Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109587 articles
Browse latest View live

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA


SERIKALI IPO KATIKA MAPITIO YA MPANGO KABAMBE WA TAIFA WA UMWAGILIAJI ILI KUFIKIA TANZANIA YA VIWANDA

0
0
Serikali imefanya mapitio ya mpango kabambe wa Taifa wa umwagiliaji wa mwaka 2002 kupitia Tume ya Taifa ya umwagiliaji ikiwa na lengo la kuongeza uzalishaji kwa hekta zaidi ya milioni moja nchini kufikia mwaka 2025 kupitia kilimo cha umwagiliaji ili kuweza kukuza uchumi, kuongeza chakula na malighafi za viwandani. 

Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi wa Mipango, Usanifu na Sekta Binafsi kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Mhandisi Muyenjwa Maugo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari. 

Bw. Maugo Alisema kuwa, Mpango huo kabambe unabanisha kuwa kupitia kilimo cha umwagiliaji chenye kutumia maji ya uhakika na kwa wakati mkulima anaweza kuzalisha awamu mbili au tatu kwa mwaka, na kuwa na uhakika wa chakula kwa kuzalisha tani nane (6) mpaka kumi (10) kwa Hekta tofauti na kilimo cha kutegemea mvua za msimu ambapo mkulima anaweza kupata tani mbili (2) za mazao kwa mwaka kwa hekta, hivyo kwa kuimarisha kilimo cha umwagiliaji malighafi za viwandani zinaweza kupatikana kwa wakati na kufikia hazima ya serikali ya kuijenga Tanzania ya viwanda. 

“Mpaka sasa eneo la hekta laki 475 ndilo linalotumika kwa kilimo cha umwagiliaji nchini ambayo ni sawa na 1.6% kati ya hekta milioni 29.4, na kuchangia asilimia 24 (24%) ya uzalishaji wa chakula nchini, tuna uwezo wa kuongeza na kufikia asilimia 50 (50%) na tuna lengo la kufikia Hekta milioni moja” Alisisitiza Maugo. Aliendelea kusema kuwa Mpaka sasa kuna skimu 2947 za kilimo cha umwagiliaji nchini ambapo skimu zinazofanya kazi ni 1976, na mpango kabambe upo na malengo ya kuzifufua skimu zisizofanya kazi ili ziweze kufanya kazi. 

Awali Mhandisi Maugo alisema kuwa mapitio ya Mpango huo kabambe wa kilimo cha umwagilaji unafanyika kwa ushirikiano wa Shirika la Maendeleo la Japan JICA. 
Kulia Mhandisi Muyenjwa Maugo, Kaimu Mkurugenzi wa Mipango Sanifu na Sekta Binafsi kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji akiongea na Muhariri wa kituo cha Televison cha StarTv, Dar es Salaam Leo Bw. Bernad James katika majadiliano maalum kuhusu, kilimo cha umwagiliaji na Tanzania ya viwanda.( Picha na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji).

NEW MILLENIUM WACHANGIA SH. MILIONI 4 MATIBABU YA MOYO KWA WATOTO

0
0

MKE wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa amewaongoza wake wa viongozi kuchangia sh. milioni nne kwa ajili ya watoto wawili wanaohitaji kufanyiwa upasuaji wa moyo.

“Kwa umoja wetu, na kwa kuguswa na uhitaji wa watoto wenye matatizo ya moyo, tuliamua tuchange fedha na zimefikia shilingi milioni nne ili tuweze kusaidia kuchangia gharama za matibabu kwa ajili ya watoto wawili,” amesema.

Ametoa kauli hiyo leo (Ijumaa, Julai 27, 2018) wakati akizungumza na baadhi ya wazazi na watumishi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili mara baada ya kuwatembelea watoto wengine waliofanyiwa upasuaji wiki hii.

Mama Majaliwa ambaye aliongozana na wake wengine wa viongozi wakiongozwa na Mwenyekiti wa New Millenium Group, Mama Mbonimpaye Mpango, alikabidhi hundi kwa wazazi wa watoto wawili ambao ni Angela Francis (2) na Sabina Mnyango (4).

Watoto hao ni miongoni mwa watoto tisa wenye umri wa miezi mitatu hadi miaka 17 ambao walipangiwa kufanyiwa upasuaji wa kufungua kifua na madaktari bingwa wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirika la Chain of Hope la Uingereza. Matibabu hayo yalianza Julai 23, mwaka huu na yanatarajiwa kukamilishwa leo.

Mke wa Waziri Mkuu Mhe. Mama Mary Majaliwa akiwakabidhi hundi ya shilingi milioni nne wazazi wa watoto Anjela Francis (4) na Sabina Mnyango (4) fedha ambazo zimetolewa na kikundi cha wake wa viongozi cha New Millenium Group kwaajili ya kulipia gharama za upasuaji wa moyo kwa watoto hao ambao wanatibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Mhe. Mama Majaliwa pamoja na wake wa viongozi walipotembelea kambi maalum ya upasuaji wa moyo kwa watoto inayofanywa na Taasisi hiyo kwa kushirikiana na wenzao wa Taasisi ya Chain of Hope ya nchini Uingereza. 
Mke wa Waziri Mkuu Mhe. Mama Mary Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wake wa viongozi, wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) pamoja na wazazi wa watoto ambao kikundi cha wake wa viongozi cha New Millenium Group kimewachangia shilingi milioni nne kwa ajili ya gharama za upasuaji wa moyo. Mhe. Mama Majaliwa pamoja na wake wa viongozi walipotembelea kambi maalum ya upasuaji wa moyo kwa watoto inayofanywa na Taasisi hiyo kwa kushirikiana na wenzao wa Taasisi ya Chain of Hope ya nchini Uingereza. 
Mke wa Waziri Mkuu Mhe. Mama Mary Majaliwa akimjulia hali mtoto aliyelazwa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) aliyefanyiwa upasuaji wa kuziba matundu ya moyo katika kambi maalum ya upasuaji wa moyo kwa watoto inayofanywa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Shirika la Chain of Hope la nchini Uingereza. Mhe. Mama Majaliwa pamoja na wake wa viongozi wa kikundi cha Millennium Group walitembelea kambi hiyo leo na kuchangia shilingi milioni nne kwa ajili ya gharama za upasuaji wa moyo kwa watoto wawili.


WFP ITAWANUFAISHA WATANZANIA - WAZIRI MKUU

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ujio wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Bw. David Beasley hapa nchini ni fursa itakayowawezesha Watanzania kunufaika kwa kiwango kikubwa katika kilimo, uhifadhi na uuzaji wa mazao ya chakula yanayolimwa hapa nchini. 

Akizungumza baada ya kukutana na Bw. Beasley jijini Dar es Salaam leo mchana (Ijumaa, Julai 27, 2018), Waziri Mkuu amesema Tanzania inatarajiwa kuwa na ziada ya chakula msimu wa mavuno utakapokamilika mwaka huu hivyo itahitaji sana kupata soko nje ya nchi ili iweze kuuza ziada hiyo.

Taarifa za Wizara ya Kilimo zinaonesha kuwa mavuno ya mazao ya chakula kama mahindi, maharage na mbaazi yatafikia tani milioni 16 wakati mahitaji ya chakula kwa Watanzania kwa mwaka ni tani milioni 13, hivyo tutakuwa na ziada ya tani milioni tatu,” amesema.

Akitoa ufafanuzi, Waziri Mkuu amesema hadi kufikia Julai 2018 ambapo msimu wa mavuno bado unaoendelea, tayari nchi ina ziada ya tani milioni moja kwani taarifa za Wizara ya Kilimo zinaonyesha kuwa tayari zimekwishavunwa tani milioni 14.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, David Beasley, kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam Julai 27, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, David Beasley, kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam Julai 27, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimikana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, David Beasley kabla ya mazungumzo yao kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam Julai 27, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

DK. KALEMANI ASHUKURU UJENZI WA HOSPITALI YA RUFAA CHATO

0
0

MBUNGE wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani (CCM), aliishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo vipya vya afya wilayani Chato. 

Hospitali hiyo kubwa ya kisasa inajengwa na serikali kwa gharama ya Sh bilioni 9.1 ambapo hadi sasa zimetolewa Sh bilioni 2 kwa ajili ya ujenzi huo. Amesema ujenzi wa hospitali kubwa ya rufaa ya kisasa inakuwa msaada kwa wananchi wa mikoa ya Geita na Kagera ambao walikuwa wakisafiri umbali mrefu kutafuta huduma za afya kwa madaktari bingwa. 

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu yake ya kibunge kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile, leo Mjini Chato, alisema kuwa anaishukuru Serikali wakati wote kwa kusaidia maendeleo ya jimbo lake hasa kwenye sekta ya afya. 

“Ninaishukuru Serikali pamoja na nawe Mheshimiwa Naibu Waziri ambaye muda wote umekuwa msaada kwetu wananchi wa Chato, kwa miaka mitatu mfululizo ninapoleta maombi yangu ya ujenzi wa vituo vya afya muda wote wizara yako imekuwa ikitupa fedha. 

“Na kukamilika kwa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa Chato, itakuwa mkombozi kwani itaweza kutoa huduma za kibingwa kwa wananchi wa Chato, Geita, Muleba na Biharamulo. 
Mbunge wa Chato, Dk. Medard Kalemani, ambaye pia ni Waziri wa Nishati, akimtambulisha kwa kina mama walioepeka watoto wao Kliniki leo, katika Hospitali Wilaya ya Chato, ambapo alitumia fursa hiyo kumtambulisha Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile. 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile, akizungumza na mmoja wa watoto katika Hoaspitali ya Wilaya ya Chato. Kulia ni Mbunge wa Chato ambaye pia Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani. 
Mbunge wa Chato, Dk. Medard Kalemani, ambaye pia ni Waziri wa Nishati, akizungumza wakati wa kumkaribisha Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile, ambaye leo amewasili Wilayani Chato kwa ziara ya kikazi. 


KIKOSI KAMILI CHA SIMBA SPORTS CLUB MSIMU WA LIGI KUU YA 2018/19

0
0


MAGOLIKIPA / WALINDA MILANGO 

1. Aishi Manula, 2. Deogratius Munishi, 3. Ally Salim 



SAFU YA ULINZI
4. Shomali Kapombe, 5. Asante Kwasi, 6. Mohammed Hussein, 7. Nickolas Gyani, 8. Paschal Wawa, 9. Erasto Nyoni, 10. James Kotei, 11. Yusufu Mlipili, 12. Paul Bukaba, 13. Vicent Costa, 14. Salim Mbonde 



VIUNGO/WINGA
15. Jonas Mkude, 16. Mzamiru Yasin, 17. Shiza Kichuya, 18. Cletus Chama, 19. Haruna Niyonzima, 20. Hassan Dilunga, 21. Mohammed Ibrahim, 22. Marcel Kaheza, 23. Abdul Hamis, 24. Rashid Juma, 25. Said Ndemla



WASHAMBULIAJI
26. Emanuel Okwi, 27. John Bocco,28. Middie Kagere, 29. Adam Salamba, 30. Mohammed Rashid.


BENCHI LA UFUNDI 
1. Patrick Aussems - Kocha Mkuu, 2. Irambona Masoud - Kocha Msaidizi, 3. Mwalami Mohammed - Kocha Wa Makipa, 4. Adel Zrane - Kocha Wa Viungo, 5. Yasin Gembe - Dakatari Wa Timu 



6. Haji Sunday Manara " Mashine " - Msemaji Wa Timu, 
7. Mwekezaji mkuu wa Timu - Mo Dewji 


Michuzi TV: TECMN YAKUTANA NA VIONGOZI WA DINI KUJADILI JINSI YA KUTOKOMEZA NDOA ZA UTOTONI

KIINGEREZA CHA SHILOLE CHATIA FOLA SHUGHULI YA AROBAINI YA MTOTO WA ZAMARADI


ZAMARADI ALIPOMTAMBULISHA RASMI MUWEWE KWENYE AROBAINI YA MTOTO WAKE

MBUNGE WA KINONDONI MHE. MTULIA AKICHEZA SINGELI NA MSAGA SUMU KATIKA CCM BONANZA LEADERS CLUB JIJINI DAR ES SALAAM

MICHUZI TV: TPA YAWAHAKIKISHIA WAFANYA BIASHARA USALAMA WA MIZIGO BANDARINI

Michuzi TV: IRENE UWOYA - MOVIE HAZILIPI KAMA TAMTHILIYA

Michuzi TV: RIPOTI KAMILI YA MAFANIKIO YA BANDARI KATIKA UTAWALA WA JPM HII HAPA

MICHUZI TV: MELI KUBWA YA KUBEBA MAGARI YATIA NANGA BANDARINI DAR ES SALAAM

MICHUZI TV: WAVAMIA YA KAMBI YA FUTURE WIFE NA MASHOGA ZAKE..


MICHUZI TV: MAJAJI WAWILI WA MAHAKAMA YA RUFANI WAAGWA KITAALUMA BAADA YA KUSTAAFU RASMI KWA MUJIBU WA SHERIA

0
0
MAJAJI na Mahakimu wameshauriwa kuzingatia sheria katika utoaji haki na wafuate miiko ya kazi zao na kuhakikisha hawafanyi wanayoyataka wao.

Ushauri huo ulitolewa mapema Julai 27, jijini Dar es Salaam na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Bernard Luanda katika hafla ya kuagwa kitaaluma yeye na Jaji mstaafu wa mahakama hiyo, Sauda Mjasiri iliyofanyika katika ukumbi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam.
Hafla hiyo ambayo iliongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Juma na kuhudhuriwa watu mbalimbali wakiwemo Majaji wa mahakama ya Rufani, Majaji wa Mahakama Kuu, Majaji wastaafu wa mahakama ya Rufani. 

“Kazi ya kutoa haki ni ngumu, wanapokuja watu mahakamani kila mtu anavutia upande wake, hivyo lazima utumie busara zako na sheria inasemaje,”alisema Jaji Mstaafu, Mhe.Luanda.
“Majaji na Mahakimu wazingatie sheria, katika mahakama kila hatua ni sheria, lakini siyo sheria tu imani ya wananchi kwa mahakama ni nguzo ya mahakama,” alisema na kuongeza wananchi ni muhimu kwa na imani na mahakama. 

Alisema wananchi wasipokuwa na imani na Mahakama ni hatari kwa kuwa wanaweza kujichukulia sheria mkononi.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) na Majaji wastaafu wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Benard Luanda (wa tatu kulia) na Mhe. Sauda Mjasiri wakiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania. 
Majaji Wastaafu wa Mahakama ya Rufani wakiwa katika nyuso za furaha mara baada ya kuagwa rasmi kitaaluma baada ya kustaafu kwa mujibu wa sheria, kushoto ni Mhe. Benard Luanda na kulia ni Mhe. Sauda Mjasiri, na katikati ni mke wa Mhe. Jaji Luanda. 
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (aliyeketi upande wa juu kulia) akiongoza hafla ya kuwaaga kitaaluma Majaji wastaafu wawili wa Mahakama ya Rufani waliomaliza muda wao kwa mujibu wa sheria, wa kwanza kulia ni Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Benard Luanda, na aliyeketi kushoto ni Jaji Mstaafu, Mhe. Sauda Mjasiri, walioketi mbele ya Wahe. Majaji kushoto ni Msajili, Mahakama ya Rufani, Mhe. John Kahyoza na kulia ni Mhe. Mpepo, Naibu Msajili Mahakama ya Rufani. 
Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi (aliyeketi mbele wa kwanza kushoto) pamoja na baadhi ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Watendaji na Watumishi wa Mahakama wakiwa katika sherehe ya kuwaaga Kitaaluma Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya Rufani waliostaafu kwa mujibu wa sheria. 


Habari za UN: WFP na serikali ya Tanzania kushirikiana kuwainua wakulima

SERIKALI YAONDOA RIBA MIKOPO YA WANAWAKE, VIJANA NA WALEMAVU

MBUNGE SINGIDA MAGHARIBI ASHRIKIANA NA WANANCHI KATA YA SEPUKA KUANDAA ENEO LA KITUO CHA AFYA

0
0
Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Mheshimiwa Elibariki Kingu, akishirikiana na wananchi wa Kata ya Sepuka mkoani humo juzi, kuandaa eneo kitakapo jengwa Kituo cha Afya cha kisasa ambacho kitagharimu shilingingi milioni 400.
Wananchi waking'oa visiki katika eneo kitakapo jengwa kituo cha Afya cha kisasa.
Kazi ya kuandaa eneo hilo ikiendelea.
Mbunge Elibariki Kingu, akiwahutubia wananchi wa Kata ya Sepuka baada ya kuandaa eneo kitakapo jengwa kituo cha afya, ambapo aliwaeleza miradi mbalimbali iliyofanywa na inayoendelea kufanywa katika jimbo hilo la uchaguzi la Singida Magharibi.
Wananchi wa Kata ya Sepuka wakimsikiliza Mbunge wao.

Uzinduzi wa Kituo Kimoja cha Urasimishaji na Uendelezaji Biashara

Viewing all 109587 articles
Browse latest View live




Latest Images