Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110021 articles
Browse latest View live

MKUU WA MAJESHI YA ULINZI JENERALI VENANCE MABEYO ATEMBELEA BANDA LA NSSF KATIKA MAONESHO YA SABNASABA

$
0
0
 Mkuu wa Majeshi  ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo akizungumza  alipotembelea banda la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF  na kuwapongeza NSSF kwa ushindi wa Jumla alipotembelea Banda la NSSF katika maonyesho ya Sabasaba , pembeni ni baadhi ya wafanyakazi wa NSSF. Picha na Mwandishi wetu. Picha na Mwandishi wetu
 Mkuu wa Majeshi  ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo akipata maelezo mbalimbali kuhusu huduma za Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kutoka kwa Kaimu meneja wa Uhusiano na Masoko Ndugu Salim Khalfan alipotembelea Banda la NSSF katika maonyesho ya Sabasaba .Picha na Mwandishi wetu
 Afisa Uhusiano wa NSSF Bi. Angella Msangi akimkabidhi zawadi za vitabu na vipeperushi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo alipotembelea banda  la NSSF katika maonyesho yanayoendelea ya sabasaba. Picha na Mwandishi wetu
Mkuu wa Majeshi  ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo akifurahia jambo na Kaimu Meneja uhusiano na Masoko wa NSSF Ndugu Salim Khalfan alipotembelea banda  la NSSF katika maonyesho yanayoendelea ya sabasaba. Picha na Mwandishi wetu. Picha na Mwandishi wetu

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YANYAKUA TUZO MBILI KWENYE MAONESHO YA SABASABA

$
0
0
  Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Utalii, Jaji Mstaafu, Thomas Mihayo ( wa tano kulia) akiwa pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Deograsius Mdamu (  wa sita kushoto)  wakiwa na Baadhi ya Waoneshaji wakifurahia ushindi wa Tuzo katika banda la Wizara ya Maliasili na Utalii. Tuzo hizo ni mshindi wa kwanza katika kipengele maalum cha Best Export Products Exhibitors na Mshindi wa pili katika kipengele cha Trade in Services  katika Maonesho hayo. Tuzo hizo zilikabidhiwa jana na Waziri Mkuu wa Jahuri ya Muungano wa Tanzania. Majaliwa Kassim Majaliwa katika viwanja vya Sabasaba. ( Picha na Lusungu Helela-MNRT)
 Muonekano mpya wa Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii sehemu ya mapokezi katika Maonesho ya 42 ya  Biashara ya Kimtaifa ya Dar es Salaam .Banda la Wizara limekuwa miongoni mwa mabanda yenye mvuto wa kipekee kutokana na utofauti wake  wa uwepo wa wanyamapori hai kama vile Simba, Chui , Chatu, Nyati, ndege wa aina mbalimbali na wale watakaopenda kuona wanyamapori hao kiingilio ni shilingi 1,000 kwa watu wazima na    500 kwa watoto wadogo. ( Picha na Lusungu Helela-MNRT)
  Baadhi ya Waoneshaji wakifurahi ushindi wa Tuzo walizokabidhiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Majaliwa Kassimu Majaliwa  katika banda la Wizara ya Maliasili na Utalii.

BENKI YA CRDB YAVUTIA WENGI MAONYESHO YA SABASABA 2018

$
0
0
Wananchi waliofika katika Maonyesho ya Sabasaba wakipata huduma za kutoa pesa na kuweka katika Mobile Branch.
Wananchi wakipata huduma za kifedha katika banda la Benki ya CRDB katika Maonyesho ya Sabasaba.
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Lumumba, Pendo Assey (kushoto), akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya CRDB, Jessica Nyachiro, alipotembelea Maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa 'Sabasaba'.

Wateja wa Benki ya CRDB wakijaza fomu kwa ajili ya kupata huduma.

Baadhi ya wateja waliofika katika banda la Benki ya CRDB katika Maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa 'Sabasaba' wakipata huduma za kutoa na kuweka fedha kwa wakala wa benki hiyo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Article 1

Trend Solar kuwafikia wananchi washio kijijini

$
0
0
Kampuni ya Trend Solar leo imezindua programu ya kisasa ya umeme ambayo itasaidia jamii kubwa ya waafrika waishio vijijini. Trend Solar ilianza huduma yake mwaka 2017, chini ya waasisi wake Irfan Mirza na Matt Tam ambao hubuni, kusambaza na pia hufadhili miradi ya umeme wa jua ambayo inalenga kuwafikia wakazi wenye kipato cha chini na maeneo ambayo umeme wa gridi haujafika.

Katika kipindi cha majaribio Trend Solar wameweza kuuza zaidi ya seti 500 kutoka kwenye maduka yao Dar es Salaam, Geita na Bagamoyo, na sasa kampuni hiyo itaongeza vifaa zaaidi Afrika Mashariki nzima ili kulifikia soko la umeme wa jua linalokadiriwa kufikia thamani ya dola za kimarekani Bilioni 3.1 barani Afrika.

Akizungumza katika uzinduzi, mwanzilishi na Mkurugenzi wa Trend Solar Bw. Irfan Mirza alisema “Kupitia Trend Solar tunawaondolea watu wetu tatizo la kusahaulika kwenye maendeleo ya kidigitali kwa kuwapatia simu ya gharama nafuu + intaneti ya bure + na vifaa vya kuchajia nyumbani. Tunaboresha zaidi biashara ya upatikanaji wa umeme mbadala na intaneti kwa kuwa kampuni ya kwanza duniani kuunganisha Simu na mfumo wa solar za majumbani (SHS).

“Katika kipindi cha majaribio tumepokea mrejesho mzuri zaidi ya tulivyotegemea na hasa baada ya kuongeza Simu janja yetu ambayo imekuwa msaada mkubwa kwa watumiaji, ambao hawakuwa na njia ya kupata intaneti hapo awali. Sasa tuko katika nafasi nzuri ya kuwafikia watu milioni 36 ambao hawapati umeme wa gridi nchini Tanzania na kuwapa fursa zaidi kunufaika na maendeleo ya kidigitali”. Aliongeza Bw. Irfan.
Balozi wa Uingereza nchini Sarah Cooke akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa wakati wa  uzinduzi wa programu ya kisasa ya umeme ambayo itasaidia jamii kubwa ya waafrika waishio vijijini wakati wa kuingia mkataba wa Maudhui na Kampuni ya StarTimes.

Balozi wa Uingereza nchini Sarah Cooke(wa pili kulia) akizindua programu ya kisasa ya umeme wa nguvu ya Jua ambapo kampuni ya Trend Solar wameingia mkataba wa Maudhui na Kampuni ya StarTimes ambao ndio mtoa huduma wa matangazo ya kidigitali mwenye watumiaji wengi zaidi barani Afrika ikiwa na watumiaji zaidi ya Milioni 10.
Mkurugenzi wa Masoko wa Startimes, Li Kun(kushoto) akimkabidhi mpira Balozi wa Uingereza nchini Sarah Cooke mara baaada ya kuzindua  programu ya kisasa ya umeme ambayo itasaidia jamii kubwa ya waafrika waishio vijijini kati ya Trend Solar na Startimes Tanzania.
Picha ya pamoja

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu yatembelea TAA kuona utendaji wake

$
0
0
 Kaimu Mkurugenzi  mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania, Richard Mayongela akimpokea mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Suleimani Kakoso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mpanda Vijijini.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Suleimani Kakoso akisalimiana na watendaji waandamizi wa Mamlaka wa Viwanja vya ndege Tanzania mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Watu Mashuhuri.
 Kaimu Mkurugenzi  mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania, Richard Mayongela  akiwasilisha taarifa ya Utendaji ya Mamlaka mara baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu uuwasili.
 Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakifuatilia taarifa ya utendaji ya Mamlaka ya Viwanja yya Ndege iliyokuwa ikiwasilishwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Richard Mayongela.
 Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha JNIA, Paul Rwegasha akitoa historia ya Jengo la kwanza la abiria wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu.
Moja ya gari jipya lililowasili kati ya sita ambayo Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania imeyanunua na kuyakabidhi kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ili kuweza kusaidia katika dharura za moto zinazoweza kutokea Kiwanjani.

Vodacom Tanzania yakabidhi zawadi kwa mshindi wa Sh. 290 M za Tusua Mapene

$
0
0
 Mshindi mkuu wa awamu ya kwanza ya promosheni ya Tusua mapene, Jackson A. Mwankemwa (51) ambaye ni mkazi wa  kijiji cha Msasani, Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, akikabidhiwa mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi  290,409,580 na mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC, Jacquiline Materu (kulia) wakati wa  hafla iliyofanyika makao makuu ya Vodacom jijini Dar es Salaam jana, katikati ni  afisa kitengo cha Kidijitali na Huduma za ziada  wa kampuni hiyo Furaha Limu.
 Mshindi mkuu wa awamu ya kwanza ya promosheni ya Tusua mapene, Jackson A. Mwankemwa (51)  ambaye ni mkazi wa  kijiji cha Msasani, Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, akikabidhiwa mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi  290,409,580 na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC, Jacquiline Materu (kulia)  huku akishuhudiwa na familia yake (wa pili kutoka kulia) ni dada yake Rose Mwankemwa, Togile Sampegete na mtoto wake wa mwisho Erick Jackson wakati wa hafla iliyofanyika makao makuu ya Vodacom Tanzania Plc jijini Dar es Salaam. Kushoto ni  Afisa  wa kitengo cha Kidijitali na Huduma za ziada  wa kampuni hiyo, Furaha Limu.
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC, Jacquiline Materu (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, mara baada ya kumkabidhi  mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi 290,409,580 mshindi mkuu wa promosheni ya Tusua mapene awamu ya kwanza, Jackson A. Mwankemwa (51)  ambaye ni mkazi wa  kijiji cha Msasani, wilayani Rungwe mkoani Mbeya.

Waziri wa Maji atembelea Shirika la Maji DAWASCO

$
0
0
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa (kulia) akipokelewa na mwenyeji wake Mkurugenzi Mkuuwa Shirika la Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASCO), Cyprian Luhemeja wakati Waziri huyo alipotembea shirika hilo mara baada ya kuteuliwa kuwa Waziri wa wizara hiyo.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa (kulia) akizungumza na wafanyakazi wa Shirika la Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASCO) wakati alipotembelea shirika hilo jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASCO) wakimsikiliza Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa (hayupo pichani) wakati waziri huyo alipotembelea shirika hilo jana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuuwa Shirika la Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASCO), Cyprian Luhemeja akitoa taarifa ya shirika hilo kwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa (hayupo pichani) wakati waziri huyo alipotembelea shirika hilo jana jijini Dar es Salaam. Picha na MAELEZO.

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA (TPC) LATOA TAARIFA YA MAFANIKO YAKE YA KIUTENDAJI KWA MWAKA 2017|2018

$
0
0
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Kanali Mstaafu, Dk. Haruni Kondo, akizungumza na waandishi wa habari, wakati alipokuwa akitoa taarifa ya mafanikio ya kiutendaji wa shirika hilo, kwa mwaka 2017\2018, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Kaimu Postamasta Mkuu wa shirika, Hassan Mwang'ombe. 
Baadhi ya viongozi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakiwa katika mkutano huo, wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi, Kanali Mstaafu, Dk. Haruni Kondo, alipokuwa akitoa taarifa ya mafaniko ya kiutendaji wa shirika kwa mwaka 2017/2018, jijini Dar es Salaam leo. 
Baadhi ya viongozi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi, Kanali Mstaafu, Dk. Haruni Kondo, alipokuwa akitoa taarifa hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Kanali Mstaafu, Dk. Haruni Kondo, akizungumza na waandishi wa habari, wakati akitoa taarifa hiyo, ya mafanikio ya kiutendaji wa shirika hilo, kwa mwaka 2017\2018, jijini Dar es Salaam leo.  
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Dk. Haruni Kondo, akijibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari, katika mkutano huo, wa kutoa taarifa ya mafanikio ya kiutendaji wa shirika hilo, kwa mwaka 2017\2018, jijini Dar es Salaam leo. 

Acting U.S. Ambassador welcomes PM Majaliwa to U.S. Embassy booth

$
0
0
Chargé d’Affaires of the U.S. Embassy in Tanzania Dr. Inmi Patterson welcomes Prime Minister Kassim Majaliwa to the U.S. Embassy booth at the Sabasaba trade fair on Wednesday, July 4. The U.S. Embassy is committed to ongoing broad engagement with the Tanzanian people to build a healthier and more prosperous Tanzania. (Photo: Courtesy of the U.S. Embassy).

UKAGUZI WA MAGARI KILIMANJARO WABAINI ,MADEREVA KUTUMIA LESENI ZA NDUGU ZAO

$
0
0
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii KAnda ya Kaskazini. 

UKAGUZI wa Magari ya Abiria pamoja na Leseni unaofanywa na Jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro umebaini udanganyifu mkubwa unaofanywa na baadhi ya Madereva wa Magari ya abiria ukiwemo kuendesha bila leseni, umri wa kuendesha gari kupitiliza huku wengine wakitumia Leseni za Ndugu zao.
Katika kituo Kikuu cha mabasi ya abiria yaendayo mikoani na yale yanayofanya safari zake ndani ya mkoa wa Kilimanjaro, Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Hamisi Issah akiwa ameongozana na Mkuu Operesheni kikosi cha usalama barabarani  Inspekta Peter Mizambwa na maofisa wengine wa Polisi wamefanya ukaguzi wa magari zaidi ya 800  ambapo yaliyobainika kuwa mabovu yalizuiliwa kuendelea na safari huku baadhi ya Madereva wakikutwa na silaha katika magari yao vikiwemo visu.
Kamanda Issah akatoa onyo kwa madereva kutembea na silaha pamoja na kujaza abiria hali inayochangia abiria kukaa katika mikao isiyo rafiki .


Mkuu wa operesheni wa kikosi cha usalama barabarani  Inspekta wa polisi Peter Mizambwa akazungumzia Operesheni Nyakua iliyoanza kwa lengo la kupunguza ajali huku baadhi ya Madereva na wananchi wakipongeza utaratibu huo.
 
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ACP Hamis Issah akimuuliza mmoja wa madereva waliokamatwa juu ya matumizi ya silaha ya Kisu kilichokutwa katika gari lake.


 Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, ACP Hamis Issah akitembelea kikuu cha Mabasi mjinib Moshi kwa ajili ya ukaguzi wa Magari ya Abiria. 
 Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,ACP.Hamis Issah akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Operesheni wa kikosi cha Usalama Barabarani Mkaguzi Peter Mizambwa wakati wa ukaguzi huo uliofanyika katika kituo kikuu cha Mabasi mjini Moshi. 
 Mkuu wa Operesheni wa Kikosi cha Usalama barabarani mkoa wa Kilimanjaro Inspekta  Peter Mizambwa akimuonesha kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ACP Hamis Issah moja ya karatasi ambazo zinatumiwa na madereva kama Leseni.

Tume ya Uchaguzi yamuaga aliyekuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi

$
0
0
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage (kulia) akimkabidhi ua aliyekuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani ikiwa ni ishara ya kumuaga na kumtakia kila la kheri katika kutekeleza majukumu ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage (katikati) akizungumza kwenye kikao cha kumuaga aliyekuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani  ambaye kwa sasa ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.Kushoto ni Mkurugenzi mpya wa Uchaguzi Dkt. Athumani Kihamia.
 Aliyekuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani  ambaye kwa sasa ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi akizungumza kwenye kikao cha Tume cha kumuaga.Katikati  ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage na  Mkurugenzi mpya wa Uchaguzi Dkt. Athumani Kihamia.
Mkurugenzi wa Habari na Elimu ya Mpiga Kura Giveness Aswile akitoa neno la kumuaga aliyekuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani  kwa niaba ya wakuu wa Idara  za Tume wenzake.Kilia ni Mkuu wa Idara ya Uendeshaji Uchaguzi Irene Kadushi.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage (kulia) akimpa mkono wa kumuaga aliyekuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani ambaye kwa sasa ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.Kushoto ni Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt. Athumani Kihamia.
Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt. Athumani Kihamia akimpa mkono wa kumuaga Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Kailima Ramadhani .Katikati ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage. Picha na Hussein Makame-NEC

NAIBU WAZIRI MABULA ASHUHUDIA MAENDELEO MAKUBWA SEKTA YA NYUMBA ZANZIBAR

$
0
0
Na Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angeline Mabulla amefanya ziara katika kisiwa cha Zanzibar na kujionea Ujenzi wa mji wa kisasa wa nyumba za kimaendeleo katika eneo la Fumba wakati wa kukabidhi nyumba 60 kwa wanunuzi wa awali.

Ujenzi wa miji huu wa kisasa wa nyumba za kimaendeleo ni mafanikio makubwa ya ujenzi wa nyumba zilizo bora, zinazozingatia mahitaji muhimu ya familia pamoja na kuzijenga kwa mpangilio maalum.

Mradi wa nyumba za Fumba ni mojawapo wa miradi mikubwa iliyoidhinishwa ambao utakuwa na nyumba 1,400 ambazo zinajengwa katika mfumo wa nyumba za chini na nyumba za ghorofa moja hadi sita ambazo utekelezaji wake utakuwa katika awamu 4, na bei ya kuanzia kwa nyumba itakuwa shilingi milioni 37 tu.

Akiongeza wakati wa ziara hiyo Mhe. Mabulla amewashauri wasimamizi wa mradi huo wa Mji wa Fumba unaotekelezwa na Kampuni ya CPS Live Company Ltd kutenga maeneo ya umma ambayo yatatumiwa na wakazi wa mji huo kwa ajili ya kupumzikia, viwanja vya michezo na maeneo ya maegesho ya magari na fukwe kwa ajili ya kupunga upepo hasa ikizingatiwa Zanzibar ina mazingira mazuri ya fukwe.

Katika ziara hii Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa Angeline Mabulla aliongozwa na Naibu Waziri wa ardhi, Maji, Nishati na Mazingira kwa upande wa Zanzibar Mheshimiwa Khamis Juma Maalim ambaye amemueleza kwamba kwa sasa Zanzibar imechukua juhudi za makusudi katika kuhakikisha suala la makaazi linaimarika kwa kasi na kuweza kukuza uchumi kama ilivyoimarika kwa nchi nyingi duniani na kueleza kuwa miji mengine 14 midogo itajengwa hapa Zanzibar.
 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa Angeline Mabulla (kushoto) akikaribishwa na Naibu Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira kwa upande wa Zanzibar Mheshimiwa Khamis Juma Maalim katika ofisi za Wizara hiyo, Unguja kisiwani Zanzibar.
 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa Angeline Mabulla (Kulia) akiongozwa na Naibu Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira kwa upande wa Zanzibar Mheshimiwa Khamis Juma Maalim wakati wa ukaguzi wa Ujenzi wa mji wa kisasa wa nyumba za kimaendeleo katika eneo la Fumba, Unguja kisiwani Zanzibar.
 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa Angeline Mabulla akiwa ameketi ndani ya moja ya nyumba za kisasa zinanzojengwa katika katika eneo la Fumba, Unguja kisiwani Zanzibar.
 Meneja Masoko wa Mradi wa ujenzi wa Mji wa maendeleo wa Fumba Bibi Fatma Musa (T-Shirt Nyekundu), akimuonesha baadhi ya nyumba zilizo kamilika ujenzi wake Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa Angeline Mabulla.
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya CPS-Lives LTD Sebastian Dietzold (mwenye suti nyeusi) akimuonesha ukubwa eneo la mradi wa nyumba zinazojengwa na kampuni hiyo Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa Angeline Mabulla.(picha Na. Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

HUYU NDIYE CHIFU WA KABILA LA WASAFWA MBEYA, CHIFU ROCKET MWASHINGA

Dakika nne za vivutio vya Utalii Mkoani Mbeya: Daraja la Mungu, Ziwa Ngozi na Kimondo.


WASHINDI WA KWANZA WA SHINDANO LA ‘TUSUA MAISHA NA GLOBAL’ WAZAWADIWA

$
0
0
WASHINDI wa kwanza wa Shindano la Tusua Maisha na Global, wamekabidhiwa zawadi zao leo katika ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza-Mori jijini Dar es Salaam.Washindi waliokabidhiwa zawadi ni Richard Tanganyika aliyejishindia pikipiki, Shaaban Kamoye aliyejishindia dinner set, Nasoro Juma aliyejishindia headphones za kisasa za Beats by Dre na Novart Magere aliyejishindia jezi, akiwa amewakilishwa na ndugu yake, Hassan Mathias.
“Najisikia furaha sana kuibuka mshindi wa pikipiki, naamini itanisaidia sana kwenye biashara yangu ya genge na mgahawa kwani mimi ni mfanyabiashara; nawasihi watu wengine pia washiriki kwenye hili shindano kwa sababu ni kweli zawadi zinatolewa bila upendeleo,” alisema Tanganyika baada ya kukabidhiwa zawadi yake ya pikipiki.

Naye Shaaban Kamoye aliyejishindia dinner set, amesema zawadi hiyo ataenda kumpa mama yake kwani yeye ndiye aliyenunua Gazeti la Amani lakini yeye (Shaaban) akaamua kujaribu bahati yake na kuibuka mshindi.
“Mimi ni mpenzi wa gazeti la Championi lakini mama ndiye aliyenunua gazeti la Amani ambalo kuponi yake ndiyo iliyoleta hii zawadi, namshukuru sana Mungu kwa hii zawadi na nitamkabidhi zawadi mama kwani japokuwa mimi ndiye niliyeshiriki, lakini yeye ndiye aliyenunua gazeti.
Namna ya kushiriki kwenye shindano hilo; nunua gazeti lolote linalochapishwa na Global Publishers, kati ya Uwazi, Amani, Ijumaa, Risasi, Ijumaa Wikienda, Championi na Sport Xtra, fungua ukurasa wa pili ambapo utakutana na kuponi yenye maelekezo ya namna ya kushiriki, jaza kuponi hiyo kisha chukua simu yako, fungua uwanja wa meseji na uitume namba maalum iliyopo kwenye kuponi kwenda namba 0719 386 533.
Ukituma meseji utakuwa umeingia moja kwa moja kwenye shindano na endapo ukibahatika kuibuka mshindi, utapigiwa simu na kupewa maelekezo ya namna ya kushiriki.“Nawasihi wasomaji wetu washiriki kwa wingi kwani kuna zawadi kibao, kila wiki pikipiki moja itakuwa inatolewa na zawadi nyingine kemkem,” alisema Antony Adam, Mkuu wa Idara ya Usambazaji na Masoko ya Global Publishers.
Mhariri wa magazeti ya Global Publishers, Aziz Hashim (katikati) akizungumza na washindi (hawapo pichani) muda mfupi kabla ya kuwakabidhi zawadi leo katika ofisi za Global Group zilizopo Sinza-Mori jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Usambazaji, Keffa Massaga, na kulia ni Meneja wa Masoko wa Global Publishers, Anthony Adam.

John Joseph akimkabidhi jezi Hassan Mathias (kushoto) ambaye ni mwakilishi wa mshindi wa jezi, Novati Magere.
Meneja wa Masoko wa Global Publishers, Anthony Adam (kulia) akimkabidhi zawadi mshindi wa head phones, Nasoro Juma.
Ofisa Usambazaji, Jimmy Haroub (kulia) akimkabidhi mshindi wa Dinner Set, Shaban Kamoge.
Washindi wakiwa katika picha ya pamoja.
Ofisa Usambazaji, Keffa Massaga (kushoto) akimkabidhi funguo mshindi wa pikipiki, Richard Tanganyika.
PICHA: RICHARD BUKOS | GPL

VOA Swahili: Duniani Leo Julai 5, 2018

Uamuzi kama Hakimu anayesikiliza kesi ya viongozi dhidi ya viongozi wa Chadema kujitoa ama la, kujulikana wiki ijayo

$
0
0
Na Karama Kenyynko, blogu ya Jamii

Uamuzi kama hakimu Hakimu Mkazi Mkuu ,Wilbard Mashauri anayeendesha kesi inayowakabili viongozi tisa wa Chadema waliomtaka ajitoe kusikiliza kesi hiyo utatolewa Julai 10, mwaka huu.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu itatoa uamuzi ambao itajulikana kama Hakimu Mashauri atajitoa ama la.

Uamuzi huo ulipaswa kutolewa leo Julai 5, 2018 na Hakimu Mashauri lakini umeahirishwa baada ya wakili wa utetezi Hekima Mwasipu kuieleza mahakama kuwa mawakili wa upande wa utetezi, Jeremiah Mtobesya na Peter Kibatala wanasikiliza kesi nyingine Mahakama Kuu,

 Upande wa mashtaka katika kesi hiyo ya uchochezi unawakilishwa na mawakili wa Serikali, Faraja Nchimbi, Dk Zainabu Mango, Paul Kadushi na Wankyo Simon.

Akijibu hoja ya kutokuwepo mawakili wa utetezi wakili  Nchimbi alieleza kuwa siyo busara  uamuzi huo kutolewa bila ya kuwepo kwa mawakili wa utetezi lakini kwa kuwa wanaamini kesi za Mahakama Kuu husikilizwa asubuhi aliomba uamuzi huo  utolewe nyakati za mchana ili mawakili hao waweze kuwepo. 

Baada ya kusikiliza hoja za upande zote, hakimu Mashauri alikubaliana na Maelezo ya upande wa utetezi na kuiahirisha kesi hadi Julai 10, 2018 ambapo atatoa uamuzi kama atajitoa katika kesi hiyo ama la

Awali, mshtakiwa Freeman Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama hicho na wenzake nane waliieleza mahakama kuwa hawana imani na Hakimu huyo Mashauri anayeiendesha kesi hiyo na kila mmoja akieleza sababu zake na kumtaka ajitoe

Wakili Peter Kibatala awali akiwasilisha hoja Julai 2,2018, alidai kuwa wateja wake wamemueleza kuwa hawana imani naye na kwamba wanaomba ajitoe kusikiliza kesi hiyo.

Washtakiwa katika Kesi hiyo  ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu na Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa kibamba John Mnyika, mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe Halima Mdee na  mbunge wa bunda, Esther Bulaya.

Wengine ni katibu mkuu wa chama hicho, Dk Vicent Mashinji, mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko.

Washtakiwa kwa pamoja wanakabiiwa na mashtaka 13, ambapo katika shtaka la kwanza la kula njama,  kwa pamoja Februari 1 na 16, 2018, Dar es Salaam walikuĺa njama pamoja na wenzao ambao hawapo mahakamani walikula njama ya kutenda kosa la kufanya mkusanyiko usio halali, mkusanyiko wenye ghasia na kukiuka tamko kutawanyika.

Kesi ya Sethi na Rugemalira yazidi kupigwa Kalenda

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa mara nyingine tena, imeipiga kalenda kesi ya Uhujumu uchumi inayomkabili, Mmiliki wa Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL, Habinder Seth na mwenzake James Rugemalira imeahirishwa hadi Julai 19/2018 sababu upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Wakili Serikali Mwandamizi, Mtalemwa Kishenyi  akisaidiana na wakili kutoka Takukuru, Leonard Swai, alidai mahakamani hapo kuwa, kesi hiyo leo imekuja kwa kutajwa na kuiomba mahakama kuahirisha kesi hiyo kwani upelelezi bado haijakamilika.

Alidai kuwa wapo kati hatua za mwisho kukamilisha upelelezi.

Kufuatia maelezo hayo, wakili wa utetezi, Hajra Mungula akisaidia na Dora Malaba, waliutaka upande wa mashtaka kuhakikisha upelelezi unakamilika kwa wakati, ili kesi iweze kuendelea.

Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi, anayesikiliza kesi hiyo, ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 19, 2018.

Sethi na Rugemarila wanakabiliwa na mashtaka  12 ya  uhujumu uchumi  kwa kula njama, kujihusisha mtandao wa uhalifu , kughushi,  kutoa nyaraka za kughushi.

Pia wanadaiwa kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu,  kutakatisha fedha  na kusababisha hasara ya Dola za Marekani 22,198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.

MWANAMUZIKI WA DRC WERRASON NGIAMA MAKANDA ATUA DAR, KUANZA NA ARUSHA KESHO JULAI 06

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
MWANAMUZIKI nguli wa muziki wa dansi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Werrason Ngiama Makanda,  amewasili nchini kwa ajili ya kufanya maonyesho tofauti katika mikoa ya Mwanza, Arusha na Dar es Salaam.
Werrason aliyewasili majira ya saa sita mchana akipokelewa na mamia ya watu pamoja na msanii wa muziki wa dansi nchini King Dodoo na mratibu wa ziara hiyo Lengos VIP.
Akizungumza baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere JKNIA, Werrason amesema kuwa amekuja kukata kiu ya wapenzi wa muziki wa dansi nchini ambao walimkosa katika shoo iliyopita.
Amesema kuwa shoo yake ya mwisho alishindwa kuja ila kwa sasa amekuja kuleta burudani iliyokosekana  baada ya kushindwa kufika.

"Nimekuja kukata burudani ya wapenzi wa soka baada ya kukosekana kwa shoo ya mwisho ila sasa hivi nipo na nimeshafika hapa wajiandae kwa burudani,"amesema Werrason.

Naye  Mratibu wa ziara ya mwanamuziki huyo, King Dodoo Labuche alisema kuwa mwanamuziki huyo amewasili tayari na  ataondoka kesho mapema kuelekea Mkoani Arusha kwa ajili ya shoo ya Kwanza na kisha siku ya Jumamosi atakuwa mkoani Mwanza na ya mwisho atamalizia hapa Dar es Salaam.

"Werrason atafanya Shoo ya kwanza mkoani Arusha siku ya Ijumaa ya Julai 6 na siku ya pili ya Julai 7, atakuwa mkoani Mwanza huku onyesho la mwisho litafanyika Mkoani Dar es Salaam'"amesema King Dodoo.
Alisema mkoani Arusha Mwamuziki huyo atafanya onyesho kwenye ukumbi wa Mjengoni Club, wakati Mwanza atafanya mambo yake kwenye ukumbi wa Rock City na Mkoa wa Dar es Salaam Life Park uliopo Mwenge (zamani Word Cinema)..                                     
 Nguli huyo wa muziki wa dansi amekuja na jumla ya wanamuziki 22 pamoja na madansa wake   ambao wote kwa pamoja watatoa burudani kwa wapenzi wa dansi nchini.                                                       
Werrason aliyeanzia katika bendi ya Wenge BCBG,  miongoni mwa wanamuziki wa Congo wanaopata nafasi za kupata mwaliko wa kuja kutoa burudani hapa nchini,  huku mratibu wa maonyesho hayo akiwataka mashabiki wajitokeze kupata burudani nzuri kutoka kwa nguli huyo.
   Mratibu wa Ziara ya Mwanamuziki Werrason King Dodoo Labuche akizungumza na waandishi wa habari baada ya msanii huyo kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa    kwa ajili ya maonyesho yake sehemu tofauti nchini. 
Mwanamuziki nguli wa muziki wa dansi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Werrason Ngiama Makanda akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa    kwa ajili ya maonyesho yake sehemu tofauti nchini.

             
Viewing all 110021 articles
Browse latest View live


Latest Images