Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110144 articles
Browse latest View live

POLISI SHINYANGA YATOA ELIMU YA USALAMA BARABARANI KWA MADEREVA NA WAMILIKI WA VYOMBO VYA MOTO

$
0
0
Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limeendesha mafunzo kuhusu masuala ya usalama barabarani kwa wamiliki na madereva wa magari,pikipiki na bajaji ikiwa ni sehemu ya njia za kukabiliana na ajali zinazojitokeza na kusababisha vifo na majeruhi. 

Mafunzo hayo yaliyofunguliwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro yamefanyika leo Alhamis Julai 12,2018 katika ukumbi wa Bwalo la Polisi mjini Shinyanga. 

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro alisema suala la utii wa sheria za barabarani ni jukumu la watu wote hivyo kila mmoja lazima azingatie sheria za barabarani ili kuepuka ajali zisizo za lazima.

"Madereva ni wadau wakuu wa kuzuia ajali za barabarani, nalipongeza jeshi la polisi kwa kuona umuhimu na wadau hawa ili kuwapa elimu hii kwani madereva wakisikiliza na kufanyia kazi elimu hii hakika ajali hazitatokea mkoani Shinyanga",alieleza Matiro.

"Ili kutokomeza ajali,ni vyema jeshi la polisi likaendelea kufanya doria katika barabara kuu, kukagua leseni na kuhakikisha magari yote mabovu hayaiingii barabarani lakini pia kutoa elimu kwa wadau wote wakiwemo wanafunzi",aliongeza Matiro.
Kulia ni Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Simon Haule akimuonesha Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ratiba ya mada zinazofundishwa kwa wamiliki na waendeshaji wa vyombo vya moto ikiwemo magari,pikipiki na bajaji.
Kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Shinyanga SSP Richard George Abwaoakiteta jambo na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Shinyanga ASP Anthony Gwandu.
Dereva na mmiliki wa Tax na pikipiki, Omari Gindu akiomba askari wa usalama barabarani 'Trafiki' nao wapewe elimu ya usalama barabarani akidai baadhi yao hawajui sheria hivyo kukamata ovyo madereva na kuchangia kutokea kwa ajali
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Simon Haule akisisitiza kuwa jeshi la polisi litaendelea kuwachukulia hatua za kisheria madereva watakaokiuka sheria za usalama barabarani.Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro . Kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Shinyanga SSP Richard George Abwao
Madereva na wamiliki wa vyombo vya moto wakiapa kuzingatia sheria za barabarani ili kutokomeza ajali mkoani Shinyanga.

utalii katika msitu wa Chome kilele cha mlima Shengena wilayani Same kutangazwa

$
0
0
Ni utalii katika msitu wa Chome hususan kilele cha mlima Shengena ambapo Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro imedhamiria kutangaza kivutio hiki ili kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea eneo hilo. 
Mkuu wa Wilaya ya  Same Mhe. Rosemary Sitaki aliongoza wataalamu 23 toka ofisi za serikali Wilayani hapo wakiratibiwa na Wakala wa Misitu (TFS)  kupanda mlima Shengena wenye urefu wa Mita 2462 toka usawa wa bahari, ambacho ni kilele cha pili kwa urefu kufuatia Mlima Kilimanjaro.
Mlima huo una vivutio  vingi vya miti, ndege, vipepeo,  nyani, mito na uoto wa asili ni raslimali kubwa. 
Ni eneo unaloona Mlima kilimanjaro kwa juu zaidi kuliko eneo jingine lolote, na linafaa kwa utalii, mazoezi ya kupanda mlima Kilimanjaro, kurekodi Sinema, hifadhi ya mazingira, uwekezaji, utafiti, vyanzo vya maji, camp site ambapo 
TFS wanafikiria kuweka "sky line"
" Ni lazima tujipange kufanya vitu tofauti ili kuwafanya watalii kuchagua Shengena" alisema DC Sitaki, huku akiwaalika wananchi na wageni  kuja kujionea uumbaji wa ajabu wa Mungu uliopo Shengena. 
Alitoa tahadhari kwa wenye nia ya kuchezea msitu huo, kwa kuwa ni moyo ya Wilaya ya Same kwani vyanzo vya maji zaidi ya 8 vinavyotegemewa na Wananchi vinaanzia msitu huo. Aliahidi kuutunza, kuulinda  kuuthamini na kuwachukulia hatua wanaouchezea. 
Timu hiyo ilitumia kati ya saa 2.30 - 2.40 kufika kileleni umbali wa Km. 5.54. 

 Mkuu wa Wilaya ya  Same Mhe. Rosemary Sitaki (kilemba cha buluu) na  wataalamu 23 toka ofisi za serikali Wilayani hapo wakipumzika baada ya  kupanda mlima Shengena wenye urefu wa mita 2462 kutoka usawa wa bahari.
 Mkuu wa Wilaya ya  Same Mhe. Rosemary Sitaki (kilemba cha buluu) akiongoza   wataalamu 23 toka ofisi za serikali Wilayani hapo wakipumzika baada ya  kupanda mlima Shengena wenye urefu wa mita 2462 kutoka usawa wa bahari.
 Mkuu wa Wilaya ya  Same Mhe. Rosemary Sitaki (kilemba cha buluu) na  wataalamu 23 toka ofisi za serikali Wilayani hapo wakiwa kwenye kilele cha  mlima Shengena wenye urefu wa mita 2462 kutoka usawa wa bahari.
Mtaalamu akitoa maelezo juu ya kilele cha mlima Shengena

KAMISHNA MKUU WA TRA ATEMBELEA WAFANYABIASHARA JIJINI DODOMA

$
0
0
*TRA yawataka wafanyabiashara wenye changamoto za kikodi kufika ofisini

NA RACHEL MKUNDAI, DODOMA
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere, amewataka wafanyabiashara wote nchini ambao wanakutana na changamoto za kikodi kuwasiliana na ofisi za TRA zilizo karibu nao ili ziweze kupatiwa ufumbuzi wa haraka.

Kamishna Kichere ameyasema hayo alipotembelea kiwanda wa DI&PC kinachotengeneza vinywaji kilichopo jijini Dodoma na kuongeza kuwa TRA ipo tayari kusikiliza changamoto zozote za kikodi kutoka kwa wafanyabiashara na itazifanyia kazi kwa kushirikiana na wafanyabiashara hao ili kuhakikisha kuwa serikali inapata mapato na wafanyabiashara wanalipa kodi zao kwa wakati. 

“Wafanyabiashara wale wenye changamoto za kikodi waje, tukae tuongee nao, na tuone namna ya kuzishughulikia na wafanyabiashara walipe kodi kwa wakati, tusonge mbele”, ameongeza Kamishna Mkuu wa TRA”, amesema Kamisha Kichere

Naye mmoja wa wakurugenzi wa kiwanda hicho Katherine Mwimbe, amesema ujio wa Kamishna Mkuu wa TRA katika kiwanda hicho umeleta faraja kwao kwa sababu wamepata fursa ya kuwasilisha kwake moja kwa moja changamoto za kikodi walizokuwa nazo na Kamishna amewahakikishia kuzifanyia kazi haraka.
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (kulia) akiwa katika kikao na uongozi wa Kiwanda cha kutengeneza vinywaji visivyo na kilevi cha DI & PC kilichopo Jijini Dodoma, wakati alipofanya ziara yake ya kikazi kiwandani hapo kusikiliza changamoto zinazowakumba Wafanyabiashara.
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (kulia) akizungumza na mmoja wa Wakurugenzi wa Kiwanda cha kutengeneza vinywaji visivyo na kilevi cha DI & PC kilichopo Jijini Dodoma, Bibi. Catherine Mwimbe wakati alipofanya ziara yake ya kikazi kiwandani hapo kusikiliza changamoto zinazowakumba Wafanyabiashara.
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (kushoto) akizungumza na Wakurugenzi wa Kiwanda cha kutengeneza vinywaji visivyo na kilevi cha DI & PC kilichopo Jijini Dodoma mara alipokamilisha ziara yake ya kikazi kiwandani hapo kusikiliza changamoto zinazowakumba Wafanyabiashara.
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (kulia) akiwa pamoja na viongozi wengine wa TRA wakitazama shamba la mizabibu ambalo ni mali ya Kiwanda cha kutengeneza vinywaji visivyo na kilevi cha DI & PC kilichopo Jijini Dodoma wakati wa ziara yake ya kikazi kiwandani hapo kusikiliza changamoto zinazowakumba Wafanyabiashara.
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (kulia) akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Kiwanda cha kutengeneza vinywaji visivyo na kilevi cha DI & PC kilichopo Jijini Dodoma, Bibi. Catherine Mwimbe wakitazama miundimbinu ya kiwandani hapo wakati wa ziara yake ya kikazi kusikiliza changamoto zinazowakumba Wafanyabiashara.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Waziri wa Afya azindua mradi wa TUWATUMIE Itilima mkoani Simiyu

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu amezindua rasmi mradi wa TUWATUMIE unaotekelezwa katika wilaya za Itilima mkoani Simiyu na Misungwi mkoani Mwanza. 

 Uzinduzi wa mradi huo unaotekelezwa na shirika la Amref Health Africa Tanzania pamoja na taasisi ya Benjamin Mkapa umefanyika katika wilaya ya Itilima, ukilenga kuboresha huduma za afya hususani huduma za uzazi ili kupunguza vifo vya akina mama na watoto chini ya miaka mitano. 

 Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Waziri Mwalimu amesema serikali itaendelea kuboresha huduma za afya ikiwemo kuongeza watumishi wa afya pamoja na kuwatumia wahudumu wa afya ngazi ya jamii ili wasaidia kutoa huduma za afya kwa wananchi. Naye Mkuu wa Miradi kutoka shirika la Amref Health Africa Tanzania, Dkt.Aisa Muya amesema utekelezaji wa mradi wa TUWATUMIE unaofadhiliwa na serikali ya Ireland kupitia shirika la Irish Aid, ulianza mwezi Disemba 2017 na unatarajiwa kufikia tamati mwezi Juni mwaka 2020 ambapo ametoa rai kwa serikali kuandaa mwongozo utakaowaajiri wasaidizi hao wa afya ngazi ya jamii baada ya kipindi cha mwaka mmoja ambacho shirika hilo litakuwa likiwalipa mishahara kukamilika.

 Amesema mradi huo ulibuniwa na shirika la Amref Health Africa Tanzania kwa kushirikiana na taasisi ya Benjamin Mkapa pamoja na Wizara ya Afya kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma (Health Promotion Unit) lengo likiwa ni kuajiri watumishi wapatao 215 wilaya za Itilima na Misungwi (Itilima wahudumu 102 na Misungwi wahudumu 113) ili wasaidie utoaji huduma za awali kwa wananchi. 

 “Asilimia 50 ya miradi yetu inatumia watoa huduma za afya ngazi ya jamii ambapo kwa mwaka huu tayari wahudumu 2,265 wamepatiwa mafunzo na majukumu yao makubwa yanaanza kwa kuwahamasisha wananchi kuzingatia usafi wa mazingira, utumiaji wa maji safi na salama, kuzuia ukatili wa kijinsia, kutoa elimu ya lishe bora, kutambua viashiria vya magonjwa hatarishi kwa akina mama”. 

Amesema Dr.Muya. Nao baadhi ya wahudumu wa afya ngazi ya jamii wilayani Itilima wamesema wako tayari kufanya kazi kwa bidii na weledi hususani kuwahamasisha wananchi kuhudhuria kliniki, kujifungulia katika vituo vya afya ili lengo la kupunguza vifo vya akina mama na watoto chini ya miaka mitano liweze kutimia.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto akiongea na Wananchi wa Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu wakati wa ufunguzi wa mradi wa Tuwatumie ambao unawaajiri wahudumu wa afya ngazi ya jamii katika vijiji vyote vya halmashauri hiyo chini ya ufadhili wa AMREF
Waziri Ummy Mwalimu akifungua mradi huo
Wadau mbalimbali wa sekta ya afya walifuatilia hotuba ya mgeni rasmi(hayupo pichani) aliyekaa kushoto ni Niall Morris Mkuu wa Arish Aid,Dar.Aisa Muya -Kaimu Mkurugenzi Mkazi Amref Tanzania(katikati) na kulia ni Dkt.Helen Senkoro Mkurugenzi wa Benjamin Mkapa Foundation
wananchi waliojitokeza kushuhudia ufunguzi wa mradi huo ambapo watoa huduma hao watakua kiungo kati ya wananchi na vituo vya kutolea huduma

KAIMU MTENDAJI KATA YA KENYAMANYORI ASIMAMISHWA KAZI KWA TUHUMA ZA UPOTEVU WA FEDHA, MIFUKO YA SARUJI 39

$
0
0
Na Frankius Cleophace,Tarime

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Mji wa Tarime mkoani Mara Elias Ntiruhungwa amemsimamisha kazi Kaimu Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kenyamanyori Laurent Marwa kwa upotevu wa fedha za Serikali pamoja na mifuko 39 ya saruji ambayo ilipaswa kujenga vyumba viwili katika Shule ya Sekondari Kenyamanyori.

Akizungumza leo, Mkurugenzi huyo amesema kuwa Kaimu huyo alienda kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Nkende na kusaini na kisha kukabidhiwa mifuko ya saruji huku akisubiliwa na wananchi waendelee na ujenzi katika Shule ya Sekondari Kenyamonyori.

Amefafanua lakini alitokemea kusikojulikna na mifuko hiyo.Pia alipotea tena na sh.80,000 zilizochangwa katika mkutano wa hadhara na Diwani wa kata hiyo kwa ajili ya kuunga mkono wananchi katika ujenzi huo.Pia Mkurugenzi ameongeza kuwa viongozi wa Serikali ya kijiji walikaa na kupitisha mitasari ili Mtendaji huyo aweze kuchukua fedha benki Sh.590,000 lakini mpaka sasa hazijulikani fedha hizo zilipo baada ya kuzitoa benki.

Hivyo ameamua kumsimamisha kazi na kudai lazima afikishwe Polisi na baadae kufikishwa mahakamani ili ajibu mashitaka yanayomkabili.“Nilimuita ofisini kwangu nikampa saa mbili ili arejeshe vitu hivyo mfano mifuko ya saruji na fedha hizo lakini mpaka sasa hajarejesha chochote.Nimeamua kumsimamisha kazi na huyo akuna haja ya kuunda tume lazima kesho afikishwe Polisi na kufikishwa Mahakamani mara moja,"amesema Elias.

Mkurugenzi amesema kuwa nia ya Serikali ni kuweka mazingira bora ya wanafunzi ili wasome lakini baaadhi ya viongozi wasiokuwa na maadili wanazidi kufanya hujuma jambo ambalo hawatalifumbia macho.

Ameongeza watachukua hatua kali kwa wale wote ambao wanakiuka maadili.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime Elias Ntiruhungwa akiongea na Vyombo vya habari ofisini kwake ambapo amesimamisha kazi Kaimu Afisa Mtendaji wa kata ya Kenyamanyori kwa sababu za ubadhilifu wa fedha za Serikali pamoja na Mifuko 39 ya saruji.

MWENGE WA UHURU UNATARAJIA KUPITIA MIRADI 67 YENYE THAMANI YA ZAIDI YA BIL.162.440 MKOANI PWANI

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,MKURANGA

MKUU wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo amepokea mwenge wa uhuru ,ukitokea jijini Dar es salaam ,ambapo ukiwa mkoani hapo unatarajiwa kupitia miradi ya maendeleo 67 yenye thamani ya sh.bilioni 162.440.8 .

Kati ya miradi hiyo ,16 itawekwa mawe ya msingi ,miradi 13 itazinduliwa ,nane itafunguliwa na 21 itakaguliwa.Akikabidhiwa mwenge huo ,wilayani Mkuranga Ndikilo alisema ,mwenge wa uhuru ukiwa mkoani humo, pia utapitia wilaya 7 na halmashauri 9#.

Alisema mwenge wa uhuru utapokea taarifa ya miradi 9 katika maeneo mbalimbali ya mkoa na wamehakikisha miradi yote itakuwa na thamani ya fedha ili wasiangukie kwenye mtego ambao uliwakumba mkoa wa Dar es salaam.

Alieleza ,miradi hiyo imetekelezwa kwa ushirikiano baina ya wananchi,serikali kuu,halmashauri na wahisani wa kitaifa na kimataifa." Kaulimbiu ya mbio za mwenge kwa mwaka huu ni ‘Elimu ni ufunguo wa maisha, wekeza sasa kwa maendeleo ya Taifa letu.’

"Katika kutekeleza ujumbe huo tumejipanga kutekeleza kwa vitendo ambapo kwenye elimu tumevuka lengo kwa kuandikisha watoto wa darasa la kwanza." alisema Ndikilo.Mkuu huyo wa mkoa alieleza ,mwaka huu lengo ilikuwa 47,686 walioandikishwa ni 52,551 sawa na asilimia 110.

Ndikilo alisema ,katika upande wa viwanda wamefanya kazi nzuri kwani kwasasa wana viwanda zaidi ya 400 vikubwa ,vya kati na vidogo."Asilimia 20 ya ajira zote viwandani Pwani ni za wazawa wa mkoa na wanatarajia kufikia asilimia 50." alielezea Ndikilo.

Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa mwaka huu Charles Kabeho, alihimiza elimu kwa watoto wote na kuwataka wazazi kuwa na mwamko wa kuwapeleka watoto shule.Mwenge huo umeanza mbio zake July 12 wilayani Mkuranga Mkoani Pwani na July 13 unatarajiwa kupokelewa wilayani Rufiji.
MKUU wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo akimpokea kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa mwaka huu ,Charles Kabeho ,wilayani Mkuranga mkoani hapo.(picha na Mwamvua Mwinyi).

WADAU WAKIWAKILISHA MASHABIKI WA SOKA WA TANZANIA HUKO URUSI KWENYE KOMBE LA DUNIA

$
0
0
Sehemu ya Watanzania walioko nchini Urusi kushuhudia kombe la dunia jijini Moscow.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA JULAI 13, 2018


WAZIRI WA AFYA AWATAKA WAGANGA WAKUU KUSIMAMIA MATUMIZI YA MAGARI YA KUBEBEA WAGONJWA

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu amepiga marufuku magari ya kubeba wagonjwa (Ambulance ) kubeba watu au kitu chochote tofauti na wagonjwa na akawaagiza Waganga wakuu wa Mikoa na Wilaya kote nchini,  kusimamia matumizi ya magari hayo na kuhakikisha yanatumika kwa matumizi yaliyokusudiwa kwa mujibu wa mwongozo.

Waziri Ummy ametoa agizo hilo Julai 12, 2018 katika uzinduzi wa Mradi wa TUWATUMIE wenye lengo la kuunganisha jamii hasa zile zilizo mbali na vituo vya tiba, ambao umezinduliwa katika Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu, kuunganisha jamii zinazoishi maeneo magumu kufikiwa  na mfumo wa Huduma za Afya ambao umelenga kupunguza vifo  vya mama na Mtoto mkoani SIMIYU.

“Nimesikitishwa sana na kitendo cha gari la kubebea wagonjwa la Halmashauri ya Mji wa Tarime mkoani Mara kubeba dawa za kulevya, ninakemea jambo hili kwa nguvu zangu zote na ninawataka waganga wakuu wa mikoa na wilaya kote nchini kusimamia matumizi ya magari ya kubebea wagonjwa “ alisema Waziri Ummy Mwalimu

“ Ni marufuku gari la kubebea wagonjwa kubeba kitu tofauti na mgonjwa, yeyote ambaye tumemkabidhi gari la kubebea wagonjwa tutamchukulia hatua kali pale ambapo atakiuka mwongozo wa matumizi ya magari ya kubebea wagonjwa, nalipongeza sana jeshi la Polisi kwa kuchukua hatua na ninamtaka Mkurugenzi wa Halmashauri husika kuwasimamisha kazi mara moja dereva na wote waliohusika na gari hilo kubeba mirungi” alisisitiza.

Akizundua mradi wa TUWATUMIE Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii, Waziri Ummy  amewashukuru  wafadhili  wa mradi huu Amref Health Africa Tanzania chini ya Ufadhili wa Serikali ya Ireland kupitia Shirika la Irish aid  ambao utatekelezwa kwa kushirikiana na Benjamin Mkapa Foundation na Halmashauri za Itilima na Misungwi(Mwanza) ukiwa na lengo la kupunguza vifo vya mama na Mtoto.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu akibonyeza kitufe ishara ya uzinduzi wa mradi wa TUWATUMIE wenye lengo la kuwatumia  Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii kuunganisha jamii zinazoishi maeneo magumu kufikiwa  na mfumo wa Huduma za Afya , katika Wilaya ya Itilima, Mkoani Simiyu Julai 12, 2018.
 Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw.Donatus Weginah akiwasilisha tarifa ya Mkoa kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii ,Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu mara baada ya kuwasili mjini Bariadi kwa ajili ya kuzindua mradi wa wa TUWATUMIE Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii kuunganisha jamii zinazoishi maeneo magumu kufikiwa  na mfumo wa Huduma za Afya, katika Wilaya ya Itilima, Mkoani Simiyu Julai 12, 2018.
 Kutoka kulia Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, Mhe. Daudi Nyalamu, Mbunge wa Itilima, mhe.Njalu Silanga na Mkurugenzi wa Benjamin Mkapa Foundation, Dkt. Hellen Senkoro wakiteta jambo wakati wa  uzinduzi wa  mradi wa wa TUWATUMIE Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii kuunganisha jamii zinazoishi maeneo magumu kufikiwa  na mfumo wa Huduma za Afya, katika Wilaya ya Itilima, Mkoani Simiyu Julai 12, 2018.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii ,Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu na Viongozi wengine wakiwa katika picha na Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii wanaotarajia kuhudumia Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, wakati wa uzinduzi wa Mradi wa TUWATUMIE wenye lengo kuwatumia Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii kutoa huduma kwa jamii, uliofanyika katika Wilaya ya Itilima, Mkoani Simiyu Julai 12, 2018.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

KAIMU MTENDAJI KATA YA KENYAMANYORI ASIMAMISHWA KAZI KWA TUHUMA ZA UPOTEVU WA FEDHA, MIFUKO YA SARUJI 39

$
0
0
Na Frankius Cleophace,Tarime

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Mji wa Tarime mkoani Mara Elias Ntiruhungwa amemsimamisha kazi Kaimu Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kenyamanyori Laurent Marwa kwa upotevu wa fedha za Serikali pamoja na mifuko 39 ya saruji ambayo ilipaswa kujenga vyumba viwili katika Shule ya Sekondari Kenyamanyori.

Akizungumza leo, Mkurugenzi huyo amesema kuwa Kaimu huyo alienda kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Nkende na kusaini na kisha kukabidhiwa mifuko ya saruji huku akisubiliwa na wananchi waendelee na ujenzi katika Shule ya Sekondari Kenyamonyori.

Amefafanua lakini alitokemea kusikojulikna na mifuko hiyo.Pia alipotea tena na sh.80,000 zilizochangwa katika mkutano wa hadhara na Diwani wa kata hiyo kwa ajili ya kuunga mkono wananchi katika ujenzi huo.Pia Mkurugenzi ameongeza kuwa viongozi wa Serikali ya kijiji walikaa na kupitisha mitasari ili Mtendaji huyo aweze kuchukua fedha benki Sh.590,000 lakini mpaka sasa hazijulikani fedha hizo zilipo baada ya kuzitoa benki.

Hivyo ameamua kumsimamisha kazi na kudai lazima afikishwe Polisi na baadae kufikishwa mahakamani ili ajibu mashitaka yanayomkabili.“Nilimuita ofisini kwangu nikampa saa mbili ili arejeshe vitu hivyo mfano mifuko ya saruji na fedha hizo lakini mpaka sasa hajarejesha chochote.Nimeamua kumsimamisha kazi na huyo akuna haja ya kuunda tume lazima kesho afikishwe Polisi na kufikishwa Mahakamani mara moja,"amesema Elias.

Mkurugenzi amesema kuwa nia ya Serikali ni kuweka mazingira bora ya wanafunzi ili wasome lakini baaadhi ya viongozi wasiokuwa na maadili wanazidi kufanya hujuma jambo ambalo hawatalifumbia macho.Ameongeza watachukua hatua kali kwa wale wote ambao wanakiuka maadili.

Afisa Mtendaji wa kijiji cha Matongo Joyce Mbusi akifafanua jinsi vikundi vya kata ya Matongo vilivyonufaika na Mikopo katoka halmashauri ya wilaya ya Tarime Mkoani Mara.
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Matongo Yohana Maisa maarufu Kunguru akisoma baadhi ya vifungu katika ilani ya chama hicho.
Viongozi hao pamoja na kamati ya siasa kata ya Matongo wakikagua ujenzi wa ofisi ya serikali ya kijiji cha Mjini kati
Viongozi hao pamoja na kamati ya siasa kata ya Matongo wakikagua ujenzi wa ofisi ya serikali ya kijiji cha Mjini kati
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Matongo Yohana Maisa maarufu Kunguru akikagua Kompyuta zilizotolewa na Mfuko wa dhamana North Mara katika shule ya Msingi Nyabichune.

HALMASHAURI YA BUHIGWE, OFISI YA MBUNGE WAANDAA MAFUNZO KWA WAJASIRIAMALI

$
0
0
Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

HALMASHAURI ya Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma kwa kushirikiana na ofisi ya mbunge wameandaa mafunzo kwa wajasiriamali wadogo wilayani humo.

Lengo ni kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri na kuongeza uelewa kwa wajasiriamali katika shughuli wanazofanya.

Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa mafunzo hayo jana wilayani Buhigwe, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Anosta Nyamoga amesema semina hiyo inamalengo matatu , moja ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ili kuwawezesha na kuwapa mafunzo wajasiriamali wadogo wadogo.

Pia kuongeza mapato kwa halmashauri kwakuwa wajasiriamali wakiongeza kipato hata pato la halmashauri linaongezeka kupitia ukusanyaji wa kodi na kuboresha maisha ya wananchi.

Amesema asilimia kubwa ya mapato ya Wilaya ya Buhigwe yanategemea ukusanyaji wa ushuru wa mazao na kodi kutoka kwa wajasiriamali wadogo , semina hiyo ya kuwajengea uwezo wajasiriamali na kufaungua masoko ya nje ya nchi kwa kuwajenga wananchi kutengeneza bidhaa zenye ubora na kutumia masoko ya ujirani mwema kuuza bidhaa zao na kuongeza kipato chao itasaidia uchumi kuongezeka.

Amesema kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2016/2017 walikusanya shilingi milioni 450 , na kwa mwaka wa fedha 2017/2018 wamekusanya milioni 550 na Malengo ya Wilaya hiyo ni kufikia kukusanya kiasi cha Sh bilioni moja ifikapo 2020 kutokana na Miundombinu ya biashara kuboresha na kukamilika kwa soko la ujirani mwa litakalo jengwa Manyovu, ambapo wanatarajia kukusanya zaidi ya milioni 100 kupitia soko hilo.

" Wilaya ya Buhigwe tumejipanga ipasavyo kuhakikisha Wananchi wetu wanatoka kwenye maisha waliyokuwa nayo ya kufanya biashara kwaajili ya kupata chakula kwa sasa tunataka waanze kufanya biashara kwa malengo zaidi kwakuwa fursa ni nyingi na Wananchi walikuwa hawazitumii tunaamini kupitia semina hii uchumi utaongezeka na manufaa watayaona", alisema mkurugenzi huyo.


Baadhi ya Wajasiriamali Wadogo wakifuatilia mafunzo yaliyokuwa yakitolewa ukumbini humo mapema jana,mafunzo hayo yaliandaliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe kwa kushirikiana na Ofisi ya Mbunge wa Manyovu .Lengo la mafunzo hayo ikiwa ni kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri na kuongeza uelewa kwa wajasiriamali katika shughuli wanazofanya.

AGIZO LA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI KWA JESHI LA MAGEREZA

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AANZA ZIARA YA WILAYA YA KISHAPU

$
0
0


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na mtoto Witness Castory wa Shule ya Awali ya Lubaga wilayani Kishapu baada ya mtoto huyo na wenzake kuimba wimbo wa kumkaribisha Waziri Mkuu kwenye viwanja vya Jengo la Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Julai 13, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO 3145 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na mbunge wa Kishapu, Mhe. Suleiman Nchambi wakati alipowasili kwenye viwanja vya Ofisi ya Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Julai 13, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack.

RAIS DKT MAGUFULI ATEUA KAMISHNA JENERALI MPYA WA MAGEREZA

$
0
0
Kamishna Jenerali Mteule wa Jeshi la Magereza,Phaustine Kasike

Introducing "Baila Baila" by Diamond Platnumz ft Miri Ben-Ari Official music video


MAZISHI YA MKE WA KIBONDE MAKABURI YA KINONDONI JIJINI DAR JIONI HII

$
0
0
 Jeneza lenye mwili wa Mke wa Mtangazaji maarufu nchini na Radio Clouds FM, Ephrahim Kibonde, marehemu Sarrah Kibonde, ukiwasili kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam jioni hii tayari kwa mazishi.
 Mtangazaji maarufu nchini na Radio Clouds FM, Ephrahim Kibonde akiwa na watoto wake wakati wa mazishi ya Mkewe, Sarrah Kibonde kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam jioni hii tayari kwa mazishi. 
 Mchungaji akitoa neno katika mazishi hayo.
 Sehemu ya Waombolezaji wakiwa kwenye mazishi ya Mke wa Mtangazaji maarufu nchini na Radio Clouds FM, Ephrahim Kibonde, marehemu Sarrah Kibonde, kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam jioni hii.

NAIBU WAZIRI MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA MAONYESHO SABASABA

$
0
0
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya  Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimsikiliza  Askari wa Usalama Barabarani Faustina Ndunguru akitoa maelezo juu ya usalama barabarani na matumizi ya alama za barabarani.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimuuliza swali kwa kutumia mfano wa picha za magari Askari wa Usalama Barabarani Faustina Ndunguru kuhusu makosa ya kuvunja sheria barabarani. 
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya  Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimsikiliza Sajent Miriam  kuhusu jinsi Polisi Jamii wanavyofanya kazi kuhudumia wananchi. Naibu Waziri huyo alitembelea banda la polisi katika viwanja vya sabasaba yanakofanyika Monyesho ya Kitaifa ya Biashara jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimsikiliza Konstebo wa Polisi, Jovin John kuhusu mbwa wa polisi wanavyoweza kusaidia katika kukamata wahalifu nchini. Naibu Waziri huyo alitembelea banda la polisi katika viwanja vya sabasaba kunakofanyika Monyesho ya Kitaifa ya Biashara jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya  Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimsikiliza Inspecta wa Polisi Alex Chandi aliyekuwa akitoa maelezo kuhusu namna gani Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) hufanya kazi kukabili wanaoleta ghasia. Wa kwanza kulia ni Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi Barbas Mwakalukwa. Naibu Waziri huyo alitembelea banda la polisi katika viwanja vya sabasaba kunakofanyika Monyesho ya Kitaifa ya Biashara jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya  Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wananchi, alipotembelea Banda la Idara ya Uhamiaji katika Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara, yanayofanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya  Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimsikiliza Inspekta  Polisi John Mabonda  wa Polisi kitengo cha malalamiko jinsi wanavyohudumia wananchi wenye uhitaji wa huduma yao. Naibu Waziri huyo alitembelea banda la polisi katika viwanja vya sabasaba kunakofanyika Monyesho ya Kitaifa ya Biashara jijini Dar es Salaam.
(Picha na Mambo ya Ndani)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Wakimbizi wanaoishi nje ya kambi za wakimbizi wapewa siku saba kurudi makambini kigoma

UHUSIANO KATI YA MWEKEZAJI NA WANANCHI WAIMARIKA

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu
Wananchi na viongozi kutoka katika vijiji saba vinavyounda Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori (WMA) ya Makao hususani Kijiji cha Makao wilayani Meatu Mkoani Simiyu, wamekiri kuwa uhusiano kati yao na Mwekezaji MWIBA HOLDINGS LTD, ambaye amewekeza katika Hifadhi ya Wanyamapori ya MWIBA katika Kijiji cha Makao kwa ajili ya kuendeleza uhifadhi na uwindaji wa kitalii umeimarika tofauti na awali.

Hayo yalibainishwa na wananchi hao wakati wa ziara ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe.Anthony Mtaka na Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu, iliyoongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa Enock Yakobo katika baadhi ya miradi na maeneo ya uwekezaji ya mwekezaji MWIBA HOLDINGS LTD  katika Hifadhi ya Wanyamapori ya MWIBA Kijiji cha Makao.

Wamesema awali kulikuwa na mgogoro ambao ulisababisha uhusiano kati wananchi na mwekezaji kuvunjika, lakini baadaye  Serikali ya Wilaya na Mkoa ziliingilia kati changamoto zote zilijadiliwa na mapungufu yote yaliyobainika yakafanyiwa kazi, ili pande zote ziweze kunufaika na uwekezaji huo.

“ Uhusiano kati ya Mwekezaji MWIBA HOLDINGS LTD sasa hivi uko vizuri, migogoro iliyokuwepo haipo tena, sasa hivi tunaendelea kuelimishana sisi kwa sisi, ili tusiingize mifugo kwenye eneo lilohifadhiwa kwa utalii maana linatusaidia na tunaendelea kuhamasishana kupambana na ujangili” alisema Andrea Yakobo Mkazi wa Kijiji cha Makao wilayani Meatu.

“Uhusiano uko vizuri, zamani wakati kuna mgogoro tulikuwa tunashuhudia mizoga ya tembo lakini sasa hivi baada ya mwekezaji kushirikiana na wananchi kila mmoja wetu amekuwa mlinzi wa wanyama walio kwenye Hifadhi ya Wanyamapori ya MWIBA, ajira watoto wetu wanapata kama tulivyokubaliana, wantusaidie kwenye elimu, afya na mengine” alisema Amosi Sitta kutoka Kijiji cha Makao.
 Mkurugenzi wa Mwiba Holdings Ltd Bw. Abdulkadiri Mohamed akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati yaUlinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu na Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu wakati wa ziara yao katika Hifadhi ya Wanyamapori ya MWIBA katika Kijiji cha Makao wilayani Meatu.
 Mkuu wa Mkoawa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka akikagua kikosi cha kuzuia ujangili katika Hifadhi ya Wanyamapori ya MWIBA Kijiji cha Makao wilayani Meatu, wakati wa ziara ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu na Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu katika Hifadhi hiyo.
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo (kushoto akizungumza jambo na Mkurugenzi wa MWIBA HOLDINGS LTD Bw. Abdulkadiri Mohamed wakati wa ziara ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu na Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu katika Hifadhi ya Wanyamapori ya MWIBA Kijiji cha Makao wilayani Meatu.
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na askari wa kikosi cha kuzuia ujangili katika Hifadhi ya Wanyamapori ya MWIBA Kijiji cha Makao wilayani Meatu, wakati wa ziara ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu na Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu katika Hifadhi hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu na Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu, Viongozi na Watumishi wa MWIBA HOLDINGS LTD wakati wa ziara ya kamati hizo  katika Hifadhi ya Wanyamapori ya MWIBA Kijiji cha Makao wilayani Meatu.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

SHIRIKA LA AFYA ULIMWENGUNI (WHO) LATOA MSAADA WA DAWA NA VIFAA TIBA KWA WIZARA YA AFYA ZANZIBAR

$
0
0
 Naibu Waziri wa Affya Zanzibar Harus Said Suleiman pamoja na Mwakilishi wa  WHO Tanzania Dkt. Adiele Onyeze wakitiliana saini makabidhiano ya Dawa na Vifaa Tiba kwaajili ya Wizara ya Afya Zanzibar katika hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Ngalawa Bububu  Zanzibar.
 Naibu Waziri wa Affya Zanzibar Harus Said Suleiman akibadilishana hati za makabidhiano ya Dawa na Vifaa Tiba na Mwakilishi wa WHO Tanzania Dkt. Adiele Onyeze katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Ngalawa Bububu Zanzibar.
 Naibu Waziri wa Affya Zanzibar Harus Said Suleiman akionesha kifaa cha kuchunguzia maradhi ya EBOLA, ( katikati) ni Mwakilishi wa Tanzania (WHO) Tanzania Dkt. Adiele Onyeze, kushoto Mkurugenzi kinga Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Fadhil Mohammed.
 Mwakilishi wa Shirika la Afya Ulimwenguni Tanzania (WHO) Dkt. Adiele Onyeze akizungumza katika hafla ya Makabidhiano ya  Dawa na Vifaa Tiba vilivyotolewa na Shirika la Afya Duniani  kwa Wizara ya Afya Zanzibar katika hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Ngalawa Bububu Mjini Zanzibar.
 Baadhi ya Dawa na Vifaa Tiba vilivyotolewa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO)  kwa Wizara ya Afya Zanzibar.
Picha na Abdalla Omar  Maelezo  - Zanzibar.
Viewing all 110144 articles
Browse latest View live




Latest Images