Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

HESLB YASOGEZA MBELE MAOMBI YA MKOPO KWA MTANDAO HADI JULAI 31


WAZIRI MKUU AHUTUBIA MKUTANO WA MAAFISA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI JIJINI DODOMA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Kikao cha Maafisa Kilimo, Mifugo na Uvuvi kilichofanyika leo kwenye  ukumbi wa Chuo cha Mipango jijini Dodoma Julai 12, 2018.
 Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Maafisa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza katika mkutano wao kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango jijini Dodoma Julai 12, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia viongozi baada ya kuhutubia  Mkutano wa Maafisa Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango jijini Dodoma leo Julai 12, 2018.  Kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Kilimo, Omary Mgumba, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Suleiman Jafo, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Mganga Mkuu Hospitali ya Mji wa Tarime, na wengine wawili wasimamishwa kazi baada ya ambulance kukamatwa na mirungi.

$
0
0
Na Frankius Cleophace Tarime.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime Elias Ntiruhungwa amewasimamisha kazi watumishi watatu akiwimo kaimu mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Tarime baada ya gari la wagonjwa la Hospitali hiyo kukamatwa likisafirisha  dawa za kulevya aina ya mirungi Wilayani Bunda Mkoani Mara Julai 11 Mwaka huu.

Waliosimamishwa kazi ni Kaimu Mganga Mkuu (DM) Dkt Innocent Kweka, Kaimu Mganga Mfawidhi Dkt Amir Kombo na katibu wa Hospitali Rwegasira Karugwa kutokana na uzembe waliofanya mpaka kitendo hicho kinafanyika.

“ Namsimamisha kazi DMO, Mganga Mfawidhi na Katibu wa hospitali kuanzia leo hadi tuakapomaliza uchunguzi wetu ambao umeanza kubaini kwa nini gari la wagojnwa lilitumika kusafirisha madawa ya kulevya .Kama hawana hatia watarudi kazini”alisema Mkurugenzi.

Ntiruhungwa amesema hawezi kuvumilia kitendo hicho ambacho kimechafua jina la Hamashauri yake na nchi kwa ujumla na kwamba yeyote ambaye atabainika kuhusika katika tukio hilo atachukuliwa hatua kali.Ameongeza kuwa tayari suala hilo linafanyiwa uchunguzi wa kina ili kubaini dereva huyo George Matai alipataje fursa ya kusafirisha madawa ya kulevya kwa kutumia gari la wagonjwa na kusema kuwa tayari amemsimamisha kazi kuanzia leo.

“Huyu dereva alichokifanya ni kitu cha kushangaza sana na kuzidi kuhaibisha Taifa kwa ujumla lazima afukuzwe kazi kwa sasa tayari anashikiliwa na Polisi na akitoka ata kama ni baada ya Miaka 20 na kama sipo Maandishi yapo atafukuzwa tu hatwezifumbia Macho suala hili”Alisema Mkurugenzi.

Mkurugenzi huyo aliwataka wakuu wa idara katika Halmashauri yake kutimiza wajibu wao kikamilifu ili kuepekuka vitendo vya aibu kama hivyo kutokea tena.Kamanda wa polisi Mkoa wa Mara(RPC) Juma Ndaki aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa dereva huyo na mtuhumiwa mwingine wanashikiliwa baada ya kukamatwa na shehena ya mirungi.
Mkurugenzi wa Halamshauri ya Mji wa Tarime Elias Ntiruhungwa akiongea na Vyombo vya habari katika ofisi yake ambapo amewachukulia hatua Viongozi watatu kutokana na sakata hilo gari la Ambulance kukutwa na dawa za kulevya Mirungi Viroba 34.

MKUTANO WA MAREJESHO WA MAAMUZI NA MAAZIMIO YA MKUTANO MKUU WA 71 WA AFYA ULIMWENGUNI YAFANA ZANZIBAR

$
0
0
Na Mwashungi Tahir
NAIBU  Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman  alisema  matarajio ya kuwapatia  wananchi huduma zilizo bora za afya  popote walipo ndio dhamira kuu ya Wizara zote za afya za Tanzania Bara na Zanzibar.

Hayo aliyasema  leo huko katika  ukumbi wa  Ngalawa Beach Resort wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mrejesho wa maamuzi  na maazimio ya mkutano  mkuu wa 71 wa Afya Ulimwenguni  .

Alisema Huduma za afya zinahitajika  kuwafikia wananchi  hivyo ili kufikia jitihada hizi Serikali zetu mbili hizi zimepiga hatua kubwa kuhakikisha kila sehemu zinawafikia walengwa bila matatizo yeyote na kwa urahisi.

Aidha alisema baada ya Mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964 nchi yetu imekuwa ikichukuwa kila jitihada ili kufikia malengo yaliyotarajiwa , hivyo nchi yetu imekuwa ni moja kati ya nchi chache Barani Afrika , zenye mtandao mzuri wa miundo mbinu ya Afya.

Amewahakikishia wananchi kuwa sasa huduma za Afya   za msingi zinapatikana katika masafa  yasiozidi kilomita nne hadi tano  hili ni jambo jema na tunapaswa kujipongeza.
 Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Harus Said Suleiman akifungua Mkutano wa Marejesho wa Maamuzi na maazimio ya Mkutano Mkuu wa (71) wa Afya Ulimwenguni katika Ukumbi wa Hoteli ya Ngalawa Mjini Zanzibar.
 Mwakilishi wa Shirika la Afya Ulimwenguni Tanzania (WHO) Dkt. Adiele Onyeze akizungumza katika Mkutano wa Marejesho wa Maamuzi na Maazimio ya Mkutano Mkuu wa (71) wa Afya Ulimwenguni katika Ukumbi wa Hoteli ya Ngalawa Mjini Zanzibar.
 Naibu Waziri wa Afya Tanzania faustine Ndugulile, akionesha kipeperushi cha  Mpango kazi kilichoandaliwa na Wizara ya Afya Tanzania katika Mkutano wa Marejesho wa Maamuzi na Maazimio ya Mkutano Mkuu wa (71) wa Afya Ulimwenguni katika Ukumbi wa Hoteli ya Ngalawa Mjini Zanzibar.
  Baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa Marejesho wa Maamuzi na Maazimio ya Mkutano Mkuu wa (71) wa Afya Ulimwenguni katika Ukumbi wa Hoteli ya Ngalawa Mjini Zanzibar.
Picha ya pamoja.
Picha na Abdalla Omar  Maelezo - Zanzibar.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Rest in Peace John Mhina

$
0
0
John Mhina (R.I.P).
It has been a very hard day, and very easy to mourn in silence; it takes away the worry of not being able to get your words out, or even just simply getting the right words out.

But silence or not, one thing which I am sure we all appreciate today, is you have made a better world, a better Tanzania through your musical contribution.

John, we have known each other for the last 45 years, from Barkeys to Tanzanite Band, Kilimanjaro Hotel, Seaview, Mount Meru Hotel, Kunduchi Beach Hotel, Nairobi and many other memorable places.

Today, I had to tear up seeing your young girl and boy at your home in Bunju, and I missed you last week at Hyatt Hotel, when Tanzanite Band was playing in a wedding ceremony, and my wife in her own hindsight asked Abraham, “where is John”? I hardly remember what Abraham told her.

I cherish the recent memory on 20 th May 2018, when you sang on my wife birthday anniversary, maybe it was a discreet divine farewell.

I and my family will have personal and special memories, of the mark you have left in our hearts, in our lives and it is very hard for me today to believe you are gone forever.

Rest in Peace my brother.

David Sowa Mgwassa
12 th July 2018.

WANANCHI WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KWA VIKUNDI VYA ULINZI SHIRIKISHI

$
0
0
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng'anzi akimpa kitambulisho mmoja wa wahitimu wa mafunzo ya Polisi Jamii wa Mtaa wa Kanisani kata ya Sokoni One jijini Arusha.
Meya wa Jiji la Arusha Bw. Kalist Lazaro akiongea na wananchi wa mtaa wa Kanisani kata ya Sokoni One kabla Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha kufunga rasmi mafunzo ya kikundi cha ulinzi shirikishi cha mtaa huo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng'anzi pamoja na wageni wengine wakiwa katika picha ya pamoja na askari wa kikundi cha Ulinzi Shirikishi cha Mtaa wa Kanisani kata ya Sokoni One kilichopo jijini Arusha. (Picha na Rashid Nchimbi wa Polisi Arusha).

Na Rashid Nchimbi wa Polisi Arusha

Wananchi wa mtaa wa Kanisani kata ya Sokoni One jijini hapa, wametakiwa kuendeleza ushirikiano uliopo baina yao na kikundi cha ulinzi shirikishi ili kuweza kuimarisha usalama katika eneo lao.

Wito huo ulitolewa jana jioni na Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng’anzi wakati alipokuwa anafunga mafunzo ya wiki mbili ya kikundi cha ulinzi shirikishi cha mtaa huo pamoja na kuwapa vitambulisho askari 16 waliopewa mafunzo hayo.

Kamanda Ng’anzi alisema mbali na askari wa kikundi hicho kufanya doria katika eneo hilo pia watahitaji kupata taarifa za uhalifu toka kwa wananchi ili waweze kubaini maeneo korofi ambapo kama zitakuwa juu ya uwezo wao watashirikiana na Jeshi la Polisi.

Aidha aliwataka askari hao kufanya kazi kwa kufuata taratibu kama jinsi walivyoelekezwa katika mafunzo yao na kutomuonea mtu yoyote hali ambayo itasidia kuimarisha mahusiano bora baina yao na wananchi.

Hata hivyoKamanda Ng’anzi  aliwataka wananchi hao nao pia wawe mstari wa mbele katika jukumu la ulinzi badala ya kutegemea baadhi ya vyombo vya ulinzi pekee kwani Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imewapa dhamana.

Naye Meya wa jiji la Arusha ambaye pia ni Diwani wa kata ya Sokoni One Bw. Kalist Lazaro aliahidi kuendeleza ushirikiano kati ya halmashauri ya jiji na Jeshi hilo katika masuala ya usalama.

Alisema askari wa Jeshi la Polisi hawawezi kuenea kila mtaa bali wananchi wanatakiwa watoe michango yao kwa kuanzisha vikundi vya ulinzi shirikishi kama wa mtaa wa Kanisani walivyofanya na kuongeza kwamba endapo kila mtaa utaanzisha vikundi hivi basi hali ya usalama jijini hapa itazidi kuimarika zaidi.

Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Polisi Jamii mkoa wa Arusha Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Edith Makweli alisema kwamba, mpaka hivi sasa mkoa wa Arusha una jumla ya vikundi vya Ulinzi Shirikishi 147 ambavyo vimeweza kushirikiana na Jeshi la Polisi na kupunguza uhalifu kwa kiasi kikubwa ambapo mwaka 2016 uhalifu ulipungua kwa asilimia 6.8 na mwaka 2017 uhalifu ulipungua kwa asilimia 17.9 ikilinganishwa na mwaka 2016.

Uwepo wa kikundi hicho chenye zaidi ya miaka 11 katika mtaa huo umeleta amani kwa wakazi hao kwani awali matukio ya uhalifu yalikuwa yanatokea mara kwa mara katika barabara kuu ya mtaa huo tofauti na sasa hali iliyomlazimu Paroko Reginald Kimati wa Kanisa ya Parokia ya Vicent Paroti apendekeze iitwe Amani road.

WAHASIBU WATATU WA TTCL KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA WIZI WAKIWA WATUMISHI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Wahasibu watatu wa shirika la Mawasiliano Tanzania, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za wizi wakiwa watumishi na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya sh milioni 57.

Akisoma hati ya mashtaka, wakili wa serikali Mwandamizi, Patrick Mwita, amewataja washtakiwa hao kuwa ni, Mercy Semwenda (49)  Flora Bwahawa (54) na Hawa Tabuyanja(54).

Mbele Hakimu Mkazi, Augustine  Rwizile imedaiwa, mshtakiwa Semwenda  peke yake anadaiwa, kati ya Januari Mosi mwaka 2017 na Septemba 21 mwaka 2017 jijini Dar es Salaam,  aliiba vocha za muda wa maongezi za TTCl zenye thamani ya sh 44,393,000/ pamoja na fedha za mauzo ya Vocha zenye thamani ya sh milioni 5,914000/

Imedaiwa kuwa, mshtakiwa alifanya uwizi huo kutokana na kamba alikuwa mfanyakazi wa TTCL kama Mhasibu.

Katika shtaka la pili imedaiwa, siku na mahali hapo, washtakiwa wote, waliisababishia Shirika la Mawasiliano  Tanzaniq, (TTCL), hasara ya sh. Milioni 57,773,122.

Hata hivyo, washtakiwa hao hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakamani hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi hadi Mahakamani kuu au kwa kupata kibali kutoka kwa DPP

Kufuatia hivyo, kesi imeahirishwa hadi Julai 24.2018 kwa ajili ya kuja kutajwa, kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika, watuhumiwa wote wamerudishwa rumande.
 Wakili anayewatetea washtakiwa hao amedai, ingawa mashtaka dhidi ya washtakiwa hao yanadhamana lakini wameshtakiwa kwa sheria ya uhujumu uchumi, basi atafuata taratibu zote za kisheria kuomba dhaman Mahakama kuu.

ROBO FAINALI YA SPRITE BBALL KINGS KUPIGWA JUNI 21 UWANJA WA NDANI TAIFA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Michuano ya Sprite BBall Kings 2018 hatua ya robo fainali Imefikia patamu baada ya timu nane kufanikiwa kuingia na sasa kila mmoja kumfahamu mpinzani wake.

Katika droo hiyo iliyochezeshwa ikishuhudiwa na viongozi wa Shirikisho la Kikapu Nchini (TBF) iliweza kupangwa mbele ya viongozi na manahodha wa timu hizo.

Baada ya kumalizika kwa droo, michezo hiyo itachezwa tarehe  21 mwezi huu wa saba, kwenye Uwanja Wa Taifa Wa Ndani, Dar Es Salaam kuanzia saa 6 mchana hadi saa 2 usiku.

Timu zilizofanikiwa kuingia na kupangwa ni  Mchenga B Ball Stars dhidi ya  St. Joseph, Temeke Heroes dhidi ya Portland, Team Kiza dhidi ya DMI, pamoja na  Water Institute dhidi ya Flying Dribblers.

Michuano ya Sprite BBall Kings 2018 yanayodhamiwa na kinywaji cha Sprite yameanza mwanzoni mwa mwezi wa sita kwa hatua ya mchujo kufanyika, timu 16 kufanikiwa kuvuka na kupigwa mechi nane zilizokutana tena na  kisha kupatikana kwa timu nane zilizoingia robo fainali.

Mshindi wa kwanza atafanikiwa kuondoka na kitita cha Milioni 10 pamoja na Kombe, Mshindi wa pili milioni 3 na mchezaji bora wa mashindano  akitwaa milioni 2 

CLEMENT SANGA AVULIWA UENYEKITI BODI WA LIGI

$
0
0
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imekubaliana na mapendekezo ya Kamati ya Sheria na Katiba ya kumsimamisha, Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Clement Sanga baada ya kukosa sifa za Uenyekiti wa Bodi hiyo. 

Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye ukumbi wa mikutano wa TFF uliopo Uwanja wa Karume mjini Dar es Salaam, Rais wa shirikisho hilo, Wallace Karia amesema kwamba hatua imefuatia Mkutano wa Juni 10 wa wanachama wa Yanga kusema bado unamtambua Yussuf Manji kama Mwenyekiti wao.

Karia amesema kwamba Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi anatakiwa awe Mwenyekiti wa klabu ya Ligi Kuu, Sanga amepoteza sifa za kuwa kiongozi Mkuu wa bodi hiyo.

"Tulipokea barua Julai 12 kutoka klabu ya Yanga ikidai kuwa Sanga hatambuliki kama Mwenyekiti wa klabu hiyo, wao Yanga wanamtambua Yussuf Manji ndiye Mwenyekiti wa klabu hiyo na katika nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi unatakiwa Uwe Mwenyekiti wa klabu yako," amesema Karia 

Katika hatua nyingine, Karia amesema Kamati ya Utendaji imempitisha rasmi Wilfred Kidao kuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kukaimu kwa muda mrefu.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF), Wallace Karia akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kumvua uenyekiti wa bodi ya Ligi Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidau.

Azam fc yatamba kumgaragaza mnyama simba fainali kagame cup

$
0
0
Na Agness Francis, Globu ya jamii

Azam fc yatamba kumgaragaza mnyama simba katika fainali za kuwania kombe  la kagame cup (cecafa).

Timu hizo zote mbili za kutoka hapa nchini ambazo zimefanikiwa kutinga fainali zitashuka dimbani kesho majira ya saa 12 jioni kuchoshana nguvu  katika uwanja wa taifa Jijini Dar es Salaam.

Mara baada ya jana azamfc kumuondosha gor mahia ya nchini kenya  katika michuano hiyo  kwa kipigo cha  mabao 2-0, sasa wanakutana na wekundu wa msimbazi katika kumjua nani ataibuka kidedea wa kombe hilo.

Akizungumza leo jijini Dar es  salaam msemaji wa azamfc Jaffary maganga amesema  kuwa kikosi chao kimejipanga vizuri kuhakikisha wanatetea ubingwa  wao wa mwaka 2015 ambapo  michuano hiyo ilifanyika kwa mara ya mwisho hapa nchini

Jaffary amesema maandalizi waliyofanya ni mazuri na ndio maana wamefanya vema  na mpka kufikia hatua hiyo.

"Tunaiheshimu simba ni timu kongwe ya muda mrefu ilio na kikosi mahiri lakini sisi azam tunaliamini benchi letu la ufundi pamoja na mwalimu,tunaahidi kufanya vizuri  kwa kumfunga simba"amesema jaffary.

Mtanange huo utakaokuwa wa ina yake wa kiburudani kwa mashabiki ,inaonyesha zahiri kuwa soka la Tanzania limezidi kuimarika katika ukanda huu wa Afrika mashariki na kati.

TaGLA YAENDELEA NA MAFUNZO YA UPANGAJI MIJI, YAJADILI MASUALA YA ELIMU NA MIUNDOMBINU

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
WAKALA wa mafunzo kwa njia ya mtandao nchini (TaGLA) wameendelea na mafunzo kwa njia ya mtandao kutoka Korea kusini kuhusiana na masuala ya utunzaji wa mazingira upangaji wa miji na utunzaji wa mazingira.

Akizungumza na vyombo vya habari mkurugenzi wa wakala hiyo Charles Senkondo ameeleza kuwa huo ni mdahalo wa pili kati ya saba inayotarajiwa kufanyika hadi kufikia oktoba mwaka huu,  na katika mdahalo huo wamejifunza uwiano wa majiji na utofauti wake kimaisha na hii husaidia kupata takwimu za uhalisia wa maisha katika majiji mbalimbali.

Senkondo ameeleza kuwa mafunzo hayo yanatolewa na profesa Heungsuk Choi kutoka chuo cha maendeleo cha korea kusini katika kueleza namna ya upangaji wa miji na majiji kisasa na kuzingatia miundombinu iliyo bora zaidi ambayo husaidia wananchi katika shughuli zao za kimaendeleo kama vile biashara na hata kirahisisha usafiri kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.

Aidha ameeleza kuwa katika mdahalo huo suala la elimu limejadiliwa na imeelezwa kuwa mazingira ya upatikanaji wa elimu lazima yaboreshwe kwani wazazi huwapeleka wanafunzi katika shule bora zaidi, hivyo shule ambazo hazina ushawishi ni vyema zikaboreshwa zaidi.

Pia Senkondo amewaomba wadau wa serikali na taasisi binafsi kuitumia wakala hiyo ili kuweza kushirikiana na Serikali katika kujenga miji na majiji.

Pia mdau wa mazingira ambaye pia ni mkurugenzi wa Legendary International Limited Kamugenyi Luteganya,  ameeleza kuwa semina hiyo ni muhimu sana katika jamii katika kuishi mazingira yaliyo bora na safi kama Korea wanavyofanya na kuboresha kwa kila hatua hivyo ni lazima wachukue ujuzi ili kuweza kuboresha makazi  nchini.

Pia ameeleza kuwa Serikali na sekta binafsi kutia mkazo katika suala la mazingira na kutoa elimu, na hii ni sambamba na kutoa sera mikakati juu ya upangaji na matumizi ya ardhi.

Washiriki wa mjadala huo wamewashauri wadau na wananchi kwa ujumla kishiriki katika midahalo hiyo ili kuweza kujifunza namna ya kuboresha na kujua uhalisia dunia inavyoshiriana katika kukuza na kujenga miji na majiji duniani.
 Mkurugenzi wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao Charles Senkondo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafunzo kwa njia ya mtandao kutoka Korea kusini kuhusiana na masuala ya utunzaji wa mazingira upangaji wa miji na utunzaji wa mazingira.
Mkurugenzi wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao Charles Senkondo  na wadau wengine wakifutialia mdahalo mubashara toka Nchini Korea Kusini.

BINGWA WA KAGAME CUP KUJULIKANA KESHO

$
0
0

 Na Khadija Seif, Globu ya Jamii.     

Michuano ya Kagame Cup 2018 yanafikia kilele chake siku ya kesho  tarehe 13 Julai  kwa kuzikutanisha Azam na Simba katika dimba la Uwanja wa Taifa.       
                                          
Katibu Mkuu wa Baraza la Vyama vya Michezo Afrika Mashariki CECAFA Nicolaus Musonye amesema  timu mbili kutoka Tanzania ambazo ni Simba na Azam zimefanikiwa kuingia fainali na zitakutana kesho ili kumfahamu Bingwa mpya wa michuano hiyo kwa mwaka 2018.

"timu zilizofanikiwa kutinga fainali ni Azam pamoja na Simba na mchezo huo utachezwa kuanzia majira ya saa 12 jioni katika Uwanja wa Taifa,"amesema Musonye

Mchuano huo utafanyika  majira ya saa 12 jioni ,huku  akiwapongeza wadau wote wa mpira Kwa kutoa michango yao kwa Hali na mali mpaka hapo walipofikia .    

Musonye ameeleza  kuwa timu 12 zote zilizoshiriki Kagame Cup zimefanya vizuri kwenye mashindano hayo na  wajitahidi, kwenye mashindano yajayo wasivunjike moyo Kwa wale wasiofanikiwa  kuingia fainali.          

Sanjari na hilo, Musonye amesema amepokea maombi kutoka nchi zingine za jirani kujiunga kwenye michuano hiyo ikiwamo Zambia,malawi pamoja na Congo .      

Musonye amewaomba  Wadau na mashabiki wa timu hizo  wajitokeze Kwa wingi na viingilio vitakuwa vya bei ya kawaida ili  watu wote waweze kumudu  kuingia japo mpaka sasa havijatangazwa rasmi alisema Musonye.

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA UJUMBE WA TAASISI YA MAENDELEO YA ODI KUTOKA NCHINI UINGEREZA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na Mkuu wa Utafiti na Mkurugenzi wa Mpango wa kusaidia Mabadiliko ya Kiuchumi kutoka Taasisi ya Maendeleo ya Kimataifa (ODI) kutoka nchini Uingereza Dkt. Dirk Willem te Verde na ujumbe wake, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais amesema Ujumbe huo unataka kutoa ushirikiano katika mpango wetu wa uchumi wa viwanda Tanzania.Katika mkutano huo ambao pia ulihudhuriwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango pamoja na Viongozi na Wataalam wa masuala ya Viwanda na Uchumi nchini.

Nae, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amesema kuwa Taasisi hiyo imekuja kufanya mazungumzo na Serikali ili kuharakisha utekelezaji wa Mpango wa Kiuchumi.

Kwa upande wake Mkuu wa Utafiti kutoka Taasisi hiyo Dkt. Dirk Willem te Verde ameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Serikali ya Tanzania katika kufanikisha mpango wa kuwa na Tanzania ya Viwanda.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza kwenye mkutano na  Mkuu wa Utafiti na Mkurugenzi wa Mpango wa kusaidia Mabadiliko ya Kiuchumi kutoka Taasisi ya Maendeleo ya Kimataifa (ODI) kutoka nchini Uingereza Dkt. Dirk Willem te Verde na Ujumbe wake ,Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Utafiti na Mkurugenzi wa Mpango wa kusaidia Mabadiliko ya Kiuchumi kutoka Taasisi ya Maendeleo ya Kimataifa (ODI) kutoka nchini Uingereza Dkt. Dirk Willem te Verde (kulia), Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (kushoto) pamoja na wajumbe wengine walishiriki mkutano huo ,Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Mkuu wa Utafiti na Mkurugenzi wa Mpango wa kusaidia Mabadiliko ya Kiuchumi kutoka Taasisi ya Maendeleo ya Kimataifa (ODI) kutoka nchini Uingereza Dkt. Dirk Willem te Verde mara baada ya kumaliza mazungumzo ,Ikulu jijini Dar es Salaam.(Picha na ofisi ya Makamu wa Rais)

ALIYEKUWA MBUNGE DIMANI ZANZIBAR APANDISHWA MAHAKAMA YA KISUTU KUJIBU TUHUMA ZA UTAPELI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii.

Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Dimani Zanzibar, Abdallah Sharia Amer, na mwenzake Julai 11, wamepandishwa katika kizimba cha mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za utapeli. Mbunge Hugo anashtakiwa pamoja na Dr. Athumani Rajabu.

Akiwasomea hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali, Janet Magoho amedai mbele ya Hakimu Mkazi Hamisi Ally kuwa, washtakiwa qametenda kosa hilo la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kati ya Julai 17 na Septemba 29 mwaka huu ndani ya Jiji la Dar es Salaam

Imedaiwa, siku hiyo washtakiwa hao kwa pamoja na kwa kudanganya walijipatia kutoka kwa Dr. Abdi Hirsi Warsame kiasi cha milioni 55 kwa kumdanganya kuwa wangemsambazia vifaa tiba vya hospitality huku wakijua kwa siyo kweli.
Hata hivyo, washtakiwa wote  wamekana kutenda kosa hilo na wamerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambapo wametakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya sh. M. 27.5 kila mmoja.
Pia ametakiwa kuwasilisha fesha taslimu kiasi cha Sh. 27.5 au kuwasilisha hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha.Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirisha hadi Julai 12 (kesho) kwa ajili ya dhamana.

KMC FC YANASA SAINI YA KIUNGO MTANZANIA ANAYEKIPIGA TUSKER FC KENYA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Timu ya KMC Fc imeendelea na usajili wake wa kuzidi kuimarisha kikosi chao kinachonolewa na Kocha Mrundi Etienne Ndayiragije kwa kumsajili kiungo mshambuliaji Abdul Hillary Hassan aliyekua anakipiga katika timu ya Tusker Fc ya Nchini Kenya.

Hillary mwenye umri wa miaka 23 na refu wa futi 6 amesaini kandarasi ya mwaka mmoja kwa ajili ya kukitumikia kikosi hicho kilichopanda ligi kuu msimu wa 2018/19.Mchezaji huyo anayetumia miguu yote kwa ufasaha amekulia katika kituo cha DYOC (Dar es saalam Youth Olimpic Centre) na msimu wa 2014-16 wa ligi kuu Tanzania Bara Aliweza kucheza timu ya African Lyon kabla ya kutimkia nchini Kenya.

Mwaka 2017, Hillary alianza kutumikia ligi kuu ya kenya na kufanikiwa kuchezea katika timu ya Tusker fc ambayo uwezo wake aliouonesha uliweza kumpa nafasi ya kuitwa timu ya taifa Kilimanjaro Stars na kushiriki michuano ya CECAFA Senior challenge cup 2017.Mchezaji huyo ametia saini kandarisi hiyo mbele ya Meneja wa timu Walter Harrison tayari kwa kuanza kazi ya kuhakikisha KMC itaendelea kusalia katika ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Mpaka sasa KMC wamefanikiwa kunasa saini za wachezaji wazoefu wa Ligi Kuu Kama Juma Kaseja kutoka Kagera, Humud, Ally Ally kutoka Stand United na wengineo.
Kiungo Mshambuliaji  Abdul Hillary Hassan akiwa pamoja na Meneja wa timu ya KMC Fc (Kushoto) Walter Harrison baada ya kusaini kandarasi ya mwaka mmoja kutumikia kikosi hicho.

RC MAKONDA AKABIDHI MWENGE WA UHURU MKOA WA PWANI.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo Julai 12 amemkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo baada ya Mwenge huo kukamilisha shughuli ya uzinduzi na uwekaji wa mawe ya msingi kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 32.

RC Makonda amesema kuwa ndani ya siku tano ambazo mwenge ulikuwa jijini Dar es salaam umefanikiwa kutembelea, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi 36 ya maendeleo kwenye wilaya zote tano. 

Aidha RC Makonda amewashukuru wananchi wa Dar es salaam kwa ushirikiano mkubwa walioonesha tangu siku mwenge ulipoingia hadi leo alipoukabidhi kwa mkoa wa Pwani.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo mapema leo baada ya Mwenge huo kukamilisha shughuli ya uzinduzi na uwekaji wa mawe ya msingi kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 32 Mkoani Dar Es Salaam.

“GHARAMA ZA UENDESHAJI WA VYAMA VIKUU VYA USHIRIKA KUDHIBITIWA”-DKT TIZEBA

$
0
0
Na Mathias Canal-WK, Bukoba-Kagera

Malalamiko ya muda mrefu ya wakulima yaliyokuwepo kwamba ushirika unatoa bei ndogo, sasa yamepatiwa muarobaini baada ya serikali kupitia kwa kina gharama za uendeshaji na uongezaji thamani kwa zao la kahawa kwa Vyama vikuu vya ushirika Mkoani Kagera.

Serikali imepiga marufuku kwa vyama hivyo vya ushirika kutoza zaidi ya shilingi 490 kwa kilo moja ya Kahawa ya maganda kama gharama za uendeshaji na uongezaji thamani, Awali maainisho ya gharama hizo yalikuwa ni makubwa ambapo kiasi cha shilingi 1350 kwa kilo moja ya Kahawa ya maganda ilianishwa kama gharama za uendeshaji.

Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba ameeleza agizo hilo Leo 12 Julai 2018 wakati akizungumza na wajumbe wa Halmshauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera kwenye Hoteli ya Bukoba Coop ambapo miongoni mwa ajenda ya kikao hicho ilikuwa ni kujadili kuhusu soko la Kahawa na uendeshaji wa ushirika.

Dkt Tizeba amewaeleza wajumbe hao kuwa amepiga marufuku hiyo kufuatia malalamiko ya wadau wa Kahawa Mkoani Kagera ambapo gharama hizo zilionekana kuwa kubwa ukilinganisha na gharama halisi.

"Ndugu zangu wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM inawezekanaje shilingi mia mbili inatozwa kama ushuru wa chama kikuu, na shilingi mia mbili tena inatozwa kama ushuru wa chama cha msingi, ni nani anaweza kukupa faida namna hii sasa rasmi ushuru huu tumeupunguza kama nilivyoeleza" Alikaririwa Mhe Tizeba
Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akitoa ufafanuzi kuhusu sintofahamu ya biashara ya kahawa wakati akizungumza kwenye mualiko maalumu na wajumbe wa Halmshauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera kwenye Hoteli ya Bukoba Coop, Leo 12 Julai 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-WK)
Wajumbe wa Halmshauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wakisikiliza ufafanuzi wa Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba kuhusu sintofahamu ya biashara ya kahawa wakati akizungumza kwenye mualiko maalumu na wajumbe wa Halmshauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa kwenye Hoteli ya Bukoba Coop, Leo 12 Julai 2018.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera Bi Costansia Buhiye akitoa neno kwa niaba wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Mkoani humo mbele ya Waziri Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba kutokana na ufafanuzi alioutoa kuhusu sintofahamu ya biashara ya kahawa wakati akizungumza kwenye mualiko maalumu na wajumbe wa Halmshauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera kwenye Hoteli ya Bukoba Coop, Leo 12 Julai 2018.
Waziri Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akijadili jambo na Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Kagera Mhe Oliver Semuguruka mara baada ya kutoa ufafanuzi kuhusu sintofahamu ya biashara ya kahawa wakati akizungumza kwenye mualiko maalumu na wajumbe wa Halmshauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera kwenye Hoteli ya Bukoba Coop, Leo 12 Julai 2018.



Tutamfunga Simba kutetea ubingwa wetu-Azam fc

$
0
0
Na Agness Francis,globu ya jamii

Azam fc yatamba kumgaragaza mnyama simba katika fainali za kuwania kombe la kagame cup (CECAFA).

Timu hizo zote mbili za kutoka hapa nchini ambazo zimefanikiwa kutinga fainali, zitashuka dimbani kesho majira ya saa 12 jioni kuchoshana nguvu katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Mara baada ya jana Azam FC kumuondosha Gor Mahia ya Nchini Kenya katika michuano hiyo kwa kipigo cha mabao 2-0, sasa wanakutana na wekundu wa msimbazi katika kumjua nani ataibuka kidedea wa kombe hilo.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam msemaji wa Azam FC Jaffary maganga amesema kuwa kikosi chao kimejipanga vizuri kuhakikisha wanatetea ubingwa wao wa mwaka 2015 ambapo michuano hiyo ilifanyika kwa mara ya mwisho hapa nchini,Jaffary amesema maandalizi waliyofanya ni mazuri na ndio maana wamefanya vema na mpaka kufikia hatua hiyo.

"Tunaiheshimu Simba ni timu kongwe ya muda mrefu ilio na kikosi mahiri lakini sisi azam tunaliamini benchi letu la ufundi pamoja na mwalimu,tunaahidi kufanya vizuri kwa kumfunga simba"amesema jaffary.

Mtanange huo utakaokuwa wa ina yake wa kiburudani kwa mashabiki ,inaonyesha zahiri kuwa soka la Tanzania limezidi kuimarika katika ukanda huu wa Afrika mashariki na kati.
Msemaji wa Azam FC Jaffary maganga

CLEMENT SANGA AVULIWA UENYEKITI BODI WA LIGI

$
0
0
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imekubaliana na mapendekezo ya Kamati ya Sheria na Katiba ya kumsimamisha, Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Clement Sanga baada ya kukosa sifa za Uenyekiti wa Bodi hiyo. 

Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye ukumbi wa mikutano wa TFF uliopo Uwanja wa Karume mjini Dar es Salaam, Rais wa shirikisho hilo, Wallace Karia amesema kwamba hatua imefuatia Mkutano wa Juni 10 wa wanachama wa Yanga kusema bado unamtambua Yussuf Manji kama Mwenyekiti wao.

Karia amesema kwamba Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi anatakiwa awe Mwenyekiti wa klabu ya Ligi Kuu, Sanga amepoteza sifa za kuwa kiongozi Mkuu wa bodi hiyo.

"Tulipokea barua Julai 12 kutoka klabu ya Yanga ikidai kuwa Sanga hatambuliki kama Mwenyekiti wa klabu hiyo, wao Yanga wanamtambua Yussuf Manji ndiye Mwenyekiti wa klabu hiyo na katika nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi unatakiwa Uwe Mwenyekiti wa klabu yako," amesema Karia 

Katika hatua nyingine, Karia amesema Kamati ya Utendaji imempitisha rasmi Wilfred Kidao kuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kukaimu kwa muda mrefu.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) Wallace Karia akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kumvua uenyekiti wa bodi ya Ligi Makamu Mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga leo Jijini Dar es Salaam.

WAZIRI KANGI LUGOLA AFANYA KIKAO NA MAAFISA,ASKARI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI, JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza wakati wa Kikao na Maafisa na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. Katikati ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye na kushoto ni Kamishna wa Usalama dhidi ya moto, Jesuald Ikonko. Kikao hicho kimefanyika ofisi ndogo ya wizara jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza wakati wa Kikao na Maafisa na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. Katikati ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye na kushoto ni Kamishna wa Usalama dhidi ya moto, Jesuald Ikonko. Kikao hicho kimefanyika ofisi ndogo ya wizara jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Operesheni Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage, akiwasilisha taarifa ya shughuli za jeshi hilo mbele ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (wapili kulia), wakati wa ziara ya waziri alipotembelea makao makuu ya jeshi hilo, jijini Dar es Salaam.
Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (hayupo pichani), wakati wa ziara ya waziri kutembelea jeshi hilo, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Viewing all 110025 articles
Browse latest View live




Latest Images