Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

WANANCHI JIMBO LA BUYUNGU WAPIGA KURA KWA AMANI NA UTULIVU

$
0
0



Baadhi ya Wakazi wa Jimbo la Buyungu waliojitokeza Kupiga Kura kumchagua Mbunge wao wakiwa kwenye mistari kuingia ndani ya Kituo cha Kupigia Kura wilayani Kakonko leo. Katika uchaguzi huo vyama 10 vya Siasa vimesimamisha wagombea.
Karani mwongozaji wa Kituo cha kupigia Kura Na. 1 katika ukumbi wa mikutano wa wilaya ya Kakonko akitoa maelekezo kwa wapiga Kura waliojitokeza kutimiza haki yao ya kikatiba ya kumchagua Mbunge wao katika jimbo la Buyungu leo.
Mkazi wa wilaya ya Kakonko akipiga kura yake kumchagua Mbunge wa Jimbo la Buyungu leo.
Mkazi wa wilaya ya Kakonko akipiga kura yake kumchagua Mbunge wa Jimbo la Buyungu leo.
Msimamizi Msaidizi wa Kituo cha Kupigia Kura akihakiki majina ya Mpiga kura katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kabla ya kumruhusu mpiga Kura kutimiza haki yake ya kushiriki kupiga Kura katika Uchaguzi mdogo wa jimbo la Buyungu leo.
Mmoja wa wapiga Kura ambaye ni mzee akipata usaidizi wa kutolewa nje ya kituo cha kupigia kura mara baada ya kupiga kura katika Uchaguzi mdogo wa Ubunge katika jimbo la Buyungu leo.
Mmoja wa wapiga Kura ambaye ni mzee akipata usaidizi wa kutolewa nje ya kituo cha kupigia kura mara baada ya kupiga kura katika Uchaguzi mdogo wa Ubunge katika jimbo la Buyungu leo.

KAMANDA ARUSHA ATHIBITISHA KUJERUHIWA KWA KADA WA CCM

$
0
0
*Azungumzia hali ya usalama maeneo yanayofanya uchaguzi


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha linamshikiliza mmoja wa wanachama wa Chadema kwa tuhuma za kumjeruhi kada wa CCM aliyefahamika kwa jina moja la Idd baada ya kuibuka kwa vurugu kati ya makundi mawili.

Akizungumza na Michuzi Blog Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Ramadhan Ng'anzi amesema tukio la vurugu hizo zimetokea leo kati ya saa nne na saa tano asubuhi eneo la Mianzini.

Amefafanua Polisi waliwahi kufika eneo la tukio na kufanikiwa kuzima vurugu hizo na kumkamata anayetuhumiwa kujeruhi na anahojiwa, huku aliyejeruhiwa naye amepatiwa matibabu.

Alipoulizwa jina la anayetuhumiwa kujeruhi Kamanda Ng'anzi amejibu kwa sasa yupo nje ya ofisi yake kwa ajili ya kufuatilia na kuangalia hali ya usalama na hasa kwenye kata zinazofanya uchaguzi unafanyika unaofanyika leo.

Hata hivyo inaelezwa kada aliyejeruhiwa ni Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kaloleni mkoani Arusha.

Kuhusu hali ya usalama amesema Mkoa wa Arusha hali ni tulivu na amani imetawala katika maeneo yote yakiwamo ya kata ambazo yanafanya uchaguzi na kwamba hata vurugu ambazo zilizotokea ni kwenye kata ambayo haina uchaguzi.

"Arusha hali ni shwari mno.Hakuna vurugu na watu wanaendelea na shughuli zao.Hata katika kata ambazo kunafanyika uchaguzi mdogo kuko shwari na mambo yanakwenda vizuri,"amesema Kamanda Ng'anzi.

MULTICHOICE TANZANIA YATOA TAARIFA KUFUATIA KUONDOLEWA KWA CHANELI ZA UMMA

Mkurugenzi Mtendaji TIC aongoza msafara wa wadau wa Serikali na Sekta binafsi kwenda nchini Korea kwa ziara ya kikazi

$
0
0
Balozi Massuka akimkaribisha nchini Korea Bw.Adonis Bitegeko ambaye ni Mkurugenzi wa Udhibiti na Mwakilishi Wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Chakula Tanzania (TFDA), moja ya taasisi muhimu za serikali zinazoshiriki katika ziara hiyo ya uhamasishaji viwanda nchini Korea. Anayeshuhudia ni Bw.Francis Mossongo, Afisa Uchumi Mwandamizi kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Tanzania.
Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Wafanyabiashara wa Dawa na Vifaa Tiba Nchini (Tanzania Association of Phramaceutical Industry, TAPI), Bw.Abbas S.Mohamed, ambaye pia ni Mkurugenzi Wa Kampuni ya Samiro Pharmaceuticals Ltd ya jijini Dar es Salaam, akipokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Incheon Seoul na Mhe. Matilda S.Massuka, Balozi Wa Tanzania nchini Korea. TAPI inashirikiana na Serikali katika kufanikisha malengo ya ziara hiyo Nchini Korea na China, wakiiwakilisha Sekta Binafsi ya Tasnia ya Dawa na Vifaa Tiba ya nchini Tanzania.
Balozi wa Tanzania nchini Korea, Mhe.Matilda S. Massuka, akimkaribisha Bw. Asgaral Alimohamed, Mwanachama Wa TAPI na Mkurugenzi Mtendaji Wa Kampuni ya Mwafrika Pharmaceutical Ltd ya jijini Tanga, baada ya kutambulishwa kwake na Bw.Geoffrey Mwambe, Mkurugenzi Mtendaji wa TIC anayeongoza ujumbe wa Tanzania, nchini humo.
Balozi wa Tanzania nchini Korea Matilda Massuka akiulaki na kuukaribisha ujumbe wa Tanzania uliowasilini Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Seoul Incheon, nchini Korea kwa ajili ya ziara ya uhamasishaji uwekezaji na biashara katika sekta ya Dawa na Vifaa Tiba nchini Tanzania. Katika hatua ya awali, Ujumbe huo unaongozwa na Bw.Geoffrey Mwambe, Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, huku Ummy Mwalimu Waziri wa Afya wa Tanzania akitarajiwa kuungana na ujumbe huo nchini Korea mapema kesho kwa zaira ya kikazi ya siku tano (5) kuanzia Agosti 11 hadi15 mwaka huu

SERIKALI YASISITIZA WAFUNGWA KUTUMIKA KATIKA SHUGHULI ZA UZALISHAJI

$
0
0

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni amekabidhi mashine 10 za kufyatulia matofali kwa jeshi la magereza la mkoa wa Lindi na kuwataka kuzitumia ipasavyo ili kukabiliana na changamoto zinazowakabili ikiwemo makazi duni.

Mashine hizo ni sehemu ya ahadi aliyoitoa mwaka mmoja na nusu uliopita baada ya kufanya ziara katika mkoa wa Lindi. Masauni alikabidhi mashine hizo katika gereza la Lindi mjini mkoani hapa na kuwataka jeshi la magereza kujipanga ipasavyo namna ya kuzitumia ili ziwe na tija na manufaa kwao.

Alisema mwaka uliopita alifanya ziara ya kukagua shughuli za magereza na kukutana na changamoto mbalimbali ikiwamo makazi duni ya nyumba za udongo hasa katika gereza la Lindi Mjini. “Nawakabidhi mashine hizi leo, natarajia kuona mabadiliko yenye tija kutoka kwenu. Mkifanya vizuri nitawatafuta wadau wengine kwa ajili ya kuongeza mashine hizi,” alisema Masauni na kuongeza kuwa;

“Nataka gereza la Lindi Mjini liwe la mfano kwa magereza ya mkoa huu. Tumieni nguvu kazi ya wafungwa mlionao kwa ajili ya kuboresha makazi yenu,” alisema Masauni. Alisema atalishangaa jeshi la magereza endapo hawatumii ipasavyo nguvu kazi ya wafungwa wakati wana changamoto mbalimbali zinazowakabili na njia za kuzitatua zipo wazi. 

Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Lindi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Rajabu Nyange, akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), baada ya kupokea mashine kumi za kufyatulia tofali ambapo ni mpango maalumu wa Serikali kuondoa changamoto za makazi ya askari magereza nchini.Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi,Shaibu Ndemanga. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akipima ukubwa wa tofali lililofyatuliwa na moja ya mashine alizokabidhi kwa uongozi wa Gereza la Mkoa wa Lindi ikiwa ni mpango maalumu wa kuondoa changamoto ya makazi kwa askari magereza nchini. Wanaoshuhudia ni viongozi wa gereza hilo wakiongozwa na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Lindi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Rajabu Nyange (kulia). Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na viongozi wa Jeshi la Magereza mkoani Lindi. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Lindi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Rajabu Nyange. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

MANONGA QUEEN'S KUINGIA KAMBINI KESHO KUJIANDAA NA LIGI DARAJA LA KWANZA KWA WANAWAKE NCHINI

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

TIMU ya wanawake kutoka jimbo la Manonga Wilayani Igunga, Mkoani Tabora itaingia rasmi kambini kesho Augusti 13, 2018 kujiandaa na michezo ya kirafiki ili kujiweka sawa na michuano ya ligi daraja la kwanza Tanzania bara inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 6 mwaka huu.

Akizungumza na Blogu ya jamii msimamizi wa kambi hiyo Bi. Pendo Ndaki ambaye pia ni Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Ziba ameeleza kuwa Manonga Queens ipo katika hali nzuri sana na wapo tayari kwa mashindano hayo.Ameeleza kuwa timu hiyo inayojiandaa na ligi daraja la kwanza nchini tayari imeanza kujifua vikali kabla michuano hiyo kuanza kwa kuanza kucheza mechi za kirafiki.

Aidha mlezi wa timu hiyo ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Manonga Mh. Seif Khamis Gulamali ameeleza kuwa wamejidhatiti kufuzu kati ya timu mbili zitakazopanda daraja na Ametoa gharama zote za awali kwa ajili ya kambi hiyo ya maandalizi.

Mh.Gulamali amehimiza wadau wengine kujitoa zaidi kwa timu hiyo ili iweze kung'ara kwa kutoa ushirikiano wa hali na mali.Timu 18 zimethibitisha kushiriki Ligi Daraja la Kwanza kwa Wanawake litakaloanza Septemba 6, mwaka huu.

Ligi hiyo itachezwa katika mfumo wa makundi na timu 2 zitapanda daraja wakati zitakazobaki zitasalia kwenye ligi daraja la Kwanza. 

Timu zilizothibitisha ushiriki wao ni:

1.Yanga Princes -Dar es Salaam
2.TSC - Mwanza 
3.Mapinduzi Princess -Tanga 
4.Migoli Queens -Iringa 
5.Ruangwa Queens -Lindi 
6.Viva FC -Mtwara 
7.Singida Warriors -Singida
8.Katoro Queens -Geita 
9.Victoria Queens -Kagera 
10.Tanzanite FC -Arusha 
11.Mapinduzi Queens -Njombe 
12.Allans Queens -Dodoma 
13.Manonga Queens -Tabora
14.Abeehe Bha Kyela FC -Mbeya
15.Kisarawe Queens -Pwani 
16.Testimony -Kilimanjaro 
17.Mbinga Queens -Ruvuma 
18.Kizuka Sekondari -Morogoro 

Timu hizo shiriki ni kwa mujibu wa Afisa habari wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) Cliford Mario Ndimbo.

Tigo washinda cheti cha ushiriki kwenye Maonesho ya Nanenane Dodoma

$
0
0
Meneja Usambazaji wa Tigo Dodoma na Kondoa, Gidion Morris akisalimiana na viongozi mbalimbali mara baaada ya kukabidhiwa cheti cha ushindi kipengele cha mawasiliano kwenye maonesho ya Nanenane juzi mkoani Dodoma.
Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde akimkabidhi cheti cha Kipengele cha Mawasiliano Kanda ya Kati kwa Meneja Usambazaji wa Tigo, Gidion Morris kwenye sherehe ya maadhimisho ya maonesho sikukuu ya wakulima Nanenane viwanja vya Nzuguni mkoani Dodoma juzi.

VIDEO - MKUU WA MKOA WA RUVUMA CHRISTINA MNDEME AAGIZA TAKUKURU KUICHUNGUZA KAMPUNI YA ARDHI PLAN

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amemwagiza kamanda wa TAKUKURU wilaya ya Mbinga kuchunguza malipo ya zaidi ya shilingi milioni 525 iliyolipwa kampuni ya ARDHI PLAN na kuzuia madai ya zaidi ya shiingi milioni 500 inayodai kampuni hiyo,kutokana na upimaji wa Ardhi usiozingatia kanuni ya matumizi bora ya Ardhi katika vijiji vya Halmashauri ya Mbinga. Ambapo kampuni hiyo ni ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashuri hiyo Gombo Samandito.

MAONYESHO YA WAKULIMA NANENANE KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI 2018

$
0
0
Wakulima wakipata maelezo kutoka kwa wataalamu wa kilimo wa halmashauri ya Wilaya ya Momba katika banda la maonyesho ya nanenane, juu ya njia rahisi ya kupanda mboga za majani kwa kutumia magunia na mifuko hususan mahali pasipo na maeneo ya kupanda bustani.
Mhifadhi wa Mazingira na kilimo hai kutoka Wilaya ya Songwe Noah Ambokile Mbilinyi akitoa maelezo kwa Eddie Mhelela kuhusu aina mpya ya maboga ambayo yana uzito wa Kilogramu 15 mpaka 25 katika banda la wilaya ya Songwe kwenye maonyesho ya nanenane.
Mwanzilishi wa kikundi cha kutunza Mazingira cha Estate Vision Amani Zakaria Elias akitoa maelezo kwa baadhi ya wananchi waliojitokeza katika banda la maonyesho ya Nanenane katika halmashauri ya Wilaya ya Ileje, kikundi hicho kimeonyesha upekee kwa kuweka miche ya miti ya mtini na mizeituni ambayo ni adimu kupatikana.
Afisa Kilimo kutoka shirika la Norwegian Christian Aid Daniel Isaack akitoa maelezo katika maonyesho ya nanenane kuhusu teknolojia rahisi ya umwagiliaji wa matone ambayo inaweza kutumia maji lita 20 kumwagilia miche 52 ya mbogamboga, wakulima takriban 50 wa wilaya ya Mbozi wameanza kutumia teknolojia hii.

WAZIRI MKUU AMUAGIZA RPC LINDI KUMKAMATA KATIBU WA TSC

$
0
0

*Ni baada ya walimu kumtuhumu kwa ulevi, rushwa, kughushi nyaraka

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Lindi, Bibi. Pudencis Protas kumkamata Kaimu Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) wa wilaya ya Ruangwa Bw. Anthon Mandai kutokana na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka.

Ametoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa walimu wakimlalamikia kiongozi huyo kuwa na tabia za kudai rushwa, kutowapandisha madaraja, ulevi pamoja na kuwaita walimu hao kwenye vilabu vya pombe kwa ajili ya kuwasikiliza matatizo yao.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Agosti 12, 2018) wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Ruangwa akiwa katika siku ya mwisho ya ziara kyake ya kikazi wilayani hapa. Bw. Mandai anakaimu nafasi hiyo tangu Juni, 2012.

Amesema mbali na kulalamikiwa na walimu kwa tuhuma mbalimbali zikiwemo za ulevi na kuwaita walimu katika vilabu vya pombe pindi wanapohitaji kuhudumiwa, pia amekuwa akighushi nyaraka za mirathi, jambo linalosababisha baadhi ya familia za waliokuwa walimu kuchelewa kupata haki zao.

“Huyu Katibu ameshindwa kuwasaidia walimu katika kutatua changamoto zao na badala yake amekuwa akitumia vibaya majina ya viongozi wakuu, ambapo hata mimi alijaribu kutaka kunichakachua kwa kughushi muhtasari wa kikao cha mirathi ya Mwalimu Suwedi Chikawe akitumia jina langu kuwa nilikuwa mwenyekiti wa kikao hicho kilichokuwa na agenda ya kumbadilisha msimamizi wa mirathi aliyeteuliwa na familia jambo ambalo si la kweli,” amesema.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Agosti 12.2018, kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi Fadhili Juma, Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Hashim Mgandilwa.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Agosti 12.2018 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu Anthon Mandai, akipanda gali la Polisi mara baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, kumuagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi Pudencis Protas, kumkamata ili akajibu tuhuma zinazomkabili, Agosti 12.2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) .

TANZANIA YA PILI MICHEZO YA EAPCCO

$
0
0
Na. Jeshi la Polisi.

Michezo ya Majeshi ya Polisi Ukanda wa Afrika Mashariki (EAPCCO) imemalizika Jijini Dar es Salaam huku Jeshi la Polisi nchini likishika nafasi ya pili katika ushindi wa jumla ambapo nafasi ya kwanza imeenda Kenya na ya tatu Uganda.

Polisi Tanzania imeshika nafasi hiyo baada ya kuchukua jumla ya Medali 64, 15 za dhahabu, 25 za fedha na 24 za shaba huku Kenya ikiwa na medali 68, 25 dhahabu , fedha 20 na shaba 24.

Mshindi wa Tatu Uganda alijinyakulia Medali 36, Rwanda 27, Burundi nane, Sudani Kusini sita na Sudani moja ambapo timu za Polisi Tanzania zimetwaa ubingwa katika Soka, Mpira wa pete, Judo, na Kulenga Shabaha kwa upande wa Wanaume.

Akifunga Michezo hiyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi amewataka Wanamichezo hao kudumisha umoja na Amani katika mataifa wanayotoka ikiwemo kutumia michezo hiyo kubadilishana mbinu mbalimbali za kuzuia uhalifu.

Aliwapongeza Wanamichezo wote walioshiriki michezo hiyo kwa kuonyesha nidhamu na ushindani wa hali ya juu jambo ambalo limefanya michezo hiyo kuvutia watazamaji wengi. 

Wanamichezo wa Polisi Tanzania walioshiriki Michezo ya Wakuu wa Majeshi ya Polisi ukanda wa Afrika Mashariki (EAPCCO) iliyomalizika kwa Tanzania kushika nafasi ya pili kwa ujumla wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa  ufungaji wa michezo hiyo (Picha na Jeshi la Polisi). 
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na Wanamichezo wa Polisi Tanzania wakati wa ufungaji wa Michezo ya Wakuu wa Majeshi ya Polisi ukanda wa Afrika Mashariki (EAPCCO) iliyomalizika kwa Tanzania kushika nafasi ya pili kwa ujumla (Picha na Jeshi la Polisi). 
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akimkabidhi kombe la mshindi wa tatu nahodha wa timu ya mbio ya Polisi Tanzania wakati wa ufungaji wa Michezo ya Wakuu wa Majeshi ya Polisi ukanda wa Afrika Mashariki (EAPCCO) iliyomalizika kwa Tanzania kushika nafasi ya pili kwa ujumla (Picha na Jeshi la Polisi). 
Mwakilishi wa Jeshi la Polisi Rwanda akimkabidhi Kombe la mshindi wa Pili katika kulenga Shabaha Inspekta wa Polisi Tannzaia wakati wa ufungaji wa Michezo ya Wakuu wa Majeshi ya Polisi ukanda wa Afrika Mashariki (EAPCCO) iliyomalizika kwa Tanzania kushika nafasi ya pili kwa ujumla (Picha na Jeshi la Polisi). 
Mkuu wa Jeshi la Polisi la Kenya akimkabidhi kombe la Ubingwa wa mpira wa miguu Inspekta Hashim Abdalah kutoka Tanzania wakati wa ufungaji wa  Michezo ya Wakuu wa Majeshi ya Polisi ukanda wa Afrika Mashariki (EAPCCO) iliyomalizika kwa Tanzania kushika nafasi ya pili kwa ujumla (Picha na Jeshi la Polisi). KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

DKT. ASHATU KIJAJI: UJENZI WA VITUO VYA AFYA WAPAMBA MOTO NCHINI KOTE

$
0
0
Benny Mwaipaja, Kasulu, Kigoma 

Serikali imepanga kujenga zaidi ya vituo 120 vya afya nchini kote katika mwaka wa fedha 2018/19 ili kusogeza huduma za afya karibu zaidi na wananchi ikiwemo huduma ya mama na mtoto.

Hayo yamesemwa Mjini Kasulu, mkoani Kigoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, alipotembelea na kukagua ujenzi wa majengo mapya ya Kituo cha Afya Kiganamo, yaliyo gharimu shilingi milioni 500.

Amesema kuwa tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani imeongeza bajeti ya Wizara ya Afya kutoka shilingi bilioni 30 hadi kufikia shilingi bilioni 369, hatua iliyolenga kuboresha afya za wananchi kwa kuwa hakuna maendeleo kama wananchi watakuwa na maradhi.

“Awamu ya Tano ilianza na ujenzi wa vituo 44 vya afya na kufuatiwa na vituo 74 na sasa vituo takribani 120 vinaendelea kujengwa maeneo mbalimbali ili kutimiza lengo la kuwa na Kituo cha Afya kwa kila Kata”, alieleza Dkt. Kijaji.

Dkt. Kijaji, alisema Serikali imeweka utaratibu wa Kata ambazo zipo jirani kutumia kituo kimoja wakati lengo kuu la kujenga kituo kimoja cha afya kwa kila Kata likiendelea kutekelezwa katika uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akifurahia maelezo ya Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu Mkoani Kigoma Dkt. Mshana Dastan, kuhusu namna walivyojipanga kuhakikisha kituo hicho kinaanza kutoa huduma kwa wakati kutokana na umuhimu wake kwa wakazi wa Kasulu na maeneo yanayoizunguka Wilaya hiyo. 
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu Mkoani Kigoma, Dkt. Mshana Dastan (kushoto), akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa Chumba cha kuhifadhia maiti ikiwa ni sehemu ya majengo mapya yaliyojengwa na Serikali kwa gharama ya shilingi milioni 500, likiwemo jengo la wodi ya akina mama, maabara, nyumba ya mganga na miundombinu mingine, wakati Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), alipofanya ziara kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya kituo hicho cha afya. 


CCM YASHINDA UDIWANI KATA YA MAWENZI,KILIMANJARO

$
0
0
Na Dixon Busagaga ,Moshi.

MGOMBEA udiwani katika kata ya Mawenzi ,manispaa ya Moshi ,Apaikunda Naburi (CCM) amefanikiwa kushinda nafasi hiyo akiwashinda wagombea wengine baada ya kupata kura 400 sawa na asilimia 70.3 kati ya kura 569 zilizopigwa.

Naburi aliyekuwa diwani wa kata ya Mawenzi katika kipindi cha mwaka 2010-2015 kabla ya kushindwa na aliyekuwa Diwani wa kata hiyo ,Hawa Mushi aliyefariki dunia hivi karibuni baada ya kuugua ghafla.Mgombea huyo amefanikiwa kurejea kwenye nafasi hiyo kwa kuwashinda Afrikana Mlay wa Chadema na na Isaac Kereti wa SAU waliokuwa wakiwania kiti hicho.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi msimamizi wa uchaguzi , Erasmo Silayo alimtangaza Naburi kuwa mshindi halali wa kiti hicho huku akitaja kura za mgombea aliyefuatia kuwa ni Afrikana Mlay (Chadema) aliyepata kura 163 huku mgombea Isack Kireti (SAU) akiambulia kura 2.

.Akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi,Naburi amewashukuru wapiga kura katika kata hio huku akiwaahidi ushirikiano katika kuwatumikia.
"Idadi ya wapiga kura waliojiandikisha ni 1821, kati yao idadi halisi ya wapiga kura ni 569 ambapo kura 4 ziliharibika"alisema Silayo.
 Msimamizi wa uchaguzi , Erasmo Silayo akimtangaza Naburi kuwa mshindi halali wa kiti hicho huku akitaja kura za mgombea aliyefuatia kuwa ni Afrikana Mlay (Chadema) aliyepata kura 163 huku mgombea Isack Kireti (SAU) akiambulia kura 2.
 Msimamizi wa uchaguzi , Erasmo Silayo akimkabidhi cheti cha ushindi kwa Naburi mara baada ya kutangazwa mshindi halali wa kiti hicho huku akitaja kura za mgombea aliyefuatia kuwa ni Afrikana Mlay (Chadema) aliyepata kura 163 huku mgombea Isack Kireti (SAU) akiambulia kura 2.
 MGOMBEA udiwani katika kata ya Mawenzi ,manispaa ya Moshi ,Apaikunda Naburi (CCM) akionesha cheti chake mara baada ya kushinda nafasi hiyo akiwashinda wagombea wengine baada ya kupata kura 400 sawa na asilimia 70.3 kati ya kura 569 zilizopigwa.
Wakisherehekea ushindi wao mara baada ya kutangazwa mshindi

MKUU WA MKOA WA PWANI, MHANDISI NDIKILO ASHIRIKI UJENZI WA KITUO CHA AFYA KIRONGWE MAFIA

$
0
0


Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo (kushoto) pamoja na mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Pwani ,Ramadhani Maneno, wakishiriki katika nguvu kazi ya ujenzi wa kituo cha afya Kirongwe wilayani Mafia ,wakati wa ziara ya kamati hiyo kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM kwa kipindi cha miaka miwili na nusu ya uongozi wa serikali ya awamu ya tano. Kuanza kwa ujenzi huo imetokana serikali kutoa kiasi cha sh. milioni 500 kwa ajili ya ujenzi huo ambao utakapokamilika kituo kitahudumia takribani wakazi kutoka vijiji vingi vinavyozunguka kata ya Kirongwe .(picha na Mwamvua Mwinyi).
Sehemu ya ujenzi wa mradi wa maji safi na salama ,(inayoonekana pichani),unaojengwa kijiji cha Jibondo ,wilayani Mafia,mkoani Pwani ,ambao utakapokamilika utakaogharimu karibia bilioni mbili .(picha na Mwamvua Mwinyi).
Mkuu wa Mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo akibeba ndoo ya samaki kumimina katika beseni la mama ambae anauza biashara ya samaki kwenye mwalo wa samaki wilayani Mafia.(picha na Mwamvua Mwinyi).

Wizara ya Mambo ya Nje yahamasisha uwekezaji katika sekta ya Kilimo na Mifugo

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda amefanya mazungumzo na kampuni ya Burmeister & Partiners (PTY) LTD ya nchini Namibia tarehe 10 Agosti 2018 mjini Windhoek, Namibia.

Akiongea na uongozi wa kampuni hiyo Prof. Mkenda alieleza Tanzania ina eneo kubwa la ardhi yenye rutuba ambayo haitumiki na rasilimali watu ya kutosha hivyo ni fursa kwa mwekezaji mwenye nia thabiti kuwekeza nchini.

“Lengo la Serikali ni kupata mwekezaji aliye makini kama wewe nimeona una mradi mkubwa wa shamba la mifugo na vifaa vya kisasa kwa ajili ya machinjio nina imani ukija kuwekeza Tanzania hautajutia kabisa kwakuwa matumizi ya teknolojia ya kisasa katika miradi itaongeza thamani ya mazao na bidhaa zitakazozalishwa na kuwezesha kupatikana kwa soko la kimataifa” alisema Prof. Mkenda

Naye Mkurugenzi wa kampuni hiyo Mhandisi Hendrik Boshoff alieleza kampuni imekuwa ikifanya kazi katika mataifa mbalimbali ambapo kampuni hiyo imefungua kampuni ya maziwa nchini Rwanda ambayo inauza na kusafirisha mataifa mengine pia imewekeza nchini Angola katika miradi ya uvuvi na imekuwa ikifanya vizuri katika biashara zake zote.

Pia alisema kampuni imebobea katika miradi ya ujenzi, nishati, miradi ya maji, usafiri, usanifu majengo, ujenzi wa majengo, miradi ya machinjio, mashamba ya mifugo na pia ipo katika mpango wa kuanzisha miradi ya viwanda vya dawa za binadamu ambapo utekelezaji wake utaanza mara baada ya kukamilisha mazungumzo na wataalamu kutoka nchini Cuba.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda(kulia) akizungumza na mwakilishi wa kampuni ya Burmeister and Partners (PTY) LTD alipowatembela katika ofisi za kampuni hiyo iliyopo Windhoek, Namibia tarehe 10 Agosti 2018. Kulia kwa Katibu Mkuu ni ujumbe ulioambatana naye katika ziara hiyo, Mratibu wa Maendeleo na Ushirikiano wa Kimataifa katika Kilimo kutoka Wizara ya Kilimo Tanzania, Bi. Magreth Ndaba, Mkurugenzi wa Sera na Mipango katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki , Bw. James Lugaganya na Balozi wa Tanzania nchini Namibia, Mhe. Sylivester Ambokile. 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Burmeister & Partners (PYT) LTD, Mhandisi Hendrik Boshoff akielezea usanifu wa miradi mbalimbali unaofanywa na kampuni ya Burmeister & patners (PTY) LTD. 
Sehemu ya ofisi iliyosanifiwa na kampuni hiyo. 
Prof. Mkenda akifafanua tunu na rasilimali zilizopo nchini ambazo ni fursa kwa uwekezaji. 


Taasisi ya RSA yafanya Kongamano Dodoma Dhima kuu ikiwa ni Mabadiliko ya Sheria ya Usalama Barabarani

$
0
0
Na. Vero Ignatus Dodoma. 

Taasisi ya mabalozi wa usalama barabarani nchini wamefanya kongamano la siku Mkoani Dodoma dhima kuu ikiwa '' Mabadiliko ya sheria ni muhimu katika kuimarisha usalama nchini''

Kongamano hilo limefanyika kwasababu ya mkono mabadiliko ya sheria za usalama barabarani kushirikiana /kuwahusisha viongozi wanaohusika na mambo ya kisera na waunge mkono mabadiliko ya sheria hiyo. 

Mkurugenzi wa habari na mawasiliano RSA, ambae pia ni mjumbe wa Baraza la Taifa usalama barabarani Augustus Fungo amesema kuwa wanahitaji mabadiliko ya sheria ya usalama barabarani kwani iliyopo haikidhi na imepitwa na wakati kwani ilitungwa mwaka 1983. 

'' Wakati sheria hii ikitungwa sayansi na teknolojia ilikuwa haijashika kasi kama ilivyo sasa, barabara zetu, vyombo vya moto vilikuwa vichache tofauti na miaka ya leo'' alisemaFungo.

Kwa upande wake Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Tanzania Fortunatus Musilim amewapongeza RSA kwa ushirikiano wao na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa mbalimbali pale ajali inapotokea na hata pale sheria zinapovunjwa hata uhalifu unapotokea. 
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini Patrobas Katambi ambae pia alimuwakilisha mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahengeakizungumza katika kongamano la Usalama. Barrabarani lililoandaliwa na Mabalozi wa usalama barabarani( RSA) na kufanyika katika Ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Dodoma jana. Picha na Vero Ignatus
 Mwalimu wa Elimu ya Usalama barabrani ambae pia ni mmoja wa Baraza la Usalama. Barabarani Nchini. Picha na Vero Ignatus
 Mkuu wa wilaya ya Gairo Siriel Mchembe akizungumza katika kongamano hilo Jijini Dodoma. Picha na Vero Ignatus
Mkurugenzi wa Huduma ya Sheria Nchini Marlin Komba Akiwa na Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama barabarani Nchini Fortunatus Musilim. Picha na Vero Ignatus. 
 Wa kwanza kushoto ni mwenyekiti wa Mabalozi wa Usalama Barabarani Nchini (RSA) John Seka akifuatiwa na Kamanda wa Polisi Kikosi chq Usalama Barabarani SACP Fortunatus Musilim, Mkuu wa wilaya ya Gairo Siriel Mchembe, Mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini Patrobas Katambi, Mkuu wa Polisi kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Iringa Kamotta, na Mkurugenzi wa Huduma ya sheria Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Marlin Komba. Picha na Vero Ignatus. 

LUGOLA AAGIZA POLISI KUWAKAMATA WALIOFANYA UFISADI SEKTA YA MICHEZO

$
0
0

Na Felix Mwagara, MOHA

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amemtaka Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Bunda kuwakamata watu walioshiriki kuwatapeli wananchi katika Sekta ya michezo wilayani humo, Mkoa wa Mara.

Watu hao ambao walitangaza kuanzisha ligi wilayani humo na kuzitaka timu za mpira wa miguu kata mbalimbali zichangie fedha na baadaye ligi hiyo haikufanyika na watu hao walikimbia na fedha hizo na kufanya wananchi hao waandamane wakitaka fedha zao zirudishwe.

Waziri Lugola akizungumza na mamia ya wananchi wa Mji wa Bunda baada ya kulizindua Bonanza la Amani wilayani humo, alisema kitendo walichokifanya watu hao ni ufiadi mkubwa hivyo lazima wakamatwe ili iwe funzo kwa wale wote wenye tabia ya kufanya ufisadi wa aina hiyo katika sekta ya michezo nchini.

“Nimeambiwa wanamichezo ambao walichangishwa waliandamana mpaka kwa Mkuu wa Wilaya kuelezea jinsi walivyoibiwa na watu hao, hata hivyo Mkuu wa Wilaya alitangaa watu hao warudishe fedha hizo, ila mimi nahitaji hawa watu wakamatwe haraka iwezekanavyo, huu ni ufisadi mkubwa na hakika Serikali hii ya awamu ya nne haitakubaliana na ufisadi huo.

Aliongeza kua, mahakama ya ufisadi inahitaji wateja hivyo waliofanya wizi huo pia ni mafisadi hivyo lazima wakamatwe haraka iwezekanavyo ili sheria ichukue mkondo wake. Aidha, Bonanza ambalo alilizindua waziri huyo, linatarajiwa kufanyika nchini nzima limezinduliwa mjini humo na baadaye litafanyika nchi nzima likiwa na lengo kuu kutangaza amani nchini.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>

MADIWANI WAWILI CUF MAFIA WARUDI CCM LEO

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,MAFIA

MADIWANI wawili kutoka chama cha wananchi (CUF) kata ya Kilindoni na Jibondo ,wilayani Mafia ,Mkoani Pwani, wamejihudhuru nyadhifa zao na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi(CCM) ,kutokana na chama tawala kurudisha heshima na kuwa sikivu nchini.

Madiwani hao wamerudi CCM katika ziara ya kamati ya siasa mkoani Pwani ,iliyoweka kambi siku mbili wilayani humo,kutembelea miradi na kukagua utekelezaji wa chama hicho . Aliyekuwa diwani wa Jibondo Hassan Mohammed Hassan ,alisema amefanya maamuzi hayo kutokana na chama walichokuwepo kukosa mwelekeo na kukosa sera zinazojiuza. 

Alisema ,kata ya Jibondo ilikuwa na wafuasi wa CCM ambapo ilipofika 2004 wengi wao walihamia upinzani kutokana na baadhi ya mambo kutokwenda wanavyotaka.“Nampongeza Rais Dk.Magufuli, mkuu wa mkoa wa Pwani, wilaya na CCM Mafia na mkoa kwa juhudi zao katika kuinua uchumi wa nchi na kukuza sekta ya viwanda na uwekezaji” alibainisha Hassan. 


Aliyekuwa diwani wa Jibondo wilayani Mafia Hassan Mohammed Hassan ,akimpa mkono Mwenyekit wa Chama Cha Mapinduzi,Mkoani Pwani Ramadhani Maneno baada ya kujihudhuru nyadhifa yake na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi(CCM) (picha na Mwamvua Mwinyi).KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

DKT ASHATU KIJAJI AINYOOSHEA KIDOLE WAKALA WA MAJENGO-TBA

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, Kasulu, Kigoma

Naibu Waziri wa Fefha na Mipango. Dkt. Ashatu Kijaji, ameiagiza Wakala wa majengo Tanzania-TBA, kutekeleza kwa wakati mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri ya Mji wa Kasulu Mkoani Kigoma ili kuiepusha Serikali kutumia fedha nyingi kutokana na kuongezeka kwa gharama za miradi husika kunakotokana na ucheleweshwaji huo.

Dkt. Kijaji ametoa kauli hiyo baada ya kukagua maendelelo ya ujenzi wa Ofisi mpya za Halmashauri ya Mji wa Kasulu zinazojengwa na Serikali kwa zaidi ya shilingi bilioni 2.5 na kutaarifiwa kuwa TBA, wamechelewa kuanza ujenzi huo kwa zaidi ya miezi 12 wakati fedha zilikwisha tolewa na Serikali.

Aliishauri TBA kujipanga kukamilisha miradi inayopewa na Serikali kwa wakati kwa kuongeza idadi ya wataalam wanaoweza kusimamia miradi mingi inayotekelezwa na wakala huo.

"Pesa zipo, Serikali haiwezi kuanza kutekeleza mradi wowote kama hakuna pesa, ni jukumu lenu kama TBA kuhakikisha mnawezesha mradi huu ukamilike kwa wakati ili tupate thamani halisi ya fedha za mradi" alisisitiza Dkt. KijajiDkt. Kijaji alitoa wito kwa wakazi wa Mji wa Kasulu na Kigoma kwa ujumla kuchangamkia fursa za ujenzi wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali katika maeneo yao kwani lengo la Serikali kujenga miradi hiyo ni kuwawezesha pia wananchi kiuchumi.

Hatua hiyo inafuatia taarifa iliyotolewa na Mhandisi wa ujenzi wa Jengo hilo la Ofisi ya Halmashauri ya Mji wa Kasulu, Bw. Abubakari Basuka, kwamba miongoni mwa changamoto inayoukabili mradi huo ni ukosefu wa mafundi mchundo na vibarua ambapo imeelezwa kuwa vijana wengi katika eneo la mradi hawajitumi kufanyakazi.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto), akiwasili kukagua mradi wa Ujenzi wa Jengo la Ofisi mpya za Halmashauri ya Mji wa Kasulu, Mkoani Kigoma, katikati ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu, Bi. Fatina Hussein Laay, na kulia ni Mhandisi wa mradi huo Bw. Abubakari Basuka.
Mhandisi wa mradi wa Ujenzi wa Jengo la Ofisi mpya za Halmashauri ya Mji wa Kasulu Mkoani Kigoma Bw. Abubakari Basuka (aliyevaa kofia) akisoma taarifa fupi ya Mradi kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), wa tatu Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Simon Anange.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu Bi. Fatina Hussein Laay (kushoto), akieleza umuhimu wa kukamilika kwa ujenzi wa jengo la Ofisi za Halmashauri yake ya Mji kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (katikati) kwa kuwa ofisi zinazotumika sasa hazikidhi mahitaji, wa pili kulia ni Kamishna wa Kodi za Ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania - TRA, Bw. Elijah Mwandumbya.
Muonekano wa mradi wa Ujenzi wa Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Mji Mkoani Kigoma litakalo gharimu takribani Sh. Bilioni 2.5.

Serikali ya Sierra Leone yatembelea bodi ya mikopo kujifunza utendaji wa bodi katika utoaji wa mikopo

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii .

SERIKALI ya Sierra Leone kupitia wizara Elimu na Ufundi na Elimu ya Juu umetembelea Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Nchini (HESLB) kujifunza na bodi hiyo inavyotoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu .

Ujio huo umekaa kwa wiki moja katika bodi hiyo ikiwa ni kuangalia namna ya kuweza kujifunza na kwenda kuanzihsa chombo hicho nchini Sierra Leone.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Nchini (HESLB) , Abdulzaq Badru amesema kuwa nchi sierra leone kufika hapo ni kutokana na umahiri katika uchakataji wa mikopo kwa wanafunzi kwa elimu ya juu.

Amesema kuwa ujumbe huo umepita katika nchi ya Ghana na kisha Tanzania kuangalia namna ya uendeshaji wa bodi katika utoaji wa mikopo.

Ujumbe huo uliongozwa na Naibu Waziri wa Elimu , Ufundi na Elimu ya Juu ya Nchini Sierra Leone Dkt. Turad Senesie , Naibu Katibu Mkuu Wizara fedha Mr. Matthew Dingie , Naibu Mkurugenzi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii na Bima Mohammed Gondoe na wajumbe wengine.

Naibu Waziri wa Elimu , Ufundi na Elimu ya Juu ya Nchini Sierra Leone Dkt. Turad Senesie amesema HESLB inafanya vizuri katika uchakataji wa mikopo na kusema kuwa wanatarajia kuanzisha chombo kama hicho nchini kwao.
Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Nchini (HESLB) , Abdulzaq Badru akizungumza na waandishi wa habari  (hawapo pichani) wakati wa kuwaaga ujumbe wa Sierra Leone waliotembelea bodi hiyo.
Naibu Waziri wa Elimu , Ufundi na Elimu ya Juu ya Nchini Sierra Leone Dkt. Turad Senesie akizungumza na waandishi habari kuhusiana na alichojifunza katika bodi ya mikopo.
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images