Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

NAIBU WAZIRI AWESO AMSIMAMISHA KAZI MHANDISI WA MAJI KOROGWE MJI

0
0

NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso amemsimamisha Mhandisi wa Maji Halmashauri ya Wilaya Korogwe Mji Joseph Mcharo kwa kutumia force accout kwenye mradi wa zaidi ya Milioni 700 bila ya kibali toka Wizara hiyo.

Agizo la kusimamishwa kwa Mhandisi huyo alilitoa jana wakati akikagua mradi miwili ya maji ya Mtonga ambao umetumia zaidi ya milioni 700 na msambiazi ambao umetumia zaidi ya milioni 600 ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya mkoa wa Tanga ambayo ilianza juzi wilayani Handeni.

Alisema mradi huo ulitakiwa kutumia kiasi cha shilingi Milioni 500 na wataalamu hao wakaubadilisha na kuufanya uwe wa milioni 700 ingawa bado unaendelea kusuasua jambo ambalo linaonyesha ubadhirifu wa fedha za Serikali .
 
Akiwa kwenye mradi wa Mtonga baada ya kumalizika kuukagua alitilia mashaka na ndipo alipoamuru mhandisi huyo kumpatia maelezo ya kina kuhusiana na mradi huo lakini pia hakuridhika na maelezo hayo na kuagiza kuwa atapeleka wataalamu kutoka wizara ili kuweza kuhakiki thamani ya fedha na ubora mrai huo.

“Kwa kweli mimi hapa sijaridhika na utekelezaji wa mradi huu unaonekana upo chini ya kiwango na ucheleweshwaji huku wananchi wakiendelea kupata tabu hivyo nitatuma wataalamu kutoka wizarani waje kuhakiki mradi huo”Alisema
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kulia akizungumza na Mhandisi wa Maji Korogwe Mji Joseph Mcharo kabla ya kumsimamisha kazi kulia ni Kaimu Mkuu wa wilaya ya Korogwe Godwin Gondwe
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kushoto akizungumza na watendaji wa Halmshauri ya Korogwe Mji wakati wa ziara yake 

NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kulia akimsikiliza kwa umakini Kaimu Mkuu wa wilaya ya Korogwe Godwin Gondwe wakati wa ziara yake.


Maoni ya Wananchi wa DODOMA Juu ya Gawio na Ujenzi wa Daraja la Selander

DC Ilala aagiza NEMC kuvunja nyumba Tabata

0
0
Na Heri Shaban 

MKUU wa Wilaya ya Ilala Dar es Salaam Sophia Mjema ameagiza Baraza la Hafidhi ya Mazingira (NEMC) kivunja nyumba zilizopo mpaka wa Ubungo na Wilaya ya Ilala mto Tenge. 

Tamko hilo lilitolewa Dar es Salaam jana wakati wa ziara yake wilayani Ilala iliyolenga kutatatua kero za wananchi wilayani humo .Akitoa agizo hilo kwa Mratibu wa Mazingira Kanda Mashariki( NEMC) Jaffar Chingaga Mjema alilitaka Baraza hilo kutekeleza agizo la uvunjaji nyumba zote zilizofanya uharibifu eneo la mto Tenge 

"Naagiza ofisini yako ya NEMC ije ivunje nyumba hizi ili upanuzi wa mto uweze kufanyika nyumba zote ziache mita 60 kwa ajili ya hifadhi mto wa bonde la mto Tenge "amesema Mjema. Amesema mara baada kuvunjwa kwa nyumba hizo atawasiliana na Mkuu wa wilaya ya Ubungo waweze kumchukulia hatua watendaji wa Manispaa yake wakiotoa kibali cha eneo la hifadhi ya bonde la mto huo .

Amesema ifikie wakati kila mtu afuate sheria na ajue kwamba Serikali ipo sio kila kitu kuvunja sheria hivyo katika hili sheria itafuatwa. Aidha amesema hivi karibuni katika Wilaya ya Ilala zoezi la urasilimishaji makazi linatarajia kuanza, hivyo washirikiane wote na kutenga maeno ya huduma za jamii ili yawepo. 

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Ardhi Manispaa ya Ilala Paulo Mbembelwa amesema mtu yoyote katika eneo lake anayo mamlaka ya kujenga lakini kabla kujenga lazima afute kibali Halmashauri ardhi mali ya Serikali. Mbembelwa amewataka watendaji na wenyeviti wa Serikali ya mtaa kushirikiana wote kulinda mipaka ya wananchi wao kwani ni moja ya jukumu la kazi yao. 

Naye mwananchi Fadhiri Msangi ameomba Serikali kuchukua hatua za haraka ili kupanua mto huo ili wasikumbwe tena na mafuriko na waliohusika wachukuliwe hatua. "Zamani katika Mtaa huu magari yalikuwa yanapita kwa sasa shida iliyopo tunashindwa kupita hata njia ya zarula wajawazito wakiumwa au yakitokea matukio ya uharifu kutokana na mto kuhamia Wilaya ya Ilala, kutoka wilaya ya Ubungo "alisema Msangi.
Mkuu wa wilaya ya Ilala SOPHIA MJEMA akiwa katika ziara yake ya kutatua kero za wananchi wa Kata ya TABATA Dar es Salam Leo kuhusiana na mpaka wa Wilaya ya Ilala na Ubungo,pichani eneo la Mto Tenge Kata ya TABATA (Picha na Heri Shaban)


SERIKALI KUANGALIA UWEZEKANO WA KUDHIBITI UINGIZWAJI WA CHUMVI KUTOKA NJE YA NCHI-NYONGO

0
0
NA MWAMVUA MWINYI, BAGAMOYO

NAIBU Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo, amesema serikali ina angalia namna ya kutumia chumvi inayozalishwa hapa nchini na kudhibiti uingizaji wa chumvi kutoka nje ya nchi. Pamoja na hilo ,serikali imeshaondoa kodi 11 ambazo zilikuwa kikwazo katika uzalishaji chumvi hivyo ni wakati muafaka wachimbaji wa mashamba ya chumvi wakanufaika na soko la ndani na nje ya nchi .

Akizungumza na uongozi wa machimbo ya chumvi ya kampuni ya uzalishaji chumvi ya H.J .Stanley Ltd,iliyopo kijiji cha Kitame ,Bagamoyo mkoani Pwani alisema, haiwezekani watanzania wakatumia zao hilo mtambuka nchi za jirani wakati wapo wazalishaji wengi nchini. Aliwapa changamoto wazalishaji hao ,kuhifadhi chumvi yao kwenye viwango bora ili kuendana na soko la ushindani.

"Eneo la Mashariki mwa nchi chumvi inayotumiwa inatoka nchi ya Kenya huku chumvi ya Uvinza Kigoma asilimia 30 inatumika eneo la Magharibi mwa Tanzania na asilimia 70 inauzwa nchi ya Congo" alifafanua Nyongo.

Nyongo aliwasisitiza ,kuhifadhi kwenye mifuko yenye uzito mbalimbali kuanzia robo kilo, kilo moja kwani kampuni hiyo inahifadhi mifuko ya kilo 50 ili kugusa matakwa ya kila mlaji. Naibu waziri huyo wa madini aliwaasa wachimbaji wakubwa ,kuwawezesha wachimbaji wadogo nao waweze kuingiza chumvi sokoni. Akizungumzia malalamiko aliyofikishiwa kuhusu kodi ambayo ni kero inayotozwa na TANAPA katika eneo hilo ,Nyongo alieleza amelichukua na atayafikisha katika mamlaka husika.

Awali mkurugenzi wa kampuni hiyo ,Richard Stanley alilalamikia kodi inayotozwa wakati wa kupita kwenye eneo la hifadhi ya Taifa (TANAPA)ambapo gari la tani 10 ,tani mbili zote zinaishia kulipa kodi hiyo.

Nae mkuu wa wilaya ya Bagamoyo,alhaj Majid Mwanga alielezea juu ya suala la mpaka ambapo baada ya kupanuliwa kijiji hicho kilionekana kiko ndani ya hifadhi ya Saadani hivyo taratibu zinaendelea na muda si mrefu litatatuliwa."Lengo la serikali ni kuhakikisha migogoro inakwisha ,ila ninaomba muendelee kuheshimu mipaka ya hifadhi zetu ili kuishi kwa amani na kufanya shughuli zenu bila vikwazo " alisema alhaj Mwanga.

Alhaj Mwanga ,alisema mgogoro wa mpaka ulikuwepo Saadan ,Matipwili,Gongo,Kitame na Java ambapo kwa sasa tatizo hilo limeisha kwa eneo la Java na Saadan .Kampuni hiyo imeajiri watu 27 na inazalisha tani kati ya 6,000 na 4,000 kwa mwaka na ilianza uzalishaji mwaka 1948.
NAIBU Waziri wa Madini ,Stanslaus Nyongo (wa pili kulia) ,akizungumza wakati alipokwenda kutembelea machimbo ya chumvi na kuzungumza na uongozi wa machimbo ya chumvi ya kampuni ya uzalishaji chumvi ya H.J .Stanley Ltd,kijiji cha Kitame Bagamoyo Mkoani Pwani. wa kwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Majid Mwanga.

ZIARA YA DC HAPI KINONDONI YAIBUA MADUDU YALIYOPO SERIKALI ZA MITAA

0
0

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Ally Hapi ameibua madudu yaliyokuwa katika serikali za mtaa na kuzipa ufumbuzi.

Hapi amebaini madudu hayo ikiwa ni siku ya pili toka aanze ziara yake ya kutembelea kata zote za wilaya ya Kinondoni kusikiliza na kutatua kero za wananchi. Akiwa katika Kata ya Kinondoni Hapi ametembelea mradi wa ujenzi wa mtaro na Barabara ya Best Bite,kuweka jiwe la Msingi wa Ofisi ya Mtaa.

Katika hatua nyingine Dc Hapi alimuagiza mtendaji wa Mtaa wa Kata hiyo nPeter Mayanja kuambatana na askari kwenda katika ofisi za kata kuchukua barua ambayo awali Mtendaji huyo alisema inamfanya ashindwe kuleta gari la kubeba takataka kwenye Mtaa wake ambalo tatizo hilo limekua kero kubwa kwa wananchi.

“Askari mmoja namuagiza mara moja aende na mtendaji huyu kuniletea hiyo barua ambayo anadai imetoka kwa mkurugenzi na kumzuia kuleta gari la kuzoa takataka, na azilete kabla sijaondoka hapa haiwezekani kero ndogo kama hiyo ya takataka mkuu wa wilaya aifanyie kazi wakati kuna watendaji wanaoweza kutatua kwa haraka," amesema Hapi.

Baada ya muda barua umfikia Dc Hapi ilionyesha haimzuii yeye kuleta gari la kubeba takataka hizo na mtendaji huyo kuonekana kama mbabaishaji.Hivyo DC Hapi kuamuru awaombe radhi wananchi wake kwa kutowaletea gari hilo kwa wakati.“Nawaomba radhi wananchi wangu mimi nimekosa na sitarudia tena,” amesema Peter Mayanja.Aidha DC Hapi ameweza kutembelea kikundi cha vijana wanaojihusisha na ufundi wa kutengeneza bidhaa za vyuma maarufu kama “welding” ambacho amewapa shilingi laki tano kama kuwapa nguvu zaidi vijana hao kuboresha kazi zao.

Pia DC Hapi amemuagiza Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Kinondoni kumkamata na kumuweka ndani saa 48 mmiliki wa kampuni ya Total West Solution kwa kile kinachodaiwa kukaidi agizo la DC Hapi.La kuwalipa kwa awamu tatu wafanyakazi wa kampuni hiyo stahiki zao baada ya kuachishwa kazi kwenye kampuni hiyo.

“OCD nahitaji umtafute na kumuweka ndani saa 48 mmiliki huyo wa kampuni na timu yangu ya wanasheria ifuatilie suala hilo la wananchi hawa kulipwa,” DC Hapi.Kero hiyo imetolewa mbele ya DC na mmoja wa wafanyakazi hao Rasuli Khamis Mkazi wa Kinondoni ambaye pia ni Kiongozi wa wafanyakazi hao waliofukuzwa kazi kwenye kampuni hiyo.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Ally Hapi akiwahutubia Wananchi wa Kinondoni wakati wa ziara yake hapo jana ya kutembelea kata zote za wilaya hiyo,kusikiliza na kutatua kero za Wananchi, Katika ziara hiyo Mh.Hapi alizisikiliza kero mbalimbali za Wananchi na kuzipatai ufumbuzi hapo hapo
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Ally Hapi akikagua miundo mbinu ya maji wakati wa ziara yake hapo jana ya kutembelea kata zote za wilaya hiyo,kusikiliza na kutatua kero za Wananchi, Katika ziara hiyo Mh.Hapi alizisikiliza kero mbalimbali za Wananchi na kuzipatai ufumbuzi hapo hapo.

TRC RELI TV: UJENZI WA RELI YA KISASA, MAANDALIZI YA UTANDIKA.

KUMBUKUMBU YA SIKU YA MASHUJAA, AMANI NA UZALENDO KWA TAIFA LETU

0
0

Na Emmanuel J. Shilatu
Leo ni Julai 25 siku ya Maadhimisho ya Mashujaa waliopambana kwa hali na mali kutetea nchi yetu ya Tanzania katika maeneo mbalimbali.

Hawa walimea uzalendo mkubwa, mwili na nafsi zao walikubali kuviweka rehani kwa ajili ya Tanzania. Bado tunawakumbuka na kuwaombea kheri kutokana na kujali na kudumisha misingi ya amani.

Misingi mizuri iliyojengwa na waasisi wa Taifa, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume , imesababisha Wananchi wa Tanzania kwa muda mrefu kuishi kwa amani na utulivu, huku wakifanya mambo yao kwa uhuru bila ya kuingiliwa na mtu yeyote wa ndani ama wa nje.
Tofauti na mataifa mengine, Watanzania wako huru zaidi kwenda kokote wanakotaka na hata kuishi ama kufanya kazi au biashara bila ya bughudha yeyote endapo kanuni, taratibu na sheria za nchi zitafuatwa ama kuzingatiwa vyema. Hali hiyo ni tofauti kabisa na nchi nyingine zikiwamo zile za jirani zetu kama Kenya, Rwanda, Burundi, Kongo na hata Uganda, nchi ambazo kwa kiasi kikubwa ukabila na chokochoko za kisiasa zimetamalaki kuanzia ngazi za kijiji hadi Taifa. Hapa kwetu tumeishi kama Ndugu bila ya u-rangi, udini, ukabila wala harakati za kiitikadi na kisiasa kutugawa.
Jambo la kushangaza ni kuwa misingi hiyo ya amani na utulivu iliyogharamikiwa na Waasisi wetu, hivi sasa ipo shakani na hatarini kutoweka kwani ilishaanza kuchezewa na chokochoko za aina mpya ya siasa (kwa maana ya ukosefu wa uvumilivu na uchu wa madaraka) iliyoanza kurindima katika siku za hivi karibuni.

Tukiwa tunawakumbuka Mashujaa hao inabidi nasi tujitathmini nafasi yetu kwa Taifa letu endapo inaedana na hali ya uzalendo. Hali ilivyo sasa kiwango cha uzalendo kimeshuka sana. Mtu yupo radhi kulalamika na kudai haki pasipo kutimiza wajibu wake kwa Taifa. Wameshajiuliza, wamelifanyia nini Taifa kabla ya kudai haki?

Vijana walio wengi wameweka pembeni uzalendo wa kulipenda Taifa lao kiasi cha kufikia hatua ya kukufuru kwa maneno ya kashfa dhidi ya Taifa lao. Hali hiyo ni tofauti kabisa na mataifa mengine ambayo hatuoni wakiyakashifu mataifa yao hadharani. Hii tabia ya kujivua nguo hadharani ni kwa faida ya nani?
Hapo hapo utakuta kuna baadhi ya Watanzania wanenda nchi za kimataifa na kuanza kuikashfu nchi yao kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vya kimataifa. Laiti kama Wazee wetu waliotutangulia wangekuwa na akili mbovu kama hizi, leo hii sidhani kama tungelikuta Taifa hili likiwa salama kama lilivyo. Umejiuliza haya ya kulichafua Taifa letu unataka uache urithi gani kwa vizazi vijavyo kwa Taifa letu?

Vijana wengi wa Leo, wananyooshewa vidole kwa kutothamini tunu ya kuwa Mtanzania. Je, U-Miongoni mwao? Kwako uzalendo ni nini? Kwako amani unailindaje?
Ndugu zangu, Wapo wanaosema kuwa amani ni sawa na yai mkononi, ukilivunja hautaweza kuliunganisha kamwe; wengine wanasema kuwa amani haina bei na ikipotea haina soko la kununua. Tuitunze amani yetu na kamwe tusiizoee wala kuichoka, tuige uzalendo waliokuwa nao Mashujaa wetu ambao walihakikisha amani ya nchi wanailinda vilivyo kwa machozi, jasho na damu.

*Shilatu E.J*
0767488622

MAKAMU WA RAIS AZINDUA SHAMBA LA MISITU LA SERIKALI WILAYANI ILEJE

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amezindua shamba la miti katika hifadhi ya Misitu Iyondo Mswima lililopo Katengele wilayani Ileje mkoani Songwe ikiwa ni siku ya nne ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Songwe.

Shamba hilo lililo chini ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ni moja kati ya mashamba mapya yakiwemo Biharamulo (Chato Geita), Buhigwe (Kigoma) na Mpepo (Mbinga, Ruvuma).

Akisoma taarifa ya Shamba hilo kwa Makamu wa Rais, Mkurugenzi wa Mipango –Wakala wa Misitu Tanzania Bw. Mohamed Kilongo amesema kuwa mpaka shamba la miti la Iyondo Mswima limeweza kutoa ajira kwa wananchi 400 katika msimu wa kupanda miti, pia shamba limetoa ajira zingine 200 wakati huu wa maandalizi ya bustani ya miti, hekta 201 zimepandwa miti kama sehemu ya upanuzi wa mashamba ya miti ya Serikali ambapo bustani yenye jumla ya miche 430,000 kwa ajili ya upandaji miti wa mwaka 2018/2019.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Katengele ambapo shamba la misitu la Serikali Iyondo Mswima limezinduliwa, Makamu wa Rais amewataka wananchi hao kutunza na kuyalinda mazingira kwa kupanda miti kwa wingi ambapo kila mwaka wananchi watapewa miche 50,000 na Wakala wa Huduma za Misitu wa Serikali. 

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya shamba la Misitu kutoka kwa Mkurugenzi wa Mipango-Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Bw. Mohamed Kilongo kwenye uzinduzi wa shamba la misitu la Serikali la Iyondo-Mswima wilayani Ileje ikiwa siku ya nne ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkano Songwe.  
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akikata utepe wakati wa kuzindua shamba la misitu la Serikali la Iyondo-Mswima wilayani Ileje ikiwa siku ya nne ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkano Songwe.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa kijiji cha Sange wilayani Ileje ikiwa siku ya nne ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkano Songwe.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa kijiji cha Katengele mara baada ya kuzindua shamba la misitu la Serikali la Iyondo-Mswima wilayani Ileje ikiwa siku ya nne ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkano Songwe. (Picha na Makamu wa Rais).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mbuge wa Jimbo la Ileje Mhe. Janeth Mbene mara baada ya kuwasili kwenye uzinduzi wa shamba la misitu la Serikali la Iyondo-Mswima wilayani Ileje ikiwa siku ya nne ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkano Songwe. 
Kikundi cha Ngoma cha Sange kikitumbuiza ngoma ya Ling'oma wakati wa kumkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye kijiji cha Sange wilayani Ileje ikiwa siku ya nne ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani Songwe. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) .




Article 10

0
0

JARIDA LA WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI – “ARDHI NI MTAJI” 

TOLEAO Na. 9 LA JARIDA LA WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imetoa Jarida lake la mwaka (2018) – ARDHI NI MTAJI (Toleo Na. 9). Jarida hili haliuzwi. Kuna nakala chache ambazo zitapatikana Wizarani – Dodoma na katika Kanda ya Dar es Salaam (Magogoni, Kivukoni) katika Kitengo cha Huduma kwa mteja.

Aidha Jarida hili litapatikana pia hivi karibuni kwenye Tovuti ya Wizara (www.lands.go.tz)

Mwananchi pata nakala yako upate kuhabarika kuhusu shughuli na Matukio mbalimbali ya Utekelezaji ya Wizara.

Na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

TARURA BAHI WAMWAGIWA SIFA

0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akifanya uhakiki wa vipimo vya upana wa Daraja la Chipanga kama vinaendana na BOQ.

Ujenzi wa daraja la Chipanga lililopo wilayani Bahi Mkoani Dodoma limeleta faraja kwa wananchi na viongozi wa wilaya hiyo huku wakimwagia sifa Wakala wa Barabara wa Mijini na Vijijini (TARURA) kwa usimamizi mzuri. 

Hali hiyo imejidhihirisha leo katika ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo alipokuwa akikagua miradi ya maendeleo wilayani Bahi. 

Akizungumzia kufurahishwa na ujenzi huo, Mbunge wa Jimbo la Bahi Omary Baduel amewapongeza TARURA kwa ujenzi wa daraja hilo kubwa na barabara zake kwa ubora wa hali ya juu ikilinganishwa na siku za nyuma kabla TARURA haijaanza. 

Daraja la Chipanga ni daraja kubwa lenye urefu wa mita 45 na limegharimu Sh. bilioni 2.18 na litakuwa mkombozi kwa wananchi wa Chipanga ambao walikuwa wanateseka kwa miaka yote. 

Katika ziara hiyo, Waziri Jafo amefanikiwa pia kutembelea ujenzi wa kituo cha Afya Bahi kinacho karabatiwa na serikali kwa Sh.Milioni 500 ambapo hadi sasa kazi ya ujenzi imekamilika na wananchi wameanza kupata huduma katika majengo hayo yaliyojengwa kisasa.
Daraja la Chipanga lililo katika hatua za mwisho za umaliziaji wilayani Bahi.
Zoezi la ukaguzi wa miradi likiendelea wilayani Bahi.
Mbunge wa jimbo la Bahi Omary Baduel akiishukuru serikali kwa kufanikisha miradi ya maendeleo wilayani Bahi.

WAZIRI KANGI LUGOLA ATEMBELEA KITUO CHA POLISI MURIET JIJINI ARUSHA

0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akiangalia pikipiki zilizotolewa na wadau wa kupinga vita uhalifu kwa Kituo cha Polisi Muriet, kilichopo Kata ya Muriet. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Ramadhani Ng’anzi.Waziri Lugola yupo jijini Arusha kwa ziara ya kikazi.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, akifafanua jambo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola(wapili kushoto), alipotembelea nyumba za askari polisi zinazoonekana pichani, katika eneo la Kata ya Muriet,jijini Arusha.Kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,Ramadhani Ng’anzi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na wananchi wa Kata ya Muriet, baada ya kutembelea Kituo cha Polisi na nyumba za askari polisi zilizopo eneo hilo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (kulia) na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Ramadhani Ng’anzi (kushoto) kutembelea Kituo cha Polisi cha Muriet (kinachoonekana pichani) na nyumba za askari polisi zilizopo katika eneo hilo wakati wa ziara yake jijini Arusha. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

MICHUZI TV: JWTZ YAADHIMISHA SIKU YA MASHUJAA KWA KUFANYA USAFI

WANAFUNZI WAIPONGEZA RITA UHAKIKI WA VYETI VYA KUZALIWA NA VIFO KWA NJIA YA MTANDAO

0
0
Na Leandra Gabriel, blogu ya jamii

SERIKALI ikiwa inaendelea uwekaji wa mifumo ya utoaji huduma kwa njia ya kielekroniki katika taasisi zake kwa upande wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) umepiga hatua kubwa katika hilo katika kuhakikisha huduma zitolewazo kwa wananchi zinakidhi haja zao.

Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam Ofisa Habari wa RITA Jafari Malema amesema mifumo hiyo ya kielekroniki ni ya Usajili wa Vizazi na vifo unaojulikana kama Birth Registration Fourth Generation (BRS4), Mfumo wa malipo ya ada ya huduma wa Serikali, Government elecronic Payment Gateway (GePG) na Mfumo wa Uhakiki wa vyeti vya kuzaliwa na vifo kwa wanafunzi wanaoomba mikopo ya elimu ya juu na watu wengine.

Malema ameeleza kuwa "Kwa kuwa mwaka jana tulipata changamoto ya idadi kubwa ya wanafunzi kufikika katika ofisi zetu na kusababisha msongamano ndiyo maana mwaka huu tumekuja na suluhisho la kudumu na tumefanikiwa kwa asilimia 98 ya uhakiki na kuwajibu wanafunzi," ameeleza.

Ameeleza hadi sasa wamepokea jumla ya maombi 95,561 kati ya hayo maombi 94,344 sawa na asilimia 99 yamefanyiwa kazi na kujibiwa na maombi 1217 sawa na asilimia 1.3 yanaendelea kufanyiwa kazi na kati ya maombi yote yaliyojibiwa ni maombi 92,304 sawa na asilimia 98 yamehakikiwa na hayana mapugufu yoyote na maombi 2040 sawa na asilimia 2 yameonekana kuwa na mapungufu na yanafanyiwa marekebisho.

Akieleza utofauti wa kiutendaji kwa sasa ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo huduma zilitolewa kwa mifumo ya kizamani ya karatasi, Malema ameeleza kuwa mfumo huo umekuwa rahisi zaidi katika utoaji wa huduma ukilinganisha na miaka iliyopita kwani huduma zote hufanyika kwa njia mtandao wanachotakiwa ni kutembelea tovuti ya http://uhakiki.rita.go.tz/uhakiki.

 Afisa Mawasiliano  wa (RITA) Jafari Malema akizungumza na Michuzi Blog kuhusu Wananchi kuwasilisha nyaraka halisi na kuacha kutumia nyaraka bandia ambazo hazitoki (RITA).Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii.
 Afisa Mawasiliano  (RITA) Jafari Malema kushoto na Afisa Masoko RITA, Edwin Mbekenga, wakionesha vyeti feki vya kuzaliwa.(picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
Maofisa wa (RITA) wakiendela na kazi ya uhakiki wa vyeti vya kuzaliwa 
Makao Makuu jijini Dar as Salaam.

MAHAKAMA YAKUBALI OMBI LA UPANDE WA JAMUHURI KESI YA VIGOGO CHADEMA IENDELEE

0
0
*Ni kutaka iendelee na kupanga kusoma usikilizwaji wa awali

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imekubaliana na ombi la upande wa Jamuhuri la kutaka kesi ya kufanya mkusanyiko usio halali na uchochezi inayowakabili viongozi tisa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ikiwemo Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe iendelee na kupanga kusoma usikilizwaji wa awali (PH)
Julai 31 mwaka 2018.

Pia Mahakama imeruhusu upande wa mashtaka kuanza usikilizwaji wa kesi hiyo mara moja baada ya PH kusomwa. Hayo yamefikiwa leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri baada ya kesi hiyo kuja kwa kutajwa kutokana na kusimama kupisha maamuzi ya mahakama kuu. 

Kutokana na maombi ya upande wa mashtaka yaliyokuwa yakiomba mahakama kuu kufanyia marejeo mwenendo wa kesi yao juu ya uamuzi wa mahakama ya Kisutu.Hata hivyo, Julai 20 mwaka 2018 Mahakama Kuu ilitoa uamuzi na kutupilia mbali maombi hayo kwa kuwa yalikuwa ni batili na kwamba yalikosa vigezo kisheria.

Mapema Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi aliomba Mahakama kulipangia shauri hilo tarehe ya kuwasomea washtakiwa  PH kwa kuwa uamuzi wa mahakama kuu ulishatoka na ombi la utetezi kutupiliwa mbali. "Mheshimiwa, shauri hili leo limekuja kwa kutajwa kwa sababu tulikuwa tunasubiri maamuzi ya Mahakama Kuu, lakini kwa kuwa maamuzi yameishatolewa.

"Tunaomba tarehe ya kuja kuwasomea washtakiwa PH na kuanza kusikilizwa siku hiyo hiyo mfululizo kwa tarehe zitakazopangwa na mahakama," ameeleza Nchimbi,Hata hivyo, Wakili wa utetezi Nashon Nkungu kwa niaba Peter Kibatala na Jeremiah Mtobesya wanaowatetea washtakiwa amedai kuwa baada ya uamuzi ule wa Mahakama Kuu, washtakiwa wamefaili kusudio la kukata rufaa mahakama ya Rufani ambayo ilipokelewa Julai 20 mwaka 2018
Baadhi ya viongozi  wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

MAKAMU WA RAIS APOKEWA KWA SHANGWE MKOANI MBEYA

0
0
 Wakazi wa Mbalizi wakiwa wamejitokeza kwa wingi kumpokea Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliposimama na kuwasalimia wakati akiwasili mkoani Mbeya tayari kwa ziara ya kuhamasisha shughuli za  maendeleo mkoani  humo ( Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza mbele ya Wakazi wa mji wa Mbalizi (hawapo pichani) waliojitokeza kumpokea wakati akiwasili mkoani Mbeya tayari kwa ziara ya kuhamasisha shughuli za  maendeleo mkoani Mbeya. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wakazi wa Mbalizi waliojitokeza kumpokea wakati akiwasili mkoani Mbeya tayari kwa ziara ya kuhamasisha shughuli za  maendeleo mkoani Mbeya. ( Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AELEZEA MIRADI YA MAENDELEO INAYOTEKELEZWA

0
0
MSEMAJI Mkuu wa Serikali Dk.Hassan Abbasi ameelezea kinachoendelea katika utekelezaji wa ahadi za Serikali huku akitumia nafasi hiyo kuwasisitiza wanahabari wote nchini kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa maadili ya kiwango cha juu.

Akizungumza na waandishi mbalimbali Mjini Dodoma Dk.Abbasi ameanza kwa kuwapongeza waandishi wa habari kwa ushirikiano ambao wamekuwa wamekuwa wakiutoa katika kusaidia mwaka wa fedha 2017/2018 katika kusaidia kuhabarisha umma masuala mbalimbali ya utekelezaji wa shughuli za Serikali.

Hata hivyo amesema bado wamendelea kushuhudia kuwepo kwa vitendo vya ukiukwaji wa maadili ya taaluma kwani pale Serikali itakapochokua hatua kusiwe na lawama.Pamoja na hayo akafafanua mambo mbalimbali nchini ambapo katika hali ya uchumi Dk.Abbasi amesema hadi Machi mwaka 2017 pato la Taifa lilikuwa kwa wastani wa asilimia 7.1 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 7.0 kwa mwaka 2016.

Amesema ukuaji huo ulitokana na na utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo na kuimarika kwa shughuli za kiuchimi."Kilimo kutoka asilimia 2.1 hadi asilimia 3.6, mawasiliano kutoka asilimia 13.0 hadi asilimia 14.7, madini kutoka asilimia 11.5 hadi asilimia 17.7 na ujenzi kutoka asilimia 13.0 hadi asilimia 14.1,"amesema Dk.Abbasi.

Pia amesema maji kutoka asilimia 4.3 hadi asilimia 16.7 , uchukuzi kutoka asilimia 11.8 hadi asilimia 16.6, elimu kutoka asilimia 8.1 hadi asilimia 8.5 na afya kutoka asilimia 5.2 hadi asilimia 5.9.Kwa taarifa zaidi kuhusu ambacho Dk.Abbasi amekielezea kwa watanzania kupitia waandishi wa habari na kufafanua kwa kina kupitia maelezo yake ambayo yamewekwa kama yalivyo

HAPA CHINI


Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza atembelea Benki Kuu, JWTZ NA TAKUKURU

0
0
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania,  Prof. Florens Luoga amelipongeza Jeshi la Magereza kwa kuendelea kutoa mchango wake katika kudumisha hali ya ulinzi na usalama nchini kupitia majukumu yake ya uhifadhi salama wa wafungwa na utoaji wa huduma za urekebishaji kwani Amani na Usalama ni msingi wa maendeleo katika nchi yoyote duniani.
Prof. Luoga amesema hayo wakati wa mazungumzo katika ziara ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Phaustine Kasike alipotembelea Benki Kuu ya Tanzania ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake  za kujitambulisha kwa viongozi mbalimbali wa kitaifa tangu ateulie kuwa Mkuu wa Jeshi hilo Julai13, 2018.
Aidha, Profesa Luoga amelishauri Jeshi la Magereza kuongeza ubunifu katika miradi ya uzalishaji mali kwa kufanya utafiti utakaoongeza ubora  wa bidhaa mbalimbali zinazozalishwa ili kuendana na mahitaji ya soko la ndani na hata nje ya nchi kwa kuwa taasisi kama magereza inaaminika.
“Jambo kubwa ni kubadili mtazamo na namna ya kufikiri kwa kusoma alama za nyakati na mabadiliko ya ulimwengu, kila kitu kinawezekana”. Amesisitiza Prof. Luoga.
Prof. Luoga ameahidi kuwa Benki Kuu ya Tanzania ipo tayari kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Magereza hasa katika ushauri wa kitaalam pale itakapohitajika kufanya hivyo ili kufikia malengo mahususi.
Ameongeza kuwa Taasisi anayoiongoza italipa ushirikiano Jeshi la Magereza kwa kuliunganisha na wadau mbalimbali watakaofanya kazi na Jeshi hilo kufanikisha majukumu yake pale fursa za kufanya hivyo zitakapojitokeza.
Wakati huo huo, Kamishna Jenerali Kasike amekutana na Uongozi wa juu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU)  ulioongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo Valentino Mlowola.
Mkurugenzi Mlowola amemhakikishia Kamishna Kasike ushirikiano wa dhati kwa kuwa vyombo hivyo viwili ni miongoni mwa taasisi  zinazosimamia utekelezaji wa sheria nchini hivyo ukaribu wao katika utendaji hauepukiki.
“Msingi wa amani katika nchi umewekezwa katika vyombo vyetu, kwahiyo ushirikiano ni muhimu sana”. Amesema Mlowola.
Kamishna Jenerali Kasike yuko katika ziara ya kujitambulisha kwa viongozi mbalimbali wa kitaifa ikiwa pia ni sehemu ya kuelezea majukumu ya msingi ya Jeshi la Magereza ambayo ni pamoja na uhifadhi salama wa wahalifu na utoaji wa huduma za urekebishaji kwa wafungwa ili wawe raia wema pindi wamalizapo vifungo vyao.
 Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akisalimiana na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Flolens Luoga alipotembelea Benki Kuu ya  Tanzania katika ziara yake ya kujitambulisha kwa Viongozi waandamizi Serikalini leo Julai 25, 2018, jijini Dar es Salaam.

 Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akiteta jambo na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Flolens Luoga(kulia) alipotembelea Benki Kuu ya Tanzania kwa lengo la kujitambulisha leo Julai 25, 2018.
 Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akiwa na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed alipomtembelea Ofsini kwake leo Julai 25, 2018 jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU nchini, Valentino Mlowola akimkabidhi nembo ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike kama inavyoonekana katika picha alipotembelea Taasisi hiyo leo Julai 25, 2018

BENKI YA KCB YADHAMIRIA KUWAINUA WAFANYABIASHARA WADOGO NA WAKATI (SME)

0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB  Tanzania Cosmas Kimario akizungumza katika warsha ya mafunzo ya kuwasaidia wafanyabiashara wadogo kukuza ujuzi na uendeshaji wa biashara pamoja na misingi ya ulipaji kodi yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
 Wafanyabiashara wakiwa wanafuatilia kongamano lililoandaliwa na Benki ya KCB lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam

Mkufunzi wa masuala ya Kodi Charles Adolf kutoka Adolf Tax Consul akizungumza na wafanyabiashara na  kuwahimiza wapate elimu ya kodi ili kusaidia ongezeko la pato la taifa katika Kongamano lililoandaliwa na Benki ya KCB Leo Jijini Dar es Salaam

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
BENKI ya KCB Tanzania imeendelea kuonyesha dhamira ya kuwaendeleza wafanya biashara wadogo na wa kati (SME) kwa kuendesha kongamano la pili kwa wafanya biashara zaidi ya 200 jijini Dar es Salaam.

Benki hiyo imeandaa Biashara Club ambayo ni mpango maalum  unaowasaidia wafanya biashara kukuza ujuzi katika maswala ya fedha, uendeshaji wa biashara na kanuni na misingi ya kulipa kodi pamoja na kuwapa fursa za kukuza mahusiano yao na wafanya biashara wengine ndani na nje ya nchi.

Semina hiyo iliyofanyika katika Hotel ya Serena ilikusanya wafanyabiashara na wajasiriamali kutoka nyanja tofauti, wakiwa na changamoto mbali mbali za kibiashara zikiwemo rasilimali, ushindani, uelewa finyu katika maswala ya kodi na nyinginezo. Nia kubwa na KCB Bank ni kutaka kuwafundisha wafanyabiashara njia bora ya kukabiliana na changamoto zinazowakumba.

Akiongea katika warsha hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Bank Bw. Cosmas Kimario, alisema “Hakuna biashara inayofanikiwa bila changamoto. Hizi zipo ili zikupe chachu, uzikabili, usonge mbele. Wanaokimbia changamoto huanguka kibiashara ama huendesha biashara zisizo endelevu.”

Katika ushauri wake alisisitiza kwamba namna pekee ya kuzikabili changamoto hizo ni “ubunifu, kujali muda, kwenda kwa wakati, kufahamu kanuni muhimu za nchi na za kisheria katika biashara.”

Mkufunzi wa masuala ya Kodi Charles Adolf kutoka Adolf Tax Consul  aliwahimiza wafanyabiashara hao kuhusu muhimu wa kuelewa mfumo wa kodi hapa nchini na ni kwa namna gani unagusa biashara biashara zao. “Hamna taifa linaloendelea bila kodi lakini pia ili kushiriki kikamilifu katika kujenga uchumi imara ni lazima tulipe kodi.”

Mbali na kufaidika na ujuzi wa mambo kupitia semina na safai mbalimbali zinazoandaliwa na kitengo cha “Biashara Club”, wanachama pia watafaidika kwa kujenga uhusiano wa kibiashara baina yao ambao utapelekea wao kuongeza si ujuzi wa kibiashara tu, bali pia kupanua wigo wa biashara zao. KCB Bank inatambua umuhimu wa wafanya biashara wadogo na wakati katika kukuza uchumi wa nchi lakini pia inatambua kwamba uchumi hautakuwa kama wafanya biashara hao hawatakuwa na nyenzo sahihi za kibiashara.

Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wametakiwa kutobweteka kutokana na mafanikio mazuri ya kutoa huduma bora za matibabu ya moyo wanayoyapata

0
0
Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wametakiwa kutobweteka kutokana na mafanikio mazuri ya kutoa huduma bora za matibabu ya moyo wanayoyapata bali waendelee kujitoa katika kuokoa maisha ya wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo. 

Rai hiyo imetolewa hivi karibuni na Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Doroth Gwajima alipokuwa akizungumza na wafanyakazi katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo uliopo Jijini Dar es Salaam.

Dkt. Gwajima alisema hivi sasa Taasisi hiyo imekuwa tegemeo kubwa kwa wagonjwa wa moyo kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati hivyo basi ufanyaji kazi kwa ufanisi utasaidia wananchi wengi kuendelea kupata huduma za matibabu ya moyo hapa nchini.

“Jamii ya Tanzania inatambua kazi kubwa na nzuri inayofanywa na JKCI, nawasihi wafanyakazi msikubali changamoto yoyote ile inayowakabili ikaitoa Taasisi hii katika mstari wa mafanikio mliyoyapata”.
Habari zaidi SOMA HAPA
Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Doroth Gwajima akimkabidhi tuzo ya utendaji kazi bora wa Idara ya Magonjwa ya Moyo ambayo ni moja ya Kurugenzi tano za Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Kaimu Mkurugenzi wa Idara hiyo ambaye pia ni daktari bingwa wa Magonjwa ya Moyo Peter Kisenge. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimpongeza Mkuu wa Idara ya Rasilimali Watu Ghati Chacha kwa ajili ya utendaji kazi mzuri wa Kurugenzi ya Utawala na Fedha walioufanya kwa kipindi cha miezi mitatu wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza washindi iliyofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo. Kulia ni Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Doroth Gwajima.
Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt. Doroth Gwajima akimkabidhi Tuzo ya utendaji kazi bora wa Kitengo cha manunuzi David Kakoti wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) katika hafla fupi ya kuzipongeza Idara na Vitengo vilivyofanya kazi vizuri kwa kipindi cha miezi mitatu. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi.
Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akitoa mada wakati wa kikao na wafanyakazi wa Taasisi hiyo pamoja na viongozi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kilichofanyika kivi karibuni katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo uliopo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Tiba Tanzania Dkt. Doroth Gwajima akimkabidhi Tuzo daktari bingwa wa upasuaji wa Moyo Dkt. Evarist Nyawawa kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kutokana utendaji kazi bora wa kitengo cha upasuaji wa Moyo wakati wa kikao na wafanyakazi wa Taasisi hiyo pamoja na wawakilishi kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto jana katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.Picha na Brighton James -JKCI.

GOFU LUGALO YATAMBA KUIBUKA NA USHINDI MASHINDANO YA WAZI YA MUFINDI (MUFINDI OPEN)

0
0
Na Luteni Selemani Semunyu.

Klabu ya Gofu ya jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania ya Lugalo imetamba kuendeleza wimbi la ushindi katika Mchezo huo kupitia timu yake yenye wachezaji 30 inayotarajia kusafiri kuelekea Mufindi mkoani Iringa kushiriki mashindano ya wazi ya Mufindi yanayotarajiwa kufanyika Julai 27 hadi Julai 29 katika Viwanja vya Klabu hiyo 

Akizungumza na Waandishi wa habari mwenyekiti wa Klabu ya Gofu ya Lugalo Brigedia Jenerali Michael Luwongo Mstaafu alisema Timu inatarjiwa kuondoka Julai 26 kuelekea Mufindi ambapo mbali na wachezaji wa Ridhaa wapo wachezaji wa kulipwa Sita ambao nao wamejipanga kufanya vyema..

“ Tunawachezaji wengi nyota na chipukizi wengine wapo kwenye majukumu ya kazi lakini wengine wako katika kuwakilisha nchi katika mashindano ya Kimataifa kwa kuwa tuna vipaji vya kutosha tutapeleka Timu nzuri na kupata Ushindi” Alisema Brigedia Jenerali Mstaafu Luwongo.

Brigedia Jenerali Mstaafu Luwongo aliwataja Wachezaji wa Kulipwa wa Klabu ya Lugalo watakaowakilisha katika Mashindano hayo kuwa ni David Helela, Abdalah Yusuph, Geofrey Leverian na Brison Nyenza , Iddi Mzaki aliyechukua nafasi ya tatu katika mashindano ya wazi ya Lugalo na Athumani Chiundu.
 Mshindi wa kwanza wanawake kutoka klabu ya Gofu ya Lugalo Habiba Likuli akipiga mpira wakati wa mashindano ya wazi ya Lugalo Jijini Dar es Salaam anayemuangalia ni Amanda Mlula wa klabu hiyo( Picha na Luteni Selemani Semunyu)
Baadhi ya Wachezaji wa klbu ya Golf ya Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania ya Lugalo wakiwa katika mazaoezi katika uwanja wa Klabu hiyo Jijini Dar es Salaam( Picha na Luteni Selemani Semunyu).

Viewing all 109602 articles
Browse latest View live




Latest Images