Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

WIVU WA MAPENZI WASABABISHA ASKARI POLISI KUJIUA KWA KUJIPIGA RISASI MARA

$
0
0
*Kamanda wa Polisi aelezea tukio hatua kwa hatua...asema kabla ya kujiua aliandika ujumbe

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

KAMANDA wa Polisi Mkoani ya Mara Juma Ndaki amethibitisha kutokea kwa tukio la askari Polisi PC Nelson William G 3777 kujiua kwa kujipiga risasi kwasababu za wivu wa mapenzi. 

Akizungumza na Michuzi Blog kwa njia ya simu leo jioni hii Kamanda Ndaki amesema askari huyo amejipiga risasi leo saa 8:30 mchana akiwa eneo la kambi za Polisi alikokuwa anaishi. 

Amefafanua kabla ya kujipiga risasi ameacha ujumbe kuwa ameamua kujua kutokana  na wivu wa mapenzi kwa madai amekuwa hana mahusiano mazuri na mwanamke wake ambaye alikuwa ni mpenzi wake. 

Kamanda Ndaki amesema askari huyo kabla ya kuchukua uamuzi huo aliingia pia kwenye malumbano na mpenzi wake baada ya kwenda kwenye chumba cha mpenzi wake na kisha kuamua kuharibu mali alizonunua. 

Amesema baada ya tukio hilo la kuharibiwa mali mwanamke aliamua kwenda kutoa taarifa Polisi, kitendo ambacho askari William hakikumfurahisha kwani aliona kama amedhalilishwa. 

Hivyo akaona njia pekee ni kuchukua uamuzi wa kujiua na ilipofika muda huo akaamua kujiua kwa kujipiga risasi. 

Kamanda Ndaki alipoulizwa kama kuna mtu yoyote amekamatwa amejibu hakuna kwani askari ameacha ujumbe kuwa amejiua kwasababu hizo ambazo kimsingi ni wivu.

Amesema kwa sasa mwili wa askari huyo umehifadiwa chumba cha kuhifadhia maiti wakati taratibu za mazishi zikiendelea. 

Alipoulizwa kama askari huyo alikuwa wakiishi akiishi pamoja na mpenzi wake huyo,Kamanda Ndaki amejibu hawakuwa wakiishi pamoja kwani mwanamke alikuwa ana chumba chake na askari alikuwa anaishi kambini. 

POLISI DAR WANASA WATUHUMIWA WANAOJIHUSISHA NA UHALIFU

$
0
0

Na Hadija Seif, Globu ya jamii 
JESHI  la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam limefanikiwa kukamata watuhumiwa mbalimbali wanaojihusisha na uharifu uporaji,ukabaji pamoja na unyang'anyi .  
  
Akizungumza leo Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Liberatus Sabas amesema jana saa 03:30 raia wema walitoa taarifa  kuwa kuna mtu mmoja anamiliki silaha ambapo ufuatiliaji ulifanyika haraka na ndipo alikamatwa mtuhumiwa huyo.

Amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa Temeke kisuma Bar maarufu Kama Sugar Ray'' akiwa na bastola iliyotengenezwa Jamhuri ya CZECH yenye namba ya usajili A.368021.

Kamanda Sabas amesema jina la mtuhumiwa huyo limehifadhiwa na kwa sababu za kiupelelezi. 
  
Aidha  amesema watuhumiwa wengine wamekamatwa maeneo ya Kariakoo akiwewemi Amin Kimaro( 55)mkazi wa Manzese na wenzake watatu.

Amefafanua sababu za kukamatwa kwa kosa la kughushi hundi za benki mbalimbali jijini na kuziweka hundi hizo katika akaunti ya benki ili kufanikiwa kuiba fedha walizokusudia.

JESHI LA POLISI RUVUMA LAENDESHA MAFUNZO KWA MADEREVA WA MAGARI YA MALORI, MASAFA MAREFU

$
0
0
Na Ripota Wetu, Globu ya jamii

SERIKALI ya Mkoa wa Ruvuma, kupitia Jeshi la Polisi limeendesha mafunzo rasmi kwa madereva wa Malori yanayofanya safari za masafa marefu na mafupi kwa lengo la kupunguza ajali za barabarani.

Miongoni mwa madereva waliopewa mafunzo ni madereva wa magari makubwa wanaobeba makaa ya mawe kutoka mkoani Ruvuma kwenda mikoa mingine pamoja na nchi jirani.

Taarifa kwa vyombo vya habari imesema kuwa katika mafunzo hayo madereva wametakiwa kuzingatia sheria za barabarani kwa lengo la kujikinga na ajali ambazo husababisha vifo na majeruhi.

Semina hiyo imetolewa na Jeshi la Polisi mkoa katika eneo la Kitai wilayani Mbinga ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Mkoa wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme ya kuwataka wadau kuungana katika kuzuia ajali za barabarani.

 Kauli mbiu ya mafunzo hayo inasema hivi "Ruvuma bila ajali inawezekana"
"Usalama unaanza na mimi".

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA KUAGANA NA MABALOZI WATATU WALIOMALIZA MUDA WAO HAPA NCHINI

$
0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Sweden hapa nchini anayemaliza muda wake Katarina Rangnitt mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwatambulisha Baadhi ya Viongozi (hawaonekani pichani ) kwa Balozi wa Sweden hapa nchini anayemaliza muda wake Katarina Rangnitt mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Sweden hapa nchini anayemaliza muda wake Katarina Rangnitt mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mchumi kutoka Ubalozi wa Sweden True Schedvin
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi zawadi Balozi wa Norway anayemaliza muda wake hapa nchini Hanne-Marie Kaarstad mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Norway anayemaliza muda wake hapa nchini Hanne-Marie Kaarstad mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Balozi wa Malawi anayemaliza muda wake hapa nchini Hawa Olga Ndilowe mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa zawadi Balozi wa Malawi anayemaliza muda wake hapa nchini Hawa Olga Ndilowe mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

Introducing Epofresh - Nyau ft Tonch x Clint (produced by elie piano)

$
0
0
Epo-fresh Music is a new studio based in Dar-es-Salaam, Tanzania which produces all types of modern music. Welcome to listen to its club banger "Nyau" its first official release featuring @tonch_tz X @clintfierce. The song was produced by @elie.piano under @epofresh_music studios. 
The song is surely going to be a club favorite as it introduces a new dance style #NyauStyle to be featured on its forthcoming video. 🐱 @epofresh_music presents its first official release . A club banger! - "Nyau" featuring @tonch_tz X @clintfierce Produced by @elie.piano . Enjoy!

TRC RELI TV: Shuhudia Wakazi wa DAR wakifurahia usafiri wa Treni za Pugu na Ubungo

MAJALIWA AKUTANA NA WATALAAMU WA UTAFITI WA MAZAO YA KILIMO

$
0
0


Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Watafiti  wa Mazao ya Kilimo  kutoka Kituo cha Utafiti  cha Mikocheni jijini Dar es salaam, Wakala wa Mbegu za Kilimo  (ASA) na Taasisi ya Utafiti  wa Kilimo Tanzania, kwenye makazi yake jijini Dar es salaam Julai 11, 2018.  Wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga na Wa pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo  Tanzania, Bw. Japhet Justine.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kuhifadhi misitu yote iliyoko ndani ya Jiji la Dodoma

$
0
0
Halmashauri ya Jiji la Dodoma imesaini hati ya makubaliano inayoipa mamlaka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)  ya kupanda na kustawisha miti, na kuhifadhi misitu yote iliyopo ndani ya Jiji la Dodoma kwa lengo la kuikijanisha Dodoma. 
 Dodoma imekuwa ni Halmashauri ya kwanza nchini kufanya Makubaliano ya aina hiyo yaliolenga kukabiliana na changamoto ya hali ya hewa na kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2015/2020 inayoelekeza serikali kuongeza eneo la kupanda miti kutoka hekta 60,000 mwaka 2015 hadi hekta 130,000 mwaka 2020. 
 Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi wakati akiongea na Waandishi wa Habari mara baada ya kusainiana makubaliano hayo jijini humo leo.
"Siku ya Leo tumefanya jambo la kihistoria na wenzetu Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania – TFS, kama mnavyojua Dodoma ni mji mkuu wa Serikali, kama jiji tumeona tuna changamoto ya hali ya hewa na niwashukuru TFS kuona jambo hili ni la muhimu/
 "Tumeingia mkataba wa makubaliano kwamba TFS watahifadhi misitu yote iliyoko ndani ya Jiji la Dodoma na kama haitoshi katika maeno yote tutakayopimwa kama hifadhi ya ardhi kwa ajili ya kupanda miti watapanda miti na maeneo yote ya vilima ndani ya jiji la Dodoma watayahudumia kwa kuwa kwa mujibu wa sheria maeneo hayo hayamilikishi hivyo ni mali ya serikali, lakini na maeneo yote yenye vyanzo vya maji kwa maana ya mita 60 kutoka kwenye mabwawa ya maji TFS watayahudumia," alisema Mkurugenzi huyo. 
 Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania – TFS Professa Dos Santos Silayo anasema jiji la Dodoma limekuwa na ongezeko kubwa la watu linalosababisha ongezeko la shughuli za kiuchumi ambazo zinahitaji mifumo mizuri ya kimazingira ili kukabiliana na hali yoyote inayoweza kusababishwa na maongezeko hayo. 
Professa Silato anasema ni kwa sababu hiyo wameamua kuchukua jukumu la kuhakikisha mifumo ya kiikolojia inakuwepo salama kwa mana ya kuwepo kwa uoto wa kijani, uoto wa miti na mimea katika maeneo mbalimbali ili kuhakikisha kwamba wakazi wa Dodoma wanaishi katika mazingira ambayo yana afya. 
Professa anaongeza kuwa watahuhisha Jiji la Dodoma kwa kuanza kupanda miti maeneo ambayo yameonekana kuharibika au hayakuwa na uoto huku maeneo ambayo yanaonekana kuhitaji kuhifadhiwa ili kurudi kwenye uoto wake kuyahifadhi na katika kutekeleza hayo wamekubaliana na jiji kutafuta rasilimali fedha, rasilimali watu na vifaa vya kutekeleza kazi hiyo. 
 “Sisi kama Wakala wa Huduma za Misitu tumeshajipanga kuwa na rasilimali watu, tumejipanga kuwa na usafiri maalum kwa ajili ya kazi hii lakini pia fedha ambapo katika mwaka huu wa fedha takriban milioni 300 tumezitenga kwa ajili ya kuanza kutekeleza jukumu hili! Fedha hizi zinaweza kuwa kidogo lakini kwa kuwa tunashirikiana na jiji tutaangalia ni wapi tunaweza kupata fedha zaidi na pale itakapoonekana zinahitajika rasilimali zaidi ya hizi nilizosema basi tuko tayari kuziongeza ili tufikie malengo kwa haraka zaidi na kwa spindi ambayo kila mtu anaitarajia,” anasema Professa Silayo. 
 Meneja wa Kanda ya Kati ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Mathew Kiondo anayesimamia moja kwa moja utekelezaji wa makubalianao hayo anasema kanda yake itahakikisha inasimamia kikamilifu utekelezaji wa makubaliano hayo ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inayolenga kulinda rasilimali za misitu na kuboresha mazingira.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania – TFS Professa Dos Santos Silayo akizungumza na waandishi wa Habari (hawako pichani). Kushoto ni  Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi (kushoto) akimuonyesha Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania – TFS Professa Dos Santos Silayo maeneo waliyokubalina katika hati ya makubaliano inayoipa mamlaka TFS kupanda na kustawisha miti, na kuhifadhi misitu yote iliyopo ndani ya Jiji la Dodoma kwa lengo la kuikijanisha Dodoma mara baada ya wotw kusaini hati hiyo mapema hivi leo jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi (kushoto) na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania – TFS Professa Dos Santos Silayo wakisaini hati ya makubaliano inayoipa mamlaka TFS kupanda na kustawisha miti, na kuhifadhi misitu yote iliyopo ndani ya Jiji la Dodoma kwa lengo la kuikijanisha Dodoma mapema hivi leo jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi (kushoto) na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania – TFS Professa Dos Santos Silayo wakikabidhiana hati hati ya makubaliano inayoipa mamlaka TFS kupanda na kustawisha miti, na kuhifadhi misitu yote iliyopo ndani ya Jiji la Dodoma kwa lengo la kuikijanisha Dodoma mara baada ya wotw kusaini hati hiyo mapema hivi leo jijini Dodoma.

Rc Geita Akagua Miradi ya Huduma za Jamii, Ahimiza Ukamilishwaji Wake kwa Wakati

$
0
0

Na Boazi Mazigo, Afisa Habari Geita

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel ameendelea kufuatilia hatua za utekelezaji wa Miradi mbalimbali Mkoani Geita kwa kufanya ziara na kuona miradi inayotekelezwa kwa fedha za Huduma kwa Jamii (CSR) kutoka Mgodi wa Dhahabu Geita (GGM).
Ametembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Mzunguko wa Kisasa (Round About) inayojengwa Halmashauri ya Mji wa Geita. Amewapongeza mafundi, akashauri ujenzi uendelee siku zote ili kazi hiyo ikamilike kwa wakati.
Mhandisi Gabriel amesema na wasimamizi wa mradi kwa kusema, ‘zingatieni thamani ya fedha (Value for Money) na ubora, lakini pia ikibidi mnara unaojengwa ukamilike kabla ya mwaka kuisha kwa kuwa sisi waandisi tukiwa na sikikuu nchi haitajengwa’. Pia amesifu usanifu wa mchoro wa Mnara utakao kaa katikati ya Round About hiyo ukiwa na uwakilishi wa vitu mbalimbali mfano alama ya Mwenge wa Uhuru (uwakilishi wa taifa letu), Matofali ya Dhahabu (alama ya utajiri wa madini) lakini pia itakuwepo saa ambayo inaonyesha kiwango cha joto.
Kwa upande mwingine, Mhandisi Gabriel ameushukuru uongozi wa Mgodi wa GGM baada ya kutembelea na kuona jumla ya mifuko ya saruji 2,136 iliyopelekwa Halmashauri ya Mji Geita katika utekelezaji wa Ujenzi wa Miundombinu ya  Elimu na Afya kisha kujionea hatua ya uchimbaji wa msingi wa ujenzi wa Shule ya Msingi ya Kisasa inayoanza kujengwa eneo la Magogo lililotengwa kwa ajili ya Shule. Mkuu wa Mkoa kwa mara nyingine akasema; angependa kuona ujenzi wa Shule hiyo inaanza mara moja, maboma yakamilike ndani ya miezi mwili na nusu, kisha ukamilishaji ufuatie na yeye atashiriki kwa kuwa msimamizi wa shughuli ya ujenzi akizingatia thamani ya fedha hivyo aliwataka wananchi kuanza usafi mara moja kwani tayari baadhi ya vifaa vya ujenzi kwa nguvu za wananchi vipo kwenye eneo hilo.
Mkuu wa Mkoa alisisitiza kwa kusema, “kwa kuwa tunatekeleza Ilani ya Uchaguzi ya  Chama Tawala CCM, na kwa kasi ninayoiona, tukikaa vizuri kufikia mwakani, Zahanati kila Kijiji tunamaliza kabla ya Uchaguzi Mdogo wa mwaka 2019 kwani maboma yakikamilika tutakuwa juu ya asilimia 80 upande wa Sekta ya Afya. Hata kwa upande wa elimu, maendeleo siyo mabaya” aliongeza.
Alipofika Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Mhandisi Gabriel aliona mifuko 680 ya saruji na kupokea taarifa iliyoeleza kuwa bado mifuko 1,459 haijawasilishwa na kwamba kufikia wiki ijayo itakuwa imefika. Lakini pia aliagiza ujenzi uanzewiki inayofuata kwakuwa anapanga kutembelea utekelezaje wake.
Miongoni mwa alioambatana nao katika ziara hiyo ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mhe. Herman C. Kapufi, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Geita pamoja na wawakilishi wa Mgodi wa Dhahabu Geita GGM
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel akishukuru uongozi wa Mgodi wa GGM baada ya kutembelea na kuona jumla ya mifuko ya saruji 2,136 iliyopelekwa Halmashauri ya Mji Geita katika utekelezaji wa Ujenzi wa Miundombinu ya  Elimu na Afya kisha kujionea hatua ya uchimbaji wa msingi wa ujenzi wa Shule ya Msingi ya Kisasa inayoanza kujengwa eneo la Magogo lililotengwa kwa ajili ya Shule.
 Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel akitembezwa kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Geita
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel akikagua maendeleo ya ujenzi wa mzunguko wa kisasa (Round About) inayojengwa Halmashauri ya Mji wa Geita.

WAZIRI KANGI LUGOLA ATEMBELEA KIWANDA CHA MAGEREZA UKONGA, JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akisalimiana na maofisa wa Jeshi la Magereza, baada ya kuwasili kwa ziara ya kikazi katika Chuo cha Magereza ,kilichopo Ukonga,jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akipita mbele ya Maofisa wa Jeshi la Magereza, baada ya kuwasili kwa ziara ya kikazi katika Chuo cha Magereza ,kilichopo Ukonga,jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akimsikiliza Inspekta Carlos Hanga(kulia) , wakati alipotembelea Kiwanda cha Magereza Ukonga,kinachojishughulisha na uchongaji wa thamani za ndani na ufumaji wa nguo,jijini Dar es Salaam.Waziri Lugola yuko kwenye ziara ya kikazi baada ya kuteuliwa kuongoza wizara hiyo
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akikagua ubora wa samani inayotengenezwa katika Kiwanda cha Magereza, kilichopo Gereza la Ukonga,jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara ya kutembelea Jeshi la Magereza.Kulia  ni Kamishna wa Jeshi la Magereza, Dk.Juma Malewa.
Inspekta wa Jeshi la Magereza, Carlos Hanga akitoa maelezo ya kiufundi kwaWaziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, ambaye yuko katika ziara ya kikazi katika Kiwanda cha Gereza kilichopo Ukonga,jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

MICHUZI TV: Ruaha Marathon kuchangia upanuzi wa kituo cha Afya Ngome Iringa

$
0
0
Na Francis Godwin wa Michuzi TV, Iringa

NEWS ALERT: Mfanyabiashara wilayani Gairo mkoa wa morogoro akamatwa na madini nyumbani kwake

$
0
0
Na George Binagi, Morogoro
 Naibu Waziri wa Madini Mhe.Doto Mashaka Biteko leo amekamata madini ya vito aina Rhodilite (BOFYA HAPA kuyajua)  yanayokadiriwa kuwa tani saba katika nyumba ya mchimbaji na mfanyabiashara mmoja wa madini iliyopo Kata ya Magoweko wilaya ya Gairo mkoani Morogoro.
Aliyekamatwa na madini hayo ambayo bado thamani yake haijafahamika ni Bw.James Mnene ambaye ni mchimbaji na mmiliki wa kampuni ya madini ya JJ.Mnene & Partiners inayojishughulisha na uchimbaji wa madini ya vito katika machimbo ya Rubeho wilayani Gairo.
Mfanyabishara huyo amejitetea kwamba alikuwa ametunza madini hayo nyumbani kwake huku akitafuta soko na kuomba asamehewe kwani yuko tayari kufuata taratibu za biashara ya madini.
Nyumba ya mfanyabiashara aliyekutwa amehifadhi madini ya vito wilayani Gairo 
Madini hayo yakiwa nyumbani kwa mfanyabishara huyo
Mashine iliyokutwa nyumbani kwa mfanyabiashara huyo ambayo ilikuwa ikitumika kusagia mawe ya madini hayo
Naibu Waziri Biteko (kushoto) akizungumza baada ya kufika nyumbani kwa mfanyabishara huyo (katikati). Mfanyabiashara huyo ametiwa nguvuni kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria ambapo anatuhumiwa kukweka kulipa mapato ya serikali kwani tangu mwaka 2013 amelipa shilingi laki nne

HABARI ZA UMOJA WA MATAIFA KUTOKA NEW YORK LEO JULAI 11, 2018

UINGEREZA NJE!!

$
0
0
 Mojawapo ya mbwembwe za mashabiki wapatao 7, 000 wa Uingereza waliomiminika jijini Moscow, wengine wakiwa wamevalia visibao kama kocha wao Gareth Southgate zimezimika  usiku huu ambapo badala ya kurudisha mwali nyumbani inabidi warudi labda na ushindi wa tatu. 
Croatia usiku huu imekuwa nchi 'tofauti' ya 13th kutinga fainali ya Kombe la Dunia la soka na ya 10 kutoka Ulaya kwa kuipiga Uingereza goli 2-1 katika dakika 120 baada ya kufungana 1-1 katika dakika 90 za kawaida. Shujaa wa Croatia yenye watu milioni 4 alikuwa ni huyo  Mario Mandzukic aliyetia kimiani bao katika dakika ya 11 kabla ya filimbi ya mwisho kwa pasi tamu ya kichwa toka kwa Ivan Perisic.

BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO 11.07.2018


MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA ATOA MAFUNZO KWA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI MDOGO

$
0
0


Na Monica Laurent, Dar es salaam.

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imetoa mafunzo maalumu kwa watumishi wa ofisi yake ili kuwajegea uwezo wa kufanya uangalizi wa uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika tarehe 12 Agosti 2018 katika jimbo la Buyungu na kata 79.

Mafunzo hayo yamefanyika jana Julai 11, 2018 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ambapo mada mbalimbali zimewasilishwa zikiwemo mada juu ya Elimu ya Maadili ya Vyama vya Siasa, Haki na wajibu wa Vyama vya Siasa, wajibu wa Msajili wa Vyama vya Siasa, matendo yanayokatazwa na Sheria ya Gharama za Uchaguzi na Sheria ya Vyama vya Siasa, Umuhimu wa kujaza fomu za gharama za Uchaguzi.

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo, Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Mhe. Jaji Francis S.K. Mutungi amewawataka watumishi hao kufanya kazi kwa ueledi na kwa kufuata sheria za nchi.

“ kila mmoja wetu atambue kuwa ofisi yetu imepewa dhamana kubwa ya kusimamia Sheria ya Gharama za Uchaguzi ya mwaka 2010 na Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992 ili kudumisha demokrasia ya vyama vingi nchini, ni wajibu wetu kufanya kazi kwa ueledi na kwa mujibu wa sheria” amesisitiza Jaji Mutungi

Naye Bi. Piencia C. Kiure mmoja wa wakufunzi katika mafunzo hayo ambaye ni Msajili Msaidizi anayeshughulika na masuala ya Gharama za Uchaguzi na Elimu kwa Umma amesisitiza umuhimu wa wagombea na vyama vya Siasa kurejesha fomu za Gharama za uchaguzi zinazobainisha mapato na maksio ya kiwango cha matumizi wakati wa uteuzi,kampeni na uchaguzi ndani ya muda uliotengwa kisheria ili kuepuka ukiukwaji wa sheria ya Gharama za Uchaguzi.

Watumishi pia wamesisitizwa kuhakikisha wanavikumbusha vyama vya siasa na wagombeakunadi sera za vyama kwa kusimamia maadili ya vyama vya siasa ili kuendelea kudumisha amani ya nchi.

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ni taasisi yenye wajibu wa kisheria wa kufanya uangalizi wa mwenendo wa chaguzi zinazofanyika kwa ajili ya kuhakikisha kuwa wagombea na vyama vya siasa vinatekeleza matakwa ya sheria kwa kuepuka vitendo ambavyo vimekatazwa na sheria hizi ili kuimarisha demokrasia ya vyama vingi.
Msajili wa Vyama vya Siasa Mhe. Jaji Francis  Mutungi akionesha kitabu chenye kuelimisha uma juu ya makatazo yaliyomo katika Sheria ya Gharama za Uchaguzi wakati wa Mafunzo ya Watumishi yaliyofanyika jana Julai 11, 2018 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa
Msajili wa Vyama vya Siasa, Mhe. Jaji Francis  Mutungi akifungua mafunzo kwa watumishi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Msajili Msaidizi anayeshughulikia Gharama za Uchaguzi na Elimu kwa Umma Bi. Piencia Kiure,(Picha zote na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
Msajili Msaidizi anayeshughulikia Gharama za Uchaguzi na Elimu kwa ummaPiencia Kiure, akitoa mwongo zo juu ya jinsi ya fomu za gharama za uchaguzi ambazo hubainisha mapato na matumizi ya wagomea na vyama vya siasa wakati wa uchaguzi.
Mwanasheria Mwandamizi Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Bi. Monica Mwailolo akiwakilisha mada wakati wa mafunzo.

KIWANDA CHA SUKARI KAGERA CHAAGIZWA KUACHA URASIMU KATIKA KUUZA SUKARI WANAYOZALISHA

$
0
0
Na Mathias Canal-WK, Misenyi-Kagera

Uongozi wa kiwanda cha Sukari Kagera umeagizwa kuacha urasimu katika mfumo wa uuzaji wa Sukari wanayozalisha badala yake kuingiza mtaani kwa wingi Sukari kwa wananchi ili kuepuka kadhia ya upungufu wa huduma hiyo muhimu katika jamii.

Agizo hilo limetolewa na Mawaziri wa sekta ya Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba na waziri wa sekta ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Charles Mwijage wakati wakizungumza na uongozi wa kiwanda hicho Jana 11 Julai 2018 walipotembela kiwanda cha Sukari wakiwa kwenye ziara ya siku tatu ya kikazi Mkoani humo iliyoanza Juzi 10 Julai 2018.

Mawaziri hao kwa kauli moja wametoa siku 14 kwa kiwanda hicho kuongeza kasi ya uzalishaji kutoka uzalishaji wa Sukari kwa Tani 350-360 kwa siku ili kufikia walau Tani 450 mpaka 500 kwa siku kwani kufanya hivyo wataimalisha uwezo wa Sukari kupatikana kwa wingi kwa wananchi hivyo kuondoa usumbufu wa gharama katika ununuzi wa bidhaa hiyo.

Aidha, Mawaziri hao wametoa kalipio Kali kwa uongozi wa kiwanda hicho kwa kuwa na mawakala wachache wa usambazaji wa sukari jambo ambalo linapelekea ushindani wa kibiashara kuwa mchache mbinu inayopelekea Sukari kuuzwa kwa gharama isiyokuwa rafiki kwa watumiaji.

Walisema kuwa ndani ya muda mfupi uongozi wa kiwanda hicho unapaswa kutathmini upya namna ya kuongeza Uwekezaji ili kurahisisha huduma za wananchi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020 hatimaye kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ifikapo mwaka 2025.
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akikagua uzalishaji wa sukari wakati walipotembelea kiwanda cha Sukari Kagera wakiwa kwenye ziara ya siku tatu ya kikazi Mkoani humo iliyoanza Jana 10 Julai 2018, Jana 11 Julai 2018. 
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Charles Mwijage wakikagua eneo linalo wakati walipotembelea kiwanda cha Sukari wakiwa kwenye ziara ya siku tatu ya kikazi Mkoani humo iliyoanza Jana 10 Julai 2018, Jana 11 Julai 2018. 


RAIS DK MAGUFULI AMTEUA CASMIR SUMBA KYUKI KUWA MWENYEKITI WA BODI YA UTT AMIS

Dereva wa daladala aibuka kidedea na Renault Kwid ya M-Pesa

$
0
0

 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr Binilith Mahenge (kulia) akimkabidhi funguo za gari  mshindi wa shindano la Vodacom Mpesa Aloyce Mnyamagola alilojishindia katika promosheni inayoendelea ya 'Tumia M-Pesa ushinde gari'. 
 Mshindi wa gari  aina ya Renault Kwid kutoka Vodacom Mpesa, Aloyce Mnyamagola akifungua mlango wa gari aliloshinda mara baada ya kukabidhiwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr Binilith Mahenge jijini Dodoma jana, wanaoshuhudia ni maofisa mbalimbali kutoka Vodacom
 Mshindi wa Shilingi milioni 1ya shindano la Vodacom Mpesa Japhet Isaya Mkazi wa Hombolo Mkoani Dodoma akipokea hundi jana katika sherehe za kukabidhi zawadi kwa washindi wa Kanda ya kati zilizofanyika Jijini Dodoma.

TAARIFA YA KUHAMA KWA MAKAO MAKUU YA OFISI ZA PPRA

Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images