Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 242 | 243 | (Page 244) | 245 | 246 | .... | 3270 | newer

  0 0

  the EALA sittings ended yesterday with legislators passing a crucial Bill and adjourning debate on another.

  The Bill that sailed through the House is the East African Community Holidays Bill 2013.  With the passing of the Bill, East Africans are expected to observe the east African Community day on November 30th as a Public Holiday in all Partner States.

  If the EAC Heads of State give a nod to the Bill, then the day shall be an opportunity to reflect on the vision of integration and to celebrate the progress made and on-going activities and programmes to further the objects of the Treaty.

  At the same time, the official celebrations shall be held in rotational order in the Partner States, celebrating African renaissance and honouring citizens who have championed the cause of integration. The Bill read by Hon Mike Sebalu on behalf of Hon Abubakar Zein Abubakar hopes to provide a legal basis for holidays in the Community and makes provision for remuneration of employees who may be required to work on a holiday and situations where the said holiday falls on a Sunday.  

  The Bill recognises all the independence days celebrated in the Partner States as days off for the staff of all organs and institutions of the Community.  The same applies for the religious holidays currently observed including: Good Friday and Easter Monday as well as the Eidd El-Haj, Eid-Ul-Azha and Eidd-El-Ul.  The International Women’s Day commemorated globally on March 8 shall also be kept and observed by the EAC.

  At debate time, the motion was supported by Hon Patricia Hajabakiga, Hon Dora Byamukama, Hon Peter Mathuki and the Chair of the Council of Ministers, Hon Shem Bageine.


  The debate was preceded by the tabling of the Report by the Committee on Regional Affairs and Conflict Resolution.  The Committee considered the Bill and incorporated a number of views and proposals for consideration and adoption.The Bill now awaits assent from the EAC Heads of State before it becomes Community law.

  Meanwhile, the debate on the Disaster Risk Reduction and Management Bill, 2013 was adjourned under Rule 31 of the Rules of Procedure following a request by the Chair of the Council of Ministers, Hon Shem Bageine.  
  The Bill sponsored by Hon Patricia Hajabakiga seeks to provide a legal framework for intervention and assistance for people affected by climate change and natural hazard-related disasters.

  It further anticipates the protection of the natural environment through integration of comprehensive DRR and Management practices in the Community and the creation of a regional mechanism that would enable  a timely intervention in disaster situations.

  The Council according to Hon Bageine hopes to re-introduce the Bill with changes as may be necessary once the Protocol on Peace and Security is accomplished.

  0 0
 • 08/30/13--20:00: ngoma azipendazo ankal
 • Ngoma ya Los Lobos ya 'La Bamba' ilibamba kinoma

  0 0

   Elizabeth Michael Aka Lulu akitoa Shukrani kwaWadau wote waliojitokeza katika Usiku wake wa uzinduzi wa Filamu yake Mpya iitwayo Foolish Age uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City Usiku wa Kuamkia Leo
   Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Proin Promotions Limited Geofrey Lukaza (Kushoto) akiwa na Waifu wake Groly Lukaza (katikakati) pamoja na Pedeshee Mamaa Ng'onzi wakijiachia Mbele ya Kamera ya Lukaza Blog usiku wa kuamkia Leo katika uzinduzi wa Filamu ya Lulu iitwayo Foolish Age katika Ukumbi wa Mlimani City chini ya kampuni ya Proin Promotions Limited
   Lady Jay Dee aka Anaconda akitoa Burudani katika Uzinduzi wa Filamu mpya ya Lulu iitwayo Foolish Age iliyotengenezwa na Kampuni ya Proin Promotions Limited, Lady Jay Dee akiwa pamoja na Machozi Band walitoa Bururdani Safi Sana katika Uzinduzi huo Uliofanywa na Kampuni ya Proin Promotions Limited katika Ukumbi wa Mlimani City usiku wa Kuamkia Leo
  Msanii Barnaba akitoa burudani katika uzinduzi wa Filamu mpya ya Lulu uliofanya na Kampuni ya Proin Promotions Limited katika ukumbi wa Mlimani City Usiku wa Kuamkia leo

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0  0 0

  Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda akiwasisitizia wahitimu na wageni (hawako pichani) waliofika katika mahafali ya kwanza na ya pili ya Chuo cha Ufugaji Nyuki Tabora kuwa serikali lazima ijenge Chuo KIkubwa Cha Ufugaji Nyuki Tabora.

  SERIKALI imeahidi kujenga chuo kikubwa cha mafunzo ya ufugaji nyuki katika eneo la Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki mkoani Tabora ili kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya kwanza Barani Afrika katika uzalishaji wa mazao yatokanayo na nyuki.

  Ahadi hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda aliyekuwa Mgeni Rasmi katika mahafali ya kwanza na ya pili ya Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji nyuki Tabora alipokuwa akiwahutubia wahitimu kabla ya kuwatunuku vyeti na zawadi.

  Mhe. Pinda alisema pamoja na mapungufu ya chuo hicho yaliyotokana na tabia ya kuhamisha mafunzo yake mara kwa mara kwenda kwenye vyuo mbalimbali vya Wizara ya Maliasili na utalii nchini, chuo kina umuhimu mkubwa kutokana na kuwa ni chuo pekee katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika.

  “Siku za nyuma chuo kiliweza kupata watu kutoka nchi za nje kuja kujifunza, hivyo serikali haiwezi kukiacha solemba! Kama tumeweza kujenga Chuo kikubwa cha Serikali za Mitaa, Hombolo kinachotufanya tushindwe kujenga chuo kikubwa hivi ni nini? Kwamba hatuoni thamani yake? Si kweli, miaka kumi ijayo thamani yake itaonekana tu,” alisema Mhe. Waziri Mkuu.

  Aliongeza kuwa, tatizo la kutoendelezwa kwa chuo hicho wakati mwingine kunatokana na viongozi kutojua kinachoendelea, hivyo aliomba uongozi kuwakilisha mpango mkakati wake ili serikali iweze kuipembua na kuona wapi pakuanzia.

  Aidha, Mhe. Pinda aliipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii kwa uamuzi wake wa kukirudisha Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki mkoani Tabora na kutoa onyo kwa yoyote atakayetaka kujaribu kukihamisha tena kutofanya hivyo ili serikali iweze kujipanga na kusonga mbele.

  Aliongeza kuwa, Tanzania ina hifadhi za misitu na maji ya kutosha inayotoa fursa ya kuzalisha asali nyingi, hivyo amewaasa wananchi kuchangamkia fursa hiyo ili kuiwezesha nchi kushika namba moja kwa nchi za Bara la Afrika zinazozalisha asali.

  “Tanzania hivi sasa inapitwa na Ethopia kwa uzalishaji asali, nchi ambayo haina misitu yakutosha, hili haliwezekani tuangalie mpango mikakati yetu. Ufugaji asali hauhitaji mtaji mkubwa, na soko lake ni la uhakika, tumshinde Ethiopia na hili linawezekana kama tutapanua mawazo yetu juu ya sekta hii,” alisema Mhe. Pinda.

  Kwa upande wake, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Khamis Kagasheki, alimshukuru Waziri Mkuu kwa moyo wake wakusimamia kidete sekta ya ufugaji nyuki nchini na kutoa fursa za ajira kwa wananchi wengi.

  Aidha, Mhe. Pinda alisisitiza kiu yake ya kuona Tanzania inazalisa asali nyingi kwa kuwaahidi wahitimu kuwapa zawadi ya mizinga 100 endapo wataunga na kuunda kikundi cha ufugaji nyuki na kutumia elimu waliopata kuweza kujipatia kipato.

  Katika kusisitiza hilo Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Bi. Fatma Mwasa naye aliwahidi wahitimu ambao ni wakazi wa mkoa wake, kuunda vikundi vya watu waiopungua kumi kwa kikundi ili aweze kuwapatia mtaji wa mizinga.

  0 0


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,(katikati) akifuatana na ujumbe wake walipotembelea katikaa kituo cha ufugaji wa ngombe wa maziwa kwa Familia ya Bw.Captein Nchini Uholanzi katika ziara ya Kiserikali.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Frank Captein,wakati alipotembelea ndama wadogo jinsi wanavyolelewa katika famili ya BW.Captein,Nchini Uholanzi akiwa katika ziara ya kiserikali na ujumbe wake.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Frank Captein,namna ya utengeneza ji wa Jibini (Cheese)alipotembelea eneo hilo akiwa na ujumbe wake.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Mkurugenzi wa Kituo cha habari kwa wafugaji wa Ngo'mbe wa maziwa Reimond Van Gent,alipofika kuangalia familia ya ufugaji wa Ngo'mbe wa maziwa na utengenezaaji wa Jibini (Cheese) akiwa katika ziara nchini Uhiolanzi .
  Waziri wa Ardhi,Maji,Makaazi na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban,akitia saini na Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Mafuta ya Shell ya uholanzi na Serikali za Afrika Mashariki Axel Knospe,(kushoto)makubaliano ya ushiriano katika sekta ya gesi na mafuta katika ukumbi wa ofisi ya kampuni hiyo Mjini Uholanzi alipokuwa katika ziara ya Kiserikali,ujumbe ulioongozwa na Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dk.AliMohamed Shein.
  Waziri wa Ardhi,Maji,Makaazi na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban,akibadilishana hati ya makubaliano baada ya kutia saini na Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Mafuta ya Shell ya uholanzi na Serikali za Afrika Mashariki Axel Knospe,(kushoto)makubaliano ya ushiriano katika sekta ya gesi na mafuta katika ukumbi wa ofisi ya kampuni hiyo Mjini Uholanzi alipokuwa katika ziara ya Kiserikali,ujumbe ulioongozwa na Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dk.AliMohamed Shein.[Picha na Ramadhan Othman,Uholanzi.]

  0 0  VIDEO YA MPAMBANO KATI YA MADA MAUGO NA THOMAS MASHALI ITAWAJIA BAADAE

  0 0

  Kundi la kwanza la wasanii watakaotumbuiza katika tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2013 limewasili mkoani Kigoma kwa ajili ya onyesho hilo. Wasanii hao 8 ni kati ya 12 watakaopanda katika jukwaa moja uwanja wa Lake Tanganyika siku ya Jumamosi.

  Kundi la pili la wasanii ambao ni Profesa Jay, Diamond, Lady Jaydee na Barnaba wanatarajiwa kuwasili siku ya Jumamosi asubuhi.

  Baada ya kupata mlo wa mchana ulioandaliwa na mwenyeji wao ambaye ni Doctor Gerrard Mipango wasanii hao walipata nafasi ya kutembelea makumbusho ya Doctor Livingistone yaliyoko Ujiji na kujionea historia mbalimbali ya mzungu huyo anayetambuliwa kama mvumbuzi wa Ziwa Tanganyika na pia kuona maeneo biashara ya utumwa ilipokuwa ikifanyika na kujifunza kuhusu asili ya wenyeji wa Mkoa wa Kigoma.
  Wasanii wakiwa katika eneo la mbele ya makumbusho ya Doctor Livingstone.
  Wakali wa muziki katika picha ya pamoja na wenyeji wao mkoani Kigoma.
  Mwasiti akisoma njia zilizotumika wakati wa biashara ya utumwa.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI 

  0 0

  Meneja Kiongozi,Uhusiano NSSF Makao makuu jijini Dar,Eunice Chiume  akizungumza mapema leo kwenye semin ya FURSA iliyofanyika kwenye ukumbi wa Pentecoste Ligula B,uliopo mkabala na Kituo cha Vijana Mtwara,kulia ni Meneja wa NSSF mkoani Mtwara Bwa.Stanley Mullanzi na kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Vipindi Clouds Media Group,Ruge Mutahaba pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Iramba (ambaye pia ni mzaliwa wa Newala mkaoni Mtwara),Mh.Yahya Nawanda wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa ukumbini humo.Semina hiyo inaratibiwa na Clouds Media Group na kufadhiriwa na NSSF,Lake Oil,Zantel,MaxMalipo na wengineo imewashirikisha wadau mbalimbali wa Mtwara na vitongoji vyake wakiwemo wasanii wa muziki wa kizazi kipya.
    Baadhi ya Wakazi wa Mji wa Mtwara na vitongoji vyake wakifuatilia kwa makini  yaliyokuwa yakijiri kwenye semina ya Fursa kwa Vijana iliyofanyika mapema leo ndani ya ukumbi wa  Pentecoste Ligula B,uliopo mkabala na Kituo cha Vijana mkoani Mtwara.
   Mkuu wa Wilaya ya Iramba (ambaye pia ni mzaliwa wa Newala mkaoni Mtwara),Mh.Yahya Nawanda akizungumza na wakazi wa mji wa Mtwara waliojitokeza kwa wingi kwenye semina ya Fursa kwa Vijana mapema leo,Mh.Yahya alizunguma mengi zikiwemo fursa mbalimbali zinazopatikana ndani ya mkoa wa Mtwara na Singida namna ya kuzifanyia kazi katika suala zima la kujikwamua na maisha. 
  Mkurugenzi wa Vipindi Clouds Media Group,Ruge Mutahaba  akihitimisha semina ya Fursa kwa Vijana mapema leo mchana,ndani ya ukumbi wa ukumbi wa Pentecoste Ligula B,uliopo mkabala na Kituo cha Vijana Mtwara,kulia kwake ni Meneja Kiongozi,Uhusiano NSSF Makao makuu jijini Dar,Eunice Chiume pamoja na Meneja wa NSSF mkoani Mtwara Bwa.Stanley Mullanzi.Semina ya Fursa kwa vijana tayari imekwishafanyika mikoa ya Tabora,Kigoma,Singida na sasa Mtwara.
  PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPO.COM

  0 0

   Mbunge wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Shrose Bhanji akizungumza kwenye hafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na Alicia K Designs kwa ajili ya kuwapa wanawake mbinu za ujasiriamali katika ukumbi wa Mezaluna jijini Arusha.
   Mbunge wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Shyrose Bhanji (wa pili kulia) akiwasha Mshumaa, ishara ya upendo wakati wa hafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na Alicia K Designs. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Alicia Matasia, Mwanamitindo ambaye ni mke wa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Faraja Kota Nyalandu na Mjasiriamali wa jijini Arusha, Isabela Mwampamba.
   Mbunge wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Shyrose Bhanji (wa pili kulia) na Mwanamitindo, Faraja Kota Nyalandu wakikata Keki wakati hafla ya Chakula cha jioni,iliyofanyika Mezaluna jijini Arusha.
   Mbunge wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Shyrose Bhanji (wa pili kulia) akimlisha Keki Mjasiriamali wa jijini Arusha, Isabela Mwampamba wakati wa hafla ya usiku iliyoandaliwa na Alicia K Designs, shoto ni Mkurugenzi wa taasisi hiyo,Alicia Matasia na Mwanamitindo, Faraja Kota Nyalandu
   Burudani ya nguvu ilikuwepo kuwafanya wasichana na wanawake waliohudhuria kuburudika vilivyo.
  Mkurugenzi wa Alicia K Designs, Alicia Matasia akitoa neno la shukrani kwa wageni waliofika kwenye hafla hiyo.

  0 0

   Taswira za askari wa jadi wa jimbo la Tyrol huko Alpbach nchini Austia wakiingia kwa gwaride rasmi lililoandaliwa kwa heshima ya Rais Jakaya Kikwete aliye katika mkutano wa Kamisheni ya Ulaya mjini humo. Historia ya askari hawa, wanaojulikana kama Schuetzenkompanie, inakwenda miaka ya 1810 wakati wa vita na watu wa Bavaria. Soma historia yao BOFYA HAPA
   Sungusungu hao wakiendelea kuwasili
   Kila mmoja ana gobole lililotengenezwa kienyeji
   Watoto kwa wakubwa wamevutiwa na Sungusungu hao
   Gwaride rasmi
   Mdau anajiunga na Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Austria Mhe Heinz Fischer (katikati), Rais wa Kamisheni ya Ulaya Mhe Jose Manuel Barroso (wa pili kushoto), Rais wa Mkutano wa Alpbach Dr Franz Fischer (kushoto) pamoja na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akifuatiwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Profesa Rwekaza Mukandala

  0 0
 • 08/31/13--06:46: Article 6

 • You are cordially invited to a fashion showcase to present a collection of upcoming Tanzanian designers who will be given the opportunity to participate in the International Fashion Showcase 2014 in conjunction with London Fashion Week Feb 2014.
  This will be an elegant and exquisite night, hosted by TAWA and the Tanzania High Commission, London, at Tanzania House in Bond Street.


  Venue: Tanzania House, 3 Stratford Place, W1C 1AS

  Date: Saturday 7thSeptember 2013

  Time: Doors will open at 6pm


  This is a TICKET ONLY event. Tickets must be bought online, and brought to the event. Tickets will not be sold on the door.


  The event can be viewed Facebook using this link:


  All event information and tickets are available on:


  Limited parking is available on roads surrounding the venue. Parking is free from 6.30pm on single yellow lines and free from 4.30pm in selected marked bays. The venue is opposite Bond Street Station which is on the Jubilee Underground Line.


  For more information email:

                                                                                  

  Thank you and we hope to see you at this amazing event!  If you or anyone you know is an upcoming Tanzanian fashion designer interested in taking part in the Fahari Passion Showcase for the chance to be chosen to take part in the International Showcase at LFW 2014, contact TAWA at info@tawa-uk.com.


  0 0

  Na Abdulaziz Video,Dodoma

  WAKULIMA wa zao la korosho nchini wametakiwa kubadili mitazamo yao kuona zao hilo kuwa la kudumu badala ya kuliona la kujikimu kwa muda na kusababisha kushuka kwa uchumi wao, na kuendelea kuwa masikini, kila mwaka.

  Hayo yamebainishwa na waziri wa Kilimo, chakula na ushirika Mhandisi Christopher Chiza wakati alipokuwa anafungua mkutano wa wadau wa korosho wa siku mbili ulifanyika mjini Dodoma.

  Chiza aliyasema hivi sasa za la korosho linazidi kupanuka kiuzalisha kwa kuongezeka kutoka wilaya 34 hadi 41 na mikoa tisa mipya inayolima zao hilo Mbeya, Iringa,Njombe, Morogoro,Dodoma Singida Alisema kuwa zao hilo bado halijaweza kutoa tija kwa wakulima, kwa hiyo aliwataka watendaji kutumia vyema kikao hicho kujadili kwa kirefu juu kuleta mabadiliko kwa wakulima na kuondokana na umasikini.

  Waziri Chiza alifananisha na mazao mengine ya kudumu kama, Kahawa, migomba ya ndizi, Pamba ambayo yaliweza kuleta sura nzuri ya kiuchumi kwa wakulima wa mazao hayo.

  Hata hivyo aligusia swala zima la ubanguaji wa zao la Korosho, kuwepo na jopo maalumu ambalo litaweza kukaa pamoja na kuhakikisha zao hilo linabanbuliwa nchini.

  Aliongeza korosho inayosafirishwa ghafi inasababisha hali ya wakulima kuendelea kuwa masikini.

  Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania Anna Abdallah alisema kuwa viwanda bado vinashikiliwa na wafanyabaishara wabangue hapa hapa nchini.

  Alisema kuwa korosho ghafi soko lake liko sehemu moj tu ni nchini india jambo linalosababisha kuleta mgongano wa kimaslai kati ya wanunuzi watendaji wa sekta ya ushirika na walimu
  Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika,Eng. Christopher Chiza akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa korosho wa siku mbili ulifanyika mjini Dodoma.
  Baandi ya Wajumbe wakiwa kwenye mkutano huo.

  0 0

  Mshindi wa taji la Taifa la Miss Utalii Tanzania 2012/2013, Hadija Saidi Juma Mswaga, ambaye pia ni Miss Utalii Morogoro 2012/13, ataondoka nchini 28-9-2013 kwenda nchini Equatorial Guinea, ambako Fainali za Dunia za Miss Tourism World 2013/14 zinafanyika Tarehe 12-10-2013 katika ukumbi wa kimataifa wa Sipopo Conference Centre Malabo Equatorial Guinea. 

  Kwa mujibu wa Taarifa iliyo tolewa na Fredy Njeje, mkurugenzi wa Habari na Masoko wa Miss Tourism Tanzania Organisation (MTTO), jumla ya washiriki kutoka nchi 126 Duniani watashiriki katika mashindano hayo ya Dunia,ambayo mwaka Jana yalifanyika nchini Thailand ambapo mrembo Tatyana Maksimova kutoka nchini Urusi alishinda Taji la Miss Tourism World 2012/13.

  Hii itakuwa ni mara ya nne kwa Tanzania kushiriki mashindano hayo ya Miss Utalii Dunia, ambapo kila mwaka kuanzia mwaka 2005 tumeshinda mataji, Mataji hayo na washindi kutoka Tanzania katika mabano ni Miss Tuourism World 2005- Africa (Witness Manwingi – Tanzania), Miss Tourism World 2006 – SADC (Killy Janga – Tanzania), Miss Tourism World 2007 – Africa (Lillian Cyprian – Tanzania), Miss Tourism World 2008- Internet ( Lilly Kavishe – Tanzania) na Miss Tourism Model Of The World 2006 –Personality ( Witness Manwingi – Tanzania).

  Tangu mwaka 2008, Tanzania haikushiriki katika mashindano hayo kutokana na kutokana na kukosa wadhamini wa safari hizo na matatizo mengine ya kiufundi yaliyo pelekea mashindano hayo kutofanyika nchini tangu 2008- 2010. Njeje alisema kuwa, Miss Utalii Tanzania 2012/2013, Hajija Saidi Juma Msugwa, anajukumu zito zaidi ya washiriki wengine wote walio tangulia kwani anakazi ya kwenda kulinda heshima ya Tanzania na kudumisha rekodi ya Miss Utalii Tanzania ya kutokushindwa katika mashindano yoyote ya kimataifa na Dunia. Nae Miss Utalii Tanzania 2012/13, Hajija Saidi Juma Mswaga, amesema kuwa anatambua jukumu kubwa na zito alilonalo la sio kutangaza Utalii na Utamaduni wa Tanzania tu, bali kulinda heshima ya Tanzania na Mashindano ya Miss Utalii Tanzania ya kutowahi kushindwa katika mashindano yoyote ya kimataifa. “Nawaomba watanzania waniombee na kunipa ushirikiano wa hali na mali katika kufanikisha maandalizi yangu na safari ya kupeperusha bendera ya Taifa katika medani ya kimataifa”.

  Shindano la Miss Tourism World 2013, litarushwa na kuonyeshwa LIVE katika nchi zaidi 130 Duniani kote na kushudiwa na zaidi ya watazamaji 650 Milioni Duniani kote, huku washiriki wakipewa fulsa ya kuonyesha vivutio vya utalii vya nchi zao, kupitia vyombo mbalimbali vya habari vya Televisheni, Majarida na Mitandao.

  0 0

  Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo nchini (WAMA),mama Salma Kikwete (kulia) akizungumza na washiriki wa warsha ya utoaji Haki juu ya kutokomeza matumizi mabaya ya madaraka yanayoambatana na rushwa ya ngono mara baada ya kukabidhiwa kitabu cha mwongozo wa namna ya kushughulikia mashauri mbalimbali ya kisheria alichokabidhiwa na Rais wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania Mh. Jaji Engera Kileo leo jijini Dar es salaam.
  Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo nchini (WAMA) mama Salma Kikwete (kushoto) akizungumza jambo na Bi. Salome Anyoti Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya Jinsia, Usawa na Uwezeshaji wa Wanawake leo jijini Dar es salaam.
  Baadhi ya Washiriki wa warsha ya utoaji Haki juu ya kutokomeza matumizi mabaya ya madaraka yanayoambatana na rushwa ya ngono wakiwemo waheshimiwa Majaji wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa wakati wa warsha hiyo ya siku 1.
  Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo nchini (WAMA) , mama Salma Kikwete (kulia) akiagana na viongozi wa Chama Cha Majaji Wanawake Tanzania mara baada ya kufungua wa warsha ya siku 1 ya utoaji Haki juu ya kutokomeza matumizi mabaya ya madaraka yanayoambatana na rushwa ya ngono.
  Washiriki wa warsha ya utoaji Haki juu ya kutokomeza matumizi mabaya ya madaraka yanayoambatana na rushwa ya ngono wakiwa katika picha ya pamoja na mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) leo jijini Dar es salaam.Picha na Aron Msigwa - MAELEZO

  0 0

  Aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Judith Mtawali (kulia) ambaye amestaafu rasmi kwa mujibu wa sheria ya Utumishi wa Umma akikata keki wakati wa sherehe iliyoandaliwa na watumishi wa Idara ya Wakimbizi kwa ajili ya kumuaga na kumtakia maisha mema yenye mafanikio maishani mwake. Hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Michokeni Resort Centre, jijini Dar es Salaam.
  Watumishi wa Idara ya Wakimbizi wakipeleka zawadi zao kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Judith Mtawali ambaye amestaafu rasmi kwa mujibu wa sheria ya Utumishi wa Umma. Hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Michokeni Resort Centre, jijini Dar es Salaam.
  Aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Judith Mtawali ambaye amestaafu rasmi kwa mujibu wa sheria ya Utumishi wa Umma akizungumza kwa furaha kwa kuwashukuru watumishi wa Idara ya Wakimbizi kwa zawadi nyingi walizompa pamoja na kumtakia heri maishani mwake. Aidha, Mtawali aliwaomba watumishi hao waendelee kufanya kazi kwa uadilifu na hatimaye watakuja kufanikiwa maishani mwao. Hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Michokeni Resort Centre, jijini Dar es Salaam.
  Watumishi wa Idara ya Wakimbizi wakichukua chakula katika hafla hiyo iliyofanyika kwa ajili ya kumuaga aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Judith Mtawali ambaye amestaafu rasmi kwa mujibu wa sheria ya Utumishi wa Umma. Hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Michokeni Resort Centre, jijini Dar es Salaam.
  Aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Judith Mtawali (katikati waliokaa) ambaye amestaafu rasmi kwa mujibu wa sheria ya Utumishi wa Umma akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa idara hiyo mara baada ya kupokea zawadi mbalimbali kutoka kwa watumishi hao. Kulia (waliokaa) ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara hiyo, Harrison Mseke. Hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Michokeni Resort Centre, jijini Dar es Salaam. (Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

  0 0

  Bunge la Tanzania kupitia kamati yake ya PAC litakuwa mwenyeji wa Mkutano wa 10 wa Umoja wa kamati za Bunge za Hesabu za Serikali kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara (SADCOPAC) utakaofanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 2 hadi 7 Septemba, 2013.
  Mwenyekiti wa umoja wa kamati za Bunge za Hesabu za Serikali kutoka nchi za SADC (SADCOPAC) Mhe. Sipho Makama akiwaeleza waandishi wa Habari kuhusu kufanyika kwa Mkutano huo hapa nchini kuanzia tarehe 2 hadi 7 Septemba, 2013, jijini Arusha.
  Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ambaye pia ndiye mwenyeji wa Mkutano wa mwaka wa umoja wa kamati za Bunge za Hesabu za Serikali kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara (SADCOPAC) Mhe. Zitto Kabwe akifafanua jambio kuhusu mkutano wa SADCOPAC utakafanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 2 hadi 7 Septemba, 2013. Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua shamba la Kikundi cha vijana cha Igogo wilayani Igunga akiwa katika ziara ya siku tatu mkoani Tabora Agosti 31, 2013. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Vijana Utamaduni na Michezo, Ole Gabriel. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Bandari ya Zanzibar.
   Baadhi ya wajumbe wa Baraza Kuu la UVCCM kutoa Tanzania Bara wakitoka bandarini baada ya kuwasili mjini Zanzibar kwa ajili ya kikao cha Baraza hilo kitakachofanyika kesho, Afisi Kuu ya CCM, Kisiwandui
   Baadhi yao wakisubiriana kabla ya kupanda mabasi maalum yaliyoletwa bandarini kuwabeba
   Wajumbe wakiwa katika mabasi
   Wajumbe wakiwasili Afisi Kuu ya UVCCM Zanzibar
  Kikundi cga Bras Band cha UVCCM Zanzibar kikijifua kwa mazoezi kwa ajili ya mkutano wa kesho.Imetayarishwa na theNkoromo Blog

older | 1 | .... | 242 | 243 | (Page 244) | 245 | 246 | .... | 3270 | newer