Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110164 articles
Browse latest View live

MFAHAMU JONATHAN, MTOTO WA MIAKA 12 ALIYEANDIKA KITABU KWA KUTUMIA MACHO

$
0
0
Na Leandra Gabriel, blogu ya jamii

WAKATI baadhi ya watu wengi walio na ulemavu kuona hawawezi kufanya chochote hali imekua tofauti kwa mtoto Jonathan Bryan aishiye Wiltshire huk Uingereza.

Jonathan alizaliwa miaka 12 iliyopita akiwa na matatizo mbalimbali katika mfumo mzima wa mjongeo wa mwili na amekuwa akisaidiwa na kiti walemavu (wheel chair)

Muda wote wa maisha yake wazazi wake wamekuwa wakitumia ishara za mwili kama kutabasamu katika kuwasiliana naye, walimu waligundua matatizo yake katika kujifunza hivyo hawakumfundisha kusoma wala kuandika.

Mama wa mtoto huyo Chantal Bryan alianza kubadili maisha ya mtoto huyo baada ya kutenga masaa kadhaa ya kumfundisha kusoma na kuandika na hadi kufikia miaka 9 Jonathan aliweza kutamka chochote alichohitaji.

Kwa msaada wa E-Tran frame mfumo ambao huusisha vifaa vyenye rangi na herufi na mtu anayewasiliana kwa kubeba mbele yao na kufuata kile ambacho anataka kukitaja umemsaidia Jonathan katika kuwasiliana na hata kuandika kitabu kinachohusu maisha yake cha "Iam Voice of Voiceless" kwa kutumia macho yake.

Katika kitabu hicho Jonathan ameandika kuhusu watoto kupewa nafasi ya kujifunza, kusoma na kuandika na hata kama mwili wake upo sawa ila akili yake inaweza kuwa makini.

RAIS WA TBF AKAWABIDHI BENDERA TIMU WAZALENDO YA KIKAPU

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Timu  ya Taifa ya 3x3  ijulikanayo kwa jina Wazalendo inatarajia kuondoka siku ya Ijumaa  kuelekea nchini Madagascar kwa ajili ya kushiriki Mashindano ya 3x3 Africa Basketball Qualifiers 2018 ambayo yatashirikisha nchi 16 ikiwemo Tanzania.

Katika mashindano hayo timu nne kati ya hizo zitapata nafasi ya kushiriki Fainali za Africa, Afrobasket 3x3  zitakazofanyika nchini Togo, mwezi October, 2018.

Katika timu ya Tanzania inashirikisha baadhi ya wachezaji ambao walishiriki mashindano ya 3x3 FIBA Zone V U18 ambayo yalifanyika hapa Tanzania na kufanikiwa  kuchukua nafasi ya pili na kufanikiwa kuingia mashindano ya Afro basket U18 yatayofanyika nchini Mali, baadae mwaka huu. 

Wachezaji watakaowalisha katika michuano hiyo nchini Madagascar ni 

1. ABBA PATRICK ROBERT 
2. HAJI RASHID MBEGU 
3. CHARLES ALBERT MAYOMBO  
4. RASHID TARIQ HAROUN MAARIFA 
5. JOVIN CHARLES NGOWE  
6. MWALIMU HERI KIJOGOO  
7. BARAKA NSAJI 
8. PHINIAS STEPHEN KASHABI 
9. JONAS MUSHI

Viongozi watakaoambatana na timu hiyo ni 
1. KARABANI LAWRENCE KARABANI- Meneja wa timu na Mkuu wa Msafara 
2. ROBERT MNENDE MANYERERE - Kocha
3. SHABANI MAHOBONYA - Afisa

Magessa ameishukuru Serikali, wazazi, makocha na  wadau wa kikapu mbali mbali ikiwemo kampuni ya Factory Media Production ambayo kwa sehemu kubwa imefanikisha safari hii, na wadau wengine ambao wameendelea kushirikiana nasi katika kuiandaa timu hii. Anakaribisha wadau wengine na mashirika mbalimbali kuendelea kushirikiana nasi katika kuendeleza mchezo wa kikapu Tanzania. 


MAKAMU WA RAIS AFUNGUA KONGAMANO LA SIKU LA BIASHARA NA UWEKEZAJI KATI YA TANZANIA NA MALAWI MKOANI MBEYA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Paulo Sango alipolitembelea banda la Wizara ya Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano kwenye kabla ya ufunguzi wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi kwenye ukumbi wa Royal Tughimbe mkoani Mbeya leo tarehe 26, Julai 2018.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya Huduma za TTCL kutoka kwa Afisa Huduma kwa Wateja Bi. Niva Frankie Mkwe kabla ya ufunguzi wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi kwenye ukumbi wa Royal Tughimbe mkoani Mbeya leo tarehe 26, Julai 2018. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)  
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi kwenye ukumbi wa Royal Tughimbe mkoani Mbeya leo tarehe 26, Julai 2018. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)  
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Amos Makala akihutubia wakati wa kuwakaribisha wageni kwenye ufunguzi wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi kwenye ukumbi wa Royal Tughimbe mkoani Mbeya leo tarehe 26, Julai 2018.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati),Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Amos Makala (kushoto) pamoja na Waziri wa Viwanda Biashara na Utalii wa Malawi Mhe. Hon Henry Mussa (MB) wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi kwenye ukumbi wa Royal Tughimbe mkoani Mbeya leo tarehe 26, Julai 2018. (Picha na Ofisi ya  Makamu wa Rais)

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA WFP

$
0
0
   
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani World Food Programme (WFP) David Beasley zawadi ya Picha moja ya mbuga za wanyama zilizopo nchini pamoja na kinyago cha mpingo mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini Michael Dunford mara baada ya mazungumzo na ujumbe huo wa Shirika hilo la kimataifa Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkurugenzi wa kanda wa (WFP)  Bi. Lola Castro mara baada ya mazungumzo na ujumbe huo wa Shirika hilo la kimatifa Ikulu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini Michael Dunford pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Agustine Mahiga wakishuhudia. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani World Food Programme (WFP) David Beasley pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Agustine Mahiga mara baada mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani World Food Programme (WFP) David Beasley wanne kutoka (kushoto) Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Agustine Mahiga watatu kutoka kulia, Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Omary Mgumba wapili kutoka kulia, Balozi Zuhura Bundala wakwanza kushoto akifatiwa na na Mkurugenzi wa kanda wa (WFP) Bi. Lola Castro pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini Michael Dunford watatu kutoka kushoto. PICHA NA IKULU .

SPIKA NDUGAI, WAJUMBE WA KAMATI YA BUNGE YA HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII WAKUTANA NA KUZUNGUMZA NA AFISA MTENDAJI MKUU WA VSO LEO BUNGENI JIJINI DODOMA.

$
0
0
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa tatu kushoto) akimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Voluntary Services Overseas (VSO), Dkt. Philip Goodwin (wa tano kulia) pale ugeni kutoka Shirika hilo ulipomtembelea leo tarehe 26 Julai 2018 Ofisini kwake Jijini Dodoma
Spika wa Bunge (katikati) na Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakimsikiliza Mkuu wa masuala ya Usimamizi wa tafiti na Tathmini kutoka Shirika la Kimataifa ya Voluntary Services Overseas (VSO), Ndg. Innocent Augustino (kushoto) wakati wa kikao kilichokuwa kinaeleza Shughuli Mbali mbali zinazofanywa na Shirika hilo, tukio lililofanyika leo tarehe 26 Julai 2018 Ukumbi wa Spika Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge (katikati) na Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu kutoka Shirika la Kimataifa la Voluntary Services Overseas (VSO), Dkt. Philip Goodwin (kushoto) wakati wa kikao kilichoelezea Shughuli Mbali mbali zinazofanywa na Shirika hilo, tukio lililofanyika leo tarehe 26 Julai 2018 Ukumbi wa Spika Bungeni Jijini Dodoma.(PICHA NA DEONISIUS SIMBA - OFISI YA BUNGE) .
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Voluntary Services Overseas (VSO), Dkt. Philip Goodwin alipomtembelea leo tarehe 26 Julai 2018 Ofisini kwake Jijini Dodoma. 

Watoto saba wafanyiwa upasuaji wa moyo kambi maalum ya matibabu ya siku tano inayoendelea katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)

$
0
0
Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao kutoka Shirika la Chain of Hope la nchini Uingereza wakimfanyia upasuaji wa kuziba matundu na kurekebisha mishipa ya moyo ambayo imekaa vibaya mtoto mwenye umri wa miezi mitatu katika kambi maalum ya upasuaji ya siku tano inayoendelea katika Taasisi hiyo. Jumla ya watoto saba wameshafanyiwa upasuaji na hali zao zinaendelea vizuri. 
Kazi ya kumfanyia upasuaji wa kuziba matundu na kurekebisha mishipa ya moyo ambayo imekaa vibaya mtoto mwenye umri wa miezi mitatu ikiendelea.Picha na Brighton James - JKCI

SHULE YA SEKONDARI YA KISIMIRI YAPONGEZWA KWA KUSHIKA NAFASI PILI KITAIFA MATOKEO KIDATO CHA SITA

$
0
0
Na Woinde Shizza, Arusha 

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru mkoani Arusha Christopher Kazeri amewapongeza walimu wa Shule ya Sekondari Kisimiri kwa kufanikisha kushika nafasi ya pili kitaifa matokeo ya mtihani wa kidato cha sita.

Nafasi ya kwanza katika matokeo ya mtihani imeshikwa na Shule ya Sekondari Kibaha kati ya shule 543 zilizofanya mtihani huo.Akizungumza leo wakati akitoa pongezi hizo Kazeri amesema walimu wa Shule ya Sekondari Kisimiri kwa jitihada zao wamefanikisha shule hiyo kushika nafasi ya pili kitaifa katika matokeo ya kidato cha sita kwa mwaka huu 2018.

Pia amewataka walimu hao kuongeza bidii katika ufundishaji ili kupata matokeo mazuri zaidi kwa kushika nafasi ya kwanza kitaifa katika matokeo ya mitihani ijayo.Akiwa shuleni hapo pamoja na kutoa pongezi kwa walimu, wazazi na wanafunzi amepata nafasi ya kusikiliza na kutatuo changamoto zinazowakabili walimu kwa lengo la kuleta tija zaidi kwenye taaluma ya Shule hiyo.

Kwa upande wa Makamu Mkuu wa shule ya Sekondari Kisimiri Mwalimu John Awe amesema kuwa mojawapo ya mbinu zilizotumika kuhakikisha shule hiyo inapata matokeo mazuri illikuwa kutoa mafunzo ya ziada kwa wanafunzi waliokuwa na uwezo mdogo.

"Hivyo walimu walitenga muda wa ziada kuwafundisha wanafunzi hao ambao wengi wao walifanya vibaya kwenye mtihani wa utamirifu (MOCK) kwa kupata alama sifuri,"amesema.
Pia amesema walimu wa shule hiyo wana moyo wa kufundisha na kufafanua kwenda darasani ni suala moja na kufundisha kama inavyotakiwa na wanafunzi kuelewa ni jambo jingine .

Wakati walimu nao walimu wametoa changamoto zinazoikabili shule hiyo ikiwamo ya uhaba wa viti vya walimu 50 na madawati ya wanafunzi 300.Pi walimu hao wamehitaji ufafanuzi wa maslai yao kama watumishi ikiwemo kupanda daraja.Akitoa ufafanuzi wa masuala ya watumishi Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu Grace Mbilinyi amesema kutokana na mchakato wa kuwabaini watumishi hewa na wenye vyeti vya kugushi Serikali ilisitasha upandaji madara kwa watumishi wa umma.

"Ila kwa sasa maelekezo mbalimbali yanatolewa.Kuhusu malipo ya likizo ni vema walimu mkaweka viambatanisho vyote muhimu vikiwemo vyeti vya watoto vya kuzaliwa na vyeti vya ndoa,"amesema.Aidha katika matokeo haya ya shule ya Sekondari Kisimiri imeonesha kuweka rekodi nzuri ya kufanya vizuri katika matokeo ya mitihani hiyo ya kidato cha sita.

"Kwani kwa miaka 3 mfululizo imekuwa kwenye kundi la shule tatu bora kitaifa.Mwaka 2016 ilishika nafasi ya kwanza, mwaka 2017 ikashika nafasi ya tatu na kwa mwaka huu 2018 imeshika nafasi ya pili kitaifa."Kwa watahiniwa wetu 67 kupata daraja la kwanza na la pili ikiwa 51 kati yao wamepata daraja la kwanza na 16 kupata daraja la pili,"amefafanua.

Imeelezwa matokeo ya Sekondari ya Kisimiri imezidi kuutangaza mkoa wa Arusha wenye shule 31 zenye watahiniwa zaidi ya 30 za Serikali na binafsi.

HALMASHAURI YA MERU YASHIKA NAFASI YA KWANZA UMITASHUMTA

$
0
0
Na Woinde Shizza,Arusha 

OFISA Elimu Msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwalimu Sara Kibwana amesema halmashauri hiyo imeibuka mshindi wa kwanza na wa jumla ngazi ya Mkoa kwenye mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) yaliyofanyika Juni 6 mwaka huu.

Akizungumza leo wilayani hapa amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Meru imezawadiwa vikombe vitano kutokana na kuwa mshindi wa kwanza kwenye mpira wa miguu wavulana na mpira wa wavu wasichana.Ameongeza pia mpira wa mikono wasichana na mpira wa kengele pia ilikuwa mshindi wa pili kwenye mchezo wa mpira wa wavu wavulana.

Kibwana amesema siri ya ushindi huo ni pamoja na maandalizi mazuri yaliyofanyika kwani halmashauri hiyo ilitoa maelekezo zaidi ya miezi 9 iliyopita kwa walimu wakuu wa shule za msingi.Ambapo yalilenga kuhakikisha kila wiki wanafunzi wanakua na siku za kufanya michezo.Pia maandalizi yalikuwa mazuri wakati wa michezo kwani wachezaji walijiandaa kikamilifu kwa kukaa siku tano kambini.

Wakati huo huo Ofisa Utamaduni wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Senyaeli Pallangyo amesema uchaguzi wa wachezaji umefanyika kwa kuzingatia viwango vilivyofanyika kuanzia ngazi ya chini hadi Wilaya."Ushindi huo mkubwa ikiwa ni pamoja na uwezo wa makocha sambamba na wachezaji kuwa na nidhamu ya hali ya juu na kufuata taratibu za michezo,"amesema .

Jumla ya wachezaji 25 kutoka timu mbalimbali za Halmashauri ya Wilaya ya Meru na makocha wanne wamechaguliwa kuunda timu ya Mkoa wa Arusha .Imeelezwa kuwa ikumbukwe Halmashauri ya Wilaya ya Meru kwa mwaka huu imekuwa mshindi wa kwanza na wa jumla kwa ngazi ya Mkoa wa Arusha wenye Halmashauri 7.
Picha ni vikombe ambavyo halmashauri ya meru imevishinda (picha na Woinde Shizza,Arusha0.

UCHAGUZI WA CHAMA CHA GOFU TANZANIA KUFANYIKA AGOSTI 18 MWAKA HUU.

$
0
0
NA Agness Francis ,globu ya jamii

Baraza la michezo (BMT) linatangaza kufanya uchaguzi wa chama cha gofu Tanzania  (TGU)

Uchaguzi huo unatarajia kufanyika agosti 18  mwaka huu katika  klabu ya viwanja vya gymkhana mkoani Morogoro.

Ambapo fomu zitatolewa bure katika ofisi za baraza  zilizopo uwanja wa taifa Jijini Dar es Salaam au kupatikana kwenye tovuti ambayo ni wwwnationalsportscouncil,Fomu hizo zitaanza kuchukuliwa  kuanzia tarehe  26 hadi 18 agosti mwaka huu,ambapo usajili utafanyika siku moja kabla ya uchaguzi huo.

Nafasi  zinazogombaniwa  ni Rais,makamu wa rais,katibu wa heshima,muweka hazina,katibu mashindano,handicap Secretary.

Sifa zinazohitajika kwa mgombea  ni awe raia wa Tanzania ,awe mzoefu wa uongozi pamoja na taaluma za uongozi wa mazoezi,awe na ujuzi wa mchezo wa gofu,awe hajatenda kosa lolote la jinai.


DK. KIGWANGALLA AAGIZA WAVAMIZI MAENEO YA HIFADHI MKOANI KIGOMA WAHAME MARA MOJA

$
0
0
Na Hamza Temba-Kigoma

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla ameagiza wavamizi wote waliopo ndani ya Pori la Akiba Kigosi/Moyowosi na Hifadhi ya Msitu wa Makere mkoani Kigoma waondoke mara moja kupisha maeneo hayo yaendelee kuhifadhiwa kwa mujibu wa Sheria.

Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo jana alipokuwa akizungumza na uongozi wa mkoa wa Kigoma, ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya kikazi mkoani humo. Alisema taarifa za kiitelijensia zinaonyesha kuwa wengi wa wavamizi hao ambao wameanzisha makazi, kilimo na ufugaji ni raia kutoka nchi jirani ambao pia wamekuwa wakijihusisha na uharibifu wa mazingira na vitendo vya ujangili.

"Haivumiliki kwa kiongozi yeyote mzalendo kwa nchi yake ambaye anajua kabisa maeneo yetu yamewekwa akiba kwa ajili ya uhifadhi na tunawazuia hata wananchi raia kuyatumia alafu wanakuja raia wa nchi nyingine wanaachiwa wafanye wanavyotaka, hapana hili halikubaliki" alisisitiza Dk. Kigwangalla huku akiutaka uongozi wa Mkoa huo usaidie kusimamia Sheria na wavamizi hao waondoke mara moja.

Aidha, ametoa kipindi cha miezi mitatu kwa watu wote waliovamia maeneo ya kinga za hifadhi (bafa) ambayo ni mita 500 kutoka mpaka wa hifadhi na vijiji waondoke kwa hiari yao wenyewe kabla ya kuondolewa kwa nguvu.

Katika hatua nyingine, Waziri Kigwangalla ameliagiza Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania TANAPA kushirikiana na uongozi wa mkoa wa Kigoma na Halmashauri husika pamoja na Wakala wa Huduma za Barabara TANROADS katika ujenzi wa barabara inayounganisha Hifadhi ya Taifa ya Gombe na Mkoa huo na maeneo mengine.

Alisema, Serikali ya awamu ya tano imepanga kufungua Sakiti mpya za utalii ikiwemo ya Kanda ya Magharibi ambayo inaujumuisha mkoa wa Kigoma, hivyo ni lazima miundombinu ya barabara ijengwe na kuimarishwa ipitike muda wote ili hifadhi hizo zitumike zaidi kibiashara na ziweze kuchangia ipasavyo kwenye pato la Taifa kuliko ilivyo hivi sasa.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa, Muongoza Watalii wa Hifadhi ya Taifa ya Gombe, Iddi Kaluse kuhusu Maporomoko ya Maji ya Kakombe ambayo ni kivutio kikubwa cha utalii ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Gombe alipotembelea hifadhi hiyo jana wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Kigoma.

Baadhi ya Sokwe Mtu katika Hifadhi ya Taifa Gombe.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia Sokwe Mtu katika Hifadhi ya Taifa Gombe alipotembelea hifadhi hiyo jana wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi mkoani Kigoma.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipanda mlima kwa ajili ya kuwaona Sokwe Mtu katika Hifadhi ya Taifa Gombe alipotembelea hifadhi hiyo jana wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi mkoani Kigoma.

Msafara wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ukielekea Hifadhi ya Taifa Gombe kwa kutumia usafiri wa boti.

DIWANI MWINGINE CHADEMA AJIUZULU MBEYA

MSANII WA KUCHONGA VINYAGO TANZANIA ATOA ZAWADI KWA RAIS PUTIN WA URUSI KWA KUFANIKISHA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA.

$
0
0
Na Dixon Busagaga, Moshi.
MSANII wa Sanaa za Uchongaji Vinyago Bw. Athumani Mwariko ametoa Kinyago cha Kiafrika kama zawadi kwa Rais wa Urusi ,Vladimir Putin ikiwa ni zawadi kwa nchi hiyo kuandaaa na kufanikisha fainali za Fifa za Kombe la Dunia.
Mwariko ambaye pia ni Mkurugenzi wa taasisi ya Sanaa ya Kilimanjaro Cultural Heritage Centre ya mkoani Kilimanjaro alisema zawadi hiyo itawasilishwa kwa Rais Putin kupitia kwa Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe.

Akizungumza na wanahabari, Bw. Mwariko alisema zawadi hiyo kwa Rais Putin inatokana na uandaaji mzuri wa mazingira uliopelekea kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa fainali hizo zilizomalizika hivi karibuni katika miji mbalimbali nchini Urusi.
“Michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu tumeweza kushuhudia mazingira tofauti kattika maandalizi yake ,kufanyika hadi kumalizika kwake ,fainali za mwaka huu zimekuwa na utofauti mkubwa sana ukilinganisha na zile zilizopita,”alisema Mwariko.
MSANII wa Sanaa za Uchongaji Vinyago ,Athumani Mwariko akiwa na Kinyago chake alichokichinga. 

MBARAWA AAGIZA DAWASCO KUWEKA MITA ZA PRE PAID KATIKA VIWANDA VYOTE JIJINI DAR

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
WAZIRI  wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa amewaagiza Shirika la Maji safi na Maji taka (DAWASCO) kubadilisha mita zote za maji kwa viwanda vyote vya Dar es Salaam na wale wateja wakubwa.

Hayo ameyasema leo alipotembelea viwanda vya Azam Bakheresa, Pepsi na Coca Cola ili kuweza kuona kila mteja anapata maji kwa maslahi anayoyahitaji.

Prof Mbarawa amesema kuwa amewaagiza DAWASCO kufunga mita za malipo ya kabla  (Pre Paid) zitazomuwezesha mteja kununua maji kulingana na matumizi yake ambapo atahitaji kulipia kwanza kabla ya kupatiwa maji na hela itakapomalizika maji hayatatoka.

"Mfumo huu wa mita za malipo ya kabla (Pre Paid) utamfanya mteja atumie maji kulingana na mahitaji yake na atalipia maji kabla na hela yake itakapoisha maji hayatatoka na hilo litasaidia kwa kila kufahamu matumizi yake sahihi ya maji,"amesema Prof Mbarawa.

Ameeleza kuwa, viwanda vyote na wateja wakubwa watafungiwa mita hizo ambazo zitakuwa zinaendeshwa kwa mfumo wa kidigitali na utasaidia kusimamia maji yanayostahili kutumika pia fedha wanazostahili kuzipata kutoka katika maji hayo.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa akizungumza na wananchi wa eneo la Mwenge akiwaelezea mfumo mpya wa mita za malipo ya kabla (Pre Paid) utakaoanza kutumika hivi karibuni. Hayo aliyasema katika ziara yake katika Viwanda mbalimbami leo Jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maji safi na Maji taka (DAWASCO) Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mfumo mpya wa mita za malipo ya kabla (Pre Paid) baada ya kumaliza ziara ya kutembelea viwanda mbalimbali Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa akizungumza na baadhi ya viongozi wa Kiwanda cha Soda Pepsi alipotembelea kiwanda hicho kwa ajili ya kukagua mita za maji iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa akikagua mita ya maji katika Kiwanda cha Pepsi leo Jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAHAKAMA YAPOKEA BARUA YA KUFUTWA KAZI ALIYEKUWA MHASIBU WA TAKUKURU

$
0
0
*Ni anayetuhumiwa kumiliki mali isiyolingana na kipato chake

Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imepokea barua ya kufutwa kazi kwa aliyekuwa Mhasibu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru), Godfrey Gugai kama kielelelezo namba sita katika kesi ya utakatishaji na kumiliki mali isiyolingana na kipato chake inayomka bili Gugai na wenzake watatu

Uamuzi huo umetolewa leo mahakamani hapo na Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba kutokana na pingamizi la upande wa utetezi waliokuwa wanapinga shahidi wa kwanza wa upande wa Jamuhuri kutoa kielelezo hicho wakidai kuwa siyo mtu husika.
Katika pingamizi lao Wakili wa utetezi Alex Mgongolwa alidai mahakamani hapo kuwa, shahidi Huyo hapaswi kutoa kielelezo hicho kwa kuwa siyo mtu aliyeandika barua hiyo na wala haielewi vile vile hakikuwa mikononi mwake.
Akitoa uamuzi wa kupokea kielelezo hicho, Hakimu Simba amesema, kifungu cha 34(b)(1) walichotumia upande wa utetezi kuwasilisha pingamizi hilo hakiusiani kabisa na mazingira ya kesi hiyo,"Shahidi Huyo Ayoub Akida katika ushahidi wake alidai yeye ni afisa Utumishi Mkuu wa Takukuru, ambaye ndie anahusika katika kutunza mafaili ya wafanyakazi ikiwemo barua hiyo ya kufutwa kazi.
Amesema sababu zilizowasilishwa katika pingamizi la upande wa uetezi za kutaka barua hiyo isipokelewe mahakamani kama kielelezo hazina msingi hivyo zimekataliwa na barua imepokelewa kama kielelezo Namba 6. Amesema shahidi ndiyo mtu sahihi anayepaswa kuwasilisha kielelezo hiki mahakamani kwani yeye ndie anayetunza mafaili yote ya wafanyakazi wa Takukuru na kwamba alihusika katika suala la kujadiliwa nidhamu ya mshtakiwa Gugai.
Mbali na Gugai, washtakiwa wengine, ni George Makaranga, Leonard Aloys na Yasin Katera.Washtakiwa hao wanakabiliwa na makosa 43, kati ya hayo 19 ni ya kughushi, 23 ni utakatishaji fedha na moja ni kumiliki mali zilizozidi kipato halali.Gugai anakabiliwa na kosa la kumiliki mali kinyume na kipato chake, ambapo alitenda kosa hilo kati ya January 2005 na Decemba 2015.

Inadaiwa akiwa jijini Dar es Salaam kama mwajiriwa wa TAKUKURU alikuwa akimiliki mali za zaidi ya Sh 3.6 bilioni ambazo hazilingani na kipato chake cha awali na cha sasa cha zaidi ya Tsh.milioni 800,huku akishindwa kuzitolea maelezo.

MAHAKAMA YATAJA TAREHE YA KUWASOMEA MAELEZO YA AWALI VIGOGO SIMBA, AKIWAMO AVEVA

$
0
0
Na Ripota wa Globu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Agosti 3 Mwaka huu inatarajia kuwasomea maelezo ya awali, (PH) viongozi  wa Klabu ya Simba, akiwemo Rais wake Evans Aveva na Makamu wake ambao  wanakabiliwa na kesi ya kughushi na kutakatisha fedha.

Hakimu Mkazi  Mkuu wa Mahakama  hiyo, Thomas Simba ameeleza hayo leo ambapo kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.Wakili wa Serikali Mwandamizi, Shadrack Kimaro ameiomba Mahakama kuipangia kesi hiyo tarehe nyingine ya kuja kuwasomea washtakiwa hao PH.

Aidha Kimaro ameieleza Mahakama hiyo kuwa kuanzia sasa, kesi hiyo  itakuwa ikiendeshwa na maofisa kutoka ofisi ya  DPP wakishirikiana na maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru).Wakili Nehemia Nkoko na Nestory Wandiba, waliutaka upande wa kuharakisha kuwasomea maelezo ya awali wateja wao kwa sababu wanaendelea kuteseka mahabusu.
Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 3 mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya  (PH).Washtakiwa wengine  ni  Zacharia Hanspoppe ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Klabu ya Simba na mfanyabiashara, Franklin Lauwo, ambao mpaka sasa bado hawajakamatwa.

Washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka 10 ikiwemo kughushi ambapo inadaiwa kati ya   Machi 10 na 16 mwka 2016, Aveva na Nyange waliandaa nyaraka za kuhamisha dola za kimarekani 3000,000 kutoka kwenye akaunti ya klabu ya Simba kwenda kwenye akaunti ya Aveva wakijua kuwa wanachofanya ni kosa.

JIJI LA DAR ES SALAAM

$
0
0
Sehemu ya jiji   la Dar es salaam linavyoonekana katika picha iliyopigwa kutoka angani  hivi karibuni. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI 26.07.2018

Naibu Katibu Mkuu ataka vikwazo vya lugha kuondolewa kwenye mitaala Afrika

$
0
0
Na Mwandishi wetu
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Elimu ya Ufundi, Avemaria Semakafu ametaka kuvunjwa kwa vikwazo vya lugha vinavyosababisha mkanganyiko wa utoaji elimu barani Afrika kwa kutumia Kiswahili.

Alisema mataifa ya Afrika yamekuwa yakibabaika katika matumizi ya lugha za kikoloni ambazo zimesababisha pia kuwa na ulingafu dhaifu wa utoaji elimu kwa bara hili.

Alisema hayo kwenye kongamano la Mataifa zaidi ya 16 yaliyo Kusini mwa Jangwa la Sahara ambayo yamekuwa yakikutana kuanzia Jumatano kujadiliana namna bora ya kutengeneza mitaala na vifaa vya kufundishia ili kuboresha mbinu za kufundisha na kujifunza.

Alisema ipo haja ya kuondokana na mifumo ya mapokeo ambayo imejaa taratibu za kikoloni zinazompima mtu kwa mitihani na akifeli kuonekana hana uwezo, wakati waliofeli ndio wanafanya vyema katika maisha ya kawaida ya kila siku.

Akizungumza na wawakilishi hao ambao wanashiriki katika kongamano la siku tatu katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Kinondoni Dar Es Salaam, Naibu Katibu Mkuu huyo alisema ipo haja ya kuangalia mfumo mzima na kupata vigezo halali vya kutathmini mafanikio ya elimu kwa kuangalia elimu yenyewe mitaala na namna ya uwekaji wa ulinganifu wa matokeo.

Alitaka mataifa ya Afrika kutumia lugha moja ya Kiswahili katika ufundishaji ili kuondokana na kikwazo cha lugha ambacho alisema ni moja ya kifaa cha utamaduni wa utoaji elimu.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Elimu ya Ufundi, Dk . Avemaria Semakafu akifungua kongamano la kikanda kuhusu ulinganifu wa mafunzo, mitaala, mafunzo kwa walimu na vifaa vya kufundishia mataifa zaidi ya 16 yaliyo Kusini mwa Jangwa la Sahara ili kubadilishana uzoefu wa namna ya kushirikiana na kufanyakazi kimtandao ili kuboresha mazingira ya kujifunza kwa mamilioni ya wanafunzi kwenye nchi hizo liliofanyika jijini Dar es Salaam. Kongamano hili limeandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni-UNESCO na linaendeshwa na mtandao wa TALENT.
Mkurugenzi wa UNESCO kanda ya Afrika Mashariki na Afisa Mwakilishi wa Unesco nchini, Ann Therese Ndong- Jatta akizungumzia umuhimu wa mafunzo hayo wakati wa kongamano la kikanda kuhusu ulinganifu wa mafunzo, mitaala, mafunzo kwa walimu na vifaa vya kufundishia lililokutanisha nchi 16 ili kutekeleza moja ya malengo ya maendeleo endelevu SDGs, lengo la nne lililofanyika Jijini Dar es Salaam. Kongamano hili limeandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na linaendeshwa na mtandao wa TALENT.
Mratibu wa mtandao wa watoa elimu na mafunzo kwa mabadiliko (TALENT) kutoka UNESCO Dakar, Valérie Djioze-Gallet akizungumzia madhumuni kuratibu kongamano hilo la kikanda linalojadili kuhusu ulinganifu wa mafunzo, mitaala, mafunzo kwa walimu na vifaa vya kufundishia ili kukabiliana na changamoto zilizopo katika sekta ya elimu hasa kwenye nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara (SSA) ili kufikia lengo la nne la maendeleo endelevu (SDGs) katika elimu. Kongamano hili limeandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na linaendeshwa na mtandao wa TALENT.

Baadhi ya wadau kutoka nchi mbalimbali wakifuatilia mada kwenye kongamano la kikanda linalohusu ulinganifu wa mafunzo, mitaala, mafunzo kwa walimu na vifaa vya kufundishia ili kukabiliana na changamoto zilizopo katika sekta ya elimu hasa kwenye nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara (SSA).
Baadhi ya wanakamati ya maandalizi ya kongamano hilo kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Elimu ya Ufundi, Dk . Avemaria Semakafu katika picha ya pamoja ya washiriki wa kongamano la kikanda kuhusu ulinganifu wa mafunzo, mitaala, mafunzo kwa walimu na vifaa vya kufundishia mataifa zaidi ya 16 yaliyo Kusini mwa Jangwa la Sahara ili kubadilishana uzoefu wa namna ya kushirikiana na kufanyakazi kimtandao ili kuboresha mazingira ya kujifunza kwa mamilioni ya wanafunzi kwenye nchi hizo liliofanyika jijini Dar es Salaam. Kongamano hili limeandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni-UNESCO na linaendeshwa na mtandao wa TALENT.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Halmashauri ya Bagamoyo yajadili majibu ya hoja mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali

$
0
0
MKAGUZI wa ndani wa halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo Bw. Paschal Shindai ameisihi taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) na Jeshi la polisi kuwasilisha nyaraka za malipo ambazo amesema zipo mikononi mwao kwa miaka 10 sasa ili waweze kufunga hoja.
Aidha ameweka bayana kwamba kati ya hoja 79 zilizokuwepo katika halmashauri hiyo, hoja 62 zilipata majibu ya kuridhisha na kufungwa ambapo 17 hazijafungwa hadi sasa
Bw . Shindai aliyasema hayo katika kikao maalum kilicholenga kupokea na kujadili majibu ya hoja mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG)mwaka 2016/2017kilichowashirikisha madiwani, katibu tawala wa mkoa wa Pwani (RAS) na mkaguzi mkuu wa nje wa mkoa. 
Bw.  Shindai alisema katika ukaguzi maalum uliofanyika mwaka wa fedha 2008/2009 imebainika hati za malipo zenye thamani ya milioni 158.347.155 hazikupatikana kukamilisha zoezi la ukaguzi na kwamba hati zote za malipo ambazo hazijapatikana kwa ajili ya ukaguzi maalum zilikuwa kwenye vyombo vya upelelezi vya TAKUKURU na jeshi la polisi . 
Alisema ofisi yake imeshachukua hatua ya kuandika barua za kuomba taasisi hizo ziwasilishe nyaraka hizo za malipo kwa ajili ya ukaguzi lakini hazijawasilishwa na kusababisha hoja kushindwa kufungwa. 
 Kamati ya ukaguzi iliitaka menejimenti ifuatilie nyaraka hizo na kama kuna sababu za kutopewa nyaraka hizo basi TAKUKURU itoe kwa maandishi.Kwa upande wake,  kamati ya fedha imeunga mkono maamuzi ya maoni hayo ya kamati ya ukaguzi. 
 Pamoja na hayo Bw. Shindai alielezea pia kuna hati za malipo zenye thamani ya zaidi ya milioni 92.935 kwa mwaka 2008/2009 kipindi cha ukaguzi maalum hazikupatikana na hazijakaguliwa . Hata hivyo  amesema kuna kesi na mashauri mbalimbali yaliyoko mahakamani na hadi  kufikia mwaka wa fedha 2012/2013 halmashauri ilikuwa bado ina mashauri 33 mahakamani . 
 "Katika ufuatiliaji wa hoja kwa miaka ya nyuma mwaka wa fedha 2008/2009,2010/2011,2012/2013,2013/2014 na mwaka 2015/2016 hoja 17 hazijafungwa.
"Hoja za ukaguzi kwa mwaka husika yaani mwaka wa fedha 2016/2017 hoja 20 kati ya hizo tisa zimefungwa na 11 hazijafungwa", alisisitiza Bw. Shindai. Katibu tawala wa mkoa wa Pwani Bw. Zuberi Samataba alisema atawasiliana na kamanda wa TAKUKURU mkoa Suzan Raymond na jeshi la polisi ili kuangalia namna ya kupata nyaraka ama taarifa za kimaandishi ili hoja ziweze kufungwa . Aliipongeza halmashauri hiyo kwa kupata hati safi mwaka huu . 
 " Kuweni makini wakati wa kuandaa taarifa za mahesabu. Shirikianeni na muwe kitu kimoja baina ya wataalmu,watendaji,mkurugenzi na madiwani "alisema Bw. Samataba. 
 Mkurugenzi wa halmashauri ya Bagamoyo, Fatuma Latu alipokea ushauri na maelekezo waliyopatiwa na kudai watayafanyia kazi .
  Kikao maalum kilicholenga kupokea na kujadili majibu ya hoja mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG)mwaka 2016/2017 kilichowashirikisha madiwani wa Bagamaoyo na mkaguzi mkuu wa nje wa mkoa
 Mkaguzi wa ndani wa halmashauri ya Bagamoyo Bw. Paschal Shindai akizungumza katika kikao maalum cha  kujadili majibu ya hoja mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG)mwaka 2016/2017,kilichowashirikisha madiwani, katibu tawala wa mkoa wa Pwani (RAS) na mkaguzi mkuu wa nje wa mkoa.
Katibu tawala wa mkoa wa Pwani Zuberi Samataba  akizungumza jambo katika kikao maalum kilicholenga kupokea na kujadili majibu ya hoja mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG)mwaka 2016/2017,kilichowashirikisha madiwani wa Bagamaoyo na mkaguzi mkuu wa nje wa mkoa. Habari na picha na Na Mwamvua Mwinyi, Pwani

TAARIFA KWA UMMA: UFAFANUZI KUHUSU UPOTOSHWAJI WA BEI ZA MAFUTA

$
0
0
image001



1. UTANGULIZI
Moja ya majukumu ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) katika kudhibiti sekta ndogo ya mafuta ni pamoja na kushamirisha ushindani kwa kuweka mizania sawa ya ushindani; na kumlinda mtumiaji wahuduma. Katika kutimiza jukumu hili, EWURA hukokotoa bei kikomo za mafuta kwa nchi nzima ikizingatia gharama halisi za uagizaji wa mafuta ambazo hujumuisha bei ya mafuta katika soko la dunia, gharama za usafirishaji, kodi na tozo mbalimbali za serikali, faida ya wafanyabiashara na gharama za usafirishaji ndani ya nchi.
Kwa sasa mafuta yanapokelewa katika Bandari za Dar es Salam, Tanga na Mtwara, hivyo kuchochea uwepo na tofauti za bei Kikomo. Bei hizo kikomo hutangazwa kila Jumatano ya kwanza ya mwezi kwa kutumia kanuni maalum (Petroleum Pricing Setting Rules) iliyopitishwa kwa mujibu washeria.    
Kwa mujibu wa kanuni hiyo, bei yamafuta katika soko la dunia inayotumika katikakukokotoa bei ya mafuta kwa mwezi husika hapanchini ni ile ya miezi miwili ya nyuma kabla ya mafuta hayo kuanza kutumika. Kwa Mfano, bei za mafuta hapa nchini kwa mwezi Agosti, 2018 zita kokotolewa kwa kuzingatia bei zamafuta katika soko la dunia za mwezi Juni, 2018.

2. KIINI CHA TOFAUTI ZA BEI YA MAFUTA KATI YA DAR ES SALAAM NA TANGA KWA MWEZI JULAI 2018
Bei za mafuta kwa mwezi Julai 2018 zimeonekana kuwa na tofauti kubwa kati ya mafuta yaliyoingizwa nchini kupitia bandari ya Dar es Salaam na ile ya Tanga. Tofauti hiyo ya bei za mafuta inatokana  na sababu mbili kama zilivyoelezwa hapa chini-:
(a) Shehena zote za mafuta ya Petroli na Dizeli inayotumika kwa sasa ilikokotolewa kwa bei ya soko la Dunia la Mei 2018, bei ambazo kimsingi zimepanda kutokana na bei za soko la dunia kwa Mwezi Mei kupanda.
(b) Tofauti na mafuta yaliyopokelewa bandari ya Dar es Salaam, Mafuta Bandari ya Tanga kwa mara ya Mwisho yalinunuliwa Mwezi Aprili, 2018, ambapo bei zake katika soko la Dunia la Machi, 2018 ilikuwa haijapanda kama ilivyopanda kwa Mwezi Mei, 2018.
Kwa kuwa Tanga wameendelea kutumia mafuta yaliyoingizwa Machi, 2018, bei zake zimekuwa za chini ikilinganishwa na mafuta yanayopitia Bandari ya Dar es Salaam. (Mara ya mwisho kukokotoa bei ya mafuta yaliyopokelewa kupitia bandari ya Tanga ilikuwa mwezi Mei, 2018, na bei hiyo ilikokotolewa kwa kuzingatia kuwa mafuta hayo yalinunuliwa kwa bei ya soko la dunia ya mwezi Machi 2018.)
Bei ya reja reja kwa mkoa wa Tanga ni Sh 2,234/lita kwa Petroli na Sh 2,168/lita kwa  Dizeli, wakati kwa mkoa wa Dar es Salaam ni Sh 2,409/lita kwa Petroli na Sh 2,329/lita kwa Dizeli. Hivyo bei za mafuta kwa mkoa wa Tanga ziko chini kwa kiasi cha Sh 175/lita kwa Petroli na Sh 161/lita kwa  Dizeli ukilinganisha na bei za mkoa wa Dar es Salaam. Kwa sababu hiyo mafuta ya Tanga yamekuwa na bei ya chini kuliko yanayotokea Bandari ya Dar es Salaam.

3. ONYO:
EWURA inatoa onyo Kali kwa wote wanaosambaza habari za kupotosha kwa suala hili kwani kinachofanyika ni kutaka kuvuruga soko hatua ambayo itatafsiriwa kama ni uhujumu uchumi. Hivyo basi atakayebainika atachukuliwa hatua kali za kisheria.
IMETOLEWA NA:
Idara ya Mawasiliano na Uhusiano
Julai 26, 2018
Dodoma.



Viewing all 110164 articles
Browse latest View live




Latest Images