Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109941 articles
Browse latest View live

Rock City Marathon yazinduliwa jijini Mwanza

$
0
0
Mwanza, 24 Juni, 2018: Msimu wa tisa wa mbio za Rock City Marathon umezinduliwa rasmi jijini Mwanza mwishoni mwa wiki hii huku wito ukitolewa kwa wadau wa utalii na michezo nchini hususani Kanda ya Ziwa kutumia mbio hizo kutangaza fursa na vivutio vya utalii vinavyopatikana katika kanda hiyo. 

Uzinduzi wa mbio hizo zinazoratibiwa na kampuni ya Capital Plus International kwa kushirikiana na Chama cha Riadha Mkoa wa Mwanza (MWAA) ulihusisha pia wawakilishi wa wakuu wa mikoa yote ya kanda ya Ziwa ikiwa ni mikoa ya Simiyu, Geita, Shinyanga, Mara na Kagera. 

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw Mongella katika hafla fupi ya uzinduzi huo iliyofanyika ukumbi wa Rock City Mall jijini humo, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Bi. Merry Tesha alisema ipo haja ya wadau wa utalii na michezo katika kanda hiyo kuhakikisha kwamba wanayatumia vizuri mashindano hayo katika kuhakikisha fursa na vivutio vya utalii vilivyopo kwenye ukanda huo vinatangazwa ipasavyo. 

“Ndio maana serikali tunafarijika sana tunapoona sekta binafsi inajiinua na kubuni mbinu bora kabisa hasa kupitia michezo ili kuiboresha zaidi sekta hii ya utalii hususani kwa kanda yetu ya Ziwa ambayo kwa sasa ipo kwenye mabadiliko makubwa,’’ Alisema. 

Akizungumzia maendeleo ya mchezo huo Bi Tesha alisema ipo haja kwa wadau kuhakikisha wanatumia vizuri mwamko wa mkubwa mashirika na taasisi mbalimbali hapa nchini ambazo zimeamua kuunga mkono mchezo huo katika kuinua vipaji vipya. 

“Niombe sana kila kiongozi mwenye dhamana ya kusimamia mchezo huu katika ngazi tofauti tofauti, idara mbali mbali na vyama mbali mbali, tulirudishe taifa kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.’’ Alisema. 
 Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Bi. Merry Tesha (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa msimu wa tisa wa mbio za Rock City Marathon 2018  kwenye hafla fupi iliyofanyika ukumbi wa Rock City Mall jijini Mwanza mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mwenyekiti wa mbio hizo, Zenno Ngowi, (Kushoto kwake), Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi (alievaa suti nyeusi) pamoja na Mwakilishi wa Chama cha Riadha Mkoa wa Mwanza (MWAA), Benjamini Nyagabona (alivaa kofia). 
 Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Bi. Merry Tesha akizungumza kwenye uzinduzi huo pamoja na mambo mengine alitoa wito kwa wadau wa utalii na michezo nchini hususani Kanda ya Ziwa kutumia mbio hizo kutangaza fursa na vivutio vya utalii vinavyopatikana katika kanda hiyo.
 Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi akizungumza kwenye uzinduzi huo.
 Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mbio za Rock City Marathon Bw Zenno Ngowi akizungumza kwenye hafla hiyo.
 Mgeni rasmi ambaye Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Bi. Merry Tesha akiwa kwenye picha ya pamoja na wawakilishi wa mikoa yote ya Kanda ya Ziwa waliohudhuria uzinduzi huo.


DK. KIGWANGALLA AELEZA MSIMAMO WA TANZANIA ULIVYOPENYA KWENYE ITIFAKI YA UTALII NA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI YA EAC

MWENYEKITI WA CCM TARIME ACHANGIA MILL 6 NA MIFUKO 100 YA SARUJI HARAMBEE YA UJENZI WA KANISA PAROKIA YA ROGORO MASANGA.

$
0
0
Na Frankius Cleophace Tarime.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilayani Tarime Mkoani Mara Marwa Daud Ngicho amechangia Kiasi Cha Shilingi Mill6 na Mifuko 100 ya Saruji kwa ajili ya Ujenzi wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Rogoro Masanga wilayani Tarime Mkoani Mara.

Ngicho amesema kuwa kama kiongozi ni wajibu wake wa kuchangia Ujuenzi wa Nyumba ya Bwana ili waumini wazidi kuombea Viongozi wanaotawala Nchi ya Tanzania na Ulimwengu akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pome Magufuli.

“Mimi kama kiongozi nimeambatana na Wafanyakazi wangu wa Mgodini kwa ajili ya kufanikisha zoezi zima naanza kuchangia Millioni Tano na Mifuko Miamoja hapa hapa naomba Waumini wote na Viongozi kuniunga Mkono ili kufanikisha Zoezi ili” alisema Ngicho.

Mwenyekiti ameongeza kuwa Jamii inayomwamini Mwenyezi Mungu haina budi kuondokana na kuamini Miungu badala ya Mungu huku akipiga vita Waganga wanapiga ramli Chonganishi na kusema kuwa wao kama Viongozi hawatawafumbia Macho kwani wanaweza Kuchocheanakusababisha Upotevu wa Amani.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilayani Tarime Mkoani Mara Marwa Daud Ngicho akionyesha Kiasi ch Shilingi Millioni Sita Waumini wa kanisa la Rogoro katika harambee ya Ujenzi wa kanisa hilo la Romani Katoliki .
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilayani Tarime Mkoani Mara Marwa Daud Ngicho akikabidhi Mwenyekiti wa Parokia ya Rogoro Masanga Sebastian Siyange Kiasi cha Shilingi Millioni Sita kwa ajili ya ujenzi wa kanisa hilo.
Waumini wa kanisa la Rogoro wakiwa katika Misa takatifu kabla ya harambee hiyo.
Kanisa Jipya la Parokia ya Rogoro Masanga Wilayani Tarime Mkoani Mara linalojengwa
Viongozi mbalimbali wakiwemo Waumini wa kanisa hilo wakikagua Ujenzi wa kanisa hilo.

HALOTELI YABORESHA MFUMO WA MAUZO NA USAJILI WA LAINI ZA SIMU

$
0
0
Kampuni ya mawasiliano ya simu ya Halotel, imetangaza kuboresha mfumo wake wa mauzo na usajili wa laini za simu na sasa watakaofanya hivyo ni mawakala waliothibitishwa.

Uamuzi huo ni mkakati wa kudhibiti usajili na mauzo ya laini za simu za Halotel ikiwa ni hatua ya kukabiliana na udukuzi au udanganyifu wowote unaoenda kinyume na sheria za mawasiliano nchini.

Akizungumza na waandishi wa Habari, Mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa Halotel, Mhina Semwenda amesema kampuni hiyo imepunguza idadi ya mauzo ya laini za simu kwa mawakala, lakini pia mawakala watauziwa laini nyingine mpya mara tu watakapokuwa wamemaliza mauzo ya laini za simu za awali pamoja na kuthibitisha kuwa laini walizopewa zimesajiliwa kwa wateja kwa kufuata taratibu zote za usajili zilizowekwa na mamlaka husika”.

“Tumeweka mfumo thabiti wa kudhibiti uuzaji wa laini za simu na usajili kutoka kwa mawakala wetu, hili pia limeambatana na uhakiki na usajili mpya wa mawakala wote wanauoza laini za simu za Halotel. Alisema Mhina na Kuongeza,

“Tumewekeza kwenye teknolojia ya kisasa zaidi itakayogundua na kuzuia udukuzi wa aina yoyote ya mifumo ya mawasiliano, Tunafanya haya yote ili kuongeza ufanisi pamoja na kuwadhibiti watu wenye nia ovu ya kutumia miundombinu ya mawasiliano kuvunja sheria” alisema Semwenda.

Alisisitiza kuwa mara zote, kampuni hiyo inafuata kanuni na sheria zilizopo ndiyo maana imekuwa ikiwekeza fedha nyingi ili kufikisha huduma bora kwa Watanzania hivyo haipo tayari kushuhudia watu wenye niaovu wakiharibu malengo mema yaliyopo.

“Uwekezaji mkubwa uliofanywa kwa miaka miwili iliyopita nimatokeo ya ushirikiano mwema baina ta Tanzania na Vietnam. Ni uhusiano huo uliochangia kukuza biashara na uwekezaji kati ya nchi hizi mbili hivyo Halotel itaendelea kuzingatia sheria na kanuni za nchi pamoja na kuendelea kuboresha na kutoa huduma zenye gharama nafuu kwa Watanzania,” alisema Semwenda.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mhina Semwenda Halotel akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu uboreshwaji wa mfumo wa uuzaji na usajili wa laini za simu. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Halotel Stella Pius. 

MAELFU WAHUDHURIA MASHINDANO YA MBIO ZA MBUZI ZA ROTARY JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Fursa ya kwanza ya uandaaji wa mashindano maarufu ya mbio za mbuzi imekua ya mafanikio kwa Klabu ya Rotary ya Oysterbay. Tukio hilo lenye burudani ya aina yake lilikwenda kwa Motto wa ‘Wakanda Goat are You’, na kuvuatia watu zaidi ya 4,500 waliokusanyika katika eneo la The Green, Oysterbay kwa ajili ya kushuhudia mashindano hayo. 

Matukio muhimu yaliyofuata baada ya mbio hizo ni mchezo wa bahati nasibu ambao uliwezeshwa na wafadhili wa hapa nyumbani pamoja na gwaride la kuonyesha mavazi, ambapo watu mbalimbali walipata fursa ya kuonyesha mavazi yao aina ya Wakanda kwa kurejelea mafanikio ambayo muvi ya Marvel ya ‘Black Panther’ imeyapata kwa mwaka huu.

Ni mwaka wa kumi na nane mfululizo wa mashindano hayo lakini kwa mwaka wa kwanza chini ya Rotary Goat Races, tukio hili maarufu la kifamilia lilivutia maelfu ya watu siku ya tarehe 23 Juni. Tukio hilo likifanyika katika eneo la ‘The Green’ chini ya motto wa ‘Wakanda Goat are You”, wahudhuriaji walifurahia aina saba za mbio, vyakula vya aina mbalimbali vya hapa nyumbani, zawadi kubwa mbalimbali za bahati nasibu, michezo ya kuweka dau na gwaride la ushindani la mavazi ya Wakanda.

Mashindano hayo yalianza kwa mbuzi kusimama kwenye mstari wa mwanzo wa mashindano, huku watazamaji wakivuta pumzi kuona mbuzi wanavyopigania ushindi wa kuwa namba moja.

KAtika raundi ya kwanza Mbuzi aliyeibuka kidedea ni namba 8 ambapo zawadi yake ilidhaminiwa na Kampuni ya vinywaji ya CocaCola, Raundi ya pili mbuzi namba 7 aliibuka mshindi na zawadi yake kudhaminiwa na East Africa TV/Radio huku raundi ya tatu mbuzi namba tisa akikiibuka mshindi na zawadi yake kudhaminiwa na Kampuni ya Aggreko. 
Washiriki wa mashindano ya mbio za mbuzi wakiwa wamewabeba mbuzi wao tayari kushiriki mbio hizo wakati wa hafla ya mashindano hayo maarafu ambayo yaliyofanyika katika eneo la The Green, Oysterbay jijini Dar es Salaam wikiendi hii. Kwa mwaka huu mashindano hayo ya kufana yaliandaliwa na Klabu ya Rotary Dar es salaam, Oysterbay ambapo yalivutia zaidi ya watu 4,500 huku yakiwa chini ya Motto wa ‘Wakanda Goat Are You’? yakirejerelea mafanikio ambayo muvi ya Marvel ya ‘Black Panther’ imeyapata kwa mwaka huu.
Washiriki wa mashindano ya mbio za mbuzi wakiwakimbiza mbuzi wao wakati wa hafla ya mashindano hayo maarafu ambayo yaliyofanyika katika eneo la The Green, Oysterbay jijini Dar es Salaam wikiendi hii. Kwa mwaka huu mashindano hayo ya kufana yaliandaliwa na Klabu ya Rotary Dar es salaam, Oysterbay ambapo yalivutia zaidi ya watu 4,500 huku yakiwa chini ya Motto wa ‘Wakanda Goat Are You’? yakirejerelea mafanikio ambayo muvi ya Marvel ya ‘Black Panther’ imeyapata kwa mwaka huu.
Anne Saels, Rais wa Klabu ya Rotary Dar es salaam, Oysterbay akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya mashindano ya mbio za mbuzi yaliyofanyika katika eneo la The Green, Oysterbay jijini Dar es Salaam wikiendi hii. Kwa mwaka huu mashindano hayo ya kufana yaliandaliwa na Klabu ya Rotary Dar es salaam, Oysterbay ambapo yalivutia zaidi ya watu 4,500 huku yakiwa chini ya Motto wa ‘Wakanda Goat Are You’? yakirejerelea mafanikio ambayo muvi ya Marvel ya ‘Black Panther’ imeyapata kwa mwaka huu.
Anne Saels, Rais wa Klabu ya Rotary Dar es salaam, Oysterbay akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya mashindano ya mbio za mbuzi yaliyofanyika katika eneo la The Green, Oysterbay jijini Dar es Salaam wikiendi hii. Kwa mwaka huu mashindano hayo ya kufana yaliandaliwa na Klabu ya Rotary Dar es salaam, Oysterbay ambapo yalivutia zaidi ya watu 4,500 huku yakiwa chini ya Motto wa ‘Wakanda Goat Are You’? yakirejerelea mafanikio ambayo muvi ya Marvel ya ‘Black Panther’ imeyapata kwa mwaka huu. 
Anne Saels, Rais wa Klabu ya Rotary Dar es salaam, Oysterbay akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya mashindano ya mbio za mbuzi yaliyofanyika katika eneo la The Green, Oysterbay jijini Dar es Salaam wikiendi hii. Kwa mwaka huu mashindano hayo ya kufana yaliandaliwa na Klabu ya Rotary Dar es salaam, Oysterbay ambapo yalivutia zaidi ya watu 4,500 huku yakiwa chini ya Motto wa ‘Wakanda Goat Are You’? yakirejerelea mafanikio ambayo muvi ya Marvel ya ‘Black Panther’ imeyapata kwa mwaka huu.

WAZIRI WA AFYA ASEMA HAKUNA EBOLA NCHINI ILA KUNA HATARI YA KUUPATA

$
0
0
*Ataja hatua ambazo wanazochukua kukabiliana nao kote nchini 
*Akiri kuripotiwa homa ya Chikungunya,  Dengue katika Jiji la Dar 

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema hakuna ugonjwa wa Ebola nchini ila kuna hatari ya kuupata.

Hivyo amewahakikishia Watanzania kutokuwa na hofu ha kueleza Serikali imeshachukua hatua mbalimbali za kukabiliana na ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kuweka mashine za kupima ugonjwa huo katika mipaka yote nchini na kuweka vituo vya matibabu kote kila mkoa.

Waziri Mwalim ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumzia homa ya Chikungunya na Dengue ambapo amekiri kuwepo kwa wananchi waliougua magonjwa hayo.Kuhusu Ebola amesema hawajapokea wala kupata  taarifa za mtu yoyote kuugua ugonjwa huo nchini.

"Hatuna mgonjwa wa Ebola ila tupo katika nchi sita ambazo zipo hatarini kupata ugonjwa huo kutokana na kupakana na nchi ya Congo ambayo  iripotiwa watu 43 kuugua Ebola."Pia kuna muingiliano mkubwa wa watu nchini kwetu.Hivyo kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) tupo hatarini kuupata,"amefafanua.

Waziri Mwalim amesema Wizara ya Afya na Serikali kwa ujumla tayari wamejipanga kukabiliana na Ebola kwa kuchukua hatua mbalimbali ikiwamo kuunda timu maalum ya kufuatilia.Pia wametenga maeneo ya kutoa huduma za afya kila mkoa iwapo kutabainika kuna mgonjwa wa Ebola amebainika iwe rahisi kupatiwa matibabu.

WANANCHI KAKONKO WASHAURI KUSHIRIKIANA NA VIONGOZI WAO KUJENGA NYUMBA ZA ASKARI

$
0
0
Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

WANANCHI wa Vijiji vya Kinyinya na Nyagwijima katika Kata ya Mgunzu wilayani Kakonko mkoani Kigoma, wametakiwa kushirikiana na viongozi wao kujenga nyumba za askari kwa lengo la kupunguza vitendo vya utekaji katika eneo la Kosovo wilayani humo.

Akizungumza jana kwenye mkutano wa kusikiliza kero za wananchi na kuhamasisha maendeleo kwa wananchi Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala amesema katika Wilaya ya Kakonko masuala ya utekaji yamepungua.

Ameongeza yamebaki katika maeneo machache ambayo hayafikiki kiurahisi huku akiwahimiza wananchi kutoa ushirikiano kujenga nyumba za askari ili wakae maeneo hayo na kukomesha vitendo hivyo."Wananchi wanatakiwa kujitoa kwa michango na kujitoa wenyewe kujenga, kwakuwa wanatekwa na kuporwa mali zao ni wananchi wenyewe.

"Serikali inatoa msaada mkubwa wa Kuleta maendeleo kwa wananchi, hivyo wanatakiwa kujitoa katika vijiji vyao kutokomeza vitendo hivyo.Niwaombe viongozi wa Kijiji muendelee kuhimiza suala hili la kujenga nyumba,"amesisitiza.Aidha amewataka wananchi kuwapuuza wale wote wanao wadanganya na kuwashawishi wasijitolee kuleta maendeleo.Kwa upande wa Diwani wa Kata ya Mgunzu Andrea Mashama amesema mkapa sasa wanaendelea kuhimiza wananchi kujitolea.

"Tumeitisha mkutano na tukakubaliana kila mwananchi kuchanga Sh.1000, hivyo wananchi wanaendelea na michango kufanikisha ujenzi wa nyumba ya Mganga na Kituo cha Afya na kufanya shughuli zingine za maendeleo kwa wananchi wote wa Kinyinya na Nyagwijima,"amesema.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi akiwamo Joachim Jolamu amesema wananchi wanaumia kwani wamekuwa waikiibiwa mazao pamoja na fedha."Tukuahidi mkuu tutahakikisha tunafanikisha ujenzi ili tuwe salama,"amesisitiza.
 Mkuu wa Wilaya hiyo,Kanali Hosea Ndagala akizungumza kwenye mkutano  mbele ya Wananchi wakati wa kusikiliza kero za wananchi na kuhamasisha maendeleo kwa wananchi .
 WANANCHI wa Vijiji vya Kinyinya na Nyagwijima katika Kata ya Mgunzu wilayani Kakonko mkoani Kigoma, wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya hiyo,Kanali Hosea Ndagala kwenye mkutano wa kusikiliza kero za wananchi na kuhamasisha maendeleo kwa wananchi .

MKURUGENZI MTENDAJI WA TASAF AWAFUNDA MAAFISA UFUATILIAJI-TMOs.

$
0
0
Na Estom Sanga-TASAF.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF-bwana Ladislaus Mwamanga amewataka Maafisa Ufuatiliaji wa Mfuko huo –TMOs- kutekeleza majukumu yao kwa uaminifu na kuzingatia maslahi ya taifa .

Akifungua mafunzo ya Maafisa Ufuatiliaji kutoka mikoa ya Arusha, ,Kilimanjaro,Singida,Tanga , Mbeya ,Iringa,Katavi,Njombe,Songwe ,Ruvuma na Rukwa katika ofisi za TASAF jijini Dar es salaam ,Mwamanga amesema utendaji kazi wa Watumishi hao unapaswa kuendana na matakwa ya Serikali ya kuhimiza uwajibikaji na kufanya kazi kwa kujituma kwa maslahi ya Wananchi.

Aidha Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TASAF amesema maeneo ya Utekelezaji wa Shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini nchini kote yameonyesha mafanikio ya kujivunia na hivyo kinachotakiwa kwa sasa ni kuandaa mazingira wezeshi na kuwapatia mbinu sahihi Walengwa za kuendesha shughuli za uzalishaji mali ili hatimaye waweze kuondokana na umaskini. 

Bwana Mwamanga pia amewaagiza Maafisa Ufuatiliaji hao kujenga mahusiano mema na Idara nyingine zilizoko kwenye maeneo yao ya kazi ili kuweka mazingira rafiki kwao kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi unaokusudiwa.Ameonya kuwa pale ambapo utendaji kazi wa Maafisa hao utabainika kutoridhisha , Uongozi hautasita kuchukuwa hatua zinazopaswa kulingana na taratibu za utumishi wa Umma , kwani amesema Wananchi hususani Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wanahitaji huduma bora na si vinginevyo.

Mafunzo hayo yanayotolewa kwa Kanda ,yanaendeshwa na Wataalamu kutoka Chuo cha Uhasibu Arusha yanalenga kuwapatia Maafisa Ufuatiliaji hao stadi sahihi za uongozi na kuboresha usimamizi mzuri wa shughuli za Taasisi, mbinu bora ya usimamizi wa shughuli za Mpango na kutatua changamoto zinazojitokeza kwa wakati na ufanisi .

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF unaendesha Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaohudumia takribani Kaya Milioni Moja na Laki Moja nchini kote kwa lengo la kuboresha maisha ya kaya husika huku mkazo maalum ukiwekwa katika sekta za Elimu, Afya,Lishe na Uzalishaji Mali ili kuongeza kipato cha Walenga na jamii inayowazunguka.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Ladislaus Mwamanga (aliyesimama) akitoa hotuba ya ufunguzi kwenye mafunzo ya Maafisa Ufuatiliaji wa TASAF yanayofanyika kwenye ukumbi wa taasisi hiyo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Maafisa Ufuatiliaji wa TASAF –TMOs wakisikiliza hotuba ya ufunguzi wa Mafunzo ikitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Ladislaus Mwamanga(hayupo pichani)
Baadhi ya Maafisa Ufuatiliaji wa TASAF –TMOs wakisikiliza hotuba ya ufunguzi wa Mafunzo ikitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Ladislaus Mwamanga (hayupo pichani)
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Ladislaus Mwamanga (katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na wakurugenzi,meneja na Maafisa Ufuatiliaji wa TASAF baada ya kufungua mafunzo yao kwenye Ofisi za taasisi hiyo jijini Dar es salaam leo.


Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi kufuatia vifo vya watu 14 ajalini Mkuranga Pwani

$
0
0


 Muonekano wa basi dogo mara baada ya kupata ajali hiyo na kupelekea vifo vya watu 14
 Pichani ni sehemu ya tukilo la ajali iliyosaabisha vifo vya watu 14 waliopoteza maisha baada ya basi dogo walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori la kubebea mchanga katika eneo la Dundani Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani.Ajali hiyo imetokea leo Juni 25i, 2018 Alfajiri wakati basi dogo lililowabeba wanafamilia, ndugu na jamaa waliokuwa wakielekea Msata kuhudhuria sherehe za kumaliza mafunzo ya kijeshi kwa mtoto wao, kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa linatoka Dar es Salaam kwenda Dundani kuchukua mchanga.

KAMPUNI YA KANTON INVESTMENT, HALMASHAURI YA HANDENI WASAINI MAKUBALIANO KUENDELEZA ZAO LA MUHOGO

$
0
0
Na Grace Semfuko, Maelezo

HALMASHAURI ya Wilaya ya Handeni mkoani Tanga imewekeana saini na Kampuni ya Kanton Investment kutoka Jamhuri ya Watu wa China kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata zao la mihogo, ikiwa ni juhudi za Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kuvutia wawekezaji nchini.

Ujenzi wa kiwanda hicho utakaogharimu Dola milioni 10 unatarajia kuchakata tani 200 za mihogo pamoja na kusafirisha tani 400,000 za wanga kutoka katika tani milioni 1.6 za mihogo mibichi itayosafirishwa nchini China.

Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki Wilayani Handeni na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kanton Investment, John Rwehumbiza wakati wa hafla ya utiaji saini wa maktaba wa makubaliano hayo iliyohudhuriwa na viongozi wa Serikali.

Rwehumbiza amesema kampuni hiyo imeanza majaribio ya kununua na kusafirisha nje ya nchi zao la Muhogo na kuonesha kupendwa raia wa China, na hivyo kuahidi kufanya uwekezaji kwa kujenga kiwanda cha wanga na kununua mihogo ya wakulima na kuisafirisha nchini humo.

Aidha ameongeza kampuni yake pia imepanga kutoa elimu kwa wakulima wa zao la muhogo kuhusu mbinu bora za uzalishaji wa zao hilo ambalo litawawezesha kutoa faida kubwa na hasa ukizingatia walaji wengi wa zao hilo wanatoka nje ya nchi ikiwepo China na Japan.

Wakati huohuo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, William Mafukwe amesema Ofisi yake itahakikisha inaweka mazingira mazuri kwa wawekezaji hao ili wafanye kazi katika mazingira wezeshi kama ilivyokusudiwa ili kuweza kuwanufaisha wakulima wa Wilaya hiyo.
 Mojawapo ya shamba la Muhogo uliostawi katika kijiji cha Kwamsisi Wilayani Handeni kwa ajili ya malighafi itakayotumika katika mradi wa kiwanda cha kuchakata muhogo

 Bw. Sultan Mbuji mkulima wa zao la muhogo akitoka shambani kwake kuvuna zao la muhogo huko Wilayani Handeni 


Katikati ni  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. William Mafukwe akikabidhiana mkataba na Mkurugenzi wa  Kampuni ya Kanton Investment Bw. John Rwehumbiza mara baada ya kusainiwa huko Handeni Tanga.

WATAALAM WA BIMA NCHINI WAHIMIZWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI, KUBUNI BIDHAA MPYA

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 

WADAU na wataalam wa masuala ya Bima nchini wameshauriwa kufanya kazi kwa weledi,kujiheshimu na kubuni bidhaa mpya na za bei nafuu ili kuwafikia wananchi wote.

Ushauri huo umetolewa jana na Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Bima Nchini (TIRA)Dk. Baghayo Saqware wakati akiwahutubia wanafunzi wanaosoma kozi ya Bima katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) mara baada ya matembezi ya utambuzi wa Bima yaliyoanzia katika viunga vya IFM hadi Karimjee.

"Watoa huduma za bima nchini lazima tuwe na wajihi au taswira njema kwa jamii inayo tuzunguka ,kwani jamii hiyo ndiyo walaji wa bidhaa za bima."Hivyo basi hatunabudi kujiheshimu na hatupaswi kuonekana matapeli,wahuni. Tuoneshe heshima mbele za wananchi wote ili wawe na uthuubutu wa kuwa na bima,” amesema Dk Saqware.

Amewataka wataalamu wa bima kuwa wabunifu kwa kubuni bidhaa mbalimbali na kuongeza ufahamu wa bima kwa wananchi kwani bima ni kinga na bima ni muhimu kwa kila mwananchi kuwa nayo kwa ajili mali na maisha.Mkuu wa Idara ya wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Dk. Mussa Juma amesema IFM kila mwaka hufanya matembezi hayo kwa lengo la kujenga uwelewa kwa wananchi wajuwe umuhimu wa bima katika kuweka kinga ya mali na maisha.

Amesema matembezi yao ni kuwaelimisha wananchi ikiwa kwa kutoa elimu kwa njia mbalimbali ikiwemo kutoa vipeperushi kwa mtu mmoja mmoja pamoja kueleza aina za bima zinazopatikana kwa bei nafuu ili wananchi wa kipato cha chini waweze kumudu.Aidha Dk. Juma amesema kuna changamoto ya wataalamu wa bima na kuongeza pamoja na changamoto za uchache huo bado wanajitahidi kuwafikia wananchi kwa kadri wawezavyo.

Hata hivyo Sekta hiyo inakumbwa na changamoto ya uwelewa mdogo kwani watu wengi hawajui umuhimu wa bima, hivyo lazima jitihada za msingi zifanyike.
Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Bima Nchini (TIRA) Dk. Baghayo Saqware akizungumza wanafunzi wa Chuo cha IFM wanaosoma masuala ya bima baada ya kufanya matembezi ya kuhamasisha wananchi kujua umuhimu wa bima.
Mkuu wa Idara ya wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Dk Mussa Juma akizungumza kuhusiana na Chuo kilivyojipanga katika utoaji elimu ya bima kwa vijana na wanaohitaji kutokana na kuwa na soko kubwa la ajira.
Mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) anaesomea Bima ,Mkagambage Kyaruzi akizungumza na waandishi kitu ambacho kimemsukuma kusomea bima . 
Matembezi ya wanafunzi wa chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Mawakala wa Bima

KATIBU MKUU WA CCM DKT BASHIRU ALLY AONGOZA KIKAO CHA CCM NA UJUMBE WA CPC LEO JIJINI DODOMA

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally akiongoza kikao cha Wajumbe wa chama cha kikomonisti Cha china (CPC) kwa ajili ya maandalizi ya Uwekaji wa jiwe la msingi chuo cha chama Kibaha pamoja na Mkutano wa CPC na Africa leo katika ukumbi wa Kamati Kuu ya CCM, ndani ya Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete nje kidogo ya Mji wa Dodoma. 
Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally akipeana Mkono na Naibu Mkurugenzi wa Mambo ya Afrika katika chama cha Kikomonisti China Wang Heming mara baada ya kikao cha maandalizi ya Uwekaji wa jiwe la msingi chuo cha chama Kibaha pamoja na Mkutano wa CPC na Africa leo katika ukumbi wa Kamati Kuu ya CCM, ndani ya Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete nje kidogo ya Mji wa Dodoma.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati kuu ya Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi akizungumza,leo katika ukumbi wa Kamati Kuu ya CCM, ndani ya Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete nje kidogo ya Mji wa Dodoma.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati kuu ya Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi akipokea zawadi toka kwa mjumbe wa CPC.
Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally (kulia) akikabidhiwa zawadi ya Picha ya Utamaduni toka kwa Naibu Mkurugenzi wa Mambo ya Afrika katika chama cha Kikomonisti China Wang Heming leo katika ukumbi wa Kamati Kuu ya CCM, ndani ya Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete nje kidogo ya Mji wa Dodoma.(Picha na Fahadi Siraji wa UVCCM)
Picha Mbali mbali za pamoja kati ya Viongozi wa CCM pamoja na Ujumbe wa chama cha Kikomonisti nchini china leo katika ukumbi wa Kamati Kuu ya CCM, ndani ya Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete nje kidogo ya Mji wa Dodoma.

NBS kuendelea kuzalisha takwimu zenye ubora kusaidia Serikali katika Maendeleo Endelevu

WAKULIMA 11,177 WA UFUTA WANUFAIKA NA MRADI WA FARM AFRIKA-DKT TIZEBA

$
0
0
Na Mathias Canal-WK, Dar es salaam

Utekelezaji wa mradi wa Farm Afrika kwa kipindi cha miaka mitatu umeweza kuwafikia wakulima takribani 11,177 ambapo kati yao wanawake ni 5,474 na wanaume ni 5,703 huku kati ya wakulima hao vijana wakiwa ni takribani 5,821 yaani zaidi ya nusu (52%) kutoka wilaya ya Bahi, Manyoni na Babati.

Hayo yamebainishwa juzi 22 Juni 2018 na Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa zao la ufuta pamoja na mjadala wa mapendekezo juu ya uboreshaji wa masoko ya ufuta, kwenye hafla iliyofanyika Golden Tulip Hoteli Jijini Dar es salaam.

Dkt Tizeba alipongeza jitihada hizo kwani zinachangia kukuza kipato cha wakulima na uchumi wa nchi kwa kuingiza fedha za kigeni huku akiwataka watumishi mbalimbali kuwaunganisha wakulima wadogo wadogo katika masoko rasmi na kujenga uelewa wao juu ya vichocheo na fursa za ushiriki endelevu.

Waziri huyo wa kilimo alilishukuru shirika la Farm Afrika kwa kuona umuhimu na fursa zilizopo katika kilimo cha ufuta katika mikoa ya Dodoma, Singida na Manyara hivyo kuwanufaisha wakulima kupitia mbinu bora za kilimo cha kisasa katika zao hilo.
Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa zao la ufuta pamoja na mjadala wa mapendekezo juu ya uboreshaji wa masoko ya ufuta, kwenye hafla iliyofanyika Golden Tulip Hoteli Jijini Dar es salaam, Juzi 22 Juni 2018.


Mkurugenzi Mtendaji wa Farm Afrika Ndg Ryan Whalen akizungumza wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa zao la ufuta pamoja na mjadala wa mapendekezo juu ya uboreshaji wa masoko ya ufuta, kwenye hafla iliyofanyika Golden Tulip Hoteli Jijini Dar es salaam, Juzi 22 Juni 2018. 
Baadhi ya wadu waliohudhuria mkutano wa wadau wa zao la ufuta pamoja na mjadala wa mapendekezo juu ya uboreshaji wa masoko ya ufuta, wakimsikiliza kwa makini Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba kwenye hafla iliyofanyika Golden Tulip Hoteli Jijini Dar es salaam, Juzi 22 Juni 2018.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

KITUO CHA UWEKEZAJI TANZANIA (TIC) CHAENDELEA KUTANUA WIGO KWA WAWEKEZAJI


FRIEDKIN CONSERVATION FUND WATOA MILIONI 253 KUDHIBITI UJANGILI WA FARU SERENGETI

$
0
0
Ulinzi wa Faru katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti na maeneo ya jirani, unatarajiwa kuimarika zaidi baada ya kuanza mradi maalum wa Faru kufungwa vifaa vya technolojia za kisasa na hivyo kuwalinda na matishio ya ujangili ama kupotea.

Faru ni miongoni mwa wanyama ambao wapo hatarini, kutoweka duniani, kutokana na kuwindwa na majangili, ambao wamekuwa wakiuza pembe zao na hivyo serikali imekuwa na mikakati kadhaa ya kuimarisha ulinzi wao.

Akizungumza na wanahabari, Mwakilishi mkazi wa shirika la uhifadhi la kimataifa la Frankfurt zoological Society moja ya mashirika yanayoratibu mradi huo, Gerald Bigulube alisema mradi huo wa aina yake barani Afrika, unatarajiwa kuimalisha ulinzi na ufatiliaji wa faru katika eneo la Seregeti.

Alisema mradi huo unatarajiwa kutumia zaidi ya sh 253 milioni, zilizotolewa na shirika la uhifadhi la Friedkin Conservation Fund(FCF) na unaratibiwa pia na Shirika la hifadhi za Taifa(TANAPA) na Taasisi ya utafiti wa Wanyamapori(TAWIRI). Bigulube alisema, tayari utekelezaji wa mradi huo, umeanza, ambapo mwaka jana faru 21 walifungwa vifaa maalum digital VHF na mwaka huu wengine watafungwa vifaa vya kisasa zaidi kutumia mfumo wa LoRa(LoRa System).

"lengo letu kama wahifadhi ni kuhakikisha Faru waliopo nchini wanaongezeka zaidi sambamba na wanyama wengine ambao maisha yao yamekuwa hatarini wakiwepo Tembo ambao nao tayari kuna miradi ya kuwafunga vifaa vya kisasa ili kuwafatilia "alisema

Pacha walioungana Muhimbili kupelekwa Saudi Arabia kwa matibabu zaidi

$
0
0
Watoto pacha Maryness Benatus Bernado na Anisia Benatus Bernado waliozaliwa wakiwa wameungana ambao kwa sasa wamelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) tangu mwezi Februari mwaka huu, wanatarajiwa kupelekwa nchini Saudia Arabia ndani ya wiki mbili kuanzia sasa kwa ajili ya matibabu zaidi ikiwemo kuangalia uwezekano wa kuwatenganisha.

Hayo yameelezwa leo na Kaimu Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania, Bandar Abdullah Al-Hazzan alipotembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili kuangalia watoto hao. Watoto hawa wameungana kuanzia sehemu ya tumboni hadi chini.“Tumekuwa na uzoefu mkubwa sana wa kuwatenganisha watoto pacha waliozaliwa wakiwa wameungana kuanzia miaka ya 1990 ambapo hadi hivi sasa watoto zaidi 35 kutoka nchi mbalimbali duniani waliozaliwa wakiwa wameungana tulifanikiwa kuwatenganisha,” alisema Kaimu Balozi Al-Hazzan

Amesema kwamba kutokana na uzoefu mkubwa walionao, nchi yake kupitia Mfalme wa nchi hiyo ameagiza watoto hao wapelekwe Saudi Arabia kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya ubingwa wa juu.Mbali na hayo Serikali ya Saudi Arabia imesema itagharamia usafiri, malazi pamoja na matibabu hivyo wamemuhakikishia mama wa pacha hao kwamba matibabu yatakwenda vizuri na watarejea nchini wakiwa salama.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru amemshukuru Mfalme wa Saudi Arabia na Serikali yake kwa ujumla kwa ushirikiano mkubwa wanaoendelea kuutoa kwa Serikali ya Tanzania hususani katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.Prof. Museru ameiomba Serikali ya Saudi Arabia kuendelea kushirikiana na Tanzania katika sekta ya Afya katika kuangalia maeneo yenye upungufu wa wataalamu pamoja na maeneo mengine zikiwamo huduma za upasuaji.

Kwa upande wake Mama wa watoto hao, Bi. Jonesia Jovitus amemshukuru Mfalme wa Saudia Arabia kupitia Ubalozi wake hapa nchini Tanzania kwa msaada alioupata kwani anaamini kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu watoto wake watapata huduma ya matibabu kulingana na uzoefu ulipo nchini humo. Watoto hao kwa pamoja wana uzito wa kilo 7 na gramu 40, walizaliwa Wilayani Misenyi, Mkoani Kagera tarehe 29 Januari, 2018.
 Kaimu Balozi wa Saudia Arabia nchini Tanzania, Bandar Abdullah Al-Hazzan akiwa na watoto pacha waliungana, Maryness Benatus Bernado na Anisia Benatus Bernado ambao wamebebwa na mama yao, Jonesia Jovitus. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru.Watoto hao wanatarajiwa kupelekwa nchini Saudia Arabia ndani ya wiki mbili kuanzia sasa kwa ajili ya matibabu zaidi ikiwemo kuangalia uwezekano wa kuwatenganisha.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Museru akimsikiliza balozi huyo kabla ya kuwatembelea wodini watoto pacha leo tarehe 25 Juni, 2018. Kushoto ni Mkurugenzi wa ubalozi huo, Fahad Ali Al Qahtani.
 Kaimu Balozi wa Saudia Arabia nchini Tanzania, Bandar Abdullah Al-Hazzan na Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Museru wakielekea wodini kuwaona watoto pacha walioungana leo tarehe 25 Juni, 2018.
Kaimu Balozi wa Saudia Arabia nchini Tanzania, Bandar Abdullah Al-Hazzan na Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Museru wakiwa katika picha ya pamoja leo tarehe 25 Juni, 2018.

BENKI YA POSTA YATOA MSAADA

$
0
0

 Meneja  mawasiliano wa Benki ya TPB chichi Banda, kushoto akimkabidhi Meneja wa Kituo cha soba House Twalibu Hassani kulia kituo hicho kilichopo Mjimwema kata ya Ungidoni Kigamboni katika maadhimisho ya kupinga Vita  matumizi ya Dawa za Kulevya ambaye imefanyika Kitaifa jana, wakati wa kukabidhi vyakula mbalimbali pamoja na mafuta ya kula yenye thamani isiopungua shilingi milioni Moja,

MTOTO PEKEE WA KIUME WA D'BANJ AFARIKI DUNIA NCHINI NIGERIA

$
0
0
*Ni baada ya kutumbukia kwenye bwawa la kuogelea la nyumbani 

Na Zainab Nyamka, Globu ya jamii

MWANAMUZIKI wa nchini Nigeria Dapo Oyebanjo ‘D’banj’ amepoteza mtoto wake wa kiume wa pekee baada ya kutumbukia kwenye bwawa la kuogelea na kufariki dunia jana nchini Nigeria.

D’banj akiwa Los Angels kwenye tuzo za muziki za BET, msanii huyo aliweza kupewa taarifa za kifo za mtoto wake anayejulikana kwa jina la  Daniel Oyebanjo III  kuwa amezama na kufa maji.

Imeripotiwa kuwa mtoto huyo, Daniel Oyebanjo III, alizama kwenye bwawa la kuogelea (swimming pool) lililopo nyumbani kwa mwanamuziki huyo huko Ikoyi, jijini Lagos.

Hivyo D’banj aliripoti kifo cha mwanaye huyo wa mwaka mmoja kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram kwa kuweka picha iliyotawaliwa na rangi nyeusi ikiambatana na ujumbe uliosomeka “Nyakati ngumu, lakini Mungu wangu ni mwaminifu, wakati wote na daima.”

Imethibitishwa kuwa mke wa mwanamuziki huyo, Lineo Didi alikuwa nyumbani wakati tukio hilo likitokea na haijajulikana kama kuna mtu aliyekuwa kwenye bwawa hilo huku.

Mapema wiki hii D’ banj katika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram ikiwa ni siku ya kina baba ‘Father’s Day’ akiwa anamvalisha mwanae pampers.

TAMASHA LA ASAS MTOTO DAY OUT KUFANYIKA JUNI 30 DAR KWA KIINGILIO CHA 5000/-

$
0
0
*Ni tamasha maalum kwa watoto, lashesheni michezo ya kila aina kwa watoto

TAMASHA la Mtoto Day Out ambalo limebeba jina la Asas Mtoto Day Out linatarajia kufanyika Juni 30 mwaka huu katika Viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam kwa kiingilio cha Sh.5000 tu.

Imefahamika kuwa mtoto atacheza michezo ya kila aina huku mzazi akiingia bure huku ikifafanuliwa Mtoto Day Out ni tamasha kwa ajili ya watoto kukutana kwa wingi kucheza na kufurahi pamoja.

Akizungumzia leo jijini Dar es Salaam Mratibu wa tamasha hilo Dina Marious amesema tamasha hilo litawapa nafasi watoto kucheza michezo ya kila aina na kuonesha vipaji, huku wakijishinidia zawadi mbalimbali. 

"Moja ya haki za watoto ni kucheza na katika kucheza hujifunza mambo mbalimbali.Michezo kwa watoto isiwe kero kwa mzazi bali nafasi ya mtoto kujifunza na kuchangamsha akili yake."Katika michezo kuna michezo ya kushindana ambayo ni jambo jema kwa watoto kupanda ndani yao ari ya ushindani hata katika maisha ya baadae."Wazazi kawaida wana Outing zao za kikubwa na watoto huishia mara moja moja kupelekwa kwenye michezo,"amesema,

Ameongeza kupitia tamasha la Mtoto Day Out wanataka liwe tamasha la watoto kama ambavyo watu wazima wana matamasha yao na kufafanua "unapotoka na mtoto wako kuja Mtoto Day Out unamtoa yeye Out si wewe".Amesema kuwa hiyo ni mara ya tatu kwa tamasha hilo kufanyika na kufafanua tamasha la safari hii litafanyika Viwanja vya Posta Kijitonyama Sayansi jijini.Muda wa kuanza kwa tamasha hilo ni kuanzia saa nne asubuh mpaka saa 12 jioni na kutakuwa na michezo ya kila aina kwa watoto.

Baadhi ya michezo hiyo ni jumping castles, face painting, train, magari ya kuendesha,climber,mabembea,swimming pools,water slides,football arena na sarakasi.Marious amesema pia kutakuwa na kona ya michezo ya watoto wadogo wa mwaka hadi miaka 3, kona ya watoto kusoma vitabu na kuchora.Pia atakuwepo Mchekeshaji Mpoki ambaye atasasherehesha watoto huku msanii Msami akiwachezesha watoto. Katika tamasha hilo vyakula uwanjani vitakuwepo na wazazi watawanunulia watoto kwa bei nafuu kabisa.

"Tamasha hili linafanyika kwa udhamini wa Asas_dairies, Finca microfinance bank,majibora, ara juice, bagtriks, swahilifastfood,saloon ya watoto ya kiddieskingdomtz,dinamarios coconut baby oil, efmtanzania na tvetanzania ."Tunapenda kuwakaribisha wazazi na watoto kutakuwa na timu kubwa ya kuangalia watoto kwa kushirikiana na wazazi.
Mratibu wa tamasha la ASAS Mtoto Day Out Dina Marios akizungumza mapema leo mbele ya Waandishi wa habari kuhusu tamasha hilo,linalotarajia kufanyika Juni 30 mwaka huu katika Viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam,ambapo kiingilio kimetajwa kuwa ni Sh.5000 tu,Pichani kulia ni Mmoja w Waratiu wa tamasha hilo Glory Shayo na kushoto ni Meneja Masoko wa kampuni ya ASAS Jimmy Kiwelu.
Mkutano huo ukiendelea na Waandishi mapema leo jijini Dar 
Balozi wa ASAS Mujuni Sylivery maarufu kwa jina la Mpoki akiwaonesha Waandishi wa Habari baadi ya bidhaa zinazotengenezwa na kampuni hiyo,huku akiwashauri wazazi kuhakikisha wanawapa furaha watoto wao kwa kuwapeleka kwenye tamasha hilo ambapo amewahakikishia amejiandaa vema kwa ajili ya kuwafurahisha. 
Meneja Masoko wa ASAS Jimmy Kiwelu akizungumza mbele ya Waandishi wa habari mapema leo jijini Dar,kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya tamasha la Asas Mtoto Day Out,Kiwelu amesema wanatambua umuhimu wa watoto kushiriki kwenye michezo mbalimbali, hivyo wakaona iko haja ya wao kuhakikisha tamasha hilo linafanikiwa ili kuwapa nafasi watoto kukutana na kucheza kwa pamoja.Amesema Asas siku zote wamekuwa wakiamini katika kuhakikisha mtoto anakuwa na furaha kwani furaha ya mtoto ndio furaha kwa mzazi/mlezi. 

Viewing all 109941 articles
Browse latest View live




Latest Images