Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109591 articles
Browse latest View live

VIONGOZI WA NGAZI MBALIMBALI NA WANANCHI WASHIRIKI KATIKA MAZISHI YA BABA YAKE MZAZI MAMA SALMA KIKWETE

0
0
Na Hadija Seif, Globu ya Jamii
VIONGOZI wa ngazi mbalimbali Serikalini , viongozi wastaafu pamoja na mamia ya wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam wameshiriki katika mazishi ya mzee Rashid Mkwachu ambaye ni baba yake mzazi Mke wa Rais mstafu Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikwete.

Mwili wa mzee Mkwachu umezikwa leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam. Alifikwa na umauti Julai 19 mwaka huu  na chanzo cha kifo chake kimeelezwa na Msemaji wa familia ya Kikwete Ridhawani Kikwete kuwa mzee huyo amefariki kutokana na magonjwa ya utu uzima kwani umri wake ulikuwa zaidi ya miaka 100.

Kabla ya mwili kufikishwa makaburi ya Kisuti ibada na dua kumuombea marehemu mzee Mkwachu zilifanyika nyumbani kwa Rais mstaafu Jakaya Kikwete Msasani jijini Dar es Salaam. Baadhi ya viongozi walioshiriki kwenye maziko hayo ni Rais Mstaafu Al haji Ali Hassan Mwinyi,  Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa.

Akizungumza kwenye msiba huo Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry amesema maisha ya binadamu ya kuishi kwenye ulimwengu ni mafupi sana na kwa kawaida ni kati ya miaka 63 na ikitoa zaidi ya hapo ni zawadi tu.

Amesema kuwa viumbe vyote ni vinamuda wake wa kuondoa kwenye huu ulimwengu na hakuna ambaye ataishi milele na kufafanua na kufa si kutoweka moja kwa moja bali ni utaratibu wa maisha ya kutoka kwenye ulimwengu na kwenda akhera.

Kwa upande wake Mjuukuu wa Marehemu Mzee Mkwachu ambaye pia ni Msemaji wa Familia Ridhwan Kikwete alieleza kilichokuwa kikimsumbua babu yake ni magonjwa ya utu uzima. Ametumia nafasi hiyo kuwashukuru woye ambao wamepata nafasi kwa namna moja a nyingine kuungana nao katiki kipindi hiki ambacho cha majonzi wako.

Waombolezaji walioungana katika maziko ya Baba mzazi wa mke wa Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Mzee Rashid Mkwachu, aliyefariki dunia jana Alhamisi, Julai 19, 2018, ambapo maziko ya marehemu yamefanyika katika Makaburi ya Kisutu, jijini Dar es Salaam leo Julai 20, 2018.
Mtoto wa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, Ridhiwan Kikwete akitoa salamu za shukrani kwa waombolezaji waliounga nao katika maziko ya  Baba mzazi wa Mama Salma Kikwete, Mzee Rashid Mkwachu, aliyefariki dunia jana Alhamisi, Julai 19, 2018, ambapo maziko ya marehemu yamefanyika katika Makaburi ya Kisutu, jijini Dar es Salaam leo Julai 20, 2018.
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete akiaga mara baada ya kumaliza maziko ya  Baba mzazi wa Mama Salma Kikwete, Mzee Rashid Mkwachu, aliyefariki dunia jana Alhamisi, Julai 19, 2018, ambapo maziko ya marehemu yamefanyika katika Makaburi ya Kisutu, jijini Dar es Salaam leo Julai 20, 2018.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiaga mara baada ya kumaliza maziko ya Baba mzazi wa Mama Salma Kikwete, Mzee Rashid Mkwachu, aliyefariki dunia jana Alhamisi, Julai 19, 2018, ambapo maziko ya marehemu yamefanyika katika Makaburi ya Kisutu, jijini Dar es Salaam leo Julai 20, 2018.
Rais Mstaafu awamu ya pili Mhe. Alhaji Al-Hassan Mwinyi akiaga mara baada ya kumaliza maziko ya Baba mzazi wa Mama Salma Kikwete, Mzee Rashid Mkwachu, aliyefariki dunia jana Alhamisi, Julai 19, 2018, ambapo maziko ya marehemu yamefanyika katika Makaburi ya Kisutu, jijini Dar es Salaam leo Julai 20, 2018.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiwaaga marais wastaafu wa pili Mhe. Alhaji Al-Hassan Mwinyi (katikati) na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete mara baada ya mara baada ya kumaliza maziko ya  Baba mzazi wa Mama Salma Kikwete, Mzee Rashid Mkwachu, aliyefariki dunia jana Alhamisi, Julai 19, 2018, ambapo maziko ya marehemu yamefanyika katika Makaburi ya Kisutu, jijini Dar es Salaam leo Julai 20, 2018.
Rais Mstaafu awamu ya pili Mhe. Alhaji Al-Hassan Mwinyi akiaga na aliyekuwa Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova mara baada ya kumaliza maziko ya Baba mzazi wa Mama Salma Kikwete, Mzee Rashid Mkwachu, aliyefariki dunia jana Alhamisi, Julai 19, 2018, ambapo maziko ya marehemu yamefanyika katika Makaburi ya Kisutu, jijini Dar es Salaam leo Julai 20, 2018.

WAFICHUENI WASAMBAZAJI NA WAUZAJI WA MADAWA YA KULEVYA ILI KUOKOA VIJANA - KABEHO

0
0
Na Mwamvua Mwinyi, Chalinze
WANANCHI wametakiwa kufichua watu wanaojihusisha katika matumizi ya madawa ya kulevya ikiwa ni pamoja na wasambazaji na wauzaji ili kupunguza tatizo la kuweka rehani baadhi ya vijana ambao ndio nguvu kazi. 
Akizungumza Chalinze,Bagamoyo mkoani Pwani ,katika mbio za mwenge wa uhuru ,kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa ,Charles Kabeho alisema ,matumizi ya madawa hayo ni janga kubwa ndani ya jamii.

"Nawaomba wananchi msiogope kuwafichua wahusika hata kama ni ndugu yako ,jirani, kwani wanaojiingiza katika wimbi hilo wapo miongoni mwetu. Jengeni ushirikiano na vyombo vya ulinzi na usalama ikiwemo jeshi la polisi ,ili hali kukabiliana na tatizo hili" alisisitiza Kabeho, akiongeza: "Niwaase ," walioathirika na madawa hayo wajitambue kwa kuacha ,wasikate tamaa,kwani wanaweza kufanya biashara ndogondogo kwa lengo la kujipatia kipato"

Awali mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Alhaj Majid Mwanga akipokea mwenge wa uhuru kutokea Kibaha Mjini alisema, mwenge huo utapitia miradi 15 iliyogharimu sh.bilioni 121.459.3. Pamoja na hayo ,alhaj Mwanga alieleza Chalinze pia ni halmashauri inayoongoza kwa makusanyo ya mapato ya ndani kwa zaidi ya asilimia 100.
Mkoa wa Pwani ulipokea mwenge wa Uhuru 12 July mwaka huu kutokea Dar es salaam ,ambapo ulipitia miradi ya maendeleo 67 yenye thamani ya sh.bilioni 162.440.8, kupitia wilaya saba na halmashauri tisa. Kati ya miradi hiyo miradi 16 iliwekwa mawe ya msingi ,miradi 12 kati ya 13 iliyolengwa kuzinduliwa ilizinduliwa ,nane ilifunguliwa na miradi 21 imekaguliwa .
 Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akiwa katika mapokezi ya mwenge wa Uhuru Chalinze.
 Mkurugenzi wa halmashauri ya Chalinze Edes Lukoa katika mapokezi ya mwenge wa Uhuru Chalinze.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, alhaj Majid Mwanga akipokea mwenge wa Uhuru ukitokea halmashauri ya Kibaha Mjini kwa mkuu wa wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama 

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 20.07.2018

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII DK. HAMISI KIGWANGALLA ATEMBELEA PORI LA AKIBA MASWA

0
0
.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia akioneshwa ramani ya Pori la Akiba Maswa na Meneja wa pori hilo, Lusajo Masinde (kushoto kwake) wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za uhifadhi katika wilaya ya Meatu mkoani Simiyu jana. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua moja ya eneo la "camp" ya kitalii katika Pori la Akiba Maswa wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za uhifadhi katika wilaya ya Meatu mkoani Simiyu jana. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, viongozi wa Pori la Akiba Maswa na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Makao wakiangalia mandhari ya Pori la Akiba Maswa lililopo wilaya ya Meatu mkoani Simiyu wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za uhifadhi mkoani humo jana. 

KATIBU MKUU WIZARA YA UJENZI AWATAKA WAHANDISI WASHAURI KUZINGATIA WELEDI WA KAZI

WAZIRI MHAGAMA AMPA MWEZI MMOJA MKANDARASI KUKAMILISHA UJENZI BARABARA YA KUUNGANISHA DARAJA LA NYERERE NA KIGAMBONI

0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama amempa mwezi mmoja mkandarasi anayejenga kwa kiwango cha lami barabara yenye urefu wa kilometa mbili inayounganisha Daraja la Nyerere na barabara ya Kibada-Feri iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam, kukamilisha kazi  hiyo hadi tarehe 31 Agosti, mwaka huu, ili kurahisisha mawasiliano kwa wananchi wanaovuka daraja hilo.
Waziri Mhagama ameyasema hayo wakati akikagua  ujenzi wa barabara hiyo na kujionea uendeshaji wa shughuli  katika daraja la Nyerere, ambapo amefafanua kuwa kutokamilika kwa ujenzi wa barabara hiyo kunasababisha kero  kwa wananchi wanaovuka kwa miguu na wanaotumia vyombo vya usafiri kushindwa kupita kwa urahisi, hali inayochangia kupungua kwa mapato yanayokusanywa darajani hapo.
“Hii barabara ni ya msingi kwani kutokamilika kwake ndo maana hata magari madogo hayapendi kutumia hii njia, Mkandarasi huyu ameomba mara mbili kuongezewa muda kukamilisha kazi hii na sasa tunampa muda tena, nataka kazi hii ikamilike kwani baada ya  kukamilisha ujenzi wa daraja hili tulitegemea kuwa mapato tutakayo kusanya hapa yatatuwezesha kulipa gharama tulizotumia kuwekeza na kujenga daraja hili, lakini nimejaribu kuangalia makusanyo ya tangu mwaka 2016/2017 na mwaka 2017/2018 inakuwa kidogo sana ikilinganishwa na mapato ya mwaka 2016, hili lazima liangaliwe,   tunataka daraja hili liendelee kutoa huduma na liendelee kuleta faida kwenye mfuko na ukizingatia fedha hizi ni za wanachama zilizotumika” Amesema Mhagama.
Waziri Mhagama amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuhakikisha unawekwa mfumo bora wa utambuzi wa vyombo vya usafiri vinavyovuka darajani hapo ili kujua gharama halisi ya tozo kwa vyombo vya usafiri vinavyovuka darajani  hapo na kuepuka upotevu wa mapato kutokana na kutokuwa na mfumo wenye kutambua tozo halisi kwa vyombo hivyo.
“Nataka Mkurugenzi ushughulikie kwa haraka sana mfumo wa utambuzi wa vyombo vya usafiri vinavyovuka hapa. Tumejifunza mfumo wa malipo ni wa kielektroniki lakini utaratibu wa  utambuzi wa vyombo vya usafiri vinavyovuka hapa kwa kuangalia tu kwa macho na uhakika huo wa tozo kwa chombo cha usafiri inategeea sana na huyo mkadiriaji, lazima tuwe na utaratibu wa mfumo mzuri wa kielekroniki wa kufanya kazi hii ili tuweze kujipima vizuri katika ukusanyaji wa mapato tunayo kusanya hapa bila hivyo tutakuwa tunapoteza mapato mengi” Amesema Mhagama.
Kwa upande wao Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), William Erio na na Mkandarasi wa barabara hiyo, Mhandisi Jamal Mruma wote kwa pamoja
wamemuhakikishia Waziri Mhagama kutekeleza maagizo hayo kwa wakati ili kuondoa usumbufu uliopo kwa sasa kwa wananchi wanaotumia  daraja hilo  na kuweza kuongeza makusanyo ya mapato yanayotokana na tozo za vyombo vya usafiri vinavyovuka katika daraja hilo.
Barabara hiyo inajengwa na Kampuni ya China Railway Construction Agency Group, kwa gharama ya shilingi bilioni 21.1, ambapo tayari kampuni hiyo imeshalipwa kiasi cha shilingi bilioni 10.5. Kukamilika kwa barabara hiyo kutaongeza mapato yanayotokana na tozo za vyombo vya usafiri vinavyovuka Darajani hapo ambapo tangu Daraja hilo lianze kufanya kazi mwezi Mei, 2016 hadi Juni 2018,  takribani shilingi bilioni 17.1 zimekusanywa na kwa wastani kila mwezi mapato ya shilingi milioni 600 hukusanywa.
 Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akimueleza jambo Mhandisi Jamal Mruma, anayejenga kwa kiwango cha lami barabara yenye urefu wa  kilometa mbili inayo unganisha Daraja la Nyerere na barabara ya Kibada -Feri iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam wakati akikagua ujenzi wa daraj hilo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. William Erio
 Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Bw. William Erio wakimsikiliza  Mhandisi Jamal Mruma, anayejenga kwa kiwango cha lami barabara yenye urefu wa  kilometa mbili inayo unganisha Daraja la Nyerere na barabara ya Kibada -Feri iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam wakati akikagua ujenzi wa daraj hilo.
Mmoja wa Wananchi akikamilisha taratibu za malipo katika Daraja la Nyerere lililopo Kigamboni jijini Dar es Salaam. Daraja la kigamboni tangu lianze kufanya kazi  mwezi Mei mwaka 2016 hadi Juni 2018, takribani shilingi bilioni 17.1 zimekusanywa na  kwa wastani kila mwezi mapato ya shilingi milioni 600 hukusanywa.

MAKAMISHNA WA TANZANIA NA ZAMBIA WAKUTANA KUMALIZA KERO ZA MPAKA WA TUNDUMA

0
0

Na Emmanuel Madafa, Michuzi TV, Mbeya

KESI YA TUHUMA ZA MAUAJI YA KUKUSUDIA YAKWAMA MAHAKAMANI

0
0
*Ni baada ya gari ya kubeba mahabusu kuharibika

Na Dixon Busagaga, Moshi

KESI ya tuhuma za mauaji ya kukusudia linalomkabili mmilikiwa wa Shule ya Sekondari ya Scolastica Edward Shayo na wenzake wawili limehairishwa kwa mara ya tatu sasa na sababu ya kuahirishwa ikitajwa imetokana na kuharibika kwa gari la kubebea mahabusu.

Kwa jana kesi hiyo ilipangwa kuendelea kwa hatua ya usomaji wa maelezo ya mashahidi kwa ajili ya kufunga ushahidi kabla ya shauri hilo kuhamishiwa Mahakama Kuu. Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Sophia Masati alieleza kuwa shauri hiyo itatajwa kwa ajili ya usomaji wa maelezo ya mashahidi Agosti 3,mwaka huu.

“Kesi hii imeahirishwa hadi Agosti 3 mwaka huu kwa ajili ya kuja kusoma maelezo ya mashahidi wa kesi hii,"amesema Hakimu huyo.Kabla ya kutajwa kwa mara nyingine kwa shauri jana, Julai 6 mwaka huu Hakimu mkazi wa mahakama ya hakimi mkazi ,Moshi ,Julieth Mawole aliieleza maelezo ya ushahidi wa shauri hilo utatolewa .

Kwa mara ya kwanza usomaji wa maelezo ya kufunga ushahidi uliahirishwa baada ya washtakiwa kushindwa kufikishwa mahakamani.Sababu za kutofika kwa washtakiwa mahakamani hapo zilitajwa kuwa ni mkanganyiko wa tarehe iliyopangwa na mahakama hiyo ambayo ilikua ni June 29 mwaka huu kutofautiana na ile iliyowasilishwa Mahabausu Gereza la Karanga ambayo ilitajwa kuwa ni Julai 29 ,mwaka huu.

Maelezo hayo yaliwasilishwa mahakamani hapo na Wakili wa Serikali,Agatha Pima alipoomba kupangwa kwa tarehe nyingine kwa ajili ya kuendelea kwa hatua ya Kufunga Ushahidi kwenda Mahakama kuu.Ombi hilo lilipingwa na Wakili wa upande wa utetezi anaye mtetea Mshtakiwa wa Pili katika shauri hilo ,Edward Shayo,Elikunda Kipoko akieleza kutoridhishwa na maelezo ya upande wa Jamhuri .


UTAFITI WABAINI KATIKA KILA HEKTA MOJA YA SHAMBA LA MPUNGA PANYA HUPOTEZA GUNIA TISA

0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

UTAFITI uliofanywa na Chuo Kiku cha Sokoine (SUA) umeonesha kuwa katika kila hekta moja ya shamba la mpunga la umwagiliaji hupoteza gunia tisa za mpunga kutokana na kushambuliwa na panya.

Kwa mujibu wa SUA utafiti huo ulianza kufanyika mwaka 2015 baada ya chuo hicho kupata malalamiko mengi kutoka kwa wakulima wa zao la mpunga ambao walidai kuwa panya ndio adui yao mkubwa.

Akizungumzia utafiti huo jijini Dar es Salaam Profesa Loth Mulungu ambaye ni Mtafiti Mdhibiti wa viumbe hai na uharibifu amesema kutokana na utafiti huo hivi sasa tayari wamegundua vizuizi na mitego ambayo ni sumu kubwa kwa panya wanaokula mipunga katika mashamba.

Akifafanua zaidi kwenye Maonyesho ya 13 Vyuo Vikuu ya Elimu ya Juu Tanzania (TCU) yanayofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam Profesa Mulungu wanatumia vizuizi na mitego kwa ajili ya kuwakamata panya wanaoshambulia mpunga ambao tayari ulishakomaa katika shamba.

"Kwa siku tunatega panya zaidi ya mia mbili ambao hao wangekuwa wameingia kwenye shamba la mpunga wangekuwa wameshambilia zaidi mpunga ambao uliokuwa unasubiriwa kuvunwa,"amesema Profesa Malungu.

Pia amesema lengo lao kubwa ni kuongeza ufanisi katika uthibiti wa panya kwenye mashamba ya umwagiliaji na kwamba wadudu wengi waharibifu wakiwemo panya wanapenda kuvamia katika mashamba ya umwagiliaji kwa sababu mwaka mzima mashamba hayo yana mazao tofauti na yale mashamba yanayotegemea mvua za masika.

Hata hivyo amesema katika nchi ya Asia tayari wamefanikiwa kwa kutumia njia ya kuweka vizuizi na mitego katika mashamba ya panya."SUA tunataka kuipeleka teknolojia hiyo mpya katika mikoa inayolima mpunga kama vile Morogoro ,Iringa,Mvomero na Kilombero.

CCM YAZINDUA KAMPENI KATA YA MAWENZI, YAAHIDI KUSIMAMIA, KUTOA FURSA ZA MAENDELEO KWA WANANCHI

0
0
CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimezindua rasmi kampeni za uchaguzi mdogo Kata ya Mawenzi ilipo Moshi Mjini huku kikitumia nafasi hiyo kuahidi kuenddelea kusimamia na kutoa fursa nyingi zaidi za maendeleo kwa wananchi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo wa kampeni hizo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole amesisitiza CCM kuendelea kusimamia na kutoa fursa nyingi zaidi za kimaendeleo kwa wananchi wa Moshi Mjini katika Kata ya Mawenzi.

Polepole amewaomba wananchi wa Kata ya Mawenzi kumpatia kura za ushindi mgombea wa CCM Apaikunda Ayo Naburi kuwa Diwani wa Kata hiyo ili awe kiungo cha fursa zitokanazo na Serikali ya CCM kwa wananchi wake.

Akifafanua kuhusu fursa hizo za wananchi Polepole amesema CCM imejipanga kuhakikisha wananchi wanapata mikopo ya Halmashauri bila usumbufu, mizengwe wala riba.

Pia wafanyabiashara wadogo wadogo waendelee kufanya shughuli zao kwa utaratibu mzuri pasina usumbufu na Vijana wa bodaboda na bajaji watazamwe katika jicho la utu, usawa na haki katika shughuli zao za usafirishaji wa abiria katikati ya mji wa Moshi.

"Naomba mtupatie Apaikunda awe jicho letu, mtu tunaye muamini, ndio kiungo akisema nasi tunatoa maelekezo kwa manufaa ya wananchi," amesema Polepole.

Uzinduzi huo wa kampeni, ni muendelezo wa mikutano ya kampeni ya uchaguzi Mdogo katika kata na majimbo ambapo CCM inaendelea kunadi Sera zake bora kwa wananchi.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole  akiwahutubia Wananchi na wafuasi wa chama hicho wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo,
amesisitiza CCM kuendelea kusimamia na kutoa fursa nyingi zaidi za kimaendeleo kwa wananchi wa Moshi Mjini katika Kata ya Mawenzi.

CHILIGATI AKABIDHI MKURABITA KWA NJOOLAY.

0
0

JOSEPH MPANGALA

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za wanyonge Tanzania MKURABITA,Balozi Daniel Ole Njoolai ameiomba Halmashauri kote nChini Kuhakikisha zinasaidia Mpango wa kurasimisha ardhi ili wananchii waweze kupatiwa hati zitakazowawezesha kujikwamua kiuchumi.

Hayo yameyasema katika makabidhiano ya uongozi wa Kamati Hiyo ambayo ilikuwa ikiongozwa na Kaptein Mstaafu John Chiligati katika kipindi cha Miaka Mitatu Jijini Dodoma.

Balozi Njoolay amesema katikakipindi chake cha uongozi kama mkuu wa mkoa kwa miaka 16 tayari anazifaham Halmashauri hivyo kuziomba kushirikiana ili kuwezesha Wananchi kuweza kurasimisha ardhi na Biashara.

“Mimi nimefanyakazi kama mkuu wa Mkoakwa Miaka 16 Nazifaham Halmashauri,Nitumia nafasi hii kuziomba Halmashauri Zitusaidie sana,ziwe positive kwa swala hili watu wao ndio Tunawasaidia kwa sababu Bila halmashauri hakuna Kitu”amesema Balozi Njoolay

Naye Mwenyekiti Mstaafu wa kamati hiyo Kaptein Mstaafu John Chiligati amesema wananchii wa Vijijini ambao wanakadiriwa kufikia asilimia 80 hawana uwelewa wa Urasimishaji ingawa wanamashamba Makubwa lakini hayana hati ya Umiliki hivyo kuendelea kubaki kuwa masikini.

“Wananchii wetu wa Vijijini karibu asilimia 80%mtu ambaye anamigomba yake mihogo yake kila kitu anacho halafu anasema masikini wakati Duniani kote Mtu ambaye anamiliki Ardhi anaitwa LandLord yaan ni mtu ambaye yuko vizuri lakini siri yake ni kwamba hii mali aliyonayo bado haitambuliki na yeyote”Amesema Chiligati Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za wanyonge Tanzania MKURABITA Ulianzishwa mwaka 2004 na tayari umefika katika mikoa 27,23 mikoa ya Tanzania Bara na mikoa 4 ya Zanzibar na tayari hati hati elf 71 na 51 na zimewawezesha kukopa shilingi Billlion 5.5 kutoka katika taasisi mbalimbali za kifedha
Mwenyekiti Mstaafu wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za wanyonge Tanzania (MKURABITA), Kapteni Mstaafu John Chiligati akimkabidhi kitabu cha mwongozo, Mwenyekiti mpya wa Kamati hiyo, Balozi Daniel Ole Njoolay mbele ya wajumbe na watendaji wa kamati hiyo jijini Dodoma.

Mwenyekiti mpya wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za wanyonge Tanzania (MKURABITA), Balozi Daniel Ole Njoolay akizunguza mbele ya watendaji na jumbe wapya MKURABITA katika kikao elekezi kilichofanyika jijini Dodoma.

CHADEMA SIRARI WAMFUTIA UANACHAMA KIONGOZI BAADA YA KUMTUHUMU KUTAFUNA FEDHA ZA KUNUNUA JENEZA

0
0
Na Frankius Cleophace, Tarime

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo( Chadema)Kata ya Sirari wilayani Tarime mkoani Mara kimemvua uongozi na kumfutia uanachama aliyekuwa Mwenezi wa kata hiyo Samwel Kijiji Mwita kutokana na tuhuma za upotevu wa fedha Sh.80,000 zilizochangwa kwa ajili ya kununua jeneza katika msiba wa aliyekuwamwanachama wa chama hicho marehemu Chacha Makuri.

Mwita Isansi ni Mwenyekiti wa Chadema Kata ya Sirari amesema wameamua kumfutia uanachama Mwita kutokana na tuhuma hizo za upotevu wa fedha.Mwita amesema kuwa zilichangwa ni Sh.320,000 kwa lengo la kununu jeneza nchini Kenya lakini baadae zilipungua Sh.80,000.

“Baada ya upotevu wa fedha hizo sisi kama viongozi tulijichanga ili kununua jeneza baada ya msiba tumemuita kamati ya maadili takribani mara mbili lakini hajaweza kuitikia na maamuzi yetu ni kumfuta uanachama na kumvua uongozi kwahiyo mpaka sasa siyo kiongozi,” amesema Mwita.

Mwenyekiti huyo ametoa mwito kwa viongozi wengine kuendelea kuzingatia maadili ya uongozi na sikufanya ubadhilifu wowote na kusema kuwa chama kitaendelea kuchukua hatua kali kwa viongozi ambao wanaenda kinyume na maadili ya uongozi.

Aidha Mwenyekiti wa kijiji cha Sokoni Denson Makanya amesema kuwa licha ya kutafuna fedha hizo bado Mwenezi huyo amekuwa akituhumiwa kwa makosa mbalimbali na tayari alishaandikiwa barua ya onyo juu ya vitendo vyake alivyokuwa akifanya akiwa kiongozi ndani ya jamii.

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI AFANYA ZIARA MKOANI ARUSHA

0
0

Na Kumbuka Ndatta,Arusha

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdalla Ulega ametembele taasisi za Serikali zilizopo chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na wadau wengine wa sekta ya mifugo na uvuvi.

Akitoa taarifa fupi kwa Naibu waziri,Mkurugenzi wa Wakala wa vyuo vya Mafunzo ya Mifugo (LITA) Kampasi ya Tengeru Joseph Msemwa amemweleza Ulega kuwa kazi kubwa ya LITA ni kutoa mafunzo ya muda mrefu na muda mfupi,kufanya utafiti na ushauri elekezi na uzalishaji Mali.

Pia mafunzo hayo yamejikita katika fani ya afya ya mifugo na uzalishaji.Aidha mafunzo hayo yanalenga kutoa watalaam wenye ujuzi wa hali ya juu katika fani za ufugaji.Amesema lengo ni kuwa na mtazamo wa Kujiajiri na kuendesha miradi mbalimbali ya kibiashara.

Msemwa amemwambia Naibu Waziri baadhi ya changamoto zinazoikabili Kampasi hiyo kuwa ni uchakavu wa majengo,huduma duni za maji,upungu wa watumishi na Muundo wa Wakala.Kwa upande wa Mtendaji Mkuu wa LITA (CEO)Magreth Pallangyo pamoja na kupokea maagizo kutoka kwa Naibu Waziri,ameahidi kuyatekeleza maagizo yote yaliyotolewa na kuyashughukia ipasavyo.

Akihutubia watumishi waliofika katika ukumbi wa Kampasi ya Tengeru Ulega amesema kuwa vyuo hivi vya mafunzo ya mifugo ndio nguzo mama katika kuchochea maendeleo ya uchumi wa Taifa letu."Wakufunzi wa Vyuo hivi vya Mifugo jitahidi sana kuhusianisha kile mnachokifundisha darasani na mazingira halisi ya itanzania.

"Toeni elimu bora ili muweze kuwasaidia vijana hawa na taifa kwa ujumla.Vijana hawa wakitoka hapa tunataka waone kuwa wamezungukwa na fursa za kiuchumi," amesema Ulega.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiangalia ng`ombe wa uhimilishaji katika kituo cha Taifa cha(NAIC) kilichpo Usa River jijini Arusha.
 Mkufunzi mwandamizi wa kitengo cha teknolojia ya maziwa,Theresia Teti  akimwelezea  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega namna ya usindikaji wa maziwa jijini Arusha.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiangalia namna ya uhimilishaji unavyofanyoka katika kituo cha Taifa cha(NAIC) kilichopo Usa River jijini Arusha.Picha na Emmanuel Massaka,MMG Arusha)
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akitembelea shamba la samaki Shazan lililopo jijini Arusha.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JULAi 21, 2018

CHUO CHA MZUMBE WAFANYA UDAHILI WA WANAFUNZI WAPYA NDANI YA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA

0
0


Meneja wa Mawasiliano wa Chuo Kikuu Mzumbe Rosada Fredrick akizungumza na waandishi kufanya udahili katika maonesho ya Vyuo Vikuu.
Wanfunzi wakipata maelezo katika banda la Chuo Kikuu Mzumbe.

CHUO Kikuu Mzumbe kimesema kuwa katika maonesho vyuo vikuu katika viwanja vya Mnazi mmoja wanadahili moja kwa moja kwa njia kieletroniki kwa wale wanaotaka kujiunga na chuo hicho.

Akizungumza katika maonesho hayo Meneja Mawasiliano wa Chuo hicho Silvia Lupembe amesema  katika maonesho hayo watanzania watumie fursa ya kupata taarifa za chuo hicho na wataotaka kujiunga watafanya udahili kwa kupata muongozo kwa watumishi waliopo katika maonesho. 

Amesema Chuo Kikuu Mzumbe kinahistoria katika utoaji wa elimu bora hivyo ni fursa katika maonesho kwa wananchi kutembelea na kupata taarifa za chuo.

Lupembe amesema wakati kuwa dirisha liko wazi  kwa waombaji kuomba kwa njia ya kieletroniki.

"Tunajivunia katika utoaji wa elimu bora  kwa wanafunzi hivyo ni fursa kwao  vijana kujiunga na chuo hicho"amesena.

Costech:tafiti zote lazima zipate vibali

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
TAFITI zote lazima ziombewe vibali kabla ya kuanza kufanya utafiti huo ikiwa kuhakikisha tafiti zinakuwa na viwango vinavyoendana taratibu zilizowekwa na Tume ya  Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech)

Akizungumza katika Maonesho Mkutubi wa Costech Amedeus Maro amesema kuwa mtu akipata kibali cha kufanya utafiti baada ya kukamilika lazima apeleke kabla kwenda katika matumizi mengine.

Amesema kuwa kunatofauti  kati tafiti za kitaaluma na tafiti kwa ajili ya kutumika katika umma ambazo zinahitajika kuangaliwa njia zilizotumika kwa kuangalia masilahi mapana ya umma.

Amesema kuwa zinazofanywa na vyuo mwenye dhamana ni mkuu wa Chuo ndiye anayetambulika na Costech na wanafunzi wa nje ya nchi wanaotaka kufanya utafiti lazima waombe Costech kutokana kuwa hakuna mahusiano na mkuu wa chuo cha nje ya nchi.

Maro amesema kuwa wananchi na watafiti kuweza kufanya mawasiliano na Costech kabla ya kufanya utafiti na bila kufanya hivyo hatua kali atachukuliwa kwa mtu atakayefanya utafiti. 
 Mkutubi wa Costech Amedeus Maro akizungumza na mwananchi aliotembelea banda la Costech katika Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
 Meneja wa Miradi wa Magilatech , Godwin Mloka akizungumza na wananchi kuhusiana na ugunduzi wa technolojia Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Afisa wa Tehama wa Costech Alfred Nyoni akizungumza na wananchi waliotembelea banda la Costech katika Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

MAKAMU WA RAIS AWASILI MKOANI SONGWE KWA ZIARA YA KIKAZI

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili mkoani Songwe na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa Songwe Mhe. Lt. Mstaafu Chiku Galawa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makala na Viongozi wengine wa Chama na Serikali katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Songwe. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimia baadhi ya viongozi wa Chama cha CCM,mara baada ya kuwasili mkoani Songwe na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa Songwe Mhe. Lt. Mstaafu Chiku Galawa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makala na Viongozi wengine wa Chama na Serikali katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Songwe. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

RAIS DKT MAGUFULI ATOA POLE KWA RAIS MSTAAFU DKT KIKWETE KWA KUFIWA NA BABA MZAZI WA MKEWE MAMA SALMA KIKWETE

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alipofika kutoa pole kwa kufiwa na baba mzazi wa mkewe Mama Salma Kikwete, Marehemu Mzee Rashid Mkwachu, nyumbani kwa wafiwa Msasani jijini Dar es salaam leo Julai 21, 2018
 Mama Janeth Magufuli, Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alipofika kutoa pole kwa kufiwa na baba mzazi wa mkewe Mama Salma Kikwete, Marehemu Mzee Rashid Mkwachu, nyumbani kwa wafiwa Msasani jijini Dar es salaam leo Julai 21, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole mke wa Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mama salma Kikwete, kwa kufiwa na baba yake mzazi Marehemu Mzee Rashid Mkwachu, nyumbani kwa wafiwa Msasani jijini Dar es salaam leo Julai 21, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli, Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete na wanafamilia wakiomba dua walipofika kutoa pole kwa kufiwa na baba mzazi wa mkewe Mama Salma Kikwete, Marehemu Mzee Rashid Mkwachu, nyumbani kwa wafiwa Msasani jijini Dar es salaam leo Julai 21, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mama Janeth Magufuli wakiagana na mke wa Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Mama Salma Kikwete baada da ya kutoa pole kwa kufiwa na baba yake mzazi  Marehemu Mzee Rashid Mkwachu, nyumbani kwa wafiwa Msasani jijini Dar es salaam leo Julai 21, 2018

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na ndugu wa  Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete baada da ya kutoa pole kwa kufiwa na baba yake mzazi  wa Mama Salma, Marehemu Mzee Rashid Mkwachu, nyumbani kwa wafiwa Msasani jijini Dar es salaam leo Julai 21, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mama Janeth Magufuli wakisindikizwa na Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete baada ya kutoa pole kwa kufiwa na baba yake mzazi  Mama Salma, Marehemu Mzee Rashid Mkwachu, nyumbani kwa wafiwa Msasani jijini Dar es salaam leo Julai 21, 2018. Picha na IKULU

CHUO CHA KODI WAANZISHA KLABU MPYA KATIKA SHULE ZA SEKONDARI NA VYUO ILI KUJENGEA UWELEWA WANAFUNZI KUHUSU KODI

0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

CHUO Cha Kodi (ITA)kimeanzisha klabu mpya katika shule za sekondari na vyuo ili kuanza kuwajenga na kuwaandaa  wanafunzi kujifunza masuala mbalimbali yanayohusu kodi na umuhimu wake kwa Taifa.

Akizungumza katika Maonyesho ya 13 ya Vyuo Vikuu ya Elimu ya Juu Tanzania (TCU)yanayofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam Ofisa Udahili wa ITA Pascal Gomba amesema kila mwanannchi anahitajika kujua elimu ya kodi ili awe analipa kodi kwa wakati.

"Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)iliamua kuanzisha klabu za wanafunzi mashuleni kwa ajili ya kueneza elimu kwa watu wengi zaidi.Tunaamini utararibu huu utaongeza chachu ya wananchi kulipa kodi kwa maslahi ya Taifa letu,"amesema.Gomba amefafanua klabu hizo zimeanzia kwa shule za sekondari zilizopo Mkoa wa Dar es Salaam na ametaja baadhi ya shule hizo ni Jangwani,Zanaki,Kibasila,Kisutu,Loyora na Makongo.

"Kujiunga katika klabu za kodi ni moja ya mikakati ya TRA kuhakikisha elimu ya kodi inafahamika kwa kila mwananchi kuanzia ngazi ya wanafunzi hadi watu wazima,"ameongeza  Gomba.Wakati huo huo amesema uchumi wa Tanzania unakuwa kwa sababu ya ukusanyaji mzuri wa kodi na wananchi wenyewe kujituma kulipa kodi kwa hiari.

Hata hivyo Gomba amewataka wanafunzi kujiunga katika chuo cha ITA kwani  Serikali inahitaji zaidi wataalamu wa ukusanyaji wa kodi kwa manufaa ya taifa.Kuhusu uwepo wao kwenye maonesho hayo, Gomba amesema lengo kuu ni kuwaonesha wanafunzi na wananchi kwa ujumla kozi zinazotolewa katika chuo chao.

Amesema taasisi za Serikali na za binafsi zinahitaji mtu mwenye ujuzi wa ukusanyaji wa kodi kwa ajili ya kufanya shughuli zao za uzalishaji.

"Kuna umuhimu mkubwa kwa vijana wa Tanzania na hata wale watu wazima kujiunga katika Chuo cha Kodi,"amesema na kuongeza kwa sasa wanaendelea kupokea wanafunzi kwa ajili ya mwaka wa masomo wa 2018.

Moja ya maofisa wa chuo cha kodi akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda hilo.

CHUO CHA MAJI WAHIMIZA VIJANA WALIOSOMA MASOMO YA SAYANSI KUJIUNGA KATIKA CHUO HICHO

0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii.

CHUO cha Maji kimesema changamoto kubwa iliyopo katika sekta ya maji nchini ni uhaba wa watalaamu ,hivyo jukumu la chuo hicho kuendelea kuandaa watalaamu  ambao watakuwa watakuwa wamebobea katika eneo sekta ya maji ili kuondoa changamoto hiyo.

Katika kuhakikisha changamoto hiyo inamalizwa Chuo hicho kimetoa rai kwa Watanzania na hasa vijana ambao wamesoma masomo ya sayansi na kufaulu vizuri wakajiunga na chuo hicho kwani tayari wameanza kupokea maombi ya wanaotaka kujiunga na chuo hicho kwa mwaka wa masomo unaonza 2018.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam katika Maonyesho ya 13 ya Vyuo Vikuu ya Elimu ya Juu Tanzania (TCU) na Ofisa Masoko wa Chuo cha Maji Ghanima Chanzi.Amesema kuwa chuo hicho kimedhamiria kuondoa changamoto hiyo kuwa kuhakikisha wanapatikana wahitimu waliohitimu masomo yanayotolewa na chuo hicho kwa ajili ya kulitumikia taifa kaika eneo la sekta ya maji.

"Wapo watalaam ambao wanatoa huduma katika eneo hilo lakini bado kuna changamoto kubwa , hivyo jukumu letu ni kuwapika watalaam ambao ndio wenye kujua vema eneo la maji."Hivyo kadri ambavyo wahitimu wataendelea kumaliza chuoni hapo watakwenda kuondoa changamoto maana tutakuwa tunaongeza watalaam mwaka hadi mwaka.Hivyo kikubwa tunaomba Watanzania kujiunga kwenye chuo chetu  ili waje kuwa wahandisi wa maji,"amesema.

Hivyo amesisitiza wanafunzi wasome masomo ya sayansi ili wawe wataalam wa maji na kufafanua wameanza kupokea maombi kupitia tovuti ya www.waterinstitute.ac.tz.Amefafanua wanafunzi wanaosoma masuala ya maji katika chuo cha maji wengi wao wanapata ajira kwani wanahitajika zaidi na kueleza waliohitimu mwaka jana hakuna ambaye amebaki mtaani.

Kuhusu mafunzo yanayotolewa chuoni hapo amesema yapo katika ngazi ya Stashahada na Shahada na baadhi ya kozi zinazotolewa ni Uhandisi wa usambazaji maji na usafi wa mazingira,Uhandisi na umwagiliaji, Ubora wa maji (maabara),Maji na hali ya hewa na Uchimbaji visima.

Moja wa Maofisa wa chuo cha maji akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea katika banda lao katika maonesho ya vyuo vikuu yanayofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Viewing all 109591 articles
Browse latest View live




Latest Images