Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109999 articles
Browse latest View live

SPIKA WA BUNGE APOKEA BARUA YA KUJIUZULU KWA MBUNGE WA MONDULI


MBWA HAJAPOTEA ALIKUWA MAFUNZONI BWALO LA POLISI OYSTERBAY - ACP MWAKALUKWA

MWANAHABARI SHADRACK SAGATI KUAGWA KESHO VIWANJA VYA MNAZI MMOJA

$
0
0
Aliyekuwa Ofisa Habari wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Shadrack Sagati enzi za uhai wake.

Dkt. Shein akutana na kufanya mazungumzo na Meya wa Jimbo la Gorontalo na Kiongozi wa Kampuni ya gesi nchini Indonesia

$
0
0
Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar 
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo amefanya mazungumzo na Makamo wa Rais wa Indonesia Muhammad Jusuf Kalla ambapo katika mazungumzo hayo viongozi hao walisisitiza haja ya kuzidisha ushirikiano katika sekta za maendeleo. Viongozi hao walifanya mazungumzo katika Ofisi ya Makamo wa Rais wa Indonesia Muhammad Jusuf Kalla iliyopo mjini Jakarta Indonesia, ambapo mkutano huo pia ulihudhuriwa na Mawaziri wa pande zote mbili. 
 Katika mazungumzo hayo Rais Dk. Shein alimpongeza Makamo wa Rais wa nchi hiyo kwa muwaliko wake huo muhimu ambao unaimarisha uhusiano na ushirikiano wa kihistoria uliopo kati ya Indonesia na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jumla na makhsusi kwa Zanzibar. 
 Dk. Shein alimueleza Makamo huyo wa Rais wa Indonesia kuwa Tanzania inajivunia kwa kiasi kikubwa uhusiano na ushirikiano wa kihistoria uliopo baina ya pande mbili hizo ambao umeasisiwa na viongozi wakuu wa nchi hizo tokea miaka ya sitini na kuahidi kuwa utaendelezwa. 

Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Meya wa Jimbo la Gorontalo Prof.Nelson Pamalingo wakati wa mkutano na Meya huyo yaliyogusia zaidi katika ushikiano wa kilimo cha Minazi. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa Hoteli ya  Borobudur Mjini Jakarta, Indonesia katika ziara ya kikazi kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Mohammed Jusuf Kalla.
 Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) na Ujumbe wake katika mazungumzo na  Meya wa Jimbo la Gorontalo Prof. Nelson Pamalingo (kulia) wakati wa mkutano na Meya huyo yaliyogusia zaidi katika ushikiano wa kilimo cha Minazi hafla ya mazungumzo hayo ilifanyika katika ukumbi wa Hoteli ya  Borobudur Mjini Jakarta,Indonesia katika ziara ya kikazi kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Mohammed Jusuf Kalla
Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Meya wa Jimbo la Gorontalo Prof.Nelson Pamalingo(katikati) na Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi katika Ujumbe wake Rais (kushoto) na Viongozi waliuongama na Mstahiki Meya  wakiwa katika Picha ya pamoja mara baada ya mazungungumzo ya pamoja yaliyofanyika  katika ukumbi wa Hoteli ya  Borobudur Mjini Jakarta,Indonesia katika ziara ya kikazi kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Mohammed Jusuf Kalla.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Kiongozi wa Kampuni ya Mafuta na Gesi ya Pertamina  ya Jakarta Nchini Indonesia  Bw.Daniel S.Purba akiwa na ujumbe wa kampuni hiyo walipofika  kwa mazungumzo  katika ukumbi  wa  Ofisi ya Jumuiya ya   Wafanyabiashara na Wenyeviwanda ya Indonesia (KADIN)   Mjini Jakarta Indonesia Rais akiwa katika ziara ya kikazi ya siku saba kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Mhe.Mohammed Jusuf Kalla


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimsikiliza Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Malaysia pia akiwakilisha Tanzania Nchini Indonesia Mhe.Dkt Ramadhani Kitwana Dau (wa pili kulia)wakati wa mazungumzo na Uongozi wa Kampuni ya Mafuta na Gesi ya Pertamina ya Jakarta Nchini Indonesia,(hawapo pichani ) katika Ukumbi wa Ofisi ya Jumuiya ya   Wafanyabiashara na Wenyeviwanda ya Indonesia (KADIN)   Mjini Jakarta Indonesia ,katika ziara ya kikazi ya siku saba kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Mhe.Mohammed Jusuf Kalla
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akiwa na ujumbe wake katika mazungumzo na Uongozi wa Kampuni ya Mafuta na Gesi ya Pertamina  ya Jakarta Nchini Indonesia,unaoongozwa na Kiongozi Daniel S.Purba (wa pili kulia) mazungumzo hayo yalifanyika jana katika ukumbi wa  Ofisi ya Jumuiya ya   Wafanyabiashara na Wenyeviwanda ya Indonesia (KADIN)    Mjini Jakarta Indonesia ,katika ziara ya kikazi ya siku saba kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Mhe.Mohammed Jusuf Kalla. Picha na Ikulu.

BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO 01.08.2018

RAIS MAGUFULI AAPISHA WAKUU WA MIKOA, MAKATIBU WAKUU, MAKATIBU TAWALA WA MIKOA NA MANAIBU KATIBU WAKUU IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Brigedia Jenerali Nicodemus Elias Mwangela kuwa mkuu wa mkoa wa Songwe  kwenye hafla iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 1, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli   akimuapisha Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera  kwenye hafla iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 1, 2018 .
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akimuapisha Ally Salum Hapi kuwa mkuu wa mkoa wa Iringa  kwenye hafla iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 1, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akimuapisha  Andrew Wilson Massawe kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu kwenye hafla iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 1, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akimuapisha Jilly Elibariki maleko kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara wenye hafla iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 1, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akimuapisha Kalolina Albert Mthapula kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara  kwenye hafla iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 1, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akimuapisha  Dkt. Jim james Yonazi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano)  kwenye hafla iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 1, 2018
 Viongozi wa dini wakiomba dua kwenye hafla ya kuapisha wateule mbalimbali iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 1, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiongea baada ya kuapisha viongozi wateule  kwenye hafla iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 1, 2018.
Picha na IKULU
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Jaji Kiongozi Dkt. Fereshi wakiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Wakuu, Naibu makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa na Katibu wa Mikoa walioapishwa kwenye hafla iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 1, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Jaji Kiongozi Dkt. Fereshi wakiwa katika picha ya pamoja Wakuu wa Mikoa wa Zamani na   walioapishwa kwenye hafla iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 1, 2018.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TAWLA yazungumzia vikwazo vinavyozuia ongezeko la ushiriki na uwakilishi wa wanawake katika uongozi na shughuli za siasa

$
0
0
Josephine Arnold Wakili wa Chama cha Wanasheria wanawake TAWLA akifungua semina ya matekelezo ya Mradi wenye lengo la kuchangia ongezeko la ushiriki na uwakilishi wa wanawake katika ngazi mbalimbali za uongozi na shughuli za kisiasa kwa ujumla wake 

Moja ya Shughuli ndani ya mradi huo ni pamoja na kumiarisha uwezo wa vikundi / Majukwaa ya wanawake katika ngazi ya wilaya za mkoa wa Dar es salaam ili waweze kuongelea changamoto zinazowazuia kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za kisiasa, Walioshiriki katika semina hiyo ni vikundi na majukwaa ya wanawake katika ngazi za kata na wilaya za mkoa wa dar es salaam. Semina hiyo imefanyika kwenye hoteli ya New Africa leo.
Isabella Nchimbi Mwanasheria wa Chama cha Wawanasheria Wanawake akitoa mada katika semina hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam.
Josephine Arnold Wakili wa Chama cha Wanasheria wanawake TAWLA na Bi. Sara Kinyaga wakifurahia jambo kabla ya kuanza kwa semina hiyo.
Mwezeshaji wa Semina hiyo Sara Kinyaga akitoa mada katika semiha hiyo
Picha mbalimbali zikionyesha baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa katika semina hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya New Africa leo.

Fichueni wale wote wanaofanya ujanja katika fedha za miradi-Jaffo

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI )Selemani Jaffo amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala walioapishwa na Rais Dk. John Magufuli wakasimamie miradi yote ya serikali na kuwafichua wale wote wanaofanya ujanja katika fedha za miradi zinazotengwa na serikali.

Pia ametoa siku 10 kwa mikoa yote ambayo bado haijawasilisha mpaka leo ripoti ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) kwasilisha katika siku hizo ili shughuli zingine za maendeleo ziendelee.Amsema bado wapo watendaji wanafanya kazi kwa mazoea  kwa kura fedha ya serikali bila ya wogo wowote ni lazima wawajibike  wanaofanya hivyo kwa wakuu wa mikoa na makatibu tawala  kuwafichua walafi hao.

Jaffo amesema serikali imeweka vipaumbele vyake katika  baadhi ya sekta kama vile, Sekta ya afya, elimu na barabara hivyo amewataka wateule hao wakasimamie miradi hiyo ambayo ina umuhimu mkubwa kwa wananchi.Hayo aliyasema  Jafo  wakati alipokutana na Wakuu wa Mikoa Wapya na Makatibu Tawala Mikoa mara baada ya kuapishwa  na kuwataka kufanya kazi kwa uadilifu na kuwa na nidhamu ya muda  na kujua kila mtu mipaka yake.

Amesema wadhifa waliopewa ni mkubwa hivyo kila wakati wanatakiwa wanyamazishe vilio vya wananchi pale wanapopata na changamoto ya aina yeyote.“Hakunba atakayenyamazisha kelele za wananchi isipokuwa ni Wakuu wa Mikoa pamoja na Katibu Tawala “alisema Jaffo.Pia alisema katika suala la elimu kila shule ya msingi na sekondari inatakiwa kuwa na walimu wa kutosha na kusiwe na walimu wachache na sehemu nyingine kuwe na walimu wengi.

Akizungumzia miundombinu ya barabara alisema, Tanzania inaingia katika mfumo wa viwanda hivyo mfumo wa barabara kwa mijini na vijijini unatakiwa kukamilika ili viwanda viweze kufanya kazi yake vile inavyoitakiwa.“Maagizo hayo yote ni ya kwenu hivyo mnatakiwa muyachukue ili mukayafanyie kazi vile inavyotakiwa kufanywa”alisema.

Vilevile ,aliwataka viongozi hao waache utamaduni wa kukaa ofisini na badala yake watembelee miradi yote inayosimamiwa na Halmashauri ili kuondoa ubadhirifu . Wakati huo huo,Katibu Mkuu wa TAMISEMI Injinia Musa Iyombe ,aliwataka Wakuu wa Mikoa hiyo wafanye kazi kwa kufuata maadili yanavyotaka.“Katika ufanyaji wenu wa kazi msivuke mipaka mtaanza kuleta shida ,ni lazima kila kiongozi asome mipaka yake ya kazi “alisema Iyombe
 Waziri  wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi)Selemani Jaffo akizungumza wakuu wa mikoa wapya pamoja na makatibu tawala mara baada ya kuapishwa kwa ajili ya kuwapa misingi ya kufanya kazi katika vituo vyao katika hafla iliyofanyika Ofisi za Tamisemi jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tamisemi, Josephat Kandege akizungumza namna ya kushughulika katika miundombinu ya mikoa katika mkutano wa wakuu wa mikoa wapya pamoja na makatibu Tawala iliyofanyika  katika Ofisi za Tamisemi jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tamisemi, Mhandisi Mussa Lyombe akizungumza juu ya mipaka ya kazi kwa wakuu wa mikoa na makatibu tawala wapya katika iliyofanyika  katika Ofisi za Tamisemi jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wakuu wa Mikoa wapya waliopishwa
Baadhi ya Makatibu Tawala walioapishwa

Wadau waiomba serikali kuwekeza katika Lugha ya Kiswahili

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
Wadau wa elimu wameiomba serikali kuwekeza katika lugha ya kiswahili ili kiweza kufundisha wanafunzi na kuelewa pamoja kufaulu masomo kwa kutumia lugha hiyo.

Wakizungumza katika mdahalo wa lugha ya Kiswahili kuhusu kutumika katika masomo yote kwa shule ya msingi ,Sekondari  na vyuo vikuu wamesema kunahitaji uwekezaji wa lugha ya kiswahili licha wanafunzi wanafaulu masomo yanayofundiahwa kiingereza kuliko somo la Kiswahili.

Mdahalo uliandaliwa na Haki Elimu kwa kushirikisha wadau namna ya lugha ya kiswahili kutumika katika kufundishia.

Akizungumza katika ufunguzi wa mdahalo huo Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Haki Elimu Dk.John Kalage amesema kuwa mjadala huo ni muhimu kwa nchi katika kutathimini kwa kina nafasi ya lugha ya kiswahili ya kujifundishia na kujifunzia katika lengo la utoaji wa elimu nchini na dira ya nchi ya kuwa la Uchumi wa kati ifikapo 2025.

Amesma mdahalo huo ni kuishauri serikali katika kufikia mwafaka juu ya suala la lugha ya kiswahili kutumika katika kufundishia na kujifunzia.

Kalage amesema nyenzo muhimu katika maendeleo ya ustawi wa taifa lolote lugha ya kufundishia ndio nyenzo kubwa ya kuhamisha maarifa ,Stadi,Ujunzi na tamadini kutoka kizazi kimoja kwenda kingine.

Kwa upande wa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kandege amesema kiswahili kiwekezwe kama uwekezaji mingine katika nchi.
Amesema kuwa na lugha ya kiingereza kina umuhimu wake na sio kuacha kabisa.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika Haki Elimu, Dk. John Kalage akifungua mdahalo wa lugha ya Kiswahili juu ya kutumika katika masomo yote kwa shule ya msingi, Sekondari  na vyuo vikuu  jijini Dar as Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
 Mhadhiri kutoka chuo Kikuu cha Dar as Salaam Dkt.Michael Kadeghe akiwasilisha  mada katika mdahalo wa lugha ya Kiswahili juu ya kutumika katika masomo yote kwa shule ya msingi, Sekondari  na vyuo vikuu jijini Dar as Salaam.
 Mhadhiri wa chuo Kikuu cha Dar as Salaam Profesa Martha Qorro akiwasilisha mada katika mdahalo wa lugha ya Kiswahili juu ya kutumika katika masomo yote kwa shule ya msingi, Sekondari  na vyuo vikuu jijini Dar as Salaam.
Sehemu ya wadau mbalimbali  wa elimu  wakiwa katika mdahalo wa lugha ya Kiswahili juu ya kutumika katika masomo yote kwa shule ya msingi, Sekondari  na vyuo vikuuuliofanyika jijini Dar as Salaam.

Mimi Msafiri by Gaby Kababa Nkomba & Dekula Band in Stockholm, Sweden

NSSF KUSHIRIKI MAONESHO YA WAKULIMA NANE NANE MKOANI SIMIYU

$
0
0
Shirika la la Taifa la Hifadhi ya jamii NSSF linashiriki kwenye maonesho ya wakulima NANE NANE yaliyoanza tarehe moja mwezi wa nane katika viwanja vya Nyakabunda mkoani Simiyu. 

Kaimu meneja Uhusiano na Masoko wa NSSF Salim Khalfan amesema kuwa mwaka huu wameshiriki tena ambapo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye banda lao kwa ajili ya kujua masuala mbali mbali. 

“Tumejipanga vyema kwenye maonesho ya mwaka huu, tunaomba wananchi wajitokeze kwa wingi katika banda letu kujionea mambo mbali mbali tynayoyafanya ” Khalfan amesema kuwa katika banda la NSSF wananchi wataweza kupata elimu juu ya mafao yanayotolewa na Shirika kama vile mafao ya matibabu ambayo kwa kiasi kikubwa yamesaidia sana kuimarisha sekta ya afya hapa nchini. 

Pia amesema kuwa kutakuwepo na zoezi la uandikishaji kwa wananchi ambao wako kwenye sekta isiyo rasmi na wataweza kujiunga na NSSF kufaidika na mafao yanayotolewa. “Kutakuwepo na zoezi la kuandikisha wanachama wapya kwenye maonesho hayo ya nanenane hivyo ni wakati pekee kuja kujiandikisha “Alisema Khalfan. 

Tunapoazimisha sikukuu ya wakulima nchini ,NSSF inatoa fursa mbali mbali kwa wakulima zikiwemo mkulima kuweza kujiandikisha na kuchangia kwa kiasi cha shilingi elfu ishirini tu kila wmezi na kufaidika na mafao yanayotolewa baada ya kukidhi sifa stahili za kuwa mwananchama wa Hiari. 

Huu ni muendelezo wa Shirika la NSSF kushiriki katika maonesho ya wakulima ya nane nane ambayo kwa namna moja ama nyingine yanasaidia kutangaza fursa mbali mbali kwa wakulima nchini. 


Imetolewa na Kitengo cha Uhusiano na Masoko 
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF

CHANGAMOTO YA SOKO YAPELEKEA WAKULIMA WA ZAO LA KOROSHO MKINGA KUUZA NCHINI KENYA

$
0
0

KUTOKUWEPO kwa soko la uhakika wa zao la Korosho wilayani Mkinga mkoani Tanga kumepelekea baadhi ya wakulima kulazimika kuyasafirisha nchini Kenya kwa njia za panya kwa ajili ya kuuza ili waweze kupata fedha papo kwa papo badala ya kuuza kwa mfumo wa stakabadhi ghalani ambako wakati mwengine malipo yanachelewa kuwafikia.

Hayo yalibainishwa na Katibu wa Kikundi Kinachojushughulisha na Uzalishaji wa miche ya Korosho kilichopo Kijiji cha Horohoro kilichopo mpakani mwa Tanzania na Kenya (Kikohoki) Khalfan Mang’ana wakati wa zoezi la kutoa elimu kwa wakulima wa Korosho mkoa wa Tanga,juu ya matumizi sahihi na salama ya viwatilifu vya Mikorosho vinavyosambazwa na serikali kupitia Bodi ya Korosho Tanzania.

Alisema hali hiyo inatokana na wakati mwengine soko la kutokuwa zuri na kutokana na kuwa mpakani wanalazimika kuzisafirisha korosho zao tani kwa tani kwenda nchini Kenya ili kuweza kupata bei nzuri na soko ambalo linawawezesha kunufaika na kilimo hicho.

“Korosho nyingi tani kwa tani zinasafirishwa kwenda nchini Kenya kwasababu tupo mpakani ukienda ghalani unaambiwa kilo ni sh.2000 lakini kule nchini Kenya wananunua kilo 150 hadi 170 na ndio maana Korosho nyingi zinakwenda huko na hilo linatokana na kutokuwa kwa uzibiti wa bei hauridhishi “Alisema.

Mkazi wa Kijiji cha Gezani Kata ya Mkinga Hafidhi Mamboleo akiwa anapulizia dawa mikorosho 
 Sehemu ya viwatilifu vilivypo kwenye ghala la Mkinga
Afisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho Tanzania,Bryson Mshana kulia akitoa elimu kwa wakulima wa zao la Korosho Kijiji cha Horohoro wilayani Mkinga  kuhusu umuhimu wa matumizi sahihi nasalama viwatilifu vinavyosambazwa na serikali kupitia na bodi ya korosho Tanzania lililoanza mikoa ya Mtwara na Lindi,Ruvuma na sasa Tanga watakwenda Pwani na mikoa inayolima korosho

BALOZI KAMALA ATEMBELEA VITUO VYA AFYA ,ZAHANATI NA KUWEKA MIKAKATI YA UFUMBUZI HUDUMA ZA MAMA NA MTOTO

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Nkenge Balozi Dr.Deodorus Kamala ametoa kiasi cha shilingi (milioni tano na laki sita ) 5,600,000/-kwa ajili ununuzi wa masanduku ya kubebea vifaa vya huduma ya kwanza (First Aid Kit) kwenye zahanati 10 za Halmashauri ya Missenyi,Masanduku hayo yakiwa na vitu muhimu vinavyohitajika kwa dharula mbalimbali.

Dr.Diodorus Buberwa Kamala amesema hayo alipofanya ziara katika Vituo vya Afya na zahanati kujionea changamoto na hali ya uwepo wa dawa na kuweka mikakati ya ufumbuzi katika huduma za Mama na Mtoto,Katika ziara hiyo ameongozana na Meneja wa MSD kanda ya Kagera na Geita Bwana Egidius Rwezaula .Amezitaja Zahanati zilizopewa (First Aid Kit) ni Kashanga, Buyango, Bugandika,Kitobo, Kanyigo,Minziro ,Kyaka,Kilimilile,Bugorora pamoja na Kakindo .
Bango la Zahanati ya Kashanga iliyopo Kata ya Bwanjai Wilayani Missenyi.
Balozi Kamala amepongeza hali ya utoaji na ubora wa huduma za afya Wilayani Missenyi na kuwapongeza MSD kwa kazi nzuri na kubwa inayofanywa ambayo imepelekea kwa kiasi kikubwa huduma za Afya kupatikana .Kwa upande wake Meneja wa Msd kanda ya Kagera na Geita Egidius Rwezaula amesema kuwa kazi ya kuyafikisha masanduku hayo kwenye zahanati hizo inaanza kufanyika na kwamba hali ya huduma ni nzuri na Dawa zote muhimu zinapatikana kwa (asilimia 97).
Kwa upande wake Meneja wa Msd kanda ya Kagera na Geita Egidius Rwezaula pichani kulia amesema kuwa kazi ya kuyafikisha masanduku hayo kwenye zahanati hizo inaanza kufanyika na kwamba hali ya huduma ni nzuri na Dawa zote muhimu zinapatikana kwa (asilimia 97)
Muonekano wa Majengo ya Zahanati ya Bugorora
Balozi Dr.Deodorus Kamala akiongea na wagonjwa waliofika katika ahanati ya Buyango pindi alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za afya katika Vituo vya Afya na Zahanati Wilayani Missenyi.

MAOFISA WA JESHI LA MAGEREZA WAASWA KUZINGATIA MAADILI YA KAZI

$
0
0
Na Lucas Mboje, Magereza;

KAMISHNA Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike amewataka Maofisa na askari wa Jeshi hilo kujiepusha na vitendo vilivyo kinyume na maadili ya kazi yao, badala yake wazingatie kanuni, miiko na maadili ya uendeshaji wa Jeshi la Magereza.

Kamishna Jenerali Kasike ametoa rai hiyo jana Agosti 1, 2018 wakati akiongea na Maofisa na askari wa Jeshi la Magereza Mkoani Arusha alipofanya ziara ya kikazi Mkoani humo.Alisema kuna upungufu katika uzingatiaji wa maadili kwa baadhi ya Maofisa na askari hususani mahusiano mabaya ya askari na wafungwa ikiwemo tabia za askari kuingiza simu magerezani.

Amesema hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa kwa maofisa na askari watakaobainika kufanya vitendo hivyo ikiwemo kuwajibishwa na kufukuzwa kazi."Mnajua kabsaa gharama za kujihusisha na tabia hizi za mahusiano mabaya na wafungwa nawaasa mzingatie maadili mnapotekeleza majukumu yenu ya kazi". Alisisitiza Kamishna Jenerali Kasike. 

Kuhusu agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu kujitosheleza kwa chakula cha wafungwa Kamishna Jenerali Kasike amesena kwa sasa Jeshi hilo linakamilisha mpango kazi wake utakaowezesha utekelezaji wa agizo hilo.Amewataka askari wote nchini kujiandaa kisaikolojia kutekeleza agizo hilo bila kisingizio chochote kwani Jeshi la Magereza linazo rasilimali za kutosha kutekeleza agizo hilo.

"Tunayo ardhi yakutosha, nguvu kazi ya wafungwa ipo hivyo agizo la Rais na Amiri Jeshi Mkuu lazima litekelezwe bila kisingizio chochote". Alisema Jenerali Kasike.Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike yupo katika ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Arusha ambapo lengo la ziara hiyo ni kukagua utendaji kazi pamoja na kuzungumza na Maofisa na askari wa Jeshi hilo.

AIRTEL YA WASHIRIKI BONANZA KUJEGA AFYA

$
0
0
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayoongoza kwa kutoa huduma bora za Smartphone kupitia kitengo chake cha rasilimali watu wameandaa bonanza la michezo lililowashirikisha wafanyakazi wake wote kwa lengo la kujenga afya za wafanyakazi hao pamoja na kuongeza ushirikiano eneo la kazi.

Akiongea mara baada ya tamasha hilo kuisha Mkuu wa kitengo cha Rasilimali Watu alisema “Airtel tunatambua jitihada za serikali zinazosisitiza kuboresha na kuweka mzingira rafiki sehemu za kazi, pia Airtel tunafahamu sana umuhimu wa michezo na mazoezi kwa afya za wafanyakazi wetu, Hivyo ndio maana tumeona ni vyema kukutana kwa michezo kama hivi ili kuwasaidia wafanyakazi kurelax na kubadilishana mawazo wakiwa katika mazingira tofauti” 

Katika Bonaza hilo la muziki na mchezo wafanyakazi wengi walifurahia zaidi mchezo wa kupigiana penati ambao washiriki walikuwa ni wasichana wote kwa mgawanyo wa vitengo vyao vya kazi kikiwemo kitengo cha ofisi ya Mkurugenzi mkuu kinachoundwa na rasilimali watu na udhibiti huduma, kitengo cha masoko, huduma kwa wateja, kitengo cha mauzo, ununuzi na ugavi, pamoja na kitengo fedha na mipango.

katika mchezo huo ushiriki ulikuwa wenye uvutano mkubwa kwa mzunguko wa  ngazi ya mtoano na kuwa wenye ushindani mkali zaidi pale ambapo walibaki vinara watatu ambao ni kitengo cha Huduma kwa wateja waliokichapa kitengo cha fedha na mipango kwa goli 6 huku wao wakiambuia goli tano na kuwafanya kitengo cha huduma kwa wateja kuibuka washindi wa ujumla na kubeba kombe la ushindi wa mchezo huo.
Mchezaji wa Kitengo cha Fedha cha Airtel Bi Foibe Simon akipiga penati dhidi ya kitengo cha huduma kwa wateja wakati wa  Bonanza la Familia ya wafanyakazi wa Airtel lililofanyika  kwa lengo la kujenga afya na kuhamasisha wafanyakazi wa Airtel kuendelea kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wake.
  Meneja Rasilimali watu Pamela Mwandetele akipiga penati wakati wa bonanza Bonanza la wafanyakazi wa Airtel lililofanyika mwishoni mwa wiki  kwa lengo la kujenga afya na kuhamasisha wafanyakazi wa Airtel kuendelea kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wake.
 Kushoto ni kocha wa timu ya kitengo cha fedha cha Airtel bw Sylivester  Nsabi (Gadiola) na Nahodha wa timu hiyo Bi Foibe Saimon wakipokea kombe la ushindi wa pili toka kwa Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Bw, Isack Nchunda wapilitoka kushoto akiwa na Mkurugenzi wa kitengo cha Fedha Bw Nishant Mohan. Bonanza la wafanyakazi wa Airtel lililofanyika mwishoni mwa wiki  kwa lengo la kujenga afya na kuhamasisha wafanyakazi wa Airtel kuendelea kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wake.
 Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Bw, Isack Nchunda akikabidhi zawadi ya kombe la mshindi wa pili kwa Nahodha wa timu ya kitengo cha Fedha na Mipango cha Airtel Bi Foibe Saimon mara baada ya kumalizika kwa bonanza la wafanyakazi wa Airtel lililofanyika mwishoni mwa wiki kwa lengo la kujenga afya na kuhamasisha wafanyakazi wa Airtel kuendelea kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wake.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Sunil Colaso (watatu toka kushoto) akikabidhi zawadi ya kombe kwa washindi wa kwanza  ambao ni kitengo cha huduma kwa wateja walipoibuka washindi kwa kukiladha kitengo cha fedha na mipango kwa golo za penati 6-5 wakati wa Bonanza la wafanyakazi wa Airtel lililofanyika mwishoni  mwa wiki.  Kitengo hicho pia watapata zawadi ya kwenye kupata chakula cha mchana kwenye hotel ya nyota tatu wote wakiwa wamelipiwa gharama zote na Airtel.
 Wafanyakazi wa Airtel kitengo cha huduma kwa wateja wakishangilia na Kombe lao mara baada ya kushinda nafasi ya kwanza kwenye bonanza la Airtel Familia lilifanyika mwishoni mwa wiki hii. Airtel imefanya bonanza hilo la lawafanyakazi ambapo wasichana toka vitengo mbalimbali ndani ya kampuni hiyo walishindani kupiga penati ambapo kitengo cha huduma kwa wateja waliibuka washindi kwa penati 6-5 dhidi ya kitengo cha Mipango na fedha cha Airtel.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


ZAO LA MCHIKICHI KUMALIZA UHABA WA MAFUTA NCHINI

$
0
0


SEKTA ya kilimo ni mhimili wa uchumi wa Taifa na inategemewa katika kuifikisha Tanzania kwenye uchumi wa kati ifikapo 2025, kupitia viwanda kwa sababu kilimo ndicho kitawezesha viwanda kwa kuvipatia malighafi.

Kutokana na umuhimu wa sekta hiyo katika kukuza uchumi wa nchini, serikali imekuwa ikifanya juhudi kubwa kuhakikisha inaiboresha ili iweze kuwa na tija na kufikia malengo iliyojiwekea.

Sekta hiyo mbali na kuwa mhimili wa uchumi wa Taifa, pia imekuwa ikichangia pato la mkulima mmoja mmoja, kaya na pia ni tegemeo la mapato ya fedha za ndani na za kigeni.Kufuatia hali hiyo, Serikali imeweka msisitizo katika kusimamia mazao makuu matato ya biashara ambayo ni pamba, chai, kahawa, korosho na tumbaku ambayo uzalishaji wake umeonyesha tija.

Baada ya kupata mafanikio katika mazao hayo Serikali kwa sasa inaboresha kilimo cha mazao ya alizeti, ufuta, michikichi ili kuzalisha mafuta ya kula ya kutosha kwa kutumia mazao hayo na mbegu za pamba.Itakumbukwa kwamba kila mwaka, Serikali inatumia sh. bilioni 600 kwa ajili ya kuagiza mafuta ghafi ya kula kutoka nje ili kukidhi mahitaji kwa kuwa kiwango kinachozalishwa nchini hakitoshi.

Jumia yasisitiza kuuza bidhaa bora na halisi mtandaoni

$
0
0
 Katika kuwajengea Watanzania mazingira salama na rahisi ya kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao, Jumia imesisitiza kuwa bidhaa zote zinazopatikana kwenye mtandao wake ni halisi na zenye bora wa hali ya juu kutoka kwa kampuni na wafanyabiashara wanaoaminika Tanzania na duniani kote.

Kwa watanzania wengi dhana ya kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao bado ni ngeni na haijazoeleka. Miongoni mwa sababu zinazopelekea hali hiyo ni; uaminifu kwa sababu hakuna mawasiliano ya moja kwa moja baina ya muuzaji na mnunuzi, hofu ya wizi wa mitandaoni kutokana na upya wa huduma hii pamoja na changamoto ya maendeleo ya kiteknolojia ambayo watu wengi bado hawajafikiwa nayo.

Watanzania wengi wamezoea kwenda maduka moja kwa moja pale wanapohitaji kununua bidhaa kwa sababu hupata wasaa wa kuziona, kuzishika, kuzijaribisha, kufanya makubaliano ya bei ili kujiridhisha zaidi kabla ya kukata shauri la kununua.

Akizungumzia juu ya faida ambazo zimeletwa na mfumo wa manunuzi kwa njia ya mtandao kwa wafanyabiashara na wateja wa Kitanzania, Mkuu wa Masoko wa Jumia Tanzania, kampuni inayoongoza kwa huduma za manunuzi mtandaoni Afrika, Bw. Albany James amebainisha kuwa mfumo huu upo kwa ajili ya kuwarahisishia wateja huduma za kufanya manunuzi pamoja na kuongeza thamani kwa wafanyabiashara.

JENGENI DARAJA USIKU NA MCHANA- KWANDIKWA

$
0
0
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa amemtaka Mkandarasi anayejenga Daraja la Magara linalounganisha Wilaya ya Babati na Mbulu kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha ujenzi wake unakamilika kwa haraka na ubora unaotakiwa ili kuwaondolea wananchi kero ya usafiri inayowakabili.

Akizungumza mara baada ya kukagua daraja hilo, Kwandikwa amesema tayari kiasi cha shilingi bilioni 1.4 kimelipwa kama malipo ya awali hivyo Mkandarasi aongeze kasi na kulimaliza daraja hilo pamoja na barabara unganishi zenye urefu wa Kilomita 4.9 katika kipindi cha miezi 24.

“Daraja hili likikamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa litahamasisha shughuli za biashara na uzalishaji kati ya Mbulu na Babati na hivyo kuchochea uchumi wa wilaya hizo” amesema Kwandikwa.Aidha amemtaka Mkandarasi China Railway Seventh Group (CRSG) anaejenga daraja hilo kutoa fursa za ajira kwa wakazi wa Wilaya za Mbulu na Babati katika kuharakisha ujenzi wake.

Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) Mkoa wa Manyara, Mhandisi Bashiri Rwesingisa amemhakikishia Naibu Waziri Kwandikwa kuwa ujenzi wa Daraja la Magala ni Sehemu ya Mkakati wa Serikali wa kuijenga barabara ya Kutoka Mbuyu wa Mjerumani hadi Mbulu kwa Lami ambapo tayari upembuzi yakinifu kwa ajil ya ujenzi huo umekamilika.
Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) Mkoa wa Manyara, Mhandisi Bashiri Rwesingisa akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa (aliyevaa kofia) kuhusu hatua iliyofikia ya maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Mizani ya kudumu katika eneo la Mwada-Mbuyu wa Mjerumani, Wilayani Babati. Mkoani Manyara.
Muonekano wa mto Manyara ambapo linajengwa daraja la Magara lenye urefu wa mita 84, wilayani Babati Mkoani Manyara. Daraja hilo linatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi 24.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa akitoa maelekezo kwa Uongozi wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Mkoa wa Manyara kuhusu kuzingatia viwango katika ukarabati wa barabara sehemu ya mlima Magara kwa kiwango cha zege mara baada ya kukagua maendeleo ya mradi huo, Mkoani Manyara.
Mafundi wakindelea na ujenzi wa barabara sehemu ya Magara kwa kiwango cha zege, Mkoani Manyara.
Muonekano wa barabara Magara-Mbulu ambayo inafanyiwa ukarabati na Wakala wa Barabara Nchini (TNAROADS) kwa kiwango cha zege,Mkoani Manyara.

MAZINGAOMBWE NI SAYANSI, WANASAYANSI CHIPUKIZI WATHIBITISHA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

WANAFUNZI wa shule mbalimbali za Sekondari nchini wamekutana na kuonesha mawazo yao ya kiugunduzi kupitia taasisi ya Young Scientist (YS) na kuiomba Serikali kuwasaidia ili kufanikiwa katika kutimiza ndoto zao.

Katika hali ya kushangaza na kuvutia zaidi wanafunzi wa shule ya sekondari Vingunguti jijini Dar es salaam walionesha mazingaombwe kama vile kupoteza na kuirudisha sarafu, kujitoboa sehemu za miili yao na kudhibitisha kwamba dhana ya mazingaombwe ni sayansi na si usihiri (uchawi) kama inavyofahamika na watu wengi.

Akizungumza na Michuzi blogu mmoja wa wanafunzi hao Neema Julius ameeleza kuwa jamii itambue kuwa mazingaombwe ni sayansi inayotumika kila siku katika mazingira yetu na kwa utafiti wao wamegundua hakuna dhana ya ushirikina katika hilo.

Aidha wanafunzi kutoka shule ya sekondari Same wamegundua umeme wa utokanao na mitetemo, sauti na upepo na wameona umeme huo utafaa katika maeneo ya vijijini kwani changamoto zake ni chache ila kutokana na vifaa na uwekezaji wameiomba serikali kutoa msaada ili waweze kukamilisha ndoto zao za kuwasaidia wananchi kupata nishati ya umeme.

Pia shule ya Sekondari ya Mtakatifu Joseph Kolping baada ya kuona ongezeko la ajali za barabari wakaona watafute mbinu ya kudhibiti na wakaja na dhana ya matumizi ya roboti kuwa mlinzi na mwongozaji wa watumiaji wa barabara na kuripoti kila aina ya kosa linalotendeka.
 Mwanzilishi mwenza wa YST, Dr. Gosbert Kamugisha akipata maelezo kuhusu matumizi ya umeme wa upepo, sauti, na mtetemo kutoka kwa mwanafunzi wa Same Sekondari, Samwel Osebius.
 Mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya mtakatifu Joseph Kolping, Fransisco Solomon akionesha roboti waliyoitengeneza kwa ajili ya kulinda  barabarani.
Mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya Vingunguti, Neema Julius akieleza namna mazingaombwe yana uhalisia wa sayansi tofauti na wanajamii wanavyofikiri.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, JAPHET HASUNGA AWAASA WATUMISHI WA TFS KANDA YA KUSINI

$
0
0
Watumishi wa Wakala wa Huduma Tanzania (TFS) wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni na sheria za utumishi wa Umma ili kuleta ufanisi wakati wanapotekeleza majukumu yao ya uhifadhi.

Rai hiyo imetolewa jana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga wakati alipowatembelea jana watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) kanda ya Kusini kwa ajili ya kuzungumza nao ikiwa ni muendelezo ya ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani Mtwara kwa ajili ya kushughulikia changamoto za Maliasili, Malikale na Uendelezaji Utalii.

Amewataka kufanya kazi kwa uadilifu wa hali ya juu na yeyote atakayetuhumiwa kupokea rushwa hata kama hajapokea rushwa hiyo kutoka wafugaji kwa makubaliano ya kuingiza mifugo hifadhini kwa makubaliano ya malipo atashughulikiwa ipasavyo.Aliongeza kuwa endapo watumishi hao wataweza kutekeleza majukumu yao ipasavyo hakuna kiongozi yeyote watakayesumbuana nao.

‘’Tunataka mfanye kazi zenu za uhifadhi kwa weledi wa hali ya juu na mkifanya vizuri basi nakuwa nimefanya mimi na mkifanya vibaya mnakuwa mnaniangusha mimi hivyo sitokubali’’ alisisitiza Naibu Waziri Hasunga.
Aidha, Amewata wafanye kazi kwa kushirikiana na jamii kwa vile hakuna shughuli yeyote itakayofanikiwa endapo wananchi wataachwa nyuma.

‘’Tunataka jamii ione faida ya moja kwa moja kwa kupata elimu kuhusu uhifadhi pamoja na kushirikishwa kwenye masuala yote ya misitu ili waweze kutoa ushirikiano wakati ukataji miti unapofanyika popote pale’’
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza na Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) wa kanda ya Kusini, Ebramtino Mgiye mara baada ya kuwasili jana kwenye ofisi za TFS kanda ya Kusini kwa ajili ya kuzungumza nao ikiwa ni muendelezo ya ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani Mtwara kwa ajili ya kushughulikia changamoto za Maliasili, Malikale na Uendelezaji Utalii.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza na watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzani (TFS) wakati alipowatembelea jana kwenye ofisi za TFS kanda ya Kusini ikiwa ni muendelezo ya ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani Mtwara kwa ajili ya kushughulikia changamoto za Maliasili, Malikale na Uendelezaji Utalii.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga(katikakati) akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kuzungumza na Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania kwenye ofisi za TFS kanda ya Kusini ikiwa ni muendelezo ya ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani Mtwara kwa ajili ya kushughulikia changamoto za Maliasili, Malikale na Uendelezaji Utalii.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Viewing all 109999 articles
Browse latest View live




Latest Images