Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110031 articles
Browse latest View live

WATANZANIA CHANGAMKIENI KUSHIRIKI TAMASHA LA KIMATAIFA LA TUBINGEN,UJERMANI

$
0
0

Habari njema kwa Watanzania wapenda maendeleo kwa fursa kubwa huko ughaibuni katika tamasha kubwa la kimataifa linaloitwa Afrobeats Summer Festival litakalofanyika Tubingen nchini Ujerumani. 
Mratibu wa tamasha hilo nchini, Shamsa Danga, amesema, hii ni kwa wale wote wenye nia ya dhati ya kukutana na wadau na wawekezaji wa Ujerumani kwa lengo la kupanua wigo wa kibiashara kimataifa katika nyanja zote ikiwemo sanaa ya muziki, uchongaji, uchoraji na ngoma za asili. 
Tamasha hilo litakalochukua siku nne kufanyika kuanzia Agosti 9-12 mwaka huu, litahusisha mambo mbalimbali yanayotoa fursa kwa fani zote zitakazopata wahusika. 
Ndio maana msisitizo mkubwa umewekwa kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi kushiriki. 
Aidha, tamasha hilo linawakaribisha watu binafsi, taasisi, makampuni, wajasiriamali, wakulima, wafanyabiashara na wadau wa kada mbalimbali. 
Kwa watakaokuwa tayari na kutaka maelezo zaidi wapige simu namba +255713 457743 (Shamsa Danga) au +491715176779 au watembelee: www.gabs-germany.com

RAIS AAGIZA SH. MILIONI 308 ZA MAADHIMISHO YA SIKU YA MASHUJAA ZITUMIKE KUBORESHA BARABARA

$
0
0
 RAIS Dkt. John Magufuli ameagiza sh. milioni 308 zilizotengwa kwa ajili ya Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa, zitumike kuboresha  miundombinu ya barabara jijini Dodoma.

Ametaja miundombinu hiyo ni pamoja na taa za kuongezea magari  katika barabara ya Kisasa na taa za barabarani kwenye barabara mpya ya Emmaus-African Dream yenye urefu wa kilomita 1.4, ambayo kwa sasa inajengwa kwa kiwango cha lami.


Taarifa hiyo imetolewa na Waziri Mkuu leo (Ijumaa, Juni 29, 2018), wakati akizindua kituo cha polisi kinachohamishika katika hafla iliyofanyika eneo la Kisasa, jijini Dodoma. Kila ifikapo Julai 25 ya kila mwaka Tanzania huadhimisha siku ya mashujaa. 

“Sasa kutokana na msongamano uliopo ambao unaweza kusababisha ajali, Mheshimiwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Magufuli ameamua fedha zote zilizoandaliwa kwa ajili ya maadhimisho hayo zitumike kuboresha barabara,” amesema

Waziri Mkuu amesema Rais Dkt Magufuli anawataka  Watanzania wote waadhimishe siku hiyo ya kumbukumbu ya mashujaa kwa kufanya usafi katika  maeneo yaliyo jirani na makazi yao pamoja na yale ambayo wamezikwa mashujaa ikiwa ni njia ya kuwaenzi.


Kufuatia uamuzi huo, Waziri Mkuu amewaagiza Wakuu wa Mkoa waratibu zoezi hilo kwenye maeneo yao.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameliagizaJeshi la Polisi  lianze kujikita kwenye matumizi ya mifumo ya kiulinzi ya kielektroniki yaaniCity Surveillance Sytemsili limudu kudhibiti hali ya sasa ya uhalifu. 

Amesema kutokana na kuwepo kwa mapinduzi makubwa ya kiteknolojia duniani, hususani kwenye nyanja mbalimbali ikiwemo eneo la ulinzi wa raia na mali zao, hivyo ni wakati muafaka sasa kwa Jeshi la Polisi lianze kutumia teknolojia za kisasa.

“Usimikaji wa mifumo hiyo si tu utasaidia kupunguza uhalifu na kuongeza usalama wa wananchi na mali zao lakini pia utaongeza imani kwa wafanyabiashara na watalii wanaotembelea nchi yetu,” amesema.

Pia Waziri Mkuu amewasisitiza wakazi wa eneo hilo kukitumia vizuri kituo hicho ni kwa kupeleka taarifa za uhalifu. “Aidha, naomba niwasisitize kituo hiki ni cha muda, hivyo  uongozi wa eneo hili ni lazima uje na mkakati wa kupata kituo cha kudumu,”.

Ufunguzi wa kituo hicho ambacho ni kati ya vituo vitano vilivyogharimu sh. milioni 250 vilivyotolewa na Benki ya Equity mkoani Dodoma; umehudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni.

Wengine ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Vijana, Ajira, Kazi na Wenye Ulemavu, Anthony Mavunde, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Giles Mroto na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Equity, Joseph Iha.

HOTUBA YA MHESHIMIWA KASSIM M. MAJALIWA (MB.), WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, WAKATI WA KUAHIRISHA MKUTANO WA 11 WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA TAREHE 29 JUNI 2018

$
0
0
UTANGULIZI

Shukrani
  1. Mheshimiwa Spika,awali ya yote namshukuru sana Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutufikisha siku hii ya leo tukiwa na afya njema ambapo tunahitimisha Mkutano wa 11 ulioanza Jumanne tarehe 3 Aprili 2018.

  1. Mheshimiwa Spika,nakushukuru wewe binafsi, Mheshimiwa Naibu Spika, Waheshimiwa Wenyeviti wa Bunge na Waheshimiwa Wabunge wote kwa kushiriki kikamilifu katika mkutano huu tangu tulipoanza vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge na baadaye Mkutano wa Bunge. Katika mkutano huu, tumeweza kutekeleza kikamilifu wajibu wetu wa Kikatiba kwa kujadili na kupitisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2018/2019. Mtakubaliana nami kuwa Bajeti hii inatoa mwelekeo mzuri wa utekelezaji wa ahadi mbalimbali za Serikali kwa wananchi, kama zilivyoainishwa kupitia Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015 – 2020 pamoja na maelekezo ya Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akifungua rasmi Bunge la Kumi na Moja tarehe 20 Novemba 2015.

Salamu za Pole
Mheshimiwa Spika, tarehe 26 Mei, 2018 Bunge lako tukufu lilipokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mheshimiwa Kasuku Samson Bilago, aliyekuwa Mbunge wa Buyungu, Kigoma. Nitumie nafasi hii kukupa pole wewe binafsi Mheshimiwa Spika, Bunge lako tukufu, Mke, Watoto, familia ya marehemu na wananchi wote wa Buyungu kwa kumpoteza mwakilishi wao huyo aliyekuwa na mchango mzuri kwenye Bunge letu tukufu.Vilevile, nitumie fursa hii kutoa salamu za pole kwa Mheshimiwa Stephen Hillary Ngonyani Mbunge wa Korogwe Vijijini na Mheshimiwa Angelina Sylvester Mabula, Mbunge wa Ilemela, Mwanza, kwa kufiwa na wenza wao.
Kusoma hotuba yote BOFYA HAPA

Michuzi TV LIVE: International conference on planning and development 2018

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JUNI 30, 2018

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA NAIBU KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed ambapo walikutana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mohammed V mjini Casablanca Morocco,Makamu wa Rais alikuwa njiani kuelekea nchini Mauritania ambako mkutano wa 31 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika . (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)​

BARAZA LA UUGUZI LAWATIA HATIANI WAUGUZI WAKUNGA SITA

$
0
0
Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) limewakuta na hatia na kuwapa karipio kali la maandishi Wauguzi Wakunga sita katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa kushindwa kutimiza majukumu yao ya kitaaluma wakati wakitoa huduma kwa mgonjwa.
Katika kikao chake cha 193 kilichofanyika tarehe 28 Juni, 2018 katika Ofisi za Baraza hilo zilizopo Kibaha, Mkoani Pwani, chini ya Mwenyekiti wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Bw. Abner Mathube, lilisikiliza shauri la ukwiukwaji wa maadili ya kazi lililotokea katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro ambapo mama mjamzito alilalamika kutokupatiwa huduma stahiki alipowasili hospitalini hapo hali iliyosababisha mama kukosa mtoto.
Pamoja na karipio hilo, Wauguzi Wakunga wameonywa kuwa endapo watarudia kosa hilo, Baraza la Wauguzi na Ukunga Tanzania, halitasita kuwachukulia hatua kali zaidi za ikiwemo kuwafutia usajili.

Akizungumza na wanahabari, Msajili wa TNMC Bi. Agnes Mtawa amesema katika kikao hicho, Baraza limejadili suala la baadhi ya watu wanaogushi vyeti na leseni za taaluma ya uuguzi na ukunga ambapo limebaini kuwa katika robo mwaka Aprili-Juni, 2018 watu watano walitambuliwa kugushi vyeti na leseni hivyo wamepelekwa kwenye vyombo vya dola ili hatua stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao.
Aidha, Baraza limewabaini watu 15 wanaojitambulisha kuwa ni wauguzi lakini kanzi data ya Baraza hilo imeonesha kuwa vyeti hivyo siyo halali na leseni wanazotumia ni za kugushi. Kwakuwa watu hawa wapo mikoa mbalimbali hapa nchini Baraza linawataka kujisalimisha mara moja kabla halijawafuata huko waliko.
Baraza linatoa onyo kali na kuwataka watu wanao ghushi vyeti na leseni za kitaaluma ya Uuguzi na Ukunga kuacha kuacha tabia hiyo mara moja kwani hatua kazi zitachukuliwa dhidi yao ikiwemo kufikishwa kwenye vyombo vya dola.

Katikati ni Mwenyekiti wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) Bw. Abner Mathube akiongoza kikao cha baraza hilo Kibaha, Mkoani Pwani. Kushoto kwake ni Msajili wa Bazara Bi. Agnes Mtawa

Dawa za kulevya zilivyopoteza ndoto yangu ya kuzaa - Leija

$
0
0

Msichana Leija Chawe, muathirika wa dawa za kulevya kwa takribani miaka 15  anasimulia. Kisa kilichomkuta baada ya kutumia dawa za kulevya. Ni katika maadhimisho ya kitaifa ya kupiga vita dawa za kulevya duniani ambayo nchini Tanzania kitaifa yaliyofanyika Mkoani Iringa.

 Anatokea katika kituo cha kusaidia waathirika wa dawa hizo cha Mtwivila Iringa ( Iringa Sobber House). 

Nilianza kutumia dawa za kulevya nikiwa na umri wa miaka 15 tu, wakati huo nikiwa kidato cha pili.
Nilianza kwa kutumia bangi, nikafuatia Heroine na baadae nikaja kutumia dawa za kulevya aina ya Cocaine.
Nilijingiza kutumia dawa za kulevya kupitia mwanaune ambaye alikuwa Boyfriend wangu. Nilivuta madawa wakati wa muda wa masomo, baada ya muda wa masomo na kabla ya kulala.

Lakini namshukuru mungu leo ameweza kunisaidia nikasimama mbele za watu, wakati natumia dawa hizi nilikuwa sitambuliki, nilikuwa nanyanyapaliwa, kutengwa, nilikuwa nikiitwa majina mbalimbali kama mteja, changudoa na majina mengine ambayo hayafai katika Jamii.

 Nilikuwa nikilala makaburuni na wakati mwingine nje ya maduka. Nilikuwa nikifanya kazi mbalimbali ambazo hazifai kwa mtoto wa kike, nilikuwa nikizika watoto wachanga wanaofariki mahospitalini, nilichimba makaburi na kukaa makaburini nikisubiri watu wanaokuja kuloga usiku kwa ajili ya kiwazindika mazindiko yao. 

Nilikuwa nikipita sehemu mbalimbali kufanya matukio ya kuiba, kukaba na kufanya vitu vingine ambavyo havifai katika Jamii. Nilitengwa na familia na Mimi pia nilijitenga nayo na Jamii nzima kwa ujumla kwani nilikuwa mchafu, nilikuwa siogi kwa wakati, nilikuwa naoga kwa wiki mara moja saa nyingine ilikuwa inapita mwezi bila kuoga.

Madhara makubwa niliyoyapata kwa kutumia dawa za kulevya ni pamoja na kuharibu kizazi changu na kupoteza kabisa uwezo wa  kuja kuzaa na mimi siku moja kuitwa mama.
Mtoto wa kike unapotumia dawa za kulevya inakufanya usipate hedhi vizuri kila mwezi, hii ilinipelekea kuharibu kizazi changu na kuharibu vitu vingine katika mfumo wangu wa uzazi, lakini namshukuru mungu siku ya leo nimekaa hapa mbele yenu ni mzima na ninaendelea vizuri na ninaishi bila ya kutumia dawa za kulevya.

Nawaasa watoto wa kike wenzangu, mimi sikupenda kutumia dawa  za kulevya ilinitokea kwa sababu ya kufuata mkumbo wa mwanaume nilijikuta nikijiingiza kwenye kuvuta bangi kisha heroine na cocaine, nasikitika sana ninapoona vijana wenzangu hadi sasa wanatumia dawa za kulevya. Nawaambia vijana wenzangu maisha bila ya dawa za kulevya inawezekana,

SUMATRA YAANZA KUTEKELEZA AGIZO LA NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI NA MAWASILIANO

$
0
0
Na EmanuelMadafa,Mbeya.

MAMLAKA ya Udhibiti na Usafirishaji wa Nchi Kavu na Reli, (SUMATRA),imeanza kutekeleza agizo la Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi . Atashasta Nditiye,ambalo lilielekeza kuanza kutoa elimu kwa wadau na watumiaji usafiri njia ya reli ili kupunguza vitendo vya uhujumu uchumi vinavyofanywa na watu ambao si waadilifu.

Akizungumza Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya Mdhibiti na Mkaguzi wa Usalama wa Reli, kutoka Mamlaka ya Udhibiti SUMATRA, Mhandisi . Hanya Mbawala,amesema tayari Mamlaka hiyo imenza kutekeleza agizo la Waziri ambapo wameanza kutoa elimu hiyo kwa wananchi wanaoishi pembezoni mwa reli hiyo katika stesheni ya Chimala.

Amesema, kazi ya kitengo cha reli ndani ya SUMATRA ni kuhakikisha usafiri wa reli unakua salama na uhakika na jambo hilo linafanyika kwa kitengo kuendesha kaguzi za mara kwa mara ikiwa na kuishauri serikali na TAZARA kwa ujumla ya nini kifanyike.

Amefafanua kuwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mwezi Mei mwaka huu akiwa Ifakara, alitoa maagizo ambayo tayari mamlaka imeanza kuyafanyia kazi, hivyo hatua iliyopo kwa sasa ni kutoa elimu kwa wadau na watumiaji wa reli kuanzia eneo la Makambako hadi Tunduma.
Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya Ndugu Rubeni Mfune akizungumza na Viongozi wa vijiji na wananchi (hawapo pichani)ambao wana ishi maeneo ya jirani na njia ya Reli ya Tazara katika Stesheni ya Chimala Wilayani humo .
Mdhibiti na Mkaguzi wa Uslama wa Reli, kutoka Mamlaka ya Udhibiti SUMATRA, Eng. Hanya Mbawala akisisitiza jambo katika mkutano na wananchi na watendaji wa vijiji (hawapo pichani) ambao wanaishi pembezoni na njia ya reli ya Tazara katika stesheni ya Chimala wilayani Mbarali Mkoani Mbeya June 29 ,2018.

Meneja Usalama wa Reli ya Tazara Ndugu Sadick Anthony akizungumza na wananchi na Viongozi wa vijiji wanaoishi pembezoni mwa reli ya Tazara (hawapo pichani)katika mkutano ulioitishwa na Mamlaka ya Sumatra kwa lengo la kutoa elimu juu ya ulinzi wa reli ya Tazara .
Wananchi na Viongozi wanaoishi pembezoni mwa Reli ya Tazara katika Stesheni ya Chimala Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya wakisikiliza kwa makini maelezo yanayotolewa katika mkutano uliotishwa na viongozi wa Sumatra na Tazara katika kutoa elimu ya ulinzi wa Reli hiyo.

BENKI YA WATU WA ZANZIBAR YATIMIZA MIAKA 52 TANGU KUANZISHWA KWAKE,YATOA NENO KWA WATANZANIA

$
0
0
Na Emmanuel Massaka, Globu ya jamii

BENKI ya Watu wa Zanzibar(PBZ),leo imefanya Sherehe ya kutimiza miaka 52 tangu kuanzishwa kwake ambapo uongozi wa benki hiyo umewaomba Watanzania kuhakikisha wanafungua akaunti kwao. 

Pia benki hiyo imewahakikishia Watanzania kuendelea kutoa huduma bora kutoka wa watumishi ambao wanaifanya kazi yao kwa weledi mkubwa.

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam leo na Meneja Mkaguzi wa ndani wa Benk ya Watu  wa Zanzibar wa tawi la Tazara, Suleiman Ali Seleiman  baada ya kukata keki katika hafla ya kutimiza miaka hiyo 52 tangu kuazishwa kwake.

Akizungumza leo na Blogu ya jamii Suleiman  ametoa mwito kwa wananchi kujiunga na benki hiyo ili kurahisisha shughulizao na hasa zinazohusu huduma za kibenki.
 Picha ya pamoja
 Meneja wa mkaguzi wa ndani wa Benk ya watu wa Zanzibar tawi la Tazara Suleiman Ali Suleiman akimlisha keki mteja katika hafla ya miaka 52 tangu kuazishwa kwake.
 Meneja wa mkaguzi wa ndani wa Benk ya watu wa Zanzibar tawi la Tazara Suleiman Ali Suleiman akimlisha keki Meneja tawi ta Tazara,Fatma Khamis Mohad leo katika hafla ya kuazimisha miaka 52.
Meneja wa mkaguzi wa ndani wa Benk ya watu wa Zanzibar tawi la Tazara Suleiman Ali Suleiman akimlisha keki mteja katika hafla ya miaka 52 tangu kuazishwa kwake.

EXCLUSIVE: NAY WA MITEGO ALIVYO CHAPA NDANI YA MISS MBEYA 2018

MKEMIA MKUU WA SERIKALI AZUNGUMZIA NAMNA WANAVYOCHUNGUZA DAWA ZA KULEVYA

MAMBO MUHIMU YANAYOPATIKANA KATIKA RIPOTI YA UTAFITI WA UHISANI NCHINI ILIYOANDALIWA NA FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

$
0
0
TANZANIANS  the community and even in developing various social services in order to help the country move forward.

That has been said earlier yesterday in Dar es Salaam and Member of the Board of Directors of the Foundation for Civil Society Bi. Neziah Mahenge when the report will launch a special research about philanthropy and the culture of volunteering in Tanzania.

The report involving a survey conducted between February to April and involve organizations Foundation for Civil Society (FCS) in collaboration with the Forum for Philanthropy Tanzania (Tanzania Philanthropy Forum) with the aim of obtaining the necessary information about the status of the charity or voluntary basis to communities in Tanzania.
Member of the Board of Directors of the Foundation for Civil Society Neziah Mahenge explaining in detail the elements found in the report of the Study of Philanthropy in Tanzania.
Analyst and author of the research report of Tanzania Uhisania Mr. Tom Were he criticized the report early yesterday city Dar es Salaam.

Member of the board stressed the importance of the individual as well as private institutions, especially social functioning continued commitment in various development projects and stop the practice of waiting for the government to do everything.

He went on to stress that it is better to participate in various activities to development as one of the best ways to help the government in raising several projects including education, health, construction, and not to facilitate only financially but even in helping to bring donors who will achieve this exercise is also big stage.

"But also in the form of volunteers to Tanzania direction, its not too bad for Tanzanians to demonstrate that they have the heart to offer to help, but also in efforts to bring development to support multi-service social state shows we are still well" said Neziah.



RC MAKONDA ATANGAZA FURSA KWA JKT NA MGAMBO

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii

MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewataka vijana waliohitimu mafunzo ya JKT na Mgambo na hawana kazi wafike katika ofisi ili kushirikiana katika kuweka jiji katika hali ya usafi.

Makonda ameeleza hayo jana alipokuwa akifanya mazungumzo na viongozi wa Jeshi la kujenga taifa watokao katika Wilaya 5 za jiji, Makonda ameeleza kuwa licha ya kuweka  kila mkakati ikiwemo kutoa wito na rai kuhusu suala la usafi lakini bado jiji limekuwa chafu.

Ameeleza kuwa vijana hao watokao katika jiji la Dar es salaam wafike ofisini kwake Julai 6 ili kupata maelekezo kuhusiana na utaratibu mpya.

Kuhusiana na kazi zitakazofanywa na vijana hao Makonda ameeleza, watakaa na watendaji na kujua makampuni yanayofanya usafi na kama yanatekeleza majukumu hayo, kujua mahali ambapo wananchi wanatupa taka na kama kampuni zinazokusanya taka zinatoa risiti na kukamata kila anayetupa na asilimia 50 ya faini itakuwa sehemu ya ujira kwa vijana hao na atakayekamatwa akiwa hana fedha atafanya usafi kwa juma zima.

Aidha ameziagiza Manispaa zote ndani ya mwezi huu wa saba kila mfanyabiashara aliyepewa leseni awe na sehemu ya kutupa taka na vituo vya daladala viwe na sehemu maalumu ya kutupa ,Aidha amewataka makandarasi wote wa usafi katika ngazi zote kuwasilisha mikataba yao katika ofisi yake kuanzia Julai 4 hadi 6 ili iweze kupitiwa na tume iliyoundwa.

Pia amewashukuru wananchi na vyama mbalimbali ambavyo hujitolea kufanya usafi ili kuliweka jiji katika hali ya usafi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akizungumza na vyombo vya habari juu ya mkakati wa kusimamia usafi katika jiji la Dar es salaam.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFUNGUA JENGO LA BIASHARA LA NHC SINGIDA,AITAKA KUWAFIKIA WATU WA CHINI

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) lina jukumu kubwa la kuhakikisha sekta hiyo inakua na kuwafikia watu wa kipato cha chini.Amesema ya Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli inahimiza uchumi wa viwanda, hivyo sekta ya nyumba ina mchango mkubwa sana katika kuchochea ukuaji wa viwanda.

Ameyasema hayo leo (Jumamosi, Juni 30,2018) wakati akizindua mradi wa Singidani Commecial Complex, mjini Singida. Jengo hilo la biashara na ofisi limejengwa na NHC kwa ajili ya kupangisha wafanyabiashara na taasisi mbalimbali.

Waziri Mkuu amesema sekta ya nyumba ni mtambuka kwa kuwa huchochea ukuaji wa uchumi, kutoa ajira na kukuza uwekezaji wa viwanda vya vifaa vya ujenzi kama saruji, mabati, nondo, marumaru na vinginevyo, ambavyo vinafungua fursa kubwa ya ukuaji wa viwanda.Hivyo, Waziri Mkuu amesema wadau mbalimbali wanapaswa kuitazama sekta ya nyumba kama sekta mtambuka katika kuleta maendeleo endelevu ya uchumi na jamii kwa ujumla.

“Napenda kutoa pongezi kwa Shirika la Nyumba la Taifa kwa kujenga jengo hili zuri na la kisasa kabisa hapa mjini Singida. Vilevile, jengo hili limeboresha na kupendezesha mandhari ya mji wa Singida kwa kiwango kikubwa kabisa,” amesema. 

Waziri Mkuu amesema amefurahi kusikia jengo hilo limesanifiwa na ujenzi wake kusimamiwa na Watanzania wenyewe, wakandarasi washauri wakiwa ni NHC wenyewe na kwamba Watanzania zaidi ya 600 walipata ajira wakati wa ujenzi.Awali, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Bw. Felix Maagi alisema mradi wa jengo hilo la ofisi na biashara la Singidani lililogharimu sh. bilioni 3.4 ulianza Januari 26, 2015 na kukamilika Februari 17, 2018 na linatarajia kuliingizia shirika pango ya sh. milioni 420 kwa mwaka. Tayari asilimia 50 ya jengo hilo limepangishwa.

Mkurugenzi huyo alisema mbali na mradi huo wa Singidani, pia shirika limeendelea kukua na kuimarika katika utendaji wake ambapo thamani ya mali zote imeongozeka kutoka sh. trilioni 1.7 mwaka 2011 mpaka kufikia sh. trilioni 4.8 mwaka 2018.

Bw. Maagi alisema mapato ya shirika yamekua kutoka sh. bilioni 40 kwa mwaka 2011 hadi kufikia sh. bilioni 154 mwaka 2018.” Pia shirika linalipa gawio la Serikali kila mwaka na gawio hilo limekua kutoka sh. milioni 250 mwaka 2011 hadi sh. bilioni 1.2 kwa mwaka 2018,”Uzinduzi huo ulihudhuriwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi, wabunge wa mkoa wa Singida, viongozi wa dini na maafisa wa Serikali.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
41193 - DODOMA.
JUMAMOSI, JUNI 30, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (kushoto) wakifurahia baada ya Waziri Mkuu kufungua Jengo la Biashara la Singidani lililojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) mjini Singida Juni 30, 2018. Kulia ni Mbunge wa Singida Mjini, Mussa Sima na wapili kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Singida, Juma Kilimba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


NIDA KUTUMIA MAONESHO YA BIASHARA KUTOA VITAMBULISHO KWA WAKAZI WA MKOA DAR

$
0
0
MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imewataka wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam ambao hawana vitambulisho vya Taifa kufika kwenye banda lao lililopo Maonesho ya biashara ya kimataifa Sabasaba jijini Dar es Salaam ili wapate vitambulisho.

Akizungumza leo kwenye maonesho hayo Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Rose Joseph amesema pamoja na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu NIDA na majukumu yake pia wameamua kutumia maonesho hayo kutoa vitambulisho kwa wananchi wa mkoa huo.

Amesema kuwa hivyo kwa anayehitaji kitambulisho cha Taifa atatakiwa kuwa na viambatanisho muhimu vikiwemo cheti cha kuzaliwa, cheti cha taaluma, leseni au kadi ya bima ya afya.Amesema kwa watakaofika wakiwa na vielelezo vyao itakuwa rahisi kujaziwa fomu na kisha kupata kitambulisho cha taifa ambacho kina umuhimu mkubwa na ni vema kila mwananchi mwenye sifa akikapata.

“Tumeamua kutumia maonesho ya biashara ya kimataifa ya 42 kuhakikisha wananchi wa Dar es salaam ambao hawakuwa na vitambulisho vya taifa basi wanavipata.“Kwa hapa kwenye maonesho tutatoa vitambulisho kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam tu na wale wananchi wa mikoa mingine wao watapata kupitia ofisi zetu zilizoko mikoani,”amesema.

Amefafanua changamoto kubwa iliyopo katika kuandikisha vitambulisho vya taifa ni baadhi ya watu kutokuwa na viambatanishi muhimu ,hivyo wanashauri ni vema kila anayekwenda kuchukua kitambulisho akawa na vilelezo vyote muhimu.Wakati huo amesema NIDA kwa kutambua uwepo wa makundi yenye mahitaji maalumu nchini , ipo katika mchakato wa kutoa vitambulisho kwa kundi la watu wenye ulemavu wa kusikia.

Amefafanua baada ya hapo watakwenda kwenye makundi mengine na lengo ni kuhakikisha nao wanakuwa na vitambulisho vya taifa.

“Ni jukumu letu kuhakikisha vitambulisho vya taifa kila mtanzania mwenye sifa anakuwa nacho, hivyo tumeamua kuanzisha mpango maalum ambao huu utajikita kusajili makundi maalumu na tutaanza na kundi la watu wenye ulemevu wa kusikia.Tutakuwa na wakalimani ili kuhakikisha tunafanikisha mpango huo na tunatarajia kupata ushirikiano kutoka kwa viongozi wao,”amesema.

Bi. Rose Joseph Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA akifafanua jambo wakati alipkuwa akihijiwa na waandishi wa habari kwenye maonyesho ya biashara ya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam yanayoandaliwa na Mamlaka ya Mendeleo ya Biashara TANTRADE.
Baadhi ya wananchi mbalimbali wakipata maelezo kwa mmoja wa wafanyakazi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa katika Maonesho ya Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam leo.
Muonekano wa Banda la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA katika maonesho ya Sabasaba.

WANAOTUMIA WATOTO YATIMA, WAISHIO MAZINGIRA MAGUMU KAMA KITEGA UCHUMI SASA KUKIONA

$
0
0
Na Emmanuel Masaka,Globu ya jamii 

MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ametangaza vita na watu wenye tabia za kuwachukuwa watoto yatima,walemavu na waishio katika Maisha magumu kama mitaji ya kujinufaisha watakamatwa na kuchukuliwa hatua Kali za kisheria.

Makonda ametoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya matokeo ya utafiti wa idadi ya Watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani kinyume na Sheria hali inayosababisha kushindwa kutumia fursa ya elimu bure iliyotolewa na Rais John Magufuli jambo ambalo Makonda ameapa kulivalia njuga.

Kwa mujibu wa utafiti huo umebaini Mkoa wa Dar es salaam pekee una jumla ya watoto 3,312 wanafanya kazi mitaani na kati ya hao watoto 2,984 walionekana wakifanya kazi nyakati za mchana na 328 wanafanya kazi nyakati za usiku.

"Idadi hiyo ya watoto wanaoishi mitaani ni matokeo ya kukosekana kwa misingi bora ya familia na mmonyoko wa maadili ndio maana niliamua kuunda tume ya kupitia sheria ya mtoto na mikataba ya kimataifa ambayo itasaidia kuweka haki stahiki za watoto,"amefafanua. 

Aidha amewaonya watu wenye tabia ya kuwapatia ombaomba fedha barabarani kuwa ndio wanaohalalisha uwepo wa watu hao ambapo amesema kama mtu anataka kweli kusaidia waishio maisha magumu wapeleke misaada kwenye vituo vilivyopo kwa mujibu wa sheria kwani vituo hivyo vinafuatilia mienendo ya watoto kitabia, elimu na matibabu.

Ambapo ukimpa fedha mtoto barabarani unatengeneza mazingira ya kuwa na fedha ambayo hana uhalali nayo na anapokuwa mtu mzima anakuwa mkabaji,mporaji na kuchoma visu watu wasio na hatia.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa shirika la Babawatoto Center Bwana Mgunga Mwa Mnyenyelwa amempongeza Makonda kwa kutafuta haki ya mtoto alietelekezwa kwani kupitia mchakato huo limewezesha watoto wengi kuingia kwenye mfumo rasmi wa kupata fedha ya matunzo kila mwezi pamoja na bima ya matibabu Bure.

Amesema utafiti huo umefanywa na shirika la Babawatoto Center for Children and Youth.kupitia mradi wa USAID Kizazi Kipya kwenye mikoa mitano ambapo wamebaini nusu ya watoto wa mitaani wanapatikana mkoa wa Dar es salaam
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wanaowatumia watoto yatima,walemavu waishio,mazingira magumu kama mitaji ya kujinufaisha,ameeleza kuwa watu hao wakibainika watakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
Mkurugenzi wa Shirika la Babawatoto Sente,Mgunga Mwa Mnyenyelwa akimkabidhi ripoti ya matokeo ya utafiti wa idadi ya watoto wanaoishi na kufanya kazi mtaani kinyume cha sheria,Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda.
Picha ya pamoja

WAFANYABIASHARA WA DHAHABU MARA WAONDOKANA NA ADHA.

$
0
0
Na Frankius Cleophace, Musoma.

Wafanyabiashara wa Madini kutoka Migodi mbalimbali ya Dhahabu Mkoani Mara wameondokana na adha waliyokuwa wakiipata ya kusafirisha Mchanga wa dhahabu kwaajili ya kuchenjua Mkoani Mwanza kabla ya katazo la serikali baada ya kufunguliwa kwa kiwanda cha FRAMAL INVESTMENT LTD Manispaa ya Musoma mkoani Mara kwaajili ya uchenjuaji wa dhahabu.

Mmilikiwa kiwanda hicho FRANK MALIMA anasema awali alikuwa na kiwanda Mkoani Mwanza lakini baada ya Serikali kuzuia usafirishaji wa Mchanga wa Dhahabu kutoka Mkoa mmoja hadi mwingine ameamua kufungua kiwanda Mkoani Mara kwaajili ya kutoa huduma kwa wafanyabiashara wa Madini.

Frank amesema kuwa Mkoa wa Mara unazalisha sana Dhahabu hivyo ameamua kufungua kiwanda hicho kwa lengo la kutekeleza Serikali ya Viwanda ikiwa ni pamoja na kuwasaidia Wafanyabiashara hao.

Ameongeza kuwa Kwasasa kiwanda hicho kina uwezo wa kuchenjua tani 1.5 ya Dhahabu kwa saa 24 hatua ambayo Mmiliki huyo amesema bado kumeonaka kuwepo na upungufu wa Mashine hizo na hivyo kuwa katika harakati za kutengeneza Mashine zingine ambazo anaamini zitasaidia kukidhi Mahitaji.

Nao baadhi ya wafanyabiashara wa Madini wakatoa pongezi kwa Mmiliki wa kiwanda hicho na kusema kulikuwa na changamoto kubwa kabla ya kuwepo kwa kiwanda hicho.
Mitambo kwa ajili ya Uchenjuaji wa Dhahabu katika Kiwanda hicho kilichopo Mjini Musoma Mkoani Mara.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha FRAMAL INVESTMENT LTD Frank Malima akionyesha baadhi ya Mitambo katika Kiwanda hicho
Gari la kampuni hiyo ambalo linafanya hughuli za Usafirishaji wa Mchanga huo.
Mkurugenzi wa Kiwanda hicho akiongea na Vyombo vya habari ofisini Kwake.

MICHUZI TV EXCLUSIVE: NAY WA MITEGO ALIVYOCHAPA NDANI YA MISS MBEYA 2018...

KAMISHNA MKUU WA TRA AWAHIMIZA WANANCHI KULIPA KODI KWA WAKATI

$
0
0
Na Veronica Kazimoto,Dar es Salaam

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere ametoa wito kwa wananchi kujenga tabia ya kulipa kodi mbalimbali kwa wakati ikiwepo Kodi ya Majengo ili kuepuka usumbufu unajitokeza tarehe za mwisho za kulipa kodi hizo.

Akizungumza leo na wananchi waliotembelea banda la TRA katika maonyesho ya 42 ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba, Kamishna Mkuu huyo amesema kuwa, wananchi wengi husubiri tarehe za mwisho ili kulipa kodi suala linalosababisha foleni na malalamiko kutoka kwa wananchi hao.

“Tumetangaza kwa muda mrefu kuhusu kulipa Kodi hii ya Majengo lakini hamkutaka kulipa kwa wakati, matokeo yake foleni imekuwa kubwa na sasa mnaanza kulalamika kwamba mnachelewa kupata huduma. Jengeni tabia ya kulipa kodi kwa wakati ili muweze kuondokana na usumbufu huu usio wa lazima,” alisema Kichere.

Kamishna Mkuu Kichere ameongeza kuwa, kodi ya majengo ya mwaka 2018/19 inaaza kulipwa tarehe 1 Julai 2018 na mwisho wa kulipa kodi hiyo ni tarehe 30 Juni, 2019. Hivyo, wananchi waanze kulipa mapema ili kuondoa usumbufu wa kukaa kwenye foleni.Naye mwananchi aliyetembelea banda la TRA kwa ajili ya kulipa Kodi ya Majengo Shabani Mkolimwa, amefurahishwa na huduma alizozipata katika banda hilo na kuiomba Mamlaka kusogeza huduma hizo karibu na maeneo wanayoishi.

“Leo nimefurahi sana kwasababu nimepata huduma za TRA na huduma za benki ndani ya banda moja. Ninaiomba TRA ituletee huduma hizi kwenye Serikali zetu za Mitaa ili iwe rahisi kwetu kupata huduma hizi za TRA kwa haraka,” alisema Mkolimwa.

Mamlaka ya Mapato Tanzania imeshiriki katika Maonyesho ya Sabasaba na banda lake lipo mkabala na banda la Azam ambapo pamoja na kupokea maoni kutoka kwa wananchi, huduma mbalimbali zinatolewa ikiwa ni pamoja na Kulipa Kodi ya Majengo, Usajili wa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) na Elimu ya Mlipakodi
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere (kulia) akizungumza na wananchi waliotembelea Banda la TRA katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba kwa ajili ya kulipa Kodi ya Majengo wakati Kamishna Mkuu huyo alipotembelea banda hilo kuona huduma mbalimbali zinazotolewa kwa wananchi. 
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere (katikati) akikagua bili ya Kodi ya Majengo aliyopewa mteja (kulia) wakati alipotembelea banda la TRA katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba kuona huduma mbalimbali zinazotolewa kwa wananchi. Kushoto ni Meneja wa Huduma wa TRA Bi. Honester Ndunguru.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere (katikati) akijibu hoja za mteja aliyempigia simu wakati alipotembelea banda la TRA katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba kuona huduma mbalimbali zinazotolewa kwa wananchi. Kushoto ni Afisa Kodi Bi. Levina Shirima na kulia ni Meneja wa Huduma Bi. Honester Ndunguru.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere akimsikiliza Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Temboni iliyopo jijini Dar es Salaam Ally abdallah (kulia) wakati alipotembelea banda la TRA katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba kuona huduma mbalimbali zinazotolewa kwa wananchi. Kushoto ni Mwanafunzi mwenzake Safinia Shani. 
Baadhi ya wateja wakitoka katika Banda la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) lililopo mkabala na banda la Azam ndani viwanja vya Sabasaba. PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO
Viewing all 110031 articles
Browse latest View live




Latest Images