Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

VYUO MBALIMBALI HAPA NCHINI VYATAKIWA KUHAMASISHA WATOTO WA KIKE KUPENDA MASOMO YA SAYANSI

$
0
0
Na Pamela Mollel,Arusha

Vyuo mbalimbali nchini vimetakiwa kuhamasisha wanafunzi wa kike kupenda kusoma masomo ya sayansi kuanzia ngazi za chini ili kuondoa changamoto ya uhaba wa wanasayansi wa kike uliopo hapa nchini. 

Aidha imeelezwa kuwa, kumekuwepo na uhaba mkubwa wa wanasayansi wanawake katika sekta mbalimbali hali inayochangiwa na kuwepo Kwa idadi ndogo ya wanafunzi wa kike wanaohitimu vyuoni. 

Hayo yalisemwa Jana na Mkurugenzi wa ufuatiliaji na udhibiti kutoka baraza la elimu ya ufundi, Dokta Annastella Sigwejo wakati akifungua kongamamno la kiteknolojia lililowashirikisha wanavyuo mbalimbali na makampuni jijini Arusha. Alisema kuwa, ili kuhakikisha tunapata wanasayansi wa kutosha ni lazima tuanze kuhamasisha wanafunzi wakiwa tangu ngazi za chini mashuleni ili wajijengee tabia ya kupenda masomo hayo hadi kufikia ngazi za juu .

Dokta Sigwejo alisema kuwa,kwa sasa hivi ambavyo nchi yetu inahamasisha Tanzania ya viwanda ni lazima kuwepo na wataalamu wanasayansi wa kutosha ambao wataweza kuziba mapengo mbalimbali yaliyopo na hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuhamasisha wanavyuo kupenda masomo ya sayansi. 

Kwa upande wa Mkuu wa idara ya Tehama upande wa taalamu kutoka Chuo cha Uhasibu Arusha, Pamela Chogo alisema kuwa, kongamano hilo ni la kwanza kufanyika jijini Arusha ambapo wameweza kuwakutanisha wanafunzi wa vyuo mbalimbali wanaosoma masomo ya sayansi jijini hapa pamoja na makampuni ili wajadili changamoto mbalimbali zilizopo .

Alisema kuwa, kumekuwepo na changamoto kubwa ya makampuni mengi kutokupenda na kuzidhamini Kazi zinazozalishwa na wazawa, hivyo kupitia kongamano hilo wanavyuo wataweza kuonyesha Kazi zao Kwa makampuni mbalimbali ili waweze kuzitambua na kuanza kuzitumia. 
Mkurugenzi wa ufuatiliaji na udhibiti kutoka baraza la elimu ya ufundi, Dokta Annastella Sigwejo wakati akifungua kongamamno la kiteknolojia lililowashirikisha wanavyuo mbalimbali na makampuni jijini Arusha,Chuo cha Uhasibu Arusha(Habari Picha na Pamela Mollel Arusha)
Mkuu wa Idara ya Tehama upande wa taalamu kutoka Chuo cha Uhasibu Arusha, Pamela Chogo akizungumza na waandishi wa habari , alisema kongamano hilo ni la kwanza kufanyika jijini Arusha ambapo wameweza kuwakutanisha wanafunzi wa vyuo mbalimbali wanaosoma masomo ya sayansi jijini hapa pamoja na makampuni ili wajadili changamoto mbalimbali zilizopo .
Kaimu Meneja Mamlaka ya Mawasiliano kanda ya Kaskazini Francis Msungu,akizungumza na vyombo vya habari alisema ni vyema watumiaji wa mitandao wakafanya matumizi salama ya kuelimisha na kuhabarisha zaidi
Wadau wa mkutano huo.


WAZIRI UMMY ATEMBELEA TAASISI YA SARATANI YA OCEAN ROAD,AWATAKA WAKAMILISHE HARAKA UFUNGAJI WA MASHINE MPYA ZA MIONZI

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu (Mb), amefanya ziara ya kikazi katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road ili kukagua utoaji wa huduma za Matibabu katika Hospitali hiyo. 

Katika ziara hiyo, Mhe. Waziri alifahamishwa kwamba mashine zote za tiba ya mionzi ya nje inafanya kazi vizuri na huduma zinaendelea kutolewa kwa wagonjwa.Pia wakati wa ziara hiyo, Mhe.Ummy alitumia fursa hiyo kuzungumza na wagonjwa mbalimbali waliokuwa wakipata huduma za tiba ya mionzi hospitalini hapo, huku baadhi ya wagonjwa walitoa malalamiko kwa Waziri kuwa, wamekuwa wakitumia muda mrefu kusubiri kupata huduma hususani huduma za mionzi ya nje. 

Kufuatia hali hiyo, mhe. Ummy alitoa maelekezo kwa uongozi wa Hospitali kuhakikisha wanaweka utaratibu mzuri ambao utapunguza muda kwa wagonjwa kusubiri huduma za mionzi ikiwemo kuwepo na ratiba ambayo kila mgonjwa atajua anafika saa ngapi kupata tiba hiyo.

Vile vile, mhe. Ummy alitembelea kitengo cha utoaji wa huduma za mionzi ya ndani ambapo alijionea changamoto ya kutokufanya kazi kwa mashine hizo za utoaji wa mionzi ya ndani kutokana na kukosekana kwa vifaa vya 'transfer tubes' na 'gyn applicators'.

Kufuatia hali hiyo mhe.Ummy alitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Ocean Road, Dkt.Julius Mwaiselage kuhakikisha kuwa mashine hizo zinafanya ndani ya siku 2 kwa kuazima hivyo vifaa hivyo kutoka Hospitali ya Bugando ili kurudisha huduma hizo kwa wagonjwa ambao wengi ni wanawake wenye tatizo la Saratani ya Mlango wa Kizazi.

"Naelekeza kuwa fanyeni utaratibu wa kupata kifaa kilichoharibika mapema iwezekanavyo" alisema mhe.Ummy.Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road , Dkt.Julius Mwaiselage alimhakikishia mhe.Waziri kuwa atajitahidi ili vifaa vilivyoharibika vinapatikana ndani ya siku mbili kutoka Hospitali Bugando na pia wameagiza vifaa hvyo kutoka kiwandani nje ya nchi kwa gharama ya Euro 43,200.00 
Mkurugenzi wa taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dkt Julius Mwaiselage akitoa maelezo kwa Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu juu ya ufanisi wa mashine mpya na yakisasa ya mionzi iliyopo katika taasisi hiyo.

 Mashine mpya na yakisasa ya mionzi iliyopo katika taasisi hiyo.


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisikiliza malalamiko ya mama aliekuwa akisubiri matibabu ya ugonjwa wa kansa katika taasisi hiyo ya Ocean Road. Wa katikati ni Mkurugenzi wa taasisi hiyo Dkt. Julius Mwaiselage.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimsililiza ndugu wa moja kati ya wagonjwa waliofika Hospitalini hapo kupata huduma za matibabu ya Saratani.

WAZIRI MKUU AONGOZA MAADHIMISHO YA KITAIFA YA SIKU YA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA MKOANI IRINGA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipeperusha bendera aliyokabidhiwa na wananchi waliofanya matembezi ya kutoa elimu kwa wananchi yaliyofanyika kwa siku tatu mkoani Iringa wakati wa maadhimisho ya kitaifa ya siku ya kupambana na dawa za kulevya Duniani.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea bendera kutoka kwa wananchi waliofanya matembezi ya kutoa elimu kwa wananchi yaliyofanyika kwa siku tatu mkoani Iringa wakati wa maadhimisho ya kitaifa ya siku ya kupambana na dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika katika kiwanja cha Kichangani mkoani Iringa leo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa(katikati) akiwapungia mikono wakati alipokuwa anapokea maandamano ya wananchi pamoja na wadau mbalimbali wa kupambana na dawa za kulevya wakati wa maadhimisho ya kitaifa ya siku ya kupambana na dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika katika kiwanja cha Kichangani mkoani Iringa leo. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza na kushoto ni  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mh. Jenista Mhagama.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa(kulia) akizungumza jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mh. Jenista Mhagama wakati wa maadhimisho ya kitaifa ya siku ya kupambana na dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika katika kiwanja cha Kichangani mkoani Iringa leo.
Baadhi ya wananchi pamoja na wadau wa kupambana na dawa za kulevya wakipita kwa bashasha mbele ya mgeni rasmi wakati wa maadhimisho ya kitaifa ya siku ya kupambana na dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika katika kiwanja cha Kichangani mkoani Iringa leo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Kamishna wa Sheria Edwin Kakolaki alipotembelea banda la mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevyawakati wa maadhimisho ya kitaifa ya siku ya kupambana na dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika katika kiwanja cha Kichangani mkoani Iringa leo.

UBALOZI WA TANZANIA NCHINI URUSI WATOA SOMO KWA WAMILIKI WA KAMPUNI YA UTALII NCHINI HUMO

$
0
0
BALOZI wa Tanzania nchini Urusi, Meja Jenerali Simon Mumwi leo ameendesha semina kwa wamiliki wa kampuni za uandazi wa ziara za  watalii (Tour Operators) jijini Moscow ili kuwapa ufahamu wa vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini Tanzania.

Semina hizo ambazo hufanyika mara moja kila mwezi, zinalenga kuongeza idadi ya watalii kutoka Urusi na nchi za jirani wanaotembelea Tanzania.

Akizungumza katika hafla hiyo, Balozi Mumwi alisema kuwa semina hizo zimekuwa na manufaa makubwa kwani katika kipindi kifupi zimesaidia sana kuongeza idadi ya watalii wanaotoka Urusi kwenda nchini Tanzania, ambapo alisema "katika kipindi cha miaka 10, idadi ya watalii kutoka Urusi imeongezeka kutoka 1,500 mpaka 15,000 mwishoni mwa mwaka 2015."
Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Meja Jenerali Simon Mumwi akizungumza wakati akifungua semina ya siku moja ya kuhamasisha utalii wa Tanzania nchini Urusi, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Ubalozi, 51 Ulitsa Bolshaya Nikitskaya, Jijini Moscow, nchini Urusi. wanufaika wa semina hiyo walikuwa ni waendeshaji wa ziara za Utalii kutoka nchini Urusi.
Afisa Mawasiliano wa Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi anayeshughulia pia maswala ya Utalii, Biashara na Uwekezaji, George Lengeju akieleza jambo kuhusiana na vivutio mbalimbali vilivyopo nchini Tanzania, katika semina ya siku moja kwa wamiliki wa kampuni za uandazi wa ziara za watalii (Tour Operators) nchini Urusi, iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Ubalozi, 51 Ulitsa Bolshaya Nikitskaya, Jijini Moscow.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Safari ambaye ndiye aliyewezesha kuwakutanisha wadau wa masuala ya utalii nchini Urusi, Galina Modestova akizungumzia vivutio mbalimbali vilivyopo nchini Tanzania kwa lugha ya kirusi.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

OFISI YA ROCK CITY MARATHON MWANZA YAZINDULIWA

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Bi. Merry Tesha (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ofisi ya Kanda ya Ziwa ya mbio za Rock City Marathon zilizopo kwenye la jengo la Rock City Mall jijini Mwanza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mbio hizo uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini humo. 
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Bi. Merry Tesha (kushoto) akipokea maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa mbio za Rock City Marathon Bw Zenno Ngowi (Kulia) kuhusu nafasi ya mbio hizo katika kutangaza fursa na vivutio vya utalii vilivyopo Kanda ya Ziwa mara baada ya kuzindua ofisi ya Kanda ya Ziwa ya mbio hizo zilizopo kwenye la jengo la Rock City Mall jijini Mwanza.
Mratibu wa mbio za Rock City Marathon kutoka kampuni Capital Plus International (CPI) Naftal Kasara (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Bi. Merry Tesha zawadi ya fulana za Rock City Marathon baada ya kuzindua ofisi ya Kanda ya Ziwa ya mbio hizo zilizopo kwenye la jengo la Rock City Mall jijini Mwanza. 
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Bi. Merry Tesha (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa mbio hizo mara baada ya kuzindua ofisi ya Kanda ya Ziwa ya mbio za Rock City Marathon zilizopo kwenye la jengo la Rock City Mall jijini Mwanza. Miongoni mwao ni pamoja na Mwenyekiti wa mbio hizo, Zenno Ngowi, (wa pili kushoto). 
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Bi. Merry Tesha (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Chama cha Riadha Mkoa wa Mwanza (MRAA mara baada ya kuzindua ofisi ya Kanda ya Ziwa ya mbio za Rock City Marathon zilizopo kwenye la jengo la Rock City Mall jijini Mwanza. 

Uwezo wa Wataalam Kupandikiza Figo Waimarishwa Muhimbili

$
0
0
Katika kipindi cha miezi minane Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imefanikiwa kupandikiza figo wagonjwa 10 kwa mafanikio makubwa ambapo katika kambi ya tatu ya upandikizaji figo, upasuaji umefanywa na watalaam wa MNH kwa zaidi ya silimia 80, huku wakisimamiwa na watalaam kutoka Hospitali ya Saifee ya nchini India.

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 26 Juni, 2018 jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru amesema MNH ilianza upandikizaji figo Novemba 2017 kwa kupandikiza mgonjwa mmoja ambapo Aprili 2018 wagonjwa wanne walipandikizwa figo na Juni 24 hadi 25, 2018 wagonjwa watano wamepandikizwa figo.

‘‘Pamoja na upasuaji huo kufanyika, mwaka 2016 hospitali ilipeleka watalaam wake nchini India kujengewa uwezo wa kupandikiza figo hivyo napenda kuwafahamisha kuwa tangu tumeanza upandikizaji wa figo tunaendelea kupata mafanikio makubwa kwa baadhi ya watalaam wetu wa ndani kuwa na uwezo wa kushika hatamu ya kufanya wenyewe katika mchakato mzima wa uchunguzi hadi kupandikiza figo,’’amesema Prof. Museru.

‘‘Tunaamini katika kambi mbili zinazokuja za upasuaji wa kupandikiza figo, madaktari wa upasuaji wazalendo watafikia kiwango cha asilimia 100. Hii ni hatua kubwa sana katika kipindi cha miezi minane kwani mara ya kwanza walikuja watalaam wote wanaohitajika wapatao 15, tulipofanya mara ya pili walipungua wakaja watalaam saba na safari hii mara ya tatu wamepungua wamekuja watano tu, tunaamini wataendelea kupungua katika kambi tatu zijazo na hatimaye kusimama wenyewe na kufanya kwa viwango na ubora uleule,” amesisitiza Prof. Museru.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 26 Juni, 2018 kuhusu wagonjwa watano kupandikizwa figo katika hospitali hii. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Figo na Mfumo wa Mkojo, Dkt. Mustafa Khokhawala, Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Mishipa ya Damu, Dkt. Aliasgar Behranwala na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Figo na Mfumo wa Mkojo, Dkt. Raval Ashiq Ali Ahmad, wote kutoka Hospitali ya Saifee iliyopo Mumbai nchini India. 
Kulia ni Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Figo na Mfumo wa Mkojo, Dkt. Njiku Kim, Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Figo na Mfumo wa Mkojo, Dkt. Victor Sensa naDkt. Isaack Mlatie ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Figo na Mfumo wa Mkojo- wote wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari.
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Figo na Mfumo wa Mkojo, Dkt. Isaack Mlatie akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu hospitali hii kufanikiwa kupandikiza figo kwa wagonjwa watano.
Baadhi ya wakurugenzi wa Muhimbili wakifuatilia mkutano huo leo.
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Mishipa ya Damu, Dkt. Aliasgar Behranwala kutoka Hospitali ya Saifee iliyopo Mumbai nchini India na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Figo na Mfumo wa Mkojo, Dkt. Njiku Kim wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakipandikiza figo mmoja wa wagonjwa watano walipatiwa huduma hiyo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MNADHIMU MKUU JWTZ AWAONYA ASKARI WAPYA KUTOJIINGIZA KATIKA SIASA

$
0
0
MNADHIMU Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Yacoub Mohamed amewaonya askari wapya wa jeshi hilo kutojiingiza katika masuala ya siasa.

Aidha hakusita kuwapa tahadhari zaidi kwamba atakayebainika atachuliwa hatua kali za kinidhamu ikiwano kufukuzwa jeshini.

"Jeshini hakuna siasa, hapa mnaenda kutekeleza Katiba ya nchi, jukumu lenu kubwa ni kulinda mipaka ya nchi, Katiba na maelekezo kutoka kwa viongozi wenu," alisema Luteni Jenerali Mohamed.Mafunzo hayo yalihusisha vijana 2,253 yalifanyika kwa miezi 4 katika Shule ya Mafunzo ya Awali ya Kijeshi (RTS), Kihangaiko iliyopo Bagamoyo Pwani.

Kwa upande Kaimu Mkuu wa Shule hiyo Kanali Sijaona Myala alisema kazi ya jeshi ni kuandikisha askari kwa ajili ya kulinda mipaka ya nchi na vita."Kazi ya jeshi ni kuandikisha askari na si ajira, ikitokea vita hata hawa wote wakifa, tutaandikisha wengine," alisema Kanali Myala.


Mbali ya kufungwa kwa mafunzo hayo, askari waliohitimu walionyesha maonyesho ya ukakamavu, sarakasi na vikwazo.
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Yacoub Mohamed akikagua gwariide la askari wapya wa JWTZ waliomaliza mafunzo yao ya awali katika Shule ya Kijeshi RTS Kihangaiko iliyopo Bagamoyo, Pwani nyuma mwisho ni Kaimu Mkuu wa Shule hiyo Kanali Sijaona Myala.
Maofisa wa JWTZ wakiongoza Gwaride wakati wa kufunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa askari wapya 2,253 yaliyofanyika Shule ya Mafunzo ya Awali ya Kijeshi RTS Kihangaiko Bagamoyo mkoani Pwani. 
Mwalimu wa moja ya michezo ya ukakamavu akionyesha namna ya kupita chini ya moto wakati wa maonyeshi yaliyofanyika chuoni hapo.
Askari wapya wakipimana nguvu kwa kuzichapa mbele ya mgeni rasmi Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Lutena Jenerali Yacoub Mohamed aliyefunga mafunzo ya awai ya askari hao 2,253 yalifanyika Shule ya Mafunzo ya Awali ya Kijesjhi (RTS) Kihangaiko Bagamoyo Pwani. 
Askari wapya wakimsikiliza mgeni rasmi Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Yacoub Mohamed alipokuwa akizungumza nao kabla ya kufunga mafunzo yao ya kundi la 38A/17 lililokuwa na askri 2253. 
Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Yacoub Mohamed katikati akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa jeshi waliopop kazini pamoja na wastaafu wakati wa kufunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa askari 2253 yaliyofanyika Shule ya Mafunzo ya Aawali ya Kijeshi RTS Kihangaiko Pwani. 

TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI IMETOA MAFUNZO MAALUM KWA WAHANDISHI

$
0
0

Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imetoa Mafunzo maalum kwa wahandisi watakaosimamia ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji kwenye skimu kumi na sita(16) zitakazojengwa mwaka ujao wa fedha, 2018/2019 kutoka kwenye kanda nane (8) za Tume ya Taifa ya umwagiliaji, Halmashauri za wilaya pamoja na wakandarasi, ikiwa na lengo la kuwajengea uwezo uelewa na uzoefu zaidi wahandisi hao katika usimamizi wa mikataba na ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji.

Akizungumza katika warsha hiyo ya mafunzo ya siku tatu iliyofanyika Mkoani Shinyanga, Kaimu Mkurugenzi wa uendelezaji wa miundombinu ya Umwagiliaji kutoka Tume hiyo Mhandisi, Pascal Shayo, alisema kuwa Tume imetoa Mwongozo wa ujenzi wa skimu za umwagiliaji na alisisitiza ya kuwa, wahandisi waliopewa mafunzo hayo wanatakiwa wasimamie ujenzi wa skimu hizo kwa kufuata mafunzo waliyoyapata ili kuhakikisha miundombinu hiyo inajengwa kwa kiwango kinachotakiwa.

“Mhandisi atakayeshindwa kusimamia vizuri atachukuliwa hatua kwani kwa kupitia mafunzo haya wameshapata uelewa wa kutosha.”Alisisitiza

Kwa Upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango Sanifu na Uratibu wa Sekta Binafsi kutoka katika Tume hiyo Mhandisi Muyenjwa Maugo alisema warsha hiyo ina lengo la kuhakikisha miradi yote ya umwagiliaji inajengwa katika kiwango elekezi na wananchi wanapata huduma iliyokusudiwa katika kilimo cha umwagiliaji na kuzalisha mazao bora.

“Lengo kubwa ni kujenga uwezo kwa wahandisi na wataalam wa umwagiliji ili kuweza kusimamia miradi ya umwagiliaji kwa ufanisi, na kupitia miradi hii tunaweza kuwafundisha wahandisi namna ya kutumia mwongozo uliyopo katika kusimamia shughuli za umwagiliaji.” Alibainisha Maugo.

Awali imeelezwa kuwa ,ujenzi wa skimu hizo kumi na sita (16) utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 6.5 ambazo ni mkopo kutoka serikali ya Japani kupitia shirika lake la maendeleo la kimataifa (JICA).


Katika picha kutoka kushoto, Kaimu Mkurugenzi Muhandisi Willson Karumuna, Kaimu Mkurugenzi Mhandisi Pascal Shayo, Kaimu Mkurunzi Msaidizi Mhandisi Ntonda Kimasa na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Mhandisi Muyenjwa Maugo wakifuatila Jambo katika Mafunzo ya wahandisi na wataalam kutoka katika Halmashauri kwenye warsha ya Mafunzo, yalihusu ujenzi wa skimu za umwagiliaji iliyofanyika mkoani Shinyanga.
Katika Picha wahandisi na wataalam wakiwa katika hatua ya mafunzo kwa vitendo katika eneo la Nyida, mara baada ya warsha ya mafunzo iliyohusu ujenzi wa skimu za umwagiliaji iliyofanyika Mkoani Shinyanga.


MISS MBEYA YARUDI KIVINGINE.

RC TABORA AAGIZA KUCHUKULIWA HATUA KWA WATENDAJI WALIOSABABISHA KUWEPO HOJA ZA CAG

$
0
0
NA TIGANYA VINCENT,RS TABORA

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ameuagiza Katibu Tawala Mkoa (RAS) kuwachukuliwa hatua Wakuu wa Idara wote waliosababisha kuibuka kwa hoja za ukaguzi wa Hesabu za serikali katika Halmashauri mkoani humo.

Aliyasema hayo jana wilayani Nzega kwenye baraza maalumu la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo la kujadili na kujibu hoja za Mkaguzi wa hesabu za serikali kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30 mwaka huu.

Mwanri aliwataka RAS kuanza kuwachukulia hatua kwa kuwaondoa Wakuu wote wa Idara ambao wamekwenda kinyume cha taratibu na hivyo kuzisababishia Halmashauri zao kuwa na hoja.

Alisema hoja nyingi ambazo zimeibuka zinasababishwa na wakati mwingine manunuzi yaliyofanyika kukosa viambatanisho kama vile stakabadhi za malipo yaliyofanyika na nyingine kutofuata taratibu za manunuzi jambo ambalo linaloelekea katika matumizi mabaya ya fedha za umma.Mwanri alisema Serikali haiwezi kumvumilia Mtendaji au Mkuu yoyote wa Idara ambaye hana nidhafu katika matumizi ya fedha za umma na hivyo kusababisha hasara ambayo inapelekea baadhi ya miradi kutokamilika.

Mkuu huyo wa Mkoa alitoa Mwezi mmoja hoja zote zilizotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali zinapata majibu ikiwa na kuwachukulia hatua wale wote watakaobainika kusababishia Halmashauri ya Wilaya ya Nzega hasara.Alimwagiza Katibu Tawala Mkoa kuhakikisha kwa wale ambao walisababisha hasara Halmashauri hiyo kuwasiliana na Tamisemi hata kama wamehama warudishwe waje wajibu hoja zinazowakabili.

Katika hatua nyingine aliitaka Halmashauri hiyo kuja na utaratibu wa kulipa madeni ikiwa ni pamoja na ile asilimia 10 kwa ajili ya vijana , wanawake na walemavu.Alisema kuwa utaratibu huo ni lazima pia uonyesha jinsi pesa hizo zitakavyorejeshwa ili watu wengine waweze kukopa.

Naye Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Robert Makungu aliwataka watendaji mbalimbali kuwa na uzalendo wakati wa utekelezaji wa majukumu yao ya kuwahudumia wananchi ili kuhakikisha kila wanachokifanya kinazingatia maslahi mapana ya umma.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggre Mwanri akitoa maoni wakati wa Kikao maalumu cha Baraza la Madiwani cha kujadili ya kupitia taarifa ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kilichofanyika jana katika Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Robert Makungu akitoa maoni yake wakati wa Kikao maalumu cha Baraza la Madiwani cha kujadili ya kupitia taarifa ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kilichofanyika jana katika Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggre Mwanri akitoa ufafanuzi juu ya hoja mbalimbali wakati wa Kikao maalumu cha Baraza la Madiwani cha kujadili ya kupitia taarifa ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kilichofanyika jana katika Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
Mkaguzi Mkuu wa Nje wa Mkoani Tabora kutoka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) Mohamed Msangi alitoa taarifa ya ukaguzi wakati wa Kikao maalumu cha Baraza la Madiwani cha kujadili ya kupitia taarifa ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kilichofanyika jana katika Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega wakiwa katika Kikao maalumu cha Baraza la Madiwani cha kujadili ya kupitia taarifa ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kilichofanyika jana katika Halmashauri ya Wilaya ya Nzega

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA UGENI KUTOKA LIWALE MKOANI LINDI

$
0
0
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akisalimiana na Mbunge wa Liwale Mhe. Zuberi kuchauka (kulia) na Ndg. Jivunie Mbunda (aliebebwa) ambae ni mlemavu wa kimo kutoka Liwale Mkoani Lindi walipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akizungumza na Mbunge wa Liwale Mhe. Zuberi kuchauka (kulia) pamoja na wanandoa Ndg. Jivunie Mbunda ambae ni mlemavu wa kimo (kushoto) na Mkewe Ndg. Amina Mbunda wote kutoka Liwale Mkoani Lindi (wa pili kushoto) walipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mbunge wa Liwale Mhe. Zuberi kuchauka (kulia) na Wana ndoa Ndg. Amina Mbunda (kushoto) na Mumewe Ndg. Amina Mbunda (aliebebwa) ambae ni mlemavu wa kimo kutoka liwale Mkoani Lindi walipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE

MEDDIE KAGERE ATUA SIMBA KWA DAU LA MILIONI 120

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Mabingwa wa ligi kuu Tanzania BaraKlabu ya Simba imefanikiwa kunasa saini ya mshambuliaji wa Gor Mahia FC Meddie Kagere kwa donge nono kuja kuwatumikia wanamsimbazi hao kwa kandarasi ya miaka miwili.

Simba wamewapiku mahasimu wao wakubwa Yanga ambao walionesha nia ya kumtaka kabla ya kuzidiwa kete na wanamsimbazi hao.Kagere aliyetua jana nchini akiambatana na wakala wake amesaini donge nono la Dola 603,000 sawa na milioni 120 na mshahara wa dola 4,500 sawa na Milion tisa kwa mwezi.

Mshambuliaji huyo wa kutumainiwa katika klabu ya Gor Mahia mwenye asili ya Rwanda ataanza kutumikia klabu ya Simba baada ya kumalizika kwa mashindano ya Kombe la Shirikisho hatua ya makundi ambapo wapo kundi moja na Yanga.

Kagere alikua moto wa kuotea mbali katika mashindano ya Sportpesa yaliyofanyika mwaka huu nchini Kenya akiwafunga Simba katika mchezo wa fainali.Baada ya usajili huo Simba imeonyesha kulipa kisasi kwa Yanga wakikumbuka msimu wa 2012 na 2013 wakiwapita njia za mkato na kuwasajili Haruna Niyonzima na Mbuyu Twite ambapo kwa sasa Simba wamewasha moto wakionekana wamedharia kuunda kikosi bora kwa msiku wa 2018/19.


DK. KIGWANGALLA AFUNGUA WARSHA YA KITAIFA YA WADAU WANAOPINGA VITENDO VYA UHALIFU DHIDI WANYAMAPORI NA MISITU NCHINI

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akifungua warsha ya siku moja ya wadau wa kitaifa wa kupinga vitendo vya uhalifu dhidi ya wanyamapori na misitu nchini jijini Dodoma leo Juni 26, 2018. Warsha hiyo imelenga kujadili na kuainisha mahitaji na vipaombele vya sekta ya mahakama na mashtaka ya kudhibiti uhalifu huo. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Iddi Mfunda (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Mashtaka, Biswalo Mganga (wa pili kulia) na Mkuu wa ofisi wa Shirika la Ufuatiliaji wa Wanyamapori (TRAFFIC), Julie Thomson (kulia) wakiimba wimbo wa Taifa wakati wa warsha ya siku moja ya wadau wanaopinga vitendo vya uhalifu dhidi ya wanyamapori na misitu nchini jijini Dodoma leo Juni 26, 2018. 
Baadhi ya wadau wa kitaifa walioshiriki hafla hiyo wakiimba wimbo wa Taifa.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akifungua warsha ya siku moja ya wadau wa kitaifa wa kupinga vitendo vya uhalifu dhidi ya wanyamapori na misitu nchini jijini Dodoma leo Juni 26, 2018. Warsha hiyo imelenga kujadili na kuainisha mahitaji na vipaombele vya sekta ya mahakama na mashtaka ya kudhibiti uhalifu huo. 
Picha ya pamoja ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na wadau wa kitaifa wa kupinga vitendo vya uhalifu dhidi ya wanyamapori na misitu nchini. (Picha na Hamza Temba-Wizara ya Maliasili na Utalii)

WATU MILIONI 125 WAKO HATARINI KUATHIRIWA NA KEMIKALI AINA YA ‘ASBESTOS”

$
0
0
Na EmanuelMadafa,Mbeya.

Imeelezwa kuwa watu wapatao milioni 270 wanahusika na ajali za kemikali maeneo ya kazi na watu milioni 160 wanasumbuliwa na magonjwa yanayotokana na madhara ya kemikali Duniani .

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali, Christopher Anyango, kwenye ufunguzi wa mafunzo ya kuelimisha wadau wa madini, wakiwemo wachimbaji, wachenjuaji pamoja na wasambazaji wa vifaa vya kemikali Wilayani Chunya, Mkoani Mbeya.

Amesema, kati yao watu milioni 125 duniani, wako katika hatari ya kudhurika na kemikali aina ya ‘asbestos” huku 90,000 wakipoteza maisha kila mwaka na kwamba madini hayo yanatumiwa zaidi kwenye viwanda vya kutengenezea mabati.

Aidha Mkurugenzi huyo amedai kuwa ukiachana na shughuli za kwenye madini, pia kemikali hiyo ya “asbestos” hutumika kutengenezea mabati na watu wanatumia bidhaa hii kwenye ujenzi wa nyumba hivyo ni vema watengenezaji wa vifaa hivyo wakapatiwa elimu jinsi ya njia bora ya kutumia kemikali hii ili isilete madhara kwa binadamu.

Hata hivyo , amesema kwenye madini mbalimbali kemikali zinazotumiwa ni Sodium Cyanide na Sulphuric Acid na nyinginezo ambazo zote ni hatari kwa afya na mazingira na pia ni kemikali bashirifu hivyo matumizi yake na usimamizi unahitaji uelewa unaojitosheleza ili kuzuia madhara yanayoweza kujitokeza.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Rehema Madusa akifungua mafunzo hayo, amewataka wakemia wanahusika na upimaji wa sampuli za madini kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa waledi kwa lengo la kuwasaidia wananchi eza kupata dhahabu sanjali na kusaidia kupatikana kwa mrahaba wa serikali.
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali, Christopher Anyango, akisoma hotuba kwenye ufunguzi wa mafunzo ya kuelimisha wadau wa madini, wakiwemo wachimbaji, wachenjuaji pamoja na wasambazaji wa vifaa vya kemikali Wilayani Chunya, Mkoani Mbeya.
Wadau wa madini, wakiwemo wachimbaji, wachenjuaji pamoja na wasambazaji wa vifaa vya kemikali wakiwa makini katika ufunguzi wa semina iliyoandaliwa na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali katika ukumbi wa mikutano wa Wilayani Chunya, Mkoani Mbeya.
Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Rehema Madusa akifungua mafunzo kwa wadau wa madini, wakiwemo wachimbaji, wachenjuaji pamoja na wasambazaji wa vifaa vya kemikali Wilayani Chunya, Mkoani Mbeya.
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema Madusa (katikati ) na viongozi kutoka ofisi ya mkemia walioketi katika picha ya pamoja na wadau wa madini, wakiwemo wachimbaji, wachenjuaji pamoja na wasambazaji wa vifaa vya kemikali Wilayani Chunya katika picha ya pamoja.

BALOZI MIGIRO AZINDUA RASMI JUMUIYA YA WATANZANIA WAISHIO UINGEREZA-ATUK

$
0
0
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Dkt. Asha-Rose Migiro,  alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za uzinduzi wa Jumuiya Mwamvuli ya Watanzania waishio nchini Uingereza na Ireland ya Kaskazini iitwayo ATUK –Association of Tanzanians in the UK zilizofanyika mjini Reading tarehe 23 Juni, 2018. Jumuiya hii inatokana na muungano wa jumuiya za diaspora kutoka mikoa mbalimbali ya hapa Uingereza na wanachama wa kujitegemea. 

Wajumbe wa Kamati ya Muda iliyoratibu kuanzishwa kwa ATUK walipongeza na kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli za kupambana na ufisadi, kusimamia uwazi na uwajibikaji katika utumishi wa umma na kuongeza kasi ya kujenga uchumi wa viwanda. Kauli mbiu ya hafla hii ilikuwa “UMOJA NI NGUVU, TANZANIA YA VIWANDA INAWEZEKANA”. Hivyo mojawapo ya malengo ya kuanzishwa kwa ATUK ni kujenga umoja na kukusanya nguvu za kuchangia jitihada za kujenga uchumi wa viwanda nchini mwetu.

Akihutubia hadhara hiyo Balozi Migiro aliwapongeza ATUK na alihimiza umoja na kukumbusha kwamba wakati wote Mhe. Rais amekuwa akisisitiza umoja wa Watanzania bila kujali tofauti zao kwani umoja ni nyenzo muhimu ya kujiteletea maendeleo. Hivyo Balozi Migiro aliwashukuru kwa Muungano huo na kueleza kwamba wakiendeleza mshikamano wataweza kuchangia kwa ufanisi jitihada kubwa za Mhe. Rais Magufuli na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuwaletea maendeleo Watanzania wote.
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Dkt. Asha-Rose Migiro akiitazama keki iliyoandaliwa wakati wa uzinduzi rasmi wa Jumuiya ya Watanzania waishio Uingereza (Association of Tanzanians in the UK-ATUK) 
Mhe. Balozi Migiro akifurahia jambo na sehemu ya Watanzania walioshiriki uzinduzi huo 
Sehemu ya Watanzania na wageni waalikwa waliohudhuria tukio hilo la kihistoria .

DOKTA PHILIP MPANGO AHITIMISHA MJADALA WA BAJETI BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akihitimisha hoja ya mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka 2018/19, Bungeni, Dodoma, ambapo ameahidi kusimamia mapato na matumizi ya fedha za umma kwa ufanisi na kuwatahadharisha wabadhilifu wa fedha za umma kuwa ni sawa na kula sumu. 
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Naibu wake Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), wakifuatilia hoja za Mawaziri wakati wa kuhitimisha hoja ya mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka 2018/19, Bungeni, Dodoma. 
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akijibu hoja mbalimbali za wabunge wakati wa kuhitimishwa kwa hoja ya mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka 2018/19, Bungeni Dodoma, ambapo alizitaka Halmashauri kuendelea kubuni miradi ya kimkakati ili kujiongezea kipato.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), na Waziri wa Madini, Mhe. Anjellah Kairuki (Mb), wakijadili jambo muda mfupi baada ya kuhitimishwa kwamjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka 2018/19, Bungeni Dodoma.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto), akipongezwa na Mbunge wa Kiembe Samaki Mhe. Ibrahim Raza kwa hitimisho zuri la Hoja ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa kusisitiza weledi katika usimamizi wa fedha za umma.

 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akipongezwa na Mbunge wa Kwimba Mhe. Mansoor Sharif, baada ya kuhitimisha ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mipango madhubuti ya kufikia uchumi wa kati. 


MTANZANIA ANAYEISHI UJERUMANI AANDAA MAFUNZO YA DANSI IJUMAA HII

$
0
0
Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
Watanzania wenye vipaji wametakiwa kutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza na wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika mafunzo ya kucheza yatakayoendeshwa na Mtanzania Emanuel Houston anayeishi Nchini Ujerumani.
Emanuel aliyewasili usiku wa 9 akiwa ameambatana na mkewe pamoja na wageni wengine na kupokelewa na baba yake mzazi Lusi Houston ambao kwa pamoja watatoa mafunzo ya kudansi kwa watanzania wenye vipaji.

Hii ni mara ya pili kwa Emanuel kuja nchini Tanzania kutoa mafunzo baada ya March mwaka jana kutoa elimu hiyo kwa vijana na kuonesha muitikio mzuri.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere JNIA  Emanuel  amesema kuwa anafurahi kuja Tanzania kwa mara nyingine tena kuja kutoa elimu ya dansi kwa vijana wa kitanzania na kwa mwaka huu mafunzo hayo yatakuwa kwa siku moja.

"Nafurahi kuja Tanzania kwa mara nyingine tena na kwa mwaka huu mafunzo haya yatakuwa kwa siku moja ambayo itakuwa ni Ijumaa nannawataka vijana wajitokeza kwa wingi,"amesema Emanuel.

"Mbali na kupata mafunzo hayo kwa sasa natafuta wadhamini watakaosaidiana na mimi kwani nina malengo ya kuwapatia fursa vijana watakaofanya vizuri wawili kwenda nchini Ujerumani kwa mafunzo zaidi ya kudansi, ambapo mimi nitataka wawakatie tiketi ila gharama zingine zote zitakua ni juu yangu,"amesema.
Emanuel amesema kuwa ameambatana na wanafunzi wake ambao wanadansi katika shuke yake nchini Ujerumani wenye umri takribani miaka 65 na bado wana nguvu ambapo kwa pamoja watashirikiana kutoa mafunzo hayo.
Baba mzazi Luis Houston amesema kwanza anafurahi sana wamefika salama nchini kwani yeye ni mtanzania ila ameishi miaka 40 nchini Ujerumani na bado hajasahau kuja nyumbani kutoa mafunzo hayo ambayo yana tija kwa vijana wenye vipaji.
Amesema kuwa watanzania wajitokeze kwa wingi kuja kupata mafunzi hayo kwa mwaka huu yatakayofanyika Oysterbay wakiwa na mwenyeji wao Benard Paul 'Ben Pol'.
Emanuel pamoja na baba yake wana shule ya mafunzo ya dansi nchini Ujerumani wakifundisha watu wa rika mbalimbali.
Mtanzania anayeishi Ujerumani Emanuel Houston akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa ajili ya mafunzo ya dansi kwa vijana wenye vipaji nchini yatakayofanyika ijumaa.
Baba mzazi Luis Houston akizungumza na waandishi  wa habari baada ya mtoto wake Emanuel Houston (kulia) kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa ajili ya mafunzo ya dansi kwa vijana wenye vipaji yatakayokuwa siku ya Ijumaa.
Picha ya Pamoja ya Emanuel Houston (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na mkewe na baba yake  Luis Houston na wageni wengine waliofika kwenye mafunzo ya dansi yatakayoendeshwa Ijumaa hii.
Picha na Zainab Nyamka Globu ya Jamii.

BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA ZISIPOKOMESHWA ATHARI KUBWA KUONGEZEKA

$
0
0
Biashara ya dawa za kulevya zisipokomeshwa na kuachwa ikaendelea nchini, athari zaidi  ikiwemo kuingiliwa kwa misingi ya kiutawala na wafanyabiashara wa dawa hizo kwa manufaa yao wao wenyewe binafsi zitaendelea kujitokeza kwani dawa za kulevya  limekuwa tatizo kubwa katika ulimwengu mkubwa na hata katika nchi ya Tanzania.
Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama ameyasema hayo, wakati wa kilele cha maadhimisho ya Kitaifa ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya duniani iliyokwenda kwa kaauli mbiu ‘Tujenge Maisha yetu, Jamii yetu na Utu wetu bila Dawa za Kulevya’ iliyofanyika leo Mkoani Iringa.
Amesema matumizi na biashara ya dawa za kulevya yameendelea kusababisha madhara makubwa sana katika nchi ya Tanzania yakiwemo ya kiafya, madhara katika jamii inayotuzunguka, kiuchumi,  kimazingira, kisiasa na hata kiusalama.
Ameongeza kuwa matumizi ya dawa za kulevya ambayo kwa kiasi kikubwa watumiaji wake ni vijana yanaathari kubwa na hatari ya kupoteza nguvu kazi ya taifa letu hivyo, kwani wao ni tegemeo la taifa hasa katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo endelevu, .matuimizi ya dawa za kulevya yasipopigwa vita na kuzuiliwa yataathiri uchumi wa nchi yetu, uzalishaji maadili, jamii na usalama kwa ujumla wa taifa letu.
“Mapambano  dhidi ya dawa za kulevya ni vita kubwa inayohitaji nguvu ya pamoja kwani madhara yake ni makubwa kwa jamii yetu hasa kwa vijana ambao ni nguvu kazi kwa taifa letu.., Ni ukweli usiopingika kuwa maendeleo ya usatawi wa taifa duniani  na hata katika nchi yetu yanategemea sana  nguvu kazi na hasa nguvu kazi ya vijana”, amesema Mhagama.
Pia amesema, mabinti wengi ambao wako katika umri wa, kusaidia kuongeza nguvu kazi katika nchi yetu wanakatishwa ndoto zao kwa kutumia dawa hizi na hata kupata madhara yanawasababishia matatizo mbali mbali jambo ambalo ni la kusikitisha sana
“Ni matarijio yangu kupitia maadhimisho haya ya siku ya leo wananchi wa mkoa wa Iringa, watakumbushwa na kuhamasishwa kushirikiana na serikali katika kupambana na vita hii kwani watumiaji wa dawa za kulevya ni watanzania wenzetu, tunaishi nao kila siku, ni vijana wetu tuliowazaa ni watoto wetu, hivyo ni wakati muafaka kwa kila mmoja wetu kusoma sheria kuhusu uuzaji utumiaji wa dawa za kulevya sambamba na ufahahamu wa athari za dawa hizo hapa nchini.
Amesema, kwa mujibu wa utafiti wa nguvu kazi wa mwaka 2014 inaonesha kuwa, nguvu kazi ya vijana wenye umri kati ya miaka 15 and 35 ni takribani watanzania  milioni 12.5 ambao ni sawa na asilimia 56 ya nguvu kazi yote ya nchi yetu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mh. Jenista Mhagama akizungumza  na wananchi wa mkoa wa Iringa  wakati wa maadhimisho ya kitaifa ya siku ya kupambana na dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika katika kiwanja cha Kichangani mkoani Iringa leo.

BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 26.06.2018

Bilioni 77 za Mradi wa Tscp zatekeleza Agizo Rais JPM Jijini Dodoma.

$
0
0
Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI. 
 Mradi wa Mpango Miji Mkakati ‘Tanzania Strategic Cities Project’ maarufu kama Tscp unaosimamiwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI umetekeleza Agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa Fedha zaidi ya Tsh. Bil 77 kwa ajili ya kujenga miundombinu katika Jiji la Dodoma. 
 Akizungumza katika hafla ya utiaji saini miradi hiyo itakayotekelezwa kupitia mradi wa Tscp Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Selemani Jafo amesema mradi huu wa kimkakati umelenga kubadilisha kabisa muonekano wa Jiji la Dodoma kwa kutekeleza yale aliyoagiza Mhe.Rais alipotangaza kuipandisha hadhi iliyokuwa Manispaa ya Dodoma kuwa Jiji. 
 “Jiji hili lazima liwe la tofauti, lenye hadhi ya Makao Makuuu ya Nchi na livutie kuliko majiji yote Tanzania, tutaweka miundombinu ambayo itabadilisha kabisa muonekano wa Jiji, itaongeza fursa za biashara na kuwapunguzia kabisa adha wananchi wetu katika maeneo ambayo wamekuwa wakiyalalamikia. Tuna imani kupitia kazi itakayofanyika hapa mtu aliyeondoka Dodoma mwaka huu akirudi baada ya miaka miwili tutamshika mkono kumuelekeza mitaa ya Jiji la Dodoma, hapatakuwa kama palivyo sasa na mabadiliko yatayofanyika ni ya kimataifa” Alisema Jafo. 
 Kupitia hafla hiyo Mhe. Jafo aliwatahadharisha wakandarasi washauri wa mradi kusimamia mradi huo kwa mujibu wa taratibu na sheria na kuhahakisha thamani ya fedha inaonekana kwa kila kipengele kitakachotekelezwa. 
 “Mkandarasi mshauri wajibu wenu ni kuhakikisha kila kilichoainishwa kiinafanyika kwa wakati na kwa usahihi wakati huo huo kumshauri mteja wao ambaye ni Halmashuri kufanya yale yote yanayotakiwa ili kazi iende sawa na kumsimamia mkandarasi kufanya kazi hiyo kwa ubora wa hali ya juu na endapo utaenda kinyume na haya Wizara yangu haitasita kukuchukulia hatua kwa mujibu wa sharia” alisema Jafo. 
 Alimazia kuwa Ofisi ya Rais TAMISEMI inatekeleza miradi mikubwa mitatu kwa fedha za mkopo toka Benki ya Dunia yenye lengo la kuimarisha na kuboresha Halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji pamoja na Mkoa mzima wa Dar es Salamm ili mamlaka hizo ziweze kukua kulingana mabadiliko tunayokwenda nayo kuelekea uchumi wa kati na ziweze kutoa huduma bora kwa wananchi wake. Jafo alitaja miradi mikubwa ya miundombinu inayosimamiwa na Ofisi yake kuwa ni Mradi wa Mpango Miji Mkakati (Tscp) unatekelezwa kwenye Majiji na Manispaa 8 na Dodoma ikiwa ndani ya mradi huu ambao utagharimu jumla ya fedha za kitanzania sh Bil 840, Mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam(Dmdp) ambao ni maalumu kwa kushughulikia changamoto za Jiji la Dar es salaam nao utagharimu Tsh. Bil 660 pamoja na Mradi wa Uendelezaji na Uboreshaji wa Halmashauri za Miji(Ulgsp) unatekelezwa katika Miji 18 na unagharimu Tsh. Bil. 650. 
 Naye Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma Mhe. Anthony Mavunde akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa miradi ya miundombinu katika Jiji la Dodoma ameishukuru Serikali kwa kuleta Fedha kwa ajili ya ujenzi wa miradi itakayofungua milango ya maendeleo katika Jiji la Dodoma. 
 Pia aliwakumbusha wananchi wa Dodoma kuitumia fursa hii ya upatikanaji wa miradi mikubwa kama chachu ya maendeleo ambayo itakuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla na kubadilisha maisha kutoka yalivyo sasa na kuwa bora zaidi. 
 Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Bilinith Mahenge amesema miradi hii ni fedha nyingi sana na Serikali imeamua kuwekeza katika Jiji hili hivyo yeye kama msimamizi Mkuu wa shughuli za Mkoa huu atahakikisha atasimamia kwa karibu miradi hii ili ikamilike kwa wakati na kwa ubora wa hali ya juu. 
 Akiwasilisha taarifa mradi Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi ametaja kazi zitakazofanyika kupitia mradi wa TSCP kuwa ni Ujenzi wa barabara za Lami Km 26.6, Taa za barabrani 913, mfereji mkubwa wa kusafirishia maji ya mvua Km 6.5, Ujenzi wa Stendi ya Kisasa, Soko kuu la Kisasa, vizimba 7 vya kukusanyia taka, kituo kikuu cha kuegeshea malori pamoja na bustani ya kupumzikia yenye viwanja mbalimbali vya michezo. 
 Aliongeza kuwa barabara za lami zitajengwa maeneo ya katikati ya mji, pembezoni pamoja na barabara moja kubwa ya mchepuko zitajengwa kwa kiwango cha Lami Ngumu (Concret Asphat) na zitakuwa na eneo la waenda kwa miguu, mifereji ya maji ya mvua pamoja na Taa za barabara zinazotumia nguvu ya jua. 
 Akizungumzai ujenzi wa stendi ya kisasa itakayojengwa eneo la Nzuguni Kunambi amesema itajengwa kwenye eneo lenye ukubwa wa Ekari 87 itakua na uwezo wa kuegesha Mabasi Makubwa 250, Mabasi madogo na magari ndogo 600, Bajaji 300 na pia itakua na maeneo makubwa ya biashara pamoja na eneo maalumu kwa ajili ya wafanyabiashara ndogondogo (Machinga) pamoja na mama lishe. Kazi hii inaanza rasmi Julai Mosi,2018 na itachukua muda wa miezi 15 hadi kukamilika kwake.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini miradi mikubwa ya uboreshaji wa miundombinu katika Jiji la Dodoma itakayogharimu zaidi ya Fedha za Kitanzania Tsh. Bil 77 pembeni  yake ni Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi.
Huu ndio muonekano wa Stendi ya Kisasa itakayojengwa katika Jiji la Dodoma kupitia mradi wa Tscp


Mstahiki Meya wa Manispaa ya Dodoma Mhe. Davis Mwamfupe(Pili kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Jiji Godwin Kunambi(kwanza kushoto) wakiwa na wakandarasi wakisaini mikataba ya ujenzi wa miundombinu katika Jiji la Dodoma.
  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Dodoma Mhe. Davis Mwamfupe(kulia) akimkabidhi Mkandarasi Mkataba wa Ujenzi wa baadhi ya Miundombinu katika Jiji la Dodoma.
Huu ndio muonekano wa Soko la Kisasa litakalojengwa katika Jiji la Dodoma kupitia mradi wa Tscp.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images