Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

DK.SHEIN ATEMBELA OFISI ZA KIWANDA CHA MAFUTA YA NAZI

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Meneja Mauzo wa Kiwanda cha mafuta ya Nazi cha Samani Island Virgin Coconut Oil Manufacture kiliopo Jimbaran Bali Nchini Indonesia wakati alipotembelea Ofisi hizo jana akiwa katika ziara ya mualiko wa Makamo wa Rais wa Indonesia Mhe.Mohamed Jusuf Kalla
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Malaysia pia akiiwakilisha Tanzania Nchini Ind0nesia Mhe.Dkt.Ramadhan Kitwana Dau, (kulia) na Meneja Mauzo wa Kiwanda cha mafuta ya Nazi cha Samani Island Virgin Coconut Oil Manufacture kiliopo Jimbaran Bali Nchini Indonesia Nd,Iwayan Sundarma wakiangalia burudani baada ya mapokezi katika ofisi za kiwanda hicho alipotembelea jana akiwa katika ziara ya mualiko wa Makamo wa Rais wa Indonesia Mhe.Mohamed Jusuf Kalla

Meneja Mauzo wa Kiwanda cha mafuta ya Nazi cha Samani Island Virgin Coconut Oil Manufacture kiliopo Jimbaran Bali Nchini Indonesia Nd,Iwayan Sundarma (kushoto) akitoa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na ujumbe wake walipotembela jana Ofisi za Kiwanda hicho kiliopo Jimbaran Bali Nchini Indonesia, akiwa katika ziara ya mualiko wa Makamo wa Rais wa Indonesia Mhe.Mohamed Jusuf Kalla,

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pamoja na Ujumbe wake (hawapo pichani) jana walipotembelea Kiwandani hapo waliweza kuona bidhaa mbali mbali zinazotokana na nazi ambazo hutengenezwa kwa kupitia Kiwanda cha mafuta ya Nazi cha Samani Island Virgin Coconut Oil Manufacture kiliopo Jimbaran Bali Nchini Indonesia ambapo bidhaa hizo huzwa katika Nchi mbali mbali Duniani
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa na ujumbe wake (kushoto) wakizungumza na Uongozi wa Kiwanda cha mafuta ya Nazi cha Samani Island Virgin Coconut Oil Manufacture katika Ofisi ziliopo Jimbaran Bali Nchini Indonesia walipotembelea jana katika ziara ya mualiko wa Makamo wa Rais wa Indonesia Mhe.Mohamed Jusuf Kalla.Picha na Ikulu

DK.SHEIN AKUTANA NA MKURUGENZI KAMPUNI YA UTALIII

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Utalii Mjini Bali nchini Indonesia Nd,Abubakar Mansoer jana walipokutana kwa mazungumzo katika Hoteli ya Discovery Kartika Plaza akiwa katika ziara ya mualiko wa Makamo wa Rais wa Indonesia Mhe.Mohamed Jusuf Kalla
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Utalii Mjini Bali nchini Indonesia Nd,Abubakar Mansoer (katikati) pamoja na Viongozi wa pande mbili hizo walipokutana jana kwa mazungumzo katika Hoteli ya Discovery Kartika Plaza katika ziara ya mualiko wa Makamo wa Rais wa Indonesia Mhe.Mohamed Jusuf Kalla,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ahaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) pamoja na ujumbe wake walishiriki katika swala ya Ijumaa iliyoswaliwa katika Msikiti Masjid Hudal Islamiya wa Mjini Bali Indonesia katika ziara ya mualiko wa Makamo wa Rais wa Indonesia Mhe.Mohamed Jusuf Kalla,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ahaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Malaysia pia akiiwakilisha Tanzania Nchini Indonesia Mhe.Dkt.Ramadhan Kitwana Dau, pamoja na ujumbe wake wakitoka katika swala ya Ijumaa iliyoswaliwa katika Msikiti Masjid Hudal Islamiya wa Mjini Bali Indonesia katika ziara ya mualiko wa Makamo wa Rais wa Indonesia Mhe.Mohamed Jusuf Kalla.Picha na Ikulu

Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) Agnes Kijo afanya zaiara ya kushtukiza mpaka wa Tanzania na Kenya

$
0
0
 Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) Agnes Kijo  akiteta jambo na watumishi wa mamlaka hiyo kwenye  mpaka wa Tanzania na Kenya nchini Horohoro katikati ni Mkaguzi Mfawidhi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) mpakani mwa Tanzania na Kenya (Horohoro) Thomas Nkondola
 Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) Agnes Kijo akisisitiza jambo wakati akiongea na watumishi wa mamlaka hiyo kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya wa Horohoro . 
Mkaguzi iwa chakula wa Mamlaka ya Chakula na Dawa katika mpaka wa Tanzania na Kenya (Horohoro) Thomas Nkondola kushoto akimuonyesha kitu Kaimu  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) Agnes Kijo mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza eneo hilo

Introducing "Moyo" by Kassim Mganga

Introducing "Gone Now" by Eddy The Great & Kamili Freeman

WANARIADHA POLISI WAAGWA, WATAKIWA KUTANGULIZA UZALENDO

$
0
0
Na Rashid Nchimbi wa Polisi Arusha
Timu ya riadha ya Polisi imeagwa jana mchana na kuondoka leo kuelekea jijini Dar es salaam kwa ajili ya Michezo ya Shirikisho la Majeshi ya Polisi ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (EAPCCO GAMES).
Akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Afisa Mnadhimu wa Jeshi hilo mkoani hapa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Yusuf Ilembo aliwataka askari hao kutanguliza uzalendo kwa Jeshi la Polisi na nchi kwa ujumla hivyo wajitume kwa uwezo wao wote ili waweze kuibuka na ushindi mnono.
“Ingawa tuna wawakilishi katika michezo mbalimbali lakini Jeshi la Polisi lina mategemeo makubwa juu ya mchezo wa riadha hivyo naimani mtachukua medali zote na hatimaye kuwa washindi”. Alisema Afisa Mnadhimu huyo.
Wanariadha hao Kumi na Nane walioweka kambi kwa muda wa miezi sita eneo la Ilboru wilaya ya Arumeru watashiriki Mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza tarehe 06 Agosti jijini Dar es saalam kwa kukimbia mbio ndefu na mbio za kati.
Akizungumzia maandalizi ya kambi hiyo, Msimamizi wa Michezo toka Shule ya Mafunzo ya Polisi Moshi, Inspekta Emmanuel Mtatifikolo alisema wana matumaini makubwa ya kushinda nafasi za juu na hawataliangusha Jeshi la Polisi japokuwa kuna nchi tishio kama vile Kenya na Uganda.
Afisa Mnadhimu wa Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Yusuf Ilembo akiwa katika picha ya pamoja na wanariadha hao pamoja na viongozi wa Polisi ngazi ya mkoa 
(Picha na Rashid Nchimbi wa Polisi Arusha)

DKT. SHEIN AKUTANA NA MKURUGENZI KAPUNI YA UTALII YA MJINI BALI, INDONESIA

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Utalii Mjini Bali nchini Indonesia Ndg. Abubakar Mansoer jana walipokutana kwa mazungumzo katika Hoteli ya Discovery Kartika Plaza  akiwa katika ziara ya mualiko wa Makamo wa Rais wa Indonesia Mhe.Mohamed Jusuf Kalla
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akiongea na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Utalii Mjini Bali nchini Indonesia Ndg. Abubakar Mansoer  walipokutana kwa mazungumzo katika Hoteli ya Discovery Kartika Plaza
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Utalii Mjini Bali nchini Indonesia Nd,Abubakar Mansoer (katikati) pamoja na Viongozi wa pande mbili hizo   walipokutana jana kwa mazungumzo katika Hoteli ya Discovery Kartika Plaza  katika ziara ya mualiko wa Makamo wa Rais wa Indonesia Mhe.Mohamed Jusuf Kalla
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ahaj Dk.Ali Mohamed Shein  (wa pili kulia) pamoja na ujumbe wake walishiriki katika swala ya Ijumaa iliyoswaliwa katika Msikiti Masjid Hudal Islamiya wa Mjini Bali Indonesia katika ziara ya  mualiko wa Makamo wa Rais wa Indonesia Mhe.Mohamed Jusuf Kalla
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ahaj Dk.Ali Mohamed Shein  (katikati) akifuatana na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Malaysia pia akiiwakilisha Tanzania Nchini Indonesia Mhe.Dkt.Ramadhan Kitwana Dau, pamoja na ujumbe wake wakitoka katika swala ya Ijumaa iliyoswaliwa katika Msikiti Masjid Hudal Islamiya wa Mjini Bali Indonesia wakatika ziara ya  mualiko wa Makamo wa Rais wa Indonesia Mhe.Mohamed Jusuf Kalla. Picha na IKULU.
Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

MPANGO KABAMBE WA MAENDELEO YA KILIMO AWAMU YA PILI KUELEKEA TANZANIA YA VIWANDA

$
0
0
Kuelekea Tanzania ya viwanda katika eneo la kilimo cha umwagiliaji, Mpango kabambe wa maendeleo ya kilimo awamu ya pili una lengo la kuimarisha kilimo cha umwagiliajiili kupunguza utegemezi wa mvua kwa kuongeza eneo la umwagiliaji nchini, kutoka hekta 461,326 mwaka 2014 hadi hekta 1,000,000 ifikapo mwaka 2025. 

Hayo yameelezwa leo wakati wa maonyesho ya wakulima nanenane katika viwanja vya Nyakabindi, Mjini Bariadi na Mhandisi Ebenezer Kombe kutoka kanda ya Umwagiliaji ya Mwanza alipokuwa akiongea na wananchi waliotembelea banda la Tume ya Taifa ya Umwagiliaji. 

Mhandisi Kombe amesema kuwa ilikufanikisha hayo, serikali itashirikiana na sekta Binafsi kuwekeza katika miundombinu ya umwagiliaji kwa kujenga mifereji mikuu, mifereji ya kati na mabwawa ya kuhifadhia maji kwenye maeneo yenye ukame. 

Aidha Bw. Kombe alisema, Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kwa kushirikiana na Halmashauri husika itahamasisha wakulima kupitia vyama vya umwagiliaji kuchangia katika ujenzi wa mifereji midogo ya kuingiza maji mashambani na kushiriki katika kuitunza mifereji hiyo. 

“Tunawafundisha wakulima kuzalisha kwa tija na ufanisi kwa kutumia miundombinu iliyopo ikiwa ni pamoja na kulima zaidi ya mara moja kwa mwaka, kwa kutumia teknolojia ya kisasa kwa mfano kilimo shadidi cha mpunga (kilimo chenye matumizi kidogo ya maji).” Alisisitiza. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>


picha kushoto Afisa kilimo kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Petro Sarawat, akimpatia kipeperushi mwananchi aliyetembelea banda hilo katika viwanja vya nane vya Nyakadindi , Bariadi Mkoani Simiyu.
Aliyevaa shati Jeupe Meneja wa kanda ya ziwa wa kampuni ya Davis and Shirtlff akiwaonyesha wakulima vifaa vinavyotumika katika kilimo cha umwagiliaji, vinavyouzwa na Kampuni hiyo katika banda la Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kwenye viwanja vya nanenane vya Nyakadindi, Bariadi Mkoani Simiyu.
Picha ya Pamoja ikonyesha baadhi ya watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji walioshiriki maonyesho wa wakulima nanenane katika viwanja vya Nyakabindi, Bariadi Mkoani Simiyu. (Habari na Picha na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Tume ya Taifa ya Umwagiliaji)


KAIMU MKURUGENZI WA TFDA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA MPAKANI MWA TANZANIA NA KENYA HOROHORO AHAIDI KUPELEKA MAABARA ZINAZOHAMISHIKA

$
0
0
KAIMU Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) Agnes Kijo amefanya ziara ya kushtukiza kwenye mpaka wa Kenya na Tanzania eneo la Horohoro wilayani Mkinga na kuridhishwa na utendaji wa watumishi hao huku akiwahaidi kupeleka maabara inayohamishika kwenye kituo hicho ili kuweza kupima dawa za malaria, ukimwi na dawa za kuulia vijidudu.

TFDA na Taasisi za serikali wanatoa huduma ya kufanya ukaguzi wa bidhaa za chakula, dawa,vipodozi, vifaa tiba na vitenganishi kwa ajili ya kuhakikisha vinaingia nchini zikiwa salama na kwamba vimeidhinishwa na mamlaka husika kabla ya kuingia nchini

Agnes aliyasema hayo wakati akiwa eneo hilo mara baada ya kuzungumza na watumishi wa mamlaka hiyo wakati wa ziara hiyo ilikuwa na lengo la kuangalia kama watendaji waliowapa dhamana kwenye vituo vya forodha wanafanya kazi kulingana na sheria, taratibu na miongozi walizowapatia ya kikaguzi kazi kubwa inafanyika kwenye vituo hivyo

Alisema hilo linatokana na eneo hilo kutokuwa na maabara inayohamishika hivyo wataiweka ili waweze kujua dalili na bidhaa kama zinazoingia wakati zinapita mpakani ziruhusiwe au kutokuziruhusu kutokana baada ya kujiridhisha iwapo zinapaswa kufanywa hivyo .
KAIMU Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) Agnes Kijo kulia akionyeshwa baadhi ya taarifa kwenye ofisi za mamlaka hiyo zilizopo eneo la Horohoro mpakani mwa Tanzania na Kenya na mkaguzi Mfawidhi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) mpakani mwa Tanzania na Kenya (Horohoro) Thomas Nkondola . mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza 
KAIMU Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) Agnes Kijo kulia akizungumza mara baada ya kufanya ziara hiyo ya kushtukiza 
 Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA)Agnes Kijo kushoto akimsikiliza kwa umakini Mkaguzi Mfawidhi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) mpakani mwa Tanzania na Kenya (Horohoro) Thomas Nkondola wakati alipofanya ziara ya kushtukiza mpakani hapo.
 Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA)Agnes Kijo kushoto akikagua bidhaa mbalimbali zilizokamatwa na mamlaka hiyo eneo la Horohoro wakati alipofanya ziara ya kushtukiza kulia ni Mkaguzi Mfawidhi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) mpakani mwa Tanzania na Kenya (Horohoro) Thomas Nkondola 
 sehemu ya bidhaa zilizokutwa eneo hilo

HAMZA TEMBA UMEONDOKA BILA KUJIBU UJUMBE WANGU ...WEWE NI MTU MWEMA

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

SAA 2:05 ya asubuhi ya jana ya Agosti 4 mwaka 2018 nilituma ujumbe mfupi wa simu ya mkononi kwa Ofisa Habari wa Wizara ya Maliasili na Utalii Hamza Temba.

Nakumbuka ujumbe huo niliutuma saa 2:05.Nikiri nimekuwa na na kawaida ya kuwasiliana mara kwa mara na Temba.Hivyo baada ya kuona kuna taarifa inasambaa mtandaoni kuhusu Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamis Kigwangala kupata ajali mkoani Manyara na hali yake ni mbaya sana.

Nikaamini mwenye majibu sahihi kuhusu taarifa ya Waziri kupata ajali atakuwa Temba.Basi nikachukua simu yangu na kuanza kupiga.Mara ya kwanza ikaaita bila kupokelewa.Nikapiga mara ya pili pia haikupokelewa. Nikapiga tena mara ya tatu nayo ikawa haina wa kuipokea.

Hivyo nakaona ngoja nitumie ujumbe mfupi wa simu. Ujumbe niliomuandika ulisema hivi "Kaka habari za asubuhi, nakutafuta plz".Ni jumbe ambao niliamini akiona basi lazima tutawasiliana.Kinachonisikitisha kumbe wakati namtumia ujumbe huo Hamnza Temba pumzi yake ilishakata.Macho yake yalishafumba. Temba kumbe alikuwa ameshalala na hataamka tena.Hakuna na uwezo wa kujibu ujumbe wa simu yangu tena.

Kwangu ni ujumbe ambao kwa mara ya kwanza nauandika kwa Temba lakini haukupata nafasi ya kujibu na hautajibiwa tena.Kwa kifupi Hamza Temba hatunaye tena.Amefariki dunia jana asubuhi mkoani Manyara baada ya gari aliyokuwa akisafiria kupata ajali.

Temba alikuwa pamoja na Waziri Dk.Kigwangala ambaye amejeruhiwa na sasa anaendelea na matibabu Hospitali ya Taifa Muhimbili.Kifo cha Temba kimeniuma sana.Ni kijana aliyeijua vema kazi yake.Hamza Temba ni Ofisa Habari wa Wizara aliyekuwa na nidhamu kwa kila mtu.Upendo , upole na ucheshi wake hauna mfano.Hakika Temba alikuwa Ofisa wa Habari wa Wizara anayejua kuishi na waandishi wa habari.

Ni ofisa habari wa wizara mwenye heshima ya hali ya ju.Hakuwa na dharau hata kidogo.Moja ya tatizo ambalo ninalo mimi binafsi ni kwamba mtu anapofanya vizuri katika kutekeleza majukumu yake huwa siwezi kuficha lazima niamwambia.Juni mwaka huu niliamua kumpigia simu Temba na mazungumzo yangu yalijikita katika kumpongeza na kumsifu kwa namna ambavyo anatekeleza majukumu yake.

DKT TIZEBA AAGIZA WAKAGUZI WA VIUATILIFU KULINDA MASLAHI YA TAIFA

$
0
0
Na Mathias Canal, WK-Morogoro

Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba leo tarehe 5 Agosti 2018 amefungua rasmi mafunzo ya wakaguzi wa viuatilifu yaani mimea na mazao katika hafla iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha kilimo (SUA) Mkoani Morogoro ambapo asilimia 99 ya washiriki wanatoka katika vituo vya ukaguzi wa mazao mipakani vikiwemo vya nchi kavu, bandarini na viwanja vya ndege.

Katika mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu katika Ukanda wa Kitropiki (Tropical Pesticide Research Institute - TPRI), Waziri Dkt Tizeba ameagiza washiriki hao Kulinda maslahi ya wakulima, walaji na Taifa kwa ujumla dhidi ya wafanyabiashara wachache wa viuatilifu wanaotaka kutajirika kwa kutuletea viuatilifu vilivyo chini ya kiwango.

Waziri huyo anayeshughulikia sekta ya kilimo nchini ameyasema hayo kwa msisitizo mkubwa huku akiwataka kutekeleza wajibu wao wa ukaguzi wa viatilifu kwa umakini, uaminifu na uadilifu mkubwa kwa kutumia Sheria na Kanuni zilizopo. Amesisitiza kuwa wataalamu hao wanapaswa kuitetea maslahi ya nchi pale inapohitajika kwa kutumia kwa umakini mkubwa kwa utashi wa Sheria na Kanuni zinazotakiwa ikiwa ni pamoja na taratibu nyingine za kisheria katika kuhusisha watumishi wengine wa Serikali kama waendesha mashtaka wa Serikali na askari.

Pia, aliwataka Wakaguzi kutoka Makao Makuu ya Wizara na Taasisi ya TPRI kuangalia namna ya kuunganisha shughuli zinazofanywa kati ya Kitengo cha afya ya mimea (PHS) na TPRI katika kuwasimamia na kuwaongoza wakaguzi kutoka katika vituo vyetu vya mipakani ili watekeleze majukumu yao kwa ufanisi na uadilifu kwa kuwapatia vitendea kazi pale fursa zinapopatikana kwa kuzingatia mahitaji.

Mgeni rasmi-Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akizungumza wakati wa mkutano wa ufunguzi wa mafunzo ya wakaguzi wa viuatilifu kwenye hafla iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha kilimo (SUA) Mkoani Morogoro leo Tarehe 5 Agosti 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)

Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akisisitiza ufanisi kazini wakati akizungumza kwenye mkutano wa ufunguzi wa mafunzo ya wakaguzi wa viuatilifu kwenye hafla iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha kilimo (SUA) Mkoani Morogoro leo Tarehe 5 Agosti 2018.
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu katika Ukanda wa Kitropiki (Tropical Pesticide Research Institute - TPRI) Dkt Margaret Mollel akitoa taarifa ya mafunzo ya wakaguzi wa viuatilifu mbele ya mgeni rasmi Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba kwenye hafla iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha kilimo (SUA) Mkoani Morogoro leo Tarehe 5 Agosti 2018.
Picha ya pamoja baada ya kumalizika mkutano wa ufunguzi wa mafunzo ya wakaguzi wa viuatilifu kwenye hafla iliyofanyika Chuo Kikuu cha kilimo (SUA) Mkoani Morogoro leo Tarehe 5 Agosti 2018.

WAZIRI MKUU AUPONGEZA UONGOZI WA MAKUMBUSHO

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameupongeza uongozi wa Makumbusho ya Taifa kwa kuchora ramani ya Tanzania katika Kijiji cha Makumbusho ambayo itatumika kwenye ujenzi wa nyumba za utamaduni wa makabila mbalimbali nchini.Amesema uamuzi huo utarahisisha watu kufika kwa urahisi katika nyumza za tamaduni za mikoa yao kwa kuwa watakuwa wanatumia ramani Tanzania.

Waziri Mkuu aliyasema hayo jana (Jumapili, Agosti 4, 2018) wakati akizungumza na wakazi wa mkoa wa Lindi kwenye kikao cha kujadili maandalizi ya Tamasha la Utamaduni wa Mtanzania katika Kijiji cha Makumbusho, jijini Dar es Salaam.


“Kwa kutumia ramani hii kila mkoa utaweza kufika kwenye eneo lake kwa kutumia ramani ya Tanzania na mkoa wa Lindi tayari umeshaoneshwa eneo lake kwa ajili ya ujenzi wa nyumba inayozingatia utamaduni wetu,” alisema.

Alisema kwa tamaduni za makabila ya mkoa wa Lindi nyumba zote hujengwa kwa udongo na kuezekwa kwa makuti upande wa maeneo ya pwani ya upande mwingine huezeka kwa nyasi, ambapo aina zote zitajengwa ili kuwakilisha tamaduni za wakazi wa mkoa huo.Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewaasa wananchi wa mkoa wa Lindi ambao kwa mwaka huu ndio waandaaji wa tamasha hilo wadumishe mshikamano wao ili waweze kutimiza malengo waliyojiwekea katika kuboresha maendeleo.

Alisema katika tamasha hilo ambalo linatarajiwa kuanza Agosti 26 hadi 29 wahakikishe wanapeleka kila kitu ambacho kinahusiana na utamaduni wa mkoa huo ili kuwawezesha Watanzania wengine wajue kama vyakula na mavazi .Pia alishauri wawepo wazee wenye kujua historia ambao watasimulia utamaduni wa wananchi wa Lindi pamoja na kutambulisha ngoma zao za utamaduni. “Halmashauri zote za mkoa wa Lindi zitumie fursa hii kutangaza vivuti vya utalii vilivyopo na Kilwa walete mtu atakayeelezea kuhusu magofu,”.



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua ramani ya muonekano mpya wa kijiji cha Makumbusho kwenye kikao cha kujadili maandalizi ya Tamasha la Utamaduni wa Tanzania katika kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam, Agosti 4, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na mkewe Mary Majaliwa wakioneshwa ramani ya muonekano mpya wa kijiji cha Makumbusho na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Profesa Audax Mabula, kwenye kikao cha kujadili maandalizi ya Tamasha la Utamaduni wa Tanzania kilichofanyika katika kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam Agosti 4, 2018, kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi, Meja General Mstaafu Said Kalembo.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza na wakazi wa Mkoa wa Lindi kwenye kikao cha kujadili maandalizi ya Tamasha la Utamaduni wa Tanzania kilichofanyika katika kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam, Agosti 4, 2018.



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akipokea hundi ya sh. 20,000,000 kutoka kwa mdau wa maendeleo ya Mkoa wa Lindi, Bw. Otieno Igogo, ikiwa ni mchango kwa alibi ya kufanikisha Tamasha la Utamaduni wa Tanzania, Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye katika kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam, Agosti 4, 2018.



Mke wa waziri Mkuu Mary Majaliwa,akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi, alipowasili kwenye kikao cha maandalizi ya Tamasha la Utamaduni wa Tanzania kwenye kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam, Agosti 4, 2018.



KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>

MKWASA AFANYIWA UPASUAJI WA MOYO INDIA.

$
0
0
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga, na mchezaji wa zamani wa timu ya Yanga na Taifa Stars  Charles Boniface Mkwasa afanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo.

Mkwasa yuko jijini New Delhi, India ambako amefanyiwa upasuaji huo mkubwa na imeelezwa bado yuko katika chumba cha usimamizi maalum, yaani ICU.

Mkwasa alisafiri takribani wiki moja iliyopita kwenda nchini India kwa ajili ya matibabu baada ya kugundulika na tatizo la moyo hapa nchini.

Mkwasa aliamua kujiuzulu nafasi yake ndani ya Yanga kwa ajili ya kujiuguza.

ARUSHA YAANZA KUONYESHA NJIA MADEREVA WASIOKUWA NA VYETI

$
0
0
Na Rashid Nchimbi wa Polisi Arusha

Jeshi la Polisi mkoani hapa kwa kushirikiana na Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) kanda ya Kaskazini wamefanikiwa kutoa mafunzo kwa madereva 350 wa magari ya abiria ambao awali walikuwa na Leseni pekee bila vyeti.

Mafunzo hayo yaliyofungwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo katika Chuo Cha Ufundi Arusha, awali yalifunguliwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng’anzi wiki mbili zilizopita.

Akizungumza katika siku hiyo ya Mahafali, Mkuu huyo wa mkoa, kwanza kabisa alilipongeza Jeshi la Polisi na Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) kwa kuamua kuendesha mafunzo hayo lakini pia kwa wahitimu wenyewe kwani ni jambo zuri na lenye maslahi kwenye maisha yao.

Alisema jitihada hizo zinalenga kupambana na ajali kwani madhara yake ni makubwa ikiwa ni pamoja na kusababisha vifo, ulemavu, kupata hasara kwenye mali lakini pia zinaweza kusababisha kutotoa fursa za ajira kwa madereva wenye matukio ya kusababisha ajali.

Mkuu huyo wa mkoa alisema pamoja na mafunzo waliyoyapata wahitimu hao lakini watatakiwa waepuke unywaji wa pombe wakati wanaendesha vyombo vya moto kwani ajali nyingi zinasababishwa na ulevi, huku akilitaka Jeshi la Polisi kupitia kitengo cha usalama Barabarani kuongeza jitihada katika kupima ulevi kwa madereva.


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo akiongea na Wahitimu wa mafunzo ya udereva wa magari ya abiria wakati wa Mahafali ya kuhitimisha mafunzo yao yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Chuo cha Ufundi Arusha.

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Arusha Mrakibu wa Polisi (SP) Joseph Charles Bukombe akiwataka Wahitimu hao wakawe mabalozi wa madereva wengine ambao hawajapata mafunzo kama hayo ili nao wajitokeze siku za usoni.(Picha na Rashid Nchimbi wa Polisi Arusha)

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Arusha Mrakibu wa Polisi (SP) Joseph Charles Bukombe akiwataka Wahitimu hao wakawe mabalozi wa madereva wengine ambao hawajapata mafunzo kama hayo ili nao wajitokeze siku za usoni.(Picha na Rashid Nchimbi wa Polisi Arusha)

Baadhi ya wahitimu waliopata mafunzo ya uendeshaji wa magari ya kubeba abiria ambayo yaliendeshwa na Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) kwa muda wa wiki mbili wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo wakati wa Mahafali hayo yaliyofanyika katika Chuo cha Ufundi Arusha. (Picha na Rashid Nchimbi wa Polisi Arusha) .

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI ATEMBELEA MTO MBEZI NA MBWENI,AZUNGUMZA NA BAADHI YA WANANCHI WALIOATHIRIWA NA MAFURIKO

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh.Daniel Chongolo akizungumza na baadhi ya Vijana wanaochimba mchanga ndani ya mto Mbezi kwa madai ya kuondoa mchanga ndani ya mto huo ili kuongeza kina chake kitakachosaidia kupunguza adha ya mafuriko yanapotokea wakati wa mvua kubwa zinaponyesha.Mh Chongolo ametembelea maeneo hayo kuona namna shughuli za uondoaji mchanga katika eneo unavyoendelea ikiwemo na kuwasikiliza Wananchi waishio kando kando ya mto huo kuhusiana na shughuli hiyo. 
Shughuli za uondoaji Mchanga ndani ya Mto Mbezi ukiendelea
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh.Daniel Chongolo (pichani kushoto) akimsikiliza Meneja wa Kampuni Benson Construction Ltd,Adam Kapama mapema leo,kuhusu shughuli nzima ya kuondoa mchanga ndani ya mto Mbezi ili kuongeza kina kitakachosaidia kupunguza adha ya mafuriko yanapotokea wakati wa mvua kubwa zinaponyesha.Mh Chongolo ametembelea maeneo hayo pamoja na Mbweni kuona athari wanayoipata Wananchi wakati mvua zinaponyesha na kusababisha adha kubwa ya mafuriko, ikiwemo pia kuwasikiliza Wananchi waishio kando kando ya maeneo hayo. 
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh.Daniel Chongolo (pichani kati) akimsikiliza mmoja wa Wakazi waishio kando kando ya Mto Mbezi,kuhusiana na shughuli nzima inayoendelea ya kuondoa mchanga ndani ya mto Mbezi ili kuongeza kina kitakachosaidia kupunguza adha ya mafuriko yanapotokea wakati wa mvua kubwa zinaponyesha.Mh Chongolo ametembelea maeneo hayo pamoja na Mbweni kuona athari wanayoipata Wananchi wakati mvua zinaponyesha na kusababisha adha kubwa ya mafuriko, ikiwemo pia kuwasikiliza Wananchi waishio kando kando ya maeneo hayo. 
Shughuli za uondoaji Mchanga ndani ya Mto Mbezi ukiendelea 
Mmoja wa Wakazi waishio Mbweni Teta,Emanuel Maingu akimuonesha Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Mh.Daniel Chongolo (pichani kulia) namna wanavyoathiriwa na tatizo la maji kutuama kwa mda mrefu wakati wa mvua zinaponyesha. Mh Chongolo ametembelea maeneo ya Mto Mbezi pamoja na Mbweni kuona athari wanayoipata Wananchi wakati mvua zinaponyesha na kusababisha adha kubwa ya mafuriko
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh.Daniel Chongolo (pichani kushoto) akimsikiliza Mmoja wa wakazi wa Mbweni Teta,Emanuel Maingu namna walivyoathirika na mafuriko ikiwemo na kutuama kwa maji muda mrefu wakati wa Mvua zinaponyesha katika maeneo yao.Mh Chongolo ametembelea maeneo ya Mto Mbezi pamoja na Mbweni kuona athari wanayoipata Wananchi wakati mvua zinaponyesha na kusababisha adha kubwa ya mafuriko.

ZIJUE AINA SITA ZA VIAZI LISHE NA FAIDA ZAKE

$
0
0
Hiza ni aina ya ya mbegu za viazi lishe zilizopo katika shamba la mfano la SUGECO Chuo Kikuu cha Kilimo Morogoro, ambalo washiriki wa mafunzo ya uongezaji thamani wa viazi lishe walitembelea mwishoni mwa mwezi uliopita, ambapo pia walijinea viazi kutoka kwa mkulima Sparta . Viazi Lishe vina asilimia kubwa ya vitamini A zinazofaa kwa afya za walaji na hasa kwa akina mama mama wanaojiandaa kupata mimba, wajawazito, waliojifungua pamoja na watoto . PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA.
KABODE 
KIEGEA 
KIAZI CHA MATAYA
KIAZI CHA EJUMULA 
KIAZI LISHE CHA KAKAMEGA 
KIAZI CHA KAKAMEGA

TAMWA YAHIMIZA MAZINGIRA SALAMA KWA WANAFUNZI SHULENI

$
0
0

VIONGOZI wa shule mbalimbali nchini Tanzania wameshauriwa kuhakikisha wanazifanya shule zao kuwa na mazingira salama, yenye utangamano, ushirikiano, upendo pamoja na furaha kwa wanafunzi ili yaweze kumjenga mtoto vema kielimu na maadili katika jamii.

Ushauri huo umetolewa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Eda Sanga alipokuwa mgeni rasmi katika sherehe za Mahafali ya nane ya Darasa la Saba ya Shule ya Msingi St. Aloysius ya Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

Alisema shuleni, watoto wanapaswa kupewe ushauri nasihi na nasaha kadri inavyoitajika, huku wakiwa huru kutoa dukuduku zao na matatizo yao kwa walimu na kuyatatua kadri ya uwezo wao.

“Kuna kila sababu watoto kupewa ujuzi wa kutumia uwezo na mikono yao kufanya kazi na ujuzi wa kutumia akili zao za sasa kutatua migogoro yao kwa ngazi yao,” alisema Bi. Sanga katika hotuba yake.Aliwataka walimu mbali na kumjenga mwanafunzi kielimu kuna haja ya kuwaandaa pia kuwa wazalendo wa taifa lao na kikazi kinachojali wasionacho kama tunavyowajali watu walionacho.

“…Shule inatazamwa kama familia nje ya familia maana watoto wanatumia muda mwingi kuwa shuleni zaidi ya ule wawapo na familia zao nyumbani. Hofu ya Mungu ndio msingi wa mafanikio katika jambo lolote kwani inamjengea mtoto ujasiri, nidhamu na usubutu, naomba haya tuyazingatie pia.

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Eda Sanga (kulia) na mgeni rasmi katika sherehe za Mahafali ya nane ya Darasa la Saba ya Shule ya Msingi St. Aloysius akimkabidhi cheti na zawadi mmoja ya wahitimu wa darasa la saba katika shule hiyo iliyopo Mbezi Beach Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Eda Sanga (kulia) na mgeni rasmi katika sherehe za Mahafali ya nane ya Darasa la Saba ya Shule ya Msingi St. Aloysius akimkabidhi cheti na zawadi mmoja ya wahitimu wa darasa la saba katika shule hiyo iliyopo Mbezi Beach Dar es Salaam. 
Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya Msingi St. Aloysius, Kenneth Sinare (katikati) akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Eda Sanga (kulia) mara baada ya hotuba yake. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Eda Sanga na mgeni rasmi katika sherehe za Mahafali ya nane ya Darasa la Saba ya Shule ya Msingi St. Aloysius ya Mbezi Beach jijini Dar es Salaam akihutubia wanamahafali na wageni waalikwa.

DIWANI VIGWAZA AANZA ZIARA YA KUTEMBELEA MIRADI VIJIJINI

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,VIGWAZA

DIWANI wa kata ya Vigwaza ,Bagamoyo , Pwani ,Mohsin Bharwani (CCM),amechangia mabati 242, mifuko ya saruji 100 na matofali 3,000 vyenye thamani takriban sh.milioni 12 katika kijiji cha Chamakweza,Mnindi na kitongoji cha Serengeti.

Amesema ametoa vifaa hivyo vya ujenzi ,ili kutekeleza ilani ya CCM na kuunga mkono juhudi za wananchi katika miradi wanayoiibua na miradi ya serikali.Bharwani alitoa michango hiyo, katika ziara yake ya kutembelea baadhi ya miradi ya maendeleo katika vijiji vilivyopo kata ya Vigwaza ,ambapo ameanza kwenye vijiji vya Chamakweza,Mnindi na kitongoji cha Serengeti.

"Shule ya msingi Chamakweza ambayo darasa moja na ofisi havina mabati nimetoa mabati 96 yenye thamani ya sh.milioni 2.8 " #"Katika kitongoji cha Serengeti kilio cha wananchi ni kupata shule ya awali ,na tunashukuru halmashauri imeleta mshauri kutoka idara ya elimu msingi kwenye mkutano huu kwani tumepata nafasi ya kumueleza adhma yetu na kutupa maelekezo" alifafanua .

Kutokana na hilo ,Bharwani alitoa ,mifuko ya saruji 50 ,matofali 2,000 ,licha ya kuendelea kwa hatua nyingine zitakazozingatia vigezo vinavyotakiwa ili kufikia hatua ya kupata kibali cha kujenga na kuwa na shule si tu ya awali bali shule ya msingi.Akiwa kijiji cha Mnindi ambacho kinaendelea na ujenzi wa zahanati alisema ,"wakati ujenzi ulipoanza alichangia mifuko 50 na kwasasa amechangia mabati 96 yenye thamani ya milioni 2.8.

"Serikali inafanya mambo makubwa kwa utkeleza miradi mbalimbali ya reli ,barabara,umeme,afya,elimu na maji hivyo lazima viongozi wa chini tuunge mkono juhudi hizo ,na kushirikiana na rais Dk.John Magufuli kutatua kero mbalimbali kuanzia ngazi ya chini ""Rais karudisha imani kwa wananchi na wadau wanaoshiriki kusaidia masuala mbalimbali, katupa jeuri CCM kutokana na kutekeleza ahadi na ilani kwa kugusa kila eneo ili kuinua maendeleo na uchumi ." alisema Bharwani.

Bharwani aliwataka ,viongozi wa kuchaguliwa na watendaji wengine kuunganisha nguvu na ya wananchi kuisaidia serikali ya CCM ili kipiga hatua zaidi wakati nchi ikielekea kwenye uchumi wa kati .Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi wa halmashauri ,Erasto Meshack kutoka idara ya elimu msingi alisema ,kwa mujibu wa miongozo kigezo cha kwanza ili shule iitwe shule inapaswa kujengwa katika eneo lisilozidi hekari kumi . .

Alieleza ,ili shule iweze kufunguliwa isipungue majengo sita,stoo,vyoo vya walimu ,wanafunzi na nyumba za walimu.Nae ,mwenyekiti wa kijiji cha Vigwaza Ramadhani Kirumbi, alimshukuru diwani huyo kwa michango yake anayojitolea ,kwani kutoa ni moyo .Alisema endapo mradi wa ujenzi wa shule ya awali ya Sekibwa kitongoji cha Serengeti ukifanikiwa utawasaidia watoto ambao hutembea zaidi ya km.tano kufuata elimu hiyo nje ya eneo hilo .Mwenyekit wa CCM kata ya Vigwaza ,Shederi Mkole ,alimpongeza Bharwani kwa kujitoa kwake kutekeleza ilani ya CCM.
DIWANI wa kata ya Vigwaza , Mkoani Pwani ,Mohsin Bharwani (CCM),akizungumza katika kijiji cha Chamakweza wakati alipofanya ziara yake katika kijiji hicho ,kijiji cha Mnindi na kitongoji cha Serengeti.(picha na Mwamvua Mwinyi)
DIWANI wa kata ya Vigwaza , Mkoani Pwani ,Mohsin Bharwani (CCM),akizungumza wakati alipotembelea baadhi ya ujenzi  wa madarasa katika kijiji cha Chamakweza wakati alipofanya ziara yake katika kijiji hicho ,kijiji cha Mnindi na kitongoji cha Serengeti.
Mkazi wa Chamakweza ,Philemon Molel akimshukuru diwani wa kata ya Vigwaza ,Mohsin Bharwani wakati alipokwenda kutembelea miradi na kijijini hapo ,kijiji cha Mnindi na kitongoji cha Serengeti. (Picha na Mwamvua Mwinyi).

SIMBA SC WAHITIMISHA KAMBI YA MAZOEZI NCHINI UTURUKI NA KUREJEA NYUMBANI

$
0
0
 Wachezaji pamoja na benchi la Ufundi  wa mabingwa wa Soka Tanzania Simba SC wakiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Atatürk  jijini Istanbul, Uturuki tayari kwa safari ya kurejea nyumbani Tanzania leo.
 Wachezaji pamoja na benchi la Ufundi  wa mabingwa wa Soka Tanzania Simba SC wakiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Atatürk  jijini Istanbul, Uturuki tayari kwa safari ya kurejea nyumbani Tanzania leo.
Wachezaji pamoja na benchi la Ufundi  wa mabingwa wa Soka Tanzania Simba SC wakiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Atatürk  jijini Istanbul, Uturuki tayari kwa safari ya kurejea nyumbani Tanzania leo.
Picha zote na Rabi Hume, Istanbul - Uturuki.

MFANYABIASHARA AMZAWADIA RC MTAKA KUTAMBUA MCHANGO WAKE KWENYE MAENDELEO YA UCHUMI WA SIMIYU

$
0
0
Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akipokea zawadi ya unga wa ngano, mafuta ya kula na sukari, kutoka kwa Elizabeth Mlanda (kulia) mke wa Mfanyabiashara Clement Mlanda wa Mjini Bariadi, Agosti 04, 2018, ikiwa ni shukrani yake kwa kutambua mchango wa Mkuu huyo wa Mkoa katika maendeleo ya Uchumi wa mkoa wa Simiyu .
Elizabeth Mlanda(kulia) mke wa Mfanyabiashara Clement Mlanda akimkabidhi Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka bahasha yenye fedha kama shukrani yake kwa kutambua mchango wa Mkuu huyo wa Mkoa katika maendeleo ya Uchumi wa mkoa wa Simiyu . 

Na Stella Kalinga, Simiyu

Bibi. Elizabeth Mlanda Mke wa Mfanyabiashara Mkubwa wa Mjini Bariadi mkoani Simiyu, Bw. Clement Mlanda Shigugulu ambaye anamiliki Hotel ya MS COMPLEX  amemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka  zawadi ya fedha taslimu (kiasi ambacho hakikutajwa),  kilo 50 za sukari, kilo 25 za unga wa ngano na lita 40 za mafuta ya kula, ikiwa ni shukrani kwake kwa namna uongozi wake ulivyochangia kuufungua mkoa wa Simiyu kiuchumi na kuwawezesha wafanyabiashara wa mkoa huo kufanya biashara katika nyakati mbalimbali.

Amesema kupitia uongozi wa Mhe. Mtaka kumekuwa na matukio makubwa  yanayochangia kuongezeka kwa mzunguko wa biashara mkoani Simiyu, ikiwemo Maonesho ya Kilimo na Sherehe za wakulima Nanenane ambayo yamewaleta watu kutoka sehemu mbalimbali hivyo kuwanufaiisha wafanyabiashara wa Simiyu hususani wamiliki wa hoteli na nyumba za kulala wageni.

" Jana nilienda Uwanja wa Nanenane nikakuta mambo mazuri, nilipokuja hotelini kwetu nako nikakuta watu wamejaa, nikamuuliza baba(mume wake) kuwa tutampa nini huyu Mkuu wa mkoa wetu kwa mambo mazuri anayotufanyia ya kutuletea maendeleo hivi na kutuletea heshima mkoa wetu mpya wa Simiyu " alisema.

"Nilimwambia mume wangu nitampa zawadi yoyote kumshukuru ili moyo wangu ufurahi, Nimemletea  mafuta ndoo mbili za lita 20, sukari kilo 50,unga wa ngano kilo 25, nampongeza sana na Mungu amzidishie aendelee na moyo huu wa kutuletea maendeleo Mkoa wetu mpya wa Simiyu" alisisitiza Bibi. Elizabeth.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amemshukuru Mfanyabiashara huyo kwa zawadi hizo na akaeleza kuwa itakuwa ni kumbukumbu katika maisha yake huku akifafanunua kuwa kazi anayoifanya ni wajibu wake katika kuwaletea wananchi.

Ameongeza kuwa mikoa mingi imekuwa kiuchumi kutokana mchango wa viongozi waliopo, waliopita kwa kushirikiana na wananchi pamoja na wafanyabiashara.

"Maendeleo ndiyo nia ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kama ilivyokuwa kwa Marais, mawaziri waliopita, na kwa mkoa wa Simiyu mchango wangu unaendeleza kile walichofanya wakuu wenzangu wa mkoa walionitangulia, Marehemu Mabiti na baba yangu Elaston Mbwilo"'alisema.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images