Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live

NHIF KAGERA YAHAMASISHA USHIRIKA AFYA KWENYE MAONESHO YA NANE NANE.

0
0
Na Editha Karlo,Kagera

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Kagera umewahamasisha wakulima kupitia vyama vya ushirika na masoko kujiunga na mpango wa ushirika afya (AMCOS)katika maonesho ya nane nane Mkoani humu yalifonyika katika viwanja vya Kakyailabwa (AMCOS)Kujiunga na mpango wa ushirika afya viwanja Kyakailabwa.

Akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Maico Gaguti Meneja wa Mfuko wa bima ya afya Mkoa wa Kagera Elias Odhiambo alisema kuwa ushirika afya ni mpango maalum wa Bima ya afya kwa wakulima ambapo mpango huo utawawezesha wakulima kuchangia mara moja gharama za matibabu na kuwa na uhakika wa matibabu kwa mwaka mzima pale wanapougua.

Odhiambo alisema watakaojiunga na mpango huu watapata matibabu kwenye vituo vya tiba vilivyosajiliwa na mfuko nchi nzima ikiwa ni pamoja na huduma za kibingwa na vipimo.

Katika viwanja vya kyakailabwa kwenye maonyesho ya sikukuu ya nane nane banda la NHIF lilisheheni huduma mbali mbali ikiwa ni pamoja na upimaji afya bila malipo kwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza, usajili wa Ushirika Afya,Toto Afya na Bima kwa wajasiliamali ambapo muitikio wa wananchi kujitokeza kupima afya zao ni mkubwa

Mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Generali Marco Gaguti alitembelea banda la NHIF na kushiriki katika upimaji wa Afya pia alihaidi kuhamasisha wakulima kujiunga na mpango huo kwaninutawasaidia wakulima kuwa na uhakika wa matibabu pale wanapougua wao na familia zao.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Maico Gaguti akipima afya kwenye banda la mfuko wa bima ya afya(NHIF)kwenye viwanja vya Kyakailabwa wakati wa sherehe za nane nane.
Meneja wa Bima ya afya Mkoa wa Kagera Elias Odhiambo akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Maico Gaguti juu ya mpango wa ushirika afya kwa wakulima
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Maico Gaguti akipata maelezo kutoka kwa mtumishi wa mfuko wa bima ya afya katika banda la NHIF baada ya kutembelea kwenye nane nane viwanja vya Kyakailabwa


MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA (TFDA) YAFUNGUA UKURASA MPYA KWA WADAU KATIKA KUANZISHA VIWANDA VYA USINDIKAJI VYAKULA NCHINI

0
0
 Wadau kutoka Umoja wa Miradi kwa Viziwi, wanaongalia kamera msitari wa mbele kulia, Fatina Huseni (wa kwanza), Tungi Kenneth (wa pili) wakimwangalia mkalimani wao Bi. Edna, wakati wakifuatilia mada zilizokuwa zinatolewa na TFDA.
 Kaimu Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula wa TFDA, Dkt. Candida Shirima, ambaye pia alimwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (katikati), Meneja wa TFDA Kanda ya Mashariki, Bw. Emmanel Alphonce (kushoto) na Kaimu Meneja wa Ukaguzi wa Chakula, TFDA Makao Makuu, Bw. Lazaro Mwambole (kulia) wakifuatilia majadiliano ya wadau wenye nia ya kuanzisha viwanda vya usindikaji chakula nchini (hawapo nchini)..
 Picha ya pamoja baina ya viongozi wa TFDA na baadhi ya watumishi wa TFDA walioshiriki Ktika kikao hicho.  Waliokaa kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula wa TFDA, Dkt. Candida Shirima, ambaye pia alimwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA (wa pili), Meneja wa TFDA Kanda ya Mashariki, Bw. Emmanel Alphonce (wa kwanza), Mwenyekiti mteule wa kikao hicho, Bw. Hussein Tarimo (wa tatu) na Meneja Ukaguzi wa Chakula, TFDA Makao Makuu, Bw. Lazaro Mwambole.
Meneja wa TFDA Kanda ya Mashariki, Bw. Emmanel Alphonce, akisisitiza jambo kwa washiriki.

Na James Ndege – Dar es Salaam
Wahenga walinena “Penye Nia Pana Njia”, leo hii, usemi huu umedhihirika kuwa kweli baada ya TFDA kufanya kikao na wadau takribani 80 kutoka mikoa mbalimbali nchini, wenye nia ya kuanzisha viwanda vya usindikaji vyakula lakini pia wale wenye nia ya kuviboresha vilivyopo. Kikao kazi hiki cha siku moja kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Margareth Ndomondo-Sigonda uliopo Makao Makuu ya TFDA, jijini Dar es Salaam tarehe 07/8/2018.

Katika hotuba ya ufunguzi wa tukio hili, Kaimu Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula wa TFDA, Dkt. Candida Shirima, ambaye pia alimwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa alisema, “Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli imeelekeza Taasisi za Serikali kuwezesha uanzishaji wa viwanda vingi nchini kwa kadri iwezekanavyo ili kuinua uchumi wa jamii na Taifa na haya ni matokeo ya utekelezaji wa maelekezo hayo ambapo tarehe 30 Julai, 2018, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu katika kikao kama hiki kilichofanyikia katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) alielekeza TFDA kuweka mazingira rafiki ya uanzishaji wa viwanda husika nchini mara moja”.

Pamoja na mambo mengine, TFDA iliwasilisha mada zinazohusu “Mahitaji Muhimu ya Kuzingatia Katika Kuanzisha Kiwanda cha Chakula na Utaratibu wa Usajili wa Majengo na Bidhaa ambapo wadau walipata fursa ya kuuliza maswali na kupata ufafanuzi kutoka kwa wataalam wa Mamlaka hali ambayo iliwafanya wadau hao kuondoa mashaka waliyokuwa nayo kuhusu changamoto walizofikiria kwamba zingeweza kuwa kikwazo katika safari ya uanzishaji na ukuzaji viwanda vya chakula nchini.

Baada ya majadiliano ya kina, kikao kiliweka maazimio ili kurahisisha uanzishaji wa viwanda kusudiwa  ambapo Meneja wa TFDA Kanda ya Mashariki, Bw. Emmanuel Alphonce aliaahidi kwamba kuanzia tarehe 09/8/2018, atateua Afisa wake mmoja ambaye atafanya kazi maalum ya kusikiliza changamoto za wadau hao na kutoa ushauri wa namna ya kuzitatua na pia kutoa namba zake za simu sanjari na za Makao Makuu kwa mtu yeyote atakayehitaji msaada zaidi ili azma ya uanzishaji viwanda vya usindikaji vyakula itimie.

TPB YAWAKUMBUKA WANAFUNZI WA SHULE YA MLALE SEKONDARI ILEJE

VOA Swahili: Duniani Leo Agosti 8, 2018

Michezo ya Majeshi ya Polisi Ukanda wa Afrika Mashariki (EAPCCO) yashika kasi jijini Dar es salaam

0
0
Na Jeshi la Polisi.
Michezo ya Majeshi ya Polisi Ukanda wa Afrika Mashariki (EAPCCO)  imeendelea kupamba moto huku Tanzania ikiwa imepata medali ya dhahabu katika mbio za mita 5000,Fedha moja na Shaba tano katika mchezo wa Karate.
Mwanariadha Fabian Nelson ndiye aliyefungua pazia kwa kuipatia Tanzania medali ya dhahabu baada ya kuwapita wenzake kutoka Kenya ambao walipata medali za fedha na Shaba.

Matumaini makubwa kwa Tanzania yapo katika mchezo wa kulenga shabaha, Judo,  Mpira wa Miguu na Riadha kwa upande wa mbio ndefu ambapo wanariadha wanaoshiriki michezo hiyo wameonyesha kiwango kikubwa.
Nahodha wa timu ya kulenga Shabaha Tanzania Inspekta  Noel seng'ng'e, amesema mchezo huo umekuwa mzuri kwani wameweza kutoa wachezaji wengi wazuri katika kulenga shabaha na wanaimani ya kuibuka na ushindi wa jumla katika mchezo huo.
Kwa Upande wake Kocha wa Timu ya Mpira wa Miguu John Tamba amesema vijana wake wako vizuri na morali ipo juu hasa ukizingatia ushindi walioupata katika mchezo wa awali baada ya kuichapa Polisi Uganda mabao 2 kwa 1.
“Mchezo unaofuata tunacheza na Rwanda hivyo tumefanya mazoezi mepesi ili kuhakikisha kuwa tunaibuka na ushindi utakaotufanya tuendelee kuongoza katika mpira wa miguu na hatimaye kuchukua ubingwa” Alisema Tamba.
Hata hivyo nchi za Rwanda, Kenya  na Uganda nazo zimeonyesha ushindani mkubwa baada ya kunyakua ushindi katika Mchezo wa Karate na mbio fupi huku wakiendelea kuchukua alama katika mpira wa mikono, pete na Karate.
Michezo inayoshindaniwa mwaka huu ni pamoja na soka ,mpira wa mikono, mpira wa wavu, mpira wa pete, Ngumi, Taekwondo, Judo na Riadha ambapo inafanyika katika Uwanja wa Taifa kwa riadha na michezo mingine inafanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
 Soka
 Volleyball
Karate

HABARI ZA UMOJA WA MATAIFA KUTOKA NEW YORK, MAREKANI

The 8th INTERNATIONAL AFRICAN FESTIVAL In TUEBINGEN,GERMANY STARTS TOMORROW TO 12th August 2018

0
0
 The biggest African festival in Germany will be held from August 9 to 12 2018 in Tübingen. It will will turn the Festplatz Tübingen into an African village displaying the very best of Africa and Africans in Germany. There, the audience is able to experience great bands and artists with live music (such as Ngoma Africa Band, X-Maleya, Saidi Kanda with Mvula Mandondo Band etc), dance performances, workshops, African food and drinks, a bazaar/market and program for children.
 Since the United Republic of Tanzania has been chosen as the focus country of this year’s Festival, Dr Abdallah Saleh Possi, Tanzania’s Ambassador for the Federal Republic of Germany will be welcomed as a special guest.
 A special highlight will be GAIEXPO (German African International Expo) to promote trade and international cooperation between African countries and Germany as well as other European countries. There will be an economic and educational forum and an open exchange on socio-cultural and economic development.
 Moreover, the visitor has the chance to get to know the wonderful continent and the people. In addition, the event promotes diversity, peace and love between people from different backgrounds. It also advocates African countries as tourist and investment destinations in addition to challenging Africans in the diaspora to play key roles in the development of their home countries.
Unlike most African festivals which are organised by non-Africans for Africans, the International Afrika Festival Tübingen is planned by Sunjo and Susan Tatah. They are both from Cameroon and work in close collaboration with a team of Africans and local German authorities.
 To enjoy the festival, visitors have the opportunity to camp and park for free. Those who like to swim and enjoy the sun can check out the swimming pool next to the festival.

For further information about the Afrika Festival, visit: www.afrikafestival.net or Facebook.com/AfricactivFestival

KATIBU WA BUNGE, WANANCHI NA WANAFUNZI WATEMBELEA BANDA LA BUNGE KATIKA MAONYESHO YA NANENANE JIJINI DODOMA

0
0
 Mwananchi Mkazi wa Jiji la Dodoma ambaye pia ni mlemavu asiyeona akiipapasa SIWA ya mfano baada ya kutembelea Banda la Ofisi ya Bunge katika Maonyesho ya Nanenane Jijini Dodoma.
 Afisa wa Ofisi ya Bunge, Ndugu Omary Machunda akitoa elimu kuhusiana na Bunge kwa wanafunzi  na raia wengine waliotembelea Banda la Ofisi ya Bunge katika maonyesho ya Nanenane Jijini Dodoma.
 Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai akipewa maelezo ya shughuli zinazofanywa na maafisa wa Ofisi ya Bunge katika maonyesho ya Nanenane Jijini Dodoma baada ya kutembelea Banda la Ofisi hiyo. Anayetoa maelezo ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu kwa Umma na Mwasiliano Bi. Zuhura Mtatifikolo.
Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai akipewa maelezo ya shughuli zinazofanywa na maafisa wa Ofisi ya Bunge katika maonyesho ya Nanenane Jijini Dodoma baada ya kutembelea Banda la Ofisi hiyo. Anayetoa maelezo ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu kwa Umma na Mwasiliano Bi. Zuhura Mtatifikolo.

BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO 08.08.2018

NSSF FUATENI WANANCHI WALIPO MSIWANGOJE WAJE OFISINI KUJIUNGA - RC KIGOMA

0
0
WATENDAJI wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii(NSSF) wametakiwa kwenda walipo wananchi ambao hawako katika sekta isiyo rasmi ili wawaze kutoa elimu ambayo itawezesha kujiunga na hatimaye wanufaike na mafao mbalimbali yanayotolewa na Mfuko huo. 
 Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga mara baada ya kutembelea banda la NSSF wakati wa kilele cha maonesho ya nane nane kwa kanda ya Magharibi yalifanyika mjini Tabora. 
 Alisema mpango huo unachama wa hiari na sekta binafsi unatakiwa kuwafikia wananchi wengi ambao wamejiari wenyewe ili nao wajiunge kwa ajili ya kujiwekea akiba ya uzeeni kupitia michango ambayo watakuwa wakichangia kila mwezi wakati wakiwa na nguvu. 
 Brigedia Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga alisema jambo hilo ni zuri kwani tangu Tanzania ipate uhuru wake mwaka 1961 hakuna Mfuko ambapo uliweza kumjali mtu asiye katika sekta isiyo rasmi na kuongeza kuwa ni jukumu la Watumishi wa NSSF kwenda kwao ili wawahimize waweze kuchangamkia fursa hiyo ambayo ni msaada kwao. 
 “Msisubiri wananchi wawafuate bali mnatakiwa kuwafuata walipo katika shughuli zao na kuwaelimisha ili hatimaye wengi wajiunge”alisema. 
 Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alisema Mfuko huo umekuja na mpango ambao umjali Mtanzania wa kipato cha chini naye kupata kiunua mgongo akichangia kwa miaka isiyopungua 15 kama alivyo mtumishi mwingine. 
 Alisema mpango huo unawahusisha watu kama vile mamalishe, boda boda, muuza karanga na wengine wote ambao walikuwa hawana mifuko ya kuchangia sasa wanatakiwa kujiunga na NSSF ili hatimaye kunufaika wakiwa wazee. 
 Naye Meneja wa NSSF Mkoa wa Tabora Nour Aziz aliwataka watu ambao sio waajiriwa katika sekta rasmi kuchangamkia kwani NSSF inawakinga na majanga ya kiuchumi na kijamii kwa kutoa mafao kulingana na taratibu zilizowekwa na hivyo kumwezesha kufanyakazi bila hofu kwa kuwa wanamwezesha kujenga maisha yao ya sasa na baadae. 
 Alisema kuwa kupitia michango ya shilingi 20,000 ambazo wanachama atatoa kila mwezi, akifikisha miezi mitatu na kuendelea atapata Kadi ya Matibabu ambayo itamwezesha yeye na watoto wake wanne na wenza kupata matibabu na huku akiba yake ikiwa palepale.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(kushoto) akitoa maelezo mafupi jana kwa mgeni wake ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga wakati walipotembelea banda la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii(NSSF) kwenye kilele cha maonesho ya nane nane kwa Kanda ya Magharibi ambayo yalifanyika mjini Tabora.
 Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii(NSSF) Mkoani Tabora Victor Mbesigwe (kulia) akitoa maelezo kwa wananchi juu ya uanachama wa hiari na jinsi mwananchi kutoka sekta binafsi navyoweza kujiunga. Alitoa amaelezo hayo leo wakati wa kilele cha maonyesho ya nane nane ambapo kwa kanda ya magharibi yalifanyika mkoani Tabora.
 Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii(NSSF) Mkoani Tabora Victor Mbesigwe (kushoto) akitoa maelezo kwa mwananchi Ngunda Shija (kulia) juu ya uanachama wa hiari na jinsi mwananchi kutoka sekta binafsi navyoweza kujiunga. Alitoa amaelezo hayo leo wakati wa kilele cha maonyesho ya nane nane ambapo kwa kanda ya magharibi yalifanyika mkoani Tabora.
Mtumishi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Tabora Ester Mng'omba (kushoto) akimsaidia Dereva wa Boda Boda kujaza fomu ya kuwa wanachama wa hiari mara baada ya kutembelea banda hilo jana wakati wa kilele cha maonyesho ya nane nane ambapo kwa kanda ya magharibi yalifanyika mkoani Tabora.
Picha na Tiganya Vincent

SHULE BORA YA WATOTO WALIO KATIKA MAZINGIRA HATARISHI KUJENGWA WILAYANI SAME.

0
0
Shirika la New Dawn Communities linalofanya kazi kata ya Njoro iliyoko Wilayani Same kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo toka Califonia nchini Marekani wameamua kujenga Shule hio tarajiwa  ambayo inategemea kupokea watoto yatima na walemavu kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha sita. 
Jiwe la msingi upande wa mabweni limewekwa na DC wa Same Mh. Rosemary Senyamule na Mch. Ron kutoka Marekani ambapo linategemea kupokea wanafunzi kuanzia Januari, 2019. 
Wadau wamepania kujenga pia tawi la Chuo kikuu cha Pippeliner (kilichopo Marekani)  katika eneo hilo. Waanza kushirikisha waliosoma chuo hicho kuchangia. 

Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe Rosemary Sitaki amewakumbusha kufuata sheria na taratibu za nchi zinazohusiana na mradi huo. Pia kawaasa kuweka utaratibu mzuri wa kuwapata watoto hao; na ametoa wito kwa wazazi na wananchi kutumia fursa hiyo badala ya kuwafungia watoto walemavu nyumbani. 
Mchungaji Mshomi ambaye ndiye mkurugenzi wa taasisi hiyo, amesema wanategemea kupokea wanafunzi zaidi ya 600 wenye uhitaji na kuwasomesha. Pia wanaendelea kushirikiana na jamii kwa huduma nyingine kama kilimo cha bustani, huduma ya maji bure, ujenzi wa barabara na wamekusudia kujenga uwanja wa kisasa wa mpira. Ameiomba jamii kuwapa ushirikiano. 
" Nawashukuru kwa kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano ya kutoa elimu bure na sera ya nchi inayotoa haki sawa ya elimu kwa watoto wakiwemo yatima na walemavu, asanteni sana"lisema DC Same. 

Yafuatayo yanafurahisha: Njoro uwanja wa mpira wa kisasa!
Njoro chuo kikuu.
Hakika
" Same is not same"


Uwekaji wa jiwe la msingi upande wa mabweni limewekwa na DC wa Same Mh. Rosemary Senyamule na Mch. Ron kutoka Marekani ambapo linategemea kupokea wanafunzi kuanzia Januari, 2019. 
 Sherehe za uwekaji jiwe la msingi
 Picha ya pamoja
Same is not the same!

JK amjulia hali Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla

0
0
Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo Jumatano Agosti 8, 2018 amemtembelea Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla aliyelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam kumjulia hali na kumpa pole kufuatia ajali ya gari aliyoipata Agosti 4, 2018 mkoani Manyara.

Clouds TV: Watoto wa Remmy Ongala Wamuenzi Baba yao kwa kuandaa Tamasha la Kimataifa

AZAM TV: HIGHLIGHTS: SIMBA 1-1 ASANTE KOTOKO (SIMBA DAY 8/8/2018)

TANZIA


BREAKING NEWZZZ: MWIGIZAJI KING MAJUTO AFARIKI DUNIA

0
0
Rais Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli siku waliopokwenda kumjulia hali King Majuto aliyelazwa katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam  Januari 31, 2018.

Msanii mkongwe  Mzee Amri Athuman al maarufu kama " King Majuto"  (pichani, enzi za uhai wake) amefariki dunia usiku huu katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es salaam alikokuwa amelazwa kwa siku kadhaa mara tu baada ya kurejea nchini kutoka nchini India alikopelekwa na serikali kwa matibabu.
Afisa habari wa Chama cha Filamu na Waigizaji, Masoud Kaftany, amethibitisha kifo cha King Majuto, wakati msanii maarufu mchekeshaji Lucas Lazaro Mhuvile maarufu kama Joti ameandika msiba huo katika mtandao wake wa Instagram, ikiambatana na picha yake akiwa na msanii Mpoki walipokwenda kumjulia hali hospiali.

Joti ameandika kwenye ukrasa wake wa Instagram: “R.I.P @Kingmajuto. metuachia Maumivu Makubwa sana ktk Tasnia ya Comedy Tanzania Sisi wanao,Tutakukumbuka kwa kazi zako,Upendo wako,Tabasamu lako Daima milele,Tulikupenda sana ila Mungu amekupenda zaidi,Pumzika kwa Amani Mzee wetu.”
Mwigizaji nyota wa vichekesho Steve Nyerere naye kwa masikitiko makubwa amethibitisha habari hiyo kwa kusema: "Kweli kaka, Mzee wetu katutoka. Tunalia kwa kumpoteza Mzee wetu..."
Muigizaji huyo alizaliwa mwaka 1948 jijini Tanga na kusoma shule Msambwini, huko huko Tanga.  Alianza fani ya kuigiza akiwa na umri mdogo wa miaka tisa, na toka wakati huo amekuwa kileleni katika fani ya uigizaji hadi mauti yalipomkuta.
Marehemu King Majuto alirejea nchini hivi karibuni akitokea nchini India alikokuwa amekwenda kwa ajili ya matibabu akisumbuliwa na ugonjwa wa tezi dume katika Hospitali ya Apollo. 
Mara aliporejea alipelekwa moja kwa moja katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya uangalizi.
Kabla ya kupelekwa nchini India Mei 4, mwaka huu, King Majuto ambaye pia alikuwa akisumbuliwa na tatizo la nyonga, alilazwa katika Hospitali ya Tumaini jijini Dar, kisha akahamishiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un 
( إِنَّا لِلّهِ وَإِنَّـا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ‎)
Pumzika kwa amani King Majuto. 
Mola aiweke roho yako mahala pema peponi... 
AMIN.

TULIMKAMATA HALIMA MDEE KWA TUHUMA ZA KUTOA LUGHA CHAFU YA MATUSI KWA RAIS AKIWA NYUMBANI KWAKE-MRAKIBU WA POLISI URAFIKI

0
0

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Urafiki, Mrakibu wa Polisi (SP) Batseba Kasanga ameileza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa alimkamata Halima Mdee kwa tuhuma za kutoa lugha chafu ya matusi kwa rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli akiwa nyumbani kwa wazazi wake.

Ameeleza kuwa, walipofika nyumbani kwa wazazi wa Mdee Ubungo Kibangu, alipokelewa na mama mzazi yake zazi ambaye baada ya kujitambukisha na mahojiani mafupi aliwaeleza wamsubiri Halima anajiandaa kwa kuwa alikuwa amepumzika kidogo.

Mrakibu Kasanga ambaye ni shahidi wa tatu wa upande wa mashtaka ameeleza hayo leo, Agosti 9,2018 wakati akitoa ushahidi dhidi ya kesi ya lugha ya matusi inayomkabili Mdee.Mdee anadaiwa, Julai 3,2017 katika Makao Makuu ya Ofisi ya Chadema,, alitamka maneno dhidi ya Rais John Magufuli kuwa “anaongea hovyohovyo , anatakiwa afungwe breki” na kwamba kitendo ambacho kingeweza kusababisha uvunjifu wa Amani.

Akiongozwa na wakili wa serikali Mwandamizi, Patrick Mwita mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amedai Julai 4, mwaka Jana, akiwa katika kituo cha polisi cha urafiki akiendelea na majukumu yake ya kawaida alipokea oda kutoka kwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kinondoni Mark Njela akimtaka kwenda nyumbani kwa wazazi wa Mdee Ubungo Kibangu kumkamata Halima Mdee kwa tuhuma za kutoa lugha ya matusi dhidi ya rais Magufuli.

Amedai baada ya kupewa oda hiyo, walikwenda kama walivyoagiza na walipofika walipokelewa na kaka wa Halima ambaye aliwaelekeza kwa mama yao.Ameendelea kudai kuwa, mama Halima aliwapokea vizuri, akaenda kuongea na Halima na akaomba wamsubiri ajiandae kwa kuwa alikuwa amepumzika kwa kidogo.

SPORTPESA YATOA TSH. MILIONI 50 KWA SIMBA SC

RAIS MUSEVENI AWASILI DAR ES SALAAM KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU MOJA NCHINI

0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere alipowasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku moja leo Agosti 9, 2018
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni (kati kati) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda baada ya kuwasili, kulia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt John Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda 

JAFO AZITAKA HALMASHAURI KUSIMAMIA VYEMA MATUMIZI.

0
0

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amewataka viongozi wa Halmashauri nchini kusimamia matumizi ya mapato yanayokusanywa katika Halmashauri zao.

Jafo ametoa kauli hiyo alipokuwa katika ukaguzi wa miradi ya maendeleo wilayani Geita na Chato katika mkoani wa Geita. Amesema Halmashauri mbalimbali zinatakiwa kusimamia vyema matumizi ya mapato hayo na kwa kiasi kikubwa yaelekezwe katika miradi ya maendeleo kwenye Halmashauri hizo kwa maslahi mapana ya wananchi.

Waziri Jafo amepongeza viongozi wa Halmashauri ya Mji wa Geita kwa usimamizi mzuri wa ukusanyaji wa mapato.Katika ziara hiyo, Waziri huyo amefanikiwa kukagua ujenzi wa soko la kisasa linalojengwa kwa fedha za ndani za Halmashauri ya mji wa Geita, barabara za lami za mji wa Geita zinazojengwa kwa mradi wa ULGSP, zahanati ya Buselesele, Kituo cha Afya Bwanga kilichopo wilayani Chato, pamoja na kutembelea shule ya sekondari Magufuli.

Akiwa Buselesele, Waziri Jafo amewahakikishia wananchi wa kata ya Buselesele kwamba serikali itajitahidi ili ijenge kituo cha afya cha kisasa katika kata hiyo ya Buselesele kutokana na idadi kubwa ya wananchi katika eneo hilo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akipata maelezo ya ujenzi wa soko kutoka kwa Mkurugenzi wa mji wa Geita
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Magufuli walipotembelewa leo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo
Mkuu wa Mkoa na Geita Mhandisi Robert Gabriel akimueleza jambo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo alipotembelea katika zahanati ya Buselesele.
Wananchi katika kituo cha afya Bwanga wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo.

Viewing all 109570 articles
Browse latest View live




Latest Images