Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110031 articles
Browse latest View live

Tigo Yazindua Kampeni mpya ya ‘Tigo Pesa ni Zaidi ya Pesa’

$
0
0
Kampuni ya Tigo Tanzania, leo imezindua kampeni ya ‘Tigo Pesa ni Zaidi ya Pesa’, kama uthibitisho kuwa huduma hiyo sasa ina hadhi ya huduma kamili ya kifedha ambayo inawapa wateja huduma za kipekee, bora na  nyingi zaidi kupitia mtandao wa simu. 

‘Tigo Pesa ni Zaidi ya Pesa’ inazingatia sifa ya Tigo kuwa mtandao pekee unaobuni huduma na bidhaa kulingana na mahitaji ya wateja ili kuboresha na kurahisisha maisha yao. 

‘Tigo Pesa imepanua wigo wa bidhaa na huduma zake na kuibua njia bora zaidi kwa wateja kufurahia huduma za haraka, uhakika na salama za kifedha popote walipo nchini Tanzania,’ Hussein Sayed, Afisa Mkuu wa  Huduma za Kifedha wa Tigo aliwaambia waandishi wa habari. 

Kama sehemu ya kampeni hii, Tigo Pesa inajivunia kuwa mtandao pekee na wa kwanza wa simu unaotoa huduma inayowezesha wateja wa Tigo kurudisha miamala ya fedha zilizotumwa kimakosa kwenda kwa wateja wenzao wa Tigo.  Huduma hiyo inayopatikana kupitia menu ya Tigo Pesa  *150*01# inawapa wateja wa Tigo uwezo wa kurudisha kwa haraka miamala yoyote ya kutuma hela ikiwa watagundua kuwa wamekosea miamala hiyo, bila ya kuhitaji msaada wa moja kwa moja kutoka kitengo cha huduma kwa wateja. 

‘Huduma hii ya kipekee ya kurudisha miamala iliyokosewa kwa haraka inajibu mahitaji ya wateja wengi ambao kwa sababu moja au nyingine wanafanya makosa pindi wanapotuma pesa. Ni huduma ya aina yake ambayo inawapa wateja uwezo zaidi juu ya miamala wanayofanya na imeundwa kwa kuzingatia vigezo vya hali ya juu vitakavyozuia matumizi mabaya ya huduma hii,’ Hussein alifafanua
Afisa Mkuu wa  Huduma za Kifedha wa Tigo, Hussein Sayed (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya ‘Tigo Pesa ni Zaidi ya Pesa.’ Tigo Pesa pia imezindua huduma mpya ya Jihudumie itakayowasaidia wateja wa Tigo kurudisha miamala ya kutuma fedha waliyokosea, bila kuhitaji msaada kutoka kitengo cha huduma kwa wateja. Kulia ni Mkuu wa Udhibiti Ubora wa Tigo Pesa, Angelica Pesha.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

VIJIJI 56 MANONGA KUPATA UMEME MWAKA WA FEDHA 2018/2019

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

MBUNGE wa Manonga Seif Gulamali ameeleza mkakati wake katika kusimamia miradi ya maendeleo kwa bajeti ya mwaka 2018/2019 ambapo amesema kuwa huduma kama afya, elimu na miundombinu ni muhimu na lazima jimboni humo.

Akizungumza na Michuzi blog Gulamali emeeleza kuwa vijiji vyote vya jimbo la Manonga vitapata umeme mwaka huu wa fedha 2018/2019.

Kuhusu huduma za afya Manonga amesema kuwa wamefanikiwa kujenga kituo cha afya kilichogharimu Sh. milioni 400 na hiyo ni katika kuwasaidia wananchi kutotembea umbali mrefu kufuata huduma za afya na kituo hicho kina jengo la upasuaji, jengo la kuhifadhia maiti, jengo la mama na mtoto, maabara ya kisasa, jengo la kufulia na nyumba ya mganga katika kituo cha afya Simbo.

Aidha ameeleza wanaelekea kupata shule ya kwanza jimbo la Manonga na shule 3 Wilaya ya Igunga kuwa na kidato cha 5 na 6 kwani hadi sasa mabweni 4 na madarasa 2 kwa ajili ya kidato cha tano na sita yamekamilika katika shule ya Sekondari Ziba.

Kuhusu ujenzi wa daraja la Manonga kutoka Choma kwenda Shinyanga ambalo limekuwa ni kilio kwa miaka 50 Gulamali ameeleza kuwa wamepata zaidi ya shilingi Milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo.Aidha ameeleza kiwanda cha pamba cha Manonga kilichokufa kwa miaka 20 kimefufuliwa na kinatoa ajira zaidi ya 500 kwa vijana wa Igunga, Tabora na nchini kwa ujumla na hii ina inatoa fursa kwa wajasiriamali hasa mama ntilie kwa kupata kipato kutokana na huduma wanazozitoa.

Kuhusu mradi mkubwa wa maji kutoka Mwanza hadi Igunga Gulamali ameiambia blogu ya jamii kuwa zaidi ya dola milioni 265 za kimarekani zimetengwa kwa ajili kutekeleza mradi huo na vijijji na kata zitapata maji kupitia mradi huo pia vijiji vya Mwisi, Mwamala na Sungwizi vitapata maji kutoka fedha kiasi ya Milioni 600 iliyotengwa kwa ajili ya mradi wa maji.

Gulamali ametoa rai kwa wananchi kutumia fursa zinazotolewa hasa katika elimu kwa kuwasihi wanafunzi kusoma kwa bidii kwani kama serikali wamewekeza sana katika elimu na watahakikisha wanatengeneza mazingira bora katika upatikanaji wa elimu bora.

MTENDAJI WA KIJIJI KURUYA APEWA SIKU 19 KUREJESHA FEDHA ALIZOTAFUNA

$
0
0
Na Frankius Cleophace, Rorya

SERIKALI imemsimamisha kazi Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Kuruya katika Kata ya Komuge wilayani Rorya mkoani Mara Mwita Mangondi kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha Sh.1,960,387 ikiwa ni pamoja na kushindwa kusomea wananchi mapato na matumizi huku akipewa siku 19 kurejesha mara moja fedha hizo.

Ofisa Mtendaji huyo amesimamishwa kazi katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Kuruya baada ya wananchi kutoa kilio chao cha muda mrefu kuhusu kutosomewa mapato na matumizi tangu Mwaka 2012 mpaka sasa.

Ambapo wamezidi kutupia lawama viongozi waliopo kuanzia ngazi za Vijiji hadi kata.Ofisa Utumishi Wilaya ya Rorya Peter Masanja akiwa katika mkutano huo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Charles Chacha amesema asimamisha kazi mtendaji huyo nakumpa siku 19 kurudisha fedha hizo. Pia anatakiwa kuripoti kila siku ofisi ya Mtendaji wa kata

Amesema kuwa kitendo cha Mtendaji huyo kufanya ubadhirifu wa fedha hizo kutokana na sheria za utumishi hawawezi kulifumbia macho hivyo amewataka wananchi kuwa wavumilivu kuhusu kumwondoa madarakani mwenyekiti wa Kijiji hicho kutokana na tuhuma walizozisema wananchi katika mkutano huo.

“Mimi Mamlaka niliyonayo ni ya kuondoa Mtendaji wa kijiji lakini sina mamlaka ya kuondoa Mwenyekiti nyie ndo wenye mamlaka mkifuata taratibu lakini kwa sasa mkimwondoa Halmashauri hautuafanya uchaguzi mpaka mwakani sasa baadhi ya maendeleo yatazidi kukwama niwasihi kuwa wavumilivu,” amesema.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Komuge William Nestory amesema kuwa endapo fedha hizo hazitarudishwa ataungana na wananchi kutoa taarifa eneo husika.Huku akiomba Ofisa utumishi kutilia mkazo kufanyika kwa mikutano ya kisheria ili wananchi wasomewe mapato na matumizi kwani suala hilo limekuwa changamoto kubwa katika vijiji vinavyounda kata yake.
Afisa utumishi Wilaya ya Rorya Mkoani Mara Peter Masanja akiongea na Wananchi katika Mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Kuruya kata ya Komuge Wilayani Rorya Mkoani Mara.
Wananchi wa kijiji cha Kuruya wakiwa katika Mkutano wa hadhara.
Wananchi wa kijiji cha Kuruya wakiwa katika Mkutano wa hadhara.
Mtendaji wa kijiji cha Kuruya Mwita Mangondi aliyesimamishwa Kazi katika Mkutano huo akijibu baadhi ya hoja za Wananchi zikiwemo tuhuma zake za ubadhilifu wa fedha.

MZEE MANGULA ATEMBELEA BANDA LA NSSF MAONESHO YA SABA SABA JIJINI DAR LEO

$
0
0
Kaimu meneja wa Uhusiano na Masoko,Salim Khalfan akitoa ufafanuzi wa huduma zinazopatikana ndani ya NSSF kwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Tanzania Bara, Philip Mangula alipotembelea banda la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF leo asubuhi kwenye maonesho ya biashara ya 42 ya kimataifa yanayoendelea jijini Dar es salam,Ndugu Mangula pia alipata fursa ya kujionea shughuli mbalimbali zitolewazo na Shirika hilo,Pichani kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Professa Godius Kahyarara

YANGA NA SIMBA UGHAIBUNI YATOA TUZO KUMUENZI ALPHONCE MODEST

$
0
0

Mchezaji Shaban Mwampambe (mwenye kipaza sauti)  akiongelea historia ya mchezajiAlphonce Modest ambaye kwa sasa ni mgonjwa siku ya Jumamosi July 7, 2018 siku ilipofanyika Old School Reunion DMV huko Marekani iliyoenda sambamba na utoaji tuzo kwa mchezaji huyo katika kumuenzi na kuthamini mchango wake kwenye soka la Tanzania enzi zake alipochezea timu za Simba, Yanga, Mlandege na timu ya Taifa.Picha na VijimamboBlog


Bongo Movie Monalisa akikabidhi tuzo ya Alphonce Modest kwa refa wa FIFA Kazi Kipenga aliyeipokea kwa niaba yake.


Refa wa FIFAKazi Kipenga akielezea jinsi alivyosaidia kumfikisha Alphonce Modest hospitali.

Agro & Poultry Tanzania @ Mlimani Conference Centre in September 2018

$
0
0
The Agro & Poultry Tanzania 2018 targets Agriculture, Irrigation,Poultry, Veterinary, Animal Feed, Vegetables, Fruit , Maize,Wheat, Tractors companies for their participation.

Minimum Booth/Stand size is 9 SQM and price for per sqm is USD 150. 
Therefore, the price for 9 SQM booth is USD 1350. We will provide them 1 table, 2 chairs, electrical socket,Company name fascia and listing in the exhibition Catalog.
Companies can take more than 9 sqm booth. i.e.. 12,15, 18, 21 etc. So the price will be adjusted to that particular space
Looking forward to hearing from you

WASHINDI WA AMSHA AMSHA USHINDE NA AIRTEL MONEY DROO YA TATU WAPATIKANA

$
0
0
Mkazi wa Morogoro, Frank Kisayo ameshinda zawadi ya televisheni ya kisasa aina ya Samsung yenye ukubwa wa inchi 32 kupitia promosheni ya Amsha Amsha Ushinde na Airtel Money ambayo inaendeshwa kampuni ya simu ya Airtel Tanzania na kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa.

Kisayo ambaye ni mkulima, alishinda televisheni hiyo kwenye droo ya tatu iliyofanyika kwenye Ofisi Makao Makuu ya Ofisi za kampuni ya simu ya Airtel jijini.

Akizungumza kwa njia ya simu mara baada kushinda droo hiyo, Kisayo alisema kuwa amefurahi sana kushinda zawadi hiyo yenye thamani si chini ya Sh750,000.

“Siamini kama nimeshinda, nasubiri kwa hamu zawadi yangu, naamini sasa suala la kununua televisheni kwangu limeisha baada ya kushinda zawadi hii nono ya droo ya Amsha Amsha,” alisema Kisayo.

Mbali ya Kisayo, pia Masoud Saleh wa Kisarawe  na Shadrack Sanga wa Manyara kila mmoja alishinda simu ya mkononi aina ya Samsung Galaxy yenye thamani Sh500,000.

Pia Eric  Samwel ambaye ni mkazi wa Tanga alijishindia jezi na tiketi ya msimu ya kuona mechi ya Yanga na Simba za msimu ujao.

Maneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando alisema kuwa mpaka sasa washindi watatu wa televisheni, simu 25 na jezi 25 wamepatikana katika droo hiyo.
Meneja Matukio wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Dangio Kaniki, akiongea na moja ya washindi wa AMSHA AMSHA USHINDE NA AIRTEL MONEY kwa kushirikiana na Sportpesa, Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja Uhusiano Sabrina Msuya Kushiriki, mteja atatakiwa kupiga *150*60# kisha kutuma pesa kwenye akaunti ya SportPesa namba 150888 kisha kuweka kubashiri.
Meneja Uhusiano SportPesa Sabrina Msuya, akiongea na moja ya washindi wa AMSHA AMSHA USHINDE NA AIRTEL MONEY kwa kushirikiana na Sportpesa, Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja Matukio Airtel Tanzania. Mteja atatakiwa kupiga *150*60# kisha kutuma pesa kwenye akaunti ya SportPesa namba 150888 kisha kuweka kubashiri.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Wananchi Mtego wa Simba wafurahia kuwashiwa umeme

$
0
0
Na Veronica Simba – Morogoro
Wananchi wa Kijiji cha Mtego wa Simba, Kata ya Mikese, Wilaya ya Morogoro Vijijini, wameshindwa kuzuia furaha yao baada ya Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, kuzindua rasmi uwashaji wa umeme katika Kijiji hicho, kupitia Mradi wa Umeme Vijijini, Awamu ya Tatu, Mzunguko wa Kwanza (REA IIIA.)
Tukio hilo la kuwasha umeme, lilifanyika Jumatano, Julai 11, 2018 na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mjini, Regina Chonjo ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa, Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, Omari Mgumba, Madiwani na Wenyeviti wa Vijiji.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi, ambao muda wote walionesha bashasha, Mgumba ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kilimo, aliishukuru Serikali kupitia Wizara ya Nishati, kwa kuendelea kutekeleza ahadi ya kuwapelekea wananchi, hususan walioko vijijini nishati ya umeme.
“Serikali iliahidi kwamba itasambaza umeme kwa vijiji vyote vilivyobaki, kwenye Awamu mbili za REA III. Tunatoa shukrani sana kwa kuja hapa leo kutekeleza ahadi hiyo kwa vitendo.”
Akizungumza katika Hafla hiyo, Naibu Waziri aliwaeleza wananchi kuwa baada ya uzinduzi huo, wataanza kuunganishiwa umeme katika nyumba zao kuanzia Ijumaa, Julai 13, mwaka huu.
“Nimeongea na Mkandarasi, kuanzia Ijumaa, zile nyumba za awali 62 zote zitawekewa umeme.”
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati) akifurahia baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa uwashaji umeme katika kijiji cha Mtego wa Simba, Kata ya Mikese, Wilaya ya Morogoro Vijijini, Jumatano, Julai 11, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mjini, Regina Chonjo na wa kwanza kulia ni Naibu Waziri wa Kilimo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, Omari Mgumba.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza wakati wa Hafla ya uzinduzi rasmi wa uwashaji umeme katika kijiji cha Mtego wa Simba, Kata ya Mikese, Wilaya ya Morogoro Vijijini, Jumatano, Julai 11, 2018.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati) akiwasha taa ya umeme, katika moja ya vyumba vya Zahanati ya Kijiji cha Towero, Kata ya Mlimani, Wilaya ya Morogoro Mjini, Jumatano, Julai 11, 2018. Naibu Waziri alitembelea Zahanati hiyo kujiridhisha endapo agizo alilotoa kwa TANESCO kuiunganishia umeme limetekelezwa. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mjini, Regina Chonjo na wa kwanza kulia ni Meneja wa TANESCO wa Kanda ya Kati, Mhandisi Athanas Nangali.
 Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu, akiwaonesha wananchi wa Kijiji cha Mtego wa Simba, Kata ya Mikese, Wilaya ya Morogoro Vijijini, kifaa kitumikacho kuwasha umeme pasipo kutandaza nyaya katika nyumba, kijulikanacho kama Umeme Tayari (UMETA). Alikuwa katika ziara ya kazi kijijini hapo ambapo alizindua rasmi uwashaji wa huduma ya umeme, Jumatano, Julai 11, 2018.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MASHAHIDI KATIKA KESI INAYOMKABILI TIDO MHANDO KUENDELEA KUSIKILIZWA JULAI 18

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii

 MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka katika kesi inayomkabili Mkurugenzi mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando utaendele kusikilizwa Julai 18 mwaka 2018.

Ushahidi dhidi ya kesi hiyo ulipaswa kuendelea kusikilizwa leo Julai 11 mwaka huu lakini Wakili wa Takukuru, Leonard Swai amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu , Huruma Shaidi kuwa shahidi waliyemtarajia atoe ushahidi amepatwa na udhuru hivyo akaomba kesi hiyo ipangiwe tarehe nyingine.Kutokana na taarifa hiyo, Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 18 mwaka huu kwa mashahidi wa upande wa mashtaka kuendelea kutoa ushahidi.

Katika kesi hiyo tayari mashahidi watatu wa upande wa mashtaka wamekwishatoa ushahidi ambao ni Ofisa uchunguzi wa Takukuru, Victor Lesuya, Mwanasheria wa TBC, Gwakisa Mlawa na Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa TBC, Clement Mshana.Tido anakabiliwa na mashtaka manne ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh.milioni 887.1

 Anadaiwa kuwa Juni 16, 2008,   akiwa  Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Tido ambaye alikuwa mkurugenzi wa TBC, kwa makusudi alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mkataba wa kuendesha na utangazaji wa vipindi vya televisheni kati ya TBC na Channel 2 Group Corporation (BV1) bila ya kupitisha zabuni, kitu ambacho ni kinyume na Sheria ya Manunuzi na kuinufaisha BVl.

Pia anadaiwa kutumia vibaya madaraka yake kwa kusaini makubaliano kwa utangazaji wa digitali duniani kati ya TBC na BVl. Agosti 11,mwaka  2008 na Septemba 2008 akiwa Dubai, mshtakiwa alisaini mkataba wa makubaliano kwa ununuzi, usambazaji kufunga vifaa vya usambazaji na mnara wa utangazaji kati ya TBC na BVI na kuifaidisha BVI.

Pia anadaiwa kusaini mkataba wa makubaliano kwa kuendesha miundombinu ya utangazaji (DTT Broadcast Infrastructure) kati ya TBC na BVI na kuinufaisha BVI.

Inadaiwa kuwa, kati ya Juni 16 na Novemba 16, 2008 akiwa UAE, Tido aliisababishia TBC hasara ya Sh. 887,122,219.19.

IGP AWAOMBA VIONGOZI WA DINI KUENDELEZA DORIA ZA KIROHO

$
0
0
Na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amewaomba Viongozi wa dini nchini kuendelea kufanya doria za kiroho huku Jeshi hilo likiendeleza doria za kimwili kwa pamoja ili kuukabili uhalifu ikiwemo mauaji yanayosababishwa na wivu wa mapenzi ambayo yameanza kuongezeka katika siku za hivi karibuni.
IGP Sirro ameyasema hayo  kwa nyakati tofauti katika Wilaya za Ukerewe na Sengerema mkoani Mwanza wakati wa Ziara yake inayoendelea katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa yenye lengo la kubaini changamoto za kiuhalifu na kuzipatia ufumbuzi wa haraka ili wananchi waendelee kufanya kazi zao kwa Amani na utulivu.
Amesema Polisi wanafanya doria za kimwili ambazo wakati mwingine hutumia nguvu kushurutisha watu kutii sheria lakini Viongozi wa dini nao wana nafasi yao katika jamii kwa kufanya doria za kiroho na kukemea maovu.
IGP Sirro amesema makosa ya mauaji yanayosababishwa na wivu wa mapenzi yameanza kujitokeza kwa kasi katika siku za karibuni hivyo viongozi wa dini wana nafasi kubwa zaidi kuwaelimisha waumini wao kabla vifo havijatokea kwa kuwa wengi wao wanakuwa nao kila siku za ibada. 
Katika hatua nyingine IGP Sirro ameahidi kuchangia Shilingi milioni kumi na tano ili kusaidia ujenzi wa kituo cha Polisi katika  Kisiwa cha Kome, Wilayani Sengerema baada ya Wananchi kuomba kujengewa kituo hicho ili kukabiliana na uhalifu.
Wakizungumza katika mkutano wa hadhara Kisiwani Kome Wananchi hao walisema kujengwa kwa kituo hicho kutasaidia kuimarisha usalam katika maeneo hayo huku wakiomba kufufuliwa kwa Vikundi vya Ulinzi Shirikishi.
IGP anaendelea na ziara yake huku akitumia usafiri wa Helkopta ili kujionea kwa uhalisia maeneo hayo ili kuweza kuzipatia ufumbuzi changamoto za uhalifu.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na Wakazi wa Kisiwa cha Kome Wilayani Sengerema mkoa wa Mara wakati wa Ziara yake ya kubaini changamoto za uhalifu na kuzipatia ufumbuzi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa. (Picha na Jeshi la Polisi)
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana na wakazi wa Wilaya ya Sengerema waliojitokeza kwa wingi kumlaki alipowasili Wilayani humo ikiwa kwa ajili ya kuendelea na Ziara yake ya kubaini changamoto za uhalifu na kuzipatia ufumbuzi.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akionyesha ukakamavu wakati wa kuimba na askari wa Kikosi cha kutuliza ghasia mkoa wa Mara baada ya kumaliza ziara yake mkoani humo ya kubaini changamoto za uhalifu na kuzipatia ufumbuzi. (Picha na Jeshi la Polisi)
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akiwasalimu viongozi wa dini kabla ya kuanza kikao nao Wilayani Serengeti ikiwa ni muendelezo wa Ziara yake ya kubaini changamoto za uhalifu na kuzipatia ufumbuzi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa. 
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana na  viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama Wilayani Ukerewe baada ya kuwasili wilayani humo kuendelea na Ziara yake ya kubaini changamoto za uhalifu na kuzipatia ufumbuzi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa. 

SERIKALI KUFUTA TOZO YA USAJILI,KUHUWISHA NA KUSHIKILIA USAJILI KWA WAWEKEZAJI WA NDANI

$
0
0

NA WAMJW-MWANZA
SERIKALI kupitia wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imefuta tozo ya usajili , kuhuwisha pamoja na kushikilia usajili wa bidhaa zao kwa wawekezaji wa ndani kupitia Mamlaka ya chakula na Dawa TFDA .
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,J insia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati alipotembelea kuangalia ujenzi wa jengo la TFDA ambalo linajengwsa Jijini Mwanza ili kusogeza huduma kwa wananchi wa mkoa huo.
“Ili kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. John Pombe Magufuli za kukuza nchi kupitia uchumi wa viwanda hivyo TFDA msiwe kikwazo kwa wawekezaji hao hivyo kuanzia leo nafuta tozo za kusajili bidhaa,kuhuwisha bidhaa na tozo ya kushikilia usajili wa bidhaa”, alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa kuendana na juhudi hizo pia Serikali  imefuta tozo ya udhibiti  ya thamani ya 0.25 za dawa,vifaa na vifaa tiba zinazoingizwa kwenye hospitali za Umma kutoka kwa wafadhili.
Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa TFDA ina wajibu wa kusimamia Tanzania isiwe jalala la bidhaa zisizo na ubora kwa watanzania hivyo wanatakiwa kuweka afya ya wananchi mbele kuliko manufaa binafsi.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Bi. Agness Kijo amesema kuwa ujenzi wa jengo hilo ukikamilika utasaidia kuhudumia huduma za kimaabara kwa bidhaa zinazoingia nchini kwani itakuwa sio lazima tena kwenda kupima bidhaa hizo jijini Dar es salaam.
 Waziri wa afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katikati akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu Wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kushoto wakati alipotembelea kukagua shughuli za ujenzi wa jengo la Mamlaka hiyo jijini Mwanza. Kulia ni Mkurugenzi wa Ubora wa Huduma za Afya kutoka Wizara ya afya Dkt. Mohammed Mohammed.
 Waziri wa afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kulia akipata maelezo juu ya sukari zinazopimwa ubora wake  kutoka kwa Mkuu wa Maabara wa TFDA  Kanda ya Ziwa Bw. Salum Kindoli wakati alipotembelea kukagua shughuli za ujenzi wa jengo la Mamlaka hiyo jijini Mwanza.
 Waziri wa afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kulia  akipata baadhi ya maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Ubora wa Huduma za Afya kutoka Wizara ya afya Dkt. Mohammed Mohammed kushoto wakati alipotembelea kukagua shughuli za ujenzi wa jengo la Mamlaka hiyo jijini Mwanza.
 Waziri wa afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katikati akikagua shughuli za ujenzi wa jengo la wodi ya mama na mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou toure wakati alipotembelea kukagua shughuli za ujenzi wa jengo hilo jijini Mwanza.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI MKUU AHUTUBIA MKUTANO WA HALMASHAURI KUU YA CCT JIJINI DODOMA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na  Makamu wa Kwanza wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Askofu Dkt. Fredrick Shoo wakati alipowasili kwenye ukumbi wa CCM jijini Dodoma kuhutubia Mkutano wa Halmashairi Kuu ya CCT Julai 12, 2018. Wapili kulia ni Mwenyekiti wa CCT, Askofu Dkt. Anilikisa Cheyo  na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Jukuiya ya Kikristo Tanzania (CCT)  jijini Dodoma, Julai 12, 2018. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCT, Askofu Dkt. Anilikisa Cheyo, na wapili kushoto ni Makamu wa Pili wa Mwenyekiti wa CCT, Askofu, Dkt. Jacob Chimeledya.
 Baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania  (CCT) wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCT jijini Dodoma Julai 12, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana  na  Makamu wa Kwanza wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo  Tanzania (CCT), Askofu Dkt. Fredrick Shoo baada ya kuhutubia Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCT jijini Dodoma Julai 12, 2018. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCT, Askofu Dkt. Anilikisa Cheyo na wapili kulia ni  Makamu wa Pili wa Mwenyekiti wa CCT, Askofu Dkt. Jacob Chimeledya. (Picha na  Ofisi ya Waziri Mkuu)

DC MONDULI AZINDUA KIWANDA KIDOGO CHA KUCHAKATA NGOZI

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe. Idd Hassan Kimanta Jumatano Julai 11, 2018 amezindua kiwanda kidogo cha kuchakata Ngozi na kutengeneza bidhaa za ngozi kiwanda hicho kipo katika kijiji cha Mswakini na kutoa vyeti kwa wanakikundi waliofuzu mafunzo.
Kiwanda hicho ni matokeo ya kikundi cha akinamama 22 ambao mwezi Agosti 2017 walijiunga pamoja na kupata ufadhili kutoka shirikikala OIKOS kwa lengo kujijenga kiuchumi kupitia Ngozi na kuunga mkono Juhudi za Serikaliya kuelekea Tanzania ya Viwanda.
Katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya huyo amewapongeza akinamama hao kwa uamuzi wao huo na kuwaahidi kuwa  kupitia halmashauri ya wilaya ya  Monduli atahakikisha wanapata Mkopo ili kuongeza mtaji.
Pia amelishukuru Shirika la Misaada la Marekani-USAID kwa kulipatia fedha shirika la OIKOS ambalo ndilo lililosimamia mchakato wote kupitia Mradi wa Ikolojia Hatarini Kaskazini mwa Tanzania.
Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe.Idd Hassan Kimanta  akikata utepe kuashiria uzinduzi kiwanda cha kuchakata bidhaa za ngozi zinazotengenezwa na kiwanda kidogo cha kuchakata Ngozi kilichopo katika kijiji cha Mswakini,wilayani Monduli
 Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe.Idd Hassan Kimanta  (pichani kati) akitazama baadhi ya bidhaa za ngozi zinazotengenezwa na kiwanda kidogo cha kuchakata Ngozi kilichopo katika kijiji cha Mswakini,wilayani humo.
 Mkuu wa Wilaya ya Monduli,Idd Hassan Kimanta akitoa vyeti kwa baadhi ya Wanakikundi waliofuzu mafunzo.
 Baadhi ya Bidhaa za ngozi zikiwa tayari kwa kuuzwa

WADAU WAKIWA MOSCOW KUSHUHUDIA UINGEREZA WAKIRUDISHWA NYUMBANI NA CROATIA

$
0
0
 
 Wadau wa Globu ya Jamii kutoka Tanzania Dhiresh Kaba, Moheel Kaba, Javier Diaz na Jay Kaba wakiwa Moscow kushuhudia kipute cha jana cha Croatia vs England
 Dhiresh Kaba akifurahia baada ya Croatia kusawazisha
Dhiresh Kaba, Moheel Kaba, Javier Diaz na Jay Kaba wakiwa Moscow kushuhudia kipute cha Croatia vs England
 Wadau Othman Tippo (kulia), Emma Rutagonya (kati) pamoja na Mboka wakiwa katika moja ya viwanja vya soka nchini Urusi kushuhudia kipute cha nusu fainali ya kombe la Dunia kati ya Croatia na England.

KMC FC YANASA SAINI YA KIUNGO MTANZANIA ANAYEKIPIGA TUSKER FC KENYA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Timu ya KMC Fc imeendelea na usajili wake wa kuzidi kuimarisha kikosi chao kinachonolewa na Kocha Mrundi Etienne Ndayiragije kwa kumsajili kiungo mshambuliaji  Abdul Hillary Hassan aliyekua anakipiga katika timu ya Tusker Fc ya Nchini Kenya.

Hillary mwenye umri wa miaka 23 na refu wa futi 6 amesaini kandarasi ya mwaka mmoja kwa ajili ya kukitumikia kikosi hicho kilichopanda ligi kuu msimu wa 2018/19.

Mchezaji huyo anayetumia miguu yote kwa ufasaha amekulia katika kituo cha DYOC (Dar es saalam Youth Olimpic Centre) na msimu wa 2014-16  wa ligi kuu Tanzania Bara Aliweza kucheza  timu ya  African Lyon  kabla ya kutimkia nchini Kenya.

 Mwaka 2017, Hillary alianza kutumikia ligi kuu ya kenya na kufanikiwa kuchezea katika timu ya Tusker fc ambayo uwezo wake aliouonesha uliweza kumpa nafasi ya kuitwa timu ya taifa Kilimanjaro Stars na kushiriki michuano ya CECAFA Senior challenge cup 2017.

Mchezaji huyo ametia saini kandarisi hiyo mbele ya Meneja wa timu Walter Harrison tayari kwa kuanza kazi ya kuhakikisha KMC itaendelea kusalia katika ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Mpaka sasa KMC wamefanikiwa kunasa saini za wachezaji wazoefu wa Ligi Kuu Kama Juma Kaseja kutoka Kagera, Humud, Ally Ally kutoka  Stand United na wengineo.
Kiungo Mshambuliaji  Abdul Hillary Hassan (kulia) akiwa pamoja na Meneja wa timu ya KMC Fc Walter Harrison (Kushoto) baada ya kusaini kandarasi ya mwaka mmoja kutumikia kikosi hicho.

TAMASHA LA MAJIMAJI SELEBUKA KUFANYIKA JUMAMOSI

$
0
0
Na Mwandishi Wetu,
TAMASHA la Majimaji Selebuka linalohusisha mashindano ya  mbio za baiskeli, riadha, ngoma za asili na Midahalo kwa wanafunzi wa shule  mbalimbali za Sekondari katika  Manispaa ya Songea mkoani RuvumaTamasha hilo linatarajiwa kufunguliwa siku ya Jumamosi katika uwanja wa  michezo wa Majimaji mjini Songea.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, mtaratibu wa Tamasha hilo Osam Ulaya alisema tamasha la mwaka huu litakuwa tofauti na matamasha mengine yaliyowahi kufanyika hapo awali.

Kwa mujibu wa Osama, Tamasha la mwaka huu litashirikisha pia vikundi vya ngoma vya asili kutoka mkoa jirani wa Mbeya,  ambavyo vitashindana na vikundi vya ngoma vilivyopo katika  manispaa ya Songea kwa lengo la kuleta hamasa na litasaidia sana kuinua kipato kwa wananchi wa manispaa  ya Songea, ambao watatumia fursa hiyo kufanya Biashara na wageni watakao udhuria.

Ulaya alisema, pia Tamasha la Mwaka huu wameongeza kipengele cha Ujasiriamali ambapo zaidi ya vikundi 10 tayari vimeshathibitisha kushiriki, sambamba na washiriki kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania.

Hata hivyo Ulaya alisema, Tamasha la 2018 linatarajiwa kuhudhuriwa na  Balozi wa Norway na Balozi wa Poland hapa nchini ambao wamependa kushiriki Tamasha hilo ambalo litakuwa chachu ya maendeleo kwa wakazi wa Songea na mkoa wa Ruvuma.

Aidha alisema,  Mdahalo wa mwaka huu utafanyika kwa lugha ya Kiswahili badala ya Kiingereza ili kutoa nafasi kwa wanafunzi wa shule za sekondari kuonesha uwezo wao katika matumizi ya lugha ya Taifa na namna wanavyoielewea  vizuri wilaya ya Songea ambayo ina fursa nyingi ambazo bado hazifanyiwa kazi.

Alisema, katika Tamasha hilo washindi watapata zawadi mbalimbali ikiwemo fedha taslimu na washindi wa kwanza hadi wa tatu katika  mchezo wa riadha watapata nafasi ya kwenda Nchini Afrika Kusini kushiriki mbio za Marathon.
Kwa upande wake, Godfre Mvulla ambaye ni  katibu wa Chama cha Mpira wa miguu Manispaa ya Songea(SUFA)alisema, katika Tamasha la Mwaka huu wachezaji wa  zamani wa Timu  za Simba na Yanga watashiriki kwa kucheza mchezo maalum.

Mvulla alisema, mchezo huo ambao utaonesha na kituo cha Azam Tv na utatangazwa  na watangazaji nguli Charles Hilary na Sued Mwingi na kiingilio katika mchezo huo itakuwa shilingi 2000 ambayo itamwezesha kila mwanachi kuhudhurioa mchezo huo.
Mratibu wa Tamasha la Majimaji Selebuka Sam Ulaya (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari mjini Songea kuhusiana na maandalizi ya Tamasha hilo linalo tarajiwa kufunguliwa siku ya Jumamosi katika Uwanja wa Michezo wa Majimaji mjini Songea. Katikati ni katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu katika  Manispaa ya Songea,  God Mvulla na Kulia mwamuzi mstaafu Mary Kapinga.

MICHUZI TV LIVE: AJALI MBEYA SASA BASI KWA MAOMBI MAZITO

WAZIRI LUGOLA ATEMBELEA IDARA YA UHAMIAJI MAKAO MAKUU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji,Dk. Anna Makakala akimkaribisha  Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola aliyefika Idara ya Uhamiaji jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya kikazi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ndani.
 Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akiangalia pasipoti ya kielektroniki inayotolewa na Idara ya Uhamiaji, alipotembelea Makao Makuu ya idara hiyo, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Msimamizi wa chumba cha Uchapaji, Mrakibu Msaidizi, Samuel Gambadu.
 Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akiongea na wananchi waliofika Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, kupata huduma mbalimbali zinazotolewa na idara hiyo.jijini Dar es Salaam. 
 Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akimuuliza swali mwananchi aliyefika Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji kupata huduma.Waziri Lugola yupo katika ziara ya kikazi.
 Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala, akizungumza na Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, aliyefika Idara ya Uhamiaji,jijini Dar es Salaam,wakati wa ziara ya kikazi.

COSTECH YASHANGAA KUIONA BARUA WALIYOIANDIKIA TWAWEZA IKIWA MTANDAONI

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

TUME ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) imesema kuwa barua iliyokuwa katika mitandao ya jamii ni yao isipokuwa wanasikitishwa kuiona katika mitandao hiyo kabla haijajibiwa na wahusika wa barua hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Costech Dk.Amos Nungu (pichani) amesema lengo la barua hiyo ilitakiwa kujibiwa na sio kusambaa katika mitandao ya jamii.

Amesema kazi ya Tume ni kuishauri Serikali katika masuala yote ya Sayansi na teknolojia na ubunifu na kuandaa vipaumbele vya utafiti pamoja na kupanga mgawanyo wa matumizi ya rasilimali wanazopewa na Serikali.

Amesema kazi zingine za tume ni kuratibu kufanya tathimini na ufatiliaji wa tafiti na uendelezaji wa Teknolojia.

Ameongeza tume inayo kamati maalumu inayohusika na utoaji wa vibali kwa tafiti mbalimbali zinazoendeshwa hapa nchini.
"Tunasikitika kuona barua tulioitoa kwa TWAWEZA inasambaa mtandaoni wakati hata majibu hajapatikana kwa wahusika,"amesema Dk.Nungu.



SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA YAWANOA VIONGOZI WANAWAKE DAR

$
0
0
Na said Mwishehe, Globu ya jamii 

SEKRETARIETI ya Maadili ya Viongozi wa Umma imeamua kuwanoa viongozi wanawake wa ngazi mbalimbali wakiwamo madiwani na wakuu wa Idara katika manispaa za Mkoa wa Dar es Salaam kwa lengo la kuwajengea uelewa kuhusu maadili ya viongozi wa umma. 

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati anafungua semina ya mafunzo hayo Kamishina wa Sekratarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Harold Nsekela amesema yatatoa fursa kwa viongozi hao kufahamu sekretarieti kuanzia majukumu, kazi na wajibu walionao katika usimamizi wa maadili.

Amefafanua sababu za kutolewa kwa mafunzo yametokana na utafiti uliofanywa mwaka 2015 kupitia taaaisi yao ya Kukuza uelewa wa wananchi kuhusu majukumu na kazi zinazotekelezwa na sekretarieti hiyo. "katika utafiti huo iliyokuwa unapoona ushiriki wa utoaji wa taarifa uliofanywa na makundi mbalimbali katika jamii kuhusu ukiukwaji wa maadili miongoni mwa viongozi wa umma. 

"Matokeo yalionesha ni asilimia moja tu ya wanawake kwenye vijiji na mitaa walishiriki kutoa taarifa za ukiukwaji wa maadili, "amesema. 

Amesema hali hiyo ililazimu Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma kuandaa mafunzo hayo katika mikoa yote inayotekelezwa mradi huo ambayo ni Mtwara, Morogoro, Iringa na Dodoma. "Lengo la mafunzo haya ni kuwajengea uelewa viongozi wanawake katika mamlaka za Serikali za mitaa kuhusu maadili ya viongozi wa umma.

Viewing all 110031 articles
Browse latest View live




Latest Images