Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA VIONGOZI WA JUMUIYA YA KIKRISTO TANZANIA (CCT) IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi Alinikisya Cheyo, aliyeongoza ujumbe wa viongozi wapya wa Jumuiya hiyo kumtembelea na kujitambulisha kwake Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 7, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Makamu wa Kwanza wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) Dkt. Frederick Shoo wakati ujumbe wa viongozi wakuu wa Jumuiya hiyo ulipomtembelea na kujitambulisha kwake Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 7, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Makamu wa Kwanza wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) Dkt. Frederick Shayowakati ujumbe wa viongozi wakuu wa Jumuiya hiyo ulipomtembelea na kujitambulisha kwake Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 7, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa watika mazungumzo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Moravian Tanzania, Alinikisya Cheyo, Makamu Mwenyekiti wa Kwanza wa Jumuiya hiyo Dkt. Frederick Shoo, Makamu wa Pili wa Mwenyekiti Dkt. Jacob Chimeledya na Katibu Mkuu wa CCT Canon Moses Matonya ujumbe huo viongozi wapya wa jumuiya hiyo ulipomtembelea na kujitambulisha kwake Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 7, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Moravian Tanzania, Alinikisya Cheyo, Makamu Mwenyekiti wa Kwanza wa Jumuiya hiyo Dkt. Frederick Shoo, Makamu wa Pili wa Mwenyekiti Dkt. Jacob Chimeledya  na Katibu Mkuu wa CCT Canon Moses Matonya baada ya ujumbe wa viongozi hao kumtembelea na kujitambulisha kwake Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 7, 2018.

13, wanaodaiwa kutuma SMS za 'ile hela tuma kwenye Namba hii' wapandishwa kizimbani.

$
0
0

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Vijana 13 wanaodaiwa kutuma sms kwa watu tofauti tofauti wamefikishwa katika mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matano likiwemo la utakatishaji wa fedha wa zaidi ya milioni 154.

Washtakiwa hao wameshtakiwa chini ya sheria ya uhujumu uchumi.

Wakisomewa mashtaka yao kwenye kesi hiyo namba 58 ya 2018 leo Agosti 7.2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Kelvin Mhina, Wakili wa Serikali Mkuu,Tumaini Kweka alidai washtakiwa hao wanakabiliwa na shtaka la kula njama, kuchapisha taarifa za uongo, mashtaka mawili ya kusambaza na shtaka moja la utakatishaji wa fedha.

Wakili, Kweka amewataja washtakiwa hao kuwa ni Boniface Maombe, David Luvanda, Moshi Sungura, Amos Bosco, Lule Kadenge, Jofrey Kapangamwaka, William Nturo, Regius Mauka, Collins Mwang'omolan Francis Kapalata, Kasonde Kapela, Enock Mwandaji na Pascal Kiatu.

Akisoma hati ya mashtaka wakili wa serikali Mwandamizi Nasoro Katuga amedai kati ya Machi 6 na Juni 2018, washtakiwa hao walikula njama kwa kutuma meseji zisizotakiwa katika maeneo ya Dar es Salaam, Rukwa na sehemu zingine ndani ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia, washtakiwa hao wanadaiwa kuchapisha taarifa za uongo zikiwa katika muundo wa jumbe fupi (SMS), kupitia mfumo wa kompyuta kwa nia ya kudanganya.Aidha washtakiwa hao wanadaiwa kusambaza Meseji za kielektroniki zisizotakiwa kupitia mfumo wa kompyuta.

Katuga ameendelea kudai kuwa, washtakiwa hao katika kipindi hicho cha Machi na Juni 2018 katika maeno hayo kwa njia ya kudanganya na kushawishi, walisambaza jumbe fupi za kielektroniki kwenda kwa watu tofauti tofauti wakionesha kuwa wanayo mamlaka ya kufanya hivyo wakati si kweli.washtakiwa hao pia wanadaiwa wakiwa katika katika maeneo hayo kwa nia ya kudanganya, walisambaza jumbe fupi kwa njia za kielektroniki zisizotakiwa.

Washtakiwa wote katika shtaka la tano wanadaiwa kati ya Machi na Juni 2018 mkoani Rukwa na katika maeneo ya Dar es Salaam na sehemu nyingine za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania washtakiwa hao moja kwa moja walijihusisha na muamala wa Sh 154,032, 830 huku wakijua fedha hizo ni zao la kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.Hata hivyo, washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo wala kutoa dhamana hadi Mahakama Kuu kwa kuwa shtaka la utakatishaji wa fedha ni miongoni kwa mashtaka yasiyo na dhamana.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo bado Haujakamilika na kesi imeahirishwa hadi Agosti 21,2018 washtakiwa wamerudishwa rumande.
 

WAZIRI MKUU, KASSIM MAJALIWA AZUNGUMZA NA WADAU KUHUSU MIKAKATI YA KUENDELEZA ZAO LA MCHIKICHI

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Kilimo Charles Tizeba, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni, Mrajis wa Vyama vya Ushirika Taifa Titto Haule, Mkuu wa JKT Meja Jenerali Martin Busungu, Mkuu wa Jeshi la Magereza Phaustin Kasike na Wadau wa zao la mchikichi, kuhusu maendeleo ya zao hilo, kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam Agosti 7, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_7460
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Kilimo Charles Tizeba, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni, Mrajis wa Vyama vya Ushirika Taifa Titto Haule, Mkuu wa JKT Meja Jenerali Martin Busungu, Mkuu wa Jeshi la Magereza Phaustin Kasike na Wadau wa zao la mchikichi, kuhusu maendeleo ya zao hilo, kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam Agosti 7, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_7465
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Kilimo Charles Tizeba, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni, Mrajis wa Vyama vya Ushirika Taifa Titto Haule, Mkuu wa JKT Meja Jenerali Martin Busungu, Mkuu wa Jeshi la Magereza Phaustin Kasike na Wadau wa zao la mchikichi, kuhusu maendeleo ya zao hilo, kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam Agosti 7, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RAIS MSTAAFU MKAPA MGENI RASMI KILELE CHA NANENANE KITAIFA 2018 SIMIYU

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu

RAIS mstaafu Mhe. Benjamini Mkapa kesho Agosti 08, atakuwa Mgen Rasmi katika Kilele cha Maonesho ya Sherehe ya wakulima Nanenane Kitaifa mwaka 2018, ambayo yanafanyika katika Uwanja wa Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

Akizungumza na vyombo vya habari , Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema Mkapa atakuwa mgeni rasmi katika madhimisho hayo akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. 

Amesema pia katika kilele cha Maadhimisho ya maonesho hayo viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali watashiriki wakiwemo Katibu Mkuu wa CCM , Dkt. Bashiru Ally Sambamba na Mawaziri, Manaibu Waziri na Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Mkuu wa wizara mbalimbali.

“Watakuwepo viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali pamoja na viongozi wa Taasisi mbalimbali za Fedha wakiwemo Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania(BOT) Prof. Florens Luoga na Mkurugenzi wa Benki ya NBC, Theobald Sabi”
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu , Mhe. Anthony Mtaka akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa mara baada ya kuwasili wilayani Busega Mkoani Simiyu, kwa ajili ya kuhitimisha Maonesho ya nanenane Kitaifa mwaka 2018, yanayofanyika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Mjini Bariadi Simiyu.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu , Bw. Jumanne Sagini(kulia) akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa mara baada ya kuwasili wilayani Busega Mkoani Simiyu, kwa ajili ya kuhitimisha Maonesho ya nanenane Kitaifa mwaka 2018, yanayofanyika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Mjini Bariadi Simiyu.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kulia) akitoa maelezo ya awali kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa(katikati) mara baada ya kuwasili wilayani Busega Mkoani Simiyu, kwa ajili ya kuhitimisha Maonesho ya nanenane Kitaifa mwaka 2018 mkoani humo, yanayofanyika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Mjini Bariadi Simiyu.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongela (kulia) wakiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa(katikati) mara baada ya kuwasili wilayani Busega Mkoani Simiyu, kwa ajili ya kuhitimisha Maonesho ya nanenane Kitaifa mwaka 2018 mkoani humo, yanayofanyika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Mjini Bariadi Simiyu.

WATEJA DSTV KUSHUHUDIA LIGI KUBWA ULIMWENGUNI KWA GHARAMA NAFUU,ZIPO ZA UINGEREZA,ISPANIA

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WATEJA wa DStv wanatarajia kuanza tena kushuhudia moja ya ligi maarufu kabisa duniani ikiwemo Ligi ya Italia– Serie A.

Hatua hiyo inakuja baada ya MultiChoice kutangaza leo jijini Dar es Salaam kuwa kuanzia msimu huu, ligi hiyo itaonyeshwa mubashara kupitia DStv.Mbali na Serie A ambapo atakuwepo nguli wa soka Cristiano Ronaldo, wateja wa DStv wataendelea kufurahia ligi na michuano mikubwa mingi duniani ikiwemo Ligi ya Uingereza (Premier League) na La Liga.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania Ronald Shelukindo amesema mbali na habari za kurudi kwa Serie A, DStv pia itaongeza maudhui zaidi katika soka msimu huu.Amesema watumiaji wa DStv Bomba, wataweza kuona zaidi ya mechi 100 katika michuano ya Serie A na Ligi Kuu ya Uingereza, huku wateja wa DStv Family wao watakuwa wakipata mechi zote 380 za michuano ya Serie A na mechi zaidi ya 120 kutoka Ligi Kuu ya Uingereza.

Ameongeza kuwa watumiaji wa kifurushi cha DStv Compact, Compact Plus na wateja wa Premium watakuwa na upatikanaji wa mechi zote za Premium League, Serie A na mechi zote 380 za La Liga.Amefafanua kuwa wanatambua msimu wa ligi kwa mwaka 2018/2019 unatarajia kuanzia na kwa Ligi Kuu ya Uingereza inaanza Ijumaa hivyo rai yao kwa wateja wao kuhakikisha wanalipia ving'amuzi vyao na wale ambao hawana basi wanunue kwa gharama ya Sh.79,000 ikiwa na ofa ya miezi miwili.

Amesema kuwa lengo lao ni kuona wateja wao wote wanapata nafasi ya kuangalia ligi mbalimbali duniani pamoja na michuano mingine ya kimataifa.Ameweka wazi kuwa baada ya michuano ya Kombe la Dunia kumalizika sawa kwa nguvu ile ile wanahamishia kwenye ligi hizo ambapo mechi zitatangazwa kwa lugha ya kiswahili kupitia watangazaji na wachambuzi maarufu nchini.Shelukindo amesema katika vifurushi vyote vya Dstv wateja wataona mechi na kufafanua kwa vifurushi cha Sh.19,000 mteja wao atashuhudia mechi 108.Amesema kauli mbiu yao katika msimu huu wa ligi Kuu mbalimbali ni kwamba "Moto hauzimwi na kama sio DStv potezea".

Wakati wanatangaza kuanza kwa ligi na namna ambavyo DStv wamejipanga vema kwa ajili ya wateja mbali ya kuwepo kwa waandishi wa habari pia walikuwepo wachezaji mpira wa miguu maarufu nchini ambapo wamepata nafasi ya kutamba kwenye timu ya taifa na kwenye vilabu vyao.
Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania Ronald Shelukindo akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika leo

Ephraem Kibonde mtangazaji maarufu wa Soka hapa nchini akizungumza (kutoka kushoto) Maulid Kitenge, Aboubakar Liongo, Edo Kumwembe wakiwa katika uzinduzi wa msimu mpya wa sokawatangazaji hao watakuwa wakiwaletea matangazo ya ligi kuu ya uingereza msimu huu kwa kiswahili.

MAKAMU WA RAIS, MAMA SAMIA AMJULIA HALI WAZIRI KIGWANGALLA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 7, Agosti 2018 amemtembelea Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kingwangalla aliyelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam ambapo alimjulia hali na kumpa pole kufuatia ajali ya gari aliyoipata Agosti 4,2018 huko Manyara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 7, Agosti 2018 amemtembelea Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kingwangalla aliyelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam ambapo alimjulia hali na kumpa pole kufuatia ajali ya gari aliyoipata Agosti 4,2018 huko Manyara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimjulia hali na kumpa pole Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam, baada ya kupata ajali ya gari Agosti 4, 2018. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

RAIS MAGUFULI AZAWADIWA KITABU CHA MWONGOZO WA SALA NA RAIS WA BARAZA LA MAASKOFU WA KANISA KATOLIKI (TEC) ASKOFU GERVAS JOHN NYAISONGA

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akifanya sala na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC) Askofu Gervas John Nyaisonga, Makamu wa Rais wa Baraza lhilo Dkt. Flavian Kasalla na Katibu Mkuu wa TEC Dkt. Charles Kitima viongozi hao wapya wa kanisa walipomtembelea na kujitambulisha kwake Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 7, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC) Askofu Gervas John Nyaisonga, Makamu wa Rais wa Baraza lhilo Dkt. Flavian Kasalla wakiwa na Katibu Mkuu wa TEC Dkt. Charles Kitima viongozi hao wapya wa kanisa walipomtembelea na kujitambulisha kwake Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 7, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC) Askofu Gervas John Nyaisonga na Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC) Dkt. Flavian Kasalla wakiwa na Katibu Mkuu wa Baraza hilo Dkt. Charles Kitima baada ya viongozi hao wapya wa kanisa kumtembelea na kujitambulisha kwake Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 7, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC) Dkt. Charles Kitima akiwa na Rais wa Baraza hilo Askofu Gervas John Nyaisonga na Makamu wa Rais wa Baraza hilo Dkt. Flavian Kasalla viongozi hao wapya wa kanisa walipomtembelea na kujitambulisha kwake Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 7, 2018.
Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC) huku Makamu wa Rais wa Baraza hilo Dkt. Flavian Kasalla wakiwa na Katibu Mkuu wa Baraza hilo Dkt. Charles Kitima ambaye anaongea na wanahabari mara baada ya viongozi hao wapya wa kanisa kumtembelea na kujitambulisha kwake Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 7, 2018

WAZIRI WA FEDHA DKT MPANGO AIPONGEZA BENKI YA AMANA KWA KUTOA HUDUMA BORA KWA JAMII

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Tanga

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amewataka wakazi wa mkoa wa Tanga kutumia fursa ya uwepo wa Amana Benki katika mkoa huo kama fursa ya kujipatia Maendeleo kutokana na benki hiyo kuwa na huduma ya mikopo isiyokuwa na riba.

Waziri Mpango amesema hayo mkoani Tanga wakati alipokuwa akimwakilisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika uzinduzi wa tawi jipya la benki hiyo katika mkoa huo."nimefurahishwa na jitihada za Amana Bank katika kutanua huduma zake kwa wananchi wa mikoani. Vilevile, nimewasisitiza wana Tanga kutumia fursa waliyopata kutoka Amana Bank kwa kuwafikishia huduma za bank hiyo kwao,ikiwemo mikopo bila riba jambo ambalo litawasaidia sana kujiinua kichumi kwa kukopa na kurejesha kwa wakati"amesema Waziri Mpango.

Akizungumza kwa niaba ya benki hiyo Mkurugenzi wa Amana Benki Dk Muhsin Masoud, amesema Benki ya Kiislamu ya Amana hapa nchini imefungua tawi lake jipya jijini Tanga ikiwa ni sehemu ya mikakati ya Benki hiyo kufikisha huduma zake kwa watu wa mikoani.mesema kuwa Benki hiyo inatarajia kufungua matawi yake mengine Zanzibar na Dodoma hivi karibuni hili kuzidi kuwasogelea wananchi nakutaja kuwa akaunti zinazopatikana katika Benki hiyo, ni akaunti ya akiba ya wanafunzi, akaunti ya akiba ya Hijja, akaunti ya akiba ya mtoto(nuru), akaunti ya akiba ya mwanamke(anisaa) na akaunti binafsi.

ametaja kuwa kwa sasa Benki hiyo ya Amana inafikisha jumla ya matawi 8, matano yakiwa Dar es Salaam, Moja Mwanza,Arusha na hilo la jijini Tanga. Amana Benki ilianzishwa mnamo Novemba 24, 2011 kwa lengo la kukidhi haja ya wateja wa kibenki nchini ya kupata huduma zinazozingatia misingi ya sharia za Kiislamu.
Waziri wa Fedha na Mipango Philip Mpango akiwa na Mkuu wa Mkoa Wa Tanga , Martin Shigela wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa Tawi Jipya la Amana Benki Mkoani Tanga.
Waziri wa Fedha na Mipango Philip Mpango akifunua kitambaa cha jiwe la Msingi wakati wa uzinduzi wa tawi jipya la Amana Benki Mkoani Tanga
Mkuu wa Mkoa wa Tanga , Martin Shigela akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tawi jipya la Amana Benki katika mkoa wake
Dk Muhsin Masoud,Mkurugenzi wa Amana Bank akielezea huduma zitakazotolewa katika tawi hilo la Mkoa wa Tanga.
Waziri wa Fedha Philip Mpango akiwa katika picha ya Pamoja na baadhi ya wateja mashuhuri wa benki hiyo wa mkoa wa Tanga.
Waziri wa Fedha akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa mkoa wa Tanga.

RAIS WA UGANDA, YOWERI MUSEVENI KUFANYA ZIARA NCHINI AGOSTI 9, 2018

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. John Magufuli (kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Uganda, Mh. Yoweri Museveni.

Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni atafanya ziara ya kikazi ya siku moja hapa nchini tarehe 09 Agosti 2018.

Taarifa hiyo imetolewa leo 07 Agosti 2018 na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa, lengo la ziara hiyo ni kuimarisha ushirikiano na ujirani mwema uliopo kati ya Tanzania na Uganda.

“Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Mheshimiwa Rais Museveni atapokelewa na mwenyeji wake Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Akiwa nchini, Mheshimiwa Rais Museveni atakutana kwa mazungumzo ya faragha na Mheshimiwa Rais Magufuli yatakayofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo yatafuatiwa na Chakula cha Mchana kilichoandaliwa na Mheshimiwa Rais Magufuli kwa heshima ya Mheshimiwa Rais Museveni.

Mheshimiwa Rais Museveni na Ujumbe wake wataondoka nchini siku hiyo hiyo kurejea Uganda.

NEC YATANGAZA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI KATIKA KATA 21

$
0
0

Hussein Makame, NEC 

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza Uchaguzi Mdogo wa Udiwani katika kata 21 za mikoa 10 ya Tanzania Bara utakaofanyika tarehe 16 Septemba mwaka huu. 

Akitoa taarifa ya uchaguzi huo jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Dkt. Athumani Kihamia, alisema fomu za uteuzi wa wagombea wa uchaguzi huo zitatolewa kati ya tarehe 17 hadi 23 Agosti mwaka huu. Aliongeza kuwa uteuzi wa wagombea utafanyika tarehe 23 Agosti wakati kampeni za Uchaguzi zitafanyika kati ya tarehe 24 Agosti hadi tarehe 15 Septemba mwaka huu. 

Dkt. Kihamia alisema kuwa Tume imetangaza uchaguzi huo baada ya kupokea taarifa ya uwepo nafasi wazi za udiwani katika kata hizo 21 zilizopo katika Halmashauri 15 kutoka kwa Waziri mwenye dhamana na Serikali za Mitaa. “Nafasi wazi za udiwani katika Kata hizo zimetokana na sababu mbalimbali zikiwepo kifo, kujiuzulu, kutohudhuria vikao na kufutwa uanachama” alisema Dkt. Kihamia na kuongeza kuwa; 

“Baada ya kupokea taarifa hiyo na kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(3) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa; Tume ina utaarifu Umma kuhusu kuwepo kwa Uchaguzi mdogo katika Kata hizo 21.” Kufuatia taarifa hiyo, Dkt. Kihamia alitoa mwaliko wa Tume kwa vyama vya siasa, wadau wote wa Uchaguzi na wananchi kwa ujumla kushiriki katika Uchaguzi huo. 

“Tume inachukua fursa hii kuviasa vyama vya siasa na wadau wote wa Uchaguzi kuzingatia matakwa ya Katiba, Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Madiwani) za mwaka 2015” alisema Dkt. Kihamia. Aidha alivitaka vyama vya siasa na wadau wa uchaguzi kuzingatia Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015 pamoja na maelekezo yote yaliyotolewa au yatakayotolewa na Tume wakati wote wa Uchaguzi mdogo. 

Uchaguzi huu mdogo wa udiwani katika kata 21 unatarajiwa kufanyika sanjari na uchaguzi mdogo wa ubunge katika majimbo ya Korogwe Vijijini, Ukonga na Monduli na kata za Tindabuligi na Kisesa katika Halmashauri ya Wilayani Meatu, uliotangazwa juzi ambao utakaofanyika siku ya Jumapili tarehe 16 Septemba mwaka huu.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt. Athumani Kihamia. 

AWESO AMLILIA RAIS MAGUFULI BARABARA YA TANGA,PANGANI SAADANI

$
0
0
SERIKALI ya awamu ya tano imeombwa kuangalia namna ya kuanza ujenzi wa barabara ya Tanga-Pangani, Saadan hadi Bagamoyo ili kuweza kumaliza kilio cha wananchi wa wilaya ya Pangani cha muda mrefu ikiwemo kufungua fursa za kiuchumi na maendeleo kwa mkoa . 

Ombi hilo lilitolewa na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso wakati akizungumza kwenye mkutano wake wa hadhara wilayani humo ambapo alisema pamoja na kuwepo kwa miradi mingi inayotekelezwa huko lakini kilio kikubwa cha wananchi wake ni ukosefu wa barabara nzuri. 

Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) alisema wakati Rais Magufuli akiomba kura kwa wananchi hao mwaka 2015 aliwaahidi wananchi ujenzi wa barabara hiyo na walikubali kumpa kura nyingi na imani kubwa kwake kwa mategemeo ya kumpata mkombozi atakae weza kumaliza kero hiyo ambayo imedumu katika awamu zote nne zilizopita bila ya mafanikio. 

“Kwenye mkutano wangu wa leo hii nipo hapa nyumbani kama Mbunge wenu kawaida na sikuja kama Naibu Waziri na jukumu la Mbunge ni kuwasemea wananchi wake Mh Rais wananchi wangu kiukweli wanalia na suala la barabara hii na hawajui hatma yake lini mradi huu utaanza”Alisema Aweso. 

Hata hivyo alisema kuzorota kwa uchumi na maisha magumu kwa wananchi wa wilaya hiyo unachangiwa kwa kiasi kikubwa na tatizo la kutokujengwa barabara ambayo ingesaidia kufungua wilaya hiyo ambayo inaonekana kama imesahaulika katika nyanja zote. 
 NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) akizungumza na wananchi wa Jimbo hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika sokoni mjini Pangani ambako pamoja na mambo mengine aliweza kusikiliza kero zao zinazowakabili
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) akiwa amebebwa juu na wananchi mara baada ya kumaliza kuwahutubia
 NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM)kulia akiwa na Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa Abdallah wakifuatilia hoja za wananchi kwenye mkutano huo
sehemu ya wananchi wa mji wa Pangani wakimfuatilia NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM)
Wananchi wakimfuatilia NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM).

RC MAKONDA ATEMBELEWA NA RAIS WA TFF, WAWEKA MIKAKATI THABITI YA KUIMARISHA MICHEZO.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo ametembelewa ofisini kwake na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF Wallace Karia na Mwenyekiti wa Michezo Mkoa wa Dar es Salaam ambapo wamefanya mazungumzo ya kuimarisha sekta ya Michezo.

Miongoni mwa mambo waliyozungumzia ni Suala la heshima iliyopata Tanzania kuwa mwenyeji wa Michuano ya Mashindano makubwa ya michezo kwa Jeshi la Polisi katika nchi za mashariki na Kati zikihusisha Nchi Saba ambapo tayari michuano hiyo imefunguliwa rasmi siku ya Jana na Waziri mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.

Aidha wamezungumzia maandalizi ya mashindano makubwa ya SECAFA Cuf kwaajili ya michuano ya AFCON yakihusisha vijana wenye umri chini ya miaka 17 yanayotaraji kufanyika August 11 Mwaka huu kwenye uwanja wa Taifa yakijumuisha mataifa 10 Afrika.

RC Makonda amesema michuano yote hiyo itafanyika Jijini Dar es salaam na kwakuwa inahusisha ugeni kutoka mataifa mbalimbali itatoa fursa kwa wananchi wa Dar es salaam hususani wenye hotel, vyakula, usafiri na wafanyabiashara kupata kipato kupitia mashinano hayo.

Kwa upande wake Rais wa TFF Wallance Karia amempongeza RC Makonda kwa jitiada za kuinua sekta ya michezo kupitia ujenzi wa uwanja wa Bandari ambapo amesema wameamua kumuomba ushirikiano kwakuwa wanaamini uwezo ukubwa alionao kwenye kusimamia jambo na kufanikisha.
 Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) Wallace Karia akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumtembelea Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuhusiana na michuano ya Vijana ya AFCON itakayofanyika mwakani hapa nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akizungumza na waandishi wa habari baada ya ujio wa Rais wa TFF Wallace Karia ofisini kwake

MKUU MPYA WA MKOA WA SONGWE BRIGEDIA JENERALI MWANGELA AWASILI KITUONI , AAHIDI KUENDELEZA MAZURI YA GALLAWA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemas Elias Mwangela amewasili katika ofisi yake mapema leo asubuhi kufuatia kuteuliwa kwake kuuongoza Mkoa wa Songwe na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe John Pombe Magufuli Julai 28, 2018.

Brigedia Jenerali Mwangela amepokelewa na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa, Wakuu wa Wilaya nne za Mkoa wa Songwe, wakurugenzi wa halmashauri tano za Mkoa huu, wakuu wa idara pamoja na watumishi wote wa ofisi yake.

Mara baada ya mapokezi hayo Brigedia Jenerali Mwangela amepokea taarifa ya makabidhiano kutoka kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe Luteni Mstaafu Chiku Gallawa katika kikao cha pamoja na wakuu wa wilaya, wakurugenzi, wakuu wa idara na wajumbe wa kamati ya ulinzi na Usalama.

Gallawa amesema kuwa anayo furaha kumkaribisha Brigedia Jenerali Mwangela na anamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe John Pombe Magufuli kwa kumteua Brigedia Jenerali Mwangela, na kuwa wale waliokuwa wakifurahia kuondoka kwake wakijua sasa wataanza kufanya kazi ndivyo sivyo wajue wamepata kiongozi ambaye ni makini zaidi”.

Ameongeza kwa kuwataka watendaji na wanasiasa waendelee kuchapa kazi kwa bidii wakiwa na lengo la kumkomboa mwananchi wa Songwe kutoka katika umasikini na kuongeza pato la mkoa na taifa.Naye Brigedia Jenerali Mwangela amemshukuru Gallawa kwa kuweka misingi mizuri ambayo imelenga kuuinua Mkoa wa Songwe kiuchumi na kuahidi kuwa atahakikisha mazuri yote atayaendeleza hasa pale alipoishia.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemas Elias Mwangela akipokelewa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe Luteni Mstaafu Chiku Gallawa mapema leo asubuhi alipowasili ofisini kwake.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemas Elias Mwangela akisalimiana na Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila mapema leo asubuhi alipowasili ofisini kwake.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemas Elias Mwangela akisaini kitabu ofisini kwake mapema leo mara baada ya kuwasili na kupokelewa na watumishi na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Songwe.KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

MBUNGE GULAMALI AELEZWA NAMNA CHUO CHA NIT KILIVYOJIPANGA KUWAPOKEA WATALAAM WA BOEING ILI KUWANOA ATCL

$
0
0
Na Francis Daudi, Glogu ya jamii

MBUNGE wa Jimbo la Manonga, Seif Khamis Gulamali amtembelea Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) ambacho kimejidhatiti kufanya mapinduzi makubwa katika sekta ya Usafirishaji nchini Tanzania kwa kuzalisha wataalamu wengi zaidi ikiwa ni sehemu ya mkakati wao wa kutekeleza azma ya Serikali ya Awamu ya tano katika kujenga Tanzania ya Viwanda. 

Akizungumza leo chuoni hapo baada ya kupokelewa na Mkuu wa chuo hicho Profesa Zacharia Mginilwa, Gulamali amesema amefurahishwa na utendaji kazi sambamba na mikakati iliyopangwa katika kuhakikisha sekta ya usafirishaji inakua zaidi.Amesema kuwa amefurahi kuona chuo alichosoma kinaendelea kuzalisha wataalamu zaidi katika sekta ya usafirishaji ambayo inachangia uchumi wa Taifa kwa asilimia kubwa.

Pia chuo hichokinaonesha jitihada za kuunga mkono juhudi za Rais Dkt John Magufuli na amehaidi kutoa ushirikiano wa hali na mali pindi itakapohitajika.

Akiwa Chuoni hapo Gulamali alipata fursa ya kutembelea Shule ya usafiri wa anga (School of Aviation) yenye madarasa ya waendesha ndege, karakana maalumu za kutengeneza injini za ndege na baadaye alitembelea idara ya ukaguzi wa magari na kueleza kufurahishwa na utendaji kazi unaofanywa kwa kutumia teknolojia ya juu.
 Mbunge wa Manonga Seif Gulamali ( kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa chuo cha usafirishaji nchini (NIT) mara baada ya kumaliza ziara yake chuoni hapo.
 Mbunge wa Manonga Seif Gulamali akikagua baadhi ya vifaa katika karakana chuoni hapo kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho Profesa Zacharia Mginilwa.
Mbunge wa Manonga Seif Gulamali akiwa katika chumba cha uongozaji wa ndege katika chuo cha usafirishaji (NIT) mara baada ya kufanya ziara  Chuoni hapo.

BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 07.08.2018


Nafasi has treats for FILM LOVERS this month

$
0
0


Tanzania's film industry has rapidly grown over the last few years to become the second largest in Africa, Nigeria being the first with its craze for Nollywood films. A craze similar to that of 'Bongo movies' in Tanzania which sees hundreds of movies being made by over 50 independent producers in Dar es Salaam.

According to research done by Media For Development International (Tanzania), distributors sell DVDs of these movies to over 25,000 video libraries around every corner of the country. Locals are able to either buy or rent these movies from video libraries or could watch them in 'video shows', make shift cinemas of which there are over 10,000, screening films country wide.
This month, Nafasi and Tanzania film lab will be treating fans of Tanzanian cinema with FATUMA, a film about the challenges of a female farmer in rural Tanzania. Fatuma has won several awards on the the international film circuit. Join on 14th of August at 7.30 pm for a chance to see the film and to talk to some of the filmmakers and actors. 


A traditional rural woman has always risked her body and soul, without reward or thanks, to farm her husband’s land and keep the family fed and cared for. She fights unfavorable weather, pests and poverty. But when Manyusi squanders her prized harvest, and schemes to marry off their daughter, Fatuma has to fight her husband.
For fans of more experimental,and artistic films Nafasi invites to join us for an exclusive exhibition on Saturday 25th of August featuring the work of Spainish video artist Lois Patino. Patino is a video and installation artist from Spain. His videos and video installations have shown in art centers including Centro Cultura San Martín (Buenos Aires, Argentina), Casa Encendida (Madrid, Spain),. His films have screened at international festivals around the world. 

ENTRY TO BOTH EVENTS IS FREE

You are all welcomed to the Tanzania Film Lab Screening of Fatuma. Get to meet some of the crew and cast of the film alongside several other filmmakers and actors on the 14th August from 7:30 pm

Mawaziri washuhudia Utekelezaji Mradi wa Umeme wa Uhakika wa Steigler's Gorge Waiva

SIMBA WATOA MSAADA KWA KITUO CHA WATOTO YATIMA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Taasisi ya Mo Dewji kwa kushirikiana na klabu ya Simba wametoa msaada wa viti vya walemavu, vyakula, vinywaji na sabuni kwa kituo cha kutunza watoto yatima wenye ulemavu cha Watoto Kwanza kilichopo Kawe jijini Dar es Salaam.
 Wachezaji wa  Simba wakitoa msaada wa viti vya walemavu, vyakula, vinywaji na sabuni kwa kituo cha kutunza watoto yatima wenye ulemavu cha Watoto Kwanza kilichopo Kawe jijini Dar es Salaam.
 Wachezaji wa  Simba wakitoa msaada wa viti vya walemavu, vyakula, vinywaji na sabuni kwa kituo cha kutunza watoto yatima wenye ulemavu cha Watoto Kwanza kilichopo Kawe jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Rabi Hume

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi atembelea Maonyesho ya Nane Nane Morogoro

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema umefika sasa kwa kwa Wizara na Taasisi zinazohusika na Sekta ya Elimu Nchini kumuandaa Mwanafunzi katika masomo ya Kilimo kuanzia ngazi ya Msingi hadi Sekondari ili atakapofikia uwezo wa kuingia chuo Kikuu awe tayari ameshaelewa nini Kilimo.
Alisema uingizwaji wa  Mitaala ya Kilimo ndani ya masomo ya kawaida maskulini itamuwezesha Wanafunzi kujitayarisha mapema katika muelekeo wa kujijengea uwezo wa ajira ya uhakika ndani ya Sekta ya Kilimo wakati amalizapo masomo yake ili aweze kujitegemea kupitia Sekta hiyo muhimu kwa uchumi wa Taifa.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa ushauri wakati akizungumza na vyombo mbali mbali vya Habari mara  baada ya kumaliza ziara yake ya kuangalia Maonyesho  mbali mbali ya Siku ya Nane Nane yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mkoani Morogoro.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akivishwa Skafu na Vijana Chipukizi wa Morogoro mara alipoingia kwenye Unjwa wa Maonyesho wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mkoani Morogoro.
 Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi akifurahia vifaa  zinazotengenezwa na mjasiriamali wa Mkoa wa Tanga
 Balozi Seif akinunua moja ya bidhaa zilizotengenezwa na Kikundi cha Wajasiri Amali kutoka Mkoani Tanga kwenye Maonyesho ya Nane Nane Morogoro.
 Moja ya Bwawa la kufugia Samaki la Chuo Kikuu cha sokoni Mkoani Morogoro ambalo Balozi Seif na Ujumbe wake walipata muda wa kulitembelea.
 Balozi Seif akiangalia ukulima wa mpunga uliooteshwa katika mfumo wa Taaluma ya kisasa kwenye Kitalu cha Kanisa la Anglican Dayosisi ya Morogoro kiliomo ndani ya Maonyesho ya Nane Nane.
Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

KONGAMANO LA AJENDA YA MSICHANA KUFANYIKA DAR ES SALAAM AGOSTI 11, 2018

Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images