Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 239 | 240 | (Page 241) | 242 | 243 | .... | 3272 | newer

  0 0


  0 0

  Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando akiongea na moja ya washindi wakati Airtel ilipochezesha droo ya saba ya washindi wa shilingi milioni moja kila siku wa promosheni ya Airtel yatosha ambapo mpaka sasa zaidi ya shilingi million 44 zimeshatolewa. Akishuhudia ni Msimamizi wa bodi ya michezo ya Bahati nasibu.
  Washindi wa siku wa shilingi milioni moja wa promosheni ya Airtel yatosha bwana Thomasi Joackim Chali na Abdallah Omari Muhomba kwa pamoja wakionyesha furaha mara baada ya kukabithiwa zawadi za pesa taslimu baada ya kuibuka washindi wa siku wa promosheni ya Airtel yatosha.

  Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel imetangaza washindi wake saba wa wiki ya saba ya Airtel Yatosha promosheni na kukabidhi zawadi za washindi wa wiki ya sita wa promosheni ya Airtel Yatosha.

  Airtel imechezesha droo ya wiki ya saba ya promosheni ya Airtel yatosha Jana katika ofisi za makao makuu ya Airtel morocco jijini Dar es saalam ambapo wateja saba wameibuka washindi wa kitita cha shilingi million 1 kila mmoja.

  Washindi hao ni pamoja na Theresia Martine Komba wa Morogoro -Mkulima, John Kimoro wa kondo Dodoma -Mwalimu, Yohanna Masunga Zengo wa Maswa Shinyanga -Mkulima, Isabellah Joseph wa Chamwino Dodoma -Mwalimu, Nassor Mohammed Nassor wa Kariakoo DSM -Mfanyabiashara, Modest Laurian Mussa wa Bukoba Kagera -Mfanyabiashara na Masanja Mwanamenda wa Nkyala Singida -Mfanyabiashara.

  Wakati huo huo Airtel imeendelea kuwazawadia wateja wake kupitia promosheni ya Airtel Yatosha ambapo washindi wa wiki ya sita nao walikabidhiwa zawadi zao ambapo kila mmoja aliondoka na shillingi milioni moja.

  Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo katika ofisi za makao makuu ya Airtel bwana Abdallah Omari Muhomba mmoja wa washindi wa million 1 alisema, "nashindwa jinsi ya kuongea lakini nawashukuru sana Airtel kwa kuweza kunizawadia shilingi milioni 1 ambazo kwangu nikama ndoto.

  Nategemea kutumia pesa hizi kujiendeleza kiuchumi na maaendeleo ya familia yangu. Binafsi nachukua fursa hii kuwaasa watanzania kushiriki katika promosheni hizi za Airtel na kwa hakika wataamka washindi kama mimi hivi leo".

  Kwa upande wake bwana Thomas Joachim Chali ambaye pia ni Mshindi wa wiki ya sita alisema, "anawashukuru Airtel kwa kuanzisha promosheni yaAirtel Yatosha , na kuahidi kuzitumia pesa zake kuendeleza na kupanua biashara kwa kuwa hiyo ndio shughuli kubwa anayoifanya".

  Akiongea wakati wa makabidhiano hayo kwa washindi hao Meneja uhusiano wa Airtel bwana Jackson Mmbando alisema, "leo tunao washindi saba waliojishindia shilingi milioni 1 kila moja katika droo ya wiki. Tumeendelea kushuhudia watanzania na wateja wetu wakiibuka mamilionea kila siku na kila mwezi kupitia promosheni hii ya Airtel Yatosha.

  Tunaahidi kuendelea kuwazawadia wateja wetu huku tukiboresha huduma zetu , na kuwapata wateja wetu huduma bora zenye gharama nafuu kupitia huduma yetu poa ya Airtel Yatosha inayomuwezesha mteja kuwasiliana na mitandao mengine ya simu za mkononi kwa bei poa na kupata vifurushi vya maongezi bila kulipia gharama ya ziada". Aliongeza Mmbando.

  Promosheni ya Airtel Yatosha bado inaendelea na wateja wetu wa Airtel Yatosha bado wananafasi ya kuendelea kujishindia pesa taslim na Nyumba mbili za kifahari zilizopo Kigamboni bado kushindaniwa.

  Droo itakayomchagua mshindi wa nyumba kwa mwezi huu inatarajiwa kuchezeshwa tarehe 5/9/2013 saa tano asubuhi. hii itachagua mshindi mmoja kati ya wateja wote waliotumia huduma ya Airtel yatosha kwa mwezi huu.

  Ili mteja wa Airtel aweze kushiriki anatakiwa kujiunga na vifurushi vya Airtel Yatosha kwa kupiga *149*99# na kujiunga na vivurushi vya Airtel Yatosha. Kila unapojiunga na kifurushi unaingia moja kwa moja kwenye droo ya kushinda.

  0 0

  Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) linatarajia kufanya mkutano maalum wa kupanga ratiba ya mashindano ya SHIMIWI ya mwaka huu utakaofanyika kesho kutwa jumamosi ya agosti 31 majira ya saa 4 asubuhi katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora zilizopo mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam.

  Kaimu Katibu Mkuu wa SHIMIWI Bw.Moshi Makuka alisema mkutano huo utawahusisha wenyeviti na makatibu wa vilabu vya michezo ya SHIMIWI kutoka katika Wizara,Idara Zinazojitegemea,Sekretarieti za Mikoa na Wakala za Serikali.

  “Wenyeviti na Makatibu wa Vilabu vinavyoshiriki michezo ya SHIMIWI mnatakiwa kuhudhuria mkutano huo bila kukosa ili kufanikisha mashindano ya SHIMIWI yatakayoanza hivi karibuni” alisema Bw.Makuka.

  Aidha,Bw.Makuka aliwataka wenyeviti na makatibu wa vilabu vyote kuja na viambatanisho muhimu kama vile barua za kuthibitisha kushiriki,fomu za usajili wa wachezaji watakaoshiriki na vikombe (kwa vilabu vilivyopata vikombe katika mashindano ya mwaka jana yaliyofanyika mjini Morogoro).

  Mashindano ya michezo ya SHIMIWI kwa mwaka huu yamepangwa kufanyika mjini Dodoma kuanzia Septemba 21 hadi oktoba 5 ambapo yatahusisha michezo ya mpira wa miguu,netiboli,kuvuta kamba,riadha,baiskeli,karata,bao na drafti.
  Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) Bw.Moshi Makuka akisisitiza umuhimu wa vilabu kuzingatia sheria,kanuni na taratibu za mashindani ya SHIMIWI leo ofisini kwake.

  0 0

  Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba (katikati) akiongea na Wawakilishi wa Wakuu wa Mikoa na Wilaya waliofika katika ofisi za Tume leo (Jumatano, Agosti 38, 2013) kuwasilisha maoni ya Baraza lao la Katiba kuhusu Katiba Mpya. Viongozi hao ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw. Abbas Kandoro (kushoto kwa Jaji Warioba), Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Leonidas Gama (kulia kwa Mwenyekiti) na Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Bw. Crispin Meela. Kushoto ni Katibu wa Tume Bw. Assaa Rashid.
  Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba (kulia) akiongea na Wawakilishi wa Wakuu wa Mikoa na Wilaya waliofika katika ofisi za Tume leo (Jumatano, Agosti 38, 2013) kuwasilisha maoni ya Baraza lao la Katiba kuhusu Katiba Mpya. Viongozi hao ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw. Abbas Kandoro (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Leonidas Gama (kulia kwa Mwenyekiti. Mwingine ni Katibu wa Tume Bw. Assaa Rashid.
  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw. Abbas Kandoro akimkabidhi Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba (katikati) maoni ya Baraza la Katiba la Wakuu wa Mikoa na Wilaya katika ofisi za Tume leo (Jumatano, Agosti 38, 2013). Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Leonidas Gama.
  Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Assaa Rashid (katikati) akiongea na Wawakilishi wa Wakuu wa Mikoa na Wilaya waliofika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo (Jumatano, Agosti 38, 2013) kuwasilisha maoni ya Baraza lao la katiba kuhusu Katiba Mpya. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw. Abbas Kandoro na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Bw. Crispin Meela. Picha na Tume ya Katiba.

  0 0

   Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania wakiwa katika kikao cha kwanza tangu bodi hiyo kuteuliwa ambapo kilijadili mambo mbalimbali yakiwemo ya uwekezaji nchini. (Picha na Francis Dande) 

  Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TPSF, Salum Shamte akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari. 
   Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye akizungumza. 
  Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Dk. Reginald Mengi akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, juu ya maazimio ya bodi hiyo kuhusu sera ya uwekezaji nchini. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa TPSF, Salum Shamte. 

  Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Dk. Reginald Mengi akifafanua jambo wakati wa kikao cha kwanza tangu bodi hiyo iteuliwe. Kushoto ni mjumbe wa Bodi hiyo, Arnold Kileo na Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye akizungumza.
  ---------------------------------------------

  SERIKALI imetakiwa kusitisha mara moja mpango wake wa ugawaji wa leseni za vitalu vya gesi hadi hapo itakapopatikana sera ya gesi ili kuwapa fursa watanzania kumiliki vitalu hivyo.


  Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Taasisi ya Uwekezaji nchini (TPSF), Dk. Reginald Mengi, alisema kuwa endapo ugawaji wa vitalu hivyo utafanyika Oktoba mwaka huu kama ilivyopangwa, watanzania hawatakuwa na uwezo wa kumiliki rasilimali hiyo.


  Dk. Mengi ambaye alikuwa akizungumzia maazimio ya bodi hiyo iliyokutana mara ya kwanza jana tangu ilipoteuliwa hivi karibuni, alisema wakati Serikali iko mbioni kufanya mnada wa vitalu hivyo saba vya gesi, hakuna kipengere kinachomwezesha mtanzania kumiliki gesi hiyo.


  Akizungumzia sera za uwekezaji kwa ujumla, Dk. Mengi alisema taasisi hiyo inaitaka Serikali kuingiza kwenye Katiba mpya inayokuja kipengere kinachowapa haki watanzania kuwa na ubia na wawekezaji wa nje badala ya kuwaachia wageni hao kumiliki rasilimali za hapa nchini kwa asilimia 100.


  Alisema hali hiyo itawawezesha watanzania kuwa na hali ya kumiliki na kulinda rasilimali zao ambazo kwa sasa zinawanufaisha zaidi wageni kuliko watanzania wenyewe.

  “Sisi tunaitaka Serikali ihakikishe kuwa shughuli yoyote ya uwekezaji wa kiuchimi, iwe na mtanzania ndani yake na watanzania hawa, wasishindwanishwe na wawekezaji wakubwa wan je,” alisema Dk. Mengi.


  Naye Makamu mwenyekiti Salum Shamte, alisema kuwa Serikali inapaswa kuhakikisha sheria ya manunuzi za umma inawanufaisha zaidi watanzania kuliko wawekezaji.


  Alisema hivi sasa kiasi kikubwa cha fedha za Bajeti ya kila mwaka, zinatumika katika kufanya manunuzi ya bidhaa na huduma na kazi hiyo imekuwa ikifanywa na wawekezaji badala ya kuwawezesha watanzania.  Akifafanua kuhusu hoja hiyo, Dk. Mengi alisema kuwa asilimia 80 ya Bajeti ya mwaka huu wa fedha, itatumika kwa ajili ya manunuzi ya umma hivyo ni vyema kazi hiyo ikafanywa na watanzania.


  “Ukiangalia bajeti ya mwaka huu, karibu asilimia 80, sawa na sh trilioni 14 zitatumika kwa ajili ya manunuzi ya bidhaa na huduma za umma. Fedha hizi zikiingia kwa watanzania, zitachangia sana kukuza uchumi wa taifa,” alisema Dk. Mengi.

  0 0

   Spika wa Bunge la Afrika Mashariki(EALA)akimsikiliza Mbunge wa bunge hilo kutoka Tanzania, Mhe Shyrose Bhanji wakati wakielekea bungeni.
   Chemba ya Bunge la Afrika Mashariki inavyoonekana wakati kikao kikiendelea 
   Wabunge wa Tanzania kwenye bunge la Afrika Mashariki(EALA)wakitoka ndani ya ukumbi wa bunge hilo leo kupinga wabunge wenzao wanaoshinikiza hoja zao kwa kutoka kwenye vikao vya bunge. Kutoka kushoto ni Mh.Twaha Taslima,Mh.Shyrose Bhanji,Mh.Abdullah Mwinyi na Mhe Nderakindo Kessy
   Mbunge wa Tanzania kwenye bunge la Afrika Mashariki(EALA) Mhe Abdullah Mwinyi akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari baada ya kutoka nje na kikao kuhairishwa hadi kesho
  Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe Ali Mzee (kulia)akizungumza na wabunge wa Tanzania kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki(EALA)kutoka kushoto ni Mh.Shyrose Bhanji,Mh.Nderakindo Kessy,Mh.Twaha Taslima na Mh. Abdullah Mwinyi.
  Kwa habari kamili tembelea Mwananchi: BOFYA HAPA

  0 0

  Nafurahi kuona maoni mbali mbali ya wadau tofauti. Kila mmoja amezungumza kwa kuzingatia maslahi ya Taifa letu. Kikubwa naomba tutofautishe uraia wa nchi mbili kwa Mtanzania mzaliwa(Maganga) VS mgeni kupata uraia wetu(Rajper).
  Maganga yeye hana shida kabisa, kwasababu uraia wake wa kuzaliwa atabaki nao, kazi kwake kuupata wa nchi nyingine kwa kufuata masharti ya hiyo nchi. Kama ni USA, basi afuate utaratibu wake lakini asipoteze uraia wa Tanzania. 
  Nadhaani wachangia mada hakuna anayemkataa Maganga kubaki na uraia wake. Sasa twende kwa Rajper, yeye anautaka uraia wetu, lazima afuate masharti yetu (magumu) kabla ya kuuchukua. Mfano kuna kitu kinaitwa birth rights ambavyo hata huku ughaibuni tunakumbana navyo. 
  Kwa nchi yetu, kutokana na umaskini wetu, lazima tuwe makini kabisa. Birth rights aliyonayo Maganga asipewe Rajper. Maganga aruhusiwe kugombea nafasi za uongozi kisiasa, Rajper hapana. Mtoto wa Maganga apewe nafasi ya kuchagua once anapotimiza 20 years kati ya birth rights za TZ au za huko alikozaliwa. Bado anaruhusiwa kuwa na uraia wa nchi mbili,lakini birth right achague. 
  Rajper akipata watoto ndani ya ardhi ya Tanzania,na mmoja wa mzazi ni Mtanzania, basi huyo ni mwenzetu, apewe birth rights.
  Vitu kama investments, lazima brith right ifanye kazi, mwekezaji lazima atoe % kwa mzawa ili kulinda raslimali zetu. Kama ni madini,basi Rajper asiruhusiwe 100% kuinvest mwenyewe,lazima kuwe na mzalendo. Akijenga nyumba, basi anakodishiwa ardhi, lakini Maganga akijenga nyumba ni yake na ardhi ni yake.
  List ni ndefu,lakini lazima tutofautishe uraia wetu na Birth rights" ambazo laziwe zitajwe kwenye katiba.
  Mungu ibariki TZ, Mungu ibariki Africa

  0 0

  Government of Japan, through the scheme of Grant Assistance for Grassroots Human Security Projects (GGHSP), has agreed to extend a grant aid of US$ 192,700 (approximately 120 million Tshs) for the Construction of a Two-storey Classroom Block at Enyoito Secondary School in Arusha District, Arusha Region.
  The contract for the project has been signed by H.E. Mr. Masaki Okada, Ambassador of Japan and the representative of the recipient secondary school. 
  The Government of Japan has been extending support to local communities in various sectors including health, education and water supply under the GGHSP scheme since 1991. 
  The Signing Ceremony was attended by H.E. Mr. Masaki Okada, Ambassador of Japan to the United Republic of Tanzania, Honourable Mr. Goodluck J. Ole-Medeye, Deputy Minister of Land, Housing and Human Settlements Development, Honourable Mr. Godbless Lema, the member of parliament from Arusha, Honourable Mr. Joshuwa Nasari, the member of parliament from Meru and representatives of respective organisation. 
  On that day, the performance of Japanese traditional drums was held as a part of the friendship activities from Yamagata-Tanzania Friendship Association, which was involved in the formation of this project.
   H.E. Masaki Okada, the Ambassador of Japan, and Hon. Goodluck J. Ole-Medeye, Deputy Minister of Land, Housing and Human Settlements Development  attend the signing ceremony of Japanese grants at Enyoito Secondary School in Arusha District, Arusha Region. From left to right: Mr. Mwatandu Jilanga, District Education Officer,Mr. Sifael Ole-Ngushwai Mollel, Regional Cultural Officer, Hon. Nyerembe D. Munasabi, District Councilor, H.E. Masaki Okada, the Ambassador of Japan, Hon. Goodluck J. Ole-Medeye, Deputy Minister of Land, Housing and Human Settlements Development and District Council Vice Chairperson, Hon. Anna Msuya
   Signing the contract, from left to right: Mr. Gibson Meiseyeki, Oltroto Ward Councilor , Mr. Saleh Mputa Mweri, the Ag. headmaster of Enyoito Secondary School, H.E. Masaki Okada, the Ambassador of Japan and Hon. Goodluck J. Ole-Medeye, Deputy Minister of Land, Housing and Human Settlements Development
   Mr. Saleh Mputa Mweri, the Ag. headmaster of Enyoito Secondary School and H.E. Masaki Okada, the Ambassador of Japan, exchange documents after signing them
   Ambassador Okada giving a speech. On his left are Mr. Sifael Ole-Ngushwai Mollel, Regional Cultural Officer and Hon. Nyerembe D. Munasabi, District Councilor. On his right is Hon. Goodluck J. Ole-Medeye, Deputy Minister of Land, Housing and Human Settlements Development
  A performance  by a Japanese traditional drum group spice up the occasion.

  0 0


  The opening ceremony will be in JB Belmont Hotel, Dar es salaam,
  starting at 9:00 a.m.

  The University Students’ Debate will be officially opened by high level East African Community and government representatives:
  ·         Hon. Secretary General East African Community Secretariat, Ambassador Dr. Richard Sezibera,
  ·         Hon. Minister for Education and Vocational Training The United Republic of Tanzania, Hon. Dr. Shukuru Jumanne Kawambwa,
  ·         Hon. Deputy Secretary General Political Federation, Mr. Charles Kinyanjui Njoroge,
  ·         Hon. Deputy Secretary General Productive and Social Sectors, Dr. Jesca Eriyo,
  ·         Chargé d´Affaire German Embassy Dar es Salaam, Dr. Hans Koeppel.

  The opening ceremony will be a unique opportunity to conduct interviews, take pictures, liaise with high level politicians as well as students from the region and get first hand insights on East African Community integration.

  About the event:
  The youth of East Africa are important stakeholder in the EAC processes and form substantial part of the population. The East African Community Youth Summit on EAC Integration and Development Processes held in Arusha, Tanzania from 2nd – 3rd November, 2007 set the precedent for youth participation in the EAC integration. The Summit acknowledged that information and education on East African Integration and development is fundamental for enhancement and sustainability of regional integration. The youth called upon the EAC Secretariat to engage young people as partners to reach out to their peers on issues of EAC Integration and processes which will empower high-level skills needed to drive national and regional development. 
   In 2012, the Secretariat held the 1st EAC University Students Debate on Regional Integration. The aim of the debate was to provide a regional platform to promote dialogue among the youth and interest them in advocating for regional integration initiatives. The 1st EAC University Students’ Debate attracted over 100 students and 15 lecturers from public, private and other higher institutions of learning. 
  As an outcome of the 1st Debate, 5 EAC Youth Ambassadors were appointed as focal points in their respective Universities. The EAC Youth Ambassadors in collaboration with the EAC Secretariat have sensitized their peers on the EAC integration processes, benefits and challenges. This has enhanced increased awareness on regional integration and networking among institutions of higher learning in the region.
   The main objective of the EAC University Students debate is to promote continuous dialogue among the youth and interest them in advocating for regional integration initiatives.
  The specific objectives are;
  1. ensure continued participation of the youth in integration matters in the EAC region;
  2. encourage networking among university students in a bid to enhance EAC Integration;
  3. popularize the EAC integration Agenda through creating platforms that encourage sharing of experiences.
  4. prepare the youth for future leadership roles; as they hold the mantle as Ambassadors of integration in the region.

  In this spirit, the EAC-NCPR is excited to announce the 2nd EAC University Students’ Debate from 2nd to 3rd September.

  Ms Lisa NIXDORF
  Support to the East African Community Integration Process
  Advisor Implementation of EAC Common Market

  0 0

  Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh. Dkt. Fenella Mukangara (kulia) akimkabidhi Bendera ya Taifa,Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigitte Alfred (katikati) anaetarajiwa kuondoka hivi karibuni kwenda nchini Indonesia kushiriki Mashindano ya Urembo wa Dunia (Miss World 2013).Kushoto ni Mlezi wa Kamati ya Miss Tanzania,Mh. Emmanuel Ole Naiko.
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Lino International Agency ambao ni Waandaaji wa Shindano la Miss Tanzania,Hashim Lundenga akimuaga Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigitte Alfred (katikati) mara baada ya kukabidhiwa Bendera ya Taifa na Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh. Dkt. Fenella Mukangara  (kulia) wakati wa hafla ya Chakula cha jioni kwa ajili ya kumuaga Mrembo huyo,iliyofanyika kwenye Hoteli ya Giraffe,Jijini Dar es Salaam usiku huu.
   Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh. Dkt. Fenella Mukangara (wa pili kulia) akitoa nasaha zake kwa Warembo wanaowania taji la Redd's Miss Tanzania 2013,wakati wa hafla ya Chakula cha jioni ikiwa ni sehemu ya kumuaga Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigitte Alfred (pili kushoto) anaetarajiwa kuondoka hivi karibuni kwenda nchini Indonesia kushiriki Mashindano ya Urembo wa Dunia (Miss World).Hafla hiyo imefanyika usiku huu kwenye Hoteli ya Giraffe,Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni kutoka wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Herman Mwasoko na kushoto ni Mlezi na shoto ni Mlezi wa Kamati ya Miss Tanzania,Mh. Emmanuel Ole Naiko.
  Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigitte Alfred akikumbatiana na Mama yake Mzazi wakati wa Kumuaga.
  Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigitte Alfred akitoa shukrani zake wakati wa hafla hiyo ya kumuaga iliyofanyika usiku huu kwenye Hoteli ya Giraffe,jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya Warembo wanaowania Taji la Redd's Miss Tanzania 2013 wakiwa kwenye hafla hiyo.


  0 0
 • 08/28/13--20:00: ngoma azipendazo ankal
 • Wapenzi wote wa Twist wanaifahamu na kuipenda ngoma hii ya Daudi Kabaka ya 'Mlofa moja'

  0 0
 • 08/29/13--00:27: yale yaleeee......
 • NAONA TUME YA VYUO VIKUU IMEKUJA NA MPYA MWAKA HUU. MADENTI KIBAO WAMEPATA NAFASI MBILIMBILI KATIKA VYUO TOFAUTI. AMA KWELI BONGO TAMBARARE.....
  MDAU UKONGA  Sn Name Gender Indexo Analysis Institution DegreeProgram modentry Modeapply
  1 Naelijwa Jack Manonge F KE01106992009 2 Hubert Kairuki Memorial University Doctor of Medicine Equivalent Non_CAS
  2 NAELIJWA Jack Manongi F KE01106992009 2 Kilimanjaro Christian Medical College Doctor of Medicine Equivalent Non_CAS
  3 BASHIRU AKHAMAD M P020306492010 2 Josiah Kibira University College Bachelor of Arts with Education form six CAS
  4 BASHIRU AKHAMAD MIGINA M P020306492010 2 Muslimu University of Morogoro BA Education Direct Non_CAS
  5 SUNDAY AGUTTU M P021500542002 2 Josiah Kibira University College Bachelor of Arts with Education form six CAS
  6 SUNDAY AGUTTU M P021500542002 2 Muslimu University of Morogoro BA Education Direct Non_CAS
  7 SAID YATERI M P021900732006 2 Teofilo Kisanji University Bachelor of Arts with Education form six CAS
  8 SAIDI MUHIFADHI YATERI M P021900732006 2 Muslimu University of Morogoro BA Education Direct Non_CAS
  9 MPAJI FAKKI JUMA F P027200492010 2 Muslimu University of Morogoro BA Education Direct Non_CAS
  10 MPAJI FAKKI JUMA F P027200492010 2 Muslimu University of Morogoro BA Education Direct Non_CAS
  11 ZAINAB ADINANI F P032400312010 2 University of Arusha Bachelor of Education form six CAS
  12 ZAINAB ADINANI MADANDI F P032400312010 2 Muslimu University of Morogoro BA Education Direct Non_CAS

  0 0

  20130817_132318
  Kulia ni Meneja Masoko wa Kampuni Afrisoft Technologies Ltd Brian Mushi, Mkurugenzi wa Ufundi wa Kampuni hiyo David Kagoma pamoja na Msimamizi wa Fedha Bw. Bujune Leo kwenye picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa huduma ya M-soka.
  -------------------------------------
  Kampuni ya Afrisoft Technologies Ltd inayojihusisha na masuala ya teknolojia zinazorahisisha maisha ya kila siku, sasa imekuja na huduma mpya ya ‘M-Soka’ ambapo mtumiaji wa mtandao wa Vodacom anaweza kufaidi huduma hiyo kwa muda wowote na kwa haraka zaidi.
  Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo, Meneja Masoko wa Kampuni hiyo Brian Godwin Mushi amesema wameamua kutengeneza huduma hiyo, kwa kuwa mpira wa miguu ni mchezo unaopendwa sana na watu wengi na hivyo ukizingatia mahitaji ya watu kutaka kujua matokeo au kujua ratiba, sasa haina haja tena kusubiri gazeti au redio ila ukiingia katika ‘M-Soka’ (Mobile Soka)unapata kila kitu moja kwa moja kupitia simu yako ya mkononi.
  Bw. Mushi amesema ukizingatia hali halisi sio kila mahali panapatikana huduma ya intaneti na sio kila mtu ana simu inayoweza kuunganishwa kwenye mtandao huo, hivyo kupitia ‘M-Soka’ unaweza kupata matokeo au ratiba kwa kutumia simu ya aina yeyote ile.
  Akitaja namba zinazotumika kupata matokeo hayo amesema kuwa ni *149*31# kwa gharama nafuu ya shilingi 40 tu.
  Amesema unaweza kupata matokeo ya mechi zilizochezwa, ratiba ya mechi zitakazofuata na pia msimamo wa ligi mbalimbali, na kuwa kama ni matokeo unaweza kupata ya leo, jana, juzi na siku moja kabla na kama ni ratiba utapata ya leo, kesho, keshokutwa na mtondogoo na kama ni msimamo unapata wa wakati huohuo(real Time).
  Pia kuna ‘option ya live’ ambayo inakuwezesha kufuatilia mpira kwa dakika hiyo hiyo hata goli likifungwa inakupa matokeo yake mpaka jina la mfungaji na dakika ambayo goli limefungwa.
  Ni njia rahisi kwa mashabiki kufuatilia matokeo ya timu yao wanayoipenda na kupata taarifa ya kila kitu ikiwemo magoli, kadi hata penati.
  Ligi zinazopatikana katika mtandao huo ni za Uingereza, Hispania, Ufaransa, Italia, Ujerumani, UEFA, Kombe la Dunia na CAF kwa shilingi 40 tu.
  Kwa mshabiki yeyote wa soka usipate tabu, chukua simu yako na uandike *149*31# na upate matokeo, ratiba na msimamo papo hapo bila shaka na kwa gharama nafuu.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Waziri wa Biashara za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Nchini Uholanzi Bibi.Lilianne Ploumen,alipofika Ofisini kwake Mjini The Hague jana akiwana ujumbe wake katika ziara ya siku tano Nchini humo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kulia) na Ujumbe wake wakiwa katika mazungumzo na Viongozi wa Serikali Nchini Uholanzi,chini ya Kiongozi wao Waziri wa Biashara za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bibi.Lilianne Ploumen,(wa pili kushoto) katika Ofisi yake katika Mji wa The Hague Nchini Uholanzi.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akibadilishana mawazo na Waziri wa Biashara za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bibi.Lilianne Ploumen,nje ya Ofisi yake katika Mji wa The Hague Nchini Uholanzi,akiwa katika ziara ya siku tano katika Mji huo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Kiongozi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Dutch Shell Peter Voser,alipofika katika Makamo Makuu ya Kampuni hiyo katika Mji wa The Hague Nchini Uholanzi jana akiwa katika ziara ya siku tano na ujumbe wake.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Kiongozi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Dutch Shell Peter Voser,(katikati) wakiwa katika mazungumzo ya pamoja na Waziri wa Ardhi,Maji Makaazi na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban,(kulia) na Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Mafuta ya Dutch Shell na Serikali za Afrika Mashariki Axel Knospe,(kushoto) mara baada ya kuwasili mkatika Mako Makuu ya kampuni hiyo Mjini The Hague akiwa katika ziara ya Ushirikiano katika kukuza Uchumi.
  Kiongozi anayeshuhulikia masuala ya Uvumbuzi wa mafuta katika nchi zilizo chini ya Jangwa la Sahara,Alastair Milne,(kushoto) akijibu suala wakati wa mazungumzo kati ya Kamapuni ya Mafuta ya Dutch Shell na Ujumbe wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akiwa katika ziara ya siku tano na ujumbe wake Nchini Uholanzi.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati)akifafanua jambo wakati wa mazungumzo kati ya Kampuni ya Mafuta ya Dutch Shell na Ujumbe wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,katika ukumbi wa Makamo Makuu ya Kampuni hiyo Mjini The Hague nchini Uholanzi,(kutoka kulia) Waziri wa Ardhi,Maji Makaazi na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban, Kiongozi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Dutch Shell Peter Voser,(kushoto) Naibu Waziri wa Mambo ya Nje ya Nchi Mahadhi Juma Maalim,na John Crocker,ni miongozi mwa Viongozi wa Kampuni ya Shell.Picha na Ramadhan Othman,Uholanzi.
  Kwa habari na picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0
 • 08/29/13--01:04: Article 14


 • 0 0

  Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Pofesa Hermas Mwansoko akifafanua jamba kwa wageni wake kutoka Msumbiji walipotembelea ofisini kwake jana ili kujifunza namna kuendesha mradi wa Ukombozi barani Afrika ambapo Tanzania ndiyo makao makuu ya mradi huo.
  Mshauri Msaidizi wa Masuala ya Viza kutoka Ubalozi wa Msumbiji hapa nchini Daniel Rui Simao akifafanua jambo katika wakati wa mazungumzo na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni hayupo pichani, kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Wapigania Uhuru kutoka Msumbiji Vicente Joao Kovek na Chifu wa Idara ya Wapinania Uhuru kutoka Msumbiji Joao Antonio Nchoyo.
  Mkurugenzi wa Idara ya Wapigania Uhuru kutoka Msumbiji Vicente Joao Kovek akifafanua jambo wakati waliofanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Idara ya mendeleo ya Utamaduni wa Tanzania hayupo pichani jana jijini Dar es Salaam,kulia ni Chifu wa Idara ya Wapinania Uhuru kutoka Msumbiji Joao Antonio Nchoyo.
  Kutoka kulia ni Chifu wa Idara ya Wapigania Uhuru kutoka Msumbiji Joao Antonio Nchoyo, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Pofesa Hermas Mwansoko,Mkurugenzi wa Idara ya Wapigania Uhuru kutoka Msumbiji Vicente Joao Kovek,Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Bibi Joyce Hagu, Mshauri Msaidizi wa Masuala ya Viza kutoka Ubalozi wa Msumbiji hapa nchini Daniel Rui Simao.na Mratibu wa Mradi wa Harakati za Ukombozi Barani Afika Tanzania Leah Elias Kihimbi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza mazungumzo kuhusu namna ya kuendesha Mradi wa Harakati za Ukombozi Barani Afrika

  0 0

  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara akielezea kufurahiswa kwake na ukuaji wa mchezo wa ngumi hapa nchini alipokutana na Bondia maarufu duniani na aliyewahi kuwa bingwa wa dunia mara mbili Francois Botha (White Buffalo) kushoto jana jijini Dar es Salaam.
  Bingwa wa dunia mara mbili wa mchezo wa ngumi Bondia Francois Botha (White Buffalo) akielezea jambo kwa waandishi wa habari alipotembelea ofisini kwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara kulia jana jijini Dar es Salaam.

  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt fenella Mukangara na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo waliokaa wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Wizara na wageni walioambatana na Botha jana jijini Dar es Salaam. Picha zote na Frank Shija - Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

  0 0


  Baada ya kuonyesha kiwango kikubwa kabisa katika mechi ya kirafiki kati ya Golden bush FC na Mwanza United uongozi wa Golden bush uko kwenye hatua za mwisho kabisa kukamilisha usajili wa beki kisiki George Magere Masatu mchezaji wa Zamani wa Pamba, Simba na timu ya taifa.

  Mazungumzo ya kumuhamisha mchezaji huyo nyota kutoka Mwanza united yanafanywa na mwanasheria wa timu ya Golden bush FC bwana Godfrey Chambua  a k a Zacharia Hans Poppe. Bwana Poppe aliyeshikana mkono na Athumani Machuppa pichani ndiye aliyewezesha usajili wa akina Athuman Machuppa na Sadik Muhimbo ambao wote wametolewa kwa mkopo timu za Sweden na DRC.

  Uwepo wa George Masatu kwenye timu yetu ya Golden bush veterans itaongeza chachu ya ushindi hasa ukitambua uwezo alionao bwana George. Tunawaomba wapenzi wetu wawe na subira wakati uongozi ukifanya kazi ya ziada kuahakiksha Masatu anatua Golden Bush  bila mizengwe.

  Golden Bush kwasasa hivi wako camp wakijiandaa na game ngumu kabisa dhidi ya Pugu Veterans, game itapigwa Pugu kajiungeni siku ya jumamosi kuanzia saa mbili kamili asubuhi.  Tunalazimika kwenda kucheza pugu baada ya timu ya TASWA kuchomoa game ambayo ilitakiwa ipigwe siku ya jumapili uwanja wa Kinesi "ST James Park"

  Imetolewa na msemaji na mchezaji mwandamizi wa golden bush FC

  Onesmo Waziri "Ticotico"

  0 0

  Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Mkoa wa Kilimanjaro, Leiya Hermenegild (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh.mil.28 Mkandarasi wa Kampuni ya uchimbaji visima ya Aqwe Drilling and Construction ya Mjini Moshi, Rishi Shah kwa ajili ya kuchimba kisima katika Chuo Kikuu cha Ushirika na Biashara cha Mjini Moshi (MUCCoBS) chuoni hapo mwishoni mwa wiki.Aliyevaa tai ni Mkuu wa chuo hicho, Profesa Faustine Bee.
  Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorice Malulu (wa tatu kulia)akielekezwa jambo na Rishi Shah  wa Kampuni ya Ukandarasi wa Uchimbaji Visima ya Aqwe Drilling and Construction ya Mjini Moshi  iyokabidhiwa hundi ya sh. mil. 28 za kuchimbia kisima cha maji katika Chuo Kikuu cha Ushirika na Biashara cha Mjini Moshi (MUCCoBS). TBL  iliyokabidhi hundi hiyo hivi karibuni chuoni hapo, imefadhili uchimbaji wakisima hicho.

  0 0

  Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akimkaribisha Wizarani Bibi Maria Gracia Pulido-Tan, Mwenyekiti wa Tume ya Ukaguzi ya Jamhuri ya Ufilipino alipofika kwa ajili ya mazungumzo. Bibi Pulido-Tan pia ni Mgombea wa Jamhuri ya Ufilipino kwenye Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa. 
  Bibi Pulido-Tan akimtambulisha kwa Balozi Mushy,  Bi. Donna Celeste Feliciano-Gatmaytan, Kaimu Balozi wa Ufilipino nchini Kenya.
  Balozi Mushy akiwa katika mazungumzo na Bibi Pulido-Tan kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano wa kimataifa.
  Baadhi ya wajumbe kutoka Ufilipino waliofuatana na Bibi Pulido-Tan.
  Mazungumzo yakiendelea.
  Picha ya pamoja.

older | 1 | .... | 239 | 240 | (Page 241) | 242 | 243 | .... | 3272 | newer