Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

WADAU SEKTA YA GESI,MAFUTA WAKUMBUSHWA KUZINGATIA SHERIA KATIKA MATUMIZI YA KEMIKALI ILI KUEPUKA MADHARA

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WADAU wa Usimamizi wa kemikali taka kutoka sekta ya mafuta na gesi kutoka taasisi za umma na binafsi wamehimizwa kuendelea kusimamia sheria,kanuni na sera kuhakikisha hakuna madhara yatakayotokana na matumizi ya kemikali.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Magdalena Mtenga wakati akifungua warsha ya Usimamizi wa Kemikali taka katika sekta ya gesi na mafuta iliyowashirikisha wadau kutoka taasisi za umma na binafsi.

Mtenga aliyemuwakilisha Mkurugenzi Ofisi ya Makamu wa Rais(Mazingira) Ester Makwahiya ,amesema ipo haja ya kukumbusha wadau umuhimu wa kuwa na matumizi sahihi ya kemikali hasa kipindi hiki cha kuelekea uchumi wa kati unaokwenda sambamba na ujenzi wa uchumi wa viwanda.Amesema matumizi ya kemikali hayaepukiki na hasa kutokana na maendeleo ya teknolojia na kwamba kemikamil inatumika katika matumizi mbalimbali yakiwamo ya viwandani na majumbani.

Amesema hivyo ipo haja ya kuwa na matumizi sahihi ya kemikali kwani iwapo hakutakuwa na matumizi sahihi kuna hatari ya kupatikana kwa madhara kwa mtumiaji."Kuna mifano ya athari ambazo zinatokana na matumizi mabaya ya kemikali na miongoni mwa athari hizo ni kupatwa kwa ulemavu wa viungo," amesema.Amesema katika kuhakikisha wananchi wanakuwa salama Serikali imechukia hatua mbalimbali za kuhakikisha kemikali inatumika katika matumizi sahihi na salama kwa kufuata sheria,kanuni,Sera na miongozo iliyopo.


Mkurugenzi Msaidizi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Bi. Magdalena Mtenga, akifungua (kwa niaba ya Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira)) warsha ya wadau wa Usimamizi wa Kemikali na Kemikali Taka za Sekta ya Mafuta na Gesi inayofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu, Dar es Salaam .

Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kulia), akiongea na washiriki wa warsha kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi, Mkurugenzi Msaidizi wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) kwa ufunguzi 
Mtaalam wa Jiolojia kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), Bw. Simon Nkenyeli (aliyesimama) akiwasilisha mada kuhusiana na masuala ya usimamizi wa petroli kwa washiriki wa warsha ya Usimamizi na Usimamizi wa Kemikali taka za sekta ya Mafuta na Gesi inaeyoendelea jijini, Dar es Salaam.

Mwanasheria kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Risper Koyi (aliyesimama) akiwasilisha mada kwa wadau kuhusiana na Mikataba ya Kimataifa ya Usimamizi wa Kemikali.

Mgeni Rasmi, Bi. Magdalena Mtenga (aliyekaa katikati) na Mkemia Mkuu wa  Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (wa pili kushoto, waliokaa) wakiwa pamoja na wadau wa warsha ya Usimamizi wa Kemikali na Kemikali taka inayofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania, Dar es  Salaam .


KAMPUNI YA KIMATAIFA VISA ON MOBILE WASHIRIKIANA NA MAXMALIPO

$
0
0
Kampuni ya kimataifa ya teknolojia ya malipo, imetangaza rasmi ushirikiano wa kimkakati kati yao na Maxcom Afrika ambayo itawawezesha wauzaji zaidi ya 30,000 kupokea malipo ya Visa kwa kutumia simu ya mkononi pamoja na mawakala 20,000 ambao watawezeshwa kupokea amana na kutoa malipo na kuunganisha watanzania na mfumo wa kimataifa wa malipo.

Kampuni ya Visa imejitolea kuleta njia rahisi zaidi, za kuaminika na salama za kufanya malipo duniani kote. Sasa, pamoja na malipo kwa kadi za plastiki, wateja wanaweza kutumia simu zao kufanya malipo kwa Visa.

Visa kwenye simu itawezesha wateja kufanya malipo mbalimbali au kutuma pesa kwa familia na marafiki, bila kukatwa malipo.

Huduma hii ambayo inatolewa kupita akaunti ya benki huunganisha akaunti ya mteja ya benki na hudumza za benki za simu bila na kuwezesha mteja kufanya malipo ya ndani nan nje ya nchi kwa kutumia huduma ya Visa kwa simu.

Pia huduma hiyo itawezesha huduma za kuweka na kutoa pesa kwa kutoka kwa mawakala wa benki maalumu na ushirikiano huo na Maxcom Afrika utahakikisha kuwa Watanzania wanaweza kulipa kwa kutumia Visa kwenye simu zao kwa wauzaji wapya zaidi ya 30,000.

"Ushirikiano huu unasisitiza jinsi Visa wamejitolea kuhakikisha na kupanua wigo wa malipo kwa malipo ya simu duniani kote, "alisema Meneja Mkuu wa Visa wa Afrika Mashariki, Sunny Walia.

Maxcom Afrika inatoa njia rahisi, salama na ya kuaminika ya kufanya malipo kwa watu binafsi na biashara nchini Tanzania.

Maxcom Afrika inawezesha malipo kwenye mtandao na moja kwa moja kwenye simu ya mkononi.
Wamejenga vipengele vya usalama kulinda wanunuzi na wauzaji wote kwa kuhakikisha taarifa za shughuli zinafichwa kwa kutumia viwango vya benki huku wakikutuma taarifa ya malipo kwa  akaunti za benki. Maxcom Afrika inatoa malipo ya hapopapo, huduma za mtandao na huduma kwa njia ya simu iliyounganishwa na terminal ya usindikaji kadi.
Viongozi wa Maxcom Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Kampuni ya Visa baada ya kuingia makubaliano ya kimkakati kwa kupokea malipo na amana kupitia mfumo wa kimataifa wa malipo


SONGWE KAMILISHENI UJENZI KWA WAKAT-NAIBU WAZIRI KWANDIKWA

$
0
0

Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias John Kwandikwa amemtaka mkandarasi China Geo- Engineering Corporation aneayejenga barabara ya Mpemba-Isongole KM 50.3 kwa kiwango cha lami kuongeza kasi ya ujenzi ili barabara hiyo ikamilike kwa muda uliopangwa. 

Amemtaka mkandarasi huyo kuongeza vifaa, wafanyakazi ili ujenzi wake ugawanywe sehemu mbili na hivyo kuwezesha ujenzi huo kukamilika ifikapo mwezi Agosti mwakani. “Kutokana na umuhimu wa barabara hii kwa uchumi wa mkoa wa Songwe hakikisheni inakamilika ili kufungua uchumi wa Wilaya ya Ileje na mkoa wa Songwe kwa ujumla”, amesema Mhe, Kwandikwa.

Barabara hiyo ambayo inaunganisha Tanzania na Malawi kupitia mto Songwe itachochea huduma za uchukuzi na kurahisisha usafiri kwa wakazi wa wilaya ya Ileje mkoani Songwe.

Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Mkoa wa Songwe mhandisi Yohana Kasaini amesema barabara hiyo inahusisha ujenzi wa madaraja makubwa manne, ya kati 14 na madogo 172, imesanifiwa kubeba magari ya aina zote na itagharimu zaidi ya shilingi bilioni 107 itakapokamilika.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Kwandikwa amekagua ujenzi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Songwe na hospitali ya Tunduma zinazojengwa na Wakala wa Majengo Nchini (TBA),mkoani Songwe na kumtaka kaimu meneja wa TBA mkoani humo msanifu majengo Christine Shayo kuhakikisha ujenzi huo licha ya kutoa fursa za ajira kwa wakazi wa maeneo hayo pia ukamilike kwa wakati na ubora uliokusudiwa.

Zaidi ya kilomita 3,856 za barabara nchini zitasanifiwa ili kujengwa kwa lami katika mwaka wa fedha 2018/2019

IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO. 

Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias John Kwandikwa akisisitiza jambo kwa wataalam wa mkandarasi China Geo-Engineering Corporation anayejenga barabara ya Mpemba-Isongole kwa kiwango cha lami alipokagua barabara hiyo.

Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias John Kwandikwa akisisitiza jambo kwa Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo nchini TBA mkoani Songwe msanifu majengo Christine Shayo, wakati wa ukaguzi wa shughuli za TBA mkoani Songwe . 
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Songwe inayojengwa na Wakala wa Majengo Nchini TBA mkoa wa Songwe. 
Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias John Kwandikwa akisisitiza jambo kwa wataalam wa mkandarasi China Geo-Engineering Corporation anayejenga barabara ya Mpemba-Isongole kwa kiwango cha lami alipokagua barabara hiyo. 

JESHI LA POLISI MBEYA LAANZISHA MSAKO WA KUWAKAMATA WATU WANAODAIWA KUFANYA UHARIBIFU WA MIUNDOMBINU

$
0
0
Na Emanuel Madafa ,Michuzi Blog -Mbeya 

Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya limeanzisha Msako wa kuwakamata watu wanaodaiwa kufanya uharibifu wa miundombinu ya maji huko katika Kijiji cha Ngole Kata ya Ilungu Wilaya ya Mbeya, Jeshi hilo tayari limeanza kutekeleza agizo hilo

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Urlich Matei amesema zoezi hilo ni utekelezaji wa agizo la Mkuu wa Mkoa wa Mbeya .

Amesema Agost 15 mwaka huu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila akiwa katika kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, alitoa agizo kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwenda kukamata wananchi wanaodaiwa kuvamia na kuharibu mradi wa maji wa kijiji jirani.

Amesema kufuatia agizo hilo, Jeshi la Polisi limeanza msako katika cha kijiji cha Ngole kuhakikisha wale wote waliohusika na uharibifu huo wanakamatwa na kufikishwa Mahakamani kwa kosa la uhujumu uchumi.

Inadaiwa kuwa uharibifu uliofanywa na wananchi hao ni kukata mabomba yaliyokuwa yametandazwa kuanzia kwenye chanzo cha maji kwenda kwenye makazi ya Kijiji jirani wakitumia vifaa mbalimbali yakiwamo majembe na mapanga.

DK.BASHIRU KUTUA ZANZIBAR KWA MARA YA KWANZA.

$
0
0
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk.Bashiru Ally anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi ya siku nne visiwani humu Agosti 17 hadi 20 mwaka huu.

Dk.Bashiru anafanya ziara hiyo kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe kushika nafasi hiyo Mei mwaka huu baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu Abdulrahman Omar Kinana kustaafu.

Akitoa taarifa ya ziara hiyo ya Katibu Mkuu huyo, Katibu wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu Taifa(NEC),Idara ya Itikadi na Uenezi CCM, Zanzibar Catherine Peter Nao, alisema CCM Zanzibar tayari kimekamilisha maandalizi yote ya mapokezi ya kiongozi huyo.

Catherine alisema katika ziara yake hiyo pamoja na mambo mengine anatarajia kuzungumza na viongozi mbalimbali wa CCM na jumuiya zake na makundi ya kutoka taasisi za vijana visiwani humu.

Aliongeza kuwa ziara hiyo ya Dk.Bashiru itakuwa ni ya kikazi na kujitambulisha kwa wana-CCM ambapo wanatakiwa kujitokeza kwa wingi katika mapokezi ya Katibu Mkuu huyo ambapo atawahutubia wanachama pamoja na wananchi kwa ujumla katika uwanja wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui saa 9 alasiri.

“Tunawaomba wanachama wote tujitokeze kwa wingi kushiriki mapokezi hayo ya kiongozi wetu mpendwa ambaye ni mara ya kwanza kuja tukitambulisha na kuzungumzia sera na masuala mbalimbali ya kuimarisha CCM na Jumuiya zake, alisema Catherine.

Akizungumzia ratiba ya ziara hiyo Katibu huyo wa Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar,Catherine alisema siku ya siku ya kesho Agosti 17 mwaka huu katibu Mkuu huyo atakutana na kuzungumza na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein.

Katibu huyo aliongeza kuwa Dk.Bashiru anatarajia kukutana na na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd.

KUSOMA ZAIDI BOFYUA HAYA>>>>>>

MAHAKAMA KUU KANDA MBEYA YAPATA JAJI MFAWIDHI

$
0
0

Na Rajabu Singana, Mahakama Kuu Mbeya

Watumishi wa Mahakama Kanda ya Mbeya wametakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano bila kujali vyeo na kufanya kazi kama timu moja, kupendana na kufuata C tatu yaani ‘Coordination, Cooperation na Consultation’ ili kuwahudumia wananchi ipasavyo.

Hayo yalisemwa na Jaji Mfawidhi mpya wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya, Mhe. Robert Makaramba alipokuwa akiongea na Watumishi wa Kanda hiyo baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi Agosti, 15 2018, katika ofisi za Mahakama Kuu mkoani Mbeya.

Mhe. Jaji Makaramba alisisitiza viongozi wa ngazi ya juu ya Kanda hiyo yaani Jaji Mfawidhi, Naibu Msajili na Mtendaji wa Mahakama kufanya kazi kwa kufuata kile alichokiita ‘utatu mtakatifu’. 

Aidha, pamoja na mambo mengine, Mhe. Makaramba alisisitiza juu ya nidhamu na uadilifu wa watumishi wa Mahakama huku akikemea Watumishi kutojihusisha na vitendo vya rushwa ili kwa pamoja kuweza kufikia malengo ya Mpango Mkakati wa miaka mitano (2015-2020) wa Mahakama. 

“Mtumishi akikamatwa kwa tuhuma za rushwa nitamsindikiza mwenyewe hadi TAKUKURU nikifika nawakabidhi wamalizane naye wenyewe” alisema Jaji Mfawidhi huyo.
Mhe Jaji Makaramba akisaini kitabu cha wageni.
Mhe. Dkt. Levira akisoma taarifa ya makabidhiano ya ofisi.
 
Watumishi wakimsikiliza Mhe. Makaramba (hayupo pichani)
Jaji Mfawidhi-Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya, Mhe. Robert Makaramba (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na baadhi ya Watumishi wa Mahakama Kanda ya Mbeya, (wa tatu kushoto) ni Mhe. Jaji Paul Joel Ngwembe, (wa pili kulia) ni Mhe. Dkt. Mary Caroline Levira, wa kwanza kulia ni Naibu Msajili-Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya, Mhe. George Herbert, wa pili kushoto ni Naibu Msajili, Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya, Mhe. William Mutaki na wa kwanza kushoto ni Mtendaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya, Bw. Moses Mwidete.

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA (TFDA) YAKUTANA NA WADAU KUJADILI UDHIBITI WA GESI TIBA NCHINI

$
0
0
Picha ya pamoja baina ya viongozi wa TFDA na wadau wa gesi tiba kutoka Serikalini na sekta binafsi nchini. waliokaa kutoka kulia ni Meneja Majaribio na Usalama wa Dawa wa TFDA, Bi Kissa Mwamwitwa aliyemwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA (wa pili), Meneja wa Vifaa Tiba, Vitendanishi na Vipodozi wa TFDA, Bi Grace Shimwela (wa tatu), Mwenyekiti mteule wa kikao hicho, Eng. Daudi Mlwale (wa kwanza) na Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto. 2. Msajili wa Dawa Mkuu wa TFDA, Bi. Rose Aaron akisisitiza jambo katika mada aliyowasilisha 3. Eng. Samwel Hayuma wa TFDA akiwasilisha mojawapo ya mada 4. Meneja Majaribio na Usalama wa Dawa wa TFDA, Bi Kissa Mwamwitwa aliyemwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA akitoa hotuba ya ufunguzi.


Msajili wa Dawa Mkuu wa TFDA, Bi. Rose Aaron akisisitiza jambo katika mada aliyowasilisha.

Eng. Samwel Hayuma wa TFDA akiwasilisha mojawapo ya mada
Meneja Majaribio na Usalama wa Dawa wa TFDA, Bi Kissa Mwamwitwa aliyemwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA akitoa hotuba ya ufunguzi

Na: James Ndege – Dar es Salaam
Mamlaka ya Chakula na Dawa imekutana na wadau wapatao 50 kujadili udhibiti wa gesi tiba (medical gases) katika ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya TFDA tarehe 16 Agosti, 2018 kwa lengo la 
kulinda afya ya jamii.

Mkutano huo umehusisha wadau bidhaa hiyo wakiwemo wazalishaji, waingizaji, wasambazaji, hospitali,
Wizara na taasisi za udhibiti za Serikali kutoka mikoa mbalimbali nchini. Katika mkutano huo, wadau 
walijadili na kuelezwa matakwa ya kisheria ya udhibiti wa bidhaa hiyo nyeti kwa afya ya binadamu.

Mamlaka imeanza udhibiti wa bidhaa hiyo ambayo ipo katika kundi la bidhaa za Vifaa Tiba kuanzia 
mwezi Aprili 2018 ambapo katika kipindi cha mpito cha mwaka mmoja, wadau wametakiwa kuwasilisha 
TFDA orodha na taarifa ya bidhaa walizo nazo kwa utambuzi (notification) na kwamba waanze utaratibu 
wa usajili kwa kuwa kipindi cha utambuzi kitamalizika mwezi Aprili 2019 na baada ya hapo bidhaa 
ambazo hazijasajiliwa na TFDA hazitaruhusiwa kuingi katika soko.

“TFDA inatarajia wadau wote kukidhi kwa hiyari matakwa ya kisheria ya udhibiti wa gesi tiba kwa muda 
uliopangwa ili kuepusha usumbufu usiokuwa wa lazima kwa wale wataokiuka maalekezo haya”, alisema
Meneja wa Majaribio na Usalama wa Dawa, Bi. Kissa Mwamwitwa, aliyemwakilisha Kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa TFDA katika hotuba yake ya ufunguzi.
Wadau hao pamoja na TFDA walikubaliana na kuweka maazimio kadhaa kwa lengo la kuwezesha zoezi
husika kufanyika kwa ufanisi, miongoni mwa maazimio hayo ni kuanzisha chama cha wadau wa gesi
tiba, kuboresha Mwongozo uliopo wa udhibiti wa gesi husika na watengenezaji wa bidhaa hiyo kuzalisha
kwa kuzingatia viwango vinavyokubalika ikiwa ni pamoja na kuweka maelezo ya kiusalama katika
bidhaa zao kwa nia ya kulinda afya ya jamii.


Kamati ya kudumu ya Bunge Viwanda, Biashara na Mazingira yaendelea na Ziara yake ya kutembelea Viwanda katika Mkoa wa Pwani

$
0
0
 Kamati ya kudumu ya Bunge Viwanda, Biashara na Mazingira yaendelea na Ziara yake ya kutembelea Viwanda katika Mkoa wa Pwani ili kusikiliza changamoto mbalimbali za Viwanda, Kamati leo tarehe 16 Ogasti, 2018 imetembelea kiwanda cha Bakhresa Food Products Ltd (BFPL) kiwanda kinachosindika matunda na vinywaji baridi, maji ya kunywa na juisi inayotokana na matunda yanayozalishwa nchini.

Kiwanda kina uwezo wa kusindika matunda tani 330 kwa siku kwa matunda yanayotoka katika mikoa ya Pwani, Lindi, Mtwara, Tanga, Iringa, Shinyanga na Tabora.

Katika Ziara hiyo kamati ya Bunge imejionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kiwanda hicho na kupongeza uongozi wa kiwanda kwa uwekezaji mkubwa uliofanyika ambao umesaidia nchi kupata kodi pia ajira kwa watanzania.

Aidha uongozi wa Kiwanda umeeleza changamoto mbalimbali wanazokutana nazo zikiwemo wingi wa taasisi za udhibiti ubora, kodi kubwa inayotozwa wakati wa uingizaji wa makasha maalumu ya kuhifandhia matunda, Stika za kodi za kieletronic (ETS), na Vikwazo visivyokuwa vya kikodi kwa bidhaa za Azam Mango na Azam energy kuuzwa kwa wateja nchini Kenya.

Kamati imehitimisha Ziara yake kwa kutembelea kiwanda cha Lodhia kilichopo Mkuranga kinachotengeza nondo, mabomba na matenki ya kuhifadhia maji.


Naibu Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stella Manyanya akiwa na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya biashara katika kiwanda cha bakhressa. 
  
 Picha ya Pamoja.
Wabunge wakitembele kiwanda cha cocakola.

MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI MKUTANO WA SIASA, ULINZI NA AMANI WA SADC NCHINI NAMIBIA

$
0
0
Pichani kulia Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali wakishirikiMkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC (SADC Organ on Politics, Defence and Security) katika ukumbi wa Mikutano wa hoteli ya Safari Court Mjini Windhoek, Namibia, usiku wa Alhamisi Agosti 16, 2018.Makamu wa Rais anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika mkutano huo.
Sehemu ya Meza kuu wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC (SADC Organ on Politics, Defence and Security) katika ukumbi wa Mikutano wa hoteli ya Safari Court Mjini Windhoek, Namibia, usiku wa Alhamisi Agosti 16, 2018.
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Demokrasia ya Watu wa Congo (DRC) Mhe. Joseph Kabila kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC (SADC Organ on Politics, Defence and Security) katika ukumbi wa Mikutano wa hoteli ya Safari Court Mjini Windhoek, Namibia, usiku wa Alhamisi Agosti 16, 2018.Makamu wa Rais anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika mkutano huo.
Katibu Mtendaji wa SADC Dkt. Stregomena Tax akizongwa na wanahabari kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC (SADC Organ on Politics, Defence and Security) katika ukumbi wa Mikutano wa hoteli ya Safari Court Mjini Windhoek, Namibia, usiku wa Alhamisi Agosti 16, 2018
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais Edgar Lungu wa Zambia baada ya kumalizika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC (SADC Organ on Politics, Defence and Security) katika ukumbi wa Mikutano wa hoteli ya Safari Court Mjini Windhoek, Namibia, usiku wa Alhamisi Agosti 16, 2018. 
Rais Edgar Lungu wa Zambia, Rais Joseph Kabila wa DRC, Rais Dkt. Hage Geingob wa Namibia na Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika kusini wakibadilishana mawazo kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC (SADC Organ on Politics, Defence and Security) katika ukumbi wa Mikutano wa hoteli ya Safari Court Mjini Windhoek, Namibia, usiku wa Alhamisi Agosti 16, 2018

KAMISHINA UNHCR AMALIZA ZIARA NCHINI, ATEMBELEA KAMBI NA KUTOA RAI

$
0
0
ZIARA ya Kamishina msaidizi (ulinzi) kutoka shirika la wakimbizi Duniani (UNHCR),Volker Turk imehitimishwa jijini Dar es salaam huku akihimiza kuwa kila mkimbizi ana haki ya kuamua aidha kurejea nchini kwake au la.

Turk amekuwa nchini kwa siku nne kuanzia Agosti 13 mpaka Agosti 16 Agosti 2018 ,Turk amehitimisha ziara yake kwa kukutana na wanahabari jijini Dar es salaam, katika ziara hiyo aliambatana na Mratibu wa tume Afrika Valentin Tapsob na Mratibu wa wakimbizi (kanda) kutoka Burundi bi. Catherine Wiesner.

Lengo la ziara hiyo ya Kamishina kutoka UNHCR ilikuwa ni kufanya majadiliano yaliyohusisha serikali na wadau kuhusu changamoto na masuluhisho kwa zaidi ya wakimbizi 34,000 na wale wanaoomba hifadhi (asylum seekers) nchini.Imeelezwa kuwa idadi kubwa ya wakimbizi waliopo nchini wanatoka katika nchi za Burundi na Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo ambapo asilimia 87 wanaishi katika kambi 3 zilizopo Mkoani Kigoma.

Kamishina Turk pia ametembelea kambi ya wakimbizi Nduta ambapo alishuhudia mchakato wa kuwarejesha makwao wakimbizi kutoka Burundi na hadi sasa zaidi ya wakimbizi 42,000 wamerejea nchini Burundi.

" Haki ya wakimbizi lazima iheshimiwe katika kuamua kurejea nchini mwao au la" amesema Turk na kuongeza kuwa maamuzi hayo yaangalie taarifa iliyotolewa bila kulazimishwa aidha arejee au la.Pia wawakilishi kutoka nchini Burundi wamekutana na Kamishina Turk na kueleza kuwa idadi ya wakimbizi imefikia 400,000 hadi kufikia Julai 31 mwaka huu.

Aidha imesemwa kuwa hali ya wakimbizi kutoka Burundi imekua chini zaidi duniani katika kupokea misaada ya kibinadamu, UNHCR na washirika wengine walipokea asilimia 12 ya dola milioni 391 za kimarekani pekee kwa mwaka 2018 na mwaka 2017 asilimia 21 ya misaada ilipokelewa kwa ajili ya wakimbizi kutoka Burundi.

Kutokana na hali hiyo Turk ameiomba jumuiya ya kimataifa kuangalia hali hiyo ya kusahaulika kwa wakimbizi katika kupatiwa misaada ya kibinaadamu.Katika ziara hiyo ambayo Kamishina Turk alikutana na mamlaka za serikali, wakuu wa balozi, wafadhili na wadau mbalimbali nchini ameaidiwa kuwa Tanzania itahakikisha maamuzi ya wakimbizi katika kurejea nchini kwao yataheshimiwa.
Kamishina msaidizi (ulinzi) kutoka shirika la wakimbizi Duniani (UNHCR),Volker Turk akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) jana jijini Dar kuhusiana na ziara yake ya siku nne,lengo ya ziara hiyo ilikuwa ni kufanya majadiliano yaliyohusisha serikali na wadau kuhusu changamoto na masuluhisho kwa zaidi ya wakimbizi 34,000 na wale wanaoomba hifadhi (asylum seekers) nchini.
Kamishina msaidizi (ulinzi) kutoka shirika la wakimbizi Duniani (UNHCR),Volker Turk akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari jana jijini Dar kuhusiana na ziara yake ya siku nne,lengo ya ziara hiyo ilikuwa ni kufanya majadiliano yaliyohusisha serikali na wadau kuhusu changamoto na masuluhisho kwa zaidi ya wakimbizi 34,000 na wale wanaoomba hifadhi (asylum seekers) nchini.Pichani kushoto ni Mratibu wa tume ya Afrika Valentin Tapsob,Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi Tanzania (UNHCR), Chansa Kapaya na kulia ni Mratibu wa wakimbizi (kanda) kutoka Burundi,Catherine Wiesner.
Baadhi ya Wanahabari wakimsikiliza Kamishina msaidizi (ulinzi) kutoka shirika la wakimbizi Duniani (UNHCR),Volker Turk alipokuwa akizungumza nao kuhusu ziara yake ya siku nne aliyoifanya nchini Tanzania

UJAMBAZI WA SILAHA UMEPUNGUA NCHINI-IGP SIRRO

$
0
0
Na Jeshi la Polisi

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro ametoa onyo kali kwa majambazi na wahalifu wengine hususani wanaotumia silaha za moto kuacha mara moja kabla ya kukutana na moto mkali wa Jeshi la Polisi ambapo pia ametoa wito kwa wazazi kuwakanya watoto wao kujihusisha na vitendo hivyo.

IGP Sirro ameyasema hayo wakati akizungumza na Wakazi wa Mto wa Mbu Tarafa ya Manyara Wilayani Monduli Mkoani Arusha wakati wa Ziara yake mkoani humo yenye lengo la kubaini changamoto za kiuhalifu na kuzitafutia ufumbuzi.Alisema hivi sasa ujambazi wa kutumia silaha umepungua kwa kiasi kikubwa na baadhi ya matukio ambayo yamekuwa yakijitokeza yanaendelea kudhibitiwa na Jeshi la Polisi.

“Nawasihi wanaofikiria kuendelea kufanya vitendo vya uhalifu ikiwemo vya utumiaji wa silaha na kuua watu waache mara moja kwa kuwa wakikutana na moto wa Jeshi la Polisi wasije wakajilaumu mana kwa sasa moto wetu ni mkali hivyo nawashauri wazazi wakanye watoto wao” Alisema Sirro.

Aidha amewataka Wakazi wa Mto wa mbu Wilayani Monduli kuendelea na shughuli zao kama kawaida kwa kuwa usalama umeimarishwa katika kupambana na wahalifu waliokuwa wakifanya vitendo vya kuwaua watu hususani wanawake ambapo katika kipindi cha hivi karibuni kuliripotiwa matukio kadhaa ambayo yalileta wasiwasi katika eneo hilo muhimu kwa utalii.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na na Wakazi wa Kata ya Mto wa Mbu Wilayani Monduli katika mkutano wa hadhara wakati wa Ziara yakeya kikazi Mkoani Arusha yenye lengo la kutatua changamoto za uhalifu (Picha na Jeshi la Polisi).
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akikagua gwaride baada ya kuwasili Shule ya Polisi Moshi zamani CCP kwa ziara ya kikazi kuangalia mwenendo wa mafunzo chuoni hapo na kuzungumza na Wakufunzi wa chuo hicho. (Picha na Jeshi la Polisi).
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana na Maofisa waliopo Shule ya Polisi Moshi zamani CCP wakati wa ziara ya kikazi kuangalia mwenendo wa mafunzo chuoni hapo na kuzungumza na Wakufunzi wa chuo hicho. (Picha na Jeshi la Polisi).
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana na Wakazi wa Kata ya Mto wa Mbu Wilayani Monduli wakati alipokwenda kuzungumza nao wakati wa Ziara yakeya kikazi Mkoa wa Arusha yenye lengo la kutatua changamoto za uhalifu (Picha na Jeshi la Polisi).

ASILIMIA 90 YA MKAKATI WA KUKUZA UCHUMI KUFIKIWA BAADA YA MIAKA MITATU-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema baada ya mitatu Serikali itakuwa imefikia asilimia 90 ya lengo iliyojiwekea la kukuza uchumi kutoka wa chini hadi wa kati kwa kupitia sekta ya viwanda.

Amesema Serikali imedhamiria kukuza uchumi waTaifa na wa wananchi ili kufikia wa kati ifikapo 2025, hivyo amewaomba wananchi waendelee kuipa ushirikiano.Waziri Mkuu aliyasema hayo jana jioni (Alhamisi, Agosti 16, 2018) alipozungumza na wananchi katika kijiji cha Chomachankola wilayani Igunga akiwa katika ziara yake ya kikazi wilayani Igunga, Tabora.

“Tunaomba Watanzania waendelee kuwa watulivu na waipe ushirikiano Serikali yao katika kipindi hiki ambacho inaendelea kutekeleza ahadi yake ya kuinua uchumi,” alisema.Kadhalika, Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali inaendelea na utekelezaji wa ahadi zote zilizotolewa na Rais Dkt. John Magufuli pamoja na zile zilizomo kwenye Ilani ya uchaguzi.

Waziri Mkuu alitaja ahadi hizo kuwa ni pamoja na ujenzi na ufufuaji wa viwanda vya kutengeneza bidhaa mbalimbali nchini, kikiwemo kiwanda cha kuchambua pamba cha Manonga.Alisema kiwanda cha kuchambua pamba cha Manonga ambacho kisimama kuchambua pamba kwa miaka 25 na sasa kimefufuliwa na kinafanya kazi, hivyo aliwaomba wananchi watoe ushirikiano kwa mwekezaji.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mitambo mipya ya kuchambua pamba inayofungwa katika kiwanda cha Manonga wilayani Igunga akiwa katika ziara ya kikazi mkoa wa Tabora Agosti 16, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa Tabora, Aggrey Mwanri. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama eneo inaposimikwa mitambo mipya ya kuchambua pamba katika kiwanda cha Manonga wilayani Igunga wakati alipokitembelea kiwanda hicho akiwa katika ziara ya kikazi mkoa wa  Tabora, Agosti 16, 2018. Kiwanda hicho ambacho kilisimamisha uzalishaji miaka 25 iliyopita kimefufuliwa na wamiliki wake , Chama Kikuu cha Ushirika cha mkoa wa Tabora, Igembensabo na Kampuni ya M/S Rajani Metals and Machinery kutokana na hamasa kubwa ya uchumi wa viwanda inayofanywa na serikali. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Chomachankola wilayani Igunga akiwa katika ziara ya kikazi mkoa wa Tabora, Agosti 16, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) .

NDC wazindua Uuzaji wa Trekta za URSUS Mkoa wa Mwanza

$
0
0


Mwenyekiti wa Bodi ya NDC Dr Samuel Nyantahe akitoa maelezo juu ya mradi wa kuunganisha matrekta unaotekelezwa hapa nchini chini ya NDC wakati wa uzinduzi wa Uuzaji Trekta hizo mkoa wa Mwanza katika eneo la Viwanda Makuyuni.( 16.08.2018)
Mwakilishi kutoka Bneki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) Bw Steven Kang’ombe akitoa maelezo ya namna ya kupata mikopo ya ununuzi wa Trekta za URSUS wakati wa uzinduzi wa uuzaji Trekta hizo mkoa wa Mwanza
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Ndg John Mongella akibadilishana mawazo na viongozi mbalimbali wa Serikali wakati wa Uzinduzi wa Uuzaji wa Trekta za URSUS mkoa wa Mwanza katika eneo la Viwanda Makuyuni jana (16.08.2018)

KITILYA NA WENZAKE WAENDELEA KUSOTA RUMANDE

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

Aliyekuwa kamishna wa TRA, Harry Kitilya na waliokuwa maofisa wa benki ya Stanbic, Shose Mori Sinare na Sioi Graham Solomon wanaokabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha.

wanaendelea kusota rumande kwa takribani miaka miwili sasa. Huku upelelezi wa kesi yao ukiwa bado haujakamilika. Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa upelelezi bado haujakamilika ila  upo katika hatua za kukamilika, 

Baada ya kueleza hayo. Wakili wa utetezi Nsangizyo Nzilahulula alidai kuwa kumekuwepo na kauli za upande wa mashtaka kuwa bado kidogo wakamilishe upelelezi katika kesi hiyo ambazo ni zaidi ya mwaka sasa.

Na hakuna chochote kinachoendelea, hivyo aliiomba mahakama iwasaidie.

Baada ya kutolewa kwa Maelezo hayo , Wakili Kishenyi alieleza kuwa maombi ya kuomba msaada wa mahakama ni mapema sana kwa kuwa wanafafanya jitihada za kukamilisha upelelezi.

Hakimu Shaidi baada ya kusikiliza hoja za pande zote, amesema ameishafanya mazungumzo na upande wa mashtaka na kwamba kuna maagizo Fulani wanayafanyia kazi.

Kesi imeahirishwa hadi Agosti 31,2018.

Katika kesi hiyo, washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kutakatisha fedha.

Washtakiwa hao,  Wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Machi 2013 na Septemba 2015 wakati wa mchakato wa mkopo wa dola za Marekani 550 milioni  kwa  serikali ya Tanzania kutoka Benki ya Standard Uingereza.

Wanadaiwa kuwa  Machi 2013 jijini Dar es Salaam walijipatia Dola za Marekani 6 milioni, wakionyesha kuwa fedha hizo zilikuwa ni malipo ya ada ya uwezeshaji upatikanaji wa mkopo  na zililipwa kupitia  Kampuni ya Egma T Ltd.

Washtakiwa  hao wanadaiwa  kutakatisha fedha kwa kuhamisha, kuchukua na kuweka kiasi cha Dola za Marekani 6 milioni katika akaunti tofauti tofauti  za benki.

WAMILIKI WA VIWANDA VYA SARUJI WAAHIDI KUONGEZA UZALISHJI

$
0
0
Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya akizungumza na wadau mbalimbali wakiwemo wazalishaji wa Saruji katika mkutano wa kujadili upungufu wa Saruji nchini uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Profesa Joseph Bushweishaija akitoa maelezo kuhusioana na mkutano na huo kwa wadau wa uzalishaji wa viwanda vya saruji.
Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Uchorongaji wa Stamico, Alex Rutagwelela akizungumza na waandishi habari kuhusiana na stamico iliyojipanga katika uzalishaji wa makaa ya mawe .
Baadhi ya wazalishaji wa viwanda vya Saruji nchini.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

WAMILIKI wa Viwanda vya  Uzalishaji wa Saruji wameiahidi serikali kuongeza uzalishaji wa bidhaa hiyo ili kuondoa uhaba wa bidhaa hiyo muhimu kwa wananchi na kurudisha bei ya zamani.

Wamiliki wa viwanda hivyo wamesema hayo katika mkutano wao na Wizara ya Viwanda , Biashashara na Uwekezaji uliokuwa ukiongozwa na Naibu Waziri, Mhandisi Stella Manyanaya, ambapo walisema katika kipindi cha hivi karibuni walikuwa na changamoto ya upatikanaji wa makaa ya mawe pamoja na baadhi ya viwanda kuharibika Mitambo.

Akizungumza na wadau hao Mhandisi Manyanya amewataka wamiliki hao kuzalisha saruji ya kutosheleza nchi kwanza ndipo saruji ya zaida wauze nje ya nchi. Amesema kuwa kuuza saruji  nje ya nchi  ni fursa kiuchumi  hivyo lazima viwanda vizalishe kwa bidhaa ya kukidhi mahitaji ya ndani na nje. aidha amewataka wazalishaji wa makaa ya mawe wazalishe kwa wingi makaa hayo yatakayowezesha kuvilisha viwanda vyote vya saruji ili Tarula na Tanroad  aweze kujenga miundombinu kuelekea sehemu yanakotoka makaa ya mawe.

Shirika la Taifa la Madini (Stamico) limesema kuwa litaongeza kasi katika uzalishaji wa makaa ya mawe katika miradi yake ya Kiwira pamoja na Kaburu ili kuhakikisha viwanda vya saruji vinapata makaa ya mawe ya kutosha.

Akizungumza na waandishi habari baada ya mkutano huo na Naibu Waziri, Manyanya, Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Uchorongaji wa Stamico , Alex Rutagwelela amesema kuwa kazi yao ni kuhakikisha wanazalisha makaa ya mawe ya kutosha kwa wazalishaji wa saruji nchini.


Amesema kuwa changamoto ya viwanda vya saruji ni makaa ya  mawe hivyo kasi ya uzalishaji lazima iongezeke katika kutatua tatizo la upungufu wa saruji lisiwe la kujirudia kwa mara nyingine kutokana na kwamba miradi mingi inayotekelezwa nchini na hata nje ya nchi inahitaji saruji hiyo.

TFDA YAENDELEA NA MIKAKATI YA UHAMASISHAJI WADAU WA NDANI NA NJE YA NCHI KATIKA UWEKEZAJI WA VIWANDA VYA DAWA NCHAINI

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bi. Agnes Sitta Kijo (wa kwanza kushoto), waliosimama, akiwasilisha mada inayohusu vigezo vya uanzishaji viwanda vya dawa nchini Tanzania kwa wadau wa kongamano la biashara la kimataifa, linalofanyikia Beijing Kempinski Hotel, Lufthansa Centre, Beijing – China.


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (wa tatu kushoto), waliokaa msitari wa mbele, akifuatilia mada iliyowasilishwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bi. Agnes Sitta Kijo (hayupo pichani)

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bi. Agnes Sitta Kijo akielezea wadau uwezo wa TFDA kiutendaji ulioiwezesha kukidhi viwango vya kimataifa (ISO 9001:2015),  Maabara ya TFDA kutambuliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) pia kukidhi vigezo vya kimataifa vya umahiri wa uchunguzi wa kimaabara wa kiwango cha ISO/IEC 17025:2005

Na Gaudensia Simwanza – Dar es Salaam
TFDA inaendelea na uhamasishaji wa wadau wa ndani na nje ya nchi katika kuanzisha viwanda vya dawa nchini Tanzania. Hivi sasa, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bi. Agnes Sitta Kijo yupo nchini China kwa ajili ya kuhamasisha wadau mbalimbali wa kimataifa kuja kufanya uwekezaji huo katika nchi yetu.
Katika mada yake aliyoiwasilisha katika kongamano la kimataifa la wadau wa dawa linalofanyikia katika Beijing Kempinski Hotel, Lufthansa Centre, Beijing – China, aliwafafanulia wadau hao kuhusu vigezo vya kisheria vinavyotakiwa na  kuwahakikishia wadau hao kwamba TFDA imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji wa tasnia ya dawa na kwamba mwekezaji yeyote atakayekidhi vigezo hatakwamishwa bali atapewa ushirikiano kwa kuwa Tanzania ina dhamira ya dhati katika uanzishaji wa viwanda hususan vya dawa.

Matarajio ya TFDA kwa mikakati ya aina hii, ni kushuhudia uanzishwaji wa viwanda vya bidhaa zinazodhibitiwa na taasisi hii kwa nia ya kutosheleza mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi, kulinda afya ya jamii na kukuza uchumi wa nchi. 

Mkazi wa Kigamboni ajishindia mbuzi kutoka Jumia

$
0
0

  Mkazi wa Kigamboni jijini Dar es Salaam,  Dotto Steve amejishindia mbuzi kutoka Jumia kupitia kampeni inayoendelea sasa ya kuelekea sikukuu ya Eid Al Adha.

Kampeni hiyo imekuja kama sehemu ya Jumia kuwazawadia wateja wake mbuzi ili kunogesha shamrashamra za sikukuu ya Eid Al Adha au maarufu kama ‘Eid ya kuchinja.’ Waislamu nchini Tanzania na duniani kote wanatarajiwa kusherehekea sikukuu ya Eid siku ya Jumatano ya Agosti 22 kama ilivyotangazwa na Baraza la Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA).

Akizungumza leo wakati wa kukabidhiwa mbuzi wake aliyeshinda kwenye mtandao wa Jumia, Steve amesema kuwa yeye ni mteja mkubwa wa Jumia na alikuwa ameingia mtandaoni kwa ajili ya kununua soksi ndipo alipobahatika kujishindia mbuzi aliyefichwa ndani yake.

“Mimi ni mteja mkubwa wa Jumia katika kufanya manunuzi ya bidhaa mbalimbali. Lakini ni mfanyabiashara pia ambaye nina mchakato wa kujiunga na mtandao huu wa kuuza bidhaa mtandaoni. Ninajihisi mwenye bahati mpaka kujishindia mbuzi huyu kwa sababu niliingia mtandaoni kwa ajili ya kununua soksi.

Lakini nilishtushwa kidogo na bei ya soksi, ilikuwa kubwa tofauti na nilivyotaraji ila kwa kuwa nilizipenda zile soksi mimi nikabofya ili nizinunue. Baada ya muda mchache ndipo nikapigiwa simu na watu wa Jumia na kuniambia kuwa nimefanikiwa kumpata mbuzi aliyekuwa amefichwa mtandaoni mwao hivyo yanipasa nije kumchukua,” alielezea namna alivyoshinda Bw. Steve.

Mkurugenzi Mkuu wa Jumia Tanzania, Zadok Prescott akimkabdhi Mkazi wa Kigamboni jijini Dar es Salaam, Dotto Steve aliyejishindia mbuzi kutoka Jumia kupitia kampeni inayoendelea sasa ya kuelekea sikukuu ya Eid Al Adha ( Eid ya kuchinja) . Kampeni hiyo imekuja kama sehemu ya Jumia kuwazawadia wateja wake mbuzi ili kunogesha shamrashamra za sikukuu ya Eid Al Adha au maarufu kama ‘Eid ya kuchinja.’ Waislamu nchini Tanzania na duniani kote wanatarajiwa kusherehekea sikukuu ya Eid siku ya Jumatano ya Agosti 22 kama ilivyotangazwa na Baraza la Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA).
Mkazi wa Kigamboni jijini Dar es Salaam, Dotto Steve akifafanua zaidi mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo namna alivyojishindia zawadi hiyo,mara baada ya kukabidhiwa mbuzi wake aliyeshinda kwenye mtandao wa Jumia, jijini Dar
Mshindi wa Mbuzi akiwa na baadhi ya Viongozi waandamizi wa Jumia Tanzania katika picha ya pamoja mara baada ya makabidhiano leo.

MBUNGE CCM AIBUA UFISADI WA MILION 176 KWENYE ZIARA YA WAZIRI MKUU IGUNGA

$
0
0
Na Francis Daud, Manonga-Tabora
MBUNGE wa Jimbo la Manonga Mh. Seif Khamis Gulamali ameibua ubadhirifu mkubwa wa fedha uliofanyika ndani ya jimbo lake mbele ya Waziri mkuu Kassim Majaliwa aliyekuwa ziarani Mkoani Tabora.

 Akihutubia mbele ya mamia ya wananchi wa Manonga waliokuwa wakimshangilia muda wote Gulamali amemweleza Waziri Mkuu kuwa  kuna upotevu wa zaidi ya shilingi milioni 140 mali ya kijiji cha Bulagamilwa.

Gulamali amesema kuwa fedha hizo ambazo zilikusanywa kama mrahaba wa machimbo ya madini yaliyopo katika kijiji hicho na hata hivyo baada ya kelele za wananchi, mtendaji wa kijiji alihamishwa toka kijijini hapo baada ya wananchi kukosa imani na utendaji wake.

Aidha Mbunge huyo alifumua mradi mwingine wa ujenzi wa mashine za kukoboa mpunga katika kata ya Choma Chonkola na  Alimweleza Waziri mkuu kwamba, zaidi ya milioni 35 hazijulikani mpaka leo zilipokwenda na hakuna mashine iliyofungwa.

Akilitolea maelezo suala hilo, Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Tabora  aliposimamishwa na waziri mkuu kujibu tuhuma hizo alisema ni kweli wana faili hilo na bado wanaendelea kukusanya taarifa muhimu kabla ya kufungua mashtaka kwa wahusika.

 Maelezo hayo hayakuridhisha umma wa wana Manonga na Waziri mkuu akatoa maagizo kwa Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Tabora Francis Zuakuu kumkamata aliyekuwa mtendaji wa kijiji cha Bulagamilwa, Ntemi James kwa kuwa ndiye mtuhumiwa wa kwanza katika sekeseke hilo la upotevu wa  shilingi Milion 141 za kijiji hicho.

Aidha, Waziri mkuu amemwagiza OCD wa wilaya ya Igunga kuwasweka ndani viongozi na kamati iliyohusika na upotevu wa milioni 35 zilizotolewa na halmashauri ya wilaya ya Igunga kwa ajili ya uwekaji wa mashine za kisasa za kukuboa mpunga katika kata ya Choma Chonkola.
 Mbunge wa Manonga Seif Gulamali akizungumza na wananchi mara baada ya Waziri Mkuu kuwasili jimboni hapo katika ziara yake Mkoani Tabora.
Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa akiwa na viongozi mbalimbali wakingozwa na Mbunge wa Manonga Seif Gulamali, wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Mkoani humo.

Mavunde aahidi kutoa usafiri bure kwa wananchi Jimbo la Dodoma Mjini watakaopatwa na misiba

$
0
0

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Peter Mavunde ameahidi kutoa usafiri bure kwa wananchi wa Jimbo la Dodoma Mjini watakaopata misiba kwa kutoa gari ambalo litakaa eneo la kuhifadhia miili ya Marehemu “ MORTUARY” mahsusi kwa ajili ya kusafirisha miili ya marehemu na waombelezaji.

Mavunde ameyasema hayo leo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma alipoongoza maelfu ya wananchi wa Dodoma katika uzoezi la upimaji macho katika kambi maalum iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Ofisi ya Mbunge Dodoma Mjini,Lions Club Mzizima na Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma ambapo wananchi wanapata huduma ya bute ya upimaji macho,kupatiwa miwani na kufanyiwa upasuaji wa jicho.

Aidha,Mh Mavunde amewashukuru sana Lions Club Mzizima kwa kutoa huduma hiyo kwa wananchi wake na kuwaomba wasisite kuendelea kutoa huduma hiyo pindi watakapohitajika wakati mwingine kwa kuwa matatizo ya mtoto wa jicho ni kati ya matatizo makubwa yanayowaathiri wananchi wengi wa mkoa wa Dodoma.
Baadhi ya Wakazi wa Dodoma waliojitokeza kwa wingi leo kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Peter Mavunde katika uzoezi la upimaji macho katika kambi maalum iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Ofisi ya Mbunge Dodoma Mjini,Lions Club Mzizima na Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma
Mbunge wa Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde akipata maelezo kutoka kwa Viongozi wa Mzizima Lions Club
Mbunge wa Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde akisalimiana na baadi ya Viongozi wa Mzizima Lions Club
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images