Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

MANYAMA:SERIKALI YA AWAMU YA TANO ITAVUSHA WATANZANIA KWENDA KATIKA UCHUMI WA KATI

$
0
0
Na Chalila Kibuda , Globu ya Jamii
WAKILI wa Kujitegemea Leonard Manyama amesema kuwa serikali ya awamu ya Tano chini ya Dk.John Pombe Magufuli itawavusha watanzania kwenda katika uchumi wa maendeleo wa kufanya kazi pamoja na ulipaji wa kodi.

Manyama aliyasema hayo wakati aliposhuka katika uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akitokea nchini Marekani amesema amejifunza vitu vingi nchini Marekani ambavyo ndivyo Rais Dk.John Pombe Magufuli anapigania katika watu kufanya kazi pamoja na ulipaji wa kodi.

Amesema kuwa ulipaji wa kodi nchini Marekani ni sheria na hakuna majadiliano juu ya ulipaji wa kodi ambapo ndicho kinachofanyika sasa.

Manyama amesema maendeleo yatapatikana tu ikiwa kila mtu atafanya kazi pamoja na kulipa kodi ambayo ndio itafanya maendeleo ya kufikia uchumi wa kati.

Aidha amesema kuwa nchi hii imejaliwa rasimali za kutosha ambazo Rais anazipigania hivyo kila mtu kumuunga mkono kwa vitendo katika kufanya kazi na kusimamia rasilimali zilizopo.

“Nina imani ya Rais kuwa nilichoona nchini Marekani ndicho kinafanyika kwetu katika kuhakikisha kila mtu analipa kodi ambayo sasa indio itafanya mapinduzi katika uchumi wa kati katika uboreshaji wa miundombinu ya barabara , Afya na Mambo mengine mbalimbali”amesema Manyama.
Wakili wa Kujitegemea Leonard Manyama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo mara baada kuwasilia katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akitokea nchini Marekani.

Introducing Brand New Audio: Royazdad - Kila Kitu

CRDB BANK YAMWAGA SERA KWA WAJASIRIAMALI WANAWAKE WAFUGA KUKU UFUNGUZI WA SEMINA YAO MKURANGA MKOANI PWANI

$
0
0
Meneja wa CRDB Bank Tawi la Mbagala jijini Dar es Salaam, Midlaster Nsanzugwanko, akizungumza na Wajasiriamali wanawake wafuga kuku wa Wilaya ya Mkuranga wakati wa ufunguzi wa semina yao, ya siku mbili, iliyoandaliwa na Jukwaa la Wanawake Mkuranga na kufunguliwa na Mbunge wao, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega, ukumbi wa Flex Gardern, wilayani humo jana. Kulia ni Kaimu Meneja Biashara, Adrian Kongojole na kushoto ni Afisa Mauzo wa tawi hilo, Mohammed Madengelo. CRDB Bank imedhamini semina hiyo. 
Afisa Mauzo wa CRDB Bank, tawi la Mbagala, Mohammed Madengelo, akielezea sera za benki hiyo, kwa Wajasiriamali wanawake wafuga kuku wa Wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani, wakati wa ufunguzi wa semina yao, ya siku mbili inayoendelea ukumbi wa Flex Gardern.
Wajasiriamali wanawake wafuga kuku kutoka sehemu mbalimbali za Wilaya ya Mkuranga, wakimsikiliza Afisa Mauzo wa CRDB Bank, tawi la Mbagala, Mohammed Madengelo. 
Meneja wa CRDB Bank Tawi la Mbagala, Midlaster Nsanzugwanko (kushoto) na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake wilayani Mkuranga, Mariam Ulega, wakifurahia jambo wakati akimuonesha kitu katika kipeperushi cha benki hiyo, wakati wa semina hiyo. 
Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega, akimkabidhi cheti maalum cha Mwanamke Bora, wilayani Mkuranga, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake wilayani Mkuranga, Mariam Ulega, mara baada ya kuifungua rasmi semina hiyo.

RAIS MAGUFULI APONGEZA JIMBO LA MBULU KUPATA ASKOFU MPYA

$
0
0
RAIS John Magufuli amewapongeza wananchi wa wilaya za Mbulu, Babati na Hanang' mkoani Manyara na Karatu mkoani Arusha zinazounda Jimbo la Mbulu kwa kumpata askofu wa tano wa Jimbo hilo Anthony Lagwen. Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi ambaye alimwakilisha Rais Magufuli aliyasema hayo jana mjini Mbulu Mkoani Manyara, kwenye tukio la kusimikwa kwa askofu Lagwen.

Waziri kabudi alisema pamoja na kuwapongeza, kanisa katoliki limekuwa msaada mkubwa kwa serikali kwa kutoa huduma ya elimu, afya na maji hasa kwa watu wa kawaida. Alisema jimbo la Mbulu linaloundwa tangu mwaka 1953 limekuwa mfano wa kuigwa katika kuhakikisha jamii ya eneo hilo inapata huduma za kiroho na kimwili.
"Tunapongeza kanisa katoliki jimbo la Mbulu kwa kutoa huduma za afya ikiwemo hospitali za misheni za Dareda na Bashnet wilayani Babati," alisema.

 Alipongeza jimbo hilo kumiliki kituo cha redio Habari Njema ambacho kwa namna moja au nyingine kinatoa huduma ya uinjilishaji na kuhabarisha jamii.

"Kituo hicho cha redio kiendelee kusisitiza amani kwani bila uwepo wa amani hakutawezekana kufanyika chochote," alisema.
Alisema taasisi za dini kwa kiasi kikubwa zimechangia maendeleo mengi na ustawi wa jamii hivyo serikali itaendelea kushirikiana kwa pamoja ili kuhakikisha jamii inasonga mbele. Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Dar es salaam, mwadhama Policarp Kardinali Pengo alisema japokuwa askofu Lagweni ni mzaliwa wa jimbo la Mbulu lakini atakumbana na changamoto zile zile wanazokumbana nazo maaskofu ambao wanaongoza majimbo ambayo hawajazaliwa.

"Mimi siwezi kuona Sumbawanga ndiyo bora zaidi kuliko sehemu ninayoongoza waumini hivyo nawe waongoze waamini kama inavyopaswa kuwaongoza," alisema Kardinali Pengo.


Rais wa baraza kuu la maaskofu wakatoliki nchini (TEC) askofu wa jimbo la Mpanda, Gervas  Nyaisonga alisema askofu Lagwen ameteuliwa na Baba mtakatifu papa Francisco wakati huu ambapo wanasherehekea jubilee ya miaka 150 ya uinjilishaji. Askofu Nyaisonga alisema askofu Lagwen baada ya kupata nafasi hiyo anapaswa kuwaangalia usoni waumini ili kuzidi kuwajenga kiroho.


Mkuu wa mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti alisema serikali ya mkoa huo itashirikiana na jimbo hilo katika kufanikisha ustawi wa wananchi wa eneo hilo. Mnyeti alisema askofu Lagweni amepata daraja hilo la uaskofu ambapo ni heshima kwa wananchi wa Mbulu, Manyara na Tanzania kwa ujumla.

"Japokuwa wewe umezaliwa katika jamii ya wairaqw hata ungekuwa mmeru au msukuma lakini kwa kuwa umeteuliwa kuwa askofu wa Mbulu, umepakwa mafuta kwa uwezo wa roho mtakatifu," alisema Mnyeti.

Akizungumza baada ya kusimikwa askofu Lagwen alisema anamuomba Mungu amsaidie kutimiza wajibu wake mpya wa kiroho katika kuwahudumia waamini wa eneo hilo.

Askofu Lagwen alisema wanashirikiana na serikali katika kufanikisha huduma mbalimbali na miradi ya elimu, afya, maji, mazingira, habari na nyingine. Aliwashukuru wote walifanikisha tukio hilo na akawaahidi kuwa atatoa ushirikiano unaostahili kupitia nafasi yake kwa upendo na umoja watumikie.

Askofu Anthony Lagwen alizaliwa  Julai 5 mwaka 1967 kwenye Kijiji cha Tlawi, wilayani Mbulu mkoani Manyara na kuanza masomo ya elimu ya msingi na masomo ya sekondari katika seminari ndogo ya Sanu, Jimbo Katoliki la Mbulu.

Biteko atoa wiki moja kwa muwekezaji kulipa kodi ya madini serikalini

$
0
0
Naibu waziri wa madini, Dotto Biteko akizungumza na wachimbaji wadogo wa eneo la Kilalani, baada ya kutembelea eneo hilo.

Na Zuena Msuya, Tanga

Serikali imempa muda wa wiki moja nwekezaji mmiliki wa kampuni ya Amazon Trading (T)Company Limited Abdi Hozza kuhakikisha anailipa serikali kodi ya pango ya uwekezaji kiasi cha dola za Marekani 70,020 sawa na zaidi ya shilingi milioni 140 za kitanzania anazodaiwa tangu mwaka 2011 katika machimbo ya Kalalani eneo la Umba wilayani Korogwe kutokana na leseni nane za uchimbaji wa madini kuanzialeseni namba (102-109/2001) anazomiliki .

Sambamba na hilo imeiagiza serikali ya wilaya ya Korogwe kuhakikisha inatenga maeneo ya wachimbaji wadogowadogo wa madini ili kuepusha migogoro iliyodumu kwa muda mrefu hali ambayo imeleta hali ya chuki baina ya mwekezaji na wananchi.

Waziri Biteko alitoa agizo hilo alipotembelea katika machimbo hayo juzi Jumamosi katika vijiji vya Kigwasi na Kalalani kata ya Kalalani wilayani humo. Biteko alimtaka ndani ya wiki moja mwekezaji huyo kulipa kodi hiyo ya pango anayodaiwa na serikali na amewataka wananchi kutoa ushirikiano katika kuwabaini wageni na watu wanaonunua madini kwa njia za panya.
Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko, akikagua Mabaki ya mgodi wa Amazon,ambao umesitisha uchimbaji kwa miaka mingi kutokana na Matatizo mbalimbali.

“Haiwezekani tangu madini yaanze kuchimbwa katika machimbo haya serikali haijapata kodi kutokana na mgodi huu tunakuta sifuri nimewaambia wailipe haraka nataka nikifika Dodoma kuna commitment statement mnalipa lini” alisema.

Aliongeza “Na yule anayedhani atakuja Kalalani kununua madini kwa njia ya panya muda huo umekwisha,na tumekwenda kwenye mto tumekuta mnachimba madini,sheria inakataza kuchimba madini kwenye vyanzo vya maji naomba kuanzia sasa mkaondoe vifaa vyenu kule mtoni”.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

DC JOKATE AENDELEA NA MAPAMBANO DHIDI YA WAVAMIZI WA MISITU KISARAWE

MAVUNDE AWAONDOA HOFU WAWEKEZAJI NCHINI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Anthony Mavunde amewaondoa hofu wawekezaji na kuwataka kufuata sheria za nchi pindi wanapohitaji kuja kufanya kazi nchini ili kuepuka kusumbuliwa na Serikali .

Mavunde ameyasema hayo kattika Mkutano uliondaliwa na Chama cha Wafanyakazi na Wawekezaji kutoka nchini China kwa ajili ya kuimarisha mahusiano mazuri ya kibiashara.

Akizungumza na wawekezaji hao, Mavunde amesema kuwa amefurahishwa na kukutana baina ya serikali ya Tanzania na Wawekezaji wa China ili kuzungumzia sheria za kazi na vibali vya ukaazi.

Mavunde amesema kuwa serikali ya awamu ya tano inawahitaji sana wawekezaji kwa ajili ya maendeleo ya nchini na msimamo wa serikali ni kuleta wawekezaji wengi zaidi ikiwa ni sehemu ya kutengeneza fursa za ajira kwa vijana wa kitanzania.

Amesema Mavunde," serikali ya Tanzania inawahitaji sana wawekezaji kwa ajili ya maendeleo ya nchi na msimamo wa serikali ni kuoma wawekezaji wanafuata sheria za kazi na ukaazi (uhamiaji) kwa wafanyakazi na wataalamu watakaowaleta na kuona sheria zinafuata sheria za nchi."

Amesema kuwa, anashukuru sana Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa kuweza kutafsiri sherianza kazi kutoka lugha ya Kiswahili na kwenda lugha ya Kichina kitu ambacho kitawasaidia sana kutambua kupata elimu na kufahamu sheria za kazi na Ukaazi za hapa nchini.

Akijibu swali la Mwandishi, Mavunde amesema kuwa serikali imekua inatoa vibali ya kazi kwa miaka mitano ila kama Mtaalamu huyo atakuwa bado anahitajika ili watanzania wazidi kupata ujuzi kampuni husika inaweza kukata rufaa na kuelezea sababu na kama zitakuwa na faida kwa Taifa Mtaalamu huyo ataongezewa muda.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Nchini (ATE) Dkt Aggrey Mlimuka amesema kuwa dhumuni la kuwakutanisha wawekezaji na serikali ni kuona biashara zao zinafanya kazi kwa ufanisi mkubwa.

Dkt Mlimuka amesema kuwa hii si mara ya kwanza kwa kufanya mkutano huo na wawekezaji ila kwa sasa wakaamua kuleta na watu wa serikali ambapo amekuja Waziri anayehusika na masuala ya sera, kazi na ajira kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu.

Mbali na hilo, ameongezea kuwa uwekezaji mzuri ni ule unaoendana na mazingira mazuri ya kazi pia watanzania waweze kufaidika kwani changamoto zote zinatatulika ikiwemo Ucheweleshaji wa vibali kwa wawekezaji kutokana na kutokuwa na elimu ya sheria za kazi na ukaazi za hapa nchini.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Anthony Mavunde akizungumza na wawekezaji (hawapo pichani) kuhusiana na taratibu za nchi pindi wanapohitaji kuja kuwekeza na kufanya kazi. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dkt Aggrey Mlimuka


watafiti wa kilimo na mifugo wakutana mjini Dodoma

$
0
0
 Na Bashiri Salum- Dodoma

Uwepo wa tija ndogo katika Sekta ya kilimo na taknolojia chache hapa nchini kumetokana na kutengewa kiasi kidogo cha fedha kutoka serikalini na kwa wadau wa maendeleo. Hayo yamesemwa na kaimu mtendaji mkuu wa taasisi ya Utafiti wa Kilimo TARI Dkt Degratius Rwezaura ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano uliowakutanisha watafiti wa kilimo na mifugo uliofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano wa wakala wa uhifadhi wa chakula wa taifa NFRA uliopo Dodoma.

Dkt Rwezaura amesema kwamba fedha zinzotengwa na serikali kwa ajili kufanya utafiti wa kilimo zimekuwa ndogo hivyo kushindwa kukamilisha lengo la watafiti kubuni teknolojia mbaliambali za kilimo na mifugo ambazo ni muhimu sana katika kipindi hiki cha uchumi viwanda.
Aidha Dkt Rwezaura amesema utafiti wa kilimo na mifugo hapa nchini umekuwa ukigharimu kiasi kikubwa cha fedha kwakuwa uwekezaji katika miundombinu ya utafiti ikiwemo ujenzi wa vyumba vya baridi vya kuhifadhi mbegu(cold room) na mahabara za kutosha haujafanyika kikamilifu hivyo kulazimu kuendelea kuhifadhi mbegu katika vitalu kwa kulilima kila mwaka. “Kama tungekuwa na mahabara jini tungeweza kuifadhi na kusambaza mbegu bora za kilimo na mifugo kwa wakati badala ya kulima kwenye vitalu kila mwaka ili kuepuka kuharibika kwa mbegu.” Allisema Dkt. Rwezaura

Hata hivyo amebainisha kwamba takwimu zinaonesha kuwa Serikali imenachangia asilimia 0.17 katika uwekezaji kwenye utafiti ikilinganishwa na nchi nyingine kama Uganda na Kenya ambazo katika utafiti wamewekezeza asilimia 4.6 alisema Dkt. Rwezaura “Kilimo chetu kimeendelea kukosa tija kwa sababu ya uwekezaji mdogo wa fedha kutoka kwa wafadhili na serikali ”alisistiza Dkt Rwezaura

Aidha Dkt. Rwezaura alimalizia kwa kusema kwamba lengo la mkutano huo ni kutengeneza hoja na kukutana na watunga sera ili kuweza kutafuta fedha za kuendeleza utafiti wa kilimo na mifugo kwa ajili ya upatikanaji wa malighafi za viwandani.
Naye Dkt Bakari Msangi kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia ( COSTECH) amesema kwamba Taasisi hiyo imeratibu tafiti nyingi hapa nchini kupitia mfuko wa serikali hasa katika sekta ya kilimo mifugo na uvuvi lengo likiwa ni kurahisisha ufanywaji wa tafiti mbalimbali. Aidha Dkt Msangi amebainisha kwamba watafifi wapatao 517 walijengewa uwezo kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia katika kiwango cha uzamili na uzamivu lengo ni kuwafanya waweze kuimarisha sekta ya kilimo

Hata hivyo Dkt Msangi amesisitiza kwamba kuanzia mwaka 2010-16 wameweza kupeleka kiasi cha shilingi bilioni 5. 1 kwa watafiti kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya utafiti ikiwemo ujenzi wa mahabara katika maeneo ya Zanzibari,makutopora Dodoma, Mpwapwa Naliendele na katika Mikoa ya wa Kilimanjaro.

Amesema COSTECH wamekuwa wakiratibu ujenzi wa miundombinu ya utafiti kwa sababu ya umuhimu mkubwa wa mazingira bora katika ufanyaji wa utafiti Aidha ametoa wito kwa watafiti kufanya tafiti zenye ubunifu ili kuendana na mahitaji na kuwafikiwa walengwa kwa wakati.

utafi kwa sasa unatakiwa kwenda na ubunifu kwa sababu mazao ya utati yapo mengi lakini haziendi mara kwa watumiaji kutokana na kutotumika kwa ubunifu wa kutosha hivyo kwa sasa tunasisitiza sana ubunifu kwenye tafiti ili ziweze kuwavutia walengwa. Alisema Dkt Msangi.

MAOMBI YA KUSHIRIKI KATIKA MASHINDANO YA SWAHILI FASHION WEEK WASHNGTON BENBELLA EMERGING DESIGNER YAMEANZA RASMI

$
0
0
Kwa kipindi cha miaka 10, maonyesho ya mavazi ya Swahili Fashion Week yamebaki kuwa mbele katika kutoa na kuwatengenezea njia wabunifu chipukizi katika tasnia ya mitindo Afrika mashariki na kati. Swahili fashion week kupitia shindano la kutafuta mbunifu chipukizi lijulikanalo kama Washington Benbella Emerging Designer Competition (WB-EDC) limekuwa likisherehekea vipaji vingi vya mitindo mbalimbali barani afrika na vile vile wabunifu chipukizi wamekuwa wakipata kujiamini na kuweza kuanzisha bidhaa zao.

Mwaka huu, katika mashindano haya yakiwa na dhima kuu ya “kukuza lugha ya Kiswahili” yamefungua rasmi milango kwa wabunifu vijana barani afrika kutuma maombi kwa fursa hii ya kipekee itakayo mpa nafasi ya kutambulika katika tasni ya mitindo na kupata uzoefu.

“tunafurahi  fungua awamu ya 11 ya mashindano haya, na siku zote huwa tuna furaha ya kutoa fursa za thamani kwa wabunifu chipukizi wenye vipaji na hamasa ambao watawakilisha tasnia ya mitindo barani afrika kwa miaka ijayo. Hivyo tunawasihi wabunifu wote chipukizi kuikumbatia fursa hii kwa umakini na kutuma maombi kabla ya tarehe 30 Septemba 2018 saa 12 jioni.” Alisema Afisa uhusiano wa Swahili Fashion Week, Maryam Idriss.

Chipukizi 10 watakaochaguliwa kuingia fainali, watapewa nafasi ya kuonyesha mitindo ya nguo zao katika siku ya pili ya maonyesho ya Swahili Fashion Week ambayo itakuwa ni tarehe 1 Disemba 2018, kasha majaji watachagua mshindi na atazawadia tuzo na nafasi ya kushiriki na kuonyesha mavazi yake mengi zaidi katika maonyesho ya 12 ya Swahili Fashion Week mwaka 2019.

Fomu za maombi tayari zipo kwenye tovuti www.swahilifashionweek.com, tarehe ya mwisho wa kuwasilisha fomu ni 30 Septemba  2018 saa 12 za EAT. Waombaji wanakumbushwa kusoma maelekezo kwa makini ili wawasilishe maombi kamili.

Wananchi wengi zaidi kuwezeshwa kupata msaada wa huduma za kisheria nchini

$
0
0
Msajili wa mashirika yanayotoa msaada wa sheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Bi Felistas Mushi akiongea wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka unaowakutanisha pamoja wakurugenzi na watendaji wa mashirika yanayotoa huduma za kisheria chini ya udhamini wa shirika lisilo la kiserikali la Legal Services Facility – LSF. Mkutano huo unaofanyika jijini Dodoma

Wadau kutoka Mashirika yanayotoa msaada wa kisheria wanakutana jijini Dodoma kujadili mikakati mbalimbali itayosaidia kuboresha utoaji wa huduma za msaada wa kisheria—lengo kuu likiwa ni kuwakwamua mamilioni ya watanzania wanaokabiliwa na matatizo mbalimbali ya kisheria. Kongamano hilo linawakutanisha pamoja wakurugenzi na watendaji wa mashirika yanayotoa huduma za kisheria (Regional Mentors Organizations-RMOs) yanayotekeleza miradi ya utoaji wa huduma za kisheria inayofadhiliwa na Shirika la Legal Services Facility (LSF), kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana.

Akizungumza wakati wa ufunguzi huo msajili wa mashirika yanayotoa msaada wa sheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Bi Felistas Mushi. aliwapongeza LSF kwa kusimamia mradi huo kwa takribani miaka 6 sasa na kuwawezesha wananchi hasa maskini kupata haki zao na kutumia fursa hiyo kuwahasa wananchi kuacha mila potofu zinazokandamiza haki za raia kwa ujumla

“Awali ya yote nipende kuwapongeza sana kwa kazi kubwa mnazozifanya katika kuhakikisha tunawawezesha wananchi kupata elimu juu ya maswala ya haki na sheria na kutatua migogoro mbalimbali. Mradi huu umekuwa tija kubwa kwa serikali  na wizara kwa ujumla kwani umesaidia kutatua changamoto kubwa zinazowapata jamii husuani maskini zinazosababishwa na kutoelewa misingi ya haki za binadamu, mila potofu na nyingine nyingi”

Napenda kuwaahidi serikali itaendelea kufanya kazi nanyi kwa karibu katika kuboresha mifumo ya upatikanaji wa haki, kuimarisha sera  zitakazochochea haki na usawa kwa wote hatimae kuchochea shughuli za kijamii na kiuchumi.

Kwa upande wake Meneja Mradi, Ramadhani Masele , kwa niaba ya mtendaji mkuu wa LSF alisema “Tunatarajia kuwa na mijadala kuhusiana na kazi zilizofanywa na wasaidizi wa kisheria na mashirika yanayotoa huduma za kisheria—katika swala zima la utoaji wa huduma ya kisheria nchini,” mpaka sasa LSF imeshatoa zaidi ya shilingi billion 10 katika utekelezaji wa mradi huu

Mkutano huu, kwa mujibu wa Meneja Mradi wa LSF, utapitia na kutathimini viwango na ubora wa huduma za usaidizi wa kisheria zilizotolewa na wasaidizi wa kisheria na vituo vya usaidizi wa kisheria, matatizo yaliyowakabili, na jinsi ya kuyatatua –ili kuhakikisha huduma bora za msaada wa kisheria zinawafikiwa wahitaji wengi (wanawake na wanaume maskini), hasa wale waishio vijijini.

Takribani wasaidizi 5000 wameshapatiwa mafunzo chini ya miradi mbalimbali inayofadhiliwa na shirika la LSF.  Wasaidizi hawa wanatoa msaada wa kisheria katika wilaya 158 nchi nzima, wakiwasaidia mamilioni ya watanzania maskini wanaokabiliwa na matatizo mbalimbali ya kisheria.

“Ni ukweli usiopingika kuwa wasaidizi wa kisheria wamefanya kazi kubwa, kuwakwamua watu wengi sana kutoka katika matatizo mbalimbali ya kisheria. Tunazo shuhuda na ripoti nyingi zinazothibitisha kazi hizi nzuri zilizofanywa na wasaidizi wa kisheri. Hata hivyo, pamoja na matokeo haya mazuri, lakini bado tunahitaji kuongeza nguvu zaidi na kuwasaidi wasaidizi hawa wa kisheria wafanye vizuri zaidi ya hii waliofanya. Ndio maana tumeitisha kongamano hili ili kujadili kwa pamoja namna ya kuboresha huduma za wasaidizi wa kisheria kuwafikia watu wengi zaidi, hasa hasa maeneo ya vijijini.

Jamii imeshauriwa kutumia  watoa huduma wa msaada wa kisheria kila wilaya  pindi wanapokumbwa na changamoto mbalimbali zinazopelekea uvunjwaji wa haki. Huduma hizi ni bure na zinapatikana kwa yeyote anayehitaji msaada.
Meneja Mradi wa Legal Services Facility , Ramadhani Masele akitoa mada wakati mkutano wa mwaka uliowakutanisha pamoja wakurugenzi na watendaji wa mashirika yanayotoa huduma za kisheria kwa lengo la kupanga mikakati ya namna ya kuwafikia wananchi wengi zaidi na kuwapatia msaada wa kisheria.
Washiriki katika mkutano wa mwaka uliowakutanisha pamoja wakurugenzi na watendaji wa mashirika yanayotoa huduma za kisheria wakifatilia mkutano jijini Dodoma
Msajili wa mashirika yanayotoa msaada wa sheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Bi Felistas Mushi akiwa katika picha ya pamoja na wakurugenzi na watendaji wa mashirika yanayotoa huduma za kisheria katika mkutano wa mwaka ulioandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Legal Services Facility – LSF jijini Dodoma.

STAR MEDIA YAWAOMBA RADHI WATEJA WAKE KWA KUTOPATA CHANELI ZA BURE

$
0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

STAR Media (T) Ltd, imewaomba radhi wateja wake pendwa na umma kwa ujumla kwa kutopata chaneli za bure kwa muda sasa.

Taarifa iliyotolewa  na Mkurugenzi Mtendaji Star Media(T)Wang Xiaobo amesema leo kuwa hiyo imesababishwa na kukosekana kwa elimu na mawasiliano mazuri kuhusu aina ya tofauti za dikoda (ving’amuzi) tulizonazo, ambayo yamesababisha kwa wateja wao kuendelea kulipia chaneli za bure.

"Tunapenda kuwafahamisha wateja wetu kuwa ziko aina mbili za dikoda, ya kwanza ni ile ya Chaneli za bure (FTA) ambayo mteja halazimiki kila mwezi ili kutazama chaneli za bure.

"Na nyingine ni ya chaneli za kulipia, ambayo mteja atatakiwa kulipia kifurushi chake kila mwezi," amesema

Ameongeza kwa wateja wapya, dikoda (ving’amuzi) hizo zinapatikana kwenye maduka yao pamoja na mawakala wao, lakini kwa wateja ambao tayari wameshanunua dikoda (ving’amuzi) za kulipia wanaweza kubadilisha dikoda (ving’amuzi) zao kuwa FTA kwa kutembelea katika ofisi zetu na kupata utaratibu.
 Amesisitiza Star Media (T) Ltd, itaendelea kuzingatia masharti yote ya leseni, pia inaufahamisha umma kwamba imekubali kufuata na kutekeleza maagizo ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikiwamo kulipa faini ambayo tayari imeshaanza.

Pia wanawafahamisha umma wa watanzania kwamba sasa wanaweza kuendelea kufurahia chaneli za bure na huduma zetu kwa ujumla.

MTENDAJI MKUU TFS AELEZEA JITIHADA WANAZOFANYA KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU KULINDA NA KUHIFADHI MISITU

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

MTENDAJI Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Profesa Dos Santos Silayo ameelezea jitihada mbalimbali zinazofanyika nchini katika kulinda na kuhifadhi uoto wa misitu asili nchini.

Amesema hayo akiwa eneo la Msitu wa Kazimzumbwi wilayani Kisarawe mkoani Pwani wakati wa uzinduzi wa jitihada za Tanzania kuungana na nchi nyingine za Afrika katika kuhifadhi na kuendeleza hifadhi za misitu

Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo alikuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Japhet Hasunga pamoja na mwenyeji wao Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo ambaye alitumia nafasi hiyo kuelezea jitihada zinazofanyika kulinda misitu iliyopo wilayani kwake.

Akizungumza kwenye tukio hilo Profesa Silayo amefafanua Tanzania ni mwanachama wa Afrika katika juhudi hizo za kuhifadhi na kuendeleza hifadhi za Misitu African Forest Landscape Restoration Initiatives (AFR100).

Amesema lengo kuu la juhudi hizo ni kurejesha Uoto wa Asili kwa bara la Africa kwa hekta millioni 100 ifikapo mwaka 2030 na kwamba mkakati huo ulijadiliwa na kukubalika katika mkutano wa 14 wa Misitu uliofanyika nchini Afrika Kusini mwaka 2015.

Ambapo uliliona suala hili na kuanzisha mkakati huu wa Nchi za Afrika. Pia mkatati huo wa Afrika ni kwa ajili ya kuchangia mkatati wa Dunia (Bonn Challenge) wenye lengo la kurejesha uoto wa asili kwa hekta milioni 150 ifikapo mwaka 2020 na hekta milioni 350 ifikapo mwaka 2030.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Profesa Does Santos Silayo(kulia) pamoja na Mkurugenzi mkazi wa WWF Tanzania Dk.Amani Ngusaru(kushoto) wakisaini mkataba wenye lengo la kulinda na kuhifadhi msitu wa Kazimzumbwi ,Ruvu Kusini na Vikindu wilayani Kisarawe.Wanaoahuhudia ni Mkuu wa Wilaya Kisarawe Jokate Mwegelo na Naibu Waziri Wizara ya Maliasili na Utalii Japhet Hasunga.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Profesa Does Santos Silayo(kulia) akiwa ameshikana mkono na Mkurugenzi mkazi wa WWF Tanzania Dk.Amani Ngusaru baada ya kusaini mkataba wenye lengo la kulinda na kuhifadhi msitu wa Kazimzumbwi ,Ruvu Kusini na Vikindu wilayani Kisarawe.Wanaoahuhudia ni Mkuu wa Wilaya Kisarawe Jokate Mwegelo na Naibu Waziri Wizara ya Maliasili na Utalii Japhet Hasunga.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Profesa Does Santos Silayo(kulia) pamoja na Mkurugenzi mkazi wa WWF Tanzania Dk.Amani Ngusaru wakiwa wameshika mikataba mara baada ya kusaini mkataba wenye lengo la kulinda na kuhifadhi msitu wa Kazimzumbwi ,Ruvu Kusini na Vikindu wilayani Kisarawe.Wanaoahuhudia ni Mkuu wa Wilaya Kisarawe Jokate Mwegelo na Naibu Waziri Wizara ya Maliasili na Utalii Japhet Hasunga. 


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

BONDIA VICENT MBILINYI KUPAMBANA NA SAIDI KIDEDEA SEPTEMBA 15 UWANJA WA NDANI WA TAIFA

$
0
0
Na Mwandishi Wetu

BONDIA Vicent Mbilinyi amesaini mkataba wa kuzipiga na Saidi Mpoma ‘Kidedea’ septemba 15 katika uwanja wa ndani wa Taifa

akizungumza mara baada ya kusaini mkataba uho mbilinyi amesema kuwa atafanya mazoezi ya kutosha ili aweze kushinda kwa kuwa ngumi kwake ni kazi kazi na kuwataka mashabiki wake wote kujitokeza siku hiyo kushudia mpambano uho kwani ato waangusha amejipanga vizuri

Nae Saidi Kidedea amesema anashukuru kwa kupata mpambano uho kwana yeye siku zote achaguwi mabondia kwake yoyote anaekuja mbele yake kazi anayo na amepanga kummaliza mpinzani wake katika raundi za awali ili asiwachoshe mashabiki anao wategemea

aidha ameomba wapenzi wa mchezo wa masumbwi waje kumsapoti kwani ato wahangusha ata kidogo

Na mratibu wa mpambano huo Rajabu Mhamila ‘Super D’ amesema siku hiyo kutakuwa na mapambano makubwa ambapo bondia Fred Sayuni atapambana na Haidari Mchango wakati George Dimoso atavaana na Abdallah Pazi ‘Dulla Mbabe’ na Imani Mapambano ataoneshana umwamba na Paul KamataSadiki Momba atavaana na Mohamed Kashinde na bondia machachari Tonny Rashidi atavaana na Said Zungu Ramadhani Shauri atakumbana na Saidi Amani

Mbali na mipambano hiyo ya ngumi siku hiyo pia kutakuwa na burudani mbali mbali za muziki
Mabondia Saidi Mpoma ‘Kidedea’ kushoto akitunishiana misuli na Vicent Mbilinyi baada ya kusaini mkataba wa kuzichapa Septemba 15 katika uwanja wa ndani wa Taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS

MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA KILELE CHA SHEREHE YA WAKIZIMKAZI

$
0
0


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi kombe Nahodha wa Timu ya Wavuta Kamba ya Wanawake ya Kizimkazi Dimbani Bi. Nasma Khamis mara baada ya kuibuka washindi dhidi ya timu ya Kizimkazi Mkunguni ikiwa sehemu ya sherehe ya siku ya Wakizimkazi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Hassan Khatibu Hassan wakiangalia mkoba wa wanawake uliosanifiwa na ukili waliotembelea maonyenyo ya wanawake na vijana wajasiriamali wakati wa kilele cha sherehe ya Siku ya Wakizimkazi iliyofanyika Kizimkazi Wilaya ya Kusini mkoa wa Kusini Unguja. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Kundi la Kusini Star likitumbuiza wimbo maalum wa kujali haki za mtoto haswa wa kike wakati wa kilele cha sherehe ya Siku ya Wakizimkazi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi wa wilaya ya Kusini kwenye kilele cha sherehe ya Siku ya Wakizimkazi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Timu wa Wavuta Kamba ya Wanawake ya Kizimkazi Dimbani waangalia mchezo huo baada ya kuishinda timu ya Kizimkazi Mkunguni kwenye mchezo  uliochezwa wakati wa kilele cha sherehe ya Siku ya Wakizimkazi iliyofanyika kizimkazi Wilaya ya Kusini mkoa wa Kusini Unguja. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Wakazi wa Kizimkazi wakipimana msuli kwenye mchezo wa kuvuta kamba ikiwa sehemu ya kilele cha sherehe ya Wakizimkazi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) .HABARI ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

SERIKALI YAZIFUTIA KODI TAASISI ZINAZOTOA HUDUMA

$
0
0
Na. Hassan Maabuye, Wizara ya Ardhi

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amesema serikali imefuta kodi ya pango la ardhi katika majengo na maeneo yote ya taasisi ambazo zinatoa huduma katika jamii bila kufanya biashara na kuzalishi faida. 


Waziri Lukuvi amesema hayo wakati alipofanya ziara ya utatuzi wa migogoro ya ardhi ya wakazi wa jiji la arusha ambapo ametoa agizo kwa maafisa wote wanaohusika na ukusanyaji wa kodi ya pango la ardhi kuziondoa katika orodha ya madeni taasisi binafsi, za dini, za serikali na mashirika yote ambayo hayazalishi faida.

Hata hivyo waziri Lukuvi amesema kwamba sheria hiyo imeanza kutekelezwa kuanzia tarehe 1 julai 2018 ambapo Serikali kupitia Bunge imeridhia kuondolewa kodi ya pango la ardhi taasisi za elimu, shule za msingi, sekondari, vyuo, vituo vya afya, hospitali, taasisi za umma na taasisi za dini kama misikiti na makanisa ambayo yalikuwa yanalipa kodi hiyo.

Pamoja na msamaha huo wa kodi Waziri Lukuvi amewaagiza wakurugenzi wote wa halmashauri kote nchini kupima maneo yanayotoa huduma kwa jamii ili kuitambua mipaka ya shule, zahanati na maeneo mengine na kuzipatia hati miliki za ardhi zitakazo wawezesha kutambua mipaka ya maeneo hayo lakini taasisi hizo hazitalipa kodi tena.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (katikati) akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jery Muro alipotembelea jiji la Arusha kwa ajili ya utatuzi wa migogoro ya ardhi. 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiongea wakati wa mkutano na wakazi wa jiji la Arusha, kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Fabian na kulia ni Katibu Tawala Msaidizi Miundombinu jiji la Arusha. 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiongea na wakazi wa jiji la Arusha wakati wa mkutano wa utatuzi wa migogoro ya ardhi. 


WANANCHI 2,587 KIJIJI CHA LUPEMBELWASENGA WAKABIDHIWA HATI MILIKI ZA KIMILA

$
0
0
NA FREDY MGUNDA IRINGA.

Wananchi 2,587 wa kijiji cha Lupembelwasenga Wilaya ya Iringa Vijijini wamekabidhiwa Hati za Hakimiliki ya Kimila chini ya Mradi wa LTA Uliofadhiliwa na wadau kutoka Marekani wa Feed the Future USAID.

Akizungumza wakati wa kukabidhi Hati hizo Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi  Angelina Mabula alisema kuwa katika miaka miwili ya utekelezaji,Mradi huo umeweza kutoa jumla ya Hati za Hakimiliki ya Kimila 35,286 katika vijiji 26.Mabula alisema kuwa hati hizo zitawasaidia kutenga maeneo kwa ajili ya matumizi mbalimbali kwa kuzingatia uwezo wa ardhi kuhimili idadi hiyo na kasi ya ongezeko la watu na mifugo kwa miaka mingi ijayo.

Mabula aliongezea kuwa,hatua hiyo itasaidia kupunguza migogoro ya ardhi kwa kuimarisha usalama wa miliki za ardhi na kuongeza thamani ambayo itawawezesha hata kukopesheka katika taasisi za kifedha zikiwemo benki.“Usajili wa ardhi ni muhimu kwasababu unaongeza ulinzi wa umiliki wa ardhi, unawezesha uwekezaji, unaongeza thamani ya ardhi na unapunguza migogoro ya ardhi,” alisema Mabula

Mabula aliupongeza mpango huo akisema utasaidia kupunguza eneo kubwa la ardhi ya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ambayo haijapimwa.Aidha Mabula aliwaomba Feed The Future wautanue mradi huo angalau ufike umalize kupima vijiji vyote vya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa  huku akivikumbusha vijiji vyote vya wilaya hiyo kuendelea kutoa ushirikiano kwenye miradi ambayo inasaidia kukuza maendeleo ya nchi. 
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi  Angelina Mabula akikabidhi hati za kimira kwa wananchi wa kijiji cha Lupembelwasenga Wilaya ya Iringa Vijijini  mkoani Iringa
 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi  Angelina Mabula  akiwa na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela,mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi CCM Ritta Kabati pamoja na viongozi wa LTA wakati wa ugawaji wa hati za kimila
Picha ya pamoja.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>>

Mradi wa kutoa elimu ya matumizi ya mitandao kwa wanawake waanzishwa

$
0
0
Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Women at Web Tanzania imezindua mradi maalumu wenye lengo la kutoa mafunzo ya matumizi ya mitandao ili kuongeza uwepo wa kundi hili mitandaoni.

Mradi huo unaofadhiliwa na Shirika la DW Akademie la nchini Ujerumani una lengo la kuhamasisha matumizi bora ya mitandao ikiwamo kuongeza  mijadala ya maendeleo kwa wanawake katika mitandao.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi huo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam, mmoja wa viongozi wa mradi huo Carol Ndosi amesema kwamba moja ya shughuli zitakazofanyika katika uhamasishaji huo ni mafunzo kwa wanawake yanayohusu njia za kujilinda na vurugu za mitandao, kutambua fursa zilizopo mitandaoni pamoja na mambo mengine.

Alisema kuwa kwa sasa Tanzania hakuna takwimu zilizo wazi za udhalilishaji wa wanawake kwenye mitandao japokuwa wengi waliopo wameshakutana na aina ya udhalilishaji kwenye mitandao, hasa ya kijamii.
“Idadi ya watu wanaomiliki smart phone inaongezeka hivyo kuongeza hatari za wanawake kuwa wahanga wa unyanyasi katika platform hizo, kwa hiyo kupitia mradi huu, pamoja na kuhamasisha wanawake kuongezeka kutumia hii mitandao, tutawapatia mafunzo ya namna ya kujilinda ama kutambua wale wanataka kuwafanyia ukatili.

“Lengo letu ni kuhakikisha kuwa kwa kuwa bado tuna ‘gap’ kubwa sana la wanawake kushiriki katika mijadala ya maendeleo nje ya mitandao, basi watumie fursa za mitandao kushiriki mijadala hiyo na kujiletea maendeleo,” alisema Ndosi.
Kwa kuanzia, mradi huo utaendesha mafunzo katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na pia kwa upande wa Zanzibar.

TAARIFA KWA UMMA: UANACHAMA KATIKA MFUKO WA PSSSF NA NSSF

$
0
0
Mfuko wa PSSSF unaoundwa chini ya kifungu cha 4 cha Sheria ya PSSSF umeanza rasmi Tarehe 1 Agosti, 2018. Mfuko huu ni mahsusi kwa ajili ya Watumishi wa Sekta ya Umma. Mfuko wa NSSF kwa upande mwingine umekuwa Mfuko mahsusi kwa ajili ya Wafanyakazi katika Sekta Binafsi (Private Sector) na Sekta ya isiyo rasmi (Informal Sector).

Hivyo, kwa mujibu wa Kifungu cha 5 cha Sheria ya PSSSF kikisomwa pamoja na Kifungu cha 6 cha Sheria ya NSSF mambo yafuatayo yanapaswa kuzingatiwa:-
(i)Kuanzia Tarehe 1 Agosti, 2018 waliokuwa Wanachama wa Mifuko iliyounganishwa yaani PPF, PSPF, LAPF na GEPF wamehamishiwa katika Mfuko wa PSSSF na wataendelea kuwa Wanachama na kuchangiwa katika Mfuko wa PSSSF. 

(ii)Wanachama wote wa Mfuko wa NSSF ambao wanatoka (Sekta Binafsi na Sekta ya Umma) wataendelea kuwa wanachama wa Mfuko huo na michango yao itaendelea kuwasilishwa katika Mfuko wa NSSF.

(iii)Watumishi  wapya watakaoajiriwa kuanzia Tarehe 1 Agosti, 2018 katika Utumishi wa Umma, Mashirika ya Umma na makampuni yote ambako Serikali inamiliki zaidi asilimia 30 ya hisa watatakiwa kusajiliwa katika Mfuko wa PSSSF.

(iv)Wafanyakazi watakaoajiriwa katika Sekta Binafsi (Private Sector) au kujiajiri katika Sekta isiyo rasmi (Informal Sector) watasajiliwa katika Mfuko wa NSSF kwa kuzingatia utaratibu utakaowekwa na Mfuko wa NSSF.

Tunapenda kuwaondoa wasiwasi Wanachama, Wadau wote wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii na Umma kwa ujumla kuwa huduma zote za Hifadhi ya Jamii zilizokuwa zikitolewa na Mifuko iliyounganishwa zinaendelea kutolewa kama kawaida katika Ofisi zile zile. Endapo utahitaji ufafanuzi zaidi tafadhali msisite kuwasiliana na Mamlaka (SSRA).

Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano
Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) 
S.L.P 31846
Tovuti: www.ssra.go.tz
DAR ES SALAAM
09/08/2018

KUTONYONYESHA WATOTO MAZIWA YA MAMA PEKEE KWA MIEZI SITA KUMECHANGIA UDUMAVU

$
0
0
Na Grace Gwamagobe,  Songwe

Ongezeko la hali ya udumavu Mkoani Songwe inachagizwa na kuwa ni asilimia 25 pekee ya akina mama wote wanaojifungua ndio huwanyonyesha watoto wao maziwa ya mama pekee kwa muda wa miezi sita.

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe Dkt. Kheri Kagya ameeleza kuwa udumavu mkoani hapa ni asilimia 37.7 ikiwa na maana kuwa kati ya watu 100, 37 wanatatizo la udumavu kiwango ambacho ni kikubwa licha ya Mkoa Songwe kuwa na Vyakula vya kutosha.

“Moja ya sababu kubwa ya ongezeko la udumavu Mkoani kwetu ni kutokana na akina mama wanaojifungua kutowanyonyesha watoto wao maziwa pekee kwa kipindi cha miezi sita, hali hii huwafanya watoto kukosa virutubisho muhimu katika hatua za awali za ukuaji”, amesema Dkt Kagya.

Ameongeza kuwa maziwa ya mama hujenga afya imara kwa watoto hivyo akina mama wanaojifungua wazingatie ushauri wa wataalamu wa afya wa kunyonyesha watoto maziwa ya mama pekee kwa miezi sita, na kisha kuendelea kunyonyesha na vyakula vingine mbadala mpaka mtoto afikishe umri wa miaka miwili.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe Dkt. Kheri Kagya akitoa zawadi kwa akina mama wa mfano walioweza kunyonyesha watoto wao maziwa pekee kwa muda wa miezi sita wakati wa maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji yaliyofanyika Halmashauri ya Mji wa Tunduma.
Akina mama wa mfano walioweza kunyonyesha watoto wao maziwa pekee kwa muda wa miezi sita wakiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali wanaojishughulisha na afya ya mama na mtoto mkoa wa Songwe.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>

Waziri Mwakyembe atoa ufafanuzi kuhusu isimbuzi visivyoonesha chaneli za ndani

$
0
0
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (katikati) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa ufafanuzi juu ya visimbuzi visivyoonesha chaneli za ndani mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Afisa Mwandamizi Mkuu wa Sheria toka Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) Dk. Philip Filikunjombe na kulia ni Afisa Mwandamizi Mkuu wa Masuala ya Utangazaji toka mamlaka hiyo Bw. Andrew Kisaka.

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati akitoa ufafanuzi juu ya visimbuzi visivyoonesha chaneli za ndani mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

Afisa Mwandamizi Mkuu wa Masuala ya Utangazaji toka Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) Bw. Andrew Kisaka (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (katikati) alipokutana na waandishi wa habari mapema hii leo jijini Dar es Salaam ili kutoa ufafanuzi juu ya visimbuzi visivyoonesha chaneli za ndani, kushoto ni Afisa Mwandamizi Mkuu wa Sheria toka Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) Dk. Philip Filikunjombe.Picha na –Eliphace Marwa (MAELEZO)

Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images