Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

MADAKTARI BINGWA WA MAGONJWA YA MOYO WA TAASISI YA JKCI WATOA HUDUMA ZA MATIBABU MAONYESHO YA SABASABA

$
0
0
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Delila Kimambo akitoa huduma ya ushauri kuhusu namna ya kuepukana na magonjwa ya moyo wakati wa maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo katika Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Katika Banda la Taasisi hiyo huduma za matibabu ya moyo zilitolewa bila malipo yoyote zikiwemo dawa kwa wagonjwa wanaokutwa na matatizo.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha ubora wa huduma Tulizo Shem wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) akitoa elimu kwa wananchi kuhusu magonjwa ya moyo wakati wa maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara yaliyomalizika hivi karibuni katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo katika Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Katika maonyesho hayo Taasisi hiyo ilishika nafasi ya tatu katika utoaji wa huduma kwa wananchi, huduma za matibabu ya moyo zilitolewa bila malipo yoyote zikiwemo dawa kwa wagonjwa wanaokutwa na matatizo.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Pedro Pallangyo akimwelekeza mtoto kujibu maswali kuhusu afya bora ya moyo wakati wa Maonyesho ya Kimataifa ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere yaliyomalizika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Wananchi waliotembelea banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakipata huduma ya matibabu ya moyo wakati wa maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara yaliyomalizika hivi karibuni katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo katika Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Katika maonyesho hayo Taasisi hiyo ilishika nafasi ya tatu katika utoaji wa huduma kwa wananchi kwa kutoa huduma bila malipo yoyote zikiwemo dawa na rufaa ya moja kwa moja kwa wagonjwa wanaokutwa na matatizo. Picha na JKCI

TRA YAKUSANYA TRILIONI 15.5 KWA MWAKA WA FEDHA 2017/18

$
0
0
Na Veronica Kazimoto,Dar es Salaam

Makusanyo ya kodi kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/18 yameongezeka hadi kufikia shilingi trilioni 15.5 kutoka shilingi trilioni 14.4 kwa Mwaka wa Fedha 2016/17 sawa na ongezekeo la asilimia 7.5.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa ya makusanyo ya kodi ya mwaka wa fedha 2017/18, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Richard Kayombo amesema kuwa katika mwezi Juni, 2018 pekee, TRA imekusanya jumla ya shilingi trilioni 1.5 ikilinganishwa na shilingi trilioni 1.4 kwa mwezi Juni, 2017 ambayo ni sawa na ukuaji wa asilimia 8.0.

“TRA inapenda kuwapongeza na kuwashukuru walipakodi wote ambao mchango wao umeiwezesha Serikali kupata mapato haya tunayotangaza leo kwa ajili ya kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo na za jamii zikiwemo ujenzi wa miundombinu ya reli na barabara, ununuzi wa ndege, upatikanaji wa elimu, afya na mambo mengine kwa manufaa ya watanzania wote,” alisema Kayombo.

Kayombo amezitaja sababu zilizosababisha kuongezeka kwa makusanyo hayo kuwa ni pamoja na elimu ya kodi kuzidi kueleweka kwa walipakodi na wananchi kwa ujumla, kuongeza ukaribu na walipakodi kwa kuwasikiliza na kutatua changamoto zao za kikodi, kuongezeka kwa walipakodi wapya kupitia kampeni ya kuwasajili kwa kuwafuata waliko na kurahisisha ulipaji wa kodi kwa njia ya kielektroniki.

Aidha, Mkurugenzi huyo alisema kuwa, katika Mwaka huu wa Fedha 2018/19, TRA imedhamiria kutekeleza kwa vitendo kampeni kabambe ya msamaha wa riba na adhabu kwa malimbikizo ya madeni ya nyuma na inategemea kuongeza urahisi wa kulipa madeni ambayo yalikuwa kikwazo kwa wafanya biashara wengi kulipa na hata kuendelea na biashara.

“Vilevile, mamlaka imedhamiria kuongeza kasi ya usajili wa walipakodi wapya. Hivyo, tunaendelea na kasi ya utambuzi na usajili wa wafanyabiashara wadogo ili kila mtu anayestahili kulipa kodi asajiliwe na kuchangia kikamilifu maendeleo ya Taifa,” alieleza Kayombo.

Mkurugenzi Kayombo ametoa wito kwa walipakodi na wananchi wote kuendelea kulipa kodi kwa hiari na kujenga utamaduni wa kudai Risiti za Kielektroniki za Kutolea Risiti (EFDs) kila mfanyabiashara anapofanya mauzo na mnunuzi anatakiwa kudai risiti kila anaponunua bidhaa na huduma mbalimbali.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Richard Kayombo akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa ya makusanyo ya kodi ya Mwaka wa Fedha 2017/18 ambayo yameongezeka hadi kufikia shilingi trilioni 15.5 kutoka shilingi trilioni 14.4 kwa Mwaka wa Fedha 2016/17 sawa na ongezekeo la asilimia 7.5.
Mmoja wa waandishi wa habari akiuliza swali wakati wa Mkutano wa waandishi hao ulioandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambapo Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Bw. Richard Kayombo (hayupo pichani) leo ametoa taarifa ya makusanyo ya kodi ya Mwaka wa Fedha 2017/18 ambayo yameongezeka hadi kufikia shilingi trilioni 15.5 kutoka shilingi trilioni 14.4 kwa Mwaka wa Fedha 2016/17 sawa na ongezekeo la asilimia 7.5. (PICHA NA TRA). 

BENKI YA CREDIT SUISSE KUIPATIA TANZANIA MKOPO WA DOLA MILIONI 200

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango akipokea picha ya alama ya ushirikiano ya kiasi cha Dola 500 kutoka kwa Afisa mwandamizi wa Benki ya Suisse ya Uingereza Bi. Elizabeth Muchemi, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Mchumi Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Omary Khama (kulia), anayeshughulika na maswala ya uchambuzi wa madeni akimwelezea Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kulia) kuhusu miradi mbalimbali itakayotekelezwa kutokana na pesa iliyopatikana, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Benki ya CREDIT SUISSE.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (kulia) akimshukuru Mkurugenzi Mkuu wea Benki ya Suisse Bw. Lawrence B. Fletcher kwa mikopo mbalimbali ambayo Benki hiyo imetoa kwa Serikali ya Tanzania katika Sekta mbalimbali, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.

Msajili Baraza la Uuguzi na Ukunga Nchini Atembelea Vituo vya Afya

$
0
0
Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Bi. Agnes Mtawa ametembelea Mkoa wa Shinyanga pamoja na Wilaya ya Kahama na vituo vya afya kwa nia ya kuangalia shughuli zinazofanywa na wauguzi na wakunga wa kada mbalimbali pia kuzungumza nao.

Msajili alikutana na baadhi ya wauguzi katika vituo vyao vya kazi na kuwasisitizia kuzingatia maadili wanapowahudumia wagonjwa. Pia, alifanya mkutano Mjini Kahama katika Hospitali ya wilaya na aliwakumbusha wauguzi na wakunga juu ya majukumu ya Baraza la Uuguzi na Ukunga pamoja na Misingi ya utoaji huduma ya Uuguzi na Ukunga yaani (Professional code of conduct, the guiding principles).

Katika hatua nyingine, aliwataka wauguzi na wakunga kuwa na leseni inayowaruhusu kutoa huduma, lakini pia alikemea vikali watu wanaoghushi vyeti na leseni za uuguzi na ukunga.Msajili alipata nafasi ya kujibu maswali mbalimbali ya kiutendaji pamoja na sheria inayoongoza taaluma ya uuguzi na ukunga.

Pia, alitembelea pia Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga na kuonana na wauguzi na wakunga katika maeneo yao ya kutolea huduma na kujibu maswali mbalimbali yanayohusu taaluma ya uuguzi na ukunga, sheria inayoongoza taalama ya uuguzi na ukunga nchini.
Msajili Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Bi. Agnes Mtawa akiwa ziarani mkoani Shinyanga kwa ajili ya kuzungumza na wauguzi pamoja na wakunga kuhusu utoaji wa huduma bora.
Wauguzi na wakunga wa Wilaya ya Kahama wakijiandaa kumsikiliza Msajili Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Bi. Agness Mtawa.

SERIKALI YASHAURIWA KUWEKEZA KWA WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU

$
0
0

Na Pamela Mollel,Arusha

Serikali imeshauriwa kuangalia uwezekano wa kuanza kuwekeza kwa watoto hasa wanaoishi katika mazingira Magumu ili kuepusha dhana ya kuwa na taifa lenye watoto ombaomba.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu Wa Nchi wa Shirika la Compassion Nchini, Agnes's Hotay alipokuwa kwenye Mahafali ya Nne ya kuondoka kwenye ufadhili Wa shirika hilo kwa watoto waliokuwa wakilelewa kwenye Klasta ya USA River, wilayani Arumeru, Mkoa wa Arusha baada ya kufikisha umri Wa Miaka 22 .

Hotay amesema kuwa ipo haja kwa serikali kuunga mkono jitihada zinazoonyeshwa na Mashirika , taasisi mbalimbali katika kuwahudumia watoto waliopo katika mazingira magumu kwa kuwapatia elimu na ujuzi ili waweze kujiajiri ,jambo litakalosaidia kupunguza namba ya vijana wasio na ajira .

Amesema shirika hilo hapa nchini limeifikia mikoa 17 na linafanya kazi na makanisa wenza zaidi ya 400 na linahudumia watoto zaidi ya 93,000 ikiwa lengo ni kuwaondoa watoto kwenye umasikini na kuwajengea uwezo Wa kujitegemea,kujikinga na maradhi na kuwajenga kiuchumi.

Alitoa rai kwa wahitimu kuhakikisha wanakuwa waadilifu kwa kuzingatia yale mema yote waliofundishwa na walimu wao.Awali katika risala ya wahitimu hao wapatao 78 walilishukuru shirika la Compassion kwa ufadhili huo ambao umewasaidia kuwajenga kiroho,kuwapatia Elimu ya ujasiliamali na kutaka makanisa mengine kuinga mfano huo utakao saidia kupunguza changamito za vijana.

Naye Mwenyekiti wa Klasta ya USA River ,Saluni Kisangas amesema Shirika hilo kwa kushirikiana na Makanisa wenza limekuwa likiwahudumia watoto tangia wakiwa na umri mdogo wa kuingia chekechea na punde wanapofikisha umri wa miaka 22 wanaamini umri huo wanastahili kujitegemea.

Aidha amesema katika Klasta ya USA River inayohudumia kata 4 ,tangia kuanzishwa kwa Klasta hiyo mwaka 1999 ambapo wahitimu wengi wamenufaika na Mpango huo kwa kupata ajira serikalini na baadhi yao kuchukuliwa na mashirika Mbalimbali.
Mkuu Wa Nchi wa Shirika la Compassion Nchini, Agnes's Hotay akizungumza katika Mahafali ya Nne ya kuondoka kwenye ufadhili Wa shirika hilo kwa watoto waliokuwa wakilelewa kwenye Klasta ya USA River, wilayani Arumeru, Mkoa wa Arusha .
Wahitimu

RAIS MAGUFULI KUFUNGUA MKUTANO WA KIDUNIA WA VYAMA VYA KISIASA JIJINI DAR

$
0
0


Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii
 
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Rais wa Jamhuri ya Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kufungua Mkutano wa Kidunia wa Vyama vya Siasa (Mkutano maalum kwa Kanda ya Afrika) uliondaliwa na Chama cha Kikomonisti cha Watu wa China (CPC).
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema kuwa Mkutano huo utakao husisha Vyama 40 utakuwa wa kwanza kufanyika nje ya China na wa pili baada ya ule wa uliofanyika China.

Polepole amesema ni heshima kubwa kwa Serikali ya Tanzania, Nchi na Chama cha Mapinduzi (CCM) kutokana na Mkutano huo kuhusisha pia washiriki zaidi ya 200 kutoka Afrika na nje ya Afrika.

Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Uhusiano wa Afrika (IDCPC), Wang Heming amesema kuwa Mkutano huo unafanyika Tanzania ni kutoka ushirikiano mzuri ulikuwepo baina ya China na Tanzania, pia Tanzania ni nchi ambayo imehusika katika Ukombozi wa Bara la Afrika.


Mkutano huo unatarajiwa kufanyika siku mbili ambapo utafunguliwa na Rais Magufuli, kesho Julai 17 na kufungwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi atakayemuwakilisha Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu mkutano wa kidunia wa vyama kiaiasa vya Barani Afika kwa ushirikiano na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC). Kushoto ni Mkurugenzi wa wa Mawasiliano kwa Umma, Sun Haiyan na kulia ni Naibu Mkurugenzi mkuu wa Uhusiano wa Afrika (IDCPC) Wang Heming.

Mkurugenzi wa wa Mawasiliano kwa Umma, Sun Haiyan(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu mkutano wa vyama vya siasa vipavyo 38 vilivyofika kuudhuria mkutano huo utakaofanyika kesho katika ukumbi wa hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

WAZIRI MKUU AMWAGIZA RPC SHINYANGA AWAKAMATE VIONGOZI TISA WA AMCOS YA USHETU

$
0
0
*Ni kwa upotevu wa dola za Marekani 21,000
*Wakimbia mkutano baada ya wananchi kuzomea

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Simon Haule awakamate viongozi wa Chama cha Msingi cha Mkombozi kwa upotevu wa dola za marekani 21,000 za chama hicho.

"Wabebe hawa watu, wahoji waseme hiyo fedha iko wapi na jambo la kwanza wailete hiyo fedha ya wakulima. Wakishindwa kurejesha fedha, wawekwe ndani," amesema.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumatatu, Julai 16, 2018) wakati akizungumza na mamia ya wananchi wa kijiji cha Kangeme, kata ya Ulowa katika Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama ambao alienda kuzindua mpango wa Ushirika Afya na NHIF.

Waziri Mkuu amefikia uamuzi huo baada ya kuwaita viongozi wa chama cha Mkombozi watoke hadharani na kubaini kuwa hakuwepo hata mmoja. Inadaiwa kwamba walitoroka baada ya wananchi kuanza kuzomea. 

Kamanda Haule amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Mwenyekiti, Bw. Shilinde Abdallah na mhasibu wa AMCOS hiyo, Bw. Kulwa Shinzi pamoja na wajumbe saba wa bodi ya chama hicho.

Akiwa katika tukio hilo, Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Kahama (KACU), Bw. Emmanuel Cherehani alisoma taarifa ya Chama na alipotaja bei ya tumbaku kuwa ni nzuri, wananchi walimzomea kupinga kile alichokisema. Bw. Cherehani alikuwa akitoa mafanikio ya chama hicho, na kusema kuwa bei ya tumbaku ni nzuri.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba. (kushoto) wakati alipokagua uuzaji wa tumbaku katika Chama cha Ushirika cha Msingi cha Kangeme katika Halmashauri ya Ushetu, Julai 16, 2018. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telack na wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya Maendeloeo ya Ushirika Nchini, Dkt. Titus Kamani. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kangeme kwenye Halmashauri ya Ushetu mkoani Shinyanga, Julai 16, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Fao la Ushirika Afya ambalo litawawezesha wanaushirika kunufaika na huduma zinazotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, kwenye kijiji cha Kangeme katika Halmashauri ya Ushetu mkoani Shinyanga Julai 16, 2018. Kushoto kwake ni Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba, watatu kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsi, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Bernard Konga.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi baada ya kukagua ujenzi wa zahanati ya Ukune katika Halmashauri ya Ushetu mkoani Shinyanga, Julai 16, 2018.

Rais Magufuli awaagiza viongozi wa mkoa wa Pwani na Dar es Salaam kutatua changamoto ya wafanyabiashara kando ya Morogoro road

$
0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mamia ya wananchi wa Mbezi Mwisho waliosimama katikati barabara ya Morogoro kuhusu kero zao mbalimbali wakati akitokea Kibaha Kwa mfipa mkoani Pwani ambapo aliweka jiwe la Msingi ujenzi wa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere. 
Wananchi mbalimbali wakikimbilia msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kusimama katika eneo la Mbezi Mwisho ambapo aliwahutubia wananchi hao.
Wanchi wa Mbezi Mwisho wakishangilia wakati msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ulipokuwa ukipita katika eneo la Mbezi mwisho jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Kibaha maili moja wakati akitokea Kibaha kwa mfipa mkoani Pwani ambapo aliweka jiwe la Msingi ujenzi wa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere. PICHA NA IKULU 



RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI CHUO CHA UONGOZI CHA MWALIMU JULIUS NYERERE KINACHOJENGWA KIBAHA KWA MFIPA MKOANI PWANI.

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli amesema kuwa ukombozi kwa ajili ya Uhuru ulishapita sasa ni ukombozi wa maendeleo ya Kiuchumi.

Rais Dk. Magufuli ameyasema hayo leo wakati wa kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Chuo cha Mwalimu Julius Nyerere Kinachojengwa Kwa Mufipa , Kibaha mkoani Pwani, amesema kuwa chuo hicho kikamilika kitasaidia kutoa elimu kwa makada na viongozi.

Chuo hicho kinajengwa nchini mahsusi kwa ajili vyama sita vilivyopigania ukombozi wa Afrika kwa kupata msaada na China.Vyama hivyo vilivyopigania ukombozi wa Afrika ni ZANU PF ya Zimbabwe, SWAPO - Namibia, AMPLA- Angola, ANC- Afrika Kusini pamoja na FRELIMO- Msumbiji

Katika uzinduzi huo makatibu wa Wakuu wa Vyama vya Ukombozi walihudhuria wakiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Chama cha CPC cha nchini China.Amesema kuwa CPC imekuwa mstari mbele lakini wamekwenda mbele kiuchumi.

Amesema kuwa katika chuo hicho watazaliwa wakina Nyerere wapya na Nelson Mandela , Agustino Netho na Samora Machel.Rais Magufuli amewagiza Makatibu wa Wakuu wa Vyama hivyo kufanya maandalizi mapema ya mitaala pamoja na wakufunzi ili Chuo kikamilika kila kitu kimekamilika.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri wa uhusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao wanne kutoka kushoto pamoja na Makatibu wa vyama vya, CCM, ANC, SWAPO, ZANU-PF, MPLA, FRELIMO, wakiweka mchanga kama ishara ya uwekaji wa Jiwe la msingi Ujenzi wa Chuo cha Mwalimu Julius Nyerere kinachojengwa katika eneo la Kibaha kwa mfipa mkoani Pwani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na mgeni wake Waziri wa uhusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao wanne kutoka kushoto waliokaa, viongozi wa vyama vya ANC, SWAPO,ZANU-PF, MPLA, FRELIMO pamoja na viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi CCM mara baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere kinachojengwa katika eneo la Kibaha kwa mfipa mkoani Pwani. Chuo hicho kinajengwa na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kwa gharama ya Shilingi Bilioni mia moja(100). 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mgeni wake Waziri wa uhusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao kabla ya tukio la uwekaji jiwe la msingi ujenzi wa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere kinachojengwa katika eneo la Kibaha kwa mfipa mkoani Pwani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma pamoja Sophia Shaningwa Katibu wa Chama cha SWAPO kutoka nchini Namibia huku Waziri wa uhusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao akipiga makofi mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere kinachojengwa katika eneo la Kibaha kwa mfipa mkoani Pwani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia mfano wa moja ya majengo ya chuo hicho kitakapo kamilika kujengwa. PICHA NA IKULU

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA 

BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU 16.07.2018

WAZIRI MKUU AMTAMBULISHA MKUU WA WILAYA YA KAHAMA KWA WANANCHI NA KUWEKA JIWE LA MSINGI LA KITUO CHA AFYA CHA CHELA WILAYANI KAHAMA.

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipoweka  jiwe la Msingi la Kituo cha Afya cha Chela katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama Julai 17, 2018. Watatu kushoto ni  Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige na watano kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kahama, Anamringi Macha na watatu kulia ni Mwenyeiiti wa CCM wa Mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa. Kushoto ni  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Elius Kwandikwa wapili kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Joseph Kakunda.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la Msingi la Kituo cha Afya cha Chela katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama Julai 17, 2018. Kulia ni Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack. 
 Mkuu wa wilaya ya Kahama, Anamringi Macha akiwatambulisha viongozi wa wilaya ya Kahama wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipowasalimia wananchi wa Kijiji cha Chela baada ya kuweka jiwe la Msingi la Kituo cha Afya cha Chela katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama Julai 17, 2018. Wanne kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack na kulia ni Mbunge wa Msalala Ezekiel Maige. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimtambulisha Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha  wakati alipoweka jiwe la Msingi la Kituo cha Afya cha Chela katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama Julai 17, 2018. Mkuu huyo wa wilaya aliapishwa jana asubuhi na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Teklack.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI NCHINI AKUTANA NA KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CGF) Thobias Andengenye atembelewa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP) Phaustine Kasike mapema leo asubuhi katika Makao Makuu ya Jeshi hilo yaliyopo jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi barabara ya ohio jijini Dar es Salaam. Lengo ni kujitambulisha na kukuza mahusiano kati ya vyombo hivyo viwili vya Ulinzi na Usalama.
Katika ziara hiyo Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye, alitumia fursa hiyo kumpongeza kwa kuteuliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Kamishna Jenerali wa Magereza na kumuahidi ushirikiano katika kulijenga Taifa. 
Vilevile Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike amepata fursa ya kujifunza jinsi gani Jeshi hilo linavyoendesha shughuli zake pamoja na kufanya mazungumzo ya kina na Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo.
 “Nimejifunza mengi lakini pia nashukuru kwa kupata fursa ya kutembelea na kuona ni jinsi gani tunaweza kushirikiana” alisema Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye(kulia) akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike(kushoto), baada ya kuwasili Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji yaliyopo jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi barabara ya ohio jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike(kulia) akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji yaliyopo jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi barabara ya ohio jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara yake ya kujitambulisha na kukuza mahusiano katika vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, (Kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI, KAMISHINA WA JESHI LA POLISI ZANZIBAR WALA KIAPO CHA UJUMBE TUME YA UTUMISHI

$
0
0
 Katibu Mkuu Wazira ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu akisalimiana na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Dr. Eliezer Feleshi, wakati alipoenda kuapishwa kuwa Mjumbe wa Tume ya Utumishi Jeshi la Polisi, Magereza pamoja na Uhamiaji jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu WazirI ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, akila kiapo cha uadilifu mbele ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Dk. Eliezer Feleshi kuwa Mjumbe wa Tume ya Utumishi kwa Jeshi la Polisi, Magereza, pamoja na Uhamiaji. Kiapo hicho kilifanyika katika ofisi za Mahaka Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Wazira ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu akisaini karatasi la kiapo cha kuwa Mjumbe wa Tume ya Utumishi kwa Jeshi la Polisi, Magereza, pamoja na Uhamiaji, pembeni ni Jaji Kiongozi, Dk. Eliezer Feleshi wa Mahakama Kuu ya Tanzania aliyesimamia kiapo hicho katika Ofisi za Mahakama Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam.
 Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibara, Mohamed Haji Hassan akila kiapo cha uadilifu mbele ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Dr. Eliezer Feleshi kuwa Mjumbe wa Tume ya Utumishi kwa Jeshi la Polisi, Mageereza, pamoja na Uhamiaji. Kiapo hicho kilifanyika katika ofisi za Mahaka Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika Ofisi za Mahakama Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam alipofika ofisini hapo kwaajili ya kula kiapo cha uadilifu kama mjumbe wa tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi, Magereza na Uhamiaji. Wa kwanza (kulia) ni  Jaji Kiongozi, Dk. Eliezer Feleshi wa Mahakama Kuu ya Tanzania akifuatiwa na Mohamed Haji Hassan, Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu akifafanua jambo kwa Jaji Kiongozi, Dk. Eliezer Feleshi wa Mahakama Kuu ya Tanzania wakati alipoenda kula kiapo cha kuwa Mjumbe wa Tume ya Utumishi kwa Jeshi la Polisi, Magereza na Uhamiaji, katikati ni Mohamed Haji Hassan Kamishna wa jeshi la Polisi Zanzibar. (Picha na Mambo ya Ndani)

MIPANGO YA MATUMIZI BORA YA ARDHI KWA VIJIJI VINAVYOZUIZUNGUKA HIFADHI YA SERIKALI KUU WAJA

$
0
0


Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Matumizi Bora ya Ardhi Dkt. Stephen Nindi (aliyekaa) akimsikiliza kwa makini Mtendaji Mkuu wa TFS, Prof. Dos Santos Silayo alipokuwa akiwasisitiza wajumbe wa kikao kazi kwa ajili ya kuhakikisha kunakuwepo na mipango ya matumizi bora ya ardhi kwa vijiji 120 vinavyozunguka misitu ya Hifadhi ya Serikali Kuu mapema jana.

wajumbe wa kikao kazi

WAZIRI MAHIGA APOKEA NAKALA ZA HATI ZA UTAMBULISHO KUTOKA KWA BALOZI MTEULE WA KENYA HAPA NCHINI

$
0
0
Balozi Mteule wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu akiwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb.). Mara baada ya kuwasilisha nakala hizo Mhe. Mahiga na Balozi Kazungu walipata fursa ya kuzungumza kuhusu kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya hususan kwenye sekta za biashara, uchumi na elimu. Tukio hilo lilifanyika kwenye Ofisi Ndogo ya Wizara iliyopo Jijini Dar es Salaam tarehe 16 Julai, 2018. 
Dkt. Mahiga akiendelea na mazungumzo na Balozi Mteule wa Kenya hapa nchini 
Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mazungumzo kati ya Dkt. Mahiga na Balozi Mteule wa Kenya nchini. Kushoto ni Bibi Judica Nagunwa na Bw. Magabilo Murobi 


NHIF KAGERA WATOA MSAADA WA VIFAA VYA UJENZI KWA KITUO CHA KULELEA WAZEE.

$
0
0
Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kagera

MFUKO wa Taifa wa Bima ya afya(NHIF) Mkoa wa Kagera wamekabidhi msaada wa vifaa vya ujenzi kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za watumishi wanaosaidia wazee katika kituo cha kulelea wazee cha kilima kilichopo halmashauri ya Wilaya ya Bukoba. 

Meneja wa mfuko wa bima ya afya(NHIF)Kagera Elias Odhiambo alisema kuwa huo ni utekelezaji wa ahadi ilitolewa na mfuko katika harambee ya kuchangisha fedha na vifaa vya ujenzi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za watumishi kwenye kituo cha kulelea wazee cha kiilima ambazo ziliathiriwa na tetemeko la ardhi ambapo harambee hiyo iliendeshwa na Naibu Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia na watoto Faustine Andungulile.

"NHIF leo tumetimiza ahadi yetu tuliyotoa ya kutoa msaada wa vifaa vya ujenzi kwaajili ya ujenzi wa nyumba za watumishi katika kituo hiki,hii ni sehemu ya misaada inayotolewa na mfuko kusaidia jamii katika shughuli mbalimbali za maendeleo,naamini msaada huu utasaidia ujenzi wa makazi haya"alisema

Odhiambo alisema vifaa walivyokabidhi ni mifuko 100 ya sementi na mabati 50 vifaa hivyo vyote vinathamani ya shilingi 3,100,000.Baada ya kupokea msaada huo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Salum Kijuu aliushukuru uongozi wa mfuko wa bima ya afya(NHIF)kwa kutimiza ahadi yao waliyo haidi kwa wakati.

"Meneja ninakuomba nifikishie shukrani zangu kwa Mkurugenzi mkuu wa mfuko mmetekeleza ahadi yenu mliyotoa ndani ya wakati ili kufanikisha zoezi hili la ujenzi"alisema.Kijuu aliwataka wakandarasi kuhakikisha ujenzi unafanyika kwa kasi na kukamilika kwa wakati aliwaomba pia wadau wengine kuendelea kutoa misaada ili ujenzi huo uweze kukamilika.
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali  Mstaafu Salum Kijuu  akipokea vifaa vya ujenzi ikiwemo saluji na mabati kutoka kwa Meneja wa mfuko wa bima ya afya (NHIF) Kagera Elias Odhiambo kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Kulelea Wazee 
  Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu  akiwasalimia baaddhi ya Wazee walioko kwenye kituo chao  
Sehemu ya ujenzi wa kituo hicho ukiendelea

WIZARA YA AFYA KUPELEKA MILIONI 300 HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA TABORA

$
0
0
Na .WAMJW-Tabora

Serikali kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto inatarajia kupeleka shilingi milioni 300 kwenye hospitali ya rufaa ya Mkoa ya Kitete kwa ajili ya kupanua wodi ya wazazi pamoja na ununuzi wa vifaa vya upasuaji kwa kumtoa mtoto tumboni Mkoani humo

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati alipotembelea hospitali hiyo ziara ya kikazi mkoani hapa.

"tutaleta fedha hizi kabla ya desemba mwaka huu ili kuhakikisha kila mwanamke mjamzito anajifungua salama na mtoto wake anakua salama pia"alisema Waziri Ummy.Aidha,aliwaagiza hospitali hiyo kununua vifaa vyote muhimu vinavyowezekana kuliko kusubiri wizara iwaletee'lazima mjiongeze na kuwa wabunifu muwe na vitu muhimu ili msonge mbele'alisisitiza

Hata hivyo aliwataka watumishi hao kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na miiko ya utumishi wa umma ili kuondoka malalamiko kwa wananchi wanaofika kupata huduma katika hospitali hiyo.
 Picha jengo la upasuaji lililopo katika hospitali hiyo
 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt.Gunini Kamba akimueleza Waziri wa Afya vifaa vilivyofungwa kwenye chumba cha upasuaji vilivyofungwa kwenye jengo la Upasuaji lililojengwa hospitalini hapo
 Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akimbeba mtoto mchanga aliyezaliwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Kitete Mkoani Tabora

TRA YAJA NA MKAKATI MAALUM KUONGEZA MAPATO KUPITIA SEKTA YA UTALII

$
0
0
Na Rachel Mkundai, Arusha

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imekuja na mkakati maalum wa kuhakikisha kwamba pato la Serikali na kodi stahiki inapatikana kupitia sekta ya utalii nchini.

Akizungumza Jijini Arusha, Kamishna wa Kodi za Ndani, Bwana ELIJAH MWANDUMBYAamesema kwamba, sekta ya utalii ni moja ya sekta inayoiingizia Serikali fedha nyingi za kigeni na hivyo inahitaji mkakati madhubuti ili kuongeza pato kwa Serikali

“Sekta ya utalii inaingizia serikali fedha nyingi za kigeni, TRA tumekuja na mkakati maalum ili kuhakikisha kuwa sekta hii inachangia pato la taifa kupitia kodi stahiki kwa mujibu wa sheria za kodi”, amesema Kamishna wa kodi za ndani.

Mwandumbya ameongeza kuwa kwa muda mrefu sekta ya utalii imekuwa ikifanya vizuri lakini bado inahitaji mkakati wa kuhakikisha kwamba kila pato linaloingia kupitia sekta hii linaongeza tija kwenye mapato ya nchi kupitia kodi mbalimbali kama zilivyoainishwa na sheria za kodi.

Aidha, Kamishna Mwandumbya amefafanua kuwa moja ya mikakati hiyo ni kushirikiana na taasisi zingine za serikali zilizopo kwenye sekta ya utalii zikiwemo Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na Chama cha wafanyabiashara wa Utalii (TATO) pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii na wadau wengine wanaojihusisha na utalii.
Kamishna wa Kodi za Ndani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara ya Utalii (TATO), Bw. Wilberd Chambulo wakati wa ziara yake ya kikazi Jijini Arusha yenye lengo la kuongeza mapato ya Serikali kupitia sekta ya utalii nchini.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Arusha, Bw. Faustine Mdesa (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara ya Utalii (TATO), Bw. Wilberd Chambulo wakati wa ziara ya kikazi ya Kamishna wa Kodi za Ndani Jijini Arusha yenye lengo la kuongeza mapato ya Serikali kupitia sekta ya utalii nchini.
Kamishna wa Kodi za Ndani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya (kulia) akifanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara ya Utalii (TATO), Bw. Wilberd Chambulo wakati wa ziara yake ya kikazi Jijini Arusha yenye lengo la kuongeza mapato ya Serikali kupitia sekta ya utalii nchini.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara ya Utalii (TATO), Bw. Wilberd Chambulo (kushoto) akimwelezea jambo Kamishna wa Kodi za Ndani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya pamoja na watendaji wengine wa TRA aliofuatana nao kuhusu namna sekta ya utalii nchini inavyochangia pato kubwa kwa Serikali wakati wa ziara ya kikazi ya Kamishna huyo Jijini Arusha yenye lengo la kuongeza mapato ya Serikali kupitia sekta ya utalii nchini. (PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-TRA).

WAKONTA KAPUNDA ASIMULIA ALIVYOPATA AJALI YAKE

WAZIRI MKUU AZINDUA GHALA LA KUHIFADHIA MAZAO YA WAKULIMA KATIKA KIJIJI CHA BULIGE NA KUKAGUA SHAMBA LA DENGU JIMBO LA MSALALA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akikata utepe kuzindua ghala la kuhifadhia mazao ya wakulima katika kijiji cha Bulige kwenye Halmashauri ya Msalala, Julai 17, 2018.  Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kahama, Anamringi, Macha, wapili kushoto ni Mbunge wa Msalala, Ezekiel  Maige na  wanne kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum, Aza Hilal. Kulia ni Mbunge wa Viti Maalum, Lucy Mayenga na wapili kulia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,  Elius Kwandikwa. 
 Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiweka jiwe la Msingi la ghala la kuhifadhia mazao ya wakuliama katika kijiji cha  Bulige kwenye Halmashauri ya Msalala Juali 17, 2018. Anayemsaidia ni Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige na Kulia ni Mbunge wa Viti Maalum, Lucy Mayenga.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua shamba la dengu lenye ukubwa wa ekari 10, mali ya Bw. Philipo Kapande (wapili kushoto) katika kijiji cha Jomu kwenye Halmashauri ya Msalala Julai 17, 2018. Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack. Na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua shamba la dengu lenye ukubwa wa ekari 10, mali ya Bw. Philipo Kapande (kushoto) katika kijiji cha Jomu kwenye Halmashauri ya Msalala Julai 17, 2018. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images