Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110104 articles
Browse latest View live

ELIMU WALIYOYAPATA UFUGAJI KUKU ITAWASAIDIA:ULEGA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Naibu Waziri na Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa Jimbo la Abdallah Ulega amefunga mafunzo ya siku mbili ya ufugaji wa kuku kwa Baraza la  wakina mama wa Jimbo la Mkuranga Mkoa wa Pwani.

Mafunzo hayo yaliyoendeshwa na kampuni ya AMK Gliters inayojihusisha na ufugaji wa kuku yalianza jana yakihudhuriwa na jumla ya wakina mama 326 kutoka kata mbalimbali za Mkuranga.Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo, Ulega amesema kuwa anatarajia kuona wakina mama wa jimbo la Mkuranga wanafuga kuku kwa ajili ya maendeleo pamoja na kukuza kipato chao.

Ulega amesema kuwa, elimu waliyoipata ya ufugaji wa kuku wa kibiashara utawasaidia wananchi hao kujiendeleza zaidi kiuchumi na kuwapa hamasa kuwa majukwaa kama haya yana faida kubwa kwa maendeleo ya Mkuranga.

Amesema, mafunzo ya ujasiriamali  kama haya yanawezekana ila changamoto kubwa imekuwa ni kufika kwa wakina mama hao kutokana na umbali wanapokaa ila amewaomba wasikate tamaa na kumtaka Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Jimbo la Mkuranga Mariam Ulega  kutoa taarifa ili wadau mbalimbali wawezw kujitokeza kuwawezesha pindi zinapojitokeza.

Hata hivyo Ulega, amemtaka Mwenyekiti Wa Baraza kuhakikisha vikundi vilivyojiandikisha tayari kuwa na akaunti za benki ili kuwe na nidhamu ya fedha hususani  usimamizi mzuri.Ameongezea kuwa, tayari ameshapata cherehani 50 na majora kwa ajili ya kuwapatia wakina mama na kila kata watapata cherehani 2 ikiwa ni njia nyingine ya kujiinua kiuchumi.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, (Mb) wa Mkuranga,Abdallah Ulega akizungumza na wajasiria mali katika kongamano la uwezeshaji kiuchumi lililo fanyika mkoni Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akisalimiana na Meneja wa CRDB Bank Tawi la Mbagala, Midlaster Nsanzugwanko.
Sehemu ya wajasiliamali mara wakiendelea na kongamano lililo fanyika mkoa wa Pwani.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

WANAWAKE WAJASIRIAMALI WAPATIWA KUKU 4000 WILAYANI MKURANGA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, blogu ya jamii

WANAWAKE wajasiliamali wapatao 400 Wilayani Mkuranga wamepewa mafunzo na kuku wa kufuga ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuendeleza shughuli za kijasiriamali Wilayani humo.

Akiongea na vyombo vya habari Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga ameeleza kuwa hadi kufikia mwakani akina mama wa Mkuranga watakuwa mbali sana kutokana na ufugaji huo wa kuku hao ambao watainua uchumi wa familia zao.Aidha amewataka akina Mama wa Wilaya ya Mkuranga kutumia mradi huo vizuri ili kuleta maendeleo kwani wamebahatika sana.

Naye Mkurugenzi wa Wilaya ya Mkuranga Mhandisi Mshamu Munde amesema kuwa kuku hao ni kwa ajili ya ufugaji katika kujikwamua kiuchumi na sio zawadi na amewataka akina mama hao kutumia ujuzi kuendeleza ufugaji na kuwaelimisha wengine kuhusiana na mafunzo hayo.

Pia ameeleza kuwa wajasiriamali hao wamepokea kuku 1058 kati ya kuku 4000 waliohaidiwa na akina Mama 100 wamepata kuku 10 kwa kila mmoja.

Mwenyekiti wa jukwaa la wanawake jukwaa la Wilayani Mkuranga bi. Mariam Ulega kuku 4000 ambao watagaiwa kwa akina mama 400 watagaiwa kwa wanawake wajasariamali waliohudhuria katika mafunzo hayo.Ameeleza kuwa kwa hicho kidogo wakitumie katika kuleta maendeleo yao binafsi na taifa kwa ujumla, amewataka wawe na ushirikiano ili waweze kufikia malengo yao.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,Filberto Sanga akizungumza mbee ya Wanahabari (hawapo pichani),mapema leo kuhusu kupokea kuku kwa ajili ya Wajasiliamali Wanawake mkoa wa Pwani(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
Baadhi ya kuku waliopewa Wanawake wajasiliamai wilaya ya Mkuranga kwa ajili ya ufugaji
Baadhi ya Wanawae wa Wilaya ya Mkuranga wakiwahifadhi kuku wao katika matenga ya mbao,Wanawake 400 walipata kuku 10 kila mmoja kwa ajili wa mtaji wa kufuga kuku.

CHUO CHA DIPLOMASIA CHAFANYA ZIARA YA KIKAZI NCHINI INDIA

$
0
0
Chuo cha Diplomasia Tanzania (Center for Foreign Relation -CFR) wamefanya ziara ya kikazi nchini India kuanzia tarehe 13-15 Agosti 2018. 

Ziara hiyo imekuja kufuatia mwaliko wa Taasisi ya Mafunzo ya Kidiplomasia ya India (Foreign Service Institute-FSI), na ililenga kujua shughuli za FSI na taasisi zinazoshirikiana nazo, pamoja na kujadiliana juu ya uwezekano wa kuingia katika makubaliano ya ushirikiano. 

Wajumbe wa CFR waliongozwa na Balozi Ombeni Sefue, Katibu Mkuu Kiongozi (Mst.), ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya CFR. Wajumbe wengine walikuwa ni pamoja na Kaimu Mkuu wa cha Diplomasia (CFR), Dr Bernard Achiula, Dr Lucy Shule wa CFR, Dr Richard Mbunda kutoka UDSM, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia (DAA), Bibi Justa Nyange. Kutoka ubalozi wa Tanzania nchini India, alikuwepo Balozi Baraka Luvanda na Bibi Natihaika Msuya, Afisa Mambo ya Nje.

Aidha, wajumbe hao walipata fursa ya kutoa mihadhara katika Kituo cha Stadi za Masuala ya Afrika katika Chuo Kikuu cha Nehru, Taasisi ya Stadi za Masuala ya Ulinzi na Usalama (IDSA) pamoja na Taasisi ya Tafiti Mahususi kuhusu ushirikiano baina ya Nchi za Kusini (South Cooperation Research Information System-RIS).

Kwa ujumla, ziara hiyo imekuwa ya mafanikio makubwa ambapo taasisi wenyeji zimeonesha dhamira ya dhati ya kushirikiana na CFR katika kujenga uwezo wa wanadiplomasia wa Tanzania.
Balozi Ombeni Sefue akimkabidhi Mkuu wa Taasisi ya Stadi za Masuala ya Afrika, Profesa Ajay Dubey zawadi ya Kinyago. 

WAFANYABIASHARA KIGOMA WAIOMBA SERIKALI IONDOE GHARAMA ZA VIZA NA CHANJO MIPAKANI ILI KUKUZA BIASHARA

$
0
0
Wafanyabiashara Mkoani Kigoma wameiomba Serikali kuondoa gharama za Cheti cha Matibabu na utaratibu wa Viza kwa nchi ambazo hazipo katika Jumuiya ya Afrika mashariki hasa kwa wafanyabiashara wadogo ili kuchochea biashara kati ya Mkoa huo na nchi jirani zikiwemo Burundi na Congo.

Hayo yamebainishwa Mkoani Kigoma wakati wa Mkutano kati ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, na Wafanyabiashara wa mkoa huo uliowakutanisha pia Madiwani wa Kigoma Ujiji na Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe na viongozi wengine.

Katibu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara mkoani Kigoma, Bw. Raymond Ndabhiyegetse, alisema kuwa Serikali imeweka gharama ya Viza ya Dola 50 na Dola 10 kwa ajili ya cheti cha chanjo kwa nchi ambazo si wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki jambo ambalo limekuwa kikwazo kwa wafanyabiashara wadogo ambao ndio waliokuwa chachu ya biashara mkoani Kigoma.

“Waliobaki katika biashara ni wafanyabiashara wakubwa ambao hununua bidhaa za jumla kutoka viwandani na kusababisha wafanyabiashara wadogo wa mkoa wa Kigoma kutonufaika na kusababisha mzunguko wa pesa na biashara kuwa mdogo ikilinganishwa na kipindi ambacho hakukuwa na masharti ya kulipia viza na chanjo”, alisema Bw. Ndabhiyegetse.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa pili kulia), akiwaeleza wafanyabiashara wa Manispaa ya Kigoma Ujiji umuhimu wa kutoa lisiti na kulipa kodi, wakati changaoto za biashara na nchi jirani zikitatuliwa, alipofanya Mkutano na wafanyabiashara wa Manispaa hiyo Mkoani Kigoma, wa pili kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Bw. Rashid Kassim Mchatta na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Bi. Mwanamvua Mlindoko.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa pili kulia), akiwaeleza wafanyabiashara wa Manispaa ya Kigoma Ujiji umuhimu wa kutoa lisiti na kulipa kodi, wakati changaoto za biashara na nchi jirani zikitatuliwa, alipofanya Mkutano na wafanyabiashara wa Manispaa hiyo Mkoani Kigoma, wa pili kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Bw. Rashid Kassim Mchatta na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Bi. Mwanamvua Mlindoko.
Kamishna wa Mamlaka ya Udhibiti wa Bima nchini (TIRA) Bw. Baghayo Saqware, akitoa elimu kwa wafanyabiashara wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Mkoani Kigoma kuhusu umuhimu wa Bima wakati wa Mkutano kati ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) na wafanyabiashara hao.
Mbunge wa Kigoma Mjini Mhe. Zito Kabwe, akitoa ufafanuzi kuhusu baadhi ya Kodi zinazotozwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji wakati wa Mkutano kati ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa pili kushoto) na wafanyabiashara wa Manispaa hiyo.


WABADHILIFU MALI ZA MAGEREZA KUKIONA

$
0
0

Na Deodatus Kazinja

Maafisa na askari wa Jeshi la Magereza nchini wametakiwa kuacha mara moja tabia ya kujinufaisha na mali za Jeshi hilo kinyume na utaratibu.

Hayo yalisemwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo Phaustine Kasike wakati akizungumza na maafisa na askari wa gereza Mpwapwa na Kongwa kwa nyakati tofauti alipofanya ziara ya kikazi katika vituo hivyo Agosti 14 mwaka huu.

Kamishna Kasike alisema si jambo la kificho kukuta shamba, mifugo na mali nyinginezo za gereza zinamilikiwa na kuendeshwa na mkuu wa gereza kama mali yake binafsi.

Mkuu huyo wa magereza nchini akionesha kukasirika alisema siyo siri kukuta shamba la mkuu wa gereza au mkuu wa magereza wa mkoa likiwa limestawi huku shamba la serikali limesinyaa kabisa kwa visingizio vya hali ya hewa wakati vyote viko sehemu moja na vinatumia nguvu kazi ya wafungwa na raslimali nyinginezo hizo hizo za serikali.

“Nawataka maafisa na askari ndani ya Jeshi la Magereza kutambua kuwa tabia za namna hii ndizo zimesababisha Jeshi letu kutosonga mbele. Tunatazamwa kama watu tulioshindwa kutimiza wajibu wetu kwa tabia zetu za udokozi, wizi na ubinafsi na tunaoweza kurekebisha hali hii ni sisi wenyewe” alisema Kamishna Kasike.

Akitolea mfano wa mifugo kama ng’ombe na mbuzi Jenerali Kasike alisema ni jambo la kawaida kukuta kituo kiko na idadi hiyo hiyo ya mifugo kwa miaka kadhaa bila kuongezeka mfugo hata mmoja na ikiwa kuna mabadiliko ni ya kupungua tena kwasababu ambazo hazina mashiko.

Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (katikati) akikagua moja ya nyumba zinazojengwa kwa mtindo wa kujitolea gerezani Mpwapwa. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP) Salum Omari na wa kwanza kushoto ni mkuu wa Gereza Mpwapwa Mrakibu Mwandamizi wa Magereza (SSP) Nobert Ntacho. 
Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (mwenye miwani) akikagua mradi wa ufyatuaji tofali kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za kuishi maafisa na askari kwa njia ya kujitolea. 
Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (wa kwanza kulia) akikagua shamba la mikorosho la gereza Mpwapwa alipofanya ziara ya kikazi gerezani hapo Agosti 13 mwaka huu. Shamba hilo lina ukubwa wa ekari 58 na kati ya hizo ekari 15 tayari zimeanza kutoa matunda. Kwa msimu wa mwaka 2017/18 zaidi ya kilo 2400 zilipatikana. 
Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike akisalimiana na maafisa wa gereza Mpwapwa mkoani Dodoma alipowasili kituoni hapo kwa ziara ya kikazi Agosti 14,2018. 
Baadhi ya maafisa wa gereza Kongwa mkoani Dodoma wakifuatilia kwa makini hotuba ya Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (hayupo  pichani) alipofanya ziara ya kikazi kituoni hapo Agosti 14, 2018. 
Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (katikati) akiongea na baadhi ya maafisa gereza Kongwa (hawapo pichani) alipofanya ziara ya kikazi kituoni hapo Agosti 14, 2018.Wa pili kushoto ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP) Salum Omari. Wa kwanza kushoto ni Afisa Mnadhimu katika ofisi ya Mkuu wa Magereza mkoani Dodoma Kamishna Msaidizi wa Magereza Mwaruka Dugange, wa pili kulia ni Mkuu wa gereza Kongwa Mrakibu wa Magereza John Nyonyi na wa kwanza kulia ni Mkuu wa Kambi Mkoka Mrakibu wa Magereza Felix Samson. 

WAZIRI MKUU MAJALIWA AZINDUA OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI, WAKILI MKUU WA SERIKALI NA OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA JIJINI DODOMA

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua Ofisi ya Mwanansheria Mkuu wa Serikiali, Wakili Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka jijini Dodoma Agosti 15, 2018. Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi, Meya wa Jiji la Dodoma, Profesa Devis Mwamfupe, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde, Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi, Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Adelardus Kilangi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria , Profesa Sifuni Mchome, Mkurugenzi wa Mshtaka, Biswalo Mganga na kulia ni Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Posi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi walioshirki katika uzinduzi wa Ofisi za Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wakili Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka jijini Dodoma, Agosti 15, 2018. Waliokaa wanne kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi na watatu kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde. Watatu kulia ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Adelardus Kilangi na wanne kulia ni Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi wakati alipowasili kwenye eneo la uzinduzi wa Ofisi ya Mwanansheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Jijini Dodoma, Agosti 15, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa, Paramagamba Kabudi (kushoto), Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde (wapili kushoto) na Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama vitabu wakati alipotembelea maktaba ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wakili Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka aliyoizindua jijini Dodoma, Agosti 15, 2018. Kulia ni Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

SERIKALI YAWATAKA WATANZANIA KUACHA MIGOGORO KATIKA UBIA WA UWEKEZAJI

$
0
0
Na Zuena Msuya, Kilimanjaro , 

Serikali imewataka Watanzania kuepuka migogoro katika maeno ya migodi hasa inayomilikiwa Kwa ubia na wawekezaji wazawa ili kuondoa taswira mbaya kwa wawekezaji kutoka Matifa mengine yanayokuja nchini kwa lengo la kuwekeza badala yake waungane kuweka mazingira mazuri na rafiki ya kuvutia wawekezaji hao kuwekeza nchini .

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko wakati wa ziara yake mkoani Kilimanjaro alipotembelea mgodi wa Madini wa Mega unaochimba madini ya shaba .( Mega Copper Company) uliopo katika Kijiji cha Chang`ombe wilayani Mwanga Mkoani Kilimanjaro, Kwan lengo la kumaliza mgogoro uliopo katika mgodi huo unachimba na kuchenjua madini ya Shaba.

Mgodi huo wa madini ya Shaba unaomilikiwa na Watanzania umekuwa katika migogoro ya kutoelewana wenyewe kwa wenyewe kwa zaidi ya miaka 10 sasa, Licha kumepiga hatau katika uchenjuaji wa shaba na kwamba hausafirishi madini ghafi nje ya nchi kama serikali ilivyoagiza.

Kwa mantiki hiyo, Biteko alisisitiza kuwa migogoro haipaswi kupewa nafasi na inarudisha nyuma maendeleo ya watanzania na kuleta taswira mbaya ya Uwekezaji Tanzania katika Mataifa mengine Duniani Kwani kusengskuwa na mgogoro katika mgodi huo wangekuwa wamepiga hatua zaidi kwa manufaa yao na Taifa kwa jumla.

Biteko alisema “migogoro miongoni ya wabia hasa wazawa haipaswi kufumbiwa macho na mtu yeyote Yule, ambapo alishauri kuwa kama watu, au kikundi wameingia makubaliano ya pamoja katika kuendeleza mgodi au jambo fulani basi, makubaliano hayo yapelekwe Wizara ya madini au katika mamlaka husika yasajiliwe kuepusha migogoro.
Naibu waziri wa madini, Dotto Biteko, akikagua uchimbaji sehemu ya hatua inapopitishwa Mbale ya shaba kabla ya kupatikana shaba halisi. 
Naibu Waziri wa madini, Dotto Biteko, akizungumza na akina mama wanaofanya kazi katika mgodi wa shaba wa Mega. 

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AWASILI NAMIBIA KUMWAKILISHA RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI KATIKA MKUTANO WA 38 WA SADC.

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili  Mjini Windhoek Namibia leo Agosti 15, 2018 kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katikaMkutano wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), utakaofanyika tarehe 17 – 18 Agosti 2018.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hosea Kutako mjini Windhoek Namibia, Makamu wa Rais amepokelewa na  Waziri wa Elimu ya Juu , Mafunzo na Ubunifu wa Namibia Mhe. Dkt. Itah Kandjii – Murangi , Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Christin Hoebes na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Namibia.

Hii ni sehemu ya mikutano ya awali ya maandalizi ya mkutano wa 18 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC utakaofanyika tarehe 17 na 18 Agosti 2018 mjini Windhoek, Namibia. 

Mikutano mingine ya awali ni pamoja na mkutano wa Makatibu Wakuu wa SADC uliofanyika tarehe 9 na 11 Agosti 2018 na Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa , Ulinzi na Usalama ya SADC (SADC Organ on Politics, Defence and Security) utakaofanyika tarehe 16 Agosti 2018 ambao utapitia na kujadili hali ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Kanda kwa kipindi cha Agosti 2017 hadi Agosti 2018. 

Mkutano huu utahusisha nchi tatu za SADC Organ TROIKA na wajumbe wake ambao ni Angola Mwenyekiti wa sasa wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama, Zambia ambao ni Makamu Mwenyekiti wa Organ na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ni Mwenyekiti wa Organ aliyemaliza muda wa uenyekiti wa Asasi hiyo. 
  Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akilakiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Christine Hoebes alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Hosea Kutako mjini Windhoek Namibia tayari kwa mkutano wa 38 wa SADC akimwalikilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli 
 Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akilakiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga  alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Hosea Kutako mjini Windhoek Namibia tayari kwa mkutano wa 38 wa SADC akimwalikilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli  
  Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa ameongozana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Christine Hoebes mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Hosea Kutako mjini Windhoek Namibia tayari kwa mkutano wa 38 wa SADC akimwalikilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli .




UJUMBE WA CRDB WAFANYA ZIARA TUME YA MADINI

$
0
0
Jana tarehe 14 Agosti, 2018 ujumbe kutoka CRDB ukiongozwa na Mkurugenzi wake Dk. Charles Kimei ulifanya ziara katika Ofisi za Tume ya Madini zilizopo jijini Dodoma lengo likiwa ni kufahamu majukumu na shughuli za Tume.
Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia) akibadilishana mawazo na Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya (kushoto) kwenye Ofisi za Tume ya Madini zilizopo jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia) akifafanua jambo kwenye kikao kilichoshirikisha ujumbe wake na Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya
Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya akifafanua jambo

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

JESHI LA POLISI LAWATAKA WANANCHI WILAYANI MISUNGWI MKOANI MWANZA KUTOA USHIRIKIANO KUHUSU UHALIFU UNAOENDELEA MAENEO HAYO

$
0
0

Mkuu Wa Operesheni Maalum za Jeshi La Polisi, Naibu Kamishna (DCP) Liberates Sabas, akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Kijiji cha Nyamayinza, Tarafa ya Inonelwa, Kata Gulumangu ya, Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza kuhusu kushirikiana na Jeshi la Polisi kwaajili ya kukabiliana na mauaji ya wanawake yanayotokana na imani za kishirikina yaliyotokea maeneo hayo siku za hivi karibuni. (Picha na Jeshi la Polisi).

Mkuu Wa Operesheni Maalum za Jeshi La Polisi, Naibu Kamishna (DCP) Liberates Sabas, akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Kijiji cha Nyamayinza, Tarafa ya Inonelwa, Kata Gulumangu ya, Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza kuhusu kushirikiana na Jeshi la Polisi kwaajili ya kukabiliana na mauaji ya wanawake yanayotokana na imani za kishirikina yaliyotokea maeneo hayo siku za hivi karibuni. (Picha na Jeshi la Polisi).
Mkuu Wa Operesheni Maalum za Jeshi La Polisi, Naibu Kamishna (DCP) Liberates Sabas, akizungumza na viongozi wa serikali za Mtaa na Kata katika Kijiji cha Lubili, Kata ya Lubili,Tarafa ya Mbarika wilayani Misungwi Mkoa wa Mwanza kuhusu kushirikiana na Jeshi la Polisi kwaajili ya kukabiliana na mauaji ya wanawake yanayotokana na imani za kishirikina yaliyotokea maeneo hayo siku za hivi karibuni. (Picha na Jeshi la Polisi).
Mkuu Wa Operesheni Maalum za Jeshi La Polisi, Naibu Kamishna (DCP) Liberates Sabas, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Serikali za Mtaa na Kata katika Kijiji cha Lubili, Kata ya Lubili, Tarafa ya Mbarika wilayani Misungwi Mkoa wa Mwanza baada ya kumaliza kikao.

PROFESA KABUDI ATEMA CHECHE DODOMA

$
0
0

Akerwa na maamuzi kufanyika bila Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kuarifiwa .Asema Wizara yake imeamua kubadili taswira ya Ofisi yake 

WAZIRI wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi amesema kuanzia sasa mawakili walioko kwenye Ofisi ya Mwanasheria Mkuu na wanasheria wote katika Wizara, Mamlaka za Serikali za Mitaa na taasisi za Serikali watakuwa ni Mawakili wa Serikali. 

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumatano, Agosti 15, 2018) kabla hajamkaribisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ahutubie wageni waliohudhuria uzinduzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali jijini Dodoma. 

“Kwa miaka mingi kumekuwa na ombwe la usimamizi wa wanasheria walio kwenye utumishi wa umma. Maamuzi mengi yamekuwa yakifanyika pasipo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kuwa na taarifa. Mambo yanapoharibika ndio Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inataarifiwa ili kuokoa jahazi,” alisema. 

Alisema hali hiyo kwa miaka mingi imekuwa ikiisababishia Serikali kuingia kwenye migogoro na kuingia hasara. “Baada ya mabadiliko haya, wanasheria wote walioajiriwa katika utumishi wa umma wanakuwa wanafanya kazi na kutumia mamlaka ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ndani ya wizara zao, taasisi zinazojitegemea na Mamlaka za Serikali za Mitaa,” alisema. 

“Vilevile wanasheria hao watakuwa chini ya uangalizi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Nia ya mabadiliko haya ni kumuwezesha Mwanasheria Mkuu wa Serikali awe na usimamizi juu yao na kuwazuia kufanya kazi bila kufuata maelekezo ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.” 

NJIA ZA UZAZI WA MPANGO ZATAJWA KUWA NA MANUFAA MAKUBWA KATIKA MAISHA YA BINADAMU

WAZIRI MWAKYEMBE AELEZA MASHARTI YALIYOKIUKWA NA AZAM,ZUKU,DSTV

TANZANIA YANG'ARA KONGAMANO LA WATAALAMU MAGONJWA YA DAMU (HAEMATOLOGY) BARA LA AFRIKA

$
0
0
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 

Tanzania imeng'ara kwa nchi za Afrika kwa kuwa nchi pekee ya kwanza kuandaa kongamano linalowakutanisha wataalam wa magonjwa ya damu (Haematology) kutoka mataifa mbalimbali duniani. Hayo yamezungumzwa na jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Damu (Haematology), MUHAS Prof. Julie Makani wakati akielezea mafanikio ya kongamano la wataalam wa magonjwa ya damu (Haematology) linalokutanisha watalaam wa Tanzania na mataifa mbalimbali duniani ikiwemo Bara la Afrika. 

"Nitoe pongezi kwa serikali na Rais Dkt. John Magufuli kwa kuendelea kuwekeza zaidi katika sekta ya afya na ndiyo maana kila kukicha kunakuwa na mabadiliko yanayopelekea kutokea matokeo chanya, wagonjwa badala ya kukimbilia nje ya nchi wanapata matibabu ndani" amesema Prof. Makani. 

Kongamano hilo lililoandaliwa na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) na Mfuko wa Kimataifa kusaidia masuala ya elimu Menarini (Fondazione Internazionale Menarini) la nchini Italia, ambalo limeweza kuwakutanisha madaktari bingwa ikiwemo watoa huduma ya magonjwa ya damu (Haematology) takribani nchi zipatazo 15 barani Afrika wanaojadili changamoto wanazokumbana wakati wa utoaji wa huduma ya magonjwa ya damu (Haematology). 

Aidha Prof. Makani amesema kuwa mpaka sasa Tanzania imeweza kujitahidi kufanya jitihada za kipekee katika utoaji wa huduma japo changamoto inayowakumba ni uhaba wa wataalam zaidi wanaopenda kusomea utoaji wa huduma ya magonjwa ya damu (Haematology). 
Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Damu (Haematology), MUHAS Prof. Julie Makani (kulia) akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam kuelezea mafanikio ya kongamano la kwanza la wataalam wa magonjwa ya damu (Haematology) linalokutanisha watalaam wa Tanzania na Bara la Afrika kwa ujumla. Pembeni yake ni Msimamizi wa Mafunzo hayo Prof. Lucio Luzzatto. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
 Msimamizi wa Mafunzo ya Wataalam wa magonjwa ya damu (Haematology) Prof. Lucio Luzzatto akionyesha chembe chembe zinazosababisha upungufu wa tamu mwilini wakati wakizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam. 
Wataalam wa magonjwa ya damu (Haematology) kutoka mataifa mbalimbali duniani ikiwemo bara la Afrika wakiwa katika sherehe ya kukaribishwa nchini Tanzania. 


SONGWE KAMILISHENI UJENZI KWA WAKAT-NAIBU WAZIRI KWANDIKWA

$
0
0

Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias John Kwandikwa amemtaka mkandarasi China Geo- Engineering Corporation aneayejenga barabara ya Mpemba-Isongole KM 50.3 kwa kiwango cha lami kuongeza kasi ya ujenzi ili barabara hiyo ikamilike kwa muda uliopangwa. 

Amemtaka mkandarasi huyo kuongeza vifaa, wafanyakazi ili ujenzi wake ugawanywe sehemu mbili na hivyo kuwezesha ujenzi huo kukamilika ifikapo mwezi Agosti mwakani. “Kutokana na umuhimu wa barabara hii kwa uchumi wa mkoa wa Songwe hakikisheni inakamilika ili kufungua uchumi wa Wilaya ya Ileje na mkoa wa Songwe kwa ujumla”, amesema Mhe, Kwandikwa.

Barabara hiyo ambayo inaunganisha Tanzania na Malawi kupitia mto Songwe itachochea huduma za uchukuzi na kurahisisha usafiri kwa wakazi wa wilaya ya Ileje mkoani Songwe.

Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Mkoa wa Songwe mhandisi Yohana Kasaini amesema barabara hiyo inahusisha ujenzi wa madaraja makubwa manne, ya kati 14 na madogo 172, imesanifiwa kubeba magari ya aina zote na itagharimu zaidi ya shilingi bilioni 107 itakapokamilika.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Kwandikwa amekagua ujenzi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Songwe na hospitali ya Tunduma zinazojengwa na Wakala wa Majengo Nchini (TBA),mkoani Songwe na kumtaka kaimu meneja wa TBA mkoani humo msanifu majengo Christine Shayo kuhakikisha ujenzi huo licha ya kutoa fursa za ajira kwa wakazi wa maeneo hayo pia ukamilike kwa wakati na ubora uliokusudiwa.

Zaidi ya kilomita 3,856 za barabara nchini zitasanifiwa ili kujengwa kwa lami katika mwaka wa fedha 2018/2019

IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO. 

Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias John Kwandikwa akisisitiza jambo kwa wataalam wa mkandarasi China Geo-Engineering Corporation anayejenga barabara ya Mpemba-Isongole kwa kiwango cha lami alipokagua barabara hiyo.

Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias John Kwandikwa akisisitiza jambo kwa Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo nchini TBA mkoani Songwe msanifu majengo Christine Shayo, wakati wa ukaguzi wa shughuli za TBA mkoani Songwe . 
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Songwe inayojengwa na Wakala wa Majengo Nchini TBA mkoa wa Songwe. 
Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias John Kwandikwa akisisitiza jambo kwa wataalam wa mkandarasi China Geo-Engineering Corporation anayejenga barabara ya Mpemba-Isongole kwa kiwango cha lami alipokagua barabara hiyo. 

WANAFUNZI WAZURU UBALOZI WA OMAN

$
0
0
Na Salum Vuai, ZANZIBAR 

JUKUMU la mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao katika mataifa ya nje, ni kuwaunganisha wananchi na sio kuwa karibu na serikali na viongozi pekee.

Kauli hiyo imetolewa na Balozi mdogo wa Oman aliyepo Zanzibar Dk. Ahmad Hamood Al Habsy, alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu wanaosomea diplomasia na uhusiano wa kimataifa walipomtembelea ofisini kwake Migombani mjini Unguja.

Balozi huyo alieleza kuwa, kwa kutambua hilo, amefungua milango ya ofisi yake kutoa fursa kwa wananchi mbalimbali wa Zanzibar pamoja na viongozi, kwenda kujifunza masuala muhimu kwa lengo la kuimarisha mahusiano ya kihistoria kati ya nchi yao na Oman.

Alisema, baadhi ya watu wanadhani kwamba kufanya kazi katika ofisi za kibalozi kuna mipaka inayowatenganisha mabalozi na wananchi wa kawaida, jambo alilosema sio sahihi.

Dk. Al Habsy alisema licha ya mabalozi kuwajibika kiserikali katika mataifa wanayopelekwa kufanya kazi, pia wanapaswa kuwa karibu na wananchi wa nchi za nje wanazokuweko, wakitambua kuwa nayo ni sehemu ya majukumu yao. 
BALOZI Mdogo wa Oman anayefanya kazi zake Zanzibar Dk. Ahmad Hamood Al Habsy (Kulia), akizungumza na wanafunzi wanaosomea fani ya Diplomasia na Mahusiano ya Kimataifa, wakati walipofanya ziara kwenye ofisi za ubalozi huo zilizopo Migombani mjini Zanzibar.
DK. Ahmed Hamood Al Habsy, Balozi Mdogo wa Oman visiwani Zanzigar (Kulia) na Mhadhiri wa somo la Diplomasia na Mahusiano ya Kimataifa katika Chuo Kikuu Zanzibar kilichoko Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja, Mohammed Yussuf.
WANAFUNZI, wahadhiri na baadhi ya maofisa wa Ubalozi Mdogo wa Oman mjini Zanzibar, wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mdogo Dk. Ahmad Hamood Al Habsy nje ya jengo la ubalozi huo Migombani, Zanzibar baada ya ziara ya wanafunzi hao iliyolenga kubadilishana mawazo na kujifunza shughuli za Kidiplomasia na Mahusiano ya Kimataifa. (PICHA ZOTE NA HAROUB HUSSEIN). 

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII,MHE.HASUNGA ATAKA USHIRIKISHWAJI KWENYE UHIFADHI

$
0
0
NA LUSUNGU HELELA - MANYARA 

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amewaagiza Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Taasisi zake kuwashirikisha viongozi wa mikoa na wa wilaya wakati wanapokwenda katika maeneo yao kwa ajili ya kushughulikia migogoro ardhi kati ya Hifadhi na wananchi. 

"Nasema ni marufuku kwa Watumishi wa Wizara yangu kwenda kwenye maeneo ya Hifadhi bila kushirikisha uongozi wa eneo husika kwa jambo lolote litalohusisha wananchi na Hifadhi" amesema Mhe.Hasunga. 

Aliyasema hayo jana kwenye mkutano mkoani Manyara kabla ya kumkaribisha Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.William Lukuvi kwa ajili ya kuzindua utekelezaji wa mpango na matumizi bora ya ardhi ya vijiji vinavyopakana na Hifadhi utakaotekelezwa na Hifadhi za Taifa Tanzania kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi. 

Mpango huo una lengo la kutatua migogoro ya ardhi kati ya wananchi na Hifadhi utakaoshirikisha mikoa mitano ya Manyara,Dodoma,Mara,Arusha na Simiyu kwenye vijiji vinavyozunguka Hifadhi. 

Naibu Waziri, Mhe. Hasunga alitaja mikoa itakayoanza kunufaika na mpango huo kwa awamu ya kwanza kuwa ni Manyara, Arusha na Mara yenye jumla ya vijiji 95 kati ya vijiji 392 vilivyolengwa nchi nzima. 
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza na wajumbe kwenye mkutano wa uzinduzi wa utekelezaji wa mpango na matumizi bora ya ardhi na vijiji vinavyopakana na Hifadhi unaotekelezwa na Hifadhi za Taifa Tanzania kwa kushirikiana na tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi kwenye mkutano uliofanyika jana mkoani Manyara -liowashirikisha wakurugenzi na wakuu wa wilaya watakaonufaika na mpango huo. 

 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akizungumza na wajumbe wakati wa uzinduzi wa utekelezaji wa mpango na matumizi bora ya ardhi na vijiji vinavyopakana na Hifadhi unaotekelezwa na Hifadhi za Taifa Tanzania kwa kushirikiana na tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi kwenye mkutano uliofanyika jana mkoani Manyara uliowashikisha wakurugenzi na wakuu wa wilaya watakaonufaika na mpango huo. 

 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ( wa kwanza kulia) akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti (katikati) mara baada ya kufanyika mkutano wa uzinduzi wa utekelezaji wa mpango na matumizi bora ya ardhi na vijiji vinavyopakana na Hifadhi unaotekelezwa na Hifadhi za Taifa Tanzania kwa kushirikiana na tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi kwenye mkutano uliofanyika jana mkoani Manyara uliowashirikisha wakurugenzi na wakuu wa wilaya watakaonufaika na mpango huo. Wa tatu kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Tanzania, Martin Leibook.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (katikati) pamoja na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ( wa pili kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufanyika mkutano wa uzinduzi wa utekelezaji wa mpango na matumizi bora ya ardhi na vijiji vinavyopakana na Hifadhi unaotekelezwa na Hifadhi za Taifa Tanzania kwa kushirikiana na tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi kwenye mkutano uliofanyika jana mkoani Manyara uliowashirikisha wakurugenzi na wakuu wa wilaya watakaonufaika na mpango huo. 

TAARIFA KWA UMMA: KUANZA KWA MFUKO PSSSF NA HUDUMA ZA MIFUKO YA PENSHENI ILIYOUNGANISHWA

$
0
0
Mnamo Tarehe 1 Agosti, 2018 Sheria Na. 2 ya 2018 inayounda Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) ilianza rasmi kutumika kwa mujibu wa Tangazo la Serikali Na. 375 la Tarehe 27 Julai, 2018. Sheria hii pamoja na mambo mengine inaunganisha Mifuko ya Pensheni minne (4) ambayo ni Mfuko wa PSPF, LAPF, PPF na GEPF. Kufuatia hatua hii, Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) inapenda kutoa ufafanuzi katika maeneo yafuatayo:-

1.0.Kwa mujibu wa Sheria ya PSSSF Rasilimali, Mikataba iliyoingiwa na Mifuko iliyounganishwa, Mifuko ya hiari, Madeni, Rasilimali, vitega uchumi, Ofisi pamoja na akaunti za Benki za Mifuko iliyounganishwa sasa zipo chini ya Mfuko wa PSSSF.  Hivyo:- 

(i)Waajiri wote wataendelea kuwachangia wanachama/wafanyakazi wao kupitia akaunti za Benki za Mifuko iliyounganishwa hadi hapo Mfuko wa PSSSF utakapotoa maelekezo mengine.

(ii)Uandikishwaji wa wanachama wapya wanaopaswa kusajiliwa katika Mfuko wa PSSSF utaendelea kufanyika kupitia Ofisi za Mifuko iliyounganishwa hadi hapo Mfuko wa PSSSF utakapotoa maelekezo mengine.

(iii)Wanachama, Wastaafu, Wategemezi, na wadau wengine wataendelea kupata huduma zao katika Ofisi ambazo wamekuwa wakihudumiwa siku zote hadi hapo Mfuko wa PSSSF utakapotoa maelekezo mengine.

2.0.Tunapenda kuwaondoa wasiwasi Wanachama, Waajiri na Wadau wote wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii kwamba huduma zote za Hifadhi ya Jamii zilizokuwa zikitolewa na Mifuko iliyounganishwa zinaendelea kutolewa kama kawaida katika Ofisi zile zile. Endapo utahitajika ufafanuzi zaidi tafadhali wasiliana na Mamlaka (SSRA).

Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano
Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii
S.L.P 31846
Tovuti: www.ssra.go.tz
DAR ES SALAAM
09/08/2018

MATUKIO KATIKA PICHA JUKWAA LA FURSA NA BIASHARA LINALOENDELEA MKAONI GEITA

$
0
0

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe akitizama mvinyo uitwao (Perfect Wine) iliyoandaliwa kwa matunda ya nanasi iliyotengenzwa na kikundi cha Cris Food Products wa mkoani Geita alipokuwa akitembelea mabanda ya wafanyabiashara waliyoshiriki Jukwaa la Fursa za Biashara leo katika viwanja vya Gadeco,ambapo jukwaa hilo limeandaliwa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) (pembeni kushoto) ni Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe (wa kwanza kulia) akifurahia jambo na wenzake mara baada ya kupewa magazeti ya Habari Leo na Dailynews kutoka Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) alipokuwa akitembelea mabanda ya wafanyabiashara waliyoshiriki maonesho ya Jukwaa la Fursa za Biashara lililoandaliwa na (TSN) leo mkoani Geita katika viwanja vya Gadeco (wakwanza kushoto) ni Msemaji Mkuu wa Serikali Tanzania Dkt.Hassan Abbas na wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe (wa kwanza kulia) akizungumza na watendaji wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhusu kusaidia wadau wa sekta ya filamu mkoa wa Geita kupatiwa Stika za TRA katika ofisi ya TRA mkoani hapo badala ya wasanii hao kulazimika kwenda mpaka ofisi za Dar es Salaam alipowatembea katika banda lao la Maonesho ya Jukwaa la Fursa za Biashara katika viwanja vya Gadeco,wakwanza kulia ni Mkurugenzi wa Huduma na Elimu ya Mlipa Kodi Bw.Richard Kayombo na katikati ni Meneja wa Ofisi ya TRA Mkoa wa Geita James Jilala.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe (wa kwanza kulia)akionyeshwa asali iliyopitishwa katika viwango vya kimataifa inayozalishwa katika wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita na mmoja wa wajasiriamali ambaye jina lake halikutambulika kwa harakaalipotembelea mabanda ya Maonesho ya wadau waliyoshiriki Jukwaa la Fursa za Biashara lililoandaliwa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN).
Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye pia ni Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya TSN Dkt.Hassan Abbas akitizama bidhaa za wajasiriamali waliyoshiriki Jukwaa la Biashara linalofanyika leo Mkoani Geita lililoandaliwa na (TSN ) katika maonesho yanayofanyika katika viwanja vya Gadeco Halmashauri ya Mkoa wa Geita.
Viewing all 110104 articles
Browse latest View live




Latest Images