Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 241 | 242 | (Page 243) | 244 | 245 | .... | 3283 | newer

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Ndugu Sylvester Ambokile Mwakinyule (pichani kulia) kuwa Kamishna Mkuu, Idara ya Uhamiaji.

  Taarifa iliyotolewa leo, Alhamisi, 29 Agosti, 2013 mjini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue inasema kuwa uteuzi huo umeanza jana, Agosti 28, mwaka huu, 2013.

  Ndugu Mwakinyule anachukua nafasi ya Ndugu Magnus Ulungi ambaye atapangiwa kazi nyingine.

  Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Sylvester Ambokile Mwakinyule, alikuwa Naibu Kamishna wa Uhamiaji na Mwambata wa Uhamiaji katika Ubalozi wa Tanzania, London, Uingereza.

  Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dkt. Nyamajeje Calleb Weggoro (pichani kushoto) kuwa Msaidizi wa Rais, Masuala ya Ushirikiano wa Kikanda.

  Taarifa iliyotolewa leo, Alhamisi, 29 Agosti, 2013 mjini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue inasema kuwa uteuzi huo umeanza jana Agosti 28, mwaka huu, 2013.

  Kabla ya uteuzi huu, Dkt. Nyamajeje Calleb Weggoro alikuwa Mkurugenzi wa Sekta za Uzalishaji (Productive Sectors) katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

  0 0

  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameahidi kutoa sh. milioni 10 ili kuwasaidia vijana wanaoishi kwenye kijiji cha vijana cha Tulu ambao wameamua kujitegemea kwa uzalishaji kupitia kilimo, matumizi ya misitu na ufugaji.
   
  Alitoa ahadi hiyo jana jioni (Alhamisi, Agosti 29, 2013) wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara na vijana wa kijiji hicho pamoja na wakazi wa vijiji jirani vya Tumbili na Lufwisi wilayani Sikonge mkoani Tabora.
   
  Kijiji cha Vijana cha Tulu ambacho wenyewe wanakiita Pathfinders Green City (Jiji la Watafuta Njia) kilianzishwa Aprili 2013 kikiwa ni msitu mtupu baada ya kupewa ekari 280 kutoka vijiji jirani vya Tumbili na Lufwisi. Kilianzishwa kikiwa na vijana 68 kutoka katika kata zote 17 za Wilaya ya Sikonge. Hivi sasa kijiji kina vijana 87 wakiwamo wasichana 22 na wavulana 65 wenye umri wa kati ya miaka 18 na 24.
   

  0 0

  Airtel Yatosha inazidi kupamba moto. Zimebaki siku CHACHE SANA kwa wewe MTEJA wa Airtel kuibuka mshindi wa Nyumba ya kisasa ya Airtel Yatosha iliyojengwa na Shirika la nyumba la taifa (NHC) iliyopo maeneo ya kigamboni jijini Dar es saalam.

  Meneja Uhusiano wa Airtel,Jackson Mmbando amesema “Siku ya Alhamisi tarehe 5 mwezi wa 9 ndio siku inayosubiriwa kwa hamu; ambapo tutapata mshindi wa nyumba ya pili ya promosheni ya Airtel Yatosha”

  Wewe mteja wa Airtel Yatosha bado una nafasi ya kuibuka mshindi! Ni rahisi. Piga *149*99# sasa na ujiunge na kifurushi chochote cha SIKU, WIKI AU MWEZI cha Airtel Yatosha na moja kwa moja utaingia kwenye droo ya kushinda. Kumbuka, pia kuna Tsh milioni 1 kushindaniwa kila siku. Usilaze damu! Jiunge zaidid na Airtel Yatosha, uongeze nafasi zako zakushinda! Alidokeza bw, Mmbando

  Airtel Yatosha. Na BADO!!
  Meneja Uhusiano wa Airtel,Jackson Mmbando akizungumza na waandishi wa habari.

  0 0

  Katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na matukio mengi ya ukatili dhidi ya watoto ambayo yamekuwa yakiwaathiri watoto kimwili ikiwa ni pamoja na kupoteza maisha.

  Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa kuhusu tukio la mwanafunzi aliyepigwa na mwalimu wake katika shule moja ya Msingi Wilayani Makambako na kusababishiwa maumivu makali na hatimaye mtoto huyo akawa amepoteza maisha yake. Wizara inasikitishwa na mazingira ya kifo cha mtoto ambaye alikuwa chini ya uangalizi wa mwalimu na tukio la viboko ambavyo vinahusishwa na kifo cha mtoto.

  Wizara inalaani vikali adhabu zinazotolewa kiholela kwa watoto bila kuzingatia kanuni na taratibu. Wizara inasisitiza kuzingatia utaratbu katika kuwarekebisha watoto ili adhabu ziwe na matokeo chanya kwa watoto na wanafunzi kwa ujumla. Kila mwanachi najukumu la ulinzi na usalama wa mtoto hivyo kwa pamoja tunatakiwa kushirikiana katika kuhakikisha kuwa familia na shule zetu zinakuwa mahala salama pa kuishi.

  Katika tukio lingine, Wizara inakemea tukio la mama aliyemwunguza mtoto kwa moto katika sehemu za vidole vya mikononi kama sehemu ya adhabu kwa kosa la udokozi wa chakula. Wizara inasikitishwa na taarifa kuwa mtoto huyu amesababishiwa maumivu makali mwilini na inawezekana atapoteza kabisa vidole vya mkono mmoja katika maisha yake yote. Wizara inatoa rai kuwa adhabu kama hizi zinapotolewa na mmoja wa wanafamilia inarudisha nyuma jitihada za Serikali katika kukuza maendeleo ya haki za watoto nchini.

  Aidha, kipigo cha mwanafunzi kilichosababisha kifo cha mwanafunzi na kumchoma mtoto mikononi ni matukio yanayochochewa na mitizamo finyu katika jamii katika kuwakanya watoto. Adhabu zenye madhara kwa mtoto hazimrekebishi mtoto na bala yake zinaleta madhara zaidi kwa maisha na uhai wa mtoto. Wizara inapenda kuwakumbusha wananchi kwamba Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasisitiza kuheshimu utu wa mtoto maana binadamu wote ni sawa na kwamba watoto nao wanastahili kupata haki sawa katika jamii.

  Mwisho Wizara inaendelea kuhimiza jamii kubadilika na kuhakikisha kuwa shule na familia zinakuwa salama na mahali penye amani miongoni na wanafamilia bila kusahau kulinda na kuendeleza haki za watoto.

  Wizara inatoa pole kwa wazazi, ndugu, marafiki na familia ya mwanafunzi aliyeuawa katika umri mdogo kutokana na kufanyiwa ukatili na Wizara inaomba jamii kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu.

  Erasto T. Ching’oro
  KNY KATIBU MKUU
  30 Agosti, 2013

  0 0

  Mdau Fredy Anthony ambaye ni Head of Group Research and Product Development wa Tone Multimedia Group , akiwa Nje ya ukumbi wa Dewan Tun Canselor Mara baada kupata shahada yake ya pili (Master of Business administration - Multimedia Marketing) katika Chuo kikuu cha Multimedia kilichopo Malaysia.
  Mdau Fredy Anthony akiwa katika Picha ya Pamoja na Marafiki walio msindikiza katika Mahafali hayo.

  0 0


  0 0

  Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye amezidi kujijengea heshima ndani na nje ya nchi Nasib Abdul maarufu kama Diamond anatarajiwa kupagawisha wakazi wa mkoa wa Kigoma Jumamosi hii na style ya kipekee ya ‘Kikwetu Kwetu’ kwa hisani ya bia ya Kilimanjaro.

  Msanii Diamond ataungana na wasanii wengine tisa wa muziki wa Bongo Fleva watakaotumbuiza katika tamasha la ‘Kili Music Tour 2013’ ambalo linatarajiwa kufanyika mjini Kigoma katika uwanja wa Lake Tanganyika siku ya Jumamosi.

  Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager Bwana George Kavishe alisema kuwa “tamasha la Kili Music Tour linaelekea Kigoma baada ya kufanya vizuri jijini Mbeya, Mwanza, Dodoma, Tanga na Kilimanjaro. Wasanii kumi ambao watatumbuiza Jumamosi hii ni Diamond Plutnumz, Linex, Barnaba, AT, Fid Q, Prof J, Recho, Lady Jay Dee, Roma na Ben Paul.”

  Bwana Kavishe aliendelea kufafanua kuwa amefurahishwa sana na jinsi watanzania wanavyopokea bonge la kiburudisho kutoka kwa bia yao ya Kilimanjaro. “ni faraja kubwa kuona jinsi style ya “kikwetukwetu” ilivyokubalika nchini kote. Kilimanjaro inaelewa fika kuwa watanzania wana mambo mengi sana ya kujivunia ambayo ni ya kipekee kikwetukwetu. 

  Ukiachana na bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambayo inatengenezwa Tanzania, na watanzania, kwa viungo vya kitanzania kwa ajili ya watanzania, kuna mambo mengine mengi sana ya kikwetu kwetu kama muziki wetu wa bongo fleva, dansi zetu za kiduku, kandanda letu na ushindani wa Simba na Yanga, komedi yetu iliyo tofauti kabisa n.k. “

  Kwa upande wake Diamond alisema kuwa “Kama ilivyo kauli mbiu ya tamasha hili ‘Kikwetu kwetu’ naamini nitatoa burudani kali kabisa kwa wanakigoma. Ukizingatia kuwa Kigoma ni nyumbani wanandugu zangu wategemee bonge la kiburudisho kutoka kwangu na wasanii wenzangu nitakaokuwa nao”.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) na Balozi wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt wakikata utepe kuzindua rasmi mitambo ya redio za mawasiliano katika Vituo vya Wanamaji vya Jeshi la Polisi na Jeshi la Wananchi. Mitambo hiyo imefungwa kwa hisani ya Serikali ya Marekani ambayo imegharimu Dola za Marekani milioni moja (1,000,000 USD). Redio hizo za mawasiliano zitasaidia kukabiliana na ajali pamoja na makosa yanayofanywa katika maeneo ya baharini na maziwa nchini. Uzinduzi huo umefanyika katika Kituo cha Kikosi cha Polisi Wanamaji jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi (kulia) na Balozi wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt wakiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) ujumbe ulioandikwa katika bango baada ya kukata utepe kuzindua rasmi mitambo ya redio za mawasiliano katika Vituo vya Wanamaji vya Jeshi la Polisi na Jeshi la Wananchi. Mitambo hiyo imefungwa kwa hisani ya Serikali ya Marekani ambayo imegharimu Dola za Marekani milioni moja (1,000,000 USD). Redio hizo za mawasiliano zitasaidia kukabiliana na ajali pamoja na makosa yanayofanywa katika maeneo ya baharini na maziwa nchini. Uzinduzi huo umefanyika katika Kituo cha Kikosi cha Polisi Wanamaji jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na viongozi wa Jeshi la Polisi, Jeshi la Wananchi, Marekani pamoja na waandishi wa habari kabla ya kuzindua mitambo ya redio za mawasiliano katika Vituo vya Wanamaji vya Jeshi la Polisi na Jeshi la Wananchi. Mitambo hiyo imefungwa kwa hisani ya Serikali ya Marekani ambayo imegharimu Dola za Marekani milioni moja (1,000,000 USD). Redio hizo za mawasiliano zitasaidia kukabiliana na ajali pamoja na makosa yanayofanywa katika maeneo ya baharini na maziwa nchini. Uzinduzi huo umefanyika katika Kituo cha Kikosi cha Polisi Wanamaji jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Balozi wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt akitoa hotuba yake kabla ya uzinduzi wa mitambo ya redio za mawasiliano katika Vituo vya Wanamaji vya Jeshi la Polisi na Jeshi la Wananchi. Wakwanza kutoka kulia (aliyekaa) ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi. Mitambo hiyo imefungwa kwa hisani ya Serikali ya Marekani ambayo imegharimu Dola za Marekani milioni moja (1,000,000 USD). Redio hizo za mawasiliano zitasaidia kukabiliana na ajali pamoja na makosa yanayofanywa katika maeneo ya baharini na maziwa nchini. Uzinduzi huo umefanyika katika Kituo cha Polisi Wanamaji jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Baadhi ya vifaa vya mawasiliano vilivyozinduliwa leo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi pamoja na Balozi wa Marekani nchini Alfonso Lenhardt. Vifaa hivyo vya mawasiliano vitasaidia kukabiliana na ajali pamoja na makosa yanayofanywa katika maeneo ya baharini na maziwa nchini. Uzinduzi huo umefanyika katika Kituo cha Kikosi cha Polisi Wanamaji jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0

  Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Kitengo cha Huduma Binafsi za Kibenki kwa Wateja Wakubwa cha benki hiyo jijini Dar es Salaam leo. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Mizinga Melu na kulia kwa Mengi ni Mkuu wa Kitengo hicho, Andrew Massawe.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Mizinga Melu akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Kitengo cha Huduma Binafsi za Kibenki kwa Wateja Wakubwa cha NBC jijini Dar es Salaam leo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Mizinga Melu (kushoto) akiwatambulisha baadhi ya maofisa katika kitengo hicho katika hafla hiyo.
  Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi (katikati) akifurahi na Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Mizinga Melu (kushoto) na Mkuu wa Idara ya Huduma za Kibenki kwa Wateja Wakubwa na Uwekezaji, Andre Potgieter katika hafla ya uzinduzi wa Kitengo cha Huduma Binafsi za Kibenki kwa Wateja Wakubwa cha benki hiyo jijini Dar es Salaam leo.
  Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi (katikati) akishikana mikono na Meneja Uhusiano wa NBC, Makyalen Marealle katika hafla ya uzinduzi wa Kitengo cha Huduma Binafsi za Kibenki kwa Wateja Wakubwa cha benki hiyo jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo hicho, Andrew Massawe na Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Mizinga Melu.
  Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi (katikati) akihojiwa na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari mara baada ya uzinduzi wa kitengo hicho. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Mizinga Melu.

  0 0


  0 0

   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akizungumza na Watendaji Wakuu wa Jeshi la Polisi Makao Makuu pamoja na Kanda Maalumu ya Dar es Saalam ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Kamishna wa Utawala, Rasilimali na Fedha wa Jeshi la Polisi, Clodwing Mtweve. 
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akizungumza na Watendaji Wakuu wa Jeshi la Polisi Makao Makuu pamoja na Kanda Maalumu ya Dar es Saalam ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo. Wa pili kutoka kushoto ni Kamishna wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam (CP) Suleiman Kova. Picha na mdau Felix Mwagara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


  0 0

  Msanii mkongwe wa muziki wa dansi, Muhidin Gurumo akijaribu gari dogo alilokabidhiwa na mwanamuziki wa bongo fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond ‘ kutokana na kutambua mchango wake baada ya kustaafu kazi ya muziki.
  Muhidin Gurumo akipokea funguo ya gari kutoka kwa Diamond
  Gari alilozawadiwa mzee Gurumo.

  0 0

  TFF, AZAM MEDIA ZASAINI MKATABA WA BIL. 5.5/-
  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kampuni ya Azam Media leo (Agosti 30 mwaka huu) wamesaini mkataba wa haki za kipekee za televisheni (exclusive rights) utakaoiwezesha Azam TV kuonesha mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).

  Mkataba huo wa miaka mitatu wenye thamani y ash. 5,560,800,000 umesainiwa kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais, Athuman Nyamlani amesaini kwa niaba ya TFF wakati aliyesaini kwa upande wa Azam Media ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Thys Torrington.

  Ligi Kuu ya Tanzania sasa itakuwa ikipatikana kupitia kisimbuzi (decorder) cha Azam TV kitakachokuwa na chaneli zaidi ya 50. Mechi hizo zinatarajiwa kuoneshwa moja kwa moja wakati wowote kuanzia mwezi ujao.

  Makamu wa Rais wa TFF, Nyamlani amesema udhamini huo wa televisheni ni fursa pana kwa klabu kwani zitaweza kujitangaza zaidi huku wachezaji nao wakipata soko zaidi za mpira wa miguu.

  KOCHA KIM AONGEZA MMOJA TAIFA STARS
  Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ameongeza kwenye kikosi chake beki David Mwantika kwa ajili ya mechi ya Kombe la Dunia dhidi ya Gambia itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu jijini Banjul.

  Mwantika ameitwa kwenye kikosi hicho kuziba nafasi ya beki Kelvin Yondani ambaye ni majeruhi. Wachezaji ambao ni majeruhi na Kim amewaondoa kwenye kikosi hicho ni waweze kushughulikia matibabu yao ni Athuman Idd, Shomari Kapombe na John Bocco.

  Taifa Stars imeingia kambini jana (Agosti 29 mwaka huu) na imeanza mazoezi leo jioni kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume. Timu hiyo inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager pia itakuwa ikifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa.
   
  Boniface Wambura
  Ofisa Habari
  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

  0 0

  Simply Madini is a locally owned company, specializing in importing Fine Jewelry, Fashion Jewelry, Kids Jewelry and Watches from the US top jewelers and vend to Top Ladies here in Tanzania.

  Simply Madini has been touched with Miss Tanzania involvement in charity/give back projects especially the recent one with the Abino kids in Shinyanga. ‘’To acknowledge her great job she has been doing we’ve awarded her with one of our Fine jewelry piece, ¼ ct tw white and black diamond jewelry 4-pc set’’ said Simply Madini representative Nasemba.

  Simply Madini is wishing Miss Tanzania Good-Luck on the 63rd Miss World Grand Final taking place in Indonesia –September 2013.
  Prepared by: Kikoi Innovative Media Ltd.

  0 0

  Meneja Masoko wa Mikono Business Consult Bi. Nestoria Simon (kulia) akimuelezea Bi .Anna Machanga,kuhusu faida ya moja ya vitabu vinavyopatikana katika banda lao,Katika maonesho ya Vodacom Elimu Expo yanayofanyika kwa siku tatu katika viwanja vya posta kijitonyama jijini Dar es salaam.
  Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari ya wasichana ya Premier iliyopo Bagamoyo Mkoa wa Pwani, wakifanya majarabio ya kuchanganya kemikali katika banda la shule yao katika maonesho ya Vodacom Elimu Expo yanayofanyika kwa siku tatu katika viwanja vya posta kijitonyama jijini Dar es salaam.
  Meneja Matukio wa kampuni ya T- MARC Bi. Dorris Chalambo,akizungumza na waandishi wa habari kuhusu pedi zilizozinduliwa na kampuni hiyo kwa kushirikiana na Vodacom Foundation.Pedi hizo zinapatikana katika banda la kampuni hiyo kwenye maonesho ya Vodacom Elimu Expo yanayofanyika kwa siku tatu katika viwanja vya posta kijitonyama jijini Dar es salaam.
  Waandishi wa habari wakimfanyia mahojiano Meneja Matukio wa kampuni ya T- MARC Bi.Dorris Chalambo, maonesho ya Vodacom Elimu Expo yanayofanyika kwa siku tatu katika viwanja vya posta kijitonyama jijini Dar es salaam,kuhusu na matumizi sahihi ya pedi zilizozinduliwa hivi karibuni na kampuni hiyo kwa ushirikiano na Vodacom Foundation,Anaeshuhudia kulia ni Mkuu wa Idara ya kusadia jamii(Vodacom Foundation)Yessaya Mwakifulefule.Maonesho hayo yanafanyika katika viwanja vya posta.
  Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Green Acres Innocent Maro (kushoto)akiwaelezea wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Premier ya Bagamoyo, kuhusu mafunzo yanayopatikana shuleni kwao kwa gharamaa nafuu.,wanafunzi hao walifika katika maonesho ya Vodacom Elimu Expo yanayofanyika kwa siku tatu katika viwanja vya posta kijitonyama jijini Dar es salaam.

  0 0

  Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi Morrice Oyuko kutoka ofisi ya Taifa ya Takwimu akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu ukuaji halisi wa pato la taifa kwa robo ya kwanza ya mwaka (Januari – Machi 2013) ambapo uchumi umekuwa kwa kasi ya asilimia 7.5 ukilinganishwa na kasi ya asilimia 7.4 katika kipindi kama hicho kwa mwaka 2012. Ukuaji wa shughuli za uchumi za kilimo zimekuwa kwa asilimia 1.4 ambapo shughuli za uchimbaji madini na kokoto zimeshuka kwa asilimia 4.7 ukilinganisha kwa kasi ya ukuaji wa asilimia 23.8 kwa mwaka 2012.
  Baadhi ya wafanyakazi wa ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi Morrice Oyuko wakati akiongea nao kuhusu ukuaji halisi wa pato la taifa kwa robo ya kwanza ya mwaka (Januari – Machi 2013) ambapo uchumi umekuwa kwa kasi ya asilimia 7.5 ukilinganishwa na kasi ya asilimia 7.4 katika kipindi kama hicho kwa mwaka 2013. Mkutano huo wa waandishi wa habari umefanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa NBS uliopo jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi Morrice Oyuko (hayupo pichani) wakati akiongea nao kuhusu kukua kwa pato la taifa kwa robo ya kwanza ya mwaka (Januari – Machi 2013) ambapo uchumi umekuwa kwa kasi ya asilimia 7.5 ukilinganishwa na kasi ya asilimia 7.4 katika kipindi kama hicho kwa mwaka 2013.Ukuaji wa shughuli za uchumi za kilimo zimekuwa kwa asilimia 1.4 ambapo shughuli za uchimbaji madini na kokoto zimeshuka kwa asilimia 4.7 ukilinganisha kwa kasi ya ukuaji wa asilimia 23.8 kwa mwaka 2012.Picha na Anna Nkinda - Maelezo

  0 0


  0 0

  Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman akikabidhi zawadi kwa niaba ya Mahakama kwa Balozi wa Marekani aliyemaliza muda wake, Mhe. Alfonso Lenhardt pindi alipomkaribisha mapema jana ofisini kwake Mahakama ya Rufani Tanzania kwa ajili ya kumuaga rasmi na kumpongeza kwa kumaliza muda wake.


  0 0

  Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,  Dk. Makongoro Mahanga (kulia) akioneshwa mitambo ya kuzalisha majani ya chai katika Kiwanda cha Chai cha Luponde, wilayani Njombe, alipofanya ziara ya kutembelea viwanda na mashamba ya chai  pamoja na kuzungumza na wafanyakazi. Kushoto ni Meneja wa Uzalishaji wa kiwanda hicho, Antony Mwai.
  Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,  Dk. Makongoro Mahanga akionja aina jibini (cheese) zinazozalishwa na Kiwanda cha Maziwa  cha CEFA Njombe, wilayani Njombe, alipotembelea kiwanda hicho hivi karibuni.
   Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga (kushoto) akizungumza na Meneja Biashara wa Kiwanda cha Chai Luponde, Athanas Mwasamene alipotembelea hivi karibuni  shamba la majani ya chai-dawa (herbal tea) wilayani Njombe. Dk. Mahanga alifanya ziara wilayani humo ambapo alitembelea viwanda, mashamba ya chai pamoja na kuzungumza na wafanyakazi.
   Meneja Uzalishaji wa Kiwanda cha Chai Luponde, wilayani Njombe,  Anthony Mwai (mbele) akimwonesha Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga (katikati), shehena za chai-dawa (herbal tea) zinazozalishwa kiwandani hapo, tayari kusafirishwa kuuzwa nje ya nchi. Dk. Mahanga alifanya ziara wilayani humo ambapo alitembelea viwanda, mashamba ya chai pamoja na kuzungmza na wafanyakazi.

  0 0

   Mgeni Rasmi katika Mpambano wa Kimataifa wa kuwani Mkanda wa Ubingwa wa Dunia wa WBU,kati ya Mabondia Francis Cheka wa Tanzania na Phil Williams wa Marekani,Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh. Dkt. Fenella Mukangala (mwenye koti jeupe) akimvisha Mkanda wa Ubingwa huo,Bondia Francis Cheka baada ya kumshinda kwa Point Mpinzani wake,katika Mchezo uliomalizika usiku huu kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Bingwa wa Zamani wa Masumbwi,Fransous Bhotha.
   Bondia Francis Cheka wa Tanzania (kushoto) akimrushia makonde makali mpinzani wake,Phil Williams kutoka nchini Marekani wakati wa mpambano wao wa Kimataifa kuwania Mkanda wa Ubingwa wa Dunia wa WBU,uliofanyika usiku huu kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini Dar es Salaam.Bondia Francis Cheka ameibuka kidedea baada ya kumchapa mpinzani wake huyo kwa Point.
  Bondia Phil Williams kutoka nchini Marekani (kulia) nae alikuwa akijibu mashambulizi kwa mpinzani wake,Francis Cheka.hadi mwisho wa mchezo uliokuwa wa raundi 12,Francis Cheka aliweza kuibuka Kidedea kwa kumchapa mpinzani wake huyo kwa point na kufanikiwa kumnyang'anya mkanda wa Ubingwa wa Dunia wa WBU.
   Chukua hiyoooooo...
   Hapa lazima ukae,mie ndio kisiki cha mpingo:hivyo ndivyo Bondia Francis Cheka alivyoonekana kuifanya kazi yake vilivyo.
   Refa wa Mchezo huo akimzuia Bondia Francis Cheka baada ya kumkoleza makonde kisawasawa mpinzani wake,yaliyompelekea kwenda chini.
  Mpambano ukiendelea.
  Wanahabari wakipata taswira za mpambano huo.

  VIDEO YA MCHEZO INAKUJA.

older | 1 | .... | 241 | 242 | (Page 243) | 244 | 245 | .... | 3283 | newer