Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110114 articles
Browse latest View live

TAARIFA KWA WAAJIRI: UWASILISHAJI WA MICHANGO KATIKA MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI KWA NJIA YA MTANDAO

$
0
0
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) unapenda kuwataarifu Waajiri wote Tanzania Bara na Umma kwa ujumla kwamba, huduma mpya ya uwasilishaji wa michango kwa njia ya mtandao kupitia mfumo wa malipo wa kielektroniki wa Serikali (Government Electronic Payment Gateway) inaanza kutumika rasmi kuanzia tarehe 1 Julai, 2018. 

Huduma hii, pamoja na kurahisisha ulipaji wa michango, itamwezesha Mwajiri kupata stakabadhi ya kielektroniki na kumbukumbu za mtiririko wa michango yake.

Kutumia huduma hii, mwajiri atatakiwa kufungua akaunti ya mtumiaji kwa kuingia kwenye tovuti ya Mfuko (www.wcf.go.tz) na kubofya ‘‘on line services’’ (huduma za kimtandao).
Baada ya kufungua akaunti ya mtumiaji, Mwajiri atatakiwa kufanya yafuatayo;

1.Kuhakiki taarifa za Mwajiri pamoja na kuambatisha taarifa za Wafanyakazi;
2.Kulipa michango baada ya kupata namba ya udhibiti (control number) kupitia;
i.Benki za NMB na CRDB.
ii.Huduma za kifedha za mitandao ya simu kwa kupiga namba *152*00#.
iii.Njia ya kielektroniki ya kuhamisha fedha (Electronic Money Transfer) kutoka Benki anayotumia Mwajiri kwenda katika akaunti za Mfuko zilizopo NMB na CRDB. 

Kwa mawasiliano zaidi tafadhali piga simu kwenye kituo chetu cha huduma kwa wateja (namba za simu ambazo ni bure 0800110028/0800110029) au tuma ujumbe wa barua pepe (helpdesk@wcf.co.tz). Aidha, Waajiri wote wanakaribishwa kutembelea banda la WCF lililopo katika Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl. J.K.Nyerere (Saba Saba) kwa wakati huu ambapo maonesho yanaendelea. 

Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu,
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF),
S.L.P 79655, Jengo la GEPF,
Barabara ya Bagamoyo,
DAR ES SALAAM.

RAIS DKT. MAGUFULI AZINDUA KITABU CHA DKT. REGINALD MENGI

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 02 Juni 2018, amezindua kitabu chenye historia ya maisha ya Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dkt. Reginald Abraham Mengi kinachoitwa I CAN, I MUST I WILL jijini Dar es Salaam.

Mhe. Rais Dkt. Magufuli amewataka wafanyabiashara nchini kuiga mfano wa Dkt Mengi na kupuuza maneno ya baadhi ya watu wanaowakatisha tamaa kwani hakuna Serikali yoyote duniani iliyopata maendeleo bila ya kushirikiana na sekta binafsi. Amesema hata Serikali imekuwa ikikatishwa tamaa katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kama vile ujenzi wa Reli ya Kisasa, utoaji elimu bila malipo, ununuzi wa ndege mpya saba na ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa Stiglers Gorge na mingine mingi.

Pamoja na kukatishwa tamaa huko na baadhi ya watu wasioitakia nchi maendeleo Serikali haikukata tamaa na imekuwa ikiendelea na utekelezaji wa miradi yake kwa lengo la kuwaletea watanzania maendeleo.

 ‘’Ninachotaka kuwaambia Wafanyabiashara wa Tanzania na watanzania kwa ujumla ni kuwa kitabu cha Mzee Mengi kiwe fundisho kwetu sote tunaweza kwelikweli,na mimi napenda nitoe wito kwa wafanyabiashara wote nchini ninarudia wito wangu msisikilize maneno ya watu wanaowakatisha tamaa fanyeni biashara zenu kwelikweli, wekeni uwekezaji wenu wote hakuna Serikali inayoweza kuendelea bila kutegemea sekta binafsi’’ amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amesema watanzania wakiamua wanaweza kwani Dkt. Mengi alizaliwa katika familia masikini lakini kwa kuwa aliukataa umasikini ameweza kufikia maendeleo aliyonayo hivi sasa na hivyo kuwataka watanzania wote kujiamini na kuukataa umasikini kwani tunaweza.

Aidha Rais Magufuli amewataka Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini kuwahamasisha wafanyabiashara katika nchi zao kuja kuwekeza hapa nchini kwani Tanzania ni sehemu salama kwa uwekezaji. Amesema katika historia ya mzee Mengi yapo mengi amekutana nayo ya kumkatisha tamaa lakini yeye hakukata tamaa bali aliamini anaweza na akaamua kufanya  na akaweza hivyo watanzania tuache kukatishana tamaa ili tuweze kufikia mafanikio ya kweli. Dkt. Magufuli amesema Dkt. Reginald Mengi ni mfanyabiashara wa kuigwa hapa nchini kutokana na jitihada zake mbalimbali katika mchango wa Taifa kwa kuwa chanzo cha ajira kwa watanzania na kulipa kodi kwa serikali inayokwenda kutoa huduma mbalimbali kwa watanzania wote.

Kwa upande wake Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi amempongeza Dkt. Mengi kwa uamuzi wa kuandika historia ya maisha yake na kuonyesha hatua mbalimbali alizopitia hadi kufikia mafanikio aliyonayo kwani ni watu wachache wanaoweza kufanya kitu kama hicho hasa kwa Afrika. Amesema ipo fikra kwamba watu wenye uwezo wa uandishi ni wale wenye taaluma na wasomi katika vyuo mbalimbali lakini Dkt. Mengi amevunja dhana hiyo na kuweza kuandika kitabu hicho.

Nae Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Dkt. Reginald Mengi amemshukuru Rais Dkt. John Pombne Magufuli kwa kukubali kumzindulia kitabu hicho na kuwataka watanzania kutokata tamaa katika kufikia hatua ya maendeleo kwani alichoandika yeye ni uhalisia wa maisha yake tangu akiwa masikini hadi kufikia mafanikio aliyonayo.

Dkt. Mengi amepata msukumo wa kuandika kitabu hicho cha historia ya maisha yake ili kutimiza azma ya marehemu mtoto wake Rodney Mutie Mengi aliyemtaka kuandika kitabu hicho na mambo mengine ambayo atayatimiza kadri awezavyo.

Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
02 Julai, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kitabu chenye historia ya maisha ya Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Abraham Mengi (wa tatu kulia) kinachoitwa I CAN, I MUST, I WILL kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo. Wengine pichani ni Rais Mstaafu, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Prof Rwekaza Mukandala, Mke wa Dkt. Mengi, Jacquline Mengi, Bi. Jane Goodall pamoja na watoto wa Dkt. Mengi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akionyesha kitabu chenye historia ya maisha ya Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Abraham Mengi kinachoitwa I CAN, I MUST, I WILL baada ya kukizindua kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akitoa hotuba yake katika hafla ya uzinduzi wa kitabu chenye historia ya maisha ya Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Abraham Mengi kinachoitwa I CAN, I MUST, I WILL iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP na Muandishi wa kitabu hicho,  Dkt. Reginald Abraham Mengi akizungumza na hadhara iliyofika kwenye uzinduzi wa kitabu chenye historia ya maisha yake.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akimsikilia Binti Wakonta Kapunda ambaye ni mlemavu aliyejishidia kiasi cha Dola elfu 20 kwa kutoa wazo zuri la kibiashara. Rais Magufuli amemuongezea binti hiyo kiasi cha Shilingi Milioni 10. PICHA NA IKULU

TANGAZO LA PUNGUZO LA BEI KWA TRENI YA DELUXE

UZINDUZI SOKO LA TUMBAKU RUVUMA

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe Christina Mndeme (akikagua tumbaku pichani)  amefungua soko la ununuzi wa zao la Tumbaku katika kijiji cha Suruti Wilayani Namtumbo.

Katika ufunguzi huo, Mhe Mndeme amewaasa wakulima kufuata mbinu bora za kilimo zinazotolea na Maafisa ugani  na kuacha tabia ya kuchanganya tumbaku , maji na mafuta kwa lengo la kuongeza uzito.



Mhe Mndeme ameonya Kufanya hivyo ni kosa kwani inaharibu soko la zao ambapo amekitaka chama Kikuu cha Ushirika cha SONAMCU kusambaza pembejeo kwa wakati ili wakulima waweze kuzitumia kulingana na msimu wa Kilimo.
Akihitimisha Hotuba Yake Mhe Mndeme amewataka Wadau wote kutoa ushirikiano kwa wanunuzi wa tumbaku ili biashara iwe endelevu kwa manufaa ya Taifa, na mwananchi aweze kujikomboa kiuchumi.

KAMPUNI YA ASAS YAWEKA KITENGO KUHUDUMIA WATEJA WAKUBWA, TAASISI KATIKA MAONESHO YA BIASHARA SABASABA

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
KAMPUNI ya Asas Dairies Ltd imeweka kitengo maalumu cha kuhudumia wateja wakubwa na taasisi(Corporate Sales Department) kwa lengo la kuhudumia wateja wao wanaofika kwenye banda lao katika Maonesho ya biashara ya kimataifa yanayoendelea viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko na Matukio wa Kampuni ya Asas Jimmy Kiwelu amesema hayo leo wakati anazungumzia huduma mbalimbali ambazo wanazitoa kwenye maonesho hayo ambapo wameamua kuweka eneo maalumu kwa ajili ya kufanya mazungumza na wateja wakubwa na taasisi.
“Tumeamua kuweka kitengo maalumu cha Corporate Sales Department ambacho kazi yake ni kuwahudumia wateja wakubwa na taasisi.Lengo letu ni kuwahudumia wateja wetu wote ambao wanafika kwenye banda letu,”amesema Kiwelu.
Pia amesema wameweka eneo maalumu kwa ajili ya michezo ya watoto kwani wanatambua kuwa watoto baada ya kunywa maziwa ya Asas wanahitaji kupata muda wa kufurahi kwa michezo ya aina mbalimbali.
“Lengo letu kubwa ni kuhakikisha tunawajengea watoto utamaduni wa kupenda kunywa maziwa.Kwa kupitia michezo iliyopo kwenye banda letu watoto watafurahi na wataendelea kukumbuka maziwa bora na halisi ya Asas,”amesema.
Kwa upande wa mmoja wa wafanyakazi wa kitengo cha Corporate Sales Department Elizabeth Balele amesema kuwa kazi nyingine ya kitengo hicho ni kuilezea kampuni hiyo kwa wale ambao wanahitaji kuifahamu zaidi na hasa kuhusu bidhaa zake.
“Pia tunalo jukumu la kuwaelimisha wateja wakubwa ambao wanahitaji uwakala, kununua au kuuza ambao wanahitaji kuuza bidhaa zetu katika maeneo yao husika,”amesema.
4
Meneja wa Masoko na Matukio wa Kiwanda cha ASAS DAIRIERS LTD Bw. Jimmy Kiwelo akizungumza na Mdau wa Maendeleo mkoani Iringa Bw. Fredrick Mwakalebela wakati alipotembelea katika banda la kiwanda hicho kwenye maonesho ya biashara ya Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam leo.
3
Mmoja wa wafanyakazi wa kitengo hicho cha(Coperate Sales Department)Elizabeth Balele akiwa katika eneo lake la kazi tayari kwa kuhudumia wananchi mbalimbali wanaotembelea katika banda la kiwanda hicho.
5
Mmoja wa wafanyakazi wa kitengo hicho cha(Coperate Sales Department)Elizabeth Balele akiwahudumia wananchi mbalimbali waliotembelea katika banda la kiwanda hicho.

MICHUZI TV: SPRITE BBALL KINGS YASHIKA KASI,16 BORA WAPATIKANA

DKT. SHEIN AKUTANA NA UONGOZI WA WIZARA YA NCHI OFISI YA RAIS,KATIBA,SHERIA,UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA ZANZIBAR

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais,Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi wa Mwaka 2017/2018 na Mpango kazi wa Mwaka 2018-2019, kikao hicho kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar.(Picha na Ikulu, Zanzibar.)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Haroun Ali Suleiman alipokuwa akiwasilisha muhtasari wa Utekelezaji wa Mpango kazi wa Mwaka 2017/2018 katika kikao cha siku moja cha Uongozi wa Wizara hiyo kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani), akiwepo na Naibu Waziri Mhe.Khamis Juma Mwalim.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais,Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw.Yakout Hassan Yakout (kulia) alipokuwa akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Mpango kazi wa Mwaka 2017/2018 katika kikao cha siku moja cha Uongozi wa Wizara hiyo kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati).

BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU JULAI 02, 2018


MAMLAKA HIFADHI YA NGORONGORO KULIPENDEZESHA JIJI LA DODOMA

$
0
0
Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Profesa Davis Mwamfupe (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi na Kaimu Meneja Uhusiano Mamlaka Hifadhi ya Ngorongoro, Joyce Mgaya wakisaini hati ya makubaliano ya kuboresha mandhari ya mizunguko ya magari kwenye barabara kuu za jiji hilo. Kwenye uboreshaji huo wa mandhari Mamlaka Hifadhi ya Ngorongoro itaweka vivutio mbalimbali kutangaza utalii.

Na Abuu Kimario

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imeingia makubaliano na Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuboresha mandhari ya mizunguko ya magari (roundabout) kwenye barabara kuu za jiji hilo. Makubaliano hayo yamefikiwa leo kwenye hafla ya fupi ya kutiliana saini ambapo jiji la Dodoma liliwakilishwa na Meya, Profesa Davis Mwamfupe na Mkurugenzi Mtendaji, Godwin Kunambi na upande wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro iliwakilishwa na Kaimu Meneja Uhusiano, Joyce Mgaya kwa niaba ya Mhifadhi Mkuu wa mamlaka hiyo Dkt. Fredy Manongi.

Kwenye makubaliano hayo Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imekubali kuifanyia ukarabati mizunguko mitatu ya magari ambayo ni mizunguko ya barabara kuu za Dar- es-Salaam (Shabiby), Singida na Arusha.

Akiwasilisha salamu za Mhifadhi Mkuu, Kaimu Meneja Uhusiano Mgaya amesema, uongozi wa jiji la Dodoma kuichagua mamlaka hiyo ni heshima kubwa na wanaipokea kwa mikono miwili na pia mamlaka hiyo itaendelea kushirikiana na halmashauri ya jiji kwenye kuibua fursa mbalimbali za kitalii.

Aidha, Mgaya ameongeza kuwa makubaliano hayo yaliyofikiwa ni fursa ya Halmashauri ya jiji la Dodoma na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kubadilishana uzoefu kwenye maeneo ya uhifadhi wa mazingira na kuboresha mandhari.

Kwa upande wake Meya wa Jiji la Dodoma, Mstahiki Davis Mwamfupe amesema nia ya uongozi wa jiji la Dodoma ni kulifanya liwe jiji la mfano wa kuigwa na majiji mengine ya Tanzania, barani Afrika na duniani kwa kuwa na mazingira bora kuishi na mandhari yenye kuvutia.

Nae Mkurugenzi Mtendaji, Godwin Kunambi ameishukuru Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa kukubali ombi la kutengeneza sanamu kubwa ya tembo kama ishara ya kuhifadhi historia ya chimbuko la jina la mkoa wa Dodoma. Kwa mujibu ya maelezo ya wenyeji wa mkoa huo jina Dodoma limetokana na neno la kigogo “idodomya” baada ya tembo kudidimia ardhini miaka mingi iliyopita.

KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YAKAGUA MRADI WA UBORESHAJI BANDARI YA DAR ES SALAAM

$
0
0
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, akitoa ufafanuzi kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu namna Kituo cha Mafuta (KOJ) kinavyofanya kazi, wakati kamati hiyo ilipotembelea bandari ya Dar es Salaam.
Kaimu Meneja wa Kituo cha Mafuta (KOJ), Sixtus Karia akifafanua jambo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu namna meli zinavyopakua mafuta katika kituo cha hicho katika bandari ya Dar es Salaam, wakati kamati hiyo ilipotembelea mradi wa upanuzi wa bandari hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Moshi Kakoso, akitoa maelekezo kwa uongozi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), wakati kamati hiyo ilipofanya ziara bandari ya Dar es Salaam.
Muonekano wa kazi zikiendelea kwenye mradi wa upanuzi wa gati namba 1 mpaka 7 katika bandari ya Dar es Salaam. Mradi huo unahusisha gati mpya ya kuhudumia meli za magari.

SHUGHULI ZA BUNGE ZAELEZWA KWENYE MAONESHO YA SABASABA

BENKI YA TIB CORPORATE YAWATAKA WANANCHI KUTEMBELEA BANDA LAO NDANI YA VIWANJA VYA SABASABA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Benki ya TIB Corporate imewataka wananchii kujitokeza kwenye banda lao lililopo ndani ya maonesho ya 42 ya Sabasaba na kuweza kufungua akaunti za benki hiyo ili waweze kujivunia faida kibao kwa kuweka hela zao Kwenye benki ya  TIB.

Akizungumza na Michuzi Blog Mkurugenzi wa Huduma za Matawi na Masoko wa Benki ya TIB Corporate Theresia Msoka amesema kuwa Benki ya TIB Corporate imezindua aina tofauti nne za akaunti ambazo zitamuwezesha mteja wa benki hiyo kufungua akaunti na kuhifadhi fedha zake kwa uhakika zaidi.

Amesema kuwa benki yao ni ya kibiashara ila inawahudumia wananchi wote wakiwemo watu binafsi, taasisi au makampuni pamoja na kuwawezesha kupata mikopo ya haraka sana kwa ajili ya kufungua au kuendeleza biashara zao ikiwemo viwanda.

Bi Theresia amesema kwa mwaka huu wamekuja na kauli mbili ya "JIPANGE NA TIB CORPORATE BANK" ambao wamewaletea  akaunti nne tofauti zitakazomuwezesha mwananchi kuhifadhi fedha zake na kujipatia riba kubwa zaidi kadri anavyoweka hela ukiweka fedha kwenye akaunti ya Flex inayopatikana ndani ya benki yao.
 Mkurugenzi wa Huduma za Matawi na Masoko wa Benki ya TIB Corporate Theresia Soka akielezea huduma wanazozitoa ndani ya banda lao pamoja na kuwafungulia wananchi akaunti hapo hapo kwenye maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Kibiashara yanayoendelea Katika Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar Es Salaam.
 Meneja wa Fedha wa Benki ya TIB Coorporate June Magingi na  Ofisa huduma kwa wateja  Janeth Burton (kulia) Wakimpatia maelekezo mteja aliyefika katika banda lao la maonyesho lililopo ndani ya Viwanja vya Sabasaba katika maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Kibiashara yanayofanyika Jijini Dar es Salaam.
 Ofisa Masoko wa Kampuni ya Masasi Food Production Secky Nyewa akielezea namna Benki ya TIB ilivyoweza kuwapatia mkopo na kuwezesha kufungua kwa kiwanda hicho kinachotengeneza bidhaa za chakula ndani ya  maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Kibiashara yanayofanyika ndani ya Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi akielezea jambo mbele ya Mkurugenzi wa Huduma za Matawi na Masoko Theresia Soka  wa Benki ya TIB Coorporate (kushoto) na Mkuu wa Utafiti wa Maendeleo ya Benki TIB Coorporate Dr Hildebrand Shayo alipotembelea banda ya benki hiyo ndani ya maonyesho ya 42 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea ndani ya Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.
 Wafanyakazi wa Benki ya TIB Coorporate wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya banda lao la Maonyesho kwenye Viwanja vya Sabasaba maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Kibiashara yanayofanyika Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Matawi na Masoko Benki ya TIB Coorporate Theresia Soka akimuelezea jambo Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi alipotembelea banda la maonyesho la benki ya TIB lililopo ndani ya Viwanja vya Sabasaba  katika maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Kibiashara yanayofanyika Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Utafiti wa Maendeleo ya Benki TIB Coorporate Dr Hildebrand Shayo akimuelezea jambo Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi alipotembelea banda la maonyesho la benki ya TIB lililopo ndani ya Viwanja vya Sabasaba  katika maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Kibiashara yanayofanyika Jijini Dar es Salaam.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE JULAI 3, 2018

MAKAMU WA RAIS AKIWA KATIKA MKUTANO WA UMOJA WA AFRIKA NCHINI MAURITANIA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akichangia maoni ya Tanzania juu ya masuala ya Ulinzi na Amani katika nchi za Burundi, Congo DRC, na Sudan ya Kusini wakati wa mkutano wa kawaida wa 31 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU)mjini Nouakchott, Mauritania.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Jaji wa Mahakama ya Afrika ya Binadamu na Watu Jaji Imani Mkwawa Aboud wakati wa mkutano wa 31 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika mjini Nouakchott, Mauritania. (picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

SSRA YATOA MSAADA KWA WAZEE WA KITUO CHA KUHUDUMIA WAZEE CHA FUNGAFUNGA, MOROGORO

$
0
0
Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Sarah Kibonde Msika,  akimkabidhi sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa SSRA kwa Msimamizi wa Kituo cha kuhudumia wazee cha Fungafunga, Yolanda Mkapa, kilichopo mkoani Morogoro.
Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Sarah Kibonde Msika, akitoa maelezo kuhusu msaada ambao SSRA imeutoa kwa wazee wa Kituo cha Fungafunga, Morogoro hivi karibuni. 
Msimamizi wa Kituo cha kuhudumia wazee cha Fungafunga, Yolanda Mkapa (aliyesimama) akitoa utambulisho na kuwakaribisha wawakilishi wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) ambao walifika katika Kituo cha kuhudumia wazee cha Fungafunga Mkoani Morogoro.
Mzee Joseph Kaniki, Mwenyekiti wa wazee Kituo cha Fungafunga akitoa shukrani kwa niaba ya wazee wenzake baada ya kupokea msaada wa vitu mbalimbali kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA).
Wazee wa Kituo cha Fungafunga wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA).

TBC: Ajali Iliyobadili Ndoto Za Msichana Wakonta Kapunda

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akimsalimia Binti Wakonta Kapunda ambaye ni mlemavu wa kupooza mwili mzima kutokana na ajali aliyejishidia kiasi cha Dola elfu 20 kwa kutoa wazo zuri la kibiashara. Hii ilikuwa ni wakati wa hafla ya uzinduzi wa kitabu cha maisha ya Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dkt. Reginald Abraham Mengi  ukumbi wa hoteli ya Serena jijini Dar es salaam Jumatatu Julai 2, 2018  ambapo Rais Magufuli amemuongezea binti hiyo kiasi cha Shilingi Milioni 10. Fuatilia mkasa wake katika Hadubini ya TBC katika hii video hapo chini.

HOTUBA YA RAIS DKT.JOHN MAGUFULI BAADA YA KUWAAPISHA VIONGOZI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM JUMATATU JULAI 2, 2018

BREAKING NYUZZZZZ.......: RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA BAADHI YA VIONGOZI WAKUU NA VIONGOZI WASTAAFU IKULU DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa na Katibu Mkuu Kiiongozi Balozi John Kijazi akiwasili katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam ili kukutana na kufanya mazungumzo na baadhi ya viongozi wakuu na viongozi wastaafu ambao anakutana nao kwa mara ya kwanza wote kwa pamoja.
Viongozi Wakuu wastaafu wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam tayari kukutana na kuzungumza na mwenyeji wao Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliyewaalika.
Viongozi Wakuu wastaafu wakimsikiliza Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza nao leo.

Naibu Waziri Shonza atoa wito kwa Wasanii Nchini kuhamasisha Utalii wa Ndani

$
0
0
 Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Idara  ya Utalii Hifadhi ya Taifa Ziwa Manyara Bibi. Eva Mallya (kulia) baada ya kuwasili katika  Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara (Lake Manyara National Park) ikiwa ni hatua ya kuhamasisha utalii wa ndani chini ya uratibu wa taasisi ya Tanzania Gospel Artist Network (TAGOANE)  Jijini Arusha.
 Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (wa kwanza kulia) akingalia ramani inayonyesha vivutio mbalimbali pamoja na wanyama wanaopatikana katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara jana Jijini Arusha  wakati wa ziara ya kutembele hifadhi hiyo, wengine ni Rais wa taasisi ya Tanzania Gospel Artist Network (TAGOANE) Dkt. Godwin Maimu (katikati) na kulia ni Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara Bibi. Noelia  Myonga.
 Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kulia) akipokea cover ya tairi la gari lenye nembo  ya  Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara kutoka kwa  Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara Bibi. Noelia  Myonga .
 Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) akisikiliza maelekezo  kutoka kwa Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara Bibi. Noelia  Myonga kuhusu chemchem ya maji moto ambayo inapatikana katika hifadhi  hiyo alipofanya ziara ya kuhamasisha utalii wa ndani kwa wasanii na watanzania kwa ujumla  lengo ni kuwa na utamaduni wa kutembelea vivutio hivyo .
  Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) akiangalia uoto wa asili ambao hupatikana katika Hifadhi ya Taifa ya  ya  Ziwa Manyara wakati wa ziara ya kutembelea hifadhi hiyo  hapo jana Jijini Arusha chini ya uratibu wa Taasisi ya Tanzania Gospel Artist Network (TAGOANE).
Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) akiwashukuru wasanii na wajasiriamali kutoka Jiji la Arusha ambao aliambatana nao katika ziara ya kuhamasisha  utalii wa ndani, iliyoratibiwa na Taasisi ya Tanzania Gospel Artist Network (TAGOANE) lengo ikiwa ni kuwajengea watanzania utamaduni wa kupenda kutembelea vivutio mbalimbali vilivyopo nchini ili kukuza uchumi wa nchi.  ( Picha na Lorietha Laurence-WHUSM,Arusha)

STARIMES YATOA OFA KABAMBE NDANI YA VIWANJA VYA SABASABA

$
0
0


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Kampuni ya Startimes yawataka wananchi  kujitokeza kwa wingi kujipatia ofa kabambe katika banda lao lililopo ndani ya maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya biashara kwenye Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa na Meneja Mahusiano wa Startimes Juma Suluhu Shalobalo alipozungumza na Globu ya Jamii na kuelezea ofa walizonazo ndani ya Viwanja vya Sabasaba ikiwemo punguzo la bei kwa Luninga na Ving'amuzi.

Mbali na hilo Juma amesema kuwa wana ofa nyingine kwa wananchi pindi wanapofika katika banda lao ambapo atakayepiga picha na kombe na kuiweka katika mitandao ya kijamii na na #kuhashtag basi atajipatia zawadi kutoka kampuni ya Startimes.
 Meneja Mahusiano wa Kampuni ya  Startimes Juma Suluhu Sharobaro akizungumza na Michuzi Blog kuhusu ofa walizozitoa ndani ya Sabasaba ikiwemo punguzo la bei kwa bidhaa zao pamoja na ofa kemkem kutoka katika banda lao la Maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara ndani ya Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.
  Mfanyakazi wa Kampuni ya Startimes Lulu Ibrahim akimuonyesha mteja namna ya kuperuzi kwenye simu kwa kumuonyesha APP ya Startimes inayopatikana katika simu za Smartphone zitakazomuwezesha mtumiaji kufuatilia vipindi vyote kiganjani kwake alipotembelea  banda lao ndani ya maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea Kwenye Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar Es Salaam.
 Mfanyakazi wa Kampuni ya Startimes Martha Masota akimuhudumia mteja alipotembelea  banda lao ndani ya maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea Kwenye Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar Es Salaam.
Mfanyakazi wa Kampuni ya Startimes Martin Emanuel akimuonyesha mteja aina ya king'amuzi kinachoweza kutumia Solar Energy alipotembelea  banda lao ndani ya maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea Kwenye Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar Es Salaam.
Viewing all 110114 articles
Browse latest View live




Latest Images