Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI AMTOLEA UVIVU MKANDARASI ANAYEJENGA MATANKI YA KUHIFADHIA MAJI DAR

$
0
0
*Ni baada ya kuchelewesha kukamilisha mradi uliotakiwa kumalizika mwaka 2017

Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii
WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa amemuagiza mkandarasi anayejenga matanki ya kuhifadhia maji na pampu na kusukumia maji kukamilisha mradi huo haraka hadi ifikapo mwishoni mwa Septemba mwaka huu

Amesema mkandarasi huyo Jain Irrigation system kutoka India  hadi sasa amekamilisha asilimia 87. 5 ya mradi huo ulioanza Machi mwaka 2016 na ulipaswa kukamilika Novemba mwaka 2017.

Waziri Mbarawa ameyasema hayo leo wakati wa ziara yake ya siku tatu ya  kukagua  miradi ya maji inayosimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA)  ambayo bado ipo kwenye utekelezaji katika maeneo mbalimbali jijini.

 Amesema mradi wa uboreshaji wa mfumo wa usambazaji maji jijini ni wa muhimu na utagarimu Sh. bilioni 72.43 lakini inasikitisha mpaka sasa bado hajakamilisha.

 "Mradi huu ni muhimu sana kwani watanzania wengi hasa wananaoishi hapa jijini Dar es Salaam wanachangamoto kubwa ya maji,"amesema Mbarawa.

Amesema lengo kubwa la kuanzishwa kwa mradi huo ilikuwa ni kuhakikisha changamoto za maji kwa watanzania  zinakwisha lakini mkandarasi bado analeta shida.

Kutokana na  mapungufu hayo ya Mkandarasi, Waziri Mbarawa amemuagiza Meneja mradi huo, Anil Vitankar kuhakikisha mradi huo unamalizika kwa haraka na pia amemuagiza mkandarasi huyo kuwepo kwenye eneo la mradi kwa saa 24, na kama akishindwa kumaliza mradi huo kwa wakati waliokubaliana ambao ni mwisho mwezi September basi hiyo ndio itakuwa mara yako ya mwisho kwa mkandarasi huyo kufanya kazi nchini.
  WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mbarawa (wa pili kulia), akikagua sehemu ya kuhifadhi vifaa kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa uboreshaji wa mifumo ya maji Dar es Salaam na Pwani,  unaosimamiwa na Mamalaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA).
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mbarawa, akitoka kukagua tenki la kuhifazia maji, Mabwepande, Dar es Salaam.
  Profesa Mbarawa, akizungumza na waandishi wa habari pamoja na kumpa maagizo mkandarasi wa Kampuni ya Jain Irrigation System kutoka nchini India  mara baada ya kufanya ukaguzi wa ujenzi wa mradi wa uboreshaji wa mifumo ya maji Dar es Salaam na Pwani.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


KANGI LUGOLA AREJEA JIJINI DAR ES SALAAM, AVUNJA KAMATI ZOTE ZA USALAMA BARABARANI

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye (kushoto) baada ya kurejea kutoka jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi. Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam,walijadiliana  mambo mbalimbali yanayolihusu jeshi hilo. Akiwa mkoani Mbeya Mhe. Lugola amelivunja Baraza la Taifa la Usalama Barabarani na Kamati zote za Usalama barabarani za mikoa na wilaya zote, na kusema atayaunda upya ili kupambana na janga sugu la ajali za barabarani. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akipeana mikono na   Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye(kulia), baada ya kurejea kutoka jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Video courtesy of MCL Digital

AIRTEL YAZINDUA HUDUMA YA KUTUMA PESA BURE

SPIKA NDUGAI AONGOZA WAHESHIMIWA WABUNGE KATIKA MAZISHI YA ALIYEKUWA MBUNGE WA KOROGWE VIJIJINI MHE. STEPHEN NGONYANI

$
0
0
 Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akizungumza wakati wa wa mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Korogwe Vijijini Marehemu Stephen Hillary Ngonyani yaliyofanyika leo nyumbani kwake Korogwe Jijini Tanga. kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, kazi, Vijana na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama na Kushoto ni Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakari Zuberi
 Mawaziri, Manaibu Waziri, Waheshimiwa Wabunge na Viongozi mbalimbali wa Kitaifa wakiwa katika mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Korogwe Vijijini Marehemu Stephen Hillary Ngonyani yaliyofanyika leo kijijini kwake Kwamndolwa Wilayani Korogwe Jijini Tanga.
 Wapambe wa Bunge wakibeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Korogwe Vijijini Marehemu Stephen Hillary Ngonyani tayari kwa mazishi yaliyofanyika leo Kijijini kwake Kwamndolwa Wilayani Korogwe Jijini Tanga. 

 Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Mbunge wa Korogwe Vijijini Marehemu Stephen Hillary Ngonyani katika mazishi yaliyofanyika leo kijijini kwake Kwamndolwa Wilayani Korogwe Jijini Tanga.
PICHA NA DEONISIUS SIMBA - OFISI YA BUNGE

IGP SIRRO AWASILI MWANZA KWA ZIARA YA KIKAZI KANDA YA ZIWA, ATOA MAELEKEZO KUDHIBITI AJALI ZA BARABARANI

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewasili mkoani Mwanza kwa ziara ya kikazi na Julai 5 mwaka huu anatarajiwa kufunga mafunzo katika Chuo cha Polisi Wanamaji Mwanza ambayo yana lengo la kukabiliana na uhalifu unaotokea katika Bahari, Maziwa na Mito hapa nchini.
Pamoja na ufungaji wa mafunzo hayo pia ataendelea na ziara ya kukagua utendaji wa Polisi katika baadhi ya mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa lengo la kuhakikisha uhalifu unapungua  hapa nchini ikiwemo ajali za barabarani, Maujai ya kishirikina na uhalifu katika Visiwa vilivyopo Ziwa Viktoria.


Katika ziara hiyo ya kikazi atakagua utendaji wa Polisi katika baadhi ya mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa lengo la kuhakikisha uhalifu unapungua  hapa nchini ikiwemo ajali za barabarani.
Baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Mwanza IGP Sirro amepokelewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi na kufanya kikao na Maofisa waliopo katika Mkoa huo nakuwataka kuwajibika ipasavyo kuzuia ajali za barabarani kama ilivyo kwa makosa mengine.
“Nimekuja kukagua utendaji wenu ili kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabili ili kufikia malengo tuliyojiwekea ya kuhakikisha uhalifu unapungua hapa nchini, hivyo ni imani yangu kila mmoja atawajibika kwa nafasi yake na kuwasimamia waliopo chini yake ipasavyo” Alisema IGP Sirro
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Naibu Kamishna wa Polisi DCP Ahmed Msangi amesema hali ya usalama katika mkoa huo ni shwari na suala la usalama barabarani linaendelea kusimamiwa kikamilifu kwa kushirikiana na Mamlaka nyingine zinazohusika.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akiwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza kwa ajili ya ziara ya kikazi  kwenye baadhi ya mikoa ya Kanda ya Ziwa
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akiwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Ahmed Msangi (Kulia) na Afisa Mnadhimu wa Mkoa huo Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Advera Bulimba (Kulia) baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza kwa ajili ya ziara ya kikazi kwenye baadhi ya mikoa ya Kanda ya Ziwa.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akipokea Salam ya heshima baada ya kuwasili Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa Mwanza kwa ziara ya kikazi katika baadhi ya mikao ya Kanda ya Ziwa.Kushoto ni Kamanda wa mkoa huo, Naibu Kamishna wa Polisi DCP Ahmed Msangi
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akimfariji Bi Lily Matola ambaye ni Afisa Mnadhimu Mstaafu wa Polisi mkoani Mwanza baada ya kufiwa na Mume wake Marehemu Edmund Matola. IGP Sirro yupo ziara ya kikazi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa kuangalia utendaji wa Polisi hususani katika kupunguza ajali za barabarani nchini.
Habari na Picha na Jeshi la Polisi

UTAFITI TWAWEZA: POLEPOLE AMKINGIA KIFUA RAIS DK MAGUFULI

BREAKING NEWS: WATU WATANO WAFARIKI DUNIA KATIKA AJALI USIKU HUU JIJINI MBEYA

$
0
0
Na Emmanuel Madafa, 
Globu ya Jamii, Mbeya

Watu watano wanadaiwa kufariki dunia usiku katika ajali iliyohusisha lori pamoja na gari  dogo aina ya Noah eneo la mteremko wa mlima Igawilo nje kidogo ya jiji la Mbeya.
Mwandishi wa Globu ya Jamii ambaye yuko eneo la tukio hivi sasa ameambiwa na mashuhuda wa tukio hilo kwamba huenda chanzo cha ajali hiyo ni lori ambalo liliferi breki na kuzigonga gari nyingine tatu zikiwemo za TANESCO na kampuni ya CocaCola pamoja na hiyo Noah ambayo ilikuwa na abiria watatu ambao wawili inahofiwa wamefariki papo hapo na mmoja amekimbizwa hospitali rufaa ya Mbeya kupatiwa matibabu. 
Dereva wa lori  na msaidizi  wake wanahofiwa kwamba  wamefariki dunia papo hapo na juhudi za kuondoa maiti zao zimekuwa zikiendelea wakati wa kutuma taarifa hii.
Ajali hii imekuja masaa machache tu baada ya waziri mpya wa Mambo ya Ndani Mhe. Kangi Lugola kumaliza ziara yake mkoani Mbeya ambapo pamoja na mambo mengine amevunja kamati na mabaraza ya  usalama barabarani nchi nzima kwa nia ya kujipanga upya katika kupambana na janga hilo sugu la Taifa.


KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA


MAGAZETI YA LEO IJUMAA JULAI 6, 2018

POLISI MBEYA WANAPAMBANA KUINASUA MIILI YA WATU WAWILI ILIYONG'ANG'ANIA KATIKA GARI

$
0
0
*Ni katika ajali iliyoua watu watano, kujeruhi mmoja jana usiku
 

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Mbeya amethibitisha kufariki dunia kwa watu watano baada ya kutokea ajali ya kugongana  magari matatu jana usiku na kinachoendelea asubuhi ya leo ni kuiondoa miili ya watu wawili ambayo imeng'ang'ania katika gari.

Ajali hiyo imetokea jana usiku katika eneo la Mlima Igawilo nje kigogo ya Mji wa Mbeya Mjini na kusababisha video vya watu hao. 

Akizungumza na Michuzi Blog kwa njia ya simu asubuhi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya  Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi,Urich Matei amesema katika ajali hiyo wote waliofariki ni wanaume na kwamba watu watatu walifanikiwa ukitoa miili yao eneo la ajali na kuipeleka chumba cha kuhifadhia maiti. 

"Kwa sasa asubuh hii tupo eneo ambao ajali imetokea kwani kuna miili ya watu wawili bado tunahangaika kuitoa katika gari. Imekandamizwa ndani ya gari ndogo aina ya Noah  ambayo ililaliwa na kontena. 

"Hivyo tunaendelea kuitoa miili ya watu hawa.Idadi ya watu waliokufa ni watano na majeruhi mtu mmoja. Chanzo cha ajali imetokana na lori ambalo limebeba kontena kufeli breki na kusababisha gea boksi kukatika na hivyo kupoteza muelekeo,"amesema Kamanda. 

JAFO AWAPONGEZA SIMIYU

$
0
0
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amewapongeza viongozi wa mkoa wa Simiyu na halmashauri zake kwa kusimamia vyema ujenzi wa miradi ya afya mkoani humo. 

Jafo ametoa pongezi hizo wakati akipokea vituo vya afya 38, magari ya wagonjwa matatu, magari ya kuratibu shughuli za afya sita , pamoja na vifaa vilivyofadhiliwa na shirika la Kimataifa la UNFPA wakishirikiana na KOICA. Katika makabidhiano hayo,Waziri Jafo amefurahishwa na usimamizi mzuri wa ujenzi wa miundombinu hiyo kupitia utaratibu wa FORCE ACCOUNT. 

Jafo amempongeza mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka pamoja na wabunge wa mkoa huo kwa kuwashirikisha vyema wananchi ambao wameungana na serikali yao pamoja na wadau katika kufanikisha miradi hiyo ya afya. Katika shughuli hiyo waziri Jafo amesisitiza magari hayo tisa yatumike kwaajili ya sekta ya afya na si vinginevyo. 

Wakati huo huo, Waziri Jafo amefurahishwa na wananchi wa Malya wilayani Kwimba mkoa Mwanza kwa kujenga vizuri sana majengo yao ya kituo cha afya Malya baada ya serikali kuwapatia fedha milioni 400.

Naye mbunge wa Sumve Mhe. Ndasa aliishukuru serikali na ameiomba kuwasaidia mashine ya X-Ray kituoni hapo ili wananchi waondokane na usumbufu wa kwenda hospitali ya wilaya iliyopo Ngudu.Waziri Jafo amemaliza ziara yake ya mikoa miwili ya Simiyu na Mwanza na kuelekea wilayani Bagamoyo kwaajili ya uzinduzi wa jengo la wazazi katika hospitali ya wilaya ya Bagamoyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akisikiliza maelezo kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Baadhi ya vifaa vilivyopo kwenye vituo vya afya vya mkoa huo vilivyozinduliwa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa na Mbunge wa Sumve Richard Ndassa katika uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Kituo cha Afya Malya wilayani Kwimba mkoa Mwanza.

Majengo yaliyojengwa kwa ufadhili wa shirika la UNFPA na KOICA.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akikagua ujenzi unaoendelea katika Kituo cha Afya Malya.

WAZAZI, WALEZI WATAKIWA KUFICHUA WATOTO WENYE ULEMAVU

$
0
0
Na Frankius Cleophace, Serengeti

KATA ya Manchira wilayani Serengeti mkoani Mara wameendelea kuwabaini watoto wenye ulemavu wa aina yeyote ili wapelekwe shule kwa lengo la kupata haki zao kama watoto wengine.

Hivyo wazazi na walezi wilayani humo wametakiwa kuendelea kufichua watoto wenye ulemabu ili nao wapate haki ya kupata elimu.

Hayo yamebainishwa na Ofisa Elimu Kata ya Machira  Fidel Sylivanus wakati wa tamasha lililoandaliwa na Shirika la RIGHT TO PLAY kwa lengo ni  kutoa elimu kwa jamii ili kuondokana na mila zenye madhara  ukiwemo ukeketaji kwa mtoto wa kike.Sylivanus amesema katika kata nzima tayari wamezunguka  na kubaini watoto wenye ulemavu wa aina yeyote na kuwataka wazazi na walezi kufichua watoto hao.
 
Pia amewahamiza wazazi na walezi suala la elimu kwa watoto wote bila ubaguzi wa jinsia ni muhimu huku watoto wakitaja changamoto kubwa kuwa ni wazazi kuwapatia kazi nyingi na kushindwa kufanya michezo  na kujisomea.Leah Kimaro kutoka Shirika la RIGHT TO PLAY  amesema  takribani Siku Nne amabazo shirika hilo limefanya matamasha wamefikia wananchi takribani 5000Elfu na kuweza kuwapatia ujumbe uliokusudiwa kupitia michezo mbalimbali.

 Amesema michezo hiyo iliambatana na maombi, Ngonjera, Maigizo, Mpira wa miguu kwa watoto wakike, kukimbiza kuku na kukimbia ndani ya magumia na kwamba lengo ni kukusanya jamii ili kupatiwa elimu hiyo.Aidha wananchi wamekuwa na maoni tofauti kuhusu matamasha hayo ambao yameandaliwa na Shirika la RIGHT TO PLAY kwa siku nne na kutoa elimu ilikusudiwa katika jamii wilayani Serengeti mkoani Mara.

Ambapo wameomba kuwa matamasha hayo yawe endelevu katika maeneo ya vijijini ili kuendelea kutoa elimu Katika wilaya hiyo. 
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Miseke na Wananchi wakata ya Manchira Wilayani Serengeti Mkoani Mara wakiwa katika Maandamano na Mabango yenye ujumbe mbalimbali wa kupiga Vita Ukatili kwa watoto kwenye Tamasha la Michezo lililoandaliwa na Shirika la RIGHT TO PLAY lililopo Serengeti Mkoani Mara.
Afisa Elimu kata ya Manchira Fidelis Sylivanus akisalimiana na Timu ya Mpira wa Miguu Miseke Wakubwa FC na Miseke Wadogo FC.
Afisa Elimu kata ya Manchira Fidelis Sylivanus akisalimiana na Timu ya Mpira wa Miguu wa Wasichana baina ya Timu Miseke FC na Bwitenge FC katika Viwanja vya Shule ya Msingi Miseke.
Mgeni rasmi ambaye ni Afisa Elimu Kata ya Manchira Fidels Syilivanusi akikabidhi zawadi mbalimbali kwa Washiriki wa Michezo hiyo.

HATIFUNGANI YA SH.BILIONI 120 YA TMRC YAORODHESHWA DSE

$
0
0
*CMSA yahimiza kampuni kuingia katika DSE 

NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Ashatu Kijaji amesema kuwa katika kuhakikisha mikopo ya nyumba inaanzishwa nchini, Serikali ikishirikiana na Benki ya Dunia ilianzisha mradi wa kuwezesha kuwepo kwa mfumo wa mikopo ya nyumba.

Dk.Kijaji ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam kwenye hafla ya kuorodhesha hatifungani yenye thamani ya Sh.bilioni 120 za Kampuni ya Mikopo ya Nyumba (TMRC) katika Soko la Hisa Dar es Salaam(DSE).

Amefafanua kuhusu mfumo wa mikopo ya nyumba amesema kuwa mradi huo uitwao mikopo ya nyummba ulilega kuanzisha mifumo wa mikopo ya nyumba kutokana na kufilisika kwa Benki ya Nyumba Tanzania mwaka 1995 ambayo ilikuwa inatoa mikopo ya muda mrefu kwa wateja kwa ajili ya ujenzi wa ununuzi wa nyumba za makazi.

“Mradi huu ulikuwa na maeneo makuu matatu ambayo ni uanzishwaji wa mfumo wa mikopo ya nyumba, uanzishwaji wa mfuko wa mikopo midogo midogo ya nyumba na kuendeleza mfumo wa ujenzi wa nyumba wa gharama nafuu kwa lengo la kupunguzia wananchi gharama za ujenzi na kuwa na nyumba za gharama nafuu,”amesema.

Amefafanua ili kutekeleza malengo hayo matatu Serikali ilikopa jumla ya Dola za Marekani milioni 100 mwaka 2010 kutoka benki ya dunia ili kuwezesha mradi wa mikopo ya nyumba kufikia malengo.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Ashatu Kijaji (katikati) akibonyeza kengele leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuorodhesha hatifungan za Kampuni ya Mikopo ya Nyumba(TMRC) yenye thamani ya Sh.bilioni 120 kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam(DSE).Kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya DSE Jonathan Njau na kushoto ni Ofisa Mtendaji wa Soko la Mitaji na Dhamana Nicodemas Mkama.
 .Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Ashatu Kijaji (katikati) akifafanua jambo wakati  hafla ya kuorodhesha hatifungan za Kampuni ya Mikopo ya Nyumba(TMRC) yenye thamani ya Sh.bilioni 120 kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam(DSE).Kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya DSE Jonathan Njau.

http://michuzijr.blogspot.com/2018/07/hatifungani-ya-shbilioni-120-ya-tmrc.html
 

TASWIRA YA NIC MAONYESHO YA SABASABA YANAYOENDELEA

$
0
0
Majadiliano: Viongozi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) wakijadili jambo wakati wa maonyesho ya 42 ya sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa, kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Habari cha NIC Mwanaidi Shemweta, Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Sam Kamanga,Elisante Maleko ambaye ni Mkurugenzi wa Masoko kulia anayezungumza ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NIC Thomas Msongole 
Vigogo wa NIC katika majadiliano:Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Sam Kamanga, Kaimu Mkurugenzi wa Masoko wa NIC Elisante Maleko, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NIC Thomas Msongale na Mkurugenzi wa Bima ya Mali,Aajali na Shehena Romanus Hokororo,ni wakati wa maonyesho ya 42 ya sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa. 
Picha ya pamoja ya viongozi wa NIC na wafanyakazi baada ya kunyakua ushindi katika sekta ya Bima na ushindi wa pili katika maonyesho hayo miongoni mwa washiriki wote. 

WAZIRI KANGI LUGOLA AWASHUSHA VYEO MAKAMANDA WAWILI

$
0
0
*Ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Mbeya na Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto Kagera


Na Said Mwishehe

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola ametangaza kuwashusha vyeo Makanda wa wawili kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao yakiwamo ya kushindwa kudhibiti ajali. 

Lugola ametangaza uamuzi huo leo jijini Dar es Salaam akiwa katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na kwamba hatua hizo ni kuonesha hayupo tayari kuacha makamanda na wakuu wengine wa Idara wafanya kazi kimazoea. 

Hivyo amemshusha cheo Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Mbeya pamoja na Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto Mkoa wa Kagera na wote hao umetokana na kushindwa kutekeleza majukumu yao hasa ya ajali.

Lugola amesema Kamanda wa Usalama Barabarani Mkoa wa Mbeya Leopard Funguo ambaye ni Mrakibu wa Polisi amemchukulia hatua kwa kumshusha cheo chake mara moja kutoka urakibu abaki na nyota tatu. 

Amesema sababu za kumshusha cheo hicho kunatokana na kushindwa kuchukua hatua za kudhibiti ajali za barabarani.Pia amesema juzi mkoani Kagera kulitokea ajali ya moto katika Chuo cha Ufundi Lake Zone 

Mrakibu Mwandamizi George Mrutu ambaye ni Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto katika Mkoa huo alipewa taarifa na uongozi wa chuo hicho ya kutokea kwa ajali ya moto. Lugola amesema kwa mujibu wa picha alizonazo na vyombo vya habari Mrutu anakiri kwa kinywa chake kuwa a hakwenda katika tukio kwa sababu hana gari ya zima Moto. 

Amefafanua wakati huo huo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Polisi Mkoa wa Kagera pamoja maofisa wengine wakionekana wakishirikiana na wananchi kuzima moto huo bila ya kuwa na gari la zima moto. 

"Kutokana na tukio hilo nimejiuliza imekuaje ambao hawajapewa dhamana ya kisheria ya kuzimaa moto wanakwenda pale kuzima moto na wenye dhamana ya kisheria wakashindwa kushiriki kuzima moto huo,"amesema Lugola. Amefafanua zipo kazi ambazo kikosi cha Zimamoto na Uokaoji kuna mambo wanaweza kufanya bila hata kuwa na gari ya zima moto ikiwemo ya kutoa maelekezo ya kuwaepusha wananchi ya kukaa mbali na eneo la tukio la ajali. 

Kabla ya kutangaza kumshusha cheo Lugola amempongeza Mkuu wa Kikosi cha Zima Moto na Uokoaji nchini kwa kumuondoa kamanda wa Kikosi hicho Mkoa wa Kagera. Hata hivyo amesema kumuondoa katika nafasi hiyo peke yake haotoshi, hivyo akatangaza naye ashushwe cheo kimoja abaki na nyota tatu. 

Amesema alikuwa ameamua wafukuzwe kazi wote na bahati yao yeye amezaliwa Ijumaa hivyo ameamua washushwe cheo tu badala ya kuwatimua.Pia amesema anatuma salamu kwa wakuu wa Polisi kutambua zama hizi si za mwaka 47 na kwamba chini ya utawala wa Rais John Magufuli hawatakuwa tayari kuvumilia mambo yaende bila utaratibu. 

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YATEMBELEA OFISI ZA MAMLAKA YA HALI YA HEWA NCHINI

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA), Dkt. Agnes Kijazi (kulia), akifafanua jambo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, wakati Kamati hiyo ilipokuwa kwenye ziara ya kujifunza namna mamlaka hiyo ivyofanya kazi. Katikati ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Seleman Kakoso na wa kwanza kulia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA), Dkt. Agnes Kijazi akiteta jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Seleman Kakoso, wakati kamati hiyo ilipotembelea mamlaka hiyo kukagua namna inavyofanya kazi, jijini Dar es Salaam.

 Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu Sekta ya Uchukuzi, Aunyisa Meena (kushoto), kuhusu namna walivyojipanga kuimarisha miundombinu ya miradi ya hali ya hewa kwa mwaka mpya wa fedha 2018/2019, wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miudombinu ilipotembelea Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA), jijini Dar es Salaam.

 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Seleman Kakoso, akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA), Dkt. Agnes Kijazi (katikati) na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo Dkt. Buruhani Nyenzi (kushoto), wakati kamati hiyo ilipotembelea mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.

WAKULIMA WAN UFUTA KIBITI WAZIDI KUNEEMEKA KWA BEI YA MNADA

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Wakulima wa Wilaya ya Kibiti wazidi kuneemeka na bei ya ufuta! katika mnada wa nne (4) kwa msimu huu ambapo bei ya ufuta kwa kilo imepanda kufikia sh. 3,300 kutoka sh. 3,100 ya mnada uliopita wa tarehe 19 Julai na huku bei ya chini ikiwa sh. 3,110.

Wakati huo huo ufuta ghalani umepanda kufikia tani 582.5 kutoka tani 454.8 za mnada uliopita.

Kwa ujumla wananchi wa Kibiti wameendelea kuishukuru serikali kwa kufanya maamuzi ya kuwakomboa kwa mfumo wa stakabadhi ghalani ambao kwa mara ya kwanza ufuta umekuwa wa manufaa makubwa kwa mkulima. Akifungua mnada huo, Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Mh.

Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Gulamhussein Kifu alisema hatamvumilia yeyote atakayejaribu kuuharibu ama kuuvuruga mfumo unaoendelea wa mauzo ya ufuta kwa stakabadhi ghalani ikiwa ndiyo maagizo ya serikali.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo bibi Alvera Ndabagoye alipongeza hatua iliyofikiwa na ushirikiano mzuri uliopo pande zote ambao umekuwa wa manufaa si tu kwa mkulima bali hata kwa wafanyabiashara wenyewe na serikali kwa ujumla.
Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Mh. Gulamhussein Kifu akihutubia katika mnada huo uliofanyika katika ofisi ya Mkuu wa wilaya .
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kibiti Milongo Sanga akizungumza katika mnada huo uliofanyika katika ofisi ya Mkuu wa wilaya .
Mkurugenzi wa Mtendaji wa Kibiti Alvera Ndabagoye akizungumza katika mnada huo
Watunza funguo Afisa Ushirika wa Wilaya na Mwenyekiti wa AMCOS ya Kibiti wakifungua sanduku la tenda.
baadhi ya wafanyabiashara, wakulima na watumishi waliohudhuria mnada huo.

Dk.shein Asafiri Safari Maalum Nchini Uingereza

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akiagana na Viongozi Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi Zanzibar katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume akiondoka nchini kuelekea Uingereza kwa safari maalum ya wiki tatu
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akiagana na Wazee wa Chama cha Mapinduzi CCM Zanzibar katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume akiondoka nchini kuelekea Uingereza kwa safari maalum ya wiki tatu
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein (kushoto) alipokuwa akiagana na Wazee wa Chama cha Mapinduzi CCM Zanzibar katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume akiondoka nchini akiungana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kuelekea Uingereza kwa safari maalum ya wiki tatu
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akiagana na katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume akiondoka nchini kuelekea Uingereza kwa safari maalum ya wiki tatu
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe.Ayoub Mohamed Mahmoud katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume akiondoka nchini kuelekea Uingereza kwa safari maalum ya wiki tatu
VIONGOZI mbali mbali wakimpungia mkono wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume akiondoka nchini kuelekea Uingereza kwa safari maalum ya wiki tatu,[Picha na Ikulu

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI KANGI LUGOLA AMTIMUA KAMISHANA WA MAGEREZA KWENYE MKUTANO WAKE

$
0
0
*Ni baada ya kuchelewa katika mkutano wake na waandishi wa habari
*Pia awataka makamishina na wakuu wa Idara kumuonesha Ilani ya CCM


Na Said Mwishehe,Glubu ya jamii 

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola ameamua kumtimua katika  kikao chake Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini Kamishina Jenerali Dk.Juma Malewa kwasababu za kuchelewa kuingia mkutanoni. 

Kabla ya kumtoa nje leo katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lugola alisema baada ya mkutano wake kuanza ni marufuku mtu yeyote kuingia ndani isipokuwa waandishi wa habari tu  ndio watakaoruhusiwa. 

Hivyo Dk. Malewa aliingia ukumbini saa tano na dakika tatu ambapo Waziri Lugola  akamtaka atoke nje mara moja. Pamoja na Dk.Malewa kuomba msamaha kwa Waziri iliyoambatana na saluti alimkatalia na kumuamuru atoke nje ya ukumbi na hataki yeyote ambaye yupo chini yake na hajafika ni marufuku kuingia ndani. 

Wakati huo huo kabla ya kuanza kikao hicho alitoa maagizo kwa Makamishina waliopo kwenye mkutano huo aliwataka kueleza milango yao inayoendana na Ilani ya CCM. "Nawaomba kila mmoja aoneshe Ilani ya CCM na ambaye hana anyooshe mkono juu na nitajua kama anayo au laa,"amesema Lugola. 

Hata hivyo hakuna aliyekuwa nayo na hivyo akatangaza hata mkutano ambao alitaka kuufanya kati yake na Makamishina na Wakuu wengine wa Idara alisema ameuahirisha na kila mmoja akachukue Ilani yake ndio wafanye kikao.

MICHUZI TV: TRA MKOA WA MBEYA YATHIBITISHA KUONDOKEWA NA MTUMISHI WAO

Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images