwani wa Halmashauri na Wampe Taarifa Mh. Gulamali kwa kuwa wakati Mwingine vikao huitishwa na Mbunge hapewi Taarifa na Amemuomba Mh Mbunge kuendelea na ari hiyo hasa kwenye vikao vya baraza la Madiwani ambavyo yeye ni mjumbe pia.
 Mbunge wa Manonga Seif Gulamali akizungumza katika ziara iliyofanywa na  Waziri mkuu Kassimu Majaliwa Mkoani Tabora.
Wakazi wa Jimbo la  Bukene waliojitokeza kumsikiliza Waziri Mkuu katika ziara yake Mkoani Tabora.

Wananchi Simiyu Washukuru Serikali Kujenga Daraja Ikungulyabashashi, Wakiri Mawasiliano Usafirishaji Kuimarika

$
0
0
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho akifungua Daraja la Ikungulyabashashi wilayani Bariadi mkoani Simiyu, wakati Mwenge wa Uhuru ukiwa katika mbio zake wilayani humo, Agosti 17, 2018.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Daraja la Ikungulyabashashi wilayani Bariadi mkoani Simiyu, wakati Mwenge wa Uhuru ukiwa katika mbio zake wilayani humo, Agosti 17, 2018.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho akiangalia kiatu kilichotengenezwa na Kikundi cha Vijana wa Dutwa wilayani Bariadi Mkoani Simiyu, wakati Mwenge wa Uhuru ukiwa katika mbio zake wilayani humo, Agosti 17, 2018.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho akimtwisha ndoo ya maji Bi. Joyce Paulo mkazi wa Kijiji cha Kasoli wiayani Bariadi mkoani Simiyu mara baada ya kufungua mradi wa kisima kirefu cha maji Kasoli, wakati Mwenge wa Uhuru ukiwa katika mbio zake wilayani humo, Agosti 17, 2018.

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA AGOSTI 17, 2018

DC MUHEZA AWAONYA WALANGUZI WA KOROSHO

$
0
0
MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo amewaonya walanguzi wa korosho kutoka kwa wakulima wilayani humo kuacha tabia hiyo mara moja kabla hawajakumbana na mkono wa sheria.

Badala ametaka ufuatwe utaratibu ambao umewekwa wilayani humo wa korosho hiyo kukusanywa kwenye maghala na kuuzwa kwa utaratibu uliopagwa ili mkulima aweze kunufaika na kilimo chake.

Hayo yalisemwa wakati akizungumza na mtandao huu ambapo pia aliwahimiza wananchi wilayani humo kujikita kwenye kilimo cha zao la korosho ili kunufaika nacho kutokana na uwepo wa soko la uhakika.Alisema ili kuhakikisha wanafanikisha kwenye jitihada hizo tayari wamegawa miche ya mikorosho bure 62050 ambako wananchi wamehamasika kupitia hekta 152.

Alisema pia kupitia amcos zao zamani zilikuwa zimelala lakini hivi sasa zimefufuka kutokana na kuwepo uhamasishwaji huo ambao umewawezesha kutambua umuhimu wa kilimo hicho .“Ndugu zangu wananchi limeni korosho kwani ni moja kati ya zao linalopewa kipambele na serikali ya awamu ya tano na tayari soko lake ni la uhakika hivyo walitilie mkazo kwa lengo la kunufaikanalo”Alisema DC Muheza.

Aidha alisema wilaya hiyo tayari dawa zipo kwa ajili ya wakulima hivyo watumie dawa zilizosambazwa ili kuwawezesha kulima kilimo chenye tija na cha kisasa ambacho kitawainua kimaisha.Hata hivyo aliwataka maafisa ugani watoke ofisini waende kwa wakulima kuhamasisha wananchi kutumia  dawa hizo kadiri ya vipimo vinavyohitaji ili waweze kulima kilimo chenye tija na manufaa kwao ili kuwaezesha wakulima kunufaika.

“Huko kwenye mikoa ya Lindi na Mtwara kumekuwa na ulanguzi kwenye manunuzi ya korosho hizo lakini kwetu hilo halipo ila nitoe wito kwa wale ambao wanafikiria kufanya biashara hivyo kinyume na utaratibu wao kama viongozi,serikali hawatakuwa tayari yoyote ambaye atataka kununua korosho kwa wakulima kwa bei za ulanguzi hivyo tutahakikisha anachukuliwa hatua “Alisema DC Muheza.

RAIS DKT. MAGUFULI ASAFILI KWA NDEGE YA BOEING 787-8 DREAM LINER AKIELEKEA JIJINI MWANZA

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.John Pombe Magufuli akiwasalimia abiria ndani ya ndege Boeing 787-8 Dream Liner ya shirika la ndege la Tanzania (ATCL)alipokuwa akielekea Jijini Mwanza ikiwa ni mara ya kwanza kwa Rais kusafiri kwa kutumia ndege hiyo mpya akiwa na abiria wengine.Agosti 18,2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.John Pombe Magufuli akiwa amemshika mtoto Ikrama Mahadi(Miezi-3) alipokuwa akiwasalimia abiria ndani ya ndege Boeing 787-8 Dream Liner ya shirika la ndege la Tanzania (ATCL)alipokuwa akielekea Jijini Mwanza ikiwa ni mara ya kwanza kwa Rais kusafiri kwa kutumia ndege hiyo mpya akiwa na abiria wengine.Agosti 18,2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.John Pombe Magufuli akiwasalimia abiria ndani ya ndege Boeing 787-8 Dream Liner ya shirika la ndege la Tanzania (ATCL)alipokuwa akielekea Jijini Mwanza ikiwa ni mara ya kwanza kwa Rais kusafiri kwa kutumia ndege hiyo mpya akiwa na abiria wengine.Agosti 18,2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.John Pombe Magufuli akiwa ndani ya ndege Boeing 787-8 Dream Liner ya shirika la ndege la Tanzania (ATCL)alipokuwa akielekea Jijini Mwanza ikiwa ni mara ya kwanza kwa Rais kusafiri kwa kutumia ndege hiyo mpya akiwa na abiria wengine.Agosti 18,2018. PICHA NA IKULU

ASKARI WAKIFANYA UKAGUZI WA MABASI KATIKA KITUO CHA UBUNGO

$
0
0
  Mkaguzi wa Ukaguzi wa mabasi katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Ubungo, Ibrahim Samwix akitoa maelekezo kwa askari usalama barabarani katika kituo cha ukaguzi wa mabasi cha Ubungo jijini Dar es Salaam.
 Askari wa Usalama Barabarani Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo , Nuru Hussein akimpa maelekezo dereva wakati wakifanya ukaguzi mabasi kutuo hicho,  jijini Dar es Salaam.
  Askari wa Usalama Barabarani Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo , Nuru Hussein akiwa katika uvungu wa basi katika kituo cha ukaguzi wa mabasi cha Ubungo jijini Dar es Salaam.
Askari wa Usalama Barabarani Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo , Nuru Hussein akiwa katika uvungu wa basi akimpa maelekezo fundi wa basi hilo baada ya kubaini ubovu moja ya kifaa katika basi hili  katika kituo cha ukaguzi wa mabasi cha Ubungo jijini Dar es Salaam.

DIWANI KATA YA NKENDE MJINI TARIME AELEZA MAENDELEO YALIYOFANYIKA KUANZIA 2016 HADI 2018

$
0
0
Na Frankius Cleophace, Tarime

KATA ya Nkende iliyopo Halmashauri ya Mji wa Tarime mkoani Mara katika kipindi cha mwaka 2016 hadi mwaka 2018 imetumia zaidi ya Sh.milioni 458 katika utekelezaji wa miradi mbalimbaliya Maendeleo.

Baadhi ya miradi hiyo ni ya elimu, afya, maji na miundombinu ya barabara huku wananchi wakichangiazaidi ya Sh.milioni 22.Wakati Diwani wa kata hiyo Daniel Komote akichangia zaidi ya Sh.milioni 15 kwa lengo la kutekeleza miradi hiyo ikiwa ni pamoja na kuunga juhudi za Serikali.

Hayo yamebainishwa na Diwani wa kata hiyo Komote katika kusoma taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM mbele ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho kata ya Nkende Mjini Tarime.

Komote amesema kuwa amekuwa akishawishi wananchi katika kuchangia maendeleo kupitia sekta zote bila kujali itikadi za vyama ili wananchi waweze kuondokana na adha ambao wamekuwa wakipata kutokana na ukosefu wa huduma za muhimu karibu, likiwemo suala la Afya, Elimu, na Miundombinu ya Barabara na Maji.
Diwani wa kata ya Nkende Daniel Komote akifafanua mambo yaliyofanyika kipindi cha Januari mpaka Juni 2018 katika kata yake kupitia sekta ya Afya,Maji,Elimu, Miundombinu ya Barabara na Masuala ya kijamii.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Tarime Hamis Mkaruka Kura akisisitiza jambo katika kikao hicho baada ya diwani wa kata hiyo kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya chama hicho kata ya Nkende Mjini Tarime.
Wajumbe wa kamati ya Siasa kata ya Nkende wakiwa katika kikao hicho cha kuwasilisha taarifa ya ilani ya chama hicho ngazi ya kata.
Baadhi yawageni wakiwemo Madiwani kutoka kata mbalimbali wakiwa katika kikao hicho.

ALIYETAFUNA FEDHA ZA KIJIJI CHA KURUYA SASA AREJESHA MILIONI 1.7/-

$
0
0
Na Frankius Cleophace Rorya

ALIYEKUWA Mtendaji wa Kijiji cha Kuruya Kata ya Komuge wilayani Rorya mkoani Mara Mwita Mangondi amerejesha fedha kiasi cha Sh.milioni 1.7 alizokuwa akidaiwa baada ya kuzitumia kinyume cha utaratibu.

Ambapo kutokana na tuhuma hizo alisimamishwa kazi na kupewa mwezi mmoja ili kurejesha fedha hizo za Serikali ya kijiji hichop.Akisoma mrejesho wa fedha hizo Kaimu Mtendaji wa kijiji cha Kuruya Athumani Juma amesema kuwa mtendaji huyo alisimamishwa kazi na kupewa muda ili kurejesha fedha hizo.Amesema tayari amerejesha kiasi cha Sh.1,700,000 na kubakizakiasi cha Sh.298,387 ambapo jumla alikuwa anadaiwa Sh.1,998,387.

Athumani ameongeza baada ya fedha hizo kurejeshwa tayari wametenga kiasi cha Sh. 1,000,000 kwa ajili ya ukarabati wa Shule ya Msingi kuruya.Huku kiasi kingine wakilipa wananchi ambao wanadaia serikali ya kijiji hicho.Aidha wananchi wa kijiji hicho wamedai kuwa kuna haja kubwa ya kuwekeza nguvu katika shule ya msingi mbatamo ili walimu waweze kupata vyumba vya kuishi.

“Walimu zaidi ya kumi na tano wanaishi nje ya shule kwanini hizo fedha zinazodaiwa zisipelekwe kwenye ujenzi wa nyumba za walimu shule ya msingi mbatamo , wanafunzi hawana Madawati wala vyumba vya adarasa vya kutosha,” wamesema wananchi hao.


Kaimu Mtendaji wa kijiji cha Kuruya kata ya Komuge Athumani Juma akifafanua jinsi fedha hizo zilivyolipwa zaidi ya Mill1.7 kutoka kwa aliyekuwa Afiasa mtendaji wa kijiji hicho Mwita Mangondi ambaye alisimamishwa kazi baada ya upotevu wa fedha za serikali na kupewa Mwezi Mmoja aweze kulipa fedha hizo.
Wananchi wa kijiji cha Kuruya kata ya Komuge wilayani Rorya wakiwa katika mkutano wa hadhara kwa lengo la kupewa mrejesho kuhusu fedha hizo.

Mwenyekiti wa kijiji cha Kuruya Bernard Wambura akifafanua jambo katika  mkutan huo ambapo amesema mwitikio wa vikao na Mikutano ya kijiji ni kidogo hivyo kuna haja kubwa ya kuanza kutekeleza sheria ndogo ya vijiji walizojiwekea ili wananchi washiriki Mikutano hiyo.

Mwalimu Mkuu shule ya Msingi KuruyaRobert John akifafanua changamoto ya ukosefu wa Matundu ya vyoo vya walimu jambo ambalo limesababisha walimu hao kutumia baadhi ya Matundu ya vyoo vya wanafunzi na wakati mwingine kutumia vyoo vya nyumb za walimu ambao wanaishi shuleni hapo. 


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>>

MKAZI WALAYANI CHEMBA AMSHIKA KICHWA MDAU WA MAENDELEO HAMISI MKOTYA

$
0
0
*Ni ishara ya kumuombea dua kwa Mungu,pia kumshukuru kwa kusaidia kutatua kilio chao

MKAZI wa Kijiji cha Kidoka Wilaya ya Chemba, Roza Mkali ameamua kumshika  kichwa mdau wa  maendeleo wa wilaya hiyo, Khamis Mkotya, ikiwa ni ishara ya kumwombea dua.

Pia ikiwa ni  kumshukuru baada ya kufanikisha familia hiyo na nyingine zaidi ya tano kijijini hapo kulipwa fidia ya mashamba yao yaliyokuwa yamechukuliwa na mkandarasi wakati wa ujenzi wa barabara ya Dodoma - Babati.  

Imeelezwa kuwa  wananchi hao walikata tamaa mwishoni mwa mwaka juzi kutokana na kufuatilia malipo yao bila mafanikio. Hivyo Mkotya aliguswa na kero hiyo hivyo aliamua kushirikiana nao na kuwapigania hadi walipolipwa stahiki zao. 

Juzi wakati Mkotya akitoka Dodoma kwenda Kondoa aliamua kupita kijijini hapo ndipo familia hiyo ilipomkaribisha nyumbani ili aone matunda ya kazi yake ya kuwapigania.

 Familia hiyo ilimweleza Mkotya kuwa inayofuraha kubwa kwani fedha walizopata wameweza kununua mashamba mengine na kujenga nyumba bora ya bati.
 MKAZI wa Kijiji cha Kidoka Wilaya ya Chemba, Roza Mkali akiwa amemshika kichwa mdau wa  maendeleo wa wilaya hiyo, Khamis Mkotya, ikiwa ni ishara ya kumwombea dua.
 Mdau wa Maendeleo wilaya ya Chemba,Hamis Mkotya akizungumza jambo na Mkazi wa kijiji cha Kidoka Wilayani Chemba,Roza Mkali hivi karibuni mara baada ya tatizo walilokuwa nalo kutatuliwa
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images