Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

WANAVIKUNDI WA WAMA KILANGARA LINDI WAHAMASIKA NA KUJIUNGA CHF PAPO KWA PAPO

$
0
0
 Mwanakikundi  zuhura Mnandembwe akitoa maelezo ya namna alivyohamasika na kujiunga na chf  mbele ya wananchi waliopo katika kata ya Kilangala,amewataka wananchi wasio kwenye sekta isiyo rasmi kujiunga na mfuko huu kwani ni mkombozi wa huduma za matibabu nchini,ukizingatia wengi ni wenye vipato vya wastani na visivyo vya uhakika.
 Mwananchi wa kata ya Mihumbwe  Sharifa Mzee kushoto akipata ufafanuzi wa namna ya kujiunga na mifuko ya afya ya jamii (CHF) kutoka kwa msimamizi wa NHIF na CHF mkoa wa Lindi Fortunata Raymond baada ya kuhamasika kwenye viwanja vya chama cha msingi cha ushirika (AMCOS) Kilangala.
Alamski
Wanakikundi wa WAMA kata ya kilangala wakijiandikisha kwenye mfuko wa afya ya jamii (CHF),anayeandikisha kulia ni msimamizi wa mfuko wa taifa wa bima ya afya lindi fortunata raymond,kushoto ni Mganga mfawidhi wa kata hiyo Dr. Arafa Abdallah,takribani kaya 105 zilijiunga papo kwa papo ,uandikishajii huo ulifanyika kwenye viwanja vya chama cha msingi cha mazao (AMCOS) Kilangara Mkoani Lindi.

JK na Mama Salma Kikwete walivyopokelewa kwa shangwe jijini Harare, Zimbabwe

NGOMA AFRICA BAND TAKE EUROPE BY STORM

$
0
0
One of the most wanted and successful music group, Ngoma Africa Band (Golden Voice of East Africa) also commonly known as FFU (Field Force Unit) or "Anunnaki Aliens" based in Germany, have been named and awarded  "Best African band" 2013 after thrilling over 100,000 fans at International African festival Tubingen 2013.
Ngoma Africa band's popularity is growing, having been founded 1993 by Tanzanian born Afro-pop star Ebrahim Makunja also known as Kamanda Ras Ebby Makunja "The King of Anunnaki Aliens". 
The band is famous for its thrilling shows in festivals in different parts of Europe. The band's joyful female dancers, wearing traditional costumes and dancing vigorously to their tunes, always leave fans asking for more. 
Ngoma Africa Band have a number of talented musicians including Multi-Talented soloist Christian Bakotessa aka Chris-B, Matondo Benda aka Professor Mo Benda, Flora Williams, Aj Nbongo, Jonathan Sousa aka "Jo Jo" (Crazy Drummer), Glory, Jessica Ouyah.
Most of their  their songs are in Swahili and other Eastern African languages. Reportedly with over 30 million fans worldwide they have  become a Global people's band. 

For further information about Ngoma Africa Band and to listen to their music, please visit

Ngoma Africa band in action
Multi-Talented soloist Christian Bakotessa aka Chris-B
Tanzanian born Afro-pop star Ebrahim Makunja also known as Kamanda wa FFU Ughaibuni Ras Ebby Makunja "The King of Anunnaki Aliens".
Ngoma Africa band members

//michuzi2.rssing.com/chan-7007653/article4724-live.html

SWAHILI RADIO YAZINDUA APP YA ANDROID PHONES, IPHONE, IPAD,IPOD NA BLACKBERRY

$
0
0
Swahili Radio baada ya kupokea maombi mengi ya wasikilizaji wetu kutoka sehemu mbalimbali duniani, tunapenda kuwatangazia kuwa Radio yetu kwa sasa inapatikana bila mkwaruzo katika simu za viganjani za iPhone, Blackberry, Android phones na katika kila kifaa chenye internet duniani. Endelea Kuangalia Swahili TV na kusikiliza Swahili Radio. Jinsi ya kutupata 
1. Download Tunein (Tunein ni neno moja usiache nafasi) Tunein Radio app kwa simu yako mfano; iphone, ipad,ipod,android au Blackberry
2. Baada ya ku-download , open app na nenda kwenye browser  na andika neno swahili radio kisha search.
3. Ukiona logo yetu ya swahili radio bofya na sikiliza.

TUNAPATIKANA HEWANI MASAA 24 TUKIWATANGAZIA KUTOKA JIJINI WASHINGTON D.C. TUKIWA KATIKA MAJARIBIO

Mhe. PINDA AFUNGUA KONGAMANO LA UWEKEZAJI MANYARA LEo

$
0
0
 Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda akitazama asali wakti alipotembela Banda la Halmashauri ya Wilaya Mbulu  kabla ya kufungua kongomano la  Kwanza la  Uwekezaji katika mkoa wa Manyara  mjini Babati leo 
 Waziri Mkuu, Mhe Mizengo Pinda akitazama asali wakti alipotembela Banda la Halmashauri ya Wilaya Mbulu  kabla ya kufungua kongomano la  Kwanza la  Uwekezaji katika mkoa wa Manyara  mjini Babati  leo. Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dr, Mary Nagu na Kulia ni Mkuu wa Mkoa huo, Erasto Mbwilo
 Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda  akitazama  mbolea  wakati alipotembelea  banda la kiwanda cha Mbolea cha Minjingu  kabla ya kufungua Kongamano  la Kwanza  la Uwekezaji  katika  Mkoa wa  Manyara mjini Babati leo. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Manyara, Erasto Mbwilo.
 Waziri Mkuu, Mhe Mizengo Pinda akizungumza na wanachama wa    kikundi cha ushonaji  Ufukuba  katika banda la kikundi hicho  kabla ya kufngua  Kongamano la  Kwanza la Uwekezaji katika mkoa wa  Manyara  mjini babati leo

Waziri Mkuu, Mhe Mizengo Pinda akifungua Kongamano la Kwanza la Uwekezaji  katika Mkoa wa Manyara mjini Babati leo
Baadhi ya  washiriki wa  Kongamano la Kwanza la  Uwekezaji  katika Mkoa wa Manyara  wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mhe Mizengo Pinda wakati alipofungua   kongamano hilo mjini Babati 

NIDA KUANZA KUCHUKUA ALAMA ZA VIDOLE NA PICHA KWA WAKAZI WA JIJI LA DAR

Miss Tanzania Brigitte aanza ujenzi wa bweni la wanafunzi Albino Shinyanga

$
0
0
Miss Tz 2012 Brigette Alfred aliweka jiwe la msingi katika ujenzi wa bweni la wavulana shule ya msingi Buhangija akiwa pamoja na afisa elimu wa manispaa ya Shinyanga Honoratha Ruhumbika.
Miss Tanzania Brigitte Alfred akiwa na baadhi ya wanafunzi walemavu wa ngozi wa shule ya msingi Buhangija wakinyanyua moja kati ya mabati 200 aliyonunua kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wavulana katika shule hiyo.
Miss Tz 2012 Brigette Alfred pamoja na baadhi ya wanafunzi walemavu wa ngozi wa shule ya msingi Buhangija wakinyanyua moja kati ya mabati 200 aliyonunua kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wavulana katika shule hiyo.

MREMBO wa Tanzania, Brigitte Alfred ameonyesha mfano wa kuigwa nchini katika tasnia hiyo baada ya kuanza ujenzi wa bweni la wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi (albino) katika wilaya ya Shinyanga wanaoishi katika shule maalum ya Buhangija. Tayari mrembo ameweka jiwe la msingi na kupandisha ukuta sambamba na kukabidhi mabati 200 kwa ajili ya kujengea paa la bweni hilo la wavulana lenye uwezo wa kulaza wanafunzi 50.

Makabidhiano hayo yalifanywa na mrembo huyo kwa katika hafla fupi iliyohudhuriwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Annarose Nyamubi, afisa elimu wa manispaa ya Shinyanga Honoratha Ruhumbika na walimu wa shule hiyo wakiongozwa na mwalimu mkuu, Peter Ajali. 

Briggite alisema kuwa ameamua kutimiza ahadi yake aliyoitoa mwezi Aprili mwaka huu alipotembelea Shinyanga kwa kazi za jamii na kuona changamoto za watoto wanaosoma katika shule hiyo.

Alisema kuwa mpango huo upo katika mpango wa Miss Tanzania ujulikano kwa jina la Urembo wenye malengo maalum (Beauty with Purpose) nay eye kuamua kufanya kwa vitendo.

“Ni faraja kwangu kuona kuwa ninatimiza ahadi yangu, nawashukuru wote walionisaidia ikiwa pamoja na familia yangu, na ninaomba wengine wanisaidie kwani badi kuna changamoto nyingi katika ujenzi na kazi za jamii kwa ujumla,” alisema Brigitte.

Alisema kuwa amepania kuweka historia katika fani hiyo kwani anaamini ujenzi au jingo hilo litakuwa kumbukumbu kubwa kwake tena kwa vizazi na vizazi.

Brigitte pia aliwataka wanafunzi hao kutokata tamaa hata kwa wale wasiokuwa karibu na familia zao na kwamba wamtegemee zaidi Mwenyezi Mungu kwa kuwa yeye ndiye mfariji kwa wanyonge huku akiwahimiza kuzingatia zaidi elimu kwani ndiyo msingi wa maisha yao.

 “Nilipata msukumo wa kuisaidia shule hii hususani katika ujenzi wa bweni hilo kutokana na ujio wake wa mwezi Aprili mwaka huu shuleni hapo na kujionea adha wanayopata watoto hao kutokana na msongamano mkubwa mabwenini,” alisema.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Annarose Nyamubi alimpongeza Brigitte kwa moyo huo wa kujitolea na kuwataka warembo wengine kuiga mfano wake. Nyamubi alisema kuwa alichokifanya Brigitte ni jambo la kukumbukwa nan i msaada mkubwa kwa jamii hasa kwa watu wenye ulemabu wa ngozi.

Mkuu huyo wa wilaya aliwaomba wazazi wa watoto hao kuwa na tabia ya kuwatembelea watoto wao mara kwa mara ikiwa ni pamoja na kuwachuku wakati wa likizo. Naye mwalimu mkuu wa shule hiyo Peter Ajali alisema kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo la msongamano mabwenini kwani kuna jumla ya watoto 247 huku mabweni yaliyopo yana uwezo wa kukaa watoto 148 tu.

SEMINA YA FURSA KWA VIJANA ILIVYOPOKELEWA LEO MKOANI KIGOMA

$
0
0
Mghani mahiri wa mashairi hapa nchini Mrisho Mpoto akizungumza kwa msisitizo,masuala ya fursa mbalimbali zinazopatikana katika suala zima la ujasiliamali mapema leo kwenye semina ya Fursa iliyofanyika katika ukumbi wa  Student's Center,uliopo katikati ya mji wa mkoa wa Tabora mapema leo.Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group,imefadhiriwa na shirika la NSSF;Zantel,MaxMalipo,Lake Oil. 
  Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji kutoka Clouds Media Group,Ruge Mutahaba,akizungumza mbele ya washriki wa Semina ya Fursa ndani ya ukumbi  kwenye ukumbi Student's Center uliopo katikati ya mji wa mkoa wa Tabora.
 Baadhi ya Wasanii wa muziki wa kizazi kipya wakishiriki semina ya Fursa kwa vijana ililiyofanyika leo kwenye ukumbi wa Student's Center katikati ya mji wa mkoa wa Tabora mapema leo,kutoka kulia ni Msanii Godzilla,Baba Levo,Amin,Stamina na wengineo.

 Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,Mwasiti Almas akizungumzia baadhi ya fursa alizozipata mara baada ya kujiunga na shirika la NSSF,mbele ya Washiriki wa Semina ya Fursa (hawapo pichani),kulia kwake ni Mwakilishi wa NSSF-Makao Makuu Bwa,Salim Khalfan akimsikiliza kwa makini.Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group,imefadhiriwa na shirika la NSSF;Zantel,MaxMalipo,Lake Oil.
 Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya mafuta-Lake Oil,Bwa.Ben Temu akizungumza kwenye semina ya Fursa,ambapo yeye alielezea mambo mbalimbali ikiwemo suala la vijana kuwa wenye moyo wa kujituma na kutokata tamaa mapema,alieleza kwa kuwataka vijana wawe wavumilivu na kuachana na tabia ya kujiona hawawezi kufanya jambo,kwamba kila fursa wanayokumbana nayo waitumie vizuri katika suala zima la kujikwamua na kujiendeleza kimaisha. Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group,imefadhiriwa na shirika la NSSF;Zantel,MaxMalipo,Lake Oil. 
 Sehemu ya Meza kuu.Kutoka kushoto ni Wawakilishi kutoka shirika la NSSF,Salim Khalfan (makao makuu),Alloys Banigwa (Meneja wa NSSF-Tabora),Mkuu wa Wilaya ya Iramba kutoka Mkoani Singida,Mkuu wa Wilaya ya Igunga,Mh.Elibarik Kingu,Ruge Mutahaba-Clouds Media Group, pamoja na Ben Temu kutoka kampuni ya Lake Oil.

 Semina ya Fursa ikiendelea mapema leo ndani ya ukumbi wa Student's Center katikati ya mkoa wa Tabora mapema leo.Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group,imefadhiriwa na shirika la NSSF;Zantel,MaxMalipo,Lake Oil.
 Mwakilishi wa Shiriki la NSSF kutoka Makao Makuu jijini Dar,Bwa.Salim Khalfan akielezea fursa mbalimbali zinazopatika mara mtu yeyote anayejiunga ama amejiunga na NSSF,alifafanua zaidi kuwa mtu yeyote atakayejiunga na shirika hilo atanufaika na mambo mengi,ikiwemo suala la matibabu,mikopo na mengineyo lukuki yanayopatikana ndani ya shirika hilo.Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group,imefadhiriwa na shirika la NSSF;Zantel,MaxMalipo,Lake Oil. 
PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM

USAHIHI WA MATUMIZI YA KASMA MAALUM YA UJENZI WA MIRADI YA BARABARA NCHINI

$
0
0
Tarehe 22/08/2013,  Wizara ya Ujenzi ilikutana na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kwa ajili ya kujadili Hesabu zilizokaguliwa za Fungu 98 kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012. Kikao hicho kilifanyikia katika Ofisi Ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam chini ya Uenyekiti wa Mhe. Gaudence Cassian Kayombo Mbunge wa Mbinga Mashariki, ambaye alitoa maamuzi na maelekezo rasmi ya Kamati.
 Katika kikao hicho hoja kadhaa zilijadiliwa ikiwamo hoja kuhusu Matumizi ya Kasma Maalun ya Ujenzi wa Miradi ya Barabara nchini ambayo ilitengewa kiasi cha Shs. 252,975,000,000.00. 
Katibu Mkuu (Afisa Masuhuli) wa Wizara ya Ujenzi alikiarifu kikao hicho kuwa fedha za Mradi huo Maalum zilitumika kwa ajili ya kulipia madai ya Makandarasi na Wahandisi Washauri kwa miradi ya ujenzi wa barabara inayoendelea katika mipango na bajeti ya Serikali.  Katika ujenzi wa barabara; jukumu la msingi kwa Wizara ni kulipa madai ya Makandarasi na Wahandisi Washauri.
 Aidha, alifafanua kwamba Mradi huu umekuwa na matokeo mazuri kwani ulifanikisha shughuli za ujenzi wa barabara nchini.  
Afisa masuhuli aliendelea kufafanua kwamba mradi huu wa barabara haukuwa mradi kivuli bali ulikuwa ni mradi maalum kwa lengo la kufanikisha programu ya barabara na maendeleo ya wananchi kwa ujumla. 
Tarehe 22/08/2013 na tarehe 23/08/2013 zimetolewa taarifa za upotoshaji na baadhi ya vyombo vya habari kuhusu ukweli wa suala hili ambapo baadhi ya vyombo hivyo vilinukuliwa kusema kuwa kumekuwepo na ufisadi, matumizi tata na ubadhirifu katika mradi huu. 
Wizara inapenda kuudhibitishia umma kwamba katika utekelezaji wa mradi huu hapakuwepo na ufisadi, ubadhilifu, au matumizi tata. 
Ukweli huu umethibitishwa kwa maandishi na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwamba hoja ya ukaguzi huu haikuhusu ubadhirifu au matumizi mabaya yoyote  ya fedha bali ni suala la uandishi wa vitabu vya fedha uliohitaji kuboreshwa. 
Wizara ya Ujenzi inapenda kutoa ufafanuzi huu na kuudhibitishia tena umma kwamba hakuna upotevu wowote wa fedha kama ambavyo  baadhi ya vyombo vya habari vimetaka ieleweke.
 Taarifa hii imetolewa na; 
Balozi Herbert E. Mrango
KATIBU MKUU (AFISA MASUHULI)
WIZARA YA UJENZI

SHILOLE ALIPOLONGA NA VOA ALIPOKUWA ZIARANI MAREKANI

$
0
0
Msanii Shilole alipofanya ziara yake nchini Marekani alipata ya kutembelea idhaa ya Kiswahili ya VOA na kufanya mahojiano na mpiganaji Sunday Shomari. Bofya kamshale hapo chini kuungana naye alipokuwa ndani ya studio za VOA akieleza yale aliyoyapata Marekani na siri ya staili ya muziki wake.Hii ikiwa ni sehemu ya Kwanza.

golden bush FC kupambana na Mwanza united uwanja wa kinesi jijini dar jumapili

$
0
0
Wadu, 
Tunapenda kuwapa taarifa ya game muhimu kabisa siku ya jumapili asubuhi pale uwanja wa Kinesi (Shekilango) ambapo timu mbili maarufu za veterans yaani Golden Bush FC (mabingwa wa Jiji la Dar na mikoa jirani) na maveteran wa Mwanza united zitakutana uso kwa uso katika game ya kirafiki. ni mechi ambayo hutakiwi kukosa ukizingatia umahili wa wachwzaji wa timu zote mbili. 
Mwanza united ikiongozwa na wachezaji waliotamba sana katika timu za Pamba, Simba, Yanga na timu ya taifa, hapa tunazungumzia akina George Magere Masatu ambaye ndiye nahodha wa timu, Aaron Nyanda, George Nyanda, Emmanuel Swita, Benjamin Magadula na wengine wengi.
 Golden bush FC wameweka kambi Starlight Hotel Dar es salaam ili kuweka mipango ya pamoja ndani ya siku hizi mbili zilizobaki, pamoja na kuwa na wachezaji mahili sana kama Waziri Mahadhi Mandieta, Herry Morris, Wisdom Ndlovu, Nico Nyagawa, Juma Kaseja, Amani Simba, Amri Kiemba, Salum Swedi, Salum Athuman, Kudra Omary, Abuu Mtiro, Yahaya Issa Golden bush wanajivunia kuwa kikosi kikubwa kilichosheheni wachezaji hatari chini mwalim Madaraka Seleman “Mzee Wa kiminyio”.
 Uwanja uko chini ya ulinzi makili wa polisi na mgambo wa jiji ili kuepuka tabia wa wenzetu wa mwanza kutumbukiza vitu vyao vya kishirikina.
 Karibuni sana mje mpate burudani ya kukata na Mundu.
 Ally Mayay ndiye atakuwa mwamuzi wa game hiyo.

Imetolewa na msemaji wa timu 
Onesmo Waziri “Ticotico”

Mh. Lowassa akutana na muhubiri wa kimataifa.Daniel Kolenda jijini dar

$
0
0
Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwa na muhubiri wa kimataifa.Daniel Kolenda ambaye ni mtoto wa muhubiri wa kimataifa kutoka Ujerumani Renhard Bonnke,katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Muhubiri huyo na kundi lake walimualika Mh Lowassa na mkewe kwa chakula Cha jioni.
Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa monduli Mh Edward Lowassa na mkewe mama Regina Lowassa wakiwa pamoja na wahubiri wa kimataifa kutoka Ujerumani Daniel Kolenda na Peter Kedenberg,mara baada ya chakula Cha jioni kwenye hoteli ya Serena ambapo wahubiri hao walimwalika Mh Lowassa

introducing libeneke la lightstudio blog

$
0
0
Justine kazaura is my name, i'm executive director as well as a photographer here at Light studio,
simply the best is what we do, thanks.
My name is Adelina Tibesigwa, a graphic designer, a blogger too as well as office administrator here at Light studio.......your all welcome to join us in this blog!

Michuzi Blog congratulates Lightphotostudio blog for 

your innovation, creativity and enterprising  skills in this field. Count on our support anytime, anyday. Also keep on keeping on with the good job!

-ANKAL



DOUBLE TREE BY HILTON DAR ES SALAAM YAGAWA TAA 200 NA KUTOA MAFUNZO KWA WANAFUNZI JUU YA MATUMIZI YA UMEME WA NISHATI YA JUA

$
0
0
DSC_0240
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Angellah Kairuki (Mb) akitoa risala yake kwenye hafla ya kukabidhi Taa 200 za Nishati ya Jua kwa Shule ya Msingi Mji Mpya iliyopo Mabwepande ikiwa ni mwendelezo ya kampeni iliyozinduliwa na Hoteli ya DoubleTree By Hilton jijini Dar kwa wanafunzi wa shule za msingi ambapo ameipongeza hoteli hiyo kwa kubuni kampeni kama hiyo kwani Taa hizo ni rafiki wa mazingira kwa kuwa zinatumia Nishati ya Jua zitawasaidia wanafunzi kujisomea na familia zao pia kupata Mwanga kunapokuwa tatizo la kukatika kwa Umeme na pia itaongeza ufaulu kwa Wanafunzi kwa sababu watakuwa wanauwezo wa kujisomea nyakati za usiku.
Aidha amewaasa wanafunzi hao kuzitunza taa hizo na kuzitumia kwa maelngo yaliyokusudiwa. Kushoto ni Mwenyekiti wa bodi ya Shule hiyo Epimack Vinivuni na Kulia ni Meneja Mkuu wa Hoteli ya Double Tree by Hilton Rode Perk pamoja na Mkurugenzi wa Mauzo wa Hoteli ya Double Tree by Hilton Florenso Kirambata (wa pili kulia).
DSC_0234
Mkurugenzi wa Mauzo wa Hoteli ya Double Tree by Hilton Florenso Kirambata (katikati) akitoa maelezo ya jinsi ya kutumia taa ndogo za mezani zinazotumia Nishati ya Jua na umuhimu wake tofauti na kutumia Mafuta ya Taa kwa Wanafunzi wa darasa la saba wa shule ya msingi ya Mji Mpya wakati uongozi wa hoteli hiyo ulipotembelea shule hiyo iliyopo Mabwepande kwa nia ya kuendesha mafunzo na kugawa Taa 200 bure kwa Wanafunzi hao. Kushoto ni Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Angellah Kairuki (Mb) na Kulia ni Meneja Mkuu wa Hoteli ya Double Tree by Hilton Rode Perk.
DSC_0249
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Angellah Kairuki (Mb) akikabidhi rasmi Taa hizo kwa mmoja wa Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mji Mpya iliyopo Mabwepande leo jijini Dar. Katikati ni Mkurugenzi wa Mauzo wa Hoteli ya Double Tree by Hilton Florenso Kirambata na Kulia ni Meneja Mkuu wa Hoteli ya Double Tree by Hilton Rode Perk.
DSC_0229
Mwenyekiti wa bodi ya Shule hiyo Epimack Vinivuni akitoa shukrani kwa uongozi wa hoteli ya Double Tree by Hilton kwa kuwa na mkakati madhubuti wa kuwaelimisha vijana umuhimu wa matumizi ya Umeme mbadala wa Nishati ya Jua ambao ni rafiki wa mazingira.
DSC_0226
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mji Mpya Davis Mkaruka akizungumza baada ya mafunzo yaliyolewa na Double Tree by Hilton kwa wanafunzi wa darasa la saba akisema ilikuwa ni njia nzuri ya kuwaelimisha watoto juu ya nishati ya jua na kuwa wamefurahi kupewa bure taa ndogo za mezani ambazo ni rahisi kutumia na zina faida nyingi kwao na familia zao.
DSC_0253
Wanafunzo hao wakifurahia Taa ndogo la ‘Solar Energy’ walizopewa. Nyuma ni Bw. Florenso Kirambata na Meneja Mkuu wa hoteli ya Double Tree by Hilton Hotel Rode Perk.
Hoteli ya Double Tree by Hilton Dar es Salaam leo imefanya ziara katika Shule ya Msingi Mji Mpya iliyopo Mabwepande kwa lengo la kuendesha mafunzo kwa wanafunzi wa darasa la saba kuhusu umuhimu wa umeme wa nishati ya jua.
Mafunzo hayo ni sehemu ya mkakati wa Double Tree by Hilton wa miaka miwili wa kuwakufahamisha na kuwashirikisha wanafunzi juu ya faida za nishati ya jua tofauti na matumizi ya mafuta ya taa, kuni na vyanzo vingine vya mwanga ambavyo vina madhara kwa mazingira, afya na vifaa vya nyumbani.
Katika ziara hiyo shule hapo Hoteli ya Double Tree by Hiltonimegawa kwa wanafunzi hao taa ndogo za mezani 200 zinazotumia nishati ya jua, ambazo wanafunzi hao wamekwenda nazo majumbani kwao kuzitumia kusomea usiku kwa faida yao na familia yao.

TFF yabandika majina ya waombaji uongozi kwenye uchaguzi wa TFF na Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) ili kutoa fursa kwa pingamizi.

$
0
0
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imebandika rasmi kwenye ubao wa matangazo majina ya waombaji uongozi kwenye uchaguzi wa TFF na Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) ili kutoa fursa kwa pingamizi.

Kipindi cha pingamizi kinaanza kesho (Agosti 24 mwaka huu) hadi sas 10 kamili jioni ya Agosti 26 mwaka huu ambapo waweka pingamizi wanaruhusiwa kupitia taarifa za wale wanaokusudia kuwawekea pingamizi kabla ya kuwasilisha pingamizi husika.

Kwa mujibu wa tangazo la uchaguzi, Agosti 27 hadi 29 mwaka huu ni wawekaji pingamizi na wawekewa pingamizi kufika mbele ya Kamati ya Uchaguzi kwa ajili ya kusikiliza pingamizi.

Waombaji kuwania uongozi katika TFF ambao majina yao yamebandikwa ni Athuman Jumanne Nyamlani, Jamal Emil Malinzi, Omari Mussa Nkwarulo na Richard J. Rukambura (urais). Nafasi ya Makamu wa Rais ni Imani Omari Madega, Ramadhan Omari Nassib na Walace John Karia.

Walioomba nafasi za ujumbe kuwakilisha kanda ni Kanda Namba Moja (Kagera na Geita) ni Abdallah Hussein Mussa na Kaliro Samson. Kanda Namba Mbili (Mara na Mwanza) ni Jumbe Odessa Magati, Mugisha Mujwahuzi Galibona, Samwel Nyalla na Vedastus Kalwizira Lufano.

Kanda Namba Tatu (Shinyanga na Simiyu) ni Epaphra Amana Swai, Mbasha Matutu Mong’ateko na Stanslaus Haroon Nyongo. Kanda Namba Nne (Arusha na Manyara) ni Ally Mtumwa, Elley Simon Mbise na Omari Walii Ali.

Kanda Namba Tano (Kigoma na Tabora) ni Ahmed Idd Mgoyi na Yusuf Hamisi Kitumbo. Kanda Namba Sita (Katavi na Rukwa) ni Ayoub Nyaulingo, Blassy Mghube Kiondo, Nazarius A.M. Kilungeja. Kanda Namba Saba (Iringa na Mbeya) ni Ayoub Shaibu Nyenzi, Cyprian Charles Kuyava, David Samson Lugenge, Elias Lusekelo Mwanjala, Eliud Peter Mvella na John Mwachendang’ombe Kiteve.

Waombaji wa Kanda Namba Nane (Njombe na Ruvuma) ni James Patrick Mhagama, Kamwanga Rajabu Tambwe na Stanley William Lugenge. Kanda Namba Tisa (Lindi na Mtwara) ni Athuman Kingome Kambi, Francis Kumba Ndulane na Zafarani Mzee Damoder.

Kanda Namba Kumi (Dodoma na Singida) ni Charles Komba, Hussein Zuberi Mwamba na Stewart Ernest Masima. Kanda Namba 11 (Morogoro na Pwani) ni Farid Salum Mbarak, Geoffrey Irick Nyange, Juma Abbas Pinto, Riziki Juma Majala na Twahil Twaha Njoki.

Wanaowania kuteuliwa kugombea kupitia Kanda Namba 12 (Kilimanjaro na Tanga) ni Davis Elisa Mosha na Khalid Abdallah Mohamed wakati Kanda Namba 13 (Dar es Salaam) ni Alex Chrispine Kamuzelya, Muhsin Balhabou, Omar Isack Abdulkadir, Shaffih Dauda Kajuna na Wilfred Mzigama Kidao.

Kwa upande wa TPL Board waliotangazwa kuomba kuwania uongozi wa juu ni Hamad Yahya Juma (Mwenyekiti) na Said Muhammad Said Abeid (Makamu Mwenyekiti).

Wajumbe wa Kamati ya Uendeshaji ni Kazimoto Miraji Muzo, Michael Njunwensi Kaijage, Omari Khatibu Mwindadi, Salum Seif Rupia na Silas Masui Magunguma.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

kitwanga aiagiza tume ya mazingira (NEMC) kukagua mfumo wa maji taka dar kuanzia jumatatu

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Charles Kitwanga (kati) akikagua mfumo wa majitaka katika mtaa wa Mindu, Upanga,  jijini Dar es Salaam leo, wakati akikagua mifumo ya maji taka jijini humo na kutoa agizo kwa NEMC kufanya ukaguzi wa kina kuanzia Jumatatu...(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Presentation of Credentials by His Excellency Eng. John W.H. Kijazi – High Commissioner of the United Republic of Tanzania to Sri Lanka

$
0
0
His Excellency Eng. John William Herbert Kijazi, on 12th August 2013, presented his letters of Credence to the President of the Democratic Socialist Republic of Sri Lanka, His Excellency Mahinda Rajapaksa at the Presidential Secretariat in Colombo, Sri Lanka.
His Excellency Eng. John William Herbert Kijazi proceeds  to the dais to present his Credentials to the 

President of the Democratic Socialist Republic of Sri Lanka, His Excellency Mahinda Rajapaksa 
His Excellency Eng. John William Herbert Kijazi shakes  hands with  the President of the Democratic Socialist Republic of Sri Lanka, His Excellency Mahinda Rajapaksa  before presenting  his credentials
His Excellency Eng. John William Herbert Kijazi presents his credentials to the 

President of the Democratic Socialist Republic of Sri Lanka, His Excellency Mahinda Rajapaksa 
His Excellency Eng. John William Herbert Kijazi shakes hands with the Secretary to the President after presentation of Credentials

After having their photo taken, High Commissioner Kijazi expressed his gratitude to the President of Sri Lanka for receiving his Credentials as the High Commissioner of Tanzania to Sri Lanka (with Residence in New Delhi). He also assured him of his commitment to ensure that the bonds of friendship and cooperation between Tanzania and Sri Lanka are strengthened further during his tenure as the High Commissioner of Tanzania to Sri Lanka.

His Excellency Eng. John William Herbert Kijazi signs in the Visitors Book at the Presidential Secretariat. Left if  the Head of Chancery at the Tanzania High Commission in New Delhi, India,  Ms Badriya Ramdahan Kiondo, who accompanied him  

TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 LAITIKISA TABORA USIKU HUU.

$
0
0
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Neylee akiimba kwa hisia mbele ya wakazi wa mji wa Tabora waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,linalofanyika kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani  humu.Tamasha hilo linaandaliwa na kampuni bingwa ya Burudani hapa nchini,Prime Time Promotions Ltd kwa kushirikiana na Clouds FM,na kudhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake murua kabisa cha Serengeti Premium Lager.
Abdul Kiba,msanii wa muziki wa bongofleva akiimba mbele ya umati mkubwa wa wakazi wa mji wa Tabora waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,linalofanyika kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani  humu.Tamasha hilo linaandaliwa na kampuni bingwa ya Burudani hapa nchini,Prime Time Promotions Ltd kwa kushirikiana na Clouds FM,na kudhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake murua kabisa cha Serengeti Premium Lager.
 Sehemu ya  umati wa mji wa Tabora waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,linalofanyika kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani  humu.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Linah pichani kati akiwa na madensa wake wakitumbuiza jukwaani usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 ndani ya uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani  humu.
 Anaitwa Amin,mmoja wa wasanii mahiri akiwaimbisha mashabiki wake usiku huu kwenye u kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,linalofanyika kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani  humu. Tamasha hilo linaandaliwa na kampuni bingwa ya Burudani hapa nchini,Prime Time Promotions Ltd kwa kushirikiana na Clouds FM,na kudhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake murua kabisa cha Serengeti Premium Lager.
 Ni shwangwe tu usiku huu kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani Tabora.
Wakali wa kudansi kutoka THT,wakijulikana kwa jina la Makomanda wakionesha umahiri wao wa kucheza jukwaani usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013.
 Wanamuita Mzee wa Masauti,Christian Bella akiwaimbisha mashabiki wake wa muziki wa dansi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta,liinalofanyika usiku huu kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi.
 Sehemu ya umati wa wakazi wa mji wa Tabora waliojitokeza usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 wakiwa wamewasha tochi za simu zao wakiashiria kushoo love ya pamoja
Msanii wa muziki wa bongofleva,Rachael akicheza jukwaani na mmoja wa madensa wake,huku mashabiki wake wakipiga mayowe ya shangwa kuonesha kukunwa vilivyo na msanii huyo.
 Sehemu ya  umati wa mji wa Tabora waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,linalofanyika kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani  humu.Tamasha hilo linaandaliwa na kampuni bingwa ya Burudani hapa nchini,Prime Time Promotions Ltd kwa kushirikiana na Clouds FM,na kudhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake murua kabisa cha Serengeti Premium Lager.
PICHA ZAIDI BOFA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Wimbo wa Taifa wa disco enzi hizo ulikuwa wa DeBarge wa 'Rhythm Of The Night'
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images