Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110029 articles
Browse latest View live

WAZIRI MAKAMBA AUNGANA NA WANA KIZIMKAZI KUADHIMISHA SIKU YAO, ACHANGIA MIFUKO 50 YA SARUJI NA BATI 50

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba amehidi kutoa mifuko hamsini ya saruji na bati hamsini kama mchango wake katika ujenzi wa Shule ya awali ya Kizimkazi iliyopo takiriban kilomita 61 kutoka Mjini Unguja. 

Ahadi hiyo ameitoa hii leo Shehia ya Kizimkazi- Mkunguni katika Wilaya ya Kusini, Jimbo la Makunduchi katika maadhimisho ya Siku ya Kizimkazi. “Nawapongeza sana kwa hatua hii mliyofikia na utayari wenu wa kuwekeza katika miradi mikubwa hususan elimu ambayo ndio nguzo kuu” Makamba alisisitiza. 

Waziri Makamba amewataka wana Kizimkazi kuandaa utaratibu wa kutembeleana na kubadilishana uzoefu baina yao na vijiji vya Tanzania Bara ili kudumisha Muungano na kujenga ushirikiano zaidi. “Mwakani tuweke nguvu zaidi, tuwe na vikundi vya ngoma na sanaa mbalimbali kutoka upande wa pili wa Muungano pia tutaanda ziara ya mafunzo ili kwa pamoja muweze kubadilisha uzoefu” alibainisha Makamba. 

Aidha, Waziri Makamba amewakumbusha wana Kizimkazi kuuenzi na kuulinda Muungano kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho kwa kuwa Muungano haukuanzisha undugu bali Muungano umerasimisha undugu baina yetu, na wakubainisha kuwa changamoto za Muungano zinaendelea kutafutiwa ufumbuzi. 

Awali akitoa taarifa ya ujenzi wa Shule hiyo Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Kizimkazi Bi. Rehema Ramadhani amesema kuwa Shule hiyo imeanza kujengwa kwa nguvu za wananchi na baadae kuungwa mkono na wadau mbalimbali. Bi Ramadhani amebainisha kuwa kumalizika kwa ujenzi huo itakuwa ni faraja kubwa kwa wazazi na wanafunzi kutokana na sehemu finyu na hatarishi katika jengo la awali kwa kuzingatia kuwa Shule hiyo ipo mkabala na barabara kuu. 

Aidha, imebainika kuwa tangu kuanzishwa kwa sherehe hizo za ‘Siku ya Kizimkazi’ wakazi hao wamefanikwa kujenga ukumbi wa shule kwa ajili ya kufanyia mitihani, ukarabati wa nyumba ya daktari, ujenzi wa nyumba ya mwalimu pamoja na ujenzi wa shule ya awali ambayo leo hii jiwe la msingi limewekwa. 

Sherehe hizi za Siku ya Kizimkazi huadhimishwa kila mwaka mara moja kwa lengo la kuthamini maendeleo pamoja na changamoto zinazowakabili wananchi wa Mkoa huo na kutafuta mbinu mbadala za utatuzi. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Umoja wetu, Ushirikiano wetu na Mshikamano wetu ndio ngao yetu” 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba mara baada ya kuweka jiwe la Msingi wa ujenzi wa Shule ya awali ya Kizimkazi iliyopo Shehia ya Kizimkazi- Mkunguni katika Wilaya ya Kusini, Jimbo la Makunduchi –Unguja ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za siku ya Kizimzikazi. Katika kuchangia ujenzi huo Waziri Makamba atatoa mifuko 50 ya saruji na bati 50.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akisalimiana na watoto katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi wa Shule yao ya awali Kizimkazi. Kulia ni Mkurugenzi wa Uratibu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais – Zanzibar Bw. Khalid Hamran
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akihutubia wakazi wa Kizimkazi hii leo katika Shehia ya Kizimkazi- Mkunguni katika Wilaya ya Kusini, Jimbo la Makunduchi –Unguja ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za siku ya Kizimzikazi, sherehe zilizoenda sambamba na uwekekaji wa jiwe la msingi katika shule ya awali. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria na Utawala Bora Mhe. Haroun Ali Suleiman (katikati) akimkaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mhe. January Makamba kulia sherehe za Siku ya Kizimkazi, jimboni Makunduchi. 


Jacqueline Mengi apata tuzo ya ujasiriamali wa mwaka

$
0
0
Na Mwandishi wetu
Mfanyabiashara wa Samani anayeinukia kwa kasi nchini Jacqueline Mengi amenyakua tuzo za biashara za Stevie ya Mjasiriamali wa mwaka kategori ya uzalishaji kupitia kampuni yake ya Amorette Ltd.
Katika tuzo hizo sehemu ya uzalishaji (Manufacturing), tuzo ya dhahabu ya mjasiriamali ilienda kwa watengenezaji wa lishe Hauppauge, New York Marekani na ilienda kwa Jason Provenzano, ambaye ni mwasisi na ofisa mtendaji mkuu wake.
Jacqueline Mengi atakabidhiwa tuzo hiyo Oktoba 20 mwaka huu mjini London, Uingereza.
Tuzo za dhahabu, fedha na shaba zinatolewa baada ya ushindani mkali miongoni mwa washiriki 3,900 kutoka taasisi na watu binafsi wa mataifa zaidi ya 74.
Hizi ni tuzo za kimataifa zinazotolewa katika madaraja mbalimbali ya menejimenti, kampuni, masoko, mahusiano, huduma za kijamii, ujasiriamali, utoaji wa bidhaa mpya, bidhaa mpya za tehama, tuzo kwa tovuti na zaidi.
Zaidi ya watendaji 270 duniani kote walishiriki katika kuwania tuzo hizi wakifanyiwa tathmini na majaji 12.
Jacqueline Mengi ambaye ndiye Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Amorette akizungumzia ushindi wake alisema amefurahishwa na ushindi huo ikionesha kwamba mchango wake duniani unatambuliwa.
Amorette ni kampuni ya kutengeneza samani zinazotokana na mbao zinazopatikani nchini Tanzania ikiwemo miti migumu.
Samani zinazotengenezwa huangaliwa kwa undani ili kukamilisha umaridadi wa samani. Yeye pamoja na kuwa balozi wa WildAid na akiwa ndani ya bodi kadhaa; mama wa watoto pacha wavulana; mke kwa mfanyabiashara mwenye mafanikio makubwa na akiendesha taasisi ya hisani ya elimu), Jacqueline huhakikisha anakagua kila samani inayozalishwa kiwandani kwake kabla ya kuuzwa au kusafirishwa.
Jacqueline, mzaliwa wa Tanzania, aliyefunzwa kubuni uzuri wa ndani, ni mwanzilishi na mbunifu mkuu wa Molocaho by Amorette, kampuni ya Tanzania inayojishughulisha na utengenezaji wa samani bora kwa namna mteja anavyohitaji, samani, nyuzi, taa, urembaji, samani za nje na kwenye bustani.
Molocaho, moja ya makampuni ya Afrika Mashariki ya samani yanayokua kwa kasi, imejipatia nafasi kubwa ya heshima kwa kuhakikisha kwamba inatumia mali ghafi na mbao njema pekee za Tanzania kutengeneza samani zenye kwenda kimataifa.
Jacqueline Mengi ni mojawapo ya watu wanaotambulika kirahisi kabisa nchini Tanzania. Mwaka 2000 alishinda taji la urembo la Miss Tanzania na kuiwakilisha Tanzania katika shindano la urimbwende la dunia (Miss World). Baada ya muda alipata heshima ya kuwa mmoja wa wanamuziki mahiri na kuweza kutoa nyimbo kadhaa zilizoshika chati Afrika Mashariki.
Pamoja na kuwa mrimbwende na mwanamuziki anasema mapenzi yake makubwa ni ubunifu wa uzuri wa ndani wa nyumba.
Kwa tuzo hiyo inadhihirisha kwamba Amorette ni chata ya kuaminika yenye mafanikio makubwa miongoni mwa watu wa daraja la juu nchini Tanzania.
Amorette, kampuni inayoshughulika na ubunifu wa masuala ya ndani ilianzisha programu ya kusimamia mafunzo kwa mafundi wa hapa Tanzania kuwafanya mafundi wa Tanzania kufikia uwezo wa kubuni na kutengeneza bidhaa zenye hadhi ya kimataifa.



KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA





DALADALA LAPIGA MWELEKA NA KUINGIA MTARONI

$
0
0
 Basi  la abiria lililokuwa likitoka Makumbusho  kuelekea Mbagala Rangitatu limepiga mweleka na kuingia mtaroni katika eneo la Mtoni Mtongani darajani  jijini Dar as Salaam leo, chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika kwa haraka.(picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
Break Down likiwa tayari kwa kulinyanyua gari hilo toka mtaroni.
Juhudi za kulitoa basi lililoanguka katika mtaro  zikiendelea.

KAMATI YA BUNGE YA VIWANDA YATEMBELEA KIWANDA CHA ALAF JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
KAMATI viwanda ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo imetembelea kiwanda cha kutengeneza mabati cha ALAF jijini Dar es Salaam.

Katika ziara hiyo iliyohusisha wabunge pamoja na wajumbe wa kamati hiyo ya bunge ilikuwa na leongo la kuangalia utendaji kazi wa kiwanda cha Kutengeneza mabati cha ALAF pamoja na Kuangalia changamoto mbalimbali zinazowakumba katika uendeshaji wa viwanda vya hapa nchinni.

Mwenyekiti wa Kamati ya viwanda ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Suleiman Ahmed Sadiq akizungumza na wabunge pamoja na wajumbe wa kamati hiyo amesema kuwa serikali inapaswa kuhakikisha kuwa umeme unakuwa wa uhakika ili kukuza viwanda hapa nchini.

Pia amesema kuwa serikali ikae na wenye viwanda vya ndani ili kuhakiki gharama za uzalishaji wa bidhaa mbalimbali za viwandani ili kuzuia bidhaa za enje ya nchi kuuzwa kwa gharama ya chini kuliko ya viwanda vya ndani ya nchi.

"Serikali ikae na wenye viwanda ili kuhakiki bei za uzalishaji wa bidhaa kwaajili ya kuweka bei nzuri kwa watumiaji wa bidhaa hizo za viwandani".

"Pia sisi kama wabunge tutakaa na serikali kwajiili ya kuishauri na kuieleza ni sehemu gani kunamianya ya uongezaji wa bei za bidhaa za viwandani".
Kamati hiyo ya viwanda itatembelea viwanda tisa vilivyopo hapa nchini.

Kwa upande wao kiwanda cha ALAF wameiomba serikali na shirika la Viwanda kuangalia bidhaa zenye viwango zinazoingizwa hapa nchini ili kuwa na soko linalolingana pia wameiomba serikali kuwa na umeme wa uhakika ili kukuza viwanda vya nyumbani pamoja na kukuza uzalishaji wa bidhaa za viwandani.
Katibu Mkuu wa wizara ya viwanda na biasharana viwanda prof. Joseph Buchweishaija akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha ALAF mara baada ya kamati ya viwanda ya bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kutembelea katika kiwanda cha ALAF jijini Dar es Salaam leo.
 Baadhi ya wajumbe na wabunge wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa ALAF, Dipt Mohanty jijini Dar es Salaam leo walipotembelea kiwanda cha ALAF.
 Baadhi ya wanakamati ya viwanda wakipata maelekezo walipo tembelea kiwanda cha kutengeneza Mabati cha ALAF jijini Dar es Salaam leo. 
 Wabunge na wajumbe wa kamati ya viwanda wakiwa ndani ya kiwanda kujionea utendaji kazi wa kiwanda cha ALAF hapa nchini.
 Baadhi ya Mitambo ya kutengeneza bomba za mstatili kwaajili ya kutengenezea mageti.

VIONGOZI CHADEMA WANAOKABILIWA NA KESI YA UCHOCHEZI WAWASILISHA MAOMBI YA KUTAKA KESI YAO IHAIRISHWE

$
0
0
Na Karama Kenyunko blogu ya jamii.

Viongozi tisa wa Chadema akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho Free wanaokabiliwa na kesi ya uchochezi, wamewasilisha maombi ya kutaka kesi hiyo iharishwe mpaka rufaa yao itakaposikilizwa na kutolewa maamuzi,
Maombi hayo yamewasilishwa leo Agosti 13,2018 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na wakili wa utetezi Jeremiah Mtobesya mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri.

Katika maombi yao, upande wa utetezi unaomba mahakama ya Kisutu kuahirisha kesi hiyo mpaka hapo rufaa yao waliyofungua mahakama ya Rufaa itakaposikilizwa na kutolewa maamuzi

Mapema washtakiwa walikata rufaa kupiga maamuzi ya mahakama Kuu yaliyotolewa mwezi uliopita ambayo yalitupilia mbali maombi yao ya kutaka kesi hiyo ifanyiwe marejeo juu ya uamuzi mdogo uliotolewa na mahakama ya Kisutu

Katika maombi yaliyowasilishwa na wakili wa utetezi Jeremiah Ntobesya na Peter Kibatala wanaiomba Mahakama ya Kisutu iahirishe kesi hiyo hadi Mahakama ya Rufaa itakaposikiliza rufaa yao.Pia wamewasilisha rufaa ya kutaka kusitisha usikilizwaji wa kesi yao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Wakili wa Serikali Mkuu, Mango amesema wamepokea hati ya maombi hayo namba 10.2018 na kwamba wapo tayari kuwasilisha majibu kinzani kesho.Wakili wa utetezi, Mtobesya naomba wapewe muda wa siku mbili hadi Agosti ilii waweze kufaili majibu ya nyongeza kama watakuwa nayo.

Baada ya kusikiliza pande zote mbili, Hakimu Mashauri ameamuru upande wa mashtaka kuwasilisha majibu kinzani Agosti 14.2018 na kama upande wa utetezi watakuwa na majibu ya nyongeza wayawasilishe Agosti 21, mwaka huu.

Maombi hayo sasa yatasikilizwa Agosti 21,2018 na kesi ya msingi nayo pia itatajwa Agosti 21 mwaka huu.Mbali na Mbowe, washitakiwa wengine kwenye kesi hiyo ni Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Vincent Mashinji, Mbunge wa Iringa Mjini Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu na Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa Kibamba, John Mnyika.

Washitakiwa wengine ni Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe Halima Mdee, Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya na Mbunge wa Tarime mjini, Matiko.

WATAALAM MAGONJWA YA DAMU KUTOKA AFRIKA WAKUTANA MUHIMBILI

$
0
0

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) wanafanya kongamano la kwanza na la kihistoria juu ya maendeleo mbalimbali yaliyotokea katika utoaji wa huduma ya magonjwa ya damu (Haematology) barani Afrika.

Kongamano hilo la siku nne linashirikisha nchi 15 za Afrika ikiwamo Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda, Afrika Kusini, Malawi, Zambia, Zimbabwe, Ivory coast, Swaziland, DRC, Madagascar, Ghana, Ethiopia pamoja na Burkinafaso

Akifungua kongamano hilo leo jijini Dar es Salaam, Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohamed Bakari Kambi amesema azma ya serikali ni kuendelea kuboresha huduma za afya nchini ili kuwawezesha Watanzania kupata matibabu ndani ya nchi .

‘’Miongoni mwa malengo makubwa ya serikali ya awamu ya tano ni kupanua wigo wa utoaji huduma za afya kwa wananchi na kuhakikisha huduma za kibingwa na ubingwa wa juu zinatolewa hapa hapa nchini ili kuwawezesha wananchi wengi kupata huduma hizo,’’ amesema Prof. Bakari.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru amesema kukutana kwa watalaam hao ni hatua nzuri ya kuangalia namna bora ya kutoa tiba ya kisasa kwa magonjwa ya damu na hata kuanzisha tiba hiyo sehemu za kanda ili kupunguza idadi ya wagonjwa wengi ambao wanakuja kupata huduma hiyo Muhimbili.

“MHN tumekua wenyeji wa kongamano hili ambalo limehusisha wataalam wa magonjwa ya damu kutoka nchi mbalimbali barani Afrika, hii ni heshima kubwa na itasaidia kufikia malengo ya kutoa huduma kwa wananchi wengi zaidi,’’amesema Prof. Museru.

Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Mohamed Bakari akizungumza na wataalamu wa magonjwa ya damu (Haematology) kwenye kongamano la kwanza ambalo limeandaliwa na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS). 
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akizungumza kwenye kongamano hilo baada ya kuwakaribisha wataalam wa magonjwa ya damu kutoka mataifa mbalimbali duniani. 

Wataalamu wa magonjwa ya damu kutoka nchi mbalimbali duniani wakifuatilia mkutano huo leo ambao unafanyika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Baadhi ya nchi zinazoshiriki kongamano hilo la siku nne ni Nigeria, Ghana, Bostwana, Afrika Kusini, Ufaransa, Marekani, Rwanda na Italia. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>>

DKT. BASHIRU ATOA SHUKRANI BAADA YA UCHAGUZI, AMPOKEA KUCHAMKA AKITOKEA CUF

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
KATIBU wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally ametoa shukrani wa wananchi wanaoendelea kuunga mkono katika shughuli zao za kuimarisha chama.

Akizungumza na vyombo vya habari katika ofisi ndogo za chama Lumumba jijini Dar es salaam Bashiru ameeleza kuwa chaguzi ndogo chama chao kimekuwa na mvuto tena na hii ni baada ya chama cha mapinduzi kujizolea ushindi katika jimbo la Buyungu na kata zote 77 zilizokuwa zinafanya uchaguzi wa marudio ambapo kata 41 walipita bila kupingwa na kata 36 walifanya uchaguzi na kushinda kwa kishindo na hata katika kata ambazo hazijawahi kutwaliwa na chama cha mapinduzi tangu mfumo wa vyama vingi uanze mwaka huu zimechukuliwa na CCM.

Aidha ameeleza kuwa wanafanya vizuri kwa kuwa wafanyayo yanawapa tumaini walio wengi hasa wanyonge na shabaha zao zipo katika kupambana na umaskini, kuongeza nafasi za ajira hasa katika sekta za kilimo na ufugaji, na kupambana na rushwa na ufisadi.

Pia amehimiza mshikamano ndani ya Chama kwani hadi sasa chama kimerejea katika misingi ya waasisi wake kwa kutekeleza misingi ya utu, usawa, na usawa. Na amewahaidi watanzania kufanya kazi na kutobweteka usiku na mchana.

Wakati huo huo Dkt. Bashiru amempokea aliyekuwa Mbunge wa Liwale kupitia tiketi ya CUF Zuberi Mohamed kuchamka kuwa mwanachama mpya wa CCM.

Zuberi ameeleza kuwa amehamia CCM kuunga mkono jitihada za mheshimiwa Rais ambapo ndani ya miaka 2 katika jimbo lake la Liwale wamepata huduma za msingi zikiwemo afya na utatuzi wa migogoro na akaona hana budi kufuata kasi hiyo na amewaomba wanachama wa chama cha mapinduzi wampokee wafanye kazi.Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally akizungumza mda mfupi kabla ya aliyekuwa Mbunge wa CUF katika jimbo la Liwale mkoani Lindi Zuberi Kuchauka (kulia), kutangaza kukihama Chama cha Civic United (CUF), na kujiunga na CCM, leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole.

SERIKALI KUPELEKA WATAALAMU WA UTAFITI WA MIAMBA(GST),MALIASILI NA MAZINGIRA AMANI MUHEZA

$
0
0

Waziri wa Madini Dotto Biteko juzi kulia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mhandisi Mwanasha Tumbo

SERIKALI imesema kuwa itafanya mchakato wa kuleta wataalamu wa utafiti wa miamba(GST),maliasili na mazingira kwa pamoja katika kata ya Mbomole tarafa ya Amani ili kuweza kuona uwezekano wa kuwaruhusu wananchi na wachimbaji wadogowadogo kuchimba madini katika eneo hilo.

Hayo yamesemwa na Naibu waziri wa Madini Dotto Biteko alipotembelea katika kijiji cha Sakale katika kata hiyo wakati akizungumza na wananchi waliomuelezea kero yao ya kuzuiwa na serikali kutokuchimba madini eneo hilo licha ya kuwatokuwepo na viashiria vya uharibifu wa mazingira na misitu kama serikali inavyosema.

Wakizungumza kijijini hapo wananchi hao walimueleza naibu waziri huyo kuwa madini katika eneo hilo yaligunduliwa mwaka 2013 na ni mengi yanapatikana kwenye miamba na siyo kwenye chanzo cha mto kama serikali inavyosema lakini walizuiwa kwa tahadhari ya uharibifu wa mazingira na misitu ya asili.

 
NAIBU Waziri wa Madini Dotto Biteko kushoto akimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja ya kutembelea Hifadhi ya Amani 
 
NAIBU Waziri wa Madini Dotto Biteko kulia akimsikiliza kwa umakini Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu wakati wa ziara yake ya siku moja 

NAIBU Waziri wa Madini Dotto Biteko kulia akiwa na Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu na Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo wakati wa ziara yake ya siku moja wilayanu humo 
MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu kulia akisistiza jambo wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Madini Dotto Biteko kushoto katikati ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo 
Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Sakale katika kata Mbomole Tarafa ya Amani wilayani Muheza wakati wa ziara ya Naibu.KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

MNEC SALIM ASAS AWAPONGEZA MADIWANI WA CCM WALIOSHINDA UCHAGUZI KATA 5 ZILIZOKUWA CHINI YA CHADEMA IRINGA MJINI

$
0
0
Bw. Salim Abri (ASAS) MNEC wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Iringa akiwa katika picha ya pamoja na madiwani wa CCM walioshinda katika uchaguzi wa marudio Kata tano katika manispaa ya Iringa huku wakionyesha vyeti vyao baada ya kukabidhiwa vyeti hivyo vya uteuzi na Tume ya Uchaguzi leo mjini Iringa.

Madiwani hao wa kata 5 za manispaa ya Iringa Awali zilikuwa chini ya Utawala wa CHADEMA baada ya kujiuzuru nafasi zao za udiwania kupitia chama hicho CCM iliwateua tena kugombea katika uchaguzi wa marudio ambapo madiwani hao wameibuka washindi katika uchaguzi huo.
Bw. Salim Abri (ASAS) MNEC wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Iringa akiwapongeza madiwani wa CCM walioshinda katika uchaguzi wa marudio Kata tano katika manispaa ya Iringa baada ya kukabidhiwa vyeti vyao vya uteuzi na Tume ya Uchaguzi leo mjini Iringa.
Bw. Salim Abri (ASAS) MNEC wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Iringa akiwa katika picha ya pamoja na madiwani wa CCM walioshinda katika uchaguzi wa marudio Kata tano katika manispaa ya Iringa baada ya kukabidhiwa vyeti vyao vya uteuzi na Tume ya Uchaguzi leo mjini Iringa na baadhi ya wabunge wa viti maalum CCM mkoa wa Iringa 

IGP AMPANDISHA CHEO MWANARIADHA KWA KUVUNJA REKODI

$
0
0
Na. Jeshi la Polisi
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amempandisha Cheo Mwanariadha wa Polisi Fabian Nelson kutoka Konstebo hadi Koplo baada ya kuchukua medali ya dhahabu na kuvunja rekodi ya mbio za mita 5000 katika Michezo ya Shirikisho la Wakuu wa Majeshi ya Polisi Ukanda wa Afrika Mashariki (EAPCCO) iliyomalizika mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam.

Mwanariadha huyo alikimbia dakika 13: 45: 99 na kuwashinda Wanariadha wa Jeshi la Polisi la Kenya na Uganda ambapo Tanzania ilishika nafasi ya pili katika ushindi wa jumla ambapo nafasi ya kwanza ilienda Kenya na ya tatu Uganda.

IGP Sirro alimpandisha Cheo hicho katika hafla ya kuwapongeza Wanamichezo walioshiriki Michezo hiyo katika bwalo la Maafisa wa Polisi Oystabya IGP Sirro alisema mwanariadha huyo amekuwa akionyesha juhudi katika mbio ndefu jambo ambalo limekuwa likileta sifa kwa Jeshi la Polisi na nchi kwa Ujumla.

“ KIla mmoja anastahili pongezi kutokana na kutuwakilisha vizuri katika michezo hii, hivyo tunathamini mchango wa kila mmoja kwa nafasi yake katika kuitangaza nchi yetu na nawaahidi tutaendelea kutambua mchango wa kila mmoja” Alisema Sirro

Aidha, Alisema maandalizi ya michezo ijayo yanaanza sasa ili kuhakikisha kuwa wanaendelea kufanya vizuri zaidi na kuzifanyia kazi changamoto zilizojitokeza katika michezo ya mwaka huu ikiwemo kuingia kambini mapema na kuajiri wanamichezo pindi nafasi zitakapopatikana.

Kwa upande wake Kamishna wa Polisi Jamii Mussa Alli Mussa alisema kazi iliyofanyika ni kubwa na kila mshiriki alijituma kuhakikisha kuwa Vikombe na medali zinabaki hapa nchini.

Michezo inayoshindaniwa ni pamoja na soka ,mpira wa mikono, mpira wa wavu, mpira wa pete, Ngumi, Taekwondo, Judo na Riadha ambapo nchi zilizoshiriki ni pamoja na Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Sudani, Sudani Kusini na Tanzania.

 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akimpongeza Mwanariadha wa Polisi Fabian Nelson baada ya kumpandisha cheo kutoka Kostebo mpaka Koplo kutokana na kufanya vizuri katika Michezo ya Wakuu wa Majeshi ya Polisi ukanda wa Afrika Mashariki (EAPCCO) iliyomalizika mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam (Picha na Jeshi la Polisi).
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akiwa katika picha ya pamoja na wanariadha Michezo ya Wakuu wa Majeshi ya Polisi ukanda wa Afrika Mashariki (EAPCCO) iliyomalizika mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuwapongeza Wanamichezo wote kwa kuchukua nafasi ya pili kwa ujumla (Picha na Jeshi la Polisi).

NDIKILO AIELEKEZA HALMASHAURI YA MAFIA KUWATUMIA WAWEKEZAJI KUINUA MAPATO

$
0
0

NA MWAMVUA MWINYI,MAFIA 

MKUU wa Mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,ameielekeza halmashauri ya Mafia kukaa meza moja na baadhi ya wawekezaji wilayani humo ili kuangalia namna ya kulipa kodi itakayosaidia kuondoa udumazi wa mapato kwenye halmashauri hiyo. 

Pamoja na hilo ,amewataka watanzania kuacha kuchagua kazi ,bali watumie fursa ya viwanda vingi vinavyojengwa kupata ajira .
Mkuu huyo wa mkoa huo aliyasema hayo ,wakati kamati ya siasa ya mkoa ilipokwenda kutembelea uwekezaji mkubwa wa shamba la ufugaji samaki aina ya kamba katika kiwanda cha Alpha Crust . 

Alisema ,uwekezaji huo ni mkubwa ambao umegharimu dollar za Kimarekani milioni 15 sawa na sh. bilioni 32 za Kitanzania ,hivyo ni lazima uungwe mkono kwani ni moja ya utekelezaji wa ilani ya CCM katika sekta ya uvuvi . 

Aidha, aliitaka uhamiaji pamoja na idara ya kazi kuacha urasimu katika kutoa vibali vya kuishi na vya kazi kwa wataalamu mbalimbali kutoka nje ya nchi ,wanaokuja kwa ajili ya kusimamia uzalishaji katika viwanda. 

 
Mkuu wa Mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo (mwenye shati la kijani)akiwa na mkurugenzi wa kiwanda cha Alpha Crust (wa kwanza kushoto) na wa pili kutoka kulia ni Katibu tawala Mkoa wa Pwani (RAS).(Picha na Mwamvua Mwinyi) 

TOZO MATUMIZI YA MAJI KATIKA VIWANDA LAZIMA ILIPWE KAMA SHERIA INAVYOELEKEZA –PROFESA MBARAWA

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa amewataka watu wenye viwanda kulipa tozo za shilingi 10 kwa lita ambapo baadhi yao wameshindwa kutekeleza agizo hilo licha ya kuwepo kwa sharia hiyo.

Kushindwa kulipa huko kunatokana na kiwango hicho kuwa kikubwa na kufanya sheria hiyo ishindwe kutekelezwa .

Hayo aliyasema jijini Dar es Salaama katika mkutano wa wadau mbalimbali ulioandaliwa na Bodi ya Maji ya Bonde la Mto Wami/ Ruvu kujadili tozo hiyo ambapo alitaka kufikiwa mwafaka kwa ajili ya kuanza kulipa kama sheria inavyotaka au kupunguza tozo.Amesema Wizara ilifanya mabadiliko ya viwango vya ada za matumizi mbalimbali ya maji vilivyokuwa vinatumika kuanzia mwaka 2002.

Profesa Mbarawa amesema kuwa kiwango cha tozo cha shilingi 10 kwa lita ya kilitangazwa katika gazeti la serikali na kwamba taarifa ya kawaida namba 783 ya Agosti, 2013 kilianza kutumika mwaka wa fedha 2014/2015.

"Hatua hii imefikiwa baada ya ada za awali kuwa ndogo ikilinganishwa na gharama halisi za usimamizi wa rasilimali maji.Tangu kipindi hicho baadhi ya yenu wenye viwanda mmeshindwa kutekeleza agizo hili na kuwa na sheria isiyotekelezwa hakuna maana kuendelea au ifutwe,"Waziri Mbarawa.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa akizungumza wakati akifungua mkutano wa kujadili tozo za matumizi ya maji uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali za Maji wa Wizara hiyo George Lugomela akizungumza katika mkutano wa kujadili tozo za maji pamoja na maendeleo ya bodi katika usimamizi vyanzo vya maji uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Afisa wa Maji wa Bonde la Wami/Ruvu Simon Ngonyani akizungumza kuhusiana usimamizi wa vyanzo vya maji katika mkutano wa kujadili tozo za maji uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masasi Food Industry wazalishaji wa Maji ya Lulu Charle’s Zakaria akizungumza kuhusiana na tozo hiyo biashara hiyo kuwa ni kubwa hivyo kikao kitafikia mwafaka katika mkutano wa kujadili tozo za maji uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali katika mkutano wa kujadili tozo za maji uliofanyika jijini Dar es Salaam.

JAFO AHIMIZA UWAJIBIKAJI KWA WAGANGA WAKUU WA MIKOA, WILAYA

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo amewataka Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya kusimamia ujenzi wa vituo vya afya unaoendelea kote nchini pamoja na kuweka udhibiti imara wa upotevu wa fedha ili kusiwe na upungufu wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma nchini. 

Waziri Jafo ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha Waganga Wakuu wa Mikoa na wa Halmashauri zote nchini uliofanyika katika ukumbi wa LAPF leo Jijini Dodoma.“Fanyeni kazi kwa weledi kwani msipotimiza wajibu wenu ipasavyo tudumaza afya za wananchi, natamani itakapofika mwaka 2020 kila mwananchi azungumze faraja kwenye sekta ya afya”, alisema Waziri Jafo.

Aidha,Waziri huyo alisema katika ukusanyaji wa mapato hauridhishi, hivyo kufanya vituo vingi kuwa na makusanyo madogo ya mapato ya kila siku licha ya kuwahudumia wananchi wengi. Kwa upande wa kuboresha huduma za afya nchini, Waziri Jafo alisema wakati Serikali ya Awamu ya Tano inaingia madarakani kulikuwa na vituo vya afya 115 vilivyokuwa na uwezo wa kufanya upasuaji wa dharura.

Kwa sasa vipo vituo 210 ambavyo vinatoa huduma hiyo , sawa na asilimia 95 Aliendelea kufafanua kuwa katika bajeti ya Mwaka wa Fedha 2018/2019 Serikali imetenga takribani bilioni 105 ambapo ajenda kubwa ni ujenzi wa Hospitali za Wilaya 67 hivyo kufanya vituo 307 vitakavyokuwa vinafanya upasuaji wa dharuara. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akisistiza Jambo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri uliofanyika leo katika ukumbi wa LAPF Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Afya, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Dk. Zainabu Chaula akitoa mada katika Mkutano Mkuu wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri uliofanyika leo katika ukumbi wa LAPF Jijini Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya akihimiza umuhimu wa matumizi ya takwimu afya kwenye Mkutano wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri uliofanyika leo katika ukumbi wa LAPF Jijini Dodoma
Baadhi ya washiriki wa Mkutano Mkuu wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri uliofanyika leo katika ukumbi wa LAPF Jijini Dodoma wakimsikiliza Mgeni rasmi ( hayupo pichani).

Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC wafunguliwa mjini Windhoek, Namibia

$
0
0
Mkutano wa siku mbili wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) umefunguliwa rasmi katika Hoteli ya Safari mjini Windhoek, Namibia tarehe 13 Agosti 2018.

Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huu unaongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga ambaye ameambatana na viongozi waandamizi wa Serikali ya Tanzania ambao ni pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda,Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (anayesimamia masuala ya Ujenzi) Mhandisi Joseph Myamhanga, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Evaristo Longopa; Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu na Naibu Katibu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Edwin Paul Mhede

Mkutano huu ni sehemu ya mikutano ya awali ya maandalizi ya mkutano wa 18 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC utakaofanyika tarehe 17 na 18 Agosti 2018 mjini Windhoek, Namibia. Mikutano mingine ya awali ni mkutano wa Makatibu Wakuu wa SADC uliofanyika tarehe 9 na 11 Agosti 2018 na Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa , Ulinzi na Usalama ya SADC (SADC Organ on Politics, Defence and Security) utakaofanyika tarehe 16 Agosti 2018 ambao utapitia na kujadili hali ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Kanda kwa kipindi cha Agosti 2017 hadi Agosti 2018. 

Mkutano wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama utahusisha nchi tatu za SADC Organ TROIKA na wajumbe wake ambao ni Angola (Mwenyekiti wa sasa wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama), Zambia (Makamu Mwenyekiti wa Organ) na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Mwenyekiti wa Organ aliyemaliza muda wa uenyekiti wa Asasi).

Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali utapokea, kujadili na kutolea maamuzi ya mapendekezo mbalimbali yanayotokana na mikutano ya kisekta na kamati za jumuiya kwa kipindi cha mwaka 2017/18. Pamoja na mambo mengine mkutano huu.
Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) Dkt. Stergomena L. Tax (mstari wa mbele kati) akiwa katika picha ya pamoja na Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika mara baada ya hafla ya ufunguzi wa mkutano huo mjini Windhoek, Namibia. 
Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika, Dkt. Stergomena L. Tax akitoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa Mawaziri wa SADC.Katika hotuba yake aliwasilisha taarifa fupi ya mwaka ya utekelezaji ya Jumuiya hiyo pamoja na kuishukuru Serikali ya Afrika Kusini (Mwenyekiti aliyemaliza muda) kwa uongozi na usimamizi mzuri katika kipindi chote cha Agosti 2017 hadi Agosti 2018. 
Mwenyekiti aliyemaliza muda wake na Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Afrika Kusini, Mhe Dkt. Lindiwe Sisulu (kushoto) akikabidhi nafasi ya uenyekiti kwa mwenyekiti mpya ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Namibia, Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwa. 
Mkutano ukiendelea, walioketi nyuma ya Mhe. Waziri Mahiga kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Prof. Adolf Mkenda na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Viwanda na Mawasiliano (anayeshughulikia masuala ya ujenzi) Mhandisi Joseph Nyamhanga. 
Mkutano ukiendelea, Kutoka Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Innocent Shiyo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Edwin Mhede. 
Wa kwanza kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Namibia mwenye makazi yake nchini Afrika Kusini, Mhe. Sylivester Ambokile na wajumbe wengine wa Serikali ya Tanzania wakifuatilia ufunguzi wa mkutano. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>>

MAGEREZA YAANDAA MKAKATI WA KUJITOSHELEZA KWA CHAKULA

$
0
0

Na Deodatus Kazinja

Watendaji wote ndani ya Jeshi la Magereza wametakiwa kujiandaa kisaikolojia kupokea mkakati maalum wa uzalishaji wa chakula unaolenga kujitosheleza kwa chakula cha wafungwa na ziada kuuzwa katika sehemu nyingine.

Hayo yamesemwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini Phaustine Kasike leo Agosti 13, 2018 alipokuwa akizungumza na maafisa, askari na watumishi raia wa jeshi hilo alipofanya ziara yake ya kwanza mkoani Dodoma tangu ateuliwe kushika wadhifa huo Julai 13 mwaka huu.

Kamishna Jenerali Kasike amesema maandalizi ya mkakati huo yanaendelea vizuri makao makuu ya jeshi hilo na katika kipindi kifupi kijacho maelekezo ya utekelezaji wake yatatolewa na kushushwa katika vituo vyote vya magereza kwa ngazi ya mikoa na wilaya.

Amesema mkakati huu utakapokuwa umekamilika itakuwa ndiyo dira ya utekelezaji ndani ya jeshi na utamtaka kila kiongozi kuwa na mpango kazi katika eneo lake unaokwenda sambamba na malengo mapana ya jeshi hilo.

“Ninaamini jambo hili linawezekana na kwa kuanza na raslimali chache zilizopo kwakuwa wataalam wapo, ardhi ipo na nyenzo za kuanzia zipo tukijipanga vizuri tunaweza kupata mahala pazuri pa kuanzia” Amebainisha Jenerali Kasike

Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (wa pili kushoto) akikagua moja ya nyumba za watumishi zinazojengwa gerezani hapo kwa mtindo wa kujitolea. Kushoto ni Mkuu wa Gereza Isanga Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Keneth Mwambije. 
Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (mwenye miwani) akikagua shamba la zabibu lililopo gereza Isanga mkoani Dodoma alipofanya ziara ya gerezani hapo leo Agosti 13, 2018. 
Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (wa pili kushoto) akiongea na baadhi ya maafisa na askari wa ofisi ya Mkuu wa Magereza mkoa wa Dodoma na gereza Isanga (hawapo pichani) alipofanya ziara mkoani Dodoma leo Agosti 13, 2018.Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP) Salum Omari. 
Baadhi ya maafisa na askari wa ofisi ya Mkuu wa Magereza wa Dodoma na gereza Isanga wakifuatilia kwa makini hotuba ya Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (hayupo pichani) alipofanya ziara mkoani Dodoma leo Agosti 13, 2018. 
Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike akibadilishana mawazo na Katibu Mkuu Utumishi Dr. Laurean Ndumbaro (kulia) leo Agosti 13, 2018 alipofanya ziara ya kikazi ofisini kwake jijini Dodoma. Picha zote na Jeshi la Magereza. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>


WAZIRI MKUU AWATAKA VIONGOZI WABADILIKE KIMTAZAMO

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wanaoshiriki kozi fupi ya tano ya viongozi wahakikishe watakaporudi kwenye maeneo yao ya utendaji wawe wamebadilika kimtazamo, kihoja, kiushauri pamoja na utoaji maamuzi.

Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Agosti 13, 2018) wakati akifungua kozi ya tano ya muda mfupi ya viongozi inayofanyika katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi, Kunduchi jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu amesema chuo hicho kilianzishwa kwa lengo la kulisaidia Taifa kujenga uwezo wa viongozi ili wanaohitimu mafunzo hayo wawe na uchambuzi wa kina na wa kimkakati ili kuweza kutatua mambo mbalimbali ya usalama wa Taifa na matatizo yanayotakiwa kushughulikiwa kimkakati.

“Chuo hiki kilianzishwa ili kuwaleta washiriki kutoka taasisi zote za Serikali na sekta binafsi waweze kujadili mambo mbalimbali ya kimkakati ili wanapokuwa wanatekeleza wajibu wao watambue kuwa ni kwa kiasi gani matokeo ya maamuzi yao yataathiri mambo ya kijamii, kiuchumi, uhusiano wa kidiplomasia na siasa za ndani kwa ujumla wake”.

Amesema ushirikiano kuhusu kutatua matatizo uanze wakati wa mafunzo hayo na uendelee hata hapo baadaye watakaporejea kwenye maeneo yao ya kazi. “Sisi viongozi wenu tunatarajia kuona kuwa mtakapohitimu mafunzo haya mtakuwa mmebadilika kimtizamo na kwamba taasisi zenu zitakuwa kwenye nafasi nzuri ya kuzungumza lugha moja”.

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na washiriki wa kozi fupi ya tano ya Viongozi, inayofanyika katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi, Kunduchi jijini Dar es Salaam. Agosti 13.2018 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi, akizungumza na washiriki, kwenye ufunguzi wa kozi fupi ya tano ya Viongozi, inayofanyika katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi, Kunduchi jijini Dar es Salaam. Agosti 13.2018.
 Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) Luteni Jenerali, Paul Massao, akizungumza na washiriki, kwenye ufunguzi wa kozi fupi ya tano ya Viongozi, Agosti 13.2018.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea zawadi ya tai, kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) Luteni Jenerali, Paul Massao, baada ya kufungua kozi fupi ya tano ya Viongozi, inayofanyika katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi, Kunduchi jijini Dar es Salaam. Agosti 13.2018.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea zawadi ya peni, kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) Luteni Jenerali, Paul Massao, baada ya kufungua kozi fupi ya tano ya Viongozi, inayofanyika katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi, Kunduchi jijini Dar es Salaam. Agosti 13. 2018.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa kozi fupi ya tano ya Viongozi, inayofanyika katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi, Kunduchi jijini Dar es Salaam. Agosti 13.2018.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme, baada ya ufunguzi wa kozi fupi ya tano ya Viongozi, inayofanyika katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi, Kunduchi jijini Dar es Salaam, Agosti 13.2018, katikati ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angeline Mabula.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo, baada ya ufunguzi wa kozi fupi ya tano ya Viongozi, inayofanyika katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi, Kunduchi jijini Dar es Salaam, Agosti 13.2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


DC ARUMERU AFANYA UKAGUZI WA GHAFLA WA MALORI KUTOKA NCHI JIRANI

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mh. Jerry Muro amefanya zoezi la Ukaguzi wa malori 10 yaliyokuwa yakitokea Nchi Jirani Mara baada ya kuyatilia mashaka Kutokana na Malori hayo kudaiwa kutoka Mombasa na kupitia Njia ya Namanga tukio ambalo limeonekana sio la kawaida Kwa kupitia njia ndefu ya Mombasa kwenda Dar es salaam kupitia Namanga.

Dc Muro Akiwa katika Majukumu Yake Siku ya Jumapili Jioni alishangazwa na kitendo cha Malori hayo mapya kupita katika Wilaya yake kwa kutumia boda ya Namanga badala ya kupitia Tanga mida ya jioni yakiwa na chesses number ambazo alizitilia mashaka na kuwaagiza Maofisawa TRA kuyagua Ili kujiridhisha kwanza kutokana na kuwepo Kwa tetesi ZA baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu kutaka kuhujumu Bandari Za Tanzania na Kukimbilia Nchi Jirani kutokana na Bandari Za Tanzania kuwa na Udhibiti Mzuri wa Vitendo vya Magendo na Rushwa . Dc Muro Amesema katika Wilaya Anayoiongoza ya Arumeru Kamwe haitakuwa Uchochoro wa Kupitisha Bidhaa Haramu ZA Magendo kutoka Nchi Jirani.

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA LEO JUMATATU

Wadau wa Elimu wajadili Marekebeisho ya Sheria ya Tume ya Utumishi wa Walimu

$
0
0

Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu, Bibi Winifrida Rutaindurwa akifungua mkutano wa wadau (hawapo pichani) wa kujadili marekebisho ya Sheria ya Tume ya Utumishi wa Walimu unaofanyika kwa siku mbili mjini Morogoro. Kulia ni Mkurugenzi wa Ajira na Maendeleo ya Watumishi, Bibi Christina Hape na kushoto ni Wakili Mkuu wa Serikali na Mkuu wa Kitengo cha Sheria, Tume ya Utumishi wa Walimu, Bw. Donald Chidowu
Mkurugenzi wa Ajira na Maendeleo ya Watumishi, Tume ya Utumishi wa Walimu, Bibi Christina Hape akitoa ufafanuzi wa utendaji kazi wa Tume ya Utumishi wa walimu. Katikati ni Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu, Bibi Winifrida Rutaindurwa na kushoto ni Wakili Mkuu wa Serikali na Mkuu wa Kitengo cha Sheria, Tume ya Utumishi wa Walimu, Bw. Donald Chidowu.
Wakili Mkuu wa Serikali na Mkuu wa Kitengo cha Sheria, Tume ya Utumishi wa Walimu, Bw. Donald Chidowu akiongea na wajumbe (hawapo pichani) katika mkutano wa kujadili marekebisho ya Sheria ya Tume ya Utumishi wa Walimu. Katikati ni Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu, Bibi Winifrida Rutaindurwa akifuatiwa na Mkurugenzi wa Ajira na Maendeleo ya Watumishi, Bibi Christina Hape.
Wakili Mkuu wa Serikali na Mkuu wa Kitengo cha Sheria, Tume ya Utumishi wa Walimu, Bw. Donald Chidowu akiongea na wajumbe (hawapo pichani) katika mkutano wa kujadili marekebisho ya Sheria ya Tume ya Utumishi wa Walimu. 
Washiriki wa Mkutano wa kujadili marekebisho ya Sheria ya Tume ya Utumishi wa Walimu wakichukua dondoo muhimu wakati wa mkutano. 
Afisa Sheria wa Tume ya Utumishi wa Walimu, Bw. Deogratias Haule akitoa maelezo katika mkutano wa kujadili marekebisho ya Sheria ya Tume ya Utumishi wa Walimu unaofanyika mjini Morogoro.

Rais Magufuli afanya uteuzi Mkuu wa Wilaya 1 na Wakurugenzi 41, ahamisha Wakurugenzi 19

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 13 Agosti, 2018 amefanya uteuzi wa Mkuu wa Wilaya 1, Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji 41, na amewahamisha vituo vya kazi Mkuu wa Wilaya 1 na Wakurugenzi wa Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji 19. 

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 13 Agosti, 2018  na kutangazwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi (PICHANI), Ikulu Jijini Dar es Salaam.SOMA ZAIDI HAPA CHINI 

Viewing all 110029 articles
Browse latest View live




Latest Images