Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 237 | 238 | (Page 239) | 240 | 241 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Katibu wa Itikadi na Uenezi -CCM Nape Nnauye
  -- 


  Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyomalizika leo imejadili kwa kina Masuala mbalimbali likiwemo pendekezo la Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Magharibi - Zanzibar la kumvua uanachama Ndugu Mansoor Yussuf Himid, Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Kiembesamaki.

  Baadhi ya tuhuma za Ndugu Mansoor Yussuf Himid ni pamoja na:-

  1.   Kushindwa kusimamia malengo ya CCM na kutekeleza masharti ya uanachama.

  2.   Kushindwa kutekeleza wajibu wa mwanachama na kukiuka Maadili ya Kiongozi wa CCM.

  3.   Kuikana Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010-2015 na kuisaliti CCM.

  Baada ya kujiridhisha vya kutosha na tuhuma dhidi ya Ndugu Mansoor Yussuf Himid, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) imeridhia uamuzi wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Magharibi Zanzibar wa kumfukuza uanachama. Kwa uamuzi huo wa kumvua uanachama wa CCM Ndugu Mansoor Yussuf Himid, yeye kwa sasa sio Kiongozi tena wa CCM.

  Imetolewa na:

  Nape Moses Nnauye,
  KATIBU WA NEC ITIKADI NA UENEZI CCM TAIFA
  26/08/2013


  0 0

  Mchezaji wa timu ya Klabu ya Mpo Afrika na Nahodha wa timu ya Taifa, Charles Venance akicheza wakati wa mechi ya fainali dhidi ya klabu ya Sun City wakati wa mashindano ya Safari Pool Taifa Ngazi ya Mkoa,Mkoa wa Temeke iliyofanyika mwishoni mwa wiki.
  Katibu Mkuu wa chama cha Pool Taifa(TAPA), Amos Kafwinga akimkabidhi zawadi ya fedha taslimu shilingi 350,000/= bingwa wa mchezaji mmoja mmoja wanaume(Singles), Sulemani Cato mara baada ya kumfunga Nahodha wa timu ya Taifa Charles Venance 4-2.Dar es Salam mwishoni mwa wiki.
  Baadhi ya wachezaji wa Klabu ya Mpo Afrika wakishangilia na Kikombe mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari Pool Taifa ngazi ya Mkoa,Mkoa wa Temeke iliyofanyika Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Mpo Afrika ilishinda 13-11 dhidi ya Klabu ya Sun City.

  0 0
 • 08/26/13--16:42: taarifa ya msiba
 • Familia ya Bwana Isaac Kalumuna wa Mbezi Beach Dar Es Salaam anatangaza kifo cha mkewe Annastazia Rwegasiraa Kalumuna (pichani) kilichotokea Ijumaa 23 Agosti 2013 katika Hospitali ya Massana, Mbezi. 

   Mazishi yatafanyika Alhamisi wiki hii, Agosti 29, mwaka huu, 2013 katika Kijiji cha Buganda, Kamachumu, Muleba, Mkoani Kagera. 

   Mwili utaagwa Leo Jumanne 27 Agosti nyumbani kwa marehemu, Art gallery Mbezi beach. Kwa tangazo hili, habari ziwafakie ndugu, jamaa na marafiki. 

   "Bwana ametoa Bwana ametwaa"

  0 0
 • 08/26/13--20:00: ngoma azipendazo ankal
 • Ngoma ya 'Mizele' ya Mayoni mayaula naipenda sana

  0 0
 • 08/26/13--22:03: PRAISE THE LORD
 • Hi my Friends!
  I am inviting you to join me and my family to praise our Lord as my husband survived a Plane crash last week in the Northern part of Tanzania (in the middle of Lake Manyara). All six passengers and the pilot miraculously survived. Lord has just given us a miracle in our family. Just speechless only praising the Lord. 
  Thanks and Blessing to all.
  Dr. Emeria A. Mugonzibwa-Mwanga,
  Head, Depart of Orthodontics, Paedodontics & Community Dentistry,
  Director, WHO CC Primary Oral Health Care, Planning & Research,
  MUHAS, P.O. Box 65104, Dar, Tanzania.
  Tel:  
  +255 22 2151135;  Cel: +255 713/767 606581

  0 0

   UTEUZI
  Kikao cha Halmashauri Kuu pia kimeridhia, uteuzi wa Makatibu wateule wapya wa Jumuiya za CCM, za Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Jumuia ya Wazazi na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT).

  Katika uteuzi huo mapendekezo hayo yaliyofanywa na Kamati Kuu ya CCM na kuridhiwa na NEC, kwa upande wa UVCCM ameteuliwa aliyekuwa Kaimu Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro, Sixtus Mapunda na kwa upande wa Jumuia ya Wazazi ni Mjumbe wa NEC kutoka Pemba, Seif Shabani Mohamed, huku kwa upande wa UWT akiachwa Katibu Mkuu wa sasa, Amina Makilagi.

  Mapunda atachukua nafasi iliyokuwa imneshikiwa na Martine Shigela ambaye ameongoza UVCCM kwa miaka mitano sasa, na Seif Shabani Mohammed kutoka Pemba akichukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Hamis Suleiman Dadi ambaye pia amekuwa katika wadhifa kwa miaka mitano sasa.

  Pia, NEC imeridhia mapendekezo  ya Kamati Kuu kwa ajili ya kuziba nafasi Makatibu wa CCM wa mikoa mitatu ya Morogoro, Kaskazini Pemba na Geita ambayo kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa imekuwa wazi kwa muda mrefu sasa kutrokana na sababu mbalimbali ikiwemo kifo.

  Kufuatia mapendekezo hayo ya Kamati Kuu, ambayo yameridhiwa na NEC, walioteuliwa na mikoa yao ikiwa kwenye mabano ni Msaidizi Kitengo cha  Uchaguzi, CCM Ofdisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Romuli Rojas John (Morogoro), aliyekuwa Katibu Katibu wa wilaya ya Mkinga, Kassim Mabrouk Mbarak (Kaskazini Pemba) na aliyekuwa Katibu wa CCM Igunga, Mary Maziku (Geita).

  Kuhusu sakata la madiwani wa Bukoba mjini, CCM imesema suala hilo, linaendelea kushughulikiwa ambapo baada ya kikao hicho cha NEC, Kamati kuu iliendelea kukutana na viongozi wa wilaya ya Bukoba, Mwenyekiti wa CCM na Katibu wa wilaya hiyo.

  Mapema kabla ya kikao cha NEC, Kamati Kuu ilikutana na Mbunge wa Bukoba mjini Khamis Kagasheki na Meya wa Manispaa ya Bukoba mjini na kuwahoji, wakati jana Kamati Kuu ilikutana na  Mwenyekiti na Katibu wa CCM mkoa wa Kagera.

  Taarifa Rasmi ya CCM ya majina ya Makatibu wa Wilaya walioteuliwa na NEC
   
  1. Ndugu Ashura Amanzi
  2. Ndugu Rukia Saidi Mkindu
  3. Ndugu Elias J. Mpanda
  4. Ndugu Jonathan M. Mabihya
  5. Ndugu Mulla Othman Zuberi
  6. Ndugu Jumanne Kapinga
  7. Ndugu Ali Haji Makame
  8. Ndugu Jacob G. Makune
  9. Ndugu Juma A. Mpeli
  10. Ndugu Hawa Nanganjau
  11. Ndugu Abdulrahman Shake
  12. Ndugu Subira Mohamed Ameir
  13. Ndugu Abdallah Shaban Kazwika
  14. Ndugu Juma Bakari Nachembe
  15. Ndugu Josephat Ndulango
  16. Ndugu Rajab Uhonde
  17. Ndugu Abeid Maila
  18. Ndugu Mohamed Lawa
  19. Ndugu Mariam Sangito Kaaya
  20. Ndugu Bakar Lwasa Mfaume
  21. Ndugu Julius Peter
  22. Ndugu Jumanne Kitundu Mginga
  23. Ndugu Mathias Nyombi
  24. Ndugu Mohamed Hassan Moyo

  0 0

    Rais wa Jamhuri ya Comoro, Dk Ikililou Dhoinine, akimkaribisha balozi wa heshima wa Comoro nchini Oman ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba,  Rahma Abdulrahman Al Kharoosi (Malkia wa Nyuki), katika Ikulu yake mjini Moroni
   Rais wa Jamhuri ya Comoro, Dk Ikililou Dhoinine,akiwa katika picha ya heshima na  balozi wa heshima wa Comoro nchini Oman ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba,  Rahma Abdulrahman Al Kharoosi (Malkia wa Nyuki), katika Ikulu yake mjini Moroni.Na Mpiga Picha Wetu

  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhani Dau akizungumza wakati wa hafla ya kuwaaga Wajumbe wa Bodi iliyomaliza muda wake na kuikaribisha bodi mpya katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. 

   Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhani Dau akimkabidhi zawadi Mwenyetiki wa Bodi ya NSSF, Abubakar Rajabu.
   Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya NSSF iliyomaliza muda wake, Hirdegard Mziray akipokea zawadi yake kutoka kwa Dk. Dau.
  Baadhi ya wajumbe wa bodi waliomaliza muda wao walipewa zawadi. Pichani ni Mhe Mudhihir M. Mudhihir 'Kisiki cha Mpingo' akipokea zawadi yake.

  Kwa habari kamili na picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Mmoja wa watoto wanaendelea na matibabu Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam, akiwa bize na rangi wakati walipotembelewa na mchora katuni Nathan Mpangala kupitia mradi wake wa kujitolea wa Wafanye Watabasamu, Jumamosi iliyopita. Mradi huo unaoshirikisha ndugu, jamaa, marafiki na wachoraji wenzake, ulikwenda kuwafariji kwa kuwapa zawadi kisha kuchora nao.
  Mratibu wa mradi wa kujitolea wa Wafanye Watabasamu, Katunisti Nathan Mpangala ‘Mtukwao’, akishea jambo na mmoja wa malaika Hospitali ya Taifa Muhimbili, upande wa saratani, Jumammosi iliyopita.
  Marafiki wa Wafanye Watabasamu, walionesha tabasamu mapemaaaaa.
  Sanaa inamchango mkubwa katika kupunguza msongo wa mawazo na kusahaulisha maumivu.
  Mchora vibonzo wa ITV ambaye pia ni mratibu wa Wafanye Watabasamu, Nathan Mpangala akiwa na mchora vibonzo wa baadae.
  NYUMBA TU, SIMPO. Akiendelezwa atakuja kuwa mchoraji mahiri wa majengo.
  Mchoraji katuni wa gazeti la Nipashe, Abdul King O aka ‘Kaboka mchizi’, aliungana na Wafanye Watabasamu kuwatabasamisha malaika hawa. 


  0 0
 • 08/27/13--02:48: Article 9


 • 0 0

  Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa kampuni ya Chloride Exide Bw,Gabriel Ondoyo (kulia) na  Mratibu wa Masoko wa Kampuni hiyo Bw, Robert Hiza wakikabidhi Betri za kampuni hiyo kwa  Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Dharura  'EmerGency Medicine Profesa, Victor Mwifongo kwa ajili ya magari ya kitengo hicho Dar es salaam leo kushoto ni Kaimu Dereva Mkuu Sultan Kitanga na Mkuu wa Idara ya Ufundi ENG,Leonard Elizeus
  Baadhi ya wahudumu wakiendelea na shughuli zao katika gari la wagojwa kushoto ni Nikijaeli Ngareni na Josephine Lazaro
  Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa kampuni ya Chloride Exide Bw,Gabriel Ondoyo kushoto na  Mratibu wa Masoko wa Kampuni hiyo Bw, Robert Hiza wakiwa katika picha ya pamoja baadhi ya maofisa wa kitengo hicho
  Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Dharurua  'Emergency Medicine Profesa, Victor Mwifongo kushoto akibadilishana namba za mawasiliano na  Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa kampuni ya Chloride Exide Bw,Gabriel Ondoyo  Mratibu wa Masoko wa Kampuni hiyo Bw, Robert Hiza Na Mwandishi Wetu MRATIBU wa Masoko wa Kampuni ya Chloride Exide Bw, Robert Hiza leo ametoa msaada wa Betri mbili katika kitengo cha Emergency Medicine ya hospitali ya Taifa Muhimbili . Msaada huo wa kwanza kutoa inaendana na miaka 50 ya kampuni hiyo ambapo watatoa viti mbalimbali katika hospital za Serikali vikiwemo Sola kwa ajili ya umeme wa jua . Akipokea msaada huo.Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Dharura  'Emergency Medicine Profesa, Victor Mwifongo amewashukuru kampuni ya Chloride Exide kwa kuliona hilo kwani ni mara ya kwanza katika kitengo chao kupokea msaada kama huo, na kuwaomba wadau wengine kujitokeza kusaidia vitu mbalimbali ikiwemo hata magari kama yapo tunaomba msaada maana hapa kitengo chetu ni cha mambo ya dharura na kinategemewa sana kama mnavyojua alisema Prof Victor Mwifongo Nae  Mkuu wa Madereva wa Kitengo cha Emergency Medicine Bw. Kafuru Rashidi amendelea kutoa shukrani kwa kampuni hiyo kwa kuliona hilo kwani yeye kama Dereva ameona ni jambo bora sana 

  0 0

  Afisa mauzo wa kanda ya ziwa Mohamed Kabeke akikabithi vitabu Afisa elimu msaidizi sekondari wilaya ya karagwe bi Siberia Ruboha wakati Airtel ilipotembelea wilaya ya karagwe mkoani bukoba, akishuhudia ni Meneja Mahusiano ya Kijamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi. 
  Meneja Mahusiano ya Kijamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi akimkabithi Afisa elimu msaidizi sekondari wilaya ya karagwe bi Siberia Ruboha vitabu vya ada na kiada wakati Airtel ilipotembelea wilaya ya karagwe mkoani bukoba.

  Airtel Tanzania imeendelea na mradi wake wa kusambaza vitabu katika shule ya Sekondari nchini chini ya mradi wa ‘Shule yetu’ ambapo shule mbalimbali za sekondari nchini zimenufaika na mradi.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari, Meneja Mahusiano ya Kijamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi alisema kampuni ya Airtel inaendelea kukabiliana na changamoto katika sekta ya elimu nchini hasa tatizo la vitabu vya kiada kwa shule za sekondari. Kupitia mradi wa ‘Shule yetu’ watoto wengi wa kike watanufaika kwani mradi huu unalenga hasa katika kumkwamua mtoto wa kike kutoka katika ujinga, umaskini na maradhi,”

  Hawa aliongeza kwa kusema Leo tunatoa msaada wa vitabu kwa shule ya sekondari ya Bwelanyake hapa Karagwe Bukoba ikiwa ni mwendelezo wa shughuli zetu za kijamii katika kupambana na tatizo la vitabu mashuleni. Vitabu hivi vitawawezesha wanafunzi wa shule ya Bwelanyake kupata nafasi ya kujifunza na kujisomea na kuwawezesha walimu kupata nyenzo muhimu za kufundishia.

  Kwa upande wake Afisa elimu msaidizi sekondari wilaya ya karagwe bi Siberia Ruboha alisema “elimu ndio ufunguo wa maisha hivyo tunawashukuru sana Airtel kwa kushirikiana na Serikali kupunguza tatizo la vitabu vya kiada vya shule za sekondari hapa nchini.

  Tunaamini msaada huu wa vitabu tulioupata leo utasaidia katika kuinua kiwango cha ufaulu na kuongeza taaluma zaidi kwa wanafunzi wetu na kuongeza idadi ya wanafunzi wa masomo ya sayansi hapa shuleni. /Nachukua fursa hii kuwaomba wanafunzi wavitumie fursa hii kujisomea na wavitunze vitabu hivi ili viweze kutumika na wanafunzi wengi zaidi na kutoa matunda bora na mengi zaidi.

  Mpaka sasa Airtel kupitia mradi huo imewafikia shule takribani 900 za sekondari nchi nzima kwa kuzipatia vitabu vya kiada hasa kwenye masomo ya Fizikia, Hisabati, kemia na Biolojia. mradi huu wa Shule yetu unasambaza vitabu kwa shule za sekondari kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne pamoja na vitabu vya walimu kwa ajili ya kufundishia.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Bi. Fatuma Ally akizungumza machache wakati wa uzinduzi rasmi wa ufugaji wa kuku wa kibiashara kwa Chama kimoja cha ushirika Chenye wanachama wasiopungua mia mbili ambacho tayari kimeundwa na wakazi wa wilaya hiyo.
  Baadhi ya Wadau wa Chama hicho wakifatilia maelezo wa Mkuu wa Wilaya

  Na Abdulaziz Video,Chamwino.

  Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Bi. Fatuma Ally amezindua rasmi ufugaji wa kuku kibiashara wilayani humo kwa Chama kimoja cha ushirika Chenye wanachama wasiopungua mia mbili ambacho tayari kimeundwa wilayani humo.

  Mkutano huo wa aina yake uliokutanisha baadhi ya viongozi,Mabenki,NGOS,wakulima,wafugaji,Wenye maduka,mama Ntilie,Wenye mabucha,wachuuza kuku,Wenye hoteli,Wenye mashine za kusaga na kukamua mafuta na wataaalamu wa mifugo .

  Mkutano huo uliokuwa katika sura yenye kuonyesha bayana dhana ya " SMARTPARTNERSHIP ambapo Wananchi wa wilayani Chamwino mkoani Dodoma wamehimizwa kuwekeza kwenye ufugaji kuku wa asili ili waweze kukabilina na baa la njaa linalosababishwa na mabadiliko ya tabia ya nchi.

  Akifungua mkutano wa wadau wa ufugaji kuku wilayani humo,Mkuu wa Wilaya hiyo Fatma Ally alisema ufugaji bora wa kuku wa asili unao nafasi kubwa ya kukwamua jamii kiuchumi ambapo wananchi wa wilaya hiyo kuweza kujiwezesha kujitosheleza kwa chakula kwa ufugaji kuku ili kuziba pengo la ukame kwa kuwa wananchi wataweza kununua chakula cha kutosha kwa mahitaji ya kaya zao.

  “Wilaya yetu inakabiliwa na ukame ambao hata mtama hauwezi kustawi…wananchi hawanabudi kuwekeza kwenye uzalishaji wa kuku ili kipato kitokanacho na ufugaji huo kiweze kutumika kununua chakula ” alisema Ally.

  Aliongeza kuwa “Mkutano huu unalenga kuwaktanisha wazalishaji na walaji ili kurahisisha masoko…ili kuhakikisha soko haliyumbishwi na walanguzi tutaunda ushirika wa wafugaji kuku utakaosimamia soko hilo katika wilaya yetu ”.

  Awali mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Adrian Jungu alisema tayari halmashauri yake imenunua majogoo 3400 wa kisasa na wamegaiwa kwa wafugaji wilayani humo ili kurahisisha ufugaji sambamba na ufugaji bora wa kuku wa asili.

  “Hadi sasa wilaya inakadiriwa kuwa na kuku 350,000,tunaweza kuzalisha zaidi na kuwa mkombozi wa kipato cha wananchi wetu ambao wanalazimika kujitosheleza kwa chakula kutokana na ukame” alisema Jungu na kufafanua kuwa “Ili kurahisisha ufugaji huo, wananchi tunawahamasisha wajiunge kwenye vikundi mbalimbali, viwepo vya utengenezaji chakula cha kuku, kutotolesha vifaranga, kutibu magonjwa na vya masoko nasi kuwaunga mkono.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB), Bi. Margareth Chacha akifafanua jambo katika mkutano mkuu wa wanawake Idara ya Takwimu jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa, Kamishina wa Sensa ya Watu na Makazi, Bi. Amina Said na Mwenyekiti wa Chama cha TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam, Bi.Salma Omari.

  Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

  Wanawake wametakiwa kujiunga katika vikundi (SACCOS) ili waweze kunufaika na huduma za mikopo yenye riba nafuu kutoka Benki ya Wanawake ya Tanzania (TWB) ikiwa ni juhudi za kujikwamua kimaendeleo.

  Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Wanawake Tanzania, Margareth Chacha jana wakati wa mkutano Mkuu wa Wanawake Idara ya Takwimu uliofanyika jijini Dar es salaam na benki hiyo kutambulisha huduma na bidhaa zake.

  “Wakati umefika kwa wanawake kuchangamkia fursa hii kwani Benki ya Wanawake inatoa sio tu mikopo yenye riba nafuu bali pia chaguo la muda wa marejesho kulingana na mkopaji”, alisema.

  Alisema kuwa inatoa mikopo yenye riba nafuu zaidi kuliko benki nyingine hivyo kuwashauri wanawake kujiuna katika SACCOS ambazo zitawahakikishia kuwa dhamana na amana ya mikopo hivyo kujiendeleza kimaendeleo bila vikwazo vyovyote. “Kitu cha msingi ni kuwa na wanakikundi waamimifu na daftari la akiba zinazokaguliwa..,”alisema.

  Akifafanua zaidi alisema kuwa benki hiyo ina huduma mbalimbali ikiwemo mikopo kwa walaji inayotegemea mshahara tofauti na mikopo ya biashara.

  Alisisitiza kwa taasisi nyingine za umma na binafsi kuwaalika katika sehemu za kazi ili waweze kutoa elimu kuhusu benki hiyo kwa wanawake waweze kufahamu na kutumia fursa mbalimbali zinazopatikana kupitia benki hiyo.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wanawake TUGHE ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi Slyvia Meku alisema kuwa wameamua kuwaalika wawakilishi kutoka benki hiyo ili kujua bidhaa na huduma mbalimbali zinazopatikana ukizingatia kuwa wanawake ndio walengwa wakuu. “Tumeamua kuwaalika ili kujua faida na fursa zinazopatikana kupitia benki hiyo”,alisema.

  Alisema kuwa Benki ya wanawake imekuwa mdau mkubwa katika juhudi za kumwendeleza mwanamke kwa kutoa elimu hasa kwa wanawake katika kujiendeleza kiuchumi kupitia mikopo yenye riba nafuu hivyo kuchochea kasi ya maendeleo hapa nchini.

  0 0

   Na Mwandishi Wetu 

  WAREMBO 30 wanaowania taji la Redd’s Miss Tanzania 2013, kesho wanatarajiwa kukutana rasmi na waandishi wa habari, ili kila mmoja kutoa mtazamo wake,shughuli itakavyofanyika katika hoteli ya Giraffe iliyopo Kunduchi, jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino ambao ni waandaaji wa Redd’s Miss Tanzania, Hashim Lundenga alisema, mkutano kati ya waandishi wa habari na warembo ni muhimu kuwajengea uwezo zaidi wa kujiamini.

  “Washiriki hao wataulizwa maswali mbalimbali na waandishi wa habari na wao wataeleza mtazamo wao kuhusu Redd’s Miss Tanzania, hatutawafunga, wao waandishi watakuwa huru kila mmoja kumuuliza mshiriki yoyote swali analotaka,” alisema.

  Washiriki hao ambao leo walikuwa na semina maalumu na waandaaji wa mashindano haya ambao ni Kampuni ya Lino International Agency Limited.

  Baada ya kukutana na waandishi wa habari, warembo hao wanatarajiwa kuanza ziara maalumu ya kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini kwa lengo la kuhamasisha utalii wa ndani.

  Warembo hao watakuwa kambini kwa muda wa siku 30 wakipata mafunzo mbalimbali yatakayotolewa na wataalamu kutoka katika sekta mbalimbali kama vile afya, ajira, ujasiriamali, uwekezaji na sekta ya utalii.

  Brigitte Alfred ndiye Mrembo anayeshikilia taji hilo kwa sasa, baada ya kufanikiwa kulitwaa mwishoni mwa mwaka jana.

  Meneja wa Redd’s, Victoria Kimaro naye alisema kama wadhamini wapo tayari kuhakikisha shindano hilo linafanikiwa zaidi mwaka huu kuliko kipindi chote kile.

  Kinywaji cha Redd’s Original kinazalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

  0 0
 • 08/27/13--03:43: Kutoka Bungeni Dodoma leo
 • Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Mbinga Magharibi Capt. John Komba, bungeni mjini Dodoma leo.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka bungeni mjini Dodoma leo.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, ambaye pia ni Mbunge wa Songwe, Philipo Mulugo kwenye viwanja vya bunge Mjini Dodoma leo.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

  0 0


  0 0

   Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sihaba Nkinga mwenye nguo nyekundu akipokea zawadi ya maua kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa Wizara hiyo Bibi Mwanakombo Jumaa katika hafla ya kupokea uongozi mpya leo jijini Dar es Salaam.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sihaba Nkinga mwenye nguo nyekundu akipokea zawadi ya maua kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa Shirika la Magazeti la Serikali (TSN) wakati wa hafla ya mapokezi ya kumkaribisha Katibu Mkuu huyo leo jijini Dar es Salaam 
   Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakifurahi wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ambao wameteuliwa hivi karibuni. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0
 • 08/27/13--06:56: Article 0


 • 0 0

  Waziri Membe akiwasilisha mbele ya Tume ya Marekebisho ya Katiba hoja ya kupendekeza uraia wa nchi mbili kuingizwa kwenye rasimu ya Katiba.Kulia ni Mwenyekiti wa Tume ya Katiba,Mh. Joseph Warioba pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Katiba,Mh. Jaji Augustine Ramadhan.

  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inapenda kuujulisha Umma kuwa jana tarehe 26 Agosti, 2013, Mheshimiwa Bernard K. Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa alikutana na Uongozi wa Tume ya Marekebisho ya Katiba.  Lengo la kukutana na Tume ilikuwa ni kuwasilisha pendekezo la haki ya Uraia wa nchi mbili kutamkwa na kutambuliwa kwenye Katiba mpya.

  Mheshimiwa Waziri alikutana na Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Joseph Sinde Warioba, Mwenyekiti wa Tume, Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Augustino Ramadhani, Makamu Mwenyekiti wa  Tume pamoja na Katibu wa Tume na Naibu Katibu wa Tume.


  Akiwasilisha hoja yake mbele ya Tume ya Marekebisho ya Katiba, Mheshimiwa Waziri alisema yafuatayo:-

  1.      Suala la Uraia wa Nchi mbili haliko kwenye rasimu ya sasa iliyotolewa.  Lengo la kufika Tume ni ni kuomba suala hilo liingizwe kwenye rasimu.


  2.      Amependekeza Katiba itamke kwamba, Raia wa Tanzania aliyeko nje hatafutiwa uraia wake na mtu yeyote, chombo chochote sheria au Katiba, eti tu kwa sababu raia huyo amechukua uraia nje ya nchi.


  3.      Katiba ikitamka hivyo, itungwe Sheria itakayofafanua haki, wajibu na masharti ya Mtanzania mwenye uraia wa nchi mbili.


  4.      Katika kujenga hoja hizo tatu, Tume ilielezwa faida zitakazopatikana kwa kuitambua na kuishirikisha jamii ya Watanzania waliopo ughaibuni (Diaspora).  Tume pia iliondolewa wasiwasi juu ya madai kuwa uraia wa nchi mbili unahatarisha usalama wa taifa au utawafanya baadhi ya watu kupiga kura wakiwa nje. Tume iliambiwa kuwa Sheria za Uchaguzi hutawala upigaji kura kwa raia walio ndani  na nje na hauwi  holela.  Kuhusu suala la usalama, Waziri alisisitiza kama ni mashaka, basi mashaka hayo yawe kwa wageni wanaoomba uraia  nchini kuliko watanzania walioko nje.


  Katika kumalizia, Mheshimiwa Waziri alisisitiza, “bado naamini watanzania walioko nje sio wasaliti, They are just  smart citizens”.

  IMETOLEWA NA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA


older | 1 | .... | 237 | 238 | (Page 239) | 240 | 241 | .... | 3272 | newer