Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live

TAZAMA LIVE AROBAINI YA MTOTO WA ZAMARADI JIONI HII


JWTZ YASHEREHEKEA SIKU YA MASHUJAA KWA KUFANYA USAFI NA KUJITOLEA DAMU

$
0
0

Katika kuadhimisha siku ya mashujaa askari wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) nchi nzima wameitikia agizo la Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli kwamba siku hii mwaka huu itasherehekewa kwa kufanya usafi wa mazingira.
Katika Base ya Tanga wanajeshi wakiongozwa na Kamanda wa Base hiyo Brigedia Jenerali Mbaraka Mkeremy wamefanya usafi katika Hospitali ya Bombo na kujitolea damu ambapo jumla ya wanajeshi 300 wameshiriki zoezi hilo lililofanikisha kupatikana uniti 50.
 Kamanda wa Base ya JWTZ ya Tanga Brigedia Jenerali Mbaraka Mkeremy akiongoza wanajeshi 300 katika zoezi la kuchangia damu, baada ya kufanya usafi  katika Hospitali ya Bombo mjini Tanga leo Jumatano Julai 25, 2018 katika kuadhimisha siku ya mashujaa 
 Sehemu ya wanajeshi 300 katika wa Base ya Tanga wakiwa katika zoezi la kuchangia damu, baada ya kufanya usafi  katika Hospitali ya Bombo mjini Tanga leo Jumatano Julai 25, 2018 katika kuadhimisha siku ya mashujaa 

 Sehemu ya wanajeshi 300 katika wa Base ya Tanga wakiwa katika zoezi la kuchangia damu, baada ya kufanya usafi  katika Hospitali ya Bombo mjini Tanga leo Jumatano Julai 25, 2018 katika kuadhimisha siku ya mashujaa.
Picha na Sultani Kipingo, Globu ya Jamii, Tanga. 


Tanzania Yapongezwa Kwa Kazi Nzuri Ukaguzi Umoja wa Mataifa. Yamaliza kazi Rasmi na Kukabidhi Nchi ya Chile.

$
0
0
Na Ofisi ya UNBoA, New York, Marekani. 

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (CAG) Prof. Mussa Juma Assad leo tarehe 24 Julai, 2018 amekabidhi nafasi yake ya Ujumbe wa Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa (UNBoA) kwa nchi ya Chile. Makabidhiano hayo yamefanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano uliopo kwenye jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, Jijini New York nchini Marekani baada ya Tanzania kumaliza muda wake wa kipindi cha miaka sita (6) kuanzia Julai Mosi, 2012.   
Pamoja na kufanya makabidhiano hayo, CAG Prof. Assad pia amehudhuria Kikao cha Kawaida cha 72 cha Bodi hiyo na kuwasilisha jumla ya ripoti 13 za Ukaguzi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN). Ripoti hizo 13 zilizowasilishwa na Prof. Assad  na kutiwa saini na wajumbe wa Bodi ya Ukaguzi ya UN ni pamoja na Ukaguzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP), Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada kwa Wakimbizi wa Palestina na Mashariki (UNRWA), Mfuko wa Akiba kwa Watumishi wa UNRWA Wakazi (UNRWA – SPF), Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Wanawake (UN – Women) na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Mazingira  (UNEP). 
Ripoti nyingine ni za Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Mazingira ulio chini ya UNDPGEF, Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Mazingira ulio chini ya Shirika UNEP-GEF, Mfuko wa Mikopo Midogo midogo ulio chini ya UNRWA - MD Shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi (UN Habitat), Shirika la Umoja wa Mataifa la Ukuzaji Mitaji (UNCDF), Mahakama ya Umoja wa Mataifa inashughulikia Mauaji ya kimbari ya Yugoslavia ya zamani (ICTY), pamoja na ripoti ya Mpango wa Kupunguza Shughuli za Mahakama za Kimataifa Zinazoshughulikia Mauaji ya Kimbari (MICT).    
Akizungumza baada ya kuwasilisha ripoti zake, Prof. Assad amesema kikao hicho ni cha mwisho kwa nchi ya Tanzania kuhudhuria kama Mjumbe wa Bodi ya UNBoA na kinatarajiwa kuhitimishwa kesho tarehe 25 Julai, 2018. Hata hivyo, Prof. Assad amefafanua kuwa Tanzania itaendelea  kuwa mjumbe mwangalizi ”Observer Member” kwenye Jopo la  Wakaguzi wa Nje wa  Umoja wa Mataifa kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo baada ya kung’atuka kwenye nafasi ya Ujumbe wa Bodi hiyo.  
Prof. Assad amesema, katika kipindi cha miaka sita ya UNBoA, Tanzania haikuwa tu Mjumbe wa UNBoA bali pia ilipata fursa ya kuongoza Bodi ya Ukaguzi wa Umoja wa Mataifa (UNBoA) kwa kipindi cha miaka miwili (2).  
2/2 
”Nimekuwa mwenyekiti wa UNBoA kwa miaka miwili mfululizo kuanzia  Januari Mosi, 2015 hadi 31 Desemba, 2016 ambapo nimekuwa na jukumu la kuwasilisha taarifa za UNBoA katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kupitia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Nilitumia fursa hiyo kumshauri Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa niaba ya UNBoA njia bora ya kuimarisha mifumo ya udhibiti katika usimamizi wa fedha pamoja na kubadili muda wa uwasilishaji wa hesabu za Mashirika ya Umoja wa Mataifa ambayo yanatoa hesabu zake mwishoni mwa mwezi Aprili”, amesema CAG Prof. Assad.  
Tanzania inaingia katika historia ya dunia kuwa nchi ya kwanza katika Ukanda wa Afrika Mashariki na ya tatu (3) Barani Afrika kuteuliwa mjumbe wa Bodi ya Ukaguzi wa Umoja wa Mataifa (UNBoA) tangu kuanzishwa kwa Bodi hiyo mwaka 1946.  Nchi nyingine za Afrika ambazo zimewahi kuwa wajumbe wa Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa ni Ghana na Afrika ya Kusini tu.   
Tanzania imekuwa mjumbe wa Bodi hiyo kuanzia  Julai Mosi, 2012 hadi tarehe 30 Juni, 2018 baada ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuteuliwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuwa mjumbe wa Bodi hiyo mnamo tarehe 11 Novemba, 2011,  kwenye Kikao cha 58 cha Baraza hilo. Tanzania ilishirikiana na wajumbe wengine wa Bodi kutoka nchi za Uingereza, China, Ujerumani na India kwa vipindi tofauti.  

 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prof. Mussa Assad (katikati ya waliokaa) akitia saini ripoti za Ukaguzi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa wakati wa Kikao cha 72 cha Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa (UNBoA) kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano uliopo kwenye Jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN) tarehe 24 Julai, 2018 jijini New York nchini Marekani. Wengine ni  Mwenyekiti wa UNBoA na  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa India Bw. Rajiv Mehrishi (wa kwanza kulia) pamoja na Rais wa Taasisi Kuu ya Ukaguzi Ujerumani Bw. Kay Sceller (wa kwanza kulia) kwa pamoja wakitia saini Ripoti 28 za Ukaguzi wa Mashirika na Mifuko ya Umoja wa Mataifa kwenye kikao hicho
 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prof. Mussa Assad (wa kwanza kushoto) akimkabidhi nafasi yake ya Ujumbe wa Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa (UNBoA) kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Chile wakati wa Kikao cha 72 cha Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa (UNBoA) kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano uliopo kwenye Jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN) tarehe 24 Julai, 2018 jijini New York nchini Marekani. Prof. Assad amekabidhi nafasi hii baada ya Tanzania kumaliza muda wake wa kipindi cha miaka sita (6) kuanzia Julai mosi, 2012.  Mwingine ni Mwenyekiti wa UNBoA na  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa India Bw. Rajiv Mehrishi akishuhudia makabidhiano hayo.
 Sehemu ya Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia mada wakati wa Kikao cha 72 cha Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa (UNBoA) kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano uliopo kwenye Jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN) tarehe 24 Julai, 2018 jijini New York nchini Marekani.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa (UNBoA) na  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa India Bw. Rajiv Mehrishi (katikati) akimshukuru na kumpongeza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prof. Mussa Assad (wa kwanza kushoto) baada ya Tanzania kumaliza muda wake wa kipindi cha miaka sita (6) kuanzia Julai mosi, 2012 cha Ujumbe wa UNBoA na kukabidhi nafasi yake kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Chile. Makabidhiano hayo yamefanyika kwenye Kikao cha 72 cha UNBoA  kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano uliopo kwenye Jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN) tarehe 24 Julai, 2018 jijini New York nchini Marekani.
Ujumbe wa Tanzania ukiwa kwenye picha ya pamoja nje ya lango la Ukumbi wa Mkutano baada ya kuhudhuria hafla ya kutia saini ripoti za Ukaguzi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na kukabidhi nafasi yake ya Ujumbe wa Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa (UNBoA) kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Chile baada ya Kikao cha 72 cha UNBoA kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano uliopo kwenye Jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN) tarehe 24 Julai, 2018 jijini New York nchini Marekani.

WAZIRI MKUU AKERWA NA HALI YA UCHAFU COCO BEACH, ataka Mamlaka za Serikali za Mitaa husika zisimamie fukwe zote nchini

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hali ya usafi Coco Beach hairidhishi na amewataka viongozi wa Manispaa ya Kinondoni wajipange ili eneo hilo liweze kuvutia.
Ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Julai 25, 2018) wakati akizungumza na wananchi mara baada ya kushiriki zoezi la usafi wa eneo hilo pamoja na wananchi na watendaji mbalimbali ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa ambayo hufanyika Julai 25, kila mwaka. 
Waziri Mkuu ambaye aliambatana na mke wake, Mary Majaliwa, alishiriki zoezi hilo kwa kufyeka nyasi, kuzoa takataka na kupanda miti kwenye ufukwe huo.Zoezi hilo limefanyika kuanzia kwenye eneo la wafanyabiashara wa mihogo kuelekea Police Officers’ Mess.

“Eneo hili nimelitembelea, bado haliridhishi kwa usafi. Nimeenda kwenye fukwe pale na kukuta takataka nyingi zimelundikwa mahali pamoja. Ni vema Manispaa ya Kinondoni na Mamlaka zote zinazosimamia usafi ziwaratibu wanaotoa huduma na wanaopata huduma ili    kuendeleza usafi wa maeneo haya nchini kote,” amesema. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary  wakifyeka nyasi kwenye  eneo la Coco Beach jijini Dar es salaam  wakati waliposhiriki  katika maadhimisho ya   Siku ya Mashujaa kwa kufanya usafi wa mazingira katika eneo hilo , Julai 25, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakiadhimisha  Siku ya Mashujaa kwa kufanya usafi katika eneo la Coco Beach jijini Dar es salaam Julai 25, 2018.
.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakipeleka uchafu kwenye gari la takataka wakati waliposhiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa kwa kufanya usafi wa mazingira kwenye eneo la Coco Beach jijini Dar es salaam Julai 25, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua  eneo la Coco Beach  baada ya kushiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa kwa kufanya usafi wa mazingira kwenye  eneo hilo Julai 25, 2018. Wapili kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ally Happy.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua  eneo la Coco Beach baada ya kushirika katika Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa kwa kufanya usafi wa mazingira katika eneo hilo Julai 25, 2018. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ally Happy. Kwa habari kamili BOFYA HAPA


BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO 25.07.2018

MAAFISA BIASHARA WAPEWA SOMO KUHUSU URASIMISHAJI

WAZIRI JAFO APONGEZA KITUO CHA AFYA BAHI KUKAMILISHA

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe.Seleman Jafo leo ameendelea na ziara yake ya kikazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Bahi kuona maendeleo ya miradi mbalimbali inayotekelezwa.

Mhe. Jafo amewapongeza viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa Kituo cha afya cha Bahi na kuweza kukamilika kwa wakati na tayari kimeanza kutoa huduma kwa wananchi. 

Akiongelea kuhusu watumishi wa huduma ya afya walioajiriwa hivi karibuni amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi tayari imepata watumishi 39 ambao watatawanywa katika Halmashauri hiyo. Amesema kutokana na Halmashauri ya Bahi kuwa naupungufu Mkubwa wa vituo vya afyaSerikali imeweza kujenga vituo vya afya vya Mundemu na Bahi ili kutoa huduma bora kwa wananchi, pia tayari Serikali imetenga shilingi Bilioni 1.5 kwa ajili ya kujenga Hospitali ya Wilaya. 

Mhe. Jafo amemuagiza wahudumu wa afya wote nchini kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi ili waweze kuvutiwa kuja kutibiwa kwenye vituo vya afya. "Nawaagiza Wasimamizi wote wa Vituo vya afya na Zahanati kuhakikisha wanatumia lugha nzuri kwa wagonjwa ili kuwavutia kuja kupata huduma za afya" Amesema Jafo.Aidha amewataka wananchi kuhakikisha wanafuata ushauri unaotolewana na wataalam ili kuboresha afya zao.

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe.Selemani Jafo akizungumza na wananchi katika Kituo cha Afya Bahi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe.Selemani Jafo akikagua maeneo mbalimbali ya kutolea huduma kituo cha Afya Bahi.

MAHAKAMA KUU KITENGO CHA MAWAKILI WANASTAHILI PONGEZI.

$
0
0
Na Bashir Yakub. 

Kawaida safu hii huandika na kufafanua masuala mbalimbali ya kisheria na mahakama. Mara nyingi huandika kuhusu ndoa, mirathi, makampuni, jinai, ardhi, na madai mengine kwa ujumla. Leo itakuwa tofauti kidogo japo ni ndani ya tasnia ya sheria humohumo. 

Nianze tu kwa kusema kuwa wakati taifa zima likifanya kazi kufikia uchumi wa kati ambao ndio dira ya mihimili yote mahakama,bunge na serikali, kuna jambo moja ambalo hatuwezi kulisahau. 

Jambo hili ni utumishi uliotukuka. Hakuna ubishi, injini ya uchumi wa kati ni watumishi. Lakini ni aina gani ya watumishi ambao ni injini ndilo litakuwa swali. Aina ya watumishi ambao wanaweza kutufikisha huko ni wale wenye moyo wa kazi, ari, uvumilivu, waelewa,na wale ambao utumishi kwao sio kazi tu ya kusubiri mshahara mwisho wa mwezi, bali pia huduma nzuri kwa watu. 

Kote duniani ambako si tu wamefikia uchumi wa kati tunaoulilia, bali pia wana uchumi wa juu kama china, amerika, na nchi za ulaya wamefikishwa hapo na watumishi bora . Waliowahi kufika huko wanajua ni namna gani watumishi wa huko wanavyotoa huduma. Unaweza kudhani unahudunmiwa na ndugu yako wa tumbo moja. 

Niseme tu kuwa watumishi wa mahakama kuu ya Dar es salaam kitengo cha mawakili wameonesha mfano wa aina hii. Ni aina ya watumishi ambao ukibahatika kuhudumiwa nao unahisi kweli umepewa huduma. Hawatachoka kukupatia maelezo, hawatachoka kukuelekeza, na hata ukitaka namba zao binafsi hukupatia, na endapo utapiga muda wowote kutaka ufafanuzi utapewa bila kukaripiwa kama ambavyo imekuwa pahala pengine pa utumishi. 



LUGOLA AIBANA KAMPUNI IRIS, AIPA SIKU 14 ITOE MAJIBU KULETA MTAMBO AU SHILINGI BILIONI 32 ZA NIDA

$
0
0
Na Felix Mwagara, MOHA 

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ameipa wiki mbili Kampuni ya Kimataifa ya Iris Corporation Berhard impe majibu ya kuwa italeta mtambo wa kutengeneza kadi ghafi au Dola za Marekani Milioni 14 sawa na zaidi ya shilingi bilioni 32 za Tanzania. 

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dodoma leo, mara baada ya kumaliza kikao na Menejimenti ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na viongozi wa Kampuni hiyo, Waziri Lugola alisema kampuni hiyo haiwezi ikacheza na fedha za Watanzania ambao ni za walipa kodi. 

Lugola aliongeza kua lazima fedha hizo au mtambo huo upatikane kwa kuwa Serikali ya Awamu ya Tano haitakubaliana na mchezo mchafu wa aina yoyote, na pia yeye kama Waziri wa Wizara hiyo anaendelea kutekeleza maagizo ya Rais Dkt John Magufuli. 

“Tumezungumza nao na tumekubaliana nao kwamba tuwape wiki mbili ili bodi ya kampuni hiyo ikakae ifanye maamuzi ya aidha waturudishie fedha zetu au walete mtambo, lakini sisi kama nchi huu mtambo muhimu sana, bado tuna uhitaji, sisi tungependa baada ya hiyo wiki mbili wafanye maamuzi ya kutuletea mtambo,” alisema Lugola. 

Aidha, Waziri Lugola amewataka wamiliki wa kampuni zilizolipwa kifisadi fedha za Mradi wa mtambo wa NIDA kujisalimisha jijini Dodoma Agosti 3 mwaka huu wakiwa na mtambo huo vinginevyo warejeshe fedha zilizotumika. 

Pia Lugola ametoa agizo kwa aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dickson Maimu na Mfanyabiashara Jack Gotham kufika ofisini kwake Agosti 3 saa 3:00 asubuhi ili kutoa maelezo yanayojitosheleza yatakayomsaidia kutoa maamuzi sahihi kuhusiana na ufisadi wa fedha zaidi ya bilioni 32 za mtambo huo ambao hadi sasa haujafika nchini. 

Lugola aliyataja kampuni hayo kuwa Gotham International ambayo imelipwa kifisadi shilingi 2,848,878,659.75, Iris Corporation Berhard ambayo imelipwa kifisadi 22,919,414,169,84, Gwiholoto Impex inayodaiwa shilingi 946,406,989,00, Sykes Travel Agent 5,979,600,00, Dk Shija Paul Rimoy 27,000,000,00, Aste Insurance 1,206,619.93, na Kampuni ya BMTL 569,192,090,00. 

Hata hivyo, Waziri Lugola aliwataka Watanzania kutowahusisha viongozi wa sasa wa NIDA na ufisadi huo kwa kuwa hawahusiki hata kidogo, matukio yote ya ufisadi yamefanywa na watangulizi wao na viongozi waliopo sasa wameletwa kuiongoza Mamlaka hiyo kwa ajili ya kuboresha utendaji wa NIDA. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kikao chake na Menejimenti ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na Uongozi wa Kampuni ya Iris Corporation Berhard. Viongozi wa kampuni hiyo wamepewa wiki mbili ili walete majibu kuwa wataleta mtambo wa kutengeneza kadi ghafi au shilingi bilioni 32 walizopewa na NIDA. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati) akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Andrew Massawe alipokua akijadili jambo katika kikao alichokiitisha Waziri huyo kwa ajili kufanya mahojiano na Wamiliki wa Kampuni ya Iris Corporation Berhard. Wapili kulia ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo, Shaiful Subhan, na Choong ambaye pia ni kiongozi mkuu wa Kampuni hiyo. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati) akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Iris Corporation Berhard, Shaiful Subhan alipokua anafafanua jambo katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa wizara hiyo, jijini Dodoma leo. Viongozi wa kampuni hiyo wamepewa wiki mbili walete majibu kuwa wataleta mtambo wa kutengeneza kadi ghafi au shilingi bilioni 32 walizopewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA). Watatu kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA, Andrew Massawe. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kikao chake na Menejimenti ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na Uongozi wa Kampuni ya Iris Corporation Berhard. Viongozi wa kampuni hiyo wamepewa wiki mbili ili walete majibu kuwa wataleta mtambo wa kutengeneza kadi ghafi au shilingi bilioni 32 walizopewa na NIDA. Wapili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA, Andrew Massawe, na wapili kulia ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo, Shaiful Subhan. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YAIPONGEZA TTCL KWA KUJENGA MAZINGIRA RAFIKI KWENYE MINARA YA SIMU NCHINI

$
0
0
Kamati ya Bunge ya Miundombinu imelipongeza Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kwa kujenga mazingira rafiki ya uwepo wa choo na kibanda cha mlinzi kwenye minara ya simu iliyojengwa na Shirika hilo maeneo mbali mbali nchini kote

Hayo yameelezwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Hawa Mchafu wakati wa ziara ya Kamati hiyo ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano kwenye kijiji cha Mbatamila kilichopo kwenye kata ya Nampungu wilayani Tunduru mkoani Ruvuma

Mhe. Mchafu amesema kuwa tumeshuhudia kuwa Shirika letu la kizalendo la TTCL pekee ndilo ambalo limejenga miundombinu rafiki ya choo na kibanda kwenye minara yao yote waliyojenga kwenye maeneo mbali mbali nchi nzima kwa ajili ya mlinzi anayelinda minara ya mawasiliano tofauti na kampuni nyingine za mawasiliano ambapo zote kwa pamoja zimepatiwa ruzuku na Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) ya kujenga minara hiyo kwenye maeneo yasiyo na mvuto wa kibiashara

“Hongereni mmepata mawasiliano ya mnara wa TTCL ambapo wamejenga miundombinu rafiki ya choo na kibanda cha mlinzi cha kupumzikia hivyo mnara utalindwa muda wote, kutakuwa hamna maambukizi ya magonjwa kwa kukosa choo”, amesema Mhe. Mchafu. Ameipongeza TTCL kwa kuwa wamejenga mnara ambao unatoa mawasiliano muda wote kwa kuwa kuna nishati ya jenereta kubwa ya kisasa
.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu (hawapo pichani) wakiwa ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Christina Mndeme (aliyekaa mbele) wakati wa ziara ya Kamati hiyo ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano kwenye mkoa huo 
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Hawa Mchafu akisikiliza kwa makini maelezo kutoka Mhandisi wa TTCL mkoa wa Ruvuma Abrahamu Msangi kuhusu mtambo wa mawasiliano ya mnara huo wakati wa ziara ya wajumbe wa Kamati hiyo (hawapo pichani) ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano kwenye kijiji cha Mbatamila kilichopo wilayani Tunduru kwenye mkoani huo
Mkuu wa Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote Mhandisi Albert Richard (wa pili kushoto) akitoa maelezo kuhusu miundombinu rafiki ya mnara wa TTCL kwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Hawa Mchafu (wa tatu kushoto) wakati wa ziara ya Kamati hiyo ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano kwenye kijiji cha Mbatamila kilichopo Wilayani Tunduru mkoani Ruvuma. Wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye 
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Hawa Mchafu (wa kwanza kushoto) akiongea na wananchi (hawapo pichani) wa kijiji cha Mbatamila kilichopo wilayani Tunduru mkoani Ruvuma kuhusu umuhimu wa kulinda miundombinu ya mawasiliano wakati wa ziara ya Kamati hiyo ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano mkoani humo. Wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhandisi Ramo Makani na Mbunge wa jimbo la Tunduru Kaskazini akifafanua jambo kwa wananchi wa kijiji cha Mbatimila (wanaomsikiliza) kilichopo wilayani Tunduru mkoani Ruvuma wakati wa ziara ya Wajumbe wa Kamati hiyo (hawapo pichani) ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano kwenye mkoa huo .



MAKAMU WA RAIS AHITIMISHA ZIARA MKOANI SONGWE NA KUSISITIZA USHIRIKIANO

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amehitimisha ziara ya siku tano Mkoani Songwe mapema leo na kusisitiza ushirikiano baina ya uongozi ili kuharakisha maendeleo.

Mhe Samia Suluhu Hassan amesema akiwa ziarani katika wilaya za Momba, Mbozi na Ileje amebaini kuwa Mkoa wa Songwe umebarikiwa kuwa na rasilimali na utajiri mkubwa kinachotakiwa ni viongozi kushirikiana katika kuwatumikia wananchi.“Nimefurahishwa na kaulimbiu yenu ya maendeleo yataletwa na sisi wenyewe kwa ushindani na ushirikiano, bila ushirikiano hakuna maendeleo, kauli mbiu hii sasa ionekane kwa vitendo”, amesisitiza.

Ameongeza kwa kuwataka watendaji na viongozi wote wapende kuwatembelea wananchi kuanzia ngazi za vijiji ili waweze kuwahudumia vizuri na sio kukaa ofisini.Mhe Samia Suluhu Hassan ameongeza kwa kuzitaka halmashauri kutenga fedha kwa ajili ya kuwakopesha wanawake na vijana na kubuni miradi mikubwa itayaowaunganisha wajasiriamali wanawake na vijana kutengeneza viwanda ili kuondokana na umasikini.

Amesema mpango wa mkoa wa kuanzisha vituo vya maendeleo vya kata utawezekana na kuwanufaisha wananchi endapo watendapo watajitoa kwa dhati kuufanikisha na mpango huu utaiwezesha Songwe kupaa kiuchumi.

Aidha Mhe Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wa Mkoa wa Songwe kuendelea kutunza mazingira kwa kupanda miti na wale walioko mipakani kuendelea kutunza amani.Naye Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa ameshukuru Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kufanya ziara mkoani Songwe kuahidi kuwa maelekezo na maagizo aliyoyatoa atayasimamia yatekelezwe.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan mapema leo akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Songwe (walioko mstari wa nyuma) kabla hajaondoka kuelekea Mkoa wa Mbeya.

MSANII WA BONGOFLEVA MCHIZI MOX: 'NAFANYA BIASHARA, NIMEPUMZIKA MUZIKI'

KUPATWA KAMILIFU NA KUREFU ZAIDI KWA MWEZI PAMOJA NA MPANGILIO WA SAYARI ANGANI

$
0
0
Dr. N. T. Jiwaji
ntjiwaji at yahoo dot com

Usiku wa Ijumaa ya tarehe 27 Julai 1016 siyo wa kukosa kuangangalia angani.  Usiku huo, Mwezi mpevu utafunikwa kabisa na kivuli cha Dunia na kusababisha kupatwa kamilifu na kuonekana wa rangi nyekundu.  Kupatwa kunatokea wakati Dunia na Mwezi zinakuwa katika mstari mnyoofu, Dunia ikiwa kati ya Jua na Mwezi.  Kupatwa huku kutukuwa wa kukolea sana na wa muda mrefu zaidi kwa karne hii.

Mwezi utafunikwa kwa muda mrefu zaidi kwa vile utakuwa na umbali mkubwa zaidi kutoka Duniani hivyo utapita ndani ya sehemu pana zaidi ya kivuli cha Dunia, na kuchukua muda mrefu zaidi kuvuka kivuli hicho. Safari hii Mwezi utabaki umepatwa kwa muda wa saa moja na dakika arobaini na tatu ambayo ni karibu masaa mawili hivi.  Kupatwa kurefu kiasi hiki ni nadra sana kwa vilie kawaida ni dakika mia tu, kwa wastani.  Kupatwa kurefu zaidi ya hii hakutatokea tena hadi baada ya miaka 105 ijayo siku ya tarehe 9 Juni, 2123.

Kupatwa kwa Mwezi kunaweza kuangaliwa kwa macho pekee bila madhara yoyote kwa vile tunafahamu kuwa mwanga wa Mwezi kawaida hautudhuru, na siku ya kupatwa mwanga unafifia hata zaidi baada ya kuzuiliwa na kivuli cha Dunia. Kupatwa kutaanza saa tatu na dakika ishirini na nne (3:24usiku) kwa kupatwa kiasi na kuanza kumegwa kingo ya mashariki ya Mwezi kwa kufunikwa na giza nyeusi ambayo itafunika Mwezi polepole hadi kufunika wote saa nne na nusu (4:30usiku), wakati ambapo Mwezi utakuwa umepatwa kamilifu na utageuka kuwa na rangi nyekundu. Hali hii ya Mwezi kuwa mwekundu wakati wa kupatwa kamilifu kutaendelea hadi saa sita na dakia kumi na tatu (6:13usiku) ambapo kupatwa kamilifu kutamalizika. Baada ya hapo kingo ya mshariku ya Mwezi itaanza kuchomoza kutoka katika kivuli na kuanza kuonesha uweupe utaongezeka polepole hadi saa saba na dakika kumi na tisa (7:19usiku) ambapo Mwezi utakuwa umeachwa na giza nyeusi, na ndio mwisho wa kukpatwa kiasi.
Pamoja na kuuona Mwezi ukiwa umepatwa kwa giza nyeusi, kuna sehemu ya kupatwa ambayo hatuwezi kutambua kwa urahisi.  Wakati huo Mwezi unakuwa umefunikwa na kivuli chepsi cha Dunia. Hali hii ya kupatwa kwepesi itaanza saa mbili na dakika kumi na nne (2:14usiku) hadi saa tatu na dakika ishirini na nne (3:24usiku) ambayo ni mwanzo wa kupatwa kiasi na kuanza kuonesha giza ukingoni mwa Mwezi.  Mwishoni tena kuna kupatwa kwepesi kuanzia mwisho wa kupatwa kisai saa saba na dakika kumi na tisa (07:19usiku) hadi saa nane na dakika ishirini na nane (08:28usiku) ambayo ndiyo mwisho kabisa wa tukio hili la kupatwa kwa Mwezi.
Ingawa Mwezi wote unamezwa ndani ya kivuli cha Dunia wakati wa  kupatwa kamilifu, Mwezi haupotei moja kwa moja kwa vile mwanga kidogo hupenya ndani ya kivuli cheusi baada ya kupindwa na angahewa ya Dunia.  Mwanga huu huwa ni wa rangi nyekundu na kusababisha Mwezi kuonekana kuwa wa rangi nyekundu muda wote ambao umepatwa kamilifu kuanzia saa 04:30usiku hadi saa 06:13usiku.  Mandhari hii ya uwekundu wa Mwezi si wa kukosa kuuona kwa sababu kukolea kiasi hiki cha kupatwa kamilifu hakutatokea kwa miaka saba ijayo hadi Septemba 7, 2025 

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

RC KIGOMA AYAONYA MASHIRIKA YANAYOSHAWISHI WAKIMBIZI WASIRUDI KWAO

$
0
0
Na Rhoda Ezekiel Kigoma

MKUU wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga ameyataka mashirika pamoja na vikundi vya wakimbizi vinavyo washawishi wakimbizi kuacha kujiandisha kurudi kwao kwa hiyari kuacha tabia hiyo.

Mkuu huyo aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na wakimbizi katika kambi ya Ndita wilayani Kibondo ambapo amesema mashirika na vikundi hivyo wanavijua endapo wataendelea na tabia hiyo watachukuliwa hatua za kisheria.

"Mashirika yanayo chochea wakimbizi na kuunga mkono upinzani nchini Burundi yataondolewa na hayata ruhusiwa kutoa huduma tena," amesema.Ameongeza kwa sasa hali ya amani na usalama kwa nchi ya Burundi ni salama na mali walizoziacha kwao bado zipo,hivyo wakimbizi warejee nyumbani kwao kwani hakuna utaratibu wa mkimbizi wa Burundi kwenda nchi ya tatu utaratibu huo ni kwa Wakongomani pekee.

AmesemakKambi ya wakimbizi sio mahali pa kudumu ni mahali pa kuhifadhi raia ambao nchini mwao kuna utishio wa kiusalama.Kwa sasa Burundi usalama upo hivyo wananchi wana wanatakiwa kurejea nchini kwao kwa hiyari na kusitokee vitisho wala ushawishi wowote."Utaratibu wa kuwapeleka raia wa Burundi nchi ya tatu ni ya haupo na Serikali ya Tanzania haitoi uraia kwa wakimbizi wa Burundi kama njia zote zimefungwa njia iliyopo ni moja tu mrejee kwenu kwa hiyari na UNHCR na IOM itahakikisha mnasafiri na mnafika kwenu mnaishi vizuri," amesema Brigedia Jenerali Maganga.

"Yapo mashirika shirika yana kwamisha mchakato huu tunawajua, niwaombe kitu kimoja kama mna maslahi yenu binafsi muyaweke pembeni hatuta wavumilia, ukiona shirika lako limeitwa ofisini kwangu jiandae kuondoka na tukifukuza hapo hakuna sehemu tena kstika Tanania hii utafanya kazi," alielezea Maganga.

Pamoja na hayo baadhi ya wakimbizi akiwemo Nkruliyabanzi Andrew amesema wao kama wakimbizi wanapenda kurejea nchini mwao lakini bado wanauoga kuwa wanaweza kurudi nchini mwao wakaanza kunynyaswa kwakuwa walikimbia.Waliomba Serikali ya Tanzania kuzungumza na Serikali ya Burundi kuingia kambini kuzungumza na wakimbizi na kuwahahikishia endapo watarudi wataishi salama wao wako tayari kurejea nchini mwao wakihakikushiwa hayo.

Uamuzi wa kuwarejesha wakimbizi walioingia nchini Tanzania 2015 ulifikiwa Mwishoni mwa mwaka 2017 ambapo pande tatu za shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR na nchi za Burundi na Tanzania kujiridhisha hali ya usalama Burundi imerejea na kuwaomba Wakimbizi warudi kwao ambapo mpaka sasa baadhi ya wakimbizi wamerejea nchini mwao kwa hiyari.
 Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga akizungumza na wakimbizi katika kambi ya Nduta wilayani Kibondo Mkoani Kigoma akiwataka kurejea Nchini kwao kwa hiyari, pembeni ni watumishi wa idara ya mambo ya ndani na Baadhi ya mashirika ya kuhudumia wakimbizI.
Baadhi ya Wananchi  wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga alipokuwa akizungumza na wakimbizi katika kambi ya Nduta wilayani Kibondo Mkoani Kigoma,  akiwataka kurejea Nchini kwao kwa hiyari.
 Burudani ya ngoma ilikuwepo 

NAIBU WAZIRI AWESO AAGIZA ALIYEKUWA MHANDISI MAJI LUSHOTO APEKEKE MIKATABA YA MRADI MAJI SHUME WIZARANI NDANI YA WIKI MOJA

$
0
0
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ameagiza aliyekuwa Mhandisi wa Maji wilaya ya Lushoto ambaye amehamishiwa Maswa mkoani Shinyanga afike wilayani humo kuchukua mikataba ya mradi wa maji Shume ndani ya wiki moja aupeleke wizarani.

Mradi huo wa ujenzi wa miundombinu ya maji Shume Manola hadi Madala unatakelezwa na mkandarasi MS Organes Contractors Co.Limited wa wilayani Lushoto ambapo unagharimu kiasi cha Bilioni 2,493,272,852.

Aweso alitoa agizo hilo jana wakati akihitimisha ziara yake wilayani Lushoto ambapo aligundua kuwepo kwa mkanganyika kwa ulipwaji wa fedha za mradi wa Maji shume ambazo zimepelekwa na serikali kwa kulipwa mkandarasi kwa kiwango tofauti kwenye mkataba mmoja.

Fedha ambazo alibaini kulipwa mkandarasi huyo kwa certificate ya kwanza mkandarasi alipaswa kulipwa kiasi cha bilioni 2.4,ya pili mkatandas alilipwa bilioni 2.4 na tatu inaonyesha alilipwa kiasi cha bilioni 2.9 jambo ambalo liliibua sintofahamu wakati wa kikao hicho baada ya kushindwa kupata maelezo halisi.

“Ndugu zangu haiwezekani mradi mmoja unakua gharama tatu tofauti ambazo zina tofautiana na ndio sababu nimelazimika kuagiza mikataba yote irudi wizara kwenda kuhakikiwa kwa lengo la kuweza kubaini gharama halisi ya mradi “Alisema.Naibu Waziri huyo alisema kutokana na kuwepo kwa dalili za ubadhirifu ndani ya mradi huo wizara haitaweza kutoa fedha katika mradi huo hadi pale wataalamu kutoka wizarani kuufanyia uchunguzi mradi huo .
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kulia akifuatilia kwa umakini mkataba wa Maji wa Shume kuangalia mapungufu yaliyopo jana kabla ya kupelekwa Wizarani katikati ni Katibu wa Naibu Waziri huyo Karim Lichela kushoto ni Mhandisi wa Mipango na Ujenzi wa Tang Uwasa Rashidi Selemani wa mwisho kushoto ni Mhandisi wa Maji Mkoa wa Tanga Ladislaus Modestus 
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso wa tatu kutoka kushoto akimsikiliza Katibu Tawala wa wilaya ya Lushoto wakati alipotembelea chanzo cha maji cha Ngulu kata ya Magamba wilayanu lushoto wakati wa ziara yake 
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akikagua tenki la Maji la Kata ya Kwamashai wilayani Lushoto wakati wa ziara yake.



Naibu Waziri kubariki Tamasha la nywele, ngozi za asili

$
0
0
NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, atakuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Kwanza la Siku ya Urembo wa Nywele na Ngozi za Asili litakalofanyika Jumamosi wiki hii viwanja vya Makumbusho ya Taifa, Posta, Dar es Salaam.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Eagle Business Consultants ya Dar es Salaam, Antu Mandoza, ilieleza kuwa tamasha hilo lina lengo la kuwahamasisha wanawake wa Kiafrika kuthamini urembo wao wa asili na kuachana na tabia ya kuutukuza utamaduni wa kimapokezi wa kubadilisha mwonekano wao.

Alisema tamasha hilo litakuwa likifanyika kila mwaka na kwamba Julai 28 itakuwa Siku ya Urembo wa Asili kwa kuanzia na Tanzania na baadaye Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.

“Onesho hili linalenga kutoa elimu kwa jamii nzima kuhusu madhara ya kiafya ya kutumia kemikali za aina mbalimbali za urembo wa nywele na uchubuaji ngozi, ili kurejesha ujasiri wa zamani wa mwanawake wa Afrika wa kujiamini na kupenda asili yake,” alisema Mandoza.Alisema alianza kampeni ya urembo wa asili kwa kupitia mitandao ya kijamii kuanzia Machi mwaka huu na amekuwa akitumia utambulisho au hashtag yanaturalhairsioushamba.

“Kampeni hii iliungwa mkono na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Ummy Mwalimu.“Mwitikio mzuri wa kampeni ya mtandaoni ndio uliofanya kuzaliwa kwa wazo la kuandaa onesho hili maalumu linalotarajiwa liwe mkombozi wa kizazi kijacho cha Afrika kwa baraka za serikali kupitia kwa Naibu Waziri, Shonza.
“Onesho hili litahudhuriwa na wasanii, wanamitindo na wataalamu mbalimbali akiwemo Dk. Andrew Foi ambaye ni daktari bingwa wa magonjwa ya ngozi atakayetoa mada kuelezea madhara ya kutumia kemikali katika urembo na kutoa siri za kuboresha nywele na ngozi kwa kutumia vitu vya asili,” alisema.

Kwa mujibu wa muandaaji huyo hakutakuwa na kiingilio chochote na wananchi wote wanakaribishwa na kuongeza kuwa kampuni yake pia inamiliki redio ya mtandaoni iitwayo radio7 www.radio7.co.tz ambayo huelimisha pamoja na kuiburudisha jamii.

Miss Dar zone 2018 kufanyika Agosti 3,Mshindi kupewa kiwanja

$
0
0
MREMBO atakayeibuka mshindi wa shindano la urembo la Miss Dar  Zone2018 anatarajiwa kupewa zawadi ya kiwanja imeelezwa.

Akizungumza na waandishi wa habari  mapema leo jijini Dar, Mratibu wa shindano hilo, Khalid Ngulume, alisema kuwa wamekuja kivingine msimu wa shindano la Miss Tanzania 2018 ,kutokana na ujio mpya wa shindano hilo na wao kama kanda wameamua kuweka zawadi ya tofauti.

"Zawadi hii ya kiwanja tutatoa kwa mshindi wa kwanza na wa pili, lakini kwa mshindi wa kwanza atapata zawadi nyingine tofauti," alisema Ngulume.Aidha, alisema kuwa kwa kufuata taratibu zilizopo, leo mchana wamepeleka  nyaraka za zawadi hizo kwa Barazaa la Sanaa Taifa (Basata) kama kanuni inavyotaka.

Aidha, alisema katika shindano hilo litakalofanyika Agosti 3 kwenye ukumbi wa Next Door Arena, wasanii Papi Kocha na Nandi wanatarajiwa kutoa burudani."Bado tupo kwenye mazungumzo na wasanii wengine kuona wanatoa burudani, lakini pia kwenye zawadi tutatoa zawadi kwa washiriki wote kama asante kwa kushiriki," alisema Ngulume.

Alisema warembo wote 27 wanaoshiriki shindano hilo Julai 29 wataingia kambini kujiandaa na shindano hilo.

Shindano hilo linadhaminiwa na  Manukato ya marcelina.

Washindi watatu wa shindano hilo watakata tiketi ya kushiriki shindano la taifa la Miss Tanzania.
Washiriki wa shindano la  urembo la Miss Dar  Zone 2018 ,wapatao 27 wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzungumza na Waandishi wa habari kuhusiana na kilele cha shindano hilo hapo Agosti 3, 2018 jijini Dar
Pichani kati ni  Mratibu wa shindano hilo, Khalid Ngulume, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar, kuhusu maandalizi ya shindano la Miss Dar zone 2018  linalotarajia kufanyika Agosti 3,katika ukumbi wa Next Door Arena,ambapo wasanii Papi Kocha na Nandi wanatarajiwa kutumbuiza,kulia ni Mmoja wa Wadhamini wa shindano hilo Matilda Marlon kupitia Manukato ya marcelina na kushoto ni Tahia Yusuph.
Walimbwenda hao wakiwa katika picha ya pamoja.

RAIS WA USWISI AONDOKA MARA BAADA YA MAPUMZIKO YAKE NCHINI

$
0
0




Rais wa Uswisi Mhe. Alain Berset akipkelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Jumatano usiku wakati akijiandaa kuondoka kurudi nyumbani baada ya kuhitimisha ziara yake binafsi ambapo alitembelea hifadhi za Taifa na Zanzibar kwa muda wa wiki mbili akiwa pamoja na familia yake.
Rais wa Uswisi Mhe. Alain Berset akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Jumatano usiku wakati akijiandaa kuondoka kurudi nyumbani baada ya kuhitimisha ziara yake binafsi ambapo alitembelea hifadhi za Taifa na Zanzibar kwa muda wa wiki mbili akiwa pamoja na familia yake. PICHA NA IKULU

Kurugenzi ya Tiba Shirikishi ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) yashika nafasi ya kwanza

$
0
0

Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Doroth Gwajima akimkabidhi tuzo ya kushika nafasi ya kwanza katika utendaji kazi bora wa kutoa huduma kwa wagonjwa kwa Kurugenzi ya Tiba Shirikishi Kaimu Mkurugenzi wa Idara hiyo ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo Delila Kimambo wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza washindi iliyofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Prof. Mohamed Janabi.
Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Doroth Gwajima akimkabidhi tuzo ya kushika nafasi ya kwanza katika kuwezesha utendaji kazi bora wa kutoa huduma kwa wagonjwa kwa Kurugenzi ya Uuguzi Kaimu Mkurugenzi wa Idara hiyo Robert Mallya wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza washindi iliyofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Prof. Mohamed Janabi.

Baadhi ya Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi (hayupo pichani) akielezea kuhusu kazi zilizofanywa na Taasisi hiyo kwa mwaka 2018 katika kikao cha wafanyakazi na viongozi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kilichofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo uliopo Jijini Dar es Salaam. Picha na Brighton James -JKCI

TPB YATOA MKOPO WA SHILINGI BILIONI 200 KWA WANAJESHI WASTAAFU

$
0
0
Na Woinde Shizza ,ARUSHA.

BENKI ya Posta ( TPB) imetoa mikopo yenye thamani ya Sh. bilioni 200 kwa wanajeshi wastaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania( JWTZ) nchini ili kujiendeleza kiuchumi na kuboresha maisha yao baada ya kustaafu .

Akizungumzia mjini Arusha Mkurugenzi wa Mikopo wa Benki hiyo Henry Jonathan amesema kuwa wametoa mikopo hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu tangu waanze kutoa mikopo.Kwani benki hiyo inaongoza kwa kutoa mikopo mingi kwa wastaafu ambayo inawasaidia kuinua hali ya maisha na kuanzisha miradi ya uzalishaji.

Amesema kwa Mkoa wa Arusha wenye jumla ya wastaafu 600 wametoa bilioni 13.7 za mikopo kwa wastaafu hao ambao ni wanufaika wakubwa wa fursa hiyo ya mikopo.“Kama unavyojua benki ya Posta inaongoza kwa kutoa mikopo kwa wastaafu ili kuboresha maisha yao na kuhamasisha uwekezaji wenye tija utakaoinua vipato vyao na jamii kwa ujumla,” amesema Mkurugenzi huyo

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanajeshi wastaafu unaofahamika kama MUWATA, Luteni Mstaafu Geofrey Wapalila amesema kuwa mikopo hiyo imewasaidia kufungua biashara na kuwa wajasiriamali hasa wanapoanza maisha uraiani hivyo kuendeleza maisha yao vizuri pia wameishukuru benki hiyo kwa kuwaamini.Pia ameiomba benki hiyo kutoa mikopo ya vifaa kwa wajasiriamali ili waweze kuzalisha kwani bado wana nguvu za kufanya shughuli za uzalishaji.

Naye mmoja wa Wastaafu hao Leonard Kilasi ameshauri wastaafu hao kukopa kwa busara na kulipa kwa wakati ili mikopo hiyo iwe na tija na kusaidia maisha yao.
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live




Latest Images