Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein arejea

0
0
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akifuatana na  Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe.Ayoub Mohamed Mahamoud (kushoto) baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume akiwa na Mkewe Mama Mwanamwema Shein pamoja na maafisa mbali mbali akitokea Nchini Uingereza katika safari  maalum.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume akiwa na Mkewe Mama Mwanamwema Shein (hayupo pichani) pamoja na Maafisa mbali mbali akitokea Nchini Uingereza kwa safari  maalum.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipokea shada la mauwa kutoka kwa Mtoto Naifat Faudh wakati wa mapokezi  mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume akiwa na Mkewe Mama Mwanamwema Shein (kushoto) pamoja na Maafisa mbali mbali akitokea Nchini Uingereza katika safari  maalum
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee na Viongozi mbali mbali  mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume akitokea Nchini Uingereza
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na   Viongozi mbalimbali  mara wa Chama na Serikali baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume akitokea Nchini Uingereza akiwa na Mkewe Mama Mwanamwema Shein pamoja na Maafisa mbali mbali  katika safari maalum. Picha na Ikulu.

AZANIA BANK YAWAKUMBUKA WASTAAFU

0
0

Katika kuendelea kusogeza huduma zake kwa wananchi zaidi na kutoa masuluhisho ya kifedha, Benki ya Azania leo imezindua huduma mbili mpya maalumu kwa ajili ya wastaafu kutoka katika mashirika mbalimbali ya kiserikali na hata ya binafsi. Huduma hizi ni Akaunti maalumu ya wastaafu (Wastaafu Akaunti) ambayo pamoja na faida nyingine za kibenki akaunti hii haitakuwa na makato yoyote na watapata ATM kadi bure huduma nyingine ambayo  Azania Bank imeiletea  kwa wastaafu ni fursa ya kupata mikopo kuweza kujikimu na kuboresha maisha yao. 
Akizungumza na vyombo vya habari katika uzinduzi wa huduma hizi Mkurugenzi wa Bank ya Azania Bw. Charles Itembe alisema Azania Bank inaendea kufanya kazi kwa bidii katika kuhakikisha inaendelea kukuza maisha ya watanzania wote kupitia huduma mbalimbali za kifedha inazozitoa. Leo Azania Bank inazindua rasmi Mikopo ya Wastaafu na pia uzinduzi wa kampeni yetu tuliyoibatiza jina la Bega kwa Bega.Mikopo hii ya wastaafu inalenga wastaafu wote wanaopata pensheni kupitia mifuko ya jamii ambapo kupitia mikopo ya wataafu mteja ataweza kufanya marejesho kwa miezi 72 yaani miaka 6.  Alielezea Zaidi Bw. Charles Itembe
Mzee Haron L Kigondo ni mmoja wa wanufaika wa huduma hii mpya ya mikopo kwa wastaafu ambapo pamoja na kushuhudia yeye kuupata mkopo wake ndani ya wiki chache tu, alisema “Mikopo hii kweli inakwenda kutupa nafasi sisi Wastaafu kuweza kuendesha maisha yetu na hata kuendesha biashara wakati tukiwa bado tunaendelea kusubiri mafao yetu, Ninaishukuru sana Azania Bank kwa wazo hili kwani litakwenda kusaidia wastaafu wengi sana kuweza kuboresha maisha pamoja na biashara zao”
Azania Bank kwa sasa ina matawi 17 ambapo ndani ya wiki 3 zijazo inategemea kuwa na matawi 19 baada ya kufungua matawi mapya Dodoma na Morogoro, pamoja na matawi haya Azania Bank inatoa huduma kupitia ATM zaidi ya 270 za Umoja Switch na hii kutoa fursa kwa mtu yoyote popote Tanzania kuweza kupata huduma za kibenki.




MKURUGENZI MBULU AGAWA BAISKELI KWA WALEMAVU

0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndg. Hudson Kamoga ametoa msaada wa baiskeli sita kwa ajili ya walemavu ili kuwasaidia katika maisha yao ya kila siku. Kamoga amewashukuru marafiki zake waliochangia katika kuboresha maisha na kuwasaidia wananchi wanyonge.

Kamoga amesema “Serikali hii inawajali wanyonge na sisi kama viongozi lazima pia tufikiri zaidi ya ukomo wa kazi zetu za kila siku katika kuwahudumia wananchi wa hali ya chini. Nafasi hii niliyopewa na Mungu kupitia kwa Mh. Rais Dr. John Pombe Magufuli ni kwa ajili ya kuwatumikia na kuwasaidia watanzania hasa wanyonge,nafasi hii ni kwa ajili ya watu ninaotakiwa kuwatumikia na si kwa ajili yangu binafsi,ndio maana ya utumishi”alisema Kamoga.

Baiskeli hizo zimetolewa na marafiki wa mkurugenzi huyo wanaotambua mchango wake katika kulitumikia taifa na kuwajali watu wanaoishi kwenye mazingira magumu, Wadau hao wameahidi kutoa vifaa vingine kila watakapokuwa na uwezo wa kifedha ili kusaidia jamii inayoishi kwenye mazingira magumu Wilayani Mbulu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndg. Hudson Kamoga akipozi kwa picha na Mzee Malkiadi Bura kutoka kata ya Masqaroda ambaye ni mlemavu wa miguu baada ya kumkabidhi baiskeli maalum kwa ajili ya kutumia katika shughuli zake wananchi walemavun wengine waliokabidhi wa baiskeli hizo ni kutoka kata za Tumati, Maghang, na Dinamu Wilayani Mbulu Mkoani Manyara.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndg. Hudson Kamoga akipiga picha ya pamoja na dada Rose Boay kutoka Haydom baada ya kumkabidhi baiskeli yake leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndg. Hudson Kamoga akipiga picha ya pamoja na mama Maria Chacha kutoka kata ya Haydom baada ya kumkabidhi baiskeli yake leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndg. Hudson Kamoga akiwa na wananchi wa Mbulu wenye ulemavu wa miguu aliowakabidhi baiskeli maalum kwa ajili ya matumizi katika shughuli zao za kila siku
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndg. Hudson Kamoga akijadiliana jambo na baadhi ya viongozi huku mama Maria Chacha kutoka kata ya Haydom kushoto na dada Rose Boay kutoka Haydom wakiwasikiliza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndg. Hudson Kamoga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na walemavu aliowapatia baiskeli.

WANAFUNZI WAASWA KUJENGA UPENDO KWENYE ELIMU

0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Seleman Jafo amewataka wanafunzi kujenga upendo na kuacha ubinafsi katika kuipambania elimu.

Jafo ameyasema hayo leo katika ziara yake alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Minaki pamoja na walimu wakuu wote wa shule za sekondari zilizopo wilayani Kisarawe Mkoani Pwani. 

Amesema ni vyema wanapoipambania elimu wakawa na upendo na kuachana na ubinafsi. Katika ziara hiyo, waziri Jafo amefanikiwa kupokea vifaa vya michezo kutoka kampuni ya vinywaji ya Coca-Cola na kuwapatia wakuu wote 22 wa shule za sekondari zilizopo wilayani Kisarawe. 

Pamoja na shughuli ya ugawaji wa vifaa vya michezo, Jafo ameungana na wananchi wa Kazimzumbwi katika zoezi la Kuboresha madarasa ya shule msingi ya kijiji hicho kwa kuchangia mifuko yote ya saruji ambayo itawezesha uwekaji wa sakafu katika madarasa yote na ofisi ya walimu ambayo hayajawekwa sakafu.

Zoezi hilo la uwekaji wa sakafu linatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi ili wanafunzi na walimu wa shule ya msingi Kazimzumbwi wapate mazingira mazuri ya kusomea na kufundishia.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Seleman Jafo akimkabidhi vifaa vya michezo Mwalimu Mkuu wa Sekondari ya Gongoni Mwl. Mohamed Kikwayu.
Baadhi ya walimu wakuu wa sekondari wilayani Kisarawe pamoja na wanafunzi wa Minaki wakiwa katika zoezi la kupokea vifaa vya michezo kutoka kampuni ya Coca-Cola.
Walimu wa shule ya Msingi Kazimzumbwi wakiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Seleman Jafo .
Wanafunzi wa Kazimzumbwi wakiwa katika picha na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Seleman Jafo 

HEAMEDA MEDICAL CLINIC ILIYOPO BUNJU B YATANGAZA KAMPENI YA KUPIMA AFYA KWA WANANCHI BURE

0
0
* Madaktari Bingwa nchini waungana na wezao kutoka India kuwahudumia wananchi,waombwa kujitokeza kwa wingi

Na Said Mwishehe, Glob ya Jamii

HEAMEDA Medical Clinic iliyopo Bunju B njia ya kuelekea Mabwepande imetangaza kambi ya uchunguzi wa afya ya magonjwa yasiyoambukiza kwa wananchi wote na kwamba hakutakuwa na gharama.

Akizungumza na Michuzi blog leo jijini Dar es Salaam Dk. Hery Mwandolela amesema wameaza kambi hiyo ya uchunguzi leo jijini Dar es Salaam kwa kupima wananchi mbalimbali waliojitokeza na kusisitiza upimaji huo ambao umeanza leo Julai 26 utaendelea hadi Julai 28 mwaka huu.

Amesema upimaji huo unafanywa na Madaktari bingwa wa hapa nchini kwa kushirikiana na madaktari bingwa kutoka nchini India na lengo kuu ni kuwawezesha wananchi kutambua afya zao mapema na iwapo watabainika kuwa na tatizo la kiafya waaze tiba mapema.

Amefafanua huduma zinazotolewa katika kambi hiyo ya uchunguzi ni pamoja na kupima magonjwa yasiyoambukizwa yakiwemo ya Moyo ,sukari,shinikizo la damu,Tenzi Dume, lehemu(cholestrol) nakiwango cha mafuta mwilini."Madaktari bingwa wa Heameda Medical Clinic kwa kushirikiana na madaktari bingwa wengine nchini pamoja na madaktari bingwa kutoka India tutatoa huduma hizo kwa kiwango cha hali ya juu.

Nakuongeza kuwa " hivyo tunaomba wananchi wajitokeze kwa wingi nakwamba huduma hii inafanyika kwa siku tatu ambapo tumeaza leo na tunaendelea kesho na keshokutwa na hakuna gharama yeyote ."amesema Dkt Mwandolela.Amesisitiza kwakutambua umuhimu wa afya yako wameamua kufanya kampeni hiyo ya kupima magonjwa hayo wakiamini ni fursa ya kila mwananchi kujitambua kiafya mapema..

Katika kampeni hiyo kwa siku ya leo ambayo ni ya kwaza idadi kubwa ya wananchi wamejitokeza lakini Dkt.Mwandolela anafafanua kwa idadi ya madaktari bingwa waliopo nivema wananchi wakaendelea kujitokeza kwani wote watahudumiwa kwakupata vipimo vya afya zao.
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo nchini Dk.Hery Mwandolewa akiwa ofisini kwake Heameda Medical Clinc Bunju B jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa sehemu ya mapokezi ndani ya Clinic hiyo
Muonekano wa moja ya chumba chenye vifaa mbalimbali kwa ajili ya uchunguzi wa magonjwa/matibabu
Muoneakano wa Clinic hiyo kwa nje

TAARIFA KUTOKA TFDA KUHUSU DAWA ZA MATIBABU YA SHINIKIZO LA DAMU NA KUFELI KWA MOYO.

TANZANIA NA MALAWI ZAJADILIANA KUONDOKANA NA CHANGAMOTO KATIKA BIASHARA

WATUMISHI JIJI LA ARUSHA WATAKIWA KUDUMISHA UPENDO NA KUFANYA KAZI KWA BIDII.

0
0
Watendaji na Watumishi wa Serikali katika jiji la Arusha wametakiwa kushirikiana,kupendana na kufanya kazi kwa bidii ili kulinda mafanikio ya kimaendeleo yaliyofikiwa na jiji hilo. 


Kauli hiyo imetolewa leo jijini Arusha na aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha ambaye sasa ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dkt. Athumani Kihamia wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya Ofisi jijini hapo. 

Akizungumza na Watumishi na Watendaji wa jiji hilo Dkt. Kihamia amewataka wafanye kazi kwa bidii na kuepuka vitendo vinavyoweza kuleta mgawanyiko miongoni mwao. Amesema katika kipindi cha uongozi wake akiwa Mkurugenzi wa jiji hilo aliwaunganisha watumishi wote akiweka msisitizo katika bidii, nidhamu ya kazi na matumizi mazuri ya rasilimali na fedha Serikali hali iliyolifanya jiji hilo kupata Hati Safi ya Matumizi ya fedha za Serikali. 

“Watumishi Wenzangu mimi nimekaa katika jiji hili kwa muda wa miaka 2, nafurahi kuwa nawaacha mkiwa na morali ya kufanya kazi na muendelee kufanya kazi kwa bidii, mzidi kupendana ili kazi mnazozifanya zifanikiwe kwa manufaa ya jiji ” Amesisitiza Dkt. Kihamia. Ameongeza kuwa ili jiji hilo liendelee kupiga hatua zaidi za Kimaendeleo, watendaji na wakuu wa Idara wana wajibu wa kufanya kazi kwa pamoja, kuaminiana na kuepuka kufanya vitendo vya dhuruma na uonevu wa aina yoyote kwa watumishi wa kada mbalimbali walio chini yao. 


JKT YAAHIDI KUJENGA MAJENGO YA KUDUMU UWANJA WA NANENANE SIMIYU

0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT) Meja Jenerali Martin Busungu ameahidi kuwa Jeshi hilo litajenga Majengo ya kudumu katika Uwanja wa Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane Kanda ya Ziwa Mashariki wa Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu, ili kuendelea kutoa elimu ya teknolojia mbalimbali za kilimo na ufugaji kwa wakulima, wafugaji na wavuvi.

Meja Jenerali Busungu ameyasema hayo wakati alipotembelea eneo la JKT lililopo Uwanja wa Nanenane Nyakabindi kwa lengo la kujionea maandalizi hayo yanayofanywa na Jeshi la Kujenga Taifa.Busungu amesema baada ya Nanenane wataanza ujenzi wa majengo ya kudumu ili wakulima, wafugaji na wavuvi wanufaike na teknolojia ya kilimo kwa muda wote.

“Mkuu wa mkoa ametupa mkakati wao kuwa kila baada ya miezi mitatu kutakuwa na maonesho katika uwanja huu, tunaahidi kujenga majengo ya kudumu hapa na maonesho yajayo miezi mitatu inayofuata wananchi watarajie kupata vitu vizuri kutoka JKT, maana JKT ni kisima cha kila kitu” alisema Meja Jenerali Busungu.

“ Katika maonesho haya watarajie kuona teknolojia mbalimbali za kilimo, ufugaji, uvuvi pia watarajie kuona bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na JKT zikiwemo bidhaa za kilimo, viwanda na kwa ndugu zangu Wanyantuzu wataona mbuzi na kondoo wa maziwa na wataona kuwa si ng’ombe tu wanaotoa maziwa” alisisitiza Meja Jenerali Busungu.Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ameishukuru JKT kwa kazi kubwa ya maandalizi ya Maonesho ya Nanenane waliyoifanya, huku akibainisha kuwa uwepo wa JKT utasaidia kuwabaadilisha vijana wa Simiyu kwa kuwa watapata fursa ya kujifunza teknolojia mbalimbali.

“ Tunawashukuru sana JKT kwa kutuamini na tunajua kuwepo JKT kutasadia kuwabadilisha vijana wa hapa kwa kuwa kuna vijana wanamaliza darasa la saba au kidato cha nne hawana pa kushika na sisi tuna vikundi vingi vya vijana , tuko tayari kuleta vikundi vyetu vya vijana kuja kujifunza hapa” alisisitiza Mtaka.Naye Mbunge wa Itilima amesema maonesho ya nanenane na uwepo wa JKT kutakuwa msaada kwa wananchi kwa kuwa watapata elimu itakayowawezesha kufanya uzalishaji wenye tija ikiwemo ufugaji wa kisasa na kilimo bora.
Mkurugenzi wa Kilimo na Mifugo katika Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Luteni Kanali Peter Lushika akitoa maelezo kwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT) Meja Jenerali Martin Busungu na Viongozi wa Mkoa wa Simiyu, wakiongozwa na Mkuu wa mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka, kuhusu Mabanda ya miifugo yaliyojengwa na jeshi hilo kwa ajili ya maonesho ya Nanenane yatakayofanyika Kitaifa, 2018 Uwanja wa Nyakabindi katika Halmashauri ya mji Bariadi .
Mkurugenzi wa Kilimo na Mifugo katika Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Luteni Kanali Peter Lushika akitoa maelezo juu ya vipando vilivyoandaliwa na jeshi hilo kwa ajili ya maonesho ya Nanenane yatakayofanyika Kitaifa Mkoani Simiyu kwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT) Meja Jenerali Martin Busungu na Viongozi wa Mkoa wa Simiyu, wakiongozwa na Mkuu wa mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka walipotembelea eneo hilo lililopo Uwanja wa Nyakabindi katika Halmashauri ya mji Bariadi.
Viongozi wa JKT na mkoa wa Simiyu wakiangalia moja ya mabwawa ya samaki yaliyoandaliwa na Jeshi la kujenga Taifa(JKT) kwa ajili ya maonesho ya Nanenane yatakayofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Nanenane wa kanda ya ziwa mashariki, uliopo Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT) Meja Jenerali Martin Busungu akisaini vitabu vya wageni vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, kabla ya kuanza kutembelea eneo la jeshi hilo lililoandaliwa kwa ajili ya maonesho ya Nanenane yatakayofanyika kitaifa mkoani humo Agosti 2018, lililopo katika Uwanja wa Nanenane uliopo Nyakabindi Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.

KATIBU MKUU CCM AVUNA WANACHAMA WAPYA KASULU ,YUMO ALIYEKUWA MBUNGE WA KASULU VIJIJINI

0
0
Na Rhoda Ezekiel Kigoma

KATIBU MKUU wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Taifa Bashiru Ally amewaapisha wanachama wapya 269 kutoka vyama vya upinzani akiwemo aliekuwa Mbunge wa jimbo la Kasulu Vijijini Agripina Buyogera na Mwenyekiti wa Chama cha NSSR Mkoa na Wilaya ya Kasulu Hitra Joseph Gelvasi Bahenga katika amkutano wa kampeni za uchaguzi Wilayani Kakonko mkoani Kigoma.

Tukio hilo lilifanyika jana Katika mkutano wa uzinduzi wa Kampeni za ubunge katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Buyungu wilayani humo wakati akimnadi mgombea wa Chama hicho ambapo wananchi hao walioamua kujiunga na CCM na kuwaomba wananchi kuendelea kukiamini na kumpa kura mgombea wao.

Amesema wanachama hao hawajawanunua ila wamevutiwa na utekelezwaji wa Ilani ya Chama na amewaahidi wananchi kabla ya uchaguzi huo kuisha watapokea vigogo wengi na watawapokea hawata wabagua wote watakaotaka kujiunga na CCM na wote wanahaki ya kujiunga.

" Milango ya wanachama wapya iko wazi na tuna wakaribisha sana na hawa ndio wamefungua mlango tunawakaribisha wote CCM haina mwenyewe wote tuna sifa ya kuwa wanachama.Sasa tunapokea wote na hatuko tayari kununua Watu kutoka vyama vingine wataona mambo wenyewe watakuja," alieleza Bashiru.

Akimkaribisha mgeni rasmi katika uzinduzi wa kampeni hizo Ally alisema CCM ni chama cha wanyonge kipo kwaajili ya kuwatetea katika kuleta maendeleo hivyo amewaomba Wanakakoko kumchagua Chiza ili akafanye kazi na Chama cha Mapinduzi.Alisema anatambua mchango wa Chiza kwa wanakakonko na yapo mengi ambayo ameyafanya kwa Jimbo la Buyungu suala la kuwashawishi wananchi wasimchague kwa kigezo kwamba ni mzee hii sio kweli wamuamini wampe kura aweze kuwaletea maendeleo zaidi.

"Tunae mgombea ambae tunamnadi kwa sifa zake angalia elimu yake busara zake mchango wake katika jamii kupitia mkutano huu wana CCM wote watakao hisika na kampeni muwe na moyo wa kuvumilia mkitupiwa matusi msirudishe matusi hayo CCM ni chama cha wastaarabu muwe wavumilivu" alisema Katibu Mkuu.
Mwanasiasa Mkongwe na aliyewahi kuwa Katibu MKuu wa chama cha CCM,Ndugu Yusuf Makamba akimtambulisha na kumnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Buyungu Mh.Christopher Chiza wakati wa uzinduzi wa Kampeni za ubunge katika uchaguzi mdogo wa Jimbo hilo wilayani Kakonko mkoani Kigoma 
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi akiwa ameambatana na mgombea Ubunge wa jimbo la Buyungu Mh.Christopher Chiza wakati wa uzinduzi wa Kampeni za ubunge katika uchaguzi mdogo wa Jimbo hilo wilayani Kakonko mkoani Kigoma.
Mwanasiasa Mkongwe na aliyewahi kuwa Katibu MKuu wa chama cha Mapinduzi (CCM),Ndugu Yusuf Makamba  akiwa katika picha ya pamoja na baaadhi ya Wabunge wa chama hicho mapema jana wakati wa uzinduzi wa Kampeni za ubunge katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Buyungu wilayani Kakonko mkoani Kigoma,Pichani kulia ni Mh Bashe,Peter Serukamba na mwisho kabisa kushoto ni Mh Nape.
Baadhi ya viongozi na Wabunge wa CCM wakifurahia shuughuli za uzinduzi wa kampeni za Ubunge ndani ya jimo hilo la Buyungu wilani Kakonko mkoani Kigoma 
Baadhi ya Wanachama na Wafuasi wa chama cha Mapinduzi (CCM),wakiwa wamebeba mabango yenye jumbe mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Kampeni za ubunge katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Buyungu wilayani humo .

HALI YANGU KWA SASA-WAKONTA

Kilosa yatenga Sh.milioni 46 za CBFM

0
0
NA SULEIMAN MSUYA, KILOSA

HALMASHAURI ya Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro imetenga Sh. milioni 46 kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ajili ya Usimamizi Shirikishi wa Misitu ya Jamii (CBFM) katika vijiji vitatu.

Hayo yamesemwa Mkuu wa Idara ya Maliasili, Ardhi na Misitu wilaya ya Kilosa, Ibrahim Ndembo wakati akizungumza na waandishi wa habari jana wilayani hapo .Ndembo alisema halmashauri imekubali kutenga fedha hizo ili kuweza kuendeleza jitihada ambazo zimefanywa na Mradi wa Kuleta Mageuzi katika Sekta ya Mkaa Tanzania (TTCS) katika vijiji 20 vya wilayani hapo.

Alisema halmashauri katika kutekeleza dhana ya CBFM iliyoanza kutekelezwa na Mradi wa TTCS wataanz katika vijiji vitatu ambavyo ni New Mamboya, Inyunywe na Nyangala kata ya Mamboya."Zipo taarifa kuwa hawa ndugu zetu wa TTCS ambao wanatekeleza dhana ya CBFM katika vijiji 20 wanatarajia kuondoka Novemba mwaka hivyo ili kuendeleza lengo lao halmashauri imetenga Sh.Mil 46 ambayo itatumika kwenye vijiji vitatu vya maeneo ya Kaskazini mwa Kilosa," alisema.

Alisema CBFM kuanzishwa katika vijiji hivyo vya New Mamboya, Inyunywe na Nyangala itasaidia kuokoa misitu ambayo inaharibiwa kwa wingi.Mkuu huyo wa idara alisema lengo lao lilikuwa ni kutekeleza dhana ya CBFM katika vijiji vitano kila mwaka wa fedha ila kutokana na uhaba wa fedha wataanza na vijiji hivyo vitatu.

Ndembo alisema matarajio yao ni kupitia Baraza la Madiwani katika mwaka wa fedha 2019/2020 watatenga fedha nyingine kwa ajili vijiji vingine vya Kaskazini hasa Dumila ili kufikia vijiji 20 mwaka 2021.Mkuu huyo wa idara alisema Kilosa ina vijiji 139 na vijiji ambavyo vinatekeleza CBFM ni 20 na vyote vipo Kusini. KUSOMA ZAIDI BONFYA HAPA>>>>>>

Kaimu Meneja Mradi wa Kuleta Mageuzi katika Sekta ya Mkaa Tanzania (TTCS), ambaye ni Ofisa Kujenga Uwezo wa Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG), Simon Lugazo akizungumza na madiwani wa Halmashauri ya Kilosa kuhusu mradi wa TTCS kufikia mwisho 2019. (Picha na Suleiman Msuya).

NAIBU WAZIRI WA NISHATI ABARIKI VIJIJI 167 KUPATA UMEME MKOANI MTWARA

0
0
Na Emmanuel Massaka, Globu ya jamii

NAIBU Waziri wa Nishati Subira Mgalu amefanya ziara katika Mkoa wa Mtwara na kubariki vijiji 167 kupata umeme katika awamu hii na hii ni katika kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)kwa kutimiza ahadi kwa wananchi.

Akizungumza na wakazi wa Mtwara katika kata ya Nanyamba, Mgalu ameeleza kuwa baada ya kusikia changamoto katika Halmashauri mpya ya Nanyamba hakuona sababu ya kutosimamia upelekaji wa huduma ya umeme Nanyamba.Na amemshukuru Mbunge na viongozi wa Mtwara kwa ushirikiano wao.

Mgalu amesema kuwa kama shirika linahudumia wateja wote bila kujali itikadi wala chama na wananchi kwao ni wateja na ahadi yao ya kuwaunganishia wateja kwa asilimia 50 kufikia 2020  lazima itimie.Aidha amelitaka Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO) kuwahudumia wananchi wa Mtwara kwa kuzingatia mkoa huo unachangia uchumi wa Taifa kutokana na uzalishaji wa korosho.

Ameagiza  shirika kuangalia na kuhakikisha huduma ya umeme inapatika.
Kuhusu  gharama ya umeme Mgalu ameeleza kuwa bei ya kuunganisha umeme wa REA 27,000 pekee na kuwataka wananchi kutumia fursa hiyo katika kuhakikisha wanapata huduma ya  umeme na amehaidi kuwatembelea tena mapema Oktoba ili kuweza kuona kama maagizo aliyotoa yamefanyiwa kazi.

Pia amehaidi  kuongeza orodha ya vijiji katika mradi huo wa umeme hasa katika maeneo muhimu kama hospitali mrad ya maji  ili shuguli ziweze kwenda sawa na wananchi kuweza kupata huduma hiyo.Kwa upende wake Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa ameeleza kuwa umeme uliopo unatosheleza licha ya kuwepo kwa changamoto katika maeneo machache na mchakato bado unaendelea, na amewataka viongozi wa kada mbalimbali kwenda na kasi ya hapa kazi tuu.

Naye mkazi wa Mtwara Rajabu Mkaika amepongeza Serikali kwa kutoa huduma ya umeme bila kujali hali zao.
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu, na viongozi wengine wa Halmashauri ya Mtwara vijijini  mkoa Mtwara wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa usambazaji umeme vijijini REA awamu ya Tatu (REAIII), kwenye kijiji cha Nalingu.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiwa na baadhi ya vingozi wa mkoa wa Mtwara wakiwa katika picha ya pamoja.
 Naibu Waziri wa Nishati,Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nalingu mkoani Mtwara wakati wa ziara yake katika Mkoa huo ,ambapo vijiji 167  vinatarajiwa kupata umeme wa REAIII   awamu ya tatu,ikiwa ni sehemu ya kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa kutimiza ahadi kwa wananchi.Katika hatua nyingine Waziri Mgalu amewaomba wananchi hao kuhakikisha wanaitunza miundombinu ya Umeme
 Sehemu ya wananchi wa kijiji cha Nalingu mkoani Mtwara wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati,Subira Mgalu.

RAIS DKT MAGUFULI ANAVYOZUNGUMIZIWA NJE YA NCHI

DAWASCO YAKAMATA WAHUJUMU MIUNDOMBINU YA MAJI

0
0
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 

Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) imekamata mashine za maji (pump) zilizokuwa zimeunganishwa kwenye mabomba ya shirika hilo na kuwauzia wananchi kinyume cha sheria. Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa operesheni maalumu ya kufichua wezi wa maji Meneja wa DAWASCO wa Magomeni Mhandisi Damson Mponjoli amesema kuwa shirika halitaacha watu wanaohujumu shirika na kuathiri wananchi wengine wasipate maji. 

Amesema kuwa licha waliojiunganishia maji kenyemela kukimbia lakini kidhibiti chao hakiwezi kukimbia hivyo hatua za kisheria zitafuata kwanza ni kujisarimisha kwenye mamlaka. Mhandisi Mponjoli amewaomba wajumbe wa serikali za mtaa kupeleka orodha ya watu 50 ili kuwawekea vizimba vya maji ili kuondoa adha ya upatikanaji wa maji katika maoeneo yao. 

Amesema kuwa miundombinu yote iliyokuwa imeunganishwa lazima ifumuliwe kutokana na watu hao kuunganisha mabomba hayo na kupitisha katika katika vyoo na mitaro ya maji machafu. Mponjoli amesema kuwa yao walijiungia maji kiholela suala ambalo linahatarisha usalama wa afya za wananchi pamoja na shirika kukosa mapato ya kuendeshea huduma ya maji katika maeneo yao.

Katika operesheni hiyo wamekamata Mashine za Kuvuta Maji kutoka katika Mabomba makubwa ya dawasco, matanki Nane(8) ya Lita 10000,5000 na lita 2000. Operesheni imefanyika katika maeneo ya Magomeni Manzese, Manzese Midizini, Manzese Kilimahewa ampapo operesheni hiyo inaendelea maeneo mengine.KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


 Meneja wa DAWASCO wa Magomeni Mhandisi Damson Mponjoli akizungumza na waandishi wa habari wakati wa operesheni maalumu ya kufichua wezi wa maji iliyofanyika katika maeneo ya Magomeni Manzese, Manzese Midizini, Manzese Kilimahewa ampapo operesheni hiyo inaendelea maeneo mengine. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 
Mashine za kuvuta maji zilizokuwa zikitumika kuiba maji na kuyaweka kwenye matanki kwa ajili ya kuyauza. 
Moja ya eneo zilipokuwa zimefungwa mashine. 
Wananchi wakichota maji katika tanki la maji lililokuwa likijazwa na kuuziwa wananchi kwa shilingi 100/- kwa ndoo. 

YALIYOJIRI KATIKA ZIARA YA TUME YA MADINI JIJINI DODOMA

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA KIWANDA CHA SODA ZA PLASTIKI SBC MBEYA

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameutaka Uongozi wa mkoa wa Mbeya kuweka mpango wa kuyatumia maji ambayo yamechakatwa kutoka kiwanda cha soda cha pepsi cha SBC Mbeya. 

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa Ufunguzi wa Kiwanda Kipya cha Soda za Chupa za Plastiki cha Pepsi, SBC Mbeya. Makamu wa Rais ambaye yupo kwenye ziara ya kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani Mbeya, ameupongeza Uongozi wa SBC Mbeya kwa kuajiri Watanzania zaidi ya asilimia 90%.

“ Niliyoayaona yamenipa moyo na nimepata mafunzo pia nitakapokwenda kwenye viwanda vingine nini niwaelekeze cha kufanya” alisema Makamu wa Rais. Makamu wa Rais amepongeza kiwanda hicho kwa kuwa walipaji wazuri wa kodi na kwa wakati. Makamu wa Rais pia alipongeza mchango kwa jamii na michango mingine katika ngazi ya Kitaifa.

Mapema, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni ya SBC Tanzania Bw. Foti Nyirenda alimueleza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznia Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwa Kiwanda kipya cha soda za chupa za plastiki ktazalisha kreti 24,000 na pia Kiwanda cha Kuchakata maji taka ambapo kiwanda hicho kinatumia zaidi ya dola laki sita kwa ajili ya shughuli za kutunza na kuboresha mazingira. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kiwanda kipya cha soda za chupa za plastiki katika kiwanda cha soda za Pepsi SBC Mbeya, wengine pichani ni Mkurugenzi Mtendaji wa SBC Tanzania Bw. Ziad El Khalil (kulia), Mkurugenzi Mkuu Bw. Avinash Jhah , Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson, Naibu Waziri Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw. Amos Makala na Meneja wa Kiwanda cha SBC Mbeya Mr. Sanam Mahambrey . (Picha na ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la uzinduzi wa kiwanda kipya cha soda za chupa za plastiki katika kiwanda cha soda za Pepsi SBC Mbeya, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa SBC Tanzania Bw. Ziad El Khalil . (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia moja ya chupa ya plastiki wakati wa uzinduzi wa kiwanda kipya cha soda za chupa za plastiki katika kiwanda cha soda za Pepsi SBC Mbeya, kulia ni Mhandisi Mkuu wa Pepsi Tanzania Bw. Prabir Bhowmick na Msimamizi wa Mitambo Bw. Odestus Kabelenga. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikitoa pongezi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa SBC Tanzania Bw. Ziad El Khalil mara baada ya kuweka jiwe la msingi la Ufunguzi wa kiwanda cha kuchakata maji taka SBC Mbeya.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea maua kutoka kwa mtoto mwenye mahitaji maalum Amina Hawa kutoka Child Support Tanzania kama ishara ya kumkaribisha alipotembelea kiwanda cha Soda za Pepsi, SBC Mbeya. 

LUBINGA AUNGURUMA KATIKA KATA YA UCHAGUZI MDOGO YA NYAMICHIGE JIMBO LA RUANGWA.

0
0
Katibu wa HKT Siasa na uhusiano wa kimataifa Cde Ngemela Lubinga ameanza ziara yake ya kampeni katika Kata ya Nyamichige wilaya ya Ruangwa na jimbo LA Ruangwa.

Katika mkutano huo cde Ngemela Lubinga aliwasisitiza wananchi wa kata ya Nyamichige wamchague diwani Ndg Mikidadi Ibadi Matauna almaarufu Mbute ambaye alihama Chama cha Chadema na kujiunga na CCM kutokana na Chama hivyo kushindwa kumpa ushirikiano wa kutosha kama diwani na kumtenga mara kwa mara anapozisifia jitihada za Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Cde Lubinga amewaomba wananchi hao wamchague diwani huyo ili kuweza kukamilisha safu ya uongozi katika jimbo hilo kwani kwa kufanya hivyo hawataipa heshima CCM peke yake kama Chama kilichowaletea maendeleo katika wilaya ya Ruangwa lakini pia itakuwa ni heshima kubwa kwa mbunge wa jimbo hilo ambaye Rais Dr John Pombe Magufuli alimpa heshima ya kuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya awamu ya tano.

Aidha cde Lubinga aliendelea kusisitiza kuwa maendeleo yanayoendelea kupatikana katika jimbo la Ruangwa ni juhudi kubwa za mbunge wa jimbo hilo Mhe Majaliwa Kasim Majaliwa,Waziri Mkuu wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Cde Lubinga amewasisitiza wananchi katika kata ya Nyamichige kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kujituma pamoja na kuhakikisha vijana wao wanawapeleka shuleni na pia kuhakikisha wanatokomeza mimba za mapema kwa watoto wa kike ili waweze kuwa viongozi wa kesho.

Mwisho cde Lubinga alichukua wasaa wake kumpongeza mbunge wa jimbo la Ruangwa Mhe Majaliwa Kasim Majaliwa kwa kuwa anaweza kuwa ni Waziri Mkuu wa kwanza kuweza kufanya ziara katika kata zote 22 za jimbo la Ruangwa na pia vijiji 88 kati ya vijiji 90 vilivyopo katika jimbo la Ruangwa kwani kwa kufanya hivyo ameonyesha mfano kama kiongozi wa kitaifa.

GEREZA KUU LA ISANGA LAAGIZWA KUTUMIA NISHATI MBADALA WA KUNI NA MKAA

0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima hii leo amefanya ziara ya kikazi katika Gereza Kuu la Isanga lililopo Jijini Dodoma na kuutaka uongozi wa Gereza hilo kuifanya Dodoma kuwa ya kijani kwa kupanda miti zaidi na kuacha matumizi yasiyoendelevu ya mkaa na kuni kama nishati ya kupikia.

Akizungumza na Uongozi wa Gereza hilo Mhe. Sima amewataka kutumia majiko banifu ili kupunguza kasi ya ukataji miti kwa matumizi ya kupikia. “Natoa wito kwenu kuanza kutumia teknolojia mbadala ya kuni na mkaa kama nishati ya kupikia na kuwaagiza kuona namna bora ya kutumia gesi ili kunusuru misitu yetu”

Pia, Waziri Sima ameagiza uongozi wa gereza hilo kutenga eneo maalumu kwa ajili ya kuotesha miti inayostahimili ukame kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwa na shamba darasa kwa watu kujifunza kilimo hicho cha miti na kutoa ushauri wa kitaalamu.

Akitoa taarifa ya Gereza hilo Naibu Kamishna wa Magereza Julius Mayenga Sang’udi amesema kuwa kwa siku gereza hilo hutumia wastani wa kuni mita za ujazo 8-10 kwa matumizi ya kupikia, kuni ambazo hutolewa katika kambi ya Mayamaya, Taasisi za Serikali na ujenzi binafsi.Kufuatia maelekezo ya Naibu Waziri, Kamishna Sang’udi amesema kuwa mpango uliopo sasa ni kugeuza changamoto kuwa fursa ikiwa ni pamoja na kuhuisha wazo la kujenga mfumo wa matumizi ya gesi na ‘biogas’ kama nishati ya kupikia.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima akisalimiana na Uongozi wa juu katika Gereza Kuu la Isanga jijini Dodoma. Ziara ya Naibu Waziri katika gereza hilo imelenga kuhimiza viongozi hao kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya ‘Dodoma ya Kijani’

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima (kushoto) akiteta jambo na Meneja wa Ranchi ya Kongwa mara baada ya kutembelea ranchi hiyo mapema leo. Pamoja na mambo mengine Naibu Waziri amemuagiza Meneja huyo kuwa na mpango kabambe wa upandaji miti katika eneo hilo.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima (kushoto) akiteta jambo na Meneja wa Ranchi ya Kongwa mara baada ya kutembelea ranchi hiyo mapema leo. Pamoja na mambo mengine Naibu Waziri amemuagiza Meneja huyo kuwa na mpango kabambe wa upandaji miti katika eneo hilo.
Meneja wa Ranchi ya Kongwa Bw. Euzebius Mutayabarwa akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) wa namna ya shughuli za hifadhi ya mazingira zinavyotekelezwa katika eneo lake. Wa kwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Joseph Sokoine na viongozi wa Wilaya ya Kongwa.
Meneja wa Ranchi ya Kongwa Bw. Euzebius Mutayabarwa akifafanua jambo kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) na ujumbe wake mara baada ya kutembelea ranchi hiyo leo iliyopo Wilayani Kongwa Jijini Dodoma.


UINGEREZA YAJIUNGA NA MATAIFA MENGINE KUSAIDIA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE KWA KUTOA MAFUNZO MAALUM KATIKA UPASUAJI WA MOYO KWA WATOTO

0
0

Madaktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Shirika la Chain of Hope la nchini Uingereza wamefanya upasuaji wa kufungua kifua kwa watoto tisa wenye umri wa miezi mitatu hadi miaka 17 kuanzia tarehe 23/07/2018 hadi leo tarehe 27/07/2018. 

Watoto waliofanyiwa upasuaji ni wale wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo ambapo madaktari wanatengeneza valve na kuziba matundu, kurekebisha mishipa ya moyo ambayo imekaa vibaya, kurekebisha mfumo wa uzungukaji wa damu katika moyo na kuweka valvu za bandia kwa wale walio na valvu za moyo zilizoharibika. 
Wagonjwa wote waliofanyiwa upasuaji hali zao zinaendelea vizuri na sita kati yao wameruhusiwa kutoka katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) na kupelekwa wodini kwa ajili ya kuendelea na matibabu. 

Kambi hiyo inaenda sambamba na utoaji wa elimu pamoja na kubadilishana ujuzi wa kazi kwa wataalamu wetu. Katika kambi hii Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo kwa watoto ni mwanamke hii imeleta hamasa kwa madaktari wetu wa kike kusomea upasuaji wa moyo ambapo kwa Tanzania hatuna Daktari wa kike wa upasuaji wa moyo wote ni wanaume. 

Hii ni kambi ya tatu ya matibabu ya moyo kwa watoto tangu kuanza kwa mwaka huu wa 2018 na ni mara ya kwanza kwa Uingereza kuja hapa nchini. Kambi nyingine zilizofanyika ni za upasuaji wa moyo wa bila kufungua kifua ambayo tuliifanya na wenzetu kutoka Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart-SACH) ya nchini Israel na Kituo cha Moyo cha Berlin (Berlin Heart Center) ya nchini Ujerumani katika kambi hii jumla ya watoto 17 walipata matibabu. Upasuaji wa kufungua kifua tulifanya na wenzetu wa Taasisi ya Open Heart Internartional (OHI)ya nchini Austarial na kufanya upasuaji kwa watoto 20. 

Kwa upande wa wamama wajawazito ni muhimu wakafanya uchunguzi (Fetal Echocardiography) wa kuangalia kama mtoto aliyeko tumboni anamatatizo ya moyo au la. Hii itasaidia kama mtoto anamatatizo ya moyo kupata matibabu mapema pindi atakapozaliwa. 

Kama mnavyofahamu matibabu ya moyo ni ya gharama hivyo basi tunaendelea kuwahimiza wananchi kujiunga na Mifuko ya Bima za Afya. 

Imetolewa na: 
Kitengo cha Uhusiano 
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete 
27/07/2018
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live




Latest Images