Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live

BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU 06.08.2018


Michuzi TV: MITIBIASHARA KUWAPA FURSA WAWEKEZAJI WA MISITU

ufunguzi rasmi wa Mashindano ya Majeshi ya Polisi ya Afrika Mashariki uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam

0
0
 Wanamichezo kutoka Jeshi la Polisi la Tanzania,  wakipita mbele ya mgeni rasmi, ambaye ni Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa, kwenye ufunguzi wa Mashindano ya Majeshi ya Polisi ya Afrika Mashariki yaliyofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam Agosti 6, 2018
 Wanamichezo kutoka Jeshi la Polisi la Rwanda  wakipita mbele ya mgeni rasmi, ambaye ni Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa, kwenye ufunguzi wa Mashindano ya Majeshi ya Polisi ya Afrika Mashariki yaliyofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam Agosti 6, 2018
 Kikundi cha Ngoma cha Maringo kikitoa burudani, kwenye ufunguzi wa Mashindano ya Majeshi ya Polisi ya Afrika Mashariki yaliyofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam Agosti 6, 2018
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia wananchi, katika ufunguzi wa Mashindano ya Majeshi ya Polisi ya Afrika Mashariki yaliyofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam Agosti 6, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipuliza filimbi kuashiria ufunguzi rasmi wa Mashindano ya Majeshi ya Polisi ya Afrika Mashariki yaliyofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam Agosti 6, 2018
Mashabiki wa timu ya Jeshi la Polisi la Tanzania, wakishangilia goli  la kwanza la Tanzania dhidi ya timu ya Jeshi la Polisi la Uganda, mara baada ya ufunguzi wa Mashindano ya Majeshi ya Polisi ya Afrika Mashariki yaliyofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam Agosti 6, 2018,(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Dkt. Kalemani aiagiza TANESCO kuanza kununua Viunganishi (Accessories) hapa nchini ifikapo Novemba, 2018

0
0
Na Rhoda James- Dar es Salaam.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ameagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ifikapo Novemba, 2018 wawe tayari wamesitisha uagizaji wa viunganishi vya miundombinu ya umeme (Accessories) kutoka nje ya nchi badala yake wanunue hapa hapa nchini.
Waziri Daktari Kalemani, ametoa agizo hilo leo tarehe 6 Agosti, 2018 wakati alipotembelea Kiwanda cha uzalishaji viunganishi cha Auto Mech Ltd kilichopo Tabata jijini Dar es Salaam ili kujionea uwezo wa Kiwanda hicho katika uzalishaji viunganishi hivyo.
“Nimekuja hapa ili kujiridhisha kama Kiwanda hiki kina uwezo wa kuzalisha viunganishi vya kutosha, nimejiridhisha kuwa, kiwanda hiki kina uwezo wa kuzalisha viunganishi hivyo, kwa hiyo nimetoa miezi mitatu ili TANESCO, REA na Wakandarasi wote kwa pamoja wajiandae sasa kunua vifaa hivi nchini.” Alisema Waziri Kalemani.
Akizungumza katika ziara hiyo alieleza kuwa, miezi mitatu iliyopita alisitisha uagizaji wa Mita za luku na Nguzo kutoka nje lakini baado kuna changamoto ya wananchi kuchelewa kuunganishiwa umeme na tatizo kubwa ni ukosefu wa viunganishi hivyo.
Pia Waziri Kalemani amesema kuwa, “nimeelezwa kuwa, kiwanda hiki kinauwezo wakuzalisha tani tano kwa siku ambapo ni kwa shifti moja lakini wana uwezo wa kuzalisha tani 15 kwa siku kwa shifti tatu”.
Aidha, Waziri Kalemani ameogeza kuwa manufaa ya kutembelea kiwanda hiki ni kujiridhisha kuwa kina uwezo mkubwa wa kuzalisha viunganishi hivyo na hatimae kuokoa gharama kubwa ya uagizaji viunganishi hivyo kutoka nje ya nchi.
“TANESCO, REA na Wakandarasi wamekuwa wakichukua miezi 6 kuagiza, miezi 3 kukamilisha taratibu za bandarini lakini sasa tukivinunua hapa nchini tutaokoa gharama kubwa na wananchi watapata ajira pamoja na kuunganishiwa umeme kwa wakati.” Alisema Waziri Kalemani.
Kwa nyakati tofauti Waziri Kalemani ametoa wito kwa Watanzania wenye uwezo wa fedha na wenye nia kuazisha viwanda vya namna hii ili kuonesha uwezo wa ndani.
Hali kadhalika, Kiwanda hiki kimeanzisha utengenezaji wa majiko ambayo yanatumia mabaki ya mbao badala ya kutumia mkaa ambao sio rafiki na mazingira, lakini sasa tunaokoa mazingira kwa kutumia nishati hii mbadala.
Kwa upande wake, Meneja wa Kiwanda hicho Mhandisi Frimos Mselle amesema kuwa, Kiwanda hiki kina uwezo mkubwa wa kuzalisha viunganishi hivi na wanaahidi na kuhakikisha Serikali kuwa, viunganishi hivyo vinapatikana kwa urahisi na vya kutosha.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kushoto mstari wa mbele) akieleza jambo wakati akikagua Viunganishi vya miundombinu ya Umeme vinavyotengenezwa katika Kiwanda cha Auto Mech Limited kilicho Tabata jijini Dar es Salaam.  Wengine katika picha ni Viongozi Waandamizi kutoka Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wakala wa Nishati Vijijini, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Viongozi kutoka kiwanda cha Auto Mech limited.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) akikagua vyuma ambavyo vinatengenezwa kwenye kiwanda cha Auto Mech Limited kilichopo Tabata jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Mashine na Vifaa ambavyo vinatengenezwa kwenye kiwanda cha Auto Mech Limited kilichopo Tabata jijini Dar es Salaam.
Meneja wa kiwanda cha Auto Mech Limited, Mhandisi Frimos Mselle (mwenye koti la jano) akitoa maelezo kwa Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (wa pili kulia) wakati alipotembelea kiwanda hicho.

JASINTA MBONEKO AKIAPISHWA KUWA MKUU WA WILAYA YA SHINYANGA

0
0
 Jasinta Venant Mboneko akila kiapo kuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga leo Jumatatu Agosti 6,2018 
Picha ya pamoja mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack,Katibu tawala mkoa,wakuu wa wilaya za Kahama,Shinyanga na Kishapu. 
Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

WATENDAJI SIMAMIENI SHERIA ILI KUTATUA UTOROSHAJI WA RASILIMALI ZA MIFUNGO - ULEGA

0
0
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdallah Ulega,amefungua rasmi maonesho ya Nane Nane kanda ya kati ambayo yanaenda sawa na Mashindano ya Nane ya Mifugo kitaifa yanayofanyika Jijini Dodoma.

Mhe.Ulega Amefungua Mashindano ya Mifugo ambayo yalianza mwaka 2011 na huwa yanafanyika Agosti 5 kila mwaka na hufanyika  Dodoma na hujumuisha Ng'ombe wa maziwa na nyama walioboreshwa pamoja na Mbuzi wa Asili.

Mhe.Ulega amesema kuwa lengo kuu la Mashindano hayo ni kutambua umuhimu na mchango wa rasmilimali za mifugo ya asili katika kuendeleza sekta ya mifugo nchini.

Aidha amesema kuwa zoezi hili linalenga kutambua juhudi na maarifa wanayotumia wafugaji wa mifugo ili kufuga kwa tija na hatimaye kuvutia wafugaji wengi na kuiga na kuingia kwenye ufugaji wenye tija kwa taifa.

Mhe.Ulega amesesisitaza kuwa Sekta ya Mifugo ni moja ya Sekta muhimu zinazochangia kupunguza umaskini wa wananchi na kukuza uchumi wa nchi kwani ni mhimili katika kuendeleza viwanda kama ilivyoainishwa katika mpango kabambe wa Mifugo Tanzania.

Hata hivyo Mhe.Ulega ametoa maagizo kwa wafugaji na wadau mbalimbali kuunda na kuimarisha vikundi na vyama vya ushiriki ili kuongeza kasi ya uwekezaji katika viwanda vya kusindika mazao ya mifugo na hatimaye kufikia malengo na kauli mbiu ya Nane Nane 2018 isomekayo ''WEKEZA''.

Aidha Mhe.Ulega ameagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha utekelezaji wa mfumo wa utoaji kinga mbalimbali za magonjwa ya mifugo uwe ni lazima kwa wafugaji wote nchi.

Kwa upande mwingine Mhe.Ulega amesema wafugaji pamoja na wafanya biasha  hawaruhusiwi kuhamisha au kusafirisha mifugo pamoja  mazao kutoka sehemu moja hadi nyingine bila kibali.

Hivyo imesababisha maeneo ya mipakani mwa nchi yetu imeshamiri biashara haramu za mifugo na mazao yake zisizo rasmi amewataka watendaji kusimamia sheria kwa kushirikiana na wadau ili kutatua changamoto ya utoroshaji wa rasilimali za mifugo yetu na mazao yake.Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi,Abdallah Ulega   akizungumza na wananchi wa mkoa wa mkoa Dodoma wakati wa kufungua rasmi maonesho Nane Nane kanda ya kati na  mashindano ya nane ya Mifungo  kitaifa yanayo fanyika katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiangalia viatu katika banda la  Magereza vinavyotegene  na ngozi katika maonesho ya Nane Nane Nane katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.
 Naibu waziri wa Mifungo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiwa ameambatana na Mkuu wa mkoa  wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge wakitembelea banda la wajasiria mali katika maonesho ya Nane Nane yanayo fanyika  katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.
 Naibu waziri wa Mifungo na Uvuvi,Abdallah Ulega  akiangalia samaki aina ya kamongo  alikaushwa  katika banda la  wajasiria mali katika maonesho ya Nane Nane yanayo fanyika  katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)

 Wafungaji mbalimbali  wakionesha mifungo yao katika mashindano ya nane ya mifungo   yanayofanyika  kitaifa katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
 Wafungaji mbalimbali  wakionesha mifungo yao katika mashindano ya nane ya mifungo   yanayofanyika  kitaifa katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)

TTCL waahidi gawio kubwa zaidi kwa serikali mwaka 2019

0
0
SHIRIKA la Mawasiliano nchini (TTCL), limeahidi kutoa gawio kubwa zaidi kwa serikali mwakani, ili fedha hizo zikasaidie katika kazi mbalimbali ukiwemo ujenzi wa miundombinu ya viwanja vya ndege vya serikali.
Hata hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Bw. Waziri Kindamba ambaye alitembelea banda la maonesho ya Kilimo la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), yanayofanyika kwenye Uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu, amesema wingi huo wa fedha utatokana na mashirika na taasisi za umma kuwaunga mkono kwa kutumia huduma mbalimbali zinazotolewa na shirika hilo.
“Mwaka huu tulitoa gawio la sh. Bil 5.1 kwa serikali, lakini ninaimani mwakani tutatoa zaidi endapo tutapata ushirikiano wa kutumiwa kwa huduma zetu kutoka kwenye taasisi nyingine za serikali, ambapo fedha hizo zinasambazwa na serikali kwenye kazi mbalimbali ukiwemo wa ujenzi wa viwanja vya ndege,” amesema Bw. Kindamba.
Bw. Kindamba ameishukuru TAA kwa kuanza kutumia huduma ya mawasiliano ya simu kutoka kwenye shirika hilo, ambapo itasaidia kukuza na kuimarisha uchumi wa nchi.  
Amesema anaahidi kuimarisha ushirikiano na TAA, na wapo tayari kutumia huduma zinazotolewa na mamlaka kwa maslahi ya nchini, ili kuimarisha na kukuza uchumi wa nchi.
“Ushirikiano wetu utasaidia kuongeza mapato, ambapo kila taasisi moja itaweza kutumia huduma na bidhaa za taasisi nyingine, kwa lengo la kuzifanya ziendelee kukua na kuimarika kiuchumi, kwani taasisi za umma zinategemeana zenyewe kwa zenyewe,” amesema.
Pia ameipongeza TAA kwa jitihada zake za kujitangaza kwa wananchi, ambapo ameitaka kuendelea kuboresha miundombinu ya viwanja vya ndege.
“Nawapongeza kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kujitangaza, naomba muendelee kuboresha viwanja vya ndege kwa maslahi ya Watanzania wote, kwa kweli najivunia sana uwepo wenu katika Nanenane “I am proud of your success’ na kweli mna iunganisha Tanzania kwa Ulimwengu,” amesema Bw. Kindamba.
  1. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (mwenye suti nyeusi) hivi karibuni akiongea na Kamati ya maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane alipotembelea banda la Mamlaka kwenye Uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba (kulia) akipata maelezo mbalimbali kutoka kwa Afisa Mipango na Takwimu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Edward Kimaro alipotembelea banda la Maonesho ya Kilimo na sherehe za Nanenane la Mamlaka, yanafanyika kwenye Uwanja wa Nyakabidni mkoani Simiyu.

 Baadhi ya wanakamati ya maonesho ya Kilimo na sherehe za Nanenane ya Mamlaka ya Viwanja wa Ndege Tanzania (TAA), wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) (mwenye suti).
 Afisa Biashara na Masoko wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bi. Herieth Nyalusi (kulia) akitoa maelezo ya ujenzi wa kiwanja kipya cha ndege cha Mkoa wa Simiyu kwa Bi. Grace Kenedy (kulia) na Bi.Magreth Lend wakazi wa Bariadi, walipotembelea banda la maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane yanayofanyika katika Uwanja wa Nyakabindi.
Raia wa China wanaofundisha kwenye shule ya ya sekondari ya J.W.Bukanga Musoma, Bi. Jane Lee (wapili kushoto) na  Bi. Cary Zhang (watatu kushoto) wakimsikiliza Afisa Usalama Mwandamizi wa Mamlaka wa Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Bakari Mwalwisi alipokuwa akitoa maelezo kuhusu vimiminika kwenye banda la maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane la Mamlaka yanayofanyika kwenye Uwanja wa Nyakabindi, mkoani Simiyu.

MAMBO KATIKA BANDA LA OFISI YA BUNGE KATIKA MAONESHO YA NANENANE JIJINI DODOMA

0
0
 Afisa wa Ofisi ya Bunge, Ndugu Partson  akimuelezea  Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma Mheshimiwa Profesa Davis Mwamfupe  orodha ya Maspika waliowahi kuongoza Bunge pamoja na Kumbi zilizowahi kutumika kuendesha vikao vya Bunge.Mheshimiwa Mwamfupe alitembelea Banda la Ofisi ya Bunge katika Maonyesho ya Nanenane yanayoendelea Jijini Dodoma.
 Afisa wa Ofisi ya Bunge, Ndugu Partson  akimuonyesha  Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma Mheshimiwa Profesa Davis Mwamfupe kitabu cha Viapo vya Waheshimiwa Wabunge cha miaka iliyopita. Mheshimiwa Mwamfupe alitembelea Banda la Ofisi ya Bunge katika Maonyesho ya Nanenane yanayoendelea Jijini Dodoma.
 Afisa wa Ofisi ya Bunge, Ndugu Partson  akimuonyesha  Mstahiki  Meya wa Jiji la Dodoma Mheshimiwa Profesa Davis Mwamfupe vazi la Spika pamoja na kumuelezea historia ya vazi hilo. Mheshimiwa Mwamfupe alitembelea Banda la Ofisi ya Bunge katika Maonyesho ya Nanenane yanayoendelea Jijini Dodoma.
Afisa wa Ofisi ya Bunge, Ndugu Omary Machunda akitoa elimu kwa umma kuhusiana na Bunge kwa wanafunzi wa Shule ya Awali ya Taqwa wakati wanafunzi hao walipotembelea Banda la Ofisi ya Bunge katika Viwanja vya Maonyesho ya Nanenane Jijini Dodoma.

TAARIFA KUTOKA IDARA YA UHAMIAJI KUHUSU KUZUILIWA KWA BAADHI YA RAIA KUONDOKA NCHINI

Amunike kocha mpya Taifa Stars

0
0
Na Zanzibar Leo 
 RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amemtambulisha winga wa zamani wa kimataifa wa Nigeria, Emmanuel Amunike kuwa kocha mpya wa timu ya taifa, Taifa Stars. Karia amemtambulisha Amunike mwenye umri wa miaka 47 katika mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika hoteli ya New Africa mjini Dar es Salaam jana baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili. 
 Amunike aliyeng’ara na Super Eagles katika fainali za Kombe la Dunia mwaka 1994 nchini Marekani akicheza wingi ya kushoto, mtihani wake wa kwanza utakuwa ni mchezo dhidi ya Uganda Septemba 8, mwaka huu mjini Kampala, kabla ya kuwafuata Cape Verde Oktoba 10 kukamilisha mechi zake za mzunguko wa kwanza kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
 Na hiyo ni baada ya Taifa Stars kulazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na Lesotho Juni 10, mwaka jana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam ikiwa chini ya kocha mzalendo, Salum Mayanga. Mayanga aliiongoza Taifa Stars kwa mara ya mwisho Machi 27, mwaka huu ikishinda 2-0 dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. 
Taifa Stars inakuwa timu ya kwanza ya taifa ya wakubwa Amunike kufundisha, baada ya awali kuwa kocha wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya kwao, Nigeria kuanzia mwaka 2014 hadi 2017. 
 Zaidi ya hapo, Amunike amefundisha klabu za Al Hazm ya Saudi Arabia, kama Kocha Msaidizi mwaka 2008 kabla ya kuhamia Julius Berger hadi mwaka 2011 alipojiunga na Ocean Boys, zote za Nigeria. 
 Alipoachana na U-17 ya Nigeria akaenda kufundisha Al Khartoum SC ya Sudan kuanzia mwaka 2017 hadi 2018 na sasa anakuja kuujaribu ‘mfupa’ uliowashinda wengi, Taifa Stars. 
 Kisoka, Amunike aliibukia klabu ya Concord mwaka 1990 kabla ya kwenda kuchezea Julius Berger 1991, zote za kwao, Nigeria baadaye Zamalek ya Misiri mwaka 1991 hadi 1994 ndipo akahamia Ulaya. 
 Alianza na klabu ya Sporting CP ya Ureno kuanzia 1994 hadi 1996 kabla ya kuhamia Barcelona ambako alicheza hadi mwaka 2000 alipohamia Albacete zote za Hispania na mwaka 2003 alijiunga na Busan I’Cons ya Korea Kusini alikocheza hadi 2004 kabla ya ku
hamia Al-Wehdat ya Jordan kumalizia soka yake.

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WA NCHI MBALIMBALI IKULU, JIJINI DAR

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na balozi wa Canada nchini aliyemaliza muda wake Mhe. Ian Myles walipokutana Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na balozi wa Ubelgiji nchini aliyemaliza muda wake Mhe. Paul Cartier walipokutana Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na Balozi wa China Mhe. Wang Ke walipokutana kwa mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono na Balozi wa Burundi nchini Mhe. Gervais Abayeho aliyemsindikiza Mjumbe maalumu wa Rais wa Burundi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Ezechiel Nibigira Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono na mjumbe maalumu wa Rais wa Burundi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Ezechiel Nibigira Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2018.

KUMBUKUMU YA MAREHEMU MAMA HELLEN BYARUGABA - KUZALIWA 19/03/1944- KUFARIKI 07/08/2014

0
0
NI MIAKA MINNE SASA TANGU UTUTOKE MPENDWA WETU, MAMA HELLEN HUBERT BYARUGABA. INGAWA ULITUTOKA GHAFLA BILA NENO LOLOTE KWETU, MATENDO YAKO YATABAKIA DAIMA NDANI MWETU NA AMANI NA UPENDO ULIVYOTUACHIA VITAENDELEA KUWA MWONGOZO KWETU.
JAPOKUWA HAUPO NASI KIMWILI LAKINI KIROHO BADO TUPO NAWE.  MAMA TULIKUPENDA SANA NA TUTAENDELEA KUKUPENDA DAIMA.
UNAKUMBUKWA SANA NA MUME WAKO LEOPOLD BYARUGABA, WATOTO WAKO HENRY, LILIAN, LEVINA, LEODGAR-ALUTA, JIMMY PAMOJA NA FAMILIA ZAO WOTE NA MARAFIKI PIA

BWANA ALITOA NA BWANA ALITWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.
AMINA

WATUMISHI NSSF WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA BIDII ILI KUFIKIA LENGO LA KUKUSANYA SHILINGI TRILLIONI 1.5

0
0
MKURUGENZI mkuu wa mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF) William Erio amewataka watumishi wa shirika hilo kufanya kazi kwa bidii na kufikia lengo la kukusanya Shilingi Trilion 1.5 na kwamba hatovumilia wazembe.

Erio aliyasema hayo jana katika mkutano wake na Wakurugenzi na Mameneja wa shirika hilo kwenye ukumbi wa NSSF Ilala Dar es Salaam.

"Mwaka jana mlipaswa kukusanya shilingi Trillion 1 lakini mlikusanya shilingi billion 700 pekee hivyo hamkufikia lengo." Mwaka huu katika mpango kazi ulioidhinishwa na Waziri mnapaswa kukusanya shilingi Trilioni 1.5 target hii lazima hifikiwe."alisema Erio 

Alisema fedha hizo zitapatikana kupitia uandikishwaji wa wanachama wapya, makusanya ya fealisema. wanachama wa zamani pamoja na fedha za pango za majengo ya shirika hilo."Hakuna haja ya kuwa na wanachama lukuki ambao hawalipi michango yao, ni lazima wafuatiliwe kwa karibu kuhakikisha michango inalipwa kwa wakati.

" Najua pia tuna majengo yetu ambayo yapo wazi hayana wapangaji, nimeshaongea na SSRA wanampango wa kufungua ofisi mikoa yote 26 ya Tanzania bara, wapange kwenye majengo yetu." alisema.Hata hivyo, Erio alisema kuwa hatomvumilia mfanyakazi mzembe ambae hatofikia malengo waliyojiwekea."Mkuu wa idara ambae hatofikia performance tuliyojiwekea sitomvumilia, naomba target tuliyoiweka ifikiwe, isipofikiwa maana yake kazi zmewashinda na Mimi sitokuvumilia." alisisitiza.

Erio alisema kuwa jukumu la kusajili wanachama wote ni la wafanyakazi wote na si idara moja pekee." Mwaka huu tunatakiwa kuandikisha wanachama wapya 417,000, NSSF inawafanyakazi 1,000 kila mfanyakazi akileta wanachama 10 kwa mwezi lazima watalipa michango na tutafikia lengo.

Akisisitiza hilo alisema malengo ya shirika yalifikiwa kwenye vikao halali vya wafanyakazi na muktasari ya yatokanavyo kwenye vikao hivyo upo, hivyo ni jukumu la kila mfanyakazi kutekeleza jukumu lake ili kufikia lengo la shirika ambalo ni kujiimarisha na kukua zaidi.

Hata hivyo kwa sasa anaendelea kusoma ripoti mbali mbali za utekelezaji alizokabidhiwa na mtangulizi wake pamoja na wakurugenzi wa kanda na kisha atafanya ziara ya kutembelea kila kitengo ili kubaini changamoto zilizopo miongoni mwa wafanyakazi na kuangalia namna ya kuziondoa.

Erio ambae awali alikuwa mkurugenzi wa PPF aliteuliwa Julai 14 mwaka huu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF akichukua nafasi ya Godius Kahyarara.
Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF) William Erio akizungumza na  Wakurugenzi na Mameneja wa shirika hilo kwenye ukumbi wa NSSF Ilala  jijini Dar es Salaam jana huku akiwataka watumishi wa shirika hilo kufanya kazi kwa bidii na kufikia lengo la kukusanya Shilingi Trilion 1.5 
 Baadhi ya Wakurugenzi na Mameneja wa shirika la NSSF  wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF) William Erio ,alipozungumza nao jana kwenye ukumbi wa NSSF Ilala  jijini Dar es Salaam kuhusiana mikakati mipya ya kuimarisha zaidi mfuko huo,ambapo Watumishi wametakiwa kufanya kazi kwa bidii na kufikia lengo la kukusanya Shilingi Trilion 1.5 . 
 Sehemu ya Viongozi wakuu wa NSSF wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu William Erio ,alipozungumza nao jana kwenye ukumbi wa NSSF Ilala  jijini Dar es Salaam kuhusiana mikakati mipya ya kuimarisha zaidi mfuko huo,ambapo Watumishi wametakiwa kufanya kazi kwa bidii na kufikia lengo la kukusanya Shilingi Trilion 1.5 . 

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO ABDALLAH ULEGA AFUNGUA MAONESHO YA NANENANE KANDA YA KATI

0
0
Na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amefungua rasmi maonesho ya Nane Nane Kanda ya kati ambayo yanaenda sawa na mashindano ya Nane ya Mifugo kitaifa yanayofanyika jijini Dodoma.

Ulega amefungua mashindano ya Mifugo ambayo yalianza mwaka 2011 na huwa yanafanyika Agosti 5  ya kila mwaka mkoani Dodoma na hujumuisha ng'ombe wa maziwa na nyama walioboreshwa pamoja na Mbuzi wa asili.Akizungumza jana Ulega amesema kuwa lengo kuu la mashindano hayo ni kutambua umuhimu na mchango wa rasmilimali za mifugo ya asili katika kuendeleza sekta ya mifugo nchini.

Aidha amesema kuwa mchakato huo linalenga kutambua juhudi na maarifa wanayotumia wafugaji wa mifugo ili kufuga kwa tija na hatimaye kuvutia wafugaji wengi na kuiga na kuingia kwenye ufugaji wenye tija kwa taifa.Ulega amesisitaza kuwa sekta ya mifugo ni moja ya Sekta muhimu zinazochangia kupunguza umaskini wa wananchi na kukuza uchumi wa nchi kwani ni mhimili katika kuendeleza viwanda kama ilivyoainishwa katika mpango kabambe wa Mifugo Tanzania.

Hata hivyo ametoa maagizo kwa wafugaji na wadau mbalimbali kuunda na kuimarisha vikundi na vyama vya ushiriki ili kuongeza kasi ya uwekezaji katika viwanda vya kusindika mazao ya mifugo na hatimaye kufikia malengo na kauli mbiu ya Nane Nane 2018 isomekayo ''WEKEZA''.Aidha Ulega ameagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha utekelezaji wa mfumo wa utoaji kinga mbalimbali za magonjwa ya mifugo uwe ni lazima kwa wafugaji wote nchi.

Pia Ulega amesema wafugaji pamoja na wafanyabiasha  hawaruhusiwi kuhamisha au kusafirisha mifugo pamoja  mazao kutoka sehemu moja hadi nyingine bila kibali.Hivyo imesababisha maeneo ya mipakani mwa nchi yetu imeshamiri biashara haramu za mifugo na mazao yake zisizo rasmi na amewataka watendaji kusimamia sheria kwa kushirikiana na wadau ili kutatua changamoto ya utoroshaji wa rasilimali za mifugo yetu na mazao yake.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiangalia viatu katika banda la Magereza vinavyotegenezwa kwa bidhaa ya ngozi katika maonesho ya Nane Nane Nane ndani ya viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.

Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiwa ameambatana na Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge wakitembelea banda la wajasiriamali katika maonesho ya Nane Nane yanayo fanyika katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiangalia samaki aina ya kamongo aliekaushwa katika banda la wajasiriamali katika maonesho ya Nane Nane yanayo fanyika ndani ya viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii).

WAZIRI LUGOLA ATOA MILION 40 UJENZI SEKONDARI JIMBONI MWIBARA, AMWAGA ZAWADI WASHINDI WA KANGI BONANZA LA MICHEZO BUTIMBA

0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Bulimba katika Kiwanja cha Mpira cha Victoria, Jimbo la Mwibara, wilayani Bunda, kabla ya Waziri huyo kugawa zawadi ya mshindi wa Bonanza la Kangi la mpira wa miguu ambapo timu ya mpira wa miguu ya Muungano pamoja na Miseni zote zinatoka Kata ya Butimba zilicheza. Lugola alitoa shilingi milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya kidato cha tano na sita katika shule ya Sekondari Bulimba. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kulia) akimuangalia Kapteni wa timu ya mpira wa miguu ya Muungano, Bwire Metwisele wakati alipokua anashangilia mara baada ya Waziri huyo kumkabidhi zawadi ya mshindi wa kwanza wa Bonanza la Kangi, kwa kuifunga timu ya Miseni magoli mawili bila. Timu zote zinatoka Kata ya Butimba wilayani Bunda, Mkoa wa Mara. Pia Lugola alitoa shilingi milioni 40 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya kidato cha tano na sita katika shule ya Sekondari Bulimba.
Mchezaji wa Timu ya Muungano ya Kata ya Butimba wilayani Bunda, Bwire Metwisele (kulia), akimdhibiti mchezaji wa timu ya Miseni, Jovin Andrew, katika mashindano ya Bonanza la Kangi lililofanyika katika kiwanja cha Victoria, Kijiji cha Bulimba. Timu ya Muungano iliifunga Miseni magoli mawili kwa bila.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kulia) akimsalimia mzee wa Kijiji cha Bulimba, Kata ya Butimba, Jimbo la Mwibara wilayani Bunda, wakati alipokua katika ziara ya kukagua mikradi ya maendeleo ndani ya Jimbo lake. Lugola pia alishiriki mashindano ya mpira wa miguu ya Bonanza la Kangi, iliyokutanisha timu mbili za Muungano na Miseni za Kata hiyo, Timu ya Muungano iliifunga Miseni magoli mawili bila. Pia katika hotuba yake, Mbunge huyo alitoa shilingi milioni 40 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya kidato cha tano na sita katika shule ya Sekondari Bulimba.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (aliyeonyesha alama ya vidole) akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu za mpira wa miguu ya Muungano pamoja na Miseni pamoja na maafisa wa Wilaya ya Bunda, kabla ya kuanza kucheza katika kiwanja cha Victoria kijijini Bulimba, Jimboni humo. Lugola alitoa zawadi ya mshindi wa mashindano hayo na pia alitoa shilingi milioni 40 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya kidato cha tano na sita katika shule ya Sekondari Bulimba. Watatu kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili. 


MBIO ZA MWENGE ZAFUNGUA OFISI ZA TANESCO WILAYA YA BAHI MKOANI DODOMA

0
0
KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Mhandisi Charles Francis Kabeho amefungua Jengo la Ofisi za Shirika la Umeme nchini (Tanesco) wilayani Bahi mkoani Dodoma ikiwa ni mpango wao wa kusogeza huduma karibu na wananchi waliopo maeneo mbalimbali hapa nchini. 

Akizungumza mara baada ya kufungua Jengo hilo Mhandisi Kabeho amepongeza juhudi zinazofanywa na shirika hilo katika kuhakikisha ofisi zao zipo kwenye mazingira mazuri ya wafanyakazi kuweza kuwahudumia wananchi kwa ufanisi wakati wanapokuwa wakifika kwenye maeneo yao kupata huduma .Alisema hatua ya wao kupanua wigo mpana wa kuwafikia wananchi itawawezesha kuondokana na changamoto mbalimbali ikiwemo kuzifuata kwa umbali mrefu hivyo jambo hilo linahitaji kupongezwa kutokana na kuona umuhimu wa kuwafikia 

“Nimependezwa na jitihada za TANESCO katika kuhakikisha wateja wanafiki wa na huduma za Umeme kwa ukaribu zaidi, nakuhudumiwa katika mazingira mazuri, hivyo niwapongeze TANESCO kwa hili lakini pia nisistize kuwa ofisi hizi ziweze kuhudumia wateja hao kwa weledi”alisemaMhandisi Kabeho .Naye Mkuuwa Wilaya ya Bahi Mwanahamisi Mkunda amemshukuru Mkuuwa Mbioza Mwenge kwa kuweza kufungua jingo hilo na kuwa hakikishia wananchi wa Bahi kuwa Huduma ya umeme sasa ipo karibu na kuwa wilaya ya Bahi sasa inauhakika wakupata hudumaza Umeme masaa 24, 

Kwa upande wake Meneja wa TANESCO wilaya ya Bahi, Mhandisi Bryceson Kitila amesema kuwaUjenzi wa jengo la Ofisi ya Bahi umetekelezwa naShirika la Umeme Tanzania kwa madhumuni ya kuongeza Ufanisi wakazi katika mji wa Bahi na vijiji vya Jirani,pia kuwezesha wananchi wa Bahi kupata Huduma Bora nayaUhakika kwa kuwa na kituo cha huduma kwa wateja(one stop shop center) hivyo mteja anaweza kupata huduma zote katika dawati moja ikiwemo na manunuzi ya umeme (LUKU). 

Mbio hizi za Mwenge wa Uhuru, zimehitimishwa katika mkoawa Dodoma ambapo zimehusishau funguaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo ikiwemo Jengo la TANESCO.
 MKUU wa wilaya ya Bahi Mwanahamisi Mkunda akitoa shukrani kwa KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Mhandisi Charles Francis Kabeho kushoto mara baada ya uzinduzi wa Jengo la Tanesco wilaya ya Bahi 
 MKUU wa wilaya ya Bahi Mwanahamisi Mkunda kulia akiwa na KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Mhandisi Charles Francis Kabeho kushoto mara baada ya uzinduzi wa Jengo la Tanesco wilaya ya Bahi 

JAFO AAGIZA WEZI WA VIFAA VYA UJENZI KITUO CHA AFYA NDAGO WAKAMATWE

0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amemuagiza Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoani Singida kupitia vyombo vya dola kuwasaka wezi wote waliiba vifaa vya ujenzi wa kituo cha afya Ndago wilayani huo na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao. 

Jafo ametoa agizo hilo leo baada ya kufanya ziara katika Kituo cha afya Ndago ambacho ni miongoni mwa vituo vya afya vilivyopokea Sh.Milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa majengo mbalimbali lakini ujenzi wake haujakamilika hadi sasa kutokana na baadhi ya vifaa kuibwa na wananchi wasio waaminifu.Katika ziara hiyo, Waziri Jafo ameonyesha kukerwa na uzembe wa usimamizi uliojitokeza katika ujenzi wa kituo hicho cha afya.

Hata hivyo, pamoja na kuagiza kusakwa kwa wezi wa vifaa, Waziri Jafo ameiagiza Ofisi ya mkoa wa Singida kufanya uchunguzi ndani ya wiki moja ili kubaini kama kuna watumishi waliohusika katika sakata hilo nao wachukuliwe hatua kali za kinidhamu.

Waziri Jafo amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Iramba kukamilisha ujenzi wa majengo hayo kabla ya mwisho wa mwezi huu wa Agosti ili wananchi wa Ndago waweze kupata huduma bora ya afya kama ilivyokusudiwa na serikali.

Aidha katika ziara hiyo waziri Jafo ametembelea na kukagua pia ujenzi wa barabara mpya ya kilometa 10 inayotoka Kiengege kwenda kata ya Ndago ambapo amepongeza Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini(TARURA) kwa kazi nzuri waliyoifanya katika ujenzi wa barabara hiyo.

Mganga mkuu wa wilaya ya Iramba akisoma taarifa ya ujenzi wa kituo cha Afya Ndago.
Baadhi ya makaravati yaliyojengwa kwa mawe ili kuwezesha barabara hiyo iweze kupitika wakati wote.
Meneja wa TARURA wilaya ya Iramba akitoa maelezo ya ujenzi wa barabara mpya. 
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ndago.
Baadhi ya vifaa vikiwemo Nondo na mifuko ya saruji ambavyo tayari zimekamatwa wakati wa ujio wa Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo.

TCRA:HAKIKISHENI TAARIFA MNAZOZITOA WAKATI WA KUSAJILI KADI ZENU ZA SIMU NI SAHIHI, VINGINEVYO SHERIA ITAFUATA MKONDO WAKE

0
0
Na. Vero Ignatus Arusha. 

Mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA imewataka wananchi kufahamu wajibu na haki zao wanazostahili  kupata kutoka kwenye mitandao inayotoa  huduma za mawasiliano sambamba na kutambua wajibu walionao kama watumiaji wa huduma za mawasiliano

Kaimu mkuu wa Kanda ya kaskazini Francis  Msungu amesema kuwa mamlaka inatoa elimu kwa wananchi kuzijua haki zao kutokana na mabadiliko yanayotokea ni mengi ya sayansi na teknolojia pamoja na maendeleo ya matumizi ya vifaa vya mawasiliano katika mitandao ya simu.

Amesema kwa sasa kumezuka wimbi la utapeli kupitia simu za mikononi,  hivyo wananchi  wametakiwa kuwa na tahadhari kubwa, wasikubali kurubuniwa katika vitu ambavyowanafahamuhawajashiriki Usitekeleze maagizo yeyote yahusuyo fedha kwa ujumbe wa maandishi,

"Mfano unatumiwa ujumbe kuwa umeshinda bahati na sibu katika
Mashindano ambayo hujashiriki, ukipokea ujumbe umetumiwa pesa na mtu usiyemfahamu usizitoe fedha hizo, hadi  uthibitishe ya kwamba zimetumwa kwa nia nzuri" 

Amewataka wananchi mara waonapo fedha imetumwa kwenye mitandao yao  na aliyezituma bado hajafahamika, ni vyema wakawa na subira hadi watakapo hakikisha zimetumwa kwa nia njema ili wasiingie kwenye matatizo."watu huwa wanakosea pia yamkini zilitumwa kwa bahati mbaya, ukiwahi kuzitoa nawe unahesabika unaiba. alisema"


Amewataka watumiaji wa simu za mkononi kufahamu kuwa zipo tahadhari za kuchukuliwa ikiwepo kusajili namba kwa majina kamili  ya muhusika kwani ni takwa la kisheria, bila kusahau kwamba kila taarifa zinazoyolewa wakati wa usajili ziwe za sahihi.Taarifa zako zikiwa za uongo hilo nikosa kisheria utapata adhabu ya kifungo au kulipa shilingi milioni 3 au vyote kwa pamoja. 


Ameshauri kwamba yeyote akipoteza simu au kadi atoe taarifa kwa jeshi la polisi na kwa mtoa huduma, samba na kuchukua tahadhari mara uokotapo simu au kadi ya simu utoe taarifa kwa usalama wako zaidi.Wananchi wote wanaotembelea maonyesho  25 ya kilimo na sherehe za nanenane kanda ya kaskazini mwaka 2018 wanashauriwa kutembelea banda la TCRA ili waweze kupata elimu zaidi ya mawasiliano.
Wa kwanza kulia ni Kaimu mkuu Kanda ya kaskazini Francis Msungu, akifuatiwa na Mhandisi Jan Kaaya wakiendelea kutoa elimu kwa baadhi ya wageni waliotembelea banda hilo katika maonesho ya 25 ya nanenane  viwanja vya TASO mkoani Arusha. 

Wananchi wakiendelea kupatiwa elimu juu ya nyenzo za mawasiliano. 


WAZIRI WA UVUVI NA MIFUGO LUHAGA MPINA ATEMBELEA BANDA LA TAASISI YA PASS KATIKA MAONESHO YA NANE NANE MKOANI SIMIYU

0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya kusaidia Sekta Binafsi zinazojihusisha na masuala ya Kilimo,Uvuvi na Ufugaji ,(PASS) Nicomed Bohay akimuonesha Waziri wa Uvuvi na Mifugo,Luhaga Mpina mfano wa Bwawa linalotumika kufugia samaki ,Mabwawa ambayo Taasisi ya PASS imekuwa ikisadia katika upatikanaji wa mikopo kwa Wafugaji wa Samaki ili waweze kufuga kisasa.
Mmoja wa wanufaika wa  huduma zinazotolewa na Taasisi binafsi ya kusaidia sekta ya Kilimo nchini (PASS) ikiwemo ya unenepeshaji wa Ngombe  Michael Tegeshi akitoa maelezo kwa Waziri wa Uvuvi na Mifugo,Luhaga Mpina alipotembelea banda la taasisi hiyo katika maonesho ya nane nane yanayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi mkoni Simiyu.
Waziri wa Uvuvi na Mifugo,Luhaga Mpina akitizama Mchele uliowekwa vizuri katika mifuko kwa ajili ya kuongeza thamani ,Mchele huo unaandaliwa na vikundi ambavyo vimepata msaada kutoa katika taassi hiyo.
Meneja wa  PASS Trust  tawi la Mtwara ,Isaac Kileo akitoa maelezo kwa Waziri wa Uvuvi na Mifugo Luhaga Mpina alipotembelea banda la taasisi hiyo katika maonesho ya nane nane yanayofanyika kitaifa katika mkoa wa Simiyu
Waziri wa Uvuvi na Mifugo,Luhaga Mpina akimsikiliza Mkurugenzi wa Biashara PASS,Kilo Rusewa alipotembelea katika Banda la taasisi hiyo katika viwanja vya nane nane mkoani Simyu.

WASICHANA 10,000 WAFIKIWA NA TASISI YA MSICHANA INITIATIVE

0
0
Na Humphrey Shao, Globu jamii

Zaidi ya Wasichana 10,000 wamefikiwa na huduma zitolewazo na tasisi ya Msichana Initiative katika kipindi cha miaka Miwili na nusu tangu kuanzishwa kwake nchini.

Hayo yamesemwa leo na Mwasisi na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo , Rebeca Gyumi alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu kongamano la Ajenda ya Msichana linalo Taraji kufanyika Agosti 11 mwaka hu katika ukumbi wa Kisenga LAPF Millennium Tower Dar es Salaam.

Gyumi amesema kuwa kupitia kongamano hilo jumla ya Washiriki 1000 watashiriki wakiwemo wasichana walio ndani ya shule na nje ya shule kutoka klabu za Msichana Café na Makundi ya watu wenye mahitaji maalum.

“kwa kipindi cha miaka miwili na nusu tangu kuanzishwa kwa tasisi hii tumeweza kuwafikia wasicha 10000 moja kwa moja hivyo katika mkutano wa mwaka huu 2018 tumekuja na kauli mbiu isemayo ‘Nafasi ya Jamii kwenye kuunda na kutetea haki za mtoto wa kike’ huku msisitizo mkubwa wa kauli hii mbiu ni kuangalia namna gani Wasichana wanazifahamu haki zao na kujua jinsi ya kuzitetea ili kuleta Mabadiliko chanya kwenye jamii” amesema Gyumi.

Gyumi alisema kuwa Mgeni rasmi katika kongamano hilo anataraji kuwa Mkurugenzi kutoka shirika la Women Fund Tanzania(WFT)Mery Lusimbi, aidha Wasichana watapata nafasi ya kuzungumzia changamaoto mbalimbali wanazozipitia .

Amesema taasisi ya Msichana Initiative ambayo inafanya kazi kwa ukaribu na serikali katika kupinga ndoa za utotoni , Unyanyasaji na ukandamizaji wa kijinsia kwa lengo la kuwapa nafsi wasichana kufikia malengo yanayotakiwa katika Maisha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Msichana Initiative, Rebeca Gyumi akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya Kongamano la Ajenda ya Msichacha linalotaraji kufanyika agosti 11 mwaka huu katika ukumbi wa Kisenga LAPF Millennium Tower Dar es Salaam.
Sehemu ya Waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo wa kutambulisha Kongamano la Ajenda ya Msichana.
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live




Latest Images