Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110089 articles
Browse latest View live

RAIS WA ZANZIBAR DK.ALI MOHAMED SHEIN AWASILI NCHINI INDONESIA LEO.

$
0
0
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein (katikati) pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Malaysia pia akiwakilisha Tanzania Nchini Indonesia Mhe.Dkt Ramadhani Kitwana Dau (kulia) na Viongozi wengine wakipewa maelekezo na Afisa Maalum mara baada ya mapokezi walipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Soekarno Hatta, Jakarta Indonesia leo wakiungana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika ziara ya siku saba Nchini humo kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Mhe.Mohammed Jusuf Kalla , [Picha na Ikulu.]31/07/2018. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Kiongozi wa Ngazi ya Juu Nchini Indonesia Daniel T.S.Simanjuntak (kushoto) mara alipowasili katika Ukumbi wa Watu Mashuhuri katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Soekarno Hatta, Jakarta leo, akifuatana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein pamoja na Viongozi mbali mbali,katika ziara ya kikazi ya siku saba kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Mhe.Mohammed Jusuf Kalla ,[Picha na Ikulu.]31/07/2018.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Malaysia pia akiwakilisha Tanzania Nchini Indonesia Mhe.Dkt Ramadhani Kitwana Dau (kulia) mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Soekarno Hatta, Jakarta Indonesia leo, akifuatana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein pamoja na Viongozi mbali mbali,katika ziara ya kikazi ya siku saba kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Mhe.Mohammed Jusuf Kalla,[Picha na Ikulu.]31/07/2018.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein (katikati) pamoja na Viongozi aliofuatana nao akiwa katika mazungumzo na Kiongozi wa Ngazi ya Juu Nchini Indonesia Daniel T.S.Simanjuntak (wa pili kulia) katika Ukumbi wa Watu Mashuhuri katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Soekarno Hatta,Jakarta leo katika ziara ya kikazi ya siku saba kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchini Indonesia Mhe.Mohammed Jusuf Kalla, [Picha na Ikulu.]31/07/2018.

UJUMBE WA WATAALAMU WA AFYA KUTOKA BRAZIL WAKUTANA NA WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR.

$
0
0
Na Ramadhani Ali – Maelezo

Ujumbe wa watu nane wa Wataalamu wa afya kutoka Serikali ya Brazil upo Zanzibar kutekeleza ombi la Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Muhamed Shein kuitaka nchi hiyo kuzidisha ushirikiano katika sekta ya Elimu, Afya na Utalii.

Ujumbe huo ukiongozwa na Mratibu Mkuu wa Kanda ya Afrika, Asia, nchi za Oceanic na Mashariki ya mbali Fabio Webber umefanya mazungumzo na Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed kujifunza changamoto zinazowakabili mama wajawazito na watoto wachanga.

Webber alisema Rais wa Zanzibar alipofanya mazungumzo na Balozi wa Brazil aliomba nchi hiyo kufungua ubalozi mdogo Zanzibar, kusaidia kuimarisha masuala ya afya na kuwajengea uwezo wafanyakazi wa sekta hiyo.Balozi wa Heshma wa Brazil hapa Zanzibar Abdulsamad Abdulrahim alisema baada ya Serikali ya Brazil kufungua Ubalozi mdogo Zanzibar, wanaelekeza nguvu zao juu ya afya ya mama mzazi na mtoto pamoja na kuwajengea uwezo wafanyakazi wa kitengo hicho.

Alisema ujumbe huo utafanya ziara katika vituo mbali mbali vya afya Unguja na Pemba kuangalia changamoto zinazowakabili mama wajawazito wakati wa kujifungua na watoto wachanga na hatiamae kuzitafutia ufumbuzi.Waziri wa Afya aliueleza ujumbe huo kuwa Serikali inaendelea kuimarisha huduma za afya ya msingi vijijini ili vituo vya afya vya huko viwe na uwezo na vifaa vya kutosha na wananchi waviamini na wavitumia.

Alisema hivi sasa kumekuwa na msongamano mkubwa wa wazazi katika Hospitali kuu ya Mnazimmoja huku vituo vya afya vijijini vyenye uwezo wa kutoa huduma za kuzalisha vinakosa wazazi kutokana na dhana kuwa huduma ni ndogo.Alisema kuimarika kwa vituo vya afya vya vijijini vinavyotoa huduma ya mama na mtoto kutaipunguzia hospitali hiyo msongomano wa wazazi na kumudu kutoa huduma zilizo bora zaidi.

Ujumbe huo umeanza kazi ya kutembelea vituo vya afya vinavyotoa huduma ya kuzalisha kuona hali halisi na kujua changamoto zinazovikabili vituo hivyo na baadae kufanya uchambuzi wa kujua masuala yanayopaswa kutekelezwa kuongeza mashirikiano .
BALOZI wa Heshima wa Brazil hapa Zanzibar, Abdulsamad Abdulrahim (suti buluu) akiwa na Ujumbe wa wataalamu wa Afya kutoka Brazil wakitembelea Kituo cha Afya Fuoni.
WAZIRI wa Afya Zanzibar Hamad Rashoid Mohamed akizungumza na Ujumbe wa Wataalam wa Afya kutoka Nchi ya Brazil Afisini kwake Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar.
UJUMBE wa wataalamu wa Afya kutoka Brazil wakiangalia takwimu za mama wajawazito wanaofika kupata huduma ya kujifungua Kituoni hapo

BALOZI MPYA WA KENYA AKARIBISHWA NCHINI TANZANIA

$
0
0

Balozi mpya wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu akitoa hotuba yake kwa wageni mbalimbali waliohudhulia dhifa iliyoandaliwa maalum kwa kumkaribisha rasmi nchini, iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam Julai 31, 2018. Kulia ni Mke wa Balozi Kazungu, Bi. Mapenzi Kazungu.
Kiongozi wa Mabalozi nchini na Balozi wa Rwanda, Eugene Kayihura akizungumza jambo kwa niaba ya Mabalozi wengine, wakati wakimkaribisha Balozi mpya wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu, katika dhifa iliyoandaliwa maalum kwa kumkaribisha rasmi nchini, iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam Julai 31, 2018. 
Kaimu Balozi wa Kenya nchini, Boniface Muhia akizungumza katika dhifa iliyoandaliwa maalum kwa kumkaribisha rasmi nchini Balozi mpya wa Kenya, Dan Kazungu, iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam Julai 31, 2018. 
Balozi mpya wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu (kushoto) akiwa katika mazungumzo yenye furaha na baadhi ya maafisa wa Ubalozi wa Kenya hapa nchini, wakati hafla fupi ya kumkaribisha Balozi huyo, iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam Julai 31, 2018.

TOTAL YAKABIDHI CHOO KWA DC SHULE YA MSINGI KIVULE DAR ES SALAAM

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema jana amepokea Msaada wa jengo la Choo cha kisasa chenye matundu 10 kilichojengwa katika Shule ya Msingi Kivule na kampuni ya Mafuta ya Total.

Akipokea msaada Kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Total nchini, Tarik Moufaddal, Dc Mjema amesema kuwa Msaada huo utasaidia kwa sehemu kubwa ya wasichana ambao walikuwa wanapata tabu ya vyoo katika shule hiyo.

Amesema kuwa shule hiyo yenye wanafunzi 3000 kwa sasa wanaweza kukabiliana na changamoto ya vyoo kwa watoto wa kike kutokana na kuongezeka kwa matundu hayo 10 ,ambayo yameelekezwa maalumu kwa ajili ya watoto wa kike.

“kwetu sisi huu ni msaada mkubwa sana kutoka Total kwani choo hichi kimegharimu Zaidi ya Shilingi Milioni 33 za kitanzania na kampuni hii imeweza kutenga Zaidi ya Milioni 700 kwa ajili ya kusaidia sehemu mbalimbali Tanzania kwanii tayari wamejenga choo kama hiki katika shule ya msingi Yombo Dovya hivyyo sisi watu wa ilala tunaomba wasiache kutukimbia kwani bado tutaitaji msaada Zaidi ya huu”amesema Dc Mjema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Total nchini Tarik Moufaddal amesema kuwa kampuni yake inaona fahari kuwa karibu na jamii kwa kuona inatoa msaada kwa watoto ili waweze kuwa katika mazingira mazuri na afya bora.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akizungumza na Wanfunzi wa Shule ya Msingi Kivule mara baada ya kupokea Msaada wa Choo Cha Matundu 10 chenye thamani ya Milioni 33
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akiwa na Mkurungenzi Mkuu wa Total Tanzania Tarik Moufaddal wakati wa kuzindua jiwe la Msingi wa choo hicho
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akiwa na Mkurungenzi Mkuu wa Total Tanzania Tarik Moufaddal wakikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa kuanza kutumika kwa choo hicho.

MPINA AJA NA MIKAKATI 15 YA MAPINDUZI MAKUBWA SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI

$
0
0
Na John Mapepele

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amezindua mikakati 15 itakayotumika kama nyenzo ya kusimamia utekelezaji wa majukumu ya wizara hiyo na kuleta mageuzi makubwa na ya muda mfupi kwenye sekta za mifugo na uvuvi kabla ya kumalizika awamu ya kwanza ya utawala wa Serikali ya awamu ya tano mwaka 2020.

Mikakati hiyo ni pamoja nakudhibiti magonjwa ya mifugo chanjo na viatilifu, mpango kazi wa kudhibiti upotevu wa mapato yatokanayo na biashara ya mifugo na mazao yake, mkakati wa usimamizi na udhibiti wa rasilimali za uvuvi nchini, mkakati wa upatikanaji wa uhakika wa malisho na maji kwa ajili ya mifugo pamoja na mkakati wa kuboresha na kuzalisha kwa wingi ng’ombe wa nyama na maziwa kwa njia ya uhimilishaji.

Mwingine ni mkakati wa kudhibiti na kuondoa migogoro baina ya wakulima, wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi, mkakati wa kuboresha uzalishaji wa kuku,mkakati wa kuanzisha na kuwezesha ushirika wa wafugaji, mkakati wa kuendeleza ukuzaji wa viumbe kwenye maji pamoja mkakati wa kufufua Shirika la Uvuvi nchini TAFICO

Akizungumza jijini Dodoma mara baada ya kuzindua mikakati hiyo, Waziri Mpina ameiagiza wizara hiyo kuunda kikosi kazi kitakachosimamia utekelezaji wake na kwamba kila baada ya miezi mitatu kufanyike tathmini na kwa watumishi wataoshindwa au kukwamisha utekelezaji wa mikakati hiyo watachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria,Kanuni na taratibu. 

Alisema mikakati hiyo ikikamilika Serikali itaweza kukusanya zaidi ya sh bilioni 100 kwa mwaka zitokanazo na sekta za mifugo na uvuvi tofauti na sh bilioni 30 zilizokusanywa katika kipindi cha mwaka 2016/2017 ambapo kwa mwaka 2017/2018 Serikali imeweza kukusanya sh bilioni 46 baada kufanyika Operesheni Sangara na Nzagamba.
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akiwaonyesha Mkakati wa kudhibiti upotevu wa mapato yatokanayo na biashara ya mifugo na mazao yake baada ya kuuzindua katiika ukumbi wa VETA Dodoma. Picha na John Mapepele
Kikosi kazi kilichoandaa mkakati wa kudhibiti magonjwa ya mifugo nchini kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina ( aliyekaa katikati)kulia ni Kaimu Katibu Mkuu Bi Selina Lyimo, kushoto Kaimu Katibu Mkuu Uvuvi Bwana Julius Mairi.Picha na John Mapepele .

MBUNGE WA JIMBO LA SINGIDA MAGHARIBI AWAPOKEA WAMAREKANI JIMBONI KWAKE

$
0
0
Mbunge wa Singida Magharibi, Mheshimiwa, Elibariki Kingu, akihutubia katika hafla ya kuwapokea viongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri kutoka Marekani waliotembelea Zahanati ya Kanisa hilo ya Kijiji cha Msungue iliyopo Kata ya Sepuka mkoani Singida jana. Zahanati hiyo inasimamiwa na kanisa hilo Dayosisi ya Kati. Dotto Mwaibale
Mkurugenzi anayesimamia Hospitali na Zahanati za Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kati, Mchungaji Manase Msengi, akimuonesha picha ya vitanda vya Hospitali vinavyo sambazwa na Bohari ya Dawa (MSD), Mkurugenzi wa Uhusiano Kati ya Sinodi ya Kusini Mashariki ya Minessota na makanisa ya nje ya Marekani, Callemia Chatelaine. Kushoto ni Mganga wa zahanati hiyo.
Mganga wa zahanati hiyo akiwaelekeza jambo wageni hao walipotembelea chumba cha maabara cha zahanati hiyo.
Mkurugenzi anayesimamia Hospitali na Zahanati za Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kati, Mchungaji Manase Msengi, akiwaelekeza jambo wageni hao eneo ilipofungwa mfumo wa maji katika zahanati hiyo.

HOTUBA YA RAIS MAGUFULI BAADA YA KUWAAPICHA, WAKUU WA MIKOA, MAKATIBU NA MANAIBU KATIBU IKULU JIJINI DAR LEO

ZAIDI YA WANAFUNZI 90 WANUSURIKA NA MOTO

$
0
0
Bweni la wavulana Shule ya msingi Giti iliyopo Wilayani Same limeteketea kwa moto baada ya moto kuunguza bweni pamoja na vitu vyote vilivyokuwemo ndani. 

Wanafunzi wote wamenusurika na moto huo, kwani moto uliwaka majira ya saa 2.00 usiku wanafunzi wakiwa katika vipindi vya usiku darasani.Wanafunzi wamepoteza kila kitu na kuhitaji msaada wa haraka ili kurudisha maisha yao katika hali ya kawaida. 

Mkuu wa Wilaya ya Same,Mh  DC Same Rosemary Senyamule  akiwa ameambatana na Kamati ya ulinzi na usalama pamoja na Afisa elimu ,walitembelea eneo la tukio na kuona uhitaji wa marakebisho ya haraka kwa jengo linalotegemea kuhamishia wanafunzi hao ili waendelee na masomo. 

DC Rosemary amewataka Wataalamu wa zimamoto na wakaguzi wa shule kufanya kaguzi za mara kwa mara katika taasisi zote ili kuchukua tahadhari za matukio kabla hayajatolea. 

Naye Mwenyekiti wa Conference kanda ya kaskazini Mch. Ijiko (kanisa la SDA) ambao ndiyo wamiliki wa shule hiyo amewaomba wadau kushirikiana nao ili kurudisha bweni hilo katika hali ya kawaida na kuwawezesha wanafunzi kurudishia mazingira bora ya kusomea.

Tukio hilo litokea Julai 29,2018 kata ya Mamba myamba Wilayani Same.
 DC Same Rosemary Senyamule (wa tatu kulia) akiwa ameambatana na Kamati ya ulinzi na usalama pamoja na Afisa elimu wakiwa katika kikao cha pamoja mara baada kutembelea eneo la tukio na kuona uhitaji wa marakebisho ya haraka kwa jengo linalotegemea kuhamishia wanafunzi hao ili waendelee na masomo. 
Muonekano wa Bweni la wavulana Shule ya msingi Giti iliyopo Wilayani Same lilivyotekea kwa moto baada ya moto kuunguza bweni pamoja na vitu vyote vilivyokuwemo ndani. 

Balozi wa Kuwait Aahidi Kuwasaidia Watoto Wenye Saratani Muhimbili

$
0
0
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jasem Al-Najem ametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kuahidi kuwasaidia watoto wenye saratani ambao wanatibiwa katika hospitali hiyo.

Katika ziara hiyo balozi huyo alimtaka Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tumaini la Maisha (TLM) katika hospitali hiyo, Dkt. Trish Scanlan kumwandikia mahitaji ambayo watoto hao wanapaswa kupatiwa ili aweze kushiriki katika kuwapatia tiba pamoja na mambo mengine. 

Balozi huyo aliongozana na Naibu Mwenyekiti wa Red Crescent kutoka Kuwait, Anwar Alhasawi, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati-Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki , Suleiman Salehe pamoja na pamoja na viongozi mbalimbali wa Lions Club ambayo imekuwa ikiwasadia watoto hao mahitaji mbalimbali.

Pia, balozi huyo alitembelea watoto wenye saratani katika jengo la watoto pamoja na kuwapatia zawaidi mbalimbali ikiwamo vifaa vya kuchezea.
Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa mwezi imekuwa ikipokea wastani wa watoto 30 hadi 40 wenye saratani ya aina mbalimbali. Wengi wa watoto wanaopokelewa wamekuwa wakisumbuliwa na saratani ya damu, jicho, figo na saratani ya matezi.
 Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jasem Al-Najem akimkabidhi zawadi mmoja wa kina mama, Martha John Zakaria anayemuuguza mtoto wake katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Kushoto ni Naibu Mwenyekiti wa Red Crescent kutoka Kuwait, Anwar Alhasawi na mwakilishi wa Jumuiya ya Red Crescent, Mayouf Alenezi.
 Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jasem Al-Najem akizungumza na wazazi wa watoto ambao wanatibiwa saratani katika hospitali hiyo. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati-Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Suleiman Saleh na Naibu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Red Crescent kutoka Kuwait, Anwar Alhasawi.
 Wazazi na watoto wakimsikiliza balozi huyo katika jengo la watoto.
 Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jasem Al-Najem akizungumza na Ofisa Mtendaji wa Tumaini la Maisha (TLM), Dkt. Trish Scanlan  baada ya ofisa huyo kumweleza mahitaji wanahitaji watoto wanaotibiwa saratani katika hospitali hiyo.  Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati-Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Suleiman Saleh, kulia ni Naibu Mwenyekiti wa Red Crescent kutoka Kuwait, Anwar Alhasawi (mwenye koti) na wengine ni wawakilishi wa Jumuiya ya Red Crescent.
Balozi huyo akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto baada ya kupewa zawadi mbalimbali.

KIWANDA CHA ZAMANI CHA VIATU CHA GEREZA KUU KARANGA, MOSHI CHABORESHWA

$
0
0
 Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akisalimiana na Mkuu wa Kiwanda cha Viatu Gereza Kuu Karanga, Moshi, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Hezron Nganoga alipotembelea kiwanda hicho kukagua maboresho ya ufungaji wa mashine mpya za kutengenezea viatu vya aina mbalimbali ikiwemo buti zinazotumiwa na Majeshi ya Ulinzi na Usalama hapa nchini leo Agosti 1, 2018.  Wengine ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo.

Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akiangalia mtambo maalum wa kukata ngozi zinazotumika kutengenezea viatu. Mtambo huu ni mpya na ni sehemu ya maboresho katika kiwanda hicho.

 Mtaalam kutoka nchini Italia akijaribisha mashine mpya ambazo zimefungwa katika Kiwanda hiki cha uzalishaji wa viatu cha Gereza Kuu Karanga(kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike.

 Maofisa Wataalam wa Jeshi la Magereza wakiendelea na majaribio ya mashine mpya katika mradi wa ubia uliokuwa mfuko wa hifadhi ya jamii wa PPF na Jeshi la Magereza. 
 Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akiangalia buti la jeshi ambalo limetengenezwa kiwandani hapo. Wengine wakiangalia viatu hivyo ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa uliokuwa mfuko wa hifadhi ya jamii wa PPF, Hosea Kashimba(wa pili kushoto) ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Onesmo Buswelu.


Mkuu wa Magereza Mkoani Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Hassan Mkwiche (wa pili kulia) akionesha eneo la uwekezaji wa kiwanda kipya katika awamu ya pili ya mradi wa kiwanda cha viatu chini ya Kampuni ya Kiwanda cha viatu Karanga (wa pili kushoto) ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Viwanda vya ngozi – Gereza Kuu Karanga, Bw. Masoud Omary (wa tatu kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(Picha zote na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Makao Makuu ya  Jeshi la Magereza).


LESENI ZA MADINI AMBAZO HAZIFANYI KAZI KUFUTWA

ZAIDI YA WANACHI 90 NGORONGORO WAPEWA MAFUNZO YA KIDIGITALI NA SHIKALA LA OXFAM

$
0
0
Na. Vero Ignatus  Ngorongoro
OXFAM kwa kushirikiana na Shirika la PALISEP wameendesha mafunzo ya teknolojia ya kidigitali kwa wananchi wilaya ya  Ngorongoro mkoani Arusha ili kuleta  maendeleo katika jamii husika. 
Maratibu wa Teknolojia kwa maendeleo shirika la Oxfam Bill Marwa amesema  wametoa mafunzo kwa wananchi zaidi ya (90)yakiwa na lengo la wao kutambua namna ya kuitumia mitandao hiyo pamoja  nyenzo mbalimbali za kidigital kwa kutuma ujumbe mfupi, kutoa taarifa kwa viongozi wao wa kijiji,kujibuwa changamoto wanazokutana nazo kwaajili ya kujiletea maendeleo.
 "Kadri miaka inavyoenda kumekuwa na ongezeko la mitandao ya kijamii ulimwenguni hivyo Oxfam kama shirika limeona upo umuhimu wa maendeleo, kupata taarifa, kutoa matokeo"alisema Bill Marwa.Washiriki wa mafunzo hayo walifundishwa sheria za mtandao 2015 pamoja na makosa ya mtandaoni, jinsi ya kutumia vifaa hivyo katika namna ambayo havivunji sheria ya nchi. 
Sambamba na hayo walifundishwa maswala Mbalimbali jinsi ya ukingi haswa kwa wanawake kulinda haki za mwanamke na kupinga ukatili wa kijinsia dhidi yao.Mafunzo hayo yaliyokuwa ya siku nne yaliyoshirikisha kata zaidi ya 10 katika wilaya ya Ngorongoro,ikiwa ni mradi wa  miaka miwili unaotekelezwa katika mikoa (4) Arusha, Geita,Kigoma,na Mtwara katika wilaya za Mtwara vijijini, Mbogwe Geita, Kibondo,na Ngorongoro. 

Mradi huo unalengo la kuwawezesha wananchi kutumia nyenzo za digitali ili kujiletea maendeleo katika jamii husika,amabapo ulianzishwa rasmi mwaka 2016 desemba na unatarajiwa kumalizika novemba 2018 ,mradi huo upo chini ya ufadhili kutoka nchini Ubelijiji. 
Meneja wa Program Shirika la Oxfam Kefar Mbogela akitoa Elimu namna ya kutumia mitandao na nyenzo mbalimbali za kidigitali bila kuleta madhara kwa jamii wala kuvunja sheria ya mitandao hiyo
Rachel yeye anasema mwanzoni alikuwa akitumia simu ya hali ya chini ambayo alikuwa hapati mambo mengi ya faida ,ila kwa sasa mara baada ya kupewa simu na Oxfam imemsaidia sana kuweza kuwasiliana na na jamii ,amesema kwasasa anaweza kupaza sauti kwa kutumia simu yake,kutatua changamoto mbalimbali na viongozi wanapoona ujumbe wake wanatatua tatizo na majibu yanapatikana kwa wakati.
Darasa la mafunzo ya kutumia nyenzo za mitandao ya kijamii na namna ya kutumia nyenzo za kidigitali yakiendelea.

DKT. NDUGULILE APIGA MARUFUKU KWA TV ZA HOSPITALI KUONESHA MUZIKI.

$
0
0
Na WAMJW - KAGERA

Naibu Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile amepiga marufuku kwa hospitali na vituo vyote vya kutolea huduma za Afya nchini kuonesha miziki katika maeneo yote yakutolea huduma na kuwataka kuweka jumbe zinazohusu Elimu Afya kwa umma pindi wanapongoja kupata huduma.

Ameyasema hayo mapema leo wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za afya katika ukumbi wa halmashauri ya Muleba katika Mkoa wa Kagera."Ni marufuku kwa hospital zote kuonesha miziki katika maeneo yote ya utoaji huduma za afya" alisema Dkt Ndugulile.

Pia Dkt. Ndugulile amemwagiza Mganga mkuu wa Wilaya ya Ngara DKt. Revokatus Ndyekobora kuhamasisha wananchi Juu ya umuhimu wa kuudhuria kliniki kwa mama mjamzito walau mara nne ndani ya kipindi chá ujauzito wake na kuhakikisha wanajifungulia katika vituo vya kutolea huduma za Afya.

"Tuongeze kasi katika kuhamasisha wakina mama wajawazito kuhudhuria kliniki, na kwenda kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma za Afya" alisema Dkt Ndugulile. Pia alisema kuwa Serikali inaendelea kuboresha sekta ya Áfya nchini kwa kutoa pesa ya ujenzi wa vituo vya kutolea huduma za Afya na kuhamasisha ushirikishwaji wa wananchi katika ujenzi wa vituo hivyo (Forced account)

"miundombinu tunaendelea kuboresha, Mkoa mzima tumeleta shilingi Bilion 5.9 kwaajili ya kuboresha vituo vya Áfya, viwili vikiwa katika Wilaya ya Ngara "alisema Dkt Ndugulile .

Naibu Waziri wa Áfya Dkt Faustine Ndugulile akikagua vifaa vya maabara katikati hospitali ya Wilaya ya Ngara mkoa wa Kagera
Naibu Waziri wa Áfya Dkt Faustine Ndugulile akikagua cheti cha Mtoto pindi alipotembelea wodi ya Watoto katika hospitali ya Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera
Naibu Waziri wa Áfya Dkt Faustine Ndugulile akiwaonesha nembo ya vifaa vya Serikali Kamati ya ulinzi na usalama ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Biharamuro Sada Malunde (wakushoto). 

RAIS MAGUFULI AHIMIZA WATENDAJI WA SERIKALI KUSIMAMIA ILANI YA CCM

$
0
0
*Awaambia katika hilo hakuna 'Neutral', agusia uwajibikaji

*Akumbusha Kafulila alivyoitwa Tumbili kwenye sakata la IPTL

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

RAIS Dk.John Magufuli amewataka viongozi wa ngazi mbalimbali nchini kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kikamilifu na kusimamia vema utekelezaji wa Ilani.

Amesema kuna watendaji wa Serikali ambao wamekuwa wakidai hawawezi kufuata Ilani kwa madai ya kuwa wapo Neutral na kwamba katika hilo hakuna Neutral kwani lazina Ilani itekelezwe.Dk.Magufuli ametoa kauli hiyo leo Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa tukio la kuwaapisha wakuu wa mikoa, Makatibu wakuu,manaibu makatibu wakuu pamoja na makatibu tawala ambao aliwateua mwishoni mwa wiki iliyopita.

Hivyo baada ya kuwaapisha viongozi hao Rais Magufuli amehimiza utendaji kazi kwa viongozi wa ngazi mbalimbali ili kuwatumikia vema Watanzania.
Amesema kuwa nchi yetu idadi ya watu ni milioni 55 hivyo waliopata nafasi imetokana na mipango ya Mungu na si kwa matakwa yao.Ameongeza kila aliyekuwa kwenye nafasi atambue yupo hapo kwasababu Mungu ameeamua na hata yeye kuwa Rais ni mpango wa Mungu.

Hivyo amewataka viongozi wote kwa ngazi mbalimbali kuanzia juu mpaka chini kila mmoja kwa nafasi yake afahamu yupo hapo kwasababu Mungu ametaka iwe hivyo na lazima wafanye kazi.Wakati anahimiza utendaji kazi na ushirikiano ameeleza umuhimu wa watendaji wa Serikali kuisimamia na kuitekeleza Ilani ya uchaguzi mkuu.
.KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

WALIMU NCHINI WATAKIWA KUTUMIA MTANDAO KUBORESHA UFUNDISHAJI WAO

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

Baadhi ya walimu wa shule za sekondari nchini ambao wameshiriki katika maonesho ya Young Scientists Tanzania yanayoendelea katika ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Nyerere, wamekubali kuwa wao ndio wamekuwa wazito kubadilika na mazingira ya teknolojia ya ufundishaji katika karne hii ya 21.

Hayo yamesemwa na Mtalaamu wa Mawasiliano kutoka Dot Tanzania , Ndimbumi Mwisongole alipokuwa akitoa majumuisho kwa walimu hao ambao wameshiriki mafunzo maalumu yaliyaondaliwa na Mfuko wa Ufadhili na Kuendeleza Ubunifu na Maendeleo ya watu (HDIF).

“tumeweza kuzungumza na walimu Zaidi ya 50 ambao wameshiriki warsha hii na wote wamekiri kuwa wao ndio wamekuwa wazito kubadilika kutokana na Teknolojia inavyokwenda katika sekta ya elimu.

Mwisngole amesema kuwa umefika wakati wa Walimu kuanza kubadilika na kutumia mtandao kwa ajili ya kupata matirio ya kufundishia ambayo wameyapata popote wanaposafiri kwenda kufundisha” amesema Mwisongole.Mwisongole ametoa wito kwa walimu wote kote nchini kuanza kutumia mtandao kwa ajili kujipatia matio ya kufundushia nakuacha kufikiaria kutembea na mavitabu mengi wakati wanaweza kutimia mtandao kuhifadhi kazi zao.

Kwa upande wake Mtengenezajai wa Vikaragosi vya Ubongo Kids Nisha Ligon amesema kuwa programu yake imekuwa kivutio kikubwa sana kwa watoto na kusaidia kuongeza uelewa mashuileni .
Kiongozi Mkuu wa Shirika la Ufadhili wa Ubunifu kwa Maendeleo ya Binadamu(HDIF), David Mc. Ginty akizungumza na Walimu wanaoshiriki Maonesho ya Wanasayansi Chipukizi ambapo tasisi yake ya HDIF ilipata Wasaa wa kutoa Mhadhara juu ya Ubunifu kwa walimu wa Masomo ya Sayansi Jijini Dar es Salaam.
Meneja Mawasilinao wa Taasisi Digital Opportunity Trust (Dot Tanzania), Ndimbumi Mwesongole akizungumza na Walimu kuhusu progarmu ya elimu kupitia mtandao kwa walimu kujipatia mtandao.
Mwanzilishi na Muongozaji wa Programu ya Vikaragosi vya kufundishia vya Ubongo Kids , Nisha Ligon akizungumza kuhusu uzoefu wake wa kufundisha kwa kutumia Vikaragosi kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari .
Mmoja wa Walimu walioshiriki katika Warsha hiyo iliyoandaliwa na HDIF akichangia mada wakati wa mafunzo.
Sehemu ya Walimu walioshiriki katika Mafunzo hayo wakifatilia kwa makini mafunzo yanayotolewa na wataalamu.

WANANCHI BAGAMOYO WAHIMIZWA KUJENGA VYOO BORA

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, BAGAMOYO

Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kwa kushirikiana na taasisi ya WEPMO (Water and Environmental Sanitation Projects Maintanance Organisation) imewahimiza wananchi kujenga vyoo bora kwani inaonyesha kaya zenye vyoo vilivyoboreshwa vyenye kutumia maji na sakafu inayosafishika ni asilimia 50 pekee.

Pande hizo zipo katika utekelezaji wa mradi wa uboreshaji wa afya na usafi wa mazingira kwa halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo.Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo, Fatuma Latu akizungumza katika utambulisho wa mradi huo utakaotekelezwa kupitia kampeni ya “Usichukulie Poa nyumba ni Choo” alisema, halmashauri imekuwa ikifanya uhamasishaji huo kupitia maafisa afya wa kata kila mara.

"Mradi huu unatekelezwa katika kata zote 11 za halmashauri ambapo wananchi wanahamasishwa kujenga vyoo bora kwa bei nafuu na kuelimishwa juu ya umuhimu wa kila nyumba kuwa na choo bora" alisema Fatuma.Fatuma aliiwashukuru taasisi ya WEPMO kwa kuja kuongeza nguvu katika uhamasishaji huu wa ujenzi wa vyoo bora.

Alielezea “Ni lazima kila mmoja afanye wajibu wake, wataalam wawajengee wananchi uelewa juu ya ujenzi na utumiaji wa vyoo bora""Ni vyema wananchi wakaelewa kwanza kabla watendaji wa kata hawajatumia nguvu na sheria kwa watakaokaidi kujenga na kutumia vyoo bora katika kaya zao kwa kuwafungulia mashauri katika mabaraza ya kata”alisisitiza.

Nae mratibu wa mradi huu wa uboreshaji wa afya na usafi wa mazingira katika halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo, Renatus Rweyemamu alisema katika utafiti wa awali uliofanywa na taasisi hiyo, hali ya afya na usafi wa mazingira inaonesha asilimia 84 pekee ndio wananchi wenye kaya zenye vyoo vya kawaida.Alisema , yaani aina yoyote ya choo kinachotenganisha kinyesi na mazingira hata vile visivyosafishika, ilihali, kaya zenye vyoo vilivyoboreshwa vyenye kutumia maji na vyenye sakafu inayosafishika ni 50% .Rweyemamu alielezea , vyoo vyenye vifaa vya kunawia mikono zikiwa ni asilimia 18 pekee. 

Alifafanua ,lengo la mradi huo ni kuongeza ufahamu kwa wananchi kutambua athari za kujisaidia ovyo katika mazingira .
Mratibu wa mradi wa Uboreshaji sekta ya Afya na usafi wa mazingira H/W Bagamoyo Renatus Rweyemamu akitoa maelezo ya mradi kwa wataalm wa halmashauri.( picha na Mwamvua Mwinyi)
Afisa Afya Wilaya ya bagamoyo Bi. Joyce Nganzo akichangia mada wakati wa utambulisho wa mradi wa uboreshaji sekta ya Afya na Usafi wa mazingira Bagamoyo.
1. Picha ya pamoja ya wataalamu wa Halmashauri, Watendaji wa kata za bagamoyo na wataalamu wa Taasisi ya WEPMO mara baada ya utambulisho wa mradi wa uboreshaji sekta ya Afya na usafi wa mazingira katika Halmashauri ya Wilaya ya bagamoyo.( picha na Mwamvua Mwinyi)

UPANDE WA MASHITAKA WAIOMBA MAHAKAMA KUSIMAMISHA USHAHIDI ULIOTOLEWA NA KATIBU MKUU TFF

$
0
0
Na Ripota maalum, Globu ya jamii

UPANDE wa mashtaka katika kesi ya kugushi na utakatishaji wa fedha inayomkabili aliyekuwa Rais wa TFF Jamal Malinzi na wenzake wameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusimamisha ushahidi uliotolewa na Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidau ili waweze kumuita mtaalam wa Sayansi ya Tehama kutoa nyaraka za email alizozitoa katika kompyuta na kuchapisha(print).

Wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru), Leornad Swai ameeleza hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, kesi hiyo ilipopangwa kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa kwa ushahidi wa Kidao.Swai amedai kesi hiyo ilipangwa kuendelea kusikilizwa, lakini imewapasa kumtumia Mtaalam wa Sayansi ya Tehama kwa kuwa yeye ndiyo aliyeta email katika kompyuta, kuichambua na kuichapisha (Print).

Na kuongeza kuwa wamefanya tafiti katika ushahidi wa vielelezo vya kielektloniki na kwamba ili kujenga msingi wa ushahidi wanaoutoa kutokana na maelekezo ya sheria ni vema wakasimamisha kwanza ushahidi uliopo ili mtu huyo aweze kutoa hizo nyaraka.Amedai kuwa, mtu huyo anauwezo wa kuitoa mahakamani kama sehemu ya kielelezo cha ushahidi na mashahidi wengine kuielezea.

WAJAWAZITO WANATAKIWA KUPATA HUDUMA ZA UZAZI BURE.

$
0
0
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesisitiza kuwa huduma za uzazi kwa wajawazito zinatolewa bila ya malipo katima Hospitali na vituo vya afya vya Serikali. 

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa ziara yake ya kujua hali ya utoaji wa huduma za afya katika Hospitali ya Rufaa Temeke, Amana na Mwananyamala leo jijini Dar es salaam. 

"Nimesikia pale wajawazito wameniambia wamekuja na vifaa vya kujifungulia kutoka majumbani mwao sitaki kusikia mwanamke mjamzito analipishwa wala kuja vifaa vya kujifungulia kwani sera yetu inasema huduma za uzazi ni bure" alisema Dkt. Ndugulile. 

Aidha Dkt. Ndugulile alisema kuwa wanawake wajawazito , watoto chini ya miaka 5 na wazee wasio na uwezo wanapata matibabu bure kulingana na sera ya Afya inavyosema. Mbali na hayo Dkt. Ndugulile amesema kuwa kila mtoa huduma anapaswa kuandika taarifa ya mgonjwa kabla na baada ya kumpa huduma katika kituo chake cha kazi.Aidha Dkt. Ndugulile aliwataka watoa dawa katika hospitali na vituo vya afya kuandika majina asilia ya dawa na siyo yale ya kampuni pamoja na kufuata muongozo wa dawa uliyowekwa na Serikali. 

"Marufuku watoa dawa kuwaandikia wagonjwa dawa na kwenda kununua nje ya kituo cha afya na badala yake dawa zote zitolewe katika hospitali au kituo cha afya kama zimeisha zinatakiwa kuagizwa kwa haraka na nauagiza uongozi wa Hospitali ya Amana kuwarudishia wagonjwa wa wodi ya watoto waliokwenda kununua dawa nje leo hii " alisema Dkt. Ndugulile. 

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Temeke Dkt. Amaan Malima amesema kuwa changamoto kubwa inayowakumba ni upungufu wa watumishi .

Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Hospitali ya Rufaa ya Amana Dkt. Meshack Shimwela amesema kuwa anaomba radhi kwa tatizo hilo lililojitokeza kwani hakuna tabia kama hiyo hospitalini hapo na amehaidi kulifanyia kazi haraka iwezekanavyo.
Naibu Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwajulia hali baadhi ya wagonjwa waliofika kupata huduma kwenye Hospitali ya Rufaa Temeke wakati wa ziara yake ya kujua hali ya utoaji huduma za afya Hospitalini hapo.
Naibu Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua akiangalia dawa zinazopatikana katika Stoo ya dawa ya Hospitali ya Rufaa Amana wakati wa ziara yake katika hospitali hiyo leo jijini Dar es salaam. 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua taarifa za maabara katika Hospitali ya Rufaa ya Temeke leo jijini Dar es salaam, katikati ni Mganga mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Amaan Malima.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA NCHI WA MAMBO YA NJE WA JAPAN, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Nchi  wa Mambo ya Nje wa Japan Masahisa Sato mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Waziri wa Nchi  wa Mambo ya Nje wa Japan Masahisa Sato zawadi ya Kinyago pamoja na Picha ya Mlima Kilimanjaro mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri wa Nchi  wa Mambo ya Nje wa Japan Masahisa Sato mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

MBWA HAJAPOTEA ILA ALIKUWA MAFUNZONI KATIKA BWALO LA POLISI-MSEMAJI JESHI LA POLISI

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MSEMAJI wa Jeshi la Polisi nchini Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Barnabas Mwakaluka amesema mbwa anayedaiwa kupotea hakuwa amepotea bali alikuwa katika mafunzo.

Amesema mbwa huyo alikuwa katika bwalo akiendelea na mafunzo na hivyo amewaomba Watanzania kufahamu hakuna mbwa aliyepotea.

Akizungumza na Michuzi Blog kwa njia ya simu leo jijini Dar es Salaam Mwakaluka amefafanua mbwa anayedaiwa kupotea yupo kwenye mikono salama ya Jeshi la Polisi na kwamba yupo kwenye mafunzo.

Amefafanua kuwa wakati wa ziara ya Waziri wa Mambo Ndani alipokwenda bandarini hakumkuta mbwa hiyo hivyo baadhi ya waandishi wakadhano amepotea lakini ukweli ni kwamba alikuwa mafunzoni.

"Mbwa yupo kwenye mikono salama na yupo kwenye mafunzo,habari ya kwamba mbwa ameonekana Kenya si kweli," amefafanua.Alipoulizwa mbwa huyo alikuwa katika mafunzo ya aina gani,Mwakaluka amejibu hawezo kuelezea aina ya mafunzo ambayo amepewa kwani hayo ni mambo ya kitaaluma na ni kwa ajili ya Polisi.

Kuhusu cheo cha mbwa huyo amesema hana cheo bali ni mbwa mwenye mafunzo ya polisi na wameamua kutoa ufafanuzi huo ili umma ujue kuwa mbwa yupo na wala hajapotea.
Viewing all 110089 articles
Browse latest View live




Latest Images