Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

MAAGIZO MAZITO YA MHE.JENISTA KWA KATIBU MKUU MPYA


AJALI YA BASI YAUA WAWILI,YAJERUHI 10

$
0
0
Na Karama Kenyunko,Globu ya jamii

WATU wawili wamefariki dunia na wengine 10 kujeruhiwa baada ya Basi la Modern Coach lililokuwa likitokea nchini Kenya kuja Dar es salaam kupata ajali katika eneo la Mbwewe, mkoani  Pwani.

Katika taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Bw. Aminiel Aligaeshi amethibitisha kupokea majeruhi hao leo  saa 12 asubuhi.  
Akizungumza na Michuzi Blog Aligaeshi amesema miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti na majeruhi wote 10 ambao wamewapokea wanaendelea vizuri. Kwa mujibu wa taarifa ni kwamba gari iliyopata ajali jali basi hilo lilikuwa na abiria 45, dereva mmoja na tingo mmoja na abiria 43.
Wakati huo huo basi la Maning nice lililokuwa likitokea Dar kwenda Masasi limepata ajali baada ya kugonga basi la Tashrif kwa nyuma na kisha kugonga magari mawili aina ya Coaster.
Ajali hiyo imetokea baada ya basi  hilo la Maning nice kuovatake eneo baya na kushindwa kurudi sehemu yake. Shuhuda wa ajali hiyo ameeleza kuwa katika Coaster hiyo, watu wengi wameumia.

BENDI YA SIKINDE NGOMA YA UKAE YATIMIZA MIAKA 40 YA KUZALIWA KWAKE

$
0
0
Na Sultani Kipingo, Globu ya Jamii
DCC Mlimani Park Orchestra (au Mlimani Park) ni bendi ya muziki wa dansi yenye makao yake jijini Dar es Salaam, Tanzania. Bendi Ilianzishwa mwezi kama huu mnamo mwaka wa 1978. Waanzilishi wa bendi hiyo ni pamoja na Muhidin Maalim Gurumo, Abdallah gama na Abel Balthazar. Hassan Bichuka na Suleiman Mwanyiro waliingia 1982 kutokea Juwata jazz. 
 Mtindo maarufu wa bendi ya DDC ni Sikinde ngoma ya ukae, yaani Sikinde Ngoma ya Nyumbani. Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, Mlimani Park iliundwa na kundi kubwa la wanamuziki kutoka bendi ya Dar International. 
Ilianza wakat Dar International ilipokodishwa na Chuo Cha Ardhi katika sherehe yao ya kuwaaga wanachuo wa zamani na kukaribisha wapya. Chuo cha Ardhi kilikodi ukumbi wa Mlimani Park kwa ajili ya shughuli hiyo. 
Wakati huo huo utawala wa Mlimani Park ulikuwa mbioni kutengeneza bendi baada ya kumalizika mkataba wa Orchestra Fukafuka katika ukumbi huo, chini ya mwanamuziki Tchimanga Assossa ambaye alikuwa amekuja na Bendi ya Fukafuka. 
Assosa alibaki nchini na alikuwa katika hatua za mwisho za kwenda kufuata wanamuziki wengine kutoka Kongo kwa ajili ya ukumbi huo. Hivyo basi Dar International wakati huo ndio wakivuma na nyimbo kama Magreti walianza kuporomosha muziki chini ya kiongozi wao Abel Balthazal. Uongozi wa Mlimani Park ulipigwa butwaa na muziki wa hawa jamaa, Abel aliitwa pembeni na kuulizwa bendi iko chini ya mkataba wa nani? Na je, wanamuziki wangeweza kukubali kuajiriwa na na Mlimani Park wakati huo ikiendeshwa na TTTS? 
Kwa vile Dar International ilikuwa ya mtu binafsi na hawakuwa na ajira yoyote ya kudumu katika bendi hiyo, haraka sana wanamuziki walikubali wazo hilo. Kesho yake viongozi wa Dar International walienda kukutana na viongozi wa ukumbi wa Mlimani Park, na wakakubaliana kuazisha kambi ya bendi mpya palepale katika ukumbi wa Mlimani. 
 Haikuwa taabu maana vyombo vilivyonunuliwa wakati wa mkataba wa Orchestra Fukafuka vilikuwa mali ya Mlimani Park kwa hiyo bendi ilianza kwa Abel kusisitiza kupata wanamuziki kama Muhidin Maalim Gurumo. 
Hapo ikumbukwe kuwa ni huyu huyu Abel ambaye ndiye aliyeisuka Dar International baada ya kuwachukua wanamuziki wote wa Safari Trippers kundi zima wakati huo, kina Kassim Mponda, Joseph Bernard, Marijani Rajabu, Ben Peti, Zito Mbunda, Bito Elias na wengine kasoro Christian Kazinduki na kutoka Tanzania Stars ya Maggot walitoka Joseph Mulenga, George Kessy , Haruna Lwali na wengineo. 
Na kwa staili hiyohiyo skwadi nzima ya Dar International ikageuka kuwa Mlimani Park. Muda mfupi kabla la hili ugomvi mkubwa ulikuwa umetokea Dar International kati ya Marijani Rajabu na Abel Balthazar katika ubishi kuhusu tungo aliyoleta Marijani ambayo Balthazar alidai kuwa ni ya Tabu Ley kwa hiyo akatunge tena, jambo lililoleta kushikana mashati, na kusababisha Marijani kusimamishwa kazi. 
Wakati yuko benchi ndipo mpango mzima wa kuhamia Mlimani ulifanyika hivyo mwenye vyombo alilazimika kumfwata tena Marijani na kumwomba aunde bendi upya, na ndipo Super Bomboka ikaundwa. Mlimani Park ikaanza ikiwa na Tchimanga Assossa ambaye safari ya kwenda kutafuta wanamuziki Kongo ikawa imekwisha. 
Na mchango wa kudumu wa Assossa wakati huo ni utunzi wa ule wimbo Gama. Muhidin Maalim Gurumo, Hassani Bitchuka, Abel Balthazar, "King" Michael Enoch, Cosmas Thobias Chidumule, Shaaban Dede, Maalim Khamis Kinyasi, Max Bushoke, Ramadhan Mwinyikondo, Hussein Jumbe, Henry Mkanyia, Julius Mzeru, Joseph Mulenga na Suleiman Mwanyiro
 Mpiga rythim guitar Abdallah Gama (kushoto) na mpiga solo Shabani Yohana Wanted
 Wapiliza saxphone wa Sikinde
 Kutoka kushoto ni Hussein Jumbe, Abdallah Kinguti, Benno Villa Anthony na Hassan Rehani Bitchuka
Muhidin Maalim Gurumo na Hassan Rehani Bitchuka
 Wapuliza trumphet wa bendi ya Mlimani Park, Mbaraka Othman (kushoto) na Hamisi Milambo

LESENI ZA MADINI SASA KUTOLEWA KWA MASHARTI MAGUMU-KAIRUKI

$
0
0

Na Asteria Muhozya, Simanjiro

Waziri wa Madini Angellah Kairuki amesema kuanzia sasa Serikali itaanza kutoa Leseni za madini biashara ya madini kwa masharti magumu huku ikimtaka kila mwombaji kutoa taarifa za mauzo ya uzalishaji, usafirishaji pamoja na mnyororo mzima wa biashara ya madini ikiwemo fedha zinazoingia nchini kutokana na biashara hiyo.

Pia, ameiagiza Tume ya Madini kuchukua hatua stahiki kwa kuhakikisha kila jambo katika mnyororo huo linasimamiwa kikamilifu na kuongeza kuwa, yeye kama waziri mwenye dhamana atahakikisha anafuatilia kila hatua itakayochukuliwa na tume hiyo.

“Tume ichukue hatua. Nitakuwa na ninyi. Msiache hata mmoja atakayekwenda kinyume na haya. Nilifanya hivyo katika Sekta ya Utumishi wa Umma hata huku kwenye sekta ya madini, sitashindwa kufanya hivyo,” alisisitiza Waziri Kairuki.Waziri kairuki aliyasema hayo jana tarehe 3 Agosti, Wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara wakati akipokea taarifa ya Kamati Maalum iliyoundwa kuchunguza mnyororo wa madini ya vito nchini.

Kamati hiyo ilifanya kazi yake kwa muda wa siku 30 kuanzia tarehe 26 Aprili, 2018 kwa jukumu la kuchunguza mnyororo wa madini ya vito kuanzia kuzalisha hadi usafirishaji nje ya nchi pamoja na kubaini sababu za utoroshaji wa madini na kupendekeza hatua za kuchukuliwa ili kuzuia utoroshaji.

Pia, aliiagiza tume ya madini kuanzia tarehe 4 Agosti, kuhakikisha inapata taarifa za uzalishaji za migodi yote inayozalisha huku akitaka migodi husika ieleze mahali inakouzia madini yao, anayeuziwa madini hayo na kuongeza kuwa, zoezi husika linawajumuisha pia dealers.
 
Waziri wa Madini Angellah Kairuki akipokea taarifa ya Kamati kutoka kwa Mwenyekiti Sam Molle (kulia). Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti (kulia) na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (kushoto0) 

Mwenyekiti wa Tume ya Madini Profesa Idris Kikula akizungumza jambo wakati wa hafla ya kupokea taarifa ya kamati iliyochunguza mnyororo wa madini ya vito kuanzia kuzalisha hadi usafirishaji nje ya nchi pamoja na kubaini sababu za utoroshaji wa madini na kupendekeza hatua za kuchukuliwa ili kuzuia utoroshaji. Anayefuatilia kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Profesa, Simon Msanjila.

Waziri wa Madini Angellah Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na Wabunge wa Kamati ya Nishati na Madini na wabunge wengine wa Mkoa wa Manyara, Kilimanjaro na Arusha.

Waziri wa Madini Angellah Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na Wataaalm wa Wizara ya Madini, Tume ya Madini , Ofisi ya Madini Mirerani, Ofisi ya Madini Mkoa wa Arusha na Mtaalam kutoka Taasisi ya Jilojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST).

UPDATES YA AJALI: WAZIRI KIGWANGALA APATA AJALI, AFISA HABARI AFARIKI DUNIA, HELIKOPTA YAWASILI KUMCHUKUA

$
0
0

Helikopta iliyowasili kumchukua Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamis Kigwangala aliyejeruhiwa kwenye ajali hiyo.

Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamis Kigwangala akipatiwa matibabu mkoani Manyara

Na Said Mwishehe,

Globu ya Jamii.
PIGO kubwa Wizara ya Malialisi na Utalii! Hivyo ndivyo unavyoweza kuelezea baada ya kutoke ajali ya gari aliyokuwa akisafiria Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamis Kigwangala ambayo imesababisha kifo cha Ofisa Habari wa Wizara hiyo, Hamza Temba (RiP).
Katika ajali hiyo ya gari kulikuwa na watu sita akiwamo Waziri Kigwangala ambaye ameumia katika mbavu, mkono na shingo na kwa sasa anapatiwa matibabu wilayani Manyara wakati wanaandaa utaratibu wa kumhamishia yeye pamoja na majeruhi wengine katika hospitali kubwa kwa matibabu zaidi.
Akizungumza kwa njia ya simu asubuhi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara Augustino Senga amesema Waziri Dk.Kigwangala alikuwa anatokea mkoani Arusha kuelekea mkoani Dodoma na alipofika eneo hilo gari yao ikatapa ajali hiyo.
Amefafanua kwa sasa ndio yupo njiani anaelekea eneo ambalo ajali imetokea lakini kwa mujibu wa wasaidizi wake ni kwamba ajal hiyo imesababisha kifo cha mwandishi wa Waziri Kigwangala.
Alipoulizwa chanzo cha ajali hiyo Kamanda Senga amesema taarifa alizonazo ni kwamba eneo hilo kuna hifadhi ya wanyama na hivyo wakati gari ya Waziri inapita kulikuwa na mnyama barabarani na hivyo dereva akawa anajaribu kumkwepa.
"Wakati anamkwepa ndipo gari ilipomshinda dereva na kusababisha kupoteza muelekeo na hivyo kupinduka na kusababisha kifo cha mwandishi huyo na wengine kujeruhiwa akiwamo Waziri Kigwangala ambaye anapatiwa matibabu pamoja na dereva wake.
"Nikifika eneo la tukio nitakuwa na nafasi nzuri ya kutaja majina ya waliokuwamo kwenye gari hilo na hali zao kiafya. Lakini hadi sasa tunazo taarifa za kifo cha mtu mmoja ambaye ni mwandishi wa Waziri,"amesema Kamanda Senga.
Pichani juu na chini ni Gari la Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamisi Kigwangwallah ambaye amepata ajali asubuhi hii akitokea Arusha katika eneo la msitu kabla ya kijiji cha Magugu maarufu kama Mguu wa Mjerumani ama Mdori. Kwa mujibu wa mbunge wa Mbulu vijijini Mhe. Flatei Massay alieleza kuwa mtu moja ambaye ni mwandishi wa habari amepoteza maisha. Inasemekana chanzo cha ajali hiyo ni Twiga aliyekuwa anakatisha barabara mbele yao na katika kumkwepa gari likapinduka.



WAKAAZI WA SIMIYU WAFURAHIA BIDHAA NDANI YA BANDA LA TIGO MAONESHO YA NANENANE

$
0
0
Wakaazi mbali mbali wa Mkoa wa Simiyu wakipatiwa huduma na mtoa huduma waTigo, Emmanuel Pius katika harakati za kununua simu za mkononi zinazotolewa kwa punguzo la bei na kampuni ya mawasiliano ya Tigo katika maonesho ya Kitaifa ya Nane Nane yanayoendelea katika Uwanja wa Nyakabindi uliopo katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mkoa wa Simiyu.
Sehemu ya Wakaazi mbali mbali wa Mkoa wa Simiyu wakipatiwa huduma huduma kutoka kwa wafanyakazi wa kampuni ya mawasiliano ya Tigo katika maonesho ya Kitaifa ya Nane Nane yanayoendelea katika Uwanja wa Nyakabindi uliopo katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mkoa wa Simiyu.

NEC yatangaza Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika Majimbo 3 na Udiwani Kata 2

$
0
0
Hussein Makame, NEC-Dodoma 

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika majimbo matatu na wa udiwani katika kata mbili za Tanzania Bara utakaofanyika Septemba 16, mwaka huu. 

Akitangaza uchaguiz huo mjini Dodoma leo, Makamu Mwenyekiti wa NEC Jaji wa Mahakama ya Rufaa Mbarouk Salim Mbarouk alisema fomu za uteuzi wa wagombea wa Majimbo hayo zitatolewa kuanzia tarehe 13 hadi 20 Agosti, mwaka huu na uteuzi utafanyika tarehe 20 Agosti, 2018 wakati kampeni zitaanza zitaanza tarehe 21 Agosti, na kumalizika tarehe 15 Septemba, mwaka huu. 

Jaji Mbarouk alisema “Tume ilipokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye kwa kuzingatia kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, aliitaarifu Tume uwepo wa nafasi wazi za Ubunge katika Majimbo matatu” 

Aliyataja majimbo hayo kuwa ni Korogwe Vijijini, Mkoa wa Tanga kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Ndugu Stephen Hilary Ngonyani, Jimbo la Ukonga Katika Mkoa wa Dar Es Salaam na Jimbo la Monduli katika Mkoa wa Arusha .Alisema wabunge wa majimbo hayo mawili Ndugu Mwita Mwikabe Waitara na Ndugu Julius Kalanga Laizer wajiuzulu uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na hivyo kupoteza sifa za kuwa Wabunge. 

“Baada ya kupokea taarifa hizo na kwa mujibu wa vifungu vya 37 (1) (b) na 46 (2) vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi inatoa taarifa kwa Umma kuwa majimbo matatu ya Korogwe Vijijini, Ukonga na Monduli yapo wazi”, alisema. Katika hatua nyingine, Jaji Mbarouk alisema kwa kuzingatia masharti ya vifungu vya 37(1)(b) (5) na 46 (2) vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Tume inatoa taarifa wa Umma kuhusu Ratiba ya uchaguzi mdogo katika majimbo hayo. 

TAARIFA ILIYOHUSU AJALI KUTOKA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII


MRADI WA UFUGAJI SAMAKI GEREZA KWAMNGUMI, WILAYA YA KOROGWE KUBORESHWA

$
0
0
Na Lucas Mboje, Magereza;

MRADI wa ufugaji wa samaki wa Gereza Kwamngumi wenye mabwawa 30 utawekewa mkakati wa kuwezesha uzalishaji wa samaki wa kutosha ili kutoa faida kubwa kwa Jeshi la Magereza pamoja na Taifa kwa ujumla.

Hayo yamesemwa leo Agosti 4, 2018 na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Phaustine Kasike katika ziara yake ya kikazi aliyoifanya kwenye mradi wa ufugaji samaki ya Gereza Kwamngumi, lililopo Wilaya ya Korogwe, Mkoa wa Tanga.

Kamishna Jenerali Kasike amesema kuwa ziara yake ililenga kujionea maendeleo ya mradi wa uzalishaji wa samaki kwenye Gereza hilo ili kuweza kuuboresha zaidi.“Nimeshuhudia eneo hili lina fursa nzuri katika ufugaji wa samaki wa aina mbalimbali kwani mabwawa yapo yakutosha na chanzo cha maji ya uhakika nitahakikisha mradi huu unasimamiwa vizuri ili ulete tija”. Alisema Jenerali Kasike.

Kabla ya kutembelea eneo la mradi wa mabwawa ya samaki, Kamishna Jenerali wa Magereza nchini amepokea taarifa ya Mkoa ya utendaji kazi wa Jeshi hilo kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Emmanuel Lwinga pamoja na kuzungumza na Maofisa na askari wa Gereza Korogwe.

Akiwasilisha taarifa yake mbele ya Kamishna Jenerali wa Magereza, Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Emmanuel Lwinga amesema kuwa magereza ya mkoa wa tanga yana fursa ya ardhi yakutosha na yenye rutuba inayofaa kwa kilimo hivyo watajitahidi kuongeza uzalishaji wa chakula cha wafungwa na mahabusu.

“Afande Jenerali nikuhakikishie tu kuwa maagizo yaliyotolewa na Rais Dkt. Magufuli kuhusu wafungwa kujitosheleza kwa chakula, sisi mkoa wa tanga tupo tayari kutekeleza jukumu hilo”. Alisema Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa.

Mradi wa uzalishaji samaki katika Gereza Kwamugumi, Wilayani Korogwe ni mojawapo ya miradi mbalimbali ya uzalishaji mali iliyoanzishwa na Jeshi hilo ambapo ikisimamiwa kimkakati wa kibiashara inaweza kuipunguzia serikali gharama za kuhudumia Jeshi la Magereza na pia kuongeza pato la kodi kwa Taifa.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(miwani) akiangalia mabwawa ya kufugia samaki katika Gereza Kwamngumi alipotembelea leo Agosti 4, 2018, Wilayani Korogwe(kushoto) ni Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Emmanuel Lwinga.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akikagua mabwawa hayo kama inavyoonekana katika picha(kushoto) ni Mkuu wa Gereza Kwamngumi, Mrakibu wa Magereza, Christopher Mwenda.
Moja ya mabwawa ya mradi wa ufugaji wa samaki katika Gereza Kwamngumi lililopo Wilaya ya Korogwe kama yanavyoonekana katika picha(Picha zote na Jeshi la Magereza).

TATIZO LA WATOTO KUTELEKEZWA WILAYANI KAKONKO LABAINIKA KUWA BADO SUGU

$
0
0
Na Rhoda Ezekiel Kigoma. 

TATIZO la Wazazi kutelekeza watoto Wilayani Kakonko Mkoani kigoma limekuwa sugu jambo ambalo linapelekea watoto wengi kukosa haki yao ya kupata elimu kama watoto wengine.

Akizungumza Mwalimu Mkuu msaidizi wa shule ya Msingi Churazo ,Silvia Mgina, alisema tangu mwaka 2014 hadi sasa wamepokea watoto 128 waliotelekezwa na wazazi wao na kushindwa kupelekwa shule; hata hivyo kwa sasa wamekwisha waandikisha watoto hao.

Hayo yalibainika jana wakati wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi katika jimbo la Buyungu, baada ya Mbunge wa jimbo la Nzega mjini Hussein Bashe alipobaini kuwepo na watoto watatu katika Kijiji cha Churazo Wilayani humo,January Magaruka (13), Erick Magaruka (11),John Magaruka (9) waliotelekezwa na wazazi wao na kulelewa na Askari Mgambo katika Kijiji hicho.

Ambapo aliwachukua watoto hao na kuwakabidhi kwa Mbunge wa Vijana wa Mkoa wa kigoma , Zainabu Katimba na Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo kuomba wawalee watoto hao na kuhakikisha wanapata elimu na malezi bora ." Nikienda katika mikutano ya kampeni huwa napenda kuzungumza na watoto ili kujua matatizo waliyonayo. 
 
Na nimebaini watoto kadhaa Wilayani Kakonko wamekimbiwa na wazazi wao na wengine wanaishi katika mazingira magumu, jamii na viongozi wa Wilaya hii wanatakiwa kufanya kazi ya ziada kuhakikisha watoto wa aina hii wanapatiwa elimu", alisema Bashe.
 Mbunge wa jimbo la Nzega mjini Hussein Bashe na Mbunge wa Viti maalumu wa vijana Mkoani Kigoma Zainabu Katimba, akikabidhi fedha za kuwanunulia nguo za shule za watoto waliotelekezwa na Wazazi wao kwa mwalimu Mkuu msaidizi Silvia Mgina.

VYUO VYA POLISI VYAWEKA MIKAKATI KUBORESHA ELIMU

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akiimba wimbo pamoja na Askari wakati wa kikao chake na Askari wanafunzi katika Chuo cha Polisi Zanzibar wakati wa ziara yake. Kulia kwake ni Kamishna wa Polisi Zanzibar Mohamed Hassan Haji na kushoto ni Mkuu wa Utawala na Fedha Kamisheni ya Polisi Zanzibar Faustine Shilogile.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana na Maofisa wa Polisi Kamisheni ya Zanzibar wakati wa Ziara yake inayoendelea katika Vyuo vya Polisi hapa nchini kwa lengo la kuboresha elimu inayotolewa na vyuo hivyo
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na Mafundi wa Nguo za Polisi waliopo katika Kiwanda cha Polisi cha kushona nguo Kamisheni ya Polisi Zanzibar wakati wa Ziara yake inayoendelea katika Vyuo vya Polisi hapa nchini kwa lengo la kuboresha elimu inayotolewa na vyuo hivyo (Picha na Jeshi la Polisi).

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amewataka Wakufunzi wa Vyuo vya Polisi vya Dar es Salaam na Zanzibar kuhakikisha wanawafundisha Askari Polisi Wanafunzi waliopo katika vyuo hivyo kwa kuzingatia mitaala iliyotolewa ili wanapotoka waweze kuwatumikia Wananchi na kupunguza uhalifu hapa nchini.

IGP Sirro ameyasema hayo kwa nyakati tofauti wakati wa ziara yake katika vyuo hivyo ambapo alizungumza na Wakufunzi pamoja na Askari wanafunzi wanaosomea vyeo mbalimbali ambapo lengo la ziara hiyo ni kukagua muenendo wa mafunzo katika vyuo vya Polisi.

Amesema lengo la mafunzo yanayotolewa katika vyuo hivyo yanapaswa kutolewa kwa weledi ili kila Askari anayehitimu aweze kupata maarifa ambayo yatawezesha kufanya kazi za Polisi vyema jambo ambalo litaendelea kupunguza uhalifu hapa nchini.

“Kila mkufunzi anapaswa ahakikishe lile somo analolifundisha wanafunzi wake wanalielewa ili kusudi kama ni Ofisa, Mkaguzi na Kiongozi mdogo ndani ya Jeshi la Polisi anafanya kazi kwa kufuata ile misingi iliyopo” Alisema Sirro.

Kwa Upande wake Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Anthony Rutta amesema lengo la mafunzo katika Chuo hicho ni kuhakikisha kila Askari anayatambua majukumu yake ili kupunguza uhalifu hapa nchini na watahakikisha ukakamavu na nidhamu inazingatiwa ili kuwa na Jeshi lenye kufuata kanuni na taratibu zilizopo.

Naye Mkuu wa Chuo cha Polisi Zanzibar Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Geofrey Kamwela amesema Chuo hicho kinakabiliwa na Changamoto mbalimbali zikiwemo za uchakavu wa miundombinu yakiwemo majengo na bwalo la Chakula ambapo IGP Sirro aliahidi kutuma fedha za awali kwa ajili ya ujenzi wa bwalo la kulia chakula chuoni hapo.

Kamwela alisema hivi sasa wanaendelea kutekeleza mradi wa kuweka mfumo wa Tehama ambao utawezesha wanafunzi kujisomea na kupata matokeo yao kwa njia ya mtandao jambo ambalo litawafanya kwenda kisasa katika utoaji wa elimu chuoni hapo.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini yupo katika ziara ya kukagua mafunzo yanayoendelea katika vyuo vya Polisi hapa nchini ili kuhakikisha kuwa mafunzo yanayotolewa yanawajenga Maofisa na Askari kufikia malengo yaliyokusudiwa ya kupunguza uhalifu hapa nchini.

WAPINZANI WABISHANE KWA HOJA WAMEFANYA NINI JIMBO LA BUYUNGU MPAKA SASA-NAPE NNAUYE

$
0
0
Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

MBUNGE wa jimbo la Mtama Nape Nnauye amewataka Wapinzani kuja kubishana kwa hoja mambo gani waliyoyafanya katika jimbo la Buyungu na CCM waliyoyafanya kuwaletea miradi ya maendeleo Wananchi wa Buyungu na sio kuwadanganya Wananchi wa Buyungu.

Pia amesema Upinzani wasipobadilika siasa Wanazozifanya kwa sasa upinzani utafutika kwa kuwa Wananchi wanaona kazi inayofanywa na serikali iliyoko madarakani na wasipo badiliku na kuacha kuisema vibaya Watakimbiwa na Viongozi wote na wanachama.

Nnauye amesema hayo leo katika kijiji cha Nyakayenzi kata ya Kasuga,Wilayani kakonko wakati akimnadi mgombea wa chama hicho, ambapo alisema wapinzani wanatakiwa kubishana kwa hoja kwa kutangaza mazuri waliyoyafanya kwa kipindi cha miaka mitatu waliyoaminiwa na wananchi wa Buyungu,  ni miradi ipi walioileta na vitu walivyovifanya.

Amesema nje ya miradi iliyotekelezwa na serikali ya chama cha mapinduzi wakati wa utawala wa mgombea ambae anagombea kiti hicho hakuna ambacho walikifanya Chadema, na wanatakiwa kuacha kuwadanganya wananchi kwamba wao wamefanya kwakuwa hawana serikali na serikali iliyopo madarakani ni ya CCM.

Amesema kwa kipindi ambacho Christopher Chiza amekuwa madarakani ameweza kuleta miradi ya kilimo cha mpunga katika skimu za umwagiliaji za Katengera na Ruhiti pamoja na umeme na miradi ya maji ambapo amewaomba Wananchi wamchague Chiza aweze kuendeleza miradi ambayo haijakamilika.
 MBUNGE wa jimbo la Mtama Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa 
kijiji cha Nyakayenzi kata ya Kasuga,Wilayani kakonko wakati akimnadi mgombea Ubunge wa chama hicho Ndugu Christopher Chiza
Baadhi ya Wananchi na wafuasi wa chama cha Mapinduzi wakifuatilia mkutano wa kampeni ,wakati Mbunge wa jimbo la Mtama Nape Nnauye alipokuwa akimnadi mgombea Ubunge wa chama hicho Ndugu Christopher Chiza katika kijiji cha Nyakayenzi kata ya Kasuga,Wilayani kakonko mkoani Kigoma.

MAVUNDE AMTOA MACHOZI YA FURAHA KIJANA MWENYE ULEMAVU MWANACHUO WA UDOM

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde leo ametimiza ahadi ya kumpatia Kijana Dominic Oscar Mbele Mwanachuo wa Chuo kikuu cha Dodoma pikipiki ya matairi matatu (bajaj) ili kumsaidia kuyafikia maeneo mbalimbali kwa haraka na kwa urahisi.

Bajaj hiyo imekabidhiwa leo na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu) Mh Stella Ikupa ambaye amemshukuru Mh Mavunde na wote waliochangia kwa moyo wao wote na kutoa rai kwa jamii kusaidia watu wenye ulemavu badala ya kuliachia jukumu hilo serikali na viongozi peke yako.

Akishukuru baada ya kukabidhiwa Bajaj hiyo Ndg Dominic Mbele ambaye ni Mwanachuo wa Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) anayesomea Shahada ya Kwanza ya masuala ya Kompyuta amemshukuru sana Mh Mavunde na wote waliomchangia kwa moyo wa kipekee wa kumsaidia kupata usafiri huo na kuahidi kuwaombea kwa Mungu ili Mungu awazidishie.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde akimkabidhi kijana Dominic Oscar Mbele ambaye ni Mwanachuo wa Chuo kikuu cha Dodoma pikipiki ya matairi matatu (bajaj) ili imsaidie kuyafikia maeneo mbalimbali kwa haraka na kwa urahisi.
kijana Dominic Oscar Mbele ambaye ni Mwanachuo wa Chuo kikuu cha Dodoma akimshukuru Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde kwa kumpatia pikipiki ya matairi matatu (bajaj) ili imsaidie kuyafikia maeneo mbalimbali kwa haraka na kwa urahisi.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu) Mh Stella Ikupa akimpa mkono wa pongezi kijana Dominic Oscar Mbele ambaye ni Mwanachuo wa Chuo kikuu cha Dodoma kwa kufanikiwa kuipata baiskeli hiyo (bajaj) ,iliyotolewa na Mh Mavunde.Aidha Mh Ikupa  rai kwa jamii kusaidia watu wenye ulemavu badala ya kuliachia jukumu hilo serikali na viongozi peke yako.

MA-DC MKOANI TABORA WAAPISHWA NA KUPEWA MAAGIZO

$
0
0

NA TIGANYA VINCENT ,TABORA

WAKUU wa Wilaya ya Tabora na Uyui wametakiwa kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii na weledi ili kuhakikisha wanaondoa matatizo mbalimbali katika maeneo yao ya utawala ili kuwasaidia wananchi kuwa na mazingira ya kujiletea maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora baada ya kuwaapisha Mkuu wa Wilaya ya Tabora Komanya Kitwala na yule wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya baada ya kuteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kushika wadhifa huo. Alisema wanatakiwa kuchapa kazi kwa bidii wakati wa kuwatumikia wananchi ili kuheshimu imani kuwa aliyowapa Rais ya kuwateua kuongoza maeneo hayo.

Mwanri alisema watakiwa kusimama katika nafasi zao kwa kutumia Sheria na taratibu zilizopo katika kukabiliana na matatizo kama vile mimba na ndoa za utotoni , utoro, uharibifu wa mazingira na uhalifu wa aina mbalimbali ili kuondoa mambo hayo ambayo yanakwamisha maendeleo ya Mkoa huo.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora aliwataka Wakuu hao wapya na wale waliopo kuhakikisha wanawahimiza wananchi Mkoani humo kukarabati na kujenga nyumba nzuri na za kisasa ili Mkoa huo nao uonekana kuwa wananchi wake wana makazi mazuri na sio kuendelea kukaa katika nyumba ambazo sio nzuri.

Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya akitoa neno la shukurani mada baada ya kuapishwa leo.
Mkuu wa Wilaya ya Tabora Komanya Kitwala akitoa neno la shukurani mada baada ya kuapishwa leo. 

Serikali Kuajiri Walimu 2000 wa Masomo ya Sayansi-Naibu waziri Kakunda

$
0
0
Na. Ofisa Habari Mufindi 

Naibu Waziri Ofisi ya Rais (OR-TAMISEMI) Mhe Joseph Kakunda, amesema serikali ipo katika hatua a mwisho kukamilisha mchakato wa kuajiri waalimu 2000 wa masomo ya sayansi ili kupunguza changamoto ya uchache wa walimu wa kada hiyo katika shule za umma nchini

Mhe. Kakunda ameyasema hayo katika shule kongwe ya Sekondari Mdabulo, akiwa kwenye ziara ya kikazi Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, baada ya Mkuu wa shule hiyo Bw. George Mgomba, kueleza changamoto ya uhaba wa walimu wa sayansi katika shule yake.

“Serikali kwa mwaka huu inaendelea na mchakato wa kuajiri walimu wa sayansi wapatao 2000 hivyo, taarifa yenu naichukua mwenyewe na kuipeleka kwa Mhe. Waziri Jafo, bila shaka walimu wawili 02 mnaowahitaji katika shule yenu mtawapata na hili nalibeba kwa ajili ya utekelezaji” alisisitiza Waziri Kakunda

Aidha, Mhe. Kakunda ameridhishwa na majengo mapya ya Shule hiyo iliyojengwa kwa mfumo wa “Force Account” kwa kuzingatia maelekezo ya kitaifa baada ya kujionea madarasa na mabweni mazuri hivyo, amesisitiza utaratibu uliotumika wa kujenga kwa njia ya Force Account uendeleee hata wakati wa mradi wa ujenzi wa mabweni utakapoanza, ambapo serikali tayari imetenga Jumla ya Tsh Milioni 100 kwa shule ya Sekondari Mdabulo.


Naibu waziri Kakunda, akiongozwa na Mkuu wa shule ya Sekondari Mdabulo kukagua madarasa na mabweni mapya yaliyojengwa SerikaliNaibu waziri Kakunda akizungumza na wananchi pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mdabulo.


Wananchi wakimiliki nyumba ni maendeleo ya Kiuchumi

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Mkurugenzi wa Fedha na Masoko wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) AlexenderNg'winamila, amesema kuwa mikopo ya nyumba kwa wananchi ikitolewa na wananchi hao wakamiliki nyumba hizo ni maendeleo katika ukuaji wa uchumi.

Alexander aliyasema hayo wakati akizindua kozi ya mafunzo kwa wafanyakazi benki kuhusiana utoaji wa mikopo ya nyumbani kwa wananchi.
Amesema kuwa katika kuelekea uchumi wa viwanda umiliki wa nyumba ni muhimu kwa kufanya wananchi wanaofanya uchumi huo kuwa na makazi bora.

Alexander amesema kuwa Taasisi ya Benki Nchini (TIOB) kwa kushirikiana Taasisi ya Utoaji wa Mikopo ya Nyumba (TMRC) katika kuandaa kozi fupi kwa ajili ya wafayakazi wa Benki kupata mbinu katika utoaji wa mikopo ya nyumba.Aidha amesema kuwa baada ya mafunzo hayo benki zikifanya kwa ufanisi zitaongeza wateja wa mikopo ya nyumba.

Nae Afisa Mtendaji Mkuu wa TMRC, Ocar Mgaya amesema mafunzo hayo yalishatolewa katika chuo cha BOT cha mwanza kwa wafanyakazi 300.Katika utoaji mikopo taasisi kulikuwa na changamoto kwa kutoa baadhi ya taasisi lakini tumeanza kutoa kwa taasisi zote za fedha ziweze kupesha mikopo ya nyumba.

Mkurugenzi wa Fedha na Masoko wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT)Alexender Ng'winamila akizungumza katika uzinduzi wa mafunzo ya utoaji mikopo ya nyumba kwa watumishi wa taasisi za fedha uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TMRC, Ocar Mgaya akizungumza kuhusiana na utaoji wa mikopo ya benki kwa ajili ya ukopeshaji wa mikopo ya nyumba kwa wananchi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi za Benki Nchini (TIOB) Patrick Mususa akizungumza juu ya uandaji wa mafunzo kwa wafanyakazi wa benki katika utoaji wa mikopo ya nyumba kwa wananchi.

WAZIRI LUGOLA AZINDUA BARAZA JIPYA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI, ATAKA LIDHIBITI AJALI NCHINI

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akimkabidhi taarifa za Baraza jipya la Taifa la Usalama Barabarani, mjumbe aliyeteua, Profesa Zakaria Mganilwa. Katikati ni Katibu Mtendaji wa Baraza hilo ambaye pia ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Fortunatus Musilimu. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akiyasoma majina ya wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dodoma leo. Lugola aliwataka wajumbe hao wahakikishe wanadhibiti ajali za barabarani nchini. Kushoto meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali, Jacob Kingu. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na wajumbe wa Baraza jipya la Taifa la Usalama Barabarani mara baada ya Baraza hilo kuzinduliwa katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dodoma leo. Lugola aliwataka wajumbe hao wahakikishe wanadhibiti ajali za barabarani nchini. Kushoto meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali, Jacob Kingu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia meza kuu), akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Jacob Kingu alipokua akifafanua masuala ya usalama barabarani, kabla ya Waziri Lugola kulizindua Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, katika ukumbi wa wizara, jijini Dodoma leo

MAKAMU WA RAIS AONGOZA KIKAO KAMATI YA MAZINGIRA YA BARAZA LA MAWAZIRI MJINI DODOMA

$
0
0


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza kikao cha Kamati ya Mazingira ya Baraza la Mawaziri kwenye ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza kikao cha Kamati ya Mazingira ya Baraza la Mawaziri kwenye ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza kikao cha Kamati ya Mazingira ya Baraza la Mawaziri kwenye ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

RAIS DKT. MAGUFULI AMPOKEA WAZIRI KIGWANGALA KATIKA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA MWALIMU JULIUS NYERERE JIJINI DAR JIONI HII

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishirikiana na Madaktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Wafanyakazi wa Kiwanja cha Ndege cha Mwalimu Julius Nyerere kumshusha kutoka kwenye ndege Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye alijeruhiwa katika ajali ya gari mkoani Manyara. Ndege hiyo iliwasili majira ya jioni katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishirikiana na Madaktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Wafanyakazi wa Kiwanja cha Ndege cha Mwalimu Julius Nyerere kumshusha kutoka kwenye ndege Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye alijeruhiwa katika ajali ya gari mkoani Manyara. Ndege hiyo iliwasili majira ya jioni katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakati akisubiri kumpokea Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye alipata ajali ya gari mkoani Manyara.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa ndani ya gari la wagonjwa kwa ajili ya kupelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Ndege maalumu iliyombeba Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye alijeruhiwa katika ajali ya gari mkoani Manyara ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere kutokea mkoani Arusha majira ya jioni.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mara baada ya kumpokea Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye alijeruhiwa katika ajali ya gari mkoani Manyara.

DK.SHEIN ATEMBELEA CHUO KIKUU CHA UDAYANA MJINI BALI,INDONESIA.

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipofuatana na mwenyeji wake Mkuu wa Chuo Kikuu cha Udayana Prof.Dr.Ida Bagus Wyasa Putra alipotembelea Chuoni hapo baada ya mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Chuo hicho kiliopo Jambaran Bali (TBC) alipokuwa katika ziara ya kikazi Nchini Indonesia kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Mohamed Jusuf Kalla,{Picha na Ikulu.] 03/08/2018.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akivalisha Shada la mauwa wakati wa mapokezi na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Udayana Prof.Dr.Ida Bagus Wyasa Putra katika Mji wa Bali Nchini Indonesia alipotembela Chuoni hapo akiwa na ujumbe wake katika ziara ya kikazi Nchini Indonesia kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Mohamed Jusuf Kalla,{Picha na Ikulu.] 03/08/2018.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akimuuliza suala Mkuu wa Chuo Kikuu cha Udayana Prof.Dr.Ida Bagus Wyasa Putra wakati wa mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Chuo hicho kiliopo Jambaran Bali (TBC) alipokuwa katika ziara ya kikazi Nchini Indonesia kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Mohamed Jusuf Kalla,{Picha na Ikulu.] 03/08/2018.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na Viongozi,Wahadhiri na Wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Udayana kiliopo Jambaran Bali (TBC)alipotembelea Chuoni hapo akiwa na Ujumbe wake katika ziara ya kikazi Nchini Indonesia kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Mohamed Jusuf Kalla,{Picha na Ikulu.] 03/08/2018.
Share
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images