Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

TRA YAJIKITA ZAIDI KUHUDUMIA WANANCHI KATIKA MAONYESHO YA SABASABA

$
0
0


Afisa Mwandamizi wa Uchambuzi wa Mifumo ya Biashara wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu Bw. Mathias Chanila akimhudumia mwananchi aliyetembelea Banda la TRA katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Huduma kwa Mlipakodi ambaye pia ni Mratibu wa Maonyesho ya 42 ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba kwa upande wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bi. Honester Ndunguru (kushoto) akiwaelezea Maafisa wa SIDO haki na wajibu wa Mlipakodi kama ilivyoainishwa katika Mkataba wa Huduma na Mlipakodi wakati walipotembelea Banda la TRA kwenye Maonyesho hayo yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Afisa Elimu na Huduma kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kikodi Temeke Bw. Paul Maghembe akimhudumia mwananchi aliyetembelea Banda la TRA katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Afisa wa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kikodi Temeke Bi. Jacqueline Fairom akimhudumia mwananchi aliyetembelea Banda la TRA katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO)

Wateja Halopesa sasa kutuma pesa bure

$
0
0
·       Sasa wataweza kutuma na kupokea pesa kutoka mitandao mingine.
 Kampuni ya mawasiliano ya simu ya Halotel imeondoa gharama za kutuma pesa kwa wateja wanaotumia huduma ya kifedha ya Halopesa, na hivi sasa wataweza kutuma pesa bure Halopesa kwenda Halopesa, huku pia ikipunguza gharama za kutuma fedha kutoka Halopesa kwenda mitandao mingine.
Kuondolewa kwa makato hayo inatafsiriwa na kampuni hiyo kama njia pekee ya kupanua wigo wa huduma za kifedha kwa mamilioni ya Watanzania ambao wanatumia huduma za kifedha kwa njia ya simu.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Halopesa, Vu Tuan Long, amesema kuwa kuondolewa kwa gharama hizo kutawezesha wateja wa mtandao huo hasa walioko katika maeneo ya vijijini kuweza kufanya miamala ya simu na kuondokana na usumbufu ambao wangeweza kuepuka kwa kutumia njia nyingine kutuma fedha ili kuokoa gharama za makato ya kufanya miamala.
“Tuna mamilioni ya watanzania ambao kwa mara ya kwanza walipata mawasiliano ya simu tulipoanzisha huduma zetu, na baada ya kuanzishwa kwa huduma ya Halopesa kwa miaka miwili sasa wateja wetu katika maeneo mbalimbali wanaweza kutuma pesa bure Halopesa kwenda Halopesa,” Alisema Long na kuongeza.
“Hii ni hatua nyingine ya kuhakikisha kwamba wateja wanakuwa na wigo mkubwa wa kuweza kukidhi mahitaji yao katika nyanja mbalimbali za kiuchumi, na kijamii kupitia huduma ya kifedha ya mtandao kwa ubora, ukaribu, uhakika  na usalama zaidi na kuepuka kwenda umbali mrefu kwaajili ya kufuata huduma za kifedha kupitia benki”. Aliongeza Long.
Aidha Mkurugenzi huyo, alibainisha kuwa, licha ya kuondoa gharama katika kutuma fedha, huduma ya kutuma fedha kutoka Halopesa kwenda mitandao mingine imepunguzwa gharama ili iwe rahisi zaidi kwa wateja wanaotuma pesa kwenda mitandao mingine ya simu pia waweze kutuma pesa kwa gharama nafuu.
“Habari njema tuliyonayo kwa wateja wetu ni kuwezeshwa kwa huduma ya Halopesa kuweza kutuma pesa kwenda mitandao yote, sasa wateja wetu wataweza kutuma pesa kwenda mitandao mingine kwa gharama nafuu zaidi kabisa,” Alihitimisha Long
Tangu kuanzishwa kwa huduma ya Halopesa tayari Mawakala Zaidi ya elfu 55,000 tayari wamejisajili na wanatoa huduma kwa zaidi ya wateja milioni moja na nusu walioenea nchi nzima.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel Nguyen Van Son pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni hiyo,Mhina Semwenda wakifungua shampeni kuashiria uzinduzi wa huduma ya wateja wa Halopesa kutuma pesa bure Halopesa kwenda Halopesa, wanaoshuhudia ni Mkuu wa kitengo cah Halopesa Vu Tuan Longa (Kulia) na Meneja biashara wa Halopesa Magesa Wandwi (Kushoto). 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel Van Nguyen Son pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni hiyo,Mhina Semwenda wakishika glasi za shampeni katika uzinduzi wa huduma ya wateja wa Halopesa itakao wawezesha kutuma pesa bure Halopesa kwenda Halopesa, wanaoshuhudia ni Mkuu wa kitengo cah Halopesa Vu Tuan Longa (Kulia) na Meneja biashara wa Halopesa Magesa Wandwi (Kushoto).
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel Van Nguyen Son pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni hiyo,Mhina Semwenda pamoja wa wafanyakazi wengine wa Halotel wakigonga glass za shampeni kuashiria uzinduzi wa huduma ya wateja wa Halopesa itakao wawezesha kutuma pesa bure Halopesa kwenda Halopesa, wanaoshuhudia ni Mkuu wa kitengo cah Halopesa Vu Tuan Longa (Kulia) na Meneja biashara wa Halopesa Magesa Wandwi (Kushoto).

Bodi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) yashiriki mafunzo ya siku mbili ya uongozi

$
0
0

Bodi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) inayoongozwa na Mwenyekiti Prof. John Kondoro imeshiriki mafunzo ya siku mbili ya uongozi kwa wajumbe wa Bodi (Board Leadership Training) yalioandaliwa na Menejimenti ya shirika la Reli na kuratibiwa na Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (Institute of Directors in Tanzania) kuanzia tarehe 2 - 3 Juni katika ukumbi wa Bodi, jengo la LAPF jijini Dodoma.

Lengo la kuandaa mafunzo ni kuwajengea uwezo wajumbe wa Bodi katika shughuli za uendeshaji wa Shirika. Bodi ya Shirika la Reli Tanzania imeundwa na wajumbe nane (8) wenye ujuzi mbalimbali kwa kufuata sheria mpya ya Reli namba 10 ya Mwaka 2017. Bodi ya Shirika la Reli ilizinduliwa rasmi tarehe 11 mwezi Juni 2018 na aliyekuwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa.

Wajumbe.

1. Prof. John Kondoro-Mwenyekiti
2. Eng. Karim Mattaka-Mjumbe
3. Dkt. Jabiri Bakari-Mjumbe
4. Masanja Kadogosa-Katibu wa bodi
5. Eng. Rogers Mativila
6. Rukia Shamte-Mjumbe
7. Edson Mweyunge-Mjumbe
8. Wolfgang Ephraim Salia-Mjumbe 9. MahamudMabuyu-Mjumbe


Katibu wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Reli Tanzania Ndugu Masanja Kadogosa akitoa mfano alipokuwa akifafanua jambo walilokuwa wakijadili katika mafunzo ya wajumbe wa Bodi mpya ya TRC yaliyofanyika jijini Dodoma, tarehe 2 Juni 2018.
Katibu wa Bodi na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Ndg. Masanja Kadogosa akiwakaribisha wajumbe wa Bodi mpya ya TRC wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa na menejimenti ya TRC.
Mjumbe wa Bodi kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (wa kwanza kulia) Eng. Mattaka akielezea jambo kwa kina huku mwenyekiti Prof. Kondoro na mwezeshaji Ndugu Said Kambi wakifuatilia kwa makini.

Dr. Jabiri Bakari (katikati) akielezea jambo kwa msisitizo wakati wa mafunzo ya wajumbe wa Bodi ya TRC yaliyoandaliwa na menejimenti ya Shirika la Reli Tanzania na kufanyika jijini Dodoma.
Picha ya pamoja ya wajumbe wa Bodi mpya ya Shirika la Reli Tanzania, waratibu kutoka Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania na Sektretarieti ya Shirika la Reli Tanzania katika jengo la LAPF jijini Dodoma.

DAKTARI BINGWA WA MAGONJWA YA MOYO WA HEAMEDA MEDICAL CLINIC ATOA USHAURI NAMNA YA KUEPUKA MAGONJWA YA MOYO

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
DAKTARI Bingwa wa magonjwa ya moyo nchini kutoka Heamedia Medical Clinic Dk. Hery Mwandolela amesema kuna umuhimu mkubwa wa kila mmoja wetu kuhakikisha anapima afya yake mara kwa mara huku akitaja sababu zinazosababisha ugonjwa wa moyo.

Pia amesema ni vema kila mtu akafahamu namba saba muhimu kwa afya yako na kusisitiza kitendo cha kuchelewa kutambua ugonjwa mapema kunasababisha gharama kubwa zaidi ya ungetambua mapema na kukika ugonjwa husika.

Dk. Hery Mwandolela amesema hayo leo kwenye mahojiano maalum wakati anazungumza na Michuzi Blog kwenye banda lake lililopo katika Maonesho ya Bishara ya kimataifa yanayoendelea viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Amesema lengo la uwepo wake kwenye banda hilo kwanza unalenga kuwakumbusha wananchi mbalimbali kutambua umuhimu wa kupima afya mara kwa mara kwani inasaidia kupunguza gharama za matibabu.

Pia amesema yupo kwenye maonesho hayo kwasababu anataka kuwafahamisha Watanzania huduma bora na za kiwango cha juu katika kutibu magonjwa ya moyo ambayo yaafanywa na madaktari wabobezi waliopo Heameda Medical Clinic iliyopo mtaa wa Fubu maeneo ya Bunju B jijini.

Dk.Mwakandolela amesema pamoja na kutoa huduma kwa kiwango cha hali ya juu wameweka gharama nafuu ambazo kila mmoja anaweza kumudu ukilinganisha na maeneo mengine.

Akifafanua zaidi kuhusu kupima afya mara kwa mara amesema magonjwa kama ya kupanda kwa shinikizo la damu na kisukari huweza kuja bila dalili yeyote na wakati mwingine yanagundulika baada ya mhusika kupata madhara makubwa.

"Njia pekee ya kukabiliana na magonjwa haya ni kujenga tabia ya kupima afya zetu hata kama hatusikii dalili zozote za ugonjwa, kwani hii itsaidia kugundua tatizo mapema na kuchukua hatua madhubuti za kukabiliana nalo.
Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo nchini kutoka Heamedia Medical Clinic Dk. Hery Mwandolela akimuelezea mwandishi wa habari Said Mwishehe wa Michuzi Media mambo mbalimbali yanayosababisha watu kukumbwa na magonjwa ya moyo katika banda la Kliniki hiyo lililopo kwenye viwanja vya maonyesho vya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Daktari  Bingwa wa magonjwa ya moyo nchini kutoka Heamedia Medical Clinic Dk. Hery Mwandolela akionyesha mfano wa moyo wa binadamu. 
Daktari  Bingwa wa magonjwa ya moyo nchini kutoka Heamedia Medical Clinic Dk.Hery Mwandolela akizungumza na mmoja wa wananchi waliotaka kupata ufafanuazi wa magonjwa ya moyo alipotembelea katika banda hilo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

CHINA KUJENGA KIWANDA CHA DAWA NA VIFAA TIBA NCHINI

WAZIRI LUGOLA AWASILI WIZARANI AFANYA KIKAO NA WATENDAJI WAKUU

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akiongozana na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mhandisi Hamad Masauni(kulia) baada ya kupokelewa  leo ofisi ndogo ya wizara,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa  Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na viongozi wengine wa wizara hiyo akiwepo Naibu Waziri, Mhandisi Hamad Masauni(wapili kushoto),Katibu Mkuu, Meja Jenerali Jacob Kingu (wapili kulia), Naibu Katibu Mkuu, Ramadhani Kailima(wakwanza kulia).Wakwanza kushoto ni aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo,Balozi Hassan Simba Yahaya.Kikao hicho kimefanyika leo,jijini Dar es Salaam. 
Naibu Waziri wa  Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza wakati wa kikao cha viongozi wakuu wa wizara hiyo,Waziri Kangi Lugola(watatu kulia), Katibu Mkuu, Meja Jenerali Jacob Kingu (wapili kulia), Naibu Katibu Mkuu, Ramadhani Kailima(wakwanza kulia) aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo,Balozi Hassan Simba Yahaya(wapili kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Usajili wa Vyama vya Kijamii, Marlin Komba(wakwanza kushoto).Kikao hicho kimefanyika leo,jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro baada ya kufika Ofisi ndogo ya wizara jijini, Dar es Salaam,leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akisalimiana na Maafisa wa Jeshi baada ya kufika Ofisi Ndogo ya wizara,jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 

TPA YAWAKUTANISHA WAFANYABIASHARA KUTOKA NCHI SABA WANAOTUMIA BANDARI ZA TANZANIA

$
0
0
Naibu Waziri, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano), Atashasta Nditiye akizungumza kuhusu Serikali wanavyopanua wigo wa kutoa huduma kupitia bandari za Tanzania wakati wa ufunguzi wa kongamano la TPA na wafanyabiashara wanaotumia bandari za Tanzania kutoka nchi za Rwanda, Uganda, Burundi, Congo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Zambia, Malawi na Comoro uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi Bandari Tanzania (TPA), Profesa Ignatus Rubaratuka akizungumzia jinsi bandari za Tanzania zilivyojipanga imara kutoa huduma kwa wateja wao bila kuleta malalamiko kwa wateja wao ili kukuzu kipato cha nchi kupitia bandari hizo wakati wa kongamano la wafanyabiashara wanaotumia bandari za Tanzania kutoka nchi saba ulioandaliwa na Mamlaka ya Usimamizi Bandari Tanzania (TPA) ili kuongeza ufanisi kwenye utendaji wa wabandari za hapa nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi Bandari Tanzania (TPA), Deusdedit Kakoko akizungumza kwenye kongamano la wafanyabiashara wanaotumia bandari za Tanzania kutoka nchi saba ulioandaliwa na Mamlaka ya Usimamizi Bandari Tanzania (TPA) ili kuongeza ufanisi kwenye utendaji wa wabandari za hapa nchini.
Baadhi ya wafanyabiashara pamoja na wadau wa mbalimbali wanaotumia bandari ya Tanzania kutoka nchi saba wakiwa kwenye kongamano la wafanyabiashara wanaotumia bandari za Tanzania kutoka nchi saba ulioandaliwa na Mamlaka ya Usimamizi Bandari Tanzania (TPA.
Naibu Waziri, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano), Atashasta Nditiye akiwa kwenye picha na wafanyabiashara kutoka nchini saba pamoja na wadau wa Mamlaka ya Usimamizi Bandari Tanzania (TPA leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Mwakilishi Mkazi wa Azania Group Rwanda na Burundi, Mpagaze Jerome akizungumza na waandishi wa habari kuhusu faida pamoja na changamoto wanazozipata kwa kutumia bandari za hapa nchini.

YALIYOJIRI LEO KWENYE BANDA LA BUNGE KATIKA MAONYESHO YA 42 YA BIASHARA YA KIMATAIFA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Tata Ole Nasha (kushoto) akipokelewa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano Ofisi ya Bunge,  Zuhura Mtatifikolo alipotembelea Banda la Bunge katika Maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea leo tarehe 3 Julai, 2018 katika Viwanja vya Julius Kambarage Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano Ofisi ya Bunge, Zuhura Mtatifikolo (wa pili kushoto) akimpatia elimu Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Tata Ole Nasha (kushoto) kuhusu Shughuli mbali mbali zinazofanywa na Bunge alipotembelea Banda la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea leo tarehe 3 Julai, 2018 katika Viwanja vya Julius Kambarage Nyerere Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mshauri wa Bunge kwa Mambo ya kisheria, Ndg. Mariam Mbarouk.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Tata Ole Nasha (kushoto) akizungumza jambo wakati alipotembelea Banda la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea leo tarehe 3 Julai, 2018 katika Viwanja vya Julius Kambarage Nyerere Jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano Ofisi ya Bunge,  Zuhura Mtatifikolo na kulia ni Mshauri wa Bunge kwa Mambo ya kisheria, Ndg. Mariam Mbarouk.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Tata Ole Nasha akisaini kitabu cha wageni baada ya kutembelea Banda la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea leo tarehe 3 Julai, 2018 katika Viwanja vya Julius Kambarage Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Maafisa kutoka Ofisi ya Bunge wakiwapatia maelezo wageni mbalimbali waliofika katika Banda la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea leo tarehe 3 Julai, 2018 katika Viwanja vya Julius Kambarage Nyerere Jijini Dar es Salaam
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano Ofisi ya Bunge, Zuhura Mtatifikolo (kushoto) akimpatia elimu kuhusu Shughuli mbalimbali zinazofanywa na Bunge mmoja ya wageni wananchi waliofika katika Banda la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea leo tarehe 3 Julai, 2018 katika Viwanja vya Julius Kambarage Nyerere Jijini Dar es Salaam.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)      

NSSF YADHAMIRIA KUTOA MIKOPO YA RIBA NAFUU KWA SEKTA ISIYO RASMI IKIWAMO YA WAJASIRIAMALI,WAENDESHA BODABODA

$
0
0

SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limedhamiria kutoa mikopo ya riba nafuu kwa sekta isiyo rasmi wakiwamo wajasiriamali, waendesha bodaboda, mamalishe, wakulima, wavuvi na wote waliojiunga kwenye vikundi rasmi vya uzalishaji mali kama VIBINDO, AMCOS, VICOBA na  SACCOS  

Akizunngumza leo kwenye Maonesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoendeelea Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam ,Kaimu Meneja na Uhusiano wa NSSF Salim Khalfan amewaambia waandishi kuwa NSSF imedhamiria kuinua maisha ya Watanzania kwa kupitia fursa hii ya mikopo ambayo itawawezesha katika kufanya maendeleo yao ya sasa na baadae.

Amesema wafaidika na mikopo hii ni wale ambao wamejiunga tayari kwenye vikundi mbali mbali ambavyo tayari vimesajiliwa na kutambulika vitawezeshwa kuweza kupata mikopo hii kupitia katika benki ya AZANIA.

Hii ni fursa pekee kwa wale ambao wako kwenye sekta isiyorasmi kuweza kujikwamua kiuchumi kupitia mikopo ya riba nafuu. Shirika la Taifa Hifadhi za jamii (NSSF) linatoa mkopo huo kwa walengwa wenye masharti na fuu na riba ndogo ya kiasi cha asilimia 12.5 ambapo kwa mtu wa kawaida anaweza kukopa na kufanyia maendeleo yoyote.

Pia mbali na wananchi waliopo kwenye sekta isiyo rasmi pia hata wananchi waliopo kwenye sekta iliyorasmi nao wananafasi ya kupata mkopo kupitia vyama vyao vya ushirika. Mbali na mikopo hiyo, wanachama watapata mafao yote sita yanayotolewa na NSSF yakiwemo matibabu bure kwa mwanachama na wategemezi wake wanne, mafao ya uzazi ambapo mwanachama mwanamke atapata asilimia 300 ya kipato chake cha mwezi pale mwanachama anapokuwa ameka akiba kwa muda wa miezi 36.

Vile vile mwanachama atapata mafao ya uzeeni pale atakapokuwa amefikisha umri wa miaka 55-60 na mwanachama awe ameshachangia angalau miezi 180. Pamoja na hayo mwanachama atapata mafao ya ulemamu pale itakapothibitika kwamba amepoteza uwezo wake wa kufanya kazi, mafao ya urithi kwa wategemezi wa mwanachama pindi mwanachama atakapofariki pamoja na msaada wa mazishi kwa mwanachama .


Waaandishi wa Habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Profesa Godius Kahyarara alipozungumza nao leo kuhusu dhamira ya Shirika hilo kutoa Mikopo ya Riba nafuu kwa sekta isiyo rasmi kama vile wajasiliamali,waendesha boda boda,Mamalishe,Wakulima,Wavuvi na wote waliojiunga kwenye vikundi rasmi vya uzalishaji mali kama AMCOS,VICOBA  pamoja na SACCOS, ndani ya Banda la Shirika hilo
 katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Profesa Godius Kahyarara akitoa ufafanuzi wa shughuli mbalimbali zitolewazo na shirika hilo mapema leo mbele ya Waaandishi wa Habari (hawapo pichani) wndani ya Banda la Shirika hilo 
katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

PROPERT INTERNATIONAL LIMITED YAWAHIMIZA WALIMU, WAUGUZI DAR KUCHANGAMKIA FURSA YA VIWANJA

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

PROPARTY International Limited imewahimiza watumishi wa umma na hasa walimu na wauguzi katika Mkoa wa Dar es Salaam kuchangamkia fursa ya kujipatia viwanja kwa bei nafuu.

Tayari Proparty International Limted imesema kuanzia Julai mwaka jana wameuza viwanja kwa watumishi wa kada hizo wapatao 2000 lakini imeendelea kuwahimiza kuchangamkia fursa hiyo kupitia mradi maalumu wa viwanja ambao umetengwa kwa ajili yao.

Hayo yamesemwa na Meneja Mauzo na Masoko Leila Maingu wakati anazungumzia kuhusu miradi mbalimbali ya viwanja ambayo wanayo kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanapata nafasi ya kumiliki kiwanja ambacho kimepimwa na kilicho maeneo sahihi kwa makazi.

Akizungumza akiwa kwenye banda lao katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam Maingu amesema kuwa wanayo miradi mingi ya “Tunawashauri walimu na wauguzi wa Mkoa wa Dar es Salaam kuchangamkia fursa ya unafuu wa bei ya viwanja vyetu.Watapa viwanja kwa gharama nafuu kwani kuna punguzo la bei kwa ajili yao.

“Tangu tuanze kuuza viwanja kwa ajili ya watumishi hao kwa mkoa wa Dar es Salaam muamko umekuwa mkubwa kwani wengi wamenunua.“Hata hivyo tunaendelea kuwasisitiza walimu na wauguzi ambao bado hawajununua viwanja waje na tutazungumza nao, lengo letu ni kuona watumishi wetu wanakuwa kwenye makazi salama,”amefafanua.
Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Property International Tanzania Leila Maingu akifafanua jambo kwa mwandishi wa habari wakati akizungumza kuhusu uuzaji wa viwanja katika miradi mbalimbali hapa nchini kutoka Kampuni hiyo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Property International Tanzania Bw. Masoud Alawi akizungumza jambo na Meneja Mauzo na Masoko Leila Maingu katika banda la kampuni hiyo lililoko kwenye viwanja vya TANTRADE Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam ambapo maonyesho ya biashara ya Sabasaba yanaendelea
Mmoja wa wafanyakazi akiwahudumia wananchi waliotembelea katika banda hilo.
Meneja Mauzo na Masoko Leila Maingu paoja na wafanyakazi wenzake wakiwahudumia wananchi mbalimbali waliofika kwenye banda hilo.

KIGWANGALLA ATOA ONYO KALI KWA WANAOCHIMBA MADINI KWENYE MSITU WA HIFADHI JIJINI MBEYA,

$
0
0
Na Hamza Temba, Mbeya

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ametoa onyo kali kwa wananchi wanaojihusisha na vitendo vya uchimbaji wa mchanga wa madini ya dhahabu (makinikia) ndani Hifadhi ya Msitu wa Palamela katika wilaya ya Chunya mkoani Mbeya.

Amesema sheria za uhifadhi na mazingira hazihusu mtu yeyote kuchimba madini katika maeneo yaliyohifadhiwa kisheria bila ya kuwa na kibali maalum kutoka mamlaka husika.Ametoa onyo hilo jana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mwaoga, wilaya ya Chunya mkoani Mbeya baada ya kukagua na kuona uharibifu mkubwa uliofanywa na wachimbaji hao kwenye hifadhi hiyo.

"Yeyote anayehitaji kuchimba madini kwenye maeneo ya hifadhi ni sharti afuate taratibu za kisheria ikiwepo kupewa kibali halali cha kufanya kazi hiyo, la sivyo tutakaowakamata tutawachukulia hatua kali za kisheria" alisema Waziri Kigwangalla.

Ili kudhibiti vitendo hivyo visiendelee, Waziri huyo ameagiza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kuweka kituo cha kudumu cha ulinzi katika eneo hilo ili kuwazuia wananchi watakaojitokeza kufanya shughuli hizo za uharibifu wa hifadhi hiyo.

Amesema, amebaini kuwa maeneo mengi makubwa ya uchimbaji wa madini katika wilaya hiyo yamemilikishwa matajiri wachache hali inayosababisha wananchi wa kawaida kukosa maeneo ya uchimbaji na hivyo kulazamika kuingia kwenye maeneo ya hifadhi.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na viongozi wengine wa Mkoa wa Mbeya akiwemo Mkuu wa Mkoa huo, Amos Makala wakitembea mwendo wa mchakamchaka alipokuwa akikagua eneo la Hifadhi ya Msitu wa Palamela wakati wa ziara yake ya kikazi ya kutatua changamoto za uhifadhi katika wilaya ya Chunya mkoani Mbeya jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makala wakikagua eneo lililoharibiwa kwa kuchimbwa mchanga wa dhahabu (makinikia) kinyume cha sheria ndani ya Hifadhi ya Msitu wa Patamela katika wikaya ya Chunya mkoani Mbeya jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua mchanga wa dhahabu (makinikia) ambao umetaifishwa na Serikali baada ya kuchimbwa kinyume cha sheria ndani ya Hifadhi ya Msitu wa Patamela katika wikaya ya Chunya mkoani Mbeya jana. Wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Amos Makala.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makala wakati wa ziara yake ya kikazi ya kutatua changamoto za uhifadhi kwenye Hifadhi ya Msitu wa Patamela katika wilaya ya Chunya mkoani Mbeya jana.

TIMU 16 BORA ZA SPRITE BBALL KINGS KUPIGWA JUMAMOSI NA JUMAPILI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Droo ya hatua ya 16 bora ya michuano ya Sprite BBall Kings imefanyika jana usiku moja kwa moja na kila timu kumfahamu mpinzani wake ikishuhudiwa na viongozi wa Shirishiko la Mpira wa Kikapu Nchini.

Timu 16 zilifanikiwa kuingia hatua hiyo baada ya kucheza mechi za mchujo mwishoni mwa wiki katika Viwanja vya JMK Youth Park zikiwa timu 50 kutoka sehemu tofauti za Jijini Dar es Salaam.Manahodha wa timu zilizofanikiwa kuingia hatua ya 16 bora wamejitapa kuondoka na ushindi kila mmoja akimtaka mpinzani wake ajipange.

Kwa upande wa Nahodha wa timu ya Mchenga BBall Stars Mohamed Yusuph ambaye timu yake itapambana na Oysterbay amesema kuwa hiyo ni mechi nzuri na itakayokuwa na ushindani mkubwa sana.Nahodha wa Portlands Denis Babu akishika nafasi ya pili ya ufungaji akiwa na Pointi 19 amesema kuwa mechi yake dhidi ya Mbezi Beach KKKT itakuwa ni mechi ngumu sana kwani hawafahamu vizuri na hata wachezaji wake wengi hajawafahamu ila anaamini ushindani utakuwa ni mkubwa.

Manahodha mbalimbali walitambiana huku wengine wakiweka wazi kuwa hawakuwa tayari kukutana na bingwa mtetezi Mchenga BBall Stars kwani wanaamini safari yao ya kwenda hatua ya nane bora ingekuwa ngumu sana.Mechu nne za kwanza zitachezwa siku ya Jumamosi katika Viwanja vya Air Wing Ukonga ikizikutanisha timu za Fast Heat dhidi ya DMI, Flying Dribblers na Ukonga Heatmen, St Joseph dhidi ya Airwing pamoja na Mbezi Beach KKKT akichuana na Portland.

Siku ya Jumapili mechi zingine nne zitachezwa kwenye Viwanja vya Bandari Kurasini zikiwakutanisha Mchenga BBall Stars dhidi ya Oysterbay, Stylers akipambana na Temeke Heroes, Mechi nyingine ni Ukonga Warriors dhidi ya The Team Kiza na mchezo wa mwisho utakuwa ni mpambano baina ya Raptors akichuana na Water Institute.Michuano ya Sprite BBall Kings 2018 yanayodhamiwa na kinywaji cha Sprite yameanza mwishoni mwa wiki kwa hatua ya mchujo kufanyika, timu 16 kufanikiwa kuvuka na zinaenda kukutana siku ya Jumamosi.

Mshindi wa kwanza atafanikiwa kuondoka na kitita cha Milioni 10 pamoja na Kombe, Mshindi wa pili milioni 3 na mchezaji bora wa mashindano akitwaa milioni 2 .



KAMPUNI YA FOSUNPHARMA YA CHINA KUJENGA KIWANDA CHA DAWA ZA BINADAMU NCHINI

NHC YALETA NYUMBA ZA BEI NAFUU KWENYE MAONESHO YA SABASABA

$
0
0

Sehemu ya Banda la Shirika la Nyumba la Taifa NHC Linavyonekana kwa nje kwenye Maoneshoi ya Biashara ya 42 Sabasaba yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Afisa Mauzo Mwandamizi wa shirika la Nyumba la Taifa NHC Joseph Haule akitoa maelezo juu ya kazi na miradi inayofanywa na shirika la nyumba katika Maonesho ya 42 ya biashara yanayoendelea  Jijini  Dar es Salaam.
 Ofisa kutoka shirika la nyumba la Taifa akionyesha moja ya nyumba za Ghrama nafuu zinazojengw ana shirika hilo katika Jiji la Dodoma.
 Sehemu ya watu waliofika kwa wingi katika banda la Shirika la nyumba kwenye Maonesho ya 42 biashara yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Maharufu kama Sabasaba.

TIA: IDADI YA WANAOJIUNGA INAONGEZEKA KILA MWAKA

$
0
0

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa TIA , Gorah Abdallah akizungumza katika Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.

Baadhi wa watendaji waliopo katika banda la Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA).
Afisa wa Idara ya Bajeti ya Serikali, Asajile Mwaipopo akizungumza na wananchi waliotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Idara ya Bajeti ya Serikali, Boniface Kilindimo
 Ofisa wa Idara ya Bajeti ya Serikali wa Wizara ya Fedha na Mipango, Boniface Kilindimo akitoa ufafanuzi kuhusiana na bajeti inavyopangwa kwa mwananchi aliyetembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere. Kushoto ni Afisa wa Idara ya Bajeti ya Serikali, Asajile Mwaipopo

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kimesema kuwa idadi ya wanaojiunga katika Taasisi hiyo imekuwa ikiongezeka kila mwaka wa masomo kutokana na usimamiaji wa misingi ya taaluma wanayoitoa.

Akizungumza katika Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere (Sabasaba), Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Taasisi hiyo, Gorah Abdallah amesema kuongezeka kwa idadi hiyo kunailazimu taasisi kuongeza miundombinu ya majengo ili kuendana na mahitaji yaliyopo.

Amesema moja ya mafanikio ya Taasisi hiyo ni wahitimu kupata kazi moja kwa moja kutokana na kuwa na taaluma bora ya kutumika na taasisi mbalimbali za serikali na binafsi.

Abdallah amesema wameweka mpango mkakati wa miaka mitano unaoanzia 2019/23 ikiwa moja ya mkakati huo ni kufanya utafiti kwa wajasiriamali waliopo nchini ili kurasimisha ujasiriamali huo.

Aidha amesema kuwa wahitimu katika taasisi hiyo ni kuwa na taaluma ya ujasirimali katika kupunguza changamoto ya ajira.

Amesema Taasisi hiyo inakwenda na mitaala ya kimataifa ili waweze kufanya kazi kwa weledi.

Gorah amesema kuwa wamejenga jengo la ghorofa saba litalochukua wanafunzi 3500 kwa wakati mmoja ambalo linatarajia kumalizika Septemba 2018 na ujenzi wa Kampasi ya Mtwara umeshakamilika na wako katika maandalizi ya kuhamia katika majengo yao na kuachana kupanga.

KIWANDA CHA DAWA KIKUBWA KUJENGWA NCHINI.

$
0
0
NA WAMJW-DAR ES SALAAM 

KIWANDA kikubwa cha kutengeneza dawa kinatarajiwa kujengwa nchini ili kupunguza adha na gharama zinazoikumba nchi wakati wa kuagiza dawa nje ya Tanzania. 

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa kujadili uwekezaji wa kiwanda cha dawa hapa nchini leo jijini Dar es salaam. 

"Leo tumekutana kujadili jinsi ya kuwekeza na kiwanda cha kutengeneza dawa cha FOSUN PHARMA kutoka nchini ili kupunguza changamoto za kuagiza dawa nje ya nchi na kutokomeza tatizo la upatikanaji wa dawa nchini", alisema Waziri Ummy .
 
 Aidha Waziri Ummy amesema kuwa kutokana na kujengwa kwa kiwanda hiko kitapunguza asilimia kubwa ya fedha inayokwenda nje kwa ajili ya manunuzi ya dawa kwani mpaka sasa asilimia 94 ya fedha zinakwenda kununua dawa nje na asilimia 6 ndiyo inannua dawa nchini. 

Waziri Ummy amesema kuwa kutokana na uwekezaji huo kutapelekea kupunguza muda wa kuagiza dawa kwani muda mwingine kunachukua miezi 9 mpaka miezi 11 kupata dawa kutoka nje ya nchi hivyo kuifanya Serikali kuagiza mzigo mkubwa zaidi ili kukimbizana na mahitaji ya Watanzania. 

"Tunatumia mda mrefu sana kupata dawa tangu tunapoagiza na wakati mwingine tunaweza kupata dawa zisizo na ubora kutokana na dawa hizo zinakaguliwa na mdhibiti wa nje hivyo zinaweza zikaruhusiwa tu na zikija kukaguliwa na mdhibiti wa ndani unaweza kukuta hazina ubora" alisema Waziri Ummy. 

Picha ya Wadau wa Masuala ya Uwekezaji na Masuala ya Afya, ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage katika Kikao cha kujadili Uwekezaji wa Kiwanda cha kutengenezea Dawa nchini na Kampuni ya Fosun Pharma kutoka nchini China.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akijadili jambo na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage katika Kikao cha kujadili Uwekezaji wa Kiwanda cha kutengenezea Dawa nchini na Kampuni ya Fosun Pharma kutoka nchini China.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisisitiza jambo mbele ya Wadau wa Masuala ya Uwekezaji na masuala ya Afya wakati akiwa katika Kikao cha kujadili Uwekezaji wa Kiwanda cha kutengenezea Dawa nchini na Kampuni ya Fosun Pharma kutoka nchini China.
Picha ya Pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage baada ya kikao cha kujadili Uwekezaji wa Kiwanda cha kutengenezea Dawa nchini na Kampuni ya Fosun Pharma kutoka nchini China.


MKEMIA MKUU WA SERIKALI ATEMBELEA MAONESHO YA KIMATAIFA YA BIASHARA (SABA SABA)

$
0
0
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kushoto) akimsikiliza Meneja Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Bi. Gaudensia Simwanza, mara baada ya kutembelea banda hilo kwenye viwanja vya Maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Saba Saba) leo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Profesa Joseph Bushweishaija (kushoto) akisalimiana na Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (katikati) mara baada ya Mkemia Mkuu wa Serikali kufika kwenye ofisi za Mamlaka hiyo zilizopo kwenye viwanja Saba Saba, Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam leo. kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Bw. Edwin Rutageruka (aliyevaa tai nyekundu)
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kushoto) akiongea na watumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) baada ya kuwatembelea kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Saba Saba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (aliyevaa suti) akimsikiliza mtumishi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alliyekuwa anamuelezea kuhusiana na uhifadhi wa mambo ya kihistoria ya kwenye vitabu kupitia muziki na makala za video alipotembelea banda la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. 

TAASISI ya House Of Vision (VHV) YANG'ARA SABASABA NA FURSA YA KUINUA VIJANA KIUCHUMI

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Globu  ya Jamii

TAASISI ya House Of Vision (VHV) inayojihusisha na ujasiriamali imejizatiti kutumia msimu huu wa sabasaba kuwasaidia vijana kutengeneza uchumi wao binafsi kutokana na ujuzi unaotolewa na taasisi hiyo.

Akizungumza na Michuzi Blog Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo bi. Zena Mulokozi ameeleza kuwa taasisi hiyo inatoa elimu ya ujasiriamali, ufugaji, mafunzo ya biashara na kujiajiri sambamba na utoaji mkopo wa fedha taslimu na vitendea kazi.
Bi. Zena emeeleza kuwa vifaa vitolewavyo kwa wanachama kama mkopo ni pamoja na pikipiki, mashine ya juice za miwa, bajaji, viwanja na mashamba.Aidha ameeleza kuwa taasisi hiyo inatoa mafunzo ya ufugaji wa kuku wa kienyeji na kisasa.
Katika maadhimisho haya ya sabasaba bi. Zena amewaomba vijana na watu wa kada mbalimbali kutumia fursa hii kujisajiri kwa vikundi kuanzia watu 15 hadi 30 na kusajiliwa katika banda lao.

Mkurugenzi wa taasisi ya ujasiriamali ya House of vision bi. Zena Mulokozi akizungumza na Michuzi Blog kuhusiana na fursa za ujasiriamali kwa vijana.

JUMA SHAROBARO ATANGAZA OFA YA STAR TIMES MSIMU HUU WA SABASABA

UZINDUZI WA KITABU CHA DKT. REGINALD MENGI

Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images