Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live

Saturday 31 August 16.30 CHAP CHAP PLASTIC and 18.30 MUZIKI with Leo Mkanyia, DDI Dancers and Hoko Roro Band at Nafasi Art Space

$
0
0
Dear All
 This Saturday CHAP CHAP PLASTIC, come and join us in making art out of plastic bags, for young and old at 16.30 Followed by music and dance at 18.30 with Leo Mkanyia, DDI dancers and Hoko Roro Band
Free!


Kijana Lelo Elvis Munis aendesha baiskeli toka chile hadi tanzania kusaidia watanzania wenzake kupata nondozzz

$
0
0
Balozi wa Tanzania Ufaransa, Mhe. Begum Taj, akiwa na Lelo Elvis Munis, kijana ambae anaendesha baiskeli yake kutoka Chile, iliyoko Marekani Latini, kurudi nyumbani Tanzania, katika juhudi za kukusanya fedha za ada ya kuwezesha vijana 10 kusomea shahada za kuhifadhi mazingira na maendeleo endelevu katika vyuo vya elimu ya juu.  
Leo Lelo alikatiza safari yake kidogo na kwenda kusalimia Ubalozini Paris. Vile vile alikaribishwa kwenye kituo cha televisheni cha France 24 na kituo cha redio cha Radio France Internationale (RFI) ambako alimhojiwa juu ya safari na malengo yake.  Mahojiano aliyofanya France 24 yanaweza kuonekana hapa http://www.france24.com/en/20130827-2013-08-27-2146-africa-news.


Kutoka Paris, Lelo ataelekea kusini mwa Ufaransa kisha atavuka mpaka kuelekea Spain na Ureno. Kwa habari zaidi juu ya safari ya Lelo na kuweza kuchangia mradi huu wa kusomesha vijana wa Tanzania, tafadhali nendeni kwenye Tovuti yake iliyopo kwenye anwani hii:    www.chiletokili.com.

UKAGUZI WA NGUVU WAKATI WA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA MARCH ON WASHINGTON,MAREKANI

$
0
0
Leo, waMarekani wameadhimisha miaka 50 tangu kufanyika kwa maandamano makubwa ya kudai haki za watu weusi. Katika maadhimisho hayo, kamera ya swahilivilla blog iliegeshwa kando ya mlango wa kuingila na kushuhudia watu maarufu hapa nchini wakipekuliwa kwa sababu za usalama kabla ya kuingia ndani sherehe hizo ambazo ambazo zimehudhuriwa na maelfu ya watu kutoka sehemu mbali mbali nchini hapa.
Tuliobahatika kuwanasa katika kamera hiyo ni pamoja na muigizaji Jamie Foxx, pale alipotolewa ndani ya gari na maofisa kuanza kupekua gari alilolipanda kabla ya kuingia ndani ya eneo la Lincoln Memorial  Washington DC. 
Mwigizaji wa filamu Angelha Bassett Evelyn alipotolewa kwenye gari lake na  maofisa kuanza kulipekua kabla ya kuingia ndani ya eneo la Lincoln Memorial  Washington DC
Mshangao mkubwa watu walioupata ni pale mtoto wa Rais wa zamani nchini Marekani John F. Kennedy, Caroline Kennedy ambae ni balozi mteule Nchini Japani, alipoingia na Cab (Taxi). cha kuchangaza pia ni pale gari lake lilipopekuliwa bila ya kujali ukubwa au cheo alichonacho na kufata sheria ya upekuzi kama wengine magari yao yalivyopekuliwa.
Muigizaji maarufu wa filamu nchini Marekani Forest Whitekar nae pia gari lake lilifanyiwa upekuzi na maofisa wa usalama baada ya kuwasili katika endeo la Sherehe za miaka 50 ya March on Washington DC
Vile vile kamera ya swahilivilla blog imemnasa Rajiv “Raj” Shah American Economic development specialist, alipotolewa nje ya gari lake na kufanyiwa upekuzi wa lazima siku ya Jumatano Aug 28, 2013 Washington DC
Watu tupo kazini..: Ofisa Usalama akifanya upekuzi wa magari ya watu maarufu yanayoelekea katika maadhimisho ya miaka 50 ya March on Washington DC siku ya jumatano Aug 28.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI 

Article 5

Mtandao wa Jinsia Tanzania Wafanya Mazungumzo na Wahariri wa Habari jijini Dar leo

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Usu Mallya (wa pili kulia) akizungumza na wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari. Alioambatana nao ni viongozi anuai, watendaji na baadhi ya wanachama wa TGNP. katika mkutano na wahabari. Sehemu ya jopo la viongozi na wanachama wa TGNP wakiorodhesha maswali ya wahariri (habapo pichani) kabla ya kuanza kuyatolea majibu kwenye mkutano huo leo. Baadhi ya wahariri kutoka vyombo vya habari jijini Dar es Salaam wakiwa katika mkutano na TGNP.

 Katika mkutano huo na wahariri TGNP imeainisha baadhi ya mafanikio na changamoto ambazo mtandao huo umezipata, ikiwa mbioni kufanya tamasha la mwaka huu ambalo litafanyika Septemba 3 hadi 6 2013, Katika viwanja vya TGNP Mabibo. 

TGNP inatarajia kutumia Tamasha la Jinsia kuwapa wanawake fursa ya kushiriki mijadala ya wazi na kupaaza sauti zao, tamasha hili litashirikisha wanawake, wanaume, Vijana na watoto zaidi ya 5000 kutoka mikoa yote ya Tanzania na nchi mbalimbali za Afrika, Ulaya na Amerika. 

TGNP imebainisha kuwa kupitia Tamasha hilo, wanawake na wanaume wanaoshiriki wanapata fursa ya kujijengea uwezo wa kutumia mbinu za kiraghibishi katika, uchambuzi wa sera , bajeti ya kijinsia, kujadili kwa pamoja na watendaji wa serikali kuu na za mitaa walioalikwa namna bora ya utoaji huduma ambazo zitamfikia kila mwananchi. 

Pamoja na mijadala hiyo ya wazi, kutakuwa na mahakama ya wananchi (Popular tribunal) itakayoendeshwa na Chama cha Majaji Wanawake (TAWJA), watunga sera, wanasheria, wanaharakati waliobobea kwenye masuala ya Kisheria na wananchi walioathiriwa na mfumo kandamizi na kukosa msaada wa kisheria au kuathika na hukumu zilizotolewa.

 Aidha siku inayofuata kutakuwepo na Bunge la wananchi ambalo litaongozwa na wanazuoni na wataalamu wa sheria na wananchi wote watapata fursa ya kushiriki kikamilifu. Mijadala mingine italenga katika masual ya haki ya uchumi kwenye upatikanaji wa huduma za msingi za jamii kama maji, afya, elimu, miundombinu na haki ya jamii katika umiliki wa rasilimali ardhi. 

Aidha suala la Katiba mpya litapewa kipaumbele katyika mijadala itakayopfanyika ikiwepo kuendelea kudai ushiriki ulio sawia katika fursa na michakato iliyosalia kufikia kupata katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AAGANA NA RAIS WA BURUNDI BAADA YA KUMALIZA MAPUMZIKO YAKE NCHINI

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza, wakati akiondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo, Agosti 29, 2013 baada ya kumaliza mapumziko yake ya siku tatu nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsindikiza Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza, wakati akiondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo, Agosti 29, 2013 baada ya kumaliza mapumziko yake ya siku tatu nchini.
Rais wa Burundi, Piere Nkurunzinza, akiagana na baadhi ya maofisa wa Ofisi ya Makamu wa Rais, waliofika uwanjani hapo kumsindikiza leo Agosti 29, baada ya Rais huyo kumaliza mapumziko yake ya siku tatu nchini. Kushoto ni Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na viongozi wengine, wakimuaga Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza, wakati akiondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo, Agosti 29, 2013 baada ya kumaliza mapumziko yake ya siku tatu nchini. Picha na OMR.

Stand up For African Mothers Campaign – Fundraising Gala Dinner

$
0
0
Montage Managing Director Ms.Teddy Mapunda speaks to the media during press conference of announcing the date for Fundraising Gala Dinner which will be on 11th October,2013  at  Dar es Salaam Serena Hotel with the aim of raising funds  for the campaign dubbed “Stand Up for African Mothers”, Dr.Jakaya Kikwete is expected to be the guest of honour.


AMREF Country Director Dr. Festus Ilako speaks to the media during press conference of announcing the date for  Fundraising Gala Dinner which will be on  11th October,2013 at Dar es Salaam Serena Hotel with the aim of raising funds for the campaign dubbed “Stand Up for African Mothers”, Dr.Jakaya Kikwete is expected to be the guest of honour,and the target is to raise 1 billion Tanzanzanian Shillings.On the left side is  Montage Managing Director Ms.Teddy Mapunda and AMREF Deputy Country Director Dr.Rita Noronha(R). 

LAW ACADEMICS CONSTITUTIONAL FORUM (LACF)

$
0
0
From August 30 -31, 2013, Nkrumah Hall, at the Mwalimu Nyerere campus of UDSM, shall be the venue of a LACF meeting to discuss and debate in an atmosphere of academic rigour and impartiality, the following key areas of the Draft Constitution, namely, ‘Citizenship’; Human Rights & Gender; ‘The Union & Union Matters’; “legislature’; ‘Judiciary’; ‘Elections & The Electoral Commission’; ‘Finances of the United Republic’; and “International Legal Dimensions of the Draft Constitution’.

Carefully selected speakers will lead the debate by focusing on the relevant provisions of the Draft Constitution, highlighting the key issues, gaps, and possible approaches for consideration, by the CRC and nation at large. They include, Prof. Mgongo Fimbo, Prof Issa G. Shivji, and Prof. Chris Maina Peter.

LACF, established in accordance with Constitution Review Act, 2012, is the collective forum of over 12 Universities, Colleges and related institutions, offering courses in the legal field. Its primary objective is to facilitate the widest possible participation of law lecturers and tutors, in the ongoing constitutional review process. 

More specifically, to bring non-partisan and expert knowledge, to the debate over the constitutional process in general, and the Draft Constitution of June 2013, in particular, and in doing so, fulfill a key and sensitive professional and civic duty to the nation.

LACF is structured around four regional chapters: Lake and Central Zone (with St Augustine University – SAUT, as Convenor); North Eastern Zone (Convenor, Tumaini University, Makumira); Southern Highlands (Convenor, Ruaha University College); and Coastal & South East (Convenor, UDSM School of Law).

LACF members will be joined by, among others, representatives of central Government (Executive, Judiciary and Legislature from both sides of the Zanzibar Channel), Youth and Student Bodies, Members of the Constitutional Review Commission (CRC), Commission for Human Right & Good Governance, Media, and representatives of civil society. 

Among invitees are also members of the diplomatic corps, whose countries have related challenges in their respective systems of Government structure, or have just emerged from a review of national Constitutions.

Dr. Khoti Chilomba Kamanga
Chair, Organising Committee of the LACF Conference

RC MULONGO AKUTANA NA MKURUGENZI WA HABARI WA MAELEZO OFISINI KWAKE

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Magessa Mulongo(kulia) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).

Angalia Bongo Views Mada kuhusu Madawa ya Kulevya

$
0
0
Kipindi cha cha BONGO VIEWS ndani ya Global Entertainment and News Network (GENN) iliyopo Kansas City nchini Marekani, siku ya jumamosi Aug 24, 2013 kilizungumzia kuhusu athari za  madawa ya kulevya Nchini Tanzania
Kipindi cha Bongo Views kitaendele tena hewani LIVE wiki hii siku ya Jumamosi Aug 30, 2013 MIDA ya Saa 5: PM kwa Saa za Marekani ya kati. Saa 6:PM jioni kwa Saa za EST US. Na Tanzania Saa 1:AM Usiku kwa wale wanaopenda kukesha wasikose kutembelea. 
 MADA: KUHUSU MUUNGANO
kuchangia kwa njia ya simu ..Utapiga simu number (913) 662-1190

Kingunge Ngombale Mwiru Avunja Ukimya Juu ya Mchakato wa Katiba Mpya

$
0
0

Mzee Kingunge Ngombale Mwiru
 Mwanasiasa Mkongwe nchini Bw.Kingunge Mwilu akisisitiza jambo wakati wa majumuisho ya maoni ya Rasimu ya katiba mpya yaliyotolewa na wanachama wa Tiba asilia kupitia mabaraza ya asasi  katika Hoteli ya Twins Park wilaya ya Bagamoyo,kushoto ni Mwenyekiti wa chama hicho Bw.Simba A. Simba.
 Mwenyekiti wa Chama cha Watabibu wa dawa  za Asili Tanzania(ATME) Bw.Simba A. Simba akifungua mkutano wa majumuisho ya maoni ya Rasimu ya katiba mpya yaliyotolewa na wanachama wa Tiba asilia kupitia mabaraza ya asasi  Hoteli ya Twins Park wilaya ya Bagamoyo.
Mwanasiasa Mkongwe nchini Bw.Kingunge Mwilu akimkabidhi cheti mmoja wa Matabibu wa tiba asilia Bw. Juma Juma wakati wa majumuisho ya maoni ya Rasimu ya katiba mpya yaliyotolewa na wanachama wa Tiba asilia kupitia mabaraza ya asasi  Hoteli ya Twins Park wilaya ya Bagamoyo wa kwanza  kushoto ni Boniventure Mwalongo Maratibu,wa pili kushoto Bw Adamu Chamwamba mwenyekiti Mkoa wa Pwani na wa tatu kushoto ni Mwenyekiti wa chama hicho Bw.Simba A. Simba.
 Wanachama na matabibu wa Tiba Asilia nchini wakifuatilia jambo kutoka kwa mgeni rasmi  Mwanasiasa Mkongwe nchini Bw.Kingunge Mwilu  wakati wa majumuisho ya maoni ya Rasimu ya katiba mpya yaliyotolewa na wanachama hao  kupitia mabaraza ya asasi  Hoteli ya Twins Park wilaya ya Bagamoyo kwanza  kushoto Bw. Adamu Chamwamba mwenyekiti Mkoa wa Pwani,katikati  ni Mwenyekiti wa chama hicho Bw.Simba A. Simba.
 Mwanasiasa Mkongwe nchini Bw.Kingunge Mwilu  katika waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa Tiba Asilia pamoja na Matabibu waliotunukiwa vyeti wakati wa majumuisho ya maoni ya Rasimu ya katiba mpya yaliyotolewa na wanachama wa Tiba asilia kupitia mabaraza ya asasi  katika Hoteli ya Twins Park wilaya ya Bagamoyo kwanza  kushoto Bw. Adamu Chamwamba mwenyekiti Mkoa wa Pwani,katikati  ni Mwenyekiti wa chama hicho Bw.Simba A. Simba.Picha zote na Lorietha Laurence-Maelezo
 --
Na Hussein Makame, MAELEZO
MWANASIASA mkongwe nchini na Mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kingunge Ngombale Mwiru amewataka Watanzania wasikubali kuyumbishwa kama nchi kuhusu umoja wa kitaifa, udugu na mshikamano na amani na utulivu wakati wa mchakato wa kutoa maoni ya kuunda katiba mpya.

Kingunge alitoa angalizo hilo kwenye mkutano wa kufunga rasmi mabaraza ya katiba yaliyo chini ya Chama cha Watabibu wa Tiba Asili (ATME) uliofanyika mjini Bagamoyo juzi.
Mwanasiasa huyo alitoa angalizo hilo baada ya kueleza kuwa kuna baadhi ya watu wakiwemo wanasisasa kutoa maoni ya kuunda katiba mpya yanayolenga kuvuruga umoja wa kitaifa, udugu na mshikamano na amani na utulivu.

Alisisitiza kuwa kwa sasa Tanzania umoja wa kitaifa tumeshika pazuri, kwenye udugu na mshikamano tumeshika pazuri, lakini kwenye utulivu na amani hali si nzuri sana baada ya kujitokeza watu wanaotaka kuuchafua.

“Kwa hiyo nasema iko kazi ya kufanya lazima tuendelee kuweka msimamo, tusikubali kuyumbishwa kama nchi, kwenye umoja wa kitaifa tumeshika pazuri, kwenye udugu na mshikamano tumeshika pazuri, kwenye utulivu na amani tumeshika pazuri ingawaje wenyewe sasa hivi tunachafua” alisema Kingunge.

Alifafanua kwa kuwataka Watanzania watoe mawazo ya kujenga na sio mawazo ya kuwagawanyisha Watanzania na kuwafanya waishi katika maisha yatakayoliangamiza taifa miaka ijayo.

Alisema kuwa kuna mwanasiasa mmoja visiwani Zanzibar amesema kuwa Muungano wa Tanzania Bara na Zanzibar mzee Karume alitishwa ndio maana akakubali kuunda muungano huo, jambo ambalo si kweli.

Akizungumzia tiba asili, Kingunge alikitaka ATME kwanza wajenge uhalali wa shughuli zinazofanywa na wanachama wake kwa kuanza kupiga vita upotoshaji wa wale ambao si watibabu wa tiba asili.

“Kupiga vita upotoshaji ni pamoja na kutazama, kufuatilia vitendo vya wanachama wenu kwa sababu wanaweza kuwa sehemu ya upotoshaji kama wanakosa uadilifu wa shughuli za tiba asili na kuingiza mazingaombwe na mambo ambayo ni ya usanii” alisema Kingune.

Aliongezakuwa kuwa tiba asili zipo na hazihitaji kupotoshwa na watabibu wa tiba hizo wanaoendesha kwa kuchanganya na ramli kwani tiba asilia ya kweli na ujanja ni upotoshaji.

Aliwashauri ATME na wanachama wake kujikita katika kufanya utafiti wa tiba mbalimbali na kutafuta ukweli juu ya mambo mbalimbali kwani kwa kufanya hivyo watapata maarifa mengi ya kuwasaidia kutoa tiba kwa uhakika.

Akisoma risala ya ATME, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Othman Shem alisema katika mabaraza ya katiba yaliyoandaliwa chini ya chama hicho, wameshirikisha mikoa 25 na wilaya 133.

Alitaja baadhi ya mambo yalipendekezwa kwenye mabaraza hayo kuwa ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaje tiba asili kuwa ni huduma ya siha, haki za binadamu liwe suala la muungano na rasilimali za taifa ziwe za Muungano.

Mabaraza hayo ya katiba chini ya ATME yalianza mikutano yake mwishoni mwa mwezi uliopita na baada ya kufunga mabaraza hayo, chama hicho kinawasilisha maoni yao leo Agosti 30 kwenye tume ya Mabadiliko ya Katiba

BAN KI MOON ALAANI KUUAWA KWA MLINZI WA AMANI WA TANZANIA DRC

$
0
0
Pichani ni walinzi wa Amani wakiwa katika moja ya doria kwenye mitaa ya mji wa Goma, mwanzoni mwa wiki hii kumetokea mapingano katika eneo la vilima vya Kibati Magharibi ya Kivu ambapo kundi la waasi la M23 lilishambulia walinzi wa amani wa Misheni ya Kutuliza Amani katika DRC ( MONUSCO) waliokuwa katika Operesheni ya kulinda raia wakishirikiana na Majeshi ya Serikali ya DRC. Shambulio hilo limesababisha mwanajeshi Mtanzania kupoteza maisha na wengine 10 wakiwamo wanajeshi wa Afrika ya Kusini wamejeruhiwa. Tukio la kushambuliwa kwa walinzi hao limelaaniwa vikali na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, na Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa. Ban Ki Moon na Baraza Kuu wametuma salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu na familia za wale waliojeruhiwa na kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Afrika ya Kusini. Aidha Baraza Kuu limesisitiza kwamba vitendo vinavyolenga kudhoofisha mamlaka ya MONUSCO havitavumiliwa.

TIMU YA SIMBA YATEMBELEA MACHIMBO YA TANZANITE ONE,MERERANI

$
0
0
Mkuu wa kituo cha polisi Mererani, Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, SP Ally Mohamed Mkalipa, akisalimiana na Abdulhalim Humudi, wakati akiikagua timu ya Simba ilipocheza juzi na timu ya Tanzanite FC, baada ya kutembelea machimbo ya madini ya Tanzanite.
Mchezaji wa timu ya soka ya Simba SC ya jijini Dar es salaam, Edward Christopher, akipatiwa huduma ya kusuguliwa kwenye saluni ya kisasa ya Nick Babershop ya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, baada ya mchezo wa kirafiki uliofanyika jana na Simba ilishinda bao 1-0.Picha na Woinde Shizza,Mererani.

Na Woinde Shizza,Manyara

Timu ya soka ya Simba SC ya Jijini Dar es salaam jana imetembelea machimbo ya madini ya Tanzanite ambapo hapa duniani yanapatikana Mji mdogo wa Mirerani, Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara,Tanzania.

Wachezaji hao wakiongozwa na viongozi wao Makamu Mwenyekiti, Joseph Itangire (Mzee Kinesi) na kocha mkuu Abdalah Kibadeni, walitembelea kampuni ya TanzaniteOne na kujionea namna shughuli za uchimbaji zinavyofanyika.

Hata hivyo, wachezaji hao wakizungumza kwenye machimbo hayo ya madini ya Tanzanite, walisema hiyo ni mara yao ya kwanza kutembelea machimbo hayo kwani awali walikuwa wanasikia Tanzanite katika vyombo vya habari pekee.

Walipotembelea machimbo hayo pia walicheza mchezo wa kirafiki na timu ya Tanzanite FC inayomilikwa na Jofrey Nyigu (Mnyalu) na wakaifunga bao 1-0 lililotiwa kimiani na mshambuliaji wao hatari Abdalah Seseme.

Seseme alifunga bao hilo baada ya kupewa pasi na Ramadhan Singano “Messi” aliyewachambua mabeki wa Tanzanite FC, Elibariki Bryson na Abdilahi Yusuph walioshindwa kumpa ulinzi kipa wao Achibald Kileo.

Baada ya kumalizika mchezo huo wa kirafiki, timu ya Simba ilikwenda kwenye saluni ya kisasa ya Nick Baber shop iliyopo Mirerani na kufanyiwa huduma ya kuchuliwa misuli, kuoga, kusuguliwa uso,miguu na kunyolewa nywele.

Mdau Ruger Kahwa kwenye ufunguzi wa AusAID Emergency Relief Supply Warehouse nchini Papua New Guinea

$
0
0
Mdau Ruger Kahwa kushoto ambaye ni mkuu wa ofisi ya United Nations Office for Coordination of Humanitarian Affairs nchini Papua New Guinea akiwa na Balozi wa Australia nchini Papua New Guinea Ms. Deborah Stokes kulia na Askofu wa jimbo Katoliki la Lae Most Rev. Christian Blouin CMM katikati kwenye hafla fupi mara baada ya ufunguzi wa AusAID emergency relief supply warehouse katika mji wa Lae nchini Papua new Guinea.

Article 19


CCM :TUTAWASAIDIA WAZEE

$
0
0
 Baadhi ya wawakilishi wa Mtandao wa Wazee wakiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye nje ya ofisi za Makao Makuu ya Chama Dodoma leo tarehe 30 Agosti 2013.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na mmoja wa wawakilishi wa Mtandao wa Wazee Bibi Koku , Wazee hao walifika Makao Makuu ya CCM kuja kuzungumza madai ya mafao yao ambayo waliahidiwa na serikali.

Farewell Cocktail for the United States Ambassador to Tanzania, Alfonso E. Lenhardt

$
0
0
The United States Ambassador to Tanzania, Alfonso E. Lenhardt, giving his farewell speech at the farewell cocktail reception held by American Chamber of Commerce in Tanzania on Wednesday, 28th of August 2013 at Hyatt Regency, Kilimanjaro Dar es Salaam.
The American Chamber of Commerce President Bhakti Shah with the AMCHAM Board members presenting their farewell gift to The United States Ambassador to Tanzania, Alfonso E. Lenhardt and his wife Jacqueline Lenhardt.
Group photo of The American Chamber of Commerce in Tanzania (AMCHAM) Board members, with the United States Ambassador to Tanzania, Alfonso E. Lenhardt and his wife Jacqueline Lenhardt at the farewell cocktail reception held by AMCHAM on Wednesday, 28th of August 2013 at Hyatt Regency, Kilimanjaro Dar es Salaam.
The United States Ambassador to Tanzania, Alfonso E. Lenhardt and his wife Jacqueline Lenhardt interacting with their guests during the farewell cocktail reception held by the American Chamber of Commerce in Tanzania (AMCHAM) on Wednesday, 28th of August 2013 at Hyatt Regency, Kilimanjaro Dar es Salaam.

UJUMBE WA ZANZIBAR WAKUTANA NA WAZIRI MKUU NA KUTEMBELEA KAMPUNI YA SAKURA NCHINI UHOLANZI

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha Waziri Mkuu wa Serikali ya Uholanzi Mark Rutte,alipofika katika Ofisi ya Waziri huyo Nchini The Hague Uholanzi akiwa katika ziara na Ujumbe aliofuatana nao.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akiwa katika mazungumzo na Waziri Mkuu wa Serikali ya Uholanzi Mark Rutte,alipofika katika Ofisi ya Waziri huyo Nchini The Hague Uholanzi akiwa katika ziara na Ujumbe aliofuatana nao,(kushoto) Waziri wa Ardhi,Maji,Makaazi na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akifuatana na Mwenyeji wake Waziri Mkuu wa Serikali ya Uholanzi Mark Rutte,baada ya mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi ya Waziri huyo Nchini The Hague Uholanzi akiwa katika ziara ya Kiserikali na Ujumbe aliofuatana nao.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Bibi Regine Aalders,kutoka Wizara ya Afya nchini Uholanzi,wakati alipotembelea katika Ofisi ya Kampuni ya Sakura Finatek jana,ambayo inatengeneza Vifaa vya maabara vya Uchunguzi wa Binadamu,nje ya Mji wa The Hague Nchini Uholanzi akiwa katika ziara ya Kiserikali.

MHE. BALOZI LIBERATA MULAMULA ATEMBELEWA NA BALOZI WA ZAMANI WA MAREKANI NCHINI TANZANIA CHARLES STITH

$
0
0
 Mhe.Balozi Liberata Mulamula, Balozi wa Jamhuri ya Muungano waTanzania nchini Marekani na Mexico akiwa katika picha ya pamoja na Mhe.Charles Stith,Balozi wa zamani wa Marekani nchini Tanzania,Tanzania House,Washington DC
Mhe.Liberata Mulamula,Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico akiwa katika picha pamoja na Mhe. Charles Stith,Balozi wa zamani wa Marekani nchi Tanzania. Kulia ni Bw.Suleiman Saleh,Afisa Ubalozi wa Tanzania Washington DC

Mhe.Liberata Mulamula, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico ametembelewa na aliyekuwa Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Charles Stith Ubalozini Tanzania House Washington DC juzi Jumatano Agosti 27,2013. Balozi Stith alifika Ubalozi hapo kusalimiana na Balozi Mulamula na kumpongeza kwa kuchaguliwa kwake kushika wadhifa wake mpya wa kuiwakilisha Tanzania nchini Marekani.

 Katika mazungumzo yao,Balozi Stith alionyesha dhamira kubwa na utayari wake kushirikiana na Mhe.Balozi Mulamula katika kujenga mashirikiano baina vyuo vikuu vya Marekani na vile vya Tanzania. Balozi Stith alimweleza Balozi Mulamula kwamba anaifahamu vizuri Tanzania na ni nchi ambayo amekuwa na mahusiano mazuri pamoja na watu wake akiwa Balozi na hadi sasa. Kwa msingi huo, Balozi Stith alibainisha umuhimu wa kuweka mkakati mahususi wa kukamilsha azma hiyo na kuahidi kwamba muda wowote kuanzia sasa yupo tayari katika kutekeleza dhamira hiyo.

A LAUGH A DAY KEEPS DOCTOR AWAY - BACK BY POPULAR DEMAND

$
0
0
HOW TO KNOW YOUR PHONE IS MADE IN  CHINA

1. It gets full after 3 minutes of charging

2. The phone has TV, Touch screen, Nail cutter, firelighter, kitochi etc.

3. Text message can be written with a toothpick.

4. There are some spelling mistakes e.g NokLa, blackderry, i-porn, samswag etc.

5. When an aeroplane passes by; it records "one missed call".

6. When a big truck hoots; it records "charger connected".

7. When a Chinese man passes by you it says "one Bluetooth device found". 

Joy, Love, and Peace.
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live




Latest Images