Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

RC BRIGEDIA JENERALI MWANGELA AKATAA OMBI LA MKANDARASI KUONGEZEWA MUDA

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemas E Mwangela akikagua ujenzi wa daraja la Kikamba linalounganisha kata ya Kapalala na Gua Wilayani Songwe, katika ziara yake ya siku mbili wilayani humo aliyoianza leo. Daraja hilo limeanza kujengwa Oktoba 20, 2017 na linatarajiwa kukamilika Septemba, 2018 likiwa limegharimu shilingi bilioni 1.4.
Ujenzi wa daraja la Kikamba linalounganisha kata ya Kapalala na Gua Wilayani Songwe ukiendelea, Daraja hilo limeanza kujengwa 20 Oktoba, 2017 na linatarajiwa kukamilika Septemba, 2018 likiwa limegharimu shilingi bilioni 1.4.

Na Grace Gwamagobe, Songwe

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemas E Mwangela amekataa ombi la Mkandarasi kutoka kampuni ya Mats Engineering Ltd Paulo Philipo Paulo la kuongezewa kipindi cha miezi miwili ili aweze kukamilisha ujezi wa Daraja la Kikamba Wilayani Songwe.

Brigedia Jenerali Mwangela amekataa ombi hilo leo alipokagua ujenzi wa daraja la Kikamba linalounganisha kata za Kapalala na Gua wilayani Songwe kwakuwa sababu alizotoa mkandarasi huyo hazijitosheleji.

Amesema daraja hilo lazima likamilike kwa muda uliopangwa ambao ni Septemba, 2018 huku mkandarasi huyo akitoa sababu kuwa atachelewa kukamilisha ujenzi huo kutokana na mvua nyingi zilizonyesha na mwamba mgumu uliopo eneo la ujenzi.

“Mkandarasi ahakikishe anafanya kazi mchana na usiku ili akamilishe ndani ya muda wa mkataba, vifaa vya kumuwezesha kufanya hivyo anavyo na ombi la kuongezewa muda wa ujenzi mimi siafikiani nalo”, amesema Brigedia Jenerali Mwangela.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Songwe Samuel Jeremia amesema yeye na viongozi wengine wataendelea kusimamia miradi ya maendeleo na katika ujenzi wa daraja hilo watahakikisha wanamsimamia mkandarasi huyo ili amalize ndani ya muda uliopangwa.

Daraja la Kikamba linaolunganisha kata za Kapalala na Gua limeanza kujengwa mwezi Oktoba 2017 na linatarajiwa kukamilia Septemba 2018 likiwa limegharimu shilingi bilioni 1.4.

NAIBU WAZIRI STELLA IKUPA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA TANO WA THTU.

0
0
Na Dixon Busagaga,Moshi.

CHAMA cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU) kimeiomba serikali kutunga sera ya uwepo wa eneo rafiki la kulelea au kunyonyeshea watoto katika sehemu za Kazi pamoja na kuunda chombo cha kusimamia utekelezwaji wa uwepo wa sera ya unaynyasaji wa kijinsia katika taaasisi za elimu ya juu nchini.

Mbali na ombi hilo THTU pia kimewasilisha ombo kwa serikali la kuundwa Vyombo vya kufuatilia waajiri ambao hawazingatii maagizo ya sera zinazotungwa na serikali ili kulinda haki na maslahi ya wafanyakazi sambamba na uwepo wa muundo wa utumishi kwa wafanyakazi waendeshaji katika taasisi za umma za elimu ya juu nchini.

Hayo yalibainishwa wakati wa mkutano mkuu wa tano wa chama hicho unaofanyika kwa siku mbili katika Chuo Kikuu cha Ushirika ,Moshi (MoCU) ukishirikisha zaidi ya wanawake 80 kutoka vyuo vikuu 36,vitatu vikiwa ni vya binafsi na 33 vya serikali .

Katika risala yao kwa mgeni rasmi ,iliyosomwa na katibu wa THTU,Amina Mdidi ,wanawake hao walisema THTU imekuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ya kutokuwepo kwa mwongozo wa mishahara au bodi ya kusimamamia na kudhibiti malipo ya watumishi kwa vyuo binafsi.

“Changamoto nyingine zinazootukabili ni baadhi ya taasisi kutolipa nauli za likizo kwa enza wa wafanyakazi wanawake (Mume) na watoto chini ya miaka mitano na ukosefu wa vituo rafiki kwa malezi ya watoto wachanga”alisema Mdidi.
Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,kazi ,Vijana,Ajira na wenyeulemavu,Stella Ikupa akitamburishwa baadhi ya viongozi walioshiriki mkutano mkuu wa tano wa Chama cha Wafanyakazi wa taasisi za elimu ya juu Tanzania (THTU) unaofanyika mjini Moshi.
Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,kazi ,Vijana,Ajira na wenyeulemavu,Stella Ikupa akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa tano wa Chama cha Wafanyakazi wa taasisi za elimu ya juu Tanzania (THTU) unaofanyika mjini Moshi.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa taasisi za elimu ya juu Tanzania (THTU) Dkt Paul Loisulie akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.
Mwenyekiti wa kamati ya Wanawake wa Chama cha Wafanyakazi wa taasisi za elimu ya juu Tanzania(THTU),Salma Fundi akizungumza katika mkutano huo.
Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Kippi Warioba akizungumza katika mkutano huo.
Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,kazi ,Vijana,Ajira na wenyeulemavu,Stella Ikupa akiwa katika picha ya pmaoja na washiriki wa mkutano huo.NA Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.




NAIBU WAZIRI STELLA IKUPA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA TANO WA THTU MKOANI KILIMANJARO

0
0
Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,kazi ,Vijana,Ajira na wenyeulemavu,Stella Ikupa akiwasili katika ukumbi wa J.K Nyerere uliopo Chuo Kikuu cha Ushirika,Moshi (MOCu) kwa ajili ya kufungua mkutano wa Tano wa chama hicho.

Na Dixon Busagaga,Moshi.

CHAMA cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU) kimeiomba serikali kutunga sera ya uwepo wa eneo rafiki la kulelea au kunyonyeshea watoto katika sehemu za Kazi pamoja na kuunda chombo cha kusimamia utekelezwaji wa uwepo wa sera ya unaynyasaji wa kijinsia katika taaasisi za elimu ya juu nchini.

Mbali na ombi hilo THTU pia kimewasilisha ombo kwa serikali la kuundwa Vyombo vya kufuatilia waajiri ambao hawazingatii maagizo ya sera zinazotungwa na serikali ili kulinda haki na maslahi ya wafanyakazi sambamba na uwepo wa muundo wa utumishi kwa wafanyakazi waendeshaji katika taasisi za umma za elimu ya juu nchini.
Hayo yalibainishwa wakati wa mkutano mkuu wa tano wa chama hicho unaofanyika kwa siku mbili katika Chuo Kikuu cha Ushirika ,Moshi (MoCU) ukishirikisha zaidi ya wanawake 80 kutoka vyuo vikuu 36,vitatu vikiwa ni vya binafsi na 33 vya serikali . 
Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,kazi ,Vijana,Ajira na wenyeulemavu,Stella Ikupa akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa tano wa Chama cha Wafanyakazi wa taasisi za elimu ya juu Tanzania (THTU) unaofanyika mjini Moshi.

Katika risala yao kwa mgeni rasmi ,iliyosomwa na katibu wa THTU,Amina Mdidi ,wanawake hao walisema THTU imekuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ya kutokuwepo kwa mwongozo wa mishahara au bodi ya kusimamamia na kudhibiti malipo ya watumishi kwa vyuo binafsi.

“Changamoto nyingine zinazootukabili ni baadhi ya taasisi kutolipa nauli za likizo kwa enza wa wafanyakazi wanawake (Mume) na watoto chini ya miaka mitano na ukosefu wa vituo rafiki kwa malezi ya watoto wachanga”alisema Mdidi.

Katika hatua nyingine ,Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania kilitoa ripoti ya utafiti juu ya utekelezaji wa sera ya maendeleo ya mwananmke na jinsia ya mwaka 2000 katika taasisi za elimu ya juu Tanzania ikionyesha aslimia 80 ya taasisi hizo zilionyesha kutokuwepo kwa masuala ya jinsia katika mpango mkakati wa taasisi.

Baadhi ya Wajumbe wakiwa katika mkutano huo.

Akisooma utafiti huo ,Mwenyekiti wa kamati ya Wanawake (THTU) taifa Salma Fundi alisema asilimia 80 ya taasisi hazikuonyesha uwepo wa mafunzo kwa wanafunzi au wafanyakazi kuhusiana na masuala ya jinsia.

“Asilimia 70 ya taasisi hazina sera ya unyanyasaji wa kijinsia ambazo ni muhimu katika kupunguza ubaguzi wa kijinsia na ukatili huku asiliamia 60 ya washiriki walikuwa na mtazamo hasi juu ya sera ya jinsia kwa kuamini ni sera inayomhusu mwanamke tu”alisema Fundi.

Katika hotuba yake Mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano huo,Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,kazi ,Vijana,Ajira na wenyeulemavu,Stella Ikupa alisema THTU kwa muda mfupi kimekuwa chama kinachotoa chachu ya maendeleo na amani ndani ya taasisi za elimu ya juu Tanzania. 

RICHARD MAYONGELA ATHIBITISHWA RASMI KUWA MKURUGENZI MKUU MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA

0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii
ALIELYEKUWA Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Tanzania Richard Mayongela athibitishwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini.

Taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habar imesema kuwa amethibitishwa kwenye nafasi hiyo  na Kaimu Mkurugenzi wa Railimali na Utawala  Lawrance Thobias wakati wa Mkutano wa Mameneja wa viwanja vya mikoani na Wakuu wa Vitengo mbalimbali vya Mamlaka.

Amefafanua kwa kueleza kwamba  amethibitisha kupokea barua ya uthibitisho huo kutoka kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwele mara baada ya kuona Utendaji wake mzuri katika Mamlaka.

Hivyo kuanzia sasa Mayongela ndio Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya viwanja vya ndege nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Tanzania Richard Mayongela

Waziri Mwakyembe kuzungumza na watendaji wakuu TRA

0
0
Na Anitha Jonas – WHUSM,Geita
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amewaahidi wadau wa sekta ya filamu  Mkoa wa Geita kufikisha  maombi yao ya kupatiwa stika za TRA kwa kazi zao kwa watendaji wakuu wa TRA iliwaweze kupatiwa stika hizo katika ofisi ya TRA za  mkoani hapo.
 Mheshimiwa Mwakyembe ametoa ahadi hiyo leo mkoani Geita katika kikao na wadau wa kisekta wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo ambapo kikao hicho kililenga  la kupata taarifa na kujua changamoto za wadau hao ili serikali iweze kuchukua hatua stahiki.
“Katika sekta ya Filamu nitazungumza na Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania ili aweze kufika mkoani hapa na timu yake kwa ajili ya kutoa mafunzo ya namna ya kuandaa miswada ya kazi za filamu kwani changamoto kubwa katika sekta ya filamu ni kuwepo na kazi nyingi zisizo na ubora,”Dkt.Mwakyembe.
Akiendelea kuzungumza na wadau hao Waziri huyo alieleza kuwa serikali kupita idara yake ya Sanaa inaangalia namna ya kutafuta wafadhili watakao toa ufadhili wa kulipia mafunzo ya huduma katika ndege ili washindi wa mashindano ya urembo waweze kupata kazi ya kutoa huduma katika  Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL).
Pamoja na hayo nae Msemaji Mkuu wa Serikali Tanzania Dkt.Hassan Abbas alitoa elimu ya matumizi ya sheria mbili  ambazo ni Sheria ya Haki yakupata taarifa ya mwaka 2016 na Sheria ya Huduma ya Habari ya mwaka 2016,ambapo sheria hizi zinazohusu sekta ya habari na kuwafafanulia waandishi wa habari mipaka yao katika mambo ya kuyatolea habari ikiwemo mambo yanayohusu usalama wa taifa.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (kulia) akizungumza na wadau wa kisekta wa Mkoa wa Geita leo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo kwa lengo la kupata taarifa za utekelezaji wa shughuli zao na kujua changamoto zao  ili serikali iweze kuchukua hatua stahiki, kutoka kushoto ni  Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel.
 Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbas (kulia) akitoa ufafafuzi wa sheria mbili zinazohusu sekta ya habari ambazo ni Sheria ya Haki ya Kupata Taarifa 2016 na Sheria ya Huduma za Habari 2016 leo Mkoani Geita katika kikao na wadau wakisekta kwa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo,kushoto ni  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe.
 Miss Geita 2018 Joyce Magesa akizungumza mbele ya Mhe.Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe leo Mkoani Geita katika kikao cha wadau wa kisekta  kuhusu dhamira yake ya kushirikiana na serikali kwa lengo la kufanya kazi za kijamii kama Kauli Mbiu ya Mashindano ya Ulimbwende Duniani mwaka 2018 inavyoelekeza kuwa ni “Urembo na Kazi kwa Maendeleo ya Jamii” nyuma yake kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel.
Wadau wa Michezo Mkoa wa Geita wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (aliyeketi watatu kushoto) mara baada ya kikao na wadau wa kisekta kilichofanyika katika ofisi za Mkuu wa Mkoa Geita leo ,wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa Geita Mhandisi Robert Gabriel  na watatu kulia ni Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbas.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MultiChoice yamwaga Bajaji 27 kwa vijana

0
0
Kampuni ya MultiChoice Tanzania imeimarisha mkakati wake wa kuwawezesha vijana wa Kitanzania kibiashara na kiuchumi kwa kuwafungulia ofisi za uwakala wa DStv na kuwadhamini vitendea kazi mbalimbali ikiwemo kompyuta na pikipiki za magurudumu matatu (Bajaj).

Katika kutimiza hilo kampuni hiyo imekabidhi ofisi na bajaji tisa kwa vijana wa mkoa wa Dar es Salaam na inatarajia kupanua mradi huo kwenda mikoa mingine ikiwemo Mwanza, Arusha, Mbeya na Dodoma.

Akizungumza katika makabidhiano ya Bajaji hizo yaliyofanyika leo Alhamisi Agosti 16 katika makao makuu ya MultiChoice Tanzania jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Mauzo wa kampuni hiyo Salum Salum, amesema hii ni awamu ya kwanza ya mradi huo ambapo wametoa jumla ya bajaji 27 kwa viunga 9 vya Dar es salaam na kwamba baada ya awamu hii watafanya tathmini na kisha kuupanua hapa Dar es Salaam ni mikoa mingine.

Amesema katika mradi huo, MultiChoice inawafadhili vijana hao ofisi za uwakala wa DStv na pia inawadhamini vitendea kazi muhimu kama vile Kompyuta na Bajaji ili viwawezeshe kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Meneja Mauzo wa MultiChoice Tanzania Salum Salum akimkabidhi ufunguo wa Bajaji mmoja wa mawakala wapya wa mauzo wa DStv wa kiunga cha Temeke Rose Haule wakati wa hafla ya kukabidhi Bajaj 27 kwa ajili ya kuwawezesha vijana katika shughuli za mauzo. Hii ni katika kuimarisha mkakati wa MultiChoice wa kuwawezesha vijana wa Kitanzania kibiashara na kiuchumi kwa kuwafungulia ofisi za uwakala wa DStv na kuwadhamini vitendea kazi mbalimbali ikiwemo kompyuta na pikipiki za magurudumu matatu (Bajaj).

“Tumekuwa tukifanya kazi na vijana wengi ambao ni mawakala wa mauzo wa kujitegemea (direct sales) lakini sasa tumeamua tuwafanye wabia wetu wa kibiashara na kuwawezesha kuendesha biashara rasmi ya uwakala wa DStv” alisema Salum na kuongeza kuwa vijana hao watakuwa wakitoa huduma katika maeneo maalum yajulikanayo kama ‘viunga’. Kila wakala atakuwa na kiunga chake, na atakuwa na jukumu la kuhakikisha wateja wa eneo lake wanahudumiwa kwa haraka

“Vijana hawa watakuwa na mtandao wa vijana wengine wa mauzo na mafundi wa kufunga DStv ambao wamepata mafunzo maalum na kuthibitishwa. Kwa hiyo, kama mteja yuko Mbagala, atahudumiwa na wakala wa kiunga cha Mbagala, hivyo hivyo aliyeko Tabata atahudumiwa na kiunga cha Tabata na hii itakuwa kwa viunga vyote ambavyo ni Mbagala, Tabata, Kigamboni, Ilala, Chang’ombe, Mbezi beach, Mbezi Kimara, Manzese na Ukonga.
Meneja Mauzo wa MultiChoice Tanzania Salum Salum (wa pili Kulia) akizungumza na kiongozi wa Kiunga cha DStv Temeke Rose Haule (wa pili Kushoto) wakati wa hafla ya kukabidhi Bajaj 27 kwa ajili ya kuwawezesha vijana katika shughuli za mauzo. Hii ni katika kuimarisha mkakati wa MultiChoice wa kuwawezesha vijana wa Kitanzania kibiashara na kiuchumi kwa kuwafungulia ofisi za uwakala wa DStv na kuwadhamini vitendea kazi mbalimbali ikiwemo kompyuta na pikipiki za magurudumu matatu (Bajaj). Kulia ni Khalfani Soni na kushoto ni Omari Ali wote wa Gongo la Mboto.

Amesema kwa kuwarasimisha vijana hawa, sasa watakuwa wanafanya biashara rasmi, wakiwa na leseni na ofisi na hivyo kuweza pia kulipa kodi stahiki kwa serikali na hivyo kuongeza mchango wao kwa uchumi wa nchi.

Wakizungumza bara baada ya kukabidhiwa bajaji hizo sambamba na laptop, wakuu wa viunga hivyo wamesema wamekuwa wakifanya kazi kama mawakala wadogo wa kujitegemea kwa muda sasa lakini walikuwa wakifanya kazi katika mazingira magumu kutokana na kutokuwa na ofisi rasmi na pia vitendea kazi hususan usafiri.

“Tulikuwa tunafanya mauzo kwa tabu sana kwani kwanza kutokuwa na ofisi ilikuwa ni vigumu kwa wateja kutupata. Pia hata ukipata mteja unalazimika kubeka vifaa kwenye usafiri usio wa uhakika kwenda kwa mteja na hii ilikuwa inapoteza muda na kuongeza gharama” alisema Rose Haule mkuu wa kiunga cha Temeke.
Wakala wa mauzo wa DStv Rose Haule wa Temeke (aliyeko ndani ya Bajaji) akifurahia na wenzake Khalfani Soni wa Gongo la Mboto, Omari Ali wa Gongo la Mboto na Sarah Makasia wa Manzese wakifurahia muda mfupi baada ya hafla ya kukabidhi Bajaj 27 kwa ajili ya kuwawezesha vijana katika shughuli za mauzo. Hii ni katika kuimarisha mkakati wa MultiChoice wa kuwawezesha vijana wa Kitanzania kibiashara na kiuchumi kwa kuwafungulia ofisi za uwakala wa DStv na kuwadhamini vitendea kazi mbalimbali ikiwemo kompyuta na pikipiki za magurudumu matatu (Bajaj).

Naye Yusuph Migeto wa kiunga cha Mbagala amesema kuwa kuwepo kwa ofisi na usafiri wa uhakika kutawahakikishia wateja wao huduma ya haraka na yenye ufanisi. “wakati mwingine wateja walikuwa wanalalamika kwa kucheleweshewa huduma kwani ukipata mteja inabidi ufuate vifaa DStv kisha uende kumfungia mteja. Hii ilikuwa inachelewesha sana. Lakini kwa sasa tutakuwa na uwezo wa kuwa na vifaa karibu na pia kuwepo kwa usafiri wa uhakika kutatufanya kufanya kazi kwa haraka zaidi”

WANANCHI ZAIDI 2000 WANUFAIKA NA MAJI SAFI SALAMA SIMIYU

0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu

Zaidi ya wananchi 2000 wa Kijiji cha Lagangabilili wilayani Itilima Mkoani Simiyu wamenufaika na mradi wa maji safi na salama na kuondokana na adha ya kutumia muda mrefu kutafuta maji kwa kusogezewa huduma ya maji karibu na makazi yao.

Hayo yamesemwa na Mhandisi wa Maji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu, Goodluck Masige wakati akitoa taarifa kwa kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho, aliyefika katika mradi wa maji wa Lagangabilili wenye thamani ya shilingi milioni 967, kwa ajili ya kufungua.

Masige amesema Mradi wa Maji wa Lagangabilili ulianza kutekelezwa mwaka 2015 na kukamilika mwaka 2018 na kuanza kutumika huku akibainisha uwezo wake kuwa, una kisima chenye uwezo wa kutoa maji lita 15,000/= kwa saa, vituo vya kuchotea maji 23 na mtandao wa maji wenye urefu wa mita 29,431.

“Kukamilika kwa mradi huu wakazi 2228 wanapata huduma ya maji safi na salama kwa ajili ya kunywa na matumizi mengineyo,mradi umepunguza muda waliokuwa wanaoutumia wananchi kutafuta maji kwa kuwasogezea huduma ya maji karibu na makazi kwa saa 24,mpaka sasa kaya 25 na taasisi za Umma 20 zimeunganishiwa maji” alisema Masige .

Awali Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe. Benson Kilangi amesema kuwa tangu Uhuru eneo hilo lilikuwa halina maji kabisa, na baada ya kupatikana kwa huduma hiyo kutapunguza adha ya uhaba wa maji, huku akibainisha kuwa Serikali inategemea mradi mkubwa kutoka Ziwa Victoria kuwa suluhisho la kudumu la changamoto ya maji ka ajili ya matumizi ya binadamu na wanyama pia.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho akimtwisha ndoo ya maji Bi. Perusi Makeleja Mkazi wa Kijiji cha Lagangabilili wilayani Itilima mara baada ya kufungua mradi wa maji utakaowahudumia zaidi ya wananchi 2000, katika mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo leo Agosti 15, 2018.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho akifungua bomba la maji kujiridhisha ikiwa linatoa maji kabla ya kuzindua mradi wa maji wa Lagangabilili wilayani Itilima wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Agosti 15, 2018.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho akiweka Jiwe la Msingi Maboresho ya Kituo cha Afya Ikindilo wilayani Itilima mkoani Simiyu, wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Agosti 15, 2018. 
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho (wa pili kulia) akiangalia baadhi ya vifaa vya maabara ya Somo la Bailojia katika Shule ya Sekondari Budalabujiga kabla ya kufungua vyumba vitatu vya maabara vya shule hiyo wilayani Itilima, wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Agosti 15, 2018.


TANAPA WAZINDUA MPANGO WA MATUMIZI BORA YA ARDHI

0
0

WAZIRI wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi, William Lukuvi amezindua mpango wa kupimwa jumla ya vijiji 392 vinavyopakana na hifadhi za Taifa nchini kwenye mikoa mitano kwa lengo la kutatua migogoro ya ardhi katika maeneo hayo.

Waziri Lukuvi akizungumza katika uzinduzi huo, uliofanyika Babati mkoa wa Manyara alisema mpango huo utasaidia kutatua migogoro baina ya vijiji na hifadhi lakini pia vijiji kuwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi.

Alisema, katika mpango huo, awamu ya kwanza itahusisha vijiji 95 katika mikoa mitatu nchini ila lengo ni kufikia mikoa mitano ya Manyara, Mara, Simiyu, Dodoma na Arusha.

“Vijiji hivi vikipimwa vitakuwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi ambapo maeneo ya makazi yatajulikana maeneo ya mifugo na maeneo ya kilimo yatatengwa” alisema .Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Japhet Hasunga,alisema Wizara hiyo, imejipanga kushirikiana na Wizara ya ardhi na wadau wengine kutatua migogoro ya ardhi.

Alisema mpango wa kupima vijiji 392 vinavyopakana na TANAPA utakuwa ni shirikishi na utasaidia sana kutatua migogoro ya uhifadhi lakini utasaidia vijiji. “Katika mpango huo,zitatolewa hati 2375 ambazo zitasaidia wananchi kumiliki maeneo yao” alisema.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akizungumza mjini Babati jana kwenye kikao cha uzinduzi wa mpango wa matumizi bora ya ardhi ya vijiji vinavyopakana na hifadhi za Taifa, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga. 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza mjini Babati kwenye uzinduzi wa mpango wa matumizi bora ya ardhi ya vijiji vinavyopakana na hifadhi za Taifa uliofanywa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi. 
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti (kulia) akimuongoza Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi, William Lukuvi kwenye uzinduzi wa mpango wa matumizi bora ya ardhi ya vijiji vinavyopakana na hifadhi za Taifa jana mjini Babati. 
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti akizungumza mjini Babati kwenye uzinduzi wa mpango wa matumizi bora ya ardhi ya vijiji vinavyopakana na hifadhi za Taifa uliofanywa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi. 


Muhimbili Yashauriwa Kuwekeza zaidi katika Mifumo ya TEHAMA

0
0
Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) umeshauriwa kuongeza kasi na kuboresha matumizi ya mifumo ya TEHAMA katika kutekeleza mipango mkakati iliyojiwekea ili kuokoa muda wa kutoa huduma na kufikia malengo yake.

Kauli hiyo imetolewa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Serikali Mtandao, Dkt. Jabir Kuwe Bakari wakati alipokua akiwasilisha mada juu ya matumizi ya TEHAMA, katika mafunzo ya utawala bora yaliyohusisha wajumbe wa bodi , wakurugenzi, wakuu wa idara pamoja na mameneja majengo wa Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Kwa mujibu wa Dkt. Jabiri, mifumo ya TEHAMA inasidia kuwasiliana kwa wakati kutoka upande mmoja na mwingine tofauti na mfumo wa kutumia karatasi katika kutekeleza majukumu mbalimbali.

Kutokana na umuhimuwa TEHAMA, amewashauri viongozi hao kuboresha mifumo ya TEHAMA kwa kutumia watalaam ambao wanaujuzi wa kutosha ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia.

“Kama nyie wenyewe mtaweza kutengeneza mfumo wa TEHAMA itakua rahisi kuboresha ama kurekebisha pale inapotokea hitilafu, tofauti na kwenda kununua mfumo kutoka nje kwani hutojua ametumia utaalam gani kutengeneza mfumo huo,’’ amesema Dkt. Jabiri. 

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Serikali Mtandao, Dkt. Jabir Bakari akitoa mada kwenye mafunzo ya uongozi bora yaliowahusisha viongozi mbalimbali wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). 

Baadhi wakurugenzi, wakuu wa idara, wakuu wa vitengo na mameneja wa majengo wakiwa kwenye mafunzo hayo katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru akipongezwa na Dkt. Kassim Hussein kutoka Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (IoDT) baada ya Dkt. Bakari kumkabidhi cheti baada ya mafunzo hayo kufungwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa hospitali hiyo, Prof. Charles Majinge. 

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Wateja Muhimbili, Aminiel Aligaesha akipokea cheti kutoka kwa Dkt. Bakari baada ya mafunzo hayo. 

KAIMU RAIS TCCIA AISHAURI SERIKALI KUTAMBUA MCHANGO KATIKA SEKTA BINAFSI KUKUZA UCHUMI

0
0

KAIMU Rais  wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Octavian Mshiu ameiyomba Serikali kutambua mchango  katika sekta binafsi (TPSF) katika kukuza uchumi wa nchi hususani katika suala la Biashara na masoko.

Aliyasema hayo jana Jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi habari mara baada ya kufanya mazungumzo na Mkurugenzi mtendaji wa TPSF, Dk. Geofrey Simbeye kuusu maadhimisho ya kutimiza miaka 30 ya kuazishwa kwa taasi ya TCCIA ambapo TPSF nao wataadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa.

Mshiu alisema serikali ya amwamu ya tano imekuwa ikitoa fursa za uwekezaji katika kampuni mbalimbali za nje ya nchi katika ujezi wa miundo mbinu hivyo kama wanaomba watambue taasisi hizo katika kukujenga uchumi ndani ya nchi.

“Watu wote tupo katika kuakikisha uchumi wa nchi yetu ianakuwa hivyo kama tukiwa na ushirikiano katika sekta binafsi na serikali lazima tutapata maendeleo,” alisema.
 Mkurugenzi wa TPSF Godfrey Siambeye kushoto akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano wa Biashara na kukuza uchumi wa wilaya, mkoa na Taifa, kulioa ni KAIMU Rais  wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Octavian Mshiu
Mkurugenzi wa TPSF Godfrey Siambeye kushoto, kulia ni KAIMU Rais  wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Octavian Mshiu wakipongeza mara baada ya mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano wa Biashara na kukuza uchumi wa wilaya, mkoa na Taifa.


WASIOWASILISHA MIKATABA KWA MWANASHERIA MKUU WAFANYe HIVYO HARAKA

0
0
Na Mwandishi Maalum, Dodoma.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Adelardus Kilangi, amezikumbusha  Wizara  na Taasisi  za Serikali ambazo bado hazijawasilisha mikataba ambayo imeombwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kwaajili ya  marejejo kufanya hivyo  mapema iwezekanavyo.

Ametoa wito huo siku ya  jumatano wiki  hii wakati wa hafla ya uzinduzi wa  Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka . Uzinduzi huo ulifanywa na Mhe.  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Kassim  Majaliwa  Jijini Dodoma.

Akielezea  Muundo  mpya wa Ofisi ya Mwanasheria  Mkuu  wa Serikali  kwa  Mhe. Waziri Mkuu na majukumu ambayo Ofisi hii imepanga kuyatekeleza. Mwanasheria Mkuu ameyataja  baadhi  hayo ni pamoja na   marejeo ( review) ya mikataba muhimu kwa lengo la kuhakikisha mikataba hiyo ina masharti yanayolinda maslahi ya  taifa.

“Tumepanga kufanya marejeo ya mikataba muhimu kwa lengo la kuhakikisha kuwa mikataba hiyo ina masharti yanayolinda maslahi ya taifa. Zoezi hili litahusisha mikataba yote ya kimataifa,  mikataba ya  uendelezaji  madini ( MDAs) na mikataba ya uzalishaji na mauzo ya gesi asilia”, ameeleza Mwanasheria Mkuu wa Serikali.Mikataba mingine itakayofanyiwa marejeo ni  mikataba inayohusu uwekezaji baina ya Tanzania na nchi nyingine pamoja na mikataba mingine ambayo Serikali ina maslahi.

“Mhe. Waziri Mkuu, ninaomba kutumia fursa hii kuzishukuru Wizara na Taasisi za Serikali kwa kuendelea kutupatia mikataba tunayoihitaji kufanyia marejeo. Kwa  Wizara na Taasisi ambazo  hazijawasilisha mikataba iliyoombwa, zinakumbushwa kufanya hivyo mapema ili shughuli hiyo ianze”.Pamoja na kufanya marejeo ya mikataba muhimu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema, Ofisi yake inapanga kuweka mfumo utakaokuwa na regista ya mikataba yote ya kimataifa ili iwe rahisi kuifanyia rejea au kupatikana pindi inapohitajika kwa matumizi mbalimbali ya kiserikali na kisheria.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Adelardus Kilangi akitoa maelezo ya muundo mpya ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali  na majukumu ya Ofisi hiyo kwa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa uzinduzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wakili Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka. Uzinduzi wa Ofisi hizo tatu ulifanywa na Waziri Mkuu siku ya Jumatano jijini  Dodoma ( picha na habari na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali) .

Wahasibu na Maafisa Tehama wa Wizara ya Habari, wanufaika na Mafunzo ya Ukusanyaji Maduhuli kieletroniki.

0
0

Mchambuzi Mkuu wa Mifumo ya Kompyuta kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bibi. Stella Nguma akifafanua jambo kwa Wahasibu na Maafisa Tehama wa Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo (hawapo katika picha) wakati wa mafunzo ya matumizi ya mfumo wa kieletroniki wa ukusanyaji maduhuli ya serikali (Government Eletroniki Payment Gateaway-GePG), leo Jijini Dodoma katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo.
Mchambuzi Mifumo ya Kompyuta kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Goodluck Mbano( aliyesimama),akitoa ufafanuzi kuhusu mfumo wa ukusanyaji wa maduhuli ya serikali kwa njia ya kieletroniki wakati wa mafunzo hayo kwa Wahasibu na Maafisa Tehama wa Wizara ya Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo leo Jijini Dodoma, katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo.
Wahasibu na Maafisa Tehama wa Wizara ya Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo ,wakifuatilia kwa makinimaelekezo yaliyokuwa yakitolewa wakati wa mafunzo ya matumizi ya mfumo wa kieletroniki wa ukusanyaji maduhuli ya serikali (Government Eletroniki Payment Gateaway-GePG) yaliyokuwa yakitolewa na wachambuzi wa mifumo kutoka Wizara ya Fedha na Mipango (hawapo katika picha), leo Jijini Dodoma katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo.(Picha na WHUSM).
Wahasibu na Maafisa Tehama wa Wizara ya Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo ,wakifuatilia kwa makinimaelekezo yaliyokuwa yakitolewa wakati wa mafunzo ya matumizi ya mfumo wa kieletroniki wa ukusanyaji maduhuli ya serikali (Government Eletroniki Payment Gateaway-GePG) yaliyokuwa yakitolewa na wachambuzi wa mifumo kutoka Wizara ya Fedha na Mipango (hawapo katika picha), leo Jijini Dodoma katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo.(Picha na WHUSM).

SPIKA AFUNGUA MAFUNZO YA KAMATI YA UNGOZI ZANZIBAR. MAASPIKA WASTAAFU WAHUDHURIA KUTOA MADA

0
0



Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai, akifungua mafunzo ya siku mbili kwa wajumbe wa Kamati ya Uongozi, Makamu Wenyeviti na Wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge yalioyoanza leo katika Ofisi Ndogo za Bunge Zanzibar.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai, akifurahi kwa pamoja na Maspika wastaafu Mhe. Anna makinda (wa kwanza kushoto) ,Spika Mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Mhe.Pandu Kificho, Mhe. Pius Msekwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zuber A Malulid, wa mwisho ni Naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia Ackson. Waheshimiwa Maspika wastaafu wamehudhuria mafunzo ya Kamati ya Uongozi, Makamu Wenyeviti na Wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge yalioyoanza leo katika Ofisi Ndogo za Bunge Zanzibar.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai, akiwa Katika picha ya pamoja washiriki wa mafunzo ambao ni Kamati ya Uongozi ya Bunge, Makamu Wenyeviti na Wajumbe wa Tume ya utumishi ya Bunge. waliokaa mbele wa kwanza ni Naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Spika Mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Pandu Kificho, Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zuber Ali Maulid, Spika Mstaafu Mhe. Anna Makinda, Spika Mstaafu Mhe. Pius Msekwa na Katibu wa Bunge Mhe. Stephen kagaigai. Mafunzo hayo yameanza leo katika Ofisi Ndogo za Bunge Zanzibar

VIONGOZI JIJI LA KAMPALA WAKIONGOZWA NA WAZIRI WAO WAJA KUJIFUNZA JIJINI DAR KWA JIJI LA DAR NAMNA LINAVYOSIMAMIA SHUGHULI ZAKE

0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MEYA wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amepokea ugeni wa viongozi mbalimbali wa Jiji la Kampala nchini Uganda wakiongozwa na Waziri wa Jiji hilo Bennie Namugwanya Bugembe ambao wamekuja kujifunza na kupata uzoefu wa kuendesha na kusimamia shughuli za Jiji.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Meya Mwita amesema anaamini viongozi hao kuna mambo mengi watajifunza kwa kipindi ambacho watakuwa katika Jiji hilo huku akiwahakikisha watapata kila wanachokitaka.

Mwita amesena kuna mambo mengi mazuri ambayo yanefanyika na yanaendelea kufanyika katika Jiji la Dar es Salaam hivyo viongozi hao wa Jiji la Kampala kuna mambo watajifunza kwa ajili ya kuliboresha Jiji lao huku akiwahimiza kibuni vyanzo vipya vya mapato ili fedha zitakazopatikana wazitumie kufanya maendeleo.

Amesema kuwa ni vema wakatambua Jiji la Dar es Salaam kupitia viongozi wake wa ngazi mbalimbali wamefanikiwa kutatua changamoto mbalimbali ikiwamo ya usafiri kwa kuanzisha huduma ya usafiri wa mabasi ya mwendo kasi pamoja na treni ya Jiji.

"Nafahamu kuna mambo mengi ya kujifunza kutoka Jiji la Dar es Salaam,hivyo niwaombe mtakapokuwa hapa kila ambacho mnataka kufahamu basi kuweni huru kuuliza watalaam na viongozi wetu ambao wapo tayari kutoa majibu.

" Tumeweka mfumo mzuri katika kukusanya kodi ni vema mkajifunza na mtakaporudi Kampala muweke mikakati ambayo itasaidia kuwaongezea mapato na hatimaye mtafanya maendeleo kwa ajili ya wananchi ambao wamewachagua,"amesema Mwita.


Baadhi ya viongozi wa Jiji la Kampala nchini Uganda wakiwa kwenye ofisi za Meya wa Jiji la Dar es Salaam ambao wamekuja kujifunza namna ya kusimamia shughuli za Jiji

Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita(kulia) akiwa na Waziri wa Jiji la Kampala nchini Uganda Bennie Namugwanya Bugembe ambaye yupo katika Jiji hilo kwa lengo la kujifunza na kubadilisha uzoefu wa kusimamia shughuli za Jiji


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

TRA YATOA ELIMU YA KODI KWA WASHIRIKI WA JUKWAA LA FURSA ZA BIASHARA GEITA

0
0
Na Veronica Kazimoto,Geita

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewaelimisha wafanyabiashara na wadau mbalimbali walioshiriki Jukwaa la Fursa za Biashara mkoani Geita na kuwafafanulia juu ya masuala mbalimbali yanayohusu kodi ikiwa ni pamoja na msamaha wa riba na adhabu kwenye malimbikizo ya madeni ya kodi. 

Akizungumza wakati akiwasilisha mada kuhusu kodi katika jukwaa hilo, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa mamlaka hiyo amewataka wafanyabiashara wenye malimbikizo ya madeni ya kodi na wale wote waliokuwa wakifanya biashara bila kusajiliwa kuchangamkia msamaha huo ipasavyo kwani hilo ni zoezi la miezi sita pekee.

"Nachukua fursa hii kutoa wito kwa wafanyabiashara wote wenye malimbikizo ya madeni ya kodi na wote waliokuwa wakifanya biashara bila kusajiliwa kuwasilisha maombi yao TRA ili waweze kupata msamaha huu wa riba na adhabu wa asilimia 100 ambapo mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 30 Novemba, 2018. 

Aidha, Mkurugenzi Kayombo amewahimiza wafanyabiashara wadogo waliopo kwenye utaratibu wa makadirio kusajiliwa na kupatiwa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) ambayo hutolewa na TRA bure bila ulazima wa kulipa kodi ya awamu ya kwanza kabla ya kuanza biashara isipokuwa ndani ya siku 90 baada ya kuanza biashara.

“Awali wafanyabiashara walikuwa wanalipa kodi mara tu baada kusajili biashara zao na kukadiriwa kodi, lakini sasa hivi tumeweka utaratibu wa kulipa kodi ndani ya siku 90 kwa awamu ya kwanza baada ya kusajiliwa na na kuanza biashara, alifafanua Kayombo.

Pamoja na mambo mengine, Kayombo amewakumbusha wafanyabiashara na washiriki wa jukwaa hilo la fursa za biashara suala zima la kutoa risiti za kielektroniki za EFD kila wanapouza bidhaa na huduma mbalimbali na kudai risti kila wanafanya manunuzi.

Vilevile, amewasisitiza wafanyabiashara wote wa Mkoa wa Geita na wilaya zake wenye changamoto mbalimbali wasisite kuonana na Meneja wa TRA mkoani humo kwa ajili ya kupata ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili ili waweze kufanya biashara zao kwa uhuru.

Jukwaa la Fursa za Biashara limeandaliwa na Ofisi ya Mkoa wa Geita kwa kushirikiana na Shirika la Magazeti ya Serikali (TSN) ambapo Mamlaka ya Mapato Tanzania imeshiriki jukwaa hilo kwa ajili ya kutoa elimu ya kodi kwa wafanyabiashara na wadau mbalimbali hususani wa mkoani hapa. 
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo akiwasilisha mada kuhusu kodi wakati wa Jukwaa la Fursa za Biashara linalomalizika leo mkoani Geita likiwa na lengo la kuibua fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo katika mkoa huo pamoja na changamoto mbalimbali kwa lengo la kupata ufumbuzi.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo akiwasilisha mada kuhusu kodi wakati wa Jukwaa la Fursa za Biashara linalomalizika leo mkoani Geita likiwa na lengo la kuibua fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo katika mkoa huo pamoja na changamoto mbalimbali kwa lengo la kupata ufumbuzi.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (aliyevaa kofia) akizungumza wakati alipotembelea banda la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakati wa maonyesho yaliyoambatana na Jukwaa la Fursa za Biashara linalomalizika leo mkoani Geita kwa lengo la kuibua fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo katika mkoa huo pamoja na changamoto mbalimbali kwa lengo la kupata ufumbuzi.


Article 4

MKUTANO WA KWANZA WA MWENYEKITI WA CHAMA CHA CUF PROF,LIPUMBA WAFANYIKA ZANZIBAR.

0
0


Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF anaetambuliwa na Msajili wa Vyama Pro,Ibrahim Haroun Lipumba akizungumza na wanachama wa chama hicho waliohudhuria katika Mkutano wake wa kwanza uliofanyika katika Ukumbi wa Baitul Yamiyn bwawani mjini Zanzibar.PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

Baadhi ya Wanachama wa chama cha Wananchi CUF waliohudhuria katika Mkutano wa Kwanza wa Mwenyekiti wa CUF anaetambuliwa na Msajili wa Vyama Pro,Ibrahim Haroun Lipumba uliofanyika katika Ukumbi wa Baitul Yamiyn bwawani mjini Zanzibar.

Baadhi ya Wanachama wa chama cha Wananchi CUF waliohudhuria katika Mkutano wa Kwanza wa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF anaetambuliwa na Msajili wa Vyama Pro,Ibrahim Haroun Lipumba uliofanyika katika Ukumbi wa Baitul Yamiyn bwawani mjini Zanzibar. 

DC HAI AAMURU KUKAMATWA KWA MWEKEZAJI SHAMBA LA KIBO AND KIKAFU ESTATE NA MWANASHERA WAKE.

0
0
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

MKUU wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya ameamuru kukamatwa na kuwekwa rumande kwa saa 48 Mkurugenzi wa Kampuni ya Tudi inayomiliki Shamba la Kibo and Kikafu Estate ,Jensen Natal pamoja na Manasheria wa kampuni hiyo,Edward Mroso.

mbali na kukamatwa kwa watu hao,Mkuu huyo wa wilaya ameamuru kushikiliwa kwa muda kwa Pasi ya kusafiria ya anayetajwa kuwa mwekezaji wa Shamba la Kibo and Kikau Estate,Trevor Robert kutokana na tuhuma za kukwepa kulipa kodi ya serikali inayokadiliwa kuwa Zaidi ya Sh Mil 700.
Askari Polisi wakiwa wamemshikilia ,Mkurugenzi wa Kampuni ya Tudeley Tanzania,Jensen Natal inayotajwa kukwepa kulipa kodi ya serikali kutokana na uwekezaji katika shamba la Kibo and Kikafu Estate,Natal amekamatwa kwa amri ya mkuu wa wilaya ya Hai.
Askari akimsindikiza Mwanasheria wa kampuni ya Tudeley Tanzania,Edward Mroso baada ya kukamatwa kwa amri ya Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya.
Mkurugenzi wa Kampuni ya TudeleyTanzania,Jensen Natal na Mwanasheria wa kampuni hiyo,Edward Mroso wakiwa kwenye gari la Polisi muda mfupi baada ya kukamatwa kwa amri ya Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya akiwa ameongozana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hiyo baada ya kutembelea Shamba la Kibo and Kikafu Estate.

MHASIBU CHUO CHA USTAWI WA JAMII AHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA MITANO

0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Aliyekuwa mhasibu wa Chuo cha ustawi wa Jamii, Gryson Mnyawami, amehukumiwa kwenda jela miaka mitano baada ya kupatikana na hata wizi wa zaidi ya sh. Milioni 9 akiwa mtumishi

Hukumu hiyo, imesomwa leo Agosti 15,2018 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Hakimu Mkazi Mkuu Janeth Mtega,

Akisoma hukumu hiyo, hakimu Mtega amesema upande wa mashtaka kupitia mashahidi wake watano wameweza kuthibitisha pasipo kuacha shaka kuwa mtuhumiwa ametenda kosa la wizi.Hata hivyo, kabla ya kusomwa kwa hukumu hiyo, Hakimu Mtega alitaka mwendesha mashtaka kusema kumbukumbu kama mshtakiwa anamakosa mengine au  La

Mwendesha Mashtaka, wakili wa Serikali Janeth Magoho ameieleza mahakama kuwa, hakuna kumbukumbu za makosa kwa mshtakiwa, hili ni kosa lake la kwanza.Mheshimiwa Hakimu, sina kumbukumbu za zamani za mshtakiwa, ila naomba mahakama kutoa adhabu kali kwa kuwa kitendo cha wizi alichofanya mshtakiwa haswa akiwa kama mtumishi wa umma ni kibaya, kinaitia hasara kubwa Serikali

Wakili Janet ameongeza, suala la wizi katika Chuo cha ustawi limekuwa likitokea mara kwa mara Kitendo cha yeye kudhulumu wanafunzi siyo haki kwani ile ni hela ya walipa kodi, adhabu kali itakuwa fundisho kwake na kwa wengine wenye tabia kama hiyo

Katika utetezi wake, mshtakiwa Mnyawami, ameiomba mahakama hiyo kumpunguzia adhabu, alikubali kulipa fedha hizo taratibu lakini taasisi ndiyo ilimkatalia,Ameongeza kuwa Dada yake ni mgonjwa na mama yake ni mjane na wote wanamtegemea yeye.

Awali ilidaiwa, May 31, 2014 katika Chuo cha ustawi wa jamii kilichopo Kijitonyama wilayani Kinondoni mtuhumiwa akiwa ameajiriwa kama mhasibu wa Chuo hicho aliiba sh, 9,714,000 Mali ya muajiriwa wake ambayo  ameipata kutokana na nafasi yake kazini hapo,

WAZIRI MKUU AAGIZA KUKAMATWA KWA MTENDAJI

0
0

*Ni baada ya upotevu wa sh. milioni 141 za kijiji

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Kamanda wa TAKUKURU wa wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Bw. Francis Zuakuu kumkamata aliyekuwa Mtendaji wa Kijiji cha Bulagamilwa, Bw. Ntemi James kwa tuhuma za kuhusika na upotevu wa sh. milioni 141 za kijiji hicho.

Ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Agosti 16, 2018) wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Igunga, akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Tabora.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo baada ya Mbunge wa Manonga, Bw. Seif Gulamali kumuomba awasaidie katika kulipatia ufumbuzi suala hilo la upotevu wa fedha za kijiji kwa kuwa ni la muda mrefu na hakuna hatua zilizochukuliwa.

Kutokana na malalamiko hayo Waziri Mkuu amemtaka kamanda wa TAKUKURU wa wilaya hiyo ahakikishe anawatafuta watu wote waliohusika na upotevu wa fedha hizo za kijiji akiwemo na alitekuwa mtendaji wa kijiji cha Bulagamilwa, ambaye kwa sasa ni Mtendaji wa kata ya Igurubi.

Katika hatua nyingine,Waziri Mkuu amewataka watumishi wa umma wilayani Igunga wahakikishe wanatimiza wajibu wao ipasavyo kwa kuwatumikia wananchi kwa weledi na ustadi bila ya ubaguzi wa aina yoyote.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga mkoani Tabora kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo, Agosti 16, 2018. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Igunga, John Mwaipopo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Baadhi ya watumishi wa Halmahauri ya wilaya ya Igunga wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao Kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo, Agosti 16, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga mkoani Tabora kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo, Agosti 16, 2018. 

Viewing all 109593 articles
Browse latest View live




Latest Images