Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109591 articles
Browse latest View live

SIMIYU YAPOKEA VITABU VYA DARASA LA NNE

0
0

Na Stella Kalinga, Simiyu

Mkoa wa Simiyu umepokea jumla ya vitabu 174,188 awamu ya kwanza kwa masomo ya Kiingereza na Hisabati, vyenye thamani ya takribani shilingi milioni 348 kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la nne, ambavyo ni sawa na uwiano wa mwanafunzi mmoja kwa kitabu kimoja.

Akizungumza na viongozi , baadhi ya walimu na wanafunzi wa mkoa wa Simiyu kabla ya kukabidhi vitabu vitabu hivyo kwa Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka Julai 05 jioni mjini Bariadi, Mwakilishi wa Taasisi ya Elimu Tanzania(TET) Bw. Didas Hamsini, amesema Taasisi hiyo imejipanga kuhakikisha vifaa vyote vya kielimu ikiwemo vitabu, vifaa vya maabara na vifaa vingine vinavyohitajika vinapatikana.

Amesema utoaji wa vitabu 29,003 kwa kila somo kwa wanafunzi wa darasa la nne Mkoani Simiyu ni sehemu ya utekelezaji wa elimu bila malipo, huku akibainisha kuwa Taasisi ya Elimu inatarajia kuzalisha vitabu 681, 527 kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la nne nchi nzima.

Afisa Elimu Mkoa wa Simiyu, Mwl. Julius Nestory amesema wamepokea vitabu awamu ya kwanza kwa masomo ya kiingereza na hisabati kwa uwiano wa kitabu kimoja mwanafunzi mmoja, huku akibainisha kuwa vitabu vilivyobaki vinatarajiwa kuletwa tena wiki ya kuanzia tarehe 16 Julai, 2018 na akawataka walimu na wanafunzi kuvitumia vitabu hivyo kama ilivyokusudiwa.

“Naishukuru sana Serikali kwa kutoa vitabu hivi hadi sasa tuna wanafunzi 53, 187 darasa wa nne na vitabu tulivyopokea kwa awamu hii kwa masomo ya Hisabati na Kiingereza, kila mwanafunzi wa Mkoa wa Simiyu atapata kitabu cha kwake, kwa masomo manne yanayobaki tumeahidiwa kuwa baada ya majuma mawili vitakuwa vimefika” alisema Afisa Elimu Mkoa.

Kwa upande wao wanafunzi wa mkoa wa Simiyu wameishukuru Serikali kwa kuwaletea vitabu, hivyo ambavyo wanaamini vitawasaidia kujisomea na kuinua ufaulu hatimaye kuufikisha mkoa huo katika mikoa kumi bora inayofanya vizuri kitaaluma.“Tunaishukuru sana Serikali kwa kuwaleta hivi vitabu, tunaamini vitawasaidia wadogo zetu wa darasa la nne kujifunza na kuongeza ufaulu na siku moja mkoa wetu na sisi utakuwa kati ya mikoa bora inayofanya vizuri kitaaluma “ alisema Liku Malisha mwanafunzi wa darasa la saba Shule ya Msingi Somanda A.


 Mwakilishi wa Taasisi ya Elimu Tanzania(TET) Bw. Didas Hamsini(kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akiwa na baadhi ya viongozi na wanafunzi wa Shule ya Msingi Somanda A vitabu vya Darasa la nne mkoani humo, makabidhiano hayo yalifanyika Julai 05, 2018 katika Viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mjini Bariadi.

 Afisa Elimu Mkoa wa Simiyu, Mwl.Julius Nestory  akihojiwa na waandishi wa habari baada ya Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka Mtaka kukabidhiwa vitabu vya Darasa la nne na Mwakilishi wa Taasisi ya Elimu Tanzania(TET) Bw. Didas Hamsini,  katika Viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini Bariadi Julai 05, 2018. 
 Mbunge wa Itilima Mkoani Simiyu,  Mhe. Njalu Silanga akihojiwa  na waandishi wa habari baada ya Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka Mtaka kukabidhiwa vitabu vya Darasa la nne na Mwakilishi wa Taasisi ya Elimu Tanzania(TET) Bw. Didas Hamsini,  katika Viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini Bariadi Julai 05, 2018. 
 Abdallah Twalib Mwanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Somanda A, akitoa shukrani kwa niaba ya wenzake mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kukabidhiwa vitabu vya Darasa la nne mkoani humo na Mwakilishi wa Taasisi ya Elimu Tanzania(TET) Bw. Didas Hamsini,  katika Viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini Bariadi. 

KUSOMA HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MSHINDI WA 11 WA DROO YA SHINDA NA TEMBOCARDVISA AKABIDHIWA TIKETI YAKE

0
0
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa akimkabidhi mfano wa tiketi ya mechi za Kombe la Dunia, Mshindi wa 11 wa droo ya Shinda na TemboCardVisa, David Hughes ambaye atasafiki kuelekea nchini Urusi kushuhudia moja ya mechi za robo fainali ya Mashindano ya Kombe la Dunia 2018. makabidhiano hayo yamefanyika leo makao makuu ya Benki ya CRDB, jijini Dar es salaam.
Mshindi wa 11 wa droo ya Shinda na TemboCardVisa, David Hughes akizungumza jambo wakati akiishukuru Benki ya CRDB kwa kuendesha droo hiyo iliyompatia ushindi wa kwenda kushuhudia moja ya mechi za Kombe la Dunia nchini Urusi.

DKT. MWAKYEMBE AKUBALI KUKUTANA NA WATOA HUDUMA ZA MAUDHUI MTANDAONI, KUJADILIANA MALIPO YA TCRA

0
0

 Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii.


 Waziri wa Habri, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amekubali kukaa na kujadiliana na Wadau wa utoaji huduma za Maudhui Mtandaoni kwa kina  na namna ya kulipia  tozo ua huduma hizo katika Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). 

 Akizungumza na watoa huduma hao mapema leo jijini Dar es Salaam, Dkt. Mwakyembe amesema kuwa Kanuni za Huduma hizo Mtandaoni zimetungwa na yeye Waziri mwenye dhamana ya Habari na TCRA ni Watekelezaji wa Sheria hizo.  ‘Milango bado ipo wazi kuhusu kanuni lakini zinarekebishika kukibainika kuwa na utata mkubwa, na pia kanuni hizi ni za wote’, amesema Dkt. Mwakyembe.

 Waziri huyo ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari na mtaalamu bingwa wa mambo sheria za mitandao, amesema kuwa kanuni hizo ni mpya ambapo wamekaa Wanasheria wa Wizara na Wataalam wa Mitandao kutoka TCRA kutengeneza kanuni hizo, hata hivyo amedai kila nchi inakuja kuiga mfano kwa Tanzania. 

 ‘Kanuni hizi zimetungwa kuangalia Mazingira ya nchi kutokana na Mitandao kuwa chanzo kikubwa cha Habari’, ameeleza Dkt. Mwakyembe Amesema Serikali ya Tanzania itafurahia kusimamia Kanuni ambazo zinaeleweka pamoja na kufuatwa na kila mtu.
 Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na michezo Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza mbele ya baadhi ya Waendesha mitandao ya kijamii mbalimbali (hawapo pichani), kuhusiana na changamoto wanazokumbana nazo kufuatia kuanza kwa utekelezaji wa kanuni za maudhui ya mtandaoni zilizoanza kutumika hivi karibuni,ambapo Waziri Mwakyembe amekubali kukutana na Wadau hao ili kuangalia maeneo ya kufanyiwa marekebisho kwa namna moja ama nyingine.

Mkutano huo umefanyika mapema leo katika ofisi za Radio7  Msasani  jijini Dar es Salaam ambapo waziri Mwakyembe alikuwa amealikwa.Pichani kulia ni Mwakilishi kutoka TCRA,Ndugu Kibaja sambamba na Mmiliki  na Mkurugenzi wa Radio 7  Online Antu Mandoza na kushoto ni Kaimu MKurugenzi Idara ya Habari MAELEZO,Patric Kipangula.
  Waziri wa Habri, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akitoa ufafanuzi kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo suala la kanuni za utoaji huduma za Maudhui Mtandaoni,alipokuwa akifanya mahojiano mafupi na kituo cha radio ya Mtandaoni Radio 7,Msasani Jijin Dar Es Salaam .  
 Mmoja wa Waendesha Mtandao wa DarMpya.Com John Marwa akiuliza moja ya swali kwa Waziri Mwakyembe kuhusiana  na kanuni/sheria za mtandao zilizoanza kutumika hivi karibuni,Mkutano huo umefanyika mapema leo katika ofisi za Radio7  Msasani  jijini Dar es Salaam ambapo waziri Mwakyembe alikuwa amealikwa.Pichani kulia ni Mwakilishi kutoka TCRA,Ndugu Kibaja sambamba na Mmiliki  na Mkurugenzi wa Radio 7  Online Antu Mandoza na kushoto ni Kaimu MKurugenzi Idara ya Habari MAELEZO,Patric Kipangulamapema leo 
 Sehemu ya Meza kuu ikichukua sehemu ya maoni yaliyokuwa yakitolewa na baadhi ya Wadau.

MADEREVA WA PIKIPIKI WAFURAHISHWA NA HUDUMA ZA TRA KATIKA MAONYESHO YA SABASABA

0
0
Na Veronica Kazimoto,Dar es Salaam

Madereva wa Pikipiki ambao ni wanachama wa Umoja wa Waendesha Pikipiki Wilaya ya Temeke (UWAPITE) wamefurahishwa na huduma zinazotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba yanayoendelea kufanyika jijini Dar es Salaam.

Madereva hao wapatao 20 wametembelea banda la TRA kwa ajili ya kusajiliwa na kupatiwa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) kwa lengo la kukatia leseni mara baada ya kumaliza mafunzo ya udereza wa pikipiki yaliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke kwa kushirikiana na Umoja huo.Akizungumza baada ya kusajiliwa madereva hao, Mwenyekiti wa Umoja huo Said Kagomba amesema kuwa, amefurahishwa na huduma nzuri waliyopatiwa na TRA ambapo wanachama wote wamesajiliwa na kupatiwa TIN kwa muda mfupi.

"Mimi kama Kiongozi wa Umoja huu nimefurahia sana huduma tuliyopata hapa TRA, kwanza tumepokelewa vizuri na kisha tumehudumiwa haraka na kila mwanachama amepatiwa cheti chake cha TIN na sasa tunaendelea na hatua nyingine ya kwenda kukata leseni," alisema Kagomba.Naye mmoja wa Madereva hao Ramadhan Mwilombwa ametoa wito kwa vijana kujiunga katika vyama mbalimbali kwa kuwa kuna faida nyingi ikiwa ni pamoja na kupata mafunzo, TIN na leseni kwa urahisi kwa sababu viongozi wa vyama husika wanajua sheria na taratibu mbalimbali.

"Ninaomba vijana wenzangu wajiunge na vyama hivi kwa sababu palipo na wengi hakiharibiki kitu. Mimi binafsi mpaka sasa nimepata faida nyingi za kujiunga na Umoja huu, kwanza nimepata mafunzo ya udereva na kujua vizuri sheria za barabarani, pili nimefahamiana na vijana wenzangu ambao nilikuwa siwafahamu, tatu nimefanikiwa kusajiliwa na TRA na kupata TIN na mwisho kiongozi wetu ametuambia tunakwenda kukata leseni," alifafanua Mwilombwa.

Mamlaka ya Mapato Tanzania inaendelea kutoa huduma mbalimbali katika Maonyesho ya Sabasaba. Miongoni mwa huduma hizo ni pamoja na kusajili walipakodi, kuelimisha wananchi umuhimu wa kulipa kodi, kutoa bili na kulipa Kodi ya Majengo.

Huduma nyingine ni kuelezea wananchi haki na wajibu wa Mlipakodi kama ilivyoainishwa katika Mkataba wa Huduma na Mlipakodi, kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya Mashine za Kielektroniki za Kutolea Risti (EFDs), kuelezea mwenendo wa makusanyo ya mapato ya Serikali, na kupokea maoni, malalamiko, mrejesho pamoja na mapendekezo mbalimbali kutoka kwa wananchi.
Wanachama wa Umoja wa Waendesha Pikipiki Wilaya ya Temeke (UWAPITE) jijini Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya banda la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakiwa wameshika Namba za Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) wakati wa Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) ya mwaka 2018.
Afisa wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Helly Shindano Akimhudumia Dereva wa Pikipiki katika banda la TRA wakati wa Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) ya mwaka 2018.
Wanachama wa Umoja wa Waendesha Pikipiki Wilaya ya Temeke (UWAPITE) jijini Dar es Salaam wakiwa katika banda la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakisubiri kupatiwa huduma ya usajili na kupewa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) wakati wa Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) ya mwaka 2018.
Afisa wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bi. Jackline Lutare akisikiliza kero za mteja katika banda la TRA wakati wa Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) ya mwaka 2018.(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA)

MultiChoice Tanzania yaibuka kidedea Sabasaba

0
0
Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa (Kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Uhusiano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana cheti na kombe baada ya banda la DStv kuibuka kidedea katika kundi la waonyeshaji wa huduma na bidhaa za teknolojia ya Mawasiliano.
Wafanyakazi na mawakala wa MultiChoice Tanzania wakishangilia ushindi mara baada ya banda lao la DStv kuibuka banda bora katika kundi la waonyeshaji wa huduma na bidhaa za teknolojia ya Mawasiliano katika maonyesho ya 42 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Uhusiano wa MultiChoice Tanzania akiwa na balozi maalum wa DStv Nancy Sumari wakionyesha cheti na Kombe walivyokabidhiwa kampuni ya MultiChoice Tanzania baada ya kuibuka banda bora katika kundi la waonyeshaji wa huduma na bidhaa za teknolojia ya Mawasiliano katika maonyesho ya 42 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam

Gari ya tatu ya M-Pesa yakabidhiwa Arusha, bado magari saba

0
0
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Richard Kwitega (katikati) akimkabidhi funguo za gari mshindi wa tatu wa gari aina ya Renault Kwid Mkomeni Ernest Mgonho (kulia) katika hafla ya kuwazawadia washindi wa M-Pesa kanda ya kaskazini baada ya kujishindia gari hilo katika bahati nasibu inayoendelea ya ‘Tumia M-Pesa ushinde gari’, kushoto ni mkuu wa Vodacom kanda ya Kaskazini Bigita Stephen.
Mke na mjukuu wa Bwana Mgomho wakishuhudia akikabidhiwa gari lake aina ya Renault Kwid na  Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Richard Kwitega(kulia) katika hafla ya kuwazawadia washindi wa M-Pesa kanda ya kaskazini.
Picha ya pamoja

TFDA iwe chachu ya Uchumi wa Viwanda nchini.

0
0
Na  WAMJW,Dar as Salaam

Mamlaka ya chakula na dawa TFDA imetakiwa kuwa chachu ya uchumi wa viwanda hususani katika kuzalisha dawa hapa nchini ili kupata matokeo chanya katika hatua ya kuinua uchumi wa viwanda.

Hayo yamezungumzwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati wa kukabidhi vyeti vya ithibaki kwa kiwango cha kimataifa ISO 17025 kwa maabara ya chakula na maikrobailojia za TFDA.

"TFDA isiwe kikwazo kwa wawekezaji nchini hususan Viwanda vya kuzalisha dawa ili kuunga mkono juhudi za Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli ya kuelekea uchumi wa viwanda"

Aidha,Waziri Ummy amesema TFDA wanawajibu wa kuwawezesha wafanyabiashara kutoa bidhaa zao wanazozileta nchini mapema zaidi Mara wanapokuwa wamejiridhisha na ubora unaokidhi afya za watanzania na kuwapa vibali mapema.Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA )Agnes's kijo amesema wanawajibu wa kuimarisha afya za watanzania na kuimarisha maabara zao kwa viwango vinavyokubalika kitaifa.

Kijo amesema vyeti hivyo vya kimataifa ni ishara kubwa inayoonyesha Kuwa TFDA inafanya kazi katika kudhibiti ubora wa bidhaa hususan vyakula na dawa ili kujenga afya za wananchi.TFDA imepokea vyeti vya uthibiti kwa kiwango cha kimataifa kwa maabara ya chakula na daea ambapo wamefanya vizuri katika upimaji wa vyakula na dawa vinavyoingia na kutoka nchini.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA na baadhi ya wadau wa afya hawapo pichani wakati wa upokeaji wa vyeti vya Ithibati kwa kiwango cha kimataifa iliyofanyika leo jijini Dar es salaam.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA Bi. Agness Kijo akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka hiyo na baadhi ya wadau wa afya hawapo pichani wakati wa upokeaji wa vyeti vya Ithibati kwa kiwango cha kimataifa iliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wa kushoto akikata utepe kuashiria kupokea rasmi vyeti vya Ithibati kwa kiwango cha kimataifa walivyopewa Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA katika hafla ya kupokea vyeti hivyo leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa Maabara wa Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA wakati wa upokeaji wa vyeti vya Ithibati kwa kiwango cha kimataifa iliyofanyika leo jijini Dar es salaam, wa pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA Bi. Agness Kijo.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)



Sehemu ya tendaji wa Mamlaka ya chakula na dawa

UBALOZI WA JAPAN WAMUUNGA MKONO WAZIRI UMMY MWALIMU KUJENGA MADARASA SITA YA SHULE YA MSINGI MWAKIDILA JIJINI TANGA

0
0


SHIRIKA la Maendeleo ya Wanawake mkoani Tanga (Tanga Women Development Initiative-TAWODE) chini ya Mwenyekiti wale Waziri Ummy Mwalimu (MB) leo wamewekeana saini ya ujenzi wa madarasa sita ya shule ya msingi kata ya Tanga sisi katika Jiji la Tanga. 

Msaada huo wenye thamani hya dola za kimarekani 84,000 (Takribani shilingi za kitanzania milioni 188) umetolewa na Serikali ya Japan kupitia Ubalozi wake nchini Tanzania kufuatia maombi ya Mwenyekiti wa TAWODE Mh Ummy Mwalimu ya kuunga mkono jitihada za serikali za kuboresha miundombinu ya elimu ya msingi na sekondari katika Jiji la Tanga. 

Akizungumza katika halfa hiyo Mh Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshida alisema serikali ya Japan imetoa fedha hizo ili kuwasaidia maendeleo ya elimu kwa Jiji la Tanga ili kutatua tatizo la mrundikaano wa wanafunzi madarasani huku akiwataka Tawode kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kikamilifu na kukamilika kwa wakati. 

Naye mgeni rasmi katika uzinduzi huo,Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu aliushukuru ubalozi wa Japan kwa kukubali ombi lao la kufadhili ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi Mwakidila ambayo ina wanafunzi zaidi ya 1400 kulinganisha na madarasa machache yaliyopo na hivyo kusababisha mrundikano mkubwa kwa wanafunzi. 

Aidha Waziri Ummy alieleza kuwa ongezeko la wanafunzi limechangiwa na uamuzi wa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli wa kutoa elimu bure hivyo wakati serikali ikiweka jitihada kubwa za kuboresha miundombinu ya elimu katika Halmashauri mbalimbali kote nchini bado zipo changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa madarasa. 
Mkurugenzi waShirika la Maendeleo ya Wanawake mkoani Tanga(Tanga Women Development Initiative-TAWODE) Tawode Fatuma Mganga kushoto akisaini na Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshida Msaada huo wenye thamani hya dola za kimarekani 84,000 (Takribani shilingi za kitanzania milioni 188) umetolewa na Serikali ya Japan kupitia Ubalozi wake nchini Tanzania kufuatia maombi ya Mwenyekiti wa TAWODE Mh Ummy Mwalimu ya kuunga mkono jitihada za serikali za kuboresha miundombinu ya elimu ya msingi na sekondari katika Jiji la Tanga. wanaoshuhudia ni Mstahiki meya wa Jiji la Tanga Alhaji Mustapha Selebosi na kulia ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji
Mkurugenzi waShirika la Maendeleo ya Wanawake mkoani Tanga(Tanga Women Development Initiative-TAWODE) Tawode Fatuma Mganga kushoto na Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshida wakionyesha hati za makubaliano ya msaada huo wenye thamani hya dola za kimarekani 84,000 (Takribani shilingi za kitanzania milioni 188) umetolewa na Serikali ya Japan kupitia Ubalozi wake nchini Tanzania kufuatia maombi ya Mwenyekiti wa TAWODE Mh Ummy Mwalimu ya kuunga mkono jitihada za serikali za kuboresha miundombinu ya elimu ya msingi na sekondari katika Jiji la Tanga.
Mkurugenzi waShirika la Maendeleo ya Wanawake mkoani Tanga(Tanga Women Development Initiative-TAWODE) Tawode Fatuma Mganga kushoto wakibalishana hati za makubaliano na Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshida Msaada huo wenye thamani hya dola za kimarekani 84,000 (Takribani shilingi za kitanzania milioni 188) umetolewa na Serikali ya Japan kupitia Ubalozi wake nchini Tanzania kufuatia maombi ya Mwenyekiti wa TAWODE Mh Ummy Mwalimu ya kuunga mkono jitihada za serikali za kuboresha miundombinu ya elimu ya msingi na sekondari katika Jiji la Tanga.
Mkurugenzi waShirika la Maendeleo ya Wanawake mkoani Tanga(Tanga Women Development Initiative-TAWODE) Tawode Fatuma Mganga kushoto akimshukuru Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshida Msaada huo wenye thamani hya dola za kimarekani 84,000 (Takribani shilingi za kitanzania milioni 188) umetolewa na Serikali ya Japan kupitia Ubalozi wake nchini Tanzania kufuatia maombi ya Mwenyekiti wa TAWODE Mh Ummy Mwalimu ya kuunga mkono jitihada za serikali za kuboresha miundombinu ya elimu ya msingi na sekondari katika Jiji la Tanga.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katika akiwa na Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshida kulia Msaada huo wenye thamani hya dola za kimarekani 84,000 (Takribani shilingi za kitanzania milioni 188) umetolewa na Serikali ya Japan kupitia Ubalozi wake nchini Tanzania kufuatia maombi ya Mwenyekiti wa TAWODE Mh Ummy Mwalimu ya kuunga mkono jitihada za serikali za kuboresha miundombinu ya elimu ya msingi na sekondari katika Jiji la Tanga. kulia ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaji Mustapha Selebosi kushoto ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji


BAADHI YA MAWAZIRI WATEMBELEA BANDA LA TRA KATIKA MAONYESHO YA SABASABA

0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenister Mhagama akimsikiliza kwa makini Afisa Mwandamizi Uchambuzi Mifumo ya Biashara Mathias Chanila wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakati Waziri huyo alipotembelea banda la TRA katika Maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) ya mwaka 2018 yanayoendelea kufanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Mhandisi Stella Manyanya (kushoto) akitoa maoni yake kwa Afisa wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Chama Siriwa (kulia) wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea banda la TRA katika Maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) ya mwaka 2018 yanayoendelea kufanyika jijini Dar es Salaam. Katikati ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenister Mhagama.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akionyeshwa bili ya majengo na Meneja wa Huduma kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bi. Honester Ndunguru wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea banda la TRA katika Maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) ya mwaka 2018 yanayoendelea kufanyika jijini Dar es Salaam.
Mwanafunzi wa Kidato cha Sita kutoka Shule ya Sekondari St. Joseph Cathedral Tax Club iliyopo jijini Dar es Salaam Bertha Bureta akimuelezea Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji faida za kulipa kodi wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea banda la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika Maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) ya mwaka 2018 yanayoendelea kufanyika jijini Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA)

MICHUZI TV: DC ILALA AWAKARIBISHA WANANCHI KUUPOKEA MWENGE WA UHURU KESHO.

0
0


MWENGE WA UHURU KUWASILI DAR KESHO UKITOKEA PEMBA


Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

MWENGE wa uhuru unataraji kuwasili kesho jijini Dar es salaam ukitokea Pemba na kufungua zaidi ya miradi 33 jijini.

Akizungumza na vyombo vya habari mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameeleza kuwa kesho asubuhi mwenge wa uhuru utapokelewa katika uwanja wa ndege wa mwalimu Julius Nyerere majira ya saa 12 asubuhi na utaanza kumulika Wilaya ya Ilala na kufungua miradi mbalimbali Wilayani humo.

Makonda ameeleza kuwa 8 Julai utapokelewa katika Wilaya ya Kigamboni, tarehe 9 utakuwa Kinondoni na kumalizia ziara Temeke.Ameeleza kuwa licha ya mwenge kumulika katika Mkoa pia utafungua miradi mbalimbali ya kimaendeleo zaidi ya 33 ikiwemo shule, madarasa sambamba na kuweka jiwe la msingi katika miradi mbalimbali ambapo ameeleza kuwa Mkoa huo ndio wenye miradi ya fedha nyingi nchini.

Aidha amewaomba wakazi ya jiji la Dar es salaam kujitokeza kwa wingi na kushiriki pamoja katika ziara ya mwenge katika kufungua miradi sambamba na kujenga undugu na urafiki.

TCAA YASHAURIWA KUWEKEZA KWENYE WATAALAMU WA NDANI

0
0

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeishauri Mamlaka ya Usafiri wa Anga Nchini (TCAA) kuwekeza kwenye rasilimali watu ili kuongeza tija kwa wataalam wa ndani mara baada mradi wa ujenzi wa rada nne kukamilika.

Akizungumza mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa rada katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Mwl. Julius Nyerere (JNIA), Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Selemani Kakoso, amesema kuwawezesha wataalam wa ndani kutawajengea uwezo wa kwenda na kasi ya teknolojia kwenye uongozaji ndege.

“Mradi huu utatumia fedha nyingi hivyo ni vyema kuzingatia wataalam wa ndani kupata elimu ya rada hizi ili mradi ukikamilika wasimamie vyema na si watalaam kutoka nje ya nchi”, amesisitiza Mhe. Kakoso.Mhe. Kakoso, amesema kuwa Kamati imeridhishwa na kasi ya ujenzi wa rada unaoendelea na kuwataka mradi ukamilike kwa kuzingatia viwango vilivyowekwa kwenye mkataba.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias Kwandikwa, amesema uboreshaji wa Viwanja vya ndege mbalimbali nchini unafanywa kwa pamoja na ufufuaji wa Shirika la Ndege ambapo mpaka sasa Serikali imeshanunua ndege sita.Naye Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari ameihakikishia Kamati kuwa mradi huo utakamilika kwa wakati na kwa viwango na kusema kuwa tayari kuna wataalam zaidi ya 20 ambao watapata mafunzo ili kuongoza rada hizo mara baada ya mradi kukamilika.
Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga, Aristide Kanje akiwaonesha Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu eneo la Chuo hicho, wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara chuoni hapo, jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Selemani Kakoso
Muonekano wa jengo la rada katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), ambalo linaendelea kujengwa, jijini Dar es Salaam. Mradi huo unatarajiwa kukamilika mwanzoni mwa mwakani.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Nchini (TCAA), Hamza Johari, akitoa ufafanuzi kwa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu, kuhusu maendeleo ya ujenzi wa rada ya kisasa inayosimikwa katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Selemani Kakoso, akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Nchini (TCAA), Hamza Johari (Kushoto), mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa rada katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias Kwandikwa.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), Richard Mayongela, akitoa ufafanuzi kwa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka hiyo, wakati Kamati hiyo ilipokuwa kwenye ziara ya mafunzo, jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa gari jipya la Zimamoto lililonunuliwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA). Gari hilo litatoa huduma katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.


Jeshi la Polisi mkoani Dodoma wanasa Wezi wa mitandaoni na wahamiaji haramu

0
0
Jeshi la Polisi mkoani Dodoma limewakamata watu wawili wanaotuhumiwa kuiba fedha kwa njia ya Mtandao, ambao wanatumia pikipiki yenye namba za usajili bandia MC. 759 AHW na Chassis namba PFZWFK47770 aina ya boxer.
  Kamanda wa polisi mkoani humo ACP Gilles Muroto aliwataja Watuhumiwa hao kuwa ni Joseph Bakari Msinati (32) Mkazi wa Frelimo Iringa na Elisha Athman Mdemu(35)Mkazi wa Kihesa Iringa,ambao walitumia pikipiki hiyo kusafiri mikoa Mbalimbali mijini na vijijini kuiba bidhaa za dukani .
 “Watuhumiwa hawa wanafika kwenye maduka na kuagiza bidhaa mbalimbali na kufanya malipo kwa njia ya mtandao wa simu, Mara baada ya kulipa na mpokeaji kujiridhisha kupokea fedha hiyo wanaondoka na bidhaa. Na baada ya dakika chache wahalifu hao wanapiga simu kwenye Kampuni namba ya huduma kwa mteja na kudai kuwa warejeshewe fedha kwa kuwa wameituma kimakosa, na bidhaa kwenda kuuzwa kwa watu wengine kwa bei nafuu,” alisema Muroto.
 Pia Kamanda alisema wamefanikiwa kumkamata Daudi Charles (25) Mkazi wa Mbagala akiwa na noti bandia 50 za shilingi elfu 10 ambazo zingekuwa halali thamani yake ni TSH. 500,000/=.
Katika tukio lingine Kamanda alisema wamekamata mali mbalimbali za Wizi zilizotokana na matukio ya Uvunjaji na uporaji ambazo ni Televisioni 3, Magodoro 4, Redio Subwoofer 3, Majiko ya gesi 2, Spika 3, Deck 3, mifuko ya Cement 5 pamoja na Kapeti 1. 
Kamanda Muroto amewataka wananchi walioibiwa kufika polisi ili kuweza kuzitambua mali zao, Pia aliwatahadharisha Waharifu kuwa Dodoma siyo mahali Salama pa kufanyia uharifu.
Wakati huo huo Jeshi la polisi mkoani Dodoma limekamata Wahamiaji haramu 40 Raia wa Ethiopia pamoja na Watanzania wanne waolikuwa wakiwasafirisha Wahamiaji hao. 
Kamanda wa polisi mkoani humo ACP Gilles Muroto amesema kwamba ahamiaji hao walikamatwa katika barabara kuu ya Dodoma kuelekea Arusha kijiji cha Kuhi kata na tarafa ya Bereko Wilayani Kondoa. 
 Alisema Wahamiaji hao walikuwa wakisafirishwa na gari lenye namba za usajili T. 898 AHM na tela namba T. 422 ADD aina ya Scania mali ya Kampuni ya SANVIC LTD. 
Watanzania waliokuwa wanawasafirisha Wahamiaji hawa ni Dereva Julius Jackson Kitoma(57) Mnyaturu na mkazi wa Ngarenaro Arusha, Abedi Raphael Nyomolelo (20) Utingo wa gari hilo na Mkazi wa Sakina Arusha. 

Wengine ni Ramadhani Salumu Mawazo (39)Mzaramo pia mkulima na mkazi wa Mbagala Dar es Salaam pamoja na Juma Ramadhani Husei (46) Mzigua, mkulima na mkazi wa Kinyerezi Dar es Salaam, aliwataja Muroto. Aidha alisema kuwa Watuhumiwa hao walitumia mbinu ya kuwafungia Wahamiaji hao kwenye Contena la Mizigo, wakiwachanganya na bidhaa walizokuwa wakizisafirisha ambazo ni maboksi yenye Vizibo vya Soda na bia kutoka Namanga- Arusha kuelekea Mbeya.
Kamanda wa polisi mkoani Dodoma  ACP Gilles Muroto akiwa na sehemu ya wahamiaji haramu 40 Raia wa Ethiopia pamoja na Watanzania wanne waolikuwa wakiwasafirisha Wahamiaji hao. 
Kamanda wa polisi mkoani Dodoma  ACP Gilles Muroto akiwa na mmoja wa watuhumiwa wawili wanaotuhumiwa kuiba fedha kwa njia ya Mtandao.

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE MIUNDOMBINU YAKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA RELI YA SGR, YAMPONGEZA RAIS MAGUFULI

VIONGOZI MBALIMBALI WAENDELEA KUTEMBELEA BANDA LA BUNGE KATIKA VIWANJA VYA SABASABA

0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana, Wazee na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama akizungumza na Maafisa wa Ofisi ya Bunge alipotembelea Banda lao katika Maonesho ya 42 ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba. Kulia ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Eng. Stella Manyanya.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana, Wazee na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Eng. Stella Manyanya  na Maafisa wa Ofisi ya Bunge alipotembelea Banda lao katika Maonesho ya 42 ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba.
 Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Adelardus Kilangi akisikiliza maelezo kuhusu shughuli mbalimbali za Bunge kutoka kwa Mwandishi  Mwandamizi wa Taarifa Rasmi za Bunge Bw. Paston Sobha alipotembelea Banda lao katika Maonesho ya 42 ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba.
 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu Jenerali Mirisho Sarakikya akisikiliza maelezo kuhusu shughuli mbalimbali za Bunge kutoka kwa Mwandishi  Mwandamizi wa Taarifa Rasmi za Bunge Bw. Paston Sobha alipotembelea Banda lao katika Maonesho ya 42 ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile akisaini Kitabu cha Wageni alipotembelea Banda la Bunge katika Maonesho ya 42 ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba.
PICHA NA BUNGE

VOA SWAHILI: HABARI ZA BURUDANI


NSSF WATOA MSAADA WA ZAIDI YA MILIONI 4.5 MANISPAA YA IRINGA NA HALMASHAURI YA IRINGA

0
0
Na Francis Godwin, Michuzi Blog, Iringa 

MFUKO  wa   hifadhi ya  jamii (NSSF)  umetoa  msaada  wa  mashuka 300 yenye  thamani ya  zaidi ya  shilingi  milioni 4.5  kwa  Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa  na  halmashauri ya  Iringa mkoani  Iringa  kwa ajili ya  kusaidia hospitali  ,zahanati na  vituo  vya afya vyenye upungufu wa mashuka ya  wagonjwa.
Akikabidhi  msaada  huo  leo  meneja  wa  NSSF  mkoa  wa Iringa  Josephat  Komba  alisema  kuwa NSSF  imetoa msaada  huo  ikiwa ni  sehemu ya  utekelezaji  wa maombi yaliyotolewa na  Halmashauri  hizo  kwa  NSSF  kuomba  kusaidiwa msaada wa mashuka.
Komba  alisema kuwa NSSF  kama  mfuko  wa  hifadhi ya jamii  unayojukumu  la kuendelea  kuunga mkono  jitihada  za  Halmashauri  nchini  katika  kutoa  huduma  za  afya na  pia  unaendelea  kuunga  mkono   jitihada  za  serikali ya  awamu ya  tano  chini ya  Rais Dkt  John Magufuli  kuona  sekta ya  afya  inaendelea  kuboreshwa  zaidi.
Kwani  alisema  NSSF pamoja  na majukumu mengine itaendelea  kuwa karibu na  jamii ya kitanzania kwani hatua  ya  waajiri kuwaunganisha  wafanyakazi wao na  NSSF  ni kutaka  kuona  maisha yao  yanaendelea  kuboreshwa  zaidi  hivyo  jukumu lao kuona  NSSF  inaendelea kuunga mkono azima ya  serikali katika  uboreshaji wa  huduma  za afya.

Meneja  wa NSSF  mkoa wa  Iringa Josephat  Komba(kushoto) akimkabidhi msaada wa  shuka  200  kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa Omary  Mkangama  kwa  ajili ya  Hospitali ya  Frelimo 
 Wafanyakazi wa  hospitali ya  Frelimo wakitandika  mashuka  yaliyotolewa na  NSSF 
 Mkurugenzi  wa Halmashauri ya Iringa Robert Masunya (kulia )  akishukuru kwa msaada wa  NSSF.
o 
Meneja  wa NSSF  mkoa wa  Iringa Josephat  Komba  (kushoto ) akimkabidhi msaada  wa mashuka  100 mkurugenzi wa  Halmashauri ya  Iringa Robert Masunya. Picha na Francis Godwin, Michuzi Blog, Iringa




PROF. MBARAWA AITISHA KIKAO CHA DHARURA KUPATA UFUMBUZI WA MRADI CHALINZE

0
0
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Prof. Makame Mbarawa ameitisha kikao cha dharura ili kupata ufumbuzi wa utekelezaji wa mradi wa maji wa Chalinze, ambao kwa muda mrefu umekua ukisuasua na kusababisha kutokamilika kwa wakati.
Kikao hicho kimefanyika katika ofisi za wizara zilizopo Dar es Salaam na kuhusisha DAWASA (wasimamizi wa mradi), Overseas Infrastructure Alliance Pvt Ltd (Mkandarasi), Shanxi Construction Engineering Group Corporation ya China (Mkandarasi-mshiriki) na WAPCOS Ltd ya India (Mtaalamu Mshauri) kwa lengo la kupatia ufumbuzi unaosababisha kusuasua kwa utekelezaji wa mradi huo.
Prof. Mbarawa ameitisha kikao hicho mara baada ya kumaliza ziara yake aliyoifanya ya kukagua maendeleo ya mradi wa maji wa awamu ya tatu ya upanuzi wa chanzo na mtandao wa maji wa Chalinze unaotekelezwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji na kusimamiwa na DAWASA na kutoridhishwa na uwezo wa mkandarasi anayetekeleza mradi.
Katika ziara hiyo Prof. Mbarawa alitembelea na kujionea kazi za upanuzi wa chanzo, ujenzi wa matenki, ulazaji wa mabomba, ujenzi wa vituo vya kuchotea maji, pamoja na ujenzi wa ofisi mpya za uendeshaji wa mradi huo.
Hata hivyo, amekerwa na kasi ya utekelezaji ya mkandarasi ambaye ameonekana kuwa na uwezo mdogo wa kufanya kazi hiyo kutokana na kusababisha mradi huo uliokuwa ukamilike tangu Februari, 2017 kuongezwa muda mara kwa mara bila mafaniko.
‘‘Nimegundua mkandarasi ndiye chanzo kikubwa cha kusuasua kwa mradi huu. Kwa kuwa kama ni pesa sio tatizo, zimekuwa zikitolewa lakini utendaji wake bado umezorota. Kwa kifupi, uwezo wa mkandarasi ni mdogo’’, alisema Prof. Mbarawa.
‘‘Mimi niliyepewa dhamana ya kusimamia sekta hii nampa muda mpaka kufikia mwezi Novemba na sio mwezi Disemba tena kama mkataba wake unavyosema, awe amekamilisha mradi huu. Vinginevyo, tutamchukulia hatua kwa kumfutia usajili na utakuwa mwisho wake kufanya kazi nchini na wala asisumbuke kuomba kazi nyingine yoyote kwa kuwa hatopata tena’’, alisisitiza Prof. Mbarawa.
Aidha, Prof. Mbarawa ameishukuru DAWASA na pamoja viongozi waliopita kwa juhudi zao za kuhakikisha mradi huo unatekelezwa vizuri na kwa wakati na kusema kuwa mradi huo kwa sasa ni lazima ukamilike ili wakazi wa maeneo ya Chalinze, Bagamoyo, Ngorongoro na Handeni waweze kupata maji.
Naye, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Dkt. Sufiani Masasi amesema watahakikisha wanasimamia maagizo ya waziri na kuchukua hatua stahiki ili mradi uweze kukamilika kwa ajili ya maendeleo ya Chalinze na maeneo ya jirani.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Chalinze (CHALIWASA), Mhandisi Christer Mchomba akisoma ripoti ya utendaji wa mamlaka hiyo kwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Prof. Makame Mbarawa na kulia ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Dkt. Sufiani Masasi.
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Prof. Makame Mbarawa akiwa kwenye mazungumzo na Wakandarasi, Mtaalam Mshauri na wasimamizi wa mradi wa Chalinze, DAWASA katika kikao kilichofanyika mara baada ya kumaliza ziara yake ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo.
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Prof. Makame Mbarawa akiangalia ujenzi wa tenki la Kihangaiko unaoendelea ikiwa ni sehemu ya mradi wa Chalinze.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Prof. Makame Mbarawa akitoa maagizo kwa Meneja Miradi Mkuu wa Kampuni ya Overseas Infrastructure Alliance Pvt Ltd, Srnivas Gonuguntla ambaye ndiye mkandarasi wa mradi wa Chalinze.

WAZIRI JENISTA MHAGAMA AIPONGEZA WCF KWA KUINGIA KWENYE MFUMO WA TEHAMA KATIKA KUTOA HUDUMA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI

0
0
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.Jenista Mhagama, amefurahishwa na mwitikio wa waajiri kujisajili na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) baada ya kuanza kushuhudia jinsi wafanyakazi wao wanavyonufaika na malipo ya Mafao ya Fidia.
Mhe. Waziri ameyasema hayo leo Julai 6, 2018 baada ya kutembelea banda la WCF kwenye maonesho ya 42 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere (Maarufu kama Sabasaba) jijini Dar es Salaam.
“Nichukue fursa hii kuwashukuru waajiri wote nchini ambao wameitikia wito wa Serikali wa kujisajili na Mfuko kwa mujibu wa Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi. Nimetaarifiwa kuwa mpaka sasa jumla ya waajiri 14,855 wamesajiliwa na Mfuko. Na kinachonifurahisha zaidi ni kwamba sasa waajiri wameanza kuona manufaa ya kuanzishwa kwa Mfuko baada ya kushuhudia jinsi wafanyakazi wao wanavyonufaika na mafao yanayolipwa na Mfuko” Alisema Mhe. Waziri.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, kwa mwaka wa fedha uliomalizika (2017/2018), tayari Mfuko ulikwishalipa mafao ya jumla ya shilingi bilioni 2.3 kwa wanufaika 812.” Alisema Bw. Mshomba.
Halikadhalika Bw. Mshomba alisema Mfuko umekuwa na faida sio tu kwa wafanyakazi na waajiri lakini pia hata kwa serikali kupitia kodi, ambapo alisema Mfuko umelipa kodi serikalini kiasi cha shilingi bilioni 3.2 kama kodi kwa mwaka wa 2016/2017 na mwaka huu ulioisha Juni 2018 tunatarajia kulipa zaidi ya shilingi bilioni 5 kama kodi ya serikali.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama, (wapili kushoto), Naibu Waziri wa Viwanda, Bishara na Uwekezaji, Mhe. Eng. Stella Manyanya, (wakwanza kushoto), na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Masha Mshomba wakipatiwa maelezo na wataalamu wa Mfumo wa Kielektroniki wa Mfuko huo, Bw.Uforo Henry, (wapili kulia) na Abdi Kalilo wakati Mhe. Waziri na Naibu Waziri walipotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonesho ya 42 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam Julai 6, 2018.
 Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, (kulia), akimuongoza Mhe. Waziri wakati akitembeela banda la Mfuko huo leo Julai 6, 2018.
.
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, WCF, Bi. Laura Kunenge (kulia) na mwenzake wa SSRA, Bi. Sara Kibonde Msika, wakibadilishana mawazo kwenye banda la WCF.
.
 Afisa Uhusoano Mwandamizi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Sebera Fulgence, (kushoto), akiwa na Justin Mwandumbya wa kitengo cha fedha
Maafisa wa WCF, Glady Madembwe, kutoka kitengo cha madai (Claims) (kushoto) na Afisa wa Afya na Usalama mahala pa kazi kutoka WCF, Bw. Robert Duguza (wapili kushoto), wakiwahudumia wananchi hawa waliotembelea banda la WCF.




HABARI ZA UMOJA WA MATAIFA KUTOKA NEW YORK LEO JULAI 6, 2018

NSSF WASHAURIWA KUWEKA DIRISHA LA KUHAMASISHA WANAUME KUPIMA UKIMWI NSSF WASHAURIWA KUWEKA DIRISHA LA KUHAMASISHA WANAUME KUPIMA UKIMWI

0
0

SHIRIKA la Taifa la Hafadhi ya Jamii (NSSF) wameshauriwa kutumia Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaa kuhamasisha wanaume wanaofika katika maonesho hayo kupima Virusi vya Ugonjwa wa UKIMWI (VVU).

Ushauri huo umetolewa leo na Waziri wa Sera, Kazi, Vijana,Ajira na Walemavu Jenista Mhagama, wakati anazungumza na uongozi pamoja na wafanyakazi wa NSSF baada ya kutembelea banda la shirika hilo ili kujionea shughuli ambazo zinatekelezwa na shirika hilo.

Waziri Mhagama pamoja na kutoa pongezi kwa NSSF kutokana na juhudi ambazo wanazifanya katika kuwahudumia Watanzania pamoja na kuunga mkono juhudi za ujenzi wa viwanda nchini kwa kujenga kiwanda cha sukari kilichopo Mbigili mkoani Morogoro ni vema wakaweka dirisha kwa ajili ya kuhamasisha wananchi kupima Vrusi vya UKIMWI.

“Niwapongeza NSSF kwa kazi nzuri ambayo mnaifanya nchini. Hata hivyo nitoe rai kwenu ni vema mkaweka na dirisha kwa ajili ya kuhamasisha wanaume kupima Virusi vya UKIMWI..Hivi karibuni Wazir Mkuu wetu Kassim Majaliwa amezindua kampeni ya kuhamasisha wananchi na hasa wanaume kupima Ukimwi. Hivyo niwaombe hata wanaume ambao wanakuja katika maoneshao nao wapime VVU.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama akizungmza na Bw. Charles Lyimo mwanachama wa Shirika la Taifa la Hafadhi ya Jamii (NSSF) huku akiwa amembeba Mtoto Martin Lyimbo aliyemkuta katika banda la hilo wakati alipotembelea kwenye maonesho ya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam na kukagua shughuli mbalimbali za (NSSF) leo. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa (NSSF) Godius Kahyarara wakati alipotembelea banda hilo kwenye maonesho ya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam leo, Kushoto ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Injinia Stella Manyanya. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama na Mkurugenzi Mkuu wa (NSSF) Godius Kahyarara wakimsikiliza Kaimu Meneja wa Uhusiano na Masoko Shirika la Hifadi ya Jamii (NSSF) Bw. Salim Khalfan wakati akitoa maelezo kwa waziri.

Viewing all 109591 articles
Browse latest View live




Latest Images