Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109587 articles
Browse latest View live

WAZIRI MKUU: MUWAFUATE WANANCHI VIJIJINI

0
0
*Ataka watenge siku tatu hadi nne waende waliko wananchi
*Asema Serikali hii haitaki mambo ya urasimu

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watumishi wote wa Serikali za Mitaa nchini watenge theluthi mbili ya muda wao wa kazi kwa kuwasikiliza wananchi na kuwahudumia.

Ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Julai 15, 2018) wakati akizungumza na watumishi na viongozi wa Halmashauri za Wilaya za Ushetu, Msalala na Kahama Mji, wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

“Jukumu la watumishi ni kuwatumikia wananchi, Serikali hii hatutaki urasimu na wala hatutarajii kuwa mtatoa huduma kwa urasimu. Lugha ya ‘njoo kesho, njoo kesho’ siyo ya kwa awamu hii.”

Amesema Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya wana jukumu la kusimamia agizo hilo kwa kuhakikisha kuwa wanatoa usafiri kwa watumishi hao ili waweze kufika vijijini kwa haraka. “Wakurugenzi wa Halmashauri simamieni zoezi hilo kwa kupanga ratiba na kutoa gari ili maafisa wanne au watano watumie gari hilo kwenda vijijini wakawahudumie wananchi.”

Amesema wananchi wengi hawana uwezo wa kusafiri kutoka vijijini hadi mijini ili kuleta matatizo yao, kwa hiyo wakifanya hivyo, watumishi watakuwa wamewapunguzia matatizo wananchi.Waziri Mkuu ambaye yuko kwenye ziara ya siku tano ya kikazi mkoani humo, amewataka watumishi wa idara ya ardhi wapime ardhi kwa wingi na watoe hati mapema ili wananchi wazitumie kuongeza mitaji.

“Pimeni ardhi na kutoa hati ili wananchi wazitumie kukopa na kupata mitaji ya kujiendeleza kiuchumi. Pia muweke mipango mizuri ya ardhi ili kuepusha migogoro baina ya wananchi.Waziri Mkuu leo anaendelea na ziara yake wilayani Kahama kwa kukagua shughuli za maendeleo na kuzungumza na wananchi.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, JULAI 15, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea eneo la Viwanda la Bukondamoyo katika Kata ya Zongomela kwenye Halmashauri ya wilaya ya Kahama Julai 15, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

UKAGUZI WA MAGARI, LESENI NA OPARESHENI YA KUKAMATA MAKOSA YA USALAMA BARABARANI JIJINI MBEYA.

0
0
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kukabiliana na vitendo vya uhalifu na ajali za barabarani ili kuhakikisha kuwa wageni na wakazi wa Mkoa huu wanaendelea kuwa salama na mali zao. Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kushirikiana na wananchi na wadau wengine wa usalama hali inayopelekea kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu pamoja na ajali za barabarani. 

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea na Oparesheni ya kukagua magari pamoja na kukamata makosa mbalimbali ya ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani. Katika Oparesheni iliyofanyika mnamo tarehe 14.07.2018 kuanzia majira ya saa 05:00 alfajiri katika Stendi Kuu ya Mabasi jumla ya Mabasi 43 yaendayo Mikoa mbalimbali yamekaguliwa kati ya hayo 38 yaliruhusiwa kuendelea na safari wakati Mabasi 05 yaligundulika kuwa na hitilafu hivyo hayakuruhusiwa kuendelea na safari hadi yatakapo tengenezwa. 

Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanya Oparesheni ya kushtukiza katika maeneo ya Kabwe, Mwanjelwa, Isanga, Soweto, Uyole na Iyunga na kufanikiwa kukamata magari 45 kati ya hayo 29 yamekutwa na makosa mbalimbali yakiwemo ya ubovu, kuvuja mafuta, kuisha kwa matairi na baadhi ya gari za abiria @ daladala kuchakaa kwa viti vya kukalia abiria.

Kufuatia Oparesheni hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya ULRICH MATEI amewataka madereva kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kuepuka ajali za mara kwa mara. 

Aidha Kamanda MATEI amewataka wamiliki wa vyombo vya moto hasa magari kujenga utaratibu wa kuyafanyia matengenezo ya mara kwa mara magari yao ili yaweze kutumika kikamilifu katika kazi ya kubeba na kusafirisha abiria vinginevyo Jeshi la Polisi litawachukulia hatua za kisheria wamiliki wote ambao magari yao yatabainika kuwa mabovu hali inayoweza kupelekea ajali.

Imesainiwa na: 
[ULRICH O. MATEI - SACP] 
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

WAZIRI MKUU AKEMEA MAHUSIANO MABAYA YA WATUMISHI KAHAMA

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekemea mahusiano mabaya baina ya watumishi wa wilaya ya Kahama na kusema wanapaswa kubadilika mara moja.

Ametoa onyo hilo leo (Jumapili, Julai 15, 2018) wakati akizungumza na watumishi na viongozi wa Halmashauri za Wilaya za Ushetu, Msalala na Kahama Mji, wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

“Hali ya mahusiano hapa Kahama ni mbaya kuliko Kishapu na Shinyanga. Mnachapa kazi vizuri lakini tatizo kubwa kila mmoja anaenda kivyake, hakuna anayemsikiliza Mkurugenzi wa Halmashauri wala Mkuu wake wa idara,” amesema.

Waziri Mkuu ambaye yuko kwenye ziara ya siku tano ya kikazi mkoani humo, amewaeleza watumishi na viongozi hao kwamba Serikali haitavumilia kuona watumishi wa aina hiyo wanaendelea kufanya kazi.

“Serikali haitavumilia kuona watumishi wakifanya mambo ya hovyo. Kahama ni wilaya yenye majaribu na Shinyanga nayo ni wilaya yenye majaribu makubwa. Kwa hiyo watumishi inabidi muwe makini, kuweni waangalifu msije mkaingia kichwakichwa kwenye majaribu haya.”

“Migogoro niliyoisikia ambayo iko hapa ni kwa sababu ninyi mmeingia kwenye biashara na kutake sides. Hapa Kahama, Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Wilaya hamuelewani, Mkurugenzi na wakuu wa idara hamuelewani, wakuu wa idara na wasaidizi wao nao pia hawaelewani,” alisema.“Napenda kusisitiza kwamba ninyio ni viongozi wa umma, kwa hiyo ni lazima mzingatie itifaki za kiuongozi, mzingatie mahusiano mema mahali pa kazi. Hatupendi viongozi muwe chanzo cha matatizo hapa Kahama,” aliwaasa.

KANISA lagawa Pikipiki kwa wachungaji,Polisi

0
0
KANISA la Pentecostal Assemblies of God (PAG), limegawa Pikipiki kwa wachungaji wake ikiwamo Kituo cha Polisi cha wilaya ya Hanang mkoani Manyara. 

Lengo la kutolewa kwa vyombo hivyo vya usafiri ni kuwawezesha Wachungaji hao kuwafikia watu wengi hususani wanaoishi pembezoni pamoja na kuunga mkono juhudi za jeshi la polisi katika kupambana na uhalifu. 

Akizungumza wakati wa Ibada fupi ya kuzindua pikipiki pamoja na kumuombea Rais Dk.n Magufuli iliyofanyia Kanisa la PAG Hanang’ Askofu Mkuu wa kanisa hilo, Daniel Awet, aliwataka kutumia pikipiki hizo kuhubiri Injili ya Yesu ili jamii inayowazunguka iache matendo ya maovu. 

“Tumieni Pikipiki hizi kama nyenzo ili Injili ifike kwa kasi kwa waamini hasa maeneo ambayo mlikuwa hamuwezi kufika lakini sasa mmepata nyenzo za kuwafikisha,” alisema Askofu Awet. Kwa upande wake Mkuu wa Kituo cha Polisi wilaya ya Hanang’, Sutibert Tryphone, alisema pikipiki waliyopewa itawasaidia kuhudumia wananchi mpaka kwenye maeneo ambayo magari hayafika. 

“Maeneo mengi ambayo hayapitiki kwa usafiri wa magari, sasa tutakuwa tunatumia pikipiki, tunaomba wadau wengine nao wajitokeze kutuunga mkono,” alisema OCD Tryphone. Naye Mchungaji Alex Mapanga wa PAG, ambaye kampuni yake iliwezesha kuagiza pikipiki hizo toka kiwandani kwa fedha zilichangwa na waamini wa kanisa hilo, alisema ataendelea kushirikiana na waamini katika kukfanikisha upatikanaji wa usafiri kwa wachungaji. 

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Hanang’ Mary Nagu, aliliomba kanisa hilo kuendelea kuliombea amani taifa na Rais John Magufuli. “Amani na utulivu ziwafanye mchape kazi ndani ya kanisa, serikalini na kwa jamii,” alisema na kuongeza, kanisa hilo limefanya jambo jema kuwawezesha wachungaji wake kupata vyombo vya usafiri.


Askofu Mkuu wa Kanisa la Pentecostal Assembilies of God (PAG), Daniel Awet akikata utepe kuzindua rassmi ugawaji wa Pipikipi 200 kwa Wachungaji wilayani Hanang' mkoani Manyara.
Sehemu ya Pikipiki 200 zilizogawiwa kwa Wachungaji wa Kanisa la Pentecostal Assemblies of God (PAG), wilayani Hanang' mkoani Manyara kwa ajili ya kazi ya kuhubiri Injili.
Mkurugenzi wa Kampuni ya MCB Investiment Mchungaji Alex Mapanga katikati akimuonyesha namba za moja ya Pikipiki zilizogawiwa kwa Wachungaji wilayani Hanang' mkoani Manyara Askofu Mkuu wa Kanisa la Pentecostal Assembilies of God (PAG), Daniel Awet.
Mkurugenzi wa Kampuni ya MCB Investiment Mchungaji Alex Mapanga akifafanua jambo kuhusu Pikipiki hizo mbele ya viongozi wa dini wakati wa zoezi la ugawaji Pikipiki hizo kwa Wachungaji.
Mkuu wa Polisi wilaya ya Hanang' mkoani Manyara (OCD), Sweetbert Tryphone akimshukuru Askofu Mkuu wa Kanisa la Pentecostal Assemblies of God (PAG), Daniel Awet mara baada ya kumkabidhi Pikipiki moja kwa ajili ya jeshi la polisi.


MAMA WA MITINDO ASIA IDAROUS KATIKA FASHION ASSOCIATION OF TANZANIA NCHINI MAREKANI

0
0
 Mwanamitindo maarufu nchini, Asia Idarous Khamsin akiwakilisha kwenye Fashion Association of Tanzania katika Annual event (global arts expo) iliyofanyika jiji ni Virginia nchini Marekani, Jumla ya Wanamitindo 13 kutoka mataifa mbalimbali waliweza kuonyesha mavazi hayo hapo. 

RPC ARUSHA ATAJA VIPAUMBELE VITANO KUELEKEA KUUSHINDA UHALIFU

0
0
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha

Jeshi la Polisi mkoani hapa kupitia Kamanda wake wa mkoa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng’anzi, limetaja mambo matano ambayo yakifanyika basi kutakuwa na mafanikio zaidi katika kuushinda uhalifu.

Akizungumza katika mahojiano yaliyofanywa na Redio Sunrise ya Jijini hapa kupitia kipindi chake cha “Kwa ajili ya Nchi yako” kinachorushwa hewani kila siku ya Ijumaa kuanzia saa 9:00 Alasiri hadi saa 10:00, Kamanda Ng’anzi alisema, kwanza kabisa kila mwananchi anatakiwa ajue ana wajibu wa kutoa taarifa za matukio ya Uhalifu na Wahalifu zinatokea katika eneo lake.

Pili alisema ni lazima askari wa Jeshi hilo watoe huduma bora na kwa kiwango cha juu kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuwasikiliza pindi wanapoeleza shida zao lakini pia kwenda haraka katika maeneo yaliyoripotiwa kutokea uhalifu.

Tatu alisema lazima kila askari adumishe na kuongeza kiwango cha nidhamu hali ambayo itasaidia baadhi ya wanaokwenda kinyume kutofanya kazi kwa mazoea na hivyo watafanya kazi kwa kufuata taratibu zilizopo.

Nne alisema askari watatakiwa kufanya kazi kwa kuheshimu Utu pamoja na kufuata Maadili ya kazi yao na tano kufanya kazi kwa Uweledi na Usasa ambapo askari atafanya kwa namna alivyofunzwa lakini pia kuendana na kasi ya ukuaji wa Teknolojia na mwisho wa siku waone kwa jinsi gani wananchi mkoani hapa wanaridhishwa na utendaji wa Jeshi hilo.
 Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng'anzi.

VIONGOZI WA SERIKALI YA KENYA WAOMBA MASHIRIKIANO BAINA YAO NA TANZANIA KUPAMBANA NA UKEKETAJI

0
0
Viongozi wa serikali nchini Kenya wameomba kuendelea kushirikiana vyema na serikali ya Tanzania katika kupinga na kupiga Vita suala la Ukeketaji kwa Watoto wa kike huku serikali ikiongoza vyema wazee wa mila baina ya nchi hizo mbili bila kutumia nguvu kwa lengo la kutokomeza Mila na desturi ambazo zimepitwa na wakati ukiwemo Ukeketaji ambao ni chanzo kikubwa cha ndoa za Utotoni.

Zacharia Marwa ni katibu wa Muungano wa koo ya Kurya nchini Kenya na Tanzania anabainisha hayo katika Mkutano wa hadhara uliofanyika maeneo ya Gokeharaka Kurya Mashariki nchini Kenya kwa kukutanisha wazee wa mila Muungano wa koo 12 wilaya ya Tarime pamoja na wazee wa mila koo 4 nchini Kenya.

Zacharia amesema kuwa ili kukomesha Ukeketaji Viongozi wa Tanzania na Kenya waendelee kushirikiana Vyema na wazee wa Mila kutoka Muungano wao bili kutumia nguvu huku elimu ikiendelea kutolewa katika jamii juu ya madhara ya ukeketaji kwa motto wa kike.
Katibu wa Muungano wa wazee wa Mila nchini Kenya, Zacharia Marwa (aliyesimama kulia) akifafanua jambo kwa Wazee wa Mila kutoka Tanzania na Kenya katika Eneo la Gokeharaka Kurya Mahariki nchini Kenya.
Irene Mukanzi ambaye ni Afisa taara ya Kehancha katika Wilaya ya kuria Magharibi akiongea na Wazee hao ambapo amesema kuwa Sheria za kupinga Ukeketaji Nchini Kenya zinaendelea kufanya kazi.
Magoko Maroa ambaye ni Chief Gokeharaka Mashariki mwa Kenya akingea na Wazee hao.
Sammy Chacha ambaye ni Chief Bukira South nchini Kenya akiongea na Wazee wa mila katika Kikao hicho cha pamoja.
Sister Stella Mgaya ambaye ni Mkurugenzi wa shirika la ATFGM Masanga Wilayani Tarime nchini Tanzania ambao wanapiga vita ukatili wa kijinsia ukiwemo ukeketaji akiongea na wazee wa Mila pande zote mbili Tanzania na Kenya na kusema kuwa baada ya kutoa Elimu ya kupinga Ukeketajia sasa wameamua kwenda nchini Kenya lengo likiwa ni kuokoa Mtoto wa Kike.
Wazee wa Mila Muungano wa koo12 Tarime nchini Tanzania wakiwa katika kikao cha pamoja na wazee wa Mila koo 4 nchini Kenya eneo la Gokeharaka Kurya Mashariki Nchini Kenya lengo ni kuzungumzia suala la kupiga Vita Ukeketaji kwa Mtoto wa kike. Habari/Picha na Na Frankius Cleophace, KENYA.

BILIONI 1.5 KUJENGA WODI YA MAMA NA MTOTO

0
0
Na Shushu Joel, Bariadi
Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya mama na Mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto  Ummy Mwalimu Jana mara baada ya kukagua ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje(OPD)  la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, ambapo ameridhishwa na ujenzi wa jengo hilo.

Waziri Ummy amewahakikishia viongozi wa mkoa wa Simiyu kuwa Serikali imetenga shilingi Bilioni 1.5 na wadau wengine wameahidi kutoa shilingi bilioni 1.1 kwa ajili ya kukamilisha wodi ya mama na mtoto mkoani humo ili kupunguza hadha ya kuwachanganya watoto na wakubwa kipindi wanapokwenda kupata matibabu.

“Simiyu katika bajeti ya Serikali imetengewa shilingi bilioni 1.5 lakini tumepata pia shilingi bilioni 1.1 kutoka kwa wafadhili kwa ajili ya ujenzi waWodi ya mama na mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, lengo letu ni kukamilisha ujenzi haraka ili tuiwezeshe Halmashauri ya Mji wa Bariadi, kuchukua majengo ambayo yanatumika sasa hivi kama Hospitali Teule ya mkoa” alisema Ummy.

Katika hatua nyingine Waziri Ummy alisema baada ya kukamilisha ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Serikali ina mpango wa kujenga Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Mashariki Mkoani Simiyu, itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga  ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Rufaa ya Bugando ambayo inahudumia mikoa takribani minane.


 Meneja wa Wakala wa Majengo nchini(TBA) Mkoa wa Simiyu Mhandisi Likimaitare Naunga (wa pili kulia) akimuonesha Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu(katikati) ramani ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, mara baada ya Waziri Ummy kutembelea na kuona maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje(OPD) la hospitali hiyo Mjini Bariadi.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akimuongoza  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto. Ummy Mwalimu , wakati alipotembelea  na kuona maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje(OPD) la hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu Mjini Bariadi.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisaini kitabu cha wageni  wakati alipotembelea  na kuona maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje(OPD) la hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu Mjini Bariadi.
 Waziri wa afya jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu sambamba na kaimu mkurugenzi wa Amref helth Africa Dr Aisa Mmmuya kulia akishuhudia tukio hilo la uzinduzi huo.
Waziri wa afya Ummy Mwalimu sambamba na mbunge wa Itilima Njalu Silanga wakielekea kuzindua mradi wa tuwatumikie.
                                (PICHA ZOTE NA SHUSHU JOEL)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

KIVUKO CHA MV. NYERERE CHAFUNGWA INJINI MPYA

0
0
Na Theresia Mwami - TEMESA
Kivuko cha MV. NYERERE kinachotoa huduma kati ya Bugorola na Ukara katika Wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza, kinafungwa injini mpya tangu kununuliwa kwake na kuanza kutoa huduma mwaka 2004.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Bugorola, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Dkt. Mussa Mgwatu alisema kivuko cha MV. Nyerere kinafungwa injini mbili mpya zenye thamani ya shilingi milioni 191 ili kuongeza ufanisi wa kivuko katika kutoa huduma kwa wananchi wa Bugorola na Ukara. Dkt. Mgwatu amewaagiza mafundi wanaofunga injini hizo wafanye kazi usiku na mchana ili waweze kukamilisha ufungaji wa injini mapema iwezekanavyo ili kivuko kiendelee kutoa huduma ya usafrishaji wa abiria na mali zao.

 Aidha, Dkt. Mgwatu amesema Serikali imedhamiria kuimarisha usafiri wa vivuko katika Ziwa Viktoria kwa kujenga vivuko vipya vitakavyotoa huduma katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya Kigongo, Busisi, Kayenze, Bezi, Chato, Bwina, Bukondo, Senga, Muharamba, Kikumbaitale, Izumacheli na Nkome pamoja na kuvifanyia ukarabati vivuko vya MV. Nyerere, MV. Misungwi, MV. Sengerema na MV. Sabasaba.

Nae meneja wa vivuko TEMESA Mhandisi Hassan Karonda amebainisha kuwa mifumo ya injini ya kivuko cha MV. NYERERE imechoka sana kwa sasa kwa kuwa ni ya muda mrefu. Alisema, injini mbili mpya pamoja na giaboksi zinazofungwa katika kivuko cha MV. Nyerere ni za aina ya Perkins zenye nguvu ya kilowatt 161 kila moja na zinafungwa na mafundi wa TEMESA kwa kushirikiana na wale wa kampuni ya Delta Industrial Equipment Limited. Aliongeza kuwa kazi ya kufunga injini itaenda sambamba na kazi ya kukipaka rangi kivuko hicho na baada ya hapo kivuko kitaendelea kutoa huduma kama hapo awali lakini kwa kasi zaidi.

Kivuko cha MV. Nyerere kina uwezo wa kubeba tani 25 sawa na abiria 100 na magari 3 kwa wakati mmoja. TEMESA inasimamia uendeshaji wa vivuko 30 vya serikali vilivyoko kwenye jumla ya vituo 19 Tanzania bara.
 Kivuko cha MV. NYERERE kinachotoa huduma kati ya Bugorola na Ukara wilayani Ukerewe mkoani Mwanza, kikiwasili upande wa Bugorola kutokea Ukara. Kivuko hiki kinafungwa “engines” mbili mpya aina ya Perkins pamoja na “gearbox” zake zenye uwezo wa kilowatt 161 kila moja, ili kukiongezea kasi pamoja na kuondoa changamoto ya moshi unaotoka pindi kinapotembea. MV. NYERERE ilijengwa mwaka 2004, inauwezo wa kubeba tani 25 ambazo ni sawa na abiria 101 na magari matatu.
   Abiria wakiwasili katika eneo la Bugorola wakitokea kisiwani Ukara wilayani Ukerewe Mkoani mwanza. Kivuko hiki kinafungwa “engines” mbili mpya aina ya Perkins pamoja na “gearbox” zake zenye uwezo wa kilowatt 161 kila moja, ili kukiongezea kasi na kuondoa changamoto ya moshi unaotoka pindi kinapotembea. MV. NYERERE ilijengwa mwaka 2004, inauwezo wa kubeba tani 25 ambazo ni sawa na abiria 101 na magari matatu.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (mwenye Kaunda suti nyeusi) akikagua “engine” moja wapo kati ya mbili zitakazofungwa kwenye kivuko cha MV. NYERERE zenye uwezo wa kilowatt 161 kila moja, ili kukiongezea kasi na kuondoa changamoto ya moshi unaotoka pindi kinapotembea. MV. NYERERE ilijengwa mwaka 2004, inauwezo wa kubeba tani 25 ambazo ni sawa na abiria 101 na magari matatu.

Picha na Theresia Mwami - TEMESA

Wachimbaji Wadogo Handeni Kunufaika na Kituo cha Umahiri

0
0
Frank Mvungi- MAELEZO, Handeni
Serikali Wilayani Handeni imewataka wananchi kutumia fursa ya kujengwa kwa Kituo cha umahiri katika Wilaya hiyo kujiletea  maendeleo kupitia sekta ya madini.
Akizungumza katika mahojiano maalum kuhusu ujenzi wa kituo hicho kinachojengwa na Wizara ya Madini kupitia mkandarasi ambaye ni SUMA JKT,  Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Godwin Gondwe amesema hiyo ni fursa  adhimu kwa wananchi wa Wilaya hiyo kwa kuwa watajengewa uwezo wa namna bora ya kushiriki katika uchimbaji wa madini kwa kuzingatia sheria na kanuni zinazosimamia sekta hiyo.
“Wananchi sasa hawatahitaji kusafiri kwenda mikoa mingine kujifunza namna ya kuchimba madini, kuchenjua na hata kushiriki katika kuendeleza sekta hii kwa kuwa kituo cha umahiri  ( Centre of  Excellence) kinajengwa hapa Handeni hivyo ni jambo la kuishukuru Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi wa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuona kuwa kuna umuhimu wa kuwainua wachimbaji wadogo kwa kuwaongezea ujuzi” Alisisitiza Mhe. Gondwe.
Akifafanua Gondwe amesema kuwa Wilaya hiyo ina hazina kubwa ya madini ya aina mbalimbali ambayo hayajachimbwa hivyo ujenzi wa kituo hicho utasaidia katika kuimarisha usimamizi wa rasilimali hizo na kuwainua wananchi kwa kuwa watachimba madini hayo kwa kuzingatia sheria ikiwemo kulipa kodi zote na hivyo kuondoa tatizo la uwepo wa wachimbaji wasiozingatia weledi na sheria ya madini.
Wizara ya Madini inayotekleza mradi huo.
 Mkuu wa Wilaya ya Handeni Bw. Godwin Gondwe akisisitiza umuhimu  wa Kituo cha umahiri  kwa wachimbaji wadogo wa madini Wilayani Handeni kinachojengwa na Wizara ya Madini ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kuinua wachimbaji hao katika Wilaya hiyo na maeneo yote ya mikoa ya jirani na Wilaya hiyo.
 Luteni  Khalfani Mturi  kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)akipokea ramani ya Kituo cha umahiri (Centre of Excellence) kwa wachimbaji wadogo wa madini kwa niaba ya meneja wa ujenzi wa SUMA JKT Kanda ya Kaskazini Meja. Daudi Zengo  kutoka kwa Mshauri muelekezi wa mradi huo Bw. Beno Matata kutoka Kampuni ya Inter Consult Ltd, mradi huo unatekelezwa na Wizara ya Madini katika Wilaya ya Handeni, kupitia Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini unaotekelezwa na Wizara ya Madini  ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi za Serikali katika kuwainua wachimbaji wadogo.
 Msanifu majengo wa Kampuni ya Inter Consult Ltd Bw. Beno Matata akieleza mikakati ya kampuni hiyo katika kuhakikisha kuwa inasimamia mradi huo wa ujenzi wa Kituo cha Umahiri kitakachowanufaisha wachimbaji wadogo kinachojengwa Wilayani Handeni ikiwa ni sehemu ya Juhudi za Serikali kupitia Wizara ya Madini kuinua wachimbaji hao.
 Mjiolojia wa Wizara ya Madini Bi. Veronica Nangale akisisisitiza jambo  kwa mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe (hayupo pichani) wakati walipomtembelea Ofisini kwake kabla ya hafla ya kukabidhiwa kwa eneo kitakapojengwa kituo  cha umahiri(Centre of Excellence) kwa wachimbaji wadogo wa madini, hafla hiyo ilifanyika Wilayani Handeni, ujenzi wa kituo hicho unafanyika kupitia  Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini unaotekelezwa na Wizara ya Madini  ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi za Serikali katika kuwainua wachimbaji wadogo.
 Luteni  Khalfani Mturi  kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) akisisitiza jambo mara baada ya kukabidhiwa eneo na ramani ya Kituo cha Umahiri kwa wachimbaji wadogo wa madini kinachojengwa na mkandarasi SUMA JKT, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Wizara ya Madini kuimarisha sekta hiyo na kuwainua wachimbaji wadogo.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

HUKUMU KESI YA WEMA SEPETU YASOGEZWA MBELE MPAKA JULAI 20

0
0
Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu akitoka mahakamani baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuahirisha kusoma hukumu dhidi ya kesi yake ya matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili yeye na wafanyakazi wake wawili.

Hukumu hiyo imesogezwa mbele na sasa itasomwa Julai 20  (Ijumaa). Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Hukumu hiyo ilipaswa kusomwa leo mapema, lakini Hakimu Simba ameiahirisha kwa kuwa kuna vitu ambavyo anatakiwa kuvifanyia uchunguzi zaidi kwa undani hivyo amesema mpaka Ijumaa ndio atatoa hukumu.

Wema alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza na wafanyakazi wake Aprili 23, 2018.

KALIUA YATOA PIKIPIKI 12 KWA MAOFISA UGANI ILI WAENDE KWA WAKULIMA

0
0
Na Tiganya Vincent, Tabora
JUMLA ya watumishi 12 wa Kada mbalimbali wa Halmashauri ya  Wilaya ya Kaliua wakabidhiwa pikipiki zenye thamani ya milioni 29  kwa ajili ya kurahisisha utoaji huduma mbalimbali kwa wakulima na wananchi wanaoishi vijijini.

Akiongea kabla ya kukabidhi pikipiki hizo jana  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Dkt. John Pima alisema kuwa lengo la utoaji pikipiki hizo ni kutaka Maofisa Ugani na Watendaji wa Kata waweze kuwafikia wakulima na wananchi mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia.

Alisema utoaji wa pikipiki hizo ni utekelezaji wa agizo la viongozi wa Kitaifa la kuwataka Maofisa Ugani kuondoka Ofisini na kwenda kwa wananchi kwa ajili ya kuwaelimisha juu kulima kilimo kilicho bora ambacho kitawawezesha kuzalisha kwa tija kwa ajili ya kuongeza kipato chao na kuwapata ziada kwa ajili ya kuuza.

Dkt. Pima alisema katika mwaka wa fedha walishatoa pikipiki 8 kwa ajili ya Maofisa Ugani Kata na Watenadaji wa Kata na wataendelea kununua pikipiki kwa kutumia mapato ya ndani hadi hapo watakapo hakikisha watumishi wa kada hiyo wanavyo vyombo vya usafiri kwa ajili ya kusaidia wananchi ikiwemo kulima kilimo bora na kusikiliza kero zao.

Alisema Halmashauri hiyo ili kuhakikisha inatekeleza agizo la viongozi imeshawasambaza Maofisa Ugani katika maeneo mbalimbali ya vijijini kwa ajili ya kuwasogeza karibu na wananchi ili watumie utaalamu wao kuwasaidia wakulima na sio kutoa maelekezo wakiwa ofisini.

Akikabidhi pikipiki Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alilipongeza Baraza la Madiwani na Menejimenti ya Halmashauri hiyo kwa kutekeleza haraka agizo la viongozi wa kitaifa la kuwataka watendaji kwenda kusikiliza kero za wananchi.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akipanda pikipiki kabla ya kuzikabidhi jana kwa Watendaji wa Kata na Maofisa Ugani wa Kata mbalimbali wilayani Kaliua ili waende vijijini kutoa  huduma kwa karibu kwa wakulima na wananchi wengine.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(kulia), Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Haruna Kasele(katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Abel Busalama (kushoto) wakijaribu pikipiki kabla ya kukabidhi jana Watendaji wa Kata na Maofisa Ugani wa Kata mbalimbali wilayani Kaliua ili ziwasaidie kwenda kutoa huduma kwa karibu kwa wakulima na wananchi wengine. Picha na Tiganya Vincent.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

NEWZ ALERT:WAZIRI MBARAWA AMNG'OA MKURUGENZI MAMLAKA YA MAJI KIGOMA

0
0
Na Editha Karlo,blog ya jamii Kigoma.

WAZIRI wa Mji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa amemuondoa kwenye nafasi yake ya Ukurugenzi wa Mamlaka ya Maji Mkoa wa Kigoma (KUWASA) Saimon Lupuga baada ya  kutoridhishwa na utendaji kazi wake.

Mbarawa amefikia hatua hiyo baada ya malalamiko ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga kuwa mamlaka hiyo na Bonde la Mto Tanganyika pamoja na wahandisi wa maji hawatoshi kwenye nafasi zao kutokana na kufanya kazi kwa mazoea.

Kutokana na hatua hiyo Waziri Mbarawa amesema atamuagiza  katibu Mkuu kuandika barua ya uhamisho wa Mkurugenzi huyo kurejeshwa Dar es Salaam kuanzia leo.
Mkurugenzi wa maji safi na taka Mkoa wa Kigoma(KUWASA)Saimon Lukuga akisikiliza maelekezo ya waziri wa maji(hayupo pichani)kwenye kikao kilichofanyika ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

ZFDA YATEKETEZA TANI 95 ZA CHAKULA NA TANI MOJA YA DAWA ZA BINADAMU ZILIZOMALIZA MUDA WA MATUMIZI

0
0
Na Ramadhani Ali, Maelezo Zanzibar
Mamlaka ya Chakula na Dawa Zanzibar (ZFDA) imejidhatiti kuhakikisha kuwa bidhaa zinazoingizwa nchini zinawafikia wananchi zikiwa salama kwa matumizi kwa lengo la kulinda afya zao.

Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti wa Usalama wa chakula wa ZFDA Dkt. Khamis Ali Omar alieleza hayo katika jaa la Kibele wakati wa kazi ya kuangamiza tani 95 za bidhaa za mchele, sembe na Unga wa ngano pamoja na tani moja ya dawa za binadamu.

Alisema bidhaa za chakula zilizoangamizwa za mfanyabiashara Mohamed Mattar ziliharibika baada ya kuhifadhiwa kwa muda mrefu katika maghala yasiyorasmi na yaliyokosa sifa za kutumika kwa kazi hiyo.

Dkt. Khamis alieleza kuwa kutokana na maghala hayo kukosa viwango vinavyokubalika na kutosajiliwa na ZFDA, mfanyabiashara Mattar alikuwa  akiweka bidhaa zake kwa siri wakati wa usiku.

Akitaja viwango vya bidhaa zilizoangamizwa, Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti na uhifadhi wa chakula wa ZFDA alisema mchele ulikua tani 52, unga wa ngano tani 37 na sembe ilikuwa tani sita.
  Fundi wa mageti akikata geti la Ghala lililokua likihifadhiwa bidhaa za Mchele, Unga wa ngano na sembe uliomaliza muda na haufai kwa matimizi ya binadamu katika mtaa wa Migombani Mjini Zanzibar.
 Sshemu ya bidhaa ya Mchele na Unga wa Ngano na Sembe zikiteremshwa katika magari kwa ajili ya Kuangamizwa katika Jaa la Kibele Wilaya ya Kati Unguja.
 Dawa za binadamu za aina mbali mbali za kuondosha maumivu na Virutubisho zilizo angamizwa katika  Jaa la Kibele Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja
 Gari la Kijiko likiangamiza Dawa za kuondosha maumivu na Virutubisho zilizoangamizwa katika  Jaa la Kibele Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Mkurungezi Idara ya Udhibiti na Usalama wa Vyakula wa ZFDA Dkt. Khamis Ali Omar akizungamza na Waandishi wa habari wakati wa zoezi la kuangamizaji Bidhaa zisizofa kwa Matumizi ya Binadamu lililofanyika katika  Jaa la Kibele Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Picha na Abdalla Omar Maelezo  -  Zanzibar.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

AIRTEL MONEY NA SPORTPESA WAENDELEA KUTOA ZAWADI KWA WASHINDI

0
0
Mshindi wa promosheni ya AMSHA AMSHA USHINDE NA AIRTEL MONEY Fredy Mduma wa Kimara DSM akikabidhiwa zawadi yake ya simu aina ya smartphone na Meneja Uhusiano SportPesa Tanzania Sabrina Msuya wakati wa kuwazadia washindi wa promosheni hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kwenye promosheni hiyo, wateja wa Airtel wanajishindia zawadi mbali mbali kwa kuweka kisha kubashiri kwenye akaunti ya SportPesa 150888. Kushoto ni Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mbando.
Mshindi wa promosheni ya AMSHA AMSHA USHINDE NA AIRTEL MONEY Mazoea Rashidi wa Keko DSM akionyesha zawadi yake ya simu aina ya smartphone na Meneja Uhusiano SportPesa Tanzania Sabrina Msuya wakati wa kuwazadia washindi wa promosheni hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kwenye promosheni hiyo, wateja wa Airtel wanajishindia zawadi mbali mbali kwa kuweka kisha kubashiri kwenye akaunti ya SportPesa 150888. Kushoto ni Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mbando na kulia ni Meneja Uhusiano SportPesa Tanzania Sabrina Msuya.

Serikali Yapongezwa Kwa Kuwainua Wanawake Sekta ya Madini

0
0
 Msanifu majengo wa Kampuni ya InterConsult Ltd Bw. Beno Matata akieleza mikakati ya kampuni hiyo katika kuhakikisha kuwa inasimamia mradi  wa ujenzi wa Kituo Maalum kitakachotumika kuwajengea uwezo wanawake wanaojishughulisha na uchimbaji wa madini, Kituo hicho kitawanufaisha wachimbaji hao ikiwa ni sehemu ya Juhudi za Serikali kupitia Wizara ya Madini kuinua wachimba hao.
 Msanifu majengo wa Kampuni ya InterConsult Ltd Bw. Beno Matata akimkabidhi Meneja wa SUMA JKT Kanda ya Kati Mhandisi David Palangyo ramani ya jengo la ghorofa tatu linalojengwa na SUMA JKT katika chuo cha madini Dodoma ikiwa ni sehemu ya mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Endelevu wa Rasilimali Madini (Sustainable Management of Mineral Resources Project- SMMRP), mradi huo unatekelezwa na Wizara ya Madini ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kuimarisha sekta hiyo na kukuza uchumi.
 Msanifu majengo wa Kampuni ya InterConsult Ltd Bw. Beno Matata akionesha mipaka ya eneo kitakapojengwa kituo maalum kitakachotumika kuwajengea uwezo wanawake wanaojuhusisha na uchimbaji wa madini kupitia chama cha wachimbaji wanawake (Women Mining Association),jengo hilo lenye gorofa tatu linajengwa katika chuo cha madini Dodoma.
  Msanifu majengo wa Kampuni ya InterConsult Ltd Bw. Beno Matata akimkabidhi Meneja wa SUMA JKT Kanda ya Kati Mhandisi David  Palangyo ramani ya jengo la kisasa la gorofa 3 linalojengwa chuo cha madini Dodoma likilenga  kuwajengea uwezo wanawake wanaojuhusisha na uchimbaji wa madini kupitia chama cha wachimbaji wanawake (Women Mining Association).


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA APOKELEWA RASMI LEO MAKAO MAKUU YA JESHI HILO

0
0
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Phaustine Kasike akipokea saluti kutoka kwa Kamishna wa Utawala wa Magereza, Gaston Sanga mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ofisi ya Makao Makuu ya Jeshi la Magereza jijini, Dar es Salaam, leo Julai 16, 2018.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akipokea salamu ya heshima kutoka kwa Gwaride maalum lililoandaliwa kwa ajili ya mapokezi yake Makao Makuu ya Jeshi hilo.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akikagua gwaride maalum lililoandaliwa na Maofisa na askari wa Jeshi la Magereza.
Kamishna Jenerali mstaafu, Dkt. Juma Malewa(suti nyeusi) akimkaribisha Kamishna Jenerali mpya wa Magereza, Phaustine Kasike mara baada ya kumaliza kukagua gwaride rasmi lililoandaliwa na maofisa na askari wa Jeshi la Magereza.

KUSANYO LA KODI MWAKA WA FEDHA 2017/2018 LAPANDA KWA ASILIMIA 7.5

0
0

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MAMLAKA ya Mapato nchini (TRA) wamefanikiwa kukusanya jumla ya shilingi Trilioni 15.5 kwa mwaka mzima wa fedha 2017/2018 kuanzia julai 2017 hadi Juni 30 2018 ukilinganisha na shilingi trilioni 14.4 zilizokusanywa mwaka wa fedha 2016/2017.

Akizungumza na waandishi wa habari  leo Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Richard Kayombo ameeleza kuwa kiasi kilichokusanywa ni sawa na asilimia 7.5 kiukuaji na kwa mwezi Juni pekee TRA imekusanya shilingi trilioni 1.5 ukilinganisha na trilioni 1.4 zilizokusanywa mwezi Juni mwaka 2017.

Aidha ameeleza kuwa sababu za kuongezeka kwa makusanyo hayo ni pamoja na uwepo wa elimu ya kodi inayowasaidia walipakodi na wananchi kwa ujumla kutambua umuhimu wa kulipa kodi, kuwa karibu na walipa kodi sambamba na kutatua changamoto zao za kikodi, kuongezeka kwa walipa kodi wapya  kupitia kampeni ya kuwasajili kwa kuwafuata waliko na kurahisisha ulipaji wa kodi kwa njia ya kielektroniki.

Pia ameeleza kuwa kwa mwaka huu wa fedha TRA imedhamiria kutekeleza kwa vitendo kampeni kabambe ya msamaha wa riba na adhabu kwa malimbikizo ya madeni ya nyuma na wanataraji kuongeza urahisi wa kulipa madeni ambayo yalikuwa kikwazo kwa wafanyabiashara wengi kulipa na hata kuendelea na biashara.

Kayombo amesema kuwa wamedhamiria kuongeza kasi ya usajili wa walipakodi wapya na wanaendelea na kasi ya utambuzi na usajili wa wafanyabiashara wadogo ili kila mtu anayestahili kulipa kodi asajiliwe na kuchangia kikamilifu maendeleo ya taifa.

Kwa niaba ya mamlaka hiyo amewashukuru na kuwapongeza walipa kodi wote ambao mchango wao umeiwezesha serikali kupata mapato ambayo yatasaidia shughuli mbalimbali za kimaendeleo kama vile ujenzi wa miundombinu,  upatikanaji wa elimu, afya na mambo mengine mengi yenye manufaa kwa watanzania wote.

Kayombo ametoa wito kwa walipa kodi wote kuendelea kulipa kodi kwa hiari na kujenga utamaduni wa kutoa na kudai risiti za kielektroniki na kutolea risiti (EFDs.)
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Richard Kayombo akizungumza na waandishi wa habari wakati wa utoaji wa taarifa ya makusanyo ya kodi kwa mwaka wa fedha 2017/2018.

KANGI LUGOLA ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA KIKOSI CHA KUTULIZA GHASIA, UKONGA JIJINI DAR

0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (watatu kutoka kushoto), akipata maelezo juu ya ubora wa silaha inayotumika katika kupambana na uhalifu baada ya kutembelea Makao Makuu ya Kikosi cha Kutuliza Ghasia, kilichopo Ukonga, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akithibitisha ubora wa silaha baada ya kutembelea Makao Makuu ya Kikosi cha Kutuliza Ghasia kilichopo Ukonga, jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Nsato Marijani (kulia), akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, baada ya waziri kutembelea Makao Makuu ya Kikosi cha Kutuliza Ghasia, kilichopo Ukonga, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mrakibu Mwandamizi, Paulo Sanga.
Sajenti wa Jeshi la Polisi, Kusekwa Machibya akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (wapili kutoka kushoto) baada ya waziri kutembelea Makao Makuu ya Kikosi cha Kutuliza Ghasia, kilichopo Ukonga, jijini Dar es Salaam. Wengine ni Maofisa wa jeshi kutoka Makao Makuu ya Polisi, walioongozana na waziri katika ziara hiyo.
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Nsato Marijani akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, baada ya waziri kutembelea Makao Makuu ya Kikosi cha Kutuliza Ghasia, kilichopo Ukonga, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Zamfuko kutua mbao fc

0
0
Na Agnes Francis, globu ya jamii.

Hatimaye klabu ya mbaofc wamefanikiwa kuinasa saini ya mchezaji  Zam Elias Zamfuko aliyekuwa akichezea timu ya Afrikan  Lyon.

Katika makubaliano baina yao kiungo mkabaji  huyo ataitumikia klabu hiyo yenye makao makuu kanda ya ziwa  mkoani mwanza kwa misimu miwili.

Klabu hiyo iliyomaliza msimu wake kwa kusua sua kwa sasa imefikisha jumla ya wachezaji 3 katika muendelezo wa usajili wake.

Ni katika harakati za kujiandaa na msimu ujao wa vodacom Tanzania bara  (VPL) 2018-2019 inayotarajia  kuanza hivi karibuni.
Kiungo mkabaji zam Elias Zamfuko alietokea african lyon akiwa ameshikilia jezi ya waajiri wake wapya  mbao fc baada ya kusaini  mkataba miwili  katika klabu hiyo.
Viewing all 109587 articles
Browse latest View live




Latest Images