Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 236 | 237 | (Page 238) | 239 | 240 | .... | 3286 | newer

  0 0

   Mwanamuziki Banana Zoro akiwa na bendi yake ya B-Band akitumbuiza katika tafrija ya Usiku wa Maafisa masoko iliyofanyika usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya Golden Tulip huku Kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia Kinywaji chake cha Tusker Lite kudhamini tafrija hiyo
  Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mh Ephraimu Mafuru akitoa neno mara baada ya kukaribishwa mbele kwa niaba ya kampuni ya Bia ya Serengeti katika tafrija ya Usiku wa Maafisa masoko iliyofanyika usiku wa kuamkia leo katika Hoteli ya Golden Tulip na kudhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia Kinywaji chake Cha Tusker Lite
   Meneja wa Kinywaji cha Tusker Sia Shayo akitoa neno mara baada ya kukaribishwa mbele kwa niaba ya kampuni ya Bia ya Serengeti katika tafrija ya Usiku wa Maafisa masoko iliyofanyika usiku wa kuamkia leo katika Hoteli ya Golden Tulip na kudhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia Kinywaji chake Cha Tusker Lite
   Baadhi ya maafisa masoko kutoka kampuni mbalimbali za hapa nchini na nje ya nchi wakisikiliza kwa makini katika tafrija ya Usiku wa Maafisa masoko iliyofanyika katika hoteli ya Golden Tulip na kudhaminiwa na Kampuni ya bia ya Serengeti Brewries Limited kupitia kinywaji chake cha Tusker
   Banana Zoro akiwa na wadau waliohudhuria tafrija ya Usiku wa Maafisa Masoko iliyofanyika Katika Hoteli ya Golden Tulip na kudhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia Kinywaji chake cha Tusker Lite, tafrija iliyofanyika usiku wa Kuamkia leo
   Baadhi ya Maafisa masoko waliohudhuria tafrija hiyo
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Brewries Limited Mh Steve Gannon akitabasamu mara baada ya Meneja Masoko wa Serengeti Brewries Limited Mh Ephraimu Mafuru (hayupo pichani) kutoa Neno lake kwa niaba ya Kampuni ya Serengeti Brewries Limited ambao Walikuwa wadhamini wa tafrija hiyo ya Usiku wa Maafisa Masoko kupitia Kinywaji Chao cha Tusker Lite.Picha Zote na Josephat Lukaza wa Http://josephatlukaza.blogspot.com

  0 0

   Mwenyekiti wa Umoja wa Makatibu Mahsusi  wa Wizara ya Nishati na Madini (TAPSEA) Marcelina Mushumbusi (katikati) akizungumza na watumishi wa Kada husika katika maadhimisho ya Siku ya Makatibu Mahsusi Tanzania, Agosti 23, 2013.  Maadhimisho hayo yalifanyika Makao Makuu ya Wizara, Dar es Salaam.

   Makatibu Mahsusi wa Wizara ya Nishati na Madini wakijadili mafanikio na changamoto ambazo wanazipata katika utendaji wao wa kazi, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Makatibu Mahsusi Tanzania.

  Makatibu Mahsusi wa Wizara ya Nishati na Madini wakiwa katika picha ya pamoja, walipokutana kuadhimisha Siku ya Makatibu Mahsusi Tanzania.

  Baadhi ya Makatibu Mahsusi wa Wizara ya Nishati na Madini wakiwa katika picha ya pamoja, walipokutana kuadhimisha Siku ya Makatibu Mahsusi Tanzania.


  Na George Mremi na 
  Hendrick Msangi

  Mwenyekiti wa Umoja wa Makatibu Mahsusi  wa Wizara ya Nishati na Madini (TAPSEA) Marcelina Mushumbusi amewataka watumishi wa Kada hiyo katika Wizara husika kufanya kazi kwa uadilifu ili kujenga uaminifu kwa mwajiri wao, Serikali na jamii nzima.

  Akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Makatibu Mahsusi Tanzania yaliyofanyika Makao Makuu ya Wizara jijini Dar es Salaam, Mushumbusi aliwasisitiza Makatibu Mahsusi hao kutoa huduma kwa weledi na kuwataka kuwa na upendo, umoja, na kusaidiana ili kufanikisha majukumu yao ya kila siku.

  Wakiadhimisha siku hiyo muhimu, Makatibu Mahsusi wa Wizara ya Nishati na Madini walikutana pamoja kujadili mafanikio na changamoto ambazo wanazipata katika utendaji wao wa kazi.

  Mushumbusi alitumia fursa hiyo kuomba Uongozi wa Wizara kutoa mafunzo ya weledi na maadili bora ya kazi kwa watumishi wa Kada hiyo.

  Aidha, alishauri watumishi wengine wote wa Wizara wapewe mafunzo ya aina hiyo kulingana na taaluma zao ili kuboresha utendaji wa kazi za serikali kwa manufaa ya Watanzania wote.

  Mwenyekiti huyo alimpongeza Katibu Mkuu wa Wizara Bw. Eliakim Maswi kwa kutoa fursa ya wao kujiendeleza kielimu  hali ambayo inawasaidia kuwa na ufanisi katika utendaji wao wa kazi.

  Aliwataka Makatibu Mahsusi kuchangamkia fursa hiyo ya elimu kwa kuongeza ujuzi katika fani yao na pia aliwapa changamoto kusoma fani nyingine ambazo zitawasaidia kuendana na mabadiliko yanayotokana na kukua kwa teknolojia duniani kote.


  0 0


  We are taking this opportunity to thank our entire fans around the globe for your support to this band.
  It is your support that makes the Ngoma Africa band prosper, without you there will be no success!
  Please, we ask you again to keep on supporting and let the band be on the top most position in every event, festival, media etc.
  Let others around you join the band at www.ngoma-africa.com
  Here they will have the opportunity to enjoy music at 


  Yours Sincerely
  NGOMA AFRICA BAND

  0 0

                        NUNUA TIKITI YAKO MAPEEEEEEEEMA USISUBIRI "BAADAEEE"

  0 0

  Courtesy of SautiZaBongo

  0 0

  Utangulizi:

  Marais wa nchi za Rwanda, Uganda na Kenya, walikutana mwanzoni mwa mwezi uliopita, ambapo mojawapo ya maazimio ya mkutano wao, ilikuwa ni kufanya Mombasa kuwa kituo cha kukusanya ushuru, na hivyo Uganda na Rwanda waanze kusafirisha mizigo yao moja kwa moja kutoka Mombasa. (Angalia ambatisho)

  Ufafanuzi:

  Chama cha Umoja wa Wasafirishaji wa Malori nchini (TATOA), kinaamini hatua hiyo itadhoofisha uchumi wa nchi yetu kwa kiasi kikubwa sana.

  Na kama serikali yetu ikipuuzia kujiondoa kwa wateja hawa wawili, Rwanda na Uganda, huenda nchi nyingine zaidi zikazidi kujiondoa kutumia bandari ya Dar es Salaam.

  TATOA inaamini maamuzi kama haya ya nchi za wenzetu ya kurahisisha taratibu za ulipaji ushuru pamoja na kuboresha utaratibu wa bandari ni muhimu kwa bandari yetu pia.

  Ripoti ya Benki ya Dunia (WB) ilidhihirisha namna ambavyo bandari ya Dar es Salaam, ufanisi ukiboreshwa, inaweza ikawa mkombozi mkubwa wa uchumi wetu.

  Faida za bandari hii kwa uchumi ni mtambuka, kwa hiyo TATOA haitapenda kuona mteja yoyote akijitoa kutumia bandari yetu, au kupungua kwa biashara kwa namna yoyote ile, na hivyo itapigania kwa kuishauri serikali katika kuboresha bandari yetu.

  TATOA ni mmoja wa wadau muhimu kwenye sekta hii ya bandari, kwani biashara yake ni kusafirisha mizigo inayofika bandari ya Dar es Salaam kuwafikishia walengwa, hasa nchi zisizo na bandari (land locked countries) kama Congo, Zambia, Rwanda, Malawi,Uganda, Zimbabwe na Burundi.

  Hivyo kuondoka au kupungua kwa namna yoyote ile kwa matumizi ya bandari yetu, ni hofu ya TATOA itaathiri uchumi kwa kiasi kikubwa.

  Ieleweke kwamba, sekta ya usafirishaji wa malori ni muhimu kwa uchumi wetu. Sekta hii inatoa zaidi ya ajira milioni moja (1) za moja kwa moja, na nyingine zaidi ya milioni tatu (3) zisizo za moja kwa moja.

  Sekta ya usafiirishaji wa malori pia, ni yapili kwenye uchangiaji wa pato la taifa (GDP).

  Sekta hii pia, ni mojawapo ya sekta chache nchini ambazo zinagusa nyanja tofauti za kiuchumi kama, huduma za simu za kutuma pesa, matairi, spea pamoja na mafuta, ambazo zote zinafaidika na sekta hii.

  Mabenki pia yamekuwa ni mojawapo ya taasisi zinazofaidika na sekta ya usafirishaji, ukiangalia kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo, huduma inayoongoza kwenye mabenki ni Vehicle Asset Financing.

  Zaidi ya hayo, TATOA pia inachangia kwa kiasi kikubwa kwenye mfuko wa barabara, ambao ndio unatumika kuboresha barabara zetu nchini, kupitia matumizi ya mafuta, ambapo malori pekee yanatumia ziadi ya lita milioni mbili na laki tisa kwa siku kati ya lita milioni tatu na nusu.

  Mwisho TATOA inaamini, uboreshaji wa reli ni muhimu kwa maendeleo ya sekta ya usafirishaji nchini, kwani miundo mbinu hii miwili, reli na barabara, inafanya kazi kwa pamoja.

  Wakati reli inaweza kufikisha mzigo mpaka stesheni, malori yatahitajika kufikisha mzigo sokoni, au mahala pengine mteja atakapohitaji.

  Mifano hai ni nchi ya Uingereza na Afrika Kusini, ambazo zina malori mengi pamoja na kuwa zina mfumo mzuri wa reli.

  Lakini kwa nchi yetu, ambayo sekta ya reli bado inaboreshwa, tunaamini malori yataendelea kuwa na umuhimu mkubwa.

  TATOA inaiomba serikali, kupitia wizara ya uchukuzi kufanyia kazi kero zilizopo katika bandari ya Dar es Salaam lakini pia kufanyia kazi mapendekezo yanayotolewa na wadau wa sekta ya usafirishaji.


  ========  ========  =======

  0 0
 • 08/24/13--00:37: Article 7


 • 0 0
 • 08/24/13--00:39: Article 6
 • Peroni Jazz Sundays VI this Sunday 25th  at Velisa’s. We have Janelle Gill hot from the DC Jazz Festival, Backed by the Best horn section in East Africa and a fabulous down south buffet for Tshs. 28,000!  Finish the weekend right !. No cover charge.


  0 0

  Kenya Port Authority (KPA) is losing business to rival Dar es Salaam port as delay in cargo clearance in Mombasa prompts traders from neighbouring countries to turn to Tanzania.
  Data from KPA shows that the Mombasa port handled 18.9 per cent less or 552,449 tonnes of cargo from Tanzania, Burundi, Rwanda and the DRC in the nine months to September.
  As a result, the port relied on Uganda and South Sudan—that have little choice on their logistic corridor—to grow its export cargo volumes to 3.9 million tonnes in the nine months compared to 3.8 million tonnes in the same period last year.
  Shippers attribute the trend to the shorter period it takes to transport cargo from the port of Dar es Salaam compared to Mombasa which is facing congestion that has seen transporters take more than a month to reach Rwanda from three weeks.
  “We are losing business to Tanzania because of inefficiency at the port,” said Gerald Kagumo, the vice chairman of East Africa Freight Forwarders Association.

  0 0

  Boniface Wambura
  Ofisa Habari
  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

  USAJILI WA WACHEZAJI 37 WAKWAMA VPL
  Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imezuia usajili wa wachezaji 37 wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kutokana na usajili wao kuwa na kasoro.

  Klabu husika zimetakiwa kurekebisha kasoro hizo kabla ya kuanza kuwatumia wachezaji hao kwenye mechi za VPL ambazo zinaanza leo (Agosti 24 mwaka huu) katika viwanja mbalimbali nchini.

  JKT Ruvu Stars inatakiwa kuwafanyia uhamisho (transfer) wachezaji Salum Machaku Salum aliyekuwa Polisi Morogoro na Emmanuel Leonard Swita (Toto Africans). Mgambo Shooting inatakiwa kuwafanyia uhamisho wachezaji Mohamed Hussein Neto (Toto Africans), Kulwa Said Manzi (Polisi Morogoro) na Mohamed Ally Samata (African Lyon).

  Pia Salum Aziz Gilla anaonekana bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Coastal Union huku kukiwa hakuna vielelezo vyovyote kutoka kwa mchezaji mwenyewe, Coastal Union au Mgambo Shooting kama ulivunjwa au umenunulia na klabu anayotaka kuchezea msimu huu.

  Tanzania Prisons inatakiwa kuwafanyia uhamisho wachezaji James Mjinja Magafu kutoka Toto Africans na Six Ally Mwasekaga (Majimaji). Nayo Coastal Union inatakiwa kumfanyia uhamisho mchezaji Kenneth Abeid Masumbuko kutoka Polisi Morogoro. 

  Kagera Sugar inatakiwa kuwafanyia uhamisho wachezaji Suleiman Kibuta Rajab (Toto Africans), Godfrey Innocent Wambura (Abajalo), Eric Mulera Muliro (Toto Africans), Adam Juma Kingwande (African Lyon) na Peter Gideon Mutabuzi (Toto Africans).

  Pia Kagera Sugar imepata Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa ajili ya mchezaji Kitagenda Hamis Bukenya, lakini bado hana kibali cha kufanyia kazi nchini (work permit).

  Kwa upande wa Ruvu Shooting inatakiwa kuwafanyia uhamisho wachezaji Abdul Juma Seif (African Lyon), Lambele Jerome Reuben (Ashanti United), Juma Seif Dion (African Lyon) na Cosmas Ader Lewis (African Lyon).

  Oljoro JKT inatakiwa kumfanyia uhamisho mchezaji Tizzo Charles Chomba kutoka Polisi Morogoro, lakini imekataliwa kumsajili mchezaji Damas Mussa Kugesha wa Mlale JKT kwa kigezo kuwa ni askari na amehamishiwa Arusha kwa ajili ya mafunzo ya kijeshi. Kama Oljoro JKT inamtaka mchezaji huyo ni lazima ifuate taratibu za usajili kwa kumfanyia uhamisho kutoka Mlale JKT.

   Nayo Mtibwa Sugar inatakiwa kuwafanyia uhamisho wachezaji Ally Shomari Sharrif (Polisi Morogoro), Salim Hassan Mbonde (Oljoro JKT U20) na Hassan Salum Mbande iliyemsajili kwenye kikosi chake cha U20 akitokea Oljoro JKT U20. 
  Ashanti United haiwezi kumtumia Said Maulid Kalikula aliyekuwa akicheza Angola kwa vile hajapata ITC. Nayo Rhino Rangers inatakiwa kuwafanyia uhamisho wachezaji Ally Ahmad Mwanyiro (Mwadui FC), Laban David Kambole (Toto Africans) na Musa Boaz Chibwabwa (Villa Squad).

  Klabu ya Simba inatakiwa kumfanyia uhamisho Betram Arcadi Mwombeki kutoka Pamba SC wakati wachezaji Gilbert John Kaze na Amisi Tambwe bado hawajapata ITC kutoka Burundi na hawana vibali vya kufanya kazi nchini. Mchezaji Joseph Owino tayari ITC imepatikana lakini hana kibali cha kufanya kazi nchini. Pia kipa Abel right Dhaila hana kibali cha kufanya kazi nchini. 
  Vilevile Simba inatakiwa kuwafanyia uhamisho wachezaji wawili iliyowasajili katika kikosi chake cha U20. Wachezaji hao ni Twaha Shekue Ibrahim kutoka Coastal Union 20 na Adeyun Saleh Seif (Oljoro JKT U20).

  Nayo Yanga inatakiwa kumfanyia uhamisho mchezaji Rajabu Zahir Mohamed kutoka Mtibwa Sugar U20 wakati Hussein Omari Javu bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Mtibwa Sugar huku kukiwa hakuna vielelezo vyovyote kutoka kwa mchezaji mwenyewe, Mtibwa Sugar au Yanga kama mkataba huo ulivunjwa au umenunulia na klabu anayotaka kuchezea msimu huu.

  Wachezaji waliosajiliwa kutoka nje ambao ITC zimefika na pia wana vibali vya kufanya kazi nchini ni Crispine Odula Wadenya kutoka Bandari ya Kenya na Yayo Wasajja Fred Lutimba kutoka URA ya Uganda waliojiunga na timu ya Coastal Union. Pia Mtanzania Hamis Thabit Nyige aliyejiunga na Yanga kutoka Ureno naye tayari na ITC.
  Kwa mujibu wa kanuni, wachezaji wote wa ridhaa (wa madaraja ya chini ikiwemo Daraja la Kwanza) wanatakiwa kufanyiwa uhamisho (transfer) kwa klabu husika kujaza fomu za uhamisho na kulipia ada Chama cha Mpira wa Miguu cha Wilaya, Chama cha Mpira wa Miguu cha Mkoa na TFF.
  Pia TFF inakumbusha kuwa wachezaji wanaotajwa kuwa wamesajiliwa kama wachezaji huru (free agent) ni lazima waoneshwe kama huko walipokuwa mikataba imekwisha au la.

  Boniface Wambura
  Ofisa Habari
  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

  0 0

   Zimbabwe haitokuwa koloni tena
   Mungu Mbariki Rais Mugabe kwa msimamo wake usiotetereka dhidi ya ushoga
  SADC, COMEASA na AU walikuja, wakaona na kuthibitisha. Hilo tu ndilo lenye mantiki kwa  Zimbabwe.

  0 0

  Na Frank Geofay wa Jeshi la Polisi,
  Windhoek Namibia. 
  Timu ya Polisi Tanzania inayoshiriki Michezo ya Umoja wa wakuu wa Polisi kusini mwa Afrika (SARPCCO) nchini Namibia imelazimishwa sare ya mabao 2 kwa 2 katika mwendelezo wa michezo hiyo. 
  Mchezo huo ambao ulichezwa katika uwanja wa Sam Njoma nje kidogo ya jiji la Windhoek ulikuwa mkali huku Tanzania ikitawala katika vipindi vyote lakini ikishindwa kutumia vizuri nafasi walizozipata. 
  Mabao ya Kongo yalifungwa katika kipindi cha kwanza na Makundi Kaluma na Kalumba Banza na ya Tanzania yalifungwa na Ahmed Bello kipindi cha kwanza na John Kanakamfumu kipindi cha pili kwa njia ya mkwaju wa penati baada ya mchezaji wa kongo kuunawa mpira katika eneo la hatari. Huu ni mchezo wa pili kwa timu ya mpira wa miguu ya Polisi Tanzania kucheza baada ya mchezo wa kwanza kukubali kichapo cha mabao 2 kwa 1 kutoka kwa Zambia. 
  Katika Mpira wa pete timu ya Polisi Tanzania iliweza kuifunga Angola 61 kwa 13.huku ikitoka sare na wenyeji Namibia kwa kufungana mabao 29 kwa 29 huku ikifungwa na Swaziland 35 kwa 25. Matokeo mengine katika mpira wa miguu ni pamoja na Zambia 2 Lesotho 0, Namibia 1 South Afrika 0. 
  Timu ya mpira wa miguu ya Tanzania itashuka dimbani tena kesho kupambana na Angola ambapo pia wanariadha wanne wataiwakilisha Tanzania katika mbio fupi za kilometa 25.
   Mshambuliaji wa Polisi Tanzania Adimini Bantu (mwenye mpira) akiwatoka mabeki wa timu ya Polisi Kongo wakati wa mchezo wao katika Michezo ya nane ya Majeshi ya Polisi kwa Nchi za Kusini mwa Afrika  (SARPCCO nchini Namibia.Timu hizo zilitoka sare ya 2 kwa 2.

  Mshambuliaji wa Polisi Tanzania Ahmed Bello (jezi ya bluu) akipambana na mchezaji wa  timu ya Polisi Kongo wakati wa mchezo wao katika Michezo ya nane ya Majeshi ya Polisi kwa Nchi za Kusini mwa Afrika  (SARPCCO nchini Namibia.Timu hizo zilitoka sare ya 2 kwa 2.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Windhoek Namibia)


  0 0

   Mpiganaji Gabriel Zacharia wa TBC akiwa kazini katika uwanja wa Taifa wa Harare, Zimbabwe, siku ya kuapishwa Rais Robert Mugabe wa nchi hiyo Agosti 22, 2013
   Ankal akiwa na mpiga picha wa Ap aliye na makao yake Johannesburg, Afrika Kusini
  Mpiganaji Oscra Mbuza wa HabariLeo akiwa katika uwanja wa Taifa wa Harare, Zimbabwe, siku ya kuapishwa Rais Robert Mugabe wa nchi hiyo Agosti 22, 2013

  0 0
 • 08/24/13--02:21: dar es salaam by night


 • 0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohamed Shein  akilakiwa na Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala baada kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Schiphol,  Uholanzi,  kuanza ziara ya kikazi ya siku tano nchini humo leo.

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amewasili nchini Uholanzi kuanza ziara rasmi ya siku tano nchini humo kufuatia mwaliko wa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Bwana Mark Rutte.
  Hapo kesho Dk. Shein atatembelea bandari ya Rottedam ambapo baadae atafanya mazungumzo na makampuni na makampuni yaliyo katika sekta ya miundombinu ya usafiri wa bahari.
  Kesho jioni atakutana na Mfalme wa Uholanzi Willem Alexander na baadae kuhudhuria chakula cha jioni kilichoandaliwa kwa heshma yake.
  Jumatano ijayo tarehe 28 Agosti, 2013 atakutana na Waziri wa Biashara ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bibi Lilianne Ploumen na pia atafanya mazungumzo na wadau katika sekta ya Nishati. Atatembelea pia Makao Makuu ya Kampuni ya Mafuta ya Shell.
  Mapema Alhamisi asubuhi Dk. Shein atakutana na Waziri Mkuu wa Uholanzi Bwana Mark Rutte. Baada ya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Uholanzi Rais wa Zanzibar atatembelea Kampuni ya vifaa vya uchunguzi wa maradhi ya Sakura ambako atabadilishana mawazo juu ya masuala ya afya kati ya Zanzibar na Uholanzi.
  Siku hiyo baadae mchana atatembelea bandari ya Scheveningen ambako atakutana na wananchama wa Muungano wa Wadau katika Sekta ya Uvuvi na kukutana pia na uongozi wa kampuni ya usindikaji na uuzaji wa mazao ya bahari nchini humo. Baadae jioni atakutana na watanzania wanaoishi nchini Uholanzi mjini The Hague.
  Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Schiphol mjini Amsterdam Dk. Shein alipokelewa na Mwakilishi wa Mfalme wa Uholanzi Kamanda Juan Irausquin, Naibu Mkurugenzi wa Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Uholanzi bwana Micheal Rauner, Balozi wa Uholanzi nchini Bwana Jaap Fredericks, Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Balozi Diodorus Kamala na Bwana Frans Hakkenberg, Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Uholanzi.
  Katika ziara hiyo Dk. Shein amefuatana Waziri Ardhi, Makazi, Maji na Nishati wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Ramadhani Abdalla Shaaban, Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Rashid Seif Suleiman, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mahadhi Juma Maalim, Mshauri wa Rais Ushirikiano wa Kimataifa, Uwekezaji na Uchumi, Balozi Mohamed Ramia na Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar Balozi Silima Kombo Haji.
  Rais na ujumbe wake wanatarajia kurejea nchini Tarehe 1 Sept, 2013.


  0 0

  Kampuni ya Neema Herbalist kwa kushirikiana na Taasisi ya Flatbelly Tanzania ama FlabelTa imejipanga kutengeneza mamia ya fursa za ajira kwa vijana wasio na ajira wanaoishi kwenye kata mbalimbali za jijini Dar Es salaam. 
   Fursa hizo za ajira zitatengenezwa kupitia Mradi wa Flatbelly Project ambao umelenga katika kuwahamasisha wananchi wa kada mbalimbali jijini Dar es salaam,kuondokana na tatizo la vitambi,unene na/ama uzito ulio kithiri kwa kutumia dawa za asili, vyakula lishe ama tibalishe. Mradi huu utawanufaisha vijana watano kutoka katika kila kata ya jiji la Dar Es salaam ambao watapatiwa mafunzo maalumu ya yatakayo wajengea uwezo wa kufanya kazi katika mradi huu. Mafunzo watakayo patiwa vijana hawa ni pamoja na NAMNA YA KUANDAA LISHE ( DIET )MAALUMU KWA WATU WENYE MATATIZO YA VITAMBI,UNENE & UZITO MKUBWA KUPITA KIASI, pamoja na JINSI YA KUKUSANYA TAARIFA ZA WATU WENYE MATATIZO YA VITAMBI, UNENE NA UZITO MKUBWA WALIOPO KATIKA MAENEO MBALIMBALI KAMA VILE MAOFISINI NA MAJUMBANI. 
  Mafunzo yatafanyika kwa muda wa wiki moja kuanzia tarehe 23 Septemba 2013 hadi tarehe 28 Septemba 2013. Baada ya mafunzo, wahitimu watapangiwa vituo vya kazi katika kata mbalimbali za jijini Dar Es salaam ambapo watapewa jukumu la kukusanya taarifa za watu wenye matatizo ya vitambi,unene na uzito kupita kiasi na kuwa andikisha katika program maalumu ya kuwasaidia kuondokana na tatizo la vitambi, unene na uzito mkubwa kwa kutumia dawa za asili, vyakula dawa na tibalishe kazi ambayo wataianza rasmi mnamo tarehe 01 OKTOBA 2013. 
  Majukumu mengine watakayo patiwa vijana hawa ni pamoja na kuandaa na kusimamia semina mbalimbali kuhusu masuala ya umuhimu wa tibalishe kwa watu mbalimbali kama vile akina mama wa majumbani na wanawake wajasiriamali wanao jihusisha na biashara ya upishi wa vyakula vya aina mbalimbali.
   Katika kuhakikisha kuwa vijana watakao patiwa mafunzo haya wanakuwa na uwezo wa kufanya kazi kwenye mradi huu kwa ufanisi mkubwa, taasisi kwa kushirikiana na kampuni ya Neema Herbalist itakuwa ikitoa warsha na semina elekezi za mara kwa mara kwa vijana hawa katika kipindi chote cha mwaka mmoja ambacho watakuwa wanafanya kazi chini ya mradi huu. 
  Mradi huu hautaishia jijini Dar Es salaam pekee, kwani baada ya vijana waliopo jijini Dar Es salaam kuanza kazi ,mradi utaelekea katika mikoa mingine ya Tanzania bara katika utaratibu na ratiba itakayo tangazwa katika blogu yetu na vyombo mbalimbali vya habari mwishoni mwa mwezi Septemba au mwanzoni mwa mwezi Oktoba 2013. 
  Sifa za kujiunga na mafunzo haya ni kuwa raia wa Tanzania mwenye elimu ya kuanzia kidato cha nne, sita na kuendelea, uwezo wa kuwasiliana kwa ufasaha kwa lugha za Kiswahili na kiingereza, uwezo wa kujieleza, umaridadi kujituma na kuwa tayari kufanya kazi kwa muda wa mwaka mmoja katika mradi huu kama Mshauri/Muelimishaji kuhusu masuala ya tibalishe. 
   KWA TAARIFA ZAIDI KUHUSU UTARATIBU WA KUJIUNGA NA MAFUNZO HAYA, TAFADHALI TEMBELEA 
  http://www.neemaherbalist.blogspot.com

  0 0

  Urban Pulse Creative Media wakishirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza wanakuletea ziara fupi ya Mh Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipokutana na Watanzania waishio Nchini Uingereza mapema Agosti 2013 Asanteni, Urban Pulse Creative

  0 0

   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akiwa na Balozi wa China nchini, Lu Youqing walipokuwa wakikagua mitambo ya kisasa ya kuunganisha mabomba ya kusafirishia gesi, katika karakana namba tano  ya Kampuni ya kichina ya CPTDC ya Ikwiriri, wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani .Profesa Muhongo alifanya ziara ya siku moja ya kukagua utekelezaji wa maandalizi ya utandazaji wa mabomba hayo ya gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.
   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa  Kampuni ya kichina ya CPTDC iliyopewa tenda ya kutandaza mabomba ya gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam, alipokuwa katika ziara ya siku moja ya kukagua utekelezaji wa maandalizi ya utandazaji wa mabomba hayo ya gesi, juzi eneo la Somanga Fungu, wilayani Kilwa, Mkoa wa Lindi.
   Sehemu ya mabomba ya gesi yakiwa eneo la kuhifadhia la Nyamwage, Rufiji
   Profesa Muhongo akiangalia kipenyo cha bomba ambacho ni mita moja
   Profesa Muhongo akioneshwa sehemu ya bomba itakayounganishwa na bomba lingine

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0


  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (kushoto), akizungumza na Mgeni Rasmi ambaye pia ni Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Mhe. Dkt. Salim Ahmed Salim kabla ya ufunguzi rasmi wa Baraza la Katiba la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba. Ufunguzi huo uliowahusisha Mabalozi Wastaafu, Watumishi wa Wizara na Taasisi na wadau wengine ulifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa chaJulius Nyerere Jijini Dar es Salaam, tarehe 26 Agosti, 2013. Wengine katika picha ni Bw. John Haule, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Balozi Mstaafu, Mhe. David Kapya. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Malkia wa Redd's Miss Ilala 2013, Doris Mollel amkimkabidhi  vitabu mwanafunzi Charles Costantino ambaye alipokea msaada huo kwa niaba ya Shule ya Msingi Guluka Kwalala, Jimbo la Ukonga, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Mollel alikabidhi vitabu 30 vyenye thamani ya sh. 300,000. Wanaoshuhudia ni Miss Ilala namba mbili Alice Issack (wa tatu kushoto), mshindi wa tatu Clara Bayo (wa pili kushoto) na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Rehema Mketo.
  Malkia wa Redd's Miss Ilala 2013, Doris Mollel akiwa na wanafunzi baada ya kukabidhi msaada wa vitabu  30 vyenye thamani ya sh. 300,000 kwa Shule ya msingi Guluka Kwalala, Jimbo la Ukonga, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
   Warembo wakifurahi pamoja na wanafunzi

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

older | 1 | .... | 236 | 237 | (Page 238) | 239 | 240 | .... | 3286 | newer