Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live

JAFO ATOA SOMO KWA WAKUU WA WILAYA WAPYA

0
0
Zulfa Mfinanga. 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amewataka Wakuu wapya wa Wilaya walioteuliwa hivi karibuni kuhakikisha wanasoma na kuzielewa sheria zinazowaongoza ili kufanya kazi kwa weledi. 

Mhe. Jafo aliyasema hayo leo Jijini Dodoma kwenye kikao kazi na Wakuu hao wa wilaya kwa lengo la kuwapa maelekezo ya kazi ambapo aliwaambia mada kuu ya kikao hicho ni mahusiano na mawasiliano kazini pamoja na kuhakikisha kuwa wanafanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizopo.

“Msiende kuwa vyanzo vya migogoro kwenye Wilaya zenu, tumekuwa tukishuhudia migogoro baina ya Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Wenyeviti wa Halmashauri, Makatibu Tawala pamoja na Wabunge, hatuwezi kwenda hivi, katengenezeni serikali” Alisema Waziri Jafo.

Hata hivyo alikemea tabia ya baadhi ya Wakuu wa Wilaya kuitumia vibaya mamlaka waliyonayo na kuwaweka watu ndani hali iliyopelekea wananchi kuichukia serikali yao, hivyo kuwataka kutumia sheria kama iliyokusudiwa na siyo kwa kuonea watu.

Aidha aliwataka Wakuu hao wapya wa Wilaya kutoa ushirikiano kwa wale wanaotekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na siyo vinginevyo ikiwa ni pamoja kusimamia miradi ya maendeleo ikiwemo uboreshaji wa miundombinu ya afya na elimu unaoendelea kote nchini.

Kwa upande mwingine Waziri Jafo amesema “Kasimamieni ukusanyaji wa mapato ya serikali kupitia mfumo wa kieletroniki sambamba na kudhibiti uvujaji wa mapato hayo, lakini pia mkadhibiti madeni kwa kuwa fedha hizo ndizo zinazotegemewa kwa ajili ya maendeleo nchini”. 

Naye Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Injinia Mussa Iyombe amewataka Wakuu hao wa wilaya kuzitendea haki nafasi walizopewa kwa kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni zilizopo hasa pale wanapomuadhibu mtumishi aliyekosea. 

“Serikali ina taratibu zake, baadhi ya wakuu wa wilaya walikuwa wanatia aibu, kama kuna mtumishi kakosea, tumia mamlaka zinazomuongoza kumshughulikia, na sio kusimamisha watu kazi hovyo, kutumbua tumbua hovyo” Alisisitiza Injinia Iyombe. 

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro kwa niaba ya wakuu wenzake wa wilaya amesema watahakikisha wanafanya kazi kwa kuzingatia kasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akisisitiza jambo kwa Wakuu wa Wilaya wapya 27 walioteuliwa hivi karibuni katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Taifa ya ukaguzi, Jijini Dodoma leo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Mussa Iyombe akisisitiza umuhimu wa kufuata sheria , taratibu na kanuni katika utekelezaji wa majukumu katika Kikao kazi cha Wakuu wa Wilaya wapya walioteuliwa hivi karibuni kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, Jijini Dodoma.
Baadhi ya Wakuu wa Wilaya wapya wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (hayupo pichani) katika Kikao kazi cha Wakuu wa Wilaya wapya walioteuliwa hivi karibuni kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, Jijini Dodoma
Baadhi ya Wakuu wa Wilaya wapya wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (hayupo pichani) katika Kikao kazi cha Wakuu wa Wilaya wapya walioteuliwa hivi karibuni kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, Jijini Dodoma

MWENYEKITI WA CCM TAIFA, DKT. JOHN MAGUFULI AENDESHA KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA

0
0
Ndugu John Pombe Joseph Magufuli Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiwa katika ukumbi wa mikutano katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba kwa ajili ya kuendesha Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM katika Ofisi ndogo ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam leo tarehe 14/08/2018. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akifafanua jambo wakati akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM katika Ofisi ndogo ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam leo tarehe 14/08/2018. 
Ndugu John Pombe Joseph Magufuli Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiwasili katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba kwa ajili ya kuendesha Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa.
Mwenyekiti wa CCM John Magufuli akisalimiana na makamu mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula na katikati ni Dk.Bashiru Ali Katibu mkuu wa CCMmjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM alipowasili katika ofisi ndogo za chama hicho zilizopo Lumumba jijini Dar es Salaam.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Katibu Mkuu wa CCM Bashiru Ally Kakurwa mara baada ya Kikao cha Kamati Kuu ya CCM katika Ofisi ndogo ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam leo tarehe 14/08/2018. PICHA NA IKULU 



TRA: MSAMAHA WA RIBA NA ADHABU YA MALIMBIKIZO YA KODI KUTOA MOTISHA KWA WAFANYABIASHARA NCHINI

0
0
Na Veronica Kazimoto,Dar es Salaam

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema kuwa msamaha wa riba na adhabu wa asilimia 100 kwenye malimbikizo ya madeni ya kodi unaotolewa ndani ya Mwaka wa Fedha 2018/19 utawasaidia wafanyabiashara kulipa kodi ya msingi na hatimaye kuwapa motisha ya kulipa kodi kwa hiari na kwa wakati.

Hayo yamesemwa leo na Kaimu Kamishna wa Walipakodi Wakubwa wa mamlaka hiyo Alfred Mregi wakati akifungua semina elekezi ya msamaha wa riba na adhabu kwenye malimbikizo ya kodi kwa wafanyabiashara iliyofanyika jijini Dar es Salaam.Mregi amesema kuwa dhumuni la semina hiyo elekezi ni kutoa uelewa wa kutosha kwa wafanyabiasha ili waweze kuwasilisha maombi yao kwa usahihi kwa lengo la kupatiwa msamaha huo.

"Leo tumekutana mahali hapa kwa lengo la kutoa elimu kwa wafanyabiashara kuhusu msamaha wa riba na adhabu kwenye malimbikizo ya madeni ya kodi ili kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wote wenye malimbikizo ya madeni wananufaika na msahamaha huo unatolewa kwa asilimia 100," alisema Mregi.Naye Naibu Kamishina wa Kodi za Ndani Abdul Zuberi amesema suala la kodi halijachwa kwa TRA peke yake bali taasisi zote za Serikali zinafanya kazi hiyo ya kuhamasisha ulipaji kodi kwa maendeleo ya watanzania wote.

"Sasa hivi kodi za ndani zimezidi kuongezeka kutokana na uhamasishaji ambao unatoa motisha kwa wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla kulipa kodi kwa maendeleo ya taifa letu," alieleza Zuberi.Kwa upande wake Mfanyabiashara mkubwa kutoka kampuni ya Super Group of Companies inayozalisha sukari ya Mtibwa na Kagera Ibrahim Ali ameishukuru TRA kwa kutoa semina elekezi na kuongeza kuwa elimu waliyoipata imewasaidia kuelewa mambo mengi kuhusiana na msamaha huo.

Msamaha wa riba na adhabu kwenye malimbikizo ya madeni ya kodi unatokana na maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli aliyoyatoa katika Mkutano wa Baraza la Wafanyabiashara (TNBC) uliofanyika Ikulu tarehe 20 Machi, 2018 ambapo wafanyabiashara walilalamikia kuwepo kwa malimbikizo makubwa ya madeni ya kodi za nyuma yakijumuisha riba na adhabu.

Kufuatia maelekezo hayo, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilifanya marekebisho kupitia Sheria ya Fedha ya mwaka 2018 na sehemu ya Sheria ya Usimamizi wa Kodi ya Mwaka 2015 ambapo katika marekebisho hayo, Waziri wa Fedha na Mipango amepewa mamlaka ya kutoa utaratibu maalum wa kumuwezesha Kamishna Mkuu wa TRA kutoa msamaha wa riba na adhabu wa hadi asilimia 100 kwenye malimbikizo ya madeni ya kodi tofauti na asilimia 50 ya hapo awali.
Kaimu Kamishna wa Walipakodi Wakubwa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alfred Mregi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua Semina elekezi ya Msamaha wa Riba na Adhabu kwenye malimbikizo ya kodi kwa wafanyabiashara iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Kamishna wa Walipakodi Wakubwa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alfred Mregi akizungumza na wafanyabiashara wakati wa Semina elekezi ya Msamaha wa Riba na Adhabu kwenye malimbikizo ya kodi kwa wafanyabiashara iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Kamishina wa Kodi za Ndani Abdul Zuberi akizungumza na wafanyabiashara wakati wa Semina elekezi ya Msamaha wa Riba na Adhabu kwenye malimbikizo ya kodi kwa wafanyabiashara iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA FRANCO MARWA - MAELEZO).
Wafanyabiashara mbalimbali wakifuatilia kwa makini Semina elekezi ya Msamaha wa Riba na Adhabu kwenye malimbikizo ya kodi iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa lengo la kutoa uelewa wa kutosha kwa wafanyabiasha hao ili waweze kuwasilisha maombi yao kwa usahihi kwa na kupatiwa msamaha huo. Semina hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.

UEFA SUPER CUP Jumatano hii kule Hispania mambo ni hivi, mambo ni moto!!

0
0
Nani atakuwa bingwa ya Super Cup, kati ya Real Madrid Na Atletico Madrid Jumatano hii? Usikose mechi hii kali ya mabingwa hawa mawili wakiwania ubingwa wa jumla wa Super Cup ndani ya DStv , Ni Jumatano hii saa 4 usiku kupitia Supersport 3 iliyopo kwenye DStv pekee kifurushi Compact kwa sh.69,000 tu!

Bila kusahau, wateja wa DStv wanaweza pakua “Download Application” ya DstvNow itakayowawezesha watanzania wengi kufurahia msimu huu wa soka kwani unachotakiwa tu ni kuwa na akaunti yako ya DStv na unaweza kutazama katika vifaa zaidi ya vinne kama vile simu, kompyuta, na televisheni ya kawaida ukiwa mahali popote wakati wowote bila gharama ya ziada! Ukiwa Na DStv, soka ni mwanzo mwisho yani Moto hauzimi, na kama sio DStv, Potezea!

Dkt Kalemani afungua mafunzo ya Wasimamizi wa miradi ya usambazaji umeme vijijini

0
0
 Wataalam wanaosimamia mradi wa usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yakitolewa na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani)wakati akifungua mafunzo hayo.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akifungua mafunzo kwa wasimamizi wa mradi wa usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) yanayofanyika katika Chuo cha Mipango jijini Dodoma.


 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani  (wa Tatu kulia waliokaa ), Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO, Dkt. Alexander Kyaruzi (wa nne kushoto),  Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya REA, Michael Nyagoga (wa Pili kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka  (wa Tatu kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Amos Maganga (wa kwanza kulia). wakiwa katika picha ya pamoja.

Waziri wa Nishati,  Dkt Medard Kalemani,  amefungua mafunzo ya siku Tano ya wasimamizi wa mradi wa usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) yanayohusisha wataalam kutoka Wizara ya Nishati, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) yanayolenga kuboresha utekelezaji wa mradi huo.

Mafunzo hayo yanayofanyika katika Chuo cha Mipango jijini Dodoma yamehudhuriwa na Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO, Dkt. Alexander Kyaruzi, Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya REA, Michael Nyagoga, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Amos Maganga. 

Akifungua mafunzo hayo, Dkt Kalemani  ametoa maagizo mbalimbali ikiwemo;  wakandarasi wa umeme vijijini mara wanapomaliza kazi za usambazaji, wanapaswa kukabidhi mradi huo kwa TANESCO na REA kabla ya kuondoka katika eneo husika ili kama kuna mapungufu, yarekebishwe kabla ya makabidhiano rasmi.

Pia amewaagiza wasimamizi wa mradi huo, kuruhusu wananchi kulipia kidogo kidogo malipo ya uunganishaji wa umeme na wanapokamilisha malipo hayo waunganishiwe umeme ndani ya Siku Saba.
Vilevile ameagiza wasimamizi  wa mradi wa REA III kutoka Wizara, TANESCO na REA kuhakikisha kuwa,   wanakuwepo katika eneo la mradi ili kusimamia wakandarasi na hivyo kuongeza kasi na ufanisi katika utekelezaji.

Aidha amegiza kuwa,  Taasisi za Serikali zinazohusika na utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini kama vile Wizara ya Fedha na Mipango na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,  zishirikishwe katika hatua mbalimbali za utekelezaji ili kutochelewesha utekelezaji wake.

Vilevile amewataka  Mameneja  wa TANESCO, kuanzisha kwa vituo vya kuhudumia wananchi  katika kila eneo nchini ili kuepusha wananchi hao kusafiri umbali mrefu na kutumia gharama kubwa katika kutafuta huduma zinazotolewa na TANESCO.

Dkt. Kalemani pia amewakumbusha watendaji wa TANESCO na REA kuhakikisha kuwa, wananunua vifaa vinavyozalishwa hapa nchini vya usafirishaji na usambazaji wa umeme kama nguzo, transfoma na mita za umeme kwani vinatosheleza mahitaji.

Maagizo mengine yaliyotolewa ni pamoja na Ofisi za TANESCO za Wilaya kuwa na stoo ya kuhifadhi vifaa vya umeme,  kuhakikisha kuwa kanuni za manunuzi hazicheleweshi utekelezaji wa mradi na wataalam hao kuhakikisha kuwa hawachelewi katika kushughulikia majalada yanayohusu miradi ya umeme.

Kwa upande wake,  Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO, alisema kuwa, maagizo ya Waziri ikiwemo suala la ufanyaji kazi kwa kasi, ufasaha na tija yatazingatiwa katika utekelezaji wa miradi hiyo.

Aliongeza kuwa,  Bodi ya Shirika hilo haitawavumilia Watendaji watakaopokea miradi kutoka kwa wakandarasi ikiwa na mapungufu na hivyo kuharibika ndani ya muda mfupi.

DKT. KIJAJI AAGIZA UCHUNGUZI UFANYIKE MRADI WA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA SHULE YA MSINGI KIGOMA

0
0
Benny Mwaipaja, WFM, Kigoma

NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, ameiagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Kigoma kufanya uchunguzi na kuchukua hatua baada ya kubaini harufu ya ufisadi katika ujenzi wa vyumba vya madarasa 9 ya shule ya msingi Kigoma yanayojengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Japan kwa gharama ya shilingi milioni 200.

Dkt. Kijaji ametoa maelekezo hayo baada ya Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Dkt. John Tlatlaa, kueleza kwamba mradi huo unahusisha ujenzi wa vyumba 10 vya madarasa na vyoo vyenye matundu 12, wakati mkataba ulioingiwa kati ya Manispaa na Mkandarasi inayoonesha kwamba yatajengwa madarasa tisa na vyoo vyenye matundu 12.

Baada ya mjadala kati yake na Kaimu Mkurugenzi huyo wa Manispaa ya Kigoma, akamwelekeza Kaimu Mkuu wa Wilaya hiyo Bi. Mwanamvua Mlindoko kuchukua hatua za kiuchunguzi.

"Mradi unaojulikana Mhe. Mkuu wa Wilaya ni wa madarasa tisa, mkandarasi akija kudai nyongeza ya malipo kwa darasa moja lililoongezeka atakuwa na haki!, ninachokichukua mimi ni taarifa hii inayoeleza kujengwa kwa madarasa tisa, hilo moja ni la kwake Mkurugenzi kichwani" alisisitiza Dkt. Kijaji

Aidha, Dkt. Kijaji alibainisha kutoridhika kwake na gharama za ujenzi wa darasa moja kwa shilingi 17m na kwamba kiasi cha shilingi milioni 200 kilichotolewa na Japan kutekeleza mradi huo kingeweza kujenga madarasa hata 20.
Sehemu ya msingi wa vyumba vya madarasa mapya yanayojengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Japan, katika Shule ya Msingi Kigoma, Manispaa ya Kigoma Ujiji, Mkoani Kigoma, kwa gharama ya zaidi ya shilingi 200m
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango. Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), (Mbele), akiwa na maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, pamoja na wataalam wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, alipofanya ziara kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa 9 yanayo jengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Japan kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 200 katika Shule ya Msingi Kigoma, iliyoko Kigoma Ujiji, mkoani Kigoma.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango. Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), (Katikati), akikagua ujenzi wa vyumba vya madarasa vinavyojengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Japan kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 200 katika Shule ya Msingi Kigoma, iliyoko Kigoma Ujiji, mkoani Kigoma.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Dkt. John Shauri Tlatlaa, akitoa ufafanuzi wa idadi ya vyumba vya madarasa katika Shule ya Msingi Kigoma kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa pili kulia), ambao unatofautiana na maelezo ya Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Bw. Sabasi Lugai, aliyetoa taarifa kwamba yako tisa, jambo lililosababisha Naibu Waziri huyo kuagiza kufanyika kwa uchunguzi wa mradi huo.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango).

TANZANIA KUHIFADHI HEKTA MILIONI 5.2 ZA MISITU ASILI IFIKAPO 2030

Muuza mitumba akabidhiwa gari na Diamond Platnumz kupitia shindano la 'nogewa ushinde' la Diamond Karanga

0
0

Msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini (Bongofleva) na Mkurugenzi wa WCB Nassib Abdull almaarufu Diamond Plutnum akimkabidhi ufunguo wa gari  mshindi wa shindano la 'Nogewa Ushinde' ,Mkazi wa ubungo ndugu Bakari Said,ambaye anajishughulisha na biashara ya kuuza mitumba,kwenye hafla fupi ya mabakabidhiano iliyofanyika leo jijini Dar.


 Shindano hilo ambalo limekuwa likiwavutia vijana wengi kutokana na zawadi mbalimbali ziilizokuwa zikitolewa,limedumu takribani mwezi mmoja sasa kupitia bidhaa za Diamond Karanga,anaeshuhudia kulia ni Afisa Mkaguzi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania Bi.Chiku Salehe .

Aidha katika hafla hiyo Mshindi Bakari Saidi alieleza kwa ufupi huku akionekana mwenye furaha tele,kuwa yeye anafanya biashara ya kuuza mitumba Ubungo jijini Dar es salaam,amesema pamoja na kuibuka mshindi bado ataendelea kutumia bidhaa hizo,Bakari akaongeza kuwa gari hilo litamkomboa kiuchumi,kwa sababu ni mara yake ya kwanza kumiliki gari,hivyo atalitumia kwa matumizi yake binafsi na baadae anaweza kuchukua uamuzi mwingine wa kulifanyia biashara ili kujiongezea kipato.
Afisa Mkaguzi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania Bi.Chiku Salehe akizungumza machache mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo kwenye tukio la Muuza Mitumba akikabidhiwa gari yake,baada ya kuibuka mshindi kwenye shindano la 'Nogewa Ushinde' kupitia bidhaa ya Diamond Karanga,Kushoto ni Msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini (Bongofleva) na Mkurugenzi wa WCB Nassib Abdull almaarufu Diamond Plutnum na kulia ni Meneja wa WCB Hamis Taletale almaarufu Babutale.

Meneja wa WCB Hamis Taletale almaarufu Babutale akitoa muongozo wa baadhi ya mambo kwa ufupi kabla ya shughuli nzima ya makabidhiano ya Gari kwa mshindi wa bidhaa ya Diamond Karaga kuanza,hafla hiyo imefanyika mapema leo kwenye Ofisi za WCB zilizoko Mbezi Beach jijini Dar  

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kushirikiana na Ubalozi wa Marekani nchini kujenga Tanzania yenye Afya Bora ya Moyo

0
0
Mkurugenzi wa Magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akielezea maendeleo ya ukarabati wa jengo la watoto kwa Naibu Balozi wa Marekani nchini Mhe. Dkt. Inmi Patterson (wa pili kulia) alipotembelea Taasisi hiyo leo kwaajili ya kuona kambi maalum ya matibabu ya moyo inayofanywa na madaktari wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Marekani (Madaktari Afrika).
Naibu Balozi wa Marekani nchini Mhe. Dkt. Inmi Patterson akitoka kuangalia ukarabati wa jengo la watoto la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) alipotembelea Taasisi hiyo leo kwaajili ya kuona kambi maalum ya matibabu ya moyo inayofanywa na madaktari wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka nchini Marekani (Madaktari Afrika).
Naibu Balozi wa Marekani nchini Mhe. Dkt. Inmi Patterson akiongea jambo na madaktari kutoka Marekani (Madaktari Afrika) walioko katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kambi maalum ya matibabu kwa wagonjwa wenye matatizo ya mfumo wa umeme wa moyo. Jumla ya wagonjwa nane wameshafanyiwa matibabu katika kambi hiyo na hali zao zinaendelea vizuri.
Naibu Balozi wa Marekani nchini Mhe. Dkt. Inmi Patterson akimsalimia mtoto Catherine Mapunda ambaye amefanyiwa upasuaji wa moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Mhe. Patterson alitembelea Taasisi hiyo leo kwaajili ya kuona kambi maalum ya matibabu ya moyo inayofanywa na madaktari wa JKCI kwa kushirikiana na wataalam kutoka nchini Marekani (Madaktari Afrika).KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

MKUU MPYA WA WILAYA YA HAI AZUNGUMZA KWA MARA YA KWANZA NA WATUMISHI WA HALMASHAURI HIYO

0
0
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.

MKUU mpya wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya amekemea vikali vitendo vya Rushwa vinavyofanywa na baadhi ya watumishi wa halmashauri ya wilaya hiyo hali iliyopelekea kutajwa kama mteja namba moja wa Taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa( TAKUKURU) katika mkoa wa Kilimanjaro.

Sabaya pia ameinyooshea kidole idara ya Ushirika katika Halmashauri hiyo ambayo inatajwa kushindwa kusimamia vyama vya ushirika hadi kupelekea kuingia mikataba aliyoitaja kuwa ya hovyo na yenye kujaa rushwa.

Katika kikao chake na watumishi wa Halmashauri ya wilaya kilicholenga kujitamburisha kwa watumishi hao Sabaya alisema Halmashauri hiyo inaongoza kwa ubadhilifu wa mali za umma na kwamba hadi sasa amepata taarifa za uwepo wa kesi nane zinazohusu rushwa.

“Mnaongoza kwa ubadhilifu na wa mali za umma,naambiwa kuna kesi nyingine zinaendelea na Takukuru inachunguza nyingine , hii ni aibu na ni fedheha kwa Halmashauri ,kama una mikono michafu hauna uhalali wa kumuubiri mtu habari njema niwaombe mbadilike”alisema Ole Sabaya.

Mkuu huyo wa wilaya alisema zipo taarifa ya kuwa katika Halmashauri hiyo kuna baadhi ya watu wamejijengea tabia ya kutaka kuonekana kama miungu watu kwa kufanya maamuzi bal ya kuwashirikisha watu wengine huku akimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo,Yohana Sintoo kulitazama hilo.

“Nimesikia wapo watu hapa ,wao mnakaa kwenye CMT(kikaocha ushauri ) mnafanya maamuzi yeye ni mungu mtu hapa ,ikifika wakati wa kutekeleza hawatekelezi ,mnawakatisha tamaa watumishi wengine walioko tayari kufany kazi ,walioko tayari kutekeleza yale tuliyoahidi wananchi tunategemea hao watu wabadilike”alisema Ole Sabaya.

 Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya akizungumza kwa mara ya kwanza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya Hai katika ukumbi wa Halmashauri hiyo. 

Mmmoja wa baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,akichangia jambo katika kutano wa Mkuu wa wilaya ya Hai na Watumishi wa Halmashauri hiyo. Katibu Tawala wa wilaya ya Hai,Upendo Wela akizungumza katika kikao hicho. Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohana Sintoo akizungumza katika kikao hicho. 

Serikali kudhibiti Uhalifu Ukanda wa Ziwa na Bahari

0
0
Na Mwandishi Wetu
Serikali imejipanga kuimarisha Ulinzi na Usalama katika Ukanda wa Ziwa na Bahari kote nchini ili kuweza kudhibiti uhalifu unaotekelezwa majini ikiwepo uvuvi haramu, usafirishaji wa magendo na uhalifu mwingine unaotokea katika maeneo ya ziwa na bahari.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya boti maalumu ya doria na ufunguzi wa Kituo cha Polisi Wanamaji, wilayani Chato, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amesema lengo la Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha inadhibiti uhalifu katika Ukanda wa Ziwa na Bahari kwa kutumia Vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyopo chini ya serikali, ili kuhakikisha wananchi wanafanya shughuli za kuchumi bila ya kuwa na wasiwasi juu ya usalama wao
Alisema moja ya changamoto kubwa aliyoelezwa wakati alivyofanya ziara ya awali wilayani Chato ni kuwepo kwa matukio ya uhalifu ziwani yaliyopelekea baadhi ya wananchi kusitisha shughuli za kiuchumi katika mwambao huo wa Ziwa Victoria.
“Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuleta maendeleo katika nyanja zote na kuwawekea mazingira mazuri wananchi wake kujishughulisha na shughuli za kiuchumi, hivyo basi tutahakikisha tunaimarisha ulinzi katika sehemu zote ambazo wananchi wanafanya shughuli zao ikiwepo ukanda wa ziwa na bahari na leo hii tunaanzia hapa wilayani Chato.
“Pia nawasihi askari polisi kufanya kazi kwa maadili na agizo hili nalitoa kwa nchi nzima na serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi aitomvumilia askari yoyote atakaebainika kuwabambikia kesi wananchi,hatua kali zitachukuliwa kwa atakaebainika” alisema Masauni ambae pia ni Mbunge wa Kikwajuni
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akiwaongoza viongozi wengine kutembelea eneo la mwambao wa Ziwa Victoria baada ya kuikabidhi boti hiyo ya doria kwa Jeshi la Polisi, kutoka kushoto ni Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Daniel Shilla, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel na Diwani wa Chato, Richard Bagolele . Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Daniel Shilla akimshukuru Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni baada ya kumkabidhi Kituo cha Polisi kinachohamishika wilayani Chato.Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyeshika koti), akishuka katika boti maalumu aliyowakabidhi Kikosi cha Polisi wilayani Chato ikiwa ni mkakati wa Serikali kupambana na uhalifu katika ukanda wa Ziwa na Bahari nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel, akishuka katika boti maalumu iliyokabidhiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani) kwa Kikosi cha Polisi Wanamaji wilayani Chato, ikiwa ni mkakati wa Serikali kupambana na uhalifu katika ukanda wa Ziwa na Bahari nchini.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MHANDISI NDIKILO AWAAHIDI UMEME WA REA AWAMU YA TATU KUWAFIKIA WANANCHI WOTE WA PWANI

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandis  Evarist Ndikilo amewaahidi wananchi wa Kijiji cha Matimbwa kata ya Yombo kuwa awamu ya tatu ya Mradi wa  Umeme wa vijijini REA utawafikia wale wote walikosa.

Hayo aliyasema mbele ya wananchi wa Kijiji hicho akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya Zainab Kawawa na Diwani wa Kata hiyo Mohamed Abdallah Usangi

Amesema kuwa, katika awamu ya kwanza na ya pili wananchi baadhi waliweza kupata umeme huo wa bei rahisi na wengine walikosa ila katika awami hii ya tatu watapita kwa ajili ya kuangalia wapi panahitajika kuwekwa nguzo za umeme.

" Awamu ya kwanza na ya pili ya umeme wa REA ilipita na ni kweli kuna baadhi ya wananchi au maeneo bado hayajafikiwa na mradi huu ila katika awamu tatu watapita kuona mahali ambapo nguzo za umeme hakuna na kuanza mchakato wa kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma ya umeme," amesema Mhandisi Ndikilo.

Mhandisi Ndikilo amesema kuwa, mbali na kuwaahidi wananchi hao bado atawasiliana na Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu na kuweza kufika nae kwa wananchi hao ili awahakikishie umeme utafika kwao hapo lini.

" ni kweli umeme utakuja hapa ila uzuri ni kuwa Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu ni mtoto wenu, mtoto wa Pwani hapa hapa atakuja na kuwahakikishia watu wa kata ya Yombo kuwa umeme utafika mpaka hapa na serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuona wananchi wanapata huduma zinazostahiki," amesema Mhandisi Ndikilo.

Hayo aliyajibu baada ya hoja ya Diwani wa Kata ya Yombo Mohamed  Usangi kuulizia mradi wa umeme wa vijijini REA ambapo kuna baadhi ya wananchi wa kata yake bado  hawajafaidika na mpaka sasa huku wakikosa huduma ya umeme.

Mbali na hilo, Mhandisi Ndikilo alijibu swali la Diwani Usangi kuhusiana na madereva wa bodaboda kukamatwa mara kwa mara na faini zao kulipishwa kubwa sana tofauti na magari ya abiria yakikamatwa.

Amesema, suala hilo ni la RPC wa mkoa lakini kwa namna ya kawaida dereva wa bodaboda anatakiwa afuate sheria ikiwemo kuvaa helment (kofia ngumu) avar viatu vilivyofunika pamoja na kuwa na leseni lakini madereva wengi wamekuwa hawajakamilisha vitu hivi, ila amesikia changamoto hiyo inayowakumba vijana na amewaahidi wananchi wa Kata ya Yombo kushirikiana nao na  kuweza kutatua tatizo hilo ikiwemo kutoa elimu kwa vijana wanaoendesha pikipiki hizo.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandis  Evarist Ndikilo akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Matimbwa kata ya Yombo Wilayani Bagamoyo.

KAMATI YA VIWANDA, BIASHARA, MAZINGIRA YA BUNGE LA TANZANIA KUFANYIA KAZI MPANGO WA ETS.

0
0
MPANGO wa uwekaji muhuri wa Kiectroniki ya kodi (Electronic tax stamp(ETS) kuongeza ukusanyaji wa mapato ya serikali kwa watengenezaji wa pombe kali kwani waingizaji wa pombe kali wa kinyemela hawatanufaika katika soko la pombe kali hapa nchini.

Hayo yamesemwa na Meneja Mkuu wa TBL kitengo cha utengenezaji wa Konyagi, Davis Deogratius wakati akitoa ripoti ya kiwanda cha kutengeneza bia cha Tanzania Breweries Limited(TBL) jijini Dar es Salaam leo wakati wajume wa kamati ya Viwanda, biashara na Mazingira walipotembelea kiwanda hicho jijini Dar es Salaam.

"ETS itasaidia sana kwa watengenezaji wa pombe kali hapa nchini na ukusanyaji wa mapato ya serikali utaongezeka kwani kunapombe kazi zinauzwa kinyemela hapa nchini."

Nae Naibu waziri wa wizara ya viwanda,biashara na uwekezaji, Mhandisi Stela manyanya w
ataishauri serikali ili mpango huo wa ETS ufwate ili kudhibiti uingizwaji wa pombe kali kinyemela na kuuza bia serikali kupata kodi.

Kwa upande wa makamu mwenyekiti wa kamati ya Viwanda,biashara na mazingira  ya Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania Innocent Bashungwa amesema kuwa viwanda vyote vya kutengeneza Mvinyo pamoja na Pombe kali lazima wafuate mpango huo kabambe wa ETS ili serikali kupata mapato stahiki.

Pia baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo wamepongeza utendaji kazi wa kiwanda cha TBL kwani mitambo mingi inatumia technolojia ya hali ya juu kwaajili ya kukidhi utendaji wao wa kazi. 
 Meneja Mkuu wa TBL kitengo cha utengenezaji wa Konyagi, Davis Deogratius akizungumza   wakati akitoa taarifa ya kiwanda cha kutengeneza bia cha Tanzania Breweries Limited(TBL) leo mara baada ya kamati ya Viwanda, biashara na Mazingira ya bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kutembelea katika kiwanda hicho leo jijini Dar es Salaam.
 Makamu mwenyekiti wa kamati ya Viwanda,biashara na mazingira  ya Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania Innocent Bashungwa akizungumza kwaajili ya kufungua kikao kilichohusihsa wabunge pamoja na wafanyakazi wa TBL jijini Dar es Salaam leo.
Naibu waziri wa wizara ya viwanda,biashara na uwekezaji, Mhandisi Stela manyanya  akizungumza mara baada ya kusikiliza ufafanuzi kutoka kwa Innocent Bashungwa akitoa taarifa ya kiwanda cha kutengeneza bia cha Tanzania Breweries Limited(TBL) leo jijini Dar es Salaam wakati kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira walipotembelea kiwanda hicho kujionea jinsi wanavyotenda kazi pamoja na changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo.
 Wajumbe na kamati ya Viwanda, biashara na Mazingira na wabunge wa bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania wakipata malezo wakati wakitembelea Kiwanda cha TBL jijini Dar es Salaam leo.
 Mtambo unao panga chupa kwenye Makreti ya bia.

DC MJEMA AAGIZA TAKUKURU KUCHUNGUZA FEDHA ZA MRADI URASIMISHAJI ARDHI KIPUNGUNI B

0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

MKUU wa Wilaya Ilala, Sophia Mjema, ameagiza Taasisi ya Kuzuia ya Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kuchunguza kamati ya mradi wa ulasimishaji ardhi katika Kata ya Kipunguni B kutokana kuwepo viashiria vya ubadhirifu wa fedha za wananchi katika mradi huo .

Dc Mjema alitoa agizo hilo, Kipunguni wilayani Ilala, jana wakati akipokea kero kutoka kwa wananchi wa eneo hilo, wakidai kuchangishwa fedha kulipia gharama za mradi huo.Wananchi wamedai kuchangishwa Sh. 50,000 kwa utambuzi na Sh. 400,000 na kamati hiyo inayojulika vinondo kwa ajili ya kupimiwa ardhi warasimishiwe makazi yao ikiwemo kupatiwa hati miliki.

Mjema alisema sheria iliyoko ni kwamba wananchi walipishwe Sh.250,000 tu, kwa ajili huduma hiyo kutoka katika kampuni ambazo ziko kisheria."Suala hili naiagiza TAKUKURU ilifanyie kazi kwa kuifanyia uchunguzi kamati hiyo, ikibainika sheri aichukue mkondo wake, lakini utaratibu ni kwamba kampuni yeyote itapima kwa Sh. 250,000 tu si zaidi ya hiyo", alisema Mjema.

Kuhusu kero ya elimu ya baadhi ya shule za kata hiyo kukosa uzio, amemuagiza Mkurugenzi wa Wilaya kuhakikisha shule hizo zinawekewa uzio haraka.Pia ameagiza kuchukuliwa hatua kwa mwalimu wa Shule ya Msingi Kipunguni B, baada kumwambia mzazi wa mmoja wa wananfunzi wazazi wao wandamane kama anaona watoto wao hawaelewi masomo.

Kero hiyo iliwakilishwa na mmoja mkazi wa Kipunguni B, aliedai kuambiwa na mwalimu wa shule hiyo, baada kuhoji kwa mwalimu huyo kuwa mtoto wake maendeleo yake si mazuri darasani.Alisema mwalimu huyo atafutwe na achukuliwe hatua za kisheria kwa kuhamasisha hayo maandamano kwani jukumu la mwalimu kufundisha sio kutaka watu waandamane.

"Naagiza kwamba ofisa wa elimu, akamtafute huyo mwalimu aliyetoa kauli hiyo kwa wanafunzi, awamu hii ya serikali ni kufanya kazi kwa wananchi", alisema.Pia, Mjema kuhusu kero ya kupandishwa kwa nauli dalala kiholela kutoka kituo cha Mombasa hadi Kipunguni, kuwa atafanya kikao kwa kushirikiana na Mamlaka ya Usafiri nchi Kavu na Majini (SUMATRA) na mwakilishi wa wananchi ili kupata usahihi wa nauli hiyo.

Alisema haiwezekani kila wakati nauli ziwe zinapandishwa kwa wananchi, na hiyo imekuwa tabia ya baadhi dalala kuwa barabara ikichimbika kidogo wanapandisha nauli hilo halitawekana.Kuhusu mikopo kwa vijana na wanawake, amewataka kujiunga katika vikundi ili wajiandikishe kwa mtendaji ili wapewe mikopo.

Alisema hiyo ni fursa wanapaswa kuichangamkia kwani ni fedha za serikali zipo kwa ajili yao ili waweze kujipatia maendeleo na miradi iko mingi kufanya.
Mkuu wa Wilaya Ilala Sophia Mjema akizungumza katika eneo la mradi kilipochimbwa kisima cha maji ambacho wananchi wamekilalamikia kuwa hakina tija.
Mkuu WaWilaya Sophia Mjema akikagua Msingi wa Zahanati ya Kipunguni B ambao umekaa kwa zaidi ya miaka mitatu bila kujengwa 

USHIRIKIANO SEKTA YA UMMA NA SEKTA BINAFSI KUIBUA MIRADI YA KIMKAKATI KUKUZA UCHUMI

0
0

Na Mwandishi Maalum, Tanga

Serikali imezitaka Wizara na Taasisi za Umma kuhakikisha zinawajibika kikamilifu kufuata hatua zote muhimu za utekelezaji wa miradi ya Ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi (Public Private Partinaship-PPP), kwa kuwa hatua hiyo itaiwezesha Serikali kupata miradi ya maendeleo yenye sifa na ubora unaotakiwa nchini.

Hayo yameelezwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Mhandisi Zena Said alipokuwa akifungua mafunzo ya siku tano ya ubia kati ya Sekta za Umma na Sekta Binafsi (PPP) kwa Maafisa wa Wizara ya Fedha na Mipango, Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) , Taasisi na Mashirika ya Umma nchini.

Alisema kuwa utaratibu huo wa PPP ni njia bora ya kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo ile ya kibajeti na kuiwezesha Serikali kuweza kufikia malengo yake katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo na kutoa huduma bora na zenye tija kwa wananchi wake. 

Mhandisi Zena aliongeza kuwa, iwapo Halmashauri nchini zitafuata utaratibu wa PPP kwa kubuni miradi yenye sifa stahiki na kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango itasaidia kufikia malengo yake ya kujitegemea.

“Kiukweli hili ni jambo la faraja na ni fursa kubwa kwa Halmashauri zetu kutumia utaratibu wa ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi kutekeleza miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii hususani ujenzi wa hospitali za kisasa, miundombinu iliyobora”alisema Bi. Zena.Mhandisi Zena alifafanua kuwa Tanzania tayari imenufaika na uwekezaji kwenye miradi ya PPP kwa kuhusisha jumla ya miradi 20 yenye thamani ya Dola za marekani Milioni 863. 39.

Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Said, akifungua mafunzo ya ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafisi katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa Tanga ulio jumuisha watendaji mbalimbali kutoka Halmashauri 60 nchini. 
Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Said, akisalimiana na mwezeshaji wa mafunzo ya ubia kati ya Sekta za Umma na Sekta Binafsi Bw. Node Ned White kutoka Benki ya Dunia, katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga. 
Kamishna wa masuala ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. John Mboya akitoa maelezo mafupi kwa mgeni rasmi (hayupo pichani) kabla ya kumkaribisha kwa ajili ya ufunguzi wa mafunzo ya ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi kwa Watumishi wa Halmashauri mkoani Tanga. 
Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Said, (wa pili kulia), (wa kwanza kulia) ni Kamishna wa masuala ya Ubia Sekta ya Umma na Binafsi (PPP) wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. John Mboya, (wa kwanza kushoto) ni Afisa Sheria Mkuu wa PPP Bi. Flora Tenga (wa pili kushoto) ni Bw. Hemedi Mpili kutoka TAMISEMI wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mafunzo ya ubia kati ya Sekta za Umma na Sekta Binafsi yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

AFRIKA KUSINI YAONESHA UTAYARI KUWA NA USHIRIKIANO SEKTA YA MADINI

0
0

Na Asteria Muhozya, Dodoma

Waziri wa Madini Angellah Kairuki jana tarehe13 Agosti alikutana na Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Mheshimiwa Thami Mseleku. Katika mkutano huo, Balozi huyo alimueleza Waziri Kairuki kuhusu utayari wa Nchi hiyo ya Afrika Kusini kuendeleza ushirikiano na Tanzania katika sekta ya madini nchini.

Ujio wa Balozi Thami Mseleku, Makao Makuu ya Wizara ya Madini, unafuatia ziara ya Kamati ya Jamii na Masuala ya usalama ya Bunge ya Jimbo la Gauteng Pretoria- Afrika Kusini ambao walifika nchini mwezi Juni mwaka huu kwa lengo la kujifunza na kupata uzoefu wa namna sekta ya madini nchini inavyoendeshwa.

Aidha, wakati wa ziara ya kamati hiyo ya Bunge hilo nchini, ilikubalika kuwa na haja ya kuwa na ushirikiano katika masuala mbalimbali ya namna ya kusimamia sekta ya madini ikiwa ni pamoja na shughuli za uchimbaji madini, kubadilishana uzoefu katika udhibiti wa uchimbaji holela wa madini, usimamizi wa migodi na wachimbaji wadogo wa madini.

Maeneo mengine ni pamoja na namna ya kuwasaidia wachimbaji wadogo nchini kutoka katika uchimbaji mdogo kwenda katika uchimbaji wa kati na hatimaye kuwa wachimbaji wakubwa.Pia, masuala ya utafiti wa miamba ya uchimbaji madini, mafunzo kwa ajili ya wataalam, kubadilishana uzoefu katika usimamizi wa sekta ya madini, masuala ya umiliki wa migodi na namna ya kuwawezesha wazawa kumiliki uchumi kupitia sekta ya madini.

Kwa upande wake, Waziri Kairuki alimhakikishia Balozi Thami kuhusu nia ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kumarisha na kukuza zaidi mahusiano baina ya nchi hizo mbili pamoja na kushughulikia changamoto zinazojitokeza katika sekta mbalimbali hususan katika sekta ya madini ili kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi hizo mbili.Vilevile, Waziri Kairuki alimueleza Balozi huyo jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara nchini ambapo ameendelea kuwakaribisha zaidi wawekezaji kutoka Afrika Kusini kuwekeza katika sekta ya madini nchini.

Vilevile, Waziri Kairuki alimpa pole Balozi huyo kufuatia kifo cha Mama Winnie Mandela aliyefariki dunia mwezi Aprili mwaka huu.

Waziri wa Madini Angellah Kairuki akimweleza jambo Balozi ya Afrika Kusini nchini Tanzania Thami Mseleku (kushoto) wakati Balozi huyo alipomtembelea Waziri kairuki ofisini kwake jijini Dodoma.

Waziri wa Madini Angellah Kairuki na Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania Thami Mseleku, wakijadiliana jambo ofisini kwa Waziri Kairuki, jijini Dodoma.

DKT. KIJAJI AAGIZA DEREVA ALIYEHAMISHWA KITUO CHA AFYA BITALE KIGOMA KURUDISHWA MARA MOJA

0
0

Na Benny Mwaipaja, WFM, Kigoma.

NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmahauri ya Wilaya ya Kigoma kumrejesha mara moja katika kituo chake cha kazi cha awali, dereva wa Kituo cha Afya Bitale, kilichoko Kata ya Bitale katika Halmashauri ya wilaya hiyo baada ya kubainika kuwa gari la kubeba wagonjwa kituoni hapo halina dereva.
Dkt. Kijaji, ametoa maelekezo hayo alipotembelea Kituo hicho cha Afya kukagua ujenzi wa majengo mapya ya Kituo hicho yatakayogharimu shilingi 400m  baada ya Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Bitale, Dkt. Norbert Nshemetse, kueleza changamoto ya upungufu wa watumishi wa kituo hicho akiwemo dereva.
Dkt. Nshemetse, pamoja na kumshukuru Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, kwa kuwapatia gari la wagonjwa (Ambulance) katika kituo hicho, alisema gari hilo halina dereva baada ya dereva wake kuhamishiwa katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma mwezi Julai, 2018.
“Katika jambo lililonishitua ni kupata taarifa kwamba dereva aliyekuwa akiendesha gari la wagonjwa hapa Kituoni amehamishwa kupelekwa kwa Mkurugenzi Mtendaji wakati anahitajika zaidi hapa kuliko huko kwa Mkurugenzi” alisikitika Dkt. Kijaji
 AC3A7908
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akitoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Wilaya ya Kigoma, kumrudisha Dereva wa gari la Kituo cha Afya cha Bitale ambaye alihamishiwa katika Ofisi ya Mkurugenzi na kukifanya kituo hicho kukosa huduma za gari kwa wagonjwa, kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Uvinza na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bi. Mwanamvua Mlindoko, wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo Mkoani Kigoma.
AC3A7887
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kulia)  akipokea taarifa ya Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Afya  Bitale kutoka kwa Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho Wilayani Kigoma Mkoani Kigoma, Dkt. Norbert Nshemetse, wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea na kukagua maendeleo ya mradi huo utakaogharimu takribani Sh. milioni 400 hadi kukamilika kwake.
AC3A7881
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Bitale Wilayani Kigoma, mkoani Kigoma, Dkt. Norbert Nshemetse akisoma taarifa ya Mradi wa Ujenzi wa miundombinu ya Kituo hicho likiwemo jengo la Wazazi, Mionzi na Kliniki  ya mama na mtoto ambapo tayari Sh. Milioni 400 zitatumika kwa kazi hiyo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>

LUGOLA ATOA ONYO KALI KWA TRAFIKI WAOMBA RUSHWA, WANAONYANYASA WAENDESHA BODABODA WAFUATA SHERIA

0
0

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Kijiji cha Igundu, Jimboni kwake Mwibara, Wilaya ya Bunda, mkoani Mara. Katika hotuba yake, Lugola alitoa onyo kwa baadhi ya polisi wa usalama barabarani kuacha tabia ya kuomba rushwa pamoja na kuwatesa kwa kuwaweka mahabusu waendesha bodaboda ambao wanaofuata sheria za usalama barabarani.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola akipiga ngoma ya asili ya Lukuyamoyo ya Kabila la Wajita wakati alipofanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi wa Mji mdogo wa Kisorya, Mwibara, Wilaya ya Bunda Mkoani Mara. Lugola alitoa ovyo kwa baadhi ya polisi wa usalama barabarani kuacha tabia ya kuomba rushwa pamoja na kuwatesa kwa kuwaweka mahabusu waendesha bodaboda ambao wanaofuata sheria za usalama barabarani. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kulia), akimkabidhi Nyajoke Masatu, Kapteni wa Timu ya Brendabuke, zawadi ya shilingi 250,000 baada ya kuwa mshindi wa kwanza kwa kuifunga kwa penati timu ya Igundu katika mashindano ya mpira wa miguu la Bonanza la Kangi, linaloendelea katika kata 12 za Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda, mkoani Mara. Katika hotuba yake, Lugola alitoa ovyo kwa baadhi ya polisi wa usalama barabarani kuacha tabia ya kuomba rushwa pamoja na kuwatesa kwa kuwaweka mahabusu waendesha bodaboda ambao wanaofuata sheria za usalama barabarani. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kushoto) akimkabidhi dawati Mkuu wa Shule ya Sekondari Mwigundu, Masele Kadoke, mara baada ya Waziri huyo kufanya mkutano wa hadhara na wananchi wa Kijiji cha Igundu, Mwibara, Wilaya ya Bunda, mkoani Mara. Lugola aliikabidhi Sekondari hiyo madawati 30 katika mkutano huo na alitoa ovyo kwa baadhi ya polisi wa usalama barabarani kuacha tabia ya kuomba rushwa pamoja na kuwatesa kwa kuwaweka mahabusu waendesha bodaboda ambao wanaofuata sheria za usalama barabarani.. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

VIDEO: Diaspora 2018 kukutana Pemba, Zanzibar

Viewing all 109607 articles
Browse latest View live




Latest Images