Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109605 articles
Browse latest View live

Mwanamuziki Saidi Kanda na Mvula-Mandondo Band kutingisha onyesho kubwa la International African Festival Tübingen, Germany 2018

0
0
Ni bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya The Mvula-Mandondo Band yenye makao yake nchini Uingereza,inayoongozwa na mwanamuziki mkongwe wa dansi Mtanzania Saidi Jumanne Kanda aliyewahi kutamba na bendi za Super Matimila, na Bima Lee. mkongwe huyo wa muziki anakiongoza kikosi chake cha Mvula-Mandondo Band katika jukwaa kubwa la maonyesho ya kimataifa ya GaiExpo trade fair yanayoambatana intern.Afrika FestivalTübingen  2018 nchini
Ujerumani ambalo mwaka  huu "Focus country Tanzania". bendi ya Mvula-Mandondo Band itapanda jukwaani kuanzia siku ya Ijumaa ya 10 Agosti 2018 hadi Jumamosi 11 Agosti 2018 Maonyesho hayo yanawashirikisha na wajasilimali ,wafanyi biashara,wasanii na wanamuziki na kuwakusanya umati watu zaidi ya laki moja katika viwanja vya Fest-latz,mjini Tübingen,kusini mwa ujerumani.bendi ya Mvula-Mando inatarajia kutumbuiza katika onyesho lingine kubwa nchini ufaransa mwezi Septemba.usikose kujumuika na waadaau wengine katika maonyesho haya makubwa ambapo wasanii na wajasilia mali toka Tanzania wakiwakilisha na kupeperusha bendera ya "Hapa Kazi Tu"


Mzimu wa Muziki Dansi kuwabangua vichwa tena Ulaya kuanzia tarehe 9-08-2018 hadi 12 -08-2018 mjini Tubingen

0
0
Ni katika viwanja vya Feste-Platz,wakati onyesho hilo la kimataifa la GaiExpo 2018 na International Afrika Festival Tubingen 2018 mwaka huu,  nchi lengwa ikiwa ni Tanzania.
Baadhi ya bendi za muziki na wasanii wa Tanzania wameshawasili nchi Ujerumani wakiwa tayari tayari kutumbuiza katika maonyesho hayo makubwa barani ulaya.
Kundi maarufu ya Ngoma Africa band aka FFU-Ughaibuni maarufu pia kwa majina kama vile "Viumbe wa ajabu Anunnki aliens" au "Watoto wa Mbwa" na mzimu wao "Bongo Dansi" kutoka special planet Bongo Land Tanzania watatingisha jukwaa siku ya jumamosi 11Agosti 2018.
Bendi hiyo iliyoanzishwa 1993 na kiongozi wake Ebrahim Makunja alimaarufu kama Kamanda Ras Makunja mkuu huyo wa viumbe wa ajabu wa Ngoma Africa band  muziki wao umewanasa washabiki wa kimataifa kwa takribani zaidi ya miaka 25 na kujizolea sifa za kimataifa majukwaani.
Miaka miwili hiliyopita waliwadatisha washabiki nchini Israeli kwenye uwanja wa  Yitzhak Rabin Square,mjini Tel Aviv. Hivi sasa wanatamba na CD yao mpya "Awamu ya Tano Uwanjani" ambayo unaweza kuisikiliza hapa www.ngoma-africa.com

MANZESE UNITED MABINGWA WAPYA NDONDO CUP 2018

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
MICHUANO ya Ndondo Cup yamefikia tamati leo baada Timu ya Manzese United kuibuka mabingwa wapya wa Ndondo Cup 2018 baada ya kuifunga timu ya Kivule kwa goli 1-0 mechi iliyofanyika leo Jijino Dar es Salaam.

Mchezo huo ulioanza majira ya 10 alasiri katika uwanja wa Bandari ulichezeshwa na Mwamuzi mwenye beji ya FIFA Hery Sasii akisaidiwa na Mwamuzi wa pembeni Soud Lila na Hellen Mduma.Mchezo huo ulianza kwa kasi katika dakika ya 9 Manzese United wanapata goli la kwanza kupitia kwa mchezaji wake Hamza lililodumu mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika.

Umakini wa safu ya ushambuliaji ya Kiluvya United iliwanyima fursa ya kusawazisha goli hilo ambapo waliweza kukosa nafasi nyingi za wazi.Kipindi cha pili kilianza Kiluvya wakisaka goli la kusawazisha ambapo mpaka dakika 90 zinamalizika Manzese walifanikiwa kushinda goli 1-0 na kuwa mabingwa wapya wa Ndondo Cup.

Mgeni rasmi wa mashindano Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shoza aliweza kukabidhi kombe kwa mabingwa wapya wa Ndondo Cup akiwa ameambataba na viongozi mbalimbali Nchini.

Fainali hiyo ya kipekee ilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, Mbunge wa Iramba Mashariki Mwingulu Nchemba aliyekabidhi hundi ya Milioni 10 kwa mabingwa, Mbunge wa Temeke Abdallah Mtolea, Mkuu wa Wilaya Temeke Felox Lyaniva, Mbunge wa Ilala Mussa Azan Zungu, Rais wa TFF Wallace Karia na Mwenyekiti wa DRFA Almas Kasongo.

Mbali na hao pia Manzese waliwakilishwa na Meya wa Jimbo la Ubungo Boniface Jacob na wasanii wanaoishi kwenyr jimbo hilo Akiwemo Msanii Madee na Shilole sambamba na viongozi wengine wa kimpira.

 Mbunge wa Iramba Mashariki Mwigulu Nchemba akikabidhi  mfano wa hundi yenye thamani ya Milioni 10 kwa Nahodha wa timu ya Manzese baada ya kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Kivule United

 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza akikabidhi kombe kwa Nahodha wa Manzese United baada ya kuibuka na ushindi wa Goli 1-0 dhidi ya Kivule United katika Mchezo uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. 

Mchezaji wa Manzese United Idd Nado akiwa amemlaza chini mchezaji wa Kivule United katika fainali ya Ndondo Cup iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam na Manzese United kufanikiwa kushinda kwa goli 1-0.
 Kikosi cha Kiluvya United wakiwa katika picha ya Pamoja
Kikosi cha Manzese United wakiwa katika picha ya pamoja

Lion Bhavin Sonigra ndiye Mwenyekiti mpya wa Klabu ya Lions ya Dar es salaam Mzizima kwa mwaka 2018/2019

0
0
Mwenyekiti wa Klabu ya Lions ya Dar es Salaam Mzizima aliyemaliza muda wake Lion Saifuddin Nagri Akimwisha cheni kwa Mwenyekiti mpya wa Klabu hiyo Lion Bhavin Sonigra kwa mwaka 2018/2019 katika hafla ilitofanyika ijumaa katika hoteli ya Best Western CBD jijini Dar es Salaam.

SERIKALI YAFANYA UTEUZI WA BAADHI YA MAKATIBU TAWALA WA WILAYA

0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapteni (Mst) George H. Mkuchika akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uteuzi wa baadhi ya Makatibu Tawala wa Wilaya katika Ukumbi wa mikutano wa Utumishi jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumidhi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika akisikiliza swali la mwaandishi wa habari (hayupo pichani) katika Ukumbi
wa Utumishi jijini Dar es Salaam mara baada ya kutangaza majina ya baadhi ya Makatibu Tawala wa Wilaya walioteuliwa na Serikali. Kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumidhi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro



WAZIRI MKUU AMJULIA HALI WAZIRI DKT. KIGWANGALA NA MSANII MAJUTO

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemtembelea na kumpa pole Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) akipatiwa matibabu baada ya kupata ajali.
Akiwa hospitalini hapo Jumapili, Agosti 5, 2018, Waziri Mkuu akiwa ameambatana na mkewe Mama Mary Majaliwa amesema amefarijika baada ya kumkuta Dkt. Kigwangalla na wagonjwa wengine waliolazwa katika hospitali hiyo wakihudumiwa vizuri.
“Hospitali ya Muhimbili ndio kimbilio letu kwa sasa na tunawashukuru madaktari na wauguzi kwa kazi nzuri mnayoifanya ambayo inaliletea heshima Taifa letu kwani hata watu wa Comoro wanakuja kutibiwa Muhimbili,” amesema.
Kwa upande wake Dkt. Kigwangalla amesema anamshukuru Mwenyezi Mungu kwa sababu ajali ilikuwa mbaya sana. 
“Ajali ilikuwa mbaya sana. Hivi sasa naongea hapa namshukuru Mungu, Serikali pamoja na madaktari na wauguzi kwa jitihada kubwa walizozifanya,”.
Dkt. Kigwangalla alipata ajali jana asubuhi (Jumamosi, Agosti 4, 2018) katikati ya vijiji vya Mdolii na Minjingu wilaya ya Babati mkoani Manyara baada ya gari lake kupinduka na kusababisha kifo cha Afisa Habari wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Hamza Temba na wengine watano akiwemo Dkt. Kigwangalla kujeruhiwa.
Pia Waziri Mkuu amjulia hali msanii maarufu wa maigizo nchini, Bw. Amri Athumani maarufu King Majuto ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akipatiwa matibabu. Amesema amefarijika kumkuta akiwa anaendelea vizuri.
Naye Mzee Majuto amesema anaishukuru Serikali kwa sababu inamuhudumia vizuri. “Mheshimiwa nakushukuru sana na naishukuru Serikali kwani hata sijui ingekuwaje kama si msaada wa Serikali. Hii ni bahati kubwa”.
Pia Waziri Mkuu amemjulia hali Bibi Hellena Baruti ambaye ni mama mzazi wa Mthamini Mkuu wa Serikali Bibi Evelyne Mugasha aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) akipatiwa matibabu.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, AGOSTI 5, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na Mkewe Mary wakimpa pole Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamisi Kigwangalla, ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, jijini Dar es salaam Agosti 5, 2018, akipewa matibabu baada ya kupata ajali.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamisi Kigwangalla, ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, jijini Dar es salaam akipatiwa matibabu baada ya kupata ajali Agosti 5, 2018,
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na Mkewe Mary wakimpa pole Msanii Amri Athumani (Mzee Majuto), ambaye amelazwa katika hospitali ya Muhimbili, jijini Dar es salaam Agosti 4, 2018, kushoto ni Mke wa Meze Majuto, Aisha Mbwa
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimjulia hali mama wa Mthamini Mkuu wa Serikali, Evelyne Mugasha wa kwanza kulia, ambaye amelazwa katika Taasisi ya Jakaya Kikwete, Muhimbili jijini Dar es salaam Agosti 4, 2018, kutoka kushoto ni Dk. Tulizo Sanga, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda,  

KESI INAYOMKABILI ALIYEKUWA MHASIBU WA TAKUKURU KUSIKILIZWA AGOSTI 13, 2018

0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imepanga Agosti 13, 2018 kuendelea kusikiliza kesi inayomkabili  aliyekuwa mhasibu wa Takukuru, Godfrey Gugai anayekabiliwa na  tuhuma ya utakatishaji na kumiliki mali isiyolingana na kipato chake inayomka bili yeye na wenzake watatu.

Kesi hiyo leo Agosti 6, 2018  ilikuja kwa ajili ya shahidi Ayoub Akida wa upande wa mashtaka kuendelea kutoa ushahidi wake ambao alisimama kuutoa kutokana na kubishania kielelezo cha barua ya kufutwa kazini kwa Gugai.

Hata hivyo, wakili wa serikali kutoka Takukuru, Vitalis Peter ameeleza mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa shahidi huyo amepata udhuru.

Aidha imedaiwa wakili wa utetezi Alex Mgongolwa amefiwa na mdogo wake, Na hivyo mahakama kulazimika kuiahirisha kesi hiyo hadi Agosti 13.

Mbali na Gugai, washtakiwa wengine, ni George Makaranga, Leonard Aloys na Yasin Katera.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na makosa 43, kati ya hayo 19 ni ya kughushi, 23 ni utakatishaji fedha na moja ni kumiliki mali zilizozidi kipato halali.

Gugai anakabiliwa na kosa la kumiliki mali kinyume na kipato chake, ambapo alitenda kosa hilo kati ya January 2005 na Decemba 2015.

Inadaiwa akiwa jijini Dar es Salaam kama mwajiriwa wa TAKUKURU alikuwa akimiliki mali za zaidi ya Sh 3.6 bilioni ambazo hazilingani na kipato chake cha awali na cha sasa cha zaidi ya  Tsh.milioni 800,huku akishindwa kuzitolea maelezo.

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WA NCHI MBALIMBALI IKULU, DAR ES SALAAM

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na balozi wa Canada  nchini aliyemaliza muda wake Mhe. Ian Myles walipokutana Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na balozi wa Ubelgiji nchini aliyemaliza muda wake Mhe.  Paul Cartier walipokutana Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na Balozi wa China Mhe. Wang Ke walipokutana kwa mazungumzo  Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono na Balozi wa Burundi nchini Mhe. Gervais Abayeho aliyemsindikiza Mjumbe maalumu wa Rais wa Burundi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Ezechiel Nibigira  Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono na mjumbe maalumu wa Rais wa Burundi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Ezechiel Nibigira  Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2018. Picha na IKULU

Dkt Kalemani azungumza na watumishi wa TANESCO, awapongeza kwa Kuchapa Kazi

0
0
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza Dodoma katika kikao kazi alichofanya na watumishi wa shirika hilo wakiwemo wajumbe wa Bodi ya Tanesco, viongozi wa menejimenti ya TANESCO, Bodi ya EWURA na watendaji wa REA. Kushoto ni Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgallu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme nchini Dkt Titto Mwinuka (Kulia) akifuatilia kwa Makini Mkutano wa Kikao Kazi Ulioitishwa Mjini Dodoma na Waziri wa Nishati Dkt Kalemani na Kuhudhuriwa na watumishi wa shirika hilo wakiwemo wajumbe wa Bodi ya Tanesco, viongozi wa menejimenti ya TANESCO, Bodi ya EWURA na watendaji wa REA.
Wajumbe wa Bodi ya Tanesco, Viongozi wa Menejimenti ya Tanesco, Bodi ya EWURA na Watendaji wa REA Wakiwa Kwenye Kikao Kazi Kilichoitishwa na Waziri wa Nishati Dkt MEDARD KALEMANI Mjini Dodoma.

Airtel yawezesha uchunguzi wa afya na matibabu BURE kwa wadau na wafanyakazi wao

0
0
Wakwanza kulia ni Mtoa huduma wa kutuo cha tiba ya Kinywa na Meno cha Elite Dental Clinic Bi Baby Luck akiwa na Muuguzi wa Kituo hicho Bi Rosemary Kwilasa wakitoa ushauri wa tiba ya meno kwa wafanyakazi wa Airtel kutoka vitengo mbalimbali pamoja na wadau wao. Airtel imefanya Gulio maalum la kuwakutanisha wadau na watoa huduma mbalimbali pamoja na wafanyakazi wake kupata huduma hizo BURE. Gulio hilo Gulio lililofanyika makao makuu ya Airtel.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imeungana na wadau wengine kutoa tiba na uchunguzi wa afya ya kinywa na meno bure ikiwa ni juhudi zake za kutambua umuhimu wa Afya ya Kinywa na Macho. Uchunguzi huo  imefanyika  kwenye makao makuu ya Airtel  na kuwafaidisha wafanyakazi kutoka vitengo mbali mbali pamoja na wadau wengine waliofika kwenye ofisi za kampuni hiyo.

Akiongea wakati wa tukio hilo Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu Airtel Bi Stella Kibacha alisema “Airtel Tanzania tunatambua watu walio kwenye ajira mbalimbali hubanwa sana na kazi na wakati mwingine kukosa muda wa kuchunguza mwenendo wa Afya zao, hii ndio imetufanya Airtel kuwaleta wadau wetu hapa ili wafanyakazi wetu pamoja na  wadau wanaotembelea jengo la Airtel kupata huduma hizi”

Kibacha aliendelea kueleza kuwa kuwa “wote tunatambua Wizara ya Afya kupitia waziri Ummy Mwalimu imekuwa mstari wa mbele kusisitiza sana swala la kulinda Afya zetu, sisi Airtel tumeona umuhimu wake pia ndio maana watoa huduma wa Afya ya kinywa Elite  wapo, Macho wapo wadau wetu International Eye Hospital na Mazoezi tumewaita Club9 Wellness Servicess kuja hapa na  wataalam wao ili kutoa ushauri wao kwa jamii hapa ofisini kwetu kwa siku nzima wafanyakazi na wadau wakaribu wapate muda wa kufanyiwa uchunguzi wa awali na kupanga muda  wao kwenda baadae kwenye vituo vya huduma hizi na kujipatia huduma kwa ufasaha zaidi”

kwa upande wake Dokta Latha Sujit wa Elite Dental Clinic alitoa wito kwa watanzania wote kuona umuhimu na kuwa na utaratibu wa kutembelea vituo vya afya na kufanya uchunguzi wa kinywa mara kwa mara.

“Sisi Elite Dental Clinic tunatoa huduma ya kuchunguza na kutibu meno, lakini wito wangu  kama daktari kwa watanzania kuhusu Afya ya Kinga ya meno msisubirie mpaka usikie maumivu au tatizo litokee, nashauri familia na jamii kwa ujumla tuwe tunatenga muda na utaratibu wakwenda kwenye vituo vya Afya popote pale kwa uchunguzi na ushauri ni muhimu sana kwa Afya zetu” alieleza Dr Latha

Gulio la Airtel mbali na kuwepo na tiba hiyo ya Kinywa  toka kwa Elite Dental Clinic na huduma za uchunguzi wa macho toka kwa International Eye Centre pia lilihudhuriwa na watoa huduma nyingine za  kijamii wakiwemo Seifi Group wanaotoa huduma za vifaa vya elimu, 1st House (kwa huduma za mikopo ya nyumba), Superdoll (kwa huduma za matairi pamoja vipuli vya vifaa vya moto), Club9 (huduma ya mazoezi na mazoezi tiba) GT Bank, pamoja na  Asas Milk.
Dokta Latha Sujit (kushoto) wa Elite Dental Clinic akiwa na Muuguzi wa Kituo hicho wakitoa ushauri wa tiba ya meno kwa mfanyakazi wa Airtel Bw James Moilo kutoka vitengo mauzo wakati Airtel ilipofanya Gulio maalum la kuwakutanisha wadau na watoa huduma mbalimbali pamoja na wafanyakazi wake kupata huduma mbalimbali BURE. Gulio hilo lililofanyika makao makuu ya Airtel.
Meneja Mauzo na Masoko wa Seifi Group Bi Zarina Riyas (mwenye baibui) akiwa na watoa huduma wengine wa kampuni hiyo wakitoa huduma kwa mfanyakazi wa Airtel wakati Airtel wa ilipofanya Gulio maalum la kuwakutanisha watoa huduma mbalimbali pamoja na wafanyakazi wake kupata huduma hizo BURE. Gulio hilo lililofanyika makao makuu ya Airtel.
Dokta Latha Sujit (kushoto) wa Elite Dental Clinic akiwa na Muuguzi wa Kituo hicho wakitoa ushauri na tiba ya meno kwa mdau wa habari mtandaoni wa Michuzi media Group Bw Ahmadi Michuzi wakati Airtel ilipofanya Gulio maalum la wadau na wafanyakazi wake kukutana na watoa huduma mbalimbali nakupata huduma mbalimbali BURE. Gulio hilo lilifanyika makao makuu ya Airtel.
Meneja Masoko wa Club9 inayojiusisha na huduma ya Mazoezi tiba Bi Janeth John akiwa na watoa huduma wengine wa kampuni hiyo wakitoa huduma kwa mmoja ya mdau wa Airtel kwenye Gulio maalum la watoa huduma mbalimbali BURE. Gulio hilo lilifanyika makao makuu ya Airtel.

JK ataka teknolojia mpya ya kilimo, Ufugaji iwafikie Wananchi

0
0
Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia sehemu ya bidhaa zilizokuwepo kwenye moja ya mabanda ya maonesho ya Wakulima, wafugaji na wavuvi kwenye maonesho ya nanenane kanda ya Mashariki yanayoendelea katika uwanja wa Mwl. J. K. Nyerere mjini Morogoro.

Na. Andrew Chimesela – Morogoro.

Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ametaka teknolojia mpya ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi inayooneshwa kipindi cha Maonesho ya maadhimisho ya Wakulima na Wafugaji maarufu kama Nanenane iwafikie wananchi ili kuwakwamua katika dimbwi la Umasikini.

Dkt. Jakaya Kikwete ametoa kauli hiyo Agosti 5 mwaka huu baada ya kutembelea vipando na mabanda ya maonesho ya Wakulima, wafugaji na wavuvi kwenye maonesho ya nanenane kanda ya Mashariki yanayoendelea katika uwanja wa Mwl. J. K. Nyerere mjini Morogoro.

Dkt. Kikwete amesema pamoja na wataalamu wa Sekta ya Kilimo, ufugaji na uvuvi kujitahidi kuvumbua teknolojia mpya katika Sekta hiyo bado teknolojia hiyo haiwafikii wananchi wa Vijijini hivyo amewataka pamoja na kuongeza jitihada za kuvumbua muhimu elimu hiyo waipeleke kwa wananchi ili kuondoa umaskini miongoni mwao.
“kazi kubwa imefanyika ya utafiti, viwango vimeongezeka sana vya Ubora, suala kubwa ni namnagani uvumbuzi unaofanywa na maabara kwenye vituo vyetu namna ya kuwafikia wakulima” alisema Dkt. Kikwete.

Aidha, Rais huyo mstaafu wa awamu ya Nne amesema ili kuondokana na umaskini kwa haraka wataalamu lwanatakiwa kutoa elimu kwa wakulima na wafugaji namna ya kulima na kufuga kibiashara na kuondokana dhana ya kufanya kazi hizo kwa ajili ya kujikimu peke yake.

Maonesho hayo ya 25 ya nanenane kanda ya Mashariki yanayofanyika katika Uwanja wa Mwl. J. K. Nyerere katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro yanajumuisha Mikoa minne ya Pwani, Tanga, Dar es Salaam na wenyeji Morogoro.

ARUSHA YAANZA KUONYESHA NJIA MADEREVA WASIOKUWA NA VYETI

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo akiongea na Wahitimu wa mafunzo ya udereva wa magari ya abiria wakati wa Mahafali ya kuhitimisha mafunzo yao yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Chuo cha Ufundi Arusha.

Na Woinde Shizza, Arusha

Jeshi la Polisi mkoani hapa kwa kushirikiana na Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) kanda ya Kaskazini wamefanikiwa kutoa mafunzo kwa madereva 350 wa magari ya abiria ambao awali walikuwa na Leseni pekee bila vyeti. Mafunzo hayo yaliyofungwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo katika Chuo Cha Ufundi Arusha, awali yalifunguliwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng’anzi wiki mbili zilizopita.

Akizungumza katika siku hiyo ya Mahafali, Mkuu huyo wa mkoa, kwanza kabisa alilipongeza Jeshi la Polisi na Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) kwa kuamua kuendesha mafunzo hayo lakini pia kwa wahitimu wenyewe kwani ni jambo zuri na lenye maslahi kwenye maisha yao. Alisema jitihada hizo zinalenga kupambana na ajali kwani madhara yake ni makubwa ikiwa ni pamoja na kusababisha vifo, ulemavu, kupata hasara kwenye mali lakini pia zinaweza kusababisha kutotoa fursa za ajira kwa madereva wenye matukio ya kusababisha ajali.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha (SACP) Ramadhani Ng'anzi akitoa shukrani zake kwa Chuo cha Ufundi Stadi ( VETA) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi mkoani hapa katika kuendesha mafunzo ya muda mfupi kwa Madereva ambao hawana vyeti.

Mkuu huyo wa mkoa alisema pamoja na mafunzo waliyoyapata wahitimu hao lakini watatakiwa waepuke unywaji wa pombe wakati wanaendesha vyombo vya moto kwani ajali nyingi zinasababishwa na ulevi, huku akilitaka Jeshi la Polisi kupitia kitengo cha usalama Barabarani kuongeza jitihada katika kupima ulevi kwa madereva.

“Pamoja na Mafunzo mliyoyapata kuwajengea uwezo lakini kama hamtaepuka unywaji wa pombe wakati mnaendesha vyombo vya moto ajali zitaendelea kutokea”. Alionya Bw. Gambo

Aliwataka Madereva hao kuwa na nyaraka zote na vifaa vyote muhimu kama Vizima Moto pindi wanapokuwa kazini na kusema ukamilifu wa vitu hivyo vitasaidia kuepusha mabishano na askari wa Usalama barabarani.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng’anzi alisema anaamini mafunzo hayo yamewajengea uwezo na kuwapa umahiri wa kuendesha magari ya abiria. Alisema mafunzo hayo yatasaidia mkoa wa Arusha kuwa ni miongoni mwa mikoa salama kwa kuepuka ajali mbaya na kuahidi kuendeleza na kuzidi kuimarisha ushikiano kati ya Jeshi hilo na Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) ili mwisho wa siku Madereva wote wapate mafunzo hayo.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Arusha Mrakibu wa Polisi (SP) Joseph Charles Bukombe akiwataka Wahitimu hao wakawe mabalozi wa madereva wengine ambao hawajapata mafunzo kama hayo ili nao wajitokeze siku za usoni.

Naye Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Arusha Mrakibu wa Polisi (SP) Joseph Charles Bukombe alisema kwamba, wahitimu hao watakuwa Mabalozi wa wenzao na kuonya kwamba wale wote ambao wanatengeneza na wanaonunua vyeti vya VETA bila kupata mafunzo watakamatwa na kufunguliwa Mashtaka.

Awali akimkaribisha Mgeni rasmi, Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Kaskazini Bw. Anjelus Ngonyani alisema kwamba ajali nyingi zinasababishwa na makosa ya kibinadamu ambayo yanatokana na kukosa mafunzo. Alisema Chuo hicho kinatoa mafunzo bora na yanayokidhi viwango na kuwataka madereva wazidi kujitokeza.
Baadhi ya wahitimu waliopata mafunzo ya uendeshaji wa magari ya kubeba abiria ambayo yaliendeshwa na Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) kwa muda wa wiki mbili wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo wakati wa Mahafali hayo yaliyofanyika katika Chuo cha Ufundi Arusha.

NEWS ALERT: MWANAHABARI MKONGWE ERNEST SUNGURA ATEULIWA KUWA KIONGOZI MKUU VYOMBO VYA HABARI VYA CCM

0
0

*Kuongoza mageuzi makubwa ya vyombo hivyo
*Ni baada ya kufanya maboresho makubwa katika tasnia ya habari nchini


Na Derek Murusuri, Dar Es Salaam


USEMI maarufu katika vitabu vifakatifu kuhusu jiwe lililokataliwa na waashi kuwa jiwe kuu la pembeni, unasadifu uteuzi wa gwiji la habari nchini, Ernest Samson Sungura, kuongoza mageuzi makubwa ya vyombo vya habari vya CCM.

Habari zilizopatikana kutoka ndani ya vyombo vya habari vya CCM zinasema kuwa uteuzi wa Comrade Sungura umetangazwa leo jijini Dar Es Salaam na Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ali, ambaye alisema uteuzi huo umeidhinishwa na Kamati Kuu ya CCM.

Comrade Sungura sasa anakuwa Kiongozi Mkuu wa vyombo vya habari vya CCM, aliyepewa jukumu kubwa la kufanya mageuzi ya kimuundo na kimfumo (restructuring) ya vyombo hivyo na kuvifanya vitoe ushindani madhubuti (competitive) katika tasnia ya habari ndani na nje ya nchi.

Kabla ya uteuzi huo, Sungura alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wakfu wa vyombo vya habari Tanzania (TMF) lakini aliondolewa katika taasisi hiyo na Bodi yake (TMF) muda mfupi baada ya kutangazwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC). 

Sungura ndiye mwasisi wa Tanzania Media Foundation (TMF), taasisi iliyoleta mageuzi makubwa katika tasnia ya habari nchini na kuifanya nchi jirani ya Kenya kuja kujifunza nchini kabla ya kuanzisha taasisi kama hiyo nchini mwao.
Comrade Sungura ndiye anatarajiwa kuviongoza vyombo vya habari vya CCM katika mageuzi haya makubwa. Vyombo hivyo ni pamoja na televisheni, redio, magazeti na vile vya mtandaoni ambavyo katika siku za karibuni vimetokea kuwa na wafuasi wengi duniani.
Pamoja na mafanikio mengine, Sungura amekuwa na rekodi nzuri na ya kipekee katika kuleta mageuzi ya kimkakati kwa taasisi za habari nchini.
Kusoma zaidi BOFYA HAPA

Kesi ya kina Mbowe yazidi kupigwa danadana.

0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuonya mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko kwa kushindwa kuwasiliana na mdhamini wake na kutoa sababu za msingi mahakamani.

Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ametoa onyo hilo leo Agosti 6,2018 wakati kesi ya kufanya maandamano yasiyo halali inayowakabili viongozi 9 wa Chadema akiwemo Mwenyekiti wao Freeman Mbowe ilipokuja kwa ajili ya washtakiwa hao kusomewa maelezi ya awali.

Kabla ya kutolewa onyo hilo, wakili wa serikali Mkuu, Faraja Nchimbi ameeleza kuwa shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya washtakiwa kusomewa PH lakini mawakili wa utetezi hawakufika mahakamani.Wakikli Hekima Masipo alidai mahakamani hapo kuwa Wakili wa washtakiwa Peter Kibatala yupo Mahakama kuu huku Jeremiah Mtobesya akiwa katika kesi nyingine Mtwara.

Hata hivyo, mahakama ilimtaka mshtakiwa wa 5, Esther Matiko ambaye hakufika mahakamani hapo tarehe iliyopita na shahidi wake akaeleza kuwa alipatwa n dharura, basi aelezee hiyo dharula yake.Matiko amedai kuwa alipigiwa simu ya dharura kwenda shuleni anaposoma mwanaye Agosti 1, 2018 na akaondoka saa 4 usiku. Ambapo baada ya kufika shule aliambiwa mtoto wake ni mgonjwa na alipompeleka hospital alikutwa na Tetekuwanga na akaambiwa apumzike kwa siku 4.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Mashauri alimuhoji Matiko kuwa mbona mdhamini wake alishindwa kuieleza mahakama kwamba amekwenda Kenya kufanya nini."Nakupa warning mara nyingine uwe muwazi, hii iwe mara ya mwisho, siku nyingine unapaswa kumueleza mdhamini wako ni dharura gani imekupata," Hakimu Mashauri.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 13.2018 kwa ajili ya washtakiwa kuja kusomewa PH.KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

Baadhi ya viongozi wa CHADEMA wakiwa kwenye moja ya chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo kusikiliza kesi  yao


ZIJUE KANUNI ZA BASATA 2018.

0
0
Na Agness Francis,Blogu ya Jamii.

BARAZA la sanaa la taifa limetoa ufafanuzi wa kanuni za baraza hilo zitakazokuwa zinatumika kuendeshea kazi za sana hapa nchini.

Kanuni hizo zilizoanza utekelezaji wake mwaka huu katika kusimamia shughuzi zote zinazohusiana na sanaa.Akifafanua kanuni hizo Afisa Sana Basata Augustino Makame leo katika ofisi zao Jijini Dar ea Salaam amesema kuwa badhi ya sehemu za kanuni hizo zimebainishwa.

Ambazo ni muundo wa baraza,usajili na vibali vya kazi,uwasilishwaji wa taarifa kwa msajili,kufutwa kwa usajili,masharti ya jumla kwa wadau wa kazi za sanaa,masharti ya jumla ya kazi za sanaa,makosa na adhabu,uzingatiaji wa sheria katika kazi za sanaa.

Afisa huyo amesema baraza ndilo litakalokuwa msajili mkuu na mtoa vibali vyote vya kufanya kazi zsanaa kwa wasajili."Msajili atato kibali na kitambulisho cha kufanya kazi za sanaa kwa mtu au kampuni iliyosajiliwa kwa mujibu wa kanuni hizo,amesema makame"

Aidha Makame amesema mtu yoyote hatoruhusiwa kufanya kazi za sanaa bila kusajiliwa na baraza au upelekwa sokoni ama kwa walaji kabla ya kupewa kibali cha kuthibitishwa kuwa na maudhui na madili kuzingatiwa,ambapo kibali kitalipwa kila mwaka kwa mujibu wa ada zitazolipwa katika halmashauri husika. Vile vile amesema shughuli zote zinazohusiana na sana zitafanyika kwa kuzingatia sheria zote za jamuhuri ya muungano wa Tanzania na kanuni zake.

Makame amemalizia kwa kusema kuwa endapo kazi ya msajili yeyote itakiuka masharti ya kanuni hizo msajili huyo atachukuliwa hatua na baraza kwa mujibu wa kanuni 64 (1) au (2),itakuwa ni kosa la jianai na kwa mtandao wowote ama chombo chochote cha habari kurusha kazi hiyo kwa namna yoyote ile.

WIZARA YA AFYA ITAENDELEA KUKARABATI NA KUPANUA VYUO VYA MAFUNZO YA AFYA NCHINI-WAZIRI UMMY

0
0
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema wizara yake itaendelea kukarabati na kupanua vyuo vya mafunzo ya afya kada ya kati nchini ili kuweza kuongeza udahili kwa wanafunzi wanaofaulu kwenye masomo ya sekondari wenye vigezo vya kuingia kwenye vyuo hivyo. 

Aliyasemma hayo leo wakati halfa ya uzinduzi na makabidhiano ya Majengo ya chuo cha Uuguzi Tanga yaliyojengwa kupitia ufadhili wa mfuko wa Dunia wa Kupambana na Ukimwi Kifua Kikuu na Malaria (Global Fund) alisema kwani ukarabati huo utasaidia kuongeza idadi kubwa ya wanafunzi watakaokuwa wakipata fursa ya kusoma kwenye vyuo hivyo. 

Alisema kutokana na ukarabati huo kwenye chuo cha Uuguzi mkoani Tanga idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa kwenye chuo hicho imeongezeka kutoka wanafunzi kutoka 190 hadi 260 ambao wameweza kupata fursa mafunzo kwenye chuo hicho ambao watasaidia kwenye kada hiyo muhimu kwa ustawi wa maendeleo. 

“Kutokana na ukarabati wa majengo haya nimeambiwa na Mkuu wa Chuo kwamba udahili wa wanafunzi kutoka 190 hadi 260 wameweza kutoa fursa kwa vijana wao kuweza kupata nafasi ya kupata mafunzo ya afya kada ya kati huwa naambiwa kwamba na dkt Guwele ambaye ni mkuu wa idara ya mafunzo na afya kada ya kati anasema wanafunzi wengi wanafaulu lakini hawapati mahali pa kuwapeleka sababu kubwa zikiwa ni miundombinu na uchakavu wa majengo na inaumiza vijana wamefaulu vizuri sana lakini hakuna nafasi“Alisema. 

“Lakini tunawashukuru Global Fund kwa ujenzi wa majengo hayo yameweza kusaidia kuongeza udahili hivyo niagize msije mkaacha wanafunzi kwa kusema hakuna nafasi..Wanafunzi waliofaulu kwenye masomo ya sekondari wenye vigezo vya kuingia kwenye vyuo vya mafunzo wachukuliwe wote wasiachwe majumbani “Alisema. 
 WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee wa Watoto Ummy Mwalimu katika akitata utepe kuashiria uzinduzi na makabidhiano ya majengo ya chuo cha Uuguzi Tanga yaliyojengwa kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa Kupambana na Ukimwi Kifua Kikuu na Malaria (Global Fund) kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella na Mkuu wa Chuo hicho Leah Makala
 WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee wa Watoto Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa uzinduzi na makabidhiano ya majengo ya chuo cha Uuguzi Tanga yaliyojengwa kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa Kupambana na Ukimwi Kifua Kikuu na Malaria (Global Fund) 
 Katikati ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiangalia namna wanafunzi wanavyojifunza kwa vitendo kumfanyia mazoezi mtoto ambaye amezaliwa akiwa hapumui vizuri 
Sehemu ya wananchi waliojitokeza kwenye uzinduzi huo



MITIBIASHARA KUWAPA FURSA MPYA WAWEKEZAJI WA MISITU TANZANIA.

0
0
Na.khadija seif ,Globu ya jamii.

Katika kuunga mkono juhudi za Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania John pombe Magufuli kukuza sekta ya viwanda Taasisi ya ki_uanachama ya African Forestry (AF) ikishirikiana na Taasisi ya Uendelezaji Misitu Tanzania (FDT) ya Mkoani Iringa wameanzisha jukwaa la kuwasaidia wawekezaji wa sekta ya kilimo cha miti nchini Tanzania,na kuwapatia taarifa na elimu ya kilimo cha miti kwa njia ya mtandao ili kuongeza chachu ya uwekezaji katika sekta ya misitu.

Aidha akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya ki_uanachama ya African Forestry (AF) Francis Rwebegora amesema Misitu hiyo ina manufaa kwa jamii kwani misitu inafaida kwani baadhi ya mazao ya misitu ni pamoja na mbao zinazotumika katika sekta ya ujenzi ,viwanda vya kutengeneza samani,magogo yanayotumika katika viwanda vya karatasi ,nguzo za umeme na simu .

Rwebegora amefafanua zaidi faida nyingine za misitu ni pamoja na udhibiti wa ongezeko la joto kwani miti hutumia hewa_ukaa,kusanisi chakula chake, utunzaji wa vyanzo vya maji ,na faida nyingine nyingi za ki_ikolojia.

Mratibu wa biashara na masoko Taasisi ya Uendelezaji misitu nchini(FDT) Emmanuel sangalah amesema wakulima watapata mafunzo stahiki kuhusu kilimo cha miti kuanzia kuandaa shamba ,upatikanaji wa mbegu bora, utunzaji wa shamba,masoko,bei na ushauri wa kitaalam kea kuongeza pato la Taifa.

Ameeleza hatua jinsi ya kujiunga na huduma hiyo kupitia simu ya kiganjani nakutembelea tovuti ya www.mitibiashara na hakuna malipo yoyote ya kujiunga na jukwaa hilo na kutoa wito kwa wakulima kujiunga ili waweze kunufaika na mazao bora.
Mkurugenzi wa Taasisi ya African Forestry (AF) Francis Rwebegora akizungumzaa na wanahabari jijini Dar es salaam leo katika ufunguzi wa   huduma ya Mitibiashara kimtandao kwa ajili ya wakulima kupata elimu jinsi ya kuandaa mashamba yao.

TAARIFA KWA MADAKTARI NCHINI

0
0

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inapenda kuwajulisha watanzania kuwa kwa kushirikiana na wataalam kutoka nchini Marekani (Madaktari Afrika) “electro physiologist” (EP) tunatarajia kufanya kambi maalum ya magonjwa ya moyo yatokanayo na mfumo wa umeme wa moyo usiofanya kazi sawasawa. Matibabu yatakayotolewa katika kambi hiyo inatarajia kuanza tarehe 11 hadi 18 Agosti 2018 ni pamoja na kuwawekea wagonjwa Pacemakers, ICDs, CRT-Ds na CRT-Ps kutokana na ugonjwa utakaogundulika.

Taasisi inawaomba madaktari wote wa Hospitali za Rufaa nchini kuwaleta wagonjwa wenye matatizo yafuatayo kwa ajili ya matibabu:

Atrioventicular block

Chronic bifascicular and tri fascicular block

Sinus node dysfunction

Complete Heart block

Tachyarrhythmias

Third degree block

Heart Failure with severe LV dysfunction (LBBB) >130m/s

Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na Dkt. Peter Kisenge kwa namba 0713 236 502 na +255 22 2151379 ambaye atawaelekeza utaratibu wa kuwatuma wagonjwa hao.


Imetolewa na:

Kitengo cha Uhusiano
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
06/08/2018

KAZI YANGU NI KUWATUMIKIA WANAKAGERA UTUMISHI ULIOTUKUKA-RC KAGERA

0
0
Na Editha Karlo,Blobu ya Jamii Kagera.

MKUU wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti amewataka wanakagera kumpa ushirikiano katika majukumu yake mapya ya kikazi aliyoanza ili kuendeleza yale mazuri yaliyofanywa na watangulizi wake.

Gaguti ameyasema hayo leo kwenye ukumbi wa halmashauri ya Bukoba baada ya kukabidhiwa ofisi na Mkuu wa Mkoa mstaafu Meja Jenerali Salum Kijuu na kumuapisha Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Rashid Mwaimu.

Alisema nafasi yake ni kuendeleza yale mazuri yaliyofanywa na watangulizi wake kwa wanakagera ili kuhakikisha Mkoa wa Kagera unasonga mbele."Ni wajibu wangu kuendeleza yale mazuri yaliyofanywa na watangulizi wangu na nina imani kubwa tutashirikiana na viongozi wenzangu na nitatoa ushirikiano wakati wowote nipo tayari"alisema Mkuu huyo wa Kagera

Gaguti alisema Mkoa wa Kagera ni Mkoa ambao upo mpakani na unapakana na nchi karibia tatu hivyo aliwataka wananchi wa Mkoa huo kutumia fursa hiyo kuuza mazao ili kuufanya Mkoa kuwa wa viwanda na wenye neema.

Mkuu wa Wilaya ya Kywerwa Rashid Mwaimu baada ya kuapishwa alisema kuwa atakwenda kusimamia mapato katika Wilaya yake na kuhakikisha yanaongezeka ili shuhuri za maendeleo ndani ya Wilaya hiyo zifanyike vizuri.

"Najua nina majukumu makubwa na kazi yangu ni kutatua matatizo ya wananchi ili Wilaya yetu iweze kufanya vizuri katika sekta za miundombinu,afya na Elimu"alisema.
Mkuu wa Mkoa mstaafu wa Kagera Meja Jenerali Salum Kijuu akimkabidhi nyaraka za ofisi mkuu wa Mkoa mpya wa Kagera Brigedia Jenerali Maico Gaguti kwenye ofisi za halmashauri ya Bukoba

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Maico Gaguti akimuapisha Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Rashid Mwaimu katika ukumbi wa halmashauri ya Bukoba.

Baadhi ya viongozi wa chama ,Serikali na kamati ya Ulinzi Mkoa wa Kagera wakishuhudia makabidhiano ya ofisi kwa Mkuu wa Mkoa na kuapishwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Rashid Mwaimu .

NEEC, UNDP na wadau wengine kufanya tafiti zitakazochochea maendeleo kwenye halmashauri

0
0


 Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananachi Kiuchumi (NEEC),Beng'i  Issa,akibadilishana nyaraka na Mkuu wa Idara ya maarifa na Ubunifu Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Margareth Nzuki (kushoto) baada ya kusaini mkataba wa kufanya kazi kati ya baraza hilo pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM).
Katibu mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC),Beng'i  Issa,akibadilishana nyaraka  na Mwakilishi wa Mkuu wa Idara ya Uchumi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Dkt. Kenneth Mdadila, (kulia) baada ya kusain Mkataba wa kufanya kazi za tafiti kati ya baraza hilo pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) pamoja na chuo hicho.
Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananachi Kiuchumi (NEEC),Bi. Beng'i  Issa katikati akisaini nyaraka ya makubaliano ya mkataba wa kufanya kazi na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP pamoja na Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF),  kushoto ni Mkuu wa Idara ya maarifa na Ubunifu ESRF,Bi. Margareth Nzuki na kulia ni Mwakilishi  wa Mkuu wa Idara ya Uchumi UDSM Dkt. Kenneth Mdadila.
(Picha na Mpiga Picha Wetu, Dar es Salaam).

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
BARAZA la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) limeingia makubaliano na taasisi ya umoja wa mataifa la maendeleo UNDP pamoja na Chuo kikuu cha Dar es salaam(UDSM) na Taasisis ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii  (ESRF) kufanya tafiti mbalimbali zitakazo wezesha halmashauri za wilaya na mikoa kuchochea maendeleo ya kiuchumi kwenye maeneo yao.

Makubaliano hayo yamesainiwa leo jijini Dar es salaam na Katibu Mtendaji wa baraza hilo,Bi.Beng’i Issa pamoja na Mkuu wa Idara ya Maarifa na Ubunifu  ESRF, Bi. Margareth Nzuki na Mwakilishi wa Mkuu wa Idara ya Uchumi UDSM,Dkt. Kenneth Mdadila ambapo taasisi hizo kwa pamoja na UNDP watashirikiana kufanya tafiti hizo.

Bi. Issa alisema tafiti hizo zitasaidia halmashauri kutambua vipaumbele vyao katika  uzalishaji, kuandaa mpango mkakati utakaowezesha kutafuta fedha kwa ajili ya kugharamia shughuli za maendeleo hususani kwa vijana.“ 

Kwa pamoja tumeamua kufanya hivi ili kuleta matokeo chanya ya tafiti na kusaidia jamii hususani katika  halmashauri zetu,” kazi za tafiti ni za kitaalam na tunataka zisaidie na hiyo ni njia muhimu katika kuunga mkono serikali ya awamu ya tano inayojenga uchumi wa viwanda, alisema Bi. Issa.

Pia alisema matokeo ya tafiti hizo pia yatasaidia baraza hilo kupata taarifa ambazo zitatumika kwenye utekelezaji wa mradi maalum wa miaka mitatu unaoratibiwa na baraza hilo kwa kushirikiana na umoja wa mataifa ambao utaanza mapema mwakani.

Alisema kazi hizo zinatarajiwa kukamilika kabla ya Desemba 2018 kwa kuwa nia ya ushirikiano huo ni kupata taarifa zitakazo tumika kuandaa andiko kubwa la mradi unaotakiwa kutekelezwa kwa miaka mitatu ijayo kati ya UNDP na baraza kuanzia Januari 2019.

Alisisistiza kuwa tafiti hizo zitatoa taarifa ambazo zitawezesha kushughulikia zaidi uwezeshaji wananchi kiuchumi kulingana na makundi yanayolegwa.

Naye Mratibu wa mradi kutoka taasisi za kiuchumi na kijamii Magreth Nzuki, alisema utafiti huo utakapo kamilika  Utaleta mageuzi katika teknolojia ya kilimo kwa kuzalisha malighafi zitakazo hitajika kwenye viwanda.
Viewing all 109605 articles
Browse latest View live




Latest Images